\id SNG - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Wimbo Ulio Bora \toc1 Wimbo Ulio Bora \toc2 Wimbo \toc3 Wim \mt1 Wimbo Ulio Bora \c 1 \p \v 1 Wimbo ulio bora wa Sulemani. \sp Mpendwa\f + \fr 1:2 \fr*\ft Kulingana na matumizi ya lugha ya Kiebrania, mnenaji wa kiume na wa kike wametofautishwa kwa kichwa cha Mpenzi na Mpendwa. Wanenaji wengine wamepewa kichwa cha Rafiki. Wakati mwingine haijulikani kwa hakika nani ananena, lakini mapokeo yamefuatwa kutambulisha wanenaji.\ft*\f* \q1 \v 2 Unibusu kwa busu la kinywa chako, \q2 kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai. \q1 \v 3 Manukato yako yananukia vizuri, \q2 jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. \q1 Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! \q1 \v 4 Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! \q1 Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. \sp Rafiki \q1 Tunakushangilia na kukufurahia, \q1 tutasifu upendo wako kuliko divai. \sp Mpendwa \q1 Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! \q1 \v 5 Mimi ni mweusi, lakini napendeza, \q2 enyi binti za Yerusalemu, \q2 mweusi kama mahema ya Kedari, \q2 kama mapazia ya hema la Sulemani. \q1 \v 6 Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, \q2 kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. \q1 Wana wa mama yangu walinikasirikia \q2 na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. \q2 Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha. \q1 \v 7 Niambie, wewe ninayekupenda, \q2 unalisha wapi kundi lako la kondoo \q2 na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. \q1 Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela \q2 karibu na makundi ya rafiki zako? \sp Rafiki \q1 \v 8 Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, \q2 fuata nyayo za kondoo, \q1 na kulisha wana-mbuzi wako \q2 karibu na mahema ya wachungaji. \sp Mpenzi \q1 \v 9 Mpendwa wangu, ninakufananisha na farasi jike \q2 aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao. \q1 \v 10 Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, \q2 shingo yako ikiwa na mikufu ya vito. \q1 \v 11 Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, \q2 vyenye kupambwa kwa fedha. \sp Mpendwa \q1 \v 12 Mfalme alipokuwa mezani pake, \q2 manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri. \q1 \v 13 Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane \q2 kati ya matiti yangu. \q1 \v 14 Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina \q2 kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi. \sp Mpenzi \q1 \v 15 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpendwa wangu! \q2 Tazama jinsi ulivyo mzuri! \q2 Macho yako ni kama ya hua. \sp Mpendwa \q1 \v 16 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! \q2 Ee, tazama jinsi unavyopendeza! \q2 Na kitanda chetu ni cha majani mazuri. \sp Mpenzi \q1 \v 17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, \q2 na mapao yetu ni miberoshi. \c 2 \sp Mpendwa \q1 \v 1 Mimi ni ua la Sharoni, \q2 yungiyungi ya bondeni. \sp Mpenzi \q1 \v 2 Kama yungiyungi kati ya miiba, \q2 ndivyo alivyo mpendwa wangu kati ya wanawali. \sp Mpendwa \q1 \v 3 Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni, \q2 ndivyo alivyo mpenzi wangu \q2 miongoni mwa wanaume vijana. \q1 Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, \q2 na tunda lake ni tamu kwangu. \q1 \v 4 Amenichukua hadi ukumbi wa karamu, \q2 na bendera ya huyu mwanaume \q2 juu yangu ni upendo. \q1 \v 5 Nitie nguvu kwa zabibu kavu, \q2 niburudishe kwa matofaa, \q2 kwa maana ninazimia kwa mapenzi. \q1 \v 6 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, \q2 na mkono wake wa kuume unanikumbatia. \q1 \v 7 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza \q2 kwa paa na kwa ayala wa shambani: \q1 Msichochee wala kuamsha mapenzi \q2 hata yatakapotaka yenyewe. \b \q1 \v 8 Sikiliza! Mpenzi wangu! \q2 Tazama! Huyu hapa anakuja, \q1 akirukaruka juu milimani \q2 akizunguka juu ya vilima. \q1 \v 9 Mpenzi wangu ni kama paa au ayala mchanga. \q2 Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu, \q1 akitazama kupitia madirishani, \q2 akichungulia kimiani. \q1 \v 10 Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, \q2 “Inuka, mpendwa wangu, \q2 mrembo wangu, tufuatane. \q1 \v 11 Tazama! Wakati wa masika umepita, \q2 mvua imekwisha na ikapita. \q1 \v 12 Maua yanatokea juu ya nchi; \q2 majira ya kuimba yamewadia, \q1 sauti za njiwa zinasikika \q2 katika nchi yetu. \q1 \v 13 Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, \q2 zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri. \q1 Inuka, njoo mpenzi wangu. \q2 Mrembo wangu, tufuatane.” \sp Mpenzi \q1 \v 14 Hua wangu penye nyufa za majabali, \q2 mafichoni pembezoni mwa mlima, \q1 nioneshe uso wako, \q2 na niisikie sauti yako, \q1 kwa maana sauti yako ni tamu, \q2 na uso wako unapendeza. \q1 \v 15 Tukamatie mbweha, \q2 mbweha wale wadogo \q1 wanaoharibu mashamba ya mizabibu, \q2 mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua. \sp Mpendwa \q1 \v 16 Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake, \q2 yeye hujilisha kati ya yungiyungi. \q1 \v 17 Hadi jua linapochomoza, \q2 na vivuli vikimbie, \q1 rudi, mpenzi wangu, \q2 na uwe kama paa, \q1 au kama ayala mchanga \q2 juu ya vilima vya Betheri. \b \c 3 \q1 \v 1 Usiku kucha kwenye kitanda changu \q2 nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; \q2 nilimtafuta, lakini sikumpata. \q1 \v 2 Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, \q2 katika barabara zake na viwanja; \q1 nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. \q2 Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata. \q1 \v 3 Walinzi walinikuta \q2 walipokuwa wakizunguka mji. \q1 Nikawauliza, “Je, mmemwona \q2 yule moyo wangu umpendaye?” \q1 \v 4 Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita \q2 nilimpata yule moyo wangu umpendaye. \q1 Nilimshika na sikumwachia aende \q2 hadi nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, \q2 katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. \q1 \v 5 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza \q2 kwa paa na kwa ayala wa shambani: \q1 Msichochee wala kuamsha mapenzi \q2 hata yatakapotaka yenyewe. \b \q1 \v 6 Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani \q2 kama nguzo ya moshi, \q1 anayenukia manemane na uvumba \q2 iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote \q2 vya mfanyabiashara? \q1 \v 7 Tazama! Ni gari la Sulemani \q2 likisindikizwa na mashujaa sitini, \q2 walio wakuu sana wa Israeli, \q1 \v 8 wote wamevaa panga, \q2 wote wazoefu katika vita, \q1 kila mmoja na upanga wake pajani, \q2 wamejiandaa kwa ajili ya vitisho vya usiku. \q1 \v 9 Mfalme Sulemani alijitengenezea gari; \q2 alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni. \q1 \v 10 Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, \q2 kitako chake kwa dhahabu. \q1 Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, \q2 gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo \q2 na binti za Yerusalemu. \q1 \v 11 Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, \q2 mkamtazame Mfalme Sulemani akiwa amevaa taji, \q1 taji ambalo mama yake alimvika \q2 siku ya arusi yake, \q2 siku ambayo moyo wake ulishangilia. \c 4 \sp Mpenzi \q1 \v 1 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpendwa wangu! \q2 Ee, jinsi ulivyo mzuri! \q1 Macho yako nyuma ya shela yako \q2 ni kama ya hua. \q1 Nywele zako ni kama kundi la mbuzi \q2 wakishuka kutoka Mlima Gileadi. \q1 \v 2 Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi, \q2 wanaotoka kuogeshwa. \q1 Kila jino lina pacha lake; \q2 hakuna hata moja lililo pekee. \q1 \v 3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu, \q2 kinywa chako kinapendeza. \q1 Mashavu yako nyuma ya shela yako \q2 ni kama vipande viwili vya komamanga. \q1 \v 4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, \q2 uliojengwa kwa madaha, \q1 juu yake zimetundikwa ngao elfu, \q2 zote ni ngao za mashujaa. \q1 \v 5 Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili, \q2 kama wana-paa mapacha \q2 wajilishao kati ya yungiyungi. \q1 \v 6 Hata kupambazuke na vivuli vikimbie, \q2 nitaenda kwenye mlima wa manemane \q2 na kwenye kilima cha uvumba. \q1 \v 7 Wewe ni mzuri kote, mpendwa wangu, \q2 hakuna hitilafu ndani yako. \b \q1 \v 8 Nenda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, \q2 nenda nami kutoka Lebanoni. \q1 Shuka kutoka ncha ya Amana, \q2 kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, \q1 kutoka mapango ya simba \q2 na kutoka mlima wapendapo kukaa chui. \q1 \v 9 Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; \q2 umeiba moyo wangu \q1 kwa mtazamo mmoja wa macho yako, \q2 kwa kito kimoja cha mkufu wako. \q1 \v 10 Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, \q2 dada yangu, bibi arusi wangu! \q1 Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, \q2 na harufu ya marhamu yako zaidi ya manukato yoyote! \q1 \v 11 Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, \q2 bibi arusi wangu; \q1 maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. \q2 Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni. \q1 \v 12 Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, \q2 bibi arusi wangu; \q1 wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, \q2 chemchemi yangu peke yangu. \q1 \v 13 Mimea yako ni bustani ya mikomamanga \q2 yenye matunda mazuri sana, \q2 yenye hina na nardo, \q1 \v 14 nardo na zafarani, \q2 mchai na mdalasini, \q2 pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, \q2 manemane na udi, \q2 na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote. \q1 \v 15 Wewe ni chemchemi ya bustani, \q2 kisima cha maji yanayotiririka, \q2 yakitiririka kutoka Lebanoni. \sp Mpendwa \q1 \v 16 Amka, upepo wa kaskazini, \q2 na uje, upepo wa kusini! \q2 Vuma juu ya bustani yangu, \q2 ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ng’ambo. \q1 Mpenzi wangu na aje bustanini mwake \q2 na kuonja matunda mazuri sana. \c 5 \sp Mpenzi \q1 \v 1 Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, \q2 bibi arusi wangu; \q1 nimekusanya manemane yangu pamoja \q2 na manukato yangu. \q1 Nimekula sega langu la asali na asali yangu; \q2 nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. \sp Rafiki \q1 Kuleni, enyi rafiki, mnywe; \q1 kunyweni ya kutosha, ee wapenzi. \b \sp Mpendwa \q1 \v 2 Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho. \q1 Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha: \q2 “Nifungulie, dada yangu, mpendwa wangu, \q2 hua wangu, usiye na hitilafu. \q1 Kichwa changu kimeloa umande, \q2 na nywele zangu manyunyu ya usiku.” \q1 \v 3 Nimevua joho langu: \q2 je, ni lazima nivae tena? \q1 Nimenawa miguu yangu: \q2 je, ni lazima niichafue tena? \q1 \v 4 Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo; \q2 moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake. \q1 \v 5 Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu, \q2 mikono yangu ikidondosha manemane, \q1 vidole vyangu vikitiririka manemane, \q2 penye vipini vya komeo. \q1 \v 6 Nilimfungulia mpenzi wangu, \q2 lakini mpenzi wangu alishaondoka; \q2 alikuwa ameenda zake. \q1 Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake. \q2 Nilimtafuta lakini sikumpata. \q2 Nilimwita lakini hakunijibu. \q1 \v 7 Walinzi walinikuta \q2 walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini. \q1 Walinipiga, wakanijeruhi, \q2 wakaninyang’anya joho langu, \q2 hao walinzi wa kuta! \q1 \v 8 Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza: \q2 mkimpata mpenzi wangu, \q1 mtamwambia nini? \q2 Mwambieni ninazimia kwa mapenzi. \sp Rafiki \q1 \v 9 Je, mpenzi wako ni bora kuliko wengine namna gani, \q2 wewe uliye mzuri kupita wanawake wote? \q1 Je, mpenzi wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani, \q2 hata unatuagiza hivyo? \sp Mpendwa \q1 \v 10 Mpenzi wangu anang’aa, tena ni mwekundu, \q2 wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu. \q1 \v 11 Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote, \q2 nywele zake ni za mawimbi \q2 na ni nyeusi kama kunguru. \q1 \v 12 Macho yake ni kama ya hua \q2 kandokando ya vijito vya maji, \q1 aliyeogeshwa kwenye maziwa, \q2 yaliyopangwa kama vito vya thamani. \q1 \v 13 Mashavu yake ni kama matuta \q2 ya mimea ya manukato. \q1 Midomo yake ni kama yungiyungi \q2 inayodondosha manemane. \q1 \v 14 Mikono yake ni fimbo za dhahabu \q2 iliyopambwa kwa krisolitho. \q1 Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyong’arishwa \q2 iliyopambwa na yakuti samawi. \q1 \v 15 Miguu yake ni nguzo za marumaru \q2 zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi. \q1 Sura yake ni kama Lebanoni, \q2 bora kama miti yake ya mierezi. \q1 \v 16 Kinywa chake chenyewe ni utamu, \q2 kwa ujumla yeye ni wa kupendeza. \q1 Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu, \q2 ee binti za Yerusalemu. \c 6 \sp Rafiki \q1 \v 1 Mpenzi wako ameenda wapi, \q2 ewe mzuri kupita wanawake wote? \q1 Mpenzi wako amegeukia njia ipi, \q2 tupate kumtafuta pamoja nawe? \sp Mpendwa \q1 \v 2 Mpenzi wangu ameenda bustanini mwake, \q2 kwenye vitalu vya vikolezo, \q1 kujilisha bustanini \q2 na kukusanya yungiyungi. \q1 \v 3 Mimi ni wake mpenzi wangu, \q2 na mpenzi wangu ni wangu; \q2 yeye hujilisha kati ya yungiyungi. \b \sp Mpenzi \q1 \v 4 Wewe ni mzuri, mpendwa wangu, kama Tirsa, \q2 unapendeza kama Yerusalemu, \q2 umetukuka kama jeshi lenye bendera. \q1 \v 5 Uyageuze macho yako mbali nami; \q2 yananigharikisha. \q1 Nywele zako ni kama kundi la mbuzi \q2 wanaoteremka kutoka Gileadi. \q1 \v 6 Meno yako ni kama kundi la kondoo \q2 wanaotoka kuogeshwa. \q1 Kila mmoja ana pacha lake, \q2 hakuna hata mmoja aliye peke yake. \q1 \v 7 Mashavu yako nyuma ya shela yako \q2 ni kama vipande viwili vya komamanga. \q1 \v 8 Panaweza kuwa na malkia sitini, \q2 masuria themanini, \q2 na mabikira wasiohesabika; \q1 \v 9 lakini hua wangu, mkamilifu wangu, \q2 ni wa namna ya pekee, \q1 binti pekee kwa mama yake, \q2 kipenzi cha yeye aliyemzaa. \q1 Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa; \q2 malkia na masuria walimsifu. \sp Rafiki \q1 \v 10 Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko, \q2 mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua, \q2 ametukuka kama nyota zinazofuatana? \sp Mpenzi \q1 \v 11 Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi \q2 ili kutazama machipuko ya bondeni, \q1 kuona kama mizabibu imechipua \q2 au kama mikomamanga imechanua maua. \q1 \v 12 Kabla sijang’amua, \q2 shauku yangu iliniweka \q2 katikati ya magari ya vita ya wakuu wangu. \sp Rafiki \q1 \v 13 Rudi, rudi, ee Mshulami; \q2 rudi, rudi ili tupate kukutazama! \sp Mpenzi \q1 Kwa nini kumtazama Mshulami, \q2 kama kutazama ngoma ya Mahanaimu\f + \fr 6:13 \fr*\ft au \ft*\fqa majeshi mawili\fqa*\f*? \b \c 7 \q1 \v 1 Ee binti ya mwana wa mfalme, \q2 tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu! \q1 Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani, \q2 kazi ya mikono ya fundi stadi. \q1 \v 2 Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo \q2 ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa. \q1 Kiuno chako ni kichuguu cha ngano \q2 kilichozungukwa kwa yungiyungi. \q1 \v 3 Matiti yako ni kama wana-paa wawili, \q2 mapacha wa paa. \q1 \v 4 Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu. \q2 Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni \q2 karibu na lango la Beth-Rabi. \q1 Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni \q2 ukitazama kuelekea Dameski. \q1 \v 5 Kichwa chako kinakuvika taji kama Mlima Karmeli. \q2 Nywele zako ni kama zulia la urujuani; \q2 mfalme ametekwa na mashungi yake. \q1 \v 6 Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza, \q2 ee pendo, kwa uzuri wako! \q1 \v 7 Umbo lako ni kama la mtende, \q2 nayo matiti yako kama vishada vya matunda. \q1 \v 8 Nilisema, “Nitakwea mtende, \q2 nami nitayashika matunda yake.” \q1 Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu, \q2 harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa, \q1 \v 9 na kinywa chako kama divai \q2 bora kuliko zote. \sp Mpendwa \q1 Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu, \q2 ikitiririka polepole juu ya midomo na meno. \q1 \v 10 Mimi ni mali ya mpenzi wangu, \q2 nayo shauku yake ni juu yangu. \q1 \v 11 Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, \q2 twende tukalale huko vijijini. \q1 \v 12 Hebu na twende mapema \q2 katika mashamba ya mizabibu \q2 tuone kama mizabibu imechipua, \q1 kama maua yake yamefunguka, \q2 na kama mikomamanga imetoa maua: \q2 huko nitakupa penzi langu. \q1 \v 13 Mitunguja hutoa harufu zake nzuri, \q2 kwenye milango yetu kuna matunda mazuri, \q1 mapya na ya zamani, \q2 ambayo nimekuhifadhia wewe, \q2 mpenzi wangu. \b \c 8 \q1 \v 1 Laiti ungekuwa kwangu kama ndugu wa kiume, \q2 ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu! \q1 Kisha, kama ningekukuta huko nje, \q2 ningekubusu, \q2 wala hakuna mtu yeyote angenidharau. \q1 \v 2 Ningekuongoza na kukuleta \q2 katika nyumba ya mama yangu, \q2 yeye ambaye amenifundisha. \q1 Ningekupa divai iliyokolezwa unywe, \q2 asali ya maua ya mikomamanga yangu. \q1 \v 3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, \q2 na mkono wake wa kuume unanikumbatia. \q1 \v 4 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza: \q2 msichochee wala kuamsha mapenzi \q2 hata yatakapotaka yenyewe. \b \sp Rafiki \q1 \v 5 Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani \q2 akimwegemea mpenzi wake? \sp Mpendwa \q1 Nilikuamsha chini ya mtofaa, \q2 huko mama yako alipotunga mimba yako, \q2 huko yeye alipata uchungu akakuzaa. \q1 \v 6 Nitie kama muhuri moyoni mwako, \q2 kama muhuri kwenye mkono wako; \q1 kwa maana upendo una nguvu kama mauti, \q2 wivu wake ni mkatili kama Kuzimu\f + \fr 8:6 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f*. \q1 Unachoma kama mwali wa moto, \q2 kama mwali mkubwa wa moto wa Mwenyezi Mungu hasa. \q1 \v 7 Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, \q2 mito haiwezi kuugharikisha. \q1 Kama mtu angetoa mali yote ya nyumbani mwake \q2 kwa ajili ya upendo, \q2 angedharauliwa kabisa. \sp Rafiki \q1 \v 8 Tunaye dada mdogo, \q2 matiti yake hayajakua bado. \q1 Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu \q2 wakati atakapokuja kuposwa? \q1 \v 9 Kama yeye ni ukuta, \q2 tutajenga minara ya fedha juu yake. \q1 Na kama yeye ni mlango, \q2 tutamzungushia mbao za mwerezi. \sp Mpendwa \q1 \v 10 Mimi ni ukuta, \q2 nayo matiti yangu ni kama minara. \q1 Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake \q2 kama yule anayeleta utoshelevu. \q1 \v 11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni; \q2 alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji. \q1 Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake \q2 shekeli elfu moja\f + \fr 8:11 \fr*\ft Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5.\ft*\f* za fedha. \q1 \v 12 Lakini shamba langu la mizabibu \q2 ambalo ni langu mwenyewe \q2 ni langu kutoa; \q1 hizo shekeli elfu moja ni kwa ajili yako, ee Sulemani, \q2 na shekeli mia mbili\f + \fr 8:12 \fr*\ft Shekeli 200 ni kama kilo 2.3.\ft*\f* ni kwa ajili \q2 ya wale wanaotunza matunda yake. \sp Mpenzi \q1 \v 13 Wewe ukaaye bustanini \q2 pamoja na rafiki mliohudhuria, \q2 hebu nisikie sauti yako! \sp Mpendwa \q1 \v 14 Njoo, mpenzi wangu, \q2 uwe kama paa \q1 au kama ayala mchanga \q2 juu ya milima iliyojaa manukato.