\id MIC - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Mika \toc1 Mika \toc2 Mika \toc3 Mik \mt1 Mika \c 1 \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Mika Mmoreshethi wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu. \b \b \q1 \v 2 Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, \q2 sikilizeni, ee dunia na wote mliomo, \q1 ili Bwana Mungu Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, \q2 Bwana kutoka Hekalu lake takatifu. \s1 Hukumu dhidi ya Samaria na Yerusalemu \q1 \v 3 Tazama! Mwenyezi Mungu anakuja kutoka mahali pake; \q2 anashuka na kukanyaga \q2 mahali palipoinuka juu pa dunia. \q1 \v 4 Milima inayeyuka chini yake \q2 na mabonde yanagawanyika \q1 kama nta mbele ya moto, \q2 kama maji yanayotiririka kasi \q2 kwenye mteremko. \q1 \v 5 Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, \q2 ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. \q1 Kosa la Yakobo ni lipi? \q2 Je, sio Samaria? \q1 Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia ni nini? \q2 Je, sio Yerusalemu? \b \q1 \v 6 “Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto, \q2 mahali pa kuotesha mizabibu. \q1 Nitayamwaga mawe yake katika bonde \q2 na kuacha wazi misingi yake. \q1 \v 7 Sanamu zake zote \q2 zitavunjwa vipande vipande; \q1 zawadi zake zote za Hekalu \q2 zitachomwa kwa moto; \q2 nitaharibu vinyago vyake vyote. \q1 Kwa kuwa alikusanya zawadi zake \q2 kutokana na ujira wa kahaba, \q1 nazo zitatumika tena \q2 kulipa mishahara ya kahaba.” \s1 Kulia na kuomboleza \q1 \v 8 Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; \q2 nitatembea bila viatu na tena uchi. \q1 Nitabweka kama mbweha \q2 na kuomboleza kama bundi. \q1 \v 9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki; \q2 limekuja kwa Yuda. \q1 Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, \q2 hata Yerusalemu kwenyewe. \q1 \v 10 Usiliseme hili huko Gathi; \q2 usilie hata kidogo. \q1 Huko Beth-le-Afra \q2 gaagaa mavumbini. \q1 \v 11 Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, \q2 ninyi mnaoishi Shafiri. \q1 Wale wanaoishi Saanani \q2 hawatatoka nje. \q1 Beth-Eseli iko katika maombolezo; \q2 kinga yake imeondolewa kwako. \q1 \v 12 Wale wanaoishi Marothi wanagaagaa kwa maumivu \q2 wakingoja msaada, \q1 kwa sababu maangamizi yamekuja \q2 kutoka kwa Mwenyezi Mungu, \q2 hata katika lango la Yerusalemu. \q1 \v 13 Enyi mnaoishi Lakishi, \q2 fungeni farasi kwenye magari ya vita. \q1 Mlikuwa chanzo cha dhambi \q2 kwa Binti Sayuni, \q1 kwa kuwa makosa ya Israeli \q2 yalikutwa kwako. \q1 \v 14 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi \q2 zawadi za kuagana. \q1 Mji wa Akzibu utaonesha wazi udanganyifu \q2 kwa wafalme wa Israeli. \q1 \v 15 Nitawaleteeni atakayewashinda \q2 ninyi mnaoishi Maresha. \q1 Yeye aliye utukufu wa Israeli \q2 atakuja Adulamu. \q1 \v 16 Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza \q2 kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia; \q1 jifanyieni upara kama tai, \q2 kwa kuwa watawaacha \q2 na kwenda uhamishoni. \c 2 \s1 Mipango ya mwanadamu na mipango ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Ole kwa wale wapangao uovu, \q2 kwa wale wapangao hila vitandani mwao! \q1 Kunapopambazuka wanalitimiza \q2 kwa sababu uko katika uwezo wao kutekeleza. \q1 \v 2 Wanatamani mashamba na kuyakamata, \q2 pia nyumba na kuzichukua. \q1 Wanamlaghai mwanaume nyumba yake, \q2 mwanadamu mwenzake urithi wake. \p \v 3 Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu asema: \q1 “Ninapanga maangamizi dhidi ya watu hawa, \q2 ambayo hamwezi kujiokoa wenyewe. \q1 Hamtatembea tena kwa majivuno, \q2 kwa kuwa utakuwa ni wakati wa maafa. \q1 \v 4 Siku hiyo watu watawadhihaki, \q2 watawafanyia mzaha \q2 kwa wimbo huu wa maombolezo: \q1 ‘Tumeangamizwa kabisa; \q2 mali ya watu wangu imegawanywa. \q1 Ameninyang’anya! \q2 Ametoa mashamba yetu kwa wasaliti.’ ” \b \q1 \v 5 Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko la Mwenyezi Mungu \q2 wa kugawanya mashamba kwa kura. \s1 Manabii wa uongo \q1 \v 6 Manabii wao husema, “Usitabiri. \q2 Usitabiri kuhusu vitu hivi; \q2 aibu haitatupata.” \q1 \v 7 Je, ingesemwa, ee nyumba ya Yakobo: \q2 “Je, Roho wa Mwenyezi Mungu amekasirika? \q2 Je, yeye hufanya vitu kama hivyo?” \b \q1 “Je, maneno yangu hayamfanyii mema \q2 yeye ambaye njia zake ni nyofu? \q1 \v 8 Siku hizi watu wangu wameinuka \q2 kama adui. \q1 Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita \q2 pasipo kujali, \q2 kama watu warudio kutoka vitani. \q1 \v 9 Unawahamisha wanawake wa watu wangu \q2 kutoka nyumba zao za kupendeza. \q1 Unaondoa baraka yangu \q2 kwa watoto wao milele. \q1 \v 10 Inuka, nenda zako! \q2 Kwa maana hapa sio mahali pako pa kupumzikia, \q1 kwa sababu pametiwa unajisi, \q2 pameharibiwa, wala hapatengenezeki tena. \q1 \v 11 Ikiwa mwongo na mdanganyifu atakuja na kusema, \q2 ‘Nitawatabiria divai na pombe kwa wingi,’ \q1 angekuwa ndiye nabii \q2 anayekubalika na watu hawa! \s1 Ahadi ya ukombozi \q1 \v 12 “Hakika nitawakusanya ninyi nyote, ee Yakobo, \q2 Hakika nitawaleta pamoja mabaki ya Israeli. \q1 Nitawaleta pamoja kama kondoo ndani ya zizi, \q2 kama kundi kwenye malisho yake, \q2 mahali hapa patakuwa na msongamano wa watu. \q1 \v 13 Yeye afunguaye njia atawatangulia; \q2 watapita kwenye lango na kutoka nje. \q1 Mfalme wao atawatangulia, \q2 Mwenyezi Mungu atakuwa kiongozi.” \c 3 \s1 Viongozi na manabii wakemewa \p \v 1 Kisha nikasema, \q1 “Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo, \q2 enyi watawala wa nyumba ya Israeli. \q1 Je, hampaswi kujua hukumu, \q2 \v 2 ninyi mnaochukia mema \q2 na kupenda maovu; \q1 ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi \q2 na kuondoa nyama kwenye mifupa yao; \q1 \v 3 ninyi mnaokula nyama ya watu wangu, \q2 mnaowachuna ngozi \q2 na kuvunja mifupa yao vipande vipande; \q1 mnaowakatakata kama nyama \q2 ya kuwekwa kwenye sufuria \q1 na kama nyama \q2 ya kuwekwa kwenye chungu?” \b \q1 \v 4 Kisha watamlilia Mwenyezi Mungu, \q2 lakini hatawajibu. \q1 Wakati huo atawaficha uso wake \q2 kwa sababu ya uovu waliotenda. \p \v 5 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu, \q2 mtu akiwalisha, \q2 wanatangaza ‘amani’; \q1 kama hakufanya hivyo, \q2 wanaandaa kupigana vita dhidi yake. \q1 \v 6 Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono, \q2 na giza, msiweze kubashiri. \q1 Jua litawachwea manabii hao, \q2 nao mchana utakuwa giza kwao. \q1 \v 7 Waonaji wataaibika \q2 na waaguzi watafedheheka. \q1 Wote watafunika nyuso zao \q2 kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.” \q1 \v 8 Lakini mimi nimejazwa nguvu, \q2 nimejazwa Roho wa Mwenyezi Mungu, \q2 haki na uweza, \q1 kumtangazia Yakobo kosa lake, \q2 na Israeli dhambi yake. \b \q1 \v 9 Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, \q2 enyi watawala wa nyumba ya Israeli, \q1 mnaodharau haki \q2 na kupotosha kila lililo sawa; \q1 \v 10 mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu \q2 na Yerusalemu kwa uovu. \q1 \v 11 Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, \q2 na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, \q2 nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. \q1 Hata hivyo wanamwegemea Mwenyezi Mungu na kusema, \q2 “Je, Mwenyezi Mungu si yumo miongoni mwetu? \q2 Hakuna maafa yatakayotupata.” \q1 \v 12 Kwa ajili yenu, \q2 Sayuni italimwa kama shamba, \q1 Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, \q2 na kilima cha Hekalu \q1 kitakuwa kichuguu \q2 kilichofunikwa na vichaka. \c 4 \s1 Mlima wa Mwenyezi Mungu \r (Isaya 2:2-4) \p \v 1 Katika siku za mwisho \q1 mlima wa Hekalu la Mwenyezi Mungu utaimarishwa \q2 kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote; \q1 utainuliwa juu ya vilima, \q2 na watu wa mataifa watamiminika humo. \p \v 2 Mataifa mengi yatakuja na kusema, \q1 “Njooni, twendeni kwenye mlima wa Mwenyezi Mungu, \q2 kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. \q1 Atatufundisha njia zake, \q2 ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” \q1 Torati itatoka Sayuni, \q2 neno la Mwenyezi Mungu litatoka Yerusalemu. \q1 \v 3 Atahukumu kati ya mataifa mengi, \q2 na ataamua migogoro ya mataifa \q2 yenye nguvu na yaliyo mbali. \q1 Watafua panga zao ziwe majembe, \q2 na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. \q1 Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, \q2 wala hawatajifunza vita tena. \q1 \v 4 Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake \q2 na chini ya mtini wake, \q1 wala hakuna mtu atakayewaogopesha, \q2 kwa kuwa Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni amesema. \q1 \v 5 Mataifa yote yanaweza kutembea \q2 katika jina la miungu yao; \q1 sisi tutatembea katika jina la Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wetu milele na milele. \s1 Mpango wa Mwenyezi Mungu \p \v 6 “Katika siku hiyo,” asema Mwenyezi Mungu, \q1 “nitawakusanya walemavu; \q2 nitawakusanya walio uhamishoni \q2 na wale niliowahuzunisha. \q1 \v 7 Nitawafanya walemavu kuwa mabaki, \q2 wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu. \q1 Mwenyezi Mungu atawatawala katika Mlima Sayuni \q2 kuanzia siku hiyo na hata milele. \q1 \v 8 Lakini kwako wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi, \q2 ee ngome ya Binti Sayuni, \q1 milki ya awali itarudishwa kwako, \q2 ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.” \b \q1 \v 9 Kwa nini sasa unalia kwa nguvu: \q2 kwani huna mfalme? \q1 Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate \q2 kama ya mwanamke \q2 aliye na uchungu wa kuzaa? \q1 \v 10 Gaagaa kwa uchungu, ee Binti Sayuni, \q2 kama mwanamke mwenye uchungu wa kuzaa, \q1 kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji \q2 ukapige kambi uwanjani. \q1 Utaenda Babeli; \q2 huko utaokolewa. \q1 Huko Mwenyezi Mungu atakukomboa \q2 kutoka mikononi mwa adui zako. \b \q1 \v 11 Lakini sasa mataifa mengi \q2 yamekusanyika dhidi yako. \q1 Wanasema, “Mwache anajisiwe, \q2 macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!” \q1 \v 12 Lakini hawayajui \q2 mawazo ya Mwenyezi Mungu; \q1 hawauelewi mpango wake, \q2 yeye awakusanyaye kama miganda \q2 kwenye sakafu ya kupuria. \q1 \v 13 “Inuka upure, ee Binti Sayuni, \q2 kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; \q1 nitakupa kwato za shaba \q2 na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” \q1 Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Mwenyezi Mungu, \q2 utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote. \c 5 \s1 Mtawala aliyeahidiwa kutoka Bethlehemu \q1 \v 1 Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi, \q2 kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu. \q1 Watampiga mtawala wa Israeli \q2 shavuni kwa fimbo. \b \q1 \v 2 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, \q2 ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, \q1 kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu \q2 yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, \q1 ambaye asili yake ni kutoka zamani, \q2 kutoka milele.” \b \q1 \v 3 Kwa hiyo Israeli utaachwa \q2 hadi mwanamke aliye na uchungu atakapozaa mwana, \q1 na ndugu zake wengine warudi \q2 kujiunga na Waisraeli. \b \q1 \v 4 Atasimama na kulichunga kundi lake \q2 katika nguvu ya Mwenyezi Mungu, \q2 katika utukufu wa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \q1 Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo \q2 ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia. \q2 \v 5 Naye atakuwa amani yao. \s1 Ukombozi na uharibifu \q1 Mwashuru atakapovamia nchi yetu \q2 na kupita katika ngome zetu, \q1 tutawainua wachungaji saba dhidi yake, \q2 hata viongozi wanane wa watu. \q1 \v 6 Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga, \q2 nchi ya Nimrodi kwa upanga. \q1 Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru \q2 atakapoivamia nchi yetu \q2 na kuingia katika mipaka yetu. \b \q1 \v 7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa \q2 katikati ya mataifa mengi \q1 kama umande kutoka kwa Mwenyezi Mungu, \q2 kama manyunyu juu ya majani, \q1 ambayo hayamngoji mtu \q2 wala kukawia kwa mwanadamu. \q1 \v 8 Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, \q2 katikati ya mataifa mengi, \q1 kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni, \q2 kama mwana simba miongoni \q2 mwa makundi ya kondoo, \q1 ambaye anaumiza vibaya na kuwararua \q2 kila anapopita katikati yao, \q2 wala hakuna awezaye kuokoa. \q1 \v 9 Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako, \q2 nao adui zako wote wataangamizwa. \p \v 10 “Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu, \q1 “nitaangamiza farasi wenu kati yenu, \q2 na kubomoa magari yenu ya vita. \q1 \v 11 Nitaiangamiza miji ya nchi yenu, \q2 na kuziangusha chini ngome zenu zote. \q1 \v 12 Nitaangamiza uchawi wenu, \q2 na hamtapiga tena ramli. \q1 \v 13 Nitaangamiza sanamu zenu, \q2 na mawe yenu ya ibada yatoke kati yenu; \q1 hamtasujudia tena \q2 kazi ya mikono yenu. \q1 \v 14 Nitang’oa nguzo za Ashera kati yenu, \q2 na kubomoa miji yenu. \q1 \v 15 Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu, \q2 kwa mataifa ambayo hayajanitii.” \c 6 \s1 Shtaka la Mwenyezi Mungu dhidi ya Israeli \p \v 1 Sikiliza asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Simama, jitetee mbele ya milima; \q2 vilima na visikie lile unalotaka kusema. \b \q1 \v 2 “Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Mwenyezi Mungu, \q2 sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. \q1 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ana shauri dhidi ya watu wake; \q2 anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. \b \q1 \v 3 “Watu wangu, nimewatendea nini? \q2 Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu. \q1 \v 4 Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa \q2 kutoka nchi ya utumwa. \q1 Nilimtuma Musa awaongoze, \q2 pia Haruni na Miriamu. \q1 \v 5 Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu \q2 alivyofanya shauri \q2 na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu. \q1 Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu hadi Gilgali, \q2 ili mfahamu matendo ya haki ya Mwenyezi Mungu.” \b \q1 \v 6 Nimjie Mwenyezi Mungu na kitu gani na kusujudu \q2 mbele za Mungu aliyetukuka? \q1 Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa, \q2 nije na ndama za mwaka mmoja? \q1 \v 7 Je, Mwenyezi Mungu atafurahishwa na kondoo dume elfu, \q2 au mito elfu kumi ya mafuta? \q1 Je, nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza \q2 kwa ajili ya kosa langu, \q1 mtoto wangu mwenyewe \q2 kwa ajili ya dhambi ya nafsi yangu? \q1 \v 8 Amekuonesha yaliyo mema, ee mwanadamu. \q2 Mwenyezi Mungu anataka nini kwako? \q1 Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, \q2 na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako. \s1 Hatia na adhabu ya Israeli \q1 \v 9 Sikiliza! Mwenyezi Mungu anauita mji: \q2 kulicha jina lako ni hekima: \q2 “Tii hiyo fimbo na yeye aliyeiamuru. \q1 \v 10 Je, bado nisahau, ee nyumba ya uovu, \q2 hazina yako uliyopata kwa udanganyifu \q1 na vipimo vilivyopunguka, \q2 ambavyo vimelaaniwa? \q1 \v 11 Je, naweza kuhukumu kuwa \q2 mtu mwenye mizani ya udanganyifu hana hatia, \q2 aliye na mfuko wa mawe ya kupimia ya uongo? \q1 \v 12 Matajiri wake ni wajeuri; \q2 watu wake ni waongo \q1 na ndimi zao zinazungumza \q2 kwa udanganyifu. \q1 \v 13 Kwa hiyo, nimeanza kukuharibu, \q2 kuwaangamiza kwa sababu ya dhambi zenu. \q1 \v 14 Mtakula lakini hamtashiba; \q2 tumbo zenu bado zitakuwa tupu. \q1 Mtaweka akiba lakini hamtaokoa chochote, \q2 kwa sababu mtakachoweka akiba \q2 nitatoa kwa upanga. \q1 \v 15 Mtapanda lakini hamtavuna; \q2 mtakamua zeituni lakini \q2 hamtatumia mafuta yake. \q1 Mtakamua zabibu \q2 lakini hamtakunywa hiyo divai. \q1 \v 16 Mmezishika sheria za Omri \q2 na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, \q2 tena umefuata desturi zao. \q1 Kwa hiyo nitakutoa kwa maangamizi \q2 na watu wako kuwa dhihaka; \q2 mtachukua dharau za mataifa.” \c 7 \s1 Taabu ya Israeli \q1 \v 1 Taabu gani hii niliyo nayo! \q1 Nimefanana na yule akusanyaye \q2 matunda ya kiangazi, \q1 aokotaye masazo baada ya kuvunwa \q2 shamba la mizabibu; \q1 hakuna kishada chenye matunda ya kula, \q2 hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani. \q1 \v 2 Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka nchi; \q2 hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki. \q1 Watu wote wanavizia kumwaga damu, \q2 kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu. \q1 \v 3 Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya, \q2 mtawala anadai zawadi, \q1 hakimu anapokea rushwa, \q2 wenye nguvu wanaamuru wanachotaka: \q2 wote wanapanga njama pamoja. \q1 \v 4 Aliye mwema kupita wote kati yao \q2 ni kama mchongoma, \q1 anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao \q2 ni mbaya kuliko uzio wa miiba. \q1 Siku ya walinzi wako imewadia, \q2 siku Mungu atakayokutembelea. \q1 Sasa ni wakati wao \q2 wa kuchanganyikiwa. \q1 \v 5 Usimtumaini jirani; \q2 usiweke matumaini kwa rafiki. \q1 Hata kwa yule alalaye kifuani mwako \q2 uwe mwangalifu kwa maneno yako. \q1 \v 6 Kwa kuwa mwana humdharau baba yake, \q2 naye binti huinuka dhidi ya mama yake, \q1 mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake: \q2 adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa. \b \q1 \v 7 Lakini mimi, namtazama Mwenyezi Mungu kwa matumaini, \q2 namngoja Mungu Mwokozi wangu; \q2 Mungu wangu atanisikia mimi. \s1 Israeli atainuka \q1 \v 8 Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu! \q2 Ingawa nimeanguka, nitainuka. \q1 Japo ninaketi gizani, \q2 Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yangu. \q1 \v 9 Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, \q2 nitabeba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, \q1 hadi atakapotetea shauri langu \q2 na kuithibitisha haki yangu. \q1 Atanileta nje kwenye mwanga, \q2 nami nitaiona haki yake. \q1 \v 10 Kisha adui yangu ataliona \q2 naye atafunikwa na aibu, \q1 yule aliyeniambia, \q2 “Yu wapi Mwenyezi Mungu, Mungu wako?” \q1 Macho yangu yataona kuanguka kwake, \q2 hata sasa atakanyagwa chini ya mguu \q2 kama tope barabarani. \b \q1 \v 11 Siku ya kujenga kuta zako itawadia, \q2 siku ya kupanua mipaka yako. \q1 \v 12 Siku hiyo watu watakuja kwako \q2 kutoka Ashuru na miji ya Misri, \q1 hata kutoka Misri hadi Mto Frati, \q2 na kutoka bahari hadi bahari, \q2 na kutoka mlima hadi mlima. \q1 \v 13 Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake, \q2 kwa sababu ya matunda ya matendo yao. \s1 Sala na sifa \q1 \v 14 Wachunge watu wako kwa fimbo yako, \q2 kundi la urithi wako, \q1 ambalo linaishi peke yake msituni, \q2 katika maeneo ya malisho yenye rutuba. \q1 Waache walishe katika Bashani na Gileadi \q2 kama ilivyokuwa siku za kale. \b \q1 \v 15 “Kama siku zile mlipotoka Misri, \q2 nitawaonesha maajabu yangu.” \b \q1 \v 16 Mataifa yataona na kuaibika, \q2 waliondolewa nguvu zao zote. \q1 Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao \q2 na masikio yao yatakuwa na uziwi. \q1 \v 17 Wataramba mavumbi kama nyoka, \q2 kama viumbe vinavyotambaa ardhini. \q1 Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; \q2 watamgeukia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa hofu \q2 nao watakuogopa. \q1 \v 18 Ni nani Mungu kama wewe, \q2 ambaye anaachilia dhambi \q1 na kusamehe makosa \q2 ya mabaki ya urithi wake? \q1 Wewe huwi na hasira milele, \q2 bali unafurahia kuonesha rehema. \q1 \v 19 Utatuhurumia tena, \q2 utazikanyaga dhambi zetu \q2 chini ya nyayo zako, \q1 na kutupa maovu yetu yote \q2 katika vilindi vya bahari. \q1 \v 20 Utakuwa wa kweli kwa Yakobo, \q2 nawe utamwonesha Ibrahimu rehema, \q1 kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu \q2 siku za kale.