\id JOS - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Yoshua \toc1 Yoshua \toc2 Yoshua \toc3 Yos \mt1 Yoshua \c 1 \s1 Mwenyezi Mungu amwagiza Yoshua \p \v 1 Baada ya kifo cha Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa: \v 2 “Mtumishi wangu Musa amekufa. Sasa basi, wewe na watu wote hawa jiandaeni kuvuka Mto Yordani kuingia nchi nitakayowapa Waisraeli karibuni. \v 3 Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Musa. \v 4 Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa\f + \fr 1:4 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Mediterania\fqa*\f* iliyo upande wa magharibi. \v 5 Hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia. \p \v 6 “Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utawaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa. \v 7 Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Musa mtumishi wangu; usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote utakapoenda. \v 8 Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi. \v 9 Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda.” \p \v 10 Ndipo Yoshua akawaagiza maafisa wa watu akisema, \v 11 “Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Tayarisheni vyakula vyenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa iwe yenu.’ ” \p \v 12 Lakini kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, Yoshua akasema, \v 13 “Kumbukeni agizo lile Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alilowapa: ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa ninyi utulivu kwa kuwapa nchi hii.’ \v 14 Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ambayo Musa aliwapa mashariki mwa Yordani, lakini wapiganaji wenu wote, wakiwa wamejiandaa kwa vita, lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu, \v 15 hadi Mwenyezi Mungu awape nao utulivu, kama alivyowatendea ninyi, hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kuimiliki nchi yenu wenyewe, ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.” \p \v 16 Ndipo wakamjibu Yoshua, “Chochote ambacho umetuagiza tutafanya na popote utakapotutuma tutaenda. \v 17 Kama vile tulivyomtii Musa kikamilifu, ndivyo tutakavyokutii wewe. Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na awe pamoja nawe tu kama vile alivyokuwa pamoja na Musa. \v 18 Yeyote atakayeasi neno lako na kuacha kuyatii maneno yako, au chochote utakachowaamuru, atauawa. Uwe imara na hodari tu!” \c 2 \s1 Rahabu na wapelelezi \p \v 1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni akawatuma wapelelezi wawili kutoka Shitimu kwa siri, akawaambia, “Nendeni mkaikague hiyo nchi, hasa Yeriko.” Nao wakaenda na kuingia kwenye nyumba ya kahaba mmoja aliyeitwa Rahabu na kukaa humo. \p \v 2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, “Tazama! Baadhi ya Waisraeli wamekuja huku usiku huu kuipeleleza nchi.” \v 3 Hivyo, mfalme wa Yeriko akatuma huu ujumbe kwa Rahabu: “Watoe wale watu waliokujia na kuingia nyumbani mwako, kwa sababu wamekuja kuipeleleza nchi yote.” \p \v 4 Lakini huyo mwanamke alikuwa amewachukua hao watu wawili na kuwaficha. Akasema, “Naam, watu hao walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka. \v 5 Giza lilipoingia, wakati wa kufunga lango la mji, watu hao waliondoka. Sijui walikokwenda. Wafuatilieni haraka. Huenda mkawapata.” \v 6 (Lakini alikuwa amewapandisha darini, na kuwafunika kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini.) \v 7 Basi hao watu wakaondoka kuwafuatilia wale wapelelezi katika njia inayoelekea vivuko vya Yordani. Mara wafuatiliaji walipotoka nje, lango likafungwa. \p \v 8 Kabla wale wapelelezi hawajalala, Rahabu akawaendea huko juu darini, \v 9 akawaambia, “Ninajua kuwa Mwenyezi Mungu amewapa nchi hii na hofu kuu imetuangukia kwa sababu yenu, kiasi kwamba wote wanaoishi katika nchi hii wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yenu. \v 10 Tumesikia jinsi Mwenyezi Mungu alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa. \v 11 Tuliposikia kuhusu hili, mioyo yetu iliyeyuka na kila mmoja alikosa ujasiri kwa sababu yenu, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni Mungu juu mbinguni na chini duniani. \v 12 Sasa basi, tafadhali niapieni kwa Mwenyezi Mungu, kwamba mtaitendea hisani jamaa ya baba yangu, kwa kuwa mimi nimewatendea hisani. Nipeni ishara ya uaminifu \v 13 kwamba mtayahifadhi maisha ya baba yangu na mama yangu, ndugu zangu wa kiume na wa kike, pamoja na wale wote walio wa kwao na kwamba mtatuokoa na kifo.” \p \v 14 Wale watu wakamhakikishia Rahabu, “Uhai wetu kwa uhai wenu! Ikiwa hutatoa habari ya nini tunachofanya, Mwenyezi Mungu atakapotupatia nchi hii, tutawatendea kwa hisani na kwa uaminifu.” \p \v 15 Kisha akawateremsha dirishani kwa kamba, kwa kuwa nyumba yake aliyokuwa anaishi ilikuwa sehemu ya ukuta wa mji. \v 16 Alikuwa amewaambia, “Nendeni vilimani ili wale wafuatiliaji wasiwapate. Jificheni huko kwa siku tatu hadi watakaporudi, hatimaye mwende zenu.” \p \v 17 Wale watu wakamwambia, “Hiki kiapo ulichotuapisha hakitatufunga, \v 18 isipokuwa, tutakapoingia katika nchi hii, utakuwa umefunga hii kamba nyekundu dirishani pale ulipotuteremshia na kama utakuwa umewaleta baba yako na mama yako, ndugu zako na jamaa yako yote ndani ya nyumba yako. \v 19 Ikiwa mtu yeyote atatoka nje ya nyumba yako akaenda mtaani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, hatutawajibika. Lakini yule ambaye atakuwa ndani pamoja nawe, mkono wa mtu yeyote ukiwa juu yake, damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu. \v 20 Lakini ikiwa utatoa habari ya shughuli yetu tunayofanya, tutakuwa tumefunguliwa kutoka kiapo hiki ulichotufanya tuape.” \p \v 21 Naye akajibu, “Nimekubali. Na iwe kama mnavyosema.” Kwa hiyo akaagana nao, nao wakaondoka. Yeye akaifunga ile kamba nyekundu dirishani. \p \v 22 Walipoondoka, wakaelekea vilimani na kukaa huko siku tatu, hadi wale waliokuwa wakiwafuatilia wakawa wamewatafuta njia nzima na kurudi pasipo kuwapata. \v 23 Ndipo wale watu wawili wakaanza kurudi. Wakashuka kutoka kule vilimani, wakavuka mto na kuja kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kumweleza kila kitu kilichowapata. \v 24 Wakamwambia Yoshua, “Hakika Mwenyezi Mungu ametupatia nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.” \c 3 \s1 Kuvuka Yordani \p \v 1 Yoshua na Waisraeli wote wakaondoka asubuhi na mapema kutoka Shitimu, wakaenda hadi Mto Yordani, ambako walipiga kambi kabla ya kuvuka. \v 2 Baada ya siku tatu maafisa wakapita katika kambi yote, \v 3 wakitoa maagizo kwa watu, wakiwaambia: “Mtakapoona Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, likichukuliwa na Walawi ambao ndio makuhani, mtaondoka hapo mlipo na kulifuata. \v 4 Ndipo mtakapotambua njia mtakayoiendea, kwa kuwa hamjawahi kuipita kabla. Lakini msisogee karibu, bali kuwe na umbali wa dhiraa elfu mbili\f + \fr 3:4 \fr*\ft Dhiraa 2,000 ni sawa na mita 900.\ft*\f* kati yenu na Sanduku.” \p \v 5 Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “Jitakaseni, kwa kuwa kesho Mwenyezi Mungu atatenda mambo ya kushangaza kati yenu.” \p \v 6 Yoshua akawaambia makuhani, “Liinueni Sanduku la Agano mkatangulie mbele ya watu.” Hivyo wakaliinua na kutangulia mbele yao. \p \v 7 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Leo nitaanza kukutukuza machoni pa Israeli yote, ili wapate kujua kuwa niko pamoja nawe kama nilivyokuwa pamoja na Musa. \v 8 Uwaambie makuhani wanaochukua Sanduku la Agano, ‘Mnapofika kwenye ukingo wa maji ya Yordani, nendeni mkasimame ndani ya mto.’ ” \p \v 9 Yoshua akawaambia Waisraeli, “Njooni hapa msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \v 10 Hivi ndivyo mtakavyojua kuwa Mungu aliye hai yupo kati yenu, na kwamba kwa hakika atawaondoa mbele yenu hao Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagirgashi, Waamori na Wayebusi. \v 11 Tazameni, Sanduku la Agano la Bwana wa dunia yote litaingia ndani ya Mto Yordani likiwa limewatangulia. \v 12 Sasa basi, chagueni watu kumi na wawili kutoka makabila ya Israeli, mtu mmoja kutoka kila kabila. \v 13 Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la Mwenyezi Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yanayotiririka kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.” \p \v 14 Basi, watu walipovunja kambi ili kuvuka Yordani, makuhani wakiwa wamebeba Sanduku la Agano waliwatangulia. \v 15 Wakati huu ulikuwa wakati wa mavuno, nao Mto Yordani ulikuwa umefurika hadi kwenye kingo zake. Ilikuwa kawaida ya Yordani kufurika nyakati zote za mavuno. Mara tu makuhani wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Agano walipofika mtoni na nyayo zao kuzama ndani ya yale maji, \v 16 maji hayo yaliyotiririka kutoka upande wa juu yaliacha kutiririka yakasimama kama chuguu mbali kabisa nao, kwenye mji ulioitwa Adamu kwenye eneo la Sarethani, wakati yale maji yaliyokuwa yanatiririka kuingia kwenye Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), yalitindika kabisa. Hivyo watu wakavuka kukabili Yeriko. \p \v 17 Wale makuhani waliobeba Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Mto Yordani, wakati Waisraeli wote wakiwa wanapita hadi taifa lote likaisha kuvuka mahali pakavu. \c 4 \s1 Ukumbusho wa kuvuka Yordani \p \v 1 Taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani, Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, \v 2 “Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja, \v 3 uwaambie wachukue mawe kumi na mbili katikati ya Mto Yordani, pale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu.” \p \v 4 Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua miongoni mwa Waisraeli, mtu mmoja kutoka kila kabila, \v 5 naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kulingana na idadi ya makabila ya Israeli, \v 6 kuwa ishara miongoni mwenu. Siku zijazo, watoto wenu watakapowauliza, ‘Ni nini maana ya mawe haya?’ \v 7 waambieni kwamba maji ya Mto Yordani yaliyokuwa yakitiririka, yalitindika mbele ya Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. Sanduku lilipovuka Yordani, maji ya Yordani yalitindika. Mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.” \p \v 8 Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na idadi ya makabila ya Israeli, kama Mwenyezi Mungu alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini. \v 9 Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mbili yaliyokuwa katikati ya Mto Yordani, mahali miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko hadi leo. \p \v 10 Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani hadi kila kitu Mwenyezi Mungu alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimekamilishwa na watu, sawasawa na vile Musa alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka, \v 11 na mara tu watu wote walipokwisha kuvuka, Sanduku la Mwenyezi Mungu na makuhani wakavuka watu wakiwa wanatazama. \v 12 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakavuka mbele ya Waisraeli, wakiwa wamejiandaa kwa vita, kama Musa alivyowaamuru. \v 13 Idadi ya wanaume elfu arobaini waliojiandaa kwa vita walivuka mbele za Mwenyezi Mungu hadi nchi tambarare za Yeriko kwa ajili ya vita. \p \v 14 Siku ile Mwenyezi Mungu akamtukuza Yoshua mbele ya Israeli yote, nao wakamheshimu siku zote za maisha yake, kama vile walivyomheshimu Musa. \p \v 15 Basi Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, \v 16 “Waamuru hao makuhani wanaolibeba Sanduku la Ushuhuda wapande kutoka ndani ya Mto Yordani.” \p \v 17 Kwa hiyo Yoshua akawaamuru hao makuhani akisema, “Pandeni kutoka ndani ya Mto Yordani.” \p \v 18 Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. Mara tu walipoiweka miguu yao ukingoni mwa mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla. \p \v 19 Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza watu walipanda kutoka Yordani na kupiga kambi huko Gilgali, kwenye mpaka wa mashariki wa Yeriko. \v 20 Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mbili waliyokuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. \v 21 Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’ \v 22 Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’ \v 23 Kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka. \v 24 Alifanya hivi ili mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa Mwenyezi Mungu ni wenye nguvu, na ili kila wakati mpate kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.” \c 5 \p \v 1 Basi wafalme wote wa Waamori magharibi mwa Yordani na wafalme wote wa Kanaani waliokuwa kwenye pwani waliposikia jinsi Mwenyezi Mungu alivyoukausha Mto Yordani mbele ya Waisraeli hata tulipokwisha kuvuka, mioyo yao ikayeyuka kwa hofu, wala hawakuwa na ujasiri tena wa kukabiliana na Waisraeli. \s1 Tohara huko Gilgali \p \v 2 Wakati huo Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Tengeneza visu vya gumegume na uwatahiri Waisraeli tena.” \v 3 Kwa hiyo Yoshua akatengeneza visu vya gumegume na kutahiri Waisraeli huko Gibeath-Haaralothi\f + \fr 5:3 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kilima cha magovi\fqa*\f*. \p \v 4 Hii ndiyo sababu ya Yoshua kufanya hivyo: Wanaume wote waliotoka Misri, wote wenye umri wa kwenda vitani, walikufa jangwani wakiwa njiani baada ya kuondoka Misri. \v 5 Watu wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, lakini watu wote waliozaliwa jangwani wakiwa safarini kutoka Misri hawakuwa wametahiriwa. \v 6 Waisraeli walitembea jangwani miaka arobaini hadi wanaume wote wale waliokuwa na umri wa kwenda vitani wakati waliondoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakumtii Mwenyezi Mungu. Kwa maana Mwenyezi Mungu alikuwa amewaapia kuwa wasingeweza kuona nchi ambayo alikuwa amewaahidi baba zao katika kuapa kutupatia, nchi inayotiririka maziwa na asali. \v 7 Kwa hiyo akawainua wana wao baada yao na hawa ndio hao ambao Yoshua aliwatahiri. Walikuwa hawajatahiriwa bado kwa sababu walikuwa safarini. \v 8 Baada ya taifa lote kutahiriwa, waliendelea kukaa kambini hadi walipopona. \p \v 9 Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Leo nimeiondoa aibu ya Wamisri kutoka kwenu.” Basi mahali pale pakaitwa Gilgali hadi leo. \p \v 10 Jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi, wakiwa wamepiga kambi huko Gilgali kwenye nchi tambarare za Yeriko, Waisraeli wakaadhimisha Pasaka. \v 11 Siku iliyofuata Pasaka, katika siku ile ile, wakala mazao ya nchi: mikate isiyotiwa chachu na nafaka za kukaanga. \v 12 Mana ilikoma siku iliyofuata baada ya Waisraeli kula chakula kilichotoka katika nchi; hapakuwa na mana tena kwa ajili ya Waisraeli, ila mwaka huo walikula mazao ya nchi ya Kanaani. \s1 Jemadari wa jeshi la Mwenyezi Mungu \p \v 13 Basi Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi. Yoshua akamwendea na kumuuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?” \p \v 14 Akajibu, “La, siko upande wowote, lakini mimi nimekuja nikiwa jemadari wa jeshi la Mwenyezi Mungu.” Yoshua akasujudu, uso wake ukigusa chini, akamuuliza, “Je, Bwana, una ujumbe gani kwa mtumishi wako?” \v 15 Jemadari wa jeshi la Mwenyezi Mungu akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali uliposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo. \c 6 \s1 Yeriko yaangamizwa \p \v 1 Basi malango ya Yeriko yalifungwa kwa uthabiti kwa sababu ya Waisraeli. Hakuna mtu yeyote aliyetoka au kuingia. \p \v 2 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na wapiganaji wake. \v 3 Zunguka mji mara moja pamoja na watu wote wenye silaha. Fanya hivi kwa siku sita. \v 4 Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo dume mbele ya Sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. \v 5 Utakapowasikia wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na wapiganaji watapanda, kila mtu akielekea mbele yake.” \p \v 6 Ndipo Yoshua mwana wa Nuni akaita makuhani na kuwaambia, “Chukueni Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu na makuhani saba wachukue baragumu za pembe za kondoo dume mbele yake.” \v 7 Naye akawaagiza watu, “Songeni mbele! Mkauzunguke mji, na walinzi wenye silaha watangulie mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu.” \p \v 8 Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba waliozibeba zile baragumu saba mbele za Mwenyezi Mungu, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu likawafuata. \v 9 Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa. \v 10 Bali Yoshua alikuwa amewaagiza watu, “Msipige ukelele wa vita; msipaze sauti zenu, wala kusema neno lolote hadi siku ile nitakayowaambia mpige kelele. Ndipo mtapiga kelele!” \v 11 Basi akalipeleka Sanduku la Mwenyezi Mungu kuzungushwa huo mji, likizungushwa mara moja. Kisha watu wakarudi kambini kulala. \p \v 12 Yoshua akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, nao makuhani wakalichukua Sanduku la Mwenyezi Mungu. \v 13 Wale Makuhani saba waliobeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la Mwenyezi Mungu, huku baragumu hizo zikiendelea kulia. \v 14 Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja na kurudi kambini. Wakafanya hivi kwa siku sita. \p \v 15 Siku ya saba, wakaamka asubuhi na mapema wakauzunguka mji kama walivyokuwa wakifanya, isipokuwa siku ile waliuzunguka mji mara saba. \v 16 Walipouzunguka mara ya saba, makuhani walipiga baragumu kwa sauti kubwa, naye Yoshua akawaamuru watu akisema, “Pigeni kelele! Kwa maana Mwenyezi Mungu amewapa mji huu! \v 17 Mji huu pamoja na vyote vilivyomo utatengewa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuangamizwa. Rahabu yule kahaba atasalimishwa, pamoja na wote walio naye nyumbani mwake, kwa sababu aliwaficha wale wapelelezi tuliowatuma. \v 18 Lakini mjiepushe na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, msije mkajiletea maangamizi kwa kuchukua chochote katika hivyo; la sivyo, mtailetea kambi ya Israeli maangamizi na taabu. \v 19 Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, lazima viletwe katika hazina yake.” \p \v 20 Baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele; kwa ile sauti ya baragumu na watu kupaza sauti, ukuta ukaanguka; hivyo kila mtu akapanda akiendelea mbele na kuuteka mji. \v 21 Wakauweka mji wakfu kwa Mwenyezi Mungu, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga: wanaume na wanawake, vijana kwa wazee, ng’ombe, kondoo na punda. \p \v 22 Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani mwa yule kahaba; mleteni pamoja na wote walio nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.” \v 23 Basi wale vijana waliofanya upelelezi wakaenda kumleta Rahabu, baba yake na mama yake, na ndugu zake na watu wote waliokuwa pamoja naye. Wakaleta jamaa yake yote na kuwaweka mahali nje ya kambi ya Israeli. \p \v 24 Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwa ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, na vyombo vya shaba na vya chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 25 Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu yule kahaba, jamaa yake yote na vyote alivyokuwa navyo, kwa sababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko, naye anaishi miongoni mwa Waisraeli hata leo. \p \v 26 Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Na alaaniwe mbele za Mwenyezi Mungu mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: \q1 “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume \q2 ataiweka misingi yake; \q1 kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho \q2 atayaweka malango yake.” \p \v 27 Hivyo Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na Yoshua, na sifa zake zikaenea katika nchi yote. \c 7 \s1 Dhambi ya Akani \p \v 1 Lakini Waisraeli hawakuwa waaminifu kuhusu vile vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa; Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alivichukua baadhi ya hivyo vitu. Hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Israeli. \p \v 2 Basi Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko waende Ai, karibu na Beth-Aveni mashariki mwa Betheli, akawaambia, “Pandeni mkaipeleleze nchi.” Basi wale watu wakapanda wakaipeleleza Ai. \p \v 3 Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Usiwachoshe watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.” \v 4 Basi wakapanda kama wanaume elfu tatu tu, lakini wakashambuliwa na wanaume wa Ai, \v 5 ambao waliwaua wanaume kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu\f + \fr 7:5 \fr*\ft au \ft*\fqa machimbo ya mawe\fqa*\f*, nao wakawauwa huko kwenye miteremko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka kwa hofu, ikawa kama maji. \p \v 6 Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu, na akabakia hapo hadi jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao. \v 7 Yoshua akasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, kwa nini umewavusha watu hawa ng’ambo ya Yordani ili kututia mikononi mwa Waamori watuangamize? Laiti tungeridhika kukaa ng’ambo ile nyingine ya Yordani! \v 8 Ee Bwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake? \v 9 Wakanaani na watu wengine wa nchi watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kufutilia jina letu duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenyewe lililo kuu?” \p \v 10 Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Simama! Unafanya nini ukilala kifudifudi? \v 11 Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa; wameiba, wamesema uongo, na wameviweka pamoja na mali yao. \v 12 Ndiyo sababu Waisraeli hawawezi kusimama dhidi ya adui zao. Wanawapa visogo na kukimbia kwa kuwa wanastahili maangamizi. Sitakuwa pamoja nanyi tena hadi mwangamize kila kitu miongoni mwenu kilichotengwa kwa maangamizi. \p \v 13 “Nenda, ukawatakase watu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa ajili ya kesho; kwa sababu hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa vimo kati yenu, ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu hadi mtakapoviondoa. \p \v 14 “ ‘Asubuhi, mtakuja kabila kwa kabila. Kisha kabila atakalolichagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele kufuatana na koo zao; nao ukoo atakaouchagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa atakayoichagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele mtu kwa mtu. \v 15 Yule atakayekutwa na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, atateketezwa kwa moto pamoja na vitu vyote alivyo navyo. Kwa kuwa amelivunja agano la Mwenyezi Mungu na kufanya kitu cha aibu katika Israeli!’ ” \p \v 16 Kesho yake asubuhi na mapema Yoshua akaamuru Israeli kuja mbele kabila kwa kabila; na kabila la Yuda likachaguliwa. \v 17 Koo za Yuda zikaja mbele, naye akawachagua Wazera. Akaamuru ukoo wa Wazera kuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ya Zabdi ikachaguliwa. \v 18 Yoshua akaamuru jamaa ya Zabdi kuja mbele mtu kwa mtu, naye Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, akachaguliwa. \p \v 19 Ndipo Yoshua akamwambia Akani, “Mwanangu, mtukuze Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, nawe ukiri kwake. Niambie ni nini ulichotenda; usinifiche.” \p \v 20 Akani akamjibu Yoshua, “Ni kweli! Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Hili ndilo nililofanya: \v 21 Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili\f + \fr 7:21 \fr*\ft Shekeli 200 ni sawa na kilo 2.3.\ft*\f* za fedha, na kabari ya dhahabu ya uzito wa shekeli hamsini\f + \fr 7:21 \fr*\ft Shekeli 50 ni sawa na gramu 600.\ft*\f*, nikavitamani na nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.” \p \v 22 Kwa hiyo Yoshua akatuma wajumbe, nao wakakimbia hadi kwenye hema. Tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa kwenye hema lake, pamoja na ile fedha chini yake. \v 23 Wakavichukua vile vitu toka kwenye hema, wakamletea Yoshua pamoja na Waisraeli wote, wakavitandaza mbele za Mwenyezi Mungu. \p \v 24 Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, lile joho, ile kabari ya dhahabu, wanawe wa kiume na wa kike, ng’ombe, punda na kondoo wake, hema lake pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori. \v 25 Yoshua akasema, “Kwa nini umetuletea taabu hii? Mwenyezi Mungu atakuletea taabu leo.” \p Ndipo Israeli yote ikampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto. \v 26 Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo hadi leo. Naye Mwenyezi Mungu akageuka kutoka hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori\f + \fr 7:26 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Bonde la Taabu\fqa*\f* tangu siku hiyo. \c 8 \s1 Mji wa Ai waangamizwa \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usivunjike moyo. Chukua jeshi lote la vita uende pamoja nalo kuishambulia Ai. Kwa kuwa nimeshamweka mikononi mwako mfalme wa Ai, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake. \v 2 Utautendea mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyotendea Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mnaweza kunyakua mali zao na mifugo yao kuwa nyara zenu. Weka waviziaji upande wa nyuma ya mji.” \p \v 3 Basi Yoshua na jeshi lote wakainuka kushambulia Ai. Akachagua mashujaa elfu thelathini walio bora miongoni mwa wapiganaji wake, akawapeleka wakati wa usiku, \v 4 akiwaagiza: “Sikilizeni kwa makini. Mtavizia nyuma ya mji. Msiende mbali sana na mji. Wote kuweni macho. \v 5 Mimi na watu walio pamoja nami tutaukabili mji, kisha itakuwa hapo watu watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo awali, sisi tutawakimbia. \v 6 Watatufuatilia hadi tutakapokuwa tumewavuta mbali na mji kwa kuwa watasema, ‘Wanatukimbia, kama walivyofanya hapo awali.’ Hivyo tutakapowakimbia, \v 7 ninyi mtainuka mtoke mafichoni na kuuteka mji. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atautia mkononi mwenu. \v 8 Mtakapokuwa mmeuteka mji, uteketezeni kwa moto. Fanyeni kama vile Mwenyezi Mungu alivyoamuru. Tazameni, nimewaagiza.” \p \v 9 Ndipo Yoshua akawatuma watu, nao wakaenda mahali pa kujificha, wakawa wanavizia kati ya Betheli na Ai, kuelekea upande wa magharibi wa Ai, lakini Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku huo. \p \v 10 Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Yoshua akakusanya jeshi lake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawaongoza kwenda Ai. \v 11 Wanajeshi wote waliokuwa pamoja na Yoshua walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini mwa Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji. \v 12 Yoshua alikuwa amewachukua watu wapatao elfu tano, akawaweka mafichoni kusubiri kushambulia, kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa mji. \v 13 Wakawaweka askari katika maeneo yao: wale wote waliokuwa kambini wakawa kaskazini ya mji na wale waliokuwa wakivizia wakawa upande wa magharibi. Usiku huo Yoshua akaenda katika lile bonde. \p \v 14 Mfalme wa Ai alipoona jambo hili, yeye pamoja na wanaume wote wa mji wakatoka kwa haraka asubuhi na mapema kukutana na Israeli katika vita mahali palipotazamana na Araba. Lakini hakujua kwamba kulikuwa kumewekwa waviziaji dhidi yake nyuma ya mji. \v 15 Yoshua na Waisraeli wote wakaruhusu kurudishwa nyuma mbele yao, na kuelekea jangwani. \v 16 Watu wote wa Ai wakaitwa ili kuwafuatia, nao wakavutwa kumfuatia Yoshua mbali na mji. \v 17 Hakuna hata mwanaume mmoja aliyebakia Ai wala Betheli ambaye hakufuatia Israeli. Wakauacha mji wazi na kuwafuatia Waisraeli. \p \v 18 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Inua huo mkuki ulio mkononi mwako kuuelekeza Ai, kwa kuwa nitautia huo mji mkononi mwako.” Hivyo Yoshua akauelekeza mkuki wake Ai. \v 19 Mara tu alipofanya hivi, wale watu waliokuwa mafichoni wakaondoka upesi kutoka mahali pao na kukimbia mbele. Wakaingia ndani ya mji, wakauteka na kuutia moto kwa haraka. \p \v 20 Wanaume wa Ai wakaangalia nyuma, wakauona moshi wa huo mji ukielekea angani, lakini hawakuwa na nafasi ya kutoroka kwa upande wowote, kwa kuwa wale Waisraeli waliokuwa wakiwakimbia kuelekea jangwani walikuwa wamegeuka nyuma kuwakabili wakimbizaji wao. \v 21 Basi Yoshua na Waisraeli wote walipoona kwamba waviziaji wameshauteka mji na moshi ulikuwa unapaa juu kwenye mji, wakawageukia wanaume wa Ai na kuwashambulia. \v 22 Wale waviziaji nao pia wakatoka nje ya mji dhidi yao, hivi kwamba wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia yeyote aliyenusurika wala aliyetoroka. \v 23 Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua. \p \v 24 Israeli ilipomaliza kuwaua wanaume wote wa Ai katika mashamba na jangwani walipokuwa wamewafukuzia, na baada ya kila mmoja wao kuuawa kwa upanga, Waisraeli wote wakarudi Ai na kuwaua wale waliokuwa wamebakia mjini. \v 25 Wanaume na wanawake elfu kumi na mbili waliangamia siku ile, yaani watu wote wa Ai. \v 26 Kwa maana Yoshua hakuurudisha ule mkono wake uliokuwa umeuinua mkuki hadi alipomaliza kuwaangamiza wote walioishi Ai. \v 27 Lakini Israeli wakajichukulia mifugo na nyara za mji huu, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwamuru Yoshua. \p \v 28 Kwa hiyo Yoshua akauchoma moto mji wa Ai na kuufanya kuwa lundo la magofu la kudumu, mahali pa ukiwa hadi leo. \v 29 Akamwangika mfalme wa Ai kwenye mti na kumwacha hapo hadi jioni. Wakati wa jua kutua, Yoshua akawaamuru wautoe mwili wake kwenye mti na kuutupa kwenye ingilio la lango la mji. Kisha wakalundika mawe mengi makubwa juu yake, ambayo yamesalia hadi leo. \s1 Agano lafanywa upya katika Mlima Ebali \p \v 30 Kisha Yoshua akajenga madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, katika Mlima Ebali, \v 31 kama Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea Mwenyezi Mungu sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani\f + \fr 8:31 \fr*\ft yaani \ft*\fqa sadaka za ushirika\fqa*\f*. \v 32 Pale mbele ya Waisraeli, Yoshua akanakili juu ya hayo mawe Torati ya Musa, aliyokuwa ameiandika. \v 33 Waisraeli wote, wakiwa na wazee wao, maafisa na waamuzi, walikuwa wamesimama pande zote mbili za Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, wakiwaelekea makuhani Walawi waliokuwa wamelibeba. Wageni walioishi miongoni mwao, pamoja na wazawa, walikuwa hapo. Nusu ya watu walisimama mbele ya Mlima Gerizimu, na nusu nyingine wakasimama mbele ya Mlima Ebali, kama vile Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameamuru hapo mwanzo alipotoa maagizo ya kuwabariki watu wa Israeli. \p \v 34 Hatimaye, Yoshua akasoma maneno yote ya sheria, yaani baraka na laana, kama vile ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati. \v 35 Hakuna neno lolote katika yale yote ambayo Musa alikuwa ameamuru ambalo Yoshua hakuwasomea kusanyiko lote la Waisraeli, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, na wageni walioishi miongoni mwao. \c 9 \s1 Udanganyifu wa Wagibeoni \p \v 1 Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia haya yote, na wale waliokuwa katika nchi ya vilima, na katika Shefela\f + \fr 9:1 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*, na katika pwani yote ya Bahari Kuu\f + \fr 9:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Mediterania\fqa*\f* hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi), \v 2 waliungana ili kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli. \p \v 3 Hata hivyo, watu wa Gibeoni waliposikia kuhusu yote Yoshua aliyowatendea watu wa Yeriko na Ai, \v 4 waliamua kufanya hila: Wakajifanya kama wajumbe wakiwa na punda waliobebeshwa mizigo ya magunia yaliyochakaa, na viriba vikuukuu vya mvinyo, vyenye nyufa zilizozibwa. \v 5 Walivaa miguuni mwao viatu vilivyoraruka na kushonwa, kisha wakavaa nguo kuukuu. Chakula chao kilikuwa mkate uliokauka na kuingia koga. \v 6 Ndipo wakamwendea Yoshua kambini huko Gilgali, wakamwambia yeye pamoja na Waisraeli, “Tumetoka katika nchi ya mbali; fanyeni mkataba nasi.” \p \v 7 Basi Waisraeli wakawaambia hao Wahivi, “Lakini huenda mnakaa karibu nasi. Twawezaje basi kufanya mkataba nanyi?” \p \v 8 Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.” \p Yoshua akawauliza, “Ninyi ni nani, na mnatoka wapi?” \p \v 9 Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri, \v 10 pia yale yote aliyowatendea wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani; huyo Sihoni mfalme wa Heshboni na Ogu mfalme wa Bashani, aliyetawala huko Ashtarothi. \v 11 Basi wazee wetu na wale wote wanaoishi katika nchi yetu walituambia, ‘Chukueni chakula cha safari; nendeni mkakutane na watu hao na kuwaambia, “Sisi tu watumishi wenu, fanyeni mapatano nasi.” ’ \v 12 Mkate huu wetu ulikuwa wa moto tulipoufunga siku tulipoanza safari kuja kwenu, lakini sasa angalia jinsi ulivyokauka na kuota ukungu. \v 13 Viriba hivi vya mvinyo vilikuwa vipya tulipovijaza, lakini ona jinsi vilivyo na nyufa. Nguo zetu na viatu vimechakaa kwa ajili ya safari ndefu.” \p \v 14 Basi Waisraeli wakavikagua vyakula vyao bila kupata shauri kutoka kwa Mwenyezi Mungu. \v 15 Ndipo Yoshua akafanya nao mkataba wa amani ili kuwaacha waishi, na viongozi wa kusanyiko wakauthibitisha kwa kiapo. \p \v 16 Siku ya tatu baada ya kufanya mkataba na Wagibeoni, Waisraeli wakapata habari kuwa watu hao ni majirani zao, walioishi karibu nao. \v 17 Ndipo Waisraeli wakasafiri, na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao: yaani Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu. \v 18 Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \p Kusanyiko lote wakanung’unika dhidi ya hao viongozi, \v 19 lakini viongozi wote wakawajibu, “Tumeshawaapia kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa hiyo hatuwezi kuwagusa sasa. \v 20 Hivi ndivyo tutakavyowafanyia: Tutawaacha waishi, ili ghadhabu isije juu yetu kwa kuvunja kiapo tulichowaapia.” \v 21 Wakaendelea kusema, “Waacheni waishi, lakini wawe wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii yote.” Hivyo ahadi waliyoweka viongozi kwao ikawa hivyo. \p \v 22 Kisha Yoshua akawaita Wagibeoni na kuwaambia, “Kwa nini mmetudanganya kwa kutuambia, ‘Tunaishi mbali nanyi,’ ilhali mnaishi karibu nasi? \v 23 Sasa mko chini ya laana: Daima mtakuwa wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.” \p \v 24 Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwaangamiza wakazi wake wote toka mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili. \v 25 Sasa tupo mikononi mwako. Tufanyieni lolote mnaloona kuwa jema na haki kwenu.” \p \v 26 Kwa hiyo Yoshua akawaokoa mikononi mwa Waisraeli, nao hawakuwaua. \v 27 Siku hiyo Yoshua akawafanya Wagibeoni wapasua kuni na wachota maji kwa ajili ya jamii na kwa ajili ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu mahali pale Mwenyezi Mungu angepachagua. Hivyo ndivyo walivyo hadi hivi leo. \c 10 \s1 Jua lasimama \p \v 1 Baada ya haya Adoni-Sedeki mfalme wa Yerusalemu alisikia kuwa Yoshua alikuwa ameteka mji wa Ai na kuuangamiza kabisa, tena alikuwa ameua mfalme wake, kama alivyofanya huko Yeriko na mfalme wake, tena ya kuwa watu wa Gibeoni walikuwa wamefanya mapatano ya amani na Waisraeli, na walikuwa wakiishi karibu yao. \v 2 Yeye na watu wake wakataharuki mno kwa kuwa Gibeoni ulikuwa mji mkubwa kama mmoja wa miji ya kifalme; ulikuwa mkubwa kuliko Ai, na watu wake wote walikuwa mashujaa wa vita. \v 3 Hivyo Adoni-Sedeki mfalme wa Yerusalemu akaomba msaada kwa Hohamu mfalme wa Hebroni, Piramu mfalme wa Yarmuthi, Yafia mfalme wa Lakishi, na Debiri mfalme wa Egloni. \v 4 Akawaambia, “Njooni mnisaidie kuipiga Gibeoni, kwa sababu imefanya mkataba wa amani na Yoshua na Waisraeli.” \p \v 5 Ndipo hao wafalme watano wa Waamori, ambao ni wafalme wa Yerusalemu, Hebroni, Yarmuthi, Lakishi na Egloni, wakaunganisha majeshi yao. Wakapanda na vikosi vyao vyote, nao wakajipanga dhidi ya Gibeoni na kuishambulia. \p \v 6 Nao Wagibeoni wakatuma ujumbe kwa Yoshua kwenye kambi ya Gilgali na kumwambia, “Usiwatelekeze watumishi wako. Panda haraka uje kwetu utuokoe! Tusaidie, kwa sababu wafalme wote wa Waamori wanaokaa nchi ya vilima wameunganisha majeshi yao pamoja dhidi yetu.” \p \v 7 Basi Yoshua akaondoka Gilgali pamoja na jeshi lake lote, wakiwepo mashujaa wote. \v 8 Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Usiwaogope watu hao, nimewatia mkononi mwako. Hakuna yeyote atakayeweza kushindana nawe.” \p \v 9 Baada ya Yoshua kutembea usiku kucha kutoka Gilgali, akawashambulia ghafula. \v 10 Mwenyezi Mungu akawafadhaisha mbele ya Waisraeli, naye Yoshua na Waisraeli wakawashinda kwa ushindi mkuu huko Gibeoni. Waisraeli wakawafukuza kwa njia inayopanda kwenda Beth-Horoni, huku wakiwaua hadi kufikia Azeka na Makeda. \v 11 Walipokuwa wanawakimbia Waisraeli kwenye barabara inayoteremka kutoka Beth-Horoni hadi Azeka, Mwenyezi Mungu akawavurumishia mawe makubwa kama mvua kutoka mbinguni, na wengi wao walikufa kwa mawe kuliko wale waliokufa kwa panga za Waisraeli. \p \v 12 Siku ile Mwenyezi Mungu alipowakabidhi Waamori kwa Waisraeli, Yoshua akanena na Mwenyezi Mungu akiwa mbele ya Waisraeli, akasema: \q1 “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, \q2 wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.” \q1 \v 13 Hivyo jua likasimama, \q2 nao mwezi ukatulia, \q1 hadi taifa hilo lilipokwisha \q2 kujilipizia kisasi kwa adui zake, \m kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari. \p Jua likasimama katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku nzima. \v 14 Hakujakuwa na siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo Mwenyezi Mungu alimsikiliza mwanadamu. Hakika Mwenyezi Mungu alikuwa akiwapigania Israeli. \p \v 15 Ndipo Yoshua akarudi kambini huko Gilgali pamoja na Israeli yote. \s1 Wafalme watano wa Waamori wauawa \p \v 16 Basi wale wafalme watano wakawa wamekimbia kujificha kwenye pango huko Makeda. \v 17 Yoshua alipoambiwa kuwa wafalme hao watano wamekutwa wakiwa wamejificha ndani ya pango huko Makeda, \v 18 akasema, “Vingirisheni mawe makubwa kwenye mlango wa pango, tena mweke walinzi wa kulilinda. \v 19 Lakini msiwaache! Wafuatieni adui zenu, washambulieni kutoka nyuma, wala msiwaache wafike kwenye miji yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewatia mkononi mwenu.” \p \v 20 Hivyo Yoshua pamoja na Waisraeli wakawaangamiza, isipokuwa wachache waliosalia walifika kwenye miji yao yenye ngome. \v 21 Basi jeshi lote likarudi salama kwa Yoshua kule kambini Makeda, na hakuna yeyote aliyetoa neno kinyume cha Waisraeli. \p \v 22 Ndipo Yoshua akasema, “Haya fungueni mdomo wa pango, mniletee hao wafalme watano.” \v 23 Kwa hiyo wakawatoa hao wafalme watano nje ya pango: wafalme wa Yerusalemu, Hebroni, Yarmuthi, Lakishi na Egloni. \v 24 Walipokuwa wamewaleta hawa wafalme kwa Yoshua, akawaita wanaume wote wa Israeli, na kuwaambia majemadari wa vita walioenda pamoja naye, “Njooni hapa mweke nyayo zenu juu ya shingo za hawa wafalme.” Basi wakaja wakaweka nyayo zao shingoni. \p \v 25 Yoshua akawaambia, “Msiogope, wala msivunjike moyo. Kuweni hodari na wenye ushujaa. Hili ndilo Mwenyezi Mungu atakalowatendea adui zenu wote mnaoenda kupigana nao.” \v 26 Ndipo Yoshua akawapiga na kuwaua wale wafalme na kuwatundika juu ya miti mitano, nao wakaachwa wakining’inia juu ya ile miti hadi jioni. \p \v 27 Wakati wa kuzama jua Yoshua akaamuru, nao wakawashusha kutoka ile miti na kuwatupa kwenye lile pango ambalo walikuwa wamejificha. Wakaweka mawe makubwa kwenye mlango wa pango, ambayo yapo hadi leo. \p \v 28 Siku ile Yoshua akateka Makeda. Akamuua kila mmoja katika ule mji, pamoja na mfalme wake kwa upanga. Hakubakiza mtu yeyote. Akamfanyia mfalme wa Makeda kama vile alivyokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko. \s1 Israeli yaangamiza miji ya kusini \p \v 29 Ndipo Yoshua akaondoka Makeda akiwa pamoja na Israeli yote hadi mji wa Libna na kuushambulia. \v 30 Mwenyezi Mungu pia akautia huo mji wa Libna pamoja na mfalme wake mikononi mwa Israeli. Yoshua akaangamiza ule mji na kila mtu aliyekuwa ndani yake kwa upanga. Hakubakiza huko mtu yeyote. Akamfanyia mfalme wa Libna kama alivyokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko. \p \v 31 Kisha Yoshua akaondoka Libna kwenda Lakishi akiwa pamoja na Israeli yote; wakajipanga dhidi yake na kuushambulia. \v 32 Mwenyezi Mungu akautia Lakishi mikononi mwa Israeli, hivyo Yoshua akauteka siku ya pili. Yoshua akauangamiza mji na kila kilichokuwa ndani yake kwa upanga, kama tu vile alivyokuwa ameufanyia mji wa Libna. \v 33 Wakati huo huo, Horamu mfalme wa Gezeri alikuwa amepanda ili kusaidia Lakishi, lakini Yoshua akamshinda pamoja na jeshi lake, hadi hapakubakia mtu yeyote. \p \v 34 Ndipo Yoshua akaondoka Lakishi kwenda Egloni akiwa pamoja na Israeli yote; wakajipanga dhidi yake na kuushambulia. \v 35 Wakauteka mji huo siku ile ile, wakaupiga kwa upanga na kumwangamiza kila mmoja aliyekuwa ndani yake, kama vile walivyokuwa wameufanyia Lakishi. \p \v 36 Kisha Yoshua na Waisraeli wote wakapanda kutoka Egloni hadi Hebroni, na kuushambulia. \v 37 Wakauteka mji na kuupiga kwa upanga, pamoja na mfalme wake, vijiji vyake na kila mmoja aliyekuwa ndani yake. Hawakubakiza mtu yeyote. Kama vile huko Egloni, waliuangamiza kabisa pamoja na kila mmoja aliyekuwa ndani yake. \p \v 38 Ndipo Yoshua na Waisraeli wote wakageuka na kushambulia Debiri. \v 39 Wakauteka mji, mfalme wake na vijiji vyake, na kuupiga kwa upanga. Kila mmoja aliyekuwa ndani yake wakamwangamiza kabisa. Hawakubakiza mtu yeyote. Wakaufanyia Debiri na mfalme wake kama vile walivyokuwa wameifanyia miji ya Libna na Hebroni na wafalme wao. \p \v 40 Hivyo Yoshua akalishinda eneo hilo lote, ikiwa ni pamoja na nchi ya vilima, na Negebu, na Shefela\f + \fr 10:40 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*, miteremko ya milima, pamoja na wafalme wake wote. Hakubakiza mtu yeyote. Akaangamiza kabisa kila kitu chenye pumzi, kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alivyokuwa ameamuru. \v 41 Yoshua akawashinda kuanzia Kadesh-Barnea hadi Gaza na kutoka eneo lote la Gosheni hadi Gibeoni. \v 42 Wafalme hawa wote pamoja na nchi zao Yoshua aliwashinda kwa wakati mmoja, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliwapigania Israeli. \p \v 43 Ndipo Yoshua akarudi pamoja na Israeli yote kwenye kambi huko Gilgali. \c 11 \s1 Wafalme wa kaskazini washindwa \p \v 1 Yabini mfalme wa Hazori aliposikia habari hizo, akatuma ujumbe kwa Yobabu mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu, \v 2 na pia kwa wafalme wa upande wa kaskazini wale waliokuwa milimani, katika Araba upande wa kusini mwa Kinerethi, katika Shefela\f + \fr 11:2 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*, na katika miinuko ya Nafoth-Dori upande wa magharibi; \v 3 kwa Wakanaani upande wa mashariki na magharibi; kwa Waamori, Wahiti, Waperizi na Wayebusi katika nchi ya vilima; na kwa Wahivi chini ya Hermoni katika eneo ya Mispa. \v 4 Wakaja na vikosi vyao vyote na idadi kubwa ya farasi na magari ya vita: jeshi kubwa, kama wingi wa mchanga ulio pwani ya bahari. \v 5 Wafalme hawa wote wakaunganisha majeshi yao na kupiga kambi pamoja kwenye Maji ya Meromu, ili kupigana dhidi ya Israeli. \p \v 6 Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Usiwaogope, kwa sababu kesho saa kama hii nitawatia wote mikononi mwa Israeli, wakiwa wameuawa. Utakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuyachoma moto magari yao ya vita.” \p \v 7 Hivyo Yoshua na jeshi lake lote wakaja dhidi yao ghafula kwenye Maji ya Meromu na kuwashambulia, \v 8 naye Mwenyezi Mungu akawatia mikononi mwa Israeli. Wakawashinda na kuwafukuza hadi Sidoni Kuu na kuwafikisha Misrefoth-Maimu, hadi Bonde la Mispa upande wa mashariki, hata pakawa hakuna yeyote aliyebaki. \v 9 Yoshua akawatendea kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru. Akakata mishipa ya nyuma ya miguu ya farasi wao na kuchoma moto magari yao ya vita. \p \v 10 Wakati huo Yoshua akarudi na kuuteka mji wa Hazori na kumuua mfalme wake kwa upanga. (Hazori ulikuwa mji mkuu wa falme hizo zote.) \v 11 Kila aliyekuwa ndani yake wakamuua kwa upanga. Wakawaangamiza kabisa, wala hawakusaza chochote chenye pumzi, na akauchoma Hazori kwa moto. \p \v 12 Yoshua akaiteka hii miji yote ya kifalme pamoja na wafalme wake, na akawaua kwa upanga. Akawaangamiza kabisa wote, jinsi Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyowaagiza. \v 13 Lakini Israeli hawakuichoma moto hata mojawapo ya miji iliyojengwa katika vilima vyao vidogo, isipokuwa mji wa Hazori, ambao Yoshua aliuchoma kwa moto. \v 14 Waisraeli wakajichukulia nyara zote na mifugo yote ya miji hii, bali waliwaua watu wote kwa upanga hadi walipowaangamiza kabisa, pasipo kumbakiza yeyote mwenye pumzi. \v 15 Kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa mtumishi wake, vivyo hivyo Musa alimwagiza Yoshua, naye Yoshua akafanya vivyo hivyo; hakukosa kufanya lolote katika yale yote Mwenyezi Mungu aliyomwagiza Musa. \p \v 16 Yoshua akaiteka nchi hii yote: nchi ya vilima, Negebu yote, eneo yote ya Gosheni, na Shefela, Araba na milima ya Israeli pamoja na materemko yake, \v 17 kuanzia Mlima Halaki ambao umeinuka kuelekea Seiri hadi Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni chini ya Mlima Hermoni. Akawateka wafalme wake wote, akawapiga na kuwaua. \v 18 Yoshua akapigana vita dhidi ya wafalme hawa wote kwa muda mrefu. \v 19 Hakuna mji wowote katika eneo hili uliofanya mkataba wa amani na Israeli, isipokuwa hao Wahivi wa Gibeoni. Wengine wote walishindwa katika vita. \v 20 Kwa maana Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, awafutilie mbali pasipo huruma, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 21 Wakati huo Yoshua akaenda kuwaangamiza Waanaki kutoka nchi ya vilima: kuanzia Hebroni, Debiri na Anabu, na kutoka nchi yote ya vilima ya Yuda, na kutoka nchi yote ya vilima ya Israeli. Yoshua akawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. \v 22 Hakuna Waanaki waliosalia katika eneo la Waisraeli; ila tu, kuna wachache waliosalia katika maeneo ya Gaza, Gathi na Ashdodi. \v 23 Hivyo Yoshua akaiteka nchi hiyo yote kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza Musa, naye Yoshua akawapa Israeli kuwa urithi wao, kulingana na walivyogawanyika katika makabila yao. \p Ndipo nchi ikawa na amani bila vita. \c 12 \s1 Orodha ya wafalme walioshindwa \lh \v 1 Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kumiliki maeneo yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni hadi Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki mwa Araba: \b \li1 \v 2 Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni. \li2 Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. \li2 \v 3 Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi\f + \fr 12:3 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Galilaya\fqa*\f* hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi\f + \fr 12:3 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari Mfu\fqa*\f*), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya miteremko ya Pisga. \b \li1 \v 4 Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei. \li2 \v 5 Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni. \b \lf \v 6 Musa, mtumishi wa \nd Bwana,\nd* na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao. \b \p \v 7 Hawa ndio wafalme ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao. \v 8 Nchi hizi ni: nchi ya vilima, Shefela\f + \fr 12:8 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*, Araba, miteremko ya milima, jangwa, na Negebu; yaani nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \b \lh Wafalme hawa walikuwa: \b \li1 \v 9 mfalme wa Yeriko; \li1 mfalme wa Ai (karibu na Betheli); \li1 \v 10 mfalme wa Yerusalemu; \li1 mfalme wa Hebroni; \li1 \v 11 mfalme wa Yarmuthi; \li1 mfalme wa Lakishi; \li1 \v 12 mfalme wa Egloni; \li1 mfalme wa Gezeri; \li1 \v 13 mfalme wa Debiri; \li1 mfalme wa Gederi; \li1 \v 14 mfalme wa Horma; \li1 mfalme wa Aradi; \li1 \v 15 mfalme wa Libna; \li1 mfalme wa Adulamu; \li1 \v 16 mfalme wa Makeda; \li1 mfalme wa Betheli; \li1 \v 17 mfalme wa Tapua; \li1 mfalme wa Heferi; \li1 \v 18 mfalme wa Afeki; \li1 mfalme wa Lasharoni; \li1 \v 19 mfalme wa Madoni; \li1 mfalme wa Hazori; \li1 \v 20 mfalme wa Shimron-Meroni; \li1 mfalme wa Akshafu; \li1 \v 21 mfalme wa Taanaki; \li1 mfalme wa Megido; \li1 \v 22 mfalme wa Kedeshi; \li1 mfalme wa Yokneamu katika Karmeli; \li1 \v 23 mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori); \li1 mfalme wa Goimu katika Gilgali; \li1 \v 24 mfalme wa Tirsa; \b \lf jumla ya wafalme thelathini na mmoja (31). \c 13 \s1 Sehemu za Kanaani ambazo hazijatwaliwa \p \v 1 Yoshua alipokuwa mzee, umri wake ukiwa umesogea sana, Mwenyezi Mungu akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado imesalia sehemu kubwa sana ya nchi ambayo haijatwaliwa. \b \lh \v 2 “Nchi iliyosalia ni hii: \b \li1 “maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: \v 3 kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani, maeneo yale matano ya watawala wa Wafilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni; \li1 nchi ya Waavi \v 4 kuanzia kusini; \li1 nchi yote ya Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na eneo la Waamori, \li1 \v 5 eneo la Wagebali; \li1 na Lebanoni yote kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi. \b \p \v 6 “Na kuhusu wakaaji wote katika maeneo ya milima, kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza, niwaondoe kwa ajili ya Waisraeli. Hakikisha umegawa nchi hii kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuagiza, \v 7 sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.” \s1 Mgawanyo wa nchi mashariki mwa Yordani \lh \v 8 Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Musa aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyowagawia. \li1 \v 9 Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, kuanzia mji ulio katikati ya bonde, likijumlisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba hadi Diboni, \v 10 nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamoni. \li1 \v 11 Vilevile ilijumlisha Gileadi, eneo la Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote ikienea hadi Saleka: \v 12 yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Musa alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao. \v 13 Lakini Waisraeli hawakuwafukuza Wageshuri na Wamaaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo. \b \li1 \v 14 Lakini kwa kabila la Lawi, Musa hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ndizo zilikuwa urithi wao, kama alivyowaahidi. \b \lh \v 15 Haya ndio maeneo ambayo Musa alikuwa amewapa kabila la Reubeni kufuatana na koo zao: \li1 \v 16 Eneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba \v 17 hadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, \v 18 Yahasa, Kedemothi, Mefaathi, \v 19 Kiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde, \v 20 Beth-Peori, miteremko ya Pisga na Beth-Yeshimothi: \v 21 miji yote ya uwanda wa juu na eneo lote la utawala wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni. Musa alikuwa amemshinda Sihoni, pia watawala wakuu wa Wamidiani, ambao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, waliokuwa wameungana na Sihoni, ambao waliishi katika nchi ile. \v 22 Pamoja na wale waliouawa katika vita, Waisraeli walikuwa wamemuua kwa upanga Balaamu mwana wa Beori aliyekuwa mwaguzi. \lf \v 23 Mpaka wa Wareubeni ulikuwa ni ukingo wa Mto Yordani. Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa Wareubeni kufuatana na koo zao. \b \lh \v 24 Haya ndio maeneo ambayo Musa alikuwa amewapa kabila la Gadi, kufuatana na koo zao: \li1 \v 25 Nchi ya Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Amoni iliyoenea hadi Aroeri, karibu na Raba; \v 26 na kuanzia Heshboni hadi Ramath-Mispa na Betonimu, na kutoka Mahanaimu hadi eneo la Debiri; \v 27 na katika bonde, Beth-Haramu, Beth-Nimra, Sukothi na Safoni na sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Sihoni mfalme wa Heshboni (upande wa mashariki mwa Mto Yordani, eneo inayoishia kwenye Bahari ya Kinerethi\f + \fr 13:27 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Galilaya\fqa*\f*). \lf \v 28 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Gadi kufuatana na koo zao. \b \lh \v 29 Haya ndio maeneo ambayo Musa alikuwa amewapa nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, kufuatana na koo zao: \li1 \v 30 Eneo lililoenea kuanzia Mahanaimu, na kujumlisha Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini, \v 31 nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). \lf Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, kufuatana na koo zao. \b \lf \v 32 Huu ndio urithi Musa alipeana alipokuwa katika tambarare za Moabu, ng’ambo ya Yordani, mashariki mwa Yeriko. \v 33 Lakini kwa kabila la Walawi, Musa hakuwapa urithi; Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi. \c 14 \s1 Mgawanyo wa nchi magharibi mwa Yordani \p \v 1 Basi haya ndio maeneo Waisraeli waliyapokea kama urithi katika nchi ya Kanaani, ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliwagawia. \v 2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru Musa. \v 3 Musa alikuwa amewapa yale makabila mawili na nusu urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi miongoni mwa hao wengine, \v 4 kwa kuwa wana wa Yusufu walikuwa makabila mawili; Manase na Efraimu. Walawi hawakupata mgawo wa ardhi, bali walipewa miji tu kwa ajili ya kuishi, pamoja na maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo yao na mali zao. \v 5 Kwa hiyo Waisraeli wakagawana ile nchi, kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \s1 Kalebu anapewa mji wa Hebroni \p \v 6 Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo Mwenyezi Mungu alimwambia Musa mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi. \v 7 Nilikuwa na umri wa miaka arobaini, wakati Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu, aliponituma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza hiyo nchi. Nami nikamletea taarifa kama kulingana na nilivyosadiki moyoni. \v 8 Lakini ndugu zangu tuliopanda nao waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa hofu. Bali mimi, nilimfuata Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa moyo wote. \v 9 Hivyo katika siku ile, Musa akaniapia, ‘Nchi ambayo umeikanyaga kwa miguu yako itakuwa urithi wako na wa watoto wako milele, kwa sababu umemfuata Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa moyo wote.’ \p \v 10 “Sasa basi, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoahidi, ameniweka hai kwa miaka arobaini na tano tangu alipomwambia Musa jambo hili, Waisraeli walipokuwa wanazunguka jangwani. Hivyo mimi hapa leo nina umri wa miaka themanini na tano! \v 11 Bado nina nguvu kama siku ile Musa aliponituma; nina nguvu za kwenda vitani sasa kama nilivyokuwa wakati ule. \v 12 Basi nipe nchi hii ya vilima, ambayo Mwenyezi Mungu aliniahidi siku ile. Wewe mwenyewe ulisikia wakati ule kwamba Waanaki walikuwa huko na miji yao ilikuwa mikubwa na yenye ngome, lakini, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, nitawafukuza watoke huko kama vile alivyonena.” \p \v 13 Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune, na akampa Hebroni kama urithi wake. \v 14 Hivyo Hebroni imekuwa mali ya Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi tangu wakati ule, kwa sababu alimwandama Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa moyo wote. \v 15 (Hebroni uliitwa Kiriath-Arba hapo mwanzo, kuitanishwa na Arba aliyekuwa mtu mkuu kupita wote miongoni mwa Waanaki.) \p Kisha nchi ikawa na amani bila vita. \c 15 \s1 Mgawo kwa Yuda \lh \v 1 Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea kufuatana na koo zao, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini. \li1 \v 2 Mpaka wao wa kusini ulianzia ghuba iliyo kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi, \v 3 ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini, kisha ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni, ukapanda hadi Adari, na ukapinda hadi Karka. \v 4 Kisha ukaendelea hadi Azmoni, na kuunganika na Kijito cha Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini. \li1 \v 5 Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia. \li1 Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia, \v 6 ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. \v 7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori, na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na miteremko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli. \v 8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi mwa Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai. \v 9 Kutoka juu ya kilima, mpaka ule ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kuteremka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu). \v 10 Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukashuka hadi Beth-Shemeshi, na kukatiza hadi Timna. \v 11 Ukaelekea hadi mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini. \li1 \v 12 Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu. \b \lf Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao. \b \s1 Nchi aliyopewa Kalebu \r (Waamuzi 1:11-15) \p \v 13 Kwa kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni. (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki.) \v 14 Kutoka Hebroni, Kalebu alifukuza hao Waanaki watatu: Sheshai, Ahimani na Talmai, wana wa Anaki. \v 15 Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu walioishi Debiri (mji wa Debiri hapo uliitwa Kiriath-Seferi). \v 16 Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.” \v 17 Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake, akaolewa naye. \p \v 18 Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?” \p \v 19 Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini. \b \s1 Miji ya Yuda \lh \v 20 Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, kufuatana na koo zao: \b \li1 \v 21 Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa: \li2 Kabseeli, Ederi, Yaguri, \v 22 Kina, Dimona, Adada, \v 23 Kedeshi, Hazori, Ithnani, \v 24 Zifu, Telemu, Bealothi, \v 25 Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori), \v 26 Amamu, Shema, Molada, \v 27 Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti, \v 28 Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia, \v 29 Baala, Iyimu, Esemu, \v 30 Eltoladi, Kesili, Horma, \v 31 Siklagi, Madmana, Sansana, \v 32 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake. \b \li1 \v 33 Katika Shefela\f + \fr 15:33 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*: \li2 Eshtaoli, Sora, Ashna, \v 34 Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu, \v 35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka, \v 36 Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 37 Senani, Hadasha, Migdal-Gadi, \v 38 Dileani, Mispa, Yoktheeli, \v 39 Lakishi, Boskathi, Egloni, \v 40 Kaboni, Lamasi, Kitlishi, \v 41 Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 42 Libna, Etheri, Ashani, \v 43 Yifta, Ashna, Nesibu, \v 44 Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 45 Ekroni, pamoja na makazi yake na vijiji vyake; \v 46 magharibi mwa Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake; \v 47 Ashdodi, makazi yake na vijiji vyake, na Gaza, makazi yake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu. \b \li1 \v 48 Katika nchi ya vilima: \li2 Shamiri, Yatiri, Soko, \v 49 Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri), \v 50 Anabu, Eshtemoa, Animu, \v 51 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na moja pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 52 Arabu, Duma, Ashani, \v 53 Yanimu, Beth-Tapua, Afeka, \v 54 Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, \v 56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa, \v 57 Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 58 Halhuli, Beth-Suri, Gedori, \v 59 Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake. \li2 \v 60 Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake. \li1 \v 61 Huko jangwani: \li2 Beth-Araba, Midini, Sekaka, \v 62 Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake. \b \p \v 63 Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, walioishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda. \c 16 \s1 Mgawo kwa Efraimu na Manase \li1 \v 1 Mgawanyo wa Yusufu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli. \v 2 Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia eneo la Waarki huko Atarothi, \v 3 ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini. \lf \v 4 Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yusufu, walipokea urithi wao. \b \b \lh \v 5 Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, kufuatana na koo zao: \b \li1 Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu, \v 6 na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmeta upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki hadi Taanath-Shilo, ukiupita hadi Yanoa upande wa mashariki. \v 7 Kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani. \v 8 Kutoka Tapua, mpaka ulienda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, kufuatana na koo zao. \li1 \v 9 Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase. \m \v 10 Hawakuwatoa Wakanaani walioishi Gezeri; hadi leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu, lakini wanatumikishwa kwa kazi ngumu. \c 17 \s1 Mgawo wa nusu nyingine ya Manase upande wa magharibi \p \v 1 Huu ndio mgawo wa kabila la Manase, mzaliwa wa kwanza wa Yusufu. Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, aliyekuwa baba wa Wagileadi, alipewa Gileadi na Bashani kwa sababu alikuwa hodari katika vita. \v 2 Kwa hiyo mgawo huu ulikuwa kwa ajili ya watu wa Manase waliokuwa wamebaki, ambao ni koo za Abiezeri, Heleki, Asirieli, Shekemu, Heferi na Shemida. Hawa ndio wanaume wale wengine wa uzao wa Manase mwana wa Yusufu kwa koo zao. \p \v 3 Basi Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase hakuwa na wana wa kiume ila binti tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. \v 4 Wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi, wakasema: “Mwenyezi Mungu alimwagiza Musa atupatie urithi miongoni mwa ndugu zetu.” Kwa hiyo Yoshua akawapa urithi pamoja na ndugu wa baba yao, kufuatana na agizo la Mwenyezi Mungu. \v 5 Zaidi ya Gileadi na Bashani mashariki mwa Yordani, fungu la Manase lilikuwa na sehemu kumi za nchi, \v 6 kwa sababu wale binti za kabila la Manase walipokea urithi pamoja na wana wa kiume. Nchi ya Gileadi ilikuwa mali ya wazao wa Manase waliobaki. \li1 \v 7 Eneo la Manase lilienea kuanzia Asheri hadi Mikmeta mashariki mwa Shekemu. Mpaka ule ulielekea upande wa kusini kutoka pale kujumuisha watu walioishi En-Tapua. \v 8 (Nchi ya Tapua ilikuwa mali ya Manase, lakini Tapua yenyewe iliyo mpakani mwa nchi ya Manase ilikuwa ya Waefraimu.) \v 9 Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwa na miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde, na kuishia kwenye bahari. \v 10 Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na likapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki. \li1 \v 11 Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na makazi yote ya miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi\f + \fr 17:11 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Nafoth-Dori\fqa*\f*). \b \p \v 12 Lakini Wamanase hawakuweza kuimiliki miji hii, kwa kuwa Wakanaani walikazana kuishi katika maeneo hayo. \v 13 Hata hivyo, Waisraeli walivyoendelea kupata nguvu waliwatumikisha Wakanaani na kuwatia katika kazi za kulazimishwa, lakini hawakuwafukuza kabisa. \p \v 14 Wana wa Yusufu wakamwambia Yoshua, “Kwa nini umetupatia sisi mgawo mmoja tu na sehemu moja tu kuwa urithi? Sisi tu watu wengi sana, na Mwenyezi Mungu ametubariki kwa wingi.” \p \v 15 Yoshua akajibu, “Kama ninyi ni wengi sana, na kama nchi ya vilima ya Efraimu ni ndogo sana kwenu, pandeni msituni mkafyeke eneo kwa ajili yenu wenyewe huko kwenye nchi ya Waperizi na Warefai.” \p \v 16 Wana wa Yusufu wakajibu, “Hiyo nchi ya vilima haitutoshi, nao Wakanaani wote wanaoishi katika tambarare wana magari ya vita ya chuma, yaani wale walio Beth-Shani na makazi yake, na wale walio katika Bonde la Yezreeli.” \p \v 17 Lakini Yoshua akanena na nyumba ya Yusufu, yaani Efraimu na Manase: “Ninyi ni wengi sana na wenye nguvu sana. Hamtakuwa na mgawo mmoja tu, \v 18 bali pia nchi hii ya vilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya vita ya chuma, na wana nguvu, mtaweza kuwafukuza humo.” \c 18 \s1 Mgawanyo wa nchi iliyobaki \p \v 1 Kusanyiko lote la Waisraeli wakakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao, \v 2 lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao. \p \v 3 Hivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, amewapa? \v 4 Chagueni watu watatu kutoka kila kabila. Nitawatuma kukagua nchi hiyo na kuandika taarifa kuhusu mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Kisha watarudi kwangu. \v 5 Mtaigawanya hiyo nchi katika sehemu saba. Yuda atabaki katika eneo lake upande wa kusini na nyumba ya Yusufu katika nchi yake upande wa kaskazini. \v 6 Baada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \v 7 Hata hivyo, Walawi hawatakuwa na sehemu miongoni mwenu, kwa maana huduma ya ukuhani kwa Mwenyezi Mungu ndio urithi wao. Nao Gadi, Reubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapata urithi wao upande wa mashariki mwa Yordani, ambako Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa.” \p \v 8 Watu hao walipokuwa wanaondoka kwenda kuikagua hiyo nchi, Yoshua akawaagiza, “Nendeni mkakague hiyo nchi na mwandike maelezo yake. Kisha mrudi kwangu, nami nitawapigia kura hapa Shilo mbele za Mwenyezi Mungu.” \v 9 Ndipo hao watu walipoondoka na kupita katika ile nchi. Wakaandika maelezo yake kwenye kitabu, mji kwa mji, katika sehemu saba na kurudisha taarifa kwa Yoshua huko kambini Shilo. \b \lh \v 10 Basi Yoshua akawapigia kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, na hapo akawagawia Waisraeli nchi kulingana na makabila yao. \s1 Mgawo kwa Benyamini \lh \v 11 Kura ya kwanza iliangukia kabila la Benyamini, kufuatana na koo zao. Eneo lao walilogawiwa lilikuwa kati ya kabila la Yuda na la Yusufu. \li1 \v 12 Upande wa kaskazini, mpaka wao ulianzia pale Yordani, kupitia kaskazini mwa mteremko wa Yeriko, na kuendelea magharibi kuingia katika nchi ya vilima, ukitokea kwenye jangwa la Beth-Aveni. \v 13 Kutoka hapo ulikatiza kwenye mteremko wa kusini mwa Luzu (yaani Betheli) na kushuka hadi Ataroth-Adari katika kilima kusini mwa Beth-Horoni ya Chini. \li1 \v 14 Kutoka kilima kinachotazamana na Beth-Horoni upande wa kusini mpaka ule ukazunguka kusini kufuatia upande wa magharibi, na ukatokezea Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu), mji wa watu wa Yuda. Huu ndio uliokuwa upande wa magharibi. \li1 \v 15 Upande wa kusini mpaka ulianzia kwenye viunga vya Kiriath-Yearimu kwa upande wa magharibi, nao ukatokeza kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa. \v 16 Mpaka ukateremka hadi shefela inayotazamana na Bonde la Ben-Hinomu, kaskazini mwa Bonde la Warefai. Ukaendelea chini kwenye Bonde la Hinomu sambamba na mteremko wa kusini mwa mji mkubwa wa Wayebusi na kisha hadi En-Rogeli. \v 17 Kisha ukapinda kuelekea kaskazini, ukaenda hadi En-Shemeshi na kuendelea hadi Gelilothi, inayotazamana na Njia ya Adumimu, ukateremka hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. \v 18 Ukaendelea upande wa mteremko wa kaskazini wa Beth-Araba ukateremka hadi Araba. \v 19 Kisha ukaenda mpaka kwenye mteremko wa kaskazini wa Beth-Hogla na kujitokeza kwenye ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, kwenye maingilio ya Yordani upande wa kusini. Huo ulikuwa mpaka wa kusini. \li1 \v 20 Nayo Yordani ikawa ndio mpaka wa upande wa mashariki. \lf Hii ndiyo ilikuwa mipaka iliyoonesha urithi wa koo za Benyamini pande zote. \b \lh \v 21 Kabila la Benyamini, kufuatana na koo zao, lilikuwa na miji ifuatayo: \li1 Yeriko, Beth-Hogla, Emeki-Kesisi, \v 22 Beth-Araba, Semaraimu, Betheli, \v 23 Avimu, Para na Ofra, \v 24 Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake. \li1 \v 25 Gibeoni, Rama na Beerothi, \v 26 Mispa, Kefira, Moza, \v 27 Rekemu, Irpeeli, Tarala, \v 28 Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. \lf Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake. \c 19 \s1 Mgawo kwa Simeoni \lh \v 1 Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, kufuatana na koo zao. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. \v 2 Ulijumuisha: \li1 Beer-Sheba (au Sheba), Molada, \v 3 Hasar-Shuali, Bala, Esemu, \v 4 Eltoladi, Bethuli, Horma, \v 5 Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, \v 6 Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na tatu pamoja na vijiji vyake. \li1 \v 7 Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, \v 8 pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii hadi Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu). \lf Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni kufuatana na koo zao. \v 9 Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda. \s1 Mgawo kwa Zabuloni \lh \v 10 Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, kufuatana na koo zao: \li1 Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. \v 11 Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea hadi kwenye bonde karibu na Yokneamu. \v 12 Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia. \v 13 Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea. \v 14 Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli. \li1 \v 15 Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake. \lf \v 16 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa Zabuloni, kufuatana na koo zao. \s1 Mgawo kwa Isakari \lh \v 17 Kura ya nne ikaangukia kabila la Isakari, kufuatana na koo zao. \v 18 Eneo lao lilijumuisha: \li1 Yezreeli, Kesulothi, Shunemu, \v 19 Hafaraimu, Shioni, Anaharathi, \v 20 Rabithi, Kishioni, Ebesi, \v 21 Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi. \li1 \v 22 Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani. \li1 Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. \lf \v 23 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, kufuatana na koo zao. \s1 Mgawo kwa Asheri \lh \v 24 Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. \v 25 Eneo lao lilijumuisha: \li1 Helkathi, Hali, Beteni, Akshafu, \v 26 Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi. \v 27 Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto. \v 28 Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu. \v 29 Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu, \v 30 Uma, Afeki na Rehobu. \li1 Ilikuwa miji ishirini na mbili, pamoja na vijiji vyake. \lf \v 31 Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. \s1 Mgawo kwa Naftali \lh \v 32 Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, kufuatana na koo zao: \li1 \v 33 Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mwaloni ulio Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani. \v 34 Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki. \li1 \v 35 Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, \v 36 Adama, Rama, Hazori, \v 37 Kedeshi, Edrei, na En-Hasori, \v 38 Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. \li1 Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake. \lf \v 39 Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Naftali, kufuatana na koo zao. \s1 Mgawo kwa Dani \lh \v 40 Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, kufuatana na koo zao. \v 41 Eneo la urithi wao lilijumuisha: \li1 Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi, \v 42 Shaalabini, Aiyaloni, Ithla, \v 43 Eloni, Timna, Ekroni, \v 44 Elteke, Gibethoni, Baalathi, \v 45 Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni, \v 46 Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa. \lf \v 47 (Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.) \lf \v 48 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Dani, kufuatana na koo zao. \s1 Mgawo kwa Yoshua \li1 \v 49 Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao, \v 50 kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera\f + \fr 19:50 \fr*\ft Unajulikana pia kama \ft*\fqa Timnath-Heresi\fqa*\ft (taz. \+xt Yoshua 24:30; Waamuzi 2:9\+xt*).\ft*\f* ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko. \b \lf \v 51 Haya ndio maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi. \c 20 \s1 Miji ya makimbilio \r (Hesabu 35:9-34) \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, \v 2 “Waambie Waisraeli, watenge miji ya kukimbilia, kama nilivyokuagiza kupitia Musa, \v 3 ili mtu yeyote atakayemuua mtu kwa bahati mbaya na pasipo kukusudia aweze kukimbilia huko na kujiepusha na mlipiza kisasi wa damu. \p \v 4 “Anapokimbilia mojawapo ya hii miji, atasimama kwenye maingilio ya lango la mji mkuu na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao. \v 5 Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru. \v 6 Huyu aliyeua atakaa kwenye mji huo hadi awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na hadi kuhani mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani mwake katika mji ambao aliukimbia.” \p \v 7 Basi wakatenga Kedeshi katika Galilaya kwenye nchi ya vilima ya Naftali, Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-Arba (yaani Hebroni) kwenye nchi ya vilima ya Yuda. \v 8 Katika upande wa mashariki mwa Yordani (ng’ambo ya Yeriko) wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase. \v 9 Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote aishiye miongoni mwao aliyemuua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji hiyo iliyotengwa na asiuawe na mlipiza kisasi wa damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko. \c 21 \s1 Miji kwa Walawi \p \v 1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli \v 2 huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Mwenyezi Mungu aliamuru kupitia Musa kuwa mtupe miji ya kuishi yenye maeneo ya malisho kwa mifugo yetu.” \b \lh \v 3 Hivyo kama vile Mwenyezi Mungu alivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo, na maeneo ya malisho ya kila mji kutoka urithi wao wenyewe. \b \li1 \v 4 Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, kufuatana na koo zao. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Haruni walipewa miji kumi na tatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini. \li1 \v 5 Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase. \li1 \v 6 Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na tatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani. \li1 \v 7 Wazao wa Merari, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na mbili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni. \b \lf \v 8 Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii na maeneo ya malisho ya kila mji, kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru kupitia kwa Musa. \b \li1 \v 9 Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina \v 10 (miji hii walipewa wazao wa Haruni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): \li2 \v 11 Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na eneo lake la malisho lililouzunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.) \v 12 Lakini mashamba na vijiji vilivyouzunguka mji walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake. \pi1 \v 13 Kwa hiyo wazao wa kuhani Haruni wakapewa Hebroni (mji mkuu wa makimbilio kwa ajili ya yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna, \v 14 Yatiri, Eshtemoa, \v 15 Holoni, Debiri, \v 16 Aini, Yuta na Beth-Shemeshi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji tisa kutoka kwa makabila haya mawili. \li1 \v 17 Kutoka kabila la Benyamini wakawapa \li2 Gibeoni, Geba, \v 18 Anathothi na Almoni, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. \lf \v 19 Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Haruni, ilikuwa kumi na tatu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. \b \lh \v 20 Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu: \li1 \v 21 Katika nchi ya vilima ya Efraimu, walipewa: \li2 Shekemu (mji wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri, \v 22 Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. \li1 \v 23 Pia kutoka kabila la Dani, wakapokea: \li2 Elteke, Gibethoni, \v 24 Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. \li1 \v 25 Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea: \li2 Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji miwili. \lf \v 26 Miji hii kumi, na maeneo ya malisho ya kila mji, ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki. \b \lh \v 27 Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: \li1 kutoka nusu ya kabila la Manase: \li2 Golani katika Bashani (mji wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji miwili; \li1 \v 28 kutoka kabila la Isakari, walipewa: \li2 Kishioni, Daberathi, \v 29 Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne; \li1 \v 30 kutoka kabila la Asheri, walipewa: \li2 Mishali, Abdoni, \v 31 Helkathi na Rehobu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. \li1 \v 32 Kutoka kabila la Naftali, walipewa: \li2 Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji mitano. \lf \v 33 Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na tatu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. \b \lh \v 34 Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa: \li1 kutoka kabila la Zabuloni: \li2 Yokneamu, Karta, \v 35 Dimna na Nahalali, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne; \li1 \v 36 kutoka kabila la Reubeni, walipewa: \li2 Bezeri, Yahasa, \v 37 Kedemothi na Mefaathi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne; \li1 \v 38 kutoka kabila la Gadi, walipewa: \li2 Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu, \v 39 Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji: miji minne. \lf \v 40 Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na mbili. \b \lf \v 41 Miji yote ya Walawi katika eneo lililomilikiwa na Waisraeli ilikuwa arobaini na nane, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji. \v 42 Kila mji kati ya miji hii ulikuwa na maeneo ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote. \b \p \v 43 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo. \v 44 Mwenyezi Mungu akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, Mwenyezi Mungu akawatia adui zao wote mikononi mwao. \v 45 Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Mwenyezi Mungu kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia. \c 22 \s1 Makabila ya mashariki kurudi nyumbani \p \v 1 Ndipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, \v 2 naye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru. \v 3 Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyowapa. \v 4 Sasa kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa ng’ambo ya Yordani. \v 5 Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa: yaani kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.” \p \v 6 Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani kwao. \v 7 (Kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi mwa Yordani pamoja na ndugu zao.) Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki, \v 8 akisema, “Rudini nyumbani kwenu na utajiri wenu mwingi, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia mavazi mengi; nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.” \p \v 9 Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo la Mwenyezi Mungu kupitia Musa. \p \v 10 Walipofika Gelilothi karibu na Yordani, katika nchi ya Kanaani, Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakajenga madhabahu ya fahari kubwa huko kando ya Yordani. \v 11 Waisraeli hao wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi karibu na Yordani kwenye upande wa Israeli, \v 12 Waisraeli hao wengine walikusanyika huko Shilo ili wapigane nao. \p \v 13 Kwa hiyo Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari, aende katika nchi ya Gileadi kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase. \v 14 Wakatuma viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka kwa kila kabila la Israeli, kila mmoja akiwa kiongozi katika jamaa miongoni mwa koo za Israeli. \p \v 15 Walipofika Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, wakawaambia: \v 16 “Kusanyiko lote la Mwenyezi Mungu wasema hivi: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli jinsi hii? Mmewezaje kumwacha Mwenyezi Mungu na kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi? \v 17 Je, dhambi ya Peori haikutosha? Hata ingawa kulikuja tauni juu ya kusanyiko la Mwenyezi Mungu, hadi leo hatujatakasika kutokana na dhambi hiyo! \v 18 Je, sasa ndiyo mnamwacha Mwenyezi Mungu? \p “ ‘Mkimwasi Mwenyezi Mungu leo, kesho atawakasirikia kusanyiko lote la Israeli. \v 19 Ikiwa nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi ya Mwenyezi Mungu, mahali Maskani ya Mwenyezi Mungu ilipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi ya Mwenyezi Mungu wala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu, isipokuwa madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \v 20 Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, je, ghadhabu haikuwapata kusanyiko lote la Israeli? Si yeye pekee aliyekufa kwa ajili ya dhambi yake.’ ” \p \v 21 Ndipo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walipowajibu viongozi wa koo za Israeli, wakisema: \v 22 “Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, Mwenyezi Mungu! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, Mwenyezi Mungu! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama huu umekuwa ni uasi au kukosa utii kwa Mwenyezi Mungu, msituache hai siku hii ya leo. \v 23 Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwacha Mwenyezi Mungu, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake, Mwenyezi Mungu mwenyewe na atupatilize leo. \p \v 24 “Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli? \v 25 Mwenyezi Mungu ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa Mwenyezi Mungu.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha Mwenyezi Mungu. \p \v 26 “Hii ndiyo sababu tulisema, ‘Tujiweke tayari na tujenge madhabahu, lakini si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa au dhabihu.’ \v 27 Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabudu Mwenyezi Mungu katika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo katika siku zijazo, wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katika Mwenyezi Mungu.’ \p \v 28 “Nasi tulisema, ‘Wakati wowote wakituambia hilo, au kuwaambia uzao wetu, tutawajibu hivi: Angalieni nakala hii ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, ambayo baba zetu waliijenga, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu, bali kama ushahidi kati yetu na ninyi.’ \p \v 29 “Hili jambo la kumwasi Mwenyezi Mungu na kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, isipokuwa madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, iliyo mbele ya Maskani yake na liwe mbali nasi.” \p \v 30 Kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko, hao wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema Wareubeni, Wagadi na Manase, wakaridhika. \v 31 Naye Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akawaambia Wareubeni, Wagadi na Manase, “Leo tunajua kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi, kwa sababu hamkukosa uaminifu kwa Mwenyezi Mungu katika jambo hili. Sasa mmewaokoa Waisraeli kutoka kwa mkono wa Mwenyezi Mungu.” \p \v 32 Ndipo Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari, na viongozi wakarudi Kanaani kutoka mkutano wao na Wareubeni na Wagadi huko Gileadi, nao wakatoa taarifa kwa Waisraeli. \v 33 Walifurahi kusikia taarifa hiyo, na wakamhimidi Mungu. Wala hawakuzungumza tena habari za kupigana vita dhidi yao ili kuharibu nchi ambayo Wareubeni na Wagadi waliishi. \p \v 34 Nao Wareubeni na Wagadi wakaita madhabahu hayo Edi\f + \fr 22:34 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Shahidi\fqa*\f*: kwa kuwa itakuwa shahidi kati yetu na ninyi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu. \c 23 \s1 Yoshua awaaga viongozi \p \v 1 Baada ya muda mrefu kupita, naye Mwenyezi Mungu akawa amewapa Israeli pumziko mbele ya adui zao wote waliowazunguka, Yoshua, wakati huo akiwa mzee na umri ukiwa umeendelea sana, \v 2 akawaita Israeli wote, wazee wao, viongozi, waamuzi na maafisa. Yoshua akawaambia: “Mimi ni mzee na umri wangu umeendelea sana. \v 3 Ninyi wenyewe mmeona kila kitu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alichowatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Ilikuwa ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyewapigania. \v 4 Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari kuu upande wa magharibi. \v 5 Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mwenyewe atawaondoa watoke mbele yenu. Atawafukuza mbele yenu, nanyi mtamiliki nchi yao, kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyowaahidi. \p \v 6 “Kuweni hodari sana, kuweni waangalifu kutii yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa, pasipo kugeuka upande wa kuume au kushoto. \v 7 Msishirikiane na mataifa yaliyobakia kati yenu, wala msiombe kwa majina ya miungu yao au kuapa kwayo. Msiitumikie wala kuisujudia. \v 8 Bali mtashikamana kwa uthabiti na Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kama vile mmefanya hadi sasa. \p \v 9 “Mwenyezi Mungu amewafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu, hadi leo hakuna yeyote aliyeweza kusimama mbele yenu. \v 10 Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapigania, kama alivyoahidi. \v 11 Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. \p \v 12 “Lakini ikiwa mtageuka na kushikamana na mabaki ya mataifa haya yaliyosalia kati yenu na kama mtaoana na kushirikiana nao, \v 13 basi mwe na hakika kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa hayo mbele yenu. Badala yake, watakuwa tanzi na mitego kwenu, mijeledi migongoni mwenu, na miiba machoni mwenu, hata mwangamie kutoka nchi hii nzuri, ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa. \p \v 14 “Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njema Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia. \v 15 Lakini kama vile kila ahadi njema ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, imekuwa kweli, vivyo hivyo Mwenyezi Mungu ataleta maovu yote kama alivyoonya, hadi awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa. \v 16 Mkilivunja agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira ya Mwenyezi Mungu itawaka dhidi yenu, basi nanyi mtaangamia kutoka nchi nzuri aliyowapa ninyi.” \c 24 \s1 Agano lafanywa upya huko Shekemu \p \v 1 Ndipo Yoshua akaita pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu. Akawaita wazee, viongozi, waamuzi na maafisa wa Israeli, nao wakaja mbele za Mungu. \p \v 2 Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Ibrahimu na Nahori, waliishi ng’ambo ya Mto\f + \fr 24:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f*, nao waliiabudu miungu mingine. \v 3 Lakini nilimwondoa baba yenu Ibrahimu kutoka nchi hiyo ng’ambo ya Mto, nami nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani, nikampa wazao wengi. Nikampa Isaka, \v 4 naye Isaka nikampa Yakobo na Esau. Esau nikampa nchi ya vilima ya Seiri, lakini Yakobo pamoja na wanawe wakashuka Misri. \p \v 5 “ ‘Kisha nikawatuma Musa na Haruni, nami nikawapiga Wamisri kwa kile nilichokitenda huko, tena nikawatoa ninyi huko. \v 6 Nilipowatoa baba zenu Misri, mlifika kwenye bahari, nao Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari ya vita na wapanda farasi hadi Bahari ya Shamu. \v 7 Lakini wakamlilia Mwenyezi Mungu wakitaka msaada, naye akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu. \p \v 8 “ ‘Nikawaleta katika nchi ya Waamori ambao waliishi mashariki mwa Yordani. Wakapigana nanyi, lakini nikawatia mikononi mwenu. Nikawaangamiza mbele yenu nanyi mkaimiliki nchi yao. \v 9 Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, alipojiandaa kupigana dhidi ya Israeli, alimwita Balaamu mwana wa Beori apate kuwalaani. \v 10 Lakini sikumkubali Balaamu, kwa hiyo aliwabariki tena na tena, nami niliwaokoa toka mkononi mwake. \p \v 11 “ ‘Ndipo mlipovuka Yordani mkafika Yeriko. Raia wa Yeriko wakapigana nanyi, kama walivyofanya Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi, lakini niliwatia mikononi mwenu. \v 12 Nikatuma nyigu mbele yenu, ambao pia waliwafukuza mbele yenu, hao wafalme wawili wa Waamori. Siyo upanga au upinde wenu wenyewe vilivyowapatia ushindi. \v 13 Hivyo nikawapa ninyi nchi ambayo hamkuitaabikia, na miji ambayo hamkuijenga, na mnaishi ndani yake, na kula kutoka mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.’ \p \v 14 “Sasa basi mcheni Mwenyezi Mungu na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ng’ambo ya Mto na huko Misri, nanyi mtumikieni Mwenyezi Mungu. \v 15 Lakini msipoona vyema kumtumikia Mwenyezi Mungu, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi Mungu.” \p \v 16 Ndipo hao watu wakajibu, “Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Mwenyezi Mungu na kuitumikia miungu mingine! \v 17 Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao. \v 18 Mwenyezi Mungu akayafukuza mbele yetu mataifa yote pamoja na Waamori, walioishi katika nchi hii. Hivyo sisi nasi tutamtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye Mungu wetu.” \p \v 19 Yoshua akawaambia watu, “Hamwezi kumtumikia Mwenyezi Mungu. Yeye ni Mungu Mtakatifu, ni Mungu mwenye wivu. Hatasamehe uasi wenu na dhambi zenu. \v 20 Ikiwa mkimwacha Mwenyezi Mungu na kuitumikia miungu migeni, atageuka na kuwaleteeni maafa na kuwaangamiza, baada ya kuwa mwema kwenu.” \p \v 21 Lakini watu wakamwambia Yoshua, “Sivyo! Sisi tutamtumikia Mwenyezi Mungu.” \p \v 22 Ndipo Yoshua akawaambia, “Ninyi mmekuwa mashahidi juu yenu wenyewe kuwa mmechagua kumtumikia Mwenyezi Mungu.” \p Nao wakajibu, “Ndiyo, tu mashahidi.” \p \v 23 Yoshua akawaambia, “Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni mliyo nayo, nanyi mtoleeni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mioyo yenu.” \p \v 24 Nao watu wakamwambia Yoshua, “Tutamtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na kumtii yeye.” \p \v 25 Siku ile Yoshua akafanya agano kwa ajili ya watu na hapo Shekemu ndipo alipowaandikia amri na sheria. \v 26 Naye Yoshua akayaandika mambo haya katika Kitabu cha Torati ya Mungu. Ndipo akalitwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko chini ya mwaloni, karibu na mahali patakatifu pa Mwenyezi Mungu. \p \v 27 Yoshua akawaambia watu wote, “Tazameni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yote Mwenyezi Mungu aliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.” \p \v 28 Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe. \s1 Kuzikwa katika nchi ya ahadi \p \v 29 Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Mwenyezi Mungu akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. \v 30 Nao wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Sera\f + \fr 24:30 \fr*\ft Unajulikana pia kama \ft*\fqa Timnath-Heresi\fqa*\ft (taz. \+xt Yoshua 19:50; Waamuzi 2:9\+xt*).\ft*\f* katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaashi. \p \v 31 Israeli wakamtumikia Mwenyezi Mungu siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kitu Mwenyezi Mungu alichowatendea Israeli. \p \v 32 Nayo ile mifupa ya Yusufu, ambayo Waisraeli waliipandisha kutoka huko Misri, wakaizika huko Shekemu kwenye eneo ambalo Yakobo alilinunua kwa wana wa Hamori baba yake Shekemu, kwa vipande mia vya fedha. Eneo hili likawa ni urithi wa uzao wa Yusufu. \p \v 33 Naye Eleazari mwana wa Haruni akafariki, akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.