\id MRK - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Marko \toc1 Marko \toc2 Marko \toc3 Mk \mt1 Marko \c 1 \ms1 Huduma ya Yahya \mr (Marko 1:1-13) \s1 Yahya atayarisha njia \r (Mathayo 3:1-12; Luka 3:1-8; Yohana 1:19-28) \p \v 1 Mwanzo wa Injili ya Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu\f + \fr 1:1 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*, \v 2 kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: \q1 “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, \q2 atakayetengeneza njia mbele yako”: \q1 \v 3 “sauti ya mtu aliaye nyikani, \q1 ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, \q2 yanyoosheni mapito yake.’ ” \m \v 4 Yahya alikuja akibatiza\f + \fr 1:4 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali.\ft*\f* huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. \v 5 Watu kutoka Yudea yote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. \v 6 Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Alikula nzige na asali ya mwitu. \v 7 Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. \v 8 Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho wa Mungu.” \s1 Isa abatizwa \r (Mathayo 3:13-17; Luka 3:21-22) \p \v 9 Wakati huo Isa akaja kutoka Nasiri ya Galilaya, naye akabatizwa na Yahya katika Mto Yordani. \v 10 Isa alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho wa Mungu akishuka juu yake kama hua. \v 11 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.” \s1 Isa ajaribiwa nyikani \r (Mathayo 4:1-11; Luka 4:1-13) \p \v 12 Wakati huo huo, Roho wa Mungu akamwongoza Isa hadi nyikani, \v 13 naye Isa akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama pori, nao malaika wakamhudumia. \ms1 Huduma ya Isa huko Galilaya \mr (Marko 1:14–9:50) \s1 Isa aanza kuhubiri \r (Mathayo 4:12-17; Luka 4:14-15) \p \v 14 Baada ya Yahya kutiwa gerezani, Isa alienda Galilaya, akaanza kuhubiri Injili ya Mungu, \v 15 akisema, “Wakati umetimia, ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Injili.” \s1 Wanafunzi wa kwanza wa Isa \r (Mathayo 4:18-22; Luka 5:1-11; Yohana 1:35-51) \p \v 16 Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi. \v 17 Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” \v 18 Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata. \p \v 19 Alipoenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. \v 20 Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Isa. \s1 Isa atoa pepo mchafu \r (Luka 4:31-37) \p \v 21 Wakaenda hadi Kapernaumu. Mara ilipofika siku ya Sabato, Isa akaingia sinagogi\f + \fr 1:21 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f*, akaanza kufundisha. \v 22 Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama walimu wa Torati. \v 23 Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye akapaza sauti akisema, \v 24 “Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!” \p \v 25 Lakini Isa akamkemea, akamwamuru, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu!” \v 26 Yule pepo mchafu akamgaragaza huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa. \p \v 27 Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” \v 28 Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya. \s1 Isa amponya mama mkwe wa Simoni na pia watu wengi \r (Mathayo 8:14-17; Luka 4:38-41) \p \v 29 Mara walipotoka katika sinagogi, walienda pamoja na Yakobo na Yohana hadi nyumbani mwa Simoni na Andrea. \v 30 Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake. \v 31 Hivyo Isa akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia. \p \v 32 Jioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Isa wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu. \v 33 Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo. \v 34 Isa akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani. \s1 Isa aenda Galilaya \r (Luka 4:42-44) \p \v 35 Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Isa akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. \v 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta, \v 37 nao walipomwona, wakapaza sauti, wakasema, “Kila mtu anakutafuta!” \p \v 38 Isa akawajibu, “Twendeni mahali pengine, kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia. Maana nilikuja kwa kusudi hili.” \v 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu. \s1 Isa amtakasa mtu mwenye ukoma \r (Mathayo 8:1-4; Luka 5:12-16) \p \v 40 Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Isa, akapiga magoti, akimwomba, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.” \p \v 41 Isa, akiwa amejawa na huruma, akaunyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!” \v 42 Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika. \p \v 43 Baada ya Isa kumwonya vikali, akamruhusu aende zake mara moja; \v 44 akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajioneshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Musa kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.” \v 45 Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Isa hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi bali alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande. \c 2 \s1 Isa amponya mtu aliyepooza \r (Mathayo 9:1-8; Luka 5:17-26) \p \v 1 Baada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba yupo nyumbani. \v 2 Watu wengi wakakusanyika, kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. \v 3 Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Isa mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. \v 4 Kwa kuwa hawakuweza kumfikisha kwa Isa kwa sababu ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa juu ya mahali Isa alikuwa, wakamshusha mtu aliyepooza akiwa amelalia mkeka wake. \v 5 Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.” \p \v 6 Basi baadhi ya walimu wa Torati waliokuwa wameketi pale wakawaza mioyoni mwao, \v 7 “Kwa nini mtu huyu anasema hivi? Huyu anakufuru! Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?” \p \v 8 Mara moja Isa akatambua rohoni mwake kile walichokuwa wanawaza mioyoni mwao, naye akawaambia, “Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? \v 9 Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’? \v 10 Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi”: Isa akamwambia yule aliyepooza, \v 11 “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.” \v 12 Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!” \s1 Isa amwita Lawi \r (Mathayo 9:9-13; Luka 5:27-32) \p \v 13 Isa akaenda tena kandokando ya Bahari ya Galilaya. Umati mkubwa wa watu wakamfuata, naye akaanza kuwafundisha. \v 14 Alipokuwa akitembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Isa akamwambia, “Nifuate.” Naye Lawi akaondoka, akamfuata Isa. \p \v 15 Isa alipokuwa ameketi akila chakula nyumbani mwa Lawi, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuwa wakila pamoja naye na wanafunzi wake, kwa maana ni watu wengi waliokuwa wakimfuata. \v 16 Walimu wa Torati waliokuwa Mafarisayo\f + \fr 2:16 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* walipomwona akila pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, wakawauliza wanafunzi wake: “Mbona Isa anakula na watoza ushuru na wenye dhambi?” \p \v 17 Isa aliposikia haya akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” \s1 Isa aulizwa kuhusu kufunga \r (Mathayo 9:14-17; Luka 5:33-39) \p \v 18 Basi wanafunzi wa Yahya pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Watu wakamjia Isa na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” \p \v 19 Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati angali pamoja nao? Wakati bwana arusi bado yuko pamoja nao, hawawezi kufunga. \v 20 Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Siku hiyo ndipo watakapofunga. \p \v 21 “Hakuna mtu ashoneaye kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, kile kiraka kipya kitachanika kutoka ile nguo iliyochakaa, nayo itachanika zaidi. \v 22 Wala hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo hiyo divai itamwagika na viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.” \s1 Isa ni Bwana wa Sabato \r (Mathayo 12:1-8; Luka 6:1-5) \p \v 23 Siku moja ya Sabato, Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke. \v 24 Mafarisayo wakamwambia, “Tazama, mbona wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato?” \p \v 25 Isa akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi yeye na wenzake walipokuwa na njaa, wakahitaji chakula? \v 26 Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani tu. Naye pia akawapa wenzake.” \p \v 27 Kisha Isa akawaambia, “Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, lakini si mwanadamu kwa ajili ya Sabato. \v 28 Hivyo, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” \c 3 \s1 Isa amponya mtu aliyepooza mkono \r (Mathayo 12:9-14; Luka 6:6-11) \p \v 1 Isa akaingia tena ndani ya sinagogi\f + \fr 3:1 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f*, na kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. \v 2 Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya huyo mtu siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. \v 3 Isa akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.” \p \v 4 Kisha Isa akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza. \p \v 5 Isa akawatazama kwa hasira watu waliomzunguka pande zote, akahuzunika sana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa umeponywa kabisa! \v 6 Kisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya njama ya kumuua Isa wakishirikiana na Maherode\f + \fr 3:6 \fr*\ft Wafuasi wa Mfalme Herode waliokubaliana na utawala wa Rumi.\ft*\f*. \s1 Makundi ya watu wamfuata Isa \p \v 7 Isa na wanafunzi wake wakaondoka huko, wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya wakamfuata. \v 8 Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, makundi ya watu wakamjia kutoka Yudea, Yerusalemu, Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, pamoja na wale wa maeneo ya Tiro na Sidoni. \v 9 Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake watayarishe mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga. \v 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa. \v 11 Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu\f + \fr 3:11 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*.” \v 12 Lakini aliwaonya wasiwaambie wengine kumhusu. \s1 Isa achagua mitume kumi na wawili \r (Mathayo 10:1-4; Luka 6:12-16) \p \v 13 Isa akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia. \v 14 Akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa naye, na awatume kwenda kuhubiri \v 15 na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. \b \lh \v 16 Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: \b \li1 Simoni (ambaye alimwita Petro); \li1 \v 17 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); \li1 \v 18 Andrea, \li1 Filipo, \li1 Bartholomayo, \li1 Mathayo, \li1 Tomaso, \li1 Yakobo mwana wa Alfayo, \li1 Thadayo, \li1 Simoni Mkananayo\f + \fr 3:18 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mzelote\fqa*\ft ; Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi.\ft*\f*, \li1 \v 19 na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa. \s1 Isa na Beelzebuli \r (Mathayo 12:22-32; Luka 11:14-23) \p \v 20 Kisha Isa alipoingia ndani ya nyumba, umati wa watu wakakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. \v 21 Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.” \p \v 22 Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli\f + \fr 3:22 \fr*\ft kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Beelzebubu\fqa*\ft , yaani mkuu wa pepo wachafu\ft*\f*! Anatoa pepo wachafu kwa nguvu ya mkuu wa pepo wachafu!” \p \v 23 Basi Isa akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani? \v 24 Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. \v 25 Nayo nyumba ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. \v 26 Na kama Shetani akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama, bali mwisho wake umetimia. \v 27 Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali yake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali yake. \v 28 Amin, nawaambia, watu wataweza kusamehewa dhambi na kufuru zao zote; \v 29 lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” \p \v 30 Isa alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.” \s1 Mama yake na ndugu zake Isa \r (Mathayo 12:46-50; Luka 8:19-21) \p \v 31 Kisha wakaja ndugu zake Isa pamoja na mama yake. Wakiwa wamesimama nje, wakamtuma mtu kumwita. \v 32 Umati wa watu walikuwa wameketi kumzunguka, nao wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.” \p \v 33 Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni nani?” \p \v 34 Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, “Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. \v 35 Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu.” \c 4 \s1 Mfano wa mpanzi \r (Mathayo 13:1-9; Luka 8:1-8) \p \v 1 Isa akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Palikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika kumzunguka, hata ikambidi Isa aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari. \v 2 Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: \v 3 “Sikilizeni! Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu \v 4 Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. \v 5 Nyingine zilianguka kwenye mwamba usio na udongo mwingi. Ziliota haraka kwa kuwa udongo ulikuwa kidogo. \v 6 Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. \v 7 Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao. \v 8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua, zikatoa mazao, moja mara thelathini, nyingine mara sitini, na nyingine mara mia moja.” \p \v 9 Kisha Isa akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” \s1 Sababu ya kufundisha kwa mifano \r (Mathayo 13:10-17; Luka 8:9-10) \p \v 10 Alipokuwa peke yake, watu waliokuwa naye pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili wakamuuliza kuhusu mifano yake. \v 11 Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa siri ya ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walio nje, kila kitu husemwa kwa mifano, \v 12 ili, \q1 “ ‘kuona waone lakini wasitambue, \q2 na kusikia wasikie lakini wasielewe; \q1 wasije wakageuka na kusamehewa!’ ” \s1 Maelezo ya mfano wa mbegu \r (Mathayo 13:18-23; Luka 8:11-15) \p \v 13 Kisha Isa akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? \v 14 Yule mpanzi hupanda neno. \v 15 Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, mara Shetani huja na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao. \v 16 Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha. \v 17 Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani. \v 18 Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno; \v 19 lakini masumbufu ya maisha haya, na udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. \v 20 Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kuzaa mazao. Wao huzaa mara thelathini, au mara sitini, au mara mia ya mbegu iliyopandwa.” \s1 Mfano wa taa \r (Luka 8:16-18) \p \v 21 Akawaambia, “Je, taa huwashwa na kufunikwa chini ya kikapu au mvunguni mwa kitanda? Je, haiwashwi na kuwekwa juu ya kinara chake? \v 22 Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. \v 23 Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” \p \v 24 Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi. \v 25 Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.” \s1 Mfano wa mbegu inayoota \p \v 26 Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. \v 27 Baada yake kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. \v 28 Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. \v 29 Mara nafaka inapokuwa imekomaa, mkulima huenda shambani na mundu kuvuna, maana mavuno yamekuwa tayari.” \s1 Mfano wa punje ya haradali \r (Mathayo 13:31-32; Luka 13:18-19) \p \v 30 Akawaambia tena, “Tuufananishe ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza? \v 31 Ni kama punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. \v 32 Lakini ikipandwa, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye kivuli chake.” \p \v 33 Kwa mifano mingine mingi kama hii Isa alinena nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulielewa. \v 34 Hakusema nao neno lolote pasipo mfano. Lakini alipokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu. \s1 Isa atuliza dhoruba \r (Mathayo 8:23-27; Luka 8:22-25) \p \v 35 Ilipokaribia jioni ya siku hiyo, Isa akawaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.” \v 36 Wakaacha umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua zingine nyingi pamoja naye. \v 37 Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. \v 38 Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?” \p \v 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, “Uwe kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa. \p \v 40 Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?” \p \v 41 Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!” \c 5 \s1 Isa amponya mtu mwenye pepo mchafu \r (Mathayo 8:28-34; Luka 8:26-39) \p \v 1 Isa na wanafunzi wake wakafika upande wa pili wa ziwa, wakaingia katika nchi ya Wagerasi. \v 2 Isa alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini, akakutana naye. \v 3 Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo. \v 4 Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia. \v 5 Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe. \p \v 6 Alipomwona Isa kwa mbali, alimkimbilia, akapiga magoti mbele yake. \v 7 Akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu\f + \fr 5:7 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f* Aliye Juu Sana? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!” \v 8 Kwa kuwa Isa alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe pepo mchafu!” \p \v 9 Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” \p Akamjibu, “Jina langu ni Legioni\f + \fr 5:9 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Jeshi\fqa*\f*, kwa kuwa tuko wengi.” \v 10 Akamsihi Isa sana asiwapeleke nje ya nchi ile. \p \v 11 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima. \v 12 Wale pepo wachafu wakamsihi Isa wakisema, “Tuamuru twende kwenye wale nguruwe. Turuhusu tuwaingie.” \v 13 Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao elfu mbili, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama. \p \v 14 Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakaenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia. \v 15 Walipofika kwa Isa, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na legioni ya pepo wachafu akiwa ameketi hapo, amevaa nguo na mwenye akili timamu. Wakaogopa. \v 16 Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine yaliyomtokea yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu, na habari za lile kundi la nguruwe pia. \v 17 Basi watu wakaanza kumwomba Isa aondoke katika nchi yao. \p \v 18 Isa alipokuwa anaingia kwenye mashua, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu akamsihi Isa waende pamoja. \v 19 Isa hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Mwenyezi Mungu, na jinsi alivyokuhurumia.” \v 20 Yule mtu akaenda zake, akaanza kutangaza katika Dekapoli mambo makuu Isa aliyomtendea. Nao watu wote wakastaajabu. \s1 Isa amponya mwanamke na kumfufua msichana \r (Mathayo 9:18-26; Luka 8:40-56) \p \v 21 Isa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu wakamzunguka hapo kando ya bahari. \v 22 Kisha mmoja wa viongozi wa sinagogi\f + \fr 5:22 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake, \v 23 akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye ataishi.” \v 24 Hivyo Isa akaenda pamoja naye. \p Umati mkubwa wa watu wakamfuata, nao watu wakawa wanamsonga. \v 25 Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na mbili. \v 26 Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya. \v 27 Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, \v 28 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikiligusa vazi lake tu, nitaponywa.” \v 29 Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa. \p \v 30 Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akageukia umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?” \p \v 31 Wanafunzi wake wakamjibu, “Unaona jinsi watu wanavyokusonga. Wawezaje kuuliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’ ” \p \v 32 Lakini Isa akaangalia pande zote ili aone ni nani aliyemgusa. \v 33 Yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni pake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. \v 34 Isa akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako.” \p \v 35 Alipokuwa bado anaongea, watu wakafika kutoka nyumbani mwa Yairo. Wakamwambia, “Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?” \p \v 36 Aliposikia hayo waliyosema, Isa akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, “Usiogope. Amini tu.” \p \v 37 Hakumruhusu mtu yeyote amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo. \v 38 Walipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi, Isa akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa. \v 39 Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, “Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu.” \v 40 Wale watu wakamcheka. \p Baada ya kuwafukuza wote nje, Isa akaenda na baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaingia ndani hadi pale alipokuwa mtoto yule. \v 41 Akamshika mtoto mkono, akamwambia, \tl “Talitha koum!”\tl* (maana yake, “Msichana, nakuambia: amka!”) \v 42 Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili). Walipoona haya, wakastaajabu sana. \v 43 Isa akawaagiza kwa ukali wasimweleze mtu yeyote jambo hilo, naye akawaambia wampe yule msichana chakula. \c 6 \s1 Isa akataliwa Nasiri \r (Mathayo 13:53-58; Luka 4:16-30) \p \v 1 Isa akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiandamana na wanafunzi wake. \v 2 Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa. \p Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! \v 3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose\f + \fr 6:3 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Yusufu\fqa*\f*, Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini. \p \v 4 Isa akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani mwake.” \v 5 Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. \v 6 Naye akashangazwa sana kwa kutoamini kwao. \s1 Isa awatuma wale kumi na wawili \r (Mathayo 10:5-15; Luka 9:1-6) \p Kisha Isa akawa anaenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha. \v 7 Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu. \p \v 8 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu. \v 9 Vaeni viatu, lakini msivae nguo ya ziada. \v 10 Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. \v 11 Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwe ushuhuda dhidi yao.” \p \v 12 Kwa hiyo wakaenenda na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi. \v 13 Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya. \s1 Yahya akatwa kichwa \r (Mathayo 14:1-12; Luka 9:7-9) \p \v 14 Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Isa lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yahya amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.” \p \v 15 Wengine wakasema, “Yeye ni Ilya.” \p Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmoja wa manabii wa zamani.” \p \v 16 Lakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, “Huyo ni Yahya, niliyemkata kichwa, amefufuliwa kutoka kwa wafu!” \p \v 17 Herode mwenyewe alikuwa ameagiza kwamba Yahya akamatwe, afungwe na kutiwa gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, ambaye Herode alikuwa amemwoa. \v 18 Yahya alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako.” \v 19 Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yahya kinyongo, akataka kumuua. Lakini hakuweza, \v 20 kwa sababu Herode alimwogopa Yahya akijua kwamba ni mtu mwenye haki na mtakatifu, hivyo akamlinda. Herode alifadhaika sana alipomsikia Yohana, lakini bado alipenda kumsikiliza. \p \v 21 Hatimaye Herodia alipata wakati mwafaka aliokuwa akiutafuta. Mfalme Herode alifanya karamu kubwa wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. \v 22 Binti Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani. \p Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu chochote utakacho, nami nitakupa.” \v 23 Tena akamwahidi kwa kiapo, akamwambia, “Chochote utakachoomba nitakupa, hata kama ni nusu ya ufalme wangu.” \p \v 24 Yule binti akatoka nje, akaenda kumuuliza mama yake, “Niombe nini?” \p Mama yake akamjibu, “Omba kichwa cha Yahya.” \p \v 25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme, akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yahya kwenye sinia.” \p \v 26 Mfalme akasikitika sana, lakini kwa sababu alikuwa ameapa viapo mbele ya wageni wake, hakutaka kumkatalia. \v 27 Mara mfalme akatuma askari mmoja wa walinzi wake kukileta kichwa cha Yahya. Akaenda na kumkata Yahya kichwa humo gerezani, \v 28 akakileta kichwa chake kwenye sinia na kumpa yule msichana, naye yule msichana akampa mama yake. \v 29 Wanafunzi wa Yahya walipopata habari hizi, wakaja na kuuchukua mwili wake, wakauzika kaburini. \s1 Isa alisha wanaume 5,000 \r (Mathayo 14:13-21; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14) \p \v 30 Wale mitume wakakusanyika kwa Isa na kumpa taarifa ya mambo yote waliyokuwa wamefanya na kufundisha. \v 31 Basi kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakawa hawana nafasi ya kula, Isa akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” \p \v 32 Hivyo wakaondoka kwa mashua peke yao, wakaenda mahali pasipo na watu. \v 33 Lakini watu wengi waliowaona wakiondoka, wakawatambua, nao wakaenda haraka kwa miguu kutoka miji yote, nao wakatangulia kufika. \v 34 Isa alipofika kando ya bahari, aliona kundi kubwa la watu, akawahurumia kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi. \p \v 35 Mchana ulipokuwa umeendelea sana, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, nazo saa zimeenda sana. \v 36 Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula.” \p \v 37 Lakini Isa akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.” \p Wakamwambia, “Je, twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili\f + \fr 6:37 \fr*\ft Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja.\ft*\f* ili tuwape watu hawa wale?” \p \v 38 Akawauliza, “Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” \p Walipokwisha kujua, wakarudi, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.” \p \v 39 Kisha Isa akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani, \v 40 nao wakaketi kwenye vikundi vya watu mia mia, na wengine hamsini hamsini. \v 41 Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. \v 42 Watu wote wakala, wakashiba. \v 43 Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. \v 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano. \s1 Isa atembea juu ya maji \r (Mathayo 14:22-33; Yohana 6:16-21) \p \v 45 Mara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua wamtangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale watu. \v 46 Baada ya kuwaaga, akaenda mlimani kuomba. \p \v 47 Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Isa alikuwa peke yake katika nchi kavu. \v 48 Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, \v 49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, \v 50 kwa sababu wote walipomwona waliogopa. \p Mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!” \v 51 Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa, \v 52 kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu. \s1 Isa awaponya wagonjwa Genesareti \r (Mathayo 14:34-36) \p \v 53 Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga. \v 54 Mara waliposhuka kutoka mashua yao, watu wakamtambua Isa. \v 55 Wakaenda katika vijiji vyote upesi, wakawabeba wagonjwa kwenye mikeka ili kuwapeleka mahali popote waliposikia kuwa Isa yupo. \v 56 Kila mahali Isa alipoenda, iwe vijijini, mijini au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni. Wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa waguse japo upindo wa vazi lake. Nao wote waliomgusa waliponywa. \c 7 \s1 Mapokeo ya wazee \r (Mathayo 15:1-20) \p \v 1 Mafarisayo\f + \fr 7:1 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na baadhi ya walimu wa Torati waliokuwa wametoka Yerusalemu wakakusanyika mbele ya Isa. \v 2 Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani bila kunawa kama ilivyotakiwa na Torati ya Wayahudi. \v 3 (Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata desturi za wazee wao. \v 4 Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi zingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba.) \p \v 5 Hivyo, wale Mafarisayo na walimu wa Torati wakamuuliza Isa, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee, na badala yake wanakula kwa mikono najisi?” \p \v 6 Isa akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa: \q1 “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, \q2 lakini mioyo yao iko mbali nami. \q1 \v 7 Huniabudu bure, \q2 nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’ \m \v 8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.” \p \v 9 Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu! \v 10 Kwa mfano, Musa alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ \v 11 Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu), \v 12 basi hawajibiki tena kumsaidia baba yake au mama yake. \v 13 Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya aina hiyo.” \s1 Vitu vinavyomnajisi mtu \r (Mathayo 15:10-20) \p \v 14 Isa akaita tena umati ule wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, na mwelewe jambo hili. \v 15 Hakuna kitu kinachomwingia mtu kimtiacho unajisi, lakini kile kimtokacho ndicho kimtiacho unajisi. [ \v 16 Kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia na asikie.]\f + \fr 7:16 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*” \p \v 17 Baada ya Isa kuacha ule umati wa watu na kuingia ndani, wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano ule. \v 18 Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi? \v 19 Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Isa alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni safi.) \p \v 20 Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. \v 21 Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, \v 22 tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. \v 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.” \s1 Imani ya mwanamke Myunani \r (Mathayo 15:21-28) \p \v 24 Ndipo Isa akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha. \v 25 Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake. \v 26 Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria. Akamsihi Isa amtoe binti yake huyo pepo mchafu. \p \v 27 Isa akamwambia, “Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” \p \v 28 Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.” \p \v 29 Ndipo Isa akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, nenda zako nyumbani; yule pepo mchafu amemtoka binti yako.” \p \v 30 Akaenda zake nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, yule pepo mchafu akiwa amemtoka. \s1 Isa amponya mtu aliyekuwa kiziwi na bubu \p \v 31 Kisha Isa akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli. \v 32 Huko, watu wakamletea Isa mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu. \p \v 33 Isa akampeleka yule kiziwi kando, mbali na watu, akatia vidole vyake masikioni mwa yule mtu. Kisha akatema mate na kuugusa ulimi wa yule mtu. \v 34 Ndipo Isa akatazama mbinguni, akashusha pumzi kwa nguvu, akamwambia, \tl “Efatha!”\tl* (yaani, “Funguka!”) \v 35 Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukaachiliwa, akaanza kuongea sawasawa. \p \v 36 Isa akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hizi. Lakini kadiri alivyowakanya, ndivyo walivyozidi kutangaza kwa bidii. \v 37 Walistaajabu mno. Wakasema, “Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!” \c 8 \s1 Isa alisha wanaume 4,000 \r (Mathayo 15:32-39) \p \v 1 Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu walikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Isa akawaita wanafunzi wake akawaambia, \v 2 “Ninahurumia umati huu wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. \v 3 Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali.” \p \v 4 Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?” \p \v 5 Isa akawauliza, “Mna mikate mingapi?” \p Wakajibu, “Tuna mikate saba.” \p \v 6 Akawaambia watu waketi chini. Akaichukua ile mikate saba na kushukuru, baadaye akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. \v 7 Walikuwa pia na visamaki vichache, Isa akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. \v 8 Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. \v 9 Watu waliokula walikuwa wapata elfu nne. Baada ya kuwaaga, \v 10 aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda sehemu za Dalmanutha. \s1 Mafarisayo waomba ishara \r (Mathayo 12:38-42) \p \v 11 Mafarisayo\f + \fr 8:11 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakaja, wakaanza kumhoji Isa. Ili kumtega, wakamwomba awaoneshe ishara kutoka mbinguni. \v 12 Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” \v 13 Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ng’ambo. \s1 Chachu ya Mafarisayo na ya Herode \r (Mathayo 16:5-12) \p \v 14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. \v 15 Isa akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.” \p \v 16 Wakajadiliana wao kwa wao, na kusema, “Anasema hivi kwa sababu hatukuleta mikate.” \p \v 17 Isa, akifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mnajadiliana kuhusu kutokuwa na mikate? Je, bado hamtambui wala hamwelewi? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? \v 18 Je, mna macho lakini mnashindwa kuona, na mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? \v 19 Nilipoimega ile mikate mitano kwa watu elfu tano, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa mabaki?” \p Wakamjibu, “Kumi na viwili.” \p \v 20 “Je, nilipoimega ile mikate saba kwa watu elfu nne, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa mabaki?” \p Wakamjibu, “Saba.” \p \v 21 Ndipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?” \s1 Isa amponya Kipofu huko Bethsaida \p \v 22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Isa amguse. \v 23 Isa akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Isa akamuuliza, “Unaona chochote?” \p \v 24 Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea.” \p \v 25 Isa akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. \v 26 Isa akamtuma nyumbani mwake, akamwambia, “Hata kijijini usiingie.” \s1 Petro amkiri Isa kuwa Al-Masihi \r (Mathayo 16:13-20; Luka 9:18-21) \p \v 27 Isa na wanafunzi wake wakaelekea vijiji vya Kaisaria-Filipi. Walipokuwa njiani, Isa akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?” \p \v 28 Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya, wengine husema ni Ilya, na bado wengine husema wewe ni mmoja wa manabii.” \p \v 29 Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” \p Petro akajibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 8:29 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*.” \p \v 30 Isa akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake. \s1 Isa atabiri kifo chake \r (Mathayo 16:21-28; Luka 9:22-27) \p \v 31 Ndipo akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa Mwana wa Adamu lazima atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na kwamba itampasa auawe lakini baada ya siku tatu afufuliwe. \v 32 Aliyasema haya waziwazi. Ndipo Petro akamchukua kando na akaanza kumkemea. \p \v 33 Lakini Isa akageuka na kuwaangalia wanafunzi wake, na akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” \p \v 34 Ndipo akawaita umati ule wa watu pamoja na wanafunzi wake, akasema, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. \v 35 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa. \v 36 Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? \v 37 Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? \v 38 Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu\f + \fr 8:38 \fr*\ft Mwana wa Adamu ni jina la Isa Al-Masihi kujishirikisha na udhaifu wa mwanadamu.\ft*\f* naye atamwonea aibu wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.” \c 9 \p \v 1 Isa akaendelea kuwaambia, “Amin, nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.” \s1 Isa abadilika sura \r (Mathayo 17:1-13; Luka 9:28-36) \p \v 2 Baada ya siku sita, Isa akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Isa akageuka sura mbele yao. \v 3 Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko vile mtu yeyote duniani angeweza kuyang’arisha. \v 4 Musa na Ilya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Isa. \p \v 5 Petro akamwambia Isa, “Mwalimu, ni vyema sisi tukae hapa. Turuhusu tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya.” \v 6 Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana. \p \v 7 Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, nayo sauti kutoka lile wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.” \p \v 8 Mara walipotazama huku na huku, hawakuona tena mtu mwingine yeyote pamoja nao isipokuwa Isa. \p \v 9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoyaona, hadi Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu. \v 10 Wakalihifadhi jambo hilo wao wenyewe, lakini wakawa wanajiuliza, “Huku kufufuka kwa wafu maana yake nini?” \p \v 11 Wakamuuliza, “Kwa nini walimu wa Torati husema kwamba ni lazima Ilya aje kwanza?” \p \v 12 Isa akawajibu, “Ni kweli, Ilya yuaja kwanza ili kutengeneza mambo yote. Mbona basi imeandikwa kwamba Mwana wa Adamu ni lazima ateseke sana na kudharauliwa? \v 13 Lakini nawaambia, Ilya amekwisha kuja, nao wakamtendea walivyopenda, kama ilivyoandikwa kumhusu.” \s1 Isa amponya kijana mwenye pepo mchafu \r (Mathayo 17:14-21; Luka 9:37-45) \p \v 14 Walipowafikia wale wanafunzi wengine, wakawakuta wamezungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa Torati wakibishana nao. \v 15 Mara wale watu walipomwona Isa, wakastaajabu sana, wakamkimbilia ili kumsalimu. \p \v 16 Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao kuhusu nini?” \p \v 17 Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea. \v 18 Kila mara huyo pepo mchafu ampagaapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.” \p \v 19 Isa akawaambia, “Enyi kizazi kisichoamini! Nitakuwa pamoja nanyi hadi lini? Nitawavumilia hadi lini? Mleteni mvulana kwangu.” \p \v 20 Nao wakamleta yule mvulana. Yule pepo mchafu alipomwona Isa, mara akamtia yule mvulana kifafa, akaanguka, akagaagaa chini huku akitokwa na povu kinywani. \p \v 21 Isa akamuuliza baba yake, “Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?” \p Akamjibu, “Tangu utoto wake. \v 22 Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie.” \p \v 23 Isa akamwambia, “Ati, ‘Kama unaweza kufanya jambo lolote’? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye.” \p \v 24 Mara baba yake yule mvulana akapaza sauti akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!” \p \v 25 Isa alipoona kwamba umati wa watu wanakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, “Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!” \p \v 26 Baada ya yule pepo mchafu kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, “Amekufa.” \v 27 Lakini Isa akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama. \p \v 28 Baada ya Isa kuingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza wakiwa peke yao, “Mbona sisi hatukuweza kumtoa huyo pepo mchafu?” \p \v 29 Isa akawajibu, “Pepo aina hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba [na kufunga]\f + \fr 9:29 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*.” \s1 Isa atabiri tena kifo chake na ufufuo \r (Mathayo 17:22-23; Luka 9:43-45) \p \v 30 Wakaondoka huko, wakapitia Galilaya. Isa hakutaka mtu yeyote afahamu mahali walipo, \v 31 kwa maana alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. Nao watamuua, lakini siku tatu baada ya kuuawa atafufuka.” \v 32 Lakini wao hawakuelewa kile alimaanisha, nao waliogopa kumuuliza maana yake. \s1 Aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni \r (Mathayo 18:1-5; Luka 9:46-48; 22:24-30) \p \v 33 Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini kule njiani?” \v 34 Lakini hawakumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu zaidi ya wote. \p \v 35 Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: “Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.” \p \v 36 Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, \v 37 “Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba\f + \fr 9:37 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu aliyenituma.” \s1 Yeyote asiye kinyume nasi yuko upande wetu \r (Luka 9:49-50) \p \v 38 Yohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamkataza, kwa sababu yeye si mmoja wetu.” \p \v 39 Isa akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu. \v 40 Kwa maana yeyote asiye kinyume chetu, yuko upande wetu. \v 41 Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Al-Masihi, hakika hataikosa thawabu yake. \s1 Kujaribiwa ili kutenda dhambi \r (Mathayo 18:6-9; Luka 17:1-2) \p \v 42 “Mtu yeyote akimsababisha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa baharini. \v 43 Mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia Jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [ \v 44 Ni mahali ambako funza wao hawafi wala moto wao hauzimiki.]\f + \fr 9:44 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \v 45 Mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia Jehanamu. [ \v 46 Ni mahali ambako funza wao hawafi wala moto wao hauzimiki.]\f + \fr 9:46 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \v 47 Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe. Ni afadhali kwako kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa Jehanamu. \v 48 Ni mahali ambako funza wao hawafi, wala moto wao hauzimiki. \m \v 49 Kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto. \p \v 50 “Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.” \c 10 \ms1 Safari ya kwenda Yerusalemu na matukio mjini \mr (Marko 10:1–12:44) \s1 Isa afundisha kuhusu talaka \r (Mathayo 19:1-12; Luka 16:18) \p \v 1 Isa akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Yudea. Umati mkubwa wa watu wakaenda kwake tena, naye akawafundisha, kama ilivyokuwa desturi yake. \p \v 2 Baadhi ya Mafarisayo\f + \fr 10:2 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?” \p \v 3 Isa akawajibu, “Je, Musa aliwaamuru nini?” \p \v 4 Wakajibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” \p \v 5 Isa akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. \v 6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke’. \v 7 ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, \v 8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. \v 9 Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” \p \v 10 Walipokuwa tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza kuhusu jambo hili. \v 11 Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. \v 12 Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.” \s1 Isa awabariki watoto wadogo \r (Mathayo 19:13-15; Luka 18:15-17) \p \v 13 Watu walikuwa wakimletea Isa watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wake wakawakemea. \v 14 Isa alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. \v 15 Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” \v 16 Akawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki. \s1 Kijana tajiri \r (Mathayo 19:16-30; Luka 18:18-30) \p \v 17 Isa alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” \p \v 18 Isa akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. \v 19 Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’ ” \p \v 20 Akamjibu, “Mwalimu, amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.” \p \v 21 Isa akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” \p \v 22 Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana. Akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi. \p \v 23 Isa akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!” \p \v 24 Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Isa akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika ufalme wa Mungu. \v 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” \p \v 26 Wanafunzi wake wakashangaa sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi awezaye kuokoka?” \p \v 27 Isa akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” \p \v 28 Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha kila kitu na kukufuata wewe!” \p \v 29 Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna mtu yeyote aliyeacha nyumba, ndugu wa kiume au wa kike, au mama au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, \v 30 ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao. \v 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wa mwisho watakuwa wa kwanza.” \s1 Isa atabiri tena kifo chake \r (Mathayo 20:17-19; Luka 18:31-34) \p \v 32 Walikuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, na Isa alikuwa amewatangulia. Wanafunzi wake walishangaa, nao watu waliowafuata walijawa na hofu. Isa akawachukua tena wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia yatakayompata. \v 33 Akasema, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atasalitiwa kwa viongozi wa makuhani na walimu wa Torati. Wao watamhukumu kifo na kumtia mikononi mwa watu wa Mataifa, \v 34 ambao watamdhihaki na kumtemea mate, watampiga na kumuua. Siku tatu baadaye atafufuka.” \s1 Ombi la Yakobo na Yohana \r (Mathayo 20:20-28) \p \v 35 Kisha Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie lolote tutakalokuomba.” \p \v 36 Naye akawaambia, “Je, mwataka niwafanyie jambo gani?” \p \v 37 Wakamwambia, “Tupe kukaa mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.” \p \v 38 Lakini Isa akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?” \p \v 39 Wakajibu, “Tunaweza.” \p Kisha Isa akawaambia, “Kikombe nikinyweacho mtakinywea na ubatizo nibatizwao mtabatizwa, \v 40 lakini kuketi mkono wangu wa kuume au wa kushoto si juu yangu mimi kuwapa. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wale walioandaliwa.” \p \v 41 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. \v 42 Lakini Isa akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa wale wanaodhaniwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu, nao wenye vyeo huonesha mamlaka yao. \v 43 Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, \v 44 na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote. \v 45 Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.” \s1 Isa amponya kipofu Bartimayo \r (Mathayo 20:29-34; Luka 18:35-43) \p \v 46 Kisha wakafika Yeriko. Isa alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo (maana yake “mwana wa Timayo”), alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. \v 47 Aliposikia kuwa ni Isa Al-Nasiri aliyekuwa anapita, akaanza kupaza sauti akisema, “Isa, Mwana wa Daudi\f + \fr 10:47 \fr*\ft Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*, nihurumie!” \p \v 48 Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya, lakini yeye akazidi kupaza sauti, akisema, “Mwana wa Daudi, nihurumie!” \p \v 49 Isa akasimama na kusema, “Mwiteni.” \p Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.” \v 50 Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Isa. \p \v 51 Isa akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?” \p Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona.” \p \v 52 Isa akamwambia, “Nenda zako, imani yako imekuponya.” Mara akapata kuona, akamfuata Isa njiani. \c 11 \s1 Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe \r (Mathayo 21:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19) \p \v 1 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage na Bethania katika Mlima wa Mizeituni. Isa akawatuma wawili wa wanafunzi wake, \v 2 akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtampata mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. \v 3 Mtu yeyote akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ mwambieni, ‘Bwana anamhitaji, na atamrudisha hapa baada ya muda mfupi.’ ” \p \v 4 Wakaenda, wakampata mwana-punda amefungwa kando ya barabara, karibu na mlango wa nyumba. \v 5 Walipokuwa wanamfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakawauliza, “Kwa nini mnamfungua huyo mwana-punda?” \v 6 Wakawajibu kama vile Isa alivyokuwa amewaagiza, nao wale watu wakawaruhusu. \v 7 Kisha wakamleta huyo mwana-punda kwa Isa na kutandika mavazi yao juu yake, naye akampanda. \v 8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyokuwa wamekata mashambani. \v 9 Kisha wale waliokuwa wametangulia mbele na wale waliokuwa wakifuata nyuma wakapaza sauti, wakisema, \q1 “Hosana!”\f + \fr 11:9 \fr*\ft Kiebrania kusema \ft*\fqa Okoa\fqa*\ft ; basi likawa neno la shangwe.\ft*\f* \b \q1 “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” \b \q1 \v 10 “Umebarikiwa ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi!” \b \q1 “Hosana kwake yeye aliye juu!” \p \v 11 Isa akaingia Yerusalemu na kwenda Hekaluni\f + \fr 11:11 \fr*\ft Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu.\ft*\f*. Akaangalia kila kitu kilichokuwamo, lakini kwa kuwa ilishakuwa jioni, akaenda zake Bethania pamoja na wale kumi na wawili. \s1 Isa aulaani mtini usiozaa \r (Mathayo 21:18-19) \p \v 12 Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Isa alikuwa na njaa. \v 13 Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. \v 14 Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo. \s1 Isa atakasa Hekalu \r (Mathayo 21:12-17; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22) \p \v 15 Walipofika Yerusalemu, Isa akaingia katika eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakinunua na kuuza humo. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, \v 16 wala hakumruhusu mtu yeyote kuchukua bidhaa kupitia ukumbi wa Hekalu. \v 17 Naye alipokuwa akiwafundisha, akasema, “Je, haikuandikwa kuwa: \q1 “ ‘Nyumba yangu itaitwa \q2 nyumba ya sala kwa mataifa yote’? \m Lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyang’anyi.’ ” \p \v 18 Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati wakapata habari hizi, nao wakaanza kutafuta njia ya kumuua, kwa kuwa walikuwa wakimwogopa, kwa sababu umati wote walishangazwa na mafundisho yake. \p \v 19 Ilipofika jioni, Isa na wanafunzi wake wakatoka nje ya mji. \s1 Mtini ulionyauka \r (Mathayo 21:20-22) \p \v 20 Kesho yake asubuhi walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. \v 21 Petro akakumbuka na kumwambia Isa, “Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!” \p \v 22 Isa akawajibu, “Mwaminini Mungu. \v 23 Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng’oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa. \v 24 Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu. \v 25 Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni mkiwa na neno na mtu, ili naye Baba\f + \fr 11:25 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. [ \v 26 Lakini kama ninyi msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]\f + \fr 11:26 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*” \s1 Swali kuhusu mamlaka ya Isa \r (Mathayo 21:23-27; Luka 20:1-8) \p \v 27 Wakafika tena Yerusalemu, na Isa alipokuwa akitembea Hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati pamoja na wazee wa watu wakamjia. \v 28 Wakamuuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka ya kufanya hayo?” \p \v 29 Isa akawajibu, “Nitawauliza swali moja. Nijibuni, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. \v 30 Je, ubatizo wa Yahya ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Niambieni!” \p \v 31 Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ \v 32 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu’ ” (waliwaogopa watu, kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yahya alikuwa nabii wa kweli); \v 33 kwa hiyo wakamjibu Isa, “Hatujui.” \p Naye Isa akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.” \c 12 \s1 Mfano wa wapangaji waovu \r (Mathayo 21:33-46; Luka 20:9-19) \p \v 1 Isa akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, na ndani yake akachimba shimo la shinikizo la kukamulia zabibu, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri hadi nchi nyingine. \v 2 Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili kuchukua sehemu yake ya mavuno ya shamba la mizabibu kutoka kwa hao wapangaji. \v 3 Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. \v 4 Kisha yule mwenye shamba akamtuma mtumishi mwingine kwao; nao wale wakulima wakampiga kichwani na kumfanyia mambo ya aibu. \v 5 Kisha akamtuma mtumishi mwingine, naye huyo wakamuua. Akawatuma wengine wengi; baadhi yao wakawapiga, na wengine wakawaua. \p \v 6 “Mwenye shamba alikuwa bado na mmoja wa kumtuma, mwanawe aliyempenda. Hatimaye akamtuma akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’ \p \v 7 “Lakini wale wapangaji wakasemezana pamoja, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, nao urithi utakuwa wetu.’ \v 8 Hivyo wakamchukua na kumuua, wakamtupa nje ya lile shamba la mizabibu. \p \v 9 “Sasa basi yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja na kuwaua hao wapangaji, kisha atawapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu. \v 10 Je, hamjasoma andiko hili: \q1 “ ‘Jiwe walilolikataa waashi \q2 limekuwa jiwe kuu la pembeni; \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu ndiye alitenda jambo hili, \q2 nalo ni la kushangaza machoni petu’?” \p \v 12 Walipotambua kuwa amesema mfano huo kwa ajili yao, wakataka kumkamata, lakini wakaogopa umati ule wa watu. Wakamwacha, wakaenda zao. \s1 Swali kuhusu kulipa kodi ya Kaisari \r (Mathayo 22:15-22; Luka 20:20-26) \p \v 13 Baadaye wakawatuma baadhi ya Mafarisayo\f + \fr 12:13 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na Maherode\f + \fr 12:13 \fr*\ft Wafuasi wa Mfalme Herode waliokubaliana na utawala wa Rumi.\ft*\f* ili wamtege Isa katika maneno yake. \v 14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? \v 15 Je, tulipe kodi au tusilipe?” \p Lakini Isa alijua unafiki wao. Akawauliza, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari\f + \fr 12:15 \fr*\ft dinari moja ilikuwa sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja.\ft*\f* niione.” \v 16 Wakamletea hiyo sarafu. Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?” \p Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” \p \v 17 Ndipo Isa akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.” \p Nao wakamstaajabia sana. \s1 Ndoa wakati wa ufufuo \r (Mathayo 22:23-33; Luka 20:27-40) \p \v 18 Kisha Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa, \v 19 wakasema, “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. \v 20 Basi kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa bila kuacha mtoto yeyote. \v 21 Wa pili akamwoa yule mjane, lakini naye akafa bila kuacha mtoto yeyote. Ikawa vivyo hivyo kwa yule wa tatu. \v 22 Hakuna hata mmoja wa hao ndugu saba aliyeacha mtoto. Hatimaye yule mwanamke naye akafa. \v 23 Basi, wakati wa ufufuo yeye atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?” \p \v 24 Isa akawajibu, “Je, hampotei kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu? \v 25 Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. \v 26 Basi kuhusu wafu kufufuliwa, je hamjasoma katika Kitabu cha Musa jinsi Mungu alivyosema na Musa kutoka kile kichaka akisema, ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo’? \v 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.” \s1 Amri kuu kuliko zote \r (Mathayo 22:34-40; Luka 10:25-28) \p \v 28 Mwalimu mmoja wa sheria akaja, akawasikia wakijadiliana. Akiona kwamba Isa amewajibu vyema, naye akamuuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” \p \v 29 Isa akajibu, “Amri iliyo kuu ndiyo hii: ‘Sikia ee Israeli. Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. \v 30 Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.’ \v 31 Ya pili ndiyo hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.” \p \v 32 Yule mwalimu wa Torati akamwambia Isa, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye. \v 33 Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, na kwa ufahamu wako wote, na kwa nguvu zako zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora kuliko kutoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu zote.” \p \v 34 Isa alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, “Wewe huko mbali na ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumuuliza maswali tena. \s1 Al-Masihi ni Mwana wa nani? \r (Mathayo 22:41-46; Luka 20:41-44) \p \v 35 Isa alipokuwa akifundisha Hekaluni, akauliza, “Imekuwaje walimu wa Torati wanasema kwamba Al-Masihi\f + \fr 12:35 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* ni Mwana wa Daudi? \v 36 Kwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, alisema: \q1 “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: \q2 “Keti mkono wangu wa kuume, \q1 hadi nitakapowaweka adui zako \q2 chini ya miguu yako.” ’ \m \v 37 Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” \p Umati ule wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha. \s1 Isa atahadharisha kuhusu walimu wa Torati \r (Mathayo 23:1-36; Luka 20:45-47) \p \v 38 Alipokuwa akifundisha, Isa alisema, “Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. \v 39 Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi\f + \fr 12:39 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f*, na kupewa nafasi za heshima katika karamu. \v 40 Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.” \s1 Sadaka ya mjane maskini \r (Luka 21:1-4) \p \v 41 Kisha Isa akaketi mkabala na sehemu ambapo sadaka zilikuwa zinawekwa na kuangalia umati wa watu wakiweka fedha zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. Matajiri wengi wakaweka kiasi kikubwa cha fedha. \v 42 Lakini mjane mmoja maskini akaja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba zenye thamani ya senti mbili. \p \v 43 Isa akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka katika sanduku la hazina zaidi ya watu wengine wote. \v 44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali yao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake, akaweka kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.” \c 13 \ms1 Unabii kuhusu mambo yajayo \mr (Marko 13:1-37) \s1 Kubomolewa kwa Hekalu kwatabiriwa \r (Mathayo 24:1-2; Luka 21:5-6) \p \v 1 Isa alipokuwa akitoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa, na majengo haya yalivyo mazuri!” \p \v 2 Ndipo Isa akajibu akasema, “Je, unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali yote yatabomolewa.” \s1 Ishara za nyakati za mwisho \r (Mathayo 24:3-14; Luka 21:7-19) \p \v 3 Isa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni mkabala na Hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamuuliza faraghani, \v 4 “Tafadhali tuambie, mambo haya yatatukia lini? Nayo dalili ya kuwa hayo yote yanakaribia kutimia itakuwa gani?” \p \v 5 Isa akawaambia: “Jihadharini mtu yeyote asiwadanganye. \v 6 Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye,’ nao watawadanganya wengi. \v 7 Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. \v 8 Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali na njaa. Haya yatakuwa ndio mwanzo wa uchungu. \p \v 9 “Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kupigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao. \v 10 Nayo Injili lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote. \v 11 Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke awali kuhusu mtakalosema. Semeni tu lolote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho Mtakatifu wa Mungu. \p \v 12 “Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, naye baba atamsaliti mtoto wake. Watoto nao wataasi dhidi ya wazazi wao na kusababisha wauawe. \v 13 Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. \s1 Chukizo la uharibifu \r (Mathayo 24:15-28; Luka 21:20-24) \p \v 14 “Mtakapoona ‘chukizo la uharibifu’ limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walio Yudea wakimbilie milimani. \v 15 Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke au kuingia ndani ili kuchukua chochote. \v 16 Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. \v 17 Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! \v 18 Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi. \v 19 Kwa maana siku hizo zitakuwa za dhiki kuu ambayo haijapata kuwa tangu mwanzo, hapo Mungu alipoumba ulimwengu, hadi leo, na wala haitakuwa tena kamwe. \p \v 20 “Kama Mwenyezi Mungu hangefupisha siku hizo, kamwe hakuna mtu yeyote angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupisha siku hizo. \v 21 Wakati huo mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Al-Masihi\f + \fr 13:21 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* huyu hapa!’ au, ‘Tazama, yuko kule,’ msisadiki. \v 22 Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule. \v 23 Hivyo jihadharini. Nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia. \s1 Kuja kwa Mwana wa Adamu \r (Mathayo 24:29-31; Luka 21:25-28) \p \v 24 “Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki, \q1 “ ‘jua litatiwa giza \q2 nao mwezi hautatoa nuru yake; \q1 \v 25 nazo nyota zitaanguka kutoka angani, \q2 na nguvu za anga zitatikisika.’ \p \v 26 “Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. \v 27 Naye atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka miisho ya dunia hadi miisho ya mbingu. \s1 Somo kuhusu mtini \r (Mathayo 24:32-35; Luka 21:29-33) \p \v 28 “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. \v 29 Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. \v 30 Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. \v 31 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. \s1 Hakuna ajuaye siku wala saa \r (Mathayo 24:36-44; Luka 17:26-30, 34-36) \p \v 32 “Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba\f + \fr 13:32 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* peke yake. \v 33 Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. \v 34 Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe. \p \v 35 “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko, \v 36 akija ghafula asije akawakuta mmelala. \v 37 Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ” \c 14 \ms1 Kufa na kufufuka kwa Isa \mr (Marko 14:1–16:20) \s1 Njama ya kumuua Isa \r (Mathayo 26:1-5; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53) \p \v 1 Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka\f + \fr 14:1 \fr*\ft Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.\ft*\f*, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Isa kwa hila na kumuua. \v 2 Lakini walisema, “Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia.” \s1 Isa apakwa mafuta huko Bethania \r (Mathayo 26:6-13; Luka 7:35-38; Yohana 12:1-8) \p \v 3 Isa alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo\f + \fr 14:3 \fr*\ft aina ya manukato yaliyotengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri\ft*\f* safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Isa. \p \v 4 Baadhi ya watu waliokuwa pale walikasirika na wakasemezana, “Upotevu huu wote wa manukato ni wa nini? \v 5 Manukato haya yangeuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu\f + \fr 14:5 \fr*\ft Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.\ft*\f*, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke. \p \v 6 Lakini Isa akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana. \v 7 Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. \v 8 Huyu mwanamke amenitendea lile aliloweza. Ameumiminia mwili wangu manukato ili kuniandaa kwa maziko yangu. \v 9 Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.” \s1 Yuda akubali kumsaliti Isa \r (Mathayo 26:14-16; Luka 22:3-6) \p \v 10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Isa kwao. \v 11 Walifurahi sana kusikia jambo hili na wakaahidi kumpa fedha. Hivyo yeye akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti. \s1 Isa ala Pasaka na wanafunzi wake \r (Mathayo 26:17-25; Luka 22:7-14, 21-23; Yohana 13:21-30) \p \v 12 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?” \p \v 13 Basi akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake, akawaambia, “Nendeni mjini. Huko mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. \v 14 Mwambieni mwenye nyumba ile atakayoingia, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba changu cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ \v 15 Atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.” \p \v 16 Wale wanafunzi wakaondoka na kwenda mjini, nao wakakuta kila kitu kama Isa alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka. \p \v 17 Ilipofika jioni, Isa akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. \v 18 Walipoketi mezani wakila, Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.” \p \v 19 Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi, Bwana?” \p \v 20 Akawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami. \v 21 Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa.” \s1 Kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana Isa \r (Mathayo 26:26-30; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25) \p \v 22 Walipokuwa wanakula, Isa akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.” \p \v 23 Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo. \p \v 24 Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. \v 25 Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.” \p \v 26 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni. \s1 Isa atabiri kuwa Petro atamkana \r (Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:31-38) \p \v 27 Isa akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: \q1 “ ‘Nitampiga mchungaji, \q2 nao kondoo watatawanyika.’ \m \v 28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.” \p \v 29 Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.” \p \v 30 Isa akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.” \p \v 31 Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo. \s1 Isa aomba katika Bustani ya Gethsemane \r (Mathayo 26:36-46; Luka 22:39-46) \p \v 32 Wakaenda mahali paitwapo Gethsemane. Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa, nami niende nikaombe.” \v 33 Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Akaanza kuhuzunika sana na kutaabika. \v 34 Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.” \p \v 35 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. \v 36 Akasema, “Abba\f + \fr 14:36 \fr*\fq Abba \fq*\ft ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni \ft*\fqa Baba.\fqa*\f*, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe.” \p \v 37 Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja? \v 38 Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.” \p \v 39 Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. \v 40 Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia. \p \v 41 Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. \v 42 Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!” \s1 Isa akamatwa \r (Mathayo 26:47-56; Luka 22:47-53; Yohana 18:1-11) \p \v 43 Isa alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, na wazee. \p \v 44 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.” \v 45 Mara Yuda akamjia Isa na kusema, “Mwalimu.” Akambusu. \v 46 Wale watu wakamkamata Isa, wakamweka chini ya ulinzi. \v 47 Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. \p \v 48 Kisha Isa akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? \v 49 Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini Maandiko sharti yatimie.” \v 50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. \p \v 51 Kijana mmoja, aliyekuwa amevaa nguo ya kitani pekee, alikuwa akimfuata Isa. Walipomkamata, \v 52 alikimbia uchi, akaliacha vazi lake. \s1 Isa mbele ya Baraza la Wayahudi \r (Mathayo 26:57-68; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24) \p \v 53 Wakampeleka Isa kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa Torati wote wakakusanyika pamoja. \v 54 Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto. \p \v 55 Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi\f + \fr 14:55 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f* lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Isa ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote. \v 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana. \p \v 57 Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: \v 58 “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” \v 59 Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana. \p \v 60 Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” \v 61 Lakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote. \p Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 14:61 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?” \p \v 62 Isa akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.” \p \v 63 Kuhani mkuu akayararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? \v 64 Ninyi mmesikia alivyokufuru. Uamuzi wenu ni gani?” \p Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo. \v 65 Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi. \s1 Petro amkana Isa \r (Mathayo 26:69-75; Luka 22:56-62; Yohana 18:15-18, 25-27) \p \v 66 Petro alipokuwa bado yuko chini uani, tazama akaja mmoja wa wajakazi wa kuhani mkuu. \v 67 Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Isa, Mnasiri.” \p \v 68 Lakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia. \p \v 69 Yule mjakazi alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.” \v 70 Lakini Petro akakana tena. \p Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo karibu na Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” \v 71 Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui huyu mtu mnayesema habari zake!” \p \v 72 Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana. \c 15 \s1 Pilato amhoji Isa \r (Mathayo 27:1-2, 11-14; Luka 23:3-25; Yohana 18:33–19:16) \p \v 1 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa Torati na Baraza la Wayahudi\f + \fr 15:1 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f* lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Isa, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. \p \v 2 Pilato akamuuliza, “Je, wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?” \p Isa akajibu, “Wewe umesema.” \p \v 3 Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. \v 4 Pilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.” \p \v 5 Lakini Isa hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa. \s1 Pilato amtoa Isa asulubiwe \r (Mathayo 27:15-26; Luka 23:13-25; Yohana 18:39–19:16) \p \v 6 Ilikuwa desturi wakati wa Sikukuu ya Pasaka kumfungulia mfungwa yeyote ambaye watu wangemtaka. \v 7 Wakati huo, mtu aliyeitwa Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wametekeleza uuaji wakati wa maasi. \v 8 Umati ule wa watu wakamjia Pilato na kumwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi yake. \p \v 9 Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie huyu mfalme wa Wayahudi?” \v 10 Kwa maana yeye alitambua kuwa viongozi wa makuhani walikuwa wamemtia Isa mkononi mwake kwa ajili ya wivu. \v 11 Lakini viongozi wa makuhani wakachochea umati ule wa watu wamwombe awafungulie Baraba badala yake. \p \v 12 Pilato akawauliza tena, “Basi mnataka nifanye nini na huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” \p \v 13 Wakapiga kelele, wakisema, “Msulubishe!” \p \v 14 Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” \p Lakini wao wakapiga kelele zaidi, wakisema, “Msulubishe!” \p \v 15 Pilato, akitaka kuridhisha umati ule wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Isa apigwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe. \s1 Askari wamdhihaki Isa \r (Mathayo 27:27-31; Yohana 19:2-3) \p \v 16 Askari wakampeleka Isa hadi kwenye ukumbi wa ndani wa jumba la kifalme, ndio Praitorio\f + \fr 15:16 \fr*\ft Praitorio ilikuwa makao makuu ya mtawala wa jimbo. Hapa ni jumba la kifalme ambapo Pontio Pilato aliishi huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu.\ft*\f*, wakakusanya kikosi kizima cha askari. \v 17 Wakamvalisha Isa joho la zambarau, wakasokota taji la miiba, wakamvika kichwani. \v 18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” \v 19 Wakampiga kwa fimbo ya mwanzi tena na tena kichwani na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake, wakamsujudia kwa kumdhihaki. \v 20 Walipokwisha kumdhihaki, wakamvua lile joho la zambarau, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakamtoa nje ili wakamsulubishe. \s1 Isa asulubishwa \r (Mathayo 27:32-44; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27) \p \v 21 Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anaingia mjini kutoka mashambani, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. \v 22 Kisha wakampeleka Isa hadi mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). \v 23 Nao wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini hakuinywa. \v 24 Basi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua. \p \v 25 Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha. \v 26 Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: \pc \sc Mfalme wa Wayahudi.\sc* \p \v 27 Pamoja naye walisulubiwa wanyang’anyi wawili, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. [ \v 28 Nalo andiko likatimizwa, lisemalo, “Alihesabiwa pamoja na watenda dhambi.”]\f + \fr 15:28 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \v 29 Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, \v 30 basi shuka kutoka msalabani na ujiokoe mwenyewe!” \p \v 31 Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani pamoja na walimu wa Torati wakamdhihaki miongoni mwao wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! \v 32 Basi huyu Al-Masihi\f + \fr 15:32 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, huyu mfalme wa Israeli, ashuke sasa msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana. \s1 Kifo cha Isa \r (Mathayo 27:45-56; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30) \p \v 33 Ilipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. \v 34 Hapo saa tisa, Isa akapaza sauti, akalia, \tl “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”\tl* (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”) \p \v 35 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni, anamwita Ilya.” \p \v 36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.” \p \v 37 Kisha Isa akatoa sauti kuu, akakata roho. \p \v 38 Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini. \v 39 Basi yule jemadari aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Isa aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu\f + \fr 15:39 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*!” \p \v 40 Palikuwa na wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome. \v 41 Hawa walifuatana na Isa na kushughulikia mahitaji yake alipokuwa Galilaya. Pia walikuwako wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye hadi Yerusalemu. \s1 Maziko ya Isa \r (Mathayo 27:57-61; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42) \p \v 42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa Siku ya Maandalizi (yaani siku moja kabla ya Sabato), \v 43 Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na alikuwa anautarajia ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa. \v 44 Pilato alikuwa akijiuliza kama Isa alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Isa alikuwa amekwisha kufa. \v 45 Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. \v 46 Hivyo Yusufu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi. \v 47 Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa. \c 16 \s1 Isa afufuka \r (Mathayo 28:1-8; Luka 24:1-12; Yohana 20:1-10) \p \v 1 Sabato ilipomalizika, Mariamu Magdalene, Mariamu mama yake Yakobo, na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Isa. \v 2 Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma, mara tu baada ya kuchomoza jua, walienda kaburini. \v 3 Njiani wakawa wanaulizana wao kwa wao, “Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe kutoka ingilio la kaburi?” \p \v 4 Lakini walipotazama, wakaona lile jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana, limekwisha kuvingirishwa kutoka pale penye ingilio la kaburi. \v 5 Walipokuwa wakiingia mle kaburini, wakamwona kijana mmoja aliyevaa joho jeupe akiwa ameketi upande wa kuume, nao wakastaajabu. \p \v 6 Yule malaika akawaambia, “Msistaajabu. Mnamtafuta Isa, Mnasiri, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza. \v 7 Lakini nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro, kwamba, ‘Anawatangulia kwenda Galilaya. Mtamwona huko kama alivyowaambia.’ ” \p \v 8 Hivyo wakatoka, wakakimbia kutoka mle kaburini wakiwa na hofu kuu na mshangao. Nao hawakumwambia mtu yeyote neno lolote, kwa sababu waliogopa. \s1 Isa amtokea Mariamu Magdalene \r (Mathayo 28:9-10; Yohana 20:11-18) \p [ \v 9 \f + \fr 16:9 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana sehemu ya \+xt Marko 16:9-20\+xt*.\ft*\f* Isa alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, aliyekuwa amemtoa pepo wachafu saba. \v 10 Mariamu akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Isa, waliokuwa wanaomboleza na kulia. \v 11 Lakini waliposikia kwamba Isa yu hai na kwamba Mariamu alikuwa amemwona, hawakusadiki. \s1 Isa awatokea wanafunzi wawili \r (Luka 24:13-35) \p \v 12 Baadaye Isa akawatokea wawili miongoni mwa wanafunzi wake walipokuwa wakienda shambani akiwa katika sura nyingine. \v 13 Nao wakarudi na kuwaambia wenzao. Lakini hawakuwasadiki wao pia. \s1 Isa awatuma wanafunzi wake \r (Mathayo 28:16-20; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8) \p \v 14 Baadaye Isa akawatokea wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakila chakula. Akawakemea kwa kutoamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao kwa kutosadiki wale waliomwona baada yake kufufuka. \p \v 15 Akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. \v 16 Yeyote aaminiye na kubatizwa\f + \fr 16:16 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali.\ft*\f* ataokoka. Lakini yeyote asiyeamini atahukumiwa. \v 17 Nazo ishara hizi zitafuatana na wanaoamini: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu; watasema kwa lugha mpya; \v 18 watashika nyoka kwa mikono yao; na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.” \s1 Isa apaa mbinguni \r (Luka 24:50-53; Matendo 1:9-11) \p \v 19 Baada ya Bwana Isa kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu. \v 20 Kisha wanafunzi wake wakatoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana Isa akatenda kazi pamoja nao na kulithibitisha neno lake kwa ishara zilizofuatana nalo.]