\id JHN - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Yohana \toc1 Yohana \toc2 Yohana \toc3 Yn \mt1 Yohana \c 1 \ms1 Utangulizi \mr (Yohana 1:1-18) \s1 Neno alifanyika mwili \p \v 1 Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. \v 2 Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. \p \v 3 Vitu vyote viliumbwa kupitia kwake, na hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa pasipo yeye. \v 4 Ndani yake kulikuwa na uzima, nao huo uzima ulikuwa nuru ya watu. \v 5 Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda. \p \v 6 Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yahya. \v 7 Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kupitia kwake watu wote waweze kuamini. \v 8 Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. \p \v 9 Nuru halisi inayomwangazia kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni. \v 10 Huyo Neno alikuwako ulimwenguni, na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua. \v 11 Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea. \v 12 Bali wote waliompokea, yaani wale walioliamini jina lake, aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu. \v 13 Hawa hawakuzaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali wamezaliwa kwa mapenzi ya Mungu. \p \v 14 Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba\f + \fr 1:14 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, amejaa neema na kweli. \p \v 15 Yahya alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’ ” \v 16 Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. \v 17 Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Musa, lakini neema na kweli zimekuja kupitia Isa Al-Masihi. \v 18 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba, ndiye ambaye amemdhihirisha. \ms1 Huduma ya Isa kabla ya kurudi Galilaya \mr (Yohana 1:19–4:54) \s1 Ushuhuda wa Yahya \r (Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18) \p \v 19 Huu ndio ushuhuda wa Yahya wakati viongozi wa Wayahudi waliwatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” \v 20 Yahya alikiri waziwazi pasipo kuficha, akasema, “Mimi si Al-Masihi\f + \fr 1:20 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*.” \p \v 21 Wakamuuliza, “Wewe ni nani, basi? Je, wewe ni Ilya?” \p Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.” \p “Je, wewe ni yule Nabii?” \p Akajibu, “Hapana.” \p \v 22 Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?” \p \v 23 Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 24 Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo\f + \fr 1:24 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f*, \v 25 wakamuuliza, “Kama wewe si Al-Masihi, wala si Ilya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza\f + \fr 1:25 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali.\ft*\f*?” \p \v 26 Yahya akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji\f + \fr 1:26 \fr*\ft au \ft*\fqa ndani ya maji\fqa*\f*, lakini kati yenu yupo mtu msiyemjua. \v 27 Yeye anakuja baada yangu, nami sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.” \p \v 28 Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ng’ambo ya Yordani, mahali Yahya alipokuwa akibatiza. \s1 Mwana-Kondoo wa Mwenyezi Mungu \p \v 29 Siku iliyofuata, Yahya alimwona Isa akimjia, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! \v 30 Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’ \v 31 Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.” \p \v 32 Kisha Yahya akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho Mtakatifu wa Mungu akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. \v 33 Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho Mtakatifu wa Mungu akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho wa Mungu.’ \v 34 Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu\f + \fr 1:34 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*.” \s1 Wanafunzi wa kwanza wa Isa \r (Mathayo 4:18-22; Marko 1:16-20; Luka 5:1-11) \p \v 35 Siku iliyofuata, Yahya alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. \v 36 Alipomwona Isa akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!” \p \v 37 Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yahya akisema haya, wakamfuata Isa. \v 38 Isa akageuka, akawaona wakimfuata, akawauliza, “Mnataka nini?” \p Wakamwambia, “Mwalimu, unaishi wapi?” \p \v 39 Isa akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!” \p Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi. \p \v 40 Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yahya alisema na kumfuata Isa. \v 41 Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masihi” (yaani Al-Masihi). \v 42 Naye akamleta kwa Isa. \p Isa akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro\f + \fr 1:42 \fr*\ft Petro kwa Kiyunani au \ft*\fqa Kefa \fqa*\ft kwa Kiaramu; maana yake \ft*\fqa Kipande cha mwamba.\fqa*\f*). \p \v 43 Siku iliyofuata Isa aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.” \p \v 44 Filipo alikuwa raia wa Bethsaida, mji walikotoka Andrea na Petro. \v 45 Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika Torati, na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani Isa Al-Nasiri, mwana wa Yusufu\f + \fr 1:45 \fr*\ft Yusufu hakuwa baba mzazi wa Isa, bali alikuwa baba mlezi.\ft*\f*.” \p \v 46 Nathanaeli akauliza, “Nasiri! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nasiri?” \p Filipo akamwambia, “Njoo uone.” \p \v 47 Isa alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake, akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake.” \p \v 48 Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?” \p Isa akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” \p \v 49 Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!” \p \v 50 Isa akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu kuliko hilo.” \v 51 Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.” \c 2 \s1 Arusi huko Kana \p \v 1 Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Isa alikuwepo. \v 2 Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. \v 3 Divai ilipokwisha, mama yake Isa akamwambia, “Wameishiwa na divai.” \p \v 4 Isa akamwambia, “Mama, kwa nini unanihusisha? Saa yangu haijawadia.” \p \v 5 Mama yake akawaambia wale watumishi, “Fanyeni lolote atakalowaambia.” \p \v 6 Basi hapo palikuwa na mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe; iliwekwa hapo kwa ajili ya desturi ya Kiyahudi ya kujitakasa; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu\f + \fr 2:6 \fr*\ft Kipipa kimoja chenye ujazo wa lita 40.\ft*\f*. \p \v 7 Isa akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi hadi juu. \p \v 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe.” \p Hivyo wakachota, wakampelekea. \v 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilishwa kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando, \v 10 akamwambia, “Watu wote hutoa divai nzuri kwanza, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa sana; lakini wewe umeiweka ile nzuri zaidi hadi sasa.” \p \v 11 Huu ndio muujiza wa kwanza wa Isa; aliufanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. \p \v 12 Baada ya hayo, Isa pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walishuka hadi Kapernaumu, wakakaa huko siku chache. \s1 Isa atakasa Hekalu \r (Mathayo 21:12-17; Marko 11:15-17; Luka 19:45-48) \p \v 13 Ilipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi\f + \fr 2:13 \fr*\ft Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.\ft*\f*, Isa alipanda kwenda Yerusalemu. \v 14 Huko uani la Hekalu aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, nao wengine walikuwa wameketi mezani wakibadili fedha. \v 15 Akatengeneza mjeledi kutokana na kamba, akawafukuza wote kutoka ua la Hekalu, pamoja na kondoo na ng’ombe. Akazipindua meza za wale wabadili fedha na kuzimwaga fedha zao. \v 16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Waondoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa biashara?” \p \v 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa imeandikwa: “Wivu wa nyumba yako utanila.” \p \v 18 Ndipo Wayahudi wakamuuliza, “Unaweza kutuonesha ishara gani ili kuthibitisha mamlaka uliyo nayo ya kufanya mambo haya yote?” \p \v 19 Isa akawajibu, “Libomoeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!” \p \v 20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita, nawe wasema utalijenga kwa siku tatu?” \v 21 Lakini yeye Hekalu alilozungumzia ni mwili wake. \v 22 Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka yale aliyokuwa amesema. Ndipo wakayaamini Maandiko na yale maneno Isa alikuwa ameyasema. \p \v 23 Ikawa Isa alipokuwa Yerusalemu kwenye Sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara na miujiza aliyokuwa akifanya, nao wakaamini katika jina lake. \v 24 Lakini Isa hakujiaminisha kwao, kwa sababu aliwajua wanadamu wote. \v 25 Hakuhitaji ushuhuda wa mtu yeyote kuhusu mwanadamu, kwa kuwa alijua yote yaliyokuwa moyoni mwa kila mtu. \c 3 \s1 Nikodemo amwendea Isa usiku \p \v 1 Basi palikuwa na mtu mmoja Farisayo, jina lake Nikodemo, mmoja wa Baraza la Wayahudi\f + \fr 3:1 \fr*\ft Baraza la Wayahudi ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f* lililotawala. \v 2 Huyu alimjia Isa usiku akamwambia, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo wewe, kama Mungu hayuko pamoja naye.” \p \v 3 Isa akamjibu, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili.” \p \v 4 Nikodemo akauliza, “Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee? Hakika hawezi kuingia mara ya pili kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!” \p \v 5 Isa akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho. \v 6 Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho. \v 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia, ‘Huna budi kuzaliwa mara ya pili.’ \v 8 Upepo huvuma kokote unakopenda. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu unakotoka wala unakoenda. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa na Roho.” \p \v 9 Nikodemo akamuuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” \p \v 10 Isa akamwambia, “Wewe ni mwalimu wa Waisraeli, nawe huelewi mambo haya? \v 11 Amin, amin ninakuambia, sisi tunazungumza lile tunalolijua na tunashuhudia lile tuliloliona. Lakini ninyi watu hamkubali ushuhuda wetu. \v 12 Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni? \v 13 Hakuna mtu yeyote aliyeenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa Adamu. \v 14 Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu, \v 15 ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele. \p \v 16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. \v 17 Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. \v 18 Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. \v 19 Hii ndiyo hukumu: Kwamba nuru imekuja ulimwenguni, nao watu wakapenda giza kuliko nuru, kwa sababu matendo yao ni maovu. \v 20 Kwa kuwa kila atendaye maovu huchukia nuru, wala haji kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. \v 21 Lakini yule aishiye kwa ukweli huja kwenye nuru, ili ionekane wazi kwamba matendo yake yametendeka katika Mungu.” \s1 Ushuhuda wa Yahya kuhusu Isa \p \v 22 Baada ya haya, Isa na wanafunzi wake walienda katika eneo la Yudea, nao wakakaa huko kwa muda na kubatiza watu. \v 23 Yahya naye alikuwa akibatiza watu huko Ainoni karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji mengi. Watu wakamjia huko ili kubatizwa. \v 24 (Hii ilikuwa kabla Yahya hajafungwa gerezani.) \v 25 Mashindano yakazuka kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yahya na Myahudi mmoja kuhusu suala la desturi ya kunawa kwa utakaso. \v 26 Wakamwendea Yahya wakamwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” \p \v 27 Yahya akawajibu, “Hakuna mtu yeyote awezaye kupata kitu chochote isipokuwa kile tu alichopewa kutoka mbinguni. \v 28 Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema, ‘Mimi si Al-Masihi\f + \fr 3:28 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, ila nimetumwa nimtangulie.’ \v 29 Bibi arusi ni wa bwana arusi. Lakini rafiki yake bwana arusi anayesimama karibu naye na kusikiliza kutoka kwake, hufurahi sana aisikiapo sauti ya bwana arusi. Kwa sababu hii furaha yangu imekamilika. \v 30 Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kupungua. \s1 Yeye aliyetoka mbinguni \p \v 31 “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. \v 32 Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake. \v 33 Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. \v 34 Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humpa Roho wake pasipo kipimo. \v 35 Baba\f + \fr 3:35 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* anampenda Mwana\f + \fr 3:35 \fr*\ft Yaani Isa Al-Masihi.\ft*\f*, naye ametia vitu vyote mkononi mwake. \v 36 Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.” \c 4 \s1 Isa azungumza na mwanamke Msamaria \p \v 1 Isa alipata habari kuwa Mafarisayo\f + \fr 4:1 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* walisikia kwamba yeye alikuwa akipata wanafunzi kuliko Yahya na kuwabatiza, \v 2 ingawa kwa kweli si Isa mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. \v 3 Bwana Isa alipojua mambo haya, aliondoka Yudea akarudi tena Galilaya. \p \v 4 Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria. \v 5 Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yusufu. \v 6 Kisima cha Yakobo kilikuwa huko. Naye Isa alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. \p \v 7 Mwanamke mmoja Msamaria alipokuja kuteka maji, Isa akamwambia, “Naomba maji ninywe.” \v 8 (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wameenda mjini kununua chakula.) \p \v 9 Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.) \p \v 10 Isa akamjibu, “Kama ungeijua karama ya Mungu, na ni nani anakuomba maji ya kunywa, ungemwomba yeye, naye angekupa maji ya uzima.” \p \v 11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana\f + \fr 4:11 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi? \v 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?” \p \v 13 Isa akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. \v 14 Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.” \p \v 15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena, wala nisije tena hapa kuteka maji!” \p \v 16 Isa akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.” \p \v 17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” \p Isa akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume. \v 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano, na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli.” \p \v 19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. \v 20 Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.” \p \v 21 Isa akamjibu, “Mwanamke, niamini: wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba\f + \fr 4:21 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. \v 22 Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. \v 23 Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii. \v 24 Mungu ni Roho, na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” \p \v 25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Al-Masihi” (yaani Aliyetiwa mafuta) “anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.” \p \v 26 Isa akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.” \p \v 27 Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au, “Kwa nini unazungumza naye?” \p \v 28 Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini, akawaambia watu, \v 29 “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Al-Masihi\f + \fr 4:29 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*?” \v 30 Basi wakamiminika watu kutoka mjini, wakamwendea Isa. \p \v 31 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Mwalimu, kula.” \p \v 32 Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.” \p \v 33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” \p \v 34 Lakini Isa akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake. \v 35 Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune’? Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa! \v 36 Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja. \v 37 Hivyo ule msemo, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. \v 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda. Wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.” \s1 Wasamaria wengi waamini \p \v 39 Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Isa kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.” \v 40 Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili. \v 41 Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini. \p \v 42 Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kwamba huyu ndiye Al-Masihi, Mwokozi wa ulimwengu.” \s1 Isa amponya mwana wa afisa \p \v 43 Baada ya zile siku mbili, Isa aliondoka kwenda Galilaya. \v 44 (Basi Isa mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.) \v 45 Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu. \p \v 46 Hivyo Isa akafika tena Kana ya Galilaya, kule alikuwa amebadili maji kuwa divai. Kulikuwa na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. \v 47 Huyo mtu aliposikia kwamba Isa alikuwa amewasili Galilaya kutoka Yudea, alimwendea na kumsihi aende akamponye mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa. \p \v 48 Isa akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.” \p \v 49 Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.” \p \v 50 Isa akamjibu, “Nenda zako, mwanao yu hai.” \p Yule afisa akaamini yale maneno Isa aliyomwambia, akaenda zake. \v 51 Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake, wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. \v 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana saa saba, ndipo homa iliisha.” \p \v 53 Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati Isa alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Isa. \p \v 54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Isa alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea. \c 5 \ms1 Huduma ya Isa huko Galilaya, na upinzani uliomkabili huko Yerusalemu \mr (Yohana 5:1–10:42) \s1 Isa amponya mtu kwenye Bwawa la Bethzatha \p \v 1 Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Isa akapanda kwenda Yerusalemu. \v 2 Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa Bethzatha\f + \fr 5:2 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Nyumba ya mizeituni\fqa*\ft ; mahali pengine limetajwa kama \ft*\fqa Bethesda \fqa*\ft kwa Kiaramu, yaani \ft*\fqa Nyumba ya huruma\fqa*\ft , na pengine kama \ft*\fqa Bethsaida\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Nyumba ya uvuvi\fqa*\f* kwa Kiebrania, ambalo lilikuwa limezungukwa na makumbi matano. \v 3 Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe. \v 4 Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule angekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao]\f + \fr 5:3-4 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f*. \v 5 Mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa miaka thelathini na nane alikuwa hapo. \v 6 Isa alipomwona akiwa amelala hapo, na akijua amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?” \p \v 7 Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana\f + \fr 5:7 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.” \p \v 8 Isa akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.” \v 9 Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea. \p Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato. \v 10 Kwa hiyo viongozi wa Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato; si halali wewe kubeba mkeka wako.” \p \v 11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ” \p \v 12 Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?” \p \v 13 Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Isa alikuwa amepotea ndani ya umati ule wa watu waliokuwa hapo. \p \v 14 Baadaye Isa akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa. Usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo baya zaidi.” \v 15 Yule mtu akaenda, akawaambia wale viongozi wa Wayahudi kuwa ni Isa aliyemponya. \s1 Uzima kupitia Mwana \p \v 16 Kwa hiyo viongozi wa Wayahudi wakaanza kumsumbua Isa, kwa sababu alikuwa anafanya mambo kama hayo siku ya Sabato. \v 17 Isa akawajibu, “Baba\f + \fr 5:17 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya kazi.” \v 18 Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumuua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu. \s1 Mamlaka ya Mwana wa Mwenyezi Mungu \p \v 19 Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake. Yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo. \v 20 Baba ampenda Mwana na kumwonesha yale ambayo yeye Baba mwenyewe anayafanya, naye atamwonesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa. \v 21 Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda. \v 22 Wala Baba hamhukumu mtu yeyote, lakini hukumu yote amempa Mwana, \v 23 ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Yeyote asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyemtuma. \p \v 24 “Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini na kuingia uzimani. \v 25 Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu\f + \fr 5:25 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*, nao watakaoisikia watakuwa hai. \v 26 Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake. \v 27 Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu. \p \v 28 “Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake, \v 29 nao watatoka makaburini. Wale waliotenda mema watafufuka wapate uzima, nao wale waliotenda maovu watafufuka ili wahukumiwe. \p \v 30 “Mimi siwezi kufanya jambo lolote peke yangu. Ninavyosikia ndivyo ninavyohukumu, nayo hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake yeye aliyenituma. \s1 Shuhuda kuhusu Isa \p \v 31 “Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. \v 32 Lakini yuko mwingine anishuhudiaye, na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli. \p \v 33 “Mlituma wajumbe kwa Yahya, naye akaishuhudia kweli. \v 34 Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu; la, bali ninalitaja hili ili ninyi mpate kuokolewa. \v 35 Yahya alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake. \p \v 36 “Ninao ushuhuda mkuu kuliko ule wa Yahya. Kazi ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, kazi hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba amenituma. \v 37 Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake, \v 38 wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye. \v 39 Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele. Maandiko haya ndio yanayonishuhudia mimi. \v 40 Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima. \p \v 41 “Mimi sikubali kutukuzwa na wanadamu, \v 42 lakini mimi ninawafahamu. Ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. \v 43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei. Lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea. \v 44 Mnawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamfanyi bidii kupata utukufu unaotoka kwa Mungu? \p \v 45 “Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba. Mshtaki wenu ni Musa, ambaye mmemwekea tumaini lenu. \v 46 Kama mngemwamini Musa, mngeniamini na mimi, kwa maana aliandika habari zangu. \v 47 Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Musa, mtaaminije ninayoyasema?” \c 6 \s1 Isa alisha wanaume 5,000 \r (Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Luka 9:10-17) \p \v 1 Baada ya haya, Isa alienda ng’ambo ya Bahari ya Galilaya (ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia). \v 2 Umati mkubwa wa watu waliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa. \v 3 Kisha Isa akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. \v 4 Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. \p \v 5 Isa alipotazama na kuona umati ule mkubwa wa watu wakimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?” \v 6 Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya. \p \v 7 Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili\f + \fr 6:7 \fr*\ft Dinari 200 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 200.\ft*\f* hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.” \p \v 8 Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia, \v 9 “Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa watu hawa wote?” \p \v 10 Isa akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi (palikuwa na wanaume wapatao elfu tano). \v 11 Ndipo Isa akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka. \p \v 12 Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote.” \v 13 Hivyo wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya ile mikate mitano ya shayiri na samaki wale wawili wadogo vilivyobakishwa na waliokula. \p \v 14 Baada ya watu kuona muujiza ule Isa aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!” \v 15 Isa akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake. \s1 Isa atembea juu ya maji \r (Mathayo 14:22-33; Marko 6:45-52) \p \v 16 Ilipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini. \v 17 Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Isa alikuwa hajajumuika nao. \v 18 Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. \v 19 Wanafunzi walipokuwa wameenda mwendo wa maili tatu au nne\f + \fr 6:19 \fr*\ft kama kilomita 5 au 6\ft*\f*, walimwona Isa akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana. \v 20 Lakini Isa akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” \v 21 Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda. \s1 Watu wanamtafuta Isa \p \v 22 Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ng’ambo waliona kwamba palikuwa na mashua moja tu, na kwamba Isa hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao. \v 23 Lakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia zikafika karibu na mahali pale walipokula mikate baada ya Bwana Isa kumshukuru Mungu. \v 24 Mara wale watu wakatambua kwamba Isa hakuwa hapo, wala wanafunzi wake. Wakaingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu ili kumtafuta Isa. \s1 Isa ni mkate wa uzima \p \v 25 Walipomkuta Isa ng’ambo ya bahari wakamuuliza, “Mwalimu, umefika lini huku?” \p \v 26 Isa akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. \v 27 Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba\f + \fr 6:27 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* Mwenyezi amemtia muhuri.” \p \v 28 Ndipo wakamuuliza, “Tufanye nini ili tupate kuitenda kazi ya Mungu?” \p \v 29 Isa akawajibu, “Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini yeye aliyetumwa naye.” \p \v 30 Hivyo wakamuuliza, “Utafanya ishara gani ya muujiza, ili tuione tukuamini? Utafanya jambo gani? \v 31 Baba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.’ ” \p \v 32 Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, si Musa aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. \v 33 Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.” \p \v 34 Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.” \p \v 35 Isa akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe. \v 36 Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini. \v 37 Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuza nje kamwe. \v 38 Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake yeye aliyenituma. \v 39 Haya ndio mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho. \v 40 Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.” \p \v 41 Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema, “Mimi ndimi mkate ulioshuka kutoka mbinguni.” \v 42 Wakasema, “Huyu si Isa, mwana wa Yusufu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?” \p \v 43 Hivyo Isa akawaambia, “Acheni kunung’unikiana ninyi kwa ninyi. \v 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho. \v 45 Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu. \v 46 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba. \v 47 Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. \v 48 Mimi ni mkate wa uzima. \v 49 Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. \v 50 Lakini hapa kuna mkate kutoka mbinguni, ambao mtu yeyote akiula, hatakufa. \v 51 Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.” \p \v 52 Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?” \p \v 53 Hivyo Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. \v 54 Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. \v 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. \v 56 Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. \v 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. \v 58 Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.” \v 59 Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi\f + \fr 6:59 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* huko Kapernaumu. \s1 Wafuasi wengi wamwacha Isa \p \v 60 Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?” \p \v 61 Isa alipojua kwamba wafuasi wake wananung’unika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi? \v 62 Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza? \v 63 Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima. \v 64 Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Isa alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti. \v 65 Akaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.” \p \v 66 Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata. \p \v 67 Hivyo Isa akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?” \p \v 68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. \v 69 Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.” \p \v 70 Ndipo Isa akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.” \v 71 (Hapa alikuwa anasema kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Isa.) \c 7 \s1 Kutokuamini kwa ndugu zake Isa \p \v 1 Baada ya mambo haya, Isa alienda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi huko walitaka kumuua. \v 2 Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. \v 3 Hivyo ndugu zake Isa wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. \v 4 Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jioneshe kwa ulimwengu.” \v 5 Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini. \p \v 6 Isa akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote. \v 7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. \v 8 Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” \v 9 Baada ya kusema hayo, akabaki Galilaya. \s1 Isa kwenye Sikukuu ya Vibanda \p \v 10 Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alienda lakini kwa siri. \v 11 Viongozi wa Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?” \p \v 12 Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Isa katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” \p Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.” \v 13 Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kwa sababu ya kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. \s1 Isa afundisha kwenye Sikukuu \p \v 14 Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Isa alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha. \v 15 Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, “Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?” \p \v 16 Ndipo Isa akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma. \v 17 Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe. \v 18 Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake. \v 19 Je, Musa hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?” \p \v 20 Ule umati wa watu wakamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?” \p \v 21 Isa akawajibu, “Nimefanya muujiza mmoja na nyote mkastaajabu. \v 22 Lakini kwa kuwa Musa aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Musa bali kwa baba zetu wa zamani), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato. \v 23 Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi Torati ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato? \v 24 Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.” \s1 Je, Isa ndiye Al-Masihi? \p \v 25 Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua? \v 26 Mbona yuko hapa anazungumza hadharani, na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Al-Masihi\f + \fr 7:26 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*? \v 27 Tunafahamu huyu mtu anakotoka, lakini Al-Masihi atakapokuja, hakuna yeyote atakayejua atokako.” \p \v 28 Ndipo Isa, akaendelea kufundisha Hekaluni, akisema, “Ninyi mnanifahamu na kujua nitokako. Mimi sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, bali yeye aliyenituma ni wa kweli na ninyi hammjui. \v 29 Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.” \p \v 30 Ndipo wakatafuta kumkamata, lakini hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijawadia. \v 31 Nao watu wengi wakamwamini, wakasema, “Je, Al-Masihi atakapokuja, atafanya miujiza mikuu kuliko aliyoifanya mtu huyu?” \s1 Walinzi wanatumwa kumkamata Isa \p \v 32 Mafarisayo\f + \fr 7:32 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakasikia watu wakinong’ona mambo kama hayo kuhusu Isa, ndipo wao pamoja na viongozi wa makuhani wakatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata. \p \v 33 Isa akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma. \v 34 Mtanitafuta lakini hamtaniona, nami niliko ninyi hamwezi kuja.” \p \v 35 Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani? \v 36 Yeye ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona,’ na, ‘nami niliko ninyi hamwezi kuja’?” \s1 Mito ya maji ya uzima \p \v 37 Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Isa akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe. \v 38 Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yanavyosema, vijito vya maji ya uzima vitatiririka kutoka ndani yake.” \v 39 Isa aliposema haya, alimaanisha Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye wote waliomwamini wangempokea. Kwa maana hadi wakati huo Roho wa Mungu alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Isa alikuwa bado hajatukuzwa. \s1 Mgawanyiko miongoni mwa watu \p \v 40 Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu miongoni mwa umati ule wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.” \p \v 41 Wengine wakasema, “Huyu ndiye Al-Masihi!” \p Lakini wengine wakauliza, “Je, Al-Masihi kwao ni Galilaya? \v 42 Je, Maandiko hayasemi kwamba Al-Masihi atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” \v 43 Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Isa. \v 44 Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa. \s1 Kutokuamini kwa viongozi wa Wayahudi \p \v 45 Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Isa, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?” \p \v 46 Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.” \p \v 47 Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika? \v 48 Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? \v 49 Lakini umati huu wa watu wasiojua Torati ya Musa, wamelaaniwa.” \p \v 50 Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Isa siku moja usiku, na alikuwa mmoja wao, akauliza, \v 51 “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?” \p \v 52 Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” \p [ \v 53 Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani mwake. \c 8 \nb \v 1 Lakini Isa akaenda katika Mlima wa Mizeituni. \p \v 2 Alfajiri na mapema Isa akaja tena Hekaluni; watu wote wakakusanyika, naye akaketi, akaanza kuwafundisha. \v 3 Walimu wa Torati na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote. \v 4 Wakamwambia Isa, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. \v 5 Katika sheria, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, hadi wafe. Sasa wewe wasemaje?” \v 6 Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. \p Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake. \v 7 Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.” \v 8 Akainama tena na kuandika ardhini. \p \v 9 Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Isa akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake. \v 10 Isa akainuka na kumwambia, “Mwanamke, wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?” \p \v 11 Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja, Bwana.” \p Isa akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako. Kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]\f + \fr 8:11 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana sehemu ya \+xt Yohana 7:53–8:11\+xt*.\ft*\f* \s1 Isa nuru ya ulimwengu \p \v 12 Kisha Isa akasema nao tena, akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata, hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” \p \v 13 Mafarisayo wakamwambia, “Ushuhuda wako haukubaliki, kwa kuwa unajishuhudia mwenyewe.” \p \v 14 Isa akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na ninakoenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakoenda. \v 15 Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu; mimi simhukumu mtu yeyote. \v 16 Lakini hata nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba\f + \fr 8:16 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, aliyenituma. \v 17 Imeandikwa katika Torati yenu kwamba ushahidi wa watu wawili ni thabiti. \v 18 Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.” \p \v 19 Ndipo wakamuuliza, “Huyo Baba yako yuko wapi?” \p Isa akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hammfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngemfahamu na Baba yangu.” \v 20 Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia. \s1 Swali kuhusu Isa ni nani \p \v 21 Isa akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.” \p \v 22 Ndipo wale Wayahudi wakasema, “Je, atajiua? Je, hii ndiyo sababu amesema, ‘Niendako mimi ninyi hamwezi kuja’?” \p \v 23 Akawaambia, “Ninyi mmetoka chini; mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu. \v 24 Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu; kwa maana msipoamini kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.” \p \v 25 Wakamuuliza, “Wewe ni nani?” \p Naye Isa akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nimekuwa nikiwaambia tangu mwanzo. \v 26 Nina mambo mengi ya kusema kuwahusu ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kuaminika, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.” \p \v 27 Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia kuhusu Baba yake wa Mbinguni. \v 28 Kisha Isa akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua Mwana wa Adamu juu, ndipo mtajua kuwa mimi ndiye yule niliyesema, na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu, bali ninasema yale tu Baba yangu amenifundisha. \v 29 Yeye aliyenituma yu pamoja nami; hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.” \v 30 Wengi waliomsikia Isa akisema maneno haya wakamwamini. \s1 Wanafunzi wa kweli \p \v 31 Kisha Isa akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. \v 32 Ndipo mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka huru.” \p \v 33 Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Ibrahimu, nasi hatujakuwa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?” \p \v 34 Isa akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. \v 35 Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima. \v 36 Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. \v 37 Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Ibrahimu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu. \v 38 Ninasema yale niliyoyaona nikiwa mbele za Baba yangu, nanyi mnafanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.” \s1 Isa na Ibrahimu \p \v 39 Wakajibu, “Baba yetu ni Ibrahimu.” \p Isa akawaambia, “Kama mngekuwa wazao wa Ibrahimu, mngefanya mambo yale aliyofanya Ibrahimu. \v 40 Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya jambo la namna hii. \v 41 Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu.” \p Wakamjibu, “Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee.” \p \v 42 Isa akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. \v 43 Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho. \v 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu, ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli, maana hamna kweli ndani yake. Anaposema uongo, yeye husema lugha yake ya asili kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo. \v 45 Lakini kwa sababu nimewaambia kweli, hamkuniamini! \v 46 Je, kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini? \v 47 Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.” \s1 Maelezo ya Isa kujihusu \p \v 48 Wayahudi wakamjibu Isa, “Je, hatuko sahihi tunaposema kwamba wewe ni Msamaria, na kwamba una pepo mchafu?” \p \v 49 Isa akawajibu, “Mimi sina pepo mchafu, bali ninamheshimu Baba yangu, nanyi mnanidharau. \v 50 Lakini mimi sitafuti utukufu wangu mwenyewe, bali yuko anayetaka kunitukuza, naye ndiye mwamuzi. \v 51 Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu, hataona mauti milele.” \p \v 52 Ndipo Wayahudi wakapaza sauti, wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu! Ibrahimu alikufa, na manabii vilevile, nawe unasema kuwa mtu akitii neno lako hatakufa milele. \v 53 Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa, na manabii ambao pia walikufa? Unafikiri wewe ni nani?” \p \v 54 Isa akawajibu, “Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu hauna maana. Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnadai kuwa ni Mungu wenu, ndiye anitukuzaye mimi. \v 55 Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake. \v 56 Baba yenu Ibrahimu alishangilia kwamba angeiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.” \p \v 57 Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, nawe wasema umemwona Ibrahimu?” \p \v 58 Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Ibrahimu hajakuwa, Mimi niko.” \v 59 Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Isa akajificha, naye akatoka Hekaluni. \c 9 \s1 Isa amponya mtu aliyezaliwa kipofu \p \v 1 Isa alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. \v 2 Wanafunzi wake wakamuuliza, “Mwalimu, ni nani aliyetenda dhambi; ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?” \p \v 3 Isa akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. \v 4 Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. \v 5 Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.” \p \v 6 Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule kipofu machoni. \v 7 Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu” (Siloamu maana yake ni Kutumwa). Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona. \p \v 8 Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, “Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?” \v 9 Wengine wakasema, “Ndiye.” \p Wengine wakasema, “Siye, bali anafanana naye.” \p Lakini yeye akawaambia, “Mimi ndiye.” \p \v 10 Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?” \p \v 11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Isa alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia, ‘Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu,’ ndipo nikanawa nami nikapata kuona!” \p \v 12 Wale wakamuuliza, “Yeye huyo mtu yuko wapi?” \p Akawajibu, “Sijui.” \s1 Mafarisayo wachunguza kuponywa kwa kipofu \p \v 13 Wakamleta yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali kwa Mafarisayo\f + \fr 9:13 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f*. \v 14 Basi siku hiyo Isa alitengeneza tope na kuyafungua macho ya huyo mtu ilikuwa Sabato. \v 15 Mafarisayo nao wakaanza kumuuliza yule mtu alivyopata kuona. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho yangu, nikanawa na sasa ninaona.” \p \v 16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” \p Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika. \p \v 17 Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho. Wasemaje kuhusu mtu huyo?” \p Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.” \p \v 18 Wale Wayahudi hawakuamini ya kuwa mtu huyo alikuwa kipofu akapata kuona, hadi walipowaita wazazi wake. \v 19 Wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu, ambaye mnasema alizaliwa kipofu? Imekuwaje basi sasa anaona?” \p \v 20 Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu na ya kuwa alizaliwa kipofu. \v 21 Lakini hatujui jinsi anavyoweza kuona sasa, wala hatujui ni nani aliyemfungua macho yake. Muulizeni; yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.” \v 22 Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi, kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Isa kuwa ndiye Al-Masihi\f + \fr 9:22 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* atafukuzwa kutoka sinagogi. \v 23 Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.” \p \v 24 Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.” \p \v 25 Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.” \p \v 26 Wakamuuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?” \p \v 27 Akawajibu, “Tayari nimekwisha kuwaambia, nanyi hamtaki kunisikiliza. Mbona mnataka kusikia tena? Je, ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?” \p \v 28 Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ndiwe mwanafunzi wake! Sisi ni wanafunzi wa Musa. \v 29 Tunajua kwamba Mungu alisema na Musa, lakini mtu huyu hatujui anakotoka.” \p \v 30 Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu! \v 31 Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii. \v 32 Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu. \v 33 Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya lolote.” \p \v 34 Wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje. \s1 Upofu wa kiroho \p \v 35 Isa aliposikia kuwa wamemfukuza atoke nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta, akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?” \p \v 36 Yule mtu akamjibu, “Yeye ni nani, Bwana\f + \fr 9:36 \fr*\ft Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.\ft*\f*? Niambie ili nipate kumwamini.” \p \v 37 Isa akamjibu, “Umekwisha kumwona; naye anayezungumza nawe, ndiye.” \p \v 38 Yule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu. \p \v 39 Isa akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona wawe vipofu.” \p \v 40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa karibu naye wakamsikia na kumwambia, “Je, kweli sisi ni vipofu?” \p \v 41 Isa akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, msingekuwa na hatia ya dhambi, lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi mna hatia. \c 10 \s1 Mchungaji mwema \p \v 1 “Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang’anyi. \v 2 Yeye anayeingia kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo. \v 3 Mlinzi humfungulia lango, na kondoo huisikia sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. \v 4 Baada ya kuwatoa wote nje, yeye hutangulia mbele yao na kondoo humfuata, kwa kuwa wanaijua sauti yake. \v 5 Lakini kondoo hawatamfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.” \v 6 Isa alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia. \p \v 7 Kwa hiyo Isa akasema nao tena, akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo. \v 8 Wote walionitangulia ni wezi na wanyang’anyi, nao kondoo hawakuwasikia. \v 9 Mimi ndimi lango. Yeyote anayeingia zizini kupitia kwangu ataokoka. Ataingia na kutoka, naye atapata malisho. \v 10 Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize. Mimi nimekuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele. \p \v 11 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. \v 12 Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Anapomwona mbwa-mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa-mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya. \v 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo. \p \v 14 “Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu, nao kondoo wangu wananijua. \v 15 Kama vile Baba\f + \fr 10:15 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, ndivyo nami ninautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. \v 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu; hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. \v 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. \v 18 Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu, na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.” \p \v 19 Waliposikia maneno haya, Wayahudi wakagawanyika. \v 20 Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.” \p \v 21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?” \s1 Isa akataliwa na Wayahudi \p \v 22 Ikafika Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu\f + \fr 10:22 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Hanukkah \fqa*\ft kwa Kiebrania\ft*\f* huko Yerusalemu. Ilikuwa majira ya baridi. \v 23 Naye Isa alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika Ukumbi wa Sulemani. \v 24 Wayahudi wakamkusanyikia, wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka hadi lini? Kama wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 10:24 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, tuambie waziwazi.” \p \v 25 Isa akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia. \v 26 Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. \v 27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata. \v 28 Nami ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. \v 29 Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote, na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. \v 30 Mimi na Baba yangu tu umoja.” \p \v 31 Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, \v 32 lakini Isa akawaambia, “Nimewaonesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni kwa ipi kati ya hiyo miujiza mnataka kunipiga mawe?” \p \v 33 Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Ingawa wewe ni mwanadamu, unajifanya kuwa Mungu.” \p \v 34 Isa akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Torati yenu kwamba, ‘Nimesema kuwa ninyi ni “miungu” ’? \v 35 Kama aliwaita ‘miungu’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka, \v 36 je, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu\f + \fr 10:36 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*’? \v 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini. \v 38 Lakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ni ndani yake.” \v 39 Ndipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao. \p \v 40 Isa akaenda tena ng’ambo ya Yordani hadi mahali Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. \v 41 Watu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yahya hakufanya muujiza wowote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” \v 42 Nao watu wengi wakamwamini Isa huko. \c 11 \ms1 Isa akamilisha huduma yake \mr (Yohana 11:1–13:30) \s1 Kifo cha Lazaro \p \v 1 Basi mtu mmoja, jina lake Lazaro, alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania, kijiji cha Mariamu na Martha dada yake. \v 2 (Huyu Mariamu, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye alimpaka Bwana Isa mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.) \v 3 Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Isa kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.” \p \v 4 Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti, bali ni wa kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.” \v 5 Isa aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro ndugu yao. \v 6 Hata hivyo, baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, alikawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi. \p \v 7 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Haya, turudi Yudea.” \p \v 8 Wanafunzi wake wakamwambia, “Mwalimu, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?” \p \v 9 Isa akawajibu, “Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wanaotembea mchana hawawezi kujikwaa, kwa maana wanaona kwa nuru ya ulimwengu huu. \v 10 Lakini wale wanaotembea usiku hujikwaa kwa sababu hawana nuru ndani yao.” \p \v 11 Baada ya kusema haya, Isa akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha.” \p \v 12 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala usingizi ataamka.” \v 13 Hata hivyo, Isa alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu. \p \v 14 Kwa hiyo Isa akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa. \v 15 Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwako huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.” \p \v 16 Tomaso (aliyeitwa Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.” \s1 Isa ndiye ufufuo na uzima \p \v 17 Isa alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne. \v 18 Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa yamkini maili mbili\f + \fr 11:18 \fr*\ft kama kilomita 3\ft*\f*, \v 19 na Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao. \v 20 Martha aliposikia kwamba Isa anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Mariamu alibaki nyumbani. \p \v 21 Martha akamwambia Isa, “Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa. \v 22 Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.” \p \v 23 Isa akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.” \p \v 24 Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.” \p \v 25 Isa akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; \v 26 na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?” \p \v 27 Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Al-Masihi\f + \fr 11:27 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.” \s1 Isa alia \p \v 28 Baada ya kusema haya, Martha alienda akamwita Mariamu dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.” \v 29 Mariamu aliposikia hivyo, akaondoka upesi, akaenda hadi alipokuwa Isa. \v 30 Isa alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha. \v 31 Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Mariamu nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani kwamba alikuwa anaenda kule kaburini kulilia huko. \p \v 32 Mariamu alipofika mahali pale Isa alipokuwa, alipiga magoti miguuni pake na kusema, “Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa.” \p \v 33 Isa alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Isa alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana. \v 34 Akauliza, “Mmemweka wapi?” \p Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.” \p \v 35 Isa akalia machozi. \p \v 36 Ndipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!” \p \v 37 Lakini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?” \s1 Isa amfufua Lazaro \p \v 38 Isa akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana kwa mara nyingine. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe liliwekwa kwenye ingilio lake. \v 39 Isa akasema, “Liondoeni jiwe.” \p Martha dada yake yule aliyekuwa amekufa akasema, “Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne.” \p \v 40 Isa akamwambia, “Sikukuambia kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” \p \v 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka kaburini. Isa akainua macho yake juu, akasema, “Baba\f + \fr 11:41 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. \v 42 Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya watu hawa waliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.” \p \v 43 Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!” \v 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. \p Isa akawaambia, “Mfungueni; mwacheni aende zake.” \s1 Njama ya kumuua Isa \r (Mathayo 26:1-5; Marko 14:1-2; Luka 22:1-2) \p \v 45 Hivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Mariamu walipoona yale Isa aliyoyatenda, wakamwamini. \v 46 Lakini baadhi yao wakaenda kwa Mafarisayo\f + \fr 11:46 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* na kuwaambia mambo Isa aliyoyafanya. \v 47 Kwa hiyo viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakaita mkutano wa Baraza la Wayahudi\f + \fr 11:47 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*. \p Wakaulizana, “Tufanyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. \v 48 Tukimwacha aendelee hivi, kila mtu atamwamini, nao Warumi watakuja na kupaharibu mahali petu patakatifu na taifa letu.” \p \v 49 Mmoja wao aliyeitwa Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka huo, akasema, “Ninyi hamjui kitu chochote! \v 50 Hamjui kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote liangamie?” \p \v 51 Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe, bali kama kuhani mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Isa angekufa kwa ajili ya taifa la Wayahudi; \v 52 wala si kwa ajili ya taifa hilo pekee, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. \v 53 Hivyo tangu siku hiyo wakawa wanafanya mipango ili wamuue Isa. \p \v 54 Kwa hiyo Isa akawa hatembei tena hadharani miongoni mwa Wayahudi, bali alijitenga akaenda sehemu iliyo karibu na jangwa kwenye kijiji kiitwacho Efraimu. Akakaa huko na wanafunzi wake. \p \v 55 Basi Pasaka ya Wayahudi ilipokuwa imekaribia, watu wengi walitoka vijijini wakaenda Yerusalemu ili wakajitakase kabla ya Pasaka. \v 56 Watu wakawa wanamtafuta Isa, nao waliposimama kwenye ua la Hekalu, waliulizana, “Je, mtu huyu hatakuja kamwe kwenye Sikukuu?” \v 57 Viongozi wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa yeyote atakayejua mahali Isa aliko, lazima atoe taarifa ili wapate kumkamata. \c 12 \s1 Mariamu ampaka Isa mafuta huko Bethania \r (Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9; Luka 7:35-38) \p \v 1 Siku sita kabla ya Pasaka, Isa alienda Bethania, makao ya Lazaro, aliyekuwa amemfufua kutoka kwa wafu. \v 2 Wakaandaa karamu kwa heshima ya Isa. Martha akawahudumia, wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Isa. \v 3 Kisha Mariamu akachukua chupa ya painti moja\f + \fr 12:3 \fr*\ft painti moja ni kama nusu lita\ft*\f* yenye manukato ya nardo\f + \fr 12:3 \fr*\ft aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri\ft*\f* safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato. \p \v 4 Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wanafunzi wa Isa, ambaye baadaye angemsaliti Isa, akasema, \v 5 “Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari mia tatu\f + \fr 12:5 \fr*\ft Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.\ft*\f*, na fedha hizo wakapewa maskini?” \v 6 Yuda hakusema hivi kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi; ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha, na akawa akiiba zile fedha. \p \v 7 Isa akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. \v 8 Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.” \s1 Njama ya kumuua Lazaro \p \v 9 Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Isa alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Isa, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Isa alikuwa amemfufua. \v 10 Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakapanga njama ya kumuua Lazaro pia, \v 11 kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake, Wayahudi wengi walikuwa wanamfuata Isa na kumwamini. \s1 Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe \r (Mathayo 21:1-11; Marko 1:1-11; Luka 19:28-40) \p \v 12 Siku iliyofuata umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu. \v 13 Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, \q1 “Hosana!”\f + \fr 12:13 \fr*\ft Kiebrania kusema \ft*\fqa Okoa\fqa*\ft ; basi likawa neno la shangwe.\ft*\f* \b \q1 “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” \b \q1 “Amebarikiwa mfalme wa Israeli!” \m \v 14 Isa akamkuta mwana-punda, akampanda, kama ilivyoandikwa, \q1 \v 15 “Usiogope, ewe Binti Sayuni; \q2 tazama, mfalme wako anakuja, \q2 amepanda mwana-punda!” \p \v 16 Wanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya. Lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye. \p \v 17 Wale waliokuwepo Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu waliendelea kushuhudia. \v 18 Na kwa sababu walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu, umati wa watu wakaenda kumlaki. \v 19 Hivyo Mafarisayo\f + \fr 12:19 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* walipoona hayo, wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!” \s1 Isa atabiri kifo chake \p \v 20 Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wameenda kuabudu wakati wa Sikukuu. \v 21 Hawa wakaenda kwa Filipo, aliyekuwa raia wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Isa.” \v 22 Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Isa. \p \v 23 Isa akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa. \v 24 Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa, huzaa mbegu nyingi. \v 25 Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. \v 26 Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu. \p \v 27 “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii’? Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu. \v 28 Baba, litukuze jina lako.” \p Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, ikasema, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.” \v 29 Umati ule wa watu waliokuwa mahali pale waliisikia ile sauti, nao wakasema hiyo ilikuwa sauti ya radi; wengine wakasema malaika ameongea naye. \p \v 30 Isa akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu. \v 31 Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. \v 32 Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.” \v 33 Isa aliyasema haya akionesha ni kifo gani atakachokufa. \p \v 34 Umati ule wa watu wakapaza sauti, wakasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba Al-Masihi\f + \fr 12:34 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* adumu milele; hivyo wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?” \p \v 35 Ndipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingali pamoja nanyi. Nendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakoenda. \v 36 Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Isa aliondoka, akajificha wasimwone. \s1 Wayahudi waendelea kutokuamini \p \v 37 Hata baada ya Isa kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini. \v 38 Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: \q1 “Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, \q2 na mkono wa Mwenyezi Mungu umefunuliwa kwa nani?” \p \v 39 Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine: \q1 \v 40 “Amewafanya vipofu, \q2 na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, \q1 ili wasiweze kuona kwa macho yao, \q2 wala kuelewa kwa mioyo yao, \q2 wasije wakageuka nami nikawaponya.” \m \v 41 Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Isa na kunena habari zake. \p \v 42 Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.\f + \fr 12:42 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* \v 43 Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zinazotoka kwa Mungu. \s1 Amwaminiye Isa hatabaki gizani \p \v 44 Isa akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali pia yeye aliyenituma. \v 45 Yeyote anionaye mimi amemwona yeye aliyenituma. \v 46 Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kila mtu aniaminiye asibaki gizani. \p \v 47 “Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. \v 48 Yuko anayehukumu yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho. \v 49 Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema. \v 50 Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.” \c 13 \s1 Isa awanawisha wanafunzi wake miguu \p \v 1 Sikukuu ya Pasaka ilikuwa imekaribia. Isa alijua kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba\f + \fr 13:1 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni; naam, aliwapenda hadi mwisho. \p \v 2 Isa alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia wazo la kumsaliti Isa ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni. \v 3 Isa, akijua kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake, na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, \v 4 aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. \v 5 Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni. \p \v 6 Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, je, wewe utaninawisha mimi miguu?” \p \v 7 Isa akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.” \p \v 8 Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” \p Isa akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.” \p \v 9 Ndipo Simoni Petro akajibu, “Usininawishe miguu peke yake, Bwana, bali pamoja na mikono na kichwa pia!” \p \v 10 Isa akamjibu, “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.” \v 11 Kwa kuwa yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema si kila mmoja aliyekuwa safi. \p \v 12 Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi yake, akarudi alikokuwa ameketi. Akawauliza, “Je, mmeelewa nililowafanyia? \v 13 Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana’; hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo. \v 14 Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. \v 15 Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi. \v 16 Amin, amin nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. \v 17 Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri kwenu mkiyatenda. \p \v 18 “Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni kutimiza andiko lisemalo, ‘Yeye aliyekula chakula changu ameinua kisigino chake dhidi yangu.’ \p \v 19 “Ninawaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye. \v 20 Amin, amin nawaambia, yeyote anayempokea yule niliyemtuma anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenituma mimi.” \s1 Isa anatabiri kusalitiwa kwake \r (Mathayo 26:20-25; Marko 14:17-21; Luka 22:21-23) \p \v 21 Baada ya kusema haya, Isa alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” \p \v 22 Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. \v 23 Mmoja wa wanafunzi wake, ambaye Isa alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Isa. \v 24 Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.” \p \v 25 Yule mwanafunzi akamwegemea Isa, akamuuliza, “Bwana, tuambie, ni nani?” \p \v 26 Isa akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.” Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni. \v 27 Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia. \p Isa akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda, litende haraka.” \v 28 Hakuna hata mmoja wa wale waliokuwa wameketi naye mezani aliyeelewa kwa nini Isa alimwambia hivyo. \v 29 Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Isa alikuwa anamwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini kitu. \v 30 Mara tu baada ya kupokea ule mkate, Yuda akatoka nje. Wakati huo ulikuwa ni usiku. \ms1 Mafundisho ya mwisho ya Bwana Isa \mr (Yohana 13:31–17:26) \s1 Isa atabiri kuwa Petro atamkana \r (Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Luka 22:31-34) \p \v 31 Baada ya Yuda kutoka nje, Isa akasema, “Sasa Mwana wa Adamu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. \v 32 Ikiwa Mungu ametukuzwa ndani ya Mwana, Mungu atamtukuza Mwana ndani yake mwenyewe, naye atamtukuza mara moja. \p \v 33 “Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi: Niendako, ninyi hamwezi kuja. \p \v 34 “Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. \v 35 Mkipendana ninyi kwa ninyi kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.” \p \v 36 Simoni Petro akamuuliza, “Bwana, unaenda wapi?” \p Isa akamjibu, “Ninakoenda huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.” \p \v 37 Petro akamuuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako.” \p \v 38 Isa akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kuutoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” \c 14 \s1 Isa awatia moyo wanafunzi wake \p \v 1 Isa akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu, mniamini pia. \v 2 Nyumbani mwa Baba\f + \fr 14:2 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningewaambia. Naenda kuwaandalia makao. \v 3 Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo nanyi mpate kuwepo. \v 4 Ninyi mnajua njia ya kufika ninakoenda.” \s1 Isa ndiye njia ya kwenda kwa Baba \p \v 5 Tomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakoenda, tutaijuaje njia?” \p \v 6 Isa akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu. \v 7 Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa mnamjua Baba yangu, tena mmemwona.” \p \v 8 Filipo akamwambia, “Bwana, tuoneshe Baba, na hiyo itatutosha.” \p \v 9 Isa akamjibu, “Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue? Mtu yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba. Sasa wawezaje kusema, ‘Tuoneshe Baba’? \v 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi. \v 11 Nisadiki mimi kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; la sivyo, niaminini kwa sababu ya zile kazi nizitendazo. \v 12 Amin, amin nawaambia, yeyote anayeniamini mimi, kazi ninazozifanya naye atazifanya. Naam, na atazifanya kazi kubwa kuliko hizi, kwa sababu mimi ninaenda kwa Baba. \v 13 Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. \v 14 Mkiniomba lolote kwa Jina langu, nitalifanya. \s1 Isa aahidi Roho wa Mungu \p \v 15 “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. \v 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. \v 17 Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi, naye anakaa ndani yenu. \v 18 Sitawaacha ninyi yatima; nitakuja kwenu. \v 19 Bado kitambo kidogo na ulimwengu hautaniona tena, ila ninyi mtaniona. Kwa kuwa mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. \v 20 Wakati huo mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, na ninyi mko ndani yangu, na mimi niko ndani yenu. \v 21 Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye. Naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” \p \v 22 Ndipo Yuda (siyo Iskariote) akamwambia, “Bwana, itakuwaje kwamba utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” \p \v 23 Isa akamjibu, “Mtu yeyote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake. \v 24 Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu, na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma. \p \v 25 “Nimewaambia mambo haya yote wakati bado niko pamoja nanyi. \v 26 Lakini huyo Msaidizi, yaani huyo Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia. \v 27 Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope. \p \v 28 “Mlisikia nikisema, ‘Ninaenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngenipenda, mngefurahi kwa kuwa naenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuliko mimi. \v 29 Nimewaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini. \v 30 Sitasema nanyi zaidi, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu anakuja, naye hana kitu kwangu, \v 31 lakini ulimwengu upate kujua kuwa ninampenda Baba, nami hufanya vile Baba alivyoniamuru. \p “Haya inukeni; twendeni zetu. \c 15 \s1 Isa mzabibu wa kweli \p \v 1 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. \v 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi linalozaa, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. \v 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi. \v 4 Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda. \p \v 5 “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote. \v 6 Mtu yeyote asipokaa ndani yangu, huyo hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. \v 7 Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa. \v 8 Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa kwa vile mnavyozaa matunda mengi, nanyi mtajidhihirisha kuwa wanafunzi wangu. \p \v 9 “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu. \v 10 Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. \v 11 Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu iwe kamili. \v 12 Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi. \v 13 Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. \v 14 Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. \v 15 Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya. Bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu. \v 16 Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi. \v 17 Amri yangu ndiyo hii: Mpendane. \s1 Ulimwengu wawachukia wanafunzi \p \v 18 “Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu. \v 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini mimi nimewachagua kutoka ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia. \v 20 Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia. \v 21 Watawatendea ninyi haya yote kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu hawamjui yeye aliyenituma. \v 22 Kama sikuja na kusema nao, hawangekuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa hawana udhuru kwa ajili ya dhambi zao. \v 23 Yeyote anayenichukia mimi, anamchukia pia na Baba yangu. \v 24 Kama sikuwa nimefanya miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine yeyote, hawangekuwa na hatia ya dhambi. Lakini sasa wameiona miujiza hii, na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. \v 25 Lakini hii ni kutimiza lile neno lililoandikwa kwenye Torati kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’ \s1 Kazi ya Roho Mtakatifu wa Mungu \p \v 26 “Lakini atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, yaani huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. \v 27 Ninyi nanyi itawapasa kushuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo. \c 16 \p \v 1 “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. \v 2 Watawatenga na masinagogi\f + \fr 16:2 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f*. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. \v 3 Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. \v 4 Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi. \p \v 5 “Sasa mimi ninaenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unaenda wapi?’ \v 6 Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. \v 7 Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; lakini nikienda nitamtuma kwenu. \v 8 Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. \v 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; \v 10 kwa habari ya haki, kwa sababu ninaenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena; \v 11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. \p \v 12 “Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. \v 13 Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonesha mambo yajayo. \v 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi. \v 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.” \s1 Huzuni itageuka kuwa furaha \p \v 16 Isa akaendelea kusema, “Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.” \p \v 17 Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninaenda kwa Baba’?” \v 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Kitambo kidogo’? Hatuelewi hilo analosema.” \p \v 19 Isa akatambua kuwa walitaka kumuuliza kuhusu hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? \v 20 Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. \v 21 Mwanamke anapokuwa na uchungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha yake ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. \v 22 Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. \v 23 Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. \v 24 Hadi sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili. \s1 Amani kwa wanafunzi \p \v 25 “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba. \v 26 Siku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu, \v 27 kwa maana Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. \v 28 Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni; sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.” \p \v 29 Ndipo wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza waziwazi, wala si kwa mafumbo. \v 30 Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.” \p \v 31 Isa akawajibu, “Je, sasa mnaamini? \v 32 Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani mwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami. \p \v 33 “Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.” \c 17 \s1 Isa ajiombea mwenyewe \p \v 1 Baada ya Isa kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema: \pm “Baba\f + \fr 17:1 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, saa imewadia. Mtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe. \v 2 Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. \v 3 Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma. \v 4 Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. \v 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujaumbwa. \s1 Isa awaombea wanafunzi wake \pm \v 6 “Nimelidhihirisha jina lako kwa wale ulionipa kutoka ulimwengu. Walikuwa wako, nawe ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako. \v 7 Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako, \v 8 kwa kuwa maneno yale uliyonipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma. \v 9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako. \v 10 Wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao. \v 11 Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. \v 12 Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia. \pm \v 13 “Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao. \v 14 Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia, kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu. \v 15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. \v 16 Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu. \v 17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndilo kweli. \v 18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. \v 19 Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli. \s1 Isa awaombea wote watakaomwamini \pm \v 20 “Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao, \v 21 ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako. Wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma mimi. \v 22 Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. \v 23 Mimi ndani yao na wewe ndani yangu: ili wawe wamekamilika katika umoja, na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi. \pm \v 24 “Baba, shauku yangu ni kwamba wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu wangu, yaani utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. \pm \v 25 “Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma. \v 26 Nimefanya jina lako lijulikane kwao, nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao, na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.” \c 18 \ms1 Kufa na kufufuka kwa Isa \mr (Yohana 18:1–20:10) \s1 Isa akamatwa \r (Mathayo 26:47-56; Marko 14:43-50; Luka 22:47-53) \p \v 1 Isa alipomaliza kuomba, akaondoka na wanafunzi wake, wakavuka Bonde la Kidroni. Upande wa pili palikuwa na bustani; yeye na wanafunzi wake wakaingia humo. \p \v 2 Basi Yuda, aliyemsaliti, alipafahamu mahali hapo, kwani Isa alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. \v 3 Hivyo Yuda akaja kwenye bustani akiongoza kikosi cha askari Warumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo\f + \fr 18:3 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f*. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha. \p \v 4 Isa, akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao, akawauliza, “Mnamtafuta nani?” \p \v 5 Wao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.” \p Isa akawajibu, “Mimi ndiye.” (Yuda, aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja nao.) \v 6 Isa alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini! \p \v 7 Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” \p Nao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.” \p \v 8 Isa akawaambia, “Nimekwisha kuwaambia kuwa mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa watu waende zao.” \v 9 Hii ilikuwa ili litimie lile neno alilosema, “Sikumpoteza hata mmoja miongoni mwa wale ulionipa.” \p \v 10 Simoni Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kuume mtumishi wa kuhani mkuu. (Mtumishi huyo aliitwa Malko.) \p \v 11 Isa akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Je, hainipasi kukinywea kikombe alichonipa Baba\f + \fr 18:11 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*?” \s1 Isa mbele ya kuhani mkuu \p \v 12 Hivyo wale askari, wakiwa na jemadari wao na maafisa wa Wayahudi, wakamkamata Isa na kumfunga. \v 13 Kwanza wakampeleka kwa Anasi, mkwewe Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule. \v 14 Kayafa ndiye alikuwa amewashauri viongozi wa Wayahudi kwamba imempasa mtu mmoja kufa kwa ajili ya watu. \s1 Petro amkana Isa \r (Mathayo 26:69-70; Marko 14:55-64; Luka 22:66-71) \p \v 15 Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walikuwa wakimfuata Isa. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia uani kwa kuhani mkuu pamoja na Isa. \v 16 Lakini Petro alisimama nje karibu na lango. Ndipo yule mwanafunzi mwingine, aliyejulikana na kuhani mkuu, akazungumza na msichana aliyekuwa analinda lango, akamruhusu Petro aingie ndani. \p \v 17 Yule msichana akamuuliza Petro, “Je, wewe pia si mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” \p Petro akajibu, “Sio mimi.” \p \v 18 Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa makaa kwa sababu palikuwa na baridi, Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto. \s1 Kuhani mkuu amhoji Isa \p \v 19 Wakati huo kuhani mkuu akawa anamuuliza Isa kuhusu wanafunzi wake na mafundisho yake. \p \v 20 Isa akamjibu, “Nimekuwa nikizungumza waziwazi mbele ya watu wote. Siku zote nimefundisha katika masinagogi\f + \fr 18:20 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* na Hekaluni, mahali Wayahudi wote hukusanyika. Sikusema jambo lolote kwa siri. \v 21 Mbona unaniuliza mimi maswali? Waulize wale waliosikia yale niliyowaambia. Wanajua niliyoyasema.” \p \v 22 Alipomaliza kusema hayo, mmoja wa askari aliyekuwa amesimama karibu naye akampiga Isa kofi usoni. Kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo unavyomjibu kuhani mkuu?” \p \v 23 Isa akamjibu akasema, “Kama nimesema jambo baya, shuhudia huo ubaya niliousema. Lakini kama nimesema yaliyo kweli, mbona umenipiga?” \v 24 Ndipo Anasi akampeleka Isa kwa kuhani mkuu Kayafa, akiwa bado amefungwa. \s1 Petro amkana Isa tena \r (Mathayo 26:71-75; Marko 14:69-72; Luka 22:58-62) \p \v 25 Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya watu waliokuwepo wakamuuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?” \p Petro akakana, akasema, “Sio mimi.” \p \v 26 Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alikuwa amemkata sikio, akamuuliza, “Je, mimi sikukuona kule bustanini ukiwa na Isa?” \v 27 Kwa mara nyingine tena Petro akakana, naye jogoo akawika wakati huo huo. \s1 Isa mbele ya Pilato \r (Mathayo 27:1-2, 11-14; Marko 15:1-5; Luka 23:1-5) \p \v 28 Ndipo viongozi wa Wayahudi wakamchukua Isa kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala Mrumi\f + \fr 18:28 \fr*\ft jumba hilo liliitwa \ft*\fqa Praitorio\fqa*\f*. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri. Ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani ya jumba kwa sababu walitaka kushiriki katika Pasaka\f + \fr 18:28 \fr*\ft Kwa sheria za Kiyahudi, wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi, na hawangeruhusiwa kushiriki katika Pasaka.\ft*\f*. \v 29 Hivyo Pilato akatoka nje walikokuwa, akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?” \p \v 30 Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu, tusingemleta kwako.” \p \v 31 Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.” \p Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu yeyote.” \v 32 Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Isa kuhusu kifo atakachokufa yapate kutimia. \p \v 33 Kwa hiyo Pilato akaingia ndani ya jumba la kifalme, akamwita Isa, akamuuliza, “Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?” \p \v 34 Isa akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe, au uliambiwa na watu kunihusu?” \p \v 35 Pilato akamjibu, “Je, mimi ni Myahudi? Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?” \p \v 36 Isa akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa viongozi wa Wayahudi. Lakini kama ilivyo, ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.” \p \v 37 Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” \p Isa akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni: ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.” \p \v 38 Pilato akamuuliza Isa, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena, akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Isa, “Sioni msingi wowote wa kumshtaki mtu huyu. \v 39 Lakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘mfalme wa Wayahudi’?” \p \v 40 Wao wakapiga kelele, wakajibu, “Si huyu mtu, bali tufungulie Baraba!” Yule Baraba alikuwa mnyang’anyi. \c 19 \s1 Isa ahukumiwa kusulubiwa \r (Mathayo 27:15-31; Marko 15:6-20; Luka 23:13-25) \p \v 1 Ndipo Pilato akamtoa Isa akaamuru apigwe mijeledi. \v 2 Askari wakasokota taji la miiba, wakamvika Isa kichwani. Wakamvalisha joho la zambarau. \v 3 Wakawa wanapanda pale alipo tena na tena, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” Huku wakimpiga makofi usoni. \p \v 4 Pilato akatoka tena nje, akawaambia wale waliokusanyika, “Tazameni, namkabidhi Isa kwenu kuwajulisha kwamba mimi sioni msingi wowote wa kumshtaki.” \v 5 Kwa hiyo Isa akatoka nje akiwa amevaa lile taji la miiba na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, “Tazameni, mtu ndiye huyu!” \p \v 6 Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!” \p Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulubishe. Lakini mimi sioni msingi wowote wa kumshtaki.” \p \v 7 Viongozi wa Wayahudi wakamjibu, “Sisi tunayo sheria, na kutokana na sheria hiyo, hana budi kufa kwa sababu yeye alijiita Mwana wa Mungu\f + \fr 19:7 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*.” \p \v 8 Pilato aliposikia haya, akaogopa zaidi. \v 9 Akaingia tena ndani ya jumba la kifalme, akamuuliza Isa, “Wewe umetoka wapi?” Lakini Isa hakumjibu. \v 10 Pilato akamwambia, “Wewe unakataa kuongea na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachia huru au kukusulubisha?” \p \v 11 Ndipo Isa akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.” \p \v 12 Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Isa, lakini viongozi wa Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, “Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu yeyote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari.” \p \v 13 Pilato aliposikia maneno haya, akamtoa Isa nje tena. Akaketi kwenye kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe (kwa Kiebrania ni Gabatha). \v 14 Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi. \p Pilato akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa mfalme wenu!” \p \v 15 Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” \p Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” \p Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, “Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.” \p \v 16 Ndipo Pilato akamkabidhi Isa kwao ili wamsulubishe. \s1 Isa asulubishwa \r (Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Luka 23:26-43) \p Kwa hiyo askari wakamchukua Isa. \v 17 Isa, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha). \v 18 Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubisha watu wawili, mmoja kila upande wake, naye Isa katikati. \p \v 19 Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Isa; likasema: \pc \sc Isa Al-Nasiri\sc* \pc \sc Mfalme wa Wayahudi.\sc* \m \v 20 Kwa kuwa mahali hapo Isa aliposulubiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini. \v 21 Viongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga, wakamwambia Pilato, “Usiandike ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba mtu huyu alisema yeye ni mfalme wa Wayahudi.” \p \v 22 Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!” \s1 Mavazi ya Isa yagawanywa \p \v 23 Askari walipokwisha kumsulubisha Isa, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono, bali limefumwa tangu juu hadi chini. \p \v 24 Wakaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani atalichukua.” \p Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema, \q1 “Wanagawana nguo zangu, \q2 na vazi langu wanalipigia kura.” \m Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari. \p \v 25 Karibu na msalaba wa Isa walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Mariamu mke wa Klopa, na Mariamu Magdalene. \v 26 Isa alipomwona mama yake mahali pale, na yule mwanafunzi aliyempenda akiwa amesimama karibu, Isa akamwambia mama yake, “Mama, huyu hapa ndiye mwanao.” \v 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Nawe huyu hapa ndiye mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Isa nyumbani mwake. \s1 Kifo cha Isa \r (Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49) \p \v 28 Baada ya haya, akijua kuwa mambo yote yamemalizika, na ili kutimiza Maandiko, Isa akasema, “Naona kiu.” \v 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachovya sifongo kwenye hiyo siki, wakaiweka kwenye ufito wa mti wa hisopo, wakampelekea mdomoni. \v 30 Baada ya kuionja hiyo siki, Isa akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake. \s1 Isa achomwa mkuki ubavuni \p \v 31 Ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, na siku iliyofuata ingekuwa Sabato maalum. Kwa kuwa viongozi wa Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe, na miili iondolewe kwenye misalaba. \v 32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa pamoja na Isa, na ya yule mwingine pia. \v 33 Lakini walipomkaribia Isa, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake. \v 34 Badala yake mmoja wa wale askari akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji. \v 35 Mtu aliyeona mambo hayo ndiye alitoa ushuhuda, nao ushuhuda wake ni kweli. Anajua kuwa anasema kweli, naye anashuhudia ili pia nanyi mpate kuamini. \v 36 Kwa maana mambo haya yalitukia ili andiko litimie, lisemalo, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” \v 37 Tena andiko lingine lasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma.” \s1 Maziko ya Isa \r (Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Luka 23:50-56) \p \v 38 Baada ya mambo haya, Yusufu wa Arimathaya, aliyekuwa mfuasi wa Isa, ingawa kwa siri kwa sababu ya kuwaogopa viongozi wa Wayahudi, alimwomba Pilato ruhusa ili kuuchukua mwili wa Isa. Pilato alimruhusu, hivyo akaja, akauchukua. \v 39 Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Isa usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini. \v 40 Wakauchukua mwili wa Isa, wakaufunga katika sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi. \v 41 Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulubiwa, na pale ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo halikuwa limezikiwa mtu bado. \v 42 Kwa hiyo, kwa kuwa ilikuwa siku ya Wayahudi ya Maandalio, nalo kaburi hilo lilikuwa karibu, wakamzika Isa humo. \c 20 \s1 Isa afufuka \r (Mathayo 28:1-8; Marko 16:1-8; Luka 24:1-12) \p \v 1 Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa bado giza, Mariamu Magdalene alienda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio. \v 2 Hivyo akakimbia kwa Simoni Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine ambaye Isa alimpenda, na kusema, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na hatujui walikomweka!” \p \v 3 Petro na yule mwanafunzi mwingine wakaondoka mara moja kuelekea kaburini. \v 4 Wote wawili walikuwa wanakimbia, lakini yule mwanafunzi mwingine akakimbia mbio kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini. \v 5 Akainama na kuchungulia mle kaburini, akaona vile vitambaa vya kitani, lakini hakuingia. \v 6 Ndipo Simoni Petro akaja akimfuata nyuma, akaingia ndani ya kaburi. Naye akaona vile vitambaa vya ile sanda vikiwa pale chini, \v 7 na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Isa. Kitambaa hicho kilikuwa kimekunjwa peke yake, mbali na vile vitambaa vya kitani vya ile sanda. \v 8 Kisha yule mwanafunzi aliyetangulia kufika kaburini akaingia ndani, akaona, na akaamini. \v 9 (Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajaelewa kutoka Maandiko kwamba ilikuwa lazima Isa afufuke kutoka kwa wafu.) \p \v 10 Kisha hao wanafunzi wakaondoka, wakarudi nyumbani mwao. \ms1 Isa aonekana baada ya kufufuka \mr (Yohana 20:11–21:25) \s1 Isa amtokea Mariamu Magdalene \r (Mathayo 28:9-10; Marko 16:9-11) \p \v 11 Lakini Mariamu Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama kuchungulia mle kaburini, \v 12 naye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Isa ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni. \p \v 13 Wakamuuliza Mariamu, “Mwanamke, mbona unalia?” \p Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu, na sijui walikomweka.” \v 14 Baada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Isa amesimama, lakini hakumtambua. \p \v 15 Isa akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?” \p Mariamu, akidhani alikuwa anaongea na mtunza bustani, akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nioneshe ulikomweka, nami nitamchukua.” \p \v 16 Isa akamwita, “Mariamu!” \p Ndipo Mariamu akamgeukia Isa na kusema naye kwa Kiebrania, “Raboni!” (maana yake “Mwalimu”). \p \v 17 Isa akamwambia, “Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba\f + \fr 20:17 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ‘Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ” \p \v 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalene akaenda kuwatangazia wanafunzi wa Isa, akisema, “Nimemwona Bwana!” Naye akawaambia kwamba Isa alikuwa amemweleza mambo hayo yote. \s1 Isa awatokea wanafunzi wake \r (Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Luka 24:36-49) \p \v 19 Ilipokuwa jioni ya siku hiyo hiyo ya kwanza ya juma, wanafunzi wake walikuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Naye Isa akawatokea, akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!” \v 20 Baada ya kusema haya, akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi wake wakafurahi sana walipomwona Bwana Isa. \p \v 21 Isa akawaambia tena, “Amani iwe nanyi! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma ninyi.” \v 22 Alipokwisha kusema haya, akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu wa Mungu. \v 23 Mkimwondolea mtu yeyote dhambi zake, zitaondolewa; na yeyote msiyemwondolea dhambi zake, hazitaondolewa.” \s1 Isa amtokea Tomaso \p \v 24 Lakini Tomaso (aliyeitwa Didimasi\f + \fr 20:24 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Pacha\fqa*\f*), mmoja wa wale kumi na wawili, hakuwa pamoja nao Isa alipokuja. \v 25 Hivyo wale wanafunzi wengine wakamwambia, “Tumemwona Bwana Isa.” \p Lakini yeye akawaambia, “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari, na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.” \p \v 26 Baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwa tena pamoja ndani ya nyumba, naye Tomaso alikuwa pamoja nao. Ndipo Isa akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi.” \v 27 Kisha akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu.” \p \v 28 Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!” \p \v 29 Isa akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.” \s1 Kusudi la kitabu hiki \p \v 30 Isa alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. \v 31 Lakini hii imeandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi\f + \fr 20:31 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake. \c 21 \s1 Isa awatokea wanafunzi saba \p \v 1 Baada ya haya Isa akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia\f + \fr 21:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Galilaya\fqa*\f*. Yeye alijionesha kwao hivi: \v 2 Simoni Petro, Tomaso (aitwaye Didimasi\f + \fr 21:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Pacha\fqa*\f*), Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo, na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. \v 3 Simoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutaenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote. \p \v 4 Mara baada ya kupambazuka, Isa akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Isa. \p \v 5 Isa akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wowote?” \p Wakamjibu, “La.” \p \v 6 Akawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu, na tazama, wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua. \p \v 7 Basi yule mwanafunzi aliyependwa na Isa akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana Isa!” Simoni Petro aliposikia kwamba ni Bwana Isa, akajifunga nguo yake (kwa kuwa alikuwa ameitoa), naye akajitosa baharini. \v 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa mia mbili\f + \fr 21:8 \fr*\ft Dhiraa 200 ni kama mita 90.\ft*\f*. \v 9 Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. \p \v 10 Isa akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.” \p \v 11 Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu ufuoni. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na watatu (153). Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. \v 12 Isa akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanafunzi aliyethubutu kumuuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa ni Bwana Isa. \v 13 Isa akaja, akachukua ule mkate, akawapa, na vivyo hivyo akawagawia wale samaki. \v 14 Hii ilikuwa mara ya tatu Isa kuwatokea wanafunzi wake baada yake kufufuliwa kutoka kwa wafu. \s1 Isa amrejesha Petro \p \v 15 Walipokwisha kula, Isa akamuuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” \p Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” \p Isa akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.” \p \v 16 Isa akamuuliza tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” \p Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” \p Isa akamwambia, “Chunga kondoo wangu.” \p \v 17 Kwa mara ya tatu Isa akamuuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” \p Petro akahuzunika sana kwa kuwa Isa alimuuliza mara ya tatu, “Unanipenda?” Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.” \p Isa akamwambia, “Lisha kondoo wangu. \v 18 Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka. Lakini utakapokuwa mzee, utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.” \v 19 Isa alisema haya ili kuashiria aina ya kifo ambacho Petro angemtukuza nacho Mungu. Kisha Isa akamwambia Petro, “Nifuate!” \p \v 20 Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Isa akiwafuata. (Huyu ndiye yule mwanafunzi aliyeegama kifuani mwa Isa walipokula naye chakula cha mwisho na kuuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”) \v 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamuuliza Isa, “Bwana, na huyu je?” \p \v 22 Isa akamjibu, “Ikiwa nataka aishi hadi nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!” \v 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Isa, uvumi ukaenea miongoni mwa ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Isa hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi hadi nitakaporudi, inakuhusu nini?” \p \v 24 Huyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya, na ndiye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. \p \v 25 Lakini kuna mambo mengine mengi ambayo Isa alifanya. Kama yote yangeandikwa, nadhani hata ulimwengu wote haungekuwa na nafasi ya kutosha kuweka vitabu ambavyo vingeandikwa.