\id NAM - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Nahumu \toc1 Nahumu \toc2 Nahumu \toc3 Nah \mt1 Nahumu \c 1 \p \v 1 Neno la unabii kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono cha Nahumu Mwelkoshi. \b \s1 Hasira ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Ninawi \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; \q2 Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. \q1 Mwenyezi Mungu hulipiza kisasi juu ya watesi wake, \q2 naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake. \q1 \v 3 Mwenyezi Mungu si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, \q2 Mwenyezi Mungu hataacha kuadhibu wenye hatia. \q1 Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, \q2 na mawingu ni vumbi la miguu yake. \q1 \v 4 Anakemea bahari na kuikausha, \q2 anafanya mito yote kukauka. \q1 Bashani na Karmeli zinanyauka \q2 na maua ya Lebanoni hukauka. \q1 \v 5 Milima hutikisika mbele yake \q2 na vilima huyeyuka. \q1 Nchi hutetemeka mbele yake, \q2 dunia na wote wanaoishi ndani yake. \q1 \v 6 Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu? \q2 Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali? \q1 Ghadhabu yake imemiminwa kama moto, \q2 na miamba inapasuka mbele zake. \b \q1 \v 7 Mwenyezi Mungu ni Mwema, \q2 kimbilio wakati wa taabu. \q1 Huwatunza wale wanaomtegemea, \q2 \v 8 lakini kwa mafuriko makubwa, \q1 ataangamiza Ninawi; \q2 atafuatilia adui zake hadi gizani. \b \q1 \v 9 Kila njama wanayopanga dhidi ya Mwenyezi Mungu \q2 yeye atalikomesha; \q2 taabu haitatokea mara ya pili. \q1 \v 10 Watasongwa katikati ya miiba \q2 na kulewa kwa mvinyo wao. \q2 Watateketezwa kama mabua makavu. \q1 \v 11 Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, \q2 ambaye anapanga njama \q1 dhidi ya Mwenyezi Mungu \q2 na kushauri uovu. \p \v 12 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, \q2 watakatiliwa mbali na kuangamia. \q1 Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, \q2 sitakutesa tena. \q1 \v 13 Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, \q2 nami nitazivunjilia mbali pingu zako.” \b \q1 \v 14 Hii ndiyo amri Mwenyezi Mungu aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: \q2 “Hutakuwa na wazao \q2 watakaoendeleza jina lako. \q1 Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kusubu \q2 zilizopo katika hekalu la miungu yenu. \q1 Nitaandaa kaburi lako, \q2 kwa maana wewe ni mwovu kabisa.” \b \q1 \v 15 Tazama, huko juu milimani, \q2 miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, \q2 ambaye anatangaza amani! \q1 Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako, \q2 nawe utimize nadhiri zako. \q1 Waovu hawatakuvamia tena; \q2 wataangamizwa kabisa. \c 2 \s1 Kuanguka kwa Ninawi \q1 \v 1 Mshambuliaji anasogea dhidi yako, Ninawi. \q2 Linda ngome yako, \q2 chunga barabara, \q2 jitieni nguvu wenyewe, \q2 kusanya nguvu zako zote! \b \q1 \v 2 Mwenyezi Mungu atarudisha fahari ya Yakobo, \q2 kama fahari ya Israeli, \q1 ingawa waangamizi wamewaacha ukiwa \q2 na wameharibu mizabibu yao. \b \q1 \v 3 Ngao za askari wake ni nyekundu, \q2 mashujaa wamevaa nguo nyekundu. \q1 Chuma kwenye magari ya vita chametameta, \q2 katika siku aliyoyaweka tayari, \q2 mikuki ya msunobari inametameta. \q1 \v 4 Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani, \q2 yakikimbia nyuma na mbele uwanjani. \q1 Yanaonekana kama mienge ya moto; \q2 yanaenda kasi kama umeme. \b \q1 \v 5 Anaita vikosi vilivyochaguliwa, \q2 lakini bado wanajikwaa njiani. \q1 Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji, \q2 ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa. \q1 \v 6 Malango ya mto yamefunguliwa wazi, \q2 na jumba la kifalme limeanguka. \q1 \v 7 Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe \q2 na upelekwe uhamishoni. \q1 Vijakazi wake wanaomboleza kama hua \q2 na kupigapiga vifua vyao. \q1 \v 8 Ninawi ni kama dimbwi, \q2 nayo maji yake yanakauka. \q1 Wanalia, “Simama! Simama!” \q2 Lakini hakuna anayegeuka nyuma. \q1 \v 9 Chukueni nyara za fedha! \q2 Chukueni nyara za dhahabu! \q1 Wingi wake hauna mwisho, \q2 utajiri kutoka hazina zake zote! \q1 \v 10 Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi! \q2 Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea, \q1 miili inatetemeka, \q2 na kila uso umebadilika rangi. \b \q1 \v 11 Liko wapi sasa pango la simba, \q2 ambapo waliwalisha watoto wao, \q1 ambapo simba dume na simba jike walienda, \q2 na wana simba pia, \q2 bila kuogopa chochote? \q1 \v 12 Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake, \q2 alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake, \q1 akijaza makao yake kwa alivyoua \q2 na mapango yake kwa mawindo. \b \q1 \v 13 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anatangaza, \q2 “Mimi ni kinyume na ninyi. \q1 Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto, \q2 na upanga utakula wana simba wako. \q2 Sitawaachia mawindo juu ya nchi. \q1 Sauti za wajumbe wako \q2 hazitasikika tena.” \c 3 \s1 Ole wa Ninawi \q1 \v 1 Ole wa mji unaomwaga damu, \q2 uliojaa uongo, \q1 uliojaa nyara, \q2 na usiokosa mateka. \q1 \v 2 Kelele za mijeledi, \q2 vishindo vya magurudumu, \q1 farasi wanaoenda mbio \q2 na mshtuo wa magari ya vita! \q1 \v 3 Wapanda farasi wanaenda mbio, \q2 panga zinametameta, \q2 na mikuki inang’aa! \q1 Majeruhi wengi, \q2 malundo ya maiti, \q1 idadi ya miili isiyohesabika, \q2 watu wanajikwaa juu ya mizoga: \q1 \v 4 haya yote kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba, \q2 anayeshawishi, bibi mkuu wa mambo ya uchawi, \q1 anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake \q2 na pia jamaa za watu kwa ulozi wake. \b \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anasema, \q2 “Mimi ni kinyume na ninyi. \q2 Nitafunika uso wako kwa gauni lako. \q1 Nitaonesha mataifa uchi wako \q2 na falme aibu yako. \q1 \v 6 Nitakutupia uchafu, \q2 nitakufanyia dharau \q2 na kukufanya kioja. \q1 \v 7 Wote wanaokuona watakukimbia na kusema, \q2 ‘Ninawi inaangamia, \q1 nani atakayeomboleza kwa ajili yake?’ \q2 Nitampata wapi yeyote wa kukufariji?” \b \q1 \v 8 Je, wewe ni bora kuliko No-Amoni\f + \fr 3:8 \fr*\ft au \ft*\fqa Thebesi\fqa*\f*, \q2 uliopo katika Mto Naili, \q2 uliozungukwa na maji? \q1 Mto ulikuwa kinga yake, \q2 nayo maji yalikuwa ukuta wake. \q1 \v 9 Kushi na Misri walikuwa nguvu zake zisizo na mpaka; \q2 Putu na Libia walikuwa miongoni mwa wale walioungana naye. \q1 \v 10 Hata hivyo alichukuliwa mateka \q2 na kwenda uhamishoni. \q1 Watoto wake wachanga walivunjwa vunjwa vipande \q2 kwenye mwanzo wa kila barabara. \q1 Kura zilipigwa kwa watu wake wenye heshima, \q2 na watu wake wote wakuu walifungwa kwa minyororo. \q1 \v 11 Wewe pia utalewa; \q2 utaenda mafichoni \q2 na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui. \b \q1 \v 12 Ngome zako zote ni kama mitini \q2 yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva; \q1 wakati inapotikiswa, \q2 tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. \q1 \v 13 Tazama vikosi vyako: \q2 wote ni wanawake! \q1 Malango ya nchi yako \q2 yamekuwa wazi kwa adui zako; \q2 moto umeteketeza mapingo yake. \b \q1 \v 14 Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako, \q2 imarisha ulinzi wako, \q1 Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi, \q2 yakanyage matope, \q2 karabati tanuru la kuchomea matofali! \q1 \v 15 Huko moto utakuteketeza, \q2 huko upanga utakuangusha chini \q2 na kama vile panzi, watakumaliza. \q1 Ongezeka kama panzi, \q2 ongezeka kama nzige! \q1 \v 16 Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako \q2 hata wamekuwa wengi kuliko nyota za angani, \q1 lakini kama nzige wanaacha nchi tupu \q2 kisha huruka na kwenda zake. \q1 \v 17 Walinzi wako ni kama nzige, \q2 maafisa wako kama makundi ya nzige \q2 wanaotua kwenye kuta wakati wa siku ya baridi; \q1 lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, \q2 na hakuna anayejua wanakoenda. \b \q1 \v 18 Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia; \q2 wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika. \q1 Watu wako wametawanyika juu ya milima \q2 bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya. \q1 \v 19 Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako; \q2 jeraha lako ni la kukuua. \q1 Kila anayesikia habari zako, \q2 hupiga makofi kwa kuanguka kwako, \q1 kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa \q2 na ukatili wako usio na mwisho?