\id PHM - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Filemoni \toc1 Filemoni \toc2 Filemoni \toc3 Flm \mt1 Filemoni \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Paulo, mfungwa wa Al-Masihi Isa, pamoja na Timotheo ndugu yetu. \po Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu, \v 2 kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kundi la waumini wanaokutana nyumbani mwako. \po \v 3 Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba\f + \fr 1:3 \fr*\ft Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi. \s1 Shukrani na maombi \p \v 4 Siku zote ninamshukuru Mungu wangu ninapokukumbuka katika maombi yangu, \v 5 kwa sababu ninasikia kuhusu imani yako katika Bwana Isa na upendo wako kwa watakatifu wote. \v 6 Naomba utiwe nguvu katika kushiriki imani yako na wengine, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu wa kila kitu chema tunachoshiriki kwa ajili ya Al-Masihi. \v 7 Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu. \s1 Paulo anamtetea Onesimo \p \v 8 Hata hivyo, ingawa katika Al-Masihi ningekuwa na ujasiri wa kukuagiza yale yakupasayo kutenda, \v 9 lakini ninakuomba kwa upendo. Mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Al-Masihi Isa, \v 10 nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo\f + \fr 1:10 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Wa manufaa\fqa*\f*, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo. \v 11 Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia. \p \v 12 Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa. \v 13 Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili. \v 14 Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari. \v 15 Huenda sababu ya Onesimo kutengwa nawe kwa muda ni ili uwe naye daima, \v 16 si kama mtumwa sasa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana Isa. \p \v 17 Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika nawe, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe. \v 18 Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi. \v 19 Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa hilo deni. Kumbuka kwamba nakudai hata nafsi yako. \v 20 Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana Isa, yaani uniburudishe moyo wangu katika Al-Masihi. \v 21 Huku nikiwa na hakika ya kutii kwako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba. \p \v 22 Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu. \b \b \s1 Salamu za mwisho \p \v 23 Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Al-Masihi Isa, anakusalimu. \p \v 24 Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu. \b \p \v 25 Neema ya Bwana Isa Al-Masihi iwe pamoja na roho zenu. Amen.