\id LUK - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Luka \toc1 Luka \toc2 Luka \toc3 Lk \mt1 Luka \c 1 \ms1 Utangulizi; kuzaliwa kwa Isa na ujana wake \mr (Luka 1:1–2:52) \s1 Utangulizi \p \v 1 Kwa kuwa watu wengi wamekaa ili kuandika habari za mambo yaliyotimizwa katikati yetu, \v 2 kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale waliokuwa mashahidi walioyaona na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, \v 3 mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo, ewe mtukufu Theofilo, \v 4 ili upate kujua ukweli kuhusu yale uliyofundishwa. \s1 Kuzaliwa kwa Yahya kwatabiriwa \p \v 5 Wakati wa utawala wa Herode mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, aliyekuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Haruni. \v 6 Zakaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Mwenyezi Mungu na maagizo yote bila lawama. \v 7 Lakini walikuwa hawana watoto, kwa sababu Elizabeti alikuwa tasa; nao wote wawili walikuwa wazee sana. \p \v 8 Siku moja ilipokuwa zamu ya kikundi cha Zakaria, yeye akifanya kazi ya ukuhani Hekaluni\f + \fr 1:8 \fr*\ft Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu.\ft*\f* mbele za Mungu, \v 9 alichaguliwa kwa kura kwa kufuata desturi za ukuhani, kuingia Hekaluni mwa Mwenyezi Mungu ili kufukiza uvumba. \v 10 Nao wakati wa kufukiza uvumba ulipowadia, wale wote waliokuwa wamekusanyika ili kuabudu walikuwa nje wakiomba. \p \v 11 Ndipo malaika wa Mwenyezi Mungu, akiwa amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia uvumba, akamtokea Zakaria. \v 12 Zakaria alipomwona huyo malaika, akafadhaika sana, akajawa na hofu. \v 13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina Yahya. \v 14 Yeye atakuwa furaha na shangwe kwako, nao watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. \v 15 Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Mwenyezi Mungu, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji chochote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu wa Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwake. \v 16 Naye atawageuza wengi wa Waisraeli warudi kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \v 17 Naye atatangulia mbele za Mwenyezi Mungu katika roho na nguvu ya Ilya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao, na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki, ili kuwaweka tayari watu walioandaliwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” \p \v 18 Zakaria akamuuliza malaika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa.” \p \v 19 Malaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Jibraili, nisimamaye mbele za Mungu, nami nimetumwa kwako ili nikuambie habari hizi njema. \v 20 Basi sasa kwa kuwa hujaamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati wake, utakuwa bubu hadi siku ile mambo haya yatakapotukia.” \p \v 21 Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zakaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni. \v 22 Alipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono. \p \v 23 Muda wake wa kuhudumu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani mwake. \v 24 Baada ya muda usio mrefu, Elizabeti mkewe akapata mimba, naye akajitenga kwa miezi mitano. \p \v 25 Elizabeti akasema, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu alilonitendea aliponipa kibali na kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.” \s1 Kuzaliwa kwa Isa kwatabiriwa \p \v 26 Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Jibraili aende Galilaya katika mji wa Nasiri, \v 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yusufu\f + \fr 1:27 \fr*\ft Yusufu hakuwa baba mzazi wa Isa, bali alikuwa baba mlezi.\ft*\f* wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Mariamu. \v 28 Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe!” \p \v 29 Mariamu akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni salamu hii ni ya namna gani. \v 30 Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu. \v 31 Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume na utamwita jina Isa. \v 32 Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Mwenyezi Mungu atampa kiti cha utawala cha Daudi baba yake. \v 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” \p \v 34 Mariamu akamuuliza huyo malaika, “Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” \p \v 35 Malaika akamjibu, “Roho wa Mungu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu\f + \fr 1:35 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*. \v 36 Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. \v 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.” \p \v 38 Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha. \s1 Mariamu aenda kumtembelea Elizabeti \p \v 39 Wakati huo Mariamu akajiandaa, akaharakisha kwenda katika mji mmoja kwenye nchi ya vilima ya Yudea. \v 40 Akaingia nyumbani mwa Zakaria na kumsalimu Elizabeti. \v 41 Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho wa Mungu, \v 42 akapaza sauti kwa nguvu, akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. \v 43 Lakini ni kwa nini mimi nimepata kibali kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? \v 44 Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliye tumboni mwangu aliruka kwa furaha. \v 45 Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Mwenyezi Mungu alilomwambia litatimizwa.” \s1 Wimbo wa Mariamu \p \v 46 Naye Mariamu akasema: \q1 “Moyo wangu wamwadhimisha Mwenyezi Mungu, \q2 \v 47 nayo roho yangu inamfurahia \q2 Mungu Mwokozi wangu, \q1 \v 48 kwa kuwa ameangalia kwa fadhili \q2 unyonge wa mtumishi wake. \q1 Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa, \q2 \v 49 kwa maana yeye Mwenye Nguvu \q2 amenitendea mambo ya ajabu: \q2 jina lake ni takatifu. \q1 \v 50 Rehema zake hudumu kizazi hadi kizazi, \q2 kwa wale wanaomcha. \q1 \v 51 Kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake; \q2 amewatawanya wale wenye kiburi \q2 ndani ya mioyo yao. \q1 \v 52 Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya utawala, \q2 lakini amewainua wanyenyekevu. \q1 \v 53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, \q2 bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. \q1 \v 54 Amemsaidia mtumishi wake Israeli, \q2 kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu \q1 \v 55 Ibrahimu na uzao wake milele, \q2 kama alivyowaahidi baba zetu.” \p \v 56 Mariamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani mwake. \s1 Kuzaliwa kwa Yahya \p \v 57 Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto wa kiume. \v 58 Majirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Mwenyezi Mungu alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye. \p \v 59 Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zakaria, ambalo ndilo jina la baba yake. \v 60 Lakini mama yake akakataa na kusema, “Hapana! Jina lake ataitwa Yahya.” \p \v 61 Wakamwambia, “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.” \p \v 62 Basi wakamfanyia Zakaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. \v 63 Akaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yahya.” \v 64 Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kuongea, huku akimsifu Mungu. \v 65 Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima ya Yudea watu walikuwa wakinena kuhusu mambo haya yote. \v 66 Kila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa pamoja naye. \s1 Unabii wa Zakaria \p \v 67 Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, naye akatoa unabii, akisema: \q1 \v 68 “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, \q2 kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa. \q1 \v 69 Naye ametusimamishia pembe\f + \fr 1:69 \fr*\fq pembe \fq*\ft inamaanisha nguvu\ft*\f* ya wokovu \q2 katika nyumba ya Daudi mtumishi wake, \q1 \v 70 (kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake \q2 watakatifu tangu zamani), \q1 \v 71 kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, \q2 na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao: \q1 \v 72 ili kuonesha rehema kwa baba zetu \q2 na kukumbuka agano lake takatifu, \q1 \v 73 kiapo alichomwapia baba yetu Ibrahimu: \q1 \v 74 kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu, \q2 tupate kumtumikia yeye pasipo hofu \q1 \v 75 katika utakatifu na haki mbele zake, \q2 siku zetu zote. \b \q1 \v 76 “Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana; \q2 kwa kuwa utamtangulia Mwenyezi Mungu \q2 na kuandaa njia kwa ajili yake, \q1 \v 77 kuwajulisha watu wake wokovu \q2 utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, \q1 \v 78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, \q2 nuru inayotoka juu itatuzukia \q1 \v 79 ili kuwaangazia wale wanaoishi gizani \q2 na katika uvuli wa mauti, \q1 kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” \p \v 80 Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionesha hadharani kwa Waisraeli. \c 2 \s1 Kuzaliwa kwa Isa \r (Mathayo 1:18-25) \p \v 1 Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Rumi. \v 2 (Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Siria.) \v 3 Kila mtu alienda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa. \p \v 4 Hivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Yudea, hadi Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. \v 5 Alienda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, aliyekuwa amemposa, na alikuwa mjamzito. \v 6 Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu wa kujifungua ukawa umetimia, \v 7 naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni. \s1 Wachungaji na malaika \p \v 8 Katika eneo lile walikuwako wachungaji waliokuwa wakikaa mashambani, wakilinda makundi yao ya kondoo usiku. \v 9 Ghafula tazama, malaika wa Mwenyezi Mungu akawatokea, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukawang’aria kotekote, wakaingiwa na hofu. \v 10 Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama, nawaletea habari njema ya furaha itakayokuwa kwa watu wote. \v 11 Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Al-Masihi\f + \fr 2:11 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, Bwana. \v 12 Hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ng’ombe.” \p \v 13 Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema, \q1 \v 14 “Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, \q2 na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.” \p \v 15 Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya yaliyotukia, ambayo Mwenyezi Mungu ametuambia habari zake.” \p \v 16 Hivyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Mariamu na Yusufu na yule mtoto mchanga akiwa amelala katika hori la kulia ng’ombe. \v 17 Walipomwona yule mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa kuhusu huyo mtoto. \v 18 Nao wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wale wachungaji wa kondoo. \v 19 Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. \v 20 Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona. \p \v 21 Hata zilipotimia siku nane, uliokuwa wakati wa kumtahiri mtoto, akaitwa Isa, jina alilopewa na malaika kabla hajatungwa mimba. \s1 Isa apelekwa Hekaluni \p \v 22 Ulipotimia wakati wa utakaso wake Mariamu kwa mujibu wa Torati ya Musa, basi Yusufu na Mariamu walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu \v 23 (kama ilivyoandikwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu, kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu”), \v 24 na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu: “Hua wawili au makinda wawili wa njiwa”. \p \v 25 Basi huko Yerusalemu kulikuwa mtu mmoja aliyeitwa Simeoni, aliyekuwa mwenye haki na mcha Mungu. Alikuwa akitazamia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu wa Mungu alikuwa juu yake. \v 26 Roho wa Mungu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Al-Masihi wa Bwana. \v 27 Simeoni, akiwa ameongozwa na Roho wa Mungu, alienda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Isa ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Torati, \v 28 ndipo Simeoni akampokea mtoto mikononi mwake na kumsifu Mungu, akisema: \q1 \v 29 “Bwana Mungu Mwenyezi, kama ulivyoahidi, \q2 sasa mruhusu mtumishi wako \q2 aende kwa amani. \q1 \v 30 Kwa maana macho yangu yameuona wokovu wako, \q2 \v 31 ulioweka tayari machoni pa watu wote, \q1 \v 32 nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu wa Mataifa \q2 na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.” \p \v 33 Naye Yusufu na mama yake mtoto wakastaajabu kwa yale yaliyokuwa yamesemwa kumhusu huyo mtoto. \v 34 Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, \v 35 ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako.” \p \v 36 Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa. \v 37 Hivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na nne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana, bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba. \v 38 Wakati huo huo, Ana alikuja akaanza kusifu, akimshukuru Mungu na kusema habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu. \p \v 39 Yusufu na Mariamu walipokuwa wamekamilisha mambo yote yaliyotakiwa na Torati ya Mwenyezi Mungu, walirudi mjini kwao Nasiri huko Galilaya. \v 40 Naye yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu, akijawa na hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. \s1 Kijana Isa Hekaluni \p \v 41 Kila mwaka Yusufu na Mariamu mama yake Isa walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka\f + \fr 2:41 \fr*\ft Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.\ft*\f*. \v 42 Isa alipokuwa na umri wa miaka kumi na mbili, walipanda kwenda kwenye Sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. \v 43 Baada ya Sikukuu kumalizika, wakati Yusufu na Mariamu mama yake walipokuwa wakirudi nyumbani, Isa alibaki Yerusalemu lakini hawakutambua. \v 44 Wao wakidhani kuwa yuko miongoni mwa wasafiri, walienda mwendo wa kutwa nzima. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na rafiki zao. \v 45 Walipomkosa walirudi Yerusalemu ili kumtafuta. \v 46 Baada ya siku tatu wakamkuta ndani ya Hekalu, akiwa ameketi katikati ya walimu wa Torati, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. \v 47 Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa, na majibu aliyoyatoa. \v 48 Yusufu na Mariamu mama yake walipomwona walishangaa. Mama yake akamuuliza, “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Tazama, mimi na baba yako tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa kila mahali.” \p \v 49 Isa akawaambia, “Kwa nini kunitafuta? Hamkujua kwamba imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba\f + \fr 2:49 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu?” \p \v 50 Lakini wao hawakuelewa maana ya lile alilowaambia. \p \v 51 Ndipo akashuka pamoja nao hadi Nasiri, naye alikuwa mtiifu kwao. Lakini mama yake akayaweka moyoni mwake mambo haya yote. \v 52 Naye Isa akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu. \c 3 \ms1 Yahya na Isa, na kujaribiwa kwa Isa \mr (Luka 3:1–4:13) \s1 Yahya atayarisha njia \r (Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Yohana 1:19-28) \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Yudea, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene, \v 2 nao Anasi na Kayafa wakiwa makuhani wakuu, neno la Mungu likamjia Yahya, mwana wa Zakaria huko jangwani. \v 3 Akaenda katika nchi yote kandokando ya Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi\f + \fr 3:3 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali.\ft*\f*. \v 4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: \q1 “Sauti ya mtu aliaye nyikani, \q1 ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, \q2 yanyoosheni mapito yake. \q1 \v 5 Kila bonde litajazwa, \q2 kila mlima na kilima vitashushwa. \q1 Njia zilizopinda zitanyooshwa, \q2 na zilizoparuza zitasawazishwa. \q1 \v 6 Nao watu wote watauona \q2 wokovu wa Mungu.’ ” \p \v 7 Yahya akaambia umati ule wa watu waliokuwa wanakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? \v 8 Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka mawe haya. \v 9 Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti. Basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.” \p \v 10 Umati ule wa watu wakamuuliza, “Inatupasa tufanyeje basi?” \p \v 11 Yahya akawaambia, “Aliye na kanzu mbili amgawie asiye nayo, naye aliye na chakula na afanye vivyo hivyo.” \p \v 12 Watoza ushuru nao wakaja ili wabatizwe, wakamuuliza, “Mwalimu na sisi inatupasa tufanyeje?” \p \v 13 Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.” \p \v 14 Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” \p Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.” \p \v 15 Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yahya angeweza kuwa ndiye Al-Masihi\f + \fr 3:15 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*. \v 16 Yahya akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji\f + \fr 3:16 \fr*\ft au \ft*\fqa ndani ya maji\fqa*\f*. Lakini atakuja aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho wa Mungu na kwa moto. \v 17 Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” \v 18 Basi, kwa maonyo mengine mengi Yahya aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema. \p \v 19 Lakini Yahya alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, \v 20 Herode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yahya gerezani. \s1 Isa abatizwa \r (Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-11) \p \v 21 Baada ya watu wote kubatizwa, Isa naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. \v 22 Roho Mtakatifu wa Mungu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.” \s1 Ukoo wa Isa \r (Mathayo 1:1-17) \p \v 23 Isa alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yusufu. \b \li1 Yusufu alikuwa mwana wa Eli, \li1 \v 24 Eli alikuwa mwana wa Mathati, \li1 Mathati alikuwa mwana wa Lawi, \li1 Lawi alikuwa mwana wa Melki, \li1 Melki alikuwa mwana wa Yana, \li1 Yana alikuwa mwana wa Yusufu, \li1 \v 25 Yusufu alikuwa mwana wa Matathia, \li1 Matathia alikuwa mwana wa Amosi, \li1 Amosi alikuwa mwana wa Nahumu, \li1 Nahumu alikuwa mwana wa Esli, \li1 Esli alikuwa mwana wa Nagai, \li1 \v 26 Nagai alikuwa mwana wa Maathi, \li1 Maathi alikuwa mwana wa Matathia, \li1 Matathia alikuwa mwana wa Semei, \li1 Semei alikuwa mwana wa Yoseki, \li1 Yoseki alikuwa mwana wa Yoda, \li1 \v 27 Yoda alikuwa mwana wa Yoanani, \li1 Yoanani alikuwa mwana wa Resa, \li1 Resa alikuwa mwana wa Zerubabeli, \li1 Zerubabeli alikuwa mwana wa Shealtieli, \li1 Shealtieli alikuwa mwana wa Neri, \li1 \v 28 Neri alikuwa mwana wa Melki, \li1 Melki alikuwa mwana wa Adi, \li1 Adi alikuwa mwana wa Kosamu, \li1 Kosamu alikuwa mwana wa Elmadamu, \li1 Elmadamu alikuwa mwana wa Eri, \li1 \v 29 Eri alikuwa mwana wa Yoshua, \li1 Yoshua alikuwa mwana wa Eliezeri, \li1 Eliezeri alikuwa mwana wa Yorimu, \li1 Yorimu alikuwa mwana wa Mathati, \li1 Mathati alikuwa mwana wa Lawi, \li1 \v 30 Lawi alikuwa mwana wa Simeoni, \li1 Simeoni alikuwa mwana wa Yuda, \li1 Yuda alikuwa mwana wa Yusufu, \li1 Yusufu alikuwa mwana wa Yonamu, \li1 Yonamu alikuwa mwana wa Eliakimu, \li1 Eliakimu alikuwa mwana wa Melea, \li1 \v 31 Melea alikuwa mwana wa Mena, \li1 Mena alikuwa mwana wa Matatha, \li1 Matatha alikuwa mwana wa Nathani, \li1 Nathani alikuwa mwana wa Daudi, \li1 \v 32 Daudi alikuwa mwana wa Yese, \li1 Yese alikuwa mwana wa Obedi, \li1 Obedi alikuwa mwana wa Boazi, \li1 Boazi alikuwa mwana wa Salmoni, \li1 Salmoni alikuwa mwana wa Nashoni, \li1 \v 33 Nashoni alikuwa mwana wa Aminadabu, \li1 Aminadabu alikuwa mwana wa Aramu, \li1 Aramu alikuwa mwana wa Esromu, \li1 Esromu alikuwa mwana wa Peresi, \li1 Peresi alikuwa mwana wa Yuda, \li1 \v 34 Yuda alikuwa mwana wa Yakobo, \li1 Yakobo alikuwa mwana wa Isaka, \li1 Isaka alikuwa mwana wa Ibrahimu, \li1 Ibrahimu alikuwa mwana wa Tera, \li1 Tera alikuwa mwana wa Nahori, \li1 \v 35 Nahori alikuwa mwana wa Serugi, \li1 Serugi alikuwa mwana wa Ragau, \li1 Ragau alikuwa mwana wa Pelegi, \li1 Pelegi alikuwa mwana wa Eberi, \li1 Eberi alikuwa mwana wa Sala, \li1 \v 36 Sala alikuwa mwana wa Kenani, \li1 Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi, \li1 Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu, \li1 Shemu alikuwa mwana wa Nuhu, \li1 Nuhu alikuwa mwana wa Lameki, \li1 \v 37 Lameki alikuwa mwana wa Methusela, \li1 Methusela alikuwa mwana wa Idrisi, \li1 Idrisi alikuwa mwana wa Yaredi, \li1 Yaredi alikuwa mwana wa Mahalaleli, \li1 Mahalaleli alikuwa mwana wa Kenani, \li1 \v 38 Kenani alikuwa mwana wa Enoshi, \li1 Enoshi alikuwa mwana wa Sethi, \li1 Sethi alikuwa mwana wa Adamu, \li1 Adamu alikuwa mwana wa Mungu\f + \fr 3:38 \fr*\ft Yaani mwana wa kiroho, bali si wa kimwili. Adamu aliumbwa moja kwa moja kutoka kwake Mwenyezi Mungu mwenyewe.\ft*\f*. \c 4 \s1 Isa ajaribiwa nyikani \r (Mathayo 4:1-11; Marko 1:12-13) \p \v 1 Isa, akiwa amejaa Roho Mtakatifu wa Mungu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho wa Mungu hadi nyikani, \v 2 ambako alijaribiwa na ibilisi kwa siku arobaini. Kwa siku zote hizo hakula chochote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa. \p \v 3 Ibilisi akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.” \p \v 4 Isa akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’ ” \p \v 5 Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonesha milki zote za dunia kwa mara moja. \v 6 Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka. \v 7 Hivyo ukinisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.” \p \v 8 Isa akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ” \p \v 9 Kisha ibilisi akampeleka hadi Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa, \v 10 kwa maana imeandikwa: \q1 “ ‘Atakuagizia malaika wake \q2 ili wakulinde kwa uangalifu; \q1 \v 11 nao watakuchukua mikononi mwao, \q2 usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ” \p \v 12 Isa akamjibu, “Imenenwa: ‘Usimjaribu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.’ ” \p \v 13 Ibilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Isa hadi wakati mwingine ufaao. \ms1 Huduma ya Isa huko Galilaya \mr (Luka 4:14–9:50) \s1 Isa aanza kuhubiri \r (Mathayo 4:12-17; Marko 1:14-15) \p \v 14 Kisha Isa akarudi hadi Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho wa Mungu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando. \v 15 Akaanza kufundisha kwenye masinagogi\f + \fr 4:15 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* yao, na kila mmoja akamsifu. \s1 Isa akataliwa Nasiri \r (Mathayo 13:53-58; Marko 6:1-6) \p \v 16 Isa akaenda Nasiri, alipolelewa, na siku ya Sabato alienda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome, \v 17 naye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa: \q1 \v 18 “Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi yu juu yangu, \q2 kwa sababu amenipaka mafuta \q2 kuwahubiria maskini Habari Njema. \q1 Amenituma kuwatangazia wafungwa \q2 kufunguliwa kwao, \q2 na vipofu kupata kuona tena, \q1 kuwaweka huru wanaoteswa, \q2 \v 19 na kutangaza mwaka wa Mwenyezi Mungu uliokubalika.” \p \v 20 Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. \v 21 Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo andiko hili limetimia mkiwa mnasikia.” \p \v 22 Watu wote walimsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yusufu\f + \fr 4:22 \fr*\ft Yusufu hakuwa baba mzazi wa Isa, bali alikuwa baba mlezi.\ft*\f*?” \p \v 23 Isa akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ” \p \v 24 Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe. \v 25 Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Ilya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima. \v 26 Hata hivyo Ilya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. \v 27 Pia palikuwa na wengi wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Al-Yasa, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa Shamu\f + \fr 4:27 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Siria\fqa*\f*.” \p \v 28 Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana. \v 29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima ambao mji huo ulikuwa umejengwa juu yake, ili wamtupe chini kutoka mteremko mkali. \v 30 Lakini yeye akapita papo hapo katikati ya umati huo wa watu akaenda zake. \s1 Isa atoa pepo mchafu \r (Marko 1:21-28) \p \v 31 Kisha Isa akashuka kwenda Kapernaumu, mji wa Galilaya, na katika siku ya Sabato akawa anafundisha. \v 32 Wakashangazwa sana na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka. \p \v 33 Ndani ya sinagogi palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu. Naye akapaza sauti kwa nguvu akisema, \v 34 “Tuache! Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!” \p \v 35 Basi Isa akamkemea yule pepo mchafu, akamwamuru, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu!” Yule pepo mchafu akamwangusha yule mtu chini mbele yao wote, akatoka pasipo kumdhuru. \p \v 36 Watu wote wakashangaa, wakaambiana, “Mafundisho haya ni ya namna gani? Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!” \v 37 Habari zake zikaanza kuenea kila mahali katika sehemu ile. \s1 Isa amponya mama mkwe wa Simoni na pia watu wengi \r (Mathayo 8:14-17; Marko 1:29-34) \p \v 38 Isa akatoka katika sinagogi, akaenda nyumbani mwa Simoni. Basi huko alimkuta mama mkwe wa Simoni akiwa ameshikwa na homa kali, nao wakamwomba Isa amsaidie. \v 39 Hivyo Isa akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka mara moja, naye akaanza kuwahudumia. \p \v 40 Jua lilipokuwa linatua, watu wakamletea Isa watu wote waliokuwa na maradhi mbalimbali, naye akaweka mikono yake juu ya kila mgonjwa, naye akawaponya. \v 41 Pepo wachafu pia wakawatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele, wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Isa akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walimjua kuwa yeye ndiye Al-Masihi.\f + \fr 4:41 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* \p \v 42 Kesho yake, kulipopambazuka, Isa alienda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke. \v 43 Lakini yeye akawaambia, “Imenipasa kuhubiri Habari Njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, kwa maana kwa kusudi hili nilitumwa.” \v 44 Naye aliendelea kuhubiri katika masinagogi ya Yudea. \c 5 \s1 Wanafunzi wa kwanza wa Isa \r (Mathayo 4:18-22; Marko 1:16-20; Yohana 1:35-51) \p \v 1 Siku moja Isa alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti\f + \fr 5:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Galilaya\fqa*\f*, watu wengi walimsonga ili wapate kusikia neno la Mungu. \v 2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao. \v 3 Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua. \p \v 4 Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, “Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki.” \p \v 5 Simoni akamjibu, “Bwana\f + \fr 5:5 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu.” \p \v 6 Nao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika. \v 7 Wakawaashiria wavuvi wenzao kwenye ile mashua nyingine ili waje kuwasaidia. Wakaja, wakajaza mashua zote mbili samaki hata zikaanza kuzama. \p \v 8 Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni pa Isa na kumwambia, “Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!” \v 9 Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wameshangazwa sana na wingi wa samaki waliokuwa wamepata. \v 10 Vivyo hivyo wenzake Simoni, yaani Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walishangazwa pia. \p Ndipo Isa akamwambia Simoni, “Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.” \v 11 Hivyo wakasogeza mashua zao hadi ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata. \s1 Isa amtakasa mtu mwenye ukoma \r (Mathayo 8:1-4; Marko 1:40-45) \p \v 12 Ikawa siku moja Isa alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Isa, alianguka chini hadi uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, “Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa.” \p \v 13 Isa akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Na mara ukoma wake ukatakasika. \p \v 14 Isa akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu yeyote, bali nenda ukajioneshe kwa kuhani na ukatoe sadaka alizoagiza Musa kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.” \p \v 15 Lakini habari zake Isa zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makundi makubwa ya watu walikuwa wakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. \v 16 Lakini mara kwa mara Isa alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba. \s1 Isa amponya mtu aliyepooza \r (Mathayo 9:1-8; Marko 2:1-12) \p \v 17 Siku moja Isa alipokuwa akifundisha, Mafarisayo\f + \fr 5:17 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na walimu wa Torati, waliokuwa wametoka kila kijiji cha Galilaya na kutoka Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi huko. Nao uweza wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yake kuponya wagonjwa. \v 18 Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Isa. \v 19 Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya matofali, wakamteremsha yule mgonjwa kwa mkeka wake hadi katikati ya umati ule pale mbele ya Isa. \p \v 20 Isa alipoiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Rafiki, dhambi zako zimesamehewa.” \p \v 21 Mafarisayo na wale walimu wa Torati wakaanza kuuliza, “Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?” \p \v 22 Isa akijua mawazo yao akawauliza, “Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? \v 23 Je, ni lipi lililo rahisi zaidi, kumwambia, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? \v 24 Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako.” \v 25 Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake, akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu. \v 26 Kila mmoja akashangaa na kumtukuza Mungu. Wakajawa na hofu ya Mungu, wakasema, “Leo tumeona mambo ya ajabu.” \s1 Isa amwita Lawi \r (Mathayo 9:9-13; Marko 2:13-17) \p \v 27 Baada ya haya, Isa alitoka na kumwona mtoza ushuru mmoja jina lake Lawi akiwa amekaa forodhani, mahali pake pa kutoza ushuru. Akamwambia, “Nifuate.” \v 28 Naye Lawi akaacha kila kitu, akaondoka, akamfuata. \p \v 29 Kisha Lawi akamfanyia Isa karamu kubwa nyumbani mwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao. \v 30 Lakini Mafarisayo na walimu wa Torati waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Isa, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?” \p \v 31 Isa akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. \v 32 Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.” \s1 Isa aulizwa kuhusu kufunga \r (Mathayo 9:14-17; Marko 2:18-22) \p \v 33 Wakamwambia Isa, “Wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.” \p \v 34 Isa akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao? \v 35 Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.” \p \v 36 Isa akawapa mfano huu, akawaambia: “Hakuna mtu achanaye kiraka kwenye nguo mpya na kukishonea kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, atakuwa amechana nguo mpya, na kile kiraka hakitalingana na ile nguo iliyochakaa. \v 37 Hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo yote itamwagika. \v 38 Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. \v 39 Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, bali husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’ ” \c 6 \s1 Isa ni Bwana wa Sabato \r (Mathayo 12:1-8; Marko 2:23-28) \p \v 1 Ikawa siku moja ya Sabato Isa alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, nao wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake. \v 2 Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya mambo yasiyo halali kufanywa siku ya Sabato?” \p \v 3 Isa akawajibu, “Je, ninyi hamjasoma alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa? \v 4 Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani tu. Naye pia akawapa wenzake.” \v 5 Kisha Isa akawaambia, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” \s1 Isa amponya mtu aliyepooza mkono \r (Mathayo 12:9-14; Marko 3:1-6) \p \v 6 Ikawa siku nyingine ya Sabato, Isa aliingia ndani ya sinagogi\f + \fr 6:6 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. \v 7 Mafarisayo na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. \v 8 Lakini Isa alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Inuka usimame mbele ya watu wote.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote. \p \v 9 Ndipo Isa akawaambia wale walimu wa Torati na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?” \p \v 10 Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha, na mkono wake ukawa umeponywa kabisa. \v 11 Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Isa. \s1 Isa achagua mitume kumi na wawili \r (Mathayo 10:1-4; Marko 3:13-19) \p \v 12 Ikawa katika siku hizo Isa alienda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. \v 13 Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume: \b \li1 \v 14 Simoni (aliyemwita Petro) na Andrea nduguye, \li1 Yakobo, \li1 Yohana, \li1 Filipo, \li1 Bartholomayo, \li1 \v 15 Mathayo, \li1 Tomaso, \li1 Yakobo mwana wa Alfayo, \li1 Simoni aliyeitwa Zelote\f + \fr 6:15 \fr*\ft Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi.\ft*\f*, \li1 \v 16 Yuda mwana wa Yakobo, \li1 na Yuda Iskariote, aliyekuwa msaliti. \s1 Isa afundisha na kuponya wagonjwa \r (Mathayo 4:23-25) \p \v 17 Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Yudea, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. \v 18 Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya. \v 19 Watu wote walikuwa wanajitahidi kumgusa kwa sababu nguvu zilikuwa zikimtoka na kuwaponya wote. \s1 Baraka na laana \r (Mathayo 5:1-12) \p \v 20 Akawatazama wanafunzi wake, akasema: \q1 “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, \q2 kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu. \q1 \v 21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, \q2 kwa sababu mtashibishwa. \q1 Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, \q2 kwa sababu mtacheka. \q1 \v 22 Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, \q2 watakapowatenga na kuwatukana \q1 na kulikataa jina lenu kama neno ovu, \q2 kwa ajili ya Mwana wa Adamu. \p \v 23 “Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii. \q1 \v 24 “Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri, \q2 kwa sababu mmekwisha kupokea faraja yenu. \q1 \v 25 Ole wenu ninyi mlioshiba sasa, \q2 maana mtaona njaa. \q1 Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, \q2 maana mtaomboleza na kulia. \q1 \v 26 Ole wenu watu watakapowasifu, \q2 kwani ndivyo baba zao walivyowasifu \q2 manabii wa uongo. \s1 Wapendeni adui zenu \r (Mathayo 5:38-48) \p \v 27 “Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. \v 28 Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. \v 29 Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. \v 30 Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. \v 31 Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi. \p \v 32 “Mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda. \v 33 Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. \v 34 Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote. \v 35 Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu. \v 36 Kuweni na huruma, kama Baba\f + \fr 6:36 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yenu alivyo na huruma. \s1 Kuwahukumu wengine \r (Mathayo 7:1-5) \p \v 37 “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa. Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni, nanyi mtasamehewa. \v 38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.” \p \v 39 Pia akawapa mfano akasema, “Je, kipofu aweza kumwongoza kipofu? Je, wote wawili hawatatumbukia shimoni? \v 40 Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, ila yule aliyehitimu aweza kuwa kama mwalimu wake. \p \v 41 “Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? \v 42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako. \s1 Mti na matunda yake \r (Mathayo 12:33-35) \p \v 43 “Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri. \v 44 Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma. \v 45 Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake. \s1 Mjenzi mwenye busara na mjenzi mpumbavu \r (Mathayo 7:24-27) \p \v 46 “Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? \v 47 Nitawaonesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. \v 48 Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. \v 49 Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.” \c 7 \s1 Isa amponya mtumishi wa jemadari \r (Mathayo 8:5-13) \p \v 1 Baada ya Isa kumaliza kusema haya yote kwa watu waliokuwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu. \v 2 Mtumishi wa jemadari mmoja Mrumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu na kufa. \v 3 Jemadari huyo aliposikia habari za Isa, aliwatuma wazee wa Wayahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari. \v 4 Wale wazee walipofika kwa Isa, wakamsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili wewe umfanyie jambo hili, \v 5 kwa sababu analipenda taifa letu tena ametujengea sinagogi.” \v 6 Hivyo Isa akaongozana nao. \p Lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani, yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia Isa, “Bwana\f + \fr 7:6 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, usijisumbue, kwani mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. \v 7 Ndiyo maana sikujiona hata ninastahili kuja kwako wewe. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. \v 8 Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.” \p \v 9 Isa aliposikia maneno haya, alishangazwa naye sana. Akageukia umati ule wa watu waliokuwa wanamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.” \v 10 Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Isa waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona. \s1 Isa amfufua mwana wa mjane \p \v 11 Baadaye kidogo, Isa alienda katika mji mmoja ulioitwa Naini. Nao wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu walienda pamoja naye. \v 12 Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mwanamke. \v 13 Bwana Isa alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.” \p \v 14 Kisha akalikaribia jeneza, akaligusa. Nao wale waliokuwa wamelibeba wakasimama. Akasema, “Kijana, nakuambia, inuka.” \v 15 Yule aliyekuwa amekufa akaketi akaanza kuongea, naye Isa akamkabidhi kwa mama yake. \p \v 16 Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.” \v 17 Habari hizi za mambo aliyoyafanya Isa zikaenea Yudea yote na sehemu zote za jirani. \s1 Isa na Yahya \r (Mathayo 11:1-19) \p \v 18 Wanafunzi wa Yahya wakamweleza Yahya mambo haya yote. Hivyo Yahya akawaita wanafunzi wake wawili \v 19 na kuwatuma kwa Bwana Isa ili kumuuliza, “Wewe ndiwe yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?” \p \v 20 Wale watu walipofika kwa Isa wakamwambia, “Yahya ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiwe yule aliyekuwa aje, au tumtazamie mwingine?’ ” \p \v 21 Wakati huo huo, Isa aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maradhi na pepo wachafu, na pia akawafungua vipofu wengi macho wakapata kuona. \v 22 Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yahya yote mnayoyaona na kuyasikia: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. \v 23 Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.” \p \v 24 Wajumbe wa Yahya walipoondoka, Isa akaanza kusema na umati wa watu kuhusu Yahya. Akawauliza, “Mlipoenda kule nyikani, mlienda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? \v 25 Kama sivyo, mlienda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha! Watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme. \v 26 Lakini mlienda kuona nini? Mlienda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. \v 27 Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa: \q1 “ ‘Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, \q2 atakayetengeneza njia mbele yako.’ \m \v 28 Nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yahya. Lakini yeye aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yahya.” \p \v 29 (Watu wote, hata watoza ushuru, waliposikia maneno ya Isa, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yahya. \v 30 Lakini Mafarisayo\f + \fr 7:30 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na wataalamu wa Torati walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yahya.) \p \v 31 Isa akawauliza, “Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Wanafanana na nini? \v 32 Wao ni kama watoto waliokaa sokoni wakiitana wao kwa wao, wakisema: \q1 “ ‘Tuliwapigia filimbi, \q2 lakini hamkucheza; \q1 tuliwaimbia nyimbo za maombolezo, \q2 lakini hamkulia.’ \m \v 33 Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali mkate wala hanywi divai, nanyi mkasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’ \v 34 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nanyi mnasema: ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ \v 35 Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli na watoto wake wote.” \s1 Isa apakwa mafuta na mwanamke mwenye dhambi \r (Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9; Yohana 12:1-8) \p \v 36 Basi Farisayo mmoja alimwalika Isa kwake ale chakula. Hivyo Isa akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kuketi mezani. \v 37 Palikuwa na mwanamke mmoja katika mji ule aliyekuwa mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Isa alikuwa akila chakula nyumbani mwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marhamu yenye manukato. \v 38 Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Isa akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato. \p \v 39 Yule Farisayo aliyemwalika Isa alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa, na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani, na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.” \p \v 40 Isa akamjibu, “Simoni, nina jambo la kukuambia.” \p Simoni akajibu, “Mwalimu, sema.” \p \v 41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari mia tano\f + \fr 7:41 \fr*\ft Dinari 500 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku mia tano.\ft*\f* na mwingine dinari hamsini. \v 42 Wote wawili walipokuwa hawawezi kulipa, aliyafuta madeni yao wote wawili. Sasa ni yupi kati yao atakayempenda zaidi yule aliyewasamehe?” \p \v 43 Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi.” \p Naye Isa akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.” \p \v 44 Kisha akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, “Je, unamwona mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu yangu, lakini huyu ameninawisha miguu kwa machozi yake, na kunifuta kwa nywele zake. \v 45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia. \v 46 Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato. \v 47 Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.” \p \v 48 Kisha akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.” \p \v 49 Lakini wale waliokuwa wameketi pamoja naye chakulani wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani ambaye hata anasamehe dhambi?” \p \v 50 Isa akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.” \c 8 \s1 Mfano wa mpanzi \r (Mathayo 13:1-9; Marko 4:1-9) \p \v 1 Baada ya haya Isa alienda, akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri Injili ya ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye, \v 2 pia baadhi ya wanawake waliokuwa wametolewa pepo wachafu na kuponywa magonjwa. Miongoni mwao alikuwa Mariamu Magdalene, aliyetolewa pepo wachafu saba; \v 3 Yoana mkewe Kuza, msimamizi wa nyumba ya watu wa nyumbani mwa Herode; Susana; na wengine wengi waliokuwa wakimhudumia kwa mali yao. \p \v 4 Umati mkubwa wa watu walipokuwa wakikusanyika, nao watu walikuwa wakimjia Isa kutoka kila mji, akawaambia mfano huu: \v 5 “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia; zikakanyagwa, nao ndege wa angani wakazila. \v 6 Mbegu nyingine zilianguka penye miamba, nazo zilipoota, hiyo mimea ikakauka kwa kukosa unyevu. \v 7 Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo ile miiba ikakua pamoja nazo, na kuisonga hiyo mimea. \v 8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri. Zikaota na kuzaa mara mia moja zaidi ya mbegu alizopanda.” \p Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti, akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” \s1 Sababu ya kufundisha kwa mifano \r (Mathayo 13:9-17; Marko 4:10-12) \p \v 9 Wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo. \v 10 Naye akasema, “Ninyi mmepewa ujuzi wa siri za ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, \q1 “ ‘ingawa wanatazama, wasione; \q2 ingawa wanasikiliza, wasielewe.’ \s1 Maelezo ya mfano wa mbegu \r (Mathayo 13:18-23; Marko 4:13-20) \p \v 11 “Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. \v 12 Zile zilizoanguka kando ya njia ni wale ambao husikia neno, naye ibilisi anakuja na kuliondoa neno kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka. \v 13 Zile mbegu zilizoanguka kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa muda mfupi, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani. \v 14 Zile mbegu zilizoanguka kwenye miiba ni mfano wa wale wanaosikia, lakini wanapoendelea husongwa na masumbufu ya maisha haya, utajiri na anasa, nao hawakui. \v 15 Lakini zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo mzuri ni mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mnyofu wa utiifu, nao kwa kuvumilia kwingi huzaa matunda. \s1 Mfano wa taa \r (Marko 4:21-25) \p \v 16 “Hakuna mtu awashaye taa na kuificha ndani ya gudulia au kuiweka mvunguni mwa kitanda. Badala yake, huiweka juu ya kinara, ili wale wanaoingia ndani waone mwanga. \v 17 Kwa maana hakuna jambo lolote lililofichika ambalo halitafichuliwa, wala lolote lililositirika ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi. \v 18 Kwa hiyo, kuweni waangalifu mnavyosikia. Kwa maana yeyote aliye na kitu atapewa zaidi. Lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho atanyang’anywa.” \s1 Mama yake na ndugu zake Isa \r (Mathayo 12:46-50; Marko 3:31-35) \p \v 19 Wakati mmoja mama yake Isa na ndugu zake walikuja kumwona, lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. \v 20 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.” \p \v 21 Isa akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulifanya.” \s1 Isa atuliza dhoruba \r (Mathayo 8:23-27; Marko 4:35-41) \p \v 22 Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka. \v 23 Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa. \p \v 24 Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana\f + \fr 8:24 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, Bwana, tunaangamia!” \p Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari. \v 25 Akawauliza wanafunzi wake, “Imani yenu iko wapi?” \p Kwa woga na mshangao wakaulizana, “Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?” \s1 Isa amponya mtu mwenye pepo mchafu \r (Mathayo 8:28-34; Marko 5:1-20) \p \v 26 Basi wakafika katika nchi ya Wagerasi, iliyo upande wa pili wa ziwa kutoka Galilaya. \v 27 Isa aliposhuka kutoka mashua na kukanyaga ufuoni, alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye kwa muda mrefu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini. \v 28 Alipomwona Isa, alipaza sauti, akajitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kuu, “Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu\f + \fr 8:28 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f* Aliye Juu Sana? Nakuomba, usinitese!” \v 29 Wakati huo Isa alikuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke huyo mtu. Mara nyingi huyo pepo mchafu alimpagaa, na hata alipofungwa kwa minyororo mikono na miguu na kuwekwa chini ya ulinzi, alikata hiyo minyororo na kupelekwa na huyo pepo mchafu kwenda nyikani. \p \v 30 Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” \p Akamjibu, “Legioni\f + \fr 8:30 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Jeshi\fqa*\f*,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno. \v 31 Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo\f + \fr 8:31 \fr*\ft Shimo hapa ina maana \ft*\fqa Abyss \fqa*\ft (yaani \ft*\fqa shimo lisilo na mwisho\fqa*\ft ), yaani \ft*\fqa Kuzimu.\fqa*\f*. \p \v 32 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu. \v 33 Wale pepo wachafu walipomtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremkia gengeni kwa kasi, likatumbukia ziwani na kuzama. \p \v 34 Wale watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe walipoona yaliyotukia, wakakimbia, wakaeneza habari hizi mjini na mashambani. \v 35 Nao watu wakatoka kwenda kujionea wenyewe yaliyotukia. Walipofika hapo alipokuwa Isa, wakamkuta yule mtu aliyetokwa na pepo wachafu amekaa karibu na Isa, akiwa amevaa nguo na mwenye akili timamu! Wakaogopa. \v 36 Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine jinsi yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu alivyoponywa. \v 37 Ndipo watu wote wa nchi ile ya Wagerasi wakamwomba Isa aondoke kwao, kwa sababu walikuwa wamejawa na hofu. Basi akaingia katika mashua, akaondoka zake. \p \v 38 Yule mtu aliyetokwa na pepo wachafu akamsihi Isa afuatane naye, lakini Isa akamuaga, akamwambia: \v 39 “Rudi nyumbani ukawaeleze mambo makuu Mungu aliyokutendea.” Kwa hiyo yule mtu akaenda, akatangaza katika mji wote mambo makuu ambayo Isa alimtendea. \s1 Isa amponya mwanamke na kumfufua msichana \r (Mathayo 9:18-26; Marko 5:21-43) \p \v 40 Basi Isa aliporudi, umati mkubwa wa watu wakampokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea. \v 41 Kisha mtu mmoja, jina lake Yairo, aliyekuwa kiongozi wa sinagogi\f + \fr 8:41 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f*, akaja na kuanguka miguuni mwa Isa, akimwomba afike nyumbani mwake, \v 42 kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na mbili, alikuwa anakufa. \p Isa alipokuwa akienda, umati wa watu wakamsonga sana. \v 43 Palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, [na alikuwa amegharimia mali yake yote kwa matibabu]\f + \fr 8:43 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* lakini hakuna yeyote aliyeweza kumponya. \v 44 Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Isa na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma. \p \v 45 Isa akauliza, “Ni nani aliyenigusa?” \p Watu wote walipokana, Petro akasema, “Bwana, umati huu wa watu wanakusonga na kukusukuma kila upande.” \p \v 46 Lakini Isa akasema, “Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka.” \p \v 47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara moja. \v 48 Basi Isa akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” \p \v 49 Isa alipokuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani mwa Yairo, yule kiongozi wa sinagogi, kumwambia, “Binti yako amekwisha kufa. Usiendelee kumsumbua Mwalimu.” \p \v 50 Isa aliposikia jambo hili, akamwambia Yairo, “Usiogope. Amini tu, naye binti yako atapona.” \p \v 51 Walipofika nyumbani mwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, pamoja na baba na mama wa yule binti. \v 52 Wakati ule ule watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili ya huyo binti. Isa akawaambia, “Acheni kulia. Huyu binti hajafa, ila amelala.” \p \v 53 Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa. \v 54 Isa akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!” \v 55 Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja. Akaamuru apewe kitu cha kula. \v 56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote kuhusu yale yaliyotukia. \c 9 \s1 Isa awatuma wale kumi na wawili \r (Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13) \p \v 1 Isa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, \v 2 kisha akawatuma waende wakahubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. \v 3 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. \v 4 Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. \v 5 Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” \v 6 Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali. \s1 Herode afadhaika \r (Mathayo 14:1-12; Marko 6:14-29) \p \v 7 Basi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yahya amefufuliwa kutoka kwa wafu. \v 8 Wengine wakasema Ilya amewatokea, na wengine kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. \v 9 Herode akasema, “Yahya nilimkata kichwa. Lakini ni nani huyu ninayesikia mambo kama haya kumhusu?” Akatamani sana kumwona. \s1 Isa alisha wanaume 5,000 \r (Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Yohana 6:1-14) \p \v 10 Mitume wake waliporudi, wakamweleza Isa yote waliyofanya. Kisha akaenda nao faraghani hadi mji uitwao Bethsaida. \v 11 Lakini umati wa watu wakafahamu alikoenda, wakamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji. \p \v 12 Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage watu hawa ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.” \p \v 13 Isa akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.” \p Nao wakajibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote.” \v 14 (Walikuwepo wanaume wapatao elfu tano.) \p Isa akawaambia wanafunzi wake, “Waketisheni katika vikundi vya watu hamsini hamsini.” \v 15 Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. \v 16 Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavibariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi ili wawagawie watu. \v 17 Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. \s1 Petro amkiri Isa kuwa Al-Masihi \r (Mathayo 16:13-19; Marko 8:27-29) \p \v 18 Siku moja Isa alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?” \p \v 19 Wakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya, wengine husema ni Ilya, na wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka.” \p \v 20 Kisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?” \p Petro akajibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 9:20 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* wa Mungu.” \p \v 21 Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo. \s1 Isa atabiri kifo chake \r (Mathayo 16:21-28; Marko 8:31–9:1) \p \v 22 Isa akasema, “Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa kutoka mauti.” \p \v 23 Kisha akawaambia wote, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake kila siku, anifuate. \v 24 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa. \v 25 Je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au kuangamiza nafsi yake? \v 26 Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba\f + \fr 9:26 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, pamoja na malaika watakatifu. \p \v 27 “Amin, nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu.” \s1 Isa abadilika sura \r (Mathayo 17:1-8; Marko 9:2-8) \p \v 28 Yapata siku nane baada ya Isa kusema hayo, aliwachukua Petro, Yohana na Yakobo, akaenda nao mlimani kuomba. \v 29 Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama miali ya radi. \v 30 Ghafula wakawaona watu wawili, ndio Musa na Ilya, wakizungumza naye. \v 31 Walionekana katika utukufu wakizungumza na Isa kuhusu kifo chake ambacho kingetokea huko Yerusalemu. \v 32 Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Isa na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. \v 33 Musa na Ilya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Isa, “Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya.” Lakini Petro hakujua alichosema. \p \v 34 Alipokuwa bado anazungumza, pakatokea wingu, likawafunika, nao wakaogopa walipoingia mle kwenye wingu. \v 35 Sauti ikatoka kwenye lile wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, niliyemchagua. Msikieni yeye.” \v 36 Baada ya sauti hiyo kusema, walimkuta Isa akiwa peke yake. Wale wanafunzi wakalihifadhi jambo hili, wala kwa wakati huo hawakumwambia mtu yeyote yale waliyokuwa wameyaona. \s1 Isa amponya kijana mwenye pepo mchafu \r (Mathayo 17:14-21; Marko 9:14-29) \p \v 37 Kesho yake waliposhuka kutoka mlimani, alikutana na umati mkubwa wa watu. \v 38 Mtu mmoja katika umati ule akapaza sauti, akasema, “Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, kwani ndiye mtoto wangu wa pekee. \v 39 Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige mayowe, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache. \v 40 Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza.” \p \v 41 Isa akawajibu, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia hadi lini? Mlete mwanao hapa.” \p \v 42 Hata yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo mchafu akamwangusha, akamtia kifafa. Lakini Isa akamkemea yule pepo mchafu amtoke, akamponya yule mtoto, na akamrudisha kwa baba yake. \v 43 Watu wote wakastaajabia uweza mkuu wa Mungu. \p Wakati bado watu walikuwa wanastaajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Isa, yeye akawaambia wanafunzi wake: \v 44 “Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu.” \v 45 Lakini wao hawakuelewa alimaanisha nini. Maana ya maneno hayo ilifichika kwao, hivyo hawakuyaelewa, nao wakaogopa kumuuliza maana yake. \s1 Ni nani atakayekuwa mkuu \r (Mathayo 18:1-5; Marko 9:33-37; Luka 22:24-30) \p \v 46 Kukazuka mabishano miongoni mwa wanafunzi kuhusu ni nani miongoni mwao atakayekuwa mkuu kuliko wote. \v 47 Lakini Isa akayatambua mawazo yao, naye akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha kando yake. \v 48 Kisha akawaambia, “Yeyote amkaribishaye mtoto huyu mdogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi, na yeyote atakayenikaribisha mimi, atakuwa amemkaribisha yeye aliyenituma. Kwa maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu, ndiye aliye mkuu kuliko wote.” \s1 Yeyote asiye kinyume nasi yuko upande wetu \r (Marko 9:38-41) \p \v 49 Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.” \p \v 50 Isa akasema, “Msimzuie, kwa sababu yeyote ambaye si kinyume nanyi, yu upande wenu.” \ms1 Safari ya Isa kwenda Yerusalemu \mr (Luka 9:51–19:44) \s1 Isa akataliwa Samaria \p \v 51 Wakati ulipokaribia wa yeye kuchukuliwa mbinguni, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu. \v 52 Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu; \v 53 lakini watu wa kijiji kile hawakumkaribisha kwa sababu alikuwa anaenda zake Yerusalemu. \v 54 Wanafunzi wake, yaani Yakobo na Yohana, walipoona hayo, wakasema: “Bwana Isa, unataka tuagize moto kutoka mbinguni ili uwaangamize?” \v 55 Isa akageuka na kuwakemea. \v 56 Naye Isa na wanafunzi wake wakaenda kijiji kingine. \s1 Gharama ya kumfuata Isa \r (Mathayo 8:19-22) \p \v 57 Walipokuwa njiani wakienda, mtu mmoja akamwambia Isa, “Nitakufuata popote utakakoenda.” \p \v 58 Isa akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.” \p \v 59 Isa akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” \p Mtu huyo akamjibu, “Bwana\f + \fr 9:59 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” \p \v 60 Isa akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu.” \p \v 61 Mtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikawaage jamaa zangu.” \p \v 62 Isa akamwambia, “Mtu yeyote ashikaye jembe kulima kisha akatazama nyuma hafai kwa ufalme wa Mungu.” \c 10 \s1 Isa awatuma sabini na wawili \p \v 1 Baada ya hayo, Bwana Isa akawachagua wengine sabini na wawili, akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda baadaye. \v 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno. \v 3 Nendeni! Tazama ninawatuma kama wana-kondoo katikati ya mbwa-mwitu. \v 4 Msichukue mkoba, wala mfuko, wala viatu, na msimsalimu mtu yeyote njiani. \p \v 5 “Mkiingia katika nyumba yoyote, kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ \v 6 Kama kuna mtu wa amani humo, basi amani yenu itakuwa juu yake. La sivyo, itawarudia. \v 7 Kaeni katika nyumba hiyo, mkila na kunywa kile watakachowapa, kwa sababu kila mtendakazi anastahili malipo yake. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba. \p \v 8 “Mkienda katika mji na watu wake wakawakaribisha, kuleni chochote kiwekwacho mbele yenu, \v 9 waponyeni wagonjwa waliomo na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umewakaribia.’ \v 10 Lakini mkiingia katika mji, nao hawakuwakaribisha, tokeni mwende katika barabara zake mkaseme: \v 11 ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoshikamana na miguu yetu, tunayakung’uta dhidi yenu. Lakini mjue kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.’ \v 12 Ninawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma kustahimili katika siku ile kuliko mji ule. \s1 Onyo kwa miji isiyotubu \r (Mathayo 11:20-24) \p \v 13 “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani, kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. \v 14 Lakini itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili katika siku ya hukumu, kuliko ninyi. \v 15 Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha! Utashushwa hadi Kuzimu\f + \fr 10:15 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Hades\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa mahali pa wafu.\fqa*\f*. \p \v 16 “Yeye awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi; naye awakataaye ninyi amenikataa mimi. Lakini yeye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.” \p \v 17 Wale sabini na wawili wakarudi kwa furaha, na kusema, “Bwana Isa, hata pepo wachafu wanatutii kwa jina lako.” \p \v 18 Isa akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi. \v 19 Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na juu ya nguvu zote za adui; wala hakuna kitu chochote kitakachowadhuru. \v 20 Basi, msifurahi kwa kuwa pepo wachafu wanawatii, bali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.” \s1 Hakuna amjuaye Baba ila Mwana \r (Mathayo 11:25-27; 13:16-17) \p \v 21 Wakati huo Isa akashangilia katika Roho wa Mungu, akasema, “Nakuhimidi Baba\f + \fr 10:21 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza. \p \v 22 “Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu. Hakuna mtu amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ni nani ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.” \p \v 23 Basi Isa akawageukia wanafunzi wake akanena nao faraghani, akawaambia, “Heri macho yanayoona yale mambo mnayoyaona. \v 24 Kwa maana nawaambia, manabii wengi na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia.” \s1 Mfano wa Msamaria mwema \p \v 25 Wakati huo mtaalamu mmoja wa Torati alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” \p \v 26 Isa akamjibu, “Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?” \p \v 27 Akajibu, “ ‘Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ” \p \v 28 Isa akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.” \p \v 29 Lakini yule mtaalamu wa Torati, akitaka kujionesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Isa, “Jirani yangu ni nani?” \p \v 30 Isa akamjibu akasema, “Mtu mmoja alikuwa akiteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, naye akaangukia mikononi mwa wanyang’anyi. Wakampiga, wakaondoka, wakamwacha akiwa karibu kufa. \v 31 Kuhani mmoja alikuwa akipitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani. \v 32 Vivyo hivyo, Mlawi mmoja naye alipofika mahali pale, alimwona, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani. \v 33 Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri alipomwona, alimhurumia. \v 34 Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka hadi kwenye nyumba ya wageni na kumtunza. \v 35 Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili\f + \fr 10:35 \fr*\ft Dinari mbili ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku mbili.\ft*\f* akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yoyote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’ \p \v 36 “Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyang’anyi?” \p \v 37 Yule mtaalamu wa Torati akajibu, “Ni yule aliyemhurumia.” \p Ndipo Isa akamwambia, “Nenda, ukafanye vivyo hivyo.” \s1 Isa awatembelea Martha na Mariamu \p \v 38 Ikawa Isa na wanafunzi wake walipokuwa wakienda Yerusalemu, akaingia kwenye kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani mwake. \v 39 Martha alikuwa na dada yake aliyeitwa Mariamu, ambaye aliketi chini miguuni mwa Bwana Isa akisikiliza yale alikuwa akisema. \v 40 Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Isa na kumuuliza, “Bwana, hujali kwamba dada yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.” \p \v 41 Lakini Bwana Isa akamjibu, “Martha, Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? \v 42 Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.” \c 11 \s1 Isa afundisha wanafunzi wake kuomba \r (Mathayo 6:9-13) \p \v 1 Siku moja, Isa alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana Isa, tufundishe kuomba, kama vile Yahya alivyowafundisha wanafunzi wake.” \p \v 2 Akawaambia, “Mnapoomba, semeni: \q1 “ ‘Baba yetu [uliye mbinguni]\f + \fr 11:2 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*, \q1 jina lako litukuzwe, \q2 ufalme wako uje. [ \q1 Mapenzi yako yafanyike \q2 hapa duniani kama huko mbinguni.]\f + \fr 11:2 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \q1 \v 3 Utupatie kila siku riziki yetu. \q1 \v 4 Utusamehe dhambi zetu, \q2 kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. \q1 Wala usitutie majaribuni \q2 [bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu]\f + \fr 11:4 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*.’ ” \p \v 5 Kisha akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu mwenye rafiki yake, naye akamwendea usiku wa manane na kumwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu, \v 6 kwa sababu rafiki yangu amekuja kutoka safarini, nami sina kitu cha kumpa ale.’ \p \v 7 “Kisha yule aliye ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe chochote.’ \v 8 Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji. \s1 Omba, tafuta, bisha \r (Mathayo 7:7-12) \p \v 9 “Kwa hiyo nawaambia: Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. \v 10 Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango. \p \v 11 “Je, kuna baba yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? \v 12 Au mtoto akimwomba yai atampa nge? \v 13 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wa Mungu wale wamwombao!” \s1 Isa na Beelzebuli \r (Mathayo 12:22-30; Marko 3:20-27) \p \v 14 Basi Isa alikuwa anamtoa pepo mchafu kutoka kwa mtu aliyekuwa bubu. Yule pepo mchafu alipomtoka yule mtu aliyekuwa bubu, akaanza kuongea, nao umati wa watu wakashangaa. \v 15 Lakini wengine wakasema, “Anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli\f + \fr 11:15 \fr*\ft au \ft*\fqa Beelzebubu\fqa*\ft ; pia \+xt 11:18, 19\+xt*\ft*\f*, yule mkuu wa pepo wachafu wote.” \v 16 Wengine ili kumjaribu wakataka awaoneshe ishara kutoka mbinguni. \p \v 17 Isa akajua mawazo yao, naye akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe itaanguka. \v 18 Kama Shetani amegawanyika mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli. \v 19 Kama mimi natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu nao je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu. \v 20 Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umewajia. \p \v 21 “Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake iko salama. \v 22 Lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye akimshambulia na kumshinda, yeye humnyang’anya silaha zake zote alizozitegemea, na kuchukua nyara. \p \v 23 “Mtu asiyekuwa pamoja nami yu kinyume nami, na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, hutawanya. \s1 Mafundisho kuhusu pepo mchafu \r (Mathayo 12:43-45) \p \v 24 “Pepo mchafu anapomtoka mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ \v 25 Naye anaporudi na kuikuta ile nyumba imefagiwa na kupangwa vizuri, \v 26 ndipo huenda na kuchukua pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza.” \p \v 27 Ikawa Isa alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katikati ya umati ule wa watu akapaza sauti akasema, “Limebarikiwa tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya!” \p \v 28 Isa akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.” \s1 Ishara ya Yona \r (Mathayo 12:38-42) \p \v 29 Umati wa watu walipokuwa wanazidi kuongezeka, Isa akaendelea kusema, “Hiki ni kizazi kiovu. Kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona. \v 30 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki. \v 31 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani. \v 32 Siku ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona. \s1 Taa ya mwili \r (Mathayo 5:15; 6:22-23) \p \v 33 “Hakuna mtu yeyote awashaye taa na kuiweka mahali palipofichika au kuifunikia chini ya bakuli. Badala yake huiweka juu ya kinara chake, ili watu wote wanaoingia waone nuru. \v 34 Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote pia umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote pia umejaa giza. \v 35 Kwa hiyo, hakikisha kwamba nuru iliyo ndani yako isiwe giza. \v 36 Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.” \s1 Isa awashutumu Mafarisayo na wataalamu wa Torati \r (Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40) \p \v 37 Isa alipomaliza kuzungumza, Farisayo\f + \fr 11:37 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* mmoja alimwalika nyumbani mwake kwa chakula. Isa akaingia na kuketi katika sehemu yake mezani. \v 38 Yule Farisayo akashangaa kwamba Isa hakunawa kwanza kabla ya kula. \p \v 39 Ndipo Bwana Isa akamwambia, “Sasa, enyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyang’anyi na uovu. \v 40 Enyi wapumbavu! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza nje ndiye alitengeneza na ndani pia? \v 41 Basi toeni sadaka ya vile mlivyo navyo, na tazama, vitu vyote vitakuwa safi kwenu. \p \v 42 “Lakini ole wenu, Mafarisayo, kwa maana mnampa Mungu zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuuza haki na upendo wa Mungu. Iliwapasa kufanya haya ya pili bila kupuuza hayo ya kwanza. \p \v 43 “Ole wenu Mafarisayo, kwa sababu ninyi mnapenda kukalia viti vya mbele katika masinagogi\f + \fr 11:43 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f*, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. \p \v 44 “Ole wenu, kwa sababu ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.” \p \v 45 Mtaalamu mmoja wa Torati akamjibu, akasema, “Mwalimu, unaposema mambo haya, unatutukana na sisi pia.” \p \v 46 Isa akamjibu, “Nanyi wataalamu wa Torati, ole wenu, kwa sababu mnawatwika watu mizigo mizito ambayo hawawezi kubeba, wala ninyi wenyewe hamwinui hata kidole kimoja kuwasaidia. \p \v 47 “Ole wenu, kwa sababu ninyi mnajenga makaburi ya manabii waliouawa na baba zenu. \v 48 Hivyo ninyi mwashuhudia na mnathibitisha kile baba zenu walichofanya. Wao waliwaua manabii, nanyi mnawajengea makaburi. \v 49 Kwa sababu ya jambo hili, Mungu katika hekima yake alisema, ‘Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na wengine watawatesa.’ \v 50 Kwa hiyo kizazi hiki kitawajibika kwa ajili ya damu ya manabii iliyomwagwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, \v 51 tangu damu ya Habili hadi damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Naam, nawaambia, kizazi hiki kitawajibika kwa haya yote. \p \v 52 “Ole wenu ninyi wataalamu wa Torati, kwa sababu mmeuondoa ufunguo wa maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.” \p \v 53 Isa alipoondoka huko, walimu wa Torati na Mafarisayo wakaanza kumpinga vikali na kumsonga kwa maswali, \v 54 wakivizia kumkamata kwa kitu atakachosema ili wamshtaki. \c 12 \s1 Maonyo dhidi ya unafiki \r (Mathayo 10:26-33) \p \v 1 Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Isa akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki wao. \v 2 Hakuna jambo lolote lililositirika ambalo halitafunuliwa, au lililofichwa ambalo halitajulikana. \v 3 Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonong’ona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa. \p \v 4 “Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. \v 5 Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo! \v 6 Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao. \v 7 Naam, hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi. \p \v 8 “Ninawaambia kwamba yeyote atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri mbele za malaika wa Mungu. \v 9 Lakini yeye atakayenikana mimi mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkana mbele ya malaika wa Mungu. \v 10 Naye kila atakayenena neno baya dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa. \p \v 11 “Watakapowapeleka katika masinagogi, na mbele ya watawala na wenye mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu namna mtakavyojitetea au mtakavyosema. \v 12 Kwa maana Roho wa Mungu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.” \s1 Mfano wa tajiri mpumbavu \p \v 13 Mtu mmoja katika umati ule wa watu akamwambia Isa, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu tugawane naye urithi wetu.” \p \v 14 Lakini Isa akamwambia, “Rafiki, ni nani aliyeniweka mimi kuwa hakimu wenu au msuluhishi juu yenu?” \v 15 Ndipo Isa akawaambia, “Jihadharini! Jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana maisha ya mtu hayatokani na wingi wa mali alizo nazo.” \p \v 16 Kisha akawaambia mfano huu: “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana. \v 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Sina mahali pa kuhifadhi mavuno yangu.’ \p \v 18 “Ndipo huyo tajiri akasema, ‘Nitafanya hivi: Nitabomoa maghala yangu ya nafaka na kujenga mengine makubwa zaidi na nihifadhi mavuno yangu yote na vitu vyangu. \v 19 Nami nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, unavyo vitu vingi vizuri ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi. Pumzika; kula, unywe, ufurahi.” ’ \p \v 20 “Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?’ \p \v 21 “Hivyo ndivyo ilivyo kwa wale wanaojiwekea mali lakini hawajitajirishi kwa Mungu.” \s1 Msiwe na wasiwasi \r (Mathayo 6:25-34) \p \v 22 Kisha Isa akawaambia wanafunzi wake: “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini. \v 23 Maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi. \v 24 Fikirini ndege! Wao hawapandi wala hawavuni, hawana ghala wala popote pa kuhifadhi nafaka; lakini Mungu huwalisha. Ninyi ni wa thamani kuliko ndege! \v 25 Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake? \v 26 Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo, kwa nini basi kuyasumbukia hayo mengine? \p \v 27 “Angalieni maua jinsi yameavyo: Hayafanyi kazi wala hayafumi. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo maua. \v 28 Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo, na kesho yanatupwa motoni, si atawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba! \v 29 Wala msisumbuke mioyoni mwenu mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. \v 30 Watu wa mataifa ya duniani husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote, lakini Baba\f + \fr 12:30 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yenu anafahamu kuwa mnahitaji haya yote. \v 31 Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia. \s1 Kuweka hazina mbinguni \r (Mathayo 6:19-21) \p \v 32 “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi ufalme. \v 33 Uzeni mali yenu mkawape maskini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, ambapo mwizi hakaribii wala nondo haharibu. \v 34 Kwa sababu mahali hazina yako ilipo, hapo ndipo moyo wako utakapokuwa pia. \s1 Kukesha \r (Mathayo 25:1-13) \p \v 35 “Kuweni tayari mkiwa mmevikwa kwa ajili ya huduma na taa zenu zikiwa zinawaka, \v 36 kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka karamu ya arusi, ili ajapo na kubisha mlango waweze kumfungulia mara moja. \v 37 Heri wale watumishi ambao bwana wao atakapokuja atawakuta wakiwa wanakesha. Amin, nawaambia, atajifunga mkanda wake na kuwaketisha ili wale, naye atakuja na kuwahudumia. \v 38 Itakuwa heri kwa watumwa hao ikiwa bwana wao atakapokuja atawakuta wamekesha hata kama atakuja usiku wa manane, au karibu na mapambazuko. \v 39 Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua saa mwizi atakuja, hangeiacha nyumba yake kuvunjwa. \v 40 Ninyi nanyi hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.” \s1 Mfano wa mtumishi mwaminifu \r (Mathayo 24:45-51) \p \v 41 Ndipo Petro akamuuliza, “Bwana Isa, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?” \p \v 42 Isa akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa? \v 43 Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. \v 44 Amin nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. \v 45 Lakini kama yule mtumishi atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga wale watumishi, wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa. \v 46 Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. Atamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wale wasioamini. \p \v 47 “Yule mtumishi anayefahamu vyema mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, atapigwa kwa mapigo mengi. \v 48 Lakini yeyote ambaye hakujua naye akafanya yale yastahiliyo kupigwa, atapigwa kidogo. Yeyote aliyepewa vitu vingi, atadaiwa vingi; na yeyote aliyekabidhiwa vingi, kwake vitatakiwa vingi. \s1 Isa kuleta mafarakano \r (Mathayo 10:34-36) \p \v 49 “Nimekuja kuleta moto duniani; laiti kama ungekuwa tayari umewashwa! \v 50 Lakini ninao ubatizo ambao lazima nibatizwe, nayo dhiki yangu ni kuu hadi ubatizo huo ukamilike! \v 51 Mnadhani nimekuja kuleta amani duniani? La, nawaambia sivyo, nimekuja kuleta mafarakano. \v 52 Kuanzia sasa, kutakuwa na watu watano katika nyumba moja, watatu dhidi ya wawili, na wawili dhidi ya watatu. \v 53 Watafarakana baba dhidi ya mwanawe na mwana dhidi ya babaye, mama dhidi ya bintiye na binti dhidi ya mamaye, naye mama mkwe dhidi ya mkwewe na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.” \s1 Kutambua majira \r (Mathayo 16:1-3) \p \v 54 Pia Isa akaambia umati ule wa watu, “Mwonapo wingu likitokea magharibi, mara mwasema, ‘Mvua itanyesha,’ nayo hunyesha. \v 55 Nanyi mwonapo upepo wa kusini ukivuma, ninyi husema, ‘Kutakuwa na joto,’ na huwa hivyo. \v 56 Enyi wanafiki! Mnajua jinsi ya kutambua kuonekana kwa dunia na anga. Inakuwaje basi kwamba mnashindwa kutambua wakati huu wa sasa? \p \v 57 “Kwa nini hamwamui wenyewe lililo haki? \v 58 Ukiwa njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani. \v 59 Nakuambia, hutatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho.” \c 13 \s1 Tubu au utaangamia \p \v 1 Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Isa habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa. \v 2 Isa akawauliza, “Mnadhani kwamba hawa Wagalilaya ambao walikufa kifo kama hicho walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? \v 3 La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo. \v 4 Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote walioishi Yerusalemu? \v 5 Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.” \s1 Mfano wa mti usiozaa matunda \p \v 6 Kisha Isa akawaambia mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaja ili kutafuta tini kwenye mti huo, lakini hakupata hata moja. \v 7 Hivyo akamwambia mtunza shamba: ‘Tazama, kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, nami sikupata hata moja. Ukate! Kwa nini uendelee kuharibu ardhi?’ \p \v 8 “Yule mtunza shamba akamjibu, ‘Bwana, uuache tena kwa mwaka mmoja zaidi, nami nitaupalilia na kuuwekea mbolea. \v 9 Nao ukizaa matunda mwaka ujao, vyema! La sivyo, uukate.’ ” \s1 Isa amponya mwanamke kilema siku ya Sabato \p \v 10 Basi Isa alikuwa akifundisha katika sinagogi\f + \fr 13:10 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* mojawapo siku ya Sabato. \v 11 Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na nane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima. \v 12 Isa alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” \v 13 Isa alipomwekea mikono yake, akasimama wima mara moja, akaanza kumtukuza Mungu. \p \v 14 Lakini kiongozi wa sinagogi akakasirika kwa sababu Isa alikuwa ameponya mtu siku ya Sabato. Akaambia umati ule wa watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi. Katika siku hizo, njooni mponywe, lakini si katika siku ya Sabato.” \p \v 15 Lakini Bwana Isa akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato? \v 16 Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti ya Ibrahimu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na nane, hakustahili kufunguliwa kutoka kifungo hicho siku ya Sabato?” \p \v 17 Aliposema haya, wapinzani wake wakaaibika, lakini watu wakafurahi kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyoyafanya. \s1 Mfano wa punje ya haradali \r (Mathayo 13:31-32; Marko 4:30-32) \p \v 18 Kisha Isa akauliza, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaufananisha na nini? \v 19 Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti, nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.” \s1 Mfano wa chachu \r (Mathayo 13:33) \p \v 20 Isa akauliza tena, “Nitaufananisha ufalme wa Mungu na nini? \v 21 Unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga hadi wote ukaumuka.” \s1 Siwajui ninyi, wala mtokako \r (Mathayo 7:13-14, 21-23) \p \v 22 Isa akapita katika miji na vijiji, akifundisha wakati alisafiri kwenda Yerusalemu. \v 23 Mtu mmoja akamuuliza, “Bwana Isa, ni watu wachache tu watakaookolewa?” \p Isa akawaambia, \v 24 “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza. \v 25 Mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’ \p “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’ \p \v 26 “Ndipo mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, tena ulifundisha katika mitaa yetu.’ \p \v 27 “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’ \p \v 28 “Ndipo kutakuwako kilio na kusaga meno, mtakapowaona Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii wote wakiwa katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi mkiwa mmetupwa nje. \v 29 Watu watatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, nao wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa karamuni katika ufalme wa Mungu. \v 30 Tazama, kuna walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, nao wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.” \s1 Isa aomboleza kwa ajili ya Yerusalemu \r (Mathayo 23:37-39) \p \v 31 Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo\f + \fr 13:31 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakamwendea Isa na kumwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” \p \v 32 Isa akawajibu, “Nendeni mkamwambie yule mbweha, ‘Ninafukuza pepo wachafu na kuponya wagonjwa leo na kesho, nami siku ya tatu nitaikamilisha kazi yangu.’ \v 33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa: kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu. \p \v 34 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka! \v 35 Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. Ninawaambia, hamtaniona tena hadi wakati ule mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Mwenyezi Mungu.’ ” \c 14 \s1 Isa nyumbani mwa Farisayo \p \v 1 Siku moja ya Sabato, Isa alipoenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimchunguza kwa makini. \v 2 Hapo mbele yake palikuwa na mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba mwili. \v 3 Isa akawauliza wale Mafarisayo na walimu wa Torati, “Je, ni halali kuponya watu siku ya Sabato au la?” \v 4 Wakakaa kimya. Hivyo Isa akamshika yule mgonjwa mkono na kumponya, akamruhusu aende zake. \p \v 5 Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng’ombe wake aliyetumbukia katika kisima siku ya Sabato, je, hamtamvuta mara moja na kumtoa?” \v 6 Nao hawakuwa na la kusema. \s1 Unyenyekevu na ukarimu \p \v 7 Alipoona jinsi wageni walivyokuwa wanachagua mahali pa heshima wakati wa kula, akawaambia mfano huu: \v 8 “Mtu akikualika arusini, usikae mahali pa mgeni wa heshima kwa kuwa inawezekana amealikwa mtu mheshimiwa kuliko wewe. \v 9 Mkifanya hivyo, yule aliyewaalika ninyi wawili atakuja na kukuambia, ‘Mpishe huyu mtu kiti chako.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kukaa katika nafasi ya chini kabisa. \v 10 Badala yake, unapoalikwa, chagua nafasi ya chini, ili yule aliyekualika atakapokuona, atakuja na kukuambia, ‘Rafiki yangu, nenda kwenye nafasi iliyo bora zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wenzako wote. \v 11 Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.” \p \v 12 Kisha Isa akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo karamu ya chakula cha mchana au cha jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako walio matajiri tu. Ukifanya hivyo, nao wanaweza kukualika kwao, nawe ukawa umepata malipo. \v 13 Bali unapoandaa karamu, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu, \v 14 nawe utabarikiwa kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa. Mungu atakulipa wakati wa ufufuo wa wenye haki.” \s1 Mfano wa karamu kuu \r (Mathayo 22:1-10) \p \v 15 Mmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Isa, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya ufalme wa Mungu!” \p \v 16 Isa akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. \v 17 Wakati wa karamu ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaambie wale walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ki tayari sasa.’ \p \v 18 “Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ \p \v 19 “Mwingine akasema, ‘Ndipo tu nimenunua jozi tano za ng’ombe wa kulimia, nami ninaenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ \p \v 20 “Naye mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’ \p \v 21 “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwagiza yule mtumishi wake, akisema, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’ \p \v 22 “Yule mtumishi akamwambia, ‘Bwana, yale uliyoniagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ \p \v 23 “Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na vijia vilivyo nje ya mji na uwalazimishe watu waingie ili nyumba yangu ijae. \v 24 Kwa maana nawaambia, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeionja karamu yangu.’ ” \s1 Gharama ya kuwa mwanafunzi \r (Mathayo 10:37-38) \p \v 25 Umati mkubwa wa watu walikuwa wakisafiri pamoja na Isa, naye akageuka, akawaambia, \v 26 “Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. \v 27 Yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. \p \v 28 “Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? \v 29 La sivyo, baada ya kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, \v 30 wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’ \p \v 31 “Au je, mfalme fulani akienda vita na mfalme mwingine, si yeye huketi chini kwanza na kufikiri: je, akiwa na jeshi la watu elfu kumi, ataweza kupigana na yule anayekuja na jeshi la watu elfu ishirini? \v 32 Ikiwa hawezi, basi yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma wajumbe na kuomba masharti ya amani. \v 33 Vivyo hivyo, yeyote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. \s1 Chumvi isiyofaa \r (Mathayo 5:13; Marko 9:50) \p \v 34 “Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, itafanywaje ili iweze kukolea tena? \v 35 Haifai ardhi wala kwa lundo la mbolea, bali hutupwa nje. \p “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” \c 15 \s1 Mfano wa kondoo aliyepotea \r (Mathayo 18:10-14) \p \v 1 Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Isa. \v 2 Lakini Mafarisayo\f + \fr 15:2 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na walimu wa Torati wakanung’unika wakisema, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao.” \p \v 3 Ndipo Isa akawaambia mfano huu: \v 4 “Ikiwa mmoja wenu ana kondoo mia moja, naye akapoteza mmoja wao, je, hawaachi wale tisini na tisa nyikani na kwenda kumtafuta huyo aliyepotea hadi ampate? \v 5 Naye akishampata, humbeba mabegani mwake kwa furaha \v 6 na kwenda nyumbani. Kisha huwaita rafiki zake na majirani, na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’ \v 7 Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu. \s1 Mfano wa sarafu iliyopotea \p \v 8 “Au ikiwa mwanamke ana sarafu za fedha kumi, naye akapoteza moja, je, hawashi taa na kufagia nyumba na kuitafuta kwa bidii hadi aipate? \v 9 Baada ya kuipata, yeye huwaita rafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile sarafu yangu ya fedha iliyopotea.’ \v 10 Vivyo hivyo, nawaambia, kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu juu ya mwenye dhambi mmoja atubuye.” \s1 Mfano wa mwana mpotevu \p \v 11 Isa akaendelea kusema: “Kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili. \v 12 Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Hivyo akawagawia wanawe mali yake. \p \v 13 “Baada ya muda mfupi, yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo, akaenda nchi ya mbali, na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. \v 14 Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote, naye akawa hana chochote. \v 15 Kwa hiyo akaenda akaajiriwa na raia mmoja wa nchi ile ambaye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. \v 16 Akatamani kujishibisha kwa maganda waliyokula wale nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa chochote. \p \v 17 “Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa! \v 18 Nitaondoka na kurudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimetenda dhambi mbele za Mungu na mbele yako. \v 19 Sistahili tena kuitwa mwanao; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ \v 20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. \p “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu. \p \v 21 “Yule mwana akamwambia baba yake, ‘Baba, nimekosa mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’ \p \v 22 “Lakini baba yake akawaambia watumishi, ‘Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake. \v 23 Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi. \v 24 Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa na sasa yu hai tena; alikuwa amepotea na sasa amepatikana!’ Nao wakaanza kusherehekea. \p \v 25 “Wakati huo, yule mwana mkubwa alikuwa shambani. Alipokaribia nyumbani, akasikia sauti ya nyimbo na watu wakicheza. \v 26 Akamwita mmoja wa watumishi na kumuuliza maana ya mambo yale. \v 27 Akamwambia, ‘Ndugu yako amekuja, naye baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu mwanawe amerudi nyumbani akiwa salama na mzima.’ \p \v 28 “Yule mwana mkubwa akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje na kumsihi. \v 29 Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Tazama! Miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana-mbuzi ili nifurahi na rafiki zangu. \v 30 Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba aliporudi nyumbani, wewe umemchinjia ndama aliyenona!’ \p \v 31 “Baba yake akamjibu, ‘Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako. \v 32 Lakini ilitubidi tufurahi na kushangilia kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa na sasa yu hai; alikuwa amepotea naye amepatikana.’ ” \c 16 \s1 Mfano wa msimamizi mjanja \p \v 1 Isa akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na msimamizi wake. Huyo msimamizi alishitakiwa kwake kwamba alikuwa akitapanya mali ya tajiri yake. \v 2 Hivyo huyo tajiri akamwita na kumuuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’ \p \v 3 “Yule msimamizi akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu ananiondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, nami ninaona aibu kuombaomba. \v 4 Najua nitakalofanya ili nikiachishwa kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani mwao.’ \p \v 5 “Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa bwana wake, mmoja mmoja. Akamuuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ \p \v 6 “Akajibu, ‘Vipimo mia moja\f + \fr 16:6 \fr*\ft ni kama lita elfu nne\ft*\f* vya mafuta ya mizeituni.’ \p “Msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati ya deni lako, ibadilishe upesi, uandike vipimo hamsini.’ \p \v 7 “Kisha akamuuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’ \p “Akajibu, ‘Vipimo elfu moja\f + \fr 16:7 \fr*\ft ni kama magunia mia moja\ft*\f* vya ngano.’ \p “Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, uandike vipimo mia nane!’ \p \v 8 “Yule bwana akamsifu yule msimamizi dhalimu kwa jinsi alivyotumia ujanja. Kwa maana watu wa dunia hii wana ujanja zaidi wanapojishughulisha na mambo ya dunia kuliko watu wa nuru. \v 9 Nawaambia, tumieni mali ya dunia kujipatia rafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele. \p \v 10 “Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, pia ni mwaminifu katika mambo makubwa. Na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo pia si mwaminifu katika mambo makubwa. \v 11 Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya kidunia, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli? \v 12 Nanyi kama hamkuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? \p \v 13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali\f + \fr 16:13 \fr*\ft au \ft*\fqa Utajiri\fqa*\ft ; yaani \ft*\fqa Mamoni \fqa*\ft kwa Kiaramu au \ft*\fqa Mamona \fqa*\ft kwa Kiyunani\ft*\f*.” \p \v 14 Mafarisayo, waliokuwa wapenda fedha, waliyasikia hayo yote na wakamcheka kwa dharau. \v 15 Isa akawaambia, “Ninyi mnajionesha kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu ni machukizo. \s1 Torati na Ufalme wa Mwenyezi Mungu \p \v 16 “Torati na Manabii vilihubiriwa hadi kuja kwa Yahya. Tangu wakati huo Injili ya ufalme wa Mungu inahubiriwa, na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu. \v 17 Lakini ni rahisi zaidi mbingu na dunia kupita kuliko hata herufi moja kuondoka katika Torati. \p \v 18 “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kumwoa mwanamke mwingine anazini, naye mwanaume amwoaye mwanamke aliyetalikiwa anazini. \s1 Tajiri na Lazaro \p \v 19 “Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa kila siku. \v 20 Hapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima. \v 21 Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kuramba vidonda vyake. \p \v 22 “Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa. \v 23 Kule Kuzimu\f + \fr 16:23 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiyunani ni \ft*\fqa Hades\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa mahali pa wafu.\fqa*\f* alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa kifuani mwake. \v 24 Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’ \p \v 25 “Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu. \v 26 Zaidi ya hayo, kati yetu na ninyi huko kumewekwa shimo kubwa, ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko wasiweze, wala mtu yeyote asiweze kuvuka kutoka huko kuja kwetu.’ \p \v 27 “Akasema, ‘Basi, nakuomba, umtume Lazaro aende nyumbani mwa baba yangu, \v 28 maana ninao ndugu watano. Awaonye, ili wasije nao wakafika mahali hapa pa mateso.’ \p \v 29 “Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wana Maandiko ya Musa na Manabii, wawasikilize hao.’ \p \v 30 “Yule tajiri akasema, ‘Hapana, baba Ibrahimu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.’ \p \v 31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Musa na Manabii, hawataweza kushawishika hata kama mtu akifufuka kutoka kwa wafu.’ ” \c 17 \s1 Kujaribiwa ili kutenda dhambi \r (Mathayo 18:6-7, 21-22; Marko 9:42) \p \v 1 Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. \v 2 Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmoja wa hawa wadogo kutenda dhambi. \v 3 Kwa hiyo, jilindeni. \p “Ndugu yako akikukosea, mwonye; naye akitubu, msamehe. \v 4 Akikukosea mara saba kwa siku moja, na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe.” \s1 Imani \p \v 5 Mitume wake wakamwambia Bwana, “Tuongezee imani.” \p \v 6 Bwana akawajibu, “Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii. \s1 Wajibu wa mtumishi \p \v 7 “Ikiwa mmoja wenu ana mtumishi anayelima shambani au anayechunga kondoo, je, mtumishi huyo arudipo atamwambia, ‘Karibu hapa keti ule chakula’? \v 8 Je, badala yake, hatamwambia, ‘Niandalie chakula, nile, jifunge unitumikie ninapokula na kunywa; baadaye unaweza kula na kunywa’? \v 9 Je, huyo mtu atamshukuru mtumishi huyo kwa kutimiza yale aliyoamriwa? \v 10 Vivyo hivyo nanyi mkishafanya mliyoagizwa, semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili; tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’ ” \s1 Isa atakasa watu kumi wenye ukoma \p \v 11 Isa alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. \v 12 Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, \v 13 wakapaza sauti, wakasema, “Isa, Bwana, tuhurumie!” \p \v 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajioneshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika. \p \v 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Isa, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. \v 16 Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria. \p \v 17 Isa akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? \v 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?” \v 19 Isa akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.” \s1 Kuja kwa Ufalme wa Mwenyezi Mungu \r (Mathayo 24:23-28, 37-41) \p \v 20 Isa alipoulizwa na Mafarisayo\f + \fr 17:20 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* ufalme wa Mungu utakuja lini, yeye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuchunguza kwa bidii, \v 21 wala watu hawatasema, ‘Huu hapa,’ au ‘Ule kule,’ kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” \p \v 22 Kisha Isa akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. \v 23 Watu watawaambia, ‘Yule kule!’ au, ‘Huyu hapa!’ Msiwakimbilie. \v 24 Kwa maana kama vile radi imulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. \v 25 Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki. \p \v 26 “Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Adamu. \v 27 Watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, hadi siku ile Nuhu alipoingia katika safina. Ndipo gharika ikaja na kuwaangamiza wote. \p \v 28 “Ndivyo ilivyokuwa katika siku za Lutu: Watu walikuwa wakila na kunywa, wakinunua na kuuza, wakilima na kujenga. \v 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ukawaangamiza wote. \p \v 30 “Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. \v 31 Siku hiyo, mtu yeyote aliye juu ya dari ya nyumba yake, hata vitu vyake vikiwa ndani ya hiyo nyumba, asishuke kuvichukua. Vivyo hivyo mtu aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua chochote. \v 32 Mkumbukeni mke wa Lutu! \v 33 Mtu yeyote anayejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa. \v 34 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa wamelala kitanda kimoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. \v 35 Wanawake wawili watakuwa wanasaga nafaka pamoja; naye mmoja atatwaliwa na mwingine ataachwa. [ \v 36 Wanaume wawili watakuwa wanafanya kazi pamoja shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.]\f + \fr 17:36 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*” \p \v 37 Kisha wakamuuliza, “Haya yatatukia wapi Bwana Isa?” \p Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, huko ndiko tai watakapokusanyika.” \c 18 \s1 Mfano wa mjane asiyekata tamaa \p \v 1 Kisha Isa akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa. \v 2 Akawaambia, “Katika mji mmoja palikuwa hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. \v 3 Katika mji huo alikuwako mjane mmoja aliyekuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ \p \v 4 “Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Ijapokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, \v 5 lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” \p \v 6 Bwana Isa akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. \v 7 Je, Mungu hatawatendea haki wateule wake wanaomlilia usiku na mchana? Je, atakawia kuwasaidia? \v 8 Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” \s1 Mfano wa Farisayo na mtoza ushuru \p \v 9 Isa akatoa mfano huu kwa wale waliojiamini kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine: \v 10 “Watu wawili walienda Hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. \v 11 Yule Farisayo, akasimama, akasali hivi na kuomba kwake mwenyewe: ‘Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang’anyi, wadhalimu, na wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. \v 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma, na natoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ \p \v 13 “Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipigapiga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’ \p \v 14 “Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana yeyote ajikwezaye atashushwa, na yeyote ajishushaye atakwezwa.” \s1 Isa awabariki watoto wadogo \r (Mathayo 19:13-15; Marko 10:13-16) \p \v 15 Pia, watu walikuwa wakimletea Isa watoto wachanga ili awaguse. Wanafunzi wake walipoona hivyo, wakawakemea. \v 16 Lakini Isa akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. \v 17 Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” \s1 Mtawala tajiri \r (Mathayo 19:16-30; Marko 10:17-31) \p \v 18 Mtawala mmoja akamuuliza Isa, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” \p \v 19 Isa akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. \v 20 Unazijua amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.’ ” \p \v 21 Akajibu, “Amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.” \p \v 22 Isa aliposikia haya, akamwambia, “Bado kuna jambo moja ulilopungukiwa. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” \p \v 23 Aliposikia jambo hili, alisikitika sana kwa maana alikuwa mtu mwenye mali nyingi. \v 24 Isa akamtazama, akasema, “Tazama jinsi ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu! \v 25 Hakika ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” \p \v 26 Wale waliosikia haya wakauliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?” \p \v 27 Isa akajibu, “Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” \p \v 28 Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, tumeacha vyote tulivyokuwa navyo tukakufuata!” \p \v 29 Isa akajibu, “Amin, nawaambia, hakuna hata mtu aliyeacha nyumba yake, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu \v 30 ambaye hatapewa mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya, na hatimaye kupata uzima wa milele ujao.” \s1 Isa atabiri tena kifo chake \r (Mathayo 20:17-19; Marko 10:32-34) \p \v 31 Isa akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa. \v 32 Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua. \v 33 Naye siku ya tatu atafufuka.” \p \v 34 Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Isa alikuwa anazungumzia nini. \s1 Isa amponya kipofu karibu na Yeriko \r (Mathayo 20:29-34; Marko 10:46-52) \p \v 35 Isa alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. \v 36 Kipofu huyo aliposikia umati wa watu wakipita, akauliza nini kilikuwa kikitendeka. \v 37 Wakamwambia, “Isa Al-Nasiri anapita.” \p \v 38 Akapaza sauti, akasema, “Isa, Mwana wa Daudi\f + \fr 18:38 \fr*\ft Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (\+xt Zaburi 89:3-4\+xt*).\ft*\f*, nihurumie!” \p \v 39 Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!” \p \v 40 Isa akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Isa akamuuliza, \v 41 “Unataka nikufanyie nini?” \p Akajibu, “Bwana, nataka kuona.” \p \v 42 Isa akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.” \v 43 Akapata kuona mara hiyo, akamfuata Isa, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu. \c 19 \s1 Zakayo mtoza ushuru \p \v 1 Isa akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. \v 2 Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. \v 3 Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Isa ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza, kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. \v 4 Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Isa, kwa sababu angeipitia njia ile. \p \v 5 Isa alipofika pale chini ya huo mkuyu, akatazama juu, akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani mwako!” \v 6 Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Isa nyumbani mwake kwa furaha kubwa. \p \v 7 Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunung’unika wakisema, “Ameenda kuwa mgeni wa mtu mwenye dhambi.” \p \v 8 Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana Isa, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.” \p \v 9 Ndipo Isa akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. \v 10 Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” \s1 Mfano wa fedha \r (Mathayo 25:14-30) \p \v 11 Walipokuwa wanasikiliza haya, Isa akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa hiyo. \v 12 Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. \v 13 Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake, na akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi hadi nitakaporudi.’ \p \v 14 “Lakini raia wa nchi yake walimchukia wakapeleka ujumbe na kusema, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu.’ \p \v 15 “Hata hivyo alirudi akiwa amekwisha kupokea mamlaka ya ufalme, akawaita wale watumishi wake aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu ni faida kiasi gani kila mmoja wao aliyopata kwa kufanya biashara. \p \v 16 “Wa kwanza akaja na kusema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia, nimepata faida mara kumi zaidi.’ \p \v 17 “Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’ \p \v 18 “Wa pili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ \p \v 19 “Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ \p \v 20 “Kisha akaja yule mtumishi mwingine, akasema, ‘Bwana, hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. \v 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mgumu. Unachukua ambapo hukuweka, na kuvuna ambapo hukupanda.’ \p \v 22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwenyewe, wewe mtumishi mwovu! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mgumu, ninayechukua nisichoweka, na kuvuna nisichopanda, \v 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu kwa watoa riba, ili nitakaporudi nichukue iliyo yangu na riba yake?’ \p \v 24 “Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu, ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha, mkampe yule mwenye kumi.’ \p \v 25 “Wakamwambia, ‘Bwana, mbona; tayari anayo mafungu kumi!’ \p \v 26 “Akawajibu, ‘Nawaambia kwamba kila aliye na kitu, ataongezewa. Lakini yule asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang’anywa. \v 27 Lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao. Waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’ ” \s1 Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe \r (Mathayo 21:1-11; Marko 11:1-11; Yohana 12:12-19) \p \v 28 Baada ya Isa kusema haya, alitangulia kupanda kwenda Yerusalemu. \v 29 Naye alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima ulioitwa Mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili, akawaambia, \v 30 “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtampata mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. \v 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.’ ” \p \v 32 Wale waliotumwa wakaenda, wakapata kila kitu kama Isa alivyowaambia. \v 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana-punda, wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?” \p \v 34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” \p \v 35 Wakamleta kwa Isa, nao baada ya kutandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, wakampandisha Isa juu yake. \v 36 Alipokuwa akienda, watu wakatandaza mavazi yao barabarani. \p \v 37 Alipokaribia mahali yanapoanzia miteremko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema: \q1 \v 38 “Amebarikiwa mfalme ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” \b \q1 “Amani mbinguni na utukufu huko juu sana.” \p \v 39 Baadhi ya Mafarisayo\f + \fr 19:39 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* waliokuwamo miongoni mwa umati ule wa watu wakamwambia, “Mwalimu, waamuru wanafunzi wako wanyamaze.” \p \v 40 Isa akawajibu, “Nawaambia ninyi, kama hawa watanyamaza, mawe yatapaza sauti.” \s1 Isa aulilia mji wa Yerusalemu \p \v 41 Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, \v 42 akisema, “Laiti ungejua, hata wewe leo, yale yangeleta amani, lakini sasa yamefichika machoni pako. \v 43 Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. \v 44 Watakuponda chini, wewe na watoto walio ndani ya kuta zako. Nao hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukutambua wakati wa kujiliwa kwako.” \ms1 Huduma ya Isa huko Yerusalemu \mr (Luka 19:45–20:47) \s1 Isa atakasa Hekalu \r (Mathayo 21:12-17; Marko 11:15-19; Yohana 2:13-22) \p \v 45 Ndipo akaingia eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza vitu humo. \v 46 Naye akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyang’anyi.’ ” \p \v 47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Lakini viongozi wa makuhani, walimu wa Torati na viongozi wa watu walikuwa wakitafuta njia ili kumuua. \v 48 Lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote walimfuata wakiyasikiliza maneno yake kwa usikivu mwingi. \c 20 \s1 Swali kuhusu mamlaka ya Isa \r (Mathayo 21:23-27; Marko 11:27-33) \p \v 1 Siku moja, Isa alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri Habari Njema, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, pamoja na wazee wa watu wakamjia. \v 2 Wakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?” \p \v 3 Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. Nijibuni: \v 4 Je, ubatizo wa Yahya ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” \p \v 5 Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ \v 6 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yahya alikuwa nabii.” \p \v 7 Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.” \p \v 8 Isa akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.” \s1 Mfano wa wapangaji waovu \r (Mathayo 21:33-46; Marko 12:1-12) \p \v 9 Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. \v 10 Wakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. \v 11 Akamtuma mtumishi mwingine, huyo naye wakampiga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. \v 12 Bado akamtuma na mwingine wa tatu, huyu pia wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba. \p \v 13 “Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa, huenda yeye watamheshimu.’ \p \v 14 “Lakini wale wapangaji walipomwona, wakasemezana wao kwa wao. Wakasema, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi na tumuue ili urithi uwe wetu.’ \v 15 Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua. \p “Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa? \v 16 Atakuja na kuwaua hao wapangaji, na kuwapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu.” \p Watu waliposikia hayo wakasema, “Mungu apishie mbali jambo hili lisitokee!” \p \v 17 Lakini Isa akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa: \q1 “ ‘Jiwe walilolikataa waashi, \q2 limekuwa jiwe kuu la pembeni’? \m \v 18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.” \p \v 19 Walimu wa Torati na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu. \s1 Swali kuhusu kulipa kodi ya Kaisari \r (Mathayo 22:15-22; Marko 12:13-17) \p \v 20 Kwa hiyo wakawa wanamchunguza na kutuma wapelelezi waliojifanya kuwa wenye haki. Walitaka kumtega kwa maneno yake, ili wampeane katika uwezo na mamlaka ya mtawala. \v 21 Hivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli. \v 22 Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?” \p \v 23 Lakini Isa akatambua hila yao, akawaambia, \v 24 “Nionesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyo juu yake ni vya nani?” \p Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” \p \v 25 Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.” \p \v 26 Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza. \s1 Ndoa wakati wa ufufuo \r (Mathayo 22:23-33; Marko 12:18-27) \p \v 27 Baadhi ya Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza, \v 28 “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. \v 29 Basi kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa, akafa bila kuzaa mtoto. \v 30 Kisha yule wa pili akamwoa huyo mjane, naye akafa bila mtoto, \v 31 naye wa tatu pia akamwoa. Vivyo hivyo ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mwanamke, na wote wakafa pasipo yeyote kupata mtoto. \v 32 Mwishowe, yule mwanamke naye akafa. \v 33 Sasa basi, siku ya ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?” \p \v 34 Isa akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. \v 35 Lakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. \v 36 Hawa hawawezi kufa tena, kwa maana wao ni kama malaika. Wao ni watoto wa Mungu, kwa sababu ni watoto wa ufufuo. \v 37 Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Mwenyezi Mungu, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’ \v 38 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa kuwa kwake wote ni hai.” \p \v 39 Baadhi ya walimu wa Torati wakasema, “Mwalimu, umesema sawasawa kabisa!” \p \v 40 Baada ya hayo hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza maswali tena. \s1 Al-Masihi ni Mwana wa nani? \r (Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37) \p \v 41 Kisha Isa akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Al-Masihi\f + \fr 20:41 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* ni Mwana wa Daudi? \v 42 Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: \q1 “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: \q2 “Keti mkono wangu wa kuume, \q1 \v 43 hadi nitakapowaweka adui zako \q2 chini ya miguu yako.” ’ \m \v 44 Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?” \s1 Isa atahadharisha kuhusu walimu wa Torati \r (Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40) \p \v 45 Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Isa akawaambia wanafunzi wake, \v 46 “Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi\f + \fr 20:46 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f*, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. \v 47 Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.” \c 21 \ms1 Unabii kuhusu mambo yajayo \mr (Luka 21:1-38) \s1 Sadaka ya mjane maskini \r (Marko 12:41-44) \p \v 1 Isa alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. \v 2 Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba. \v 3 Isa akasema, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote. \v 4 Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali yao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.” \s1 Kubomolewa kwa Hekalu kwatabiriwa \r (Mathayo 24:1-2; Marko 13:1-2) \p \v 5 Baadhi ya wanafunzi wake wakawa wanamwonesha jinsi Hekalu lilivyopambwa kwa mawe mazuri na kwa vitu vilivyotolewa kuwa sadaka kwa Mungu. Lakini Isa akawaambia, \v 6 “Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.” \s1 Ishara za nyakati za mwisho \r (Mathayo 24:3-14; Marko 13:3-13) \p \v 7 Wakamuuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatukia lini? Ni dalili gani itaonesha kwamba yanakaribia kutendeka?” \p \v 8 Isa akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate. \v 9 Lakini msikiapo habari za vita na machafuko, msiogope. Kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila ule mwisho hautakuja wakati huo.” \p \v 10 Kisha akawaambia: “Taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme mmoja dhidi ya ufalme mwingine. \v 11 Kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, na njaa kali, na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali. Pia kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni. \p \v 12 “Lakini kabla yote hayajatokea, watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawatia mikononi mwa wakuu wa masinagogi na kuwafunga magerezani. Nanyi mtapelekwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya Jina langu. \v 13 Hii itawapa nafasi ya kushuhudia. \v 14 Lakini kusudieni mioyoni mwenu msisumbuke awali kuhusu mtakalosema mbele ya mashtaka. \v 15 Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo hakuna hata adui yenu mmoja atakayeweza kushindana nayo wala kuipinga. \v 16 Mtasalitiwa hata na wazazi, ndugu, jamaa na rafiki zenu, na baadhi yenu watawaua. \v 17 Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. \v 18 Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. \v 19 Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu. \s1 Kuharibiwa kwa Yerusalemu kwatabiriwa \r (Mathayo 24:15-21; Marko 13:14-19) \p \v 20 “Mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi fahamuni kwamba kuharibiwa kwake kumekaribia. \v 21 Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo, nao wale walio mashambani wasiingie mjini. \v 22 Kwa sababu huu utakuwa ni wakati wa adhabu ili kutimiza yote yaliyoandikwa. \v 23 Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu. \v 24 Wataanguka kwa makali ya upanga, na wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote. Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie. \s1 Kuja kwa Mwana wa Adamu \r (Mathayo 24:29-35; Marko 13:24-31) \p \v 25 “Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari. \v 26 Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za angani zitatikisika. \v 27 Wakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu. \v 28 Mambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.” \s1 Somo kuhusu mtini \r (Mathayo 24:32-35; Marko 13:28-31) \p \v 29 Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. \v 30 Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. \v 31 Vivyo hivyo, mnapoyaona mambo haya yakitukia, mtambue kwamba ufalme wa Mungu umekaribia. \p \v 32 “Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. \v 33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. \s1 Himizo la kukesha \p \v 34 “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama mtego unasavyo. \v 35 Hivyo ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote wanaoishi katika uso wa dunia yote. \v 36 Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.” \p \v 37 Kila siku Isa alikuwa akifundisha Hekaluni, na jioni ilipofika, alienda zake kwenye Mlima wa Mizeituni na kukaa huko usiku kucha. \v 38 Nao watu wote walikuja asubuhi na mapema Hekaluni ili kumsikiliza. \c 22 \ms1 Kufa na kufufuka kwa Isa \mr (Luka 22:1–24:53) \s1 Yuda akubali kumsaliti Isa \r (Mathayo 26:14-16; Marko 14:10-11) \p \v 1 Wakati huu Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia. \v 2 Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wanatafuta njia ya kumuua Isa, kwa sababu waliwaogopa watu. \v 3 Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili. \v 4 Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi angeweza kumsaliti Isa. \v 5 Wakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha. \v 6 Naye akakubali, akaanza kutafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Isa kwao, ambapo hakuna umati wa watu. \s1 Maandalizi ya Pasaka \r (Mathayo 26:17-25; Marko 14:12-21; Yohana 13:21-30) \p \v 7 Basi ikawadia siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa. \v 8 Hivyo Isa akawatuma Petro na Yohana, akisema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuweze kuila.” \p \v 9 Wakamuuliza, “Unataka tukuandalie wapi?” \p \v 10 Isa akawaambia, “Tazameni, mtakapokuwa mkiingia mjini, mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni hadi kwenye nyumba atakayoingia. \v 11 Nanyi mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ \v 12 Atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, kikiwa kimepambwa vizuri. Andaeni humo.” \p \v 13 Wakaenda, nao wakakuta kila kitu kama Isa alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka. \s1 Kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana Isa \r (Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Yohana 13:36-38) \p \v 14 Wakati ulipowadia, Isa akaketi mezani pamoja na wale mitume wake. \v 15 Kisha akawaambia, “Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. \v 16 Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka hadi itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.” \p \v 17 Baada ya kukichukua kikombe, akashukuru, akasema, “Chukueni hiki mnywe wote. \v 18 Kwa maana nawaambia tangu sasa sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi ufalme wa Mungu utakapokuja.” \p \v 19 Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” \p \v 20 Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu. \v 21 Lakini mkono wake huyo atakayenisaliti uko hapa mezani pamoja nami. \v 22 Mwana wa Adamu anaenda zake kama ilivyokusudiwa. Lakini ole wake mtu huyo amsalitiye!” \v 23 Wakaanza kuulizana wenyewe ni nani miongoni mwao angeweza kufanya jambo hilo. \s1 Mabishano kuhusu ukuu \r (Mathayo 18:1-5; Marko 9:33-37; Luka 9:46-48) \p \v 24 Pia yakazuka mabishano katikati ya wanafunzi kwamba ni nani aliyeonekana kuwa mkuu kuliko wote miongoni mwao. \v 25 Isa akawaambia, “Wafalme na watu wa Mataifa huwatawala watu kwa nguvu. Nao wenye mamlaka juu yao hujiita ‘Wafadhili.’ \v 26 Lakini ninyi msifanane nao. Bali yeye aliye mkuu kuliko wote miongoni mwenu, inampasa kuwa kama yeye aliye mdogo wa wote, naye anayetawala na awe kama yeye anayehudumu. \v 27 Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule anayeketi mezani au ni yule anayehudumu? Si ni yule aliyeketi mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule anayehudumu. \v 28 Ninyi mmekuwa pamoja nami katika majaribu yangu. \v 29 Nami kama Baba\f + \fr 22:29 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu alivyonipa ufalme, nami ninawapa ninyi, \v 30 ili mpate kula na kunywa mezani pangu katika karamu ya ufalme wangu, na kukaa katika viti vya utawala, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.” \s1 Isa atabiri kuwa Petro atamkana \r (Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Yohana 13:31-38) \p \v 31 Isa akasema, “Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. \v 32 Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe baada ya kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.” \p \v 33 Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani na hata katika kifo.” \p \v 34 Isa akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika usiku wa leo, utakana mara tatu kwamba unanijua.” \s1 Mfuko, mkoba na upanga \p \v 35 Kisha Isa akawauliza, “Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?” \p Wakajibu, “La, hatukupungukiwa na kitu chochote.” \p \v 36 Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko na auchukue, na aliye na mkoba vivyo hivyo. Naye asiye na upanga, auze joho lake anunue mmoja. \v 37 Kwa sababu, nawaambia, andiko hili lazima litimizwe kunihusu, kwamba, ‘Alihesabiwa pamoja na wakosaji’; kwa kweli yaliyoandikwa kunihusu hayana budi kutimizwa.” \p \v 38 Wanafunzi wake wakamwambia, “Bwana, tazama hapa kuna panga mbili.” \p Akawajibu, “Inatosha.” \s1 Isa aomba kwenye Mlima wa Mizeituni \r (Mathayo 26:36-46; Marko 14:32-42) \p \v 39 Isa akatoka, akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata. \v 40 Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni, msije mkaingia majaribuni.” \v 41 Akajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba \v 42 akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” \v 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. \v 44 Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini. \p \v 45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wakiwa wamechoka kutokana na huzuni. \v 46 Naye akawauliza, “Mbona mmelala? Amkeni, mwombe ili msije mkaingia majaribuni.” \s1 Isa akamatwa \r (Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Yohana 18:1-11) \p \v 47 Isa alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu wakaja. Waliongozwa na Yuda, aliyekuwa mmoja wa wale kumi na wawili. Akamkaribia Isa ili ambusu. \v 48 Lakini Isa akamwambia, “Yuda, je, unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?” \p \v 49 Wafuasi wa Isa walipoona yale yaliyokuwa yanakaribia kutokea, wakasema, “Bwana, tuwakatekate kwa panga zetu?” \v 50 Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume. \p \v 51 Lakini Isa akasema, “Acheni!” Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya. \p \v 52 Kisha Isa akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? \v 53 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi Hekaluni lakini hamkunikamata. Lakini hii ni saa yenu, wakati giza linatawala!” \s1 Petro amkana Isa \r (Mathayo 26:57-75; Marko 14:53-72; Yohana 18:12-27) \p \v 54 Kisha wakamkamata Isa, wakamchukua, wakaenda naye hadi nyumbani mwa kuhani mkuu. Lakini Petro akafuata kwa mbali. \v 55 Walipokwisha kuwasha moto katikati ya ua na kuketi pamoja, Petro naye akaketi pamoja nao. \v 56 Mjakazi mmoja akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Isa!” \p \v 57 Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” \p \v 58 Baadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!” \p \v 59 Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, “Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Isa, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” \p \v 60 Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika. \v 61 Naye Bwana Isa akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” \v 62 Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi. \s1 Walinzi wamdhihaki Isa na kumpiga \r (Mathayo 26:67-68; Marko 14:65) \p \v 63 Watu waliokuwa wanamlinda Isa wakaanza kumdhihaki na kumpiga. \v 64 Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” \v 65 Wakaendelea kumtukana kwa matusi mengi. \s1 Isa mbele ya Baraza la Wayahudi \r (Mathayo 26:59-66; Marko 14:55-64; Yohana 18:28-38) \p \v 66 Kulipopambazuka, Baraza la Wazee, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, wakakutana pamoja, naye Isa akaletwa mbele yao. \v 67 Wakamwambia, “Kama wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 22:67 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, tuambie.” \p Isa akawajibu, “Hata nikiwaambia, hamtaamini. \v 68 Nami nikiwauliza swali, hamtanijibu. \v 69 Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.” \p \v 70 Wote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu\f + \fr 22:70 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*?” \p Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.” \p \v 71 Kisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.” \c 23 \s1 Pilato amhoji Isa \r (Mathayo 27:1-2, 11-14; Marko 15:1-15; Yohana 18:28–19:16) \p \v 1 Kisha umati wote wa watu wakainuka na kumpeleka Isa kwa Pilato. \v 2 Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita ni Al-Masihi\f + \fr 23:2 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, mfalme.” \p \v 3 Basi Pilato akamuuliza Isa, “Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?” \p Isa akajibu, “Wewe wasema.” \p \v 4 Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na umati ule wote, “Sioni msingi wowote wa kumshtaki mtu huyu!” \p \v 5 Lakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!” \s1 Isa apelekwa kwa Herode \p \v 6 Pilato aliposikia hayo akauliza kama huyo mtu alikuwa Mgalilaya. \v 7 Alipofahamu kwamba Isa alikuwa chini ya mamlaka ya Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa pia Yerusalemu. \p \v 8 Herode alipomwona Isa alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha. \v 9 Herode akamuuliza maswali mengi, lakini Isa hakumjibu lolote. \v 10 Wakati huo viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. \v 11 Herode na askari wake wakamdhihaki Isa na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato. \v 12 Siku hiyo, Herode na Pilato wakapata urafiki; kabla ya jambo hili walikuwa na uadui kati yao. \s1 Isa ahukumiwa kifo \r (Mathayo 27:15-26; Marko 15:6-15; Yohana 18:39–19:16) \p \v 13 Basi Pilato akawaita pamoja viongozi wa makuhani, viongozi wengine na watu, \v 14 akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami sikupata msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake. \v 15 Wala Herode hakumpata na kosa lolote, ndiyo sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lolote linalostahili kifo. \v 16 Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kumwachilia.” [ \v 17 Kwa kuwa ilikuwa lazima kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa Sikukuu.]\f + \fr 23:17 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \p \v 18 Ndipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyu! Tufungulie Baraba!” \v 19 (Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya maasi yaliyokuwa yametokea mjini, na kwa ajili ya uuaji.) \p \v 20 Pilato, akitaka kumwachia Isa, akasema nao tena. \v 21 Lakini wao wakaendelea kupiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!” \p \v 22 Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.” \p \v 23 Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu, wakidai kwamba Isa asulubiwe. Hivyo, kelele zao zikashinda. \v 24 Kwa hiyo Pilato akatoa hukumu kwamba madai yao yatimizwe. \v 25 Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Isa mikononi mwao, wamfanyie watakavyo. \s1 Isa asulubishwa \r (Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Yohana 19:17-27) \p \v 26 Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni Mkirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa. \v 27 Idadi kubwa ya watu wakamfuata Isa, wakiwamo wanawake waliokuwa wakimlilia na kumwombolezea. \v 28 Isa akawageukia, akawaambia, “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. \v 29 Kwa maana wakati utafika mtakaposema, ‘Wamebarikiwa wanawake tasa, ambao tumbo zao hazikuzaa, wala matiti yao hayakunyonyesha!’ \v 30 Ndipo \q1 “ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!” \q2 na vilima, “Tufunikeni!” ’ \m \v 31 Kwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?” \p \v 32 Watu wawili wahalifu walipelekwa pamoja na Isa ili wakasulubiwe. \v 33 Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walimsulubisha Isa pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume, na mwingine upande wake wa kushoto. \v 34 Isa akasema, “Baba\f + \fr 23:34 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. \p \v 35 Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Al-Masihi wa Mungu, Mteule wake.” \p \v 36 Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, \v 37 na wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.” \p \v 38 Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: \pc \sc Huyu ndiye\sc* \pc \sc Mfalme wa Wayahudi.\sc* \p \v 39 Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Al-Masihi? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi.” \p \v 40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu hiyo hiyo? \v 41 Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lolote.” \p \v 42 Kisha akasema, “Isa, unikumbuke utakapokuja katika ufalme wako.” \p \v 43 Isa akamjibu, “Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.\f + \fr 23:43 \fr*\ft Paradiso maana yake \ft*\fqa bustani nzuri\fqa*\ft ; hapa ni mahali zinapoenda roho za watakatifu.\ft*\f*” \s1 Kifo cha Isa \r (Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30) \p \v 44 Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, \v 45 kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. \v 46 Isa akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho. \p \v 47 Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” \v 48 Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. \v 49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wale wanawake waliokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyatazama mambo haya. \s1 Maziko ya Isa \r (Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Yohana 19:38-42) \p \v 50 Basi kulikuwa na mtu mmoja mwema na mwenye haki, jina lake Yusufu. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wayahudi\f + \fr 23:50 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*, \v 51 lakini yeye hakuwa amekubaliana na maamuzi na vitendo vya viongozi wenzake. Huyu alikuwa raia wa Arimathaya huko Yudea, naye alikuwa anaungojea ufalme wa Mungu kwa matarajio makubwa. \v 52 Yusufu alienda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Isa. \v 53 Akaushusha kutoka msalabani, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limezikiwa mtu mwingine bado. \v 54 Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza. \p \v 55 Wale wanawake waliokuwa wamekuja pamoja na Isa wakimfuata kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Isa ulivyolazwa. \v 56 Kisha wakarudi nyumbani, wakaandaa manukato na marhamu ya kuupaka huo mwili. Lakini wakapumzika siku ya Sabato kama ilivyoamriwa. \c 24 \s1 Isa afufuka \r (Mathayo 28:1-10; Marko 16:1-8; Yohana 20:1-10) \p \v 1 Siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. \v 2 Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka mdomo wa kaburi, \v 3 lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Isa. \v 4 Walipokuwa wanashangaa kuhusu jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa kama umeme wakasimama karibu nao. \v 5 Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao hadi chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? \v 6 Hayuko hapa; amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado yuko pamoja nanyi huko Galilaya kwamba: \v 7 ‘Ilikuwa lazima Mwana wa Adamu atiwe mikononi mwa watu wenye dhambi na waovu ili asulubiwe, na siku ya tatu afufuke.’ ” \v 8 Ndipo wakayakumbuka maneno ya Isa. \p \v 9 Waliporudi kutoka huko kaburini, wakawaeleza wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote mambo haya yote. \v 10 Basi Mariamu Magdalene, Yoana, na Mariamu mama yake Yakobo, pamoja na wanawake wengine waliofuatana nao ndio waliwaelezea mitume habari hizi. \v 11 Lakini hawakuwasadiki hao wanawake, kwa sababu maneno yao yalionekana kama upuzi. \v 12 Hata hivyo, Petro akainuka na kukimbia kwenda kule kaburini. Alipoinama kuchungulia, akaona vile vitambaa vya kitani, ila hakuona kitu kingine. Naye akaenda zake akijiuliza nini kilichotokea. \s1 Isa awatokea wanafunzi wawili \r (Marko 16:12-13) \p \v 13 Ikawa siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Isa walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba\f + \fr 24:13 \fr*\ft kama kilomita 11\ft*\f* kutoka Yerusalemu. \v 14 Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia. \v 15 Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Isa mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, \v 16 lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue. \p \v 17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumza wakati mnatembea?” \p Wakasimama, nyuso zao zikionesha huzuni. \v 18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiwe peke yako mgeni huku Yerusalemu, ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?” \p \v 19 Akawauliza, “Mambo gani?” \p Wakamjibu, “Mambo ya Isa Al-Nasiri. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote. \v 20 Viongozi wa makuhani na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa, nao wakamsulubisha. \v 21 Lakini tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatendeke. \v 22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtusha. Walienda kaburini leo alfajiri, \v 23 lakini hawakuukuta mwili wake. Walirudi wakasema wameona maono ya malaika ambao waliwaambia kwamba Isa yu hai. \v 24 Kisha baadhi ya wenzetu walienda kaburini wakalikuta kama vile wale wanawake walivyokuwa wamesema, lakini yeye hawakumwona.” \p \v 25 Isa akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii! \v 26 Je, haikumpasa Al-Masihi\f + \fr 24:26 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?” \v 27 Naye akianzia na Torati ya Musa na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu. \p \v 28 Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Isa akawa kama anaendelea mbele. \v 29 Lakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. \p \v 30 Alipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. \v 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, nao wakamtambua, naye akatoweka machoni pao. Hawakumwona tena. \v 32 Wakaulizana wao kwa wao, “Je, mioyo yetu haikuwaka ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” \p \v 33 Wakaondoka mara hiyo, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao wamekusanyika, \v 34 wakasema, “Ni kweli! Bwana Isa amefufuka, naye amemtokea Simoni.” \v 35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotukia njiani na jinsi walivyomtambua Isa alipoumega mkate. \s1 Isa awatokea wanafunzi wake \r (Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8) \p \v 36 Walipokuwa bado wanazungumza hayo, Isa mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!” \p \v 37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. \v 38 Lakini Isa akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? \v 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi mwenyewe. Niguseni mwone; kwa maana mzuka huna nyama na mifupa, kama mnavyoniona mimi.” \p \v 40 Aliposema haya, akawaonesha mikono na miguu yake. \v 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?” \p \v 42 Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, \v 43 naye akakichukua na kukila mbele yao. \p \v 44 Akawaambia, “Haya ndio yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu katika Torati ya Musa, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” \p \v 45 Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko Matakatifu. \v 46 Akawaambia, “Haya ndio yaliyoandikwa: Al-Masihi atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. \v 47 Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu. \v 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. \p \v 49 “Tazama nitawatumia ahadi ya Baba\f + \fr 24:49 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo kutoka juu.” \s1 Isa apaa mbinguni \r (Marko 16:19-20; Matendo 1:9-11) \p \v 50 Baada ya kuwaongoza hadi Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. \v 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. \v 52 Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. \v 53 Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu.