\id MAT - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Mathayo \toc1 Mathayo \toc2 Mathayo \toc3 Mt \mt1 Mathayo \c 1 \ms1 Maisha na huduma ya awali ya Isa \mr (Mathayo 1–4) \s1 Kumbukumbu za ukoo wa Isa Al-Masihi \r (Luka 3:23-38) \lh \v 1 Habari za ukoo wa Isa Al-Masihi mwana wa Daudi\f + \fr 1:1 \fr*\ft Mariamu, mamake Isa, na pia Yusufu, baba mlezi wa Isa, walitokea ukoo wa Mfalme Daudi. Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*, mwana wa Ibrahimu: \b \li1 \v 2 Ibrahimu akamzaa Isaka, \li1 Isaka akamzaa Yakobo, \li1 Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake, \li1 \v 3 Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, \li1 Peresi akamzaa Esromu, \li1 Esromu akamzaa Aramu, \li1 \v 4 Aramu akamzaa Aminadabu, \li1 Aminadabu akamzaa Nashoni, \li1 Nashoni akamzaa Salmoni, \li1 \v 5 Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu, \li1 Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu, \li1 Obedi akamzaa Yese, \li1 \v 6 Yese akamzaa Daudi, aliyekuwa mfalme. \b \li1 Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria. \li1 \v 7 Sulemani akamzaa Rehoboamu, \li1 Rehoboamu akamzaa Abiya, \li1 Abiya akamzaa Asa, \li1 \v 8 Asa akamzaa Yehoshafati, \li1 Yehoshafati akamzaa Yoramu, \li1 Yoramu akamzaa Uzia, \li1 \v 9 Uzia akamzaa Yothamu, \li1 Yothamu akamzaa Ahazi, \li1 Ahazi akamzaa Hezekia, \li1 \v 10 Hezekia akamzaa Manase, \li1 Manase akamzaa Amoni, \li1 Amoni akamzaa Yosia, \li1 \v 11 wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake. \b \lh \v 12 Baada ya uhamisho wa Babeli: \li1 Yekonia alimzaa Shealtieli, \li1 Shealtieli akamzaa Zerubabeli, \li1 \v 13 Zerubabeli akamzaa Abihudi, \li1 Abihudi akamzaa Eliakimu, \li1 Eliakimu akamzaa Azori, \li1 \v 14 Azori akamzaa Sadoki, \li1 Sadoki akamzaa Akimu, \li1 Akimu akamzaa Eliudi, \li1 \v 15 Eliudi akamzaa Eleazari, \li1 Eleazari akamzaa Matani, \li1 Matani akamzaa Yakobo, \li1 \v 16 naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi.\f + \fr 1:16 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* \b \lf \v 17 Hivyo, kulikuwa na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu hadi Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho wa Babeli hadi Al-Masihi. \s1 Kuzaliwa kwa Isa \r (Luka 2:1-7) \p \v 18 Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu. \v 19 Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, hivyo basi alikusudia kumwacha kwa siri. \p \v 20 Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu. \v 21 Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Isa\f + \fr 1:21 \fr*\fq Isa \fq*\ft ni \+tl Iesous\+tl* kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Yoshua \fqa*\ft au \ft*\fqa Yeshua\fqa*\ft ; maana yake \ft*\fqa Yehova ni wokovu.\fqa*\f*, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.” \p \v 22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Mwenyezi Mungu alilonena kupitia nabii, aliposema: \v 23 “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli” (maana yake, “Mungu pamoja nasi”). \p \v 24 Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya jinsi alivyoagizwa na malaika wa Mwenyezi Mungu, akamchukua Mariamu kuwa mke wake. \v 25 Lakini hawakukutana kimwili hadi Mariamu alipojifungua mwanawe\f + \fr 1:25 \fr*\ft tafsiri zingine husema \ft*\fqa kifungua mimba\fqa*\f*; akamwita jina Isa. \c 2 \s1 Wataalamu wa nyota waenda kumwona mtoto Isa \p \v 1 Baada ya Isa kuzaliwa katika mji wa Bethlehemu huko Yudea, wakati wa utawala wa Mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu \v 2 wakiuliza, “Yuko wapi huyo aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tumeona nyota yake ikitokea mashariki, nasi tumekuja kumwabudu.” \p \v 3 Mfalme Herode aliposikia jambo hili aliingiwa na hofu sana pamoja na watu wote wa Yerusalemu. \v 4 Herode akawaita pamoja viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, akawauliza ni wapi ambapo Al-Masihi\f + \fr 2:4 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* angezaliwa. \v 5 Nao wakamwambia, “Katika Bethlehemu ya Yudea, kwa maana hivyo ndivyo ilivyoandikwa na nabii: \q1 \v 6 “ ‘Nawe, Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, \q2 wewe si mdogo miongoni \q2 mwa watawala wa Yuda; \q1 kwa maana kutoka kwako atakuja mtawala \q2 atakayekuwa mchungaji \q2 wa watu wangu Israeli.’ ” \p \v 7 Ndipo Herode akawaita wale wataalamu wa nyota kwa siri na kutaka kujua kutoka kwao uhakika kamili wa wakati ile nyota ilionekana. \v 8 Kisha akawatuma Bethlehemu na kuwaambia, “Nendeni mkamtafute mtoto huyo kwa makini. Mara tu mtakapompata, nileteeni taarifa ili nami niende kumwabudu.” \p \v 9 Baada ya kumsikia mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, nao wakaifuata hadi iliposimama mahali alipokuwa mtoto. \v 10 Walipoiona ile nyota wakajawa na furaha kubwa mno. \v 11 Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakamsujudia na kumwabudu yule mtoto Isa. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane. \v 12 Kwa kuwa walikuwa wameonywa katika ndoto wasirudi kwa Herode, wakarudi nchi yao kwa njia nyingine. \s1 Yusufu, Mariamu na mtoto Isa wakimbilia Misri \p \v 13 Walipokwisha kwenda zao, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Yusufu katika ndoto akamwambia, “Amka, umchukue mtoto na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko hadi nitakapowaambia, kwa maana Herode anataka kumtafuta huyu mtoto ili amuue.” \p \v 14 Kisha Yusufu akaamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake wakati wa usiku, nao wakaenda Misri, \v 15 ambako walikaa hadi Herode alipofariki. Hili lilifanyika ili litimie lile neno Mwenyezi Mungu alilosema kupitia kwa nabii: “Nilimwita mwanangu kutoka Misri.” \p \v 16 Herode alipogundua kwamba alikuwa amedanganywa na wale wataalamu wa nyota, alikasirika sana, naye akatoa amri ya kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kurudi chini katika mji wa Bethlehemu na sehemu zote za jirani, kwa mujibu wa ule muda alioambiwa na wale wataalamu wa nyota. \v 17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, aliposema: \q1 \v 18 “Sauti ilisikika huko Rama, \q2 maombolezo na kilio kikubwa, \q1 Raheli akilia kwa ajili ya wanawe, \q2 akikataa kufarijiwa, \q1 kwa sababu hawako tena.” \s1 Kurudi Nasiri kutoka Misri \p \v 19 Baada ya Herode kufa, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Yusufu katika ndoto huko Misri \v 20 na kusema, “Ondoka, mchukue mtoto na mama yake mwende, mrudi katika nchi ya Israeli kwa sababu wale waliokuwa wakijaribu kumuua mtoto wamekufa.” \p \v 21 Basi Yusufu, akainuka, akamchukua mtoto na mama yake wakaenda hadi nchi ya Israeli. \v 22 Lakini aliposikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala huko Yudea baada ya Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Kwa kuwa alikuwa ameonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya, \v 23 akaenda kuishi katika mji ulioitwa Nasiri. Hivyo likawa limetimia neno lililonenwa na manabii waliposema, “Ataitwa Mnasiri.” \c 3 \s1 Yahya atayarisha njia \r (Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yohana 1:19-28) \p \v 1 Siku hizo Yahya alikuja akihubiri katika nyika ya Yudea, akisema, \v 2 “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” \v 3 Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema: \q1 “Sauti ya mtu aliaye nyikani, \q1 ‘Itengenezeni njia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, \q2 yanyoosheni mapito yake.’ ” \p \v 4 Basi Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. \v 5 Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Yudea yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. \v 6 Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza\f + \fr 3:6 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali.\ft*\f* katika Mto Yordani. \p \v 7 Lakini alipowaona Mafarisayo\f + \fr 3:7 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na Masadukayo\f + \fr 3:7 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; waliamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho.\ft*\f* wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? \v 8 Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. \v 9 Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya. \v 10 Hata sasa shoka limeshawekwa tayari katika shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni. \p \v 11 “Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu wa Mungu\f + \fr 3:11 \fr*\ft au \ft*\fqa katika Roho wa Mungu\fqa*\f* na kwa moto. \v 12 Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.” \s1 Isa abatizwa \r (Marko 1:9-11; Luka 3:21-22) \p \v 13 Kisha Isa akaja kutoka Galilaya hadi Mto Yordani ili Yahya ambatize. \v 14 Lakini Yahya akajitahidi kumzuia, akimwambia, “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?” \p \v 15 Lakini Isa akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yahya akakubali. \p \v 16 Naye Isa alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. \v 17 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa; ninapendezwa sana naye.” \c 4 \s1 Isa ajaribiwa nyikani \r (Marko 1:12-13; Luka 4:1-13) \p \v 1 Kisha Isa akaongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu hadi nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. \v 2 Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. \v 3 Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu\f + \fr 4:3 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*, amuru mawe haya yawe mikate.” \p \v 4 Lakini Isa akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ” \p \v 5 Ndipo ibilisi akampeleka Isa hadi mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu\f + \fr 4:5 \fr*\ft Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu.\ft*\f*, \v 6 akamwambia, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: \q1 “ ‘Atakuagizia malaika wake, \q2 nao watakuchukua mikononi mwao \q1 ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ” \p \v 7 Isa akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.’ ” \p \v 8 Kwa mara nyingine, ibilisi akampeleka Isa hadi kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonesha falme zote za dunia na fahari zake, \v 9 kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote ukinisujudia na kuniabudu.” \p \v 10 Isa akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ” \p \v 11 Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia. \s1 Isa aanza kuhubiri \r (Marko 1:14-15; Luka 4:14-15) \p \v 12 Isa aliposikia kwamba Yahya alikuwa amefungwa gerezani, alirudi Galilaya. \v 13 Akaondoka Nasiri akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulio karibu na bahari, katika nchi ya Zabuloni na Naftali, \v 14 ili kutimiza neno lililonenwa na nabii Isaya, aliposema: \q1 \v 15 “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, \q2 kwenye njia ya bahari, \q1 ng’ambo ya Yordani, \q2 Galilaya ya Mataifa: \q1 \v 16 watu wale waliokaa gizani \q2 wameona nuru kuu; \q1 nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti, \q2 nuru imewazukia.” \p \v 17 Tangu wakati huo, Isa alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” \s1 Wanafunzi wa kwanza wa Isa \r (Marko 1:16-20; Luka 5:1-11; Yohana 1:35-51) \p \v 18 Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa walikuwa wavuvi. \v 19 Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” \v 20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. \p \v 21 Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Isa akawaita. \v 22 Nao mara moja wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata. \s1 Isa afundisha na kuponya wagonjwa \r (Luka 6:17-19) \p \v 23 Isa akazunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi\f + \fr 4:23 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* yao, akihubiri Habari Njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu. \v 24 Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Siria, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya. \v 25 Makundi makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli\f + \fr 4:25 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Miji Kumi\fqa*\f*, Yerusalemu, Yudea, na kutoka ng’ambo ya Yordani. \c 5 \ms1 Mahubiri ya Mlimani \mr (Mathayo 5–7) \p \v 1 Basi Isa alipoona makundi ya watu, alipanda mlimani akaketi chini, nao wanafunzi wake wakamjia. \s1 Sifa za aliyebarikiwa \r (Luka 6:20-23) \p \v 2 Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema: \q1 \v 3 “Heri walio maskini wa roho, \q2 maana ufalme wa mbinguni ni wao. \q1 \v 4 Heri wale wanaohuzunika, \q2 maana hao watafarijiwa. \q1 \v 5 Heri walio wapole, \q2 maana hao watairithi nchi. \q1 \v 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, \q2 maana hao watatoshelezwa. \q1 \v 7 Heri wenye huruma, \q2 maana hao watapata rehema. \q1 \v 8 Heri walio na moyo safi, \q2 maana hao watamwona Mungu. \q1 \v 9 Heri walio wapatanishi, \q2 maana hao wataitwa wana wa Mungu. \q1 \v 10 Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, \q2 maana ufalme wa mbinguni ni wao. \p \v 11 “Heri ninyi watu watakapowashutumu, na kuwatesa na kunena mabaya ya aina zote dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu. \v 12 Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu. \s1 Chumvi na nuru \r (Marko 9:50; Luka 14:34-35) \p \v 13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu chochote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu. \p \v 14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. \v 15 Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliye ndani ya ile nyumba. \v 16 Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba\f + \fr 5:16 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yenu aliye mbinguni. \s1 Kutimiza Torati \p \v 17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta Torati au Manabii; sikuja kuondoa bali kutimiza. \v 18 Kwa maana, amin nawaambia, hadi mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwa Torati, hadi kila kitu kiwe kimetimia. \v 19 Kwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika ufalme wa mbinguni. \v 20 Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo\f + \fr 5:20 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na walimu wa Torati, kamwe hamtaingia katika ufalme wa mbinguni. \s1 Kuhusu hasira \r (Luka 12:57-59) \p \v 21 “Mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiue. Yeyote atakayeua atapaswa hukumu.’ \v 22 Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka\f + \fr 5:22 \fr*\ft neno la Kiaramu la dharau au dhihaka ya hali ya juu\ft*\f*,’ atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi\f + \fr 5:22 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa Jehanamu. \p \v 23 “Kwa hiyo, ikiwa unatoa sadaka yako madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako ana kitu dhidi yako, \v 24 iache sadaka yako hapo mbele ya madhabahu. Nenda kwanza ukapatane na ndugu yako; kisha urudi na ukatoe sadaka yako. \p \v 25 “Patana na mshtaki wako upesi wakati mpo njiani kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani. \v 26 Amin, nakuambia, hutatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho. \s1 Kuhusu uzinzi \p \v 27 “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ \v 28 Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. \v 29 Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa Jehanamu. \v 30 Kama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe Jehanamu. \s1 Kuhusu talaka \r (Mathayo 19:9; Marko 10:11-12; Luka 16:18) \p \v 31 “Pia ilinenwa kwamba, ‘Mtu yeyote amwachaye mkewe sharti ampe hati ya talaka.’ \v 32 Lakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini. \s1 Kuhusu kuapa \p \v 33 “Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Mwenyezi Mungu.’ \v 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; \v 35 au kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. \v 36 Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. \v 37 ‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu. \s1 Kuhusu kulipiza kisasi \r (Luka 6:29-30) \p \v 38 “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ \v 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. \v 40 Mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. \v 41 Mtu akikulazimisha kwenda maili moja\f + \fr 5:41 \fr*\ft kama kilomita 1.6\ft*\f*, nenda naye maili mbili\f + \fr 5:41 \fr*\ft kama kilomita 3.2\ft*\f*. \v 42 Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa. \s1 Wapendeni adui zenu \r (Luka 6:27-28, 32-36) \p \v 43 “Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ \v 44 Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu, na waombeeni wanaowatesa ninyi, \v 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. \v 46 Mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo? \v 47 Nanyi mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu hawafanyi hivyo? \v 48 Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. \c 6 \s1 Kuwapa wahitaji \p \v 1 “Angalieni msitende wema wenu mbele ya watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu aliye mbinguni. \p \v 2 “Hivyo mnapowapa wahitaji, msitangaze hadharani kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi\f + \fr 6:2 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* na mitaani, ili wasifiwe na watu. Amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao. \v 3 Lakini ninyi mtoapo sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume unachofanya, \v 4 ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo Baba yako wa mbinguni, yeye aonaye sirini atakupa thawabu kwa wazi. \s1 Kuhusu maombi \r (Luka 11:2-8) \p \v 5 “Nanyi mnaposali, msiwe kama wanafiki, maana wao hupenda kusali wakiwa wamesimama katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wao wamekwisha kupokea thawabu yao. \v 6 Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako. \v 7 Nanyi mnaposali msiseme maneno kama wafanyavyo watu wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. \v 8 Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba. \p \v 9 “Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba: \q1 “ ‘Baba yetu uliye mbinguni, \q2 Jina lako litukuzwe. \q1 \v 10 Ufalme wako uje. \q2 Mapenzi yako yafanyike \q2 hapa duniani kama huko mbinguni. \q1 \v 11 Utupatie riziki yetu \q2 ya kila siku. \q1 \v 12 Utusamehe deni zetu, \q2 kama sisi nasi tulivyokwisha \q2 kuwasamehe wadeni wetu. \q1 \v 13 Usitutie majaribuni, \q2 bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu \q1 [kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, \q2 na utukufu, hata milele. Amen]\f + \fr 6:13 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*.’ \m \v 14 Kwa kuwa mkiwasamehe watu wengine wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia. \v 15 Lakini msipowasamehe watu wengine makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. \s1 Kuhusu kufunga \p \v 16 “Mnapofunga, msiwe wenye huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kuwaonesha wengine kwamba wamefunga. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha kupokea thawabu yao kamilifu. \v 17 Lakini unapofunga, jipake mafuta kichwani na kunawa uso wako, \v 18 ili kufunga kwako kusionekane na watu wengine ila Baba yako anayeketi mahali pa siri; naye Baba yako aonaye sirini atakupa thawabu yako kwa wazi. \s1 Kuweka hazina mbinguni \r (Luka 12:33-34) \p \v 19 “Msijiwekee hazina duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, nao wezi huvunja na kuiba. \v 20 Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wezi hawavunji na kuiba. \v 21 Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo pia moyo wako utakapokuwa. \s1 Taa ya mwili \r (Luka 11:34-36) \p \v 22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. \v 23 Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Hivyo basi, ikiwa nuru iliyo ndani yako ni giza, je, hilo ni giza nene aje! \s1 Kutumikia Mwenyezi Mungu na mali \r (Luka 16:13; 12:22-31) \p \v 24 “Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali\f + \fr 6:24 \fr*\ft au \ft*\fqa Utajiri\fqa*\ft ; yaani \ft*\fqa Mamoni \fqa*\ft kwa Kiaramu au \ft*\fqa Mamona \fqa*\ft kwa Kiyunani\ft*\f*. \s1 Msiwe na wasiwasi \r (Luka 12:22-31) \p \v 25 “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini au mtakunywa nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? \v 26 Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao ndege? \v 27 Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake? \p \v 28 “Nanyi kwa nini mnajitaabisha kwa ajili ya mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi. \v 29 Lakini nawaambia, hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua. \v 30 Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba? \v 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ \v 32 Watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. \v 33 Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia. \v 34 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Kila siku ina masumbufu yake ya kutosha. \c 7 \s1 Kuwahukumu wengine \r (Luka 6:37-38, 41-42) \p \v 1 “Usihukumu ili usije ukahukumiwa. \v 2 Kwa maana jinsi unavyowahukumu wengine, ndivyo utakavyohukumiwa, na kwa kipimo kile upimiacho, ndicho utakachopimiwa. \p \v 3 “Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? \v 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Acha nitoe kibanzi kwenye jicho lako,’ wakati kuna boriti kwenye jicho lako mwenyewe? \v 5 Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako. \p \v 6 “Msiwape mbwa vitu vilivyo vitakatifu; wala msitupie nguruwe lulu zenu. Mkifanya hivyo, watazikanyagakanyaga na kisha watawageukia na kuwararua vipande vipande. \s1 Omba, tafuta, bisha \r (Luka 11:9-13) \p \v 7 “Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. \v 8 Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango. \p \v 9 “Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? \v 10 Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? \v 11 Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba\f + \fr 7:11 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? \v 12 Kwa hiyo chochote mnachotaka mtendewe na watu, ninyi nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii ndiyo Torati na Manabii. \s1 Mlango mwembamba na njia pana \p \v 13 “Ingieni kupitia mlango mwembamba, kwa maana lango ni pana na njia ni pana ielekeayo upotevuni, nao ni wengi wanaoingia kupitia lango hilo. \v 14 Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao. \s1 Mti na matunda yake \r (Marko 12:33-35; Luka 6:43-44) \p \v 15 “Jihadharini na manabii wa uongo, wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini ndani ni mbwa-mwitu wakali. \v 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu kwenye miiba, au tini kwenye michongoma? \v 17 Vivyo hivyo, mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. \v 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. \v 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. \v 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao. \s1 Mwanafunzi wa kweli \r (Luka 13:25-27) \p \v 21 “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. \v 22 Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’ \v 23 Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’ \s1 Mjenzi mwenye busara na mjenzi mpumbavu \r (Luka 6:47-49) \p \v 24 “Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. \v 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba. \v 26 Kila anayesikia haya maneno yangu na asiyatende ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. \v 27 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.” \p \v 28 Isa alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, \v 29 kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria. \c 8 \ms1 Mafundisho ya mifano na mazungumzo \mr (Mathayo 8–18) \s1 Isa amtakasa mtu mwenye ukoma \r (Marko 1:40-45; Luka 5:12-16) \p \v 1 Isa aliposhuka kutoka mlimani, makundi ya watu wakamfuata. \v 2 Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana\f + \fr 8:2 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, ukitaka, unaweza kunitakasa.” \p \v 3 Isa akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. \v 4 Kisha Isa akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajioneshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao.” \s1 Isa amponya mtumishi wa jemadari \r (Luka 7:1-10) \p \v 5 Isa alipoingia Kapernaumu, jemadari mmoja alimjia, kumwomba msaada, \v 6 akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani na amepooza, tena ana maumivu makali ya kutisha.” \p \v 7 Isa akamwambia, “Nitakuja na kumponya.” \p \v 8 Lakini yule jemadari akamwambia, “Bwana, mimi sistahili wewe kuingia ndani ya nyumba yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. \v 9 Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliye chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.” \p \v 10 Isa aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii. \v 11 Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni. \v 12 Lakini warithi wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwa kilio na kusaga meno.” \p \v 13 Kisha Isa akamwambia yule jemadari, “Nenda na iwe kwako sawasawa na imani yako.” Naye yule mtumishi akapona wakati ule ule. \s1 Isa amponya mama mkwe wa Petro na pia watu wengi \r (Marko 1:29-34; Luka 4:38-41) \p \v 14 Isa alipoingia nyumbani mwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. \v 15 Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia. \p \v 16 Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. \v 17 Haya yalifanyika ili litimie neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya, kwamba: \q1 “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu \q2 na akachukua magonjwa yetu.” \s1 Gharama ya kumfuata Isa \r (Luka 9:57-62) \p \v 18 Isa alipoona makundi mengi yamemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake wavuke hadi ng’ambo ya ziwa. \v 19 Kisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Isa na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata popote utakakoenda.” \p \v 20 Naye Isa akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.” \p \v 21 Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” \p \v 22 Lakini Isa akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.” \s1 Isa atuliza dhoruba \r (Marko 4:35-41; Luka 8:22-25) \p \v 23 Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata. \v 24 Ghafula, kukatokea dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Isa alikuwa amelala usingizi. \v 25 Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!” \p \v 26 Naye Isa akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nayo bahari ikatulia kabisa. \p \v 27 Wale watu wakashangaa, wakisema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!” \s1 Watu wawili wenye pepo wachafu waponywa \r (Marko 5:1-20; Luka 8:26-39) \p \v 28 Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile. \v 29 Wakapaza sauti wakisema, “Una nini nasi, Mwana wa Mungu\f + \fr 8:29 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati ulioamriwa?” \p \v 30 Mbali kidogo kutoka pale walipokuwa, kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakila. \v 31 Wale pepo wachafu wakamsihi Isa, “Ukitutoa humu, turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.” \p \v 32 Akawaambia, “Nendeni!” Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji. \v 33 Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu. \v 34 Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Isa. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao. \c 9 \s1 Isa amponya mtu aliyepooza \r (Marko 2:1-12; Luka 5:17-26) \p \v 1 Isa akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. \v 2 Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa.” \p \v 3 Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” \p \v 4 Lakini Isa akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? \v 5 Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? \v 6 Lakini nataka mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Ndipo akamwambia yule aliyepooza, “Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako.” \v 7 Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani mwake. \v 8 Umati wa watu walipoyaona haya, wakajawa na hofu ya Mungu, wakamtukuza Mungu aliyekuwa amewakabidhi wanadamu mamlaka kama haya. \s1 Isa amwita Mathayo \r (Marko 2:13-17; Luka 5:27-32) \p \v 9 Isa alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Isa akamwambia, “Nifuate.” Mathayo akasimama, akamfuata. \p \v 10 Isa alipokuwa ameketi akila chakula ndani ya nyumba ya Mathayo, watoza ushuru wengi na wenye dhambi wakaja, wakaketi kula pamoja naye na wanafunzi wake. \v 11 Mafarisayo\f + \fr 9:11 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* walipoona mambo haya, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini Mwalimu wenu anakula na watoza ushuru na wenye dhambi?” \p \v 12 Lakini Isa aliposikia hayo, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, lakini wale walio wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu. \v 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” \s1 Isa aulizwa kuhusu kufunga \r (Marko 2:18-22; Luka 5:33-39) \p \v 14 Wanafunzi wa Yahya wakaja na kumuuliza Isa, “Imekuwaje kwamba sisi na Mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?” \p \v 15 Isa akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wanawezaje kuomboleza wakati angali pamoja nao? Wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga. \p \v 16 “Hakuna mtu anayeshonea kiraka kipya kwenye nguo iliyochakaa, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye hiyo nguo, nayo hiyo nguo itachanika zaidi. \v 17 Wala watu hawaweki divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Wakifanya hivyo, viriba vitapasuka nayo divai itamwagika, navyo viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya, na hivyo divai na viriba huwa salama.” \s1 Isa amponya mwanamke na kumfufua msichana \r (Marko 5:21-43; Luka 8:40-56) \p \v 18 Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, kiongozi wa sinagogi\f + \fr 9:18 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* akaingia, akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.” \v 19 Isa akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye. \p \v 20 Wakati huo huo, mwanamke mmoja, aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake, \v 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu vazi lake, nitaponywa.” \p \v 22 Isa akageuka, naye alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa hiyo. \p \v 23 Isa alipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele, \v 24 akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. \v 25 Lakini watu walipokwisha kutolewa nje, akaingia mle ndani na kumshika yule binti mkono, naye akaamka. \v 26 Habari hizi zikaenea katika maeneo yale yote. \s1 Isa awaponya Vipofu \p \v 27 Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti na kusema, “Mwana wa Daudi\f + \fr 9:27 \fr*\ft Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*, tuhurumie!” \p \v 28 Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Isa akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?” \p Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.” \p \v 29 Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.” \v 30 Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, “Chungeni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.” \v 31 Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote. \s1 Isa amponya bubu \p \v 32 Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa. \v 33 Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea, na umati wa watu wakastaajabu na kusema, “Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli.” \p \v 34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa mkuu wa pepo wachafu.” \s1 Watendakazi ni wachache \p \v 35 Isa akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi\f + \fr 9:35 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* yao, akihubiri Habari Njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi. \v 36 Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. \v 37 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. \v 38 Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili atume watendakazi katika shamba lake la mavuno.” \c 10 \s1 Isa achagua mitume kumi na wawili \r (Marko 3:13-19; Luka 6:12-16) \p \v 1 Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina. \b \lh \v 2 Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: \b \li1 wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; \li1 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye; \li1 \v 3 Filipo, na Bartholomayo; \li1 Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; \li1 Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; \li1 \v 4 Simoni Mkananayo\f + \fr 10:4 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mzelote\fqa*\ft ; Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi.\ft*\f*, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa. \s1 Isa awatuma wale kumi na wawili \r (Marko 6:7-13; Luka 9:1-6) \p \v 5 Hawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria. \v 6 Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. \v 7 Mnapoenda, hubirini ujumbe huu, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’ \v 8 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure. \v 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu. \v 10 Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake. \p \v 11 “Mji wowote au kijiji chochote mtakapoingia, tafuteni humo mtu anayestahili, nanyi kaeni kwake hadi mtakapoondoka. \v 12 Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani. \v 13 Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi. \v 14 Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo. \v 15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo. \s1 Mateso yanayokuja \r (Marko 13:9-13; Luka 21:12-17) \p \v 16 “Tazama ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa-mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. \p \v 17 “Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao. \v 18 Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa. \v 19 Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikiria mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo. \v 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba\f + \fr 10:20 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu. \p \v 21 “Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, naye baba atamsaliti mtoto wake. Watoto nao wataasi dhidi ya wazazi wao na kusababisha wauawe. \v 22 Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. \v 23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja. \p \v 24 “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, wala mtumishi hamzidi bwana wake. \v 25 Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli\f + \fr 10:25 \fr*\ft kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Beelzebubu\fqa*\ft , yaani mkuu wa pepo wachafu\ft*\f*, je, si watawaita zaidi wale wa nyumbani mwake! \s1 Maonyo dhidi ya unafiki \r (Luka 12:1-12) \p \v 26 “Basi msiwaogope, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. \v 27 Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinong’onwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba. \v 28 Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika Jehanamu\f + \fr 10:28 \fr*\ft Jehanamu kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Gehena\fqa*\ft , yaani motoni.\ft*\f*. \v 29 Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua. \v 30 Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. \v 31 Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi. \p \v 32 “Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni. \v 33 Lakini yeyote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. \s1 Sikuleta amani, bali upanga \r (Luka 12:51-53; 14:26-27) \p \v 34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. \v 35 Kwa maana nimekuja kuleta uadui kati ya \q1 “ ‘mtu na baba yake, \q2 binti na mama yake, \q1 mkwe na mama mkwe wake; \q2 \v 36 nao adui za mtu watakuwa \q2 ni wale watu wa nyumbani mwake.’ \p \v 37 “Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. \v 38 Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. \v 39 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata. \s1 Watakaopokea thawabu \r (Marko 9:41) \p \v 40 “Mtu yeyote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi, na yeyote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye aliyenituma. \v 41 Mtu yeyote anayempokea nabii kwa kuwa ni nabii atapokea thawabu ya nabii, naye mtu anayempokea mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki atapokea thawabu ya mwenye haki. \v 42 Mtu yeyote akimpa hata kikombe cha maji baridi mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, amin, nawaambia, hataikosa thawabu yake.” \c 11 \s1 Isa na Yahya \r (Luka 7:18-35) \p \v 1 Baada ya Isa kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji ya Galilaya. \p \v 2 Yahya aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Al-Masihi\f + \fr 11:2 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Masihi, \fqa*\ft yaani \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake \v 3 ili wakamuulize, “Wewe ndiwe yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?” \p \v 4 Isa akajibu, “Rudini mkamwambie Yahya yale mnayosikia na kuyaona: \v 5 Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema. \v 6 Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.” \p \v 7 Wale wanafunzi wa Yahya walipokuwa wanaondoka, Isa akaanza kusema na umati wa watu kuhusu Yahya. Akawauliza, “Mlipoenda kule nyikani, mlienda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? \v 8 Kama sivyo, mlienda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha! Watu wanaovaa mavazi ya kifahari wako katika majumba ya wafalme. \v 9 Basi mlienda kuona nini? Mlienda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. \v 10 Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa: \q1 “ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, \q2 atakayetengeneza njia mbele yako.’ \m \v 11 Amin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yahya. Lakini aliye mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko Yahya. \v 12 Tangu siku za Yahya hadi sasa, ufalme wa mbinguni hunyakuliwa kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka. \v 13 Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri hadi wakati wa Yahya. \v 14 Ikiwa mko tayari kukubali hilo, yeye ndiye yule Ilya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja. \v 15 Yeye aliye na masikio, na asikie. \p \v 16 “Lakini kizazi hiki nikifananishe na nini? Kinafanana na watoto waliokaa sokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia, \q1 \v 17 “ ‘Tuliwapigia filimbi, \q2 lakini hamkucheza; \q1 tuliwaimbia nyimbo za maombolezo, \q2 lakini hamkuomboleza.’ \m \v 18 Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’ \v 19 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.” \s1 Onyo kwa miji isiyotubu \r (Luka 10:13-15) \p \v 20 Ndipo Isa akaanza kuishutumu miji ambayo alifanya miujiza yake mingi, kwa maana watu wake hawakutubu. \v 21 “Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. \v 22 Lakini nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili katika siku ya hukumu, kuliko ninyi. \v 23 Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha! Utashushwa hadi Kuzimu\f + \fr 11:23 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Hades\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa mahali pa wafu.\fqa*\f*. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungekuwepo hadi leo. \v 24 Lakini nakuambia kwamba, itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma kustahimili katika siku ya hukumu kuliko wewe.” \s1 Hakuna amjuaye Baba ila Mwana \r (Luka 10:21-22) \p \v 25 Wakati huo Isa alisema, “Nakuhimidi Baba\f + \fr 11:25 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. \v 26 Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza. \p \v 27 “Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia. \s1 Isa awaita waliolemewa na mizigo \p \v 28 “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. \v 29 Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu. \v 30 Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.” \c 12 \s1 Isa ni Bwana wa Sabato \r (Marko 2:23-28; Luka 6:1-5) \p \v 1 Wakati huo Isa alipitia kwenye mashamba ya nafaka siku ya Sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, nao wakaanza kuvunja masuke ya nafaka na kuyala. \v 2 Lakini Mafarisayo\f + \fr 12:2 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.” \p \v 3 Isa akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? \v 4 Aliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani tu. \v 5 Au hamjasoma katika Torati kwamba siku ya Sabato makuhani huvunja sheria ya Sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? \v 6 Nawaambia wazi kwamba, yeye aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. \v 7 Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia, \v 8 kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” \s1 Isa amponya mtu aliyepooza mkono \r (Marko 3:1-6; Luka 6:6-11) \p \v 9 Isa akaondoka mahali hapo, akaingia ndani ya sinagogi\f + \fr 12:9 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* lao, \v 10 na huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono. Wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa, wakamuuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” \p \v 11 Isa akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu, mwenye kondoo wake ambaye huyo kondoo akitumbukia shimoni siku ya Sabato hatamtoa? \v 12 Mtu ana thamani kubwa kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” \p \v 13 Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa ukawa mzima kama ule mwingine. \v 14 Lakini Mafarisayo wakatoka nje na kupanga njama ya kumuua Isa. \s1 Mtumishi aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu \p \v 15 Lakini Isa alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi walimfuata, naye akawaponya wote waliokuwa wagonjwa miongoni mwao, \v 16 akiwakataza wasiseme yeye ni nani, \v 17 ili neno lililonenwa na nabii Isaya litimie, aliposema: \q1 \v 18 “Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, \q2 mpendwa wangu, ninayependezwa naye. \q1 Nitaweka Roho wangu Mtakatifu juu yake, \q2 naye atatangaza haki kwa mataifa. \q1 \v 19 Hatagombana wala kupaza sauti, \q2 wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani. \q1 \v 20 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, \q2 na utambi unaofuka moshi hatauzima, \q1 hadi atakapoifanya haki ishinde. \q2 \v 21 Katika Jina lake mataifa \q2 wataweka tumaini lao.” \s1 Isa na Beelzebuli \r (Marko 3:20-30; Luka 11:14-23) \p \v 22 Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Isa akamponya, hata akaweza kusema na kuona. \v 23 Watu wote wakashangaa na kusema, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi\f + \fr 12:23 \fr*\ft Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*?” \p \v 24 Lakini Mafarisayo waliposikia jambo hili wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli\f + \fr 12:24 \fr*\ft au \ft*\fqa Beelzebubu\fqa*\ft ; pia \+xt 12:27\+xt*\ft*\f*, mkuu wa pepo wachafu.” \p \v 25 Isa alijua walichokuwa wakiwaza, hivyo akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja waliogawanyika dhidi yao wenyewe hawawezi kusimama. \v 26 Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama? \v 27 Nami kama natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu. \v 28 Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekuja juu yenu. \p \v 29 “Au tena, mtu anawezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali yake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali yake. \p \v 30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya. \v 31 Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa. \v 32 Mtu yeyote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote anenaye neno dhidi ya Roho wa Mungu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao. \s1 Mti na matunda yake \r (Luka 6:43-45) \p \v 33 “Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake. \v 34 Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake. \v 35 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake. \v 36 Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa maelezo kuhusu kila neno walilonena lisilo la maana. \v 37 Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” \s1 Ishara ya Yona \r (Marko 8:11-13; Luka 11:29-32) \p \v 38 Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa Torati wakamwambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” \p \v 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona. \v 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa sana kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana. \v 41 Siku ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona. \v 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani. \s1 Mafundisho kuhusu pepo mchafu \r (Luka 11:24-26) \p \v 43 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. \v 44 Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ Naye anaporudi huikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri. \v 45 Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.” \s1 Mama yake na ndugu zake Isa \r (Marko 3:31-35; Luka 8:19-21) \p \v 46 Wakati alikuwa angali anazungumza na umati wa watu, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. \v 47 Ndipo mtu mmoja akamwambia, “Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe.” \p \v 48 Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, “Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?” \v 49 Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! \v 50 Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba\f + \fr 12:50 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu wa mbinguni, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu.” \c 13 \s1 Mfano wa mpanzi \r (Marko 4:1-9; Luka 8:1-8) \p \v 1 Siku hiyo hiyo Isa akatoka nje ya nyumba, akaketi kando ya bahari. \v 2 Umati mkubwa mno wa watu wakakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari. \v 3 Ndipo akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema: “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. \v 4 Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. \v 5 Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba. \v 6 Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. \v 7 Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea. \v 8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri ambapo zilitoa mazao, nyingine mara mia moja, nyingine mara sitini, na nyingine mara thelathini. \v 9 Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” \s1 Sababu ya kufundisha kwa mifano \r (Marko 4:10-12; Luka 8:9-10) \p \v 10 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamuuliza, “Kwa nini unasema na watu kwa mifano?” \p \v 11 Akawajibu, “Ninyi mmepewa ujuzi wa siri za ufalme wa mbinguni, lakini wao hawajapewa. \v 12 Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. \v 13 Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano: \q1 “Ingawa wanatazama, hawaoni; \q2 wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi. \m \v 14 Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema: \q1 “ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa; \q2 na pia mtatazama lakini hamtaona. \q1 \v 15 Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu; \q2 hawasikii kwa masikio yao, \q2 na wamefumba macho yao. \q1 Wasije wakaona kwa macho yao, \q2 na wakasikiliza kwa masikio yao, \q2 wakaelewa kwa mioyo yao, \q1 na kugeuka nami nikawaponya.’ \m \v 16 Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia. \v 17 Amin, nawaambia, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia. \s1 Maelezo ya mfano wa mbegu \r (Marko 4:13-20; Luka 8:11-15) \p \v 18 “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi: \v 19 Mtu yeyote anaposikia neno la ufalme naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake. Hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia. \v 20 Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na hulipokea mara moja kwa furaha. \v 21 Lakini kwa kuwa hana mizizi yenye kina ndani yake, lile neno hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, yeye anarudi nyuma mara moja. \v 22 Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu anayelisikia neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. \v 23 Lakini ile mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, akizaa mara mia, au mara sitini, au mara thelathini ya mbegu iliyopandwa.” \s1 Mfano wa magugu \p \v 24 Isa akawaambia mfano mwingine, akasema: “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. \v 25 Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. \v 26 Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea. \p \v 27 “Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?’ \p \v 28 “Akawajibu, ‘Adui ndiye alifanya jambo hili.’ \p “Wale watumishi wakamuuliza, ‘Je, unataka twende tukayang’oe?’ \p \v 29 “Lakini akasema, ‘Hapana, msiyang’oe, kwa maana wakati mking’oa magugu mnaweza mkang’oa na ngano pamoja nayo. \v 30 Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja hadi wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ” \s1 Mfano wa punje ya haradali \r (Marko 4:30-32; Luka 13:18-19) \p \v 31 Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua, akaipanda shambani mwake. \v 32 Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.” \s1 Mfano wa chachu \r (Luka 13:20-21) \p \v 33 Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga hadi wote ukaumuka.” \p \v 34 Isa alinena mambo haya yote kwa umati wa watu kwa mifano, wala hakuwaambia lolote pasipo mfano. \v 35 Hii ilikuwa ili kutimiza neno lililonenwa na nabii, aliposema: \q1 “Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano; \q2 nitahubiri mambo yaliyofichika \q2 tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.” \s1 Ufafanuzi wa mfano wa magugu \p \v 36 Kisha Isa akaagana na ule umati, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.” \p \v 37 Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu. \v 38 Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. \v 39 Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika. \p \v 40 “Kama vile magugu yang’olewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. \v 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika wake, nao watakusanya kutoka ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote. \v 42 Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. \v 43 Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika ufalme wa Baba\f + \fr 13:43 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yao. Yeye aliye na masikio, na asikie. \s1 Mfano wa hazina iliyofichwa na mfano wa lulu \p \v 44 “Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba. \p \v 45 “Tena, ufalme wa mbinguni unafanana na mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta lulu safi. \v 46 Alipoipata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza vyote alivyokuwa navyo akainunua. \s1 Mfano wa wavu \p \v 47 “Tena, ufalme wa mbinguni ni kama wavu wa kuvua samaki uliotupwa baharini ukavua samaki wa kila aina. \v 48 Ulipojaa, wavuvi wakauvuta ufuoni, wakaketi na kukusanya samaki wazuri kuwaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawatupa. \v 49 Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. \v 50 Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.” \p \v 51 Isa akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?” \p Wakamjibu, “Ndiyo.” \p \v 52 Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa Torati aliyefundishwa elimu ya ufalme wa mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.” \s1 Isa akataliwa Nasiri \r (Marko 6:1-6; Luka 4:16-30) \p \v 53 Isa alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka. \v 54 Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi\f + \fr 13:54 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza? \v 55 Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si yeye aitwaye Mariamu, nao ndugu zake si Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? \v 56 Nao dada zake wote, hawako hapa pamoja nasi? Mtu huyu amepata wapi basi mambo haya yote?” \v 57 Wakachukizwa naye. \p Lakini Isa akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake.” \p \v 58 Naye hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao. \c 14 \s1 Yahya akatwa kichwa \r (Marko 6:14-29; Luka 9:7-9) \p \v 1 Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Isa, \v 2 akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yahya; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.” \p \v 3 Herode alikuwa amemkamata Yahya, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, \v 4 kwa kuwa Yahya alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” \v 5 Herode alitaka sana kumuua Yahya, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. \p \v 6 Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria. Alimfurahisha Herode sana, \v 7 kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba. \v 8 Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yahya kwenye sinia.” \v 9 Mfalme alisikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. \v 10 Hivyo akaagiza Yahya akatwe kichwa mle gerezani. \v 11 Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. \v 12 Wanafunzi wa Yahya wakaja na kuuchukua mwili wake, wakamzika. Kisha wakaenda wakamwambia Isa. \s1 Isa alisha wanaume 5,000 \r (Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14) \p \v 13 Isa aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. \v 14 Isa alipofika kando ya bahari, aliona makundi makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao. \p \v 15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makundi ya watu ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.” \p \v 16 Isa akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” \p \v 17 Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” \p \v 18 Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” \v 19 Isa akaagiza umati wa watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia ule umati. \v 20 Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. \v 21 Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto. \s1 Isa atembea juu ya maji \r (Marko 6:45-52; Yohana 6:16-21) \p \v 22 Mara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie katika mashua wamtangulie kwenda ng’ambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiaga ule umati. \v 23 Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Isa alikuwa huko peke yake. \v 24 Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. \p \v 25 Wakati wa zamu ya nne ya usiku\f + \fr 14:25 \fr*\ft yaani kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi\ft*\f*, Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. \v 26 Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa. \p \v 27 Lakini mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.” \p \v 28 Petro akamjibu, “Bwana Isa, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.” \p \v 29 Isa akamwambia, “Njoo.” \p Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Isa. \v 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, akapaza sauti na kusema, “Bwana, niokoe!” \p \v 31 Mara Isa akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?” \p \v 32 Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. \v 33 Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Isa, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu\f + \fr 14:33 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*.” \s1 Isa awaponya wagonjwa Genesareti \r (Marko 6:53-56) \p \v 34 Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti. \v 35 Watu wa eneo lile walipomtambua Isa, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, \v 36 wakamsihi awaruhusu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa, wakaponywa. \c 15 \s1 Mapokeo ya wazee \r (Marko 7:1-13) \p \v 1 Ndipo baadhi ya Mafarisayo\f + \fr 15:1 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na walimu wa Torati wakamjia Isa kutoka Yerusalemu na kumuuliza, \v 2 “Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!” \p \v 3 Isa akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? \v 4 Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ \v 5 Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’ \v 6 basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. \v 7 Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba: \q1 \v 8 “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, \q2 lakini mioyo yao iko mbali nami. \q1 \v 9 Huniabudu bure; \q2 nayo mafundisho yao \q2 ni maagizo ya wanadamu tu.’ ” \s1 Vitu vinavyomnajisi mtu \r (Marko 7:14-23) \p \v 10 Isa akaita umati wa watu waliokuwa hapo, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: \v 11 kinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.” \p \v 12 Kisha wanafunzi wake wakamjia na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa sana waliposikia yale uliyosema?” \p \v 13 Akawajibu, “Kila mmea ambao Baba\f + \fr 15:13 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu wa mbinguni hakuupanda utang’olewa. \v 14 Waacheni; wao ni viongozi vipofu, wanaoongoza vipofu. Kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.” \p \v 15 Petro akasema, “Tueleze maana ya huu mfano.” \p \v 16 Isa akawauliza, “Je, bado ninyi hamfahamu? \v 17 Je, hamwelewi kwamba chochote kiingiacho kinywani huenda tumboni, na hatimaye hutolewa nje kikiwa uchafu? \v 18 Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. \v 19 Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. \v 20 Haya ndio yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.” \s1 Imani ya mwanamke Mkanaani \r (Marko 7:24-30) \p \v 21 Isa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. \v 22 Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi\f + \fr 15:22 \fr*\ft Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.” \p \v 23 Lakini Isa hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele.” \p \v 24 Isa akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea.” \p \v 25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Isa, akasema, “Bwana, nisaidie!” \p \v 26 Isa akajibu, “Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” \p \v 27 Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwa meza za bwana zao.” \p \v 28 Ndipo Isa akamwambia, “Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka.” Naye binti yake akapona tangu saa ile. \s1 Isa aponya watu wengi \p \v 29 Isa akaondoka na kwenda kando ya Bahari ya Galilaya. Kisha akapanda mlimani, akaketi huko. \v 30 Umati mkubwa wa watu wakamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya. \v 31 Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli. \s1 Isa alisha wanaume 4,000 \r (Marko 8:1-10) \p \v 32 Kisha Isa akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Ninahurumia umati huu wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga watu wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.” \p \v 33 Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kulisha umati mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?” \p \v 34 Isa akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” \p Wakamjibu, “Tunayo mikate saba na visamaki vichache.” \p \v 35 Isa akaagiza watu wote waketi chini. \v 36 Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akamshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. \v 37 Wote wakala na kushiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. \v 38 Idadi ya watu walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto. \p \v 39 Baada ya kuaga umati wa watu, Isa aliingia katika mashua, akaenda sehemu za Magadani\f + \fr 15:39 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Magdala \fqa*\ft katika Galilaya\ft*\f*. \c 16 \s1 Kutambua majira \r (Luka 12:54-56) \p \v 1 Mafarisayo\f + \fr 16:1 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na Masadukayo\f + \fr 16:1 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; waliamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho.\ft*\f* wakamjia Isa na kumjaribu kwa kumwomba awaoneshe ishara kutoka mbinguni. \p \v 2 Isa akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’ \v 3 Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua ishara za nyakati. \v 4 Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Isa akawaacha, akaenda zake. \s1 Chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo \r (Marko 8:14-21) \p \v 5 Wanafunzi wake walipofika ng’ambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. \v 6 Isa akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.” \p \v 7 Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.” \p \v 8 Isa, akifahamu majadiliano yao, akauliza, “Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? \v 9 Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na idadi ya vikapu vilivyojaa mabaki mlivyokusanya? \v 10 Au ile mikate saba kwa watu elfu nne na idadi ya vikapu vilivyojaa mabaki mlivyokusanya? \v 11 Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” \v 12 Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi kuhusu chachu ya kutengeneza mikate, bali kuhusu mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. \s1 Petro amkiri Isa kuwa Al-Masihi \r (Marko 8:27-30; Luka 9:18-21) \p \v 13 Basi Isa alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?” \p \v 14 Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yahya; wengine husema ni Ilya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmoja wa manabii.” \p \v 15 Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” \p \v 16 Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 16:16 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, Mwana wa Mungu aliye hai.” \p \v 17 Naye Isa akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona\f + \fr 16:17 \fr*\ft neno la Kiaramu, maana yake \ft*\fqa Mwana wa Yona\fqa*\f*, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni. \v 18 Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitajenga jumuiya ya wafuasi wangu, hata malango ya Kuzimu\f + \fr 16:18 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Hades\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa mahali pa wafu.\fqa*\f* hayataweza kuwashinda. \v 19 Nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.” \v 20 Kisha akawakataza wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Al-Masihi. \s1 Isa atabiri kifo chake \r (Marko 8:31–9:1; Luka 9:22-27) \p \v 21 Tangu wakati huo, Isa alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na kwamba itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa. \p \v 22 Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea, akisema, “Haiwezekani, Bwana! Jambo hili kamwe halitakupata!” \p \v 23 Lakini Isa akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” \p \v 24 Ndipo Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. \v 25 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata. \v 26 Kwa maana itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? \v 27 Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika wake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. \v 28 Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.” \c 17 \s1 Isa abadilika sura \r (Marko 9:2-13; Luka 9:28-36) \p \v 1 Siku sita baada ya jambo hili, Isa akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapeleka juu ya mlima mrefu peke yao. \v 2 Wakiwa huko, Isa alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama nuru. \v 3 Ghafula wakawatokea mbele yao Musa na Ilya, wakizungumza na Isa. \p \v 4 Ndipo Petro akamwambia Isa, “Bwana, ni vyema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya.” \p \v 5 Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililong’aa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.” \p \v 6 Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka kifudifudi, wakajawa na hofu. \v 7 Lakini Isa akaja na kuwagusa, akawaambia, “Inukeni na wala msiogope.” \v 8 Walipoinua macho yao, hawakumwona mtu mwingine yeyote isipokuwa Isa. \p \v 9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawaagiza, “Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.” \p \v 10 Wale wanafunzi wakamuuliza, “Kwa nini basi walimu wa Torati husema kwamba ni lazima Ilya aje kwanza?” \p \v 11 Isa akawajibu, “Ni kweli, Ilya lazima aje kwanza, naye atatengeneza mambo yote. \v 12 Lakini nawaambia, Ilya amekwisha kuja, nao hawakumtambua, bali walimtendea kila kitu walichotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu pia atateswa mikononi mwao.” \v 13 Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza nao habari za Yahya. \s1 Isa amponya kijana mwenye pepo mchafu \r (Marko 9:14-29; Luka 9:37-45) \p \v 14 Walipofika penye umati wa watu, mtu mmoja akamjia Isa na kupiga magoti mbele yake, akasema, \v 15 “Bwana\f + \fr 17:15 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, mhurumie mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara kwa mara huanguka kwenye moto au kwenye maji. \v 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.” \p \v 17 Isa akajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi hadi lini? Nitawavumilia hadi lini? Mleteni mvulana hapa kwangu.” \v 18 Isa akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu saa hiyo. \p \v 19 Kisha wanafunzi wakamwendea Isa wakiwa peke yao, wakamuuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa?” \p \v 20 Akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Ninawaambia kweli, mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale,’ nao utaondoka. Wala hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwenu. [ \v 21 Lakini hali kama hii haitoki ila kwa kuomba na kufunga.]\f + \fr 17:21 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*” \s1 Isa atabiri kifo chake mara ya pili \p \v 22 Siku moja walipokuwa pamoja huko Galilaya, Isa akawaambia, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu. \v 23 Nao watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa.” Wanafunzi wakahuzunika sana. \s1 Isa na Petro watoa kodi ya Hekalu \p \v 24 Baada ya Isa na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu\f + \fr 17:24 \fr*\ft Kodi hii ilikuwa drakma mbili kwa kila mwanaume; drakma moja ilikuwa na thamani sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja.\ft*\f* wakamjia Petro na kumuuliza, “Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?” \p \v 25 Petro akajibu, “Ndiyo, yeye hulipa.” Petro aliporudi nyumbani, Isa akawa wa kwanza kulizungumzia, akamuuliza, “Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?” \p \v 26 Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” \p Isa akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa. \v 27 Lakini ili tusije tukawaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemvua. Fungua kinywa chake nawe utakuta humo fedha, ichukue ukalipe kodi yako na yangu.” \c 18 \s1 Aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni \r (Marko 9:33-37; Luka 9:46-48; 22:24-30) \p \v 1 Wakati huo, wanafunzi wakamjia Isa na kumuuliza, “Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika ufalme wa mbinguni?” \p \v 2 Isa akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. \v 3 Naye akasema: “Amin, nawaambia, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika ufalme wa mbinguni. \v 4 Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika ufalme wa mbinguni. \p \v 5 “Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi. \p \v 6 “Lakini kama mtu yeyote akimsababisha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari. \s1 Kujaribiwa ili kutenda dhambi \r (Marko 9:42-48; Luka 17:1-2) \p \v 7 “Ole kwa ulimwengu kwa sababu ya mambo yanayosababisha watu kutenda dhambi! Mambo hayo lazima yawepo, lakini ole wake mtu yule ambaye huyasababisha. \v 8 Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. \v 9 Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa Jehanamu. \s1 Mfano wa kondoo aliyepotea \r (Luka 15:1-7) \p \v 10 “Chungeni ili msimdharau mmoja wa hawa wadogo. Kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba\f + \fr 18:10 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu aliye mbinguni. [ \v 11 Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichopotea.]\f + \fr 18:11 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \p \v 12 “Mwaonaje? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je, hatawaacha wale tisini na tisa vilimani na kwenda kumtafuta huyo mmoja aliyepotea? \v 13 Naye akishampata, amin, nawaambia, hufurahi zaidi kwa ajili ya huyo kondoo mmoja kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. \v 14 Vivyo hivyo, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmoja wa hawa wadogo apotee. \s1 Ndugu yako akikukosea \p \v 15 “Ndugu yako akikukosea, nenda ukamwoneshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. \v 16 Lakini asipokusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno ‘lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu’. \v 17 Akikataa kuwasikiliza hao, waambieni kundi lenu la waumini. Naye akikataa hata kuwasikiliza kundi la waumini, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru. \p \v 18 “Amin, nawaambia, lolote mtakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote mtakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni. \p \v 19 “Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watatendewa na Baba yangu aliye mbinguni. \v 20 Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.” \s1 Kusamehe mara ngapi? \p \v 21 Kisha Petro akamwendea Isa na kumuuliza, “Bwana, ni mara ngapi nimsamehe ndugu yangu akinikosea? Hadi mara saba?” \p \v 22 Isa akamjibu, “Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. \s1 Mfano wa mtumishi asiyesamehe \p \v 23 “Kwa hiyo ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kufanya hesabu zake za fedha na watumishi wake. \v 24 Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta\f + \fr 18:24 \fr*\ft Talanta moja ni sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15.\ft*\f* elfu kumi aliletwa kwake. \v 25 Kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake akaamuru kwamba auzwe, yeye, mkewe, watoto wake na vyote alivyokuwa navyo, ili lile deni lipate kulipwa. \p \v 26 “Yule mtumishi akampigia magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ \v 27 Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake. \p \v 28 “Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari\f + \fr 18:28 \fr*\ft Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja.\ft*\f* mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’ \p \v 29 “Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ \p \v 30 “Lakini akakataa. Badala yake, alienda akamtupa gerezani hata atakapolipa hilo deni. \v 31 Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia. \p \v 32 “Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. \v 33 Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’ \v 34 Kwa hasira, yule bwana wake akamtia yule mtumishi mikononi mwa askari wa gereza ili ateswe hadi atakapolipa yote aliyokuwa anadaiwa. \p \v 35 “Hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ikiwa hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwake.” \c 19 \ms1 Safari ya kwenda Yerusalemu, na maonyo ya mwisho \mr (Mathayo 19–23) \s1 Isa afundisha kuhusu talaka \r (Marko 10:1-12) \p \v 1 Isa alipomaliza kusema maneno haya, aliondoka Galilaya, akaenda sehemu za Yudea, ng’ambo ya Yordani. \v 2 Umati mkubwa wa watu wakamfuata, naye akawaponya huko. \p \v 3 Baadhi ya Mafarisayo\f + \fr 19:3 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakamjia ili kumjaribu, wakamuuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?” \p \v 4 Akawajibu, “Je, hamkusoma kwamba hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, \v 5 naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? \v 6 Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” \p \v 7 Wakamuuliza, “Kwa nini basi Musa aliagiza mtu kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?” \p \v 8 Isa akawajibu, “Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. \v 9 Mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa sababu ya uasherati naye akaoa mke mwingine, anazini. Naye amwoaye yule mwanamke aliyeachwa pia anazini.” \p \v 10 Wanafunzi wake wakamwambia, “Kama hali ndiyo hii kati ya mume na mke, ni afadhali mtu asioe!” \p \v 11 Isa akawaambia, “Si watu wote wanaoweza kupokea neno hili, isipokuwa wale tu waliojaliwa na Mungu. \v 12 Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo; wengine wamefanywa matowashi na wanadamu; na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.” \s1 Isa awabariki watoto wadogo \r (Marko 10:13-16; Luka 18:15-17) \p \v 13 Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Isa ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta. \p \v 14 Isa akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa wale walio kama hawa.” \v 15 Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko. \s1 Kijana tajiri \r (Marko 10:17-31; Luka 18:18-30) \p \v 16 Mtu mmoja akamjia Isa na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?” \p \v 17 Isa akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.” \p \v 18 Yule mtu akamuuliza, “Amri zipi?” \p Isa akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, \v 19 waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.” \p \v 20 Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?” \p \v 21 Isa akamwambia, “Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” \p \v 22 Yule kijana aliposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi. \p \v 23 Ndipo Isa akawaambia wanafunzi wake, “Amin, nawaambia, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. \v 24 Tena nawaambia, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” \p \v 25 Wanafunzi wake waliposikia haya, walishangaa sana na kuuliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?” \p \v 26 Lakini Isa akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” \p \v 27 Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata! Tutapata nini basi?” \p \v 28 Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti kumi na viwili vya utawala, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. \v 29 Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele. \v 30 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza. \c 20 \s1 Mfano wa wafanyakazi katika shamba la mizabibu \p \v 1 “Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mtu mwenye shamba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri vibarua kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu. \v 2 Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari\f + \fr 20:2 \fr*\ft Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja.\ft*\f* moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu. \p \v 3 “Mnamo saa tatu akatoka tena, akawakuta wengine wamesimama sokoni bila kazi. \v 4 Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’ \v 5 Hivyo basi wakaenda. \p “Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. \v 6 Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’ \p \v 7 “Wakamjibu, ‘Ni kwa sababu hakuna yeyote aliyetuajiri.’ \p “Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu.’ \p \v 8 “Ilipofika jioni, yule mwenye shamba la mizabibu akamwambia msimamizi, ‘Waite hao vibarua na uwalipe ujira wao, ukianzia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’ \p \v 9 “Wale vibarua walioajiriwa saa kumi na moja wakaja, na kila mmoja wao akapokea dinari moja. \v 10 Hivyo wale walioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipokea dinari moja. \v 11 Walipoipokea, wakaanza kulalamika dhidi ya yule mwenye shamba, \v 12 wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’ \p \v 13 “Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sijakudhulumu. Je, hukukubaliana nami kwa ujira wa kawaida wa dinari moja? \v 14 Chukua ujira wako na uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu aliyeajiriwa mwisho kama nilivyokupa wewe. \v 15 Je, sina haki ya kufanya kile nitakacho na mali yangu mwenyewe? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’ \p \v 16 “Vivyo hivyo, wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.” \s1 Isa atabiri tena kifo chake \r (Marko 10:32-34; Luka 18:31-34) \p \v 17 Basi Isa alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, aliwaita kando wale wanafunzi kumi na wawili na kuwaambia, \v 18 “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa viongozi wa makuhani na walimu wa Torati. Nao watamhukumu kifo \v 19 na kumtia mikononi mwa watu wa Mataifa ili wamdhihaki na kumpiga mijeledi na kumsulubisha msalabani. Naye atafufuliwa siku ya tatu!” \s1 Ombi la mama yao Yakobo na Yohana \r (Marko 10:35-45) \p \v 20 Kisha mama yao wana wa Zebedayo akamjia Isa pamoja na wanawe, naye akapiga magoti mbele yake, akamwomba Isa amfanyie jambo fulani. \p \v 21 Isa akamuuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika ufalme wako.” \p \v 22 Isa akawaambia, “Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe nitakachonywea mimi?” \p Wakajibu, “Tunaweza.” \p \v 23 Isa akawaambia, “Kwa kweli kikombe changu mtakinywea, lakini kuketi upande wangu wa kuume au wa kushoto si langu mimi kuwapa. Nafasi hizo ni za wale ambao wameandaliwa na Baba\f + \fr 20:23 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu.” \p \v 24 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, waliwakasirikia hao ndugu wawili. \v 25 Lakini Isa akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, nao wenye vyeo huonesha mamlaka yao. \v 26 Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, \v 27 naye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu: \v 28 kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.” \s1 Isa awaponya vipofu wawili \r (Marko 10:46-52; Luka 18:35-43) \p \v 29 Isa na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu wakamfuata. \v 30 Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Isa alikuwa anapita, wakapaza sauti wakisema, “Bwana Isa, Mwana wa Daudi\f + \fr 20:30 \fr*\ft Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*, tuhurumie!” \p \v 31 Umati wa watu wakawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti wakisema, “Bwana Isa, Mwana wa Daudi, tuhurumie.” \p \v 32 Isa akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” \p \v 33 Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.” \p \v 34 Isa akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata. \c 21 \s1 Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe \r (Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19) \p \v 1 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Isa akawatuma wanafunzi wake wawili, \v 2 akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu, nanyi mtampata punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. \v 3 Mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara moja.” \p \v 4 Haya yalitukia ili litimie neno lililonenwa na nabii, aliposema: \q1 \v 5 “Mwambieni Binti Sayuni, \q2 ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, \q1 ni mpole, naye amepanda punda, \q2 juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ” \p \v 6 Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Isa alivyokuwa amewaagiza. \v 7 Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Isa akaketi juu yake. \v 8 Umati mkubwa wa watu wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kwenye miti, wakayatandaza barabarani. \v 9 Wale umati wa watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaza sauti na kusema, \q1 “Hosana\f + \fr 21:9 \fr*\ft Kiebrania kusema \ft*\fqa Okoa\fqa*\ft ; basi likawa neno la shangwe.\ft*\f*, Mwana wa Daudi!” \b \q1 “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” \b \q1 “Hosana juu mbinguni!” \p \v 10 Isa alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” \p \v 11 Wale umati wa watu wakajibu, “Huyu ni Isa, yule nabii kutoka Nasiri ya Galilaya.” \s1 Isa atakasa Hekalu \r (Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22) \p \v 12 Isa akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. \v 13 Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.” \p \v 14 Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. \v 15 Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walipoona mambo ya ajabu aliyofanya, na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu, wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika. \p \v 16 Wakamuuliza Isa, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” \p Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, \q1 “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya \q2 umeamuru sifa’?” \p \v 17 Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko. \s1 Mtini ulionyauka \r (Marko 11:12-14, 20-24) \p \v 18 Asubuhi na mapema, Isa alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. \v 19 Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka. \p \v 20 Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?” \p \v 21 Isa akawajibu, “Amin, nawaambia, mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ng’oka, ukatupwe baharini,’ litafanyika. \v 22 Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.” \s1 Swali kuhusu mamlaka ya Isa \r (Marko 11:27-33; Luka 20:1-8) \p \v 23 Isa alipoingia Hekaluni, viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakamjia alipokuwa anafundisha, wakamuuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?” \p \v 24 Isa akawajibu, “Nami nitawauliza swali moja. Mkinijibu, nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. \v 25 Je, ubatizo wa Yahya ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” \p Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ \v 26 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yahya kuwa ni nabii.” \p \v 27 Hivyo basi wakamjibu Isa, “Sisi hatujui.” \p Naye akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya. \s1 Mfano wa wana wawili \p \v 28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ \p \v 29 “Yule mwanawe akamjibu ‘Mimi sitaenda.’ Baadaye akabadili mawazo yake akaenda. \p \v 30 “Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine, akamwambia vilevile. Yeye akajibu, ‘Nitaenda, bwana,’ lakini hakuenda. \p \v 31 “Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?” \p Wakamjibu, “Ni yule wa kwanza.” \p Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika ufalme wa Mungu. \v 32 Kwa maana Yahya alikuja kwenu kuwaonesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki. \s1 Mfano wa wapangaji waovu \r (Marko 12:1-12; Luka 20:9-19) \p \v 33 “Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo la kukamulia zabibu ndani yake, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri hadi nchi nyingine. \v 34 Wakati wa mavuno ulipokaribia, akawatuma watumishi wake kwa hao wapangaji ili kukusanya matunda yake. \p \v 35 “Wale wapangaji wakawakamata wale watumishi, wakampiga mmoja, wakamuua mwingine, na yule wa tatu wakampiga mawe. \v 36 Kisha akawatuma watumishi wengine kwao, wengi kuliko wale wa kwanza, nao wale wapangaji wakawatendea vilevile. \v 37 Mwisho wa yote, akamtuma mwanawe kwao, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’ \p \v 38 “Lakini wale wapangaji walipomwona mwanawe, wakasemezana wao kwa wao, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, ili tuchukue urithi wake.’ \v 39 Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua. \p \v 40 “Basi huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyia nini hao wakulima?” \p \v 41 Wakamjibu, “Kwa hasira kuu, atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.” \p \v 42 Isa akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba: \q1 “ ‘Jiwe walilolikataa waashi \q2 limekuwa jiwe kuu la pembeni. \q1 Mwenyezi Mungu ndiye alitenda jambo hili, \q2 nalo ni la kushangaza machoni petu’? \p \v 43 “Kwa hiyo ninawaambia, ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake. \v 44 Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.” \p \v 45 Viongozi wa makuhani na Mafarisayo\f + \fr 21:45 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* waliposikia mifano ya Isa, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. \v 46 Wakatafuta njia ya kumkamata, lakini wakaogopa umati wa watu, kwa kuwa watu walimwona Isa kuwa ni nabii. \c 22 \s1 Mfano wa karamu ya arusi \r (Luka 14:15-24) \p \v 1 Isa akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, \v 2 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. \v 3 Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja. \p \v 4 “Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’ \p \v 5 “Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. \v 6 Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua. \v 7 Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto. \p \v 8 “Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. \v 9 Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ \v 10 Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni. \p \v 11 “Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi. \v 12 Mfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. \p \v 13 “Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ \p \v 14 “Kwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.” \s1 Swali kuhusu kulipa kodi ya Kaisari \r (Marko 12:13-17; Luka 20:20-26) \p \v 15 Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Isa katika maneno yake. \v 16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode\f + \fr 22:16 \fr*\ft Wafuasi wa Mfalme Herode waliokubaliana na utawala wa Rumi.\ft*\f* kwake. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonesha upendeleo. \v 17 Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?” \p \v 18 Lakini Isa alifahamu kusudi lao mbaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? \v 19 Nionesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari. \v 20 Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?” \p \v 21 Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” \p Basi Isa akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.” \p \v 22 Waliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao. \s1 Ndoa wakati wa ufufuo \r (Marko 12:18-27; Luka 20:27-40) \p \v 23 Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza swali, wakisema, \v 24 “Mwalimu, Musa alisema, ‘Mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’ \v 25 Basi palikuwa na ndugu saba miongoni mwetu. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa, na kwa kuwa hakuwa na watoto, akamwachia nduguye yule mjane. \v 26 Ikatokea vivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili, na wa tatu, hadi wote saba. \v 27 Hatimaye, yule mwanamke naye akafa. \v 28 Sasa basi, siku ya ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba, kwa kuwa wote walikuwa wamemwoa huyo mwanamke?” \p \v 29 Isa akawajibu, “Mwapotoka kwa sababu hamjui Maandiko wala uweza wa Mungu. \v 30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. \v 31 Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma kile Mungu alichowaambia, kwamba, \v 32 ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.” \p \v 33 Wale umati wa watu waliposikia hayo, walishangaa sana kwa mafundisho yake. \s1 Amri kuu kuliko zote \r (Marko 12:28-34; Luka 10:25-28) \p \v 34 Mafarisayo waliposikia kwamba Isa alikuwa amewanyamazisha Masadukayo\f + \fr 22:34 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; waliamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho.\ft*\f*, Mafarisayo wakakusanyika pamoja. \v 35 Mmoja wao, mtaalamu wa Torati, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema, \v 36 “Mwalimu, ni amri ipi katika Torati iliyo kuu kuliko zote?” \p \v 37 Isa akamjibu, “ ‘Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ \v 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. \v 39 Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ \v 40 Amri hizi mbili ndizo msingi wa Torati na Manabii.” \s1 Al-Masihi ni Mwana wa nani? \r (Marko 12:35-37; Luka 20:41-44) \p \v 41 Mafarisayo wakiwa wamekusanyika pamoja, Isa akawauliza, \v 42 “Mnaonaje kuhusu Al-Masihi\f + \fr 22:42 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*? Yeye ni mwana wa nani?” \p Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.” \p \v 43 Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, anamwita Al-Masihi ‘Bwana’? Kwa maana asema, \q1 \v 44 “ ‘Mwenyezi Mungu alimwambia Bwana wangu: \q2 “Keti mkono wangu wa kuume, \q1 hadi nitakapowaweka adui zako \q2 chini ya miguu yako.” ’ \m \v 45 Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?” \v 46 Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Isa neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali. \c 23 \s1 Isa atahadharisha kuhusu walimu wa Torati \r (Marko 12:38-40; Luka 11:39-52; 20:45-47) \p \v 1 Kisha Isa akaambia wale umati wa watu na wanafunzi wake: \v 2 “Walimu wa Torati na Mafarisayo wameketi kwenye kiti cha Musa, \v 3 hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. \v 4 Wao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza. \p \v 5 “Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao. \v 6 Wanapenda kukalia viti vya heshima katika karamu, na vile viti maalum sana katika masinagogi\f + \fr 23:6 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f*. \v 7 Hupenda kusalimiwa masokoni na kutaka watu wawaite ‘Mwalimu.’ \p \v 8 “Lakini ninyi msiitwe ‘Mwalimu,’ kwa sababu mnaye Bwana mmoja na ninyi nyote ni ndugu. \v 9 Nanyi msimwite mtu yeyote ‘Baba,’ hapa duniani, kwa maana mnaye Baba\f + \fr 23:9 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* mmoja, naye yuko mbinguni. \v 10 Wala msiitwe ‘Mwalimu,’ kwa maana mnaye mwalimu mmoja tu, ndiye Al-Masihi\f + \fr 23:10 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*. \v 11 Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu. \v 12 Kwa kuwa yeyote anayejikweza atashushwa, na yeyote anayejinyenyekeza atakwezwa. \s1 Ole saba kwa walimu wa Torati na Mafarisayo \p \v 13 “Lakini ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Kwa maana mnawafungia watu milango ya ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, nao wale wanaotaka kuingia mnawazuia. [ \v 14 Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Mnakula katika nyumba za wajane, nanyi kwa kujifanya kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo hukumu yenu itakuwa kuu zaidi.]\f + \fr 23:14 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \p \v 15 “Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, enyi wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja mwongofu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa Jehanamu mara mbili kuliko ninyi! \p \v 16 “Ole wenu, viongozi vipofu! Ninyi mwasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, amefungwa kwa kiapo chake.’ \v 17 Ninyi vipofu wapumbavu! Ni kipi kilicho kikuu zaidi: ni ile dhahabu, au ni lile Hekalu linaloifanya hiyo dhahabu kuwa takatifu? \v 18 Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu; lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu, amefungwa kwa kiapo chake’ \v 19 Ninyi vipofu! Ni kipi kikuu zaidi: ni sadaka, au ni madhabahu yanayoifanya hiyo sadaka kuwa takatifu? \v 20 Basi, mtu anayeapa kwa madhabahu, anaapa kwa hayo madhabahu na vitu vyote vilivyo juu yake. \v 21 Naye mtu anayeapa kwa Hekalu, anaapa kwa hilo Hekalu na kwa huyo akaaye ndani yake. \v 22 Naye anayeapa kwa mbingu, anaapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye anayeketi kwenye kiti hicho. \p \v 23 “Ole wenu walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnatoa zaka ya mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu zaidi ya sheria, yaani haki, huruma na uaminifu. Iliwapasa kufanya haya makuu ya sheria bila kupuuza hayo matoleo. \v 24 Ninyi viongozi vipofu, mnachuja kiroboto lakini mnameza ngamia! \p \v 25 “Ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi. \v 26 Ewe Farisayo kipofu! Safisha ndani ya kikombe na sahani kwanza, ndipo nje itakuwa safi pia. \p \v 27 “Ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo yanapendeza kwa nje, lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. \v 28 Vivyo hivyo, kwa nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu. \p \v 29 “Ole wenu, walimu wa Torati na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki. \v 30 Nanyi mwasema, ‘Kama tungeishi wakati wa baba zetu, hatungeshiriki katika kumwaga damu ya manabii!’ \v 31 Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. \v 32 Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu! \p \v 33 “Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya Jehanamu? \v 34 Kwa sababu hii, tazameni, natuma kwenu manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na kuwafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine. \v 35 Hivyo ile damu ya wenye haki wote iliyomwagwa hapa duniani, tangu damu ya Habili, aliyekuwa mwenye haki, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemuua kati ya patakatifu na madhabahu, itawajia juu yenu. \v 36 Amin, nawaambia, haya yote yatakuja kwa kizazi hiki. \s1 Isa aomboleza kwa ajili ya Yerusalemu \r (Luka 13:34-35) \p \v 37 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka! \v 38 Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. \v 39 Kwa maana nawaambia, hamtaniona tena tangu sasa hadi mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu.’ ” \c 24 \ms1 Unabii kuhusu mambo yajayo \mr (Mathayo 24–25) \s1 Kubomolewa kwa Hekalu kwatabiriwa \r (Marko 13:1-2; Luka 21:5-6) \p \v 1 Isa akatoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonesha majengo ya Hekalu. \v 2 Ndipo Isa akawauliza, “Je, mnayaona haya yote? Amin, nawaambia, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.” \s1 Ishara za nyakati za mwisho \r (Marko 13:3-23; Luka 21:7-24) \p \v 3 Isa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?” \p \v 4 Isa akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. \v 5 Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Al-Masihi\f + \fr 24:5 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*,’ nao watawadanganya wengi. \v 6 Mtasikia habari za vita na tetesi za vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. \v 7 Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. \v 8 Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa uchungu. \p \v 9 “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. \v 10 Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. \v 11 Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. \v 12 Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu, upendo wa watu wengi utapoa, \v 13 lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. \v 14 Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja. \s1 Chukizo la uharibifu \r (Marko 13:14-23; Luka 21:20-24) \p \v 15 “Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu), \v 16 basi wale walio Yudea wakimbilie milimani. \v 17 Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke ili kuchukua chochote kutoka ndani ya nyumba. \v 18 Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. \v 19 Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! \v 20 Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi au siku ya Sabato. \v 21 Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwepo tangu mwanzo wa dunia hadi sasa: wala haitakuwepo tena kamwe. \p \v 22 “Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna mtu ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupishwa. \v 23 Wakati huo mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Al-Masihi huyu hapa!’ au, ‘Al-Masihi yuko kule,’ msisadiki. \v 24 Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa. \v 25 Tazameni, nimekwisha kuwaambia mapema. \p \v 26 “Basi mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. \v 27 Kwa maana kama vile radi itokavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. \v 28 Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai. \s1 Kuja kwa Mwana wa Adamu \r (Marko 13:24-31; Luka 21:25-33) \p \v 29 “Mara baada ya dhiki ya siku zile, \q1 “ ‘jua litatiwa giza, \q2 nao mwezi hautatoa nuru yake; \q1 nazo nyota zitaanguka kutoka angani, \q2 na nguvu za anga zitatikisika.’ \p \v 30 “Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. \v 31 Naye atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine. \s1 Somo kuhusu mtini \r (Marko 13:28-31; Luka 21:29-33) \p \v 32 “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. \v 33 Vivyo hivyo, mnapoyaona mambo haya yote, mtambue kwamba wakati u karibu, hata malangoni. \v 34 Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. \v 35 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. \s1 Hakuna ajuaye siku wala saa \r (Marko 13:32-37; Luka 17:26-30, 34-36) \p \v 36 “Kwa habari ya siku ile na saa, hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba\f + \fr 24:36 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* peke yake. \v 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. \v 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hadi siku ile Nuhu alipoingia katika safina. \v 39 Nao hawakujua lolote hadi gharika ilipokuja ikawakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa atakapokuja Mwana wa Adamu. \v 40 Watu wawili watakuwa shambani, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. \v 41 Wanawake wawili watakuwa wanasaga kwa kinu cha mkono, naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. \p \v 42 “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. \v 43 Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa. \v 44 Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia. \s1 Mfano wa mtumishi mwaminifu \r (Luka 12:41-48) \p \v 45 “Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? \v 46 Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. \v 47 Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. \v 48 Lakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’ \v 49 kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi. \v 50 Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. \v 51 Atamkata vipande vipande na kumweka pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno. \c 25 \s1 Mfano wa wanawali kumi \r (Luka 12:35-40) \p \v 1 “Wakati huo, ufalme wa mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. \v 2 Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. \v 3 Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, \v 4 lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. \v 5 Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala. \p \v 6 “Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’ \p \v 7 “Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. \v 8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’ \p \v 9 “Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’ \p \v 10 “Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa. \p \v 11 “Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’ \p \v 12 “Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’ \p \v 13 “Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa. \s1 Mfano wa watumishi watatu na talanta \r (Luka 19:11-27) \p \v 14 “Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu aliyetaka kusafiri, naye akawaita watumishi wake na kuweka mali yake kwenye uangalizi wao. \v 15 Mmoja akampa talanta\f + \fr 25:15 \fr*\ft Talanta moja ilikuwa sawa na mshahara wa kibarua wa miaka 15.\ft*\f* tano, mwingine talanta mbili, na mwingine talanta moja. Kila mmoja alipewa kadiri ya uwezo wake. Kisha yeye akasafiri. \v 16 Yule aliyepewa talanta tano akaenda mara moja akafanya nazo biashara akapata talanta nyingine tano zaidi. \v 17 Yule aliyepewa talanta mbili akafanya vivyo hivyo, akapata nyingine mbili zaidi. \v 18 Lakini yule mtumishi aliyekuwa amepokea talanta moja, alienda akachimba shimo ardhini na kuificha ile talanta ya bwana wake. \p \v 19 “Baada ya muda mrefu, yule bwana wa wale watumishi akarudi na kufanya hesabu nao. \v 20 Yule mtumishi aliyepokea talanta tano akaja, akaleta nyingine tano zaidi. Akasema, ‘Bwana uliweka kwenye uangalizi wangu talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta tano zaidi.’ \p \v 21 “Bwana wake akamwambia, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’ \p \v 22 “Yule mwenye talanta mbili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, uliweka kwenye uangalizi wangu talanta mbili. Tazama nimepata hapa talanta mbili zaidi.’ \p \v 23 “Bwana wake akajibu, ‘Umefanya vizuri sana, mtumishi mwema na mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache; nami nitakuweka kuwa msimamizi wa vitu vingi. Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako!’ \p \v 24 “Kisha yule mtumishi aliyepokea talanta moja akaja, akasema, ‘Bwana, nilijua kwamba wewe ni mtu mgumu, unayevuna mahali usipopanda na kukusanya mahali usipotawanya mbegu. \v 25 Kwa hiyo niliogopa, nikaenda, nikaificha talanta yako ardhini. Tazama, hii hapa ile iliyo mali yako.’ \p \v 26 “Bwana wake akajibu, ‘Wewe mtumishi mwovu na mvivu! Ulijua kwamba ninavuna mahali nisipopanda na kukusanya mahali nisipotawanya mbegu. \v 27 Vyema basi, ingekupasa kuweka fedha yangu kwa watoa riba, ili nirudipo, nichukue ile iliyo yangu na faida yake. \p \v 28 “ ‘Basi mnyang’anyeni hiyo talanta, mkampe yule mwenye talanta kumi. \v 29 Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. \v 30 Nanyi mtupeni huyo mtumishi asiyefaa nje, kwenye giza, mahali ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ \s1 Kondoo na mbuzi \p \v 31 “Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi kwenye kiti cha enzi cha utukufu wake. \v 32 Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi. \v 33 Atawaweka kondoo upande wake wa kuume, na mbuzi upande wake wa kushoto. \p \v 34 “Ndipo Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kuume, ‘Njooni, ninyi mliobarikiwa na Baba\f + \fr 25:34 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu; urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu. \v 35 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, \v 36 nilikuwa uchi mkanivisha nguo, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.’ \p \v 37 “Ndipo wale wenye haki watakapomjibu, ‘Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa tukakulisha, au ukiwa na kiu tukakunywesha? \v 38 Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha, au ukiwa uchi tukakuvisha nguo? \v 39 Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza, au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’ \p \v 40 “Naye Mfalme atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmoja wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.’ \p \v 41 “Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika wake. \v 42 Kwa maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu nanyi hamkuninywesha, \v 43 nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa uchi nanyi hamkunivisha nguo, nilikuwa mgonjwa nanyi hamkunitunza, na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.’ \p \v 44 “Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’ \p \v 45 “Naye atawajibu, ‘Amin nawaambia, kwa jinsi hamkumtendea mmoja wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.’ \p \v 46 “Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.” \c 26 \ms1 Kufa na kufufuka kwa Isa \mr (Mathayo 26–28) \s1 Njama ya kumuua Isa \r (Marko 14:1-2; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53) \p \v 1 Isa alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake, \v 2 “Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka\f + \fr 26:2 \fr*\ft Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.\ft*\f*, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.” \p \v 3 Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa. \v 4 Wakapanga kumkamata Isa kwa siri na kumuua. \v 5 Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.” \s1 Isa apakwa mafuta huko Bethania \r (Marko 14:3-9; Luka 7:35-38; Yohana 12:1-8) \p \v 6 Isa alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma. \v 7 Naye mwanamke mmoja akamjia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya thamani kubwa. Akayamimina kichwani mwa Isa alipokuwa ameketi mezani kula chakula. \p \v 8 Lakini wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, “Upotevu huu wote ni wa nini? \v 9 Manukato haya yangeuzwa kwa bei kubwa, na fedha hizo wakapewa maskini.” \p \v 10 Isa, akijua jambo hili, akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Yeye amenitendea jambo zuri sana. \v 11 Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. \v 12 Alipomiminia haya manukato kwenye mwili wangu, amefanya hivyo ili kuniandaa kwa ajili ya maziko yangu. \v 13 Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo hii Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.” \s1 Yuda akubali kumsaliti Isa \r (Marko 14:10-11; Luka 22:3-6) \p \v 14 Kisha mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alienda kwa viongozi wa makuhani \v 15 na kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Isa mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. \v 16 Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Isa. \s1 Isa ala Pasaka na wanafunzi wake \r (Marko 14:12-21; Luka 22:7-23; Yohana 13:21-30) \p \v 17 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimjia Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?” \p \v 18 Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini, mkamwambie, ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ” \v 19 Hivyo wanafunzi wakafanya vile Isa alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka. \p \v 20 Ilipofika jioni, Isa alikuwa ameketi mezani pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. \v 21 Nao walipokuwa wakila, Isa akasema, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” \p \v 22 Wakahuzunika sana, wakaanza kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?” \p \v 23 Isa akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami ndiye atakayenisaliti. \v 24 Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu. Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa!” \p \v 25 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, akasema, “Je, ni mimi Mwalimu?” \p Isa akajibu, “Naam, wewe mwenyewe umesema.” \s1 Kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana Isa \r (Marko 14:22-26; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25) \p \v 26 Walipokuwa wanakula, Isa akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu.” \p \v 27 Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, “Nyweni nyote katika kikombe hiki. \v 28 Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. \v 29 Lakini ninawaambia, tangu sasa sitakunywa tena katika uzao huu wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba\f + \fr 26:29 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu.” \p \v 30 Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni. \s1 Isa atabiri kuwa Petro atamkana \r (Marko 14:27-31; Luka 22:31-34; Yohana 13:31-38) \p \v 31 Kisha Isa akawaambia, “Usiku huu, ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: \q1 “ ‘Nitampiga mchungaji, \q2 nao kondoo wa hilo kundi watatawanyika.’ \m \v 32 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.” \p \v 33 Petro akajibu, “Hata kama wote watakuacha, kamwe mimi sitakuacha.” \p \v 34 Isa akamjibu, “Amin, nakuambia, usiku huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” \p \v 35 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wanafunzi wale wengine wote wakasema vivyo hivyo. \s1 Isa aomba katika Bustani ya Gethsemane \r (Marko 14:32-42; Luka 22:39-46) \p \v 36 Kisha Isa akaenda pamoja na wanafunzi wake hadi kwenye bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia, “Kaeni hapa, nami niende kule nikaombe.” \v 37 Akamchukua Petro pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kufadhaika. \v 38 Kisha Isa akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe pamoja nami.” \p \v 39 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniondokee. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe.” \p \v 40 Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamuuliza Petro, “Je, ninyi hamkuweza kukesha pamoja nami hata kwa saa moja? \v 41 Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.” \p \v 42 Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, basi mapenzi yako yafanyike.” \p \v 43 Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. \v 44 Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. \p \v 45 Kisha akarudi kwa wanafunzi wake, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Tazameni, saa imefika ambapo Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. \v 46 Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!” \s1 Isa akamatwa \r (Marko 14:43-50; Luka 22:47-53; Yohana 18:1-11) \p \v 47 Alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akafika. Alikuwa amefuatana na umati mkubwa wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. \v 48 Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.” \v 49 Mara Yuda akamjia Isa na kumsalimu, “Salamu, Mwalimu!” Akambusu. \p \v 50 Isa akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.” \p Kisha wale watu wakasogea mbele, wakamkamata Isa. \v 51 Ghafula mmoja wa wale waliokuwa na Isa alipoona hivyo, akaushika upanga wake, akauchomoa na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. \p \v 52 Ndipo Isa akamwambia, “Rudisha upanga wako alani mwake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. \v 53 Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? \v 54 Lakini je, yale Maandiko yanayotabiri kwamba ni lazima itendeke hivi yatatimiaje?” \p \v 55 Wakati huo, Isa akaambia wale umati wa watu, “Je, mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata? \v 56 Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia. \s1 Isa mbele ya Baraza la Wayahudi \r (Marko 14:53-65; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24) \p \v 57 Wale waliomkamata Isa wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa Torati pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika. \v 58 Lakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia. \p \v 59 Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi\f + \fr 26:59 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f* lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Isa ili wapate kumuua. \v 60 Lakini hawakupata jambo lolote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. \p Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo \v 61 na kusema, “Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’ ” \p \v 62 Kisha kuhani mkuu akasimama na kumwambia Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” \v 63 Lakini Isa akakaa kimya. \p Ndipo kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai. Tuambie kama wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 26:63 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, Mwana wa Mungu.” \p \v 64 Isa akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote: Siku za baadaye, mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.” \p \v 65 Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia alivyokufuru. \v 66 Uamuzi wenu ni gani?” \p Wakajibu, “Anastahili kufa.” \p \v 67 Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi \v 68 na kusema, “Tutabirie, wewe Al-Masihi! Ni nani aliyekupiga?” \s1 Petro amkana Isa \r (Marko 14:66-72; Luka 22:56-62; Yohana 18:15-18, 25-27) \p \v 69 Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mjakazi mmoja akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Isa wa Galilaya.” \p \v 70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.” \p \v 71 Alipotoka nje kufika kwenye lango, mjakazi mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Isa Al-Nasiri.” \p \v 72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Mimi simjui huyo!” \p \v 73 Baada ya muda mfupi, wale waliokuwa wamesimama pale wakamwendea Petro, wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana usemi wako ni kama wao.” \p \v 74 Ndipo Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui mtu huyo!” \p Papo hapo jogoo akawika. \v 75 Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alilokuwa amesema: “Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi. \c 27 \s1 Isa apelekwa kwa Pilato \r (Marko 15:1; Luka 23:1; Yohana 18:28) \p \v 1 Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Isa ili kumuua. \v 2 Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato, aliyekuwa mtawala Mrumi. \s1 Yuda ajinyonga \r (Matendo 1:18-19) \p \v 3 Yuda, aliyemsaliti Isa, alipoona kuwa Isa amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. \v 4 Akasema, “Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.” \p Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.” \p \v 5 Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga. \p \v 6 Wale viongozi wa makuhani wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” \v 7 Hivyo basi, baada ya kushauriana, waliamua kuzitumia kununulia shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. \v 8 Hii ndiyo sababu lile shamba likaitwa Shamba la Damu hadi leo. \v 9 Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyowekewa na watu wa Israeli, \v 10 wakanunulia shamba la mfinyanzi, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoniagiza.” \s1 Pilato amhoji Isa \r (Marko 15:1-15; Luka 23:3-25; Yohana 18:28–19:16) \p \v 11 Wakati huo Isa akiwa amesimama mbele ya mtawala, mtawala akamuuliza, “Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?” \p Isa akasema, “Wewe wasema hivyo.” \p \v 12 Lakini viongozi wa makuhani na wazee walipomshtaki, hakujibu neno. \v 13 Ndipo Pilato akamuuliza, “Je, husikii ni mambo mangapi wanayokushtaki nayo?” \v 14 Lakini Isa hakumjibu hata kwa shtaka moja, kiasi kwamba mtawala alishangaa sana. \s1 Pilato amtoa Isa asulubiwe \r (Marko 15:6-15; Luka 23:13-25; Yohana 18:39–19:16) \p \v 15 Basi ilikuwa ni desturi ya mtawala kumfungua mfungwa mmoja aliyechaguliwa na umati wa watu wakati wa sikukuu. \v 16 Palikuwa na mfungwa mmoja mwenye sifa mbaya, aliyeitwa Baraba. \v 17 Hivyo umati wa watu walipokusanyika, Pilato akawauliza hao watu, “Mnataka niwafungulie yupi: Baraba au Isa aitwaye Al-Masihi?” \v 18 Kwa kuwa alitambua kwamba walikuwa wamemkabidhi Isa kwake kwa ajili ya wivu. \p \v 19 Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: “Usiwe na jambo lolote juu ya mtu huyu asiye na hatia, kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.” \p \v 20 Lakini viongozi wa makuhani na wazee wakashawishi umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe, naye Isa auawe. \p \v 21 Mtawala akawauliza tena, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?” \p Wakajibu, “Baraba.” \p \v 22 Pilato akawaambia, “Basi nifanye nini na huyu Isa aitwaye Al-Masihi?” \p Wakajibu wote, “Msulubishe!” \p \v 23 Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” \p Lakini wao wakazidi kupiga kelele, wakisema, “Msulubishe!” \p \v 24 Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lolote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya umati wa watu, akasema, “Sina hatia kwa damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!” \p \v 25 Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!” \p \v 26 Basi akawafungulia Baraba. Lakini baada ya kuamuru Isa apigwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe. \s1 Askari wamdhihaki Isa \r (Marko 15:16-20; Yohana 19:2-3) \p \v 27 Kisha askari wa mtawala wakampeleka Isa kwenye Praitorio\f + \fr 27:27 \fr*\ft Praitorio ilikuwa makao makuu ya mtawala wa jimbo. Hapa ni jumba la kifalme ambapo Pontio Pilato aliishi huko Yerusalemu, palipokuwa na kiti cha hukumu.\ft*\f*, na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. \v 28 Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha \v 29 wakasokota taji la miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” \v 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena. \v 31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili wakamsulubishe. \s1 Isa asulubishwa \r (Marko 15:21-32; Luka 23:26-43; Yohana 19:17-27) \p \v 32 Walipokuwa wakienda, wakakutana na mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. \v 33 Wakafika mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). \v 34 Hapo wakampa Isa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini alipoionja, akakataa kuinywa. \v 35 Walipokwisha kumsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”]\f + \fr 27:35 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \v 36 Kisha wakaketi, wakamchunga. \v 37 Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake hivi: \pc \sc Huyu ni Isa\sc* \pc \sc Mfalme wa Wayahudi.\sc* \p \v 38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. \v 39 Watu waliokuwa wakipita njiani wakamtukana huku wakitikisa vichwa vyao, \v 40 na kusema, “Wewe ambaye utalivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe mwenyewe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu\f + \fr 27:40 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*, shuka msalabani.” \p \v 41 Vivyo hivyo, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati pamoja na wazee wakamdhihaki, wakisema, \v 42 “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe! Yeye ni mfalme wa Israeli! Ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. \v 43 Anamwamini Mungu, basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka, kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” \v 44 Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana vivyo hivyo. \s1 Kifo cha Isa \r (Marko 15:33-41; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30) \p \v 45 Tangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote. \v 46 Ilipofika saa tisa, Isa akapaza sauti akalia, \tl “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”\tl* (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”) \p \v 47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale waliposikia hayo, wakasema, “Anamwita Ilya.” \p \v 48 Ghafula mmoja wao akaenda mbio na kuleta sifongo, akaichovya kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe. \v 49 Wengine wakasema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumwokoa.” \p \v 50 Isa alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake. \p \v 51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. \v 52 Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa. \v 53 Wakatoka makaburini, na baada ya Isa kufufuka, waliingia kwenye Mji Mtakatifu na kuwatokea watu wengi. \p \v 54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa sana, wakapaza sauti na kusema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!” \p \v 55 Wanawake wengi walikuwa pale wakitazama kwa mbali. Hawa walikuwa wamemfuata Isa tangu Galilaya ili kushughulikia mahitaji yake. \v 56 Miongoni mwao walikuwemo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo. \s1 Maziko ya Isa \r (Marko 15:42-47; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42) \p \v 57 Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Isa. \v 58 Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Isa. Pilato akaamuru apewe. \v 59 Yusufu akauchukua mwili wa Isa, akaufunga kwa kitambaa cha kitani safi, \v 60 na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake. \v 61 Mariamu Magdalene na yule Mariamu mwingine walikuwa mahali pale, wakiwa wameketi mkabala na kaburi. \s1 Walinzi pale kaburini \p \v 62 Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo\f + \fr 27:62 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakamwendea Pilato \v 63 na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu wakati alikuwa bado hai alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ \v 64 Basi uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti hadi baada ya siku tatu. La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.” \p \v 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari walinzi. Nendeni, liwekeeni ulinzi kadiri mnavyoweza.” \v 66 Hivyo basi wakaenda na walinzi ili kulilinda kaburi kwa uthabiti, wakatia muhuri kwenye lile jiwe na kuweka ulinzi. \c 28 \s1 Isa afufuka \r (Marko 16:1-10; Luka 24:1-12; Yohana 20:1-10) \p \v 1 Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene na yule Mariamu mwingine walienda kulitazama kaburi. \p \v 2 Ghafula, pakawa na tetemeko kubwa la ardhi, kwa sababu malaika wa Mwenyezi Mungu alishuka kutoka mbinguni, akaenda kwenye kaburi, akalivingirisha lile jiwe na kulikalia. \v 3 Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. \v 4 Wale walinzi wa kaburi walimwogopa sana, wakatetemeka hata wakawa kama wafu. \p \v 5 Yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope, kwa maana ninajua kuwa mnamtafuta Isa aliyesulubiwa. \v 6 Hayupo hapa, kwa kuwa amefufuka, kama alivyosema. Njooni mpatazame mahali alipokuwa amelazwa. \v 7 Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake kwamba, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu, naye anawatangulia kwenda Galilaya. Mtamwona huko.’ Sasa nimekwisha kuwaambia.” \p \v 8 Hivyo wale wanawake wakaondoka pale kaburini wakiwa wamejawa na hofu, lakini wakiwa na furaha nyingi. Wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi wake habari hizo. \v 9 Ghafula, Isa akakutana nao, akasema, “Salamu!” Wale wanawake wakamkaribia, wakaishika miguu yake, wakamwabudu. \v 10 Ndipo Isa akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.” \s1 Taarifa ya walinzi \p \v 11 Wale wanawake wakiwa njiani wakienda, baadhi ya wale askari waliokuwa wakilinda kaburi walienda mjini na kuwaeleza viongozi wa makuhani kila kitu kilichokuwa kimetukia. \v 12 Baada ya viongozi wa makuhani kukutana na wazee na kupanga njama, waliwapa wale askari kiasi kikubwa cha fedha, \v 13 wakawaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakati wa usiku na kumwiba sisi tulipokuwa tumelala.’ \v 14 Kama habari hizi zikimfikia mtawala, sisi tutamwondolea mashaka nanyi hamtapata tatizo lolote.” \v 15 Hivyo basi, wale askari wakazipokea hizo fedha nao wakafanya kama walivyoelekezwa. Habari hii imeenea miongoni mwa Wayahudi hadi leo. \s1 Isa awatuma wanafunzi wake \r (Marko 16:14-18; Luka 24:36-49; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8) \p \v 16 Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda hadi Galilaya kwenye ule mlima ambao Isa alikuwa amewaagiza. \v 17 Walipomwona, wakamwabudu; lakini baadhi yao wakaona shaka. \v 18 Isa akawajia na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. \v 19 Kwa sababu hii, nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza\f + \fr 28:19 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali.\ft*\f* kwa Jina la Baba\f + \fr 28:19 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* na la Mwana\f + \fr 28:19 \fr*\ft Yaani Isa Al-Masihi, aliye na asili ya Mwenyezi Mungu, na uhusiano wa kipekee naye.\ft*\f* na la Roho\f + \fr 28:19 \fr*\ft Ndiye anayefanya kazi ya Mwenyezi Mungu katika moyo wa mwanadamu, na kumshawishi nia yake kumfuata Isa Al-Masihi (\+xt Yohana 16:5-15\+xt*).\ft*\f* wa Mungu, \v 20 nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”