\id PSA - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Zaburi \toc1 Zaburi \toc2 Zaburi \toc3 Za \mt1 Zaburi \c 1 \ms Kitabu cha Kwanza \mr (Zaburi 1–41) \cl Zaburi 1 \s1 Furaha ya kweli \q1 \v 1 Heri mtu yule ambaye haendi \q2 katika shauri la watu waovu, \q1 wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, \q2 au kuketi katika baraza la wenye mizaha. \q1 \v 2 Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu, \q2 naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana. \q1 \v 3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa \q2 kando ya vijito vya maji, \q2 ambao huzaa matunda kwa majira yake \q1 na majani yake hayanyauki. \q2 Lolote afanyalo hufanikiwa. \s1 Huzuni ya waovu \q1 \v 4 Sivyo walivyo waovu! \q2 Wao ni kama makapi \q2 yanayopeperushwa na upepo. \q1 \v 5 Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, \q2 wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. \b \q1 \v 6 Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki, \q2 bali njia za waovu zitaangamia. \c 2 \cl Zaburi 2 \s1 Mfalme aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, \q2 na makabila ya watu kula njama bure? \q1 \v 2 Wafalme wa dunia wanajipanga \q2 na watawala wanajikusanya \q1 dhidi ya Mwenyezi Mungu \q2 na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. \q1 \v 3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao \q2 na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” \b \q1 \v 4 Yeye anayetawala mbinguni hucheka, \q2 Bwana huwadharau. \q1 \v 5 Kisha huwakemea katika hasira yake \q2 na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, \q1 \v 6 “Nimemtawaza Mfalme wangu \q2 juu ya Sayuni, \q2 mlima wangu mtakatifu.” \s1 Ushindi wa mfalme \p \v 7 Nitatangaza amri ya Mwenyezi Mungu: \b \q1 Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu; \q2 leo mimi nimekuwa Baba yako. \q1 \v 8 Niombe, nami nitayafanya mataifa \q2 kuwa urithi wako, \q2 na miisho ya dunia kuwa milki yako. \q1 \v 9 Utawapondaponda kwa fimbo ya chuma, \q2 na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” \b \q1 \v 10 Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; \q2 mwonyeke, enyi watawala wa dunia. \q1 \v 11 Mtumikieni Mwenyezi Mungu kwa hofu \q2 na mshangilie kwa kutetemeka. \q1 \v 12 Mbusu Mwana, asije akakasirika \q2 nawe ukaangamizwa katika njia yako, \q1 kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. \q2 Heri wote wanaomkimbilia. \c 3 \cl Zaburi 3 \s1 Sala ya asubuhi ya kuomba msaada \d Zaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, tazama adui zangu walivyo wengi! \q2 Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! \q1 \v 2 Wengi wanasema juu yangu, \q2 “Mungu hatamwokoa.” \b \q1 \v 3 Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote; \q2 umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. \q1 \v 4 Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, \q2 naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. \b \q1 \v 5 Ninajilaza na kupata usingizi; \q2 naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza. \q1 \v 6 Sitaogopa makumi elfu ya adui, \q2 wanaojipanga dhidi yangu kila upande. \b \q1 \v 7 Ee Mwenyezi Mungu, amka! \q2 Niokoe, Ee Mungu wangu! \q1 Wapige adui zangu wote kwenye taya, \q2 vunja meno ya waovu. \b \q1 \v 8 Kwa maana wokovu watoka kwa Mwenyezi Mungu. \q1 Baraka yako na iwe juu ya watu wako. \c 4 \cl Zaburi 4 \s1 Sala ya jioni ya kuomba msaada \d Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nijibu nikuitapo, \q2 Ee Mungu wangu mwenye haki! \q1 Nipumzishe katika shida zangu; \q2 nirehemu, usikie ombi langu. \b \q1 \v 2 Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu \q2 kuwa aibu hadi lini? \q1 Mtapenda udanganyifu \q2 na kufuata miungu ya uongo hadi lini? \q1 \v 3 Fahamuni hakika kwamba Mwenyezi Mungu amewatenga \q2 wale wamchao kwa ajili yake; \q2 Mwenyezi Mungu atanisikia nimwitapo. \b \q1 \v 4 Katika hasira yako, usitende dhambi. \q2 Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu, \q2 mkiichunguza mioyo yenu. \q1 \v 5 Toeni dhabihu zilizo haki; \q2 mtegemeeni Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 6 Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye \q2 kutuonesha jema lolote?” \q2 Ee Mwenyezi Mungu, tuangazie nuru ya uso wako. \q1 \v 7 Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa \q2 kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi. \q1 \v 8 Nitajilaza chini na kulala kwa amani, \q2 kwa kuwa wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 waniwezesha kukaa kwa salama. \c 5 \cl Zaburi 5 \s1 Sala kwa ajili ya ulinzi wakati wa hatari \d Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, tegea sikio maneno yangu, \q2 uangalie kupiga kite kwangu. \q1 \v 2 Sikiliza kilio changu ili unisaidie, \q2 Mfalme wangu na Mungu wangu, \q2 kwa maana kwako ninaomba. \q1 \v 3 Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Mwenyezi Mungu; \q2 asubuhi naleta haja zangu mbele zako, \q2 na kusubiri kwa matumaini. \b \q1 \v 4 Wewe si Mungu unayefurahia uovu, \q2 kwako mtu mwovu hataishi. \q1 \v 5 Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, \q2 unawachukia wote watendao mabaya. \q1 \v 6 Unawaangamiza wasemao uongo. \q2 Mwenyezi Mungu huwachukia \q2 wanaomwaga damu na wadanganyifu. \b \q1 \v 7 Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, \q2 nitakuja katika nyumba yako, \q1 kwa unyenyekevu, nitasujudu \q2 kulielekea Hekalu lako takatifu. \q1 \v 8 Niongoze katika haki yako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 kwa sababu ya adui zangu, \q2 nyoosha njia yako mbele yangu. \b \q1 \v 9 Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, \q2 mioyo yao imejaa maangamizi. \q1 Koo lao ni kaburi lililo wazi, \q2 kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu. \q1 \v 10 Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! \q2 Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. \q1 Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, \q2 kwa kuwa wamekuasi wewe. \b \q1 \v 11 Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi, \q2 waimbe kwa shangwe daima. \q1 Ueneze ulinzi wako juu yao, \q2 ili wale wanaolipenda jina lako \q2 wapate kukushangilia. \q1 \v 12 Kwa hakika, Ee Mwenyezi Mungu, unawabariki wenye haki, \q2 unawazunguka kwa wema wako kama ngao. \c 6 \cl Zaburi 6 \s1 Sala ya kuomba msaada wakati wa taabu \d Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi.\f + \fr 6:0 \fr*\fq Sheminithi \fq*\ft ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji.\ft*\f* Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako, \q2 wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. \q1 \v 2 Unirehemu Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana nimedhoofika; \q1 Ee Mwenyezi Mungu, uniponye, \q2 kwa maana mifupa yangu \q2 ina maumivu makali. \q1 \v 3 Nafsi yangu ina uchungu mwingi. \q2 Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini? \b \q1 \v 4 Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe, \q2 uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. \q1 \v 5 Hakuna mtu anayekukumbuka \q2 akiwa amekufa. \q1 Ni nani awezaye kukusifu \q2 akiwa Kuzimu\f + \fr 6:5 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f*? \b \q1 \v 6 Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; \q2 usiku kucha natiririsha \q2 kitanda changu kwa machozi; \q1 nimelowesha kiti changu \q2 kwa machozi yangu. \q1 \v 7 Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, \q2 yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. \b \q1 \v 8 Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, \q2 kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu. \q1 \v 9 Mwenyezi Mungu amesikia kilio changu kwa huruma, \q2 Mwenyezi Mungu amekubali sala yangu. \q1 \v 10 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, \q2 watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula. \c 7 \cl Zaburi 7 \s1 Sala ya mtu anayedhulumiwa \d Ombolezo la Daudi kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, \q2 uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, \q1 \v 2 la sivyo watanirarua kama simba \q2 na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. \b \q1 \v 3 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kama nimetenda haya \q2 na kuna hatia mikononi mwangu, \q1 \v 4 au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, \q2 au nimemnyang’anya adui yangu pasipo sababu, \q1 \v 5 basi adui anifuatie na kunipata, \q2 auponde uhai wangu ardhini \q2 na kunilaza mavumbini. \b \q1 \v 6 Amka kwa hasira yako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. \q2 Amka, Mungu wangu, uamue haki. \q1 \v 7 Kusanyiko la watu na likuzunguke. \q2 Watawale kutoka juu. \q2 \v 8 Mwenyezi Mungu na awahukumu makabila ya watu. \q1 Nihukumu Ee Mwenyezi Mungu, \q2 kwa kadiri ya haki yangu, \q1 kwa kadiri ya uadilifu wangu, \q2 Ewe Uliye Juu Sana. \q1 \v 9 Ee Mungu mwenye haki, \q2 uchunguzaye mawazo na mioyo, \q1 komesha ghasia za waovu \q2 na ufanye wenye haki waishi kwa amani. \b \q1 \v 10 Ngao yangu ni Mungu Aliye Juu Sana, \q2 anayewaokoa wanyofu wa moyo. \q1 \v 11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, \q2 Mungu anayeghadhibika kila siku. \q1 \v 12 Mtu asipotubu, \q2 Mungu ataunoa upanga wake, \q2 ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. \q1 \v 13 Ameandaa silaha zake kali, \q2 ameweka tayari mishale yake ya moto. \b \q1 \v 14 Yeye aliye na mimba ya uovu \q2 na anayechukua mimba ya ghasia huzaa uongo. \q1 \v 15 Yeye anayechimba shimo na kulifukua \q2 hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. \q1 \v 16 Ghasia anazozianzisha humrudia mwenyewe, \q2 ukatili wake humrudia kichwani. \b \q1 \v 17 Nitamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya haki yake, \q2 na nitaliimbia sifa jina la Mwenyezi Mungu Aliye Juu Sana. \c 8 \cl Zaburi 8 \s1 Utukufu wa Mwenyezi Mungu na heshima ya mwanadamu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu, \q2 tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! \b \q1 Umeuweka utukufu wako \q2 juu ya mbingu. \q1 \v 2 Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya \q2 umeamuru sifa, \q1 kwa sababu ya watesi wako, \q2 kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. \b \q1 \v 3 Nikiziangalia mbingu zako, \q2 kazi ya vidole vyako, \q1 mwezi na nyota, \q2 ulizoziratibisha, \q1 \v 4 mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, \q2 binadamu ni nani hata unamjali? \q1 \v 5 Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, \q2 ukamvika taji la utukufu na heshima. \b \q1 \v 6 Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; \q2 umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. \q1 \v 7 Mifugo na makundi yote pia, \q2 naam, na wanyama wa kondeni, \q1 \v 8 ndege wa angani na samaki wa baharini, \q2 naam, kila kinachoogelea katika njia za bahari. \b \q1 \v 9 Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu, \q2 tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! \c 9 \cl Zaburi 9\f + \fr 9 \fr*\ft Zaburi hii ikiunganishwa na ya 10 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya haki yake \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni.\f + \fr 9:0 \fr*\ft Muth-labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki.\ft*\f* Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, \q2 nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. \q1 \v 2 Nitafurahi na kushangilia ndani yako. \q2 Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. \b \q1 \v 3 Adui zangu wamerudi nyuma, \q2 wamejikwaa na kuangamia mbele zako. \q1 \v 4 Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; \q2 umeketi kwenye kiti chako cha enzi, \q2 ukihukumu kwa haki. \q1 \v 5 Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; \q2 umeyafuta majina yao milele na milele. \q1 \v 6 Uharibifu usiokoma umempata adui, \q2 umeing’oa miji yao; \q2 hata kumbukumbu lao limetoweka. \b \q1 \v 7 Mwenyezi Mungu anatawala milele, \q2 ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu. \q1 \v 8 Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, \q2 atatawala mataifa kwa haki. \q1 \v 9 Mwenyezi Mungu ni kimbilio la wanaodhulumiwa, \q2 ni ngome imara wakati wa shida. \q1 \v 10 Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, \q2 kwa maana wewe Mwenyezi Mungu, \q2 hujawaacha kamwe wanaokutafuta. \b \q1 \v 11 Mwimbieni Mwenyezi Mungu sifa, amefanywa mtawala Sayuni, \q2 tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. \q1 \v 12 Kwa maana yeye anayelipiza kisasi cha damu hukumbuka, \q2 hapuuzi kilio cha wanaoonewa. \b \q1 \v 13 Ee Mwenyezi Mungu, tazama jinsi walivyo wengi \q2 adui zangu wanaonitesa! \q2 Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, \q1 \v 14 ili niweze kutangaza sifa zako \q2 katika malango ya Binti Sayuni, \q2 na huko niushangilie wokovu wako. \q1 \v 15 Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, \q2 miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha. \q1 \v 16 Mwenyezi Mungu anajulikana kwa haki yake, \q2 waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao. \b \q1 \v 17 Waovu wataishia Kuzimu\f + \fr 9:17 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f*, \q2 naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. \q1 \v 18 Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, \q2 wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. \b \q1 \v 19 Ee Mwenyezi Mungu, inuka, usimwache binadamu ashinde. \q2 Mataifa na yahukumiwe mbele zako. \q1 \v 20 Ee Mwenyezi Mungu, wapige kwa hofu, \q2 mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu. \c 10 \cl Zaburi 10\f + \fr 10 \fr*\ft Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Sala kwa ajili ya haki \q1 \v 1 Kwa nini, Ee Mwenyezi Mungu, unasimama mbali? \q2 Kwa nini unajificha wakati wa shida? \b \q1 \v 2 Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, \q2 waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. \q1 \v 3 Hujivunia tamaa za moyo wake; \q2 humbariki mlafi na kumtukana Mwenyezi Mungu. \q1 \v 4 Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, \q2 katika mawazo yake yote \q2 hakuna nafasi ya Mungu. \q1 \v 5 Njia zake daima hufanikiwa; \q2 hujivuna na amri zako ziko mbali naye, \q2 huwacheka kwa dharau adui zake wote. \q1 \v 6 Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, \q2 daima nitakuwa na furaha, \q2 kamwe sitakuwa na shida.” \q1 \v 7 Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; \q2 shida na ubaya viko chini ya ulimi wake. \q1 \v 8 Huvizia karibu na vijiji; \q2 kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, \q2 akivizia wapitaji. \q1 \v 9 Huvizia kama simba aliye mawindoni; \q2 huvizia kumkamata mnyonge, \q1 huwakamata wanyonge na kuwaburuza \q2 katika wavu wake. \q1 \v 10 Mateka wake hupondwa, huzimia; \q2 wanaanguka katika nguvu zake. \q1 \v 11 Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, \q2 huficha uso wake na haoni kabisa.” \b \q1 \v 12 Inuka Mwenyezi Mungu! Inua mkono wako, Ee Mungu. \q2 Usiwasahau wanyonge. \q1 \v 13 Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? \q2 Kwa nini anajiambia mwenyewe, \q2 “Hataniita nitoe hesabu”? \q1 \v 14 Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, \q2 umekubali kuyapokea mkononi mwako. \q1 Mhanga anajisalimisha kwako, \q2 wewe ni msaada wa yatima. \q1 \v 15 Vunja mkono wa mtu mbaya na mwovu; \q2 mwite mtu mbaya atoe hesabu ya uovu wake \q2 ambao usingejulikana vinginevyo. \b \q1 \v 16 Mwenyezi Mungu ni Mfalme milele na milele, \q2 mataifa wataangamia watoke nchini mwake. \q1 \v 17 Unasikia, Ee Mwenyezi Mungu, shauku ya wanaoonewa; \q2 wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, \q1 \v 18 ukiwatetea yatima na waliodhulumiwa, \q2 ili mwanadamu ambaye ni udongo asiogopeshe tena. \c 11 \cl Zaburi 11 \s1 Kumtumaini Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Kwa Mwenyezi Mungu ninakimbilia. \q2 Unawezaje basi kuniambia: \q2 “Ruka kama ndege utorokee kwenye mlima wako. \q1 \v 2 Hebu tazama, waovu wanapinda nyuta zao; \q2 wanaweka mishale kwenye nyuzi zake \q1 ili wakiwa gizani, wawapige \q2 walio wanyofu wa moyo. \q1 \v 3 Wakati misingi imeharibiwa, \q2 mwenye haki anaweza kufanya nini?” \b \q1 \v 4 Mwenyezi Mungu yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; \q2 Mwenyezi Mungu yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. \q1 Huwaangalia wana wa watu, \q2 macho yake yanawachunguza. \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu huwachunguza wenye haki, \q2 lakini nafsi yake inachukia waovu \q2 na wale wanaopenda mapigano. \q1 \v 6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali \q2 na kiberiti kinachowaka; \q2 upepo wenye joto kali ndio fungu lao. \b \q1 \v 7 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye haki, \q2 yeye hupenda haki. \q2 Wanyofu watauona uso wake. \c 12 \cl Zaburi 12 \s1 Kuomba msaada \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; \q2 waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu. \q1 \v 2 Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; \q2 midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu. \b \q1 \v 3 Mwenyezi Mungu na akatilie mbali midomo yote ya hila \q2 na kila ulimi uliojaa majivuno, \q1 \v 4 ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; \q2 midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?” \b \q1 \v 5 “Kwa sababu wanyonge wanaonewa, \q2 na wahitaji wanalia kwa uchungu, \q1 nitainuka sasa,” asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Nitawalinda kutokana na wale \q2 wenye nia mbaya juu yao.” \q1 \v 6 Maneno ya Mwenyezi Mungu ni safi, \q2 kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, \q2 iliyosafishwa mara saba. \b \q1 \v 7 Ee Mwenyezi Mungu, utatuweka salama \q2 na kutulinda na kizazi hiki milele. \q1 \v 8 Watu waovu huenda wakiringa kila mahali \q2 wakati yule aliye mbaya sana \q2 ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu. \c 13 \cl Zaburi 13 \s1 Sala ya kuomba msaada \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu? Je, utanisahau milele? \q2 Utanificha uso wako hadi lini? \q1 \v 2 Nitapambana na mawazo yangu hadi lini, \q2 na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? \q2 Adui zangu watanishinda hadi lini? \b \q1 \v 3 Nitazame, unijibu, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. \q2 Yatie nuru macho yangu, \q2 ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. \q1 \v 4 Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” \q2 nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. \b \q1 \v 5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; \q2 moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. \q1 \v 6 Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, \q2 kwa kuwa amekuwa mwema kwangu. \c 14 \cl Zaburi 14 \s1 Uovu wa wanadamu \r (Zaburi 53) \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mpumbavu anasema moyoni mwake, \q2 “Hakuna Mungu.” \q1 Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa; \q2 hakuna hata mmoja atendaye mema. \b \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamu \q2 kutoka mbinguni \q1 aone kama kuna mwenye hekima, \q2 yeyote anayemtafuta Mungu. \q1 \v 3 Wote wamepotoka, \q2 wote wameoza pamoja; \q1 hakuna atendaye mema, \q2 naam, hakuna hata mmoja! \b \q1 \v 4 Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza: \q2 wale ambao huwala watu wangu \q1 kama watu walavyo mkate, \q2 hao ambao hawamwiti Mwenyezi Mungu? \q1 \v 5 Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, \q2 maana Mungu yupo pamoja na wenye haki. \q1 \v 6 Ninyi watenda maovu mnakwamisha mipango ya maskini, \q2 bali Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio lao. \b \q1 \v 7 Laiti wokovu wa Israeli \q2 ungekuja kutoka Sayuni! \q1 Mwenyezi Mungu anaporejesha \q2 wafungwa wa watu wake, \q1 Yakobo na ashangilie, \q2 Israeli na afurahi! \c 15 \cl Zaburi 15 \s1 Kitu Mwenyezi Mungu anachotaka \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaa \q2 katika Hekalu lako? \q1 Nani awezaye kuishi \q2 katika mlima wako mtakatifu? \b \q1 \v 2 Ni yule aendaye pasipo mawaa, \q2 atendaye yaliyo haki, \q1 asemaye kweli toka moyoni mwake, \q2 \v 3 na hana masingizio ulimini mwake, \q1 asiyemtenda jirani yake vibaya, \q2 na asiyemsingizia mwenzake, \q1 \v 4 ambaye humdharau mtu mbaya, \q2 lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu, \q1 yule atunzaye kiapo chake \q2 hata kama anaumia. \q1 \v 5 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, \q2 na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. \b \q1 Mtu afanyaye haya \q2 kamwe hatatikisika. \c 16 \cl Zaburi 16 \s1 Sala ya matumaini \d Utenzi wa Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, uniweke salama, \q2 kwa maana kwako nimekimbilia. \b \q1 \v 2 Nilimwambia Mwenyezi Mungu, “Wewe ndiwe Bwana wangu; \q2 pasipo wewe sina jambo jema.” \q1 \v 3 Kuhusu watakatifu walio duniani, \q2 hao ndio wenye fahari, \q2 na ninapendezwa nao. \q1 \v 4 Huzuni itaongezeka kwa wale \q2 wanaokimbilia miungu mingine. \q1 Sitazimimina sadaka za damu kwa miungu kama hiyo, \q2 au kutaja majina yao mdomoni mwangu. \b \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu umeniwekea fungu langu na kikombe changu; \q2 umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. \q1 \v 6 Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, \q2 hakika nimepata urithi mzuri. \b \q1 \v 7 Nitamsifu Mwenyezi Mungu ambaye hunishauri, \q2 hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha. \q1 \v 8 Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima. \q2 Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, \q2 sitatikisika. \b \q1 \v 9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, \q2 na ulimi wangu unashangilia; \q1 mwili wangu nao \q2 utapumzika salama, \q1 \v 10 kwa maana hutaniacha Kuzimu\f + \fr 16:10 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f*, \q2 wala hutamwacha Mtakatifu Wako \q2 kuona uharibifu. \q1 \v 11 Umenijulisha njia ya uzima; \q2 utanijaza na furaha mbele zako, \q1 pamoja na furaha ya milele \q2 katika mkono wako wa kuume. \c 17 \cl Zaburi 17 \s1 Sala ya mtu asiye na hatia \d Sala ya Daudi. \q1 \v 1 Sikia, Ee Mwenyezi Mungu, kusihi kwangu kwa haki, \q2 sikiliza kilio changu. \q1 Tega sikio kwa ombi langu, \q2 halitoki katika midomo ya udanganyifu. \q1 \v 2 Hukumu yangu na itoke kwako, \q2 macho yako na yaone yale yaliyo haki. \b \q1 \v 3 Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, \q2 ingawa umenijaribu, hutaona chochote. \q1 Nimeamua kwamba kinywa changu \q2 hakitatenda dhambi. \q1 \v 4 Kuhusu matendo ya wanadamu: \q2 kwa neno la midomo yako, \q2 nimejiepusha na njia za wenye jeuri. \q1 \v 5 Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; \q2 nyayo zangu hazikuteleza. \b \q1 \v 6 Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, \q2 nitegee sikio lako na usikie ombi langu. \q1 \v 7 Uoneshe ajabu ya upendo wako mkuu, \q2 wewe unayeokoa kwa mkono wako wa kuume \q2 wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao. \q1 \v 8 Nilinde kama mboni ya jicho lako, \q2 unifiche chini ya kivuli cha mabawa yako \q1 \v 9 kutokana na waovu wanaonishambulia, \q2 kutokana na adui wauaji wanaonizunguka. \b \q1 \v 10 Huifunga mioyo yao iliyo migumu, \q2 vinywa vyao hunena kwa majivuno. \q1 \v 11 Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, \q2 wakiwa macho, waniangushe chini. \q1 \v 12 Wamefanana na simba mwenye njaa anayewinda, \q2 kama simba mkubwa anayenyemelea mafichoni. \b \q1 \v 13 Inuka, Ee Mwenyezi Mungu, pambana nao, uwaangushe, \q2 niokoe kwa upanga wako kutoka kwa waovu. \q1 \v 14 Ee Mwenyezi Mungu, mkono wako uniokoe na watu kama hawa, \q2 kutokana na watu wa ulimwengu huu \q2 ambao fungu lao liko katika maisha haya. \b \q1 Na wapate adhabu ya kuwatosha. \q2 Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, \q2 hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. \q1 \v 15 Bali mimi nitauona uso wako katika haki; \q2 niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako. \c 18 \cl Zaburi 18 \s1 Wimbo wa Daudi wa ushindi \r (2 Samweli 22:1-51) \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliyomwimbia Mwenyezi Mungu alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Alisema hivi: \q1 \v 1 Nakupenda wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 nguvu yangu. \b \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu ni mwamba wangu, \q2 ngome yangu na mwokozi wangu; \q1 Mungu wangu ni mwamba wangu, \q2 ninayemkimbilia. \q1 Yeye ni ngao yangu na pembe\f + \fr 18:2 \fr*\fq pembe \fq*\ft inamaanisha nguvu\ft*\f* ya wokovu wangu, \q2 ngome yangu. \q1 \v 3 Ninamwita Mwenyezi Mungu anayestahili kusifiwa, \q2 nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. \b \q1 \v 4 Kamba za mauti zilinizunguka, \q2 mafuriko ya maangamizi yalinilemea. \q1 \v 5 Kamba za Kuzimu zilinizunguka, \q2 mitego ya mauti ilinikabili. \q1 \v 6 Katika shida yangu nalimwita Mwenyezi Mungu, \q2 nilimlilia Mungu wangu anisaidie. \q1 Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, \q2 kilio changu kikafika mbele zake, \q2 masikioni mwake. \b \q1 \v 7 Dunia ilitetemeka na kutikisika, \q2 misingi ya milima ikatikisika; \q2 vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. \q1 \v 8 Moshi ukapanda kutoka puani mwake, \q2 moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, \q1 makaa ya moto yanayowaka \q2 yakatoka ndani yake. \q1 \v 9 Akazipasua mbingu akashuka chini, \q2 mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. \q1 \v 10 Alipanda juu ya kerubi akaruka, \q2 akapaa juu kwa mabawa ya upepo. \q1 \v 11 Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, \q2 hema lake kumzunguka: \q2 mawingu meusi ya mvua ya angani. \q1 \v 12 Kutokana na mwanga wa uwepo wake \q2 mawingu yalisogea, \q1 ikashuka mvua ya mawe \q2 na miali ya radi. \q1 \v 13 Mwenyezi Mungu alinguruma kutoka mbinguni, \q2 sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. \q1 \v 14 Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, \q2 naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza. \q1 \v 15 Mabonde ya bahari yalifunuliwa, \q2 na misingi ya dunia ikawa wazi \q1 kwa kukaripia kwako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako. \b \q1 \v 16 Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; \q2 alinitoa kilindini cha maji makuu. \q1 \v 17 Aliniokoa kutoka adui yangu mwenye nguvu nyingi, \q2 kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. \q1 \v 18 Walinikabili siku ya msiba wangu, \q2 lakini Mwenyezi Mungu alikuwa msaada wangu. \q1 \v 19 Alinileta nje mahali penye nafasi tele, \q2 akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. \b \q1 \v 20 Mwenyezi Mungu alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; \q2 amenilipa sawasawa na usafi wa mikono yangu. \q1 \v 21 Kwa maana nimezishika njia za Mwenyezi Mungu; \q2 sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. \q1 \v 22 Sheria zake zote zi mbele yangu, \q2 wala sijayaacha maagizo yake. \q1 \v 23 Nimekuwa sina hatia mbele zake, \q2 nami nimejilinda nisitende dhambi. \q1 \v 24 Mwenyezi Mungu amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; \q2 sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake. \b \q1 \v 25 Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionesha kuwa mwaminifu, \q2 kwa asiye na hatia, unajionesha kutokuwa na hatia. \q1 \v 26 Kwa aliye mtakatifu, unajionesha kuwa mtakatifu, \q2 lakini kwa aliyepotoka, unajionesha kuwa mkaidi. \q1 \v 27 Wewe huwaokoa wanyenyekevu, \q2 lakini huwashusha wenye kiburi. \q1 \v 28 Wewe, Ee Mwenyezi Mungu, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka; \q2 Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga. \q1 \v 29 Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, \q2 nikiwa pamoja na Mungu wangu \q2 nitaweza kuruka ukuta. \b \q1 \v 30 Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, \q2 neno la Mwenyezi Mungu halina dosari. \q1 Yeye ni ngao kwa wote \q2 wanaokimbilia kwake. \q1 \v 31 Kwa maana ni nani aliye Mungu \q2 zaidi ya Mwenyezi Mungu? \q1 Ni nani aliye Mwamba \q2 isipokuwa Mungu wetu? \q1 \v 32 Mungu ndiye anivikaye nguvu \q2 na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. \q1 \v 33 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, \q2 huniwezesha kusimama mahali palipo juu. \q1 \v 34 Huifundisha mikono yangu kupigana vita; \q2 mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. \q1 \v 35 Hufanya msaada wa wokovu wako kuwa ngao yangu, \q2 nao mkono wako wa kuume hunitegemeza; \q2 msaada wako umeniinua niwe mkuu. \q1 \v 36 Huyapanua mapito yangu, \q2 ili miguu yangu isiteleze. \b \q1 \v 37 Niliwafuatia adui zangu na nikawapata, \q2 sikurudi nyuma hadi walipoangamizwa. \q1 \v 38 Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena; \q2 walianguka chini ya miguu yangu. \q1 \v 39 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; \q2 uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. \q1 \v 40 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, \q2 nami nikawaangamiza adui zangu. \q1 \v 41 Walipiga yowe, lakini hapakuwa na mtu wa kuwaokoa; \q2 walimlilia Mwenyezi Mungu, lakini hakuwajibu. \q1 \v 42 Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo; \q2 niliwamwaga nje kama tope barabarani. \b \q1 \v 43 Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu; \q2 umenifanya kiongozi wa mataifa; \q2 watu ambao sikuwajua wananitumikia. \q1 \v 44 Mara wanisikiapo hunitii, \q2 wageni hunyenyekea mbele yangu. \q1 \v 45 Wote wanalegea, \q2 wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. \b \q1 \v 46 Mwenyezi Mungu yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! \q2 Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu! \q1 \v 47 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, \q2 awatiishaye mataifa chini yangu, \q2 \v 48 aniokoaye na adui zangu. \q1 Uliniinua juu ya adui zangu; \q2 uliniokoa toka kwa watu wajeuri. \q1 \v 49 Kwa hiyo nitakusifu katika mataifa, Ee Mwenyezi Mungu; \q2 nitaliimbia sifa jina lako. \q1 \v 50 Humpa mfalme wake ushindi mkuu, \q2 huonesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, \q2 kwa Daudi na wazao wake milele. \c 19 \cl Zaburi 19 \s1 Utukufu wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, \q2 anga zahubiri kazi ya mikono yake. \q1 \v 2 Siku baada ya siku zinatoa habari, \q2 usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. \q1 \v 3 Hakuna msemo wala lugha, \q2 ambapo sauti zao hazisikiki. \q1 \v 4 Sauti yao imeenea duniani pote, \q2 nayo maneno yao yameenea \q2 hadi miisho ya ulimwengu. \b \q1 Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua, \q2 \v 5 linafanana na bwana arusi \q2 akitoka chumbani mwake, \q1 kama shujaa anavyofurahia \q2 kukamilisha kushindana kwake. \q1 \v 6 Huchomoza upande mmoja wa mbingu, \q2 na kufanya mzunguko wake \q2 hadi upande mwingine. \q2 Hakuna kilichojificha joto lake. \b \q1 \v 7 Torati ya Mwenyezi Mungu ni kamilifu, \q2 ikihuisha nafsi. \q1 Shuhuda za Mwenyezi Mungu ni za kuaminika, \q2 zikimpa mjinga hekima. \q1 \v 8 Maagizo ya Mwenyezi Mungu ni kamili, \q2 nayo hufurahisha moyo. \q1 Amri za Mwenyezi Mungu huangaza, \q2 zatia nuru machoni. \q1 \v 9 Kumcha Mwenyezi Mungu ni utakatifu, \q2 nako kwadumu milele. \q1 Amri za Mwenyezi Mungu ni za hakika, \q2 nazo zina haki. \q1 \v 10 Ni za thamani kuliko dhahabu, \q2 kuliko dhahabu iliyo safi sana, \q1 ni tamu kuliko asali, \q2 kuliko asali kutoka sega. \q1 \v 11 Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, \q2 katika kuzishika kuna thawabu kubwa. \b \q1 \v 12 Ni nani awezaye kutambua makosa yake? \q2 Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. \q1 \v 13 Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, \q2 nazo zisinitawale. \q1 Ndipo nitakapokuwa sina lawama, \q2 niwe huru na hatia kubwa. \b \q1 \v 14 Maneno ya kinywa changu \q2 na mawazo ya moyo wangu, \q1 yapate kibali mbele zako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 Mwamba wangu na Mkombozi wangu. \c 20 \cl Zaburi 20 \s1 Maombi kwa ajili ya ushindi \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki, \q2 jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako. \q1 \v 2 Na akutumie msaada kutoka patakatifu \q2 na akupatie msaada kutoka Sayuni. \q1 \v 3 Na azikumbuke dhabihu zako zote, \q2 na azikubali sadaka zako za kuteketezwa. \q1 \v 4 Na akujalie haja ya moyo wako, \q2 na aifanikishe mipango yako yote. \q1 \v 5 Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, \q2 tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. \q1 Mwenyezi Mungu na akupe haja zako zote. \b \q1 \v 6 Sasa nafahamu kuwa Mwenyezi Mungu \q2 humwokoa mpakwa mafuta wake, \q1 humjibu kutoka mbingu yake takatifu \q2 kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume. \q1 \v 7 Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, \q2 bali sisi tutalitumainia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \q1 \v 8 Wao wameshushwa chini na kuanguka, \q2 bali sisi tunainuka na kusimama imara. \b \q1 \v 9 Ee Mwenyezi Mungu, mwokoe mfalme! \q2 Tujibu tunapokuita! \c 21 \cl Zaburi 21 \s1 Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ushindi \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, mfalme huzifurahia nguvu zako. \q2 Tazama jinsi furaha yake ilivyo kuu \q2 kwa ushindi unaompa! \q1 \v 2 Umempa haja ya moyo wake \q2 na hukumzuilia maombi ya midomo yake. \q1 \v 3 Ulimkaribisha kwa baraka tele \q2 na kumvika taji la dhahabu safi kichwani pake. \q1 \v 4 Alikuomba maisha, nawe ukampa, \q2 wingi wa siku milele na milele. \q1 \v 5 Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, \q2 umeweka juu yake fahari na utukufu. \q1 \v 6 Hakika umempa baraka za milele, \q2 umemfanya awe na furaha \q2 kwa shangwe ya uwepo wako. \q1 \v 7 Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu; \q2 kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. \b \q1 \v 8 Mkono wako utawashika adui zako wote, \q2 mkono wako wa kuume utawakamata adui zako. \q1 \v 9 Wakati utajitokeza, \q2 utawafanya kama tanuru la moto. \q1 Katika ghadhabu yake Mwenyezi Mungu atawameza, \q2 moto wake utawateketeza. \q1 \v 10 Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, \q2 uzao wao kutoka wanadamu. \q1 \v 11 Ingawa watapanga mabaya dhidi yako \q2 na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa, \q1 \v 12 kwa kuwa utawafanya wakimbie \q2 utakapowalenga usoni pao \q2 kwa mshale kutoka upinde wako. \b \q1 \v 13 Ee Mwenyezi Mungu, utukuzwe katika nguvu zako, \q2 tutaimba na kusifu nguvu zako. \c 22 \cl Zaburi 22 \s1 Kilio cha uchungu na wimbo wa sifa \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri”. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? \q2 Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? \q2 Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu? \q1 \v 2 Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, \q2 hata usiku, sinyamazi. \b \q1 \v 3 Hata hivyo umesimikwa kwenye kiti cha enzi, \q2 Wewe Uliye Mtakatifu; \q2 wewe ni sifa ya Israeli.\f + \fr 22:3 \fr*\ft Tafsiri zingine zinasema \ft*\fqa uketiye juu ya sifa za Israeli.\fqa*\f* \q1 \v 4 Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, \q2 walikutumaini nawe ukawaokoa. \q1 \v 5 Walikulilia wewe na ukawaokoa, \q2 walikutegemea wewe nao hawakuaibika. \b \q1 \v 6 Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, \q2 wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau. \q1 \v 7 Wote wanaoniona wananidhihaki; \q2 wananivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao: \q1 \v 8 Wanasema, “Amtegemea Mwenyezi Mungu, \q2 basi Mwenyezi Mungu na amwokoe. \q1 Amkomboe basi, kwa maana \q2 anapendezwa naye.” \b \q1 \v 9 Hata hivyo ulinitoa tumboni, \q2 ukanifanya nikutegemee, \q1 hata nilipokuwa ninanyonya \q2 matiti ya mama yangu. \q1 \v 10 Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, \q2 toka tumboni mwa mama yangu \q2 umekuwa Mungu wangu. \q1 \v 11 Usiwe mbali nami, \q2 kwa maana shida iko karibu \q2 na hakuna wa kunisaidia. \b \q1 \v 12 Mafahali wengi wamenizunguka, \q2 mafahali wa Bashani wenye nguvu \q2 wamenizingira. \q1 \v 13 Simba wanaonguruma na kurarua mawindo \q2 wanapanua vinywa vyao dhidi yangu. \q1 \v 14 Nimemiminwa kama maji, \q2 mifupa yangu yote imeteguka viungoni. \q1 Moyo wangu umegeuka kuwa nta, \q2 umeyeyuka ndani yangu. \q1 \v 15 Nguvu zangu zimekauka kama kigae, \q2 ulimi wangu umegandamana \q2 na kaakaa la kinywa changu, \q1 kwa sababu umenilaza \q2 katika mavumbi ya kifo. \q1 \v 16 Mbwa wamenizunguka, \q2 kundi la watu waovu limenizingira; \q2 wamenidunga mikono na miguu. \q1 \v 17 Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, \q2 watu wananikodolea macho na kunisimanga. \q1 \v 18 Wanagawana nguo zangu, \q2 na vazi langu wanalipigia kura. \b \q1 \v 19 Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 usiwe mbali. \q1 Ee Nguvu yangu, \q2 uje haraka unisaidie. \q1 \v 20 Okoa maisha yangu na upanga, \q2 uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. \q1 \v 21 Niokoe kutoka kinywani mwa simba, \q2 niokoe kutoka pembe za nyati. \b \q1 \v 22 Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, \q2 katika kusanyiko nitakusifu wewe. \q1 \v 23 Ninyi ambao mnamcha Mwenyezi Mungu, msifuni! \q2 Ninyi nyote wazao wa Yakobo, mheshimuni yeye! \q2 Mcheni yeye, ninyi wazao wa Israeli! \q1 \v 24 Kwa maana hakupuuza wala kudharau \q2 mateso ya aliyeteswa; \q1 hakumficha uso wake \q2 bali alisikiliza kilio chake. \b \q1 \v 25 Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, \q2 nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanaokucha wewe. \q1 \v 26 Maskini watakula na kushiba, \q2 wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu watamsifu: \q2 mioyo yenu na iishi milele! \q1 \v 27 Miisho yote ya dunia itakumbuka \q2 na kumgeukia Mwenyezi Mungu, \q1 nazo jamaa zote za mataifa \q2 zitasujudu mbele zake, \q1 \v 28 kwa maana ufalme ni wa Mwenyezi Mungu \q2 naye huyatawala mataifa. \b \q1 \v 29 Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. \q2 Wote wanaoshuka mavumbini \q2 watapiga magoti mbele yake, \q1 wote ambao hawawezi \q2 kudumisha uhai wao. \q1 \v 30 Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; \q2 vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. \q1 \v 31 Watatangaza haki yake kwa watu \q2 ambao hawajazaliwa bado, \q2 kwa maana yeye ametenda hili. \c 23 \cl Zaburi 23 \s1 Mwenyezi Mungu mchungaji wetu \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu ndiye mchungaji wangu, \q2 sitapungukiwa na kitu. \q1 \v 2 Hunilaza katika malisho \q2 ya majani mabichi, \q1 kando ya maji matulivu huniongoza, \q2 \v 3 hunihuisha nafsi yangu. \q1 Huniongoza katika njia za haki \q2 kwa ajili ya jina lake. \q1 \v 4 Hata nikipita katikati \q2 ya bonde la uvuli wa mauti, \q1 sitaogopa mabaya, \q2 kwa maana wewe upo pamoja nami; \q1 fimbo yako na mkongojo wako \q2 vyanifariji. \b \q1 \v 5 Waandaa meza mbele yangu \q2 machoni pa adui zangu. \q1 Umenipaka mafuta kichwani pangu, \q2 kikombe changu kinafurika. \q1 \v 6 Hakika wema na upendo vitanifuata \q2 siku zote za maisha yangu, \q1 nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu \q2 milele. \c 24 \cl Zaburi 24 \s1 Mfalme mkuu \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Dunia ni mali ya Mwenyezi Mungu, na vyote vilivyomo, \q2 ulimwengu, na wote wanaoishi ndani yake, \q1 \v 2 maana aliiwekea misingi yake baharini, \q2 na kuifanya imara juu ya maji. \b \q1 \v 3 Nani awezaye kuupanda mlima wa Mwenyezi Mungu? \q2 Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? \q1 \v 4 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, \q2 yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake \q2 au kuapa kwa kitu cha uongo. \q1 \v 5 Huyo atapokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, \q2 na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. \q1 \v 6 Hiki ndicho kizazi cha wale wanaomtafuta, \q2 wale wanaoutafuta uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. \b \q1 \v 7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, \q2 inukeni enyi milango ya kale, \q2 ili mfalme wa utukufu apate kuingia. \q1 \v 8 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? \q2 Ni Mwenyezi Mungu aliye na nguvu na uweza, \q2 ni Mwenyezi Mungu aliye hodari katika vita. \q1 \v 9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, \q2 viinueni juu enyi milango ya kale, \q2 ili Mfalme wa utukufu apate kuingia. \q1 \v 10 Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? \q2 Ni Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni; \q2 yeye ndiye Mfalme wa utukufu. \c 25 \cl Zaburi 25\f + \fr 25 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Kumwomba Mwenyezi Mungu uongozi na ulinzi \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 naweka tumaini yangu. \b \q1 \v 2 Ni wewe ninayekutumainia, \q2 Usiniache niaibike, \q2 wala adui zangu wanishinde. \q1 \v 3 Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea \q2 atakayeaibishwa, \q1 bali wataaibishwa \q2 wafanyao hila bila sababu. \b \q1 \v 4 Nioneshe njia zako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 nifundishe mapito yako, \q1 \v 5 niongoze katika kweli yako na kunifundisha, \q2 kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, \q2 nalo tumaini langu liko kwako wakati wote. \q1 \v 6 Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, rehema zako kuu na upendo, \q2 kwa maana zimekuwepo tangu zamani. \q1 \v 7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu \q2 wala njia zangu za uasi, \q1 sawasawa na upendo wako unikumbuke, \q2 kwa maana wewe ni mwema, Ee Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu ni mwema na mwenye adili, \q2 kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake. \q1 \v 9 Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, \q2 naye huwafundisha njia yake. \q1 \v 10 Njia zote za Mwenyezi Mungu ni za upendo na uaminifu \q2 kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake. \q1 \v 11 Ee Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya jina lako, \q2 unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. \q1 \v 12 Ni nani basi, mtu yule anayemcha Mwenyezi Mungu? \q2 Atamfundisha katika njia \q2 atakayoichagua kwa ajili yake. \q1 \v 13 Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, \q2 nao wazao wake watairithi nchi. \q1 \v 14 Siri ya Mwenyezi Mungu iko kwa wale wamchao, \q2 yeye huwajulisha agano lake. \q1 \v 15 Macho yangu humwelekea Mwenyezi Mungu daima, \q2 kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa \q2 miguu yangu kutoka mtego. \b \q1 \v 16 Nigeukie na unihurumie, \q2 kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka. \q1 \v 17 Shida za moyo wangu zimeongezeka, \q2 niokoe katika dhiki yangu. \q1 \v 18 Uangalie mateso na shida zangu \q2 na uniondolee dhambi zangu zote. \q1 \v 19 Tazama adui zangu walivyo wengi, \q2 pia uone jinsi wanavyonichukia vikali! \q1 \v 20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe, \q2 usiniache niaibike, \q2 kwa maana nimekukimbilia wewe. \q1 \v 21 Uadilifu na uaminifu vinilinde, \q2 kwa sababu tumaini langu ni kwako, Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 22 Ee Mungu, wakomboe Israeli, \q2 katika shida zao zote! \c 26 \cl Zaburi 26 \s1 Maombi ya mtu mwema \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, nithibitishe katika haki, \q2 maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; \q1 nimemtumainia Mwenyezi Mungu \q2 bila kusitasita. \q1 \v 2 Ee Mwenyezi Mungu, unijaribu, unipime, \q2 uuchunguze moyo wangu \q2 na mawazo yangu; \q1 \v 3 kwa maana upendo wako \q2 uko mbele yangu daima, \q1 nami natembea siku zote \q2 katika kweli yako. \q1 \v 4 Siketi pamoja na watu wadanganyifu, \q2 wala siandamani na wanafiki, \q1 \v 5 ninachukia kusanyiko la watenda maovu, \q2 na ninakataa kuketi pamoja na waovu. \q1 \v 6 Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, \q2 naikaribia madhabahu yako, Ee Mwenyezi Mungu, \q1 \v 7 nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, \q2 huku nikisimulia matendo yako ya ajabu. \q1 \v 8 Ee Mwenyezi Mungu, naipenda nyumba yako unakoishi, \q2 mahali pale utukufu wako hukaa. \b \q1 \v 9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi, \q2 wala uhai wangu pamoja na wanaomwaga damu, \q1 \v 10 ambao mikononi mwao kuna mipango miovu, \q2 ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa. \q1 \v 11 Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; \q2 nikomboe na unihurumie. \b \q1 \v 12 Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; \q2 katika kusanyiko kuu nitamsifu Mwenyezi Mungu. \c 27 \cl Zaburi 27 \s1 Sala ya kusifu \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu, \q2 nimwogope nani? \q1 Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu, \q2 nimhofu nani? \q1 \v 2 Waovu watakaposogea dhidi yangu \q2 ili wale nyama yangu, \q1 adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia, \q2 watajikwaa na kuanguka. \q1 \v 3 Hata jeshi linizingire pande zote, \q2 moyo wangu hautaogopa; \q1 hata vita vitokee dhidi yangu, \q2 hata hapo nitakuwa na ujasiri. \b \q1 \v 4 Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu, \q2 hili ndilo ninalolitafuta: \q1 niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu \q2 siku zote za maisha yangu, \q1 niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu \q2 na kumtafuta hekaluni mwake. \q1 \v 5 Kwa kuwa siku ya shida, \q2 atanihifadhi salama katika maskani yake, \q1 atanificha uvulini mwa hema lake, \q2 na kuniweka juu kwenye mwamba. \q1 \v 6 Kisha kichwa changu kitainuliwa \q2 juu ya adui zangu wanaonizunguka. \q1 Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; \q2 nitamwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu. \b \q1 \v 7 Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 unihurumie na unijibu. \q1 \v 8 Moyo wangu unasema kuhusu wewe, \q2 “Utafute uso wake!” \q2 Uso wako, Mwenyezi Mungu “Nitautafuta.” \q1 \v 9 Usinifiche uso wako, \q2 usimkatae mtumishi wako kwa hasira; \q2 wewe umekuwa msaada wangu. \q1 Usinikatae wala usiniache, \q2 Ee Mungu Mwokozi wangu. \q1 \v 10 Hata baba yangu na mama yangu wakiniacha, \q2 Mwenyezi Mungu atanipokea. \q1 \v 11 Nifundishe njia yako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 niongoze katika njia iliyo nyoofu, \q2 kwa sababu ya watesi wangu. \q1 \v 12 Usiniachilie kwa nia za adui zangu, \q2 kwa maana mashahidi wa uongo \q2 wameinuka dhidi yangu, \q2 wakipumua ujeuri. \b \q1 \v 13 Nami bado nina tumaini hili: \q2 nitauona wema wa Mwenyezi Mungu \q2 katika nchi ya walio hai. \q1 \v 14 Mngojee Mwenyezi Mungu; \q2 uwe hodari na mwenye moyo mkuu, \q2 na umngojee Mwenyezi Mungu. \c 28 \cl Zaburi 28 \s1 Kuomba msaada \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ninakuita wewe, Ee Mwenyezi Mungu, Mwamba wangu; \q2 usikatae kunisikiliza. \q1 Kwa sababu ukinyamaza \q2 nitafanana na walioshuka shimoni. \q1 \v 2 Sikia kilio changu nikikuomba unihurumie, \q2 ninapokuita ili unisaidie, \q1 ninapoinua mikono yangu kuelekea \q2 Patakatifu pa Patakatifu pako. \b \q1 \v 3 Usiniburute pamoja na waovu, \q2 pamoja na hao watendao mabaya, \q1 ambao huzungumza na majirani zao maneno mazuri, \q2 lakini mioyoni mwao wameficha chuki. \q1 \v 4 Walipe sawasawa na matendo yao, \q2 sawasawa na matendo yao maovu; \q1 walipe sawasawa na kazi za mikono yao, \q2 uwalipe wanavyostahili. \q1 \v 5 Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Mwenyezi Mungu, \q2 na yale ambayo mikono yake imetenda, \q1 atawabomoa na kamwe \q2 hatawajenga tena. \b \q1 \v 6 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana amesikia kilio changu \q2 nikimwomba anihurumie. \q1 \v 7 Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu, \q2 moyo wangu umemtumaini yeye, \q2 nami nimesaidiwa. \q1 Moyo wangu unarukaruka kwa furaha \q2 nami nitamshukuru kwa wimbo. \b \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu ni nguvu ya watu wake, \q2 ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake. \q1 \v 9 Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; \q2 uwe mchungaji wao na uwabebe milele. \c 29 \cl Zaburi 29 \s1 Sauti ya Mwenyezi Mungu wakati wa dhoruba \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi mashujaa, \q2 mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu. \q1 \v 2 Mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake; \q2 mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake. \q1 \v 3 Sauti ya Mwenyezi Mungu iko juu ya maji; \q2 Mungu wa utukufu hupiga radi, \q2 Mwenyezi Mungu hupiga radi juu ya maji makuu. \b \q1 \v 4 Sauti ya Mwenyezi Mungu ina nguvu; \q2 sauti ya Mwenyezi Mungu ni tukufu. \q1 \v 5 Sauti ya Mwenyezi Mungu huvunja mierezi; \q2 Mwenyezi Mungu huvunja vipande vipande \q2 mierezi ya Lebanoni. \q1 \v 6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, \q2 Sirioni\f + \fr 29:6 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mlima Hermoni\fqa*\f* urukaruke kama mwana nyati. \q1 \v 7 Sauti ya Mwenyezi Mungu hupiga \q2 kwa miali ya radi. \q1 \v 8 Sauti ya Mwenyezi Mungu hutikisa jangwa; \q2 Mwenyezi Mungu hutikisa Jangwa la Kadeshi. \q1 \v 9 Sauti ya Mwenyezi Mungu huzalisha ayala, \q2 na huuacha msitu wazi. \q1 Hekaluni mwake wote wasema, \q2 “Utukufu!” \b \q1 \v 10 Mwenyezi Mungu huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; \q2 Mwenyezi Mungu ametawazwa kuwa Mfalme milele. \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu huwapa watu wake nguvu; \q2 Mwenyezi Mungu huwabariki watu wake kwa kuwapa amani. \c 30 \cl Zaburi 30 \s1 Maombi ya shukrani \d Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nitakutukuza wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, \q1 na hukuacha adui zangu \q2 washangilie juu yangu. \q1 \v 2 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nilikuita unisaidie \q2 na wewe umeniponya. \q1 \v 3 Ee Mwenyezi Mungu, umenitoa Kuzimu\f + \fr 30:3 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f*, \q2 umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. \b \q1 \v 4 Mwimbieni Mwenyezi Mungu, enyi watakatifu wake; \q2 lisifuni jina lake takatifu. \q1 \v 5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, \q2 bali upendo wake hudumu siku zote. \q1 Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, \q2 lakini furaha huja asubuhi. \b \q1 \v 6 Nilipofanikiwa nilisema, \q2 “Sitatikiswa kamwe.” \q1 \v 7 Ee Mwenyezi Mungu, uliponijalia, \q2 uliuimarisha mlima wangu, \q1 lakini ulipouficha uso wako \q2 nilifadhaika. \b \q1 \v 8 Kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, niliita, \q2 niliomba rehema kwa Bwana: \q1 \v 9 “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu, \q2 katika kushuka kwangu shimoni? \q1 Je, mavumbi yatakusifu? \q2 Je, yatatangaza uaminifu wako? \q1 \v 10 Ee Mwenyezi Mungu, unisikie na kunihurumia; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, uwe msaada wangu.” \b \q1 \v 11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, \q2 ulinivua gunia ukanivika shangwe, \q1 \v 12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. \q2 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakushukuru milele. \c 31 \cl Zaburi 31 \s1 Maombi na sifa kwa kuokolewa kutoka kwa adui \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, nimekukimbilia wewe, \q2 usiache nikaaibika kamwe, \q2 kwa haki yako uniokoe. \q1 \v 2 Nitegee sikio lako, \q2 uje uniokoe haraka; \q1 uwe kwangu mwamba wa kimbilio, \q2 ngome imara ya kuniokoa. \q1 \v 3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, \q2 uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako. \q1 \v 4 Uniepushe na mtego niliotegewa, \q2 maana wewe ndiwe kimbilio langu. \q1 \v 5 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, \q2 unikomboe Ee Mwenyezi Mungu, uliye Mungu wa kweli. \b \q1 \v 6 Ninawachukia wale wanaoshikilia sanamu batili; \q2 bali mimi ninamtumaini Mwenyezi Mungu. \q1 \v 7 Nitafurahia na kushangilia upendo wako, \q2 kwa kuwa uliona mateso yangu \q2 na ulijua maumivu ya nafsi yangu. \q1 \v 8 Hukunikabidhi kwa adui yangu \q2 bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi. \b \q1 \v 9 Ee Mwenyezi Mungu unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; \q2 macho yangu yanafifia kwa huzuni, \q2 nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. \q1 \v 10 Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, \q2 naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; \q1 nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, \q2 na mifupa yangu inachakaa. \q1 \v 11 Kwa sababu ya adui zangu wote, \q2 nimedharauliwa kabisa na majirani zangu, \q1 hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, \q2 wale wanaoniona barabarani wananikimbia. \q1 \v 12 Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa, \q2 nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika. \q1 \v 13 Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; \q2 vitisho viko pande zote; \q1 kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, \q2 na kula njama kuniua. \b \q1 \v 14 Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu; \q2 nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” \q1 \v 15 Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, \q2 uniokoe mikononi mwa adui zangu \q2 na wale wanifuatiao. \q1 \v 16 Mwangazie mtumishi wako uso wako, \q2 uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma. \q1 \v 17 Usiniache niaibike, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana nimekulilia wewe, \q1 bali waovu waaibishwe \q2 na kunyamazishwa Kuzimu. \q1 \v 18 Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, \q2 kwa maana kwa kiburi na dharau \q1 wao husema kwa majivuno \q2 dhidi ya wenye haki. \b \q1 \v 19 Tazama jinsi wema wako ulivyo mkuu, \q2 uliowawekea akiba wanaokucha, \q1 unaowapa wale wanaokukimbilia \q2 machoni pa watu wote. \q1 \v 20 Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako \q2 kutokana na hila za wanadamu; \q1 katika makao yako huwaweka salama \q2 kutokana na ndimi za mashtaka. \b \q1 \v 21 Atukuzwe Mwenyezi Mungu, \q2 kwa kuwa amenionesha upendo wake wa ajabu \q2 nilipokuwa katika mji uliozingirwa. \q1 \v 22 Katika hofu yangu nilisema, \q2 “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” \q1 Hata hivyo ulisikia kilio changu \q2 ukanihurumia nilipokuita unisaidie. \b \q1 \v 23 Mpendeni Mwenyezi Mungu ninyi watakatifu wake wote! \q2 Mwenyezi Mungu huwahifadhi waaminifu, \q2 lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu. \q1 \v 24 Kuweni hodari na mjipe moyo, \q2 ninyi nyote mnaomtumaini Mwenyezi Mungu. \c 32 \cl Zaburi 32 \s1 Furaha ya msamaha \d Zaburi ya Daudi. Funzo. \q1 \v 1 Heri mtu aliyesamehewa makosa yake, \q2 ambaye dhambi zake zimefunikwa. \q1 \v 2 Heri mtu yule ambaye Mwenyezi Mungu \q2 hamhesabii dhambi, \q1 na ambaye rohoni mwake \q2 hamna udanganyifu. \b \q1 \v 3 Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa \q2 kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa. \q1 \v 4 Usiku na mchana \q2 mkono wako ulinilemea, \q1 nguvu zangu zilinyonywa \q2 kama vile katika joto la kiangazi. \q1 \v 5 Kisha nikakiri dhambi yangu kwako, \q2 wala sikuficha uovu wangu. \q1 Nilisema, “Nitaungama \q2 makosa yangu kwa Mwenyezi Mungu.” \q1 Ndipo uliponisamehe \q2 hatia ya dhambi yangu. \b \q1 \v 6 Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe \q2 wakati unapopatikana, \q1 hakika maji makuu yatakapofurika \q2 hayatamfikia yeye. \q1 \v 7 Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, \q2 utaniepusha na taabu \q2 na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. \b \q1 \v 8 Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; \q2 nitakushauri na kukuangalia. \q1 \v 9 Usiwe kama farasi au nyumbu \q2 wasio na akili, \q1 ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu \q2 la sivyo hawatakukaribia. \q1 \v 10 Mtu mwovu ana taabu nyingi, \q2 bali upendo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu \q2 unamzunguka mtu anayemtumaini. \b \q1 \v 11 Shangilieni katika Mwenyezi Mungu na mfurahi, enyi wenye haki! \q2 Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo! \c 33 \cl Zaburi 33 \s1 Ukuu na wema wa Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa furaha, enyi wenye haki; \q2 wanyofu wa moyo wanapaswa kumsifu. \q1 \v 2 Msifuni Mwenyezi Mungu kwa kinubi, \q2 mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. \q1 \v 3 Mwimbieni wimbo mpya; \q2 pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe. \b \q1 \v 4 Maana neno la Mwenyezi Mungu ni haki na kweli, \q2 ni mwaminifu kwa yote atendayo. \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu hupenda uadilifu na haki; \q2 dunia imejaa upendo wake usiokoma. \b \q1 \v 6 Kwa neno la Mwenyezi Mungu mbingu ziliumbwa, \q2 jeshi lao la angani likaumbwa \q2 kwa pumzi ya kinywa chake. \q1 \v 7 Anayakusanya maji ya bahari \q2 kama kwenye chungu; \q1 vilindi vya bahari \q2 anaviweka katika ghala. \q1 \v 8 Dunia yote na imwogope Mwenyezi Mungu, \q2 watu wote wa dunia wamche. \q1 \v 9 Kwa maana Mungu alisema, na ikawa, \q2 aliamuru na ikasimama imara. \q1 \v 10 Mwenyezi Mungu huzuia mipango ya mataifa, \q2 hupinga makusudi ya mataifa. \q1 \v 11 Lakini mipango ya Mwenyezi Mungu inasimama imara milele, \q2 makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote. \b \q1 \v 12 Heri taifa ambalo Mwenyezi Mungu ni Mungu wao, \q2 watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake. \q1 \v 13 Mwenyezi Mungu hutazama chini kutoka mbinguni \q2 na kuwaona wanadamu wote; \q1 \v 14 kutoka maskani mwake huwaangalia \q2 wote wanaoishi duniani: \q1 \v 15 yeye ambaye huumba mioyo yao wote, \q2 ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda. \q1 \v 16 Hakuna mfalme anayeokoka kwa ukubwa wa jeshi lake; \q2 hakuna shujaa anayeokoka kwa wingi wa nguvu zake. \q1 \v 17 Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu, \q2 licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa. \q1 \v 18 Lakini macho ya Mwenyezi Mungu yako kwa wale wamchao, \q2 kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo, \q1 \v 19 ili awaokoe na mauti, \q2 na kuwahifadhi wakati wa njaa. \b \q1 \v 20 Sisi tunamngojea Mwenyezi Mungu kwa matumaini, \q2 yeye ni msaada wetu na ngao yetu. \q1 \v 21 Mioyo yetu humshangilia, \q2 kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. \q1 \v 22 Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 tunapoliweka tumaini letu kwako. \c 34 \cl Zaburi 34\f + \fr 34 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Sifa na wema wa Mwenyezi Mungu \d Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. \q1 \v 1 Nitamtukuza Mwenyezi Mungu nyakati zote, \q2 sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu siku zote. \q1 \v 2 Nafsi yangu itajisifu katika Mwenyezi Mungu, \q2 walioonewa watasikia na wafurahi. \q1 \v 3 Mtukuzeni Mwenyezi Mungu pamoja nami, \q2 naam, na tulitukuze jina lake pamoja. \b \q1 \v 4 Nilimtafuta Mwenyezi Mungu naye akanijibu, \q2 akaniokoa kwenye hofu zangu zote. \q1 \v 5 Wale wamtazamao hutiwa nuru, \q2 nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. \q1 \v 6 Maskini huyu alimwita Mwenyezi Mungu, naye akamsikia, \q2 akamwokoa katika taabu zake zote. \q1 \v 7 Malaika wa Mwenyezi Mungu hufanya kituo \q2 akiwazunguka wale wamchao, \q2 naye huwaokoa. \b \q1 \v 8 Onjeni mwone kwamba Mwenyezi Mungu ni mwema; \q2 heri mtu yule anayemkimbilia. \q1 \v 9 Mcheni Mwenyezi Mungu enyi watakatifu wake, \q2 kwa maana wale wamchao \q2 hawapungukiwi na chochote. \q1 \v 10 Wana simba wenye nguvu \q2 hutindikiwa na kuona njaa, \q1 bali wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu \q2 hawatakosa kitu chochote kilicho chema. \b \q1 \v 11 Njooni, watoto wangu, mnisikilize, \q2 nitawafundisha kumcha Mwenyezi Mungu. \q1 \v 12 Yeyote kati yenu anayependa uzima \q2 na kutamani kuziona siku nyingi njema, \q1 \v 13 basi auzuie ulimi wake na mabaya, \q2 na midomo yake kutokana na kusema uongo. \q1 \v 14 Aache uovu, atende mema, \q2 aitafute amani na kuifuatilia. \b \q1 \v 15 Macho ya Mwenyezi Mungu huwaelekea wenye haki, \q2 na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao. \q1 \v 16 Uso wa Mwenyezi Mungu uko kinyume na watendao maovu, \q2 ili kufuta kumbukumbu lao duniani. \b \q1 \v 17 Wenye haki hulia, naye Mwenyezi Mungu huwasikia, \q2 huwaokoa katika taabu zao zote. \q1 \v 18 Mwenyezi Mungu yu karibu na waliovunjika moyo, \q2 na huwaokoa waliopondeka roho. \b \q1 \v 19 Mwenye haki ana mateso mengi, \q2 lakini Mwenyezi Mungu humwokoa nayo yote, \q1 \v 20 huhifadhi mifupa yake yote, \q2 hata mmoja hautavunjika. \b \q1 \v 21 Ubaya utamuua mtu mwovu, \q2 nao adui za mwenye haki watahukumiwa. \q1 \v 22 Mwenyezi Mungu huwakomboa watumishi wake, \q2 yeyote anayemkimbilia yeye \q2 hatahukumiwa kamwe. \c 35 \cl Zaburi 35 \s1 Kuomba msaada: Kuokolewa kutokana na adui \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, pingana na wale wanaopingana nami, \q2 upigane na hao wanaopigana nami. \q1 \v 2 Chukua ngao na kigao. \q2 Inuka unisaidie. \q1 \v 3 Inua mkuki wako na fumo\f + \fr 35:3 \fr*\ft Fumo ni sawa na sagai, yaani mkuki mfupi.\ft*\f* lako \q2 dhidi ya hao wanaonifuatia. \q1 Iambie nafsi yangu, \q2 “Mimi ni wokovu wako.” \b \q1 \v 4 Wafedheheshwe na waaibishwe \q2 wale wanaotafuta uhai wangu. \q1 Wanaofanya shauri kuniangamiza \q2 wafukuzwe mbali kwa bumbuazi. \q1 \v 5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo, \q2 malaika wa Mwenyezi Mungu akiwafukuza. \q1 \v 6 Njia yao na iwe giza na ya utelezi, \q2 malaika wa Mwenyezi Mungu akiwafuatilia. \q1 \v 7 Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu, \q2 na bila sababu wamenichimbia shimo, \q1 \v 8 maafa na yawapate ghafula: \q2 wavu walionifichia na uwatege wenyewe, \q1 na waanguke katika shimo hilo, \q2 kwa maangamizi yao. \q1 \v 9 Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Mwenyezi Mungu \q2 na kuufurahia wokovu wake. \q1 \v 10 Nitapaza sauti yangu nikisema, \q2 “Ni nani aliye kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu? \q1 Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale waliowazidi nguvu, \q2 unawaokoa maskini na wahitaji kutokana na wanaowanyang’anya!” \b \q1 \v 11 Mashahidi wakatili wanainuka, \q2 wananiuliza mambo nisiyoyajua. \q1 \v 12 Wananilipa baya kwa jema \q2 na kuiacha nafsi yangu ukiwa. \q1 \v 13 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa gunia \q2 na nikajinyenyekeza kwa kufunga. \q1 Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa, \q2 \v 14 niliendelea kuomboleza \q2 kama vile wao ni rafiki au ndugu. \q1 Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni \q2 kama ninayemwombolezea mama yangu. \q1 \v 15 Lakini nilipojikwaa, \q2 walikusanyika kwa shangwe; \q1 washambuliaji walijikusanya dhidi yangu \q2 bila mimi kujua. \q2 Walinisingizia pasipo kukoma. \q1 \v 16 Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki, \q2 wamenisagia meno. \q1 \v 17 Ee Bwana, utatazama hadi lini? \q2 Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, \q1 okoa uhai wangu wa thamani \q2 kutokana na simba hawa. \q1 \v 18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, \q2 nitakusifu katikati ya watu wengi. \b \q1 \v 19 Usiwaache wale wanaonisimanga, \q2 wale ambao ni adui zangu bila sababu; \q1 usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu \q2 wakonyeze jicho kwa hila. \q1 \v 20 Hawazungumzi kwa amani, \q2 bali wanatunga mashtaka ya uongo \q1 dhidi ya wale wanaoishi \q2 kwa utulivu katika nchi. \q1 \v 21 Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha! \q2 Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.” \b \q1 \v 22 Ee Mwenyezi Mungu, umeona hili, usiwe kimya. \q2 Usiwe mbali nami, Ee Bwana. \q1 \v 23 Amka, inuka unitetee! \q2 Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu. \q1 \v 24 Nihukumu kwa haki yako, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, \q2 sawasawa na haki yako; \q2 usiwaache wakusimange. \q1 \v 25 Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” \q2 Au waseme, “Tumemmeza.” \b \q1 \v 26 Wote wanaofurahia dhiki yangu \q2 waaibishwe na wachanganyikiwe; \q1 hao wanaojiinua dhidi yangu \q2 wavikwe aibu na dharau. \q1 \v 27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki \q2 wapige kelele za shangwe na furaha; \q1 hebu waseme siku zote, “Mwenyezi Mungu atukuzwe, \q2 ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.” \q1 \v 28 Ulimi wangu utanena haki yako \q2 na sifa zako mchana kutwa. \c 36 \cl Zaburi 36 \s1 Uovu wa mwanadamu \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Mwenyezi Mungu. \q1 \v 1 Kuna neno moyoni mwangu \q2 kutoka kwa Mungu \q2 kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. \q1 Hakuna hofu ya Mungu \q2 mbele ya macho yake. \q1 \v 2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno \q2 hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. \q1 \v 3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, \q2 ameacha kuwa mwenye hekima au kutenda mema. \q1 \v 4 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, \q2 hujitia katika njia ya dhambi \q2 na hakatai lililo baya. \b \q1 \v 5 Upendo wako, Ee Mwenyezi Mungu, unafika hadi mbinguni, \q2 uaminifu wako hadi kwenye anga. \q1 \v 6 Haki yako ni kama milima mikubwa, \q2 hukumu zako ni kama kilindi kikuu. \q1 Ee Mwenyezi Mungu, wewe huwahifadhi \q2 mwanadamu na mnyama. \q1 \v 7 Upendo wako usiokoma \q2 ni wa thamani mno! \q1 Watu wakuu na wadogo \q2 hujificha uvulini wa mabawa yako. \q1 \v 8 Wanajifurahisha katika wingi ulio nyumbani mwako, \q2 nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. \q1 \v 9 Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, \q2 katika nuru yako twaona nuru. \b \q1 \v 10 Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, \q2 haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. \q1 \v 11 Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, \q2 wala mkono wa mwovu usinifukuze. \q1 \v 12 Tazama jinsi watenda maovu walivyoanguka: \q2 wametupwa chini, hawawezi kuinuka! \c 37 \cl Zaburi 37\f + \fr 37 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Mwisho wa mwovu na urithi wa mwenye haki \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, \q2 wala usiwaonee wivu watendao mabaya, \q1 \v 2 kwa maana watanyauka upesi kama majani, \q2 watakufa upesi kama mimea ya kijani. \b \q1 \v 3 Mtumaini Mwenyezi Mungu na utende yaliyo mema. \q2 Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. \q1 \v 4 Jifurahishe katika Mwenyezi Mungu \q2 naye atakupa haja za moyo wako. \b \q1 \v 5 Mkabidhi Mwenyezi Mungu njia yako, \q2 mtumaini yeye, naye atatenda hili: \q1 \v 6 Yeye atafanya haki yako ing’ae kama mapambazuko, \q2 na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri. \b \q1 \v 7 Tulia mbele za Mwenyezi Mungu \q2 na umngojee kwa uvumilivu; \q1 usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, \q2 wanapotekeleza mipango yao miovu. \b \q1 \v 8 Epuka hasira na uache ghadhabu; \q2 usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. \q1 \v 9 Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, \q2 bali wale wanaomtumaini Mwenyezi Mungu watairithi nchi. \b \q1 \v 10 Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, \q2 ingawa utawatafuta, hawataonekana. \q1 \v 11 Bali wanyenyekevu watairithi nchi \q2 na wafurahie amani tele. \b \q1 \v 12 Waovu hula njama dhidi ya wenye haki \q2 na kuwasagia meno, \q1 \v 13 bali Bwana huwacheka waovu, \q2 kwa sababu anajua siku yao inakuja. \b \q1 \v 14 Waovu hufuta upanga \q2 na kupinda upinde, \q1 ili wawaangushe maskini na wahitaji, \q2 kuwaua wale ambao njia zao ni nyofu. \q1 \v 15 Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, \q2 na pinde zao zitavunjwa. \b \q1 \v 16 Bora kidogo walicho nacho wenye haki \q2 kuliko wingi wa mali ya waovu wengi; \q1 \v 17 kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, \q2 lakini Mwenyezi Mungu humtegemeza mwenye haki. \b \q1 \v 18 Mwenyezi Mungu anazifahamu siku za wanyofu, \q2 na urithi wao utadumu milele. \q1 \v 19 Siku za maafa hawatanyauka, \q2 siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. \b \q1 \v 20 Lakini waovu wataangamia: \q2 Adui za Mwenyezi Mungu watakuwa \q2 kama uzuri wa mashamba, \q1 watatoweka, \q2 watatoweka kama moshi. \b \q1 \v 21 Waovu hukopa na hawalipi, \q2 bali wenye haki hutoa kwa ukarimu. \q1 \v 22 Wale wanaobarikiwa na Mwenyezi Mungu watairithi nchi, \q2 bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali. \b \q1 \v 23 Kama Mwenyezi Mungu akipendezwa na njia ya mtu, \q2 yeye huimarisha hatua zake, \q1 \v 24 ajapojikwaa, hataanguka, \q2 kwa maana Mwenyezi Mungu \q2 humtegemeza kwa mkono wake. \b \q1 \v 25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, \q2 lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa \q2 au watoto wao wakiombaomba chakula. \q1 \v 26 Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. \q2 Watoto wao watabarikiwa. \b \q1 \v 27 Acha ubaya na utende wema, \q2 nawe utaishi katika nchi milele. \q1 \v 28 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki \q2 naye hatawaacha waaminifu wake. \b \q1 Watalindwa milele, \q2 lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali. \q1 \v 29 Wenye haki watairithi nchi, \q2 na kuishi humo milele. \b \q1 \v 30 Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, \q2 nao ulimi wake huzungumza lililo haki. \q1 \v 31 Torati ya Mungu wake imo moyoni mwake; \q2 nyayo zake hazitelezi. \b \q1 \v 32 Watu waovu huvizia wenye haki, \q2 wakitafuta kuwaua; \q1 \v 33 lakini Mwenyezi Mungu hatawaacha mikononi mwao \q2 wala hatawaacha wahukumiwe \q2 kuwa wakosa wanaposhtakiwa. \b \q1 \v 34 Mngojee Mwenyezi Mungu, \q2 na uishike njia yake. \q1 Naye atakutukuza uirithi nchi, \q2 waovu watakapokatiliwa mbali, \q2 utaliona hilo. \b \q1 \v 35 Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi \q2 kama mwerezi wa Lebanoni, \q1 \v 36 lakini alitoweka upesi na hakuonekana, \q2 ingawa nilimtafuta, hakupatikana. \b \q1 \v 37 Watafakari watu wasio na hatia, \q2 wachunguze watu wakamilifu, \q2 kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani. \q1 \v 38 Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, \q2 mafanikio yao yatakatiliwa mbali. \b \q1 \v 39 Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Mwenyezi Mungu, \q2 yeye ni ngome yao wakati wa shida. \q1 \v 40 Mwenyezi Mungu huwasaidia na kuwaokoa, \q2 huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, \q2 kwa maana wanamkimbilia. \c 38 \cl Zaburi 38 \s1 Maombi ya mtu anayeteseka \d Zaburi ya Daudi. Maombi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako, \q2 wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. \q1 \v 2 Kwa kuwa mishale yako imenichoma, \q2 na mkono wako umenipiga. \q1 \v 3 Hakuna afya mwilini mwangu \q2 kwa sababu ya ghadhabu yako, \q1 mifupa yangu haina uzima \q2 kwa sababu ya dhambi zangu. \q1 \v 4 Maovu yangu yamenifunika \q2 kama mzigo mzito mno. \b \q1 \v 5 Majeraha yangu yameoza na yananuka, \q2 kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. \q1 \v 6 Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, \q2 mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. \q1 \v 7 Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, \q2 hakuna afya mwilini mwangu. \q1 \v 8 Nimedhoofika na kupondwa kabisa, \q2 nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. \b \q1 \v 9 Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku \q2 yako wazi mbele zako, \q1 kutamani kwangu sana \q2 hakufichiki mbele zako. \q1 \v 10 Moyo wangu unapigapiga, \q2 nguvu zangu zimeniishia; \q2 hata macho yangu yametiwa giza. \q1 \v 11 Rafiki na wenzangu wananikwepa \q2 kwa sababu ya majeraha yangu; \q2 majirani wangu wanakaa mbali nami. \q1 \v 12 Wale wanaotafuta uhai wangu \q2 wanatega mitego yao, \q1 wale ambao wangetaka kunidhuru \q2 huongea kuhusu maangamizi yangu; \q2 hupanga hila mchana kutwa. \b \q1 \v 13 Mimi ni kama kiziwi, asiyeweza kusikia, \q2 ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake; \q1 \v 14 nimekuwa kama mtu asiyesikia, \q2 ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. \q1 \v 15 Ee Mwenyezi Mungu, ninakungojea wewe, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, utajibu. \q1 \v 16 Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, \q2 wala wajitukuze juu yangu \q2 mguu wangu unapoteleza.” \b \q1 \v 17 Kwa maana ninakaribia kuanguka, \q2 na maumivu yangu yananiandama siku zote. \q1 \v 18 Naungama uovu wangu, \q2 ninataabishwa na dhambi yangu. \q1 \v 19 Wengi wamekua adui zangu bila sababu; \q2 wale wanaonichukia bure ni wengi. \q1 \v 20 Wanaolipa wema wangu kwa maovu \q2 hunisingizia ninapofuata lililo jema. \b \q1 \v 21 Ee Mwenyezi Mungu, usiniache, \q2 usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. \q1 \v 22 Ee Bwana Mwokozi wangu, \q2 uje upesi kunisaidia. \c 39 \cl Zaburi 39 \s1 Maombi ya mtu mwenye uchungu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu \q2 na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; \q1 nitaweka lijamu kinywani mwangu \q2 wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” \q1 \v 2 Lakini niliponyamaza na kutulia, \q2 hata pasipo kusema lolote jema, \q2 uchungu wangu uliongezeka. \q1 \v 3 Moyo wangu ulipata moto ndani yangu, \q2 nilipotafakari, moto uliwaka, \q2 ndipo nikasema kwa ulimi wangu: \b \q1 \v 4 “Ee Mwenyezi Mungu, nijulishe mwisho wa maisha yangu \q2 na hesabu ya siku zangu; \q1 nijalie kujua jinsi maisha yangu \q2 yanavyopita upesi. \q1 \v 5 Umefanya maisha yangu mafupi kama nyanda; \q2 muda wangu wa kuishi ni kama \q2 hauna thamani kwako. \q1 Maisha ya kila mwanadamu \q2 ni kama pumzi. \q1 \v 6 Hakika kila binadamu ni kama njozi \q2 aendapo huku na huko: \q1 hujishughulisha na mengi, lakini ni ubatili; \q2 anakusanya mali nyingi, \q2 wala hajui ni nani atakayejifaidi nayo. \b \q1 \v 7 “Lakini sasa Bwana, nitafute nini? \q2 Tumaini langu ni kwako. \q1 \v 8 Niokoe kutoka makosa yangu yote, \q2 usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu. \q1 \v 9 Nilinyamaza, sikufumbua kinywa changu, \q2 kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili. \q1 \v 10 Niondolee mjeledi wako, \q2 nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako. \q1 \v 11 Unakemea na kuadhibu wanadamu \q2 kwa ajili ya dhambi zao; \q1 unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: \q2 kila mwanadamu ni kama pumzi tu. \b \q1 \v 12 “Ee Mwenyezi Mungu, usikie maombi yangu, \q2 usikie kilio changu unisaidie, \q2 usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. \q1 Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, \q2 mhamiaji, kama walivyokuwa baba zangu wote, \q1 \v 13 Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena \q2 kabla sijaondoka na nisiwepo tena.” \c 40 \cl Zaburi 40 \s1 Wimbo wa sifa \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nilimngoja Mwenyezi Mungu kwa saburi, \q2 naye akanijia na kusikia kilio changu. \q1 \v 2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, \q2 kutoka matope na utelezi; \q1 akaiweka miguu yangu juu ya mwamba \q2 na kunipa mahali imara pa kusimama. \q1 \v 3 Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, \q2 wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. \q1 Wengi wataona na kuogopa \q2 na kuweka tumaini lao kwa Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 4 Heri mtu yule amfanyaye Mwenyezi Mungu kuwa tumaini lake, \q2 asiyewategemea wenye kiburi, \q2 wale wenye kugeukia miungu ya uongo. \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, \q2 umefanya mambo mengi ya ajabu. \q1 Mambo uliyopanga kwa ajili yetu \q2 hakuna awezaye kukuhesabia; \q1 kama ningesema na kuyaelezea, \q2 yangekuwa mengi mno kuyatangaza. \b \q1 \v 6 Dhabihu na sadaka hukuvitaka, \q2 lakini umefungua masikio yangu\f + \fr 40:6 \fr*\ft au \ft*\fqa bali mwili uliniandalia\fqa*\f*; \q1 sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi \q2 hukuzihitaji. \q1 \v 7 Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: \q2 imeandikwa kunihusu katika kitabu. \q1 \v 8 Ee Mungu wangu, \q2 natamani kuyafanya mapenzi yako; \q2 sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” \b \q1 \v 9 Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, \q2 sikufunga mdomo wangu, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, kama ujuavyo. \q1 \v 10 Sikuficha haki yako moyoni mwangu; \q2 ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. \q1 Sikuficha upendo wako na kweli yako \q2 mbele ya kusanyiko kubwa. \b \q1 \v 11 Ee Mwenyezi Mungu, usinizuilie huruma zako, \q2 upendo wako na kweli yako daima vinilinde. \q1 \v 12 Kwa maana taabu zisizohesabika zimenizunguka, \q2 dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. \q1 Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, \q2 nao moyo unazimia ndani yangu. \b \q1 \v 13 Ee Mwenyezi Mungu, uwe radhi kuniokoa; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie. \q1 \v 14 Wote wanaotafuta kuniua, \q2 waaibishwe na kufadhaishwa; \q1 wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, \q2 wafukuzwe mbali kwa aibu. \q1 \v 15 Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!” \q2 wafadhaishwe na iwe aibu yao. \q1 \v 16 Lakini wote wanaokutafuta \q2 washangilie na kukufurahia, \q1 wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, \q2 “Mwenyezi Mungu atukuzwe!” \b \q1 \v 17 Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji; \q2 Bwana na anifikirie. \q1 Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu; \q2 Ee Mungu wangu, usikawie. \c 41 \cl Zaburi 41 \s1 Maombi ya mtu mgonjwa \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Heri mtu yule anayemjali mnyonge, \q2 Mwenyezi Mungu atamwokoa wakati wa shida. \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, \q2 atambariki katika nchi \q2 na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. \q1 \v 3 Mwenyezi Mungu atamtegemeza akiwa mgonjwa kitandani, \q2 na atamwinua kutoka kitandani mwake. \b \q1 \v 4 Nilisema, “Ee Mwenyezi Mungu nihurumie, \q2 niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” \q1 \v 5 Adui zangu wanasema kwa hila, \q2 “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.” \q1 \v 6 Kila anapokuja mtu kunitazama, \q2 huzungumza uongo, \q1 huku moyo wake ukikusanya masingizio; \q2 kisha huondoka na kuyasambaza. \b \q1 \v 7 Adui zangu wote hunong’onezana dhidi yangu, \q2 hao huniwazia mabaya sana, wakisema, \q1 \v 8 “Ugonjwa mbaya sana umempata, \q2 kamwe hatainuka tena kitandani mwake.” \q1 \v 9 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, \q2 yule aliyekula chakula changu \q2 ameniinulia kisigino chake. \b \q1 \v 10 Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, nihurumie, \q2 ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi. \q1 \v 11 Najua kwamba wapendezwa nami, \q2 kwa kuwa adui yangu hanishindi. \q1 \v 12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza \q2 na kuniweka kwenye uwepo wako milele. \b \b \q1 \v 13 Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, \q2 tangu milele na hata milele. \qc Amen na Amen. \c 42 \ms Kitabu cha Pili \mr (Zaburi 42–72) \cl Zaburi 42 \s1 Maombi ya mtu aliye uhamishoni \d Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. \q1 \v 1 Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji, \q2 ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu. \q1 \v 2 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. \q2 Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? \q1 \v 3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu \q2 usiku na mchana, \q1 huku watu wakiniambia mchana kutwa, \q2 “Yuko wapi Mungu wako?” \q1 \v 4 Mambo haya nayakumbuka \q2 ninapoimimina nafsi yangu: \q1 Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, \q2 nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, \q1 kwa kelele za shangwe na za shukrani \q2 katikati ya umati wa watu waliosherehekea. \b \q1 \v 5 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? \q2 Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? \q1 Weka tumaini lako kwa Mungu, \q2 kwa kuwa bado nitamsifu, \q2 Mwokozi wangu na Mungu wangu. \b \q1 \v 6 Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; \q2 kwa hiyo nitakukumbuka \q1 kutoka nchi ya Yordani, \q2 katika vilele vya Hermoni, \q2 kutoka Mlima Mizari. \q1 \v 7 Kilindi huita kilindi, \q2 katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; \q1 mawimbi yako yote pamoja na viwimbi \q2 vimepita juu yangu. \b \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu huelekeza upendo wake mchana, \q2 wimbo wake uko nami usiku: \q2 maombi kwa Mungu wa uzima wangu. \b \q1 \v 9 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, \q2 “Kwa nini umenisahau? \q1 Kwa nini niendelee kuomboleza, \q2 nikiteswa na adui?” \q1 \v 10 Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali \q2 adui zangu wanaponidhihaki, \q1 wakiniambia mchana kutwa, \q2 “Yuko wapi Mungu wako?” \b \q1 \v 11 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? \q2 Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? \q1 Weka tumaini lako kwa Mungu, \q2 kwa kuwa bado nitamsifu, \q2 Mwokozi wangu na Mungu wangu. \c 43 \cl Zaburi 43\f + \fr 43:0 \fr*\ft Katika nakala za kale za Kiebrania, \+xt Zaburi 42\+xt* na \+xt 43\+xt* ni moja\ft*\f* \s1 Maombi ya mtu aliye uhamishoni yanaendelea \q1 \v 1 Ee Mungu unihukumu, \q2 nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu, \q2 niokoe na watu wadanganyifu na waovu. \q1 \v 2 Wewe ni Mungu ngome yangu. \q2 Kwa nini umenikataa? \q1 Kwa nini niendelee kuomboleza, \q2 nikidhulumiwa na adui? \q1 \v 3 Tuma hima nuru yako na kweli yako viniongoze; \q2 na vinilete hadi mlima wako mtakatifu, \q2 mahali unapoishi. \q1 \v 4 Ndipo nitaenda madhabahuni pa Mungu, \q2 kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu. \q1 Nitakusifu kwa kinubi, \q2 Ee Mungu, Mungu wangu. \b \q1 \v 5 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? \q2 Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? \q1 Weka tumaini lako kwa Mungu, \q2 kwa sababu bado nitamsifu \q2 Mwokozi wangu na Mungu wangu. \c 44 \cl Zaburi 44 \s1 Kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. \q1 \v 1 Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, \q2 baba zetu wametueleza \q1 yale uliyotenda katika siku zao, \q2 siku za kale. \q1 \v 2 Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa \q2 na ukawapanda baba zetu, \q1 uliangamiza mataifa \q2 na kuwastawisha baba zetu. \q1 \v 3 Sio kwa upanga wao waliipata nchi, \q2 wala si mkono wao uliwapatia ushindi; \q1 ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, \q2 na nuru ya uso wako, \q2 kwa kuwa uliwapenda. \b \q1 \v 4 Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, \q2 unayeamuru ushindi kwa Yakobo. \q1 \v 5 Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; \q2 kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. \q1 \v 6 Siutumaini upinde wangu, \q2 upanga wangu hauniletei ushindi; \q1 \v 7 bali wewe unatupatia ushindi juu ya adui zetu, \q2 unawaaibisha watesi wetu. \q1 \v 8 Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, \q2 nasi tutalisifu jina lako milele. \b \q1 \v 9 Lakini sasa umetukataa na kutudhili, \q2 wala huendi tena na jeshi letu. \q1 \v 10 Umetufanya tukimbie mbele ya adui, \q2 nao watesi wetu wametuteka nyara. \q1 \v 11 Umetuacha tutafunwe kama kondoo \q2 na umetutawanya katika mataifa. \q1 \v 12 Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, \q2 wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao. \b \q1 \v 13 Umetufanya lawama kwa majirani zetu, \q2 dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka. \q1 \v 14 Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa; \q2 mataifa hututikisia vichwa vyao. \q1 \v 15 Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, \q2 na uso wangu umejaa aibu tele, \q1 \v 16 kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, \q2 kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi. \b \q1 \v 17 Hayo yote yametutokea, \q2 ingawa tulikuwa hatujakusahau \q2 wala hatujaenda kinyume na agano lako. \q1 \v 18 Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; \q2 nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako. \q1 \v 19 Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, \q2 na ukatufunika kwa giza nene. \b \q1 \v 20 Kama tungekuwa tumelisahau jina la Mungu wetu \q2 au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni, \q1 \v 21 je, si Mungu angegundua hili, \q2 kwa kuwa anazijua siri za moyo? \q1 \v 22 Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; \q2 tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. \b \q1 \v 23 Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? \q2 Zinduka! Usitukatae milele. \q1 \v 24 Kwa nini unauficha uso wako \q2 na kusahau taabu na mateso yetu? \b \q1 \v 25 Tumeshushwa hadi mavumbini, \q2 miili yetu imegandamana na ardhi. \q1 \v 26 Inuka na utusaidie, \q2 utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho. \c 45 \cl Zaburi 45 \s1 Wimbo wa arusi ya kifalme \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi”. Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi. \q1 \v 1 Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema \q2 ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; \q2 ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi. \b \q1 \v 2 Wewe ni bora kuliko watu wengine wote \q2 na midomo yako imepakwa neema, \q2 kwa kuwa Mungu amekubariki milele. \q1 \v 3 Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, \q2 jivike fahari na utukufu. \q1 \v 4 Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi, \q2 kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, \q2 mkono wako wa kuume na uoneshe matendo ya kutisha. \q1 \v 5 Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme, \q2 mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako. \q1 \v 6 Ee Mungu, kiti chako cha enzi \q2 kitadumu milele na milele, \q1 fimbo ya utawala wa haki \q2 itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako. \q1 \v 7 Unaipenda haki na kuchukia uovu; \q2 kwa hiyo Mungu, Mungu wako, \q1 amekuweka juu ya wenzako, \q2 kwa kukupaka mafuta ya furaha. \q1 \v 8 Mavazi yako yote yana harufu nzuri \q2 ya manemane, udi na mdalasini; \q1 kutoka majumba ya kifalme \q2 yaliyopambwa kwa pembe za ndovu, \q1 sauti za vinanda vya nyuzi \q2 zinakufanya ufurahi. \q1 \v 9 Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa; \q2 kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri. \b \q1 \v 10 Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio: \q2 Sahau watu wako na nyumba ya baba yako. \q1 \v 11 Mfalme ameshangazwa na uzuri wako; \q2 mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako. \q1 \v 12 Binti Tiro atakuletea zawadi, \q2 watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako. \b \q1 \v 13 Ufahari wote una binti mfalme katika chumba chake; \q2 vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. \q1 \v 14 Anaongozwa kwa mfalme, \q2 akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, \q1 mabikira wenzake wanamfuata \q2 na wanaletwa kwako. \q1 \v 15 Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, \q2 na kuingia katika jumba la mfalme. \b \q1 \v 16 Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, \q2 mtawafanya wakuu katika nchi yote. \q1 \v 17 Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, \q2 kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele. \c 46 \cl Zaburi 46 \s1 Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi. \q1 \v 1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, \q2 msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. \q1 \v 2 Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa, \q2 na milima ianguke kilindini cha bahari, \q1 \v 3 hata maji yake yakinguruma na kuumuka, \q2 na milima itetemeke kwa mawimbi yake. \b \q1 \v 4 Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, \q2 mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. \q1 \v 5 Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, \q2 Mungu atausaidia asubuhi na mapema. \q1 \v 6 Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, \q2 yeye hupaza sauti yake, dunia ikayeyuka. \b \q1 \v 7 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 yu pamoja nasi; \q2 Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. \b \q1 \v 8 Njooni mkaone kazi za Mwenyezi Mungu \q2 jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. \q1 \v 9 Anakomesha vita hata miisho ya dunia, \q2 anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, \q2 anateketeza ngao kwa moto. \q1 \v 10 “Tulieni, mjue kwamba mimi ndimi Mungu; \q2 nitatukuzwa katikati ya mataifa, \q2 nitatukuzwa katika dunia.” \b \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 yu pamoja nasi; \q2 Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. \c 47 \cl Zaburi 47 \s1 Mtawala mwenye enzi yote \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. \q1 \v 1 Pigeni makofi, enyi mataifa yote, \q2 mpigieni Mungu kelele za shangwe! \q1 \v 2 Jinsi gani alivyo wa kutisha, Mwenyezi Mungu Aliye Juu Sana, \q2 Mfalme mkuu juu ya dunia yote! \q1 \v 3 Ametiisha mataifa chini yetu, \q2 watu wengi chini ya miguu yetu. \q1 \v 4 Alituchagulia urithi wetu, \q2 fahari ya Yakobo, aliyempenda. \b \q1 \v 5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, \q2 Mwenyezi Mungu kwa sauti za tarumbeta. \q1 \v 6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, \q2 mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. \b \q1 \v 7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, \q2 mwimbieni zaburi za sifa. \q1 \v 8 Mungu anayatawala mataifa, \q2 Mungu ameketi kwenye kiti chake cha enzi kitakatifu. \q1 \v 9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika \q2 kama watu wa Mungu wa Ibrahimu, \q1 kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; \q2 yeye ametukuka sana. \c 48 \cl Zaburi 48 \s1 Sayuni, mji wa Mwenyezi Mungu \d Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, \q2 katika mji wa Mungu wetu, \q2 mlima wake mtakatifu. \q1 \v 2 Ni mzuri katika kuinuka juu kwake, \q2 furaha ya dunia yote. \q1 Kama vilele vya juu vya Safoni\f + \fr 48:2 \fr*\ft au \ft*\fqa mlima mtakatifu \fqa*\ft au \ft*\fqa upande wa kaskazini\fqa*\f* ni Mlima Sayuni, \q2 mji wa Mfalme Mkuu. \q1 \v 3 Mungu yuko katika ngome zake; \q2 amejionesha mwenyewe kuwa ngome yake. \b \q1 \v 4 Wafalme walipounganisha nguvu, \q2 waliposonga mbele pamoja, \q1 \v 5 walimwona, wakashangaa, \q2 wakakimbia kwa hofu. \q1 \v 6 Kutetemeka kuliwashika huko, \q2 maumivu kama ya mwanamke \q2 mwenye uchungu wa kuzaa. \q1 \v 7 Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi \q2 zilizovunjwa na upepo wa mashariki. \b \q1 \v 8 Kama tulivyokuwa tumesikia, \q2 ndivyo tulivyoona \q1 katika mji wa Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 katika mji wa Mungu wetu: \q2 Mungu ataufanya uwe salama milele. \b \q1 \v 9 Ee Mungu, hekaluni mwako \q2 tunatafakari upendo wako usiokoma. \q1 \v 10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, \q2 sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, \q2 mkono wako wa kuume umejazwa na haki. \q1 \v 11 Mlima Sayuni unashangilia, \q2 vijiji vya Yuda vinafurahi \q2 kwa sababu ya hukumu zako. \b \q1 \v 12 Tembeeni katika Sayuni, \q2 uzungukeni mji, \q2 hesabuni minara yake; \q1 \v 13 yatafakarini vyema maboma yake, \q2 angalieni ngome zake, \q1 ili mpate kusimulia habari zake \q2 kwa kizazi kijacho. \q1 \v 14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; \q2 atakuwa kiongozi wetu hata mwisho. \c 49 \cl Zaburi 49 \s1 Upumbavu wa kutegemea mali \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. \q1 \v 1 Sikieni haya, enyi mataifa yote, \q2 sikilizeni, ninyi wote mnaoishi dunia hii. \q1 \v 2 Wakubwa kwa wadogo, \q2 matajiri na maskini pamoja: \q1 \v 3 Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, \q2 usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu. \q1 \v 4 Nitatega sikio langu nisikilize mithali, \q2 nitafafanua kitendawili kwa zeze: \b \q1 \v 5 Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, \q2 wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka, \q1 \v 6 wale wanaotegemea mali yao \q2 na kujivunia utajiri wao mwingi? \q1 \v 7 Hakuna mwanadamu yeyote \q2 awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, \q2 au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake. \q1 \v 8 Fidia ya uhai ni gharama kubwa, \q2 hakuna malipo yoyote yanayotosha, \q1 \v 9 ili aishi milele \q2 na asione uharibifu. \b \q1 \v 10 Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; \q2 wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia \q2 na kuwaachia wengine mali yao. \q1 \v 11 Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, \q2 makao yao vizazi vyote; \q1 ingawa walikuwa na mashamba \q2 na kuyaita kwa majina yao. \b \q1 \v 12 Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; \q2 anafanana na mnyama aangamiaye. \b \q1 \v 13 Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, \q2 pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. \q1 \v 14 Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini\f + \fr 49:14 \fr*\ft Kaburini hapa ina maana ya \ft*\fqa Sheol \fqa*\ft kwa Kiebrania, yaani \ft*\fqa Kuzimu.\fqa*\f*, \q2 nacho kifo kitawala. \q1 Wanyofu watawatawala asubuhi, \q2 maumbile yao yataozea kaburini, \q2 mbali na majumba yao makubwa ya fahari. \q1 \v 15 Lakini Mungu atakomboa uhai\f + \fr 49:15 \fr*\ft au \ft*\fqa nafsi\fqa*\f* wangu dhidi ya kaburi; \q2 hakika atanichukua kwake. \b \q1 \v 16 Usitishwe mtu anapotajirika, \q2 fahari ya nyumba yake inapoongezeka, \q1 \v 17 kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, \q2 fahari yake haitashuka pamoja naye. \q1 \v 18 Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, \q2 na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, \q1 \v 19 atajiunga na kizazi cha baba zake, \q2 ambao hawataona kamwe nuru ya uzima. \b \q1 \v 20 Wanadamu wenye utajiri bila ufahamu \q2 ni kama wanyama wanaoangamia. \c 50 \cl Zaburi 50 \s1 Ibada ya kweli \d Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Mwenye Nguvu, Mungu, Mwenyezi Mungu, \q2 asema na kuiita dunia, \q1 tangu mawio ya jua \q2 hadi mahali pake liendapo kutua. \q1 \v 2 Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, \q2 Mungu anaangaza. \q1 \v 3 Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, \q2 moto uteketezao unamtangulia, \q2 akiwa amezungukwa na tufani kali. \q1 \v 4 Anaziita mbingu zilizo juu, \q2 na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: \q1 \v 5 “Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, \q2 waliofanya agano nami kwa dhabihu.” \q1 \v 6 Nazo mbingu zinatangaza haki yake, \q2 kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu. \b \q1 \v 7 “Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, \q2 ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: \q2 Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu. \q1 \v 8 Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, \q2 au sadaka zako za kuteketezwa, \q2 ambazo daima ziko mbele zangu. \q1 \v 9 Sina haja na fahali wa banda lako, \q2 au mbuzi wa zizi lako. \q1 \v 10 Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, \q2 na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. \q1 \v 11 Ninamjua kila ndege mlimani, \q2 nao viumbe wa kondeni ni wangu. \q1 \v 12 Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi, \q2 kwa maana ulimwengu ni wangu, \q2 na vyote vilivyomo. \q1 \v 13 Je, mimi hula nyama ya mafahali \q2 au kunywa damu ya mbuzi? \q1 \v 14 Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, \q2 timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, \q1 \v 15 na uniite siku ya taabu; \q2 nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.” \p \v 16 Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: \q1 “Una haki gani kunena sheria zangu \q2 au kuchukua agano langu mdomoni mwako? \q1 \v 17 Unachukia mafundisho yangu \q2 na kuyatupilia mbali maneno yangu. \q1 \v 18 Unapomwona mwizi, unaungana naye, \q2 unapiga kura yako pamoja na wazinzi. \q1 \v 19 Unakitumia kinywa chako kunena maovu, \q2 na kuuongoza ulimi wako kwa hila. \q1 \v 20 Unamsengenya ndugu yako bila kukoma, \q2 na kumsingizia mwana wa mama yako. \q1 \v 21 Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, \q2 ukadhani Mimi ni kama wewe kabisa. \q1 Lakini nitakukemea \q2 na kuweka mashtaka mbele yako. \b \q1 \v 22 “Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu, \q2 ama sivyo nitawararua vipande vipande, \q2 wala hapatakuwa na yeyote wa kuwaokoa: \q1 \v 23 Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, \q2 naye aiandaa njia yake \q2 ili nimwoneshe wokovu wa Mungu.” \c 51 \cl Zaburi 51 \s1 Kuomba msamaha \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. \q1 \v 1 Ee Mungu, unihurumie, \q2 kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, \q1 kwa kadiri ya huruma yako kuu, \q2 uyafute makosa yangu. \q1 \v 2 Unioshe na uovu wangu wote \q2 na unitakase dhambi yangu. \b \q1 \v 3 Kwa maana najua makosa yangu, \q2 na dhambi yangu iko mbele yangu daima. \q1 \v 4 Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi \q2 na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, \q1 ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena, \q2 na kuwa na haki unapotoa hukumu. \q1 \v 5 Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, \q2 mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu. \q1 \v 6 Hakika wewe wapendezwa na kweli inayotoka moyoni; \q2 wanifundisha hekima ndani ya moyo wangu. \b \q1 \v 7 Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, \q2 unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. \q1 \v 8 Unipe kusikia furaha na shangwe, \q2 mifupa uliyoiponda na ifurahi. \q1 \v 9 Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, \q2 na uufute uovu wangu wote. \b \q1 \v 10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, \q2 uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. \q1 \v 11 Usinitupe kutoka mbele zako \q2 wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu. \q1 \v 12 Unirudishie furaha ya wokovu wako, \q2 unipe roho ya utii, ili initegemeze. \b \q1 \v 13 Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, \q2 na wenye dhambi watarejea kwako. \q1 \v 14 Ee Mungu, Mungu uniokoaye, \q2 niokoe na hatia ya kumwaga damu, \q2 nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. \q1 \v 15 Ee Bwana, fungua midomo yangu, \q2 na kinywa changu kitatangaza sifa zako. \q1 \v 16 Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningeileta; \q2 hufurahii sadaka za kuteketezwa. \q1 \v 17 Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; \q2 moyo uliovunjika wenye toba, \q2 ee Mungu, hutaudharau. \b \q1 \v 18 Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, \q2 ukazijenge upya kuta za Yerusalemu. \q1 \v 19 Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, \q2 sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, \q1 pia mafahali watatolewa \q2 madhabahuni mwako. \c 52 \cl Zaburi 52 \s1 Hukumu ya Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi ameenda nyumbani mwa Ahimeleki.” \q1 \v 1 Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? \q2 Kwa nini unajivuna mchana kutwa, \q2 wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? \q1 \v 2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. \q2 Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila. \q1 \v 3 Unapenda mabaya kuliko mema, \q2 uongo kuliko kusema kweli. \q1 \v 4 Unapenda kila neno lenye kudhuru, \q2 ewe ulimi wenye hila! \b \q1 \v 5 Hakika Mungu atakushusha chini \q2 kwa maangamizi ya milele: \q1 atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu \q2 kutoka hema lako, \q2 atakung’oa kutoka nchi ya walio hai. \q1 \v 6 Wenye haki wataona na kuogopa; \q2 watamcheka, wakisema, \q1 \v 7 “Huyu ni yule mtu ambaye \q2 hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, \q1 bali alitumainia wingi wa utajiri wake, \q2 na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!” \s1 Neema ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 8 Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni \q2 unaostawi katika nyumba ya Mungu, \q1 nautegemea upendo wa Mungu usiokoma \q2 milele na milele. \q1 \v 9 Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, \q2 nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. \q2 Nitakusifu mbele ya watakatifu wako. \c 53 \cl Zaburi 53 \s1 Uovu wa wanadamu \r (Zaburi 14) \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi. \q1 \v 1 Mpumbavu anasema moyoni mwake, \q2 “Hakuna Mungu.” \q1 Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, \q2 hakuna hata mmoja atendaye mema. \b \q1 \v 2 Mungu anawachungulia wanadamu chini \q2 kutoka mbinguni \q1 aone kama wako wenye akili, \q2 wowote wanaomtafuta Mungu. \q1 \v 3 Kila mmoja amegeukia mbali, \q2 wameharibika wote pamoja, \q1 hakuna atendaye mema. \q2 Naam, hakuna hata mmoja! \b \q1 \v 4 Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza: \q2 wale ambao huwala watu wangu \q1 kama watu walavyo mkate, \q2 hao ambao hawamwiti Mungu? \q1 \v 5 Hapo waliingiwa na hofu kuu, \q2 ambapo hapakuwa na hofu. \q1 Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia; \q2 uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau. \b \q1 \v 6 Laiti wokovu wa Israeli ungekuja kutoka Sayuni! \q2 Mungu anaporejesha wafungwa wa watu wake, \q2 Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi! \c 54 \cl Zaburi 54 \s1 Kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu kutokana na adui \d Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” \q1 \v 1 Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, \q2 unifanyie hukumu kwa uwezo wako. \q1 \v 2 Ee Mungu, sikia maombi yangu, \q2 usikilize maneno ya kinywa changu. \b \q1 \v 3 Wageni wananishambulia, \q2 watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, \q2 watu wasiomjali Mungu. \b \q1 \v 4 Hakika Mungu ni msaada wangu, \q2 Bwana ndiye anayenitegemeza. \b \q1 \v 5 Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, \q2 kwa uaminifu wako uwaangamize. \b \q1 \v 6 Nitakutolea dhabihu za hiari; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, nitalisifu jina lako \q2 kwa kuwa ni vyema. \q1 \v 7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, \q2 na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi. \c 55 \cl Zaburi 55 \s1 Maombi ya mtu aliyesalitiwa na rafiki \d Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, \q2 wala usidharau hoja yangu. \q1 \v 2 Nisikie na unijibu. \q1 Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa \q1 \v 3 kwa sauti ya adui, \q2 kwa kukaziwa macho na waovu, \q1 kwa sababu wananiletea mateso juu yangu \q2 na kunitukana kwa hasira zao. \b \q1 \v 4 Moyo wangu umejaa uchungu, \q2 hofu za mauti zimenishambulia. \q1 \v 5 Woga na kutetemeka vimenizunguka, \q2 hofu kuu imenigharikisha. \q1 \v 6 Nilisema, “Laiti ningekuwa na mabawa ya njiwa! \q2 Ningeruka niende mbali kupumzika. \q1 \v 7 Ningetorokea mbali sana \q2 na kukaa jangwani, \q1 \v 8 ningeharakisha kwenda mahali pa salama, \q2 mbali na tufani kali na dhoruba.” \b \q1 \v 9 Ee Bwana, uwatahayarishe waovu \q2 na uwachanganyishie semi zao, \q2 maana nimeona jeuri na ugomvi mjini. \q1 \v 10 Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, \q2 uovu na dhuluma vimo ndani yake. \q1 \v 11 Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini, \q2 vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake. \b \q1 \v 12 Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia, \q2 kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, \q2 ningejificha asinione. \q1 \v 13 Kumbe ni wewe, mwenzangu, \q2 mshiriki na rafiki yangu wa karibu, \q1 \v 14 ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri, \q2 tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu. \b \q1 \v 15 Kifo na kiwajie adui zangu ghafula, \q2 na washuke Kuzimu\f + \fr 55:15 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f* wangali hai, \q2 kwa maana uovu uko ndani yao. \b \q1 \v 16 Lakini ninamwita Mungu, \q2 naye Mwenyezi Mungu huniokoa. \q1 \v 17 Jioni, asubuhi na adhuhuri \q2 ninalia kwa huzuni, \q2 naye husikia sauti yangu. \q1 \v 18 Huniokoa nikawa salama katika vita \q2 vilivyopangwa dhidi yangu, \q2 ingawa watu wengi hunipinga. \q1 \v 19 Mungu anayemiliki milele, \q2 atawasikia na kuwaadhibu, \q1 watu ambao hawabadilishi njia zao, \q2 wala hawana hofu ya Mungu. \b \q1 \v 20 Mwenzangu hushambulia rafiki zake, \q2 naye huvunja agano lake. \q1 \v 21 Mazungumzo yake ni laini kama siagi, \q2 hata hivyo vita vimo moyoni mwake. \q1 Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, \q2 hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. \b \q1 \v 22 Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako, \q2 naye atakutegemeza, \q2 hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke. \q1 \v 23 Lakini wewe, Ee Mungu, \q2 utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. \q1 Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, \q2 hawataishi nusu ya siku zao. \b \q1 Lakini mimi ninakutumaini wewe. \c 56 \cl Zaburi 56 \s1 Kumtumaini Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Njiwa mkimya wa mbali”. Utenzi wa Daudi. Baada ya kukamatwa na Wafilisti huko Gathi. \q1 \v 1 Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; \q2 mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. \q1 \v 2 Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, \q2 wengi wananishambulia kwa kiburi chao. \b \q1 \v 3 Wakati ninaogopa, \q2 nitakutumaini wewe. \q1 \v 4 Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, \q2 katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. \q1 Mwanadamu mwenye kufa \q2 atanitenda nini? \b \q1 \v 5 Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, \q2 siku zote wanapanga njama za kunidhuru. \q1 \v 6 Wananifanyia hila, wanajificha, \q2 wanatazama hatua zangu, \q2 wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. \b \q1 \v 7 Wasiepuke kwa vyovyote, \q2 Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. \q1 \v 8 Andika maombolezo yangu; \q2 andika machozi yangu katika kitabu chako: \q2 je, haya hayapo katika kumbukumbu zako? \b \q1 \v 9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma \q2 ninapoita msaada. \q1 Kwa hili nitajua kwamba Mungu \q2 yuko upande wangu. \q1 \v 10 Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, \q2 katika Mwenyezi Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, \q1 \v 11 katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. \q2 Mwanadamu anaweza kunitenda nini? \b \q1 \v 12 Ee Mungu, nina nadhiri kwako, \q2 nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani. \q1 \v 13 Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti \q2 na miguu yangu kwenye kujikwaa, \q1 ili niweze kuenenda mbele za Mungu \q2 katika nuru ya uzima. \c 57 \cl Zaburi 57 \s1 Kuomba msaada \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. \q1 \v 1 Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, \q2 kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. \q1 Chini ya uvuli wa mabawa yako nitakimbilia \q2 hadi maafa yapite. \b \q1 \v 2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, \q2 Mungu anayetimiza makusudi yake kwangu. \q1 \v 3 Hutumana msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, \q2 akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; \q2 Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. \b \q1 \v 4 Niko katikati ya simba; \q2 nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kali, \q2 watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, \q2 ambao ndimi zao ni panga kali. \b \q1 \v 5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, \q2 utukufu wako na uenee duniani kote. \b \q1 \v 6 Waliitegea miguu yangu nyavu, \q2 nikachoshwa na dhiki. \q1 Wamechimba shimo katika njia yangu, \q2 lakini wametumbukia humo wao wenyewe. \b \q1 \v 7 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti, \q2 moyo wangu ni thabiti; \q2 nitaimba na kusifu kwa nyimbo. \q1 \v 8 Amka, nafsi yangu! \q2 Amka, kinubi na zeze! \q2 Nitayaamsha mapambazuko. \b \q1 \v 9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kati ya mataifa; \q2 nitaimba habari zako, kati ya jamaa za watu. \q1 \v 10 Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, \q2 uaminifu wako unazifikia anga. \b \q1 \v 11 Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, \q2 utukufu wako na uwe duniani pote. \c 58 \cl Zaburi 58 \s1 Mwenyezi Mungu kuwaadhibu waovu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Utenzi wa Daudi. \q1 \v 1 Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki? \q2 Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu? \q1 \v 2 La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu, \q2 na mikono yenu hueneza jeuri duniani. \q1 \v 3 Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao, \q2 toka tumboni mwa mama zao \q2 ni wakaidi na husema uongo. \q1 \v 4 Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, \q2 kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake, \q1 \v 5 ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi, \q2 hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani. \b \q1 \v 6 Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, vunja meno makali ya hao simba! \q1 \v 7 Na watoweke kama maji yanavyotiririka; \q2 wanapovuta pinde zao, mishale yao na iwe butu. \q1 \v 8 Na wawe kama konokono anayeyeyuka akitembea, \q2 kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu. \b \q1 \v 9 Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba, \q2 zikiwa mbichi au kavu, \q1 waovu watakuwa \q2 wamefagiliwa mbali. \q1 \v 10 Wenye haki watafurahi wakilipizwa kisasi, \q2 watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu. \q1 \v 11 Ndipo wanadamu watasema, \q2 “Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu, \q2 hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.” \c 59 \cl Zaburi 59 \s1 Kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Utenzi wa Daudi. Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue. \q1 \v 1 Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, \q2 unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. \q1 \v 2 Uniponye na watu watendao maovu, \q2 uniokoe kutokana na wanaomwaga damu. \b \q1 \v 3 Tazama wanavyonivizia! \q2 Watu wakali wananifanyia hila, \q1 ingawa Ee Mwenyezi Mungu, mimi sijakosea \q2 wala kutenda dhambi. \q1 \v 4 Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. \q2 Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya! \q1 \v 5 Ee Mungu, Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 uliye Mungu wa Israeli, \q1 zinduka uyaadhibu mataifa yote; \q2 usioneshe huruma kwa wasaliti waovu. \b \q1 \v 6 Hurudi wakati wa jioni, \q2 wakibweka kama mbwa, \q2 wakiuzurura mji. \q1 \v 7 Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, \q2 hutema panga kutoka midomo yao, \q2 nao husema, “Ni nani atakayetusikia?” \q1 \v 8 Lakini wewe, Mwenyezi Mungu, uwacheke; \q2 unayadharau mataifa hayo yote. \b \q1 \v 9 Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, \q2 wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, \q2 \v 10 Mungu wangu unayenipenda. \b \q1 Mungu atanitangulia, \q2 naye atanifanya niwachekelee \q2 wale wanaonisingizia. \q1 \v 11 Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, \q2 au sivyo watu wangu watasahau. \q1 Katika uwezo wako wafanye watangetange \q2 na uwashushe chini. \q1 \v 12 Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, \q2 kwa ajili ya maneno ya midomo yao, \q2 waache wanaswe katika kiburi chao. \q1 Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, \q2 \v 13 wateketeze katika ghadhabu, \q2 wateketeze hadi wasiwepo tena. \q1 Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia \q2 kwamba Mungu anatawala katika Yakobo. \b \q1 \v 14 Hurudi jioni, \q2 wakibweka kama mbwa, \q2 wakiuzurura mji. \q1 \v 15 Wanatangatanga wakitafuta chakula, \q2 wasipotosheka hubweka kama mbwa. \q1 \v 16 Lakini mimi nitaziimba nguvu zako, \q2 asubuhi nitaimba kuhusu upendo wako; \q1 kwa maana wewe ndiwe ngome yangu \q2 na kimbilio langu wakati wa shida. \q1 \v 17 Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa. \q2 Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, \q2 Mungu unayenipenda. \c 60 \cl Zaburi 60 \s1 Kuomba kuokolewa \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi”. Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Alipopigana na Waaramu kutoka Aram-Naharaimu na Aram-Soba, na Yoabu aliporudi na kuwaua Waedomu elfu kumi na mbili katika Bonde la Chumvi. \q1 \v 1 Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, \q2 umekuwa na hasira; sasa turejeshe! \q1 \v 2 Umetetemesha nchi na kuipasua; \q2 uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka. \q1 \v 3 Umewaonesha watu wako nyakati za kukata tamaa; \q2 umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha. \b \q1 \v 4 Kwa wale wanaokucha wewe, \q2 umewainulia bendera, \q2 ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. \b \q1 \v 5 Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, \q2 ili wale uwapendao wapate kuokolewa. \q1 \v 6 Mungu amenena kutoka patakatifu pake: \q2 “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi \q2 na kulipima Bonde la Sukothi. \q1 \v 7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; \q2 Efraimu ni chapeo yangu, \q2 nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. \q1 \v 8 Moabu ni sinia langu la kunawia, \q2 juu ya Edomu natupa kiatu changu; \q2 nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” \b \q1 \v 9 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? \q2 Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? \q1 \v 10 Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, \q2 na hutoki tena na majeshi yetu? \q1 \v 11 Tuletee msaada dhidi ya adui, \q2 kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. \q1 \v 12 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, \q2 naye atawaponda adui zetu. \c 61 \cl Zaburi 61 \s1 Kuomba ulinzi \d Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, sikia kilio changu, \q2 usikilize maombi yangu. \b \q1 \v 2 Kutoka miisho ya dunia ninakuita, \q2 ninakuita huku moyo wangu unadhoofika; \q1 uniongoze kwenye mwamba \q2 ulio juu kuniliko. \q1 \v 3 Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, \q2 ngome imara dhidi ya adui. \b \q1 \v 4 Natamani kukaa kwenye hema lako milele, \q2 na kukimbilia chini ya uvuli wa mabawa yako. \q1 \v 5 Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, \q2 umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako. \b \q1 \v 6 Mwongezee mfalme siku za maisha yake, \q2 miaka yake kwa vizazi vingi. \q1 \v 7 Mtawaze mbele za Mungu milele; \q2 amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde. \b \q1 \v 8 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako \q2 na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku. \c 62 \cl Zaburi 62 \s1 Mwenyezi Mungu kimbilio la pekee \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nafsi yangu inapata pumziko kwa Mungu peke yake; \q2 wokovu wangu watoka kwake. \q1 \v 2 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; \q1 yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. \b \q1 \v 3 Mtanishambulia hadi lini? \q2 Je, ninyi nyote mtanitupa chini: \q1 Mimi niliye kama ukuta ulioinama, \q2 kama uzio unaotikisika? \q1 \v 4 Walikusudia kikamilifu kumwangusha \q2 toka mahali pake pa fahari; \q2 wanafurahia uongo. \q1 Kwa vinywa vyao hubariki, \q2 lakini ndani ya mioyo yao hulaani. \b \q1 \v 5 Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, \q2 tumaini langu latoka kwake. \q1 \v 6 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; \q2 ndiye ngome yangu, sitatikisika. \q1 \v 7 Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, \q2 ndiye mwamba wangu wenye nguvu \q2 na kimbilio langu. \q1 \v 8 Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, \q2 miminieni mioyo yenu kwake, \q2 kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu. \b \q1 \v 9 Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu, \q2 nao wa ngazi ya juu ni uongo tu; \q1 wakipimwa kwenye mizani, si chochote; \q2 wote kwa pamoja ni pumzi tu. \q1 \v 10 Usitumainie udhalimu, \q2 wala ujivune kwa vitu vya wizi; \q1 ingawa utajiri wako utaongezeka, \q2 usiuweke moyoni mwako. \b \q1 \v 11 Jambo moja Mungu amelisema, \q2 mambo mawili nimeyasikia: \q1 kwamba, Ee Mungu, \q2 wewe una nguvu, \q1 \v 12 na kwamba, Ee Bwana, \q2 wewe ni mwenye upendo. \q1 Hakika utampa kila mtu thawabu \q2 kwa kadiri ya alivyotenda. \c 63 \cl Zaburi 63 \s1 Shauku kwa ajili ya uwepo wa Mwenyezi Mungu \d Zaburi ya Daudi. Alipokuwa katika Jangwa la Yuda. \q1 \v 1 Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, \q2 nakutafuta kwa moyo wote; \q1 nafsi yangu inakuonea kiu, \q2 mwili wangu unakuonea wewe shauku, \q1 katika nchi kame na iliyochoka, \q2 mahali pasipo maji. \b \q1 \v 2 Nimekuona katika mahali patakatifu \q2 na kuuona uwezo wako na utukufu wako. \q1 \v 3 Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, \q2 midomo yangu itakuadhimisha. \q1 \v 4 Nitakusifu siku zote za maisha yangu, \q2 na kwa jina lako nitainua mikono yangu. \q1 \v 5 Nafsi yangu itatoshelezwa, \q2 kama kushiba vyakula vizuri; \q1 kwa midomo iimbayo \q2 kinywa changu kitakusifu wewe. \b \q1 \v 6 Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe; \q2 ninakuwaza makesha yote ya usiku. \q1 \v 7 Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, \q2 chini ya uvuli wa mabawa yako naimba. \q1 \v 8 Nafsi yangu inaambatana nawe, \q2 mkono wako wa kuume hunishika. \b \q1 \v 9 Wale wanaotafuta uhai wangu wataangamizwa; \q2 wataenda chini kwenye vilindi vya dunia. \q1 \v 10 Watatolewa wafe kwa upanga, \q2 nao watakuwa chakula cha mbweha. \b \q1 \v 11 Bali mfalme atafurahi katika Mungu, \q2 wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, \q2 bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa. \c 64 \cl Zaburi 64 \s1 Kuomba ulinzi dhidi ya adui \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu, \q2 uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui. \q1 \v 2 Unifiche kutokana na njama za waovu, \q2 kutokana na fitina za kundi la watenda maovu. \b \q1 \v 3 Wananoa ndimi zao kama panga \q2 na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. \q1 \v 4 Hurusha mishale kutoka mavizio kwa mtu asiye na hatia, \q2 humrushia ghafula bila woga. \b \q1 \v 5 Kila mmoja humtia moyo mwenzake \q2 katika mipango mibaya; \q1 huzungumza kuhusu kuficha mitego yao, \q2 nao husema, “Ni nani ataiona?” \q1 \v 6 Hupanga njama la dhuluma na kusema, \q2 “Tumebuni mpango mkamilifu!” \q2 Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila. \b \q1 \v 7 Bali Mungu atawapiga kwa mishale, \q2 nao ghafula wataangushwa. \q1 \v 8 Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao \q2 na kuwaleta kwenye maangamizi; \q1 wote wawaonao watatikisa vichwa vyao \q2 kwa dharau. \b \q1 \v 9 Wanadamu wote wataogopa, \q2 watatangaza kazi za Mungu \q2 na kutafakari yale aliyoyatenda. \q1 \v 10 Wenye haki na wafurahi katika Mwenyezi Mungu, \q2 na wakimbilie kwake; \q2 wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye! \c 65 \cl Zaburi 65 \s1 Kusifu na kushukuru \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. \q1 \v 1 Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; \q2 kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. \q1 \v 2 Ewe usikiaye maombi, \q2 watu wote watakuja kwako wewe. \q1 \v 3 Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, \q2 wewe ulisamehe makosa yetu. \q1 \v 4 Heri wale uliowachagua \q2 na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! \q1 Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, \q2 mema ya Hekalu lako takatifu. \b \q1 \v 5 Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, \q2 Ee Mungu Mwokozi wetu, \q1 tumaini la miisho yote ya duniani \q2 na la bahari zilizo mbali sana, \q1 \v 6 uliyeumba milima kwa uwezo wako, \q2 ukiwa umejivika nguvu, \q1 \v 7 uliyenyamazisha dhoruba za bahari, \q2 ngurumo za mawimbi yake, \q2 na ghasia za mataifa. \q1 \v 8 Wale wanaoishi mbali sana \q2 wanaogopa maajabu yako, \q1 kule asubuhi ipambazukiapo \q2 na kule jioni inakofifilia \q2 umeziita nyimbo za furaha. \b \q1 \v 9 Waitunza nchi na kuinyeshea, \q2 waitajirisha kwa wingi. \q1 Vijito vya Mungu vimejaa maji \q2 ili kuwapa watu nafaka, \q2 kwa maana wewe umeviamuru. \q1 \v 10 Umeilowesha mifereji yake \q2 na kusawazisha kingo zake; \q1 umeilainisha kwa manyunyu \q2 na kuibariki mimea yake. \q1 \v 11 Umeuvika mwaka taji la baraka, \q2 magari yako yanafurika kwa wingi. \q1 \v 12 Mbuga za majani za jangwani umezineemesha; \q2 vilima vimevikwa furaha. \q1 \v 13 Malisho yamejaa makundi ya wanyama, \q2 na mabonde yamepambwa kwa mavuno; \q2 vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba. \c 66 \cl Zaburi 66 \s1 Kusifu Mwenyezi Mungu kwa ajili ya wema wake \d Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi. \q1 \v 1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! \q2 \v 2 Imbeni utukufu wa jina lake; \q2 mpeni sifa zake kwa utukufu! \q1 \v 3 Mwambieni Mungu, “Jinsi gani \q2 yalivyo ya kutisha matendo yako! \q1 Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba \q2 adui wanajikunyata mbele zako. \q1 \v 4 Dunia yote yakusujudia, \q2 wanakuimbia wewe sifa, \q2 wanaliimbia sifa jina lako.” \b \q1 \v 5 Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda, \q2 mambo ya kutisha aliyoyatenda \q2 miongoni mwa wanadamu! \q1 \v 6 Alifanya bahari kuwa nchi kavu, \q2 wakapita kati ya maji kwa miguu, \q2 njooni, tumshangilie. \q1 \v 7 Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, \q2 macho yake huangalia mataifa yote: \q2 waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. \b \q1 \v 8 Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu, \q2 sauti ya sifa yake isikike, \q1 \v 9 ameyahifadhi maisha yetu \q2 na kuizuia miguu yetu kuteleza. \q1 \v 10 Ee Mungu, wewe ulitujaribu, \q2 ukatusafisha kama fedha. \q1 \v 11 Umetuingiza kwenye nyavu \q2 na umetubebesha mizigo mizito \q2 migongoni mwetu. \q1 \v 12 Uliwaruhusu watu watukalie vichwani, \q2 tulipita kwenye moto na kwenye maji, \q1 lakini ulituleta kwenye nchi \q2 iliyojaa utajiri tele. \b \q1 \v 13 Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa \q2 na kukutimizia nadhiri zangu: \q1 \v 14 nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi \q2 na nilizotamka kwa kinywa changu \q2 nilipokuwa katika shida. \q1 \v 15 Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono \q2 na sadaka za kondoo dume, \q2 nitakutolea mafahali na mbuzi. \b \q1 \v 16 Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu, \q2 nami niwaambie aliyonitendea. \q1 \v 17 Nilimlilia kwa kinywa changu, \q2 sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu. \q1 \v 18 Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, \q2 Bwana asingekuwa amenisikiliza; \q1 \v 19 lakini hakika Mungu amenisikiliza \q2 na amesikia sauti yangu katika maombi. \q1 \v 20 Ahimidiwe Mungu, \q2 ambaye hakulikataa ombi langu, \q2 wala kunizuilia upendo wake! \c 67 \cl Zaburi 67 \s1 Mataifa wahimizwa kumsifu Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. \q1 \v 1 Mungu aturehemu na kutubariki, \q2 na kutuangazia nuru za uso wake, \q1 \v 2 ili njia zako zijulikane duniani, \q2 wokovu wako katikati ya mataifa yote. \b \q1 \v 3 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, \q2 mataifa yote na wakusifu. \q1 \v 4 Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, \q2 kwa kuwa unatawala watu kwa haki \q2 na kuongoza mataifa ya dunia. \q1 \v 5 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, \q2 mataifa yote na wakusifu. \b \q1 \v 6 Ndipo nchi itatoa mazao yake, \q2 naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. \q1 \v 7 Mungu atatubariki \q2 na miisho yote ya dunia itamcha yeye. \c 68 \cl Zaburi 68 \s1 Wimbo wa taifa wa shangwe kwa ushindi \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. \q1 \v 1 Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike, \q2 adui zake na wakimbie mbele zake. \q1 \v 2 Kama moshi unavyopeperushwa na upepo, \q2 vivyo hivyo uwapeperushe mbali, \q1 kama nta inavyoyeyuka kwenye moto, \q2 vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu. \q1 \v 3 Bali wenye haki na wafurahi, \q2 washangilie mbele za Mungu, \q2 wafurahi na kushangilia. \b \q1 \v 4 Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, \q2 mtukuzeni yeye anayepita juu ya mawingu: \q1 jina lake ni Mwenyezi Mungu, \q2 furahini mbele zake. \q1 \v 5 Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, \q2 ni Mungu katika makao yake matakatifu. \q1 \v 6 Mungu huwaweka wapweke katika jamaa, \q2 huwaongoza wafungwa wakiimba, \q2 bali waasi huishi katika nchi kame. \b \q1 \v 7 Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako, \q2 ulipopita nyikani, \q1 \v 8 dunia ilitikisika, \q2 mbingu zikanyesha mvua, \q1 mbele za Mungu, Yule wa Sinai, \q2 mbele za Mungu, Mungu wa Israeli. \q1 \v 9 Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi \q2 na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka. \q1 \v 10 Ee Mungu, watu wako waliishi huko, \q2 nawe kwa wingi wa utajiri wako \q2 uliwapa maskini mahitaji yao. \b \q1 \v 11 Bwana analitoa neno, \q2 wanawake wanaolitangaza \q2 neno hilo ni kundi kubwa: \q1 \v 12 “Wafalme na majeshi walikimbia upesi, \q2 wanawake waliobaki nyumbani waligawana nyara. \q1 \v 13 Hata unapolala kati ya mioto ya kambini, \q2 mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha, \q2 manyoya yake kwa dhahabu inayong’aa.” \q1 \v 14 Mwenyezi\f + \fr 68:14 \fr*\ft Mwenyezi hapa ina maana ya \ft*\fqa Shaddai \fqa*\ft kwa Kiebrania.\ft*\f* alipowatawanya wafalme katika nchi, \q2 ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Mlima Salmoni. \b \q1 \v 15 Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka, \q2 milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka. \q1 \v 16 Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka, \q2 kwa nini mnakazia macho kwa wivu, \q1 katika mlima Mungu anaochagua kutawala, \q2 ambako Mwenyezi Mungu mwenyewe ataishi milele? \q1 \v 17 Magari ya vita ya Mungu ni makumi ya maelfu, \q2 na maelfu ya maelfu; \q1 Bwana amekuja kutoka Sinai \q2 hadi katika patakatifu pake. \q1 \v 18 Ulipopanda juu, uliteka mateka, \q2 ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, \q1 hata kutoka kwa wale walioasi, \q2 ili wewe, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, upate kuishi huko. \b \q1 \v 19 Ahimidiwe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, \q2 ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. \q1 \v 20 Mungu wetu ni Mungu anayeokoa, \q2 Bwana Mungu Mwenyezi hutuokoa na kifo. \b \q1 \v 21 Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, \q2 vichwa vya hao wanaoenda katika njia za dhambi. \q1 \v 22 Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; \q2 nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, \q1 \v 23 ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, \q2 huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.” \b \q1 \v 24 Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, \q2 maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, \q2 yakielekea patakatifu pake. \q1 \v 25 Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, \q2 pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. \q1 \v 26 Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, \q2 msifuni Mwenyezi Mungu katika kusanyiko la Israeli. \q1 \v 27 Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza, \q2 wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda, \q2 hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali. \b \q1 \v 28 Ee Mungu, amuru uwezo wako, \q2 Ee Mungu tuoneshe nguvu zako, \q2 kama ulivyofanya hapo awali. \q1 \v 29 Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu \q2 wafalme watakuletea zawadi. \q1 \v 30 Mkemee mnyama aliye kwenye matete, \q2 kundi la mafahali kati ya ndama za mataifa. \q1 Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. \q2 Tawanya mataifa yapendayo vita. \q1 \v 31 Wajumbe watakuja kutoka Misri; \q2 Kushi atajisalimisha kwa Mungu. \b \q1 \v 32 Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, \q2 mwimbieni Bwana sifa, \q1 \v 33 mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, \q2 yeye angurumaye kwa sauti kuu. \q1 \v 34 Tangazeni uwezo wa Mungu, \q2 ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, \q2 ambaye uwezo wake uko katika anga. \q1 \v 35 Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, \q2 Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. \b \q1 Ahimidiwe Mungu! \c 69 \cl Zaburi 69 \s1 Kilio cha kuomba msaada wakati wa dhiki \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi”. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, niokoe, \q2 kwa maana maji yamenifika shingoni. \q1 \v 2 Ninazama kwenye vilindi vya matope, \q2 pasipo mahali pa kukanyaga, \q1 Nimefika kwenye maji makuu, \q2 mafuriko yamenigharikisha. \q1 \v 3 Nimechoka kwa kuomba msaada, \q2 koo langu limekauka. \q1 Macho yangu yanafifia, \q2 nikimtafuta Mungu wangu. \q1 \v 4 Wale wanaonichukia bila sababu \q2 ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; \q1 wengi ni adui kwangu bila sababu, \q2 wale wanaotafuta kuniangamiza. \q1 Ninalazimishwa kurudisha \q2 kitu ambacho sikuiba. \b \q1 \v 5 Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, \q2 wala hatia yangu haikufichika kwako. \b \q1 \v 6 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 wanaokutumaini wasiaibishwe \q2 kwa ajili yangu; \q1 wanaokutafuta wasifedheheshwe kwa ajili yangu, \q2 Ee Mungu wa Israeli. \q1 \v 7 Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, \q2 aibu imefunika uso wangu. \q1 \v 8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, \q2 mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. \q1 \v 9 Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, \q2 matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. \q1 \v 10 Ninapolia na kufunga, \q2 lazima nivumilie matusi. \q1 \v 11 Ninapovaa gunia, \q2 watu hunidharau. \q1 \v 12 Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, \q2 nimekuwa wimbo wa walevi. \b \q1 \v 13 Lakini Ee Mwenyezi Mungu, ninakuomba, \q2 kwa wakati ukupendezao; \q1 katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, \q2 unijibu kwa wokovu wako wa hakika. \q1 \v 14 Uniokoe katika matope, \q2 usiniache nizame; \q1 niokoe na hao wanaonichukia, \q2 kutoka kwa vilindi vya maji. \q1 \v 15 Usiache mafuriko yanigharikishe \q2 au vilindi vinimeze, \q2 au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. \q1 \v 16 Ee Mwenyezi Mungu, unijibu, kwa wema wa upendo wako; \q2 kwa huruma zako nyingi unigeukie. \q1 \v 17 Usimfiche mtumishi wako uso wako, \q2 uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. \q1 \v 18 Njoo karibu uniokoe, \q2 nikomboe kwa sababu ya adui zangu. \b \q1 \v 19 Unajua jinsi ninavyodharauliwa, \q2 kufedheheshwa na kuaibishwa, \q2 adui zangu wote unawajua. \q1 \v 20 Dharau zimenivunja moyo \q2 na nimekata tamaa, \q1 nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, \q2 wa kunituliza, lakini sikumpata. \q1 \v 21 Waliweka nyongo katika chakula changu \q2 na walinipa siki nilipokuwa na kiu. \b \q1 \v 22 Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, \q2 nayo iwe upatilizo na tanzi. \q1 \v 23 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, \q2 nayo migongo yao iinamishwe daima. \q1 \v 24 Uwamwagie ghadhabu yako, \q2 hasira yako kali na iwapate. \q1 \v 25 Mahali pao na pawe ukiwa, \q2 wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. \q1 \v 26 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, \q2 na kuzungumza kuhusu maumivu ya wale uliowaumiza. \q1 \v 27 Walipize uovu juu ya uovu, \q2 usiwaache washiriki katika wokovu wako. \q1 \v 28 Wafutwe kutoka kitabu cha uzima \q2 na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki. \b \q1 \v 29 Lakini mimi niko katika maumivu na dhiki; \q2 Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. \b \q1 \v 30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, \q2 nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani. \q1 \v 31 Hili litampendeza Mwenyezi Mungu kuliko ng’ombe dume, \q2 zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. \q1 \v 32 Maskini wataona na kufurahi: \q2 ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi! \q1 \v 33 Mwenyezi Mungu huwasikia wahitaji \q2 wala hadharau watu wake waliotekwa. \b \q1 \v 34 Mbingu na dunia zimsifu, \q2 bahari na vyote viendavyo ndani yake, \q1 \v 35 kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni \q2 na kuijenga tena miji ya Yuda. \q1 Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, \q2 \v 36 watoto wa watumishi wake watairithi \q1 na wale wote wanaolipenda jina lake \q2 wataishi humo. \c 70 \cl Zaburi 70 \s1 Kuomba msaada \r (Zaburi 40:13-17) \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. \q1 \v 1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie. \q1 \v 2 Wale wanaotafuta kuniua, \q2 waaibishwe na kufadhaishwa; \q1 wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, \q2 warudishwe nyuma kwa aibu. \q1 \v 3 Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!” \q2 na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. \q1 \v 4 Lakini wote wanaokutafuta \q2 washangilie na kukufurahia, \q1 wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, \q2 “Mwenyezi Mungu ni mkuu!” \b \q1 \v 5 Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji; \q2 Ee Mungu, unijie haraka. \q1 Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, usikawie. \c 71 \cl Zaburi 71 \s1 Kuomba ulinzi na msaada maishani \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, nimekukimbilia wewe, \q2 usiache nikaaibika kamwe. \q1 \v 2 Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, \q2 unitegee sikio lako uniokoe. \q1 \v 3 Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, \q2 mahali nitakapokimbilia kila wakati; \q1 toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe \q2 ni mwamba wangu na ngome yangu. \q1 \v 4 Ee Mungu wangu uniokoe kutoka mkono wa mwovu, \q2 kutoka makucha ya watu wapotovu na wakatili. \b \q1 \v 5 Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, \q2 tegemeo langu tangu ujana wangu. \q1 \v 6 Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, \q2 ulinitoa tumboni mwa mama yangu. \q2 Nitakusifu wewe daima. \q1 \v 7 Nimekuwa ishara mbaya kwa wengi, \q2 lakini wewe ni kimbilio langu imara. \q1 \v 8 Kinywa changu kimejazwa sifa zako, \q2 nikitangaza utukufu wako mchana kutwa. \b \q1 \v 9 Usinitupe wakati wa uzee, \q2 wala usiniache nguvu zangu zinapopungua. \q1 \v 10 Kwa maana adui zangu wananisengenya, \q2 wale wanaotaka kuniua wanapanga njama. \q1 \v 11 Wanasema, “Mungu amemwacha, \q2 mkimbilieni mkamkamate, \q2 kwani hakuna wa kumwokoa.” \q1 \v 12 Ee Mungu, usiwe mbali nami, \q2 njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu. \q1 \v 13 Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, \q2 wale wanaotaka kunidhuru \q2 na wafunikwe kwa dharau na fedheha. \b \q1 \v 14 Lakini mimi nitatumaini siku zote; \q2 nitakusifu zaidi na zaidi. \b \q1 \v 15 Kinywa changu kitasimulia haki yako, \q2 wokovu wako mchana kutwa, \q2 ingawa sifahamu kipimo chake. \q1 \v 16 Ee Bwana Mungu Mwenyezi, nitakuja \q2 na kutangaza matendo yako makuu, \q2 nitatangaza haki yako, yako peke yako. \q1 \v 17 Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, \q2 hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu. \q1 \v 18 Ee Mungu, usiniache, \q2 hata nikiwa mzee wa mvi, \q1 hadi nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, \q2 nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye. \b \q1 \v 19 Ee Mungu, haki yako imefika juu Lakini mimi mbingu, \q2 wewe ambaye umefanya mambo makuu. \q2 Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe? \q1 \v 20 Ingawa umenifanya nipate taabu nyingi na chungu, \q2 utanihuisha tena, \q1 kutoka vilindi vya dunia \q2 utaniinua tena. \q1 \v 21 Utaongeza heshima yangu \q2 na kunifariji tena. \b \q1 \v 22 Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi \q2 kwa ajili ya uaminifu wako; \q1 Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, \q2 nitakuimbia sifa kwa zeze. \q1 \v 23 Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha \q2 ninapokuimbia sifa, \q2 mimi, ambaye umenikomboa. \q1 \v 24 Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki \q2 mchana kutwa, \q1 kwa maana wale waliotaka kunidhuru, \q2 wameaibishwa na kufadhaishwa. \c 72 \cl Zaburi 72 \s1 Maombi kwa ajili ya mfalme \d Zaburi ya Sulemani. \q1 \v 1 Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, \q2 mwana wa mfalme kwa haki yako. \q1 \v 2 Atawaamua watu wako kwa haki, \q2 watu wako walioonewa kwa haki. \q1 \v 3 Milima italeta mafanikio kwa watu, \q2 vilima tunda la haki. \q1 \v 4 Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu \q2 na atawaokoa watoto wa wahitaji, \q2 ataponda mdhalimu. \b \q1 \v 5 Atadumu kama jua linavyodumu, kama mwezi, vizazi vyote. \q1 \v 6 Atakuwa kama mvua inavyonyesha juu ya shamba lililofyekwa, \q2 kama manyunyu yanavyonyeshea ardhi. \q1 \v 7 Katika siku zake wenye haki watastawi; \q2 mafanikio yatakuwepo hadi mwezi utakapokoma. \b \q1 \v 8 Atatawala kutoka bahari hadi bahari \q2 na kutoka Mto\f + \fr 72:8 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f* hadi miisho ya dunia. \q1 \v 9 Makabila ya jangwani watamsujudia, \q2 na adui zake wataramba mavumbi. \q1 \v 10 Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali \q2 watamletea ushuru; \q1 wafalme wa Sheba na Seba \q2 watampa zawadi. \q1 \v 11 Wafalme wote watamsujudia \q2 na mataifa yote yatamtumikia. \b \q1 \v 12 Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, \q2 aliyeonewa asiye na wa kumsaidia. \q1 \v 13 Atawahurumia wanyonge na wahitaji \q2 na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. \q1 \v 14 Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, \q2 kwani damu yao ni ya thamani machoni pake. \b \q1 \v 15 Aishi maisha marefu! \q2 Na apewe dhahabu ya Sheba. \q1 Watu wamwombee daima \q2 na kumbariki mchana kutwa. \q1 \v 16 Nafaka ijae tele katika nchi yote, \q2 juu ya vilele vya vilima na istawi. \q1 Tunda lake na listawi kama Lebanoni, \q2 listawi kama majani ya kondeni. \q1 \v 17 Jina lake na lidumu milele, \q2 na lidumu kama jua. \b \q1 Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, \q2 nao watamwita aliyebarikiwa. \b \q1 \v 18 Ahimidiwe Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, \q2 ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu. \q1 \v 19 Jina lake tukufu lihimidiwe milele, \q2 ulimwengu wote ujae utukufu wake. \qc Amen na Amen. \b \b \q1 \v 20 Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese. \c 73 \ms Kitabu cha Tatu \mr (Zaburi 73–89) \cl Zaburi 73 \s1 Haki ya Mwenyezi Mungu \d Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, \q2 kwa wale ambao mioyo yao ni safi. \b \q1 \v 2 Bali mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; \q2 nilikuwa karibu kuanguka. \q1 \v 3 Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna \q2 nilipoona kufanikiwa kwa waovu. \b \q1 \v 4 Wao hawana taabu; \q2 miili yao ina afya na nguvu\f + \fr 73:4 \fr*\ft au \ft*\fqa hawana maumivu katika kufa kwao\fqa*\f*. \q1 \v 5 Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, \q2 wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine. \q1 \v 6 Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, \q2 wamejivika jeuri. \q1 \v 7 Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, \q2 majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hayana kikomo. \q1 \v 8 Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, \q2 katika majivuno yao wanatishia kutesa. \q1 \v 9 Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, \q2 nazo ndimi zao humiliki duniani. \q1 \v 10 Kwa hiyo watu wao huwageukia \q2 na kunywa maji tele\f + \fr 73:10 \fr*\ft au \ft*\fqa na kupokea yote wasemayo\fqa*\f*. \q1 \v 11 Wanasema, “Mungu awezaje kujua? \q2 Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” \b \q1 \v 12 Hivi ndivyo walivyo waovu: \q2 siku zote hawajali, \q2 wanaongezeka katika utajiri. \b \q1 \v 13 Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, \q2 ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia. \q1 \v 14 Mchana kutwa nimetaabika, \q2 nimeadhibiwa kila asubuhi. \b \q1 \v 15 Kama ningesema, “Nitasema hivi,” \q2 ningekuwa nimewasaliti watoto wako. \q1 \v 16 Nilipojaribu kuelewa haya yote, \q2 yalikuwa magumu kwangu kuelewa. \q1 \v 17 Hadi nilipoingia patakatifu pa Mungu, \q2 ndipo nilitambua mwisho wao. \b \q1 \v 18 Hakika unawaweka mahali pa utelezi, \q2 unawaangusha chini kwa uharibifu. \q1 \v 19 Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, \q2 wanatoweshwa kabisa na vitisho! \q1 \v 20 Kama ndoto mtu aamkapo, \q2 hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, \q2 utawatowesha kama ndoto. \b \q1 \v 21 Moyo wangu ulipohuzunishwa, \q2 na roho yangu ilipotiwa uchungu, \q1 \v 22 nilikuwa mpumbavu na mjinga, \q2 nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. \b \q1 \v 23 Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, \q2 umenishika mkono wangu wa kuume. \q1 \v 24 Unaniongoza kwa ushauri wako, \q2 hatimaye utaniingiza katika utukufu. \q1 \v 25 Nani niliye naye mbinguni ila wewe? \q2 Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. \q1 \v 26 Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, \q2 bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu \q2 na fungu langu milele. \b \q1 \v 27 Wale walio mbali nawe wataangamia, \q2 unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako. \q1 \v 28 Lakini kwangu mimi, \q2 ni vyema kuwa karibu na Mungu. \q1 Nimemfanya Bwana Mungu Mwenyezi kimbilio langu; \q2 nami nitayasimulia matendo yako yote. \c 74 \cl Zaburi 74 \s1 Maombi kwa ajili ya taifa \d Utenzi wa Asafu. \q1 \v 1 Ee Mungu, mbona umetukataa milele? \q2 Mbona hasira yako inatoka moshi \q2 juu ya kondoo wa malisho yako? \q1 \v 2 Kumbuka watu uliowanunua zamani, \q2 kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: \q2 Mlima Sayuni, ambamo uliishi. \q1 \v 3 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, \q2 uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu. \b \q1 \v 4 Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, \q2 wanaweka bendera zao kama alama. \q1 \v 5 Walifanya kama watu wanaotumia mashoka \q2 kukata kichaka cha miti. \q1 \v 6 Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa \q2 kwa mashoka na vishoka vyao. \q1 \v 7 Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu, \q2 wakayanajisi makao ya Jina lako. \q1 \v 8 Walisema mioyoni mwao, \q2 “Tutawaponda kabisa!” \q1 Walichoma kila mahali Mungu \q2 alipoabudiwa katika nchi. \q1 \v 9 Hatukupewa ishara za miujiza; \q2 hakuna manabii waliobaki, \q1 hakuna yeyote kati yetu ajuaye \q2 hali hii itachukua muda gani. \b \q1 \v 10 Ee Mungu, mtesi atakudhihaki hadi lini? \q2 Je, adui watalitukana jina lako milele? \q1 \v 11 Kwa nini unazuia mkono wako, \q2 mkono wako wa kuume? \q1 Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako \q2 na uwaangamize! \b \q1 \v 12 Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, \q2 unaleta wokovu duniani. \q1 \v 13 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; \q2 ulivunja vichwa vya mnyama mkubwa wa baharini. \q1 \v 14 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani\f + \fr 74:14 \fr*\ft Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.\ft*\f*, \q2 nawe ukamtoa kama chakula kwa viumbe vya jangwani. \q1 \v 15 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, \q2 ulikausha mito iliyokuwa ikitiririka daima. \q1 \v 16 Mchana ni wako, na usiku ni wako pia; \q2 uliziweka jua na mwezi. \q1 \v 17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, \q2 ulifanya kiangazi na masika. \b \q1 \v 18 Ee Mwenyezi Mungu, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, \q2 jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako. \q1 \v 19 Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama mwitu; \q2 usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele. \q1 \v 20 Likumbuke agano lako, \q2 maana mara kwa mara mambo ya jeuri \q2 yamejaa katika sehemu za giza nchini. \q1 \v 21 Usiruhusu waliodhulumiwa warudi nyuma kwa aibu; \q2 maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako. \b \q1 \v 22 Inuka, Ee Mungu, ujitetee; \q2 kumbuka jinsi wapumbavu \q2 wanavyokudhihaki mchana kutwa. \q1 \v 23 Usipuuze makelele ya watesi wako, \q2 ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo. \c 75 \cl Zaburi 75 \s1 Mwenyezi Mungu ni mwamuzi \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu”. Zaburi ya Asafu. Wimbo. \q1 \v 1 Ee Mungu, tunakushukuru, \q2 tunakushukuru wewe, \q1 kwa kuwa jina lako li karibu; \q2 watu husimulia matendo yako ya ajabu. \b \q1 \v 2 Unasema, “Ninachagua wakati maalum; \q2 ni mimi nihukumuye kwa haki. \q1 \v 3 Dunia inapotetemeka na watu wake wote, \q2 ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara. \q1 \v 4 Kwa wale wenye majivuno ninasema, \q2 ‘Msijisifu tena,’ \q2 kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu. \q1 \v 5 Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; \q2 msiseme kwa kiburi.’ ” \b \q1 \v 6 Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi \q2 au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. \q1 \v 7 Bali Mungu ndiye ahukumuye: \q2 Humshusha huyu na kumkweza mwingine. \q1 \v 8 Mkononi mwa Mwenyezi Mungu kuna kikombe \q2 kilichojaa mvinyo unaotoka povu \q2 uliochanganywa na vikolezo; \q1 huumimina, nao waovu wote wa dunia \q2 hunywa hata tone la mwisho. \b \q1 \v 9 Bali mimi, nitatangaza hili milele; \q2 nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. \q1 \v 10 Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, \q2 bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu. \c 76 \cl Zaburi 76 \s1 Mungu wa Israeli ni mhukumu wa dunia yote \d Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo. \q1 \v 1 Katika Yuda, Mungu anajulikana, \q2 jina lake ni kuu katika Israeli. \q1 \v 2 Hema lake liko Salemu, \q2 makao yake katika Sayuni. \q1 \v 3 Huko alivunja mishale iliyowaka, \q2 ngao na panga, silaha za vita. \b \q1 \v 4 Wewe unang’aa kwa mwanga, \q2 mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori. \q1 \v 5 Mashujaa hulala wametekwa nyara, \q2 hulala usingizi wao wa mwisho; \q1 hakuna hata mmoja wa watu wa vita \q2 anayeweza kuinua mikono yake. \q1 \v 6 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, \q2 farasi na gari la vita vilikaa kimya. \q1 \v 7 Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. \q2 Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika? \q1 \v 8 Ulitamka hukumu kutoka mbinguni, \q2 nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya: \q1 \v 9 wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, \q2 kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. \q1 \v 10 Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, \q2 na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi. \b \q1 \v 11 Wekeni nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuzitimiza; \q2 nchi zote za jirani na walete zawadi \q2 kwa Yule astahiliye kuogopwa. \q1 \v 12 Huvunja roho za watawala; \q2 anaogopwa na wafalme wa dunia. \c 77 \cl Zaburi 77 \s1 Matendo makuu ya Mwenyezi Mungu yanakumbukwa \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Nilimlilia Mungu ili anisaidie, \q2 nilimlilia Mungu ili anisikie. \q1 \v 2 Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, \q2 usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka \q2 na nafsi yangu ilikataa kufarijika. \b \q1 \v 3 Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; \q2 nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. \q1 \v 4 Ulizuia macho yangu kufumba; \q2 nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema. \q1 \v 5 Nilitafakari kuhusu siku zilizopita, \q2 miaka mingi iliyopita, \q1 \v 6 nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. \q2 Moyo wangu ulitafakari \q2 na roho yangu ikauliza: \b \q1 \v 7 “Je, Bwana atakataa milele? \q2 Je, hatatenda mema tena? \q1 \v 8 Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? \q2 Je, ahadi yake imekoma nyakati zote? \q1 \v 9 Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? \q2 Je, katika hasira amezuia fadhili zake?” \b \q1 \v 10 Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: \q2 lakini nitakumbuka \q1 miaka ya mkono wa kuume \q2 wa Aliye Juu Sana.” \q1 \v 11 Nitayakumbuka matendo ya Mwenyezi Mungu; \q2 naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. \q1 \v 12 Nitazitafakari kazi zako zote \q2 na kuyawaza matendo yako makuu. \b \q1 \v 13 Ee Mungu, njia zako ni takatifu. \q1 Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? \q1 \v 14 Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, \q2 umeonesha uwezo wako kati ya mataifa. \q1 \v 15 Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, \q2 uzao wa Yakobo na Yusufu. \b \q1 \v 16 Maji yalikuona, Ee Mungu, \q2 maji yalikuona yakakimbia, \q2 vilindi vilitetemeka. \q1 \v 17 Mawingu yalimwaga maji, \q2 mbingu zikatoa ngurumo kwa radi; \q2 mishale yako ilimetameta huku na huko. \q1 \v 18 Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, \q2 umeme wako wa radi ukaangaza dunia, \q2 nchi ikatetemeka na kutikisika. \q1 \v 19 Njia yako ilipita baharini, \q2 mapito yako kwenye maji makuu, \q2 ingawa nyayo zako hazikuonekana. \b \q1 \v 20 Uliongoza watu wako kama kundi \q2 kwa mkono wa Musa na Haruni. \c 78 \cl Zaburi 78 \s1 Mwenyezi Mungu na watu wake \d Utenzi wa Asafu. \q1 \v 1 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, \q2 sikilizeni maneno ya kinywa changu. \q1 \v 2 Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, \q2 nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: \q1 \v 3 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, \q2 yale ambayo baba zetu walituambia. \q1 \v 4 Hatutayaficha kwa watoto wao; \q2 tutakiambia kizazi kijacho \q1 matendo yastahiliyo sifa ya Mwenyezi Mungu, \q2 uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. \q1 \v 5 Aliagiza amri kwa Yakobo \q2 na akaweka sheria katika Israeli, \q1 ambazo aliwaamuru baba zetu \q2 wawafundishe watoto wao, \q1 \v 6 ili kizazi kijacho kizijue, \q2 pamoja na watoto ambao watazaliwa, \q2 nao pia wapate kuwaeleza watoto wao. \q1 \v 7 Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, \q2 nao hawangesahau matendo yake, \q2 bali wangezishika amri zake. \q1 \v 8 Hawangefanana na baba zao, \q2 waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, \q1 ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwa Mungu, \q2 ambao roho zao hazikumwamini. \b \q1 \v 9 Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, \q2 walikimbia siku ya vita. \q1 \v 10 Hawakulishika agano la Mungu, \q2 na walikataa kuishi kwa sheria yake. \q1 \v 11 Walisahau aliyokuwa ameyatenda, \q2 maajabu aliyokuwa amewaonesha. \q1 \v 12 Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, \q2 huko Soani, katika nchi ya Misri. \q1 \v 13 Aliigawanya bahari akawapitisha, \q2 alifanya maji yasimame imara kama ukuta. \q1 \v 14 Aliwaongoza kwa wingu mchana, \q2 na kwa nuru ya moto usiku kucha. \q1 \v 15 Alipasua miamba jangwani \q2 na akawapa maji tele kama bahari, \q1 \v 16 alitoa vijito kutoka jabali lililochongoka, \q2 akayafanya maji yatiririke kama mito. \b \q1 \v 17 Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, \q2 wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana. \q1 \v 18 Kwa makusudi walimjaribu Mungu, \q2 wakidai vyakula walivyovitamani. \q1 \v 19 Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, \q2 “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani? \q1 \v 20 Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, \q2 vijito vikatiririka maji mengi. \q1 Lakini je, aweza kutupatia chakula pia? \q2 Je, anaweza kuwapatia watu wake nyama?” \q1 \v 21 Mwenyezi Mungu alipowasikia, alikasirika sana, \q2 moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, \q2 na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli, \q1 \v 22 kwa kuwa hawakumwamini Mungu, \q2 wala kuutumainia ukombozi wake. \q1 \v 23 Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu \q2 na kufungua milango ya mbingu, \q1 \v 24 akawanyeshea mana ili watu wale; \q2 aliwapa nafaka ya mbinguni. \q1 \v 25 Watu walikula mkate wa malaika, \q2 akawatumia chakula chote ambacho wangeweza kula. \q1 \v 26 Aliachia upepo wa mashariki kutoka mbingu \q2 na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. \q1 \v 27 Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, \q2 ndege warukao kama mchanga wa pwani. \q1 \v 28 Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, \q2 kuzunguka mahema yao yote. \q1 \v 29 Walikula na kusaza, \q2 kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani. \q1 \v 30 Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, \q2 hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao, \q1 \v 31 hasira ya Mungu ikawaka juu yao, \q2 akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, \q2 akiwaangusha vijana wa Israeli. \b \q1 \v 32 Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, \q2 licha ya maajabu yake, hawakuamini. \q1 \v 33 Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili \q2 na miaka yao katika vitisho. \q1 \v 34 Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, \q2 waliosalia walimtafuta, \q2 walimgeukia tena kwa shauku. \q1 \v 35 Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, \q2 kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. \q1 \v 36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, \q2 wakisema uongo kwa ndimi zao, \q1 \v 37 mioyo yao haikuwa thabiti kwake, \q2 wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. \q1 \v 38 Hata hivyo alikuwa na huruma, \q2 alisamehe maovu yao \q2 na hakuwaangamiza. \q1 Mara kwa mara alizuia hasira yake, \q2 wala hakuchochea ghadhabu yake yote. \q1 \v 39 Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, \q2 upepo upitao ambao haurudi. \b \q1 \v 40 Mara ngapi walimwasi jangwani \q2 na kumhuzunisha nyikani! \q1 \v 41 Walimjaribu Mungu mara kwa mara, \q2 wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. \q1 \v 42 Hawakukumbuka uwezo wake, \q2 siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, \q1 \v 43 siku aliyoonesha ishara zake za ajabu huko Misri, \q2 maajabu yake huko Soani. \q1 \v 44 Aligeuza mito yao kuwa damu, \q2 hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao. \q1 \v 45 Aliwapelekea makundi ya inzi wakawala, \q2 na vyura wakawaharibu. \q1 \v 46 Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, \q2 mazao yao kwa nzige. \q1 \v 47 Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe \q2 na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji. \q1 \v 48 Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, \q2 akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi. \q1 \v 49 Aliwafungulia hasira yake kali, \q2 ghadhabu yake, hasira na uadui, \q2 na kundi la malaika wa kuharibu. \q1 \v 50 Aliitengenezea njia hasira yake, \q2 hakuwaepusha na kifo, \q2 bali aliwaachia tauni. \q1 \v 51 Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, \q2 matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu. \q1 \v 52 Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, \q2 akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani. \q1 \v 53 Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, \q2 bali bahari iliwameza adui zao. \q1 \v 54 Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, \q2 hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa. \q1 \v 55 Aliyafukuza mataifa mbele yao, \q2 na kuwagawia nchi zao kama urithi, \q2 aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao. \b \q1 \v 56 Lakini wao walimjaribu Mungu, \q2 na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, \q2 wala hawakuzishika sheria zake. \q1 \v 57 Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, \q2 wakawa wasioweza kutegemewa \q2 kama upinde wenye kasoro. \q1 \v 58 Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia, \q2 wakachochea wivu wake kwa sanamu zao. \q1 \v 59 Mungu alipowasikia, alikasirika sana, \q2 akamkataa Israeli kabisa. \q1 \v 60 Akaiacha maskani ya Shilo, \q2 hema alilokuwa ameliweka katikati ya wanadamu. \q1 \v 61 Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, \q2 utukufu wake mikononi mwa adui. \q1 \v 62 Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, \q2 akaukasirikia sana urithi wake. \q1 \v 63 Moto uliwaangamiza vijana wao, \q2 na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, \q1 \v 64 makuhani wao waliuawa kwa upanga, \q2 wala wajane wao hawakuweza kulia. \b \q1 \v 65 Ndipo Bwana alipoamka kama kuamka usingizini, \q2 kama shujaa anavyoamka \q2 kutoka bumbuazi la mvinyo. \q1 \v 66 Aliwapiga na kuwashinda adui zake, \q2 akawatia katika aibu ya milele. \q1 \v 67 Ndipo alipoyakataa mahema ya Yusufu, \q2 hakulichagua kabila la Efraimu, \q1 \v 68 lakini alilichagua kabila la Yuda, \q2 Mlima Sayuni, ambao aliupenda. \q1 \v 69 Alijenga patakatifu pake kama vilele, \q2 kama dunia ambayo aliimarisha milele. \q1 \v 70 Akamchagua Daudi mtumishi wake \q2 na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. \q1 \v 71 Kutoka kuchunga kondoo alimleta \q2 kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, \q2 wa Israeli urithi wake. \q1 \v 72 Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, \q2 kwa mikono ya ustadi aliwaongoza. \c 79 \cl Zaburi 79 \s1 Maombi kwa ajili ya wokovu wa taifa \d Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako, \q2 wamelinajisi Hekalu lako takatifu, \q2 wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. \q1 \v 2 Wametoa maiti za watumishi \q2 kuwa chakula cha ndege wa angani \q1 na nyama ya watakatifu wako \q2 kwa wanyama wa nchi. \q1 \v 3 Wamemwaga damu kama maji \q2 kuzunguka Yerusalemu yote, \q2 wala hakuna yeyote wa kuwazika. \q1 \v 4 Tumekuwa kitu cha aibu kwa majirani zetu, \q2 cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. \b \q1 \v 5 Hata lini, Ee Mwenyezi Mungu? Je, wewe utakasirika milele? \q2 Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? \q1 \v 6 Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali, \q2 juu ya falme za hao wasioliitia jina lako, \q1 \v 7 kwa maana wamemrarua Yakobo \q2 na kuharibu nchi ya makao yake. \q1 \v 8 Usituhesabie dhambi za baba zetu, \q2 huruma yako na itujie hima, \q2 kwa maana tu wahitaji mno. \b \q1 \v 9 Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie, \q2 kwa ajili ya utukufu wa jina lako; \q1 tuokoe na kutusamehe dhambi zetu \q2 kwa ajili ya jina lako. \q1 \v 10 Kwa nini mataifa waseme, \q2 “Yuko wapi Mungu wenu?” \q1 Mbele ya macho yetu, \q2 dhihirisha kati ya mataifa \q1 kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa \q2 ya watumishi wako. \q1 \v 11 Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako; \q2 kwa nguvu za mkono wako \q2 hifadhi wale waliohukumiwa kufa. \b \q1 \v 12 Walipize majirani zetu mara saba \q2 aibu walizovurumisha kwako, Ee Bwana. \q1 \v 13 Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako, \q2 tutakusifu milele; \q1 tutasimulia sifa zako \q2 kizazi hadi kizazi. \c 80 \cl Zaburi 80 \s1 Maombi kwa ajili ya kuponywa kwa taifa \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano”. Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, \q2 wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; \q1 wewe uketiye kwenye kiti cha enzi \q2 katikati ya makerubi, angaza \q2 \v 2 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. \q1 Uamshe nguvu zako, \q2 uje utuokoe. \b \q1 \v 3 Ee Mungu, uturejeshe, \q2 utuangazie uso wako, \q2 ili tuweze kuokolewa. \b \q1 \v 4 Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 hata lini hasira yako itawaka \q2 dhidi ya maombi ya watu wako? \q1 \v 5 Umewalisha kwa mkate wa machozi, \q2 umewafanya wanywe machozi bakuli tele. \q1 \v 6 Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa majirani zetu, \q2 na adui zetu wanatudhihaki. \b \q1 \v 7 Ee Mungu wa majeshi ya mbinguni, uturejeshe; \q2 utuangazie uso wako, \q2 nasi tuweze kuokolewa. \b \q1 \v 8 Ulileta mzabibu kutoka Misri, \q2 ukawafukuza mataifa, ukaupanda. \q1 \v 9 Uliandaa shamba kwa ajili yake, \q2 mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. \q1 \v 10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, \q2 matawi yake yakafunika mierezi mikubwa. \q1 \v 11 Matawi yake yalienea hadi Baharini\f + \fr 80:11 \fr*\ft pengine ni \ft*\fqa Bahari ya Mediterania\fqa*\f*, \q2 machipukizi yake hadi kwenye Mto\f + \fr 80:11 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f*. \b \q1 \v 12 Mbona umebomoa kuta zake \q2 ili wote wapitao karibu \q2 wazichume zabibu zake? \q1 \v 13 Nguruwe mwitu wanauharibu, \q2 na viumbe wa kondeni hujilisha humo. \q1 \v 14 Turudie, Ee Mungu wa majeshi ya mbinguni! \q2 Tazama chini kutoka mbinguni na uone! \q1 Linda mzabibu huu, \q2 \v 15 mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, \q1 mwana uliyemlea \q2 kwa ajili yako mwenyewe. \b \q1 \v 16 Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, \q2 unapowakemea, watu wako huangamia. \q1 \v 17 Mkono wako na utulie juu ya mtu aliye katika mkono wako wa kuume, \q2 mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe. \q1 \v 18 Ndipo hatutakuacha tena, \q2 utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako. \b \q1 \v 19 Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, uturejeshe; \q1 utuangazie uso wako, \q2 ili tuweze kuokolewa. \c 81 \cl Zaburi 81 \s1 Wimbo wa sikukuu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; \q2 mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! \q1 \v 2 Anzeni wimbo, pigeni matari, \q2 pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri. \b \q1 \v 3 Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume \q2 wakati wa Mwandamo wa Mwezi, \q1 na wakati wa mwezi mpevu, \q2 katika siku ya Sikukuu yetu; \q1 \v 4 hii ni amri kwa Israeli, \q2 agizo la Mungu wa Yakobo. \q1 \v 5 Aliiweka iwe kama sheria kwa Yusufu \q2 alipotoka dhidi ya Misri, \q2 huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa. \b \q1 \v 6 Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; \q2 mikono yao iliwekwa huru kutoka kwa kikapu. \q1 \v 7 Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, \q2 nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; \q2 nilikujaribu katika maji ya Meriba. \b \q1 \v 8 “Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: \q2 laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli! \q1 \v 9 Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; \q2 msimsujudie mungu wa kigeni. \q1 \v 10 Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wako, \q2 niliyekutoa nchi ya Misri. \q1 Panua sana kinywa chako \q2 nami nitakijaza. \b \q1 \v 11 “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; \q2 Israeli hakunitii. \q1 \v 12 Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao \q2 wafuate mashauri yao wenyewe. \b \q1 \v 13 “Laiti watu wangu wangenisikiliza, \q2 laiti Israeli wangefuata njia zangu, \q1 \v 14 ningewatiisha adui zao kwa haraka, \q2 na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! \q1 \v 15 Wale wanaomchukia Mwenyezi Mungu wangejikunyata mbele zake, \q2 na adhabu yao ingedumu milele. \q1 \v 16 Bali ninyi mngelishwa ngano iliyo bora, \q2 na kuwatosheleza kwa asali inayotoka kwenye mwamba.” \c 82 \cl Zaburi 82 \s1 Maombi kwa ajili ya kutaka haki \d Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Mungu anaongoza kusanyiko kuu, \q2 anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: \b \q1 \v 2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki \q2 na kuonesha upendeleo kwa waovu? \q1 \v 3 Teteeni wanyonge na yatima, \q2 tunzeni haki za maskini na waliodhulumiwa. \q1 \v 4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji, \q2 wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. \b \q1 \v 5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. \q2 Wanatembea gizani; \q2 misingi yote ya dunia imetikisika. \b \q1 \v 6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; \q2 ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ \q1 \v 7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; \q2 mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” \b \q1 \v 8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, \q2 kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako. \c 83 \cl Zaburi 83 \s1 Maombi kwa ajili ya kushindwa kwa adui za Israeli \d Wimbo. Zaburi ya Asafu. \q1 \v 1 Ee Mungu, usikae kimya, \q2 usinyamaze, Ee Mungu, usikae mbali. \q1 \v 2 Tazama watesi wako wanafanya fujo, \q2 jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao. \q1 \v 3 Kwa ujanja, wanapanga njama dhidi ya watu wako; \q2 wanapanga hila dhidi ya wale unaowapenda. \q1 \v 4 Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, \q2 ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.” \b \q1 \v 5 Kwa nia moja wanapanga njama pamoja, \q2 wanafanya muungano dhidi yako, \q1 \v 6 mahema ya Edomu na Waishmaeli, \q2 ya Wamoabu na Wahagari, \q1 \v 7 Gebali\f + \fr 83:7 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bubilo\fqa*\f*, Amoni na Amaleki, \q2 Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro. \q1 \v 8 Hata Ashuru wameungana nao \q2 kuwapa nguvu wazao wa Lutu. \b \q1 \v 9 Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, \q2 na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini \q2 hapo kijito cha Kishoni, \q1 \v 10 ambao waliangamia huko Endori \q2 na wakawa kama kinyesi juu ya ardhi. \q1 \v 11 Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, \q2 watawala wao kama Zeba na Salmuna, \q1 \v 12 ambao walisema, “Na tumiliki maeneo \q2 ya malisho ya Mungu.” \b \q1 \v 13 Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, \q2 kama makapi yapeperushwayo na upepo. \q1 \v 14 Kama vile moto unavyoteketeza msitu \q2 au mwali wa moto unavyounguza milima, \q1 \v 15 wafuatilie kwa tufani yako \q2 na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako. \q1 \v 16 Funika nyuso zao kwa aibu \q2 ili watu walitafute jina lako, Ee Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 17 Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, \q2 na waangamie kwa aibu. \q1 \v 18 Hebu wajue kuwa wewe, ambaye jina lako ni Mwenyezi Mungu, \q2 kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote. \c 84 \cl Zaburi 84 \s1 Kuionea shauku nyumba ya Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 makao yako yapendeza kama nini! \q1 \v 2 Nafsi yangu inatamani sana, \q2 naam, hata kuona shauku, \q2 kwa ajili ya nyua za Mwenyezi Mungu; \q1 moyo wangu na mwili wangu \q2 vinamlilia Mungu Aliye Hai. \b \q1 \v 3 Hata shomoro amejipatia makao, \q2 mbayuwayu amejipatia kiota \q2 mahali awezapo kuweka makinda yake: \q1 mahali karibu na madhabahu yako, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 Mfalme wangu na Mungu wangu. \q1 \v 4 Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, \q2 wanaokusifu wewe daima. \b \q1 \v 5 Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, \q2 na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. \q1 \v 6 Wanapopita katika Bonde la Baka\f + \fr 84:6 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Bonde la Vilio\fqa*\f*, \q2 hulifanya mahali pa chemchemi, \q2 pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi\f + \fr 84:6 \fr*\ft au \ft*\fqa baraka\fqa*\f*. \q1 \v 7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu, \q2 hadi kila mmoja afikapo \q2 mbele za Mungu huko Sayuni. \b \q1 \v 8 Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 sikia maombi yangu; \q2 nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. \q1 \v 9 Ee Mungu, uitazame ngao yetu, \q2 mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. \b \q1 \v 10 Siku moja katika nyua zako ni bora \q2 kuliko siku elfu mahali pengine; \q1 afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu \q2 kuliko kukaa katika mahema ya waovu. \q1 \v 11 Kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu ni jua na ngao; \q2 Mwenyezi Mungu hutoa wema na heshima; \q1 hakuna kitu chema anachowanyima \q2 wale ambao hawana hatia. \b \q1 \v 12 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 heri mtu anayekutumaini wewe. \c 85 \cl Zaburi 85 \s1 Maombi kwa ajili ya ustawi wa taifa \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, ulionesha wema kwa nchi yako. \q2 Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.\f + \fr 85:1 \fr*\ft au \ft*\fqa Uliwarudisha mateka wa Yakobo.\fqa*\f* \q1 \v 2 Ulisamehe uovu wa watu wako, \q2 na kufunika dhambi zao zote. \q1 \v 3 Uliweka kando ghadhabu yako yote \q2 na umegeuka na kuiacha hasira yako kali. \b \q1 \v 4 Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, \q2 nawe uiondoe chuki yako juu yetu. \q1 \v 5 Je, utatukasirikia milele? \q2 Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? \q1 \v 6 Je, hutatuhuisha tena, \q2 ili watu wako wakufurahie? \q1 \v 7 Utuoneshe upendo wako usiokoma, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 utupe wokovu wako. \b \q1 \v 8 Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Mwenyezi Mungu; \q2 anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: \q2 lakini nao wasirudie upumbavu. \q1 \v 9 Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, \q2 ili utukufu wake udumu katika nchi yetu. \b \q1 \v 10 Upendo na uaminifu hukutana pamoja, \q2 haki na amani hubusiana. \q1 \v 11 Uaminifu huchipua kutoka nchi, \q2 haki hutazama chini kutoka mbinguni. \q1 \v 12 Naam, hakika Mwenyezi Mungu atatoa kilicho chema, \q2 nayo nchi yetu itazaa mavuno yake. \q1 \v 13 Haki itatangulia mbele yake \q2 na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake. \c 86 \cl Zaburi 86 \s1 Kuomba msaada \d Maombi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, sikia na unijibu, \q2 kwa maana mimi ni maskini na mhitaji. \q1 \v 2 Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, \q2 wewe ni Mungu wangu, \q2 mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. \q1 \v 3 Ee Bwana, nihurumie mimi, \q2 kwa maana ninakuita mchana kutwa. \q1 \v 4 Mpe mtumishi wako furaha, \q2 kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, \q2 ninainua nafsi yangu. \b \q1 \v 5 Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, \q2 umejaa upendo kwa wote wakuitao. \q1 \v 6 Ee Mwenyezi Mungu, sikia maombi yangu, \q2 sikiliza kilio changu unihurumie. \q1 \v 7 Katika siku ya shida yangu nitakuita, \q2 kwa maana wewe utanijibu. \b \q1 \v 8 Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, \q2 hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. \q1 \v 9 Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya \q2 yatakuja na kuabudu mbele zako; \q2 wataliletea utukufu jina lako. \q1 \v 10 Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu; \q2 wewe peke yako ndiwe Mungu. \b \q1 \v 11 Ee Mwenyezi Mungu, nifundishe njia yako, \q2 nami nitaenda katika kweli yako; \q1 nipe moyo usiositasita, \q2 ili niweze kulicha jina lako. \q1 \v 12 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote; \q2 nitaliadhimisha jina lako milele. \q1 \v 13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; \q2 umeniokoa kutoka vilindi vya kaburi\f + \fr 86:13 \fr*\ft Kaburi hapa ina maana ya \ft*\fqa Sheol \fqa*\ft kwa Kiebrania, yaani \ft*\fqa Kuzimu.\fqa*\f*. \b \q1 \v 14 Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; \q2 kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: \q2 watu wasiokuheshimu wewe. \q1 \v 15 Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, \q2 si mwepesi wa hasira, \q2 bali ni mwingi wa upendo na uaminifu. \q1 \v 16 Nigeukie na unihurumie; \q2 mpe mtumishi wako nguvu zako, \q2 mwokoe mwana wa mjakazi wako\f + \fr 86:16 \fr*\ft au \ft*\fqa mwokoe mwanao mwaminifu\fqa*\f*. \q1 \v 17 Nipe ishara ya wema wako, \q2 ili adui zangu waione nao waaibishwe, \q1 kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 umenisaidia na kunifariji. \c 87 \cl Zaburi 87 \s1 Sifa za Yerusalemu \d Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. \q1 \v 1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; \q2 \v 2 Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni \q2 kuliko makao yote ya Yakobo. \q1 \v 3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, \q2 ee mji wa Mungu: \q1 \v 4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu\f + \fr 87:4 \fr*\ft jina la ushairi la \ft*\fqa Misri\fqa*\f* na Babeli \q2 miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: \q1 Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, \q2 nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” \b \q1 \v 5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, \q2 “Huyu na yule walizaliwa humo, \q1 naye Aliye Juu Sana mwenyewe \q2 atamwimarisha.” \q1 \v 6 Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa: \q2 “Huyu alizaliwa Sayuni.” \q1 \v 7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, \q2 “Chemchemi zangu zote ziko kwako.” \c 88 \cl Zaburi 88 \s1 Kilio kwa ajili ya kuomba msaada \d Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu uniokoaye, \q2 nimelia mbele zako usiku na mchana. \q1 \v 2 Maombi yangu yafike mbele zako, \q2 utegee kilio changu sikio lako. \b \q1 \v 3 Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, \q2 na maisha yangu yanakaribia kaburi\f + \fr 88:3 \fr*\ft Kaburi hapa maana yake ni \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\ft ; kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol.\fqa*\f*. \q1 \v 4 Nimehesabiwa miongoni mwa wale wanaoshuka shimoni; \q2 niko kama mtu asiye na nguvu. \q1 \v 5 Nimetengwa pamoja na wafu, \q2 kama waliochinjwa walalao kaburini, \q1 ambao huwakumbuki tena, \q2 ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako. \b \q1 \v 6 Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, \q2 katika vina vya giza nene. \q1 \v 7 Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, \q2 umenigharikisha kwa mawimbi yako yote. \b \q1 \v 8 Umenitenga na rafiki zangu wa karibu \q2 na kunifanya chukizo kwao. \q1 Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka; \q2 \v 9 nuru ya macho yangu \q2 imefifia kwa ajili ya huzuni. \b \q1 Ee Mwenyezi Mungu, ninakuita kila siku, \q2 ninakunyooshea wewe mikono yangu. \q1 \v 10 Je, wewe huwaonesha wafu maajabu yako? \q2 Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu? \b \q1 \v 11 Je, upendo wako hutangazwa kaburini, \q2 uaminifu wako katika Uharibifu\f + \fr 88:11 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Abadon\fqa*\f*? \q1 \v 12 Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, \q2 au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu? \b \q1 \v 13 Lakini ninakulilia wewe, Ee Mwenyezi Mungu, unisaidie; \q2 asubuhi maombi yangu huja mbele zako. \q1 \v 14 Ee Mwenyezi Mungu, kwa nini unanikataa \q2 na kunificha uso wako? \b \q1 \v 15 Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; \q2 nimepatwa na mapigo yako, nami nimekata tamaa. \q1 \v 16 Ghadhabu yako imepita juu yangu; \q2 mapigo yako yameniangamiza. \q1 \v 17 Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko; \q2 zimenimeza kabisa. \q1 \v 18 Umeniondolea rafiki na wapendwa wangu; \q2 giza limekuwa rafiki yangu wa karibu kuliko wote. \c 89 \cl Zaburi 89 \s1 Wimbo wakati wa taabu ya kitaifa \d Utenzi wa Ethani Mwezrahi. \q1 \v 1 Nitaimba kuhusu upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu milele; \q2 kwa kinywa changu nitavijulisha \q2 vizazi vyote uaminifu wako. \q1 \v 2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele \q2 na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. \b \q1 \v 3 Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, \q2 nimemwapia mtumishi wangu Daudi, \q1 \v 4 ‘Nitaimarisha uzao wako milele \q2 na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ” \b \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, mbingu zinayasifu maajabu yako, \q2 uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu. \q1 \v 6 Kwa kuwa ni nani katika mbingu \q2 anayeweza kulinganishwa na Mwenyezi Mungu? \q1 Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni \q2 aliye kama Mwenyezi Mungu? \q1 \v 7 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, \q2 anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka. \q1 \v 8 Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 ni nani aliye kama wewe? \q1 Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni mwenye nguvu, \q2 na uaminifu wako unakuzunguka. \b \q1 \v 9 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; \q2 mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza. \q1 \v 10 Wewe ulimponda Rahabu\f + \fr 89:10 \fr*\ft jina la \ft*\fqa Misri \fqa*\ft kwa fumbo\ft*\f* \q2 kama mmoja wa waliochinjwa; \q1 kwa mkono wako wenye nguvu, \q2 uliwatawanya adui zako. \q1 \v 11 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, \q2 uliuwekea ulimwengu msingi \q2 pamoja na vyote vilivyomo. \q1 \v 12 Uliumba kaskazini na kusini; \q2 Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. \q1 \v 13 Mkono wako umejaa uwezo; \q2 mkono wako una nguvu, \q2 mkono wako wa kuume umetukuka. \b \q1 \v 14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; \q2 upendo na uaminifu vinakutangulia. \q1 \v 15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, \q2 wanaotembea katika mwanga \q2 wa uwepo wako, Ee Mwenyezi Mungu. \q1 \v 16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, \q2 wanafurahi katika haki yako. \q1 \v 17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, \q2 kwa wema wako unatukuza pembe\f + \fr 89:17 \fr*\ft pembe inawakilisha nguvu\ft*\f* yetu. \q1 \v 18 Naam, ngao yetu ni mali ya Mwenyezi Mungu, \q2 na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. \b \q1 \v 19 Ulizungumza wakati fulani katika maono, \q2 kwa watu wako waaminifu, ukasema: \q1 “Nimeweka nguvu kwa shujaa, \q2 nimemwinua kijana miongoni mwa watu. \q1 \v 20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, \q2 na nimempaka mafuta yangu matakatifu. \q1 \v 21 Kitanga changu kitamtegemeza, \q2 hakika mkono wangu utamtia nguvu. \q1 \v 22 Hakuna adui atakayemtoza ushuru, \q2 hakuna mtu mwovu atakayemtesa. \q1 \v 23 Nitawaponda adui zake mbele zake \q2 na kuwaangamiza watesi wake. \q1 \v 24 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, \q2 kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. \q1 \v 25 Nitauweka mkono wake juu ya bahari, \q2 mkono wake wa kuume juu ya mito. \q1 \v 26 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, \q2 Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’ \q1 \v 27 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, \q2 aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia. \q1 \v 28 Nitadumisha upendo wangu kwake milele, \q2 na agano langu naye litakuwa imara. \q1 \v 29 Nitaudumisha uzao wake milele, \q2 kiti chake cha utawala kama mbingu zinavyodumu. \b \q1 \v 30 “Kama wanawe wataacha amri yangu \q2 na wasifuate sheria zangu, \q1 \v 31 wakihalifu maagizo yangu \q2 na kutoshika amri zangu, \q1 \v 32 nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, \q2 uovu wao kwa kuwapiga; \q1 \v 33 lakini sitauondoa upendo wangu kwake, \q2 wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. \q1 \v 34 Mimi sitavunja agano langu \q2 wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. \q1 \v 35 Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, \q2 nami sitamdanganya Daudi: \q1 \v 36 kwamba uzao wake utaendelea milele, \q2 na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua; \q1 \v 37 kitaimarishwa milele kama mwezi, \q2 shahidi mwaminifu angani.” \b \q1 \v 38 Lakini wewe umemkataa, umemdharau, \q2 umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako. \q1 \v 39 Umelikana agano lako na mtumishi wako, \q2 na umelinajisi taji lake mavumbini. \q1 \v 40 Umebomoa kuta zake zote, \q2 na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu. \q1 \v 41 Wote wapitao karibu wamemnyang’anya mali yake; \q2 amekuwa dharau kwa majirani zake. \q1 \v 42 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, \q2 umewafanya watesi wake wote washangilie. \q1 \v 43 Umegeuza makali ya upanga wake, \q2 na hukumpa msaada katika vita. \q1 \v 44 Umeikomesha fahari yake, \q2 na kukiangusha kiti chake cha enzi. \q1 \v 45 Umezifupisha siku za ujana wake, \q2 umemfunika kwa vazi la aibu. \b \q1 \v 46 Hata lini, Ee Mwenyezi Mungu? Utajificha milele? \q2 Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini? \q1 \v 47 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. \q2 Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu! \q1 \v 48 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, \q2 au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi\f + \fr 89:48 \fr*\ft Kaburi hapa maana yake ni \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\ft ; kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol.\fqa*\f*? \b \q1 \v 49 Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, \q2 ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi? \q1 \v 50 Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, \q2 jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote, \q1 \v 51 dhihaka ambazo kwazo adui zako \q2 wamenisimanga, Ee Mwenyezi Mungu, \q1 ambazo kwazo wamesimanga \q2 kila hatua ya mpakwa mafuta wako. \b \b \q1 \v 52 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu milele! \qc Amen na Amen. \c 90 \ms Kitabu cha Nne \mr (Zaburi 90–106) \cl Zaburi 90 \s1 Umilele wa Mwenyezi Mungu na udhaifu wa mwanadamu \d Maombi ya Musa, mtu wa Mungu. \q1 \v 1 Bwana, wewe umekuwa makao yetu \q2 katika vizazi vyote. \q1 \v 2 Kabla ya kuzaliwa milima \q2 au hujaumba dunia na ulimwengu, \q2 wewe ni Mungu tangu milele hata milele. \b \q1 \v 3 Huwarudisha watu mavumbini, \q2 ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” \q1 \v 4 Kwa maana kwako miaka elfu \q2 ni kama siku moja iliyokwisha pita, \q2 au kama kesha la usiku. \q1 \v 5 Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo, \q2 nao ni kama majani machanga ya asubuhi: \q1 \v 6 ingawa asubuhi yanachipua, \q2 ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka. \b \q1 \v 7 Tumeangamizwa kwa hasira yako \q2 na tumetishwa kwa ghadhabu yako. \q1 \v 8 Umeyaweka maovu yetu mbele yako, \q2 dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako. \q1 \v 9 Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako, \q2 tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza. \q1 \v 10 Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, \q2 au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, \q2 lakini yote ni ya shida na taabu, \q2 nazo zapita haraka, nasi twatoweka. \b \q1 \v 11 Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako? \q2 Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa \q2 kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako. \q1 \v 12 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, \q2 ili tujipatie moyo wa hekima. \b \q1 \v 13 Ee Mwenyezi Mungu, uwe na huruma! Utakawia hata lini? \q2 Wahurumie watumishi wako. \q1 \v 14 Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma, \q2 ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote. \q1 \v 15 Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, \q2 kulingana na miaka tuliyotaabika. \q1 \v 16 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, \q2 utukufu wako kwa watoto wao. \b \q1 \v 17 Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; \q2 uzithibitishe kazi za mikono yetu: \q2 naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu. \c 91 \cl Zaburi 91 \s1 Mwenyezi Mungu mlinzi wetu \q1 \v 1 Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, \q2 atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.\f + \fr 91:1 \fr*\ft Mwenyezi hapa ina maana ya \ft*\fqa Shaddai \fqa*\ft kwa Kiebrania.\ft*\f* \q1 \v 2 Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, \q2 Mungu wangu, ninayemtumaini.” \b \q1 \v 3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, \q2 na maradhi ya kuambukiza ya kuua. \q1 \v 4 Atakufunika kwa manyoya yake, \q2 chini ya mabawa yake utapata kimbilio, \q2 uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. \q1 \v 5 Hutaogopa vitisho vya usiku, \q2 wala mshale urukao mchana, \q1 \v 6 wala maradhi ya kuambukiza \q2 yanayonyemelea gizani, \q2 wala tauni iharibuyo adhuhuri. \q1 \v 7 Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, \q2 kumi elfu mkono wako wa kuume, \q2 lakini haitakukaribia wewe. \q1 \v 8 Utatazama tu kwa macho yako \q2 na kuona adhabu ya waovu. \b \q1 \v 9 Ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako; \q2 naam, Mwenyezi Mungu ambaye ni kimbilio langu; \q1 \v 10 basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, \q2 hakuna maafa yatalikaribia hema lako. \q1 \v 11 Kwa kuwa atawaagiza malaika wake kwa ajili yako, \q2 wakulinde katika njia zako zote. \q1 \v 12 Watakuchukua mikononi mwao, \q2 ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe. \q1 \v 13 Utawakanyaga simba na nyoka wakali, \q2 simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. \b \q1 \v 14 Mwenyezi Mungu asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; \q2 nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu. \q1 \v 15 Ataniita, nami nitamjibu; \q2 nitakuwa pamoja naye katika taabu, \q2 nitamwokoa na kumheshimu. \q1 \v 16 Kwa siku nyingi nitamshibisha \q2 na kumwonesha wokovu wangu.” \c 92 \cl Zaburi 92 \s1 Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu \d Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. \q1 \v 1 Ni vyema kumshukuru Mwenyezi Mungu \q2 na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana, \q1 \v 2 kuutangaza upendo wako asubuhi, \q2 na uaminifu wako wakati wa usiku, \q1 \v 3 kwa zeze yenye nyuzi kumi \q2 na kwa sauti ya kinubi. \b \q1 \v 4 Ee Mwenyezi Mungu, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, \q2 nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako. \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, \q2 tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako! \q1 \v 6 Mjinga hafahamu, \q2 mpumbavu haelewi, \q1 \v 7 ingawa waovu huchipua kama majani \q2 na wote watendao maovu wanastawi, \q2 wataangamizwa milele. \b \q1 \v 8 Bali wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 utatukuzwa milele. \b \q1 \v 9 Ee Mwenyezi Mungu, hakika adui zako, \q2 hakika adui zako wataangamia. \q2 Wote watendao maovu watatawanyika. \q1 \v 10 Umeitukuza pembe\f + \fr 92:10 \fr*\ft pembe inawakilisha nguvu\ft*\f* yangu kama ile ya nyati dume, \q2 mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu. \q1 \v 11 Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, \q2 masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu. \b \q1 \v 12 Wenye haki watastawi kama mtende, \q2 watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni, \q1 \v 13 waliopandwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, \q2 watastawi katika nyua za Mungu wetu. \q1 \v 14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, \q2 watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, \q1 \v 15 wakitangaza, “Mwenyezi Mungu ni mkamilifu; \q2 yeye ni Mwamba wangu, \q2 na ndani yake hamna uovu.” \c 93 \cl Zaburi 93 \s1 Mwenyezi Mungu ni mkuu \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu; \q2 Mwenyezi Mungu amejivika utukufu \q2 tena amejivika nguvu. \q1 Dunia imewekwa imara, \q2 haitaondoshwa. \q1 \v 2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; \q2 wewe umekuwa tangu milele. \b \q1 \v 3 Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 bahari zimepaza sauti zake; \q2 bahari zimepaza sauti za mawimbi yake. \q1 \v 4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, \q2 ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: \q2 Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu. \b \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara; \q2 utakatifu umepamba nyumba yako \q2 pasipo mwisho. \c 94 \cl Zaburi 94 \s1 Mwenyezi Mungu, Mlipiza kisasi kwa ajili ya wenye haki \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, ulipizaye kisasi, \q2 Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa. \q1 \v 2 Ee Mhukumu wa dunia, inuka, \q2 uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili. \q1 \v 3 Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini waovu, \q2 hadi lini waovu watashangilia? \b \q1 \v 4 Wanamimina maneno ya kiburi, \q2 watenda maovu wote wamejaa majivuno. \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, wanawaponda watu wako; \q2 wanawatesa walio urithi wako. \q1 \v 6 Wanamchinja mjane na mgeni, \q2 na kuwaua yatima. \q1 \v 7 Nao husema, “Mwenyezi Mungu haoni, \q2 Mungu wa Yakobo hafahamu.” \b \q1 \v 8 Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu; \q2 enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima? \q1 \v 9 Je, aliyeweka sikio asisikie? \q2 Aliyeumba jicho asione? \q1 \v 10 Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu? \q2 Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa? \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu anajua mawazo ya mwanadamu; \q2 anajua kwamba ni ubatili. \b \q1 \v 12 Ee Mwenyezi Mungu, heri mtu anayeadhibishwa na wewe, \q2 mtu unayemfundisha kwa sheria yako, \q1 \v 13 unampa utulivu siku za shida, \q2 hadi shimo litakapokuwa limechimbwa \q2 kwa ajili ya mwovu. \q1 \v 14 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu hatawakataa watu wake, \q2 hatauacha urithi wake. \q1 \v 15 Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki, \q2 wote walio na mioyo minyofu wataifuata. \b \q1 \v 16 Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu? \q2 Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu? \q1 \v 17 Kama Mwenyezi Mungu hangenisaidia upesi, \q2 ningeishi katika kimya cha kifo. \q1 \v 18 Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” \q2 Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako ulinishikilia. \q1 \v 19 Wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, \q2 faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu. \b \q1 \v 20 Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe, \q2 ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake? \q1 \v 21 Huungana kuwashambulia wenye haki, \q2 kuwahukumu kufa wasio na hatia. \q1 \v 22 Lakini Mwenyezi Mungu amekuwa ngome yangu, \q2 na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia. \q1 \v 23 Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao \q2 na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao; \q2 Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, atawaangamiza. \c 95 \cl Zaburi 95 \s1 Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Njooni, tumwimbie Mwenyezi Mungu kwa furaha; \q2 tumfanyie kelele za shangwe \q2 Mwamba wa wokovu wetu. \q1 \v 2 Tuje mbele zake kwa shukrani, \q2 tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. \b \q1 \v 3 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu mkuu, \q2 mfalme mkuu juu ya miungu yote. \q1 \v 4 Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, \q2 na vilele vya milima ni mali yake. \q1 \v 5 Bahari ni yake, kwani ndiye aliyeifanya, \q2 na mikono yake iliumba nchi kavu. \b \q1 \v 6 Njooni, tusujudu, tumwabudu, \q2 tupige magoti mbele za Mwenyezi Mungu Muumba wetu, \q1 \v 7 kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, \q2 na sisi ni watu wa malisho yake, \q2 kondoo chini ya utunzaji wake. \b \q1 Mkiisikia sauti yake leo, \q2 \v 8 msiifanye mioyo yenu migumu \q2 kama mlivyofanya kule Meriba\f + \fr 95:8 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kugombana\fqa*\f*, \q1 kama mlivyofanya siku ile \q2 kule Masa\f + \fr 95:8 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kujaribiwa\fqa*\f* jangwani, \q1 \v 9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, \q2 ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu. \q1 \v 10 Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile, \q2 nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka, \q2 nao hawajazijua njia zangu.” \q1 \v 11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, \q2 “Kamwe hawataingia rahani mwangu.” \c 96 \cl Zaburi 96 \s1 Mwenyezi Mungu Mfalme mkuu \r (1 Nyakati 16:23-33) \q1 \v 1 Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya; \q2 mwimbieni Mwenyezi Mungu dunia yote. \q1 \v 2 Mwimbieni Mwenyezi Mungu, lisifuni jina lake; \q2 tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. \q1 \v 3 Tangazeni utukufu wake katika mataifa, \q2 matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. \b \q1 \v 4 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; \q2 yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. \q1 \v 5 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, \q2 lakini Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu. \q1 \v 6 Fahari na enzi viko mbele yake; \q2 nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. \b \q1 \v 7 Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi jamaa za mataifa, \q2 mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu. \q1 \v 8 Mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake; \q2 leteni sadaka na mje katika nyua zake. \q1 \v 9 Mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake; \q2 dunia yote na itetemeke mbele zake. \b \q1 \v 10 Semeni katika mataifa kwamba, “Mwenyezi Mungu anatawala.” \q1 Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; \q2 atawahukumu watu kwa uadilifu. \q1 \v 11 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; \q2 bahari na ivume, na vyote vilivyo ndani yake; \q1 \v 12 mashamba na yashangilie, \q2 pamoja na vyote vilivyomo. \q1 Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; \q2 \v 13 itaimba mbele za Mwenyezi Mungu kwa maana anakuja, \q2 anakuja kuihukumu dunia. \q1 Ataihukumu dunia kwa haki, \q2 na mataifa katika kweli yake. \c 97 \cl Zaburi 97 \s1 Mwenyezi Mungu Mtawala mkuu \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu anatawala, nchi na ifurahi, \q2 visiwa vyote vishangilie. \b \q1 \v 2 Mawingu na giza nene vinamzunguka, \q2 haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi. \q1 \v 3 Moto hutangulia mbele zake \q2 na huteketeza adui zake pande zote. \q1 \v 4 Umeme wake wa radi humulika dunia, \q2 nchi huona na kutetemeka. \q1 \v 5 Milima huyeyuka kama nta mbele za Mwenyezi Mungu, \q2 mbele za Bwana wa dunia yote. \q1 \v 6 Mbingu zinatangaza haki yake, \q2 na mataifa yote huona utukufu wake. \b \q1 \v 7 Wote waabuduo sanamu waaibishwa, \q2 wale wajisifiao sanamu: \q2 mwabuduni yeye, enyi miungu yote! \b \q1 \v 8 Sayuni husikia na kushangilia, \q2 vijiji vya Yuda vinafurahi \q2 kwa sababu ya hukumu zako, Ee Mwenyezi Mungu. \q1 \v 9 Kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; \q2 umetukuka sana juu ya miungu yote. \b \q1 \v 10 Wale wanaompenda Mwenyezi Mungu na wauchukie uovu, \q2 kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake \q2 na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu. \q1 \v 11 Nuru huangaza wenye haki \q2 na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. \q1 \v 12 Furahini katika Mwenyezi Mungu, enyi wenye haki, \q2 lisifuni jina lake takatifu. \c 98 \cl Zaburi 98 \s1 Mwenyezi Mungu Mtawala wa dunia \d Zaburi. \q1 \v 1 Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya, \q2 kwa maana ametenda mambo ya ajabu; \q1 kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu \q2 umemfanyia wokovu. \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu ameufanya wokovu wake ujulikane \q2 na amedhihirisha haki yake kwa mataifa. \q1 \v 3 Ameukumbuka upendo wake \q2 na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; \q1 miisho yote ya dunia imeuona \q2 wokovu wa Mungu wetu. \b \q1 \v 4 Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote, \q2 ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda; \q1 \v 5 mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa kinubi, \q2 kwa kinubi na sauti za kuimba, \q1 \v 6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: \q2 shangilieni kwa furaha mbele za Mwenyezi Mungu, aliye Mfalme. \b \q1 \v 7 Bahari na ivume na kila kilicho ndani yake, \q2 dunia na wote wanaoishi ndani yake. \q1 \v 8 Mito na ipige makofi, \q2 milima na iimbe pamoja kwa furaha, \q1 \v 9 vyote na viimbe mbele za Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana yuaja kuhukumu dunia. \q1 Atahukumu dunia kwa haki \q2 na mataifa kwa haki. \c 99 \cl Zaburi 99 \s1 Mwenyezi Mungu Mfalme mtakatifu \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu anatawala, \q2 mataifa na yatetemeke; \q1 anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi, \q2 dunia na itikisike. \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu ni mkuu katika Sayuni; \q2 ametukuzwa juu ya mataifa yote. \q1 \v 3 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: \q2 yeye ni mtakatifu! \b \q1 \v 4 Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, \q2 wewe umethibitisha adili; \q1 katika Yakobo umefanya \q2 yaliyo haki na sawa. \q1 \v 5 Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; \q2 yeye ni mtakatifu. \b \q1 \v 6 Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, \q2 Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; \q1 walimwita Mwenyezi Mungu, \q2 naye aliwajibu. \q1 \v 7 Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; \q2 walizishika sheria zake na amri alizowapa. \b \q1 \v 8 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 ndiwe uliyewajibu, \q1 kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, \q2 ingawa uliadhibu matendo yao mabaya. \q1 \v 9 Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, \q2 kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu. \c 100 \cl Zaburi 100 \s1 Dunia yote yaitwa kumsifu Mwenyezi Mungu \d Zaburi ya shukrani. \q1 \v 1 Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote. \q2 \v 2 Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha; \q2 njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. \q1 \v 3 Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu. \q2 Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; \q1 sisi tu watu wake, \q2 kondoo wa malisho yake. \b \q1 \v 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani \q2 na katika nyua zake kwa kusifu, \q2 mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. \q1 \v 5 Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema \q2 na fadhili zake zadumu milele; \q2 uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote. \c 101 \cl Zaburi 101 \s1 Ahadi ya kuishi kwa uadilifu na kwa haki \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nitaimba kuhusu upendo wako na haki yako; \q2 kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, nitaimba sifa. \q1 \v 2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: \q2 utakuja kwangu lini? \b \q1 Nitatembea nyumbani mwangu \q2 kwa moyo usio na lawama. \q1 \v 3 Sitaweka mbele ya macho yangu \q2 kitu kiovu. \b \q1 Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; \q2 hawatashikamana nami. \q1 \v 4 Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; \q2 nitajitenga na kila ubaya. \b \q1 \v 5 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, \q2 huyo nitamnyamazisha; \q1 mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi \q2 huyo sitamvumilia. \b \q1 \v 6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, \q2 ili waweze kuishi pamoja nami; \q1 yeye ambaye moyo wake hauna lawama \q2 atanitumikia. \b \q1 \v 7 Mdanganyifu hatakaa \q2 nyumbani mwangu, \q1 yeye asemaye kwa uongo \q2 hatasimama mbele yangu. \b \q1 \v 8 Kila asubuhi nitawanyamazisha \q2 waovu wote katika nchi; \q1 nitamkatilia mbali kila mtenda maovu \q2 kutoka mji wa Mwenyezi Mungu. \c 102 \cl Zaburi 102 \s1 Maombi ya mtu aliyechoka \d Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Mwenyezi Mungu. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, usikie maombi yangu; \q2 kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. \q1 \v 2 Usinifiche uso wako \q2 ninapokuwa katika shida. \q1 Unitegee sikio lako; \q2 ninapoita, unijibu kwa upesi. \b \q1 \v 3 Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi; \q2 mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. \q1 \v 4 Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani; \q2 ninasahau kula chakula changu. \q1 \v 5 Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu, \q2 nimebakia ngozi na mifupa. \q1 \v 6 Nimekuwa kama bundi wa jangwani, \q2 kama bundi kwenye magofu. \q1 \v 7 Nilalapo sipati usingizi; \q2 nimekuwa kama ndege mpweke \q2 kwenye paa la nyumba. \q1 \v 8 Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki; \q2 wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana. \q1 \v 9 Ninakula majivu kama chakula changu, \q2 nimechanganya kinywaji changu na machozi \q1 \v 10 kwa sababu ya ghadhabu yako kuu, \q2 kwa maana umeniinua na kunitupa kando. \q1 \v 11 Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, \q2 ninanyauka kama jani. \b \q1 \v 12 Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umeketi kwenye kiti chako cha enzi milele; \q2 sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote. \q1 \v 13 Utainuka na kuihurumia Sayuni, \q2 kwa maana ni wakati wa kumwonesha wema; \q2 wakati uliokubalika umewadia. \q1 \v 14 Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako, \q2 vumbi lake lenyewe hulionea huruma. \q1 \v 15 Mataifa wataogopa jina la Mwenyezi Mungu, \q2 wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako. \q1 \v 16 Kwa maana Mwenyezi Mungu ataijenga tena Sayuni \q2 na kutokea katika utukufu wake. \q1 \v 17 Ataitikia maombi ya mtu mkiwa, \q2 wala hatadharau hoja yao. \b \q1 \v 18 Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho, \q2 ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Mwenyezi Mungu: \q1 \v 19 “Mwenyezi Mungu alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu, \q2 alitazama dunia kutoka mbinguni, \q1 \v 20 kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa, \q2 na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.” \q1 \v 21 Kwa hiyo jina la Mwenyezi Mungu latangazwa huko Sayuni \q2 na sifa zake katika Yerusalemu, \q1 \v 22 wakati mataifa na falme zitakapokusanyika \q2 ili kumwabudu Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 23 Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu, \q2 akafupisha siku zangu. \q1 \v 24 Ndipo niliposema: \q2 “Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; \q2 miaka yako inaendelea vizazi vyote. \q1 \v 25 Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, \q2 nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. \q1 \v 26 Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu, \q2 zote zitachakaa kama vazi. \q1 Utazibadilisha kama nguo \q2 nazo zitaondoshwa. \q1 \v 27 Lakini wewe, U yeye yule, \q2 nayo miaka yako haikomi kamwe. \q1 \v 28 Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako; \q2 wazao wao wataimarishwa mbele zako.” \c 103 \cl Zaburi 103 \s1 Upendo wa Mwenyezi Mungu \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu. \q2 Vyote vilivyo ndani yangu \q2 vilihimidi jina lake takatifu. \q1 \v 2 Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu, \q2 wala usisahau wema wake wote: \q1 \v 3 akusamehe dhambi zako zote, \q2 akuponya magonjwa yako yote, \q1 \v 4 aukomboa uhai wako na kaburi, \q2 akuvika taji la upendo na huruma, \q1 \v 5 atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, \q2 ili ujana wako uhuishwe kama wa tai. \b \q1 \v 6 Mwenyezi Mungu hutenda haki, \q2 naye huwapa hukumu ya haki \q2 wote wanaodhulumiwa. \b \q1 \v 7 Alimjulisha Musa njia zake, \q2 na watu wa Israeli matendo yake. \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mwenye neema; \q2 si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo. \q1 \v 9 Yeye hatalaumu siku zote, \q2 wala haweki hasira yake milele, \q1 \v 10 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu \q2 wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. \q1 \v 11 Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia, \q2 ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; \q1 \v 12 kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, \q2 ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi. \q1 \v 13 Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, \q2 ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowahurumia wale wanaomcha; \q1 \v 14 kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, \q2 anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi. \q1 \v 15 Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, \q2 anachanua kama ua la kondeni; \q1 \v 16 upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, \q2 mahali pake hapalikumbuki tena. \q1 \v 17 Lakini kutoka milele hata milele \q2 upendo wa Mwenyezi Mungu uko kwa wale wamchao, \q2 nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: \q1 \v 18 kwa wale walishikao agano lake \q2 na kukumbuka kuyatii mausia yake. \b \q1 \v 19 Mwenyezi Mungu ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, \q2 na ufalme wake unatawala vitu vyote. \b \q1 \v 20 Mhimidini Mwenyezi Mungu, enyi malaika wake, \q2 ninyi mlio mashujaa, mnaozitii amri zake, \q2 ninyi mnaotii neno lake. \q1 \v 21 Mhimidini Mwenyezi Mungu, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, \q2 ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. \q1 \v 22 Mhimidini Mwenyezi Mungu, enyi kazi zake zote \q2 kila mahali katika milki yake. \b \q1 Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu. \c 104 \cl Zaburi 104 \s1 Kumsifu Muumba \q1 \v 1 Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu. \b \q1 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, \q2 umejivika utukufu na enzi. \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, \q2 amezitandaza mbingu kama hema, \q1 \v 3 na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. \q1 Huyafanya mawingu kuwa gari lake la vita, \q2 na hupanda kwenye mabawa ya upepo. \q1 \v 4 Huzifanya pepo kuwa wajumbe\f + \fr 104:4 \fr*\ft au \ft*\fqa malaika\fqa*\f* wake, \q2 na miali ya moto kuwa watumishi wake. \b \q1 \v 5 Ameiweka dunia kwenye misingi yake, \q2 haiwezi kamwe kuondoshwa. \q1 \v 6 Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, \q2 maji yalisimama juu ya milima. \q1 \v 7 Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, \q2 kwa sauti ya radi yako yakatoroka, \q1 \v 8 yakapanda milima, yakateremka mabondeni, \q2 hadi mahali pale ulipoyakusudia. \q1 \v 9 Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, \q2 kamwe hayataifunika dunia tena. \b \q1 \v 10 Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, \q2 hutiririka kati ya milima. \q1 \v 11 Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, \q2 punda-mwitu huzima kiu yao. \q1 \v 12 Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, \q2 huimba katika matawi. \q1 \v 13 Huinyeshea milima kutoka orofa zake, \q2 dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. \q1 \v 14 Huyafanya majani ya mifugo yaote, \q2 na mimea kwa watu kulima, \q2 wajipatie chakula kutoka ardhini: \q1 \v 15 divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, \q2 mafuta kwa ajili ya kung’arisha uso wake, \q2 na mkate wa kutia mwili nguvu. \q1 \v 16 Miti ya Mwenyezi Mungu inanyeshewa vizuri, \q2 mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. \q1 \v 17 Humo ndege hufanya viota vyao, \q2 korongo ana nyumba yake kwenye msunobari. \q1 \v 18 Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu; \q2 majabali ni kimbilio la pelele. \b \q1 \v 19 Mwezi hugawanya majira, \q2 na jua hutambua wakati wake wa kutua. \q1 \v 20 Unaleta giza, kunakuwa usiku, \q2 wanyama wote wa mwituni huzurura. \q1 \v 21 Simba hunguruma kwa mawindo yao, \q2 na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. \q1 \v 22 Jua huchomoza, nao huondoka, \q2 hurudi na kulala katika mapango yao. \q1 \v 23 Kisha wanadamu wanaenda kazini zao, \q2 katika kazi zao hadi jioni. \b \q1 \v 24 Ee Mwenyezi Mungu, jinsi matendo yako yalivyo mengi! \q2 Kwa hekima ulizifanya zote, \q2 dunia imejaa viumbe vyako. \q1 \v 25 Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, \q2 imejaa viumbe visivyo na idadi, \q2 vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. \q1 \v 26 Huko meli huenda na kurudi, \q2 pia Lewiathani\f + \fr 104:26 \fr*\ft Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.\ft*\f*, uliyemuumba acheze ndani yake. \b \q1 \v 27 Hawa wote wanakutazamia wewe, \q2 uwape chakula chao kwa wakati wake. \q1 \v 28 Wakati unawapa, \q2 wanakikusanya; \q1 unapofumbua mkono wako, \q2 wao wanashibishwa mema. \q1 \v 29 Unapoficha uso wako, \q2 wanapata hofu, \q1 unapoondoa pumzi yao, \q2 wanakufa na kurudi mavumbini. \q1 \v 30 Unapopeleka Roho wako, \q2 wanaumbwa, \q2 nawe huufanya upya uso wa dunia. \b \q1 \v 31 Utukufu wa Mwenyezi Mungu na udumu milele, \q2 Mwenyezi Mungu na azifurahie kazi zake: \q1 \v 32 yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, \q2 aigusaye milima, nayo ikatoa moshi. \b \q1 \v 33 Nitamwimbia Mwenyezi Mungu maisha yangu yote; \q2 nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. \q1 \v 34 Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, \q2 ninapofurahi katika Mwenyezi Mungu. \q1 \v 35 Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia \q2 na waovu wasiwepo tena. \b \q1 Ee nafsi yangu, msifu Mwenyezi Mungu. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 104:35 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \c 105 \cl Zaburi 105 \s1 Uaminifu wa Mwenyezi Mungu kwa Israeli \r (1 Nyakati 16:8-22) \q1 \v 1 Mshukuruni Mwenyezi Mungu, liitieni jina lake; \q2 wajulisheni mataifa aliyoyatenda. \q1 \v 2 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, \q2 waambieni matendo yake yote ya ajabu. \q1 \v 3 Lishangilieni jina lake takatifu, \q2 mioyo ya wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu na ifurahi. \q1 \v 4 Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake, \q2 utafuteni uso wake siku zote. \b \q1 \v 5 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, \q2 miujiza yake na hukumu alizozitamka, \q1 \v 6 enyi wazao wa Ibrahimu mtumishi wake, \q2 enyi wana wa Yakobo, wateule wake. \q1 \v 7 Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 hukumu zake ziko duniani kote. \b \q1 \v 8 Hulikumbuka agano lake milele, \q2 neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, \q1 \v 9 agano alilolifanya na Ibrahimu, \q2 kiapo alichomwapia Isaka. \q1 \v 10 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, \q2 kwa Israeli liwe agano la milele: \q1 \v 11 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani \q2 kuwa sehemu utakayoirithi.” \b \q1 \v 12 Walipokuwa wachache kwa idadi, \q2 wachache sana na wageni ndani yake, \q1 \v 13 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, \q2 kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. \q1 \v 14 Hakuruhusu mtu yeyote awadhulumu; \q2 kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: \q1 \v 15 “Msiwaguse niliowapaka mafuta; \q2 msiwadhuru manabii wangu.” \b \q1 \v 16 Akaiita njaa juu ya nchi \q2 na kuharibu chakula chao chote, \q1 \v 17 naye akatuma mtu mbele yao, \q2 Yusufu, aliyeuzwa kama mtumwa. \q1 \v 18 Walichubua miguu yake kwa minyororo, \q2 shingo yake ilifungwa kwa chuma, \q1 \v 19 hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, \q2 hadi neno la Mwenyezi Mungu lilipomthibitisha. \q1 \v 20 Mfalme alituma watu wakamfungua, \q2 mtawala wa watu alimwachia huru. \q1 \v 21 Alimfanya mkuu wa nyumba yake, \q2 mtawala wa vyote alivyokuwa navyo, \q1 \v 22 kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo, \q2 na kuwafundisha wazee wake hekima. \b \q1 \v 23 Kisha Israeli akaingia Misri, \q2 Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu. \q1 \v 24 Mwenyezi Mungu aliwafanya watu wake kuzaana sana; \q2 aliwafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao. \q1 \v 25 Aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, \q2 wakatenda hila dhidi ya watumishi wake. \q1 \v 26 Akamtuma Musa mtumishi wake, \q2 pamoja na Haruni, aliyemchagua. \q1 \v 27 Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, \q2 miujiza yake katika nchi ya Hamu. \q1 \v 28 Alituma giza na nchi ikajaa giza, \q2 kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake? \q1 \v 29 Aligeuza maji yao kuwa damu, \q2 ikasababisha samaki wao kufa. \q1 \v 30 Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia \q2 hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao. \q1 \v 31 Alisema, yakaja makundi ya inzi, \q2 na viroboto katika nchi yao yote. \q1 \v 32 Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe, \q2 yenye miali ya radi nchini yao yote, \q1 \v 33 akaharibu mizabibu yao na miti ya tini, \q2 na akaangamiza miti ya nchi yao. \q1 \v 34 Alisema, nzige wakaja, \q2 tunutu wasio na idadi, \q1 \v 35 wakala kila jani katika nchi yao, \q2 wakala mazao ya ardhi yao. \q1 \v 36 Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, \q2 matunda ya kwanza ya ujana wao wote. \b \q1 \v 37 Akawatoa Israeli katika nchi \q2 wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, \q1 wala hakuna hata mmoja \q2 kutoka makabila yao aliyejikwaa. \q1 \v 38 Misri ilifurahi walipoondoka, \q2 kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia. \q1 \v 39 Alitandaza wingu kama kifuniko, \q2 na moto kuwamulikia usiku. \q1 \v 40 Waliomba, naye akawaletea kware, \q2 akawashibisha kwa mkate wa mbinguni. \q1 \v 41 Alipasua mwamba, maji yakabubujika, \q2 yakatiririka jangwani kama mto. \b \q1 \v 42 Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, \q2 aliyompa Ibrahimu mtumishi wake. \q1 \v 43 Aliwatoa watu wake kwa furaha, \q2 wateule wake kwa kelele za shangwe, \q1 \v 44 akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali \q2 ambayo wengine walikuwa wameitaabikia: \q1 \v 45 alifanya haya ili wayashike mausia yake \q2 na kuzitii sheria zake. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 105:45 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \c 106 \cl Zaburi 106 \s1 Wema wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 106:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 106:48\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ni mwema; \q2 fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 2 Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Mwenyezi Mungu \q2 au kutangaza kikamilifu sifa zake? \q1 \v 3 Heri wale wanaodumisha haki, \q2 ambao daima wanafanya yaliyo mema. \q1 \v 4 Ee Mwenyezi Mungu, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, \q2 uwe msaada wangu unapowaokoa, \q1 \v 5 ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, \q2 niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, \q2 na kuungana na urithi wako katika kukusifu. \b \q1 \v 6 Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, \q2 tumekosa na tumetenda uovu. \q1 \v 7 Baba zetu walipokuwa Misri, \q2 hawakuzingatia maajabu yako, \q1 wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, \q2 bali waliasi kando ya bahari, \q2 ile Bahari ya Shamu. \q1 \v 8 Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, \q2 ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu. \q1 \v 9 Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, \q2 akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani. \q1 \v 10 Aliwaokoa mikononi mwa adui; \q2 kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa. \q1 \v 11 Maji yaliwafunika adui zao, \q2 hakunusurika hata mmoja. \q1 \v 12 Ndipo walipoamini ahadi zake, \q2 nao wakaimba sifa zake. \b \q1 \v 13 Lakini walisahau upesi aliyowatendea, \q2 wala hawakungojea ushauri wake. \q1 \v 14 Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, \q2 walimjaribu Mungu nyikani. \q1 \v 15 Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, \q2 lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha. \b \q1 \v 16 Kambini walimwonea wivu Musa, \q2 na pia Haruni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu. \q1 \v 17 Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, \q2 ikawazika Abiramu na kundi lake. \q1 \v 18 Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, \q2 mwali wa moto uliwateketeza waovu. \b \q1 \v 19 Huko Horebu walitengeneza ndama, \q2 na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma. \q1 \v 20 Waliubadilisha Utukufu wao \q2 kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani. \q1 \v 21 Walimsahau Mungu aliyewaokoa, \q2 aliyetenda mambo makuu huko Misri, \q1 \v 22 miujiza katika nchi ya Hamu \q2 na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu. \q1 \v 23 Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: \q2 kama Musa mteule wake, \q1 asingesimama kati yao na Mungu \q2 kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza. \b \q1 \v 24 Kisha waliidharau ile nchi nzuri, \q2 hawakuiamini ahadi yake. \q1 \v 25 Walinung’unika ndani ya mahema yao, \q2 wala hawakumtii Mwenyezi Mungu. \q1 \v 26 Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa \q2 kwamba atawafanya waanguke jangwani, \q1 \v 27 kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, \q2 na kuwatawanya katika nchi zote. \b \q1 \v 28 Walijifunga nira na Baali wa Peori, \q2 wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai. \q1 \v 29 Waliichochea hasira ya Mwenyezi Mungu, \q2 wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, \q2 nayo tauni ikazuka katikati yao. \q1 \v 30 Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, \q2 nayo tauni ikazuiliwa. \q1 \v 31 Hili likahesabiwa kwake haki, \q2 kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo. \b \q1 \v 32 Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Mwenyezi Mungu, \q2 janga likampata Musa kwa sababu yao; \q1 \v 33 kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, \q2 na maneno yasiyofaa yakatoka mdomoni kwa Musa. \b \q1 \v 34 Hawakuyaangamiza yale mataifa \q2 kama Mwenyezi Mungu alivyowaagiza, \q1 \v 35 bali walijichanganya na mataifa \q2 na wakazikubali desturi zao. \q1 \v 36 Waliabudu sanamu zao, \q2 zikawa mtego kwao. \q1 \v 37 Wakawatoa wana wao \q2 na binti zao dhabihu kwa mashetani. \q1 \v 38 Walimwaga damu isiyo na hatia, \q2 damu za wana wao wa kiume na wa kike, \q1 ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, \q2 nayo nchi ikanajisika kwa damu zao. \q1 \v 39 Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; \q2 kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba. \b \q1 \v 40 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawakasirikia watu wake \q2 na akauchukia sana urithi wake. \q1 \v 41 Akawakabidhi kwa mataifa \q2 na adui zao wakawatawala. \q1 \v 42 Adui zao wakawadhulumu \q2 na kuwatia chini ya mkono wao. \q1 \v 43 Mara nyingi aliwaokoa \q2 lakini walizama kwenye uasi, \q2 na wakajiharibu katika dhambi zao. \b \q1 \v 44 Lakini akaangalia mateso yao \q2 aliposikia kilio chao; \q1 \v 45 kwa ajili yao akakumbuka agano lake, \q2 na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake. \q1 \v 46 Akawafanya wahurumiwe \q2 na wote waliowashikilia mateka. \b \q1 \v 47 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tuokoe. \q2 Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, \q1 ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, \q2 na kushangilia katika sifa zako. \b \q1 \v 48 Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, \q2 tangu milele na hata milele. \q1 Watu wote na waseme, “Amen!” \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 107 \ms Kitabu cha Tano \mr (Zaburi 107–150) \cl Zaburi 107 \s1 Kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wema wake \q1 \v 1 Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa yeye ni mwema, \q2 fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 2 Waliokombolewa wa Mwenyezi Mungu na waseme hivi, \q2 wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, \q1 \v 3 wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, \q2 kutoka mashariki na magharibi, \q2 kutoka kaskazini na kusini. \b \q1 \v 4 Baadhi yao walitangatanga jangwani, \q2 hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi. \q1 \v 5 Walikuwa na njaa na kiu, \q2 nafsi zao zikadhoofika. \q1 \v 6 Ndipo walipomlilia Mwenyezi Mungu katika shida yao, \q2 naye akawaokoa kutoka taabu yao. \q1 \v 7 Akawaongoza kwa njia iliyo sawa \q2 hadi mji ambao wangeweza kuishi. \q1 \v 8 Basi na wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake usiokoma, \q2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, \q1 \v 9 kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, \q2 na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema. \b \q1 \v 10 Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, \q2 wafungwa wakiteseka katika minyororo, \q1 \v 11 kwa sababu waliasi dhidi ya maneno ya Mungu, \q1 na kudharau ushauri wa Aliye Juu Sana. \q1 \v 12 Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; \q2 walijikwaa na hapakuwa na mtu wa kuwasaidia. \q1 \v 13 Ndipo walipomlilia Mwenyezi Mungu katika shida yao, \q2 naye akawaokoa kutoka taabu yao. \q1 \v 14 Akawatoa katika giza na huzuni kuu \q2 na akavunja minyororo yao. \q1 \v 15 Basi na wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake usiokoma, \q2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, \q1 \v 16 kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba \q2 na kukata mapingo ya chuma. \b \q1 \v 17 Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, \q2 wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao. \q1 \v 18 Wakachukia kabisa vyakula vyote, \q2 wakakaribia malango ya mauti. \q1 \v 19 Ndipo walipomlilia Mwenyezi Mungu katika shida yao, \q2 naye akawaokoa kutoka taabu yao. \q1 \v 20 Akalituma neno lake na kuwaponya, \q2 akawaokoa kutoka maangamizi yao. \q1 \v 21 Basi na wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake usiokoma, \q2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. \q1 \v 22 Na watoe dhabihu za kushukuru, \q2 na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha. \b \q1 \v 23 Wengine walisafiri baharini kwa meli, \q2 walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu. \q1 \v 24 Waliziona kazi za Mwenyezi Mungu, \q2 matendo yake ya ajabu kilindini. \q1 \v 25 Kwa maana alisema na kuamsha tufani \q2 iliyoinua mawimbi juu. \q1 \v 26 Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini; \q2 katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka. \q1 \v 27 Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, \q2 ujanja wao ukafikia ukomo. \q1 \v 28 Ndipo walipomlilia Mwenyezi Mungu katika shida yao, \q2 naye akawatoa kwenye taabu yao. \q1 \v 29 Akatuliza dhoruba kwa mnong’ono, \q2 mawimbi ya bahari yakatulia. \q1 \v 30 Walifurahi ilipokuwa shwari, \q2 naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani. \q1 \v 31 Basi na wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake usiokoma, \q2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. \q1 \v 32 Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, \q2 na wamsifu katika baraza la wazee. \b \q1 \v 33 Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, \q2 chemchemi za maji zinazotiririka kuwa ardhi yenye kiu, \q1 \v 34 nchi inayozaa ikawa ya chumvi isiyofaa, \q2 kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo. \q1 \v 35 Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, \q2 nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zinazotiririka; \q1 \v 36 aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, \q2 nao wakajenga mji wangeweza kuishi. \q1 \v 37 Walilima mashamba na kupanda mizabibu, \q2 nayo ikazaa matunda mengi, \q1 \v 38 Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana, \q2 wala hakuruhusu mifugo yao kupungua. \b \q1 \v 39 Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa \q2 kwa kuonewa, maafa na huzuni. \q1 \v 40 Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu, \q2 aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia. \q1 \v 41 Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao, \q2 na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo. \q1 \v 42 Wanyofu wataona na kufurahi, \q2 lakini waovu wote watafunga vinywa vyao. \b \q1 \v 43 Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya, \q2 na atafakari upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu. \c 108 \cl Zaburi 108 \s1 Kuomba msaada dhidi ya adui \r (Zaburi 57:7-11; 60:5-12) \d Wimbo. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; \q2 nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. \q1 \v 2 Amka, kinubi na zeze! \q2 Nitayaamsha mapambazuko. \q1 \v 3 Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu, kati ya mataifa; \q2 nitaimba habari zako, katika jamaa za watu. \q1 \v 4 Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; \q2 uaminifu wako unazifikia anga. \q1 \v 5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, \q2 utukufu wako na uenee duniani kote. \b \q1 \v 6 Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, \q2 ili wale unaowapenda wapate kuokolewa. \q1 \v 7 Mungu amenena kutoka patakatifu pake: \q2 “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi \q2 na kulipima Bonde la Sukothi. \q1 \v 8 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu; \q2 Efraimu ni chapeo yangu, \q2 nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. \q1 \v 9 Moabu ni sinia langu la kunawia, \q2 juu ya Edomu natupa kiatu changu; \q2 nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” \b \q1 \v 10 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? \q2 Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? \q1 \v 11 Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, \q2 na hutoki tena na majeshi yetu? \q1 \v 12 Tuletee msaada dhidi ya adui, \q2 kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. \q1 \v 13 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, \q2 naye atawaponda adui zetu. \c 109 \cl Zaburi 109 \s1 Lalamiko la mtu aliye kwenye shida \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mungu, ninayekusifu, \q2 usiwe kimya, \q1 \v 2 kwa maana watu waovu na wadanganyifu \q2 wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; \q1 wasema dhidi yangu \q2 kwa ndimi za udanganyifu. \q1 \v 3 Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, \q2 wananishambulia bila sababu. \q1 \v 4 Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, \q2 lakini mimi ninawaombea. \q1 \v 5 Wananilipiza mabaya kwa mema, \q2 chuki badala ya urafiki wangu. \b \q1 \v 6 Agiza mtu mwovu ampinge, \q2 mshtaki\f + \fr 109:6 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Shetani\fqa*\f* asimame mkono wake wa kuume. \q1 \v 7 Anapohukumiwa, apatikane na hatia, \q2 nayo maombi yake yamhukumu. \q1 \v 8 Siku zake za kuishi na ziwe chache, \q2 nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine. \q1 \v 9 Watoto wake na waachwe yatima, \q2 mke wake na awe mjane. \q1 \v 10 Watoto wake na watangetange wakiomba, \q2 na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao. \q1 \v 11 Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, \q2 matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni. \q1 \v 12 Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema \q2 wala wa kuwahurumia yatima wake. \q1 \v 13 Uzao wake na ukatiliwe mbali, \q2 majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho. \q1 \v 14 Maovu ya baba zake na yakumbukwe \q2 mbele za Mwenyezi Mungu, \q1 dhambi ya mama yake \q2 isifutwe kamwe. \q1 \v 15 Dhambi zao na zibaki daima mbele za Mwenyezi Mungu, \q2 ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. \b \q1 \v 16 Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, \q2 bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, \q2 aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. \q1 \v 17 Alipenda kulaani, \q2 nayo laana ikampata; \q1 hakupenda kubariki, \q2 kwa hiyo baraka na ikae mbali naye. \q1 \v 18 Alivaa kulaani kama vazi lake, \q2 nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, \q2 kwenye mifupa yake kama mafuta. \q1 \v 19 Na iwe kama joho alilozungushiwa, \q2 kama mshipi aliofungiwa daima. \q1 \v 20 Haya na yawe malipo ya Mwenyezi Mungu kwa washtaki wangu, \q2 kwa wale wanaoninenea mabaya. \b \q1 \v 21 Lakini wewe, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, \q2 unitendee wema kwa ajili ya jina lako, \q2 uniokoe kwa wema wa pendo lako. \q1 \v 22 Maana mimi ni maskini na mhitaji, \q2 moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. \q1 \v 23 Ninafifia kama kivuli cha jioni, \q2 nimerushwa-rushwa kama nzige. \q1 \v 24 Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, \q2 mwili wangu umedhoofika na kukonda. \q1 \v 25 Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, \q2 wanionapo, hutikisa vichwa vyao. \b \q1 \v 26 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nisaidie, \q2 niokoe sawasawa na upendo wako. \q1 \v 27 Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, \q2 kwamba wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umetenda hili. \q1 \v 28 Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, \q2 watakaposhambulia wataaibishwa, \q2 lakini mtumishi wako atashangilia. \q1 \v 29 Washtaki wangu watavikwa fedheha, \q2 na kufunikwa na aibu kama joho. \b \q1 \v 30 Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Mwenyezi Mungu, \q2 katika umati mkubwa nitamsifu. \q1 \v 31 Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, \q2 kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu. \c 110 \cl Zaburi 110 \s1 Mwenyezi Mungu na mfalme wake mteule \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu: \q2 “Keti mkono wangu wa kuume, \q1 hadi nitakapowafanya adui zako \q2 kuwa mahali pa kuweka miguu yako.” \b \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; \q2 utatawala katikati ya adui zako. \q1 \v 3 Askari wako watajitolea kwa hiari \q2 katika siku yako ya vita. \q1 Ukiwa umevikwa fahari takatifu, \q2 kutoka tumbo la mapambazuko \q2 utapokea umande wa ujana wako\f + \fr 110:3 \fr*\ft au \ft*\fqa vijana wako watakujia kama umande\fqa*\f*. \b \q1 \v 4 Mwenyezi Mungu ameapa, \q2 naye hatabadilisha mawazo yake: \q2 “Wewe ni kuhani milele, \q2 kwa mfano wa Melkizedeki.” \b \q1 \v 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume, \q2 atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. \q1 \v 6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga \q2 na kuwaponda watawala wa dunia nzima. \q1 \v 7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia\f + \fr 110:7 \fr*\ft au \ft*\fqa Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka;\fqa*\f*; \q2 kwa hiyo atainua kichwa chake juu. \c 111 \cl Zaburi 111\f + \fr 111 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Sifa za Mwenyezi Mungu kwa matendo ya ajabu \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 111:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \b \q1 Nitamtukuza Mwenyezi Mungu kwa moyo wangu wote, \q2 katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko. \b \q1 \v 2 Kazi za Mwenyezi Mungu ni kuu, \q2 wote wanaopendezwa nazo huzitafakari. \q1 \v 3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, \q2 haki yake hudumu daima. \q1 \v 4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe, \q2 Mwenyezi Mungu ni mwenye neema na huruma. \q1 \v 5 Huwapa chakula wale wanaomcha, \q2 hulikumbuka agano lake milele. \q1 \v 6 Amewaonesha watu wake uwezo wa kazi zake, \q2 akiwapa nchi za mataifa mengine. \q1 \v 7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, \q2 mausia yake yote ni ya kuaminika. \q1 \v 8 Zinadumu milele na milele, \q2 zikifanyika kwa uaminifu na unyofu. \q1 \v 9 Aliwapa watu wake ukombozi, \q2 aliamuru agano lake milele: \q2 jina lake ni takatifu na la kuogopwa. \b \q1 \v 10 Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima, \q2 wote wanaozifuata amri zake wana busara. \q2 Sifa zake zadumu milele. \c 112 \cl Zaburi 112\f + \fr 112 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Baraka za mwenye haki \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 112:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \b \q1 Heri mtu yule amchaye Mwenyezi Mungu, \q2 mtu yule apendezwaye sana na amri zake. \b \q1 \v 2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, \q2 kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. \q1 \v 3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, \q2 haki yake hudumu milele. \q1 \v 4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, \q2 yule mwenye rehema, huruma na haki. \b \q1 \v 5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, \q2 anayefanya mambo yake kwa haki. \q1 \v 6 Hakika hatatikisika kamwe, \q2 mtu mwenye haki atakumbukwa milele. \q1 \v 7 Hataogopa habari mbaya, \q2 moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Mwenyezi Mungu. \q1 \v 8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, \q2 mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake. \q1 \v 9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; \q2 haki yake hudumu milele; \q2 pembe yake itatukuzwa kwa heshima. \b \q1 \v 10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa, \q2 atasaga meno yake na kutoweka, \q2 kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu. \c 113 \cl Zaburi 113 \s1 Kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wema wake \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 113:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 113:9\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Enyi watumishi wa Mwenyezi Mungu msifuni, \q2 lisifuni jina la Mwenyezi Mungu. \q1 \v 2 Jina la Mwenyezi Mungu na lisifiwe, \q2 sasa na hata milele. \q1 \v 3 Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, \q2 jina la Mwenyezi Mungu linapaswa kusifiwa. \b \q1 \v 4 Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya mataifa yote, \q2 utukufu wake juu ya mbingu. \q1 \v 5 Ni nani aliye kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 Yule aliyeketi kwenye kiti cha enzi huko juu, \q1 \v 6 ambaye huinama atazame chini \q2 aone mbingu na nchi? \b \q1 \v 7 Huwainua maskini kutoka mavumbini, \q2 na kuwanyanyua wahitaji \q2 kutoka lundo la majivu, \q1 \v 8 huwaketisha pamoja na wakuu, \q2 pamoja na wakuu wa watu wake. \q1 \v 9 Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, \q2 akiwa mama watoto mwenye furaha. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 114 \cl Zaburi 114 \s1 Maajabu ya Mwenyezi Mungu wakati Israeli walitoka Misri \q1 \v 1 Israeli alipotoka Misri, \q2 nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni, \q1 \v 2 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, \q2 Israeli akawa milki yake. \b \q1 \v 3 Bahari ilitazama ikakimbia, \q2 Yordani ulirudi nyuma, \q1 \v 4 milima ilirukaruka kama kondoo dume, \q2 vilima kama wana-kondoo. \b \q1 \v 5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, \q2 nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, \q1 \v 6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, \q2 enyi vilima, kama wana-kondoo? \b \q1 \v 7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, \q2 mbele za Mungu wa Yakobo, \q1 \v 8 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, \q2 mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji. \c 115 \cl Zaburi 115 \s1 Mwenyezi Mungu Mmoja wa kweli \q1 \v 1 Sio kwetu sisi, Ee Mwenyezi Mungu, sio kwetu sisi, \q2 bali utukufu ni kwa jina lako, \q1 kwa sababu ya upendo \q2 na uaminifu wako. \b \q1 \v 2 Kwa nini mataifa waseme, \q2 “Yuko wapi Mungu wao?” \q1 \v 3 Mungu wetu yuko mbinguni, \q2 naye hufanya lolote limpendezalo. \q1 \v 4 Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, \q2 zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. \q1 \v 5 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, \q2 zina macho, lakini haziwezi kuona; \q1 \v 6 zina masikio, lakini haziwezi kusikia, \q2 zina pua, lakini haziwezi kunusa; \q1 \v 7 zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, \q2 zina miguu, lakini haziwezi kutembea; \q2 wala koo zao haziwezi kutoa sauti. \q1 \v 8 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, \q2 vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. \b \q1 \v 9 Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Mwenyezi Mungu, \q2 yeye ni msaada na ngao yao. \q1 \v 10 Ee nyumba ya Haruni, mtumainini Mwenyezi Mungu, \q2 yeye ni msaada na ngao yao. \q1 \v 11 Ninyi mnaomcha, mtumainini Mwenyezi Mungu, \q2 yeye ni msaada na ngao yao. \b \q1 \v 12 Mwenyezi Mungu anatukumbuka na atatubariki: \q2 ataibariki nyumba ya Israeli, \q2 ataibariki nyumba ya Haruni, \q1 \v 13 atawabariki wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, \q2 wadogo kwa wakubwa. \b \q1 \v 14 Mwenyezi Mungu na awawezeshe kuongezeka, \q2 ninyi na watoto wenu. \q1 \v 15 Mbarikiwe na Mwenyezi Mungu \q2 Muumba wa mbingu na dunia. \b \q1 \v 16 Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Mwenyezi Mungu, \q2 lakini dunia amempa mwanadamu. \q1 \v 17 Sio wafu wanaomsifu Mwenyezi Mungu, \q2 wale wanaoshuka mahali pa kimya\f + \fr 115:17 \fr*\fq mahali pa kimya \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\ft ; kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol.\fqa*\f*, \q1 \v 18 bali ni sisi tunaomtukuza Mwenyezi Mungu, \q2 sasa na hata milele. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 115:18 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \c 116 \cl Zaburi 116 \s1 Shukrani kwa kuokolewa kutoka mauti \q1 \v 1 Nampenda Mwenyezi Mungu kwa maana amesikia sauti yangu; \q2 amesikia kilio changu ili anihurumie. \q1 \v 2 Kwa sababu amenitegea sikio lake, \q2 nitamwita siku zote za maisha yangu. \b \q1 \v 3 Kamba za mauti zilinizunguka, \q2 vitisho vya Kuzimu\f + \fr 116:3 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f* vilinipata, \q2 nikalemewa na taabu na huzuni. \q1 \v 4 Ndipo nikaliitia jina la Mwenyezi Mungu: \q2 “Ee Mwenyezi Mungu, niokoe!” \b \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu ni mwenye neema na haki, \q2 Mungu wetu ni mwingi wa huruma. \q1 \v 6 Mwenyezi Mungu huwalinda wanyenyekevu, \q2 nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. \b \q1 \v 7 Ee nafsi yangu, tulia tena, \q2 kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekuwa mwema kwako. \q1 \v 8 Kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 umeniokoa nafsi yangu na mauti, \q1 macho yangu kutokana na machozi, \q2 miguu yangu kutokana na kujikwaa, \q1 \v 9 ili niweze kutembea mbele za Mwenyezi Mungu, \q2 katika nchi ya walio hai. \q1 \v 10 Nilimwamini Mwenyezi Mungu, niliposema, \q2 “Mimi nimeteseka sana.” \q1 \v 11 Katika taabu yangu nilisema, \q2 “Wanadamu wote ni waongo.” \b \q1 \v 12 Nimrudishie Mwenyezi Mungu nini \q2 kwa wema wake wote alionitendea? \q1 \v 13 Nitakiinua kikombe cha wokovu \q2 na kulitangaza jina la Mwenyezi Mungu. \q1 \v 14 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Mwenyezi Mungu \q2 mbele za watu wake wote. \b \q1 \v 15 Kifo cha watakatifu kina thamani \q2 machoni pa Mwenyezi Mungu. \q1 \v 16 Ee Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mtumishi wako, \q2 mimi ni mtumishi wako, \q2 mwana wa mjakazi wako\f + \fr 116:16 \fr*\ft au \ft*\fqa mwanao mwaminifu\fqa*\f*; \q1 umeniweka huru \q2 toka katika minyororo yangu. \b \q1 \v 17 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru \q2 na kuliita jina la Mwenyezi Mungu. \q1 \v 18 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Mwenyezi Mungu \q2 mbele za watu wake wote, \q1 \v 19 katika nyua za nyumba ya Mwenyezi Mungu, \q2 katikati yako, ee Yerusalemu. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 116:19 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \c 117 \cl Zaburi 117 \s1 Sifa za Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu, enyi mataifa yote; \q2 mtukuzeni yeye, enyi watu wote. \q1 \v 2 Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, \q2 uaminifu wa Mwenyezi Mungu unadumu milele. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 117:2 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah.\fqa*\f* \c 118 \cl Zaburi 118 \s1 Shukrani kwa ajili ya ushindi \q1 \v 1 Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ni mwema; \q2 fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 2 Israeli na aseme sasa: \q2 “Fadhili zake zadumu milele.” \q1 \v 3 Nyumba ya Haruni na iseme sasa: \q2 “Fadhili zake zadumu milele.” \q1 \v 4 Wote wanaomcha Mwenyezi Mungu na waseme sasa: \q2 “Fadhili zake zadumu milele.” \b \q1 \v 5 Wakati wa maumivu yangu makuu, nilimlilia Mwenyezi Mungu, \q2 naye akanijibu kwa kuniweka huru. \q1 \v 6 Mwenyezi Mungu yuko pamoja nami, sitaogopa. \q2 Mwanadamu anaweza kunitenda nini? \q1 \v 7 Mwenyezi Mungu yuko pamoja nami, \q2 yeye ni msaidizi wangu. \q1 Nitawatazama adui zangu \q2 wakiwa wameshindwa. \b \q1 \v 8 Ni bora kumkimbilia Mwenyezi Mungu \q2 kuliko kumtumainia mwanadamu. \q1 \v 9 Ni bora kumkimbilia Mwenyezi Mungu \q2 kuliko kuwatumainia wakuu. \b \q1 \v 10 Mataifa yote yalinizunguka, \q2 lakini kwa jina la Mwenyezi Mungu naliwakatilia mbali. \q1 \v 11 Walinizunguka pande zote, \q2 lakini kwa jina la Mwenyezi Mungu naliwakatilia mbali. \q1 \v 12 Walinizunguka kama kundi la nyuki, \q2 lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; \q2 kwa jina la Mwenyezi Mungu naliwakatilia mbali. \b \q1 \v 13 Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, \q2 lakini Mwenyezi Mungu alinisaidia. \q1 \v 14 Mwenyezi Mungu ni nguvu yangu na wimbo wangu, \q2 yeye amefanyika wokovu wangu. \b \q1 \v 15 Sauti za shangwe na ushindi \q2 zinavuma kwenye hema za wenye haki: \q1 “Mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu \q2 umetenda mambo makuu! \q1 \v 16 Mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu \q2 umeinuliwa juu, \q1 mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu \q2 umetenda mambo makuu!” \b \q1 \v 17 Sitakufa, bali nitaishi, \q2 nami nitayatangaza matendo ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 18 Mwenyezi Mungu ameniadhibu vikali, \q2 lakini hakuniacha nife. \b \q1 \v 19 Nifungulie malango ya haki, \q2 nami nitaingia na kumshukuru Mwenyezi Mungu. \q1 \v 20 Hili ni lango la Mwenyezi Mungu \q2 ambalo wenye haki wanaweza kuliingia. \q1 \v 21 Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, \q2 umekuwa wokovu wangu. \b \q1 \v 22 Jiwe walilolikataa waashi, \q2 limekuwa jiwe kuu la pembeni. \q1 \v 23 Mwenyezi Mungu ametenda hili, \q2 nalo ni la kushangaza machoni petu. \q1 \v 24 Hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyoifanya, \q2 tushangilie na kufurahi ndani yake. \b \q1 \v 25 Ee Mwenyezi Mungu, tuokoe, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, utujalie mafanikio. \q1 \v 26 Heri yule ajaye kwa jina la Mwenyezi Mungu. \q2 Kutoka nyumba ya Mwenyezi Mungu tunakubariki. \q1 \v 27 Mwenyezi Mungu ndiye Mungu, \q2 naye ametuangazia nuru yake. \q1 Mkiwa na matawi mkononi, \q2 unganeni kwenye maandamano ya sikukuu \q2 hadi kwenye pembe za madhabahu. \b \q1 \v 28 Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, \q2 wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza. \b \q1 \v 29 Mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa kuwa ni mwema; \q2 fadhili zake zadumu milele. \c 119 \cl Zaburi 119\f + \fr 119:0 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi 22 za alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T).\ft*\f* \s1 Sifa za Torati ya Mwenyezi Mungu \s2 Kujifunza Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Heri wale walio waadilifu katika njia zao, \q2 wanaoenenda katika Torati ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 2 Heri wale wanaozishika shuhuda zake, \q2 wanaomtafuta kwa moyo wao wote. \q1 \v 3 Wasiofanya lolote lililo baya, \q2 wanaoenenda katika njia zake. \q1 \v 4 Umetoa maagizo yako \q2 ili tuyatii kwa ukamilifu. \q1 \v 5 Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara \q2 katika kuyatii maagizo yako! \q1 \v 6 Hivyo mimi sitaaibishwa \q2 ninapozingatia amri zako zote. \q1 \v 7 Nitakusifu kwa moyo mnyofu \q2 ninapojifunza sheria zako za haki. \q1 \v 8 Nitayatii maagizo yako; \q2 usiniache kabisa. \s2 Kutii Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 9 Kijana aisafishe njia yake jinsi gani? \q2 Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. \q1 \v 10 Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, \q2 usiniache niende mbali na amri zako. \q1 \v 11 Nimelificha neno lako moyoni mwangu \q2 ili nisikutende dhambi. \q1 \v 12 Uhimidiwe, Ee Mwenyezi Mungu; \q2 nifundishe maagizo yako. \q1 \v 13 Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote \q2 zinazotoka katika kinywa chako. \q1 \v 14 Ninafurahia kufuata sheria zako \q2 kama mtu afurahiaye mali nyingi. \q1 \v 15 Ninatafakari maagizo yako \q2 na kuziangalia njia zako. \q1 \v 16 Ninafurahia maagizo yako, \q2 wala sitalipuuza neno lako. \s2 Furaha katika Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 17 Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; \q2 nitalitii neno lako. \q1 \v 18 Yafungue macho yangu nipate kuona \q2 mambo ya ajabu katika sheria yako. \q1 \v 19 Mimi ni mgeni duniani, \q2 usinifiche amri zako. \q1 \v 20 Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa \q2 kwa sheria zako wakati wote. \q1 \v 21 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa, \q2 wanaoenda mbali na amri zako. \q1 \v 22 Niondolee dharau na dhihaka, \q2 kwa kuwa ninazishika sheria zako. \q1 \v 23 Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, \q2 mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako. \q1 \v 24 Sheria zako ni furaha yangu, \q2 nazo ni washauri wangu. \s2 Kuamua kuitii Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 25 Nimelazwa chini mavumbini, \q2 yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. \q1 \v 26 Nilikueleza njia zangu ukanijibu, \q2 nifundishe sheria zako. \q1 \v 27 Nijulishe mafundisho ya mausia yako, \q2 nami nitatafakari maajabu yako. \q1 \v 28 Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, \q2 uniimarishe sawasawa na neno lako. \q1 \v 29 Niepushe na njia za udanganyifu, \q2 kwa neema unifundishe sheria zako. \q1 \v 30 Nimechagua njia ya kweli, \q2 nimekaza moyo wangu katika sheria zako. \q1 \v 31 Nimeng’ang’ania sheria zako, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 usiniache niaibishwe. \q1 \v 32 Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, \q2 kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru. \s2 Maombi ili kupata ufahamu wa Torati \q1 \v 33 Ee Mwenyezi Mungu, nifundishe kuyafuata maagizo yako, \q2 nami nitayashika hadi mwisho. \q1 \v 34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako \q2 na kuitii kwa moyo wangu wote. \q1 \v 35 Niongoze kwenye njia ya amri zako, \q2 kwa kuwa huko napata furaha. \q1 \v 36 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, \q2 na siyo kwenye mambo ya ubinafsi. \q1 \v 37 Geuza macho yangu kutoka mambo yasiyofaa, \q2 uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. \q1 \v 38 Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, \q2 ili upate kuogopwa. \q1 \v 39 Niondolee aibu ninayoiogopa, \q2 kwa kuwa sheria zako ni njema. \q1 \v 40 Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! \q2 Hifadhi maisha yangu katika haki yako. \s2 Kuitumainia Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 41 Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako usiokoma unijie, \q2 wokovu wako sawasawa na ahadi yako, \q1 \v 42 ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, \q2 kwa kuwa ninalitumainia neno lako. \q1 \v 43 Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, \q2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako. \q1 \v 44 Nitaitii amri yako daima, \q2 naam, milele na milele. \q1 \v 45 Nitatembea huru, \q2 kwa kuwa nimejifunza mausia yako. \q1 \v 46 Nitasema sheria zako mbele za wafalme \q2 wala sitaaibishwa, \q1 \v 47 kwa kuwa ninazifurahia amri zako \q2 kwa sababu ninazipenda. \q1 \v 48 Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, \q2 nami ninatafakari juu ya maagizo yako. \s2 Matumaini katika Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 49 Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, \q2 kwa sababu umenipa tumaini. \q1 \v 50 Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: \q2 Ahadi yako inahifadhi maisha yangu. \q1 \v 51 Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, \q2 hata hivyo sitaiacha sheria yako. \q1 \v 52 Ee Mwenyezi Mungu, ninazikumbuka sheria zako za zamani, \q2 nazo zinanifariji. \q1 \v 53 Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, \q2 ambao wameacha sheria yako. \q1 \v 54 Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu \q2 popote ninapoishi. \q1 \v 55 Ee Mwenyezi Mungu, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, \q2 nami nitatii sheria yako. \q1 \v 56 Hili limekuwa zoezi langu: \q2 nami ninayatii mausia yako. \s2 Kujitolea katika Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 57 Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni fungu langu, \q2 nimeahidi kuyatii maneno yako. \q1 \v 58 Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, \q2 nihurumie sawasawa na ahadi yako. \q1 \v 59 Nimezifikiri njia zangu \q2 na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako. \q1 \v 60 Nitafanya haraka bila kuchelewa \q2 kuzitii amri zako. \q1 \v 61 Hata waovu wanifunge kwa kamba, \q2 sitasahau sheria yako. \q1 \v 62 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru \q2 kwa sababu ya sheria zako za haki. \q1 \v 63 Mimi ni rafiki kwa wale wote wanaokucha, \q2 kwa wote wanaofuata mausia yako. \q1 \v 64 Ee Mwenyezi Mungu, dunia imejaa upendo wako, \q2 nifundishe maagizo yako. \s2 Thamani ya Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 65 Mtendee wema mtumishi wako \q2 Ee Mwenyezi Mungu, sawasawa na neno lako. \q1 \v 66 Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, \q2 kwa kuwa ninaamini amri zako. \q1 \v 67 Kabla sijapata shida nilipotea njia, \q2 lakini sasa ninalitii neno lako. \q1 \v 68 Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, \q2 nifundishe maagizo yako. \q1 \v 69 Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, \q2 nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote. \q1 \v 70 Mioyo yao ni katili na migumu, \q2 bali mimi napendezwa na sheria yako. \q1 \v 71 Ilikuwa vyema mimi kupata shida \q2 ili nipate kujifunza maagizo yako. \q1 \v 72 Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu \q2 kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu. \s2 Haki ya Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 73 Mikono yako iliniumba na kunitengeneza, \q2 nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako. \q1 \v 74 Wale wanaokucha na wafurahie wanaponiona, \q2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako. \q1 \v 75 Ee Mwenyezi Mungu, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, \q2 katika uaminifu wako umeniadhibu. \q1 \v 76 Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, \q2 sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. \q1 \v 77 Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, \q2 kwa kuwa naifurahia sheria yako. \q1 \v 78 Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, \q2 lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako. \q1 \v 79 Wale wanaokucha na wanigeukie mimi, \q2 hao ambao wanazielewa sheria zako. \q1 \v 80 Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, \q2 ili nisiaibishwe. \s2 Maombi kwa ajili ya kuokolewa \q1 \v 81 Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, \q2 lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako. \q1 \v 82 Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; \q2 ninasema, “Utanifariji lini?” \q1 \v 83 Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, \q2 bado sijasahau maagizo yako. \q1 \v 84 Mtumishi wako itampasa angoje hadi lini? \q2 Ni lini utawaadhibu washtaki wangu? \q1 \v 85 Wenye majivuno wananichimbia mashimo, \q2 kinyume na sheria yako. \q1 \v 86 Amri zako zote ni za kuaminika; \q2 unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu. \q1 \v 87 Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, \q2 lakini sijaacha mausia yako. \q1 \v 88 Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, \q2 nami nitatii sheria za kinywa chako. \s2 Imani katika Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 89 Ee Mwenyezi Mungu, neno lako ni la milele, \q2 linasimama imara mbinguni. \q1 \v 90 Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, \q2 umeiumba dunia, nayo inadumu. \q1 \v 91 Sheria zako zinadumu hadi leo, \q2 kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia. \q1 \v 92 Kama nisingefurahia sheria yako, \q2 ningeangamia katika taabu zangu. \q1 \v 93 Sitasahau mausia yako kamwe, \q2 kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu. \q1 \v 94 Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, \q2 kwa kuwa nimetafuta mausia yako. \q1 \v 95 Waovu wanangojea kuniangamiza, \q2 bali mimi ninatafakari sheria zako. \q1 \v 96 Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, \q2 lakini amri zako hazina mwisho. \s2 Kuipenda Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. \q2 Ninaitafakari mchana kutwa. \q1 \v 98 Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu, \q2 kwa kuwa nimezishika daima. \q1 \v 99 Nina akili kuliko walimu wangu wote, \q2 kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako. \q1 \v 100 Nina ufahamu kuliko wazee, \q2 kwa kuwa ninayatii mausia yako. \q1 \v 101 Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, \q2 ili niweze kutii neno lako. \q1 \v 102 Sijaziacha sheria zako, \q2 kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. \q1 \v 103 Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, \q2 matamu kuliko asali katika kinywa changu! \q1 \v 104 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, \q2 kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu. \s2 Nuru katika Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 105 Neno lako ni taa ya miguu yangu \q2 na mwanga katika njia yangu. \q1 \v 106 Nimeapa na nimethibitisha, \q2 kwamba nitafuata sheria zako za haki. \q1 \v 107 Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 sawasawa na neno lako. \q1 \v 108 Ee Mwenyezi Mungu, pokea sifa za hiari za kinywa changu, \q2 nifundishe sheria zako. \q1 \v 109 Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, \q2 sitasahau sheria yako. \q1 \v 110 Waovu wamenitegea mtego, \q2 lakini sijayakiuka maagizo yako. \q1 \v 111 Sheria zako ni urithi wangu milele, \q2 naam ni furaha ya moyo wangu. \q1 \v 112 Nimekusudia moyoni mwangu \q2 kuyafuata maagizo yako hadi mwisho. \s2 Usalama ndani ya Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 113 Ninachukia watu wa nia mbili, \q2 lakini ninapenda sheria yako. \q1 \v 114 Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, \q2 nimeweka tumaini langu katika neno lako. \q1 \v 115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu, \q2 ili niweze kushika amri za Mungu wangu! \q1 \v 116 Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; \q2 usiache matumaini yangu yakavunjwa. \q1 \v 117 Nitegemeze, nami nitaokolewa, \q2 nami daima nitayaheshimu maagizo yako. \q1 \v 118 Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, \q2 kwa maana udanganyifu wao ni bure. \q1 \v 119 Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, \q2 kwa hivyo nazipenda sheria zako. \q1 \v 120 Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, \q2 ninaziogopa sheria zako. \s2 Busara ya kuitii Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 121 Nimetenda yaliyo haki na sawa, \q2 usiniache mikononi mwa watesi wangu. \q1 \v 122 Mhakikishie mtumishi wako usalama, \q2 usiache wenye kiburi wanidhulumu. \q1 \v 123 Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, \q2 na kuitazamia ahadi yako ya kweli. \q1 \v 124 Mtendee mtumishi wako kulingana na upendo wako \q2 na unifundishe maagizo yako. \q1 \v 125 Mimi ni mtumishi wako; nipe busara \q2 ili niweze kuelewa sheria zako. \q1 \v 126 Ee Mwenyezi Mungu, wakati wako wa kutenda umewadia, \q2 kwa kuwa sheria yako inavunjwa. \q1 \v 127 Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, \q2 naam, zaidi ya dhahabu safi, \q1 \v 128 na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, \q2 nachukia kila njia potovu. \s2 Shauku ya kuitii Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 129 Sheria zako ni za ajabu, \q2 hivyo ninazitii. \q1 \v 130 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, \q2 kunampa mjinga ufahamu. \q1 \v 131 Nimefungua kinywa changu na kuhema, \q2 nikitamani amri zako. \q1 \v 132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote \q2 wale wanaolipenda jina lako. \q1 \v 133 Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, \q2 usiache dhambi yoyote initawale. \q1 \v 134 Niokoe na uonevu wa wanadamu, \q2 ili niweze kutii mausia yako. \q1 \v 135 Mwangazie mtumishi wako uso wako \q2 na unifundishe amri zako. \q1 \v 136 Chemchemi za machozi zinatiririka machoni yangu, \q2 kwa kuwa sheria yako haifuatwi. \s2 Haki ya Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 137 Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni mwenye haki, \q2 sheria zako ni sahihi. \q1 \v 138 Sheria ulizoziweka ni za haki, \q2 ni za kuaminika kikamilifu. \q1 \v 139 Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu \q2 wanayapuuza maneno yako. \q1 \v 140 Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, \q2 mtumishi wako anazipenda. \q1 \v 141 Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, \q2 sisahau mausia yako. \q1 \v 142 Haki yako ni ya milele, \q2 na sheria yako ni kweli. \q1 \v 143 Shida na dhiki zimenipata, \q2 lakini amri zako ni furaha yangu. \q1 \v 144 Sheria zako ni sahihi milele, \q2 hunipa ufahamu ili nipate kuishi. \s2 Maombi kwa ajili ya kuokolewa \q1 \v 145 Ee Mwenyezi Mungu, ninakuita kwa moyo wangu wote, \q2 nami nitayatii maagizo yako. \q1 \v 146 Ninakuita; niokoe \q2 nami nitazishika sheria zako. \q1 \v 147 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; \q2 nimeweka tumaini langu katika neno lako. \q1 \v 148 Sikufumba macho yangu usiku kucha, \q2 ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. \q1 \v 149 Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, \q2 uyahifadhi maisha yangu, \q2 sawasawa na sheria zako. \q1 \v 150 Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, \q2 lakini wako mbali na sheria yako. \q1 \v 151 Ee Mwenyezi Mungu, hata hivyo wewe u karibu, \q2 na amri zako zote ni za kweli. \q1 \v 152 Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako \q2 kwamba umezithibitisha ili zidumu milele. \s2 Maombi kwa ajili ya msaada \q1 \v 153 Yaangalie mateso yangu, uniokoe, \q2 kwa kuwa sijasahau sheria yako. \q1 \v 154 Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, \q2 uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako. \q1 \v 155 Wokovu uko mbali na waovu, \q2 kwa kuwa hawatafuti maagizo yako. \q1 \v 156 Ee Mwenyezi Mungu, huruma zako ni kuu, \q2 uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako. \q1 \v 157 Adui wanaonitesa ni wengi, \q2 lakini mimi sitaziacha sheria zako. \q1 \v 158 Ninawatazama wasioamini kwa chuki, \q2 kwa kuwa hawalitii neno lako. \q1 \v 159 Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; \q2 Ee Mwenyezi Mungu, uyahifadhi maisha yangu, \q2 sawasawa na upendo wako. \q1 \v 160 Maneno yako yote ni kweli, \q2 sheria zako zote za haki ni za milele. \s2 Kujiweka wakfu kwa Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 161 Watawala wamenitesa bila sababu, \q2 lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako. \q1 \v 162 Nafurahia ahadi zako \q2 kama mtu aliyepata mateka mengi. \q1 \v 163 Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, \q2 lakini napenda sheria yako. \q1 \v 164 Ninakusifu mara saba kwa siku, \q2 kwa ajili ya sheria zako za haki. \q1 \v 165 Wanaopenda sheria yako wana amani tele, \q2 wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza. \q1 \v 166 Ee Mwenyezi Mungu, ninangojea wokovu wako, \q2 nami ninafuata amri zako, \q1 \v 167 Ninazitii sheria zako, \q2 kwa sababu ninazipenda mno. \q1 \v 168 Nimetii mausia yako na sheria zako, \q2 kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako. \s2 Furaha katika Torati ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 169 Ee Mwenyezi Mungu, kilio changu na kifike mbele zako, \q2 nipe ufahamu sawasawa na neno lako. \q1 \v 170 Maombi yangu na yafike mbele zako, \q2 niokoe sawasawa na ahadi yako. \q1 \v 171 Midomo yangu na ibubujike sifa, \q2 kwa kuwa unanifundisha maagizo yako. \q1 \v 172 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, \q2 kwa kuwa amri zako zote ni za haki. \q1 \v 173 Mkono wako uwe tayari kunisaidia, \q2 kwa kuwa nimechagua mausia yako. \q1 \v 174 Ee Mwenyezi Mungu, ninatamani wokovu wako, \q2 na sheria yako ni furaha yangu. \q1 \v 175 Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, \q2 na sheria zako zinitegemeze. \q1 \v 176 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. \q2 Mtafute mtumishi wako, \q2 kwa kuwa sijasahau amri zako. \c 120 \cl Zaburi 120 \s1 Kuomba msaada dhidi ya wadanganyifu \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Katika dhiki yangu namwita Mwenyezi Mungu, \q2 naye hunijibu. \q1 \v 2 Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe kutoka midomo ya uongo \q2 na ndimi za udanganyifu. \b \q1 \v 3 Atakufanyia nini, \q2 au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? \q1 \v 4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, \q2 kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. \b \q1 \v 5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, \q2 kwamba naishi katikati ya mahema ya Kedari! \q1 \v 6 Nimeishi muda mrefu mno \q2 miongoni mwa wale wanaochukia amani. \q1 \v 7 Mimi ni mtu wa amani; \q2 lakini ninaposema, wao wanataka vita. \c 121 \cl Zaburi 121 \s1 Mwenyezi Mungu mlinzi wetu \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Nayainua macho yangu natazama milima: \q2 msaada wangu utatoka wapi? \q1 \v 2 Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu, \q2 Muumba wa mbingu na dunia. \b \q1 \v 3 Hatauacha mguu wako uteleze, \q2 yeye akulindaye hatasinzia, \q1 \v 4 hakika, yeye alindaye Israeli \q2 hatasinzia wala hatalala usingizi. \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu anakulinda, \q2 Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume, \q1 \v 6 jua halitakudhuru mchana, \q2 wala mwezi wakati wa usiku. \q1 \v 7 Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote, \q2 atayalinda maisha yako, \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka, \q2 tangu sasa na hata milele. \c 122 \cl Zaburi 122 \s1 Sifa kwa Yerusalemu \d Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. \q1 \v 1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, \q2 “Twende nyumbani mwa Mwenyezi Mungu.” \q1 \v 2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama \q2 malangoni mwako. \b \q1 \v 3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji \q2 ulioshikamana pamoja. \q1 \v 4 Huko ndiko makabila hukwea, \q2 makabila ya Mwenyezi Mungu, \q1 kulisifu jina la Mwenyezi Mungu kulingana na maagizo \q2 waliopewa Israeli. \q1 \v 5 Huko viti vya hukumu hukaa, \q2 viti vya ufalme vya nyumba ya Daudi. \b \q1 \v 6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: \q2 “Wote wanaokupenda na wawe salama. \q1 \v 7 Amani na iwe ndani ya kuta zako, \q2 na usalama ndani ya ngome zako.” \q1 \v 8 Kwa ajili ya ndugu na rafiki zangu, \q2 nitasema, “Amani iwe ndani yako.” \q1 \v 9 Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 nitatafuta mafanikio yako. \c 123 \cl Zaburi 123 \s1 Kuomba rehema \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Ninayainua macho yangu kwako, \q2 kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi. \q1 \v 2 Kama vile macho ya watumwa \q2 yatazamavyo mkono wa bwana wao, \q1 kama vile macho ya mjakazi \q2 yatazamavyo mkono wa bibi yake, \q1 ndivyo macho yetu yamtazamavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 hadi atakapotuhurumia. \b \q1 \v 3 Uturehemu, Ee Mwenyezi Mungu, uturehemu, \q2 kwa maana tumevumilia dharau nyingi. \q1 \v 4 Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, \q2 dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno. \c 124 \cl Zaburi 124 \s1 Shukrani kwa ukombozi wa Israeli \d Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. \q1 \v 1 Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu; \q2 Israeli na aseme sasa: \q1 \v 2 kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu, \q2 watu walipotushambulia, \q1 \v 3 hasira yao ilipowaka dhidi yetu, \q2 wangetumeza tukiwa hai, \q1 \v 4 mafuriko yangegharikisha, \q2 maji mengi yangetufunika, \q1 \v 5 maji yaendayo kasi \q2 yangetuchukua. \b \q1 \v 6 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, \q2 ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. \q1 \v 7 Tumeponyoka kama ndege \q2 kutoka mtego wa mwindaji; \q1 mtego umevunjika, \q2 nasi tumeokoka. \q1 \v 8 Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu, \q2 Muumba wa mbingu na dunia. \c 125 \cl Zaburi 125 \s1 Usalama wa watu wa Mwenyezi Mungu \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Wale wamtumainio Mwenyezi Mungu ni kama Mlima Sayuni, \q2 ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. \q1 \v 2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, \q2 ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowazunguka watu wake \q2 sasa na hata milele. \b \q1 \v 3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi \q2 waliyopewa wenye haki, \q1 ili wenye haki wasije wakatumia \q2 mikono yao kutenda ubaya. \b \q1 \v 4 Ee Mwenyezi Mungu, watendee mema walio wema, \q2 wale walio wanyofu wa moyo. \q1 \v 5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, \q2 Mwenyezi Mungu atawafukuza pamoja na watenda maovu. \b \q1 Amani iwe juu ya Israeli. \c 126 \cl Zaburi 126 \s1 Kurejeshwa kutoka uhamisho \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu alipowarejesha mateka Sayuni, \q2 tulikuwa kama watu walioota ndoto. \q1 \v 2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko, \q2 ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. \q1 Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, \q2 “Mwenyezi Mungu amewatendea mambo makuu.” \q1 \v 3 Mwenyezi Mungu ametutendea mambo makuu, \q2 nasi tumejaa furaha. \b \q1 \v 4 Ee Mwenyezi Mungu, turejeshee watu wetu waliotekwa, \q2 kama vijito katika Negebu. \q1 \v 5 Wapandao kwa machozi \q2 watavuna kwa nyimbo za shangwe. \q1 \v 6 Yeye azichukuaye mbegu zake \q2 kwenda kupanda, huku akilia, \q1 atarudi kwa nyimbo za shangwe, \q2 akichukua miganda ya mavuno yake. \c 127 \cl Zaburi 127 \s1 Bila Mwenyezi Mungu, kazi ya mwanadamu haifai \d Wimbo wa kwenda juu. Wa Sulemani. \q1 \v 1 Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba, \q2 wajengao hufanya kazi bure. \q1 Mwenyezi Mungu asipoulinda mji, \q2 walinzi wakesha bure. \q1 \v 2 Mnajisumbua bure kuamka mapema \q2 na kuchelewa kulala, \q1 mkitaabikia chakula: \q2 kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake. \b \q1 \v 3 Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, \q2 uzao ni zawadi kutoka kwake. \q1 \v 4 Kama mishale mikononi mwa shujaa \q2 ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. \q1 \v 5 Heri mtu ambaye podo lake \q2 limejazwa nao. \q1 Hawataaibishwa wanaposhindana \q2 na adui zao langoni. \c 128 \cl Zaburi 128 \s1 Thawabu ya kumtii Mwenyezi Mungu \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu, \q2 wanaoenda katika njia zake. \q1 \v 2 Utakula matunda ya kazi yako; \q2 baraka na mafanikio vitakuwa vyako. \q1 \v 3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao \q2 ndani ya nyumba yako; \q1 wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni \q2 kuizunguka meza yako. \q1 \v 4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa \q2 mtu amchaye Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayuni \q2 siku zote za maisha yako, \q1 na uone mafanikio ya Yerusalemu, \q2 \v 6 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. \b \q1 Amani iwe juu ya Israeli. \c 129 \cl Zaburi 129 \s1 Maombi dhidi ya adui za Israeli \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Wamenitesa sana tangu ujana wangu; \q2 Israeli na aseme sasa: \q1 \v 2 wamenitesa sana tangu ujana wangu, \q2 lakini bado hawajanishinda. \q1 \v 3 Wakulima wamelima mgongo wangu, \q2 na kufanya mifereji yao mirefu. \q1 \v 4 Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki; \q2 amenifungua toka kamba za waovu. \b \q1 \v 5 Wale wote wanaoichukia Sayuni \q2 na warudishwe nyuma kwa aibu. \q1 \v 6 Wawe kama majani juu ya paa, \q2 ambayo hunyauka kabla hayajakua; \q1 \v 7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, \q2 wala akusanyaye kujaza mikono yake. \q1 \v 8 Wale wapitao karibu na wasiseme, \q2 “Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako; \q2 tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.” \c 130 \cl Zaburi 130 \s1 Kumngojea Mwenyezi Mungu \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Mwenyezi Mungu. \q2 \v 2 Ee Bwana, sikia sauti yangu. \q1 Masikio yako na yawe masikivu \q2 kwa kilio changu unihurumie. \b \q1 \v 3 Kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, \q2 Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama? \q1 \v 4 Lakini kwako kuna msamaha, \q2 kwa hiyo wewe unaogopwa. \b \q1 \v 5 Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea, \q2 katika neno lake naweka tumaini langu. \q1 \v 6 Nafsi yangu inamngojea Bwana \q2 kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, \q1 naam, kuliko walinzi \q2 waingojeavyo asubuhi. \b \q1 \v 7 Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu, \q2 maana kwa Mwenyezi Mungu kuna upendo usiokoma, \q2 na kwake kuna ukombozi kamili. \q1 \v 8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli \q2 kutoka dhambi zao zote. \c 131 \cl Zaburi 131 \s1 Kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu \d Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. \q1 \v 1 Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 macho yangu hayajivuni; \q1 sijishughulishi na mambo makuu kunizidi \q2 wala mambo ya ajabu mno kwangu. \q1 \v 2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; \q2 kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, \q1 kama mtoto aliyeachishwa kunyonya \q2 ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu. \b \q1 \v 3 Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu \q2 tangu sasa na hata milele. \c 132 \cl Zaburi 132 \s1 Maskani ya Mungu ya milele huko Sayuni \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, mkumbuke Daudi \q2 na taabu zote alizozistahimili. \b \q1 \v 2 Aliapa kiapo kwa Mwenyezi Mungu \q2 na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: \q1 \v 3 “Sitaingia nyumbani mwangu \q2 au kwenda kitandani mwangu: \q1 \v 4 sitaruhusu usingizi katika macho yangu, \q2 wala kope zangu kusinzia, \q1 \v 5 hadi nitakapompatia Mwenyezi Mungu mahali, \q2 makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” \b \q1 \v 6 Tulisikia habari hii huko Efrata, \q2 tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara\f + \fr 132:6 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Kiriath-Yearimu\fqa*\f*: \q1 \v 7 “Twendeni kwenye makao yake, \q2 na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; \q1 \v 8 inuka, Ee Mwenyezi Mungu, uje mahali pako pa kupumzikia, \q2 wewe na Sanduku la nguvu zako. \q1 \v 9 Makuhani wako na wavikwe haki, \q2 watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” \b \q1 \v 10 Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, \q2 usimkatae mpakwa mafuta wako. \b \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu alimwapia Daudi kiapo, \q2 kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: \q1 “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe \q2 kwenye kiti chako cha ufalme, \q1 \v 12 kama wanao watashika agano langu \q2 na sheria ninazowafundisha, \q1 ndipo wana wao watakalia kiti chako cha ufalme \q2 milele na milele.” \b \q1 \v 13 Kwa maana Mwenyezi Mungu ameichagua Sayuni, \q2 amepaonea shauku pawe maskani yake: \q1 \v 14 “Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; \q2 hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, \q2 kwa sababu nimepaonea shauku: \q1 \v 15 Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: \q2 nitashibisha maskini wake kwa chakula. \q1 \v 16 Nitawavika makuhani wake wokovu, \q2 nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. \b \q1 \v 17 “Hapa nitamchipushia Daudi pembe\f + \fr 132:17 \fr*\ft pembe inawakilisha nguvu\ft*\f*, \q2 na kuweka taa kwa ajili ya masiya\f + \fr 132:17 \fr*\ft yaani \ft*\fqa mpakwa mafuta\fqa*\f* wangu. \q1 \v 18 Adui zake nitawavika aibu, \q2 bali taji kichwani pake litang’aa sana.” \c 133 \cl Zaburi 133 \s1 Sifa za pendo la undugu \d Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. \q1 \v 1 Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza \q2 ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! \q1 \v 2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, \q2 yakitiririka kwenye ndevu, \q1 yakitiririka kwenye ndevu za Haruni, \q2 hadi kwenye upindo wa mavazi yake. \q1 \v 3 Ni kama umande wa Hermoni \q2 ukianguka juu ya Mlima Sayuni. \q1 Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake, \q2 naam, uzima hata milele. \c 134 \cl Zaburi 134 \s1 Wito wa kumsifu Mwenyezi Mungu \d Wimbo wa kwenda juu. \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu, \q2 ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 2 Inueni mikono yenu katika patakatifu \q2 na kumsifu Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 3 Naye Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia, \q2 awabariki kutoka Sayuni. \c 135 \cl Zaburi 135 \s1 Wimbo wa sifa kwa Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 135:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah \fqa*\ft pia \+xt 135:3, 21\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Lisifuni jina la Mwenyezi Mungu, \q2 msifuni, enyi watumishi wa Mwenyezi Mungu, \q1 \v 2 ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, \q2 katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. \b \q1 \v 3 Msifuni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwema, \q2 liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. \q1 \v 4 Kwa maana Mwenyezi Mungu amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, \q2 Israeli kuwa hazina yake ya pekee. \b \q1 \v 5 Ninajua ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mkuu, \q2 kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote. \q1 \v 6 Mwenyezi Mungu hufanya lolote apendalo, \q2 mbinguni na duniani, \q2 katika bahari na vilindi vyake vyote. \q1 \v 7 Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; \q2 hupeleka miali ya radi pamoja na mvua \q2 na huleta upepo kutoka ghala zake. \b \q1 \v 8 Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, \q2 mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama. \q1 \v 9 Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, \q2 dhidi ya Farao na watumishi wake wote. \q1 \v 10 Aliyapiga mataifa mengi, \q2 na akaua wafalme wenye nguvu: \q1 \v 11 Mfalme Sihoni na Waamori, \q2 Ogu mfalme wa Bashani \q2 na wafalme wote wa Kanaani: \q1 \v 12 akatoa nchi yao kuwa urithi, \q2 urithi kwa watu wake Israeli. \b \q1 \v 13 Ee Mwenyezi Mungu, jina lako ladumu milele, \q2 kumbukumbu za fahari zako, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, kwa vizazi vyote. \q1 \v 14 Maana Mwenyezi Mungu atawathibitisha watu wake, \q2 na kuwahurumia watumishi wake. \b \q1 \v 15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, \q2 zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. \q1 \v 16 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, \q2 zina macho, lakini haziwezi kuona; \q1 \v 17 zina masikio, lakini haziwezi kusikia, \q2 wala hakuna pumzi katika vinywa vyao. \q1 \v 18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, \q2 vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. \b \q1 \v 19 Ee nyumba ya Israeli, msifuni Mwenyezi Mungu; \q2 ee nyumba ya Haruni, msifuni Mwenyezi Mungu; \q1 \v 20 ee nyumba ya Lawi, msifuni Mwenyezi Mungu; \q2 ninyi mnaomcha, msifuni Mwenyezi Mungu. \q1 \v 21 Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka Sayuni, \q2 msifuni yeye aishiye Yerusalemu. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 136 \cl Zaburi 136 \s1 Wimbo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ni mwema. \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 2 Mshukuruni Mungu wa miungu. \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 3 Mshukuruni Bwana wa mabwana: \qr Fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 4 Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 5 Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 6 Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 7 Ambaye aliumba mianga mikubwa, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 8 Jua litawale mchana, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 9 Mwezi na nyota vitawale usiku, \qr Fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 10 Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 11 Na kuwatoa Israeli katikati yao, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 12 Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, \qr Fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 13 Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 14 Na kuwapitisha Israeli katikati yake, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 15 Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 16 Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 17 Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 18 Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 19 Sihoni mfalme wa Waamori, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 20 Ogu mfalme wa Bashani, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 21 Akatoa nchi yao kuwa urithi, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 22 Urithi kwa Israeli mtumishi wake, \qr Fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 24 Alituweka huru toka adui zetu, \qr Fadhili zake zadumu milele. \q1 \v 25 Ambaye humpa chakula kila kiumbe. \qr Fadhili zake zadumu milele. \b \q1 \v 26 Mshukuruni Mungu wa mbinguni, \qr Fadhili zake zadumu milele. \c 137 \cl Zaburi 137 \s1 Maombolezo ya Israeli uhamishoni \q1 \v 1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza \q2 tulipokumbuka Sayuni. \q1 \v 2 Kwenye miti ya huko \q2 tulitundika vinubi vyetu, \q1 \v 3 kwa maana huko hao waliotuteka \q2 walitaka tuwaimbie nyimbo; \q1 watesi wetu walidai nyimbo za furaha; \q2 walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja \q2 kati ya nyimbo za Sayuni!” \b \q1 \v 4 Tutaimbaje nyimbo za Mwenyezi Mungu, \q2 tukiwa nchi ya kigeni? \q1 \v 5 Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, \q2 basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. \q1 \v 6 Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu \q2 kama sitakukumbuka wewe, \q1 kama nisipokufikiri Yerusalemu \q2 kuwa furaha yangu kubwa. \b \q1 \v 7 Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu, \q2 siku ile Yerusalemu ilipoanguka. \q1 Walisema, “Bomoa, bomoa \q2 hata misingi yake!” \b \q1 \v 8 Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, \q2 heri yeye atakayekulipiza wewe \q2 kwa yale uliyotutenda sisi: \q1 \v 9 yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga \q2 na kuwaponda juu ya miamba. \c 138 \cl Zaburi 138 \s1 Maombi ya shukrani \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu, kwa moyo wangu wote, \q2 mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. \q1 \v 2 Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, \q2 nami nitalisifu jina lako \q1 kwa ajili ya upendo wako \q2 na uaminifu, \q1 kwa maana umeitukuza ahadi yako \q2 zaidi ya jina lako. \q1 \v 3 Nilipoita, ulinijibu; \q2 ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. \b \q1 \v 4 Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Mwenyezi Mungu, \q2 wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. \q1 \v 5 Wao na waimbe kuhusu njia za Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana utukufu wa Mwenyezi Mungu ni mkuu. \b \q1 \v 6 Ingawa Mwenyezi Mungu yuko juu, \q2 humwangalia mnyonge, \q1 bali mwenye kiburi \q2 yeye anamjua kutokea mbali. \q1 \v 7 Nijapopita katikati ya shida, \q2 wewe unayahifadhi maisha yangu, \q1 unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, \q2 kwa mkono wako wa kuume unaniokoa. \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu atatimiza kusudi lake kwangu, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako wadumu milele: \q2 usiziache kazi za mikono yako. \c 139 \cl Zaburi 139 \s1 Mwenyezi Mungu asiyeweza kukwepwa \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, umenichunguza \q2 na kunijua. \q1 \v 2 Unajua ninapoketi na ninapoinuka; \q2 unatambua mawazo yangu tokea mbali. \q1 \v 3 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; \q2 unaelewa njia zangu zote. \q1 \v 4 Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, \q2 wewe walijua kikamilifu, Ee Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 5 Umenizingira nyuma na mbele; \q2 umeweka mkono wako juu yangu. \q1 \v 6 Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, \q2 ni ya juu sana kwangu kuyafikia. \b \q1 \v 7 Niende wapi nijiepushe na Roho yako? \q2 Niende wapi niukimbie uso wako? \q1 \v 8 Nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; \q2 nikifanya vilindi\f + \fr 139:8 \fr*\ft Vilindi ina maana ya \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\ft ; kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol.\fqa*\f* kuwa kitanda changu, \q2 wewe uko huko. \q1 \v 9 Nikipanda juu kwa mabawa ya mapambazuko, \q2 nikikaa pande za mbali za bahari, \q1 \v 10 hata huko mkono wako utaniongoza, \q2 mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. \b \q1 \v 11 Nikisema, “Hakika giza litanificha \q2 na nuru inayonizunguka iwe usiku,” \q1 \v 12 hata giza halitakuwa giza kwako, \q2 usiku utang’aa kama mchana, \q2 kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. \b \q1 \v 13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; \q2 uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. \q1 \v 14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa \q2 kwa namna ya ajabu na ya kutisha; \q1 kazi zako ni za ajabu, \q2 ninajua hayo kikamilifu. \q1 \v 15 Umbile langu halikufichika kwako, \q2 nilipoumbwa mahali pa siri. \q1 Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, \q2 \v 16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. \q1 Siku zangu zote ulizonipangia \q2 ziliandikwa katika kitabu chako \q2 kabla haijakuwa hata moja. \b \q1 \v 17 Tazama jinsi yalivyo ya thamani \q2 mawazo yako kwangu, Ee Mungu! \q2 Jinsi jumla yake ilivyo kubwa! \q1 \v 18 Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi \q2 kuliko mchanga: \q2 niamkapo, bado niko pamoja nawe. \b \q1 \v 19 Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! \q2 Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! \q1 \v 20 Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, \q2 adui zako wanatumia vibaya jina lako. \q1 \v 21 Ee Mwenyezi Mungu, je, nisiwachukie wanaokuchukia? \q2 Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? \q1 \v 22 Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, \q2 ninawahesabu ni adui zangu. \b \q1 \v 23 Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, \q2 nijaribu na ujue mawazo yangu. \q1 \v 24 Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, \q2 uniongoze katika njia ya milele. \c 140 \cl Zaburi 140 \s1 Kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu \d Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, niokoe, kutoka kwa watu waovu; \q2 nilinde na watu wenye jeuri, \q1 \v 2 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, \q2 na kuchochea vita siku zote. \q1 \v 3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, \q2 sumu ya nyoka iko midomoni mwao. \b \q1 \v 4 Ee Mwenyezi Mungu, niepushe na mikono ya waovu; \q2 nilinde na watu wenye jeuri \q2 wanaopanga kunikwaza miguu yangu. \q1 \v 5 Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, \q2 wametandaza kamba za wavu wao, \q2 wametega mitego kwenye njia yangu. \b \q1 \v 6 Ee Mwenyezi Mungu, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” \q2 Ee Mwenyezi Mungu, usikie kilio changu na kunihurumia. \q1 \v 7 Ee Bwana Mungu Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, \q2 unikingaye kichwa changu siku ya vita: \q1 \v 8 Ee Mwenyezi Mungu, usiwape waovu matakwa yao, \q2 usiache mipango yao ikafanikiwa, \q2 wasije wakajisifu. \b \q1 \v 9 Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida \q2 zilizosababishwa na midomo yao. \q1 \v 10 Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! \q2 Na watupwe motoni, \q1 katika mashimo ya matope, \q2 wasiinuke tena kamwe. \q1 \v 11 Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; \q2 maafa na yawawinde watu wenye jeuri. \b \q1 \v 12 Najua kwamba Mwenyezi Mungu huwapatia maskini haki, \q2 na kuitegemeza njia ya mhitaji. \q1 \v 13 Hakika wenye haki watalisifu jina lako, \q2 na waadilifu wataishi mbele zako. \c 141 \cl Zaburi 141 \s1 Maombi ya kuhifadhiwa dhidi ya uovu \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, ninakuita, njoo kwangu hima. \q2 Sikia sauti yangu ninapokuita. \q1 \v 2 Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; \q2 kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni. \b \q1 \v 3 Ee Mwenyezi Mungu, weka mlinzi kinywani mwangu, \q2 weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu. \q1 \v 4 Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya, \q2 nisije nikashiriki katika matendo maovu \q1 pamoja na watu watendao mabaya, \q2 wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa. \b \q1 \v 5 Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; \q2 na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. \q2 Kichwa changu hakitalikataa. \b \q1 Hata hivyo, maombi yangu daima \q2 ni kinyume cha watenda maovu. \q1 \v 6 Watawala wao watatupwa chini \q2 kutoka majabali, \q1 waovu watajifunza kwamba maneno yangu \q2 yalikuwa kweli. \q1 \v 7 Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, \q2 ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” \b \q1 \v 8 Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, \q2 ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. \q1 \v 9 Niepushe na mitego waliyonitegea, \q2 kutokana na mitego iliyotegwa na watenda maovu. \q1 \v 10 Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe, \q2 wakati mimi ninapita salama. \c 142 \cl Zaburi 142 \s1 Maombi ya kuokolewa dhidi ya watesi \d Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi. \q1 \v 1 Namlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti, \q2 napaza sauti yangu kwa Mwenyezi Mungu anihurumie. \q1 \v 2 Namimina malalamiko yangu mbele zake, \q2 mbele zake naeleza shida zangu. \b \q1 \v 3 Roho yangu inapozimia ndani yangu, \q2 wewe ndiwe unajua njia zangu. \q1 Katika njia ninayopita, \q2 watu wameniwekea mtego. \q1 \v 4 Tazama kuume kwangu na uone, \q2 hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. \q1 Sina kimbilio, \q2 hakuna anayejali maisha yangu. \b \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, nakulilia wewe, \q2 nasema, “Wewe ni kimbilio langu, \q2 fungu langu katika nchi ya walio hai.” \q1 \v 6 Sikiliza kilio changu, \q2 kwa sababu mimi ni mhitaji sana; \q1 niokoe na wale wanaonifuatilia, \q2 kwa kuwa wamenizidi nguvu. \q1 \v 7 Nifungue kutoka kifungo changu, \q2 ili niweze kulisifu jina lako. \b \q1 Ndipo wenye haki watanizunguka, \q2 kwa sababu ya wema wako kwangu. \c 143 \cl Zaburi 143 \s1 Maombi ya kuokolewa dhidi ya adui \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ee Mwenyezi Mungu, sikia sala yangu, \q2 sikiliza kilio changu unihurumie; \q1 katika uaminifu na haki yako \q2 njoo unisaidie. \q1 \v 2 Usimhukumu mtumishi wako, \q2 kwa kuwa hakuna mtu aliye hai \q2 mwenye haki mbele zako. \b \q1 \v 3 Adui hunifuatilia, \q2 hunipondaponda chini; \q1 hunifanya niishi gizani \q2 kama wale waliokufa zamani. \q1 \v 4 Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, \q2 moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. \b \q1 \v 5 Nakumbuka siku za zamani; \q2 natafakari juu ya kazi zako zote, \q1 naangalia juu ya kazi \q2 ambazo mikono yako imezifanya. \q1 \v 6 Nanyoosha mikono yangu kwako, \q2 nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. \b \q1 \v 7 Ee Mwenyezi Mungu, unijibu haraka, \q2 roho yangu inazimia. \q1 Usinifiche uso wako, \q2 ama sivyo nitafanana na wale wanaoshuka shimoni. \q1 \v 8 Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, \q2 kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. \q1 Nioneshe njia nitakayoiendea, \q2 kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. \q1 \v 9 Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe na adui zangu, \q2 kwa kuwa nimejificha kwako. \q1 \v 10 Nifundishe kufanya mapenzi yako, \q2 kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, \q1 Roho wako mwema na aniongoze \q2 katika nchi tambarare. \b \q1 \v 11 Ee Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, \q2 kwa haki yako nitoe katika taabu. \q1 \v 12 Kwa upendo wako usiokoma, \q2 nyamazisha adui zangu; \q1 waangamize watesi wangu wote, \q2 kwa kuwa mimi ni mtumishi wako. \c 144 \cl Zaburi 144 \s1 Mfalme amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi \d Zaburi ya Daudi. \q1 \v 1 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu Mwamba wangu, \q2 aifundishaye mikono yangu vita, \q2 na vidole vyangu kupigana. \q1 \v 2 Yeye ni Mungu wangu wa upendo na ulinzi wangu, \q2 ngome yangu na mwokozi wangu, \q1 ngao yangu, ninayemkimbilia, \q2 ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. \b \q1 \v 3 Ee Mwenyezi Mungu, mwanadamu ni nini hata umjali, \q2 Binadamu ni nini hata umfikirie? \q1 \v 4 Mwanadamu ni kama pumzi, \q2 siku zake ni kama kivuli kinachopita. \b \q1 \v 5 Ee Mwenyezi Mungu, pasua mbingu zako, ushuke, \q2 gusa milima ili itoe moshi. \q1 \v 6 Peleka umeme uwatawanye adui, \q2 lenga mishale yako uwashinde. \q1 \v 7 Nyoosha mkono wako kutoka juu, \q2 nikomboe na kuniokoa \q1 kutoka maji makuu, \q2 kutoka mikononi mwa wageni \q1 \v 8 ambao vinywa vyao vimejaa uongo, \q2 na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. \b \q1 \v 9 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, \q2 kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia, \q1 \v 10 kwa Yule awapaye wafalme ushindi, \q2 ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake, \q2 kutokana na upanga hatari. \b \q1 \v 11 Nikomboe na uniokoe \q2 kutoka mikononi mwa wageni \q1 ambao vinywa vyao vimejaa uongo, \q2 na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. \b \q1 \v 12 Kisha wana wetu wakati wa ujana wao \q2 watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, \q1 binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa \q2 kurembesha jumba la kifalme. \q1 \v 13 Ghala zetu zitajazwa \q2 aina zote za mahitaji. \q1 Kondoo wetu watazaa kwa maelfu, \q2 kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu; \q1 \v 14 maksai wetu watakokota \q2 mizigo mizito. \q1 Hakutakuwa na kubomoka kuta, \q2 hakuna kuchukuliwa mateka, \q1 wala kilio cha taabu \q2 katika barabara zetu. \b \q1 \v 15 Heri watu ambao hili ni kweli; \q2 heri wale ambao Mwenyezi Mungu ni Mungu wao. \c 145 \cl Zaburi 145\f + \fr 145:0 \fr*\ft Zaburi hii imetungwa kila mstari (ikiwa ni pamoja na 13b) ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.\ft*\f* \s1 Wimbo wa kusifu ukuu na wema wa Mwenyezi Mungu \d Wimbo wa sifa. Wa Daudi. \q1 \v 1 Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, \q2 nitalisifu jina lako milele na milele. \q1 \v 2 Kila siku nitakusifu \q2 na kulitukuza jina lako milele na milele. \b \q1 \v 3 Mwenyezi Mungu ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, \q2 ukuu wake haupimiki. \q1 \v 4 Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, \q2 watasimulia matendo yako makuu. \q1 \v 5 Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, \q2 nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. \q1 \v 6 Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, \q2 nami nitatangaza matendo yako makuu. \q1 \v 7 Wataadhimisha wema wako mwingi, \q2 na wataimba kwa shangwe kuhusu haki yako. \b \q1 \v 8 Mwenyezi Mungu ni mwenye neema na mwingi wa huruma, \q2 si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. \q1 \v 9 Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wote, \q2 ana huruma kwa vyote alivyovifanya. \q1 \v 10 Ee Mwenyezi Mungu, vyote ulivyovifanya vitakusifu, \q2 watakatifu wako watakutukuza. \q1 \v 11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako \q2 na kusema kuhusu ukuu wako, \q1 \v 12 ili watu wote wajue matendo yako makuu \q2 na utukufu wa fahari ya ufalme wako. \q1 \v 13 Ufalme wako ni ufalme wa milele, \q2 mamlaka yako hudumu vizazi vyote. \b \q1 Mwenyezi Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake zote \q2 na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. \q1 \v 14 Mwenyezi Mungu huwategemeza wote waangukao, \q2 na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao. \q1 \v 15 Macho ya watu wote yanakutazama, \q2 nawe huwapa chakula chao wakati wake. \q1 \v 16 Waufumbua mkono wako, \q2 watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. \b \q1 \v 17 Mwenyezi Mungu ni mwenye haki katika njia zake zote, \q2 na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. \q1 \v 18 Mwenyezi Mungu yu karibu na wote wamwitao, \q2 karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. \q1 \v 19 Huwatimizia wamchao matakwa yao, \q2 husikia kilio chao na kuwaokoa. \q1 \v 20 Mwenyezi Mungu huwalinda wote wanaompenda, \q2 bali waovu wote atawaangamiza. \b \q1 \v 21 Kinywa changu kitazinena sifa za Mwenyezi Mungu. \q2 Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu \q2 milele na milele. \c 146 \cl Zaburi 146 \s1 Kumsifu Mwenyezi Mungu mwokozi \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu!\f + \fr 146:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 146:10\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi Mungu, \q2 \v 2 Nitamsifu Mwenyezi Mungu maisha yangu yote; \q1 nitamwimbia Mungu wangu sifa \q2 wakati wote ningali hai. \q1 \v 3 Usiweke tumaini lako kwa wakuu, \q2 kwa wanadamu ambao hufa, \q2 ambao hawawezi kuokoa. \q1 \v 4 Roho yao itokapo hurudi mavumbini, \q2 siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma. \b \q1 \v 5 Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, \q2 ambaye tumaini lake ni katika Mwenyezi Mungu, Mungu wake, \q1 \v 6 Muumba wa mbingu na nchi, \q2 na bahari na vyote vilivyomo: \q1 Mwenyezi Mungu anayedumu kuwa mwaminifu \q2 milele na milele. \q1 \v 7 Naye huwapatia haki waliodhulumiwa, \q2 na kuwapa wenye njaa chakula. \q1 Mwenyezi Mungu huwaweka wafungwa huru, \q2 \v 8 Mwenyezi Mungu huwafumbua vipofu macho, \q1 Mwenyezi Mungu huwainua waliolemewa na mizigo yao, \q2 Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki. \q1 \v 9 Mwenyezi Mungu huwalinda wageni \q2 na kuwategemeza yatima na wajane, \q2 lakini hupinga njia za waovu. \b \q1 \v 10 Mwenyezi Mungu atamiliki milele, \q2 Mungu wako, ee Sayuni, \q2 kwa vizazi vyote. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 147 \cl Zaburi 147 \s1 Kumsifu Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 147:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 147:20\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, \q2 jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye! \b \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu hujenga Yerusalemu, \q2 huwakusanya Israeli walio uhamishoni. \q1 \v 3 Anawaponya waliovunjika mioyo \q2 na kuvifunga vidonda vyao. \b \q1 \v 4 Huzihesabu nyota \q2 na huipa kila moja jina lake. \q1 \v 5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, \q2 ufahamu wake hauna kikomo. \q1 \v 6 Mwenyezi Mungu huwahifadhi wanyenyekevu \q2 lakini huwashusha waovu hadi mavumbini. \b \q1 \v 7 Mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa shukrani, \q2 mpigieni Mungu wetu kinubi. \q1 \v 8 Yeye huzifunika anga kwa mawingu, \q2 huinyeshea ardhi mvua, \q2 na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima. \q1 \v 9 Huwapa chakula mifugo \q2 na pia makinda ya kunguru yanapolia. \b \q1 \v 10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, \q2 wala furaha yake kwenye miguu ya shujaa. \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu hupendezwa na wale wamchao, \q2 wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma. \b \q1 \v 12 Mtukuze Mwenyezi Mungu, ee Yerusalemu, \q2 msifu Mungu wako, ee Sayuni, \q1 \v 13 kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako \q2 na huwabariki watu wako walio ndani yako. \q1 \v 14 Huwapa amani mipakani mwenu \q2 na kukushibisha kwa ngano safi kabisa. \b \q1 \v 15 Hutuma amri yake duniani, \q2 neno lake hukimbia kasi. \q1 \v 16 Anatandaza theluji kama sufu \q2 na kutawanya umande kama majivu. \q1 \v 17 Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. \q2 Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake? \q1 \v 18 Hutuma neno lake na kuviyeyusha, \q2 huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka. \b \q1 \v 19 Amemfunulia Yakobo neno lake, \q2 sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. \q1 \v 20 Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, \q2 hawazijui sheria zake. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 148 \cl Zaburi 148 \s1 Mwito kwa ulimwengu kumsifu Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 148:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 148:7, 14\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, \q2 msifuni juu vileleni. \q1 \v 2 Msifuni, enyi malaika wake wote, \q2 msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. \q1 \v 3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, \q2 msifuni yeye, enyi nyota zote zinazong’aa. \q1 \v 4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, \q2 na ninyi maji juu ya anga. \q1 \v 5 Vilisifu jina la Mwenyezi Mungu \q2 kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa. \q1 \v 6 Aliviweka mahali pake milele na milele, \q2 alitoa amri ambayo haibadiliki milele. \b \q1 \v 7 Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka duniani, \q2 ninyi wanyama wakubwa wa baharini, \q2 na vilindi vyote vya bahari, \q1 \v 8 miali ya radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, \q2 pepo za dhoruba zinazotimiza amri zake, \q1 \v 9 ninyi milima na vilima vyote, \q2 miti ya matunda na mierezi yote, \q1 \v 10 wanyama pori na mifugo yote, \q2 viumbe vidogo na ndege warukao, \q1 \v 11 wafalme wa dunia na mataifa yote, \q2 ninyi wakuu na watawala wote wa dunia, \q1 \v 12 vijana wa kiume na wanawali, \q2 wazee na watoto. \b \q1 \v 13 Wote na walisifu jina la Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana jina lake pekee limetukuka, \q2 utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. \q1 \v 14 Amewainulia watu wake pembe\f + \fr 148:14 \fr*\ft pembe inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme\ft*\f*, \q2 sifa ya watakatifu wake wote, \q2 ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 149 \cl Zaburi 149 \s1 Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wema wake \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 149:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 149:9\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya, \q2 sifa zake katika kusanyiko la watakatifu. \b \q1 \v 2 Israeli na washangilie katika Muumba wao, \q2 watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao. \q1 \v 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza \q2 na wampigie muziki kwa matari na kinubi. \q1 \v 4 Kwa maana Mwenyezi Mungu anapendezwa na watu wake, \q2 anawavika wanyenyekevu taji la wokovu. \q1 \v 5 Watakatifu washangilie katika heshima hii, \q2 na waimbe kwa shangwe vitandani mwao. \b \q1 \v 6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao \q2 na upanga ukatao kuwili mikononi mwao, \q1 \v 7 ili walipize mataifa kisasi \q2 na adhabu juu ya mataifa, \q1 \v 8 wawafunge wafalme wao kwa minyororo, \q2 wakuu wao kwa pingu za chuma, \q1 \v 9 ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. \q2 Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu. \c 150 \cl Zaburi 150 \s1 Msifuni Mwenyezi Mungu kwa ukuu wake \q1 \v 1 Msifuni Mwenyezi Mungu.\f + \fr 150:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Hallelu Yah\fqa*\ft ; pia \+xt 150:6\+xt*.\ft*\f* \b \q1 Msifuni Mungu katika patakatifu pake, \q2 msifuni katika mbingu zake kuu. \q1 \v 2 Msifuni kwa matendo yake makuu, \q2 msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. \q1 \v 3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, \q2 msifuni kwa kinubi na zeze, \q1 \v 4 msifuni kwa matari na kucheza, \q2 msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, \q1 \v 5 msifuni kwa matoazi yaliayo, \q2 msifuni kwa matoazi yavumayo sana. \b \q1 \v 6 Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu. \b \q1 Msifuni Mwenyezi Mungu!