\id ZEC - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Zekaria \toc1 Zekaria \toc2 Zekaria \toc3 Zek \mt1 Zekaria \c 1 \s1 Wito wa kumrudia Mwenyezi Mungu \p \v 1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema: \p \v 2 “Mwenyezi Mungu aliwakasirikia sana baba zako wa zamani. \v 3 Kwa hiyo waambie watu: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Nirudieni mimi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \v 4 Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema Mwenyezi Mungu. \v 5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? \v 6 Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu? \p “Kisha walitubu na kusema, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ” \s1 Maono ya kwanza: Mtu katikati ya miti ya mihadasi \p \v 7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido. \p \v 8 Wakati wa usiku nilipata maono, na tazama, mbele yangu palikuwa na mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia, na weupe. \p \v 9 Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?” \p Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonesha kuwa ni nini.” \p \v 10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma waende duniani kote.” \p \v 11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa Mwenyezi Mungu, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.” \p \v 12 Kisha malaika wa Mwenyezi Mungu akasema, “Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, utazuia hadi lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?” \v 13 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami. \p \v 14 Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, \v 15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’ \p \v 16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa juu ya Yerusalemu,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \p \v 17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi na Mwenyezi Mungu atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ” \s1 Maono ya pili: Pembe nne na mafundi wanne \p \v 18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! \v 19 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hizi?” \p Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.” \p \v 20 Kisha Mwenyezi Mungu akanionesha mafundi wanne. \v 21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?” \p Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.” \c 2 \s1 Maono ya tatu: Mtu mwenye kamba ya kupimia \p \v 1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu palikuwa na mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! \v 2 Nikamuuliza, “Unaenda wapi?” \p Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.” \p \v 3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye \v 4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. \v 5 Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’ \p \v 6 “Njooni! Njooni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asema Mwenyezi Mungu, “kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asema Mwenyezi Mungu. \p \v 7 “Njoo, ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!” \v 8 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake, \v 9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtajua kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma. \p \v 10 “Shangilia na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asema Mwenyezi Mungu. \v 11 “Mataifa mengi yataunganishwa na Mwenyezi Mungu siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu, nanyi mtajua kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma kwenu. \v 12 Mwenyezi Mungu atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu. \v 13 Tulieni mbele za Mwenyezi Mungu, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.” \c 3 \s1 Maono ya nne: Mavazi safi kwa ajili ya kuhani mkuu \p \v 1 Kisha akanionesha Yoshua\f + \fr 3:1 \fr*\ft Kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Yeshua\fqa*\ft , maana yake \ft*\fqa Yehova ni wokovu.\fqa*\f*, kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Mwenyezi Mungu, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki. \v 2 Mwenyezi Mungu akamwambia Shetani, “Mwenyezi Mungu akukemee Shetani! Mwenyezi Mungu, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?” \p \v 3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. \v 4 Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.” \p Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.” \p \v 5 Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Mwenyezi Mungu akiwa amesimama karibu. \p \v 6 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamwamuru Yoshua: \v 7 “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Ikiwa utatembea katika njia zangu na kushika maagizo yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa. \p \v 8 “ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninaenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. \v 9 Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja. \p \v 10 “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.” \c 4 \s1 Maono ya tano: Kinara cha taa cha dhahabu na mizeituni miwili \p \v 1 Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizini. \v 2 Akaniuliza, “Unaona nini?” \p Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. \v 3 Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.” \p \v 4 Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?” \p \v 5 Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?” \p Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.” \p \v 6 Kisha akaniambia, “Hili ni neno la Mwenyezi Mungu kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho wangu Mtakatifu,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \p \v 7 “Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa, na watu wakishangilia na kusema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ” \p \v 8 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likanijia: \v 9 “Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma mimi kwenu. \p \v 10 “Ni nani atakayeidharau siku ya mambo madogo? Macho saba ya Mwenyezi Mungu, yanayozunguka dunia yote, yatashangilia yatakapoona jiwe la juu kabisa likiwa mkononi mwa Zerubabeli!” \p \v 11 Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyo upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?” \p \v 12 Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?” \p \v 13 Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?” \p Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.” \p \v 14 Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.” \c 5 \s1 Maono ya sita: Kitabu kinachoruka \p \v 1 Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kinachoruka! \p \v 2 Akaniuliza, “Unaona nini?” \p Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka, chenye urefu wa dhiraa ishirini\f + \fr 5:2 \fr*\ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\ft*\f*, na upana wa dhiraa kumi\f + \fr 5:2 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa mita 4.5.\ft*\f*.” \p \v 3 Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atafukuziwa mbali, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atafukuziwa mbali. \v 4 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa Jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ” \s1 Maono ya saba: Mwanamke ndani ya kikapu \p \v 5 Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.” \p \v 6 Nikamuuliza, “Ni kitu gani?” \p Akanijibu, “Ni kikapu cha kupimia.” Kisha akaongeza kusema, “Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.” \p \v 7 Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuwako mwanamke ameketi! \v 8 Akasema, “Huu ni uovu,” tena akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu. \p \v 9 Kisha nikatazama juu: na pale mbele yangu, palikuwa na wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi. \p \v 10 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Wanakipeleka wapi hicho kikapu?” \p \v 11 Akanijibu, “Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.” \c 6 \s1 Maono ya nane: Magari manne ya vita \p \v 1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! \v 2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, \v 3 la tatu lilivutwa na farasi weupe, na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. \v 4 Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani, bwana wangu?” \p \v 5 Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. \v 6 Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi, na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.” \p \v 7 Hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote. \p \v 8 Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaoenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho wangu Mtakatifu katika nchi ya kaskazini.” \s1 Taji kwa ajili ya Yoshua \p \v 9 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 10 “Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku hiyo hiyo nenda nyumbani mwa Yosia mwana wa Sefania. \v 11 Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uliweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki. \v 12 Umwambie hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Huyu ndiye mtu anayeitwa Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 13 Ni yeye atakayejenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki kwenye kiti cha enzi. Atakuwa kuhani kwenye kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa na amani kati ya hao wawili.’ \v 14 Taji litatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 15 Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, nanyi mtajua kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa bidii.” \c 7 \s1 Sio kufunga, bali ni haki na rehema \p \v 1 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. \v 2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Mwenyezi Mungu \v 3 kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?” \p \v 4 Kisha neno la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni likanijia kusema: \v 5 “Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? \v 6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu? \v 7 Je, haya sio maneno ya Mwenyezi Mungu aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefela\f + \fr 7:7 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f* zikiwa zimekaliwa na watu?’ ” \p \v 8 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia tena Zekaria: \v 9 “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Fanyeni hukumu za haki, onesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. \v 10 Msimdhulumu mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’ \p \v 11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. \v 12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama gumegume, na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni aliyatuma kwa Roho wake Mtakatifu kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, alikasirika sana. \p \v 13 “ ‘Nilipoita, hawakusikiliza; kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \v 14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ” \c 8 \s1 Mwenyezi Mungu anaahidi kuibariki Yerusalemu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni likanijia tena. \p \v 2 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.” \p \v 3 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni utaitwa Mlima Mtakatifu.” \p \v 4 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Kwa mara nyingine tena wanaume na wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. \v 5 Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.” \p \v 6 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \p \v 7 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi. \v 8 Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.” \p \v 9 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa. \v 10 Kabla ya wakati huo, hapakuwa na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake. \v 11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \p \v 12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao. \v 13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.” \p \v 14 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonesha huruma,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \v 15 “hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope. \v 16 Haya ndio mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, \v 17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia haya yote,” asema Mwenyezi Mungu. \p \v 18 Neno la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni likanijia tena. \p \v 19 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Saumu ya mwezi wa nne, ya mwezi wa tano, ya mwezi wa saba, na ya mwezi wa kumi zitakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.” \p \v 20 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja, \v 21 na wenyeji wa mji mmoja wataenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi Mwenyezi Mungu, na kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Mimi mwenyewe ninaenda.’ \v 22 Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni na kumsihi.” \p \v 23 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watang’ang’ania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ” \c 9 \s1 Hukumu juu ya adui za Israeli \p \v 1 Neno la unabii: \q1 Neno la Mwenyezi Mungu liko kinyume na nchi ya Hadraki \q2 na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, \q1 kwa kuwa macho ya watu na ya makabila yote ya Israeli \q2 yako kwa Mwenyezi Mungu; \q1 \v 2 pia juu ya Hamathi inayopakana nayo, \q2 juu ya Tiro na Sidoni, \q2 ingawa wana ujuzi mwingi sana. \q1 \v 3 Tiro amejijengea ngome imara, \q2 amelundika fedha kama mavumbi, \q2 na dhahabu kama taka za mitaani. \q1 \v 4 Lakini Bwana atamwondolea mali yake \q2 na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, \q2 naye atateketezwa kwa moto. \q1 \v 5 Ashkeloni ataona hili na kuogopa; \q2 Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, \q1 pia Ekroni, kwa sababu \q2 matumaini yake yatanyauka. \q1 Gaza atampoteza mfalme wake \q2 na Ashkeloni ataachwa pweke. \q1 \v 6 Wageni watakalia mji wa Ashdodi, \q2 nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. \q1 \v 7 Nitaondoa damu vinywani mwao, \q2 chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. \q1 Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu, \q2 nao watakuwa viongozi katika Yuda, \q2 naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi. \q1 \v 8 Lakini nitailinda nyumba yangu \q2 dhidi ya majeshi ya wanyang’anyi. \q1 Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena, \q2 kwa maana sasa ninawachunga. \s1 Kuja kwa Mfalme wa Sayuni \q1 \v 9 Shangilia sana, ee Binti Sayuni! \q2 Piga kelele, Binti Yerusalemu! \q1 Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, \q2 ni mwenye haki, naye ana wokovu, \q2 ni mpole, naye amepanda punda, \q2 mwana-punda, mtoto wa punda. \q1 \v 10 Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu \q2 na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, \q2 nao upinde wa vita utavunjwa. \q1 Atatangaza amani kwa mataifa. \q2 Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, \q2 na kutoka Mto\f + \fr 9:10 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f* hadi mwisho wa dunia. \q1 \v 11 Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya agano langu nawe, \q2 nitawaacha huru wafungwa wako \q2 watoke kwenye shimo lisilo na maji. \q1 \v 12 Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini; \q2 hata sasa ninatangaza kwamba \q2 nitawarejesheeni maradufu. \q1 \v 13 Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu, \q2 nitamfanya Efraimu mshale wangu. \q1 Nitawainua wana wako, ee Sayuni, \q2 dhidi ya wana wako, ee Uyunani, \q2 na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita. \s1 Mwenyezi Mungu atatokea \q1 \v 14 Kisha Mwenyezi Mungu atawatokea; \q2 mshale wake utamulika kama radi. \q1 Bwana Mungu Mwenyezi atapiga tarumbeta, \q2 naye atatembea katika tufani za kusini, \q2 \v 15 na Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atawalinda. \q1 Wataangamiza na kushinda \q2 kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. \q1 Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo; \q2 watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia \q2 kwenye pembe za madhabahu. \q1 \v 16 Mwenyezi Mungu, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo \q2 kama kundi la watu wake. \q1 Watang’ara katika nchi yake \q2 kama vito vya thamani kwenye taji. \q1 \v 17 Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! \q2 Nafaka itawastawisha vijana wanaume, \q2 nayo divai mpya vijana wanawake. \c 10 \s1 Mwenyezi Mungu ataitunza Yuda \q1 \v 1 Mwombeni Mwenyezi Mungu mvua wakati wa vuli; \q2 ndiye Mwenyezi Mungu atengenezaye mawingu ya tufani. \q1 Huwapa watu manyunyu ya mvua, \q2 pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu. \q1 \v 2 Sanamu huzungumza udanganyifu, \q2 waaguzi huona maono ya uongo; \q1 husimulia ndoto ambazo si za kweli, \q2 wanatoa faraja batili. \q1 Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo \q2 walioteseka kwa kukosa mchungaji. \b \q1 \v 3 “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, \q2 nami nitawaadhibu viongozi; \q1 kwa kuwa Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 atalichunga kundi lake, \q2 nyumba ya Yuda, \q1 naye atawafanya kama farasi \q2 mwenye kiburi akiwa vitani. \q1 \v 4 Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni, \q2 kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema, \q2 kutoka kwake utatoka upinde wa vita, \q2 kutoka kwake atatoka kila mtawala. \q1 \v 5 Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa \q2 wanaokanyaga barabara za matope \q2 wakati wa vita. \q1 Kwa sababu Mwenyezi Mungu yu pamoja nao, \q2 watapigana na kuwashinda wapanda farasi. \b \q1 \v 6 “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda \q2 na kuiokoa nyumba ya Yusufu. \q1 Nitawarejesha kwa sababu \q2 nina huruma juu yao. \q1 Watakuwa kama watu ambao \q2 sijawahi kuwakataa \q1 kwa sababu mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao, \q2 nami nitawajibu. \q1 \v 7 Waefraimu watakuwa kama mashujaa, \q2 mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai. \q1 Watoto wao wataona na kufurahi, \q2 mioyo yao itashangilia katika Mwenyezi Mungu. \q1 \v 8 Nitawaashiria na kuwakusanya ndani. \q2 Hakika nitawakomboa, \q1 nao watakuwa wengi \q2 kama walivyokuwa mwanzoni. \q1 \v 9 Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa, \q2 hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali \q2 watanikumbuka mimi. \q1 Wao na watoto wao watanusurika katika hatari \q2 nao watarudi. \q1 \v 10 Nitawarudisha kutoka Misri \q2 na kuwakusanya toka Ashuru. \q1 Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni, \q2 na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha. \q1 \v 11 Watapita katika bahari ya mateso; \q2 bahari iliyochafuka itatulizwa \q2 na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. \q1 Kiburi cha Ashuru kitashushwa, \q2 nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka. \q1 \v 12 Nitawaimarisha katika Mwenyezi Mungu, \q2 na katika jina lake watatembea,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \c 11 \q1 \v 1 Fungua milango yako, ee Lebanoni, \q2 ili moto uteketeze mierezi yako! \q1 \v 2 Piga yowe, ee msunobari, \q2 kwa kuwa mwerezi umeanguka; \q2 miti ya fahari imeharibiwa! \q1 Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, \q2 msitu mnene umefyekwa! \q1 \v 3 Sikiliza yowe la wachungaji; \q2 malisho yao manono yameangamizwa! \q1 Sikia ngurumo za simba; \q2 kichaka kilichostawi sana \q2 cha Yordani kimeharibiwa! \s1 Wachungaji wawili \p \v 4 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. \v 5 Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. \v 6 Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.” \p \v 7 Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililodhulumiwa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi. \v 8 Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu. \p Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao, \v 9 nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.” \p \v 10 Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua agano nililofanya na mataifa yote. \v 11 Likatanguka siku hiyo; kwa hiyo wale waliodhulumiwa katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la Mwenyezi Mungu. \p \v 12 Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha. \p \v 13 Naye Mwenyezi Mungu akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. \p \v 14 Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli! \p \v 15 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. \v 16 Kwa maana ninaenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao. \q1 \v 17 “Ole wa mchungaji asiyefaa, \q2 anayeliacha kundi! \q1 Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume! \q2 Mkono wake na unyauke kabisa, \q2 jicho lake la kuume lipofuke kabisa!” \c 12 \s1 Adui za Yerusalemu kuangamizwa \p \v 1 Neno la unabii: Hili ni neno la Mwenyezi Mungu kuhusu Israeli. \b \p Mwenyezi Mungu, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: \v 2 “Nitaenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia. \v 3 Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe. \v 4 Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa wazimu,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa. \v 5 Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ni Mungu wao.’ \p \v 6 “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake. \p \v 7 “Mwenyezi Mungu atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa kuliko ile ya Yuda. \v 8 Katika siku hiyo, Mwenyezi Mungu atawakinga wale wanaoishi Yerusalemu, ili aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Mwenyezi Mungu akiwatangulia. \v 9 Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. \s1 Kumwombolezea yule aliyechomwa mkuki \p \v 10 “Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema\f + \fr 12:10 \fr*\ft au \ft*\fqa Roho wa neema\fqa*\f* na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. \v 11 Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. \v 12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao, \v 13 ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, \v 14 na koo zote zilizobaki na wake zao. \c 13 \s1 Kutakaswa dhambi \p \v 1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi. \p \v 2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi. \v 3 Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la Mwenyezi Mungu.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo. \p \v 4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu. \v 5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’ \v 6 Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’ \s1 Mchungaji apigwa, nao kondoo watawanyika \q1 \v 7 “Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, \q2 dhidi ya mtu aliye karibu nami!” \q2 asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \q1 “Mpige mchungaji, \q2 nao kondoo watatawanyika, \q1 nami nitageuza mkono wangu \q2 dhidi ya walio wadogo, \q1 \v 8 katika nchi yote,” asema Mwenyezi Mungu, \q2 “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; \q2 hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake. \q1 \v 9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto; \q2 nitawasafisha kama fedha isafishwavyo \q2 na kuwajaribu kama dhahabu. \q1 Wataliitia Jina langu \q2 nami nitawajibu; \q1 nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ \q2 nao watasema, ‘Mwenyezi Mungu ni Mungu wetu.’ ” \c 14 \s1 Mwenyezi Mungu yuaja kutawala \p \v 1 Siku ya Mwenyezi Mungu inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu. \p \v 2 Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji wataenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini. \p \v 3 Kisha Mwenyezi Mungu atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita. \v 4 Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. \v 5 Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye. \p \v 6 Siku hiyo hakutakuwa na nuru, baridi wala theluji. \v 7 Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na Mwenyezi Mungu. Jioni inapofika nuru itakuwepo. \p \v 8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki\f + \fr 14:8 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Chumvi \fqa*\ft au \ft*\fqa Bahari Mfu\fqa*\f*, na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi\f + \fr 14:8 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Mediterania\fqa*\f* wakati wa kiangazi na wakati wa masika. \p \v 9 Mwenyezi Mungu atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwa Mwenyezi Mungu mmoja, na jina lake litakuwa jina pekee. \p \v 10 Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba\f + \fr 14:10 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Nchi tambarare\fqa*\f*. Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. \v 11 Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama. \p \v 12 Hii ndiyo tauni ambayo Mwenyezi Mungu atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. \v 13 Katika siku hiyo Mwenyezi Mungu atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana. \v 14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na mavazi. \v 15 Tauni ya aina hiyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walio kwenye kambi za adui. \p \v 16 Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. \v 17 Ikiwa taifa lolote la dunia hawataenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, mvua haitanyesha kwao. \v 18 Ikiwa watu wa Misri nao hawataenda kushiriki, hawatapata mvua. Mwenyezi Mungu ataleta juu yao tauni ambayo itayapiga mataifa ambayo hayataenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. \v 19 Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayataenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. \p \v 20 Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: “Takatifu kwa Mwenyezi Mungu”. Navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. \v 21 Kila chungu kilicho Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.