\id LEV - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Mambo Ya Walawi \toc1 Mambo Ya Walawi \toc2 Walawi \toc3 Law \mt1 Mambo Ya Walawi \c 1 \s1 Sadaka ya kuteketezwa \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwita Musa na kusema naye kutoka Hema la Kukutania, akamwambia, \v 2 “Sema na Waisraeli, uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu anayeleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ng’ombe, au la kondoo na mbuzi. \p \v 3 “ ‘Ikiwa sadaka hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kutoka kundi la ng’ombe, atamtoa ng’ombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa Mwenyezi Mungu. \v 4 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. \v 5 Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Mwenyezi Mungu, kisha wana wa Haruni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania. \v 6 Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande. \v 7 Wana wa Haruni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto. \v 8 Kisha hao wana wa Haruni walio makuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama, juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. \v 9 Ataziosha sehemu za ndani za yule mnyama pamoja na miguu yake kwa maji; naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \p \v 10 “ ‘Ikiwa sadaka ni sadaka ya kuteketezwa kutoka kundi la kondoo au mbuzi, atamtoa dume asiye na dosari. \v 11 Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za Mwenyezi Mungu, nao wana wa Haruni walio makuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu. \v 12 Atamkata vipande vipande, naye kuhani atavipanga, pamoja na kichwa na mafuta ya mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. \v 13 Ataosha sehemu za ndani na miguu kwa maji, naye kuhani atavileta vyote na kuvichoma juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \p \v 14 “ ‘Ikiwa sadaka inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu ni sadaka ya kuteketezwa ya ndege, atamtoa hua au kinda la njiwa. \v 15 Kuhani atamleta kwenye madhabahu, naye atamvunja shingo na kumnyofoa kichwa na kumchoma juu ya madhabahu. Damu yake itachuruzishwa ubavuni mwa madhabahu. \v 16 Ataondoa kifuko cha chakula pamoja na uchafu wake na kuvitupa upande wa mashariki wa madhabahu, mahali pale penye majivu. \v 17 Atampasua na kumweka wazi katika mabawa yake, lakini asimwachanishe kabisa, kisha kuhani ataichoma juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \c 2 \s1 Sadaka ya nafaka \p \v 1 “ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi Mungu, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake, \v 2 naye atapeleka kwa makuhani wana wa Haruni. Kuhani atachukua konzi moja unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote, na kuviteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \v 3 Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Haruni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \p \v 4 “ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa, itakuwa ya unga laini: iwe maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu na iliyopakwa mafuta. \v 5 Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta, bila chachu. \v 6 Vunjavunja na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka. \v 7 Ikiwa sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta. \v 8 Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Mwenyezi Mungu; mkabidhi kuhani, ambaye ataipeleka madhabahuni. \v 9 Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu katika hiyo sadaka ya nafaka, na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \v 10 Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Haruni na wanawe; ni sehemu ya sadaka takatifu sana kati ya sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \p \v 11 “ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Mwenyezi Mungu ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \v 12 Unaweza kuzileta kwa Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza. \v 13 Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote. \p \v 14 “ ‘Ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwa Mwenyezi Mungu, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto. \v 15 Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka. \v 16 Kuhani atateketeza ile sehemu ya kumbukumbu katika hiyo sadaka ya nafaka iliyopondwa, na mafuta, pamoja na uvumba wote, kuwa sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \c 3 \s1 Sadaka ya amani \p \v 1 “ ‘Ikiwa mtu anatoa sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Mwenyezi Mungu. \v 2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani, wana wa Haruni, watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu. \v 3 Katika hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: sehemu za ndani na mafuta yote yanayoungana nazo, \v 4 figo zote pamoja na mafuta yaliyozifunika karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini; utayaondoa pamoja na figo. \v 5 Kisha wana wa Haruni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyo juu ya kuni zinazowaka; ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \p \v 6 “ ‘Akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kuwa sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, atamtoa dume au jike asiye na dosari. \v 7 Akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Mwenyezi Mungu. \v 8 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu. \v 9 Katika hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo, \v 10 figo mbili pamoja na mafuta yanayozifunika yaliyo karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo utayaondoa pamoja na figo. \v 11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \p \v 12 “ ‘Ikiwa sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Mwenyezi Mungu. \v 13 Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu. \v 14 Katika ile sadaka anayotoa, atatoa hii sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo, \v 15 figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. \v 16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Mwenyezi Mungu. \p \v 17 “ ‘Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’ ” \c 4 \s1 Sadaka ya dhambi \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote afanyapo dhambi bila kukusudia na akatenda lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Mwenyezi Mungu: \p \v 3 “ ‘Ikiwa kuhani aliyepakwa mafuta amefanya dhambi na kuwaletea watu hatia, lazima alete kwa Mwenyezi Mungu fahali mchanga asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya dhambi aliyotenda. \v 4 Atamkabidhi huyo fahali kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Mwenyezi Mungu. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo fahali na kumchinja mbele za Mwenyezi Mungu. \v 5 Kisha kuhani huyo aliyepakwa mafuta atachukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuileta katika Hema la Kukutania. \v 6 Atachovya kidole chake katika hiyo damu, na kuinyunyiza sehemu yake mara saba mbele za Mwenyezi Mungu, mbele ya pazia la mahali patakatifu. \v 7 Kisha kuhani atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri iliyo mbele za Mwenyezi Mungu katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ya huyo fahali ataimwaga chini ya hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka kwenye ingilio la Hema la Kukutania. \v 8 Atayaondoa mafuta yote ya fahali huyo wa sadaka ya dhambi: mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani au zile zinazounganika nazo, \v 9 figo zote mbili na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo zote, \v 10 kama vile mafuta yanavyoondolewa kutoka kwa ng’ombe aliyetolewa sadaka ya amani. Kisha kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. \v 11 Lakini ngozi ya huyo fahali na nyama zake zote, pamoja na kichwa na miguu yake, sehemu za ndani na matumbo, \v 12 yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi hadi mahali palipo safi, ambapo majivu hutupwa; naye atamchoma kwa moto wa kuni juu ya lundo la majivu. \p \v 13 “ ‘Ikiwa jumuiya yote ya Israeli watatenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Mwenyezi Mungu, hata kama jumuiya hawafahamu jambo hilo, wana hatia. \v 14 Wanapotambua dhambi waliyoitenda, lazima kusanyiko walete fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi, na kuikabidhi mbele ya Hema la Kukutania. \v 15 Wazee wa jumuiya wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo fahali mbele za Mwenyezi Mungu, naye huyo fahali atachinjwa mbele za Mwenyezi Mungu. \v 16 Kisha kuhani aliyepakwa mafuta ataingiza sehemu ya damu ya huyo fahali ndani ya Hema la Kukutania. \v 17 Atachovya kidole chake kwenye damu na kuinyunyiza mara saba mbele za Mwenyezi Mungu mbele ya hilo pazia. \v 18 Atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu yaliyo mbele za Mwenyezi Mungu katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu ya kuteketezea sadaka, penye ingilio la Hema la Kukutania. \v 19 Atayaondoa mafuta yote ya yule fahali na kuyateketeza juu ya madhabahu, \v 20 naye atamfanyia fahali huyu kama alivyomfanyia yule fahali mwingine wa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii kuhani atawafanyia watu upatanisho, nao watasamehewa. \v 21 Kisha atamchukua yule fahali nje ya kambi na kumteketeza kama alivyomteketeza yule wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya jumuiya. \p \v 22 “ ‘Wakati kiongozi ametenda dhambi bila kukusudia na kufanya yaliyokatazwa katika amri yoyote ya Mwenyezi Mungu, Mungu wake, ana hatia. \v 23 Atakapofahamishwa dhambi aliyotenda, ni lazima alete beberu asiye na dosari kuwa sadaka yake. \v 24 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha yule mbuzi na kumchinja mahali pale sadaka za kuteketezwa huchinjiwa mbele za Mwenyezi Mungu. Hii ni sadaka ya dhambi. \v 25 Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketeza, na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. \v 26 Atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu, kama alivyoteketeza mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho wa dhambi kwa ajili ya yule mtu, naye atasamehewa. \p \v 27 “ ‘Kama mtu katika jumuiya ametenda dhambi pasipo kukusudia, na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Mwenyezi Mungu, yeye ana hatia. \v 28 Atakapofahamishwa dhambi aliyoitenda, ni lazima alete mbuzi jike asiye na dosari kuwa sadaka yake kwa ajili ya dhambi aliyotenda. \v 29 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na kumchinjia mahali pa kuteketezea sadaka. \v 30 Kisha kuhani atachukua sehemu ya ile damu kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. \v 31 Atayaondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kwenye sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa. \p \v 32 “ ‘Akileta mwana-kondoo kuwa sadaka yake ya dhambi, atamleta jike asiye na dosari. \v 33 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo mwana-kondoo na kumchinja kwa ajili ya sadaka ya dhambi mahali ambako sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa. \v 34 Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia juu ya pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na ile damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu. \v 35 Ataondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kutoka kwa mwana-kondoo wa sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu juu ya zile sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa. \c 5 \s1 Sadaka zingine za kuondoa dhambi \p \v 1 “ ‘Ikiwa mtu ametenda dhambi kwa sababu hakusema alipotakiwa kutoa ushahidi hadharani kuhusu jambo aliloona au kujua habari zake, yeye atastahili adhabu. \p \v 2 “ ‘Au mtu akitambua kuwa ana hatia, kama vile akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vinavyotambaa ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia. \p \v 3 “ ‘Au akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu chochote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia. \p \v 4 “ ‘Au kama mtu ameapa kufanya kitu chochote bila kufikiri, kiwe chema au kibaya, kwa vyovyote mtu aweza kuapa bila kujali, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia. \p \v 5 “ ‘Mtu yeyote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, ni lazima akiri ni kwa njia gani ametenda dhambi, \v 6 na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, ni lazima alete kwa Mwenyezi Mungu kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake. \p \v 7 “ ‘Lakini kama huyo mtu hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda wawili wa njiwa kwa Mwenyezi Mungu ikiwa ni adhabu kwa ajili ya dhambi yake: mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. \v 8 Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza ndege mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo na kuacha kichwa chake kikining’inia, \v 9 naye atanyunyiza sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi kwenye pembe za madhabahu. Damu iliyobaki lazima ichuruzwe chini ya madhabahu. Hii ni sadaka ya dhambi. \v 10 Kisha kuhani atamtoa yule ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa, na hivyo kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa. \p \v 11 “ ‘Ikiwa basi hawezi kupata hua wawili au makinda wawili wa njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efa\f + \fr 5:11 \fr*\ft Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.\ft*\f* ya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya dhambi. \v 12 Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi. \v 13 Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yoyote ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ” \s1 Sadaka ya hatia \p \v 14 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: \v 15 “Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Mwenyezi Mungu, huyo mtu ataleta kwa Mwenyezi Mungu kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari, na mwenye thamani halisi ya fedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia. \v 16 Ni lazima alipe kwa yale aliyoshindwa kufanya kuhusu vitu vitakatifu, kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani ile na kuitoa yote kwa kuhani, ambaye atamfanyia upatanisho kwa huyo kondoo dume kama sadaka ya dhambi, naye atasamehewa. \p \v 17 “Kama mtu akifanya dhambi, na kutenda yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu. \v 18 Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi. Kwa njia hii, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa. \v 19 Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya Mwenyezi Mungu.” \c 6 \s1 Kurudisha kilichochukuliwa \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: \v 2 “Mtu yeyote akitenda dhambi, naye si mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu kwa kumdanganya jirani yake kuhusu kitu fulani alichokabidhiwa, au kimeachwa chini ya utunzaji wake, au kimeibwa, au kama akimdanganya, \v 3 au akiokota mali iliyopotea na akadanganya kuihusu, au kuapa kwa uongo, au kama akitenda dhambi yoyote ambayo watu wanaweza kuitenda; \v 4 wakati akitenda dhambi hizo na kuwa mwenye hatia, ni lazima arudishe kile alichokuwa amekiiba au amekichukua kwa dhuluma, au alichokuwa amekabidhiwa, au mali iliyokuwa imepotea akaipata, \v 5 au chochote alichokuwa amekiapia kwa uongo. Lazima akirudishe kikamilifu, na aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, vyote ampe mwenye mali siku ile anapeleka sadaka yake ya hatia. \v 6 Kisha kama adhabu lazima amletee kuhani, yaani kwa Mwenyezi Mungu, kuwa sadaka yake ya hatia, kondoo dume kutoka kundi lake asiye na dosari, mwenye thamani kamili. \v 7 Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu, naye atasamehewa kwa kosa lolote katika mambo aliyoyatenda lililomfanya kuwa na hatia.” \s1 Sadaka ya kuteketezwa \p \v 8 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: \v 9 “Mpe Haruni na wanawe agizo hili: ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa itabaki kwenye moto juu ya madhabahu usiku kucha, hadi asubuhi, nao moto lazima uwe unaendelea kuwaka juu ya madhabahu. \v 10 Kisha kuhani atavaa mavazi yake ya kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani mwilini wake, na aondoe majivu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo moto umeteketeza juu ya madhabahu, na kuyaweka kando ya madhabahu. \v 11 Kisha atayavua mavazi haya na kuvaa mengine, naye achukue yale majivu nje ya kambi na kuyapeleka mahali palipo safi. \v 12 Moto ulio juu ya madhabahu lazima uwe unaendelea kuwaka; kamwe usizimike. Kila asubuhi kuhani ataongeza kuni na kupanga sadaka ya kuteketezwa juu ya moto, na kuteketeza mafuta ya wanyama wa sadaka za amani juu yake. \v 13 Moto lazima uendelee kuwaka juu ya madhabahu mfululizo, kamwe usizimike. \s1 Sadaka ya nafaka \p \v 14 “ ‘Haya ndio masharti ya sadaka ya nafaka: Wana wa Haruni wataileta mbele za Mwenyezi Mungu, mbele za madhabahu. \v 15 Kuhani atachukua konzi moja ya unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote ulio juu ya sadaka ya nafaka, na kuteketeza sehemu hiyo ya kumbukumbu juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \v 16 Haruni na wanawe watakula sehemu iliyobaki, lakini italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu, nao wataila katika ua wa Hema la Kukutania. \v 17 Kamwe haitaokwa na chachu; nimewapa kama fungu lao la sadaka iliyotolewa kwangu kwa moto. Ni takatifu sana, kama vile ilivyo sadaka ya dhambi na ya hatia. \v 18 Kila mwanaume mzao wa Haruni aweza kuila. Ni fungu lake milele la sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto kwa vizazi vijavyo. Chochote kinachozigusa kitakuwa kitakatifu.’ ” \p \v 19 Tena Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 20 “Hii ni sadaka ambayo Haruni na wanawe wanapaswa kuleta kwa Mwenyezi Mungu siku atakapopakwa mafuta: sehemu ya kumi ya efa\f + \fr 6:20 \fr*\ft Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.\ft*\f* ya unga laini kama sadaka ya kawaida ya nafaka. Nusu yake ataitoa asubuhi na nusu nyingine jioni. \v 21 Iandae kwa mafuta kwenye kikaango; ilete ikiwa imechanganywa vizuri, na utoe hiyo sadaka ya nafaka ikiwa imevunjwa vipande vipande kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \v 22 Mwanawe atakayeingia mahali pake kama kuhani aliyepakwa mafuta ndiye atakayeiandaa. Ni fungu la milele la Mwenyezi Mungu, nalo litateketezwa kabisa. \v 23 Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itateketezwa kabisa; kamwe haitaliwa.” \s1 Sadaka ya dhambi \p \v 24 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 25 “Mwambie Haruni na wanawe: ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi itachinjiwa mbele za Mwenyezi Mungu mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa; ni takatifu sana. \v 26 Kuhani anayeitoa ndiye atakayeikula; itakuliwa katika mahali patakatifu, katika ua wa Hema la Kukutania. \v 27 Chochote kitakachogusa nyama yoyote ya hiyo sadaka kitakuwa kitakatifu; na kama damu ya hiyo sadaka itadondokea juu ya vazi, lazima ulifulie mahali patakatifu. \v 28 Chungu cha udongo kitakachopikiwa nyama lazima kivunjwe, lakini kama imepikiwa kwenye chombo cha shaba, chombo hicho kitasuguliwa na kusuuzwa kwa maji. \v 29 Kila mwanaume katika jamaa ya kuhani aweza kula nyama hiyo; ni takatifu sana. \v 30 Lakini kila sadaka ya dhambi ambayo damu yake imeletwa ndani ya Hema la Kukutania kufanya upatanisho katika Mahali Patakatifu kamwe haitaliwa; lazima iteketezwe. \c 7 \s1 Sadaka ya hatia \p \v 1 “ ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya hatia, ambayo ni takatifu sana: \v 2 Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, nayo damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu. \v 3 Mafuta yake yote yatatolewa sadaka: mafuta ya mkia, na mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani, \v 4 figo zote mbili pamoja na mafuta yanayozifunika karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo yataondolewa pamoja na hizo figo. \v 5 Kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia. \v 6 Mwanaume yeyote katika jamaa ya kuhani aweza kuila, lakini lazima iliwe mahali patakatifu; ni takatifu sana. \p \v 7 “ ‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawasawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho. \v 8 Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuichukua ngozi ya mnyama yule aliyetolewa iwe yake. \v 9 Kila sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni au kupikwa katika sufuria au katika kikaango itakuwa ya kuhani anayeitoa. \v 10 Nayo kila sadaka ya nafaka, iwe imechanganywa na mafuta au iko kavu, itakuwa ya wana wa Haruni, nayo itagawanywa sawa kati yao. \s1 Sadaka ya amani \p \v 11 “ ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya sadaka ya amani ambayo mtu aweza kuileta kwa Mwenyezi Mungu: \p \v 12 “ ‘Ikiwa mtu atatoa sadaka ya amani kwa ajili ya kuonesha shukrani, pamoja na sadaka hii ya shukrani, atatoa maandazi yasiyotiwa chachu yaliyochanganywa na mafuta, mikate myembamba isiyotiwa chachu na iliyopakwa mafuta, na maandazi ya unga laini uliokandwa vizuri na kuchanganywa na mafuta. \v 13 Pamoja na sadaka yake ya amani ya shukrani, ataleta sadaka ya maandazi yaliyotengenezwa kwa chachu. \v 14 Ataleta moja ya kila aina ya andazi kuwa sadaka, matoleo kwa Mwenyezi Mungu; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani. \v 15 Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku hiyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu chochote hadi asubuhi. \p \v 16 “ ‘Lakini ikiwa sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake. \v 17 Nyama yoyote ya sadaka inayobaki hadi siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto. \v 18 Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, Mwenyezi Mungu hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi. Mtu atakayekula sehemu yake yoyote atahesabiwa hatia. \p \v 19 “ ‘Nyama inayogusa chochote kilicho najisi kamwe haitaliwa; lazima iteketezwe kwa moto. Kuhusu nyama nyingine, mtu yeyote aliyetakaswa anaweza kuila. \v 20 Lakini kama mtu yeyote najisi akila nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu, huyo mtu lazima akatiliwe mbali na watu wake. \v 21 Kama mtu yeyote akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni uchafu wa mwanadamu, au mnyama najisi, au kitu chochote kilicho najisi, kitu cha kuchukiza, kisha akala nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ” \s1 Kula mafuta na kunywa damu kwakatazwa \p \v 22 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 23 “Waambie Waisraeli: ‘Msile mafuta yoyote ya ng’ombe, kondoo wala mbuzi. \v 24 Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na wanyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yoyote, lakini kamwe msiyale. \v 25 Mtu yeyote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwa Mwenyezi Mungu kwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. \v 26 Popote mtakapoishi, kamwe msile damu ya ndege yeyote wala ya mnyama. \v 27 Mtu yeyote atakayekula damu lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ” \s1 Fungu la makuhani \p \v 28 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 29 “Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote aletaye sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu ataleta sehemu ya sadaka hiyo kama dhabihu yake kwa Mwenyezi Mungu. \v 30 Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. \v 31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Haruni na wanawe. \v 32 Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo. \v 33 Mwana wa Haruni atoaye damu na mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake. \v 34 Kutoka kwa sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa, pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Haruni na wanawe kuwa fungu lao la milele kutoka kwa Waisraeli.’ ” \p \v 35 Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, ambazo zilitengwa kwa ajili ya Haruni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu ili kumtumikia Mwenyezi Mungu katika kazi ya ukuhani. \v 36 Siku ile walipopakwa mafuta, Mwenyezi Mungu aliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la milele kwa vizazi vijavyo. \p \v 37 Basi haya ndio masharti kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia, sadaka ya kuwekwa wakfu, na sadaka ya amani, \v 38 ambayo Mwenyezi Mungu alimpa Musa juu ya Mlima Sinai siku ile alipowaagiza Waisraeli walete sadaka zao kwa Mwenyezi Mungu, katika Jangwa la Sinai. \c 8 \s1 Kuwekwa wakfu kwa Haruni na wanawe \r (Kutoka 29:1-37) \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waletee Haruni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu. \v 3 Kisha kusanya watu wote kwenye ingilio la Hema la Kukutania.” \v 4 Musa akafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza, na watu wakakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania. \p \v 5 Musa akawaambia kusanyiko, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu ameagiza lifanyike.” \v 6 Kisha Musa akamleta Haruni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji. \v 7 Akamvika Haruni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho, na kumvalisha kizibau. Pia akamfunga hicho kizibau kiunoni mwake kwa mshipi uliofumwa kwa ustadi. \v 8 Akaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu\f + \fr 8:8 \fr*\ft Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.\ft*\f* kwenye hicho kifuko. \v 9 Kisha akamvika Haruni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, lile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 10 Kisha Musa akachukua mafuta ya upako, na kuipaka maskani ya Mungu na kila kitu kilichokuwamo; hivyo akaviweka wakfu. \v 11 Akanyunyiza sehemu ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akaipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote, pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu. \v 12 Akamimina sehemu ya hayo mafuta ya upako kichwani mwa Haruni, akampaka mafuta ili kumweka wakfu. \v 13 Kisha akawaleta wana wa Haruni mbele, akawavika makoti, akawafunga mishipi na kuwavika vilemba, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 14 Kisha akamtoa fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nao Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 15 Musa akamchinja yule fahali na akachukua sehemu ya hiyo damu, kisha kwa kidole chake akaitia kwenye pembe zote za madhabahu ili kutakasa madhabahu. Akaimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. Kwa hiyo akayaweka wakfu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu. \v 16 Pia Musa akachukua mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani, na kipande kirefu cha ini, na figo zote mbili pamoja na mafuta yake, akayateketeza juu ya madhabahu. \v 17 Lakini fahali, ikiwa pamoja na ngozi yake na nyama yake na sehemu zake za ndani na matumbo, akaiteketeza nje ya kambi, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 18 Kisha Musa akamleta kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 19 Ndipo Musa akamchinja yule kondoo dume na kunyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. \v 20 Musa akamkata yule kondoo dume vipande vipande na kukiteketeza kichwa, vile vipande na yale mafuta. \v 21 Kisha akamsafisha sehemu za ndani na miguu kwa maji, na kumteketeza yule kondoo dume mzima juu ya madhabahu kuwa sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 22 Kisha Musa akamleta yule kondoo dume wa pili, ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 23 Musa akamchinja yule kondoo dume, akaichukua sehemu ya damu yake na kuipaka juu ya ncha ya sikio la kuume la Haruni, na juu ya kidole gumba cha mkono wake wa kuume na juu ya kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. \v 24 Pia Musa akawaleta hao wana wa Haruni mbele, akaipaka sehemu ya hiyo damu kwenye ncha za masikio yao ya kuume, juu ya vidole gumba vya mikono yao ya kuume, na juu ya vidole vikubwa vya miguu yao ya kuume. Kisha akanyunyiza damu pande zote za madhabahu. \v 25 Akachukua mafuta ya mnyama, mafuta ya mkia, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani, kipande kirefu cha ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, na paja la kulia. \v 26 Kisha kutoka kwa kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichokuwa mbele za Mwenyezi Mungu, akachukua andazi moja, na jingine lililotengenezwa kwa mafuta, na mkate mwembamba; akaviweka hivi vyote juu ya mafungu ya mafuta ya mnyama, na juu ya lile paja la kulia. \v 27 Akaviweka hivi vyote mikononi mwa Haruni na wanawe, na kuviinua mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. \v 28 Kisha Musa akavichukua kutoka mikononi mwao na kuviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kuwa sadaka ya kuwekwa wakfu, harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \v 29 Kisha akachukua kidari, kilicho fungu la Musa la kondoo dume kwa ajili ya kuwekwa wakfu, na kukiinua mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 30 Kisha Musa akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Haruni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Haruni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao. \p \v 31 Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe, “Pikeni hiyo nyama kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na muile hapo pamoja na mkate kutoka kikapu cha sadaka ya kuweka wakfu, kama nilivyoagiza: ‘Haruni na wanawe wataila.’ \v 32 Kisha mteketeze nyama na mikate iliyobaki. \v 33 Msitoke kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa muda wa siku saba, hadi siku zenu za kuwekwa wakfu ziwe zimetimia, kwa kuwa muda wenu wa kuwekwa wakfu utakuwa siku saba. \v 34 Lile lililofanyika leo liliagizwa na Mwenyezi Mungu ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. \v 35 Lazima mkae kwenye ingilio la Hema la Kukutania usiku na mchana kwa siku saba, na kufanya lile Mwenyezi Mungu analolitaka, ili msife; kwa kuwa hilo ndilo nililoamriwa.” \v 36 Kwa hiyo Haruni na wanawe wakafanya kila kitu Mwenyezi Mungu alichoamuru kupitia kwa Musa. \c 9 \s1 Makuhani waanza huduma yao \p \v 1 Katika siku ya nane, Musa akawaita Haruni na wanawe, na wazee wa Israeli. \v 2 Akamwambia Haruni, “Chukua ndama dume kwa ajili ya sadaka yako ya dhambi, na kondoo dume kwa sadaka yako ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, nao uwalete mbele za Mwenyezi Mungu. \v 3 Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, \v 4 na pia maksai na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya amani, ili kutoa dhabihu mbele za Mwenyezi Mungu, pamoja na sadaka ya nafaka iliyochanganywa na mafuta. Kwa kuwa leo Mwenyezi Mungu atawatokea.’ ” \p \v 5 Wakavileta vile vitu Musa alivyowaagiza mbele ya Hema la Kukutania, na kusanyiko lote wakakaribia na kusimama mbele za Mwenyezi Mungu. \v 6 Ndipo Musa akasema, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu alilowaagiza mlifanye, ili utukufu wa Mwenyezi Mungu upate kuonekana kwenu.” \p \v 7 Musa akamwambia Haruni, “Njoo madhabahuni utoe dhabihu ya sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, kuwa upatanisho kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya watu. Kisha utoe sadaka ya upatanisho kwa ajili ya watu, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoagiza.” \p \v 8 Hivyo Haruni akaja madhabahuni na kumchinja yule ndama kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe. \v 9 Wanawe wakamletea damu, naye akachovya kidole chake katika hiyo damu, akaitia kwenye pembe za madhabahu, nayo damu iliyobaki akaimwaga chini ya madhabahu. \v 10 Juu ya madhabahu akateketeza mafuta, figo na kipande kirefu cha ini kutoka hiyo sadaka ya dhambi, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \v 11 Akateketeza nyama na ngozi nje ya kambi. \p \v 12 Kisha Haruni akachinja sadaka ya kuteketezwa. Wanawe wakamletea damu, naye akainyunyiza pande zote za madhabahu. \v 13 Wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu. \v 14 Akasafisha sehemu za ndani na miguu, akaviteketeza juu ya sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu. \p \v 15 Kisha Haruni akaleta sadaka ile iliyokuwa kwa ajili ya watu. Akachukua yule mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu, akamchinja na kumtoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kama alivyofanya kwa ile ya kwanza. \p \v 16 Haruni akaleta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama ilivyoelekezwa. \v 17 Pia akaleta sadaka ya nafaka, akachukua konzi moja na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi. \p \v 18 Akachinja maksai na kondoo dume kuwa sadaka ya amani kwa ajili ya watu. Wanawe Haruni wakampa ile damu, naye akainyunyiza pande zote za madhabahu. \v 19 Lakini sehemu zile za mafuta ya yule maksai na ya yule kondoo dume, yaani mafuta ya mkia, yaliyofunika tumbo, ya figo na kipande kirefu cha ini, \v 20 hivi vyote wakaviweka juu ya vidari, kisha Haruni akayateketeza hayo mafuta ya wanyama juu ya madhabahu. \v 21 Haruni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za Mwenyezi Mungu ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Musa alivyoagiza. \p \v 22 Kisha Haruni akainua mikono yake kuwaelekea watu na kuwabariki. Naye baada ya kutoa dhabihu ya sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani, akashuka chini. \p \v 23 Kisha Musa na Haruni wakaingia kwenye Hema la Kukutania. Walipotoka nje, wakawabariki watu. Nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukawatokea watu wote. \v 24 Moto ukaja kutoka kwa uwepo wa Mwenyezi Mungu, ukaiteketeza ile sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sehemu ya mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wote walipoona jambo hili, wakashangilia kwa furaha na kusujudu. \c 10 \s1 Kifo cha Nadabu na Abihu \p \v 1 Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtolea Mwenyezi Mungu moto usio halali, kinyume na agizo la Mungu. \v 2 Hivyo moto ukaja kutoka kwa uwepo wa Mwenyezi Mungu na kuwateketeza, nao wakafa mbele za Mwenyezi Mungu. \v 3 Kisha Musa akamwambia Haruni, “Hili ndilo alilonena Mwenyezi Mungu, aliposema: \q1 “ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia \q2 nitajionesha kuwa mtakatifu; \q1 machoni pa watu wote \q2 nitaheshimiwa.’ ” \m Haruni akanyamaza. \p \v 4 Musa akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjomba wake Haruni, akawaambia, “Njooni hapa. Ondoeni miili ya ndugu zenu mbele ya mahali patakatifu, mkaipeleke nje ya kambi.” \v 5 Hivyo wakaja na kuwaondoa, wakiwa bado wamevalia makoti yao ya ibada, wakawapeleka nje ya kambi, kama Musa alivyoamuru. \p \v 6 Ndipo Musa akamwambia Haruni pamoja na wanawe, Eleazari na Ithamari, “Msifunue vichwa vyenu wala msirarue mavazi yenu, la sivyo mtakufa na Mwenyezi Mungu ataikasirikia jumuiya nzima. Lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli, wanaweza kuwaombolezea wale ambao Mwenyezi Mungu amewaangamiza kwa moto. \v 7 Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta ya Mwenyezi Mungu ya upako yako juu yenu.” Hivyo wakafanya kama vile Musa alivyosema. \p \v 8 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Haruni, \v 9 “Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. \v 10 Ni lazima mtenganishe kati ya kilicho kitakatifu na kilicho cha kawaida, kati ya kilicho najisi na kilicho safi, \v 11 na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazo Mwenyezi Mungu aliwapa kupitia Musa.” \p \v 12 Musa akamwambia Haruni pamoja na wanawe waliosalia, Eleazari na Ithamari, “Chukueni sadaka ya nafaka iliyobaki kutoka kwa sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, muile hapo kando ya madhabahu ikiwa imeandaliwa bila chachu, kwa sababu ni takatifu sana. \v 13 Mtaila katika mahali patakatifu kwa sababu ni fungu lenu na fungu la wana wenu la sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, kwa maana hivyo ndivyo nilivyoamriwa. \v 14 Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila katika mahali patakatifu; mmepewa wewe na wanao kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli. \v 15 Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya wanyama wa sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako na wanao milele, kama Mwenyezi Mungu alivyoagiza.” \p \v 16 Musa alipouliza kuhusu mbuzi aliyetolewa sadaka ya dhambi na kugundua kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Haruni waliobaki. Akawauliza, \v 17 “Kwa nini hamkula sadaka ya dhambi katika eneo la mahali patakatifu? Ni takatifu sana. Mlipewa ninyi ili kuondoa hatia ya jumuiya kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho mbele za Mwenyezi Mungu. \v 18 Kwa kuwa damu yake haikuletwa ndani ya Mahali Patakatifu, mngemla mbuzi huyo katika sehemu ya mahali patakatifu kama nilivyoagiza.” \p \v 19 Haruni akamjibu Musa, “Leo wanangu wametoa sadaka zao za dhambi na sadaka zao za kuteketezwa mbele za Mwenyezi Mungu, lakini mambo kama haya yamenitokea mimi. Je, Mwenyezi Mungu angependezwa kama ningekuwa nimekula sadaka ya dhambi leo?” \v 20 Musa aliposikia haya, akaridhika. \c 11 \s1 Vyakula najisi na visivyo najisi \r (Kumbukumbu 14:3-21) \p \v 1 Mwenyezi Mungu akawaambia Musa na Haruni, \v 2 “Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote wanaoishi juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala: \v 3 Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua. \p \v 4 “ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua, hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. \v 5 Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. \v 6 Sungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. \v 7 Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, hacheui; huyo ni najisi kwenu. \v 8 Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu. \p \v 9 “ ‘Kuhusu viumbe wote wanaoishi ndani ya maji ya bahari na vijito, mtakula wale wote wenye mapezi na magamba. \v 10 Lakini viumbe wote ndani ya bahari au vijito wasio na mapezi na magamba, wakiwa miongoni mwa makundi au viumbe wote ndani ya maji, hao ni machukizo kwenu. \v 11 Nao watakuwa machukizo kwenu. Msile nyama yao, nayo mizoga yao itakuwa machukizo. \v 12 Chochote kinachoishi ndani ya maji ambacho hakina mapezi na magamba kitakuwa chukizo kwenu. \p \v 13 “ ‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu, \v 14 mwewe mwekundu, aina zote za mwewe mweusi, \v 15 aina zote za kunguru, \v 16 mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za kipanga, \v 17 bundi, mnandi, bundi mkubwa, \v 18 mumbi, mwari, nderi, \v 19 korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo. \p \v 20 “ ‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu. \v 21 Lakini kuna viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi. \v 22 Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi. \v 23 Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu. \s1 Wanyama walio najisi \p \v 24 “ ‘Mtajinajisi kwa wanyama hawa. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi hadi jioni. \v 25 Yeyote atakayebeba mizoga ya viumbe hawa ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 26 “ ‘Kila mnyama mwenye ukwato ulioachana lakini haukugawanyika kabisa, au yule asiyecheua, huyo ni najisi kwenu; yeyote agusaye mzoga wowote wa hao atakuwa najisi. \v 27 Miongoni mwa wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne, wale wanaotembea kwa vitanga vyao ni najisi kwenu; yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi hadi jioni. \v 28 Yeyote atakayebeba mizoga yao ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi hadi jioni. Wanyama hawa ni najisi kwenu. \p \v 29 “ ‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yoyote ya mijusi mikubwa, \v 30 guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga. \v 31 Miongoni mwa wanyama wote wanaotambaa juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi hadi jioni. \v 32 Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi hadi jioni, kisha kitakuwa safi tena. \v 33 Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho. \v 34 Chakula chochote ambacho chaweza kuliwa lakini kikawa kimeingia maji kutoka chungu hicho ni najisi, na kitu chochote cha majimaji ambacho chaweza kunyweka kutoka chungu hicho ni najisi. \v 35 Chochote ambacho mzoga utaangukia kitakuwa najisi. Jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi. \v 36 Lakini chemchemi au kisima, mahali yanapokusanyika maji, patakuwa safi; lakini yeyote atakayegusa moja ya mizoga hii ni najisi. \v 37 Kama mzoga ukianguka juu ya mbegu zozote ambazo ni za kupanda, zinabaki safi. \v 38 Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu. \p \v 39 “ ‘Kama mnyama ambaye mnaruhusiwa kumla akifa, yeyote atakayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hadi jioni. \v 40 Yeyote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi hadi jioni. Yeyote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 41 “ ‘Kila kiumbe kinachotambaa juu ya ardhi ni chukizo; kisiliwe. \v 42 Msile kiumbe chochote kinachotambaa juu ya ardhi, kiwe kinachotambaa kwa tumbo lake, au kinachotambaa kwa miguu minne au kwa miguu mingi; ni chukizo. \v 43 Msijitie unajisi kwa kiumbe chochote kati ya hivi. Msijitie unajisi kwa viumbe hivyo au kutiwa unajisi navyo. \v 44 Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi. \v 45 Mimi ndimi Mwenyezi Mungu niliyewapandisha mtoke Misri ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo kuweni watakatifu kwa sababu Mimi ni mtakatifu. \p \v 46 “ ‘Haya ndio masharti kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kiendacho juu ya ardhi. \v 47 Ni lazima mpambanue kati ya kilicho najisi na kilicho safi, kati ya viumbe hai vinavyoweza kuliwa na vile visivyoweza kuliwa.’ ” \c 12 \s1 Utakaso baada ya kuzaa mtoto \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waambie Waisraeli: ‘Mwanamke ambaye atapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume atakuwa najisi kwa siku saba, kama anavyokuwa najisi wakati wa siku zake za hedhi. \v 3 Naye huyo mtoto atatahiriwa siku ya nane. \v 4 Kisha ni lazima huyo mwanamke asubiri kwa siku thelathini na tatu, ndipo atakaswe kutoka damu kwake. Hataruhusiwa kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kuingia mahali patakatifu, hadi siku za kutakaswa kwake zimetimia. \v 5 Kama alimzaa mtoto wa kike, mwanamke huyo atakuwa najisi kwa majuma mawili, kama wakati wake wa hedhi. Kisha atasubiri kwa siku sitini na sita, ndipo atatakaswa kutoka damu kwake. \p \v 6 “ ‘Siku zake za utakaso kwa ajili ya mwana au binti zitakapotimia, mwanamke huyo atamletea kuhani kwenye ingilio la Hema la Kukutania mwana-kondoo mwenye umri wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au hua kwa ajili ya sadaka ya dhambi. \v 7 Atavitoa mbele za Mwenyezi Mungu ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na kisha atatakasika kutokana na kutokwa na damu. \p “ ‘Haya ndio masharti kwa ajili ya mwanamke atakayezaa mtoto wa kiume au wa kike. \v 8 Kama huyo mwanamke hana uwezo wa kumpata mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda wawili wa njiwa, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.’ ” \c 13 \s1 Masharti kuhusu magonjwa ya ngozi yaambukizayo \p \v 1 Mwenyezi Mungu akawaambia Musa na Haruni, \v 2 “Iwapo mtu yeyote atakuwa na uvimbe, au upele, au alama nyeupe juu ya ngozi yake, ambayo yaweza kuwa ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza\f + \fr 13:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa ukoma\fqa*\ft ; ni neno lililotumika kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi, ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi (pia \+xt 13:47\+xt*)\ft*\f*, ni lazima aletwe kwa kuhani Haruni, au kwa mmoja wa wanawe, hao makuhani. \v 3 Kuhani atachunguza hicho kidonda kilichopo juu ya ngozi yake, na kama nywele za mahali palipo na kidonda zimebadilika kuwa nyeupe, na ikiwa kidonda kimeingia ndani ya ngozi, basi ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, yaani ukoma. Kuhani atakapomchunguza, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. \v 4 Kama alama juu ya ngozi yake ni nyeupe, lakini haionekani kuingia ndani ya ngozi, na nywele kwenye alama hiyo hazijageuka kuwa nyeupe, kuhani atamtenga mtu aliyeambukizwa kwa siku saba. \v 5 Siku ya saba, kuhani atamchunguza, na kama hakuona badiliko kwenye kile kidonda na hakijaenea juu ya ngozi, atamtenga kwa siku nyingine saba. \v 6 Siku ya saba kuhani atamchunguza tena, na kama kidonda kimepungua na hakijaenea juu ya ngozi, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa ni safi; ni upele tu. Ni lazima mtu huyo afue mavazi yake, naye atakuwa safi. \v 7 Lakini ikiwa ule upele utaenea katika ngozi yake baada ya yeye kujionesha kwa kuhani na kutangazwa kuwa safi, ni lazima aende tena kwa kuhani. \v 8 Kuhani atamchunguza, na kama upele umeenea kwenye ngozi, atamtangaza kuwa najisi, kwani ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. \p \v 9 “Wakati mtu yeyote ana ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, ni lazima aletwe kwa kuhani. \v 10 Kuhani atamchunguza na kama kuna uvimbe mweupe katika ngozi ambao umefanya nywele kuwa nyeupe, na kama kuna nyama mbichi ndani ya uvimbe, \v 11 ni ugonjwa sugu wa ngozi, na kuhani atamtangaza kuwa najisi. Hatamtenga tena kwa sababu ni najisi tayari. \p \v 12 “Ikiwa ugonjwa utakuwa umeenea kwenye ngozi yake yote kwa kadiri kuhani atakavyoweza kuona, kwamba umeenea kwenye ngozi yote ya huyo mgonjwa kutoka kichwani hadi wayo, \v 13 kuhani atamchunguza, na kama ugonjwa umeenea mwili mzima, atamtangaza huyo mtu kuwa safi. Kwa kuwa mwili wote umekuwa mweupe, yeye ni safi. \v 14 Lakini itokeapo nyama mbichi kwenye ngozi yake, atakuwa najisi. \v 15 Kuhani atakapoiona hiyo nyama mbichi, atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Hiyo nyama mbichi ni najisi, ana ugonjwa wa kuambukiza. \v 16 Hiyo nyama mbichi ikigeuka na kuwa nyeupe, ni lazima amwendee kuhani. \v 17 Kuhani atamchunguza, na kama vidonda vimekuwa vyeupe, kuhani atamtangaza mgonjwa huyo kuwa safi; kisha atakuwa safi. \p \v 18 “Wakati mtu ana jipu juu ya ngozi yake nalo likapona, \v 19 napo mahali palipokuwa na jipu pakatokea uvimbe mweupe, au alama yenye wekundu na weupe, ni lazima akajioneshe kwa kuhani. \v 20 Kuhani atapachunguza, na kama uvimbe umeingia ndani ya ngozi, na nywele zimegeuka kuwa nyeupe, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza uliojitokeza pale jipu lilipokuwa. \v 21 Lakini ikiwa kuhani anapopachunguza pakawa hapana nywele nyeupe ndani yake, wala hapakuingia ndani ya ngozi, na pameanza kupungua, basi kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba. \v 22 Kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. \v 23 Lakini ikiwa ile alama haijabadilika wala kuenea, ni kovu tu kutokana na jipu, kuhani atamtangaza kuwa safi. \p \v 24 “Wakati mtu ameungua kwenye ngozi yake, pakatokea alama yenye wekundu na weupe, au alama nyeupe ikaonekana penye nyama mbichi pale palipoungua, \v 25 kuhani ataichunguza ile alama, na kama nywele zilizo juu yake zimegeuka kuwa nyeupe, na panaonekana kuingia ndani ya ngozi, basi huo ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza ambao umetokea katika jeraha la moto. Kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. \v 26 Lakini kuhani akipachunguza na akaona kwamba hakuna nywele nyeupe kwenye alama ile, wala hapakuingia ndani ya ngozi, na pamepungua, basi kuhani atamtenga kwa siku saba. \v 27 Siku ya saba kuhani atamchunguza tena, na kama unaenea kwenye ngozi, kuhani atamtangaza kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. \v 28 Lakini, kama alama ile haikubadilika na wala haijaenea kwenye ngozi, napo pamepungua, ni uvimbe kutokana na jeraha la moto, na kuhani atamtangaza kuwa safi; ni kovu tu kutokana na kuungua. \p \v 29 “Ikiwa mwanaume au mwanamke ana kidonda juu ya kichwa au juu ya kidevu, \v 30 kuhani atakichunguza kile kidonda, na kama ataona kuwa kimeingia ndani ya ngozi, na nywele zilizo juu yake ni njano na nyembamba, kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi; ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza wa kichwa au kidevu. \v 31 Lakini kama kuhani akichunguza aina hii ya kidonda, kionekane kuwa hakijaingia ndani ya ngozi, na hakuna nywele nyeusi juu yake, basi atamtenga mtu huyo kwa siku saba. \v 32 Siku ya saba kuhani atachunguza kidonda kile, na kama hakijaenea, na hakuna nywele za manjano juu yake, wala haukuingia ndani ya ngozi, \v 33 mtu huyo ni lazima anyolewe, isipokuwa mahali palipo na ugonjwa, naye kuhani atamtenga kwa siku nyingine saba. \v 34 Siku ya saba kuhani atachunguza tena kidonda kile; ikiwa hakijaenea kwenye ngozi na hakikuingia ndani ya ngozi, kuhani atamtangaza kuwa safi. Lazima afue nguo zake, naye atakuwa safi. \v 35 Lakini ikiwa kidonda kitaenea katika ngozi baada ya kutangazwa kuwa safi, \v 36 kuhani atamchunguza, na kama kidonda kimeenea kwenye ngozi, kuhani hana haja ya kutazama kama kuna nywele za manjano; mtu huyo ni najisi. \v 37 Hata hivyo, katika uchunguzi wake akiona hapajabadilika, na nywele nyeusi zimeota juu yake, huyo mtu amepona. Yeye si najisi; kuhani atamtangaza kuwa safi. \p \v 38 “Ikiwa mwanaume au mwanamke ana alama nyeupe juu ya ngozi yake, \v 39 kuhani atamchunguza, na kama alama hizo zina weupe uliofifia, ni vipele visivyo na madhara vilivyojitokeza kwenye ngozi; mtu huyo ni safi. \p \v 40 “Wakati mwanaume hana nywele naye ana upara, yeye ni safi. \v 41 Ikiwa hana nywele kwenye ngozi ya kichwa chake, na ana upara kwenye paji, ni safi. \v 42 Lakini kama ana kidonda chenye wekundu na weupe kwenye kichwa chake chenye upara, au kwenye paji la uso, ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza unaojitokeza kichwani au kwenye paji lake la uso. \v 43 Kuhani atamchunguza, na kama kidonda kilichovimba juu ya kichwa chake au kwenye paji la uso ni chekundu au cheupe kama ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, \v 44 mtu huyo ni mgonjwa, na ni najisi. Kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya kidonda kwenye kichwa chake. \p \v 45 “Mtu mwenye ugonjwa kama huo wa kuambukiza ni lazima avae nguo zilizoraruka, awachilie nywele zake bila kuzichana, afunike sehemu ya chini ya uso wake, na apige kelele, ‘Najisi! Najisi!’ \v 46 Kwa muda wote atakaokuwa na ugonjwa huo wa kuambukiza atabaki kuwa najisi. Ni lazima aishi peke yake; ni lazima aishi nje ya kambi. \s1 Masharti kuhusu upele \p \v 47 “Kuhusu vazi lolote lililoharibiwa na maambukizo ya ukoma, liwe ni vazi la sufu au kitani, \v 48 vazi lolote lililofumwa au kusokotwa la kitani au sufu, ngozi yoyote au chochote kilichotengenezwa kwa ngozi: \v 49 ikiwa maambukizo kwenye vazi, ngozi, au vazi lililofumwa au kusokotwa la kitani au sufu, au kitu chochote cha ngozi, ni rangi ya kijani au nyekundu, huo ni ukoma unaoenea, na ni lazima kuhani aoneshwe. \v 50 Kuhani atachunguza ukoma huo na kulitenga vazi hilo kwa siku saba. \v 51 Siku ya saba atalichunguza, na kama ukoma umeenea kwenye vazi, au vazi lililofumwa au kusokotwa, au ngozi, kwa vyovyote vile itumikavyo, ni ukoma wa kuangamiza; vazi hilo ni najisi. \v 52 Ni lazima achome vazi hilo, liwe ni la sufu au kitani kilichofumwa au kusokotwa, au kitu chochote cha ngozi chenye maambukizo; kwa kuwa ni ukoma wa kuangamiza, vazi lote ni lazima lichomwe moto. \p \v 53 “Lakini kuhani akilichunguza na akaona kuwa ule ukoma haujaenea kwenye vazi, au vazi lililofumwa au kusokotwa, au kitu cha ngozi, \v 54 ataagiza kwamba vazi lenye maambukizo lisafishwe. Kisha atalitenga kwa siku nyingine saba. \v 55 Baada ya vazi lenye maambukizo kusafishwa, kuhani atalichunguza, na kama ukoma haujaonesha badiliko lolote, hata kama haujaenea, ni najisi. Lichome kwa moto, iwe ukoma umeenea upande mmoja au mwingine. \v 56 Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kuoshwa, basi atararua sehemu iliyoambukizwa ya vazi, au ngozi, au vazi lililofumwa au kusokotwa. \v 57 Lakini ikijitokeza tena kwenye vazi, au vazi lililofumwa au kusokotwa, ama kitu cha ngozi, ule ni ukoma unaoenea; chochote chenye ukoma ni lazima kichomwe kwa moto. \v 58 Vazi, au vazi lililofumwa au kusokotwa, au kitu chochote cha ngozi, baada ya kusafishwa na kuondolewa ukoma, ni lazima lioshwe tena, ili liwe safi.” \p \v 59 Haya ndio masharti kuhusu maambukizo ya ukoma kwenye mavazi ya sufu au kitani, mavazi yaliyofumwa au kusokotwa, ama kitu chochote cha ngozi, kwa ajili ya kuvitangaza kuwa safi au najisi. \c 14 \s1 Kutakasa kutoka maambukizo ya magonjwa ya ngozi \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Haya ndio masharti yanayomhusu mtu mgonjwa wakati wa ibada yake ya utakaso, anapoletwa kwa kuhani: \v 3 Kuhani ataenda kumchunguza nje ya kambi. Kama mtu huyo atakuwa amepona ugonjwa wake wa ngozi wa kuambukiza, \v 4 kuhani ataagiza vitu vifuatavyo viletwe kwa ajili ya mtu atakayetakaswa: ndege wawili safi walio hai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu, na hisopo. \v 5 Kisha kuhani ataagiza kwamba mmoja wa ndege wale achinjwe kwenye chungu chenye maji safi. \v 6 Kisha kuhani atamchukua ndege aliye hai na kumtumbukiza pamoja na mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo ndani ya damu ya yule ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi. \v 7 Atamnyunyizia yule mwenye ugonjwa wa kuambukiza maji hayo mara saba, na kumtangaza kuwa safi. Kisha atamwachia yule ndege aliye hai aende zake kwenye mashamba. \p \v 8 “Huyo mtu atakayetakaswa ni lazima afue nguo zake, anyoe nywele zake zote, na aoge kwa maji; ndipo atakapotakasika. Baada ya hili anaweza kuingia kambini, lakini ni lazima akae nje ya hema lake kwa siku saba. \v 9 Siku ya saba ni lazima anyoe nywele zake zote; yaani anyoe nywele za kichwa, ndevu zake, kope zake na nywele nyingine zote. Ni lazima afue nguo zake, na aoge kwa maji, naye atakuwa safi. \p \v 10 “Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi ya efa\f + \fr 14:10 \fr*\ft Sehemu tatu za kumi ya efa ni sawa na kilo 3.\ft*\f* ya unga laini uliochanganywa na mafuta, kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja\f + \fr 14:10 \fr*\ft Kipimo cha ujazo, sawa na lita 0.3.\ft*\f* ya mafuta. \v 11 Kuhani anayemtangaza kuwa safi atamkabidhi mtu huyo atakayetakaswa pamoja na sadaka zake zote mbele za Mwenyezi Mungu katika ingilio la Hema la Kukutania. \p \v 12 “Kisha kuhani atamchukua mmoja wa wale kondoo dume na kumtoa kuwa sadaka ya hatia, pamoja na ile logi moja ya mafuta; ataviinua mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. \v 13 Atamchinja huyo kondoo katika mahali patakatifu ambapo sadaka ya dhambi na ile ya kuteketezwa huchinjiwa. Kama ilivyo sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia ni ya kuhani; ni takatifu sana. \v 14 Kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya hatia na kuitia kwenye ncha ya sikio la kuume la yule atakayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. \v 15 Kisha kuhani atachukua sehemu ya ile logi ya mafuta, ayamimine kwenye kiganja cha mkono wake mwenyewe wa kushoto, \v 16 na achovye kidole chake cha shahada cha mkono wake wa kuume kwenye mafuta yaliyo kwenye kiganja chake, na kwa kidole hicho anyunyize mafuta hayo mara saba mbele za Mwenyezi Mungu. \v 17 Kuhani atampaka yule anayetakaswa sehemu ya mafuta yaliyobaki kiganjani kwenye ncha ya sikio lake la kuume, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume, mahali palepale alipompaka damu ya sadaka ya kuondoa hatia. \v 18 Kuhani atayapaka mafuta yaliyobaki kwenye kiganja chake juu ya kichwa cha yule anayetakaswa, na kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu. \p \v 19 “Kisha kuhani atatoa dhabihu ya sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwa ajili ya yule atakayetakaswa kutoka unajisi wake. Baada ya hayo, kuhani atachinja sadaka ya kuteketezwa \v 20 na kuitoa juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya nafaka ili kumfanyia upatanisho, naye atakuwa safi. \p \v 21 “Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, lazima achukue mwana-kondoo wa kiume mmoja kuwa sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho, pamoja na sehemu ya kumi ya efa\f + \fr 14:21 \fr*\ft Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na lita 2.\ft*\f* ya unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka, logi moja ya mafuta, \v 22 na hua wawili au makinda wawili wa njiwa, kile atakachoweza kupata, mmoja kwa sadaka ya dhambi, na mwingine kwa sadaka ya kuteketezwa. \p \v 23 “Katika siku ya nane, lazima avilete vitu hivyo kwa kuhani, kwa ajili ya kutakaswa kwake kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Mwenyezi Mungu. \v 24 Kuhani atamchukua mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia, pamoja na ile logi ya mafuta ya kuinuliwa mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. \v 25 Atamchinja huyo mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia. Kisha ataichukua sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, na aipake pia kwenye kidole gumba cha mkono wa kuume wa huyo mtu, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. \v 26 Kuhani atamiminia sehemu ya mafuta kwenye kiganja chake cha mkono wa kushoto, \v 27 na kwa kidole chake cha shahada cha mkono wa kuume, atamnyunyizia yule anayetakaswa yale mafuta yaliyo kwenye kiganja chake mara saba mbele za Mwenyezi Mungu. \v 28 Atampaka mafuta yaliyobaki kwenye kiganja chake katika sehemu zote, kama alivyompaka damu ya sadaka ya hatia: yaani kwenye ncha ya sikio la kuume la yule anayetakaswa, kwenye kidole gumba cha mkono wake wa kuume, na kidole kikubwa cha mguu wake wa kuume. \v 29 Kuhani atayapaka mafuta yaliyobaki katika kiganja chake kwenye kichwa cha yule anayetakaswa, na kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu. \v 30 Kisha atatoa dhabihu wale hua ama makinda wa njiwa ambao yule mtu ataweza kuwapata, \v 31 mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya yule anayetakaswa.” \p \v 32 Haya ndio masharti kwa mtu yeyote mwenye ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza, na ambaye hana uwezo wa kutoa sadaka za kawaida kwa ajili ya kutakaswa kwake. \s1 Kutakaswa upele \p \v 33 Mwenyezi Mungu akawaambia Musa na Haruni, \v 34 “Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani ninayowapa kuwa milki yenu, nami nikaweka ukoma\f + \fr 14:34 \fr*\ft ugonjwa wowote wa ngozi wa kuambukiza; pia hutumiwa kwa maambukizi kwenye mawe au matofali ya nyumba\ft*\f* unaoenea kwenye nyumba katika nchi ile, \v 35 ni lazima mwenye nyumba hiyo akamwambie kuhani, ‘Nimeona kitu fulani kinachofanana na ukoma kwenye nyumba yangu.’ \v 36 Kuhani ataagiza vitu vyote vitolewe ndani ya nyumba, kabla hajaenda kuchunguza kama ina ukoma huo, ili kitu chochote ndani ya nyumba kisitangazwe kuwa najisi. Baada ya hili, kuhani ataingia ndani na kuikagua hiyo nyumba. \v 37 Atachunguza ukoma huo katika kuta za nyumba hiyo, nazo kama zina rangi ya kijani kibichi au wekundu, na kuna mibonyeo ndani ya ukuta, \v 38 kuhani atatoka na kufunga mlango wa nyumba hiyo kwa siku saba. \v 39 Siku ya saba, kuhani atarudi kuikagua nyumba. Kama ukoma umeenea juu ya kuta, \v 40 ataagiza kwamba mawe yote yaliyoambukizwa yaondolewe na kutupwa katika eneo lililo najisi nje ya mji. \v 41 Kuta zote za ndani ya nyumba hiyo ni lazima zikwanguliwe, na kifusi chake kitupwe mahali najisi nje ya mji. \v 42 Kisha watachukua mawe mengine na kujenga palipobomolewa kwa udongo mpya wa mfinyanzi, na wapake nyumba hiyo chokaa. \p \v 43 “Ikiwa ukoma huo utatokea tena ndani ya ile nyumba baada ya mawe kuondolewa, na nyumba kukwanguliwa na kupakwa chokaa, \v 44 kuhani ataenda kuikagua, na kama ukoma umeenea ndani ya nyumba, basi ni ukoma unaoharibu; nyumba hiyo ni najisi. \v 45 Ni lazima ibomolewe: mawe yake, mbao na chokaa yote; vyote vikatupwe nje ya mji mahali palipo najisi. \p \v 46 “Yeyote atakayeingia katika nyumba hiyo ikiwa imefungwa, atakuwa najisi hadi jioni. \v 47 Yeyote atakayelala au kula ndani ya nyumba hiyo ni lazima afue nguo zake. \p \v 48 “Lakini ikiwa kuhani atakuja kuikagua na kukuta kuwa ukoma haujaenea tena baada ya nyumba kupakwa chokaa, ataitangaza nyumba ile kuwa safi, kwa sababu ukoma umekwisha. \v 49 Ili kuitakasa nyumba hiyo, mwenye nyumba ataleta ndege wawili, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo. \v 50 Atamchinja mmoja wa wale ndege kwenye chungu chenye maji safi. \v 51 Kisha atachukua mti wa mwerezi, hisopo, kitani nyekundu na ndege aliye hai, na kuvitumbukiza ndani ya damu ya ndege aliyechinjwa pamoja na maji safi, na kuinyunyizia nyumba ile mara saba. \v 52 Ataitakasa nyumba kwa damu ya yule ndege, maji safi, ndege aliye hai, mti wa mwerezi, hisopo na uzi mwekundu. \v 53 Kisha atamwachia yule ndege aliye hai huru mashambani nje ya mji. Kwa njia hii atafanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ile, nayo itakuwa safi.” \p \v 54 Haya ndio masharti kuhusu aina yoyote ya ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza\f + \fr 14:54 \fr*\ft yaani \ft*\fqa ukoma\fqa*\ft ; ni neno lililotumika kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi, ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi\ft*\f*, kidonda chochote, \v 55 ukoma katika vazi au ndani ya nyumba, \v 56 kwa uvimbe, upele, au alama nyeupe katika ngozi, \v 57 kupambanua wakati kitu fulani ni safi au najisi. \p Haya ndio masharti kuhusu magonjwa ya ngozi ya kuambukiza na ukoma. \c 15 \s1 Kutokwa na usaha usababishao unajisi \p \v 1 Mwenyezi Mungu akawaambia Musa na Haruni, \v 2 “Semeni na Waisraeli mwaambie: ‘Mtu yeyote anapotokwa na usaha mwilini, usaha huo ni najisi. \v 3 Iwe unaendelea kutiririka kutoka mwilini mwake au umeziba, utamfanya najisi. Hivi ndivyo usaha wake utakavyomletea unajisi: \p \v 4 “ ‘Kitanda chochote atakacholalia mtu mwenye kutokwa na usaha kitakuwa najisi, na chochote atakachokalia kitakuwa najisi. \v 5 Yeyote atakayegusa kitanda chake ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \v 6 Yeyote atakayeketi juu ya kitu chochote alichokalia mwenye kutokwa na usaha, ni lazima afue nguo zake, na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 7 “ ‘Yeyote atakayemgusa mtu mwenye kutokwa na usaha, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 8 “ ‘Ikiwa mtu mwenye kutokwa na usaha atamtemea mate mtu ambaye ni safi, mtu huyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 9 “ ‘Kila tandiko ambalo mtu huyo atalikalia wakati wa kupanda mnyama litakuwa najisi, \v 10 na yeyote atakayegusa kitu chochote alichokuwa amekalia atakuwa najisi hadi jioni. Yeyote atakayeinua vitu hivyo ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 11 “ ‘Yeyote atakayeguswa na mtu anayetokwa na usaha bila kunawa mikono yake kwa maji, ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 12 “ ‘Chungu cha udongo kitakachoguswa na mtu huyo ni lazima kivunjwe, na kifaa chochote cha mbao kitaoshwa kwa maji. \p \v 13 “ ‘Mtu atakapotakasika kutoka usaha wake, atahesabu siku saba kwa utakaso wake. Ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji safi, naye atatakasika. \v 14 Siku ya nane, atachukua hua wawili au makinda wawili wa njiwa, aje mbele za Mwenyezi Mungu kwenye ingilio la Hema la Kukutania, na kumpa kuhani. \v 15 Kuhani atawatoa dhabihu, mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii atafanya upatanisho mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya huyo mtu kwa sababu ya kutokwa usaha kwake. \p \v 16 “ ‘Mtu akitokwa na shahawa, ni lazima aoge mwili mzima kwa maji, na atakuwa najisi hadi jioni. \v 17 Vazi lolote ama ngozi yoyote yenye shahawa juu yake ni lazima ioshwe kwa maji, na itakuwa najisi hadi jioni. \v 18 Ikiwa mtu atalala na mwanamke, na kukawa na kutoka kwa shahawa, ni lazima wote waoge kwa maji, nao watakuwa najisi hadi jioni. \p \v 19 “ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 20 “ ‘Chochote atakacholalia wakati wake wa hedhi kitakuwa najisi, na chochote atakachokikalia kitakuwa najisi. \v 21 Yeyote atakayegusa kitanda chake ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \v 22 Yeyote atakayegusa chochote atakachokalia ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \v 23 Kiwe ni kitanda ama chochote alichokuwa amekikalia, ikiwa mtu yeyote atakigusa, atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 24 “ ‘Ikiwa mwanaume atalala naye na ile damu ya mwezi ikamgusa, atakuwa najisi kwa siku saba; kitanda chochote atakachokilalia huyo mwanaume kitakuwa najisi. \p \v 25 “ ‘Ikiwa mwanamke atatokwa na damu kwa siku nyingi zaidi ya siku zake za mwezi, au amekuwa na damu inayoendelea zaidi ya kipindi chake, atakuwa najisi kwa kipindi chote cha shida hiyo, kama ilivyokuwa katika siku za hedhi yake. \v 26 Kitanda chochote atakachokilalia huyo mwanamke wakati anaendelea kutokwa na damu kitakuwa najisi, kama kilivyokuwa kitanda chake wakati wa siku zake za hedhi, na chochote atakachokalia kitakuwa najisi, kama wakati wake wa hedhi. \v 27 Yeyote agusaye vitu hivyo atakuwa najisi; ni lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni. \p \v 28 “ ‘Atakapotakasika kutoka hedhi yake, ni lazima ahesabu siku saba, na baada ya hapo atakuwa ametakasika kabisa. \v 29 Siku ya nane ni lazima achukue hua wawili au makinda wawili wa njiwa, na kumletea kuhani kwenye mlango wa Hema la Kukutania. \v 30 Kuhani atatoa dhabihu, mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na huyo mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Kwa njia hii, atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu kwa sababu ya unajisi wa kutokwa damu kwake. \p \v 31 “ ‘Ni lazima uwatenge Waisraeli kutokana na vitu ambavyo vinawafanya najisi, ili wasife katika unajisi wao kwa kunajisi makao yangu\f + \fr 15:31 \fr*\ft yaani \ft*\fqa maskani ya Mungu\fqa*\f* yaliyo katikati yao.’ ” \p \v 32 Haya ni masharti kwa ajili ya mtu mwenye kutokwa na usaha, kwa ajili ya yeyote atakayetokwa na shahawa, \v 33 kwa ajili ya mwanamke katika siku zake za hedhi, kwa ajili ya mwanaume au mwanamke atokwaye na usaha, na kwa ajili ya mwanaume alalaye na mwanamke ambaye ni najisi. \c 16 \s1 Siku ya Upatanisho \p \v 1 Mwenyezi Mungu akasema na Musa baada ya kifo cha wale wana wawili wa Haruni waliokufa walipokaribia mbele za Mwenyezi Mungu. \v 2 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: “Mwambie ndugu yako Haruni asije wakati wowote anaotaka ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, nyuma ya pazia pale mbele ya kiti cha rehema kile kilicho juu ya Sanduku la Agano, la sivyo atakufa, kwa sababu huwa ninatokea ndani ya wingu juu ya kile kiti cha rehema. \p \v 3 “Hivi ndivyo Haruni atakavyoingia katika Mahali Patakatifu: atachukua fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. \v 4 Atavaa koti takatifu la kitani, pamoja na nguo za ndani za kitani; atafunga mshipi wa kitani kiunoni, na kuvaa kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu, kwa hiyo ni lazima aoge kwa maji kabla ya kuyavaa mavazi hayo. \v 5 Atachukua beberu wawili kutoka kwa jumuiya ya Israeli kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. \p \v 6 “Haruni atamtoa huyo fahali kwa ajili ya sadaka yake ya dhambi ili afanye upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na nyumba yake. \v 7 Kisha atawachukua wale beberu wawili na kuwaleta mbele za Mwenyezi Mungu kwenye ingilio la Hema la Kukutania. \v 8 Haruni atapiga kura kwa ajili ya hao mbuzi wawili, mmoja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na mwingine kwa ajili ya kubebeshwa dhambi\f + \fr 16:8 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Azazeli\fqa*\ft , maana yake \ft*\fqa mbuzi wa ondoleo la dhambi\fqa*\ft ; pia \+xt 16:10, 26\+xt*\ft*\f* za Israeli. \v 9 Haruni atamleta yule mbuzi ambaye kura ya Mwenyezi Mungu imemwangukia na kumtoa dhabihu kwa ajili ya sadaka ya dhambi. \v 10 Lakini mbuzi aliyechaguliwa kwa kura kuwa wa kubebeshwa dhambi atatolewa akiwa hai mbele za Mwenyezi Mungu, atumike kwa kufanya upatanisho kwa kumwacha aende jangwani akiwa amebebeshwa dhambi. \p \v 11 “Haruni atamleta yule fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake mwenyewe, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake na nyumba yake, naye atamchinja huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi yake mwenyewe. \v 12 Atachukua chetezo kilichojaa makaa yanayowaka kutoka madhabahuni mbele za Mwenyezi Mungu, na konzi mbili za uvumba laini uliosagwa vizuri wenye harufu, na kuvipeleka nyuma ya pazia. \v 13 Ataweka uvumba juu ya moto mbele za Mwenyezi Mungu, na moshi wa uvumba utafunika kile kiti cha rehema kilicho juu ya Ushuhuda, ili asife. \v 14 Atachukua sehemu ya damu ya fahali, na kwa kidole chake atanyunyiza sehemu ya mbele ya kiti cha rehema; kisha atanyunyiza sehemu ya hiyo damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kiti cha rehema. \p \v 15 “Kisha atamchinja mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu, na kuichukua damu yake nyuma ya pazia, na aifanyie kama alivyofanya kwa damu ya fahali: Atanyunyiza juu ya kiti cha rehema na mbele yake. \v 16 Kwa njia hii atafanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu kwa sababu ya unajisi na uasi wa Waisraeli, kwa dhambi zao zozote. Atafanya hivyo kwa ajili ya Hema la Kukutania, ambalo liko miongoni mwao katikati ya unajisi wao. \v 17 Mtu yeyote haruhusiwi kuwa ndani ya Hema la Kukutania, kuanzia wakati Haruni anapoingia kufanya upatanisho katika Patakatifu pa Patakatifu, hadi atakapotoka nje, baada ya kujifanyia upatanisho yeye mwenyewe na nyumba yake, pamoja na jumuiya yote ya Israeli. \p \v 18 “Kisha atatoka aje kwenye madhabahu yaliyo mbele za Mwenyezi Mungu na kufanya upatanisho kwa ajili yake. Atachukua sehemu ya damu ya fahali na sehemu ya damu ya mbuzi, na kuiweka kwenye pembe za madhabahu. \v 19 Atanyunyiza sehemu ya hiyo damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, ili kuitakasa na kuiweka wakfu kutokana na unajisi wa Waisraeli. \p \v 20 “Haruni atakapokuwa amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, atamleta mbele yule mbuzi aliye hai. \v 21 Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, ili kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo. \v 22 Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote hadi mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani. \p \v 23 “Kisha Haruni ataenda ndani ya Hema la Kukutania na kuvua yale mavazi ya kitani aliyoyavaa kabla ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu, naye atayaacha pale. \v 24 Ataoga kwa maji katika mahali patakatifu na kuvaa mavazi yake ya kawaida. Kisha atatoka na kutoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yake na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya watu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe, na kwa ajili ya watu. \v 25 Pia atachoma mafuta ya mnyama wa sadaka ya dhambi juu ya madhabahu. \p \v 26 “Yule mtu anayemwachia yule mbuzi wa kubebeshwa dhambi ni lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji; baadaye anaweza kuingia kambini. \v 27 Yule fahali na mbuzi waliotolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambao damu yao ilikuwa imeletwa Patakatifu pa Patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho, ni lazima watolewe nje ya kambi. Ngozi zao, nyama, na matumbo vitateketezwa kwa moto. \v 28 Mtu atakayevichoma ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; baadaye ataweza kuingia kambini. \p \v 29 “Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Katika siku ya kumi ya mwezi wa saba ni lazima mfunge, wala msifanye kazi yoyote, iwe mzawa au mgeni anayeishi miongoni mwenu, \v 30 kwa sababu siku hii upatanisho utafanyika kwa ajili yenu ili kuwatakasa. Kisha mtakuwa safi mbele za Mwenyezi Mungu kutokana na dhambi zenu zote. \v 31 Ni Sabato ya mapumziko, na lazima mfunge; ni agizo la kudumu. \v 32 Kuhani ambaye amepakwa mafuta na kuwekwa wakfu ili kuingia mahali pa baba yake kama kuhani mkuu atafanya upatanisho. Atavaa mavazi matakatifu ya kitani, \v 33 na kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, na pia kwa ajili ya makuhani, pamoja na jumuiya yote ya watu. \p \v 34 “Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu: Upatanisho utafanywa mara moja tu kwa mwaka kwa ajili ya dhambi zote za Waisraeli.” \p Ndivyo ilivyofanyika, kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa. \c 17 \s1 Kunywa damu kunakatazwa \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Sema na Haruni na wanawe, pamoja na Waisraeli wote, uwaambie: ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloagiza: \v 3 Mwisraeli yeyote atakayetoa dhabihu ya ng’ombe, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake, \v 4 badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu mbele ya Maskani ya Mwenyezi Mungu, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; amemwaga damu, na ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. \v 5 Hii ni ili Waisraeli wamletee Mwenyezi Mungu dhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwa Mwenyezi Mungu, katika ingilio la Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu kuwa sadaka za amani. \v 6 Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu ya Mwenyezi Mungu katika ingilio la Hema la Kukutania, na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \v 7 Kamwe wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa vizazi vijavyo.’ \p \v 8 “Waambie: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi miongoni mwao atakayetoa sadaka ya kuteketezwa au dhabihu \v 9 bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. \p \v 10 “ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye atakula damu yoyote, nitakuwa kinyume chake, na nitamkatilia mbali na watu wake. \v 11 Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu. \v 12 Kwa hiyo, ninawaambia Waisraeli, “Hakuna hata mmoja wenu anayeruhusiwa kula damu, wala mgeni anayeishi miongoni mwenu haruhusiwi kula damu.” \p \v 13 “ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye atamwinda mnyama au ndege anayeruhusiwa kuliwa ni lazima aimwage damu na kuifunika kwa udongo, \v 14 kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msile damu ya kiumbe chochote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni damu yake; yeyote atakayekula damu lazima akatiliwe mbali.” \p \v 15 “ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni; kisha atakuwa ametakaswa. \v 16 Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ” \c 18 \s1 Uhusiano wa kukutana kimwili kinyume cha Torati \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \v 3 Msifanye kama wafanyavyo huko Misri, mahali mlipokuwa mnaishi, wala msifanye kama wanavyofanya katika nchi ya Kanaani, mahali ninapowapeleka. Msifuate matendo yao. \v 4 Ni lazima mzitii sheria zangu, na mwe waangalifu kuzifuata amri zangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \v 5 Zishikeni amri zangu na sheria zangu, kwa maana mtu anayezitii ataishi kwa hizo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 6 “ ‘Hakuna mtu yeyote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 7 “ ‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye. \p \v 8 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako. \p \v 9 “ ‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine. \p \v 10 “ ‘Usikutane kimwili na binti ya mwanao ama binti ya binti yako; utajivunjia heshima. \p \v 11 “ ‘Usikutane kimwili na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako. \p \v 12 “ ‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako. \p \v 13 “ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu. \p \v 14 “ ‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako. \p \v 15 “ ‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye. \p \v 16 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako. \p \v 17 “ ‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti ya mwanawe au binti ya binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu. \p \v 18 “ ‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi. \p \v 19 “ ‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi. \p \v 20 “ ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi. \p \v 21 “ ‘Usimtoe kafara mtoto wako yeyote kwa Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 22 “ ‘Usikutane kimwili na mwanaume vile mwanaume anavyokutana kimwili na mwanamke; hilo ni chukizo. \p \v 23 “ ‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu. \p \v 24 “ ‘Msijitie unajisi kwa njia yoyote katika hizi, kwa sababu hivi ndivyo mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu yalivyojitia unajisi. \v 25 Hata nchi ilitiwa unajisi, hivyo nikaiadhibu kwa dhambi zake, nayo nchi ikawatapika wakazi wake. \v 26 Lakini ni lazima mzitunze amri zangu na sheria zangu. Wazawa na wageni wanaoishi miongoni mwenu kamwe wasifanye mambo yoyote ya machukizo haya, \v 27 kwa kuwa mambo haya yote yalifanywa na watu walioishi katika nchi hii kabla yenu, na nchi ikawa najisi. \v 28 Mkiinajisi nchi, itawatapika kama ilivyowatapika mataifa yaliyowatangulia. \p \v 29 “ ‘Kila mtu atakayefanya mojawapo ya machukizo haya, watu hao ni lazima wakatiliwe mbali na watu wao. \v 30 Shikeni maagizo yangu, wala msifuate desturi za machukizo yoyote yaliyofanywa kabla hamjafika katika nchi hii, na kujitia unajisi kwa hayo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ” \c 19 \s1 Sheria mbalimbali \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Sema na kusanyiko lote la Waisraeli, uwaambie: ‘Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi, Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni mtakatifu. \p \v 3 “ ‘Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \p \v 4 “ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya kusubu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \p \v 5 “ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu. \v 6 Sadaka hiyo italiwa siku hiyo hiyo mnayoitoa, au kesho yake; chochote kitakachobaki hadi siku ya tatu lazima kiteketezwe kwa moto. \v 7 Kama sehemu yoyote ya sadaka hiyo italiwa siku ya tatu, itakuwa si safi, nayo haitakubaliwa. \v 8 Yeyote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake. \p \v 9 “ ‘Unapovuna mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako. \v 10 Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p \v 11 “ ‘Usiibe. \p “ ‘Usiseme uongo. \p “ ‘Msidanganyane. \p \v 12 “ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu, na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 13 “ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako. \p “ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi. \p \v 14 “ ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 15 “ ‘Usipotoshe haki; usioneshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki. \p \v 16 “ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. \p “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 17 “ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake. \p \v 18 “ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 19 “ ‘Mtazishika amri zangu. \p “ ‘Usiwaache mifugo wako wakazaana na wa aina tofauti. \p “ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako. \p “ ‘Usivae vazi lililofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti. \p \v 20 “ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mjakazi aliyeposwa na mwanaume mwingine, ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru. \v 21 Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Mwenyezi Mungu. \v 22 Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake. \p \v 23 “ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa. \v 24 Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa Mwenyezi Mungu. \v 25 Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezewa. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p \v 26 “ ‘Msile nyama yoyote yenye damu ndani yake. \p “ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi. \p \v 27 “ ‘Msikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu. \p \v 28 “ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 29 “ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu. \p \v 30 “ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 31 “ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p \v 32 “ ‘Ukiwa mbele ya mzee, simama ili kuonesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 33 “ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase. \v 34 Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p \v 35 “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. \v 36 Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa\f + \fr 19:36 \fr*\ft Efa kilikuwa kipimo cha vitu vikavu.\ft*\f* halali, na hini\f + \fr 19:36 \fr*\ft Hini kilikuwa kipimo cha vitu vimiminika.\ft*\f* halali. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri. \p \v 37 “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \c 20 \s1 Adhabu kwa ajili ya dhambi \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waambie Waisraeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi Israeli atakayemtoa kafara mtoto wake yeyote kwa Moleki lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe. \v 3 Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa kafara mmoja wa watoto wake kwa Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu. \v 4 Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho yao wakati mtu huyo anapomtoa kafara mmoja wa watoto wake kwa Moleki, nao wakaacha kumuua, \v 5 mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo pamoja na jamaa yake, nami nitawakatilia mbali yeye na watu wote waliofanya ukahaba na Moleki. \p \v 6 “ ‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayeenda kwa waaguzi na wenye pepo, na hivyo kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake. \p \v 7 “ ‘Jitakaseni basi, nanyi kuweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \v 8 Shikeni amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, niwafanyaye ninyi watakatifu. \p \v 9 “ ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani baba yake au mama yake, lazima auawe. Amemlaani baba yake au mama yake, nayo damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. \p \v 10 “ ‘Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe. \p \v 11 “ ‘Kama mtu atakutana kimwili na mke wa baba yake, hakumheshimu baba yake. Mwanaume huyo na mwanamke huyo wote wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe. \p \v 12 “ ‘Ikiwa mtu atakutana kimwili na mke wa mwanawe, lazima wote wawili wauawe. Walichokifanya ni upotovu; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe. \p \v 13 “ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe. \p \v 14 “ ‘Ikiwa mwanaume ataoa binti pamoja na mama yake, huo ni uovu. Wote watatu ni lazima wachomwe moto, ili pasiwepo na uovu kati yenu. \p \v 15 “ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mnyama, ni lazima auawe, na pia ni lazima mnyama huyo auawe. \p \v 16 “ ‘Kama mwanamke atamsogelea mnyama kukutana naye kimwili, muueni mwanamke huyo pamoja na mnyama pia. Lazima wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe. \p \v 17 “ ‘Ikiwa mtu atamwoa dada yake, binti aliyezaliwa na baba yake au mama yake, nao wakakutana kimwili, ni aibu. Lazima wakatiliwe mbali machoni pa watu wao. Huyo mwanaume amemwaibisha dada yake, hivyo atawajibika kwa ajili ya uovu huo. \p \v 18 “ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na mwanamke aliye katika hedhi yake, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao. \p \v 19 “ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo. \p \v 20 “ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na shangazi yake, amemwaibisha mjomba wake. Nao watawajibika kwa ajili ya uovu huo; watakufa bila kuzaa mtoto. \p \v 21 “ ‘Ikiwa mwanaume ataoa mke wa ndugu yake, hili ni tendo chafu; amemwaibisha ndugu yake. Nao hawatazaa mtoto. \p \v 22 “ ‘Zishikeni amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike. \v 23 Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nilichukizwa sana nao. \v 24 Lakini niliwaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye amewatenga kutoka mataifa. \p \v 25 “ ‘Kwa hiyo, ninyi lazima mweze kutofautisha kati ya wanyama walio safi na wasio safi, pia kati ya ndege wasio safi na walio safi. Msijitie unajisi kutokana na mnyama yeyote, au ndege, wala kiumbe chochote kinachotambaa juu ya ardhi, ambavyo nimevitenga kuwa najisi kwa ajili yenu. \v 26 Mtakuwa watakatifu kwangu, kwa sababu Mimi, Mwenyezi Mungu, ni mtakatifu, nami nimewatenga kutoka mataifa kuwa wangu mwenyewe. \p \v 27 “ ‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’ ” \c 21 \s1 Sheria kwa ajili ya makuhani \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Sema na makuhani, wana wa Haruni, uwaambie: ‘Kamwe kuhani asijitie unajisi kwa ajili ya mtu wake yeyote anayekufa, \v 2 isipokuwa jamaa wake wa karibu, kama vile mama yake au baba yake, mwanawe au binti yake, ndugu yake, \v 3 au dada yake asiyeolewa ambaye anamtegemea kwa kuwa hana mume, kwa ajili ya hao aweza kujitia unajisi. \v 4 Kamwe asijitie unajisi mwenyewe kutokana na wale watu ambao anahusiana nao kwa kuoana, na hivyo kujitia unajisi. \p \v 5 “ ‘Kamwe makuhani wasinyoe nywele za vichwa vyao wala wasinyoe pembeni mwa ndevu zao, au kuweka chale kwenye miili yao. \v 6 Lazima wawe watakatifu kwa Mungu wao, na kamwe wasilinajisi jina la Mungu wao. Kwa sababu ndio wanaotoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu, chakula cha Mungu wao, hivyo lazima wawe watakatifu. \p \v 7 “ ‘Kamwe wasioe wanawake waliojinajisi kwa ukahaba, au waliopewa talaka na waume wao, kwa sababu makuhani ni watakatifu kwa Mungu wao. \v 8 Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu Mimi Mwenyezi Mungu ni mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi kuwa watakatifu. \p \v 9 “ ‘Ikiwa binti ya kuhani anajitia unajisi kwa kufanya ukahaba, anamwaibisha baba yake; lazima achomwe kwa moto. \p \v 10 “ ‘Kuhani mkuu, yule miongoni mwa ndugu zake ambaye amekwisha kupakwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake, na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa, wala asirarue nguo zake. \v 11 Kamwe asiingie mahali palipo maiti ndani. Kamwe asijitie unajisi, hata kwa ajili ya baba yake au mama yake, \v 12 wala asiondoke mahali patakatifu pa Mungu wake au kupanajisi, kwa sababu amewekwa wakfu kwa mafuta ya Mungu wake. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 13 “ ‘Mwanamke atakayeolewa na kuhani lazima awe bikira. \v 14 Kamwe asimwoe mjane, au mwanamke aliyepewa talaka, wala mwanamke aliyejinajisi kwa ukahaba, bali atamwoa tu bikira kutoka miongoni mwa watu wake, \v 15 na hivyo hatawatia unajisi wazao wake miongoni mwa watu wake. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nimfanyaye mtakatifu.’ ” \p \v 16 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 17 “Mwambie Haruni: ‘Kwa vizazi vijavyo, hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake. \v 18 Hakuna mtu mwenye dosari yoyote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili, \v 19 hakuna mtu mwenye mguu au mkono uliolemaa, \v 20 au mwenye kibiongo au aliyedumaa, au aliye na tatizo la macho, au aliye na uvimbe wenye usaha au majipu, au aliyehasiwa. \v 21 Hakuna mzao wa kuhani Haruni mwenye kilema chochote atakayekaribia kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu. Kama ana kilema, kamwe asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake. \v 22 Anaweza kula chakula kitakatifu sana cha Mungu wake, pia hata chakula kitakatifu. \v 23 Lakini kwa sababu ya kilema chake, kamwe asikaribie pazia wala kukaribia madhabahu, asije akanajisi mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, niwafanyaye watakatifu.’ ” \p \v 24 Basi Musa akanena na Haruni, na wanawe, na Waisraeli wote. \c 22 \s1 Matumizi ya sadaka takatifu \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Mwambie Haruni na wanawe kushughulikia kwa uangalifu sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwangu, ili wasilinajisi Jina langu takatifu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 3 “Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa yeyote wa wazao wako ni najisi, naye akakaribia sadaka takatifu zile Waisraeli wanazoweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 4 “ ‘Ikiwa mzao wa Haruni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu hadi atakasike. Pia atakuwa najisi akigusa kitu chochote kilicho najisi kutokana na kugusa maiti, au akigusa mtu aliyetokwa na shahawa, \v 5 au akigusa kitu chochote kinachotambaa kimfanyacho mtu najisi, au mtu yeyote awezaye kumtia unajisi, hata unajisi uwe gani. \v 6 Mtu anayegusa kitu chochote cha aina hiyo atakuwa najisi hadi jioni. Kamwe hatakula sadaka yoyote takatifu hadi yeye mwenyewe awe ameoga kwa maji. \v 7 Jua linapotua, atakuwa safi, na baadaye anaweza kula sadaka takatifu, kwa kuwa ni vyakula vyake. \v 8 Kamwe asile nyama ya mzoga wala iliyoraruliwa na wanyama pori, naye akatiwa unajisi kwa hilo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 9 “ ‘Makuhani lazima washike maagizo yangu ili wasiwe na hatia, wakafa kwa kuyadharau. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu ninayewafanya watakatifu. \p \v 10 “ ‘Hakuna mtu yeyote asiye wa jamaa ya kuhani anayeruhusiwa kula sadaka takatifu, hata mgeni wa kuhani au mfanyakazi wake haruhusiwi kuila. \v 11 Lakini ikiwa kuhani amenunua mtumwa kwa fedha, au mtumwa amezaliwa katika nyumba ya kuhani huyo, mtumwa huyo aweza kula chakula cha huyo kuhani. \v 12 Ikiwa binti ya kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, binti huyo haruhusiwi kula chochote cha matoleo matakatifu. \v 13 Lakini ikiwa binti ya kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, na akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula chochote katika chakula hiki. \p \v 14 “ ‘Ikiwa mtu yeyote amekula sadaka takatifu kwa makosa, lazima atoe malipo ya sadaka hiyo kwa kuhani na kuongeza sehemu ya tano ya thamani ya sadaka hiyo. \v 15 Kamwe makuhani wasiinajisi sadaka takatifu ambayo Waisraeli wameitoa kwa Mwenyezi Mungu \v 16 kwa kuwaruhusu kuzila sadaka hizo takatifu, na hivyo kuwaletea hatia ya kudaiwa malipo. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu niwafanyaye watakatifu.’ ” \s1 Dhabihu zisizokubalika \p \v 17 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 18 “Sema na Haruni na wanawe, na Waisraeli wote uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari, \v 19 lazima amtoe mnyama dume asiye na dosari, akiwa ng’ombe, mbuzi au kondoo, ili aweze kukubalika kwa niaba yako. \v 20 Kamwe usitoe kitu chochote chenye dosari kwa sababu hakitakubaliwa kwa niaba yako. \v 21 Mtu yeyote aletapo sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu kutoka kundi la ng’ombe au la mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike. \v 22 Kamwe usimtolee Mwenyezi Mungu mnyama aliye kipofu, aliyejeruhiwa wala aliye kilema, au chochote kilicho na uvimbe, au chenye upele au vidonda vinavyotoka usaha. Kamwe chochote cha aina hii kisiwekwe juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu ya kuteketezwa kwa moto. \v 23 Lakini unaweza ukamtoa ng’ombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa kuwa sadaka ya hiari, lakini hii haitakubalika kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri. \v 24 Kamwe usimtolee Mwenyezi Mungu mnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au kuhasiwa, au kuraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye hivi katika nchi yako mwenyewe, \v 25 na kamwe usikubali wanyama wa aina hii kutoka mkono wa mgeni ili kuwatoa wanyama hao kuwa chakula kwa Mungu wako. Wanyama hao hawatakubaliwa kwa niaba yako, kwa sababu wana vilema, nao wana dosari.’ ” \p \v 26 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 27 “Ndama, mwana-kondoo au mwana-mbuzi anapozaliwa, atabaki na mama yake kwa siku saba. Kuanzia siku ya nane na kuendelea anaweza kukubaliwa kuwa sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto. \v 28 Usimchinje ng’ombe na ndama wake, au kondoo na kitoto chake siku moja. \p \v 29 “Unapomtolea Mwenyezi Mungu dhabihu ya shukrani, itoe kwa namna ambayo itakubalika kwa niaba yako. \v 30 Ni lazima iliwe siku hiyo hiyo, pasipo kubakiza chochote hadi asubuhi. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 31 “Shikeni maagizo yangu na kuyafuata. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 32 Msilinajisi Jina langu takatifu. Lazima nikubalike kuwa mtakatifu kwa Waisraeli. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu ninayewafanya watakatifu, \v 33 na niliyewatoa katika nchi ya Misri niwe Mungu wenu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \c 23 \s1 Sikukuu zilizoamriwa \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamriwa, sikukuu zilizoamriwa za Mwenyezi Mungu, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu. \s2 Sabato \p \v 3 “ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu. \s2 Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu \r (Hesabu 28:16-25) \p \v 4 “ ‘Hizi ni sikukuu za Mwenyezi Mungu zilizoamriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamriwa: \v 5 Pasaka ya Mwenyezi Mungu huanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. \v 6 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa kwanza, Sikukuu ya Mwenyezi Mungu ya Mikate Isiyotiwa Chachu huanza; kwa siku saba, mtakula mikate isiyotiwa chachu. \v 7 Katika siku ya kwanza, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. \v 8 Kwa siku saba mtamletea Mwenyezi Mungu sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku hiyo ya saba mtafanya kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida.’ ” \s2 Malimbuko \p \v 9 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 10 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa nafaka ya kwanza mtakayovuna. \v 11 Naye atauinua huo mganda mbele za Mwenyezi Mungu ili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato. \v 12 Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwa Mwenyezi Mungu dhabihu ya kuteketezwa kwa moto ya mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari, \v 13 pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi ya efa\f + \fr 23:13 \fr*\ft Sehemu mbili za kumi ya efa ni sawa na kilo mbili.\ft*\f* ya unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto; hii itakuwa sadaka iliyo harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hini\f + \fr 23:13 \fr*\ft Robo ya hini ni sawa na lita moja.\ft*\f* ya divai. \v 14 Kamwe msile mkate wowote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, hadi siku ile mtakayomletea Mungu wenu sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi. \s2 Sikukuu ya Majuma \r (Hesabu 28:26-31) \p \v 15 “ ‘Tangu siku ile iliyofuata Sabato, siku mliyotoa sadaka ya mganda wa kuinuliwa, hesabuni majuma saba kamili. \v 16 Mtahesabu siku hamsini hadi siku inayofuata Sabato ya saba, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwa Mwenyezi Mungu. \v 17 Kutoka popote mnapoishi, mtaleta mikate miwili iliyotengenezwa kwa sehemu mbili za kumi ya efa moja ya unga laini, uliookwa kwa chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwa Mwenyezi Mungu. \v 18 Toeni pamoja na hiyo mikate wana-kondoo saba, kila mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, na fahali mchanga, na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu, pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, sadaka iliyotolewa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. \v 19 Kisha toeni dhabihu ya beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili, kila mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya amani. \v 20 Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhani. \v 21 Siku hiyo hiyo mtatangaza kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mtakapoishi. \p \v 22 “ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ” \s2 Sikukuu ya Tarumbeta \r (Hesabu 29:1-6) \p \v 23 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 24 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na Sabato ya mapumziko, kusanyiko takatifu la ukumbusho litakaloadhimishwa kwa kupiga tarumbeta. \v 25 Msifanye kazi zenu zozote za kawaida, lakini toeni sadaka kwa Mwenyezi Mungu iliyoteketezwa kwa moto.’ ” \s2 Siku ya Upatanisho \r (Hesabu 29:7-11) \p \v 26 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 27 “Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, na kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu. \v 28 Msifanye kazi siku hiyo, kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ambapo upatanisho unafanyika kwa ajili yenu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \v 29 Mtu ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. \v 30 Mtu atakayefanya kazi siku hiyo nitamwangamiza kutoka miongoni mwa watu wake. \v 31 Hamtafanya kazi kamwe. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo popote mnapoishi. \v 32 Ni Sabato ya mapumziko kwenu, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.” \s2 Sikukuu ya Vibanda \r (Hesabu 29:12-40) \p \v 33 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 34 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu ya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba kwa Mwenyezi Mungu. \v 35 Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida. \v 36 Kwa siku saba toeni sadaka kwa Mwenyezi Mungu za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida. \p \v 37 (“ ‘Hizi ni sikukuu za Mwenyezi Mungu zilizoamriwa, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu kwa kuleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu za kuteketeza kwa moto: sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, dhabihu na sadaka za vinywaji zitahitajika kila siku. \v 38 Sadaka hizi ni nyongeza ya zile mnazozitoa katika Sabato za Mwenyezi Mungu, na pia ni nyongeza ya matoleo yenu ya chochote mlichoweka nadhiri, na sadaka zenu zote za hiari mnazozitoa kwa Mwenyezi Mungu.) \p \v 39 “ ‘Basi kuanzia siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, baada ya kuvuna mazao yote ya nchi, mtaadhimisha sikukuu kwa Mwenyezi Mungu kwa siku saba; siku ya kwanza ni Sabato ya mapumziko, na pia siku ya nane ni Sabato ya mapumziko. \v 40 Siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa siku saba. \v 41 Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa Mwenyezi Mungu kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni mwezi wa saba. \v 42 Mtaishi katika vibanda kwa siku saba: Wazawa wote wa Waisraeli wataishi katika vibanda, \v 43 ili wazao wenu wajue kuwa niliwafanya Waisraeli waishi kwenye vibanda nilipowatoa Misri. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ” \p \v 44 Kwa hiyo Musa akawatangazia Waisraeli sikukuu zilizoamriwa na Mwenyezi Mungu. \c 24 \s1 Mafuta na mikate mbele za Mwenyezi Mungu \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. \v 3 Nje ya pazia la Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Haruni ataziwasha taa mbele za Mwenyezi Mungu kuanzia jioni hadi asubuhi daima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. \v 4 Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Mwenyezi Mungu lazima zihudumiwe daima. \p \v 5 “Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi ya efa\f + \fr 24:5 \fr*\ft Sehemu mbili za kumi ya efa ni sawa na kilo mbili.\ft*\f* ya unga kwa kila mkate. \v 6 Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Mwenyezi Mungu juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. \v 7 Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto. \v 8 Mikate hii itawekwa mbele za Mwenyezi Mungu kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa agano la kudumu. \v 9 Hii ni mali ya Haruni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao milele la sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto.” \s1 Mwenye kukufuru apigwa mawe \p \v 10 Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alienda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli. \v 11 Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Mwenyezi Mungu kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Musa. (Mama yake aliitwa Shelomithi binti Dibri, wa kabila la Dani.) \v 12 Nao wakamweka mahabusu hadi mapenzi ya Mwenyezi Mungu yawe wazi kwao. \p \v 13 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: \v 14 “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote watampiga mawe. \v 15 Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake. \v 16 Yeyote atakayekufuru Jina la Mwenyezi Mungu ni lazima auawe. Kusanyiko lote watampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la Mwenyezi Mungu, ni lazima auawe. \p \v 17 “ ‘Kama mtu yeyote atamuua mtu mwingine, ni lazima auawe. \v 18 Mtu yeyote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai. \v 19 Ikiwa mtu yeyote atamjeruhi jirani yake, chochote alichomtenda naye atatendewa: \v 20 iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa. \v 21 Yeyote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini yeyote auaye mtu, lazima auawe. \v 22 Mtakuwa na sheria hiyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ” \p \v 23 Kisha Musa akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \c 25 \s1 Mwaka wa Sabato \r (Kumbukumbu 15:1-11) \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa katika Mlima Sinai, \v 2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike sabato kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. \v 3 Kwa miaka sita mtapanda mazao katika mashamba yenu, nanyi kwa miaka sita mtaikata mizabibu yenu matawi na kuvuna mazao yake. \v 4 Lakini katika mwaka wa saba, nchi lazima iwe na sabato ya mapumziko, sabato kwa Mwenyezi Mungu. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi. \v 5 Msivune chochote kinachoota chenyewe, wala kuvuna zabibu zenu ambazo hamkuzihudumia. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko. \v 6 Chochote nchi itoacho katika mwaka wa sabato kitakuwa chakula chenu wenyewe, watumishi wenu wa kiume na wa kike, mfanyakazi aliyeajiriwa, na mkazi wa muda anayeishi miongoni mwenu, \v 7 vilevile malisho ya mifugo yenu na wanyama pori katika nchi yenu. Chochote nchi itakachozalisha kinaweza kuliwa. \s1 Mwaka wa Yubile \p \v 8 “ ‘Hesabu sabato saba za miaka saba, yaani miaka saba mara saba, ili sabato saba za miaka saba ziwe muda wa miaka arobaini na tisa. \v 9 Ndipo tarumbeta itapigwa kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho, piga tarumbeta katika nchi yako yote. \v 10 Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni Yubile\f + \fr 25:10 \fr*\ft Yubile ni baragumu iliyopigwa kila mwaka wa hamsini; ni Sabato ya nchi ya kila mwaka wa hamsini uliokuwa mwaka wa ukombozi, yaani kuachia huru.\ft*\f* kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake. \v 11 Mwaka wa hamsini utakuwa Yubile kwenu, msipande wala msivune kile kinachoota chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa. \v 12 Kwa kuwa ni Yubile, nayo itakuwa takatifu kwenu; mtakula tu kile kilichotoka moja kwa moja mashambani. \p \v 13 “ ‘Katika huu Mwaka wa Yubile, kila mmoja atarudi kwenye mali yake mwenyewe. \p \v 14 “ ‘Ikiwa utauza ardhi kwa mmoja wa wazawa wa nchi yako, au ukinunua ardhi kutoka kwake, mmoja asimpunje mwingine. \v 15 Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kulingana na hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye muuzaji ataiuza kwako kulingana na hesabu ya miaka iliyobaki ya kuvuna mavuno. \v 16 Miaka inapokuwa mingi, utaongeza bei, nayo miaka ikiwa michache, utapunguza bei, kwa sababu kile anachokuuzia kwa hakika ni hesabu ya mazao. \v 17 Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p \v 18 “ ‘Fuateni amri zangu na mwe waangalifu kutii amri zangu, nanyi mtaishi salama katika nchi. \v 19 Kisha nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba na kuishi humo kwa salama. \v 20 Mwaweza kuuliza, “Tutakula nini katika mwaka wa saba ikiwa hatutapanda wala kuvuna mazao yetu?” \v 21 Nitawaletea baraka ya pekee katika mwaka wa sita, ili nchi iweze kuzalisha mazao ya kuwatosha kwa miaka mitatu. \v 22 Mnapopanda mwaka wa nane, mtakula mavuno ya miaka iliyopita, na mtaendelea kuyala mazao hayo hadi mvune mavuno ya mwaka wa tisa. \p \v 23 “ ‘Kamwe ardhi isiuzwe kwa mkataba wa kudumu, kwa sababu nchi ni mali yangu, nanyi ni wageni na wapangaji wangu. \v 24 Katika nchi yote mtakayoshika kuwa milki yenu, ni lazima mtoe ukombozi wa ardhi. \p \v 25 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini na akauza baadhi ya mali yake, ndugu yake wa karibu atakuja na kukomboa kile ndugu yake alichokiuza. \v 26 Iwapo mtu huyo hana jamaa wa karibu wa kukomboa mali hiyo kwa ajili yake, lakini yeye mwenyewe akafanikiwa na kupata mali itoshayo kuikomboa, \v 27 ataamua tena thamani yake kwa miaka tangu alipoiuza, na kurudisha kiasi kilichobaki cha thamani kwa mtu aliyekuwa amemuuzia mali hiyo, naye ataweza kuirudia mali yake. \v 28 Lakini kama hatapata njia ya kumlipa mnunuzi, ile mali aliyouza itabaki kumilikiwa na mnunuzi hadi Mwaka wa Yubile. Mali hiyo itarudishwa Mwaka wa Yubile, naye ataweza kuirudia mali yake. \p \v 29 “ ‘Ikiwa mtu atauza nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta, yeye anayo haki ya kuikomboa mwaka mzima baada ya mauzo ya hiyo nyumba. Wakati huo anaweza kuikomboa. \v 30 Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa Mwaka wa Yubile. \v 31 Lakini nyumba zilizo vijijini bila ya kuwa na kuta zilizozizunguka zitahesabiwa kama mashamba. Zinaweza kukombolewa, nazo zirudishwe Mwaka wa Yubile. \p \v 32 “ ‘Walawi siku zote wana haki ya kukomboa nyumba zao katika miji ya Walawi wanayoimiliki. \v 33 Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wowote wanaoushikilia itarudishwa Mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli. \v 34 Lakini maeneo ya malisho yaliyo mali ya miji yao kamwe yasiuzwe, ni milki yao ya kudumu. \p \v 35 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe kati yako, msaidie vile ungemsaidia mgeni au mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi kati yako. \v 36 Usichukue riba wala faida yoyote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi kati yako. \v 37 Usimkopeshe fedha ili alipe na riba, wala usimuuzie chakula kwa faida. \v 38 Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, niliyekuleta kutoka nchi ya Misri nikupe nchi ya Kanaani, nami niwe Mungu wako. \p \v 39 “ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini kati yako, naye akajiuza kwako, usimfanye atumike kama mtumwa. \v 40 Atatendewa kama mfanyakazi aliyeajiriwa, au kama mkazi wa muda katikati yako; naye atatumika hadi Mwaka wa Yubile. \v 41 Ndipo yeye na watoto wake wataachiwa, naye atarudi kwa watu wa ukoo wake, na kwenye mali ya baba zake. \v 42 Kwa sababu Waisraeli ni watumishi wangu niliowaleta kutoka nchi ya Misri, kamwe wasiuzwe kama watumwa. \v 43 Usiwatawale kwa ukatili, lakini utamcha Mungu wako. \p \v 44 “ ‘Watumwa wako wa kiume na wa kike watatoka katika mataifa yanayokuzunguka; unaweza kununua watumwa kutoka kwao. \v 45 Pia unaweza kununua baadhi ya wakazi wa muda wanaoishi kati yako, na jamaa ya koo zao waliozaliwa katika nchi yako; nao watakuwa mali yako. \v 46 Unaweza kuwafanya hao kuwa urithi wa watoto wako, na unaweza kuwafanya watumwa kwa maisha yao yote. Lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili. \p \v 47 “ ‘Ikiwa mgeni au mkazi wa muda katikati yako atakuwa tajiri, na mmoja wa wazawa wa nchi yako akawa maskini, naye akajiuza kwa yule mgeni anayeishi katikati yako, au kwa mmoja wa jamaa wa koo za wageni, \v 48 anayo haki ya kukombolewa baada ya kujiuza. Mmoja wa jamaa zake aweza kumkomboa: \v 49 Mjomba wake, au binamu yake, au yeyote aliye ndugu wa damu katika ukoo wake aweza kumkomboa. Au akifanikiwa, anaweza kujikomboa mwenyewe. \v 50 Yeye na huyo aliyemnunua watahesabu muda kuanzia mwaka aliojiuza hadi Mwaka wa Yubile. Bei ya kuachiwa kwake itakadiriwa kulingana na ujira unaolipwa mfanyakazi wa kuajiriwa kwa idadi ya hiyo miaka. \v 51 Ikiwa imebaki miaka mingi, ni lazima atalipia ukombozi wake fungu kubwa la bei iliyolipwa kumnunua. \v 52 Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake, naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake. \v 53 Atatendewa kama mtu wa kuajiriwa mwaka hadi mwaka; lazima uone kwamba yule aliyemnunua hamtawali kwa ukatili. \p \v 54 “ ‘Hata ikiwa hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, yeye na watoto wake wataachiwa katika Mwaka wa Yubile, \v 55 kwa kuwa kwangu, Waisraeli ni watumishi. Ni watumishi wangu niliowatoa kutoka nchi ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \c 26 \s1 Thawabu ya utii \r (Kumbukumbu 7:12-24; 28:1-14) \p \v 1 “ ‘Msijitengenezee sanamu, au kusimamisha sanamu ya kuchonga, au jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu ili kulisujudia. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \p \v 2 “ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 3 “ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu, \v 4 nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. \v 5 Kupura nafaka kwenu kutaendelea hadi wakati wa kuvuna zabibu. Na kuvuna zabibu kutaendelea hadi wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu. \p \v 6 “ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu. \v 7 Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu. \v 8 Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu. \p \v 9 “ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika agano langu na ninyi. \v 10 Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya. \v 11 Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia. \v 12 Nitatembea kati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. \v 13 Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja nira yenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu. \s1 Adhabu ya kutokutii \r (Kumbukumbu 28:15-68) \p \v 14 “ ‘Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote, \v 15 nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu zote, na hivyo mkavunja agano langu, \v 16 ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kudhoofisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu watazila. \v 17 Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza. \p \v 18 “ ‘Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. \v 19 Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi, na kuifanya anga iliyo juu yenu iwe kama chuma, na ardhi yenu kama shaba. \v 20 Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake. \p \v 21 “ ‘Kama mtaendelea kuwa na uadui nami, na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili. \v 22 Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ng’ombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu. \p \v 23 “ ‘Ikiwa pamoja na mambo haya hamtakubali maonyo yangu lakini mkaendelea kuweka uadui nami, \v 24 mimi mwenyewe nitaweka uadui nanyi, na kuwatesa kwa ajili ya dhambi zenu mara saba zaidi. \v 25 Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni kati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu. \v 26 Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba. \p \v 27 “ ‘Kama hata baada ya haya bado hamtanisikiliza lakini mkaendelea kuweka uadui nami, \v 28 ndipo katika hasira yangu nitaweka uadui nanyi, nami mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. \v 29 Mtakula nyama ya wana wenu na nyama ya binti zenu. \v 30 Nitaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia, nibomoe madhabahu yenu ya kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi. \v 31 Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu. \v 32 Nitaiharibu nchi, ili adui zenu watakaoishi humo washangae. \v 33 Nitawatawanya ninyi miongoni mwa mataifa, na kuufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itaharibiwa, nayo miji yenu itakuwa magofu. \v 34 Ndipo nchi itafurahia sabato zake muda wote ule itakapokuwa ukiwa, nanyi mkiwa katika nchi ya adui zenu. Ndipo nchi itapumzika na kufurahia sabato zake. \v 35 Wakati wote nchi itakapobaki ukiwa, itapumzika na kufurahia sabato zake ambazo haikuzipata mlipokuwa mnaishi humo. \p \v 36 “ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ijapokuwa hakuna anayewafukuza. \v 37 Watajikwaa mmoja juu ya mwingine kama watu wakimbiao upanga, hata ingawa hakuna anayewafuatia. Hivyo hamtaweza kusimama mbele ya adui zenu. \v 38 Mtaangamia kati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala. \v 39 Wenzenu watakaobaki wataangamia katika nchi za adui zao kwa sababu ya dhambi zao; pia kwa sababu ya dhambi za baba zao wataangamia. \p \v 40 “ ‘Lakini kama watatubu dhambi zao na dhambi za baba zao, udanganyifu wao dhidi yangu na uadui wao kwangu, \v 41 ambao ulinifanya niwe na uadui nao hata nikawapeleka katika nchi ya adui zao, wakati mioyo yao isiyotahiriwa itanyenyekea na kutubu dhambi yao, \v 42 nami nitakumbuka agano langu na Yakobo, na agano langu na Isaka, na agano langu na Ibrahimu, nami nitaikumbuka nchi. \v 43 Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia sabato zake wakati itakuwa ukiwa bila wao. Wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu. \v 44 Lakini pamoja na hili, wakati watakuwa katika nchi ya adui zao, sitawakataa wala kuwachukia kiasi cha kuwaangamiza na kuvunja agano langu nao. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \v 45 Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano langu na baba zao, ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 46 Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo Mwenyezi Mungu alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kupitia kwa Musa. \c 27 \s1 Kukomboa kile kilicho cha Mwenyezi Mungu \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Kama mtu yeyote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana, \v 3 thamani ya kukomboa mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini itakuwa shekeli hamsini\f + \fr 27:3 \fr*\ft Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600.\ft*\f* za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu; \v 4 ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini\f + \fr 27:4 \fr*\ft Shekeli 30 za fedha ni sawa na gramu 360.\ft*\f*. \v 5 Kama ni mtu mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini\f + \fr 27:5 \fr*\ft Shekeli 20 za fedha ni sawa na gramu 240.\ft*\f*, na mwanamke shekeli kumi\f + \fr 27:5 \fr*\ft Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 120.\ft*\f*. \v 6 Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatu\f + \fr 27:6 \fr*\ft Shekeli tatu za fedha ni sawa na gramu 36.\ft*\f* za fedha. \v 7 Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tano\f + \fr 27:7 \fr*\ft Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 180.\ft*\f*, na mwanamke shekeli kumi. \v 8 Kama mtu yeyote anayeweka nadhiri ni maskini mno kuweza kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile yule anayeweka nadhiri anaweza kulipa. \p \v 9 “ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, mnyama huyo aliyetolewa kwa Mwenyezi Mungu anakuwa mtakatifu. \v 10 Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri. Kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, ni watakatifu. \v 11 Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi, yaani yule asiyekubalika kuwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, \v 12 ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo, kama ni mzuri au mbaya. Thamani yoyote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa. \v 13 Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake. \p \v 14 “ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo, kama ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa. \v 15 Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa yake tena. \p \v 16 “ ‘Ikiwa mtu ataweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa Mwenyezi Mungu, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri\f + \fr 27:16 \fr*\ft Homeri moja ni sawa na efa 10, ambazo ni sawa na kilo 100.\ft*\f* moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha. \v 17 Akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa hiyo hiyo. \v 18 Lakini akiliweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka wa Yubile unaofuata, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. \v 19 Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena. \v 20 Kama pengine halikomboi shamba hilo, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa. \v 21 Shamba hilo litakapoachiwa Mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwa Mwenyezi Mungu, nalo litakuwa mali ya makuhani. \p \v 22 “ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu shamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake, \v 23 kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu lazima alipe thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu. \v 24 Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. \v 25 Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu\f + \fr 27:25 \fr*\ft Shekeli moja ya mahali patakatifu ni sawa na gramu 11.\ft*\f*: gera ishirini kwa shekeli. \p \v 26 “ ‘Hata hivyo, hakuna mtu atakayemweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya Mwenyezi Mungu; awe ng’ombe au kondoo, ni wa Mwenyezi Mungu. \v 27 Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa. \p \v 28 “ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu\f + \fr 27:28 \fr*\fq akakiweka wakfu \fq*\ft ina maana ya kumpa Mwenyezi Mungu kabisa, daima, bila kurudiwa.\ft*\f* kwa Mwenyezi Mungu, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Mwenyezi Mungu. \p \v 29 “ ‘Mtu yeyote aliyewekwa wakfu ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe. \p \v 30 “ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, iwe ni nafaka kutoka kwa ardhi, au tunda kutoka kwa miti, ni mali ya Mwenyezi Mungu; ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. \v 31 Kama mtu akikomboa chochote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake. \v 32 Zaka yote ya kundi la ng’ombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa kitu kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu. \v 33 Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Akimbadili, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ” \p \v 34 Haya ndio maagizo Mwenyezi Mungu aliyompa Musa juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.