\id JER - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Yeremia \toc1 Yeremia \toc2 Yeremia \toc3 Yer \mt1 Yeremia \c 1 \p \v 1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini. \v 2 Neno la Mwenyezi Mungu lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, \v 3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, hadi mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni. \b \s1 Wito wa Yeremia \p \v 4 Neno la Mwenyezi Mungu lilinijia, kusema, \q1 \v 5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua; \q2 kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum; \q2 nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.” \p \v 6 Nami nikasema, “Aa, Bwana Mungu Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.” \p \v 7 Lakini Mwenyezi Mungu akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. \v 8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema Mwenyezi Mungu. \p \v 9 Kisha Mwenyezi Mungu akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. \v 10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung’oa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.” \p \v 11 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?” \p Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.” \p \v 12 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.” \p \v 13 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena, “Unaona nini?” \p Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.” \p \v 14 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote wanaoishi katika nchi. \v 15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya utawala \q2 katika maingilio ya malango ya Yerusalemu, \q1 watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka, \q2 na dhidi ya miji yote ya Yuda. \q1 \v 16 Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu \q2 kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi, \q1 kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine \q2 na kuabudu kazi za mikono yao. \p \v 17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao. \v 18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo. \v 19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema Mwenyezi Mungu. \c 2 \s1 Israeli amwacha Mwenyezi Mungu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu lilinijia kusema, \v 2 “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: \b \p “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, \q2 jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi \q1 na kunifuata katika jangwa lile lote, \q2 katika nchi isiyopandwa mbegu. \q1 \v 3 Israeli alikuwa mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu, \q2 kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; \q1 wote waliomwangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, \q2 nayo maafa yaliwakumba,’ ” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 4 Sikia neno la Mwenyezi Mungu, ee nyumba ya Yakobo, \q2 nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli. \p \v 5 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q1 “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, \q2 hata wakatangatanga mbali nami hivyo? \q1 Walifuata sanamu batili, \q2 nao wenyewe wakawa batili. \q1 \v 6 Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu, \q2 aliyetupandisha kutoka Misri \q1 na kutuongoza kupitia nyika kame, \q2 kupitia nchi ya majangwa na mabonde, \q1 nchi ya ukame na giza, \q2 nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake \q2 wala hakuna mtu aishiye humo?’ \q1 \v 7 Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu \q2 ili mpate kula matunda yake \q2 na utajiri wa mazao yake. \q1 Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, \q2 na kuufanya urithi wangu chukizo. \q1 \v 8 Makuhani hawakuuliza, \q2 ‘Yuko wapi Mwenyezi Mungu?’ \q1 Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; \q2 viongozi waliasi dhidi yangu. \q1 Manabii walitabiri kwa jina la Baali, \q2 wakifuata sanamu batili. \b \q1 \v 9 “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. \q1 \v 10 Vuka, nenda ng’ambo hadi pwani ya Kitimu\f + \fr 2:10 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Kipro\fqa*\ft , kisiwa katika Bahari ya Mediterania\ft*\f* nawe uangalie, \q2 tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, \q2 uone kama kumeshawahi kuwa kitu kama hiki. \q1 \v 11 Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? \q2 (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) \q1 Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao \q2 kwa sanamu batili. \q1 \v 12 Shangaeni katika hili, ee mbingu, \q2 nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 13 “Watu wangu wametenda dhambi mbili: \q2 Wameniacha mimi, \q2 niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, \q1 nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, \q2 visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji. \q1 \v 14 Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa? \q2 Kwa nini basi amekuwa mateka? \q1 \v 15 Simba wamenguruma; \q2 wamemngurumia. \q1 Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; \q2 miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu. \q1 \v 16 Pia watu wa Memfisi\f + \fr 2:16 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Nofu\fqa*\f* na Tapanesi \q2 wamekupiga fuvu la kichwa. \q1 \v 17 Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe \q2 kwa kumwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wako \q2 alipowaongoza njiani? \q1 \v 18 Sasa kwa nini uende Misri \q2 kunywa maji ya Shihori\f + \fr 2:18 \fr*\ft kijito kinachoelekeza maji katika Mto Naili\ft*\f*? \q1 Nawe kwa nini kwenda Ashuru \q2 kunywa maji ya Mto\f + \fr 2:18 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f*? \q1 \v 19 Uovu wako utakuadhibu; \q2 kurudi nyuma kwako kutakukemea. \q1 Basi kumbuka, utambue \q2 jinsi lilivyo jambo ovu na chungu kwako \q1 unapomwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wako, \q2 na kutokuwa na hofu yangu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \b \q1 \v 20 “Zamani nilivunja nira yako \q2 na kukatilia mbali vifungo vyako; \q2 ukasema, ‘Sitakutumikia!’ \q1 Hakika, kwenye kila kilima kirefu \q2 na chini ya kila mti uliotanda matawi yake \q2 ulijilaza kama kahaba. \q1 \v 21 Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana, \q2 mkamilifu na wa mbegu nzuri. \q1 Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami, \q2 ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu? \q1 \v 22 Hata ujisafishe kwa magadi \q2 na kutumia sabuni nyingi, \q2 bado doa la hatia yako liko mbele zangu,” \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \q1 \v 23 “Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi, \q2 sijawafuata Mabaali’? \q1 Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni; \q2 fikiri uliyoyafanya. \q1 Wewe ni ngamia jike mwenye mbio \q2 ukikimbia hapa na pale, \q1 \v 24 punda-mwitu aliyezoea jangwa, \q2 anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: \q1 wakati wake wa kuhitaji mbegu \q2 ni nani awezaye kumzuia? \q1 Madume yoyote yanayomfuatilia \q2 hayana haja ya kujichosha; \q2 wakati wa kupandwa kwake yatampata tu. \q1 \v 25 Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu, \q2 na koo lako liwe limekauka. \q1 Lakini ulisema, ‘Haina maana! \q2 Ninaipenda miungu ya kigeni, \q2 nami lazima niifuatie.’ \b \q1 \v 26 “Kama vile mwizi anavyoaibika akikamatwa, \q2 hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa: \q1 wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao, \q2 makuhani wao na manabii wao. \q1 \v 27 Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’ \q2 nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’ \q1 Wamenipa visogo vyao \q2 wala hawakunigeuzia nyuso zao; \q1 lakini wakiwa katika taabu, wanasema, \q2 ‘Njoo utuokoe!’ \q1 \v 28 Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? \q2 Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa \q2 wakati mko katika taabu! \q1 Kwa maana mna miungu mingi \q2 kama mlivyo na miji, ee Yuda. \b \q1 \v 29 “Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu? \q2 Ninyi nyote mmeniasi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 30 “Nimeadhibu watu wako bure tu, \q2 hawakujirekebisha. \q1 Upanga wako umewala manabii wako \q2 kama simba mwenye njaa. \p \v 31 “Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Mwenyezi Mungu: \q1 “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli \q2 au nchi ya giza nene? \q1 Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, \q2 hatutarudi kwako tena’? \q1 \v 32 Je, mwanamwali husahau vito vyake, \q2 au bibi arusi mapambo yake ya arusi? \q1 Lakini watu wangu wamenisahau mimi, \q2 tena kwa siku zisizo na hesabu. \q1 \v 33 Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi! \q2 Hata wale wanawake wabaya kuliko wote \q2 wanaweza kujifunza kutokana na njia zako. \q1 \v 34 Katika nguo zako watu huona \q2 damu ya uhai ya maskini wasio na hatia, \q2 ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba. \q1 Lakini katika haya yote \q2 \v 35 unasema, ‘Sina hatia; \q2 Mungu hajanikasirikia.’ \q1 Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema, \q2 ‘Mimi sijatenda dhambi.’ \q1 \v 36 Kwa nini unatangatanga sana, \q2 ukibadili njia zako? \q1 Utakatishwa tamaa na Misri \q2 kama ulivyokatishwa na Ashuru. \q1 \v 37 Pia utaondoka mahali hapo \q2 ukiwa umeweka mikono kichwani, \q1 kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewakataa wale unaowatumainia; \q2 hutasaidiwa nao. \c 3 \s1 Israeli asiye mwaminifu \q1 \v 1 “Kama mtu akimpa talaka mkewe, \q2 naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine, \q1 je, huyo mume aweza kumrudia tena? \q2 Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa? \q1 Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi: \q2 Je, sasa utanirudia tena?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 2 “Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone. \q2 Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe? \q1 Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi, \q2 ukakaa kama mtu anayehamahama jangwani. \q1 Umeinajisi nchi \q2 kwa ukahaba wako na uovu wako. \q1 \v 3 Kwa hiyo mvua imezuiliwa, \q2 nazo mvua za vuli hazikunyesha. \q1 Hata hivyo, una uso usio na haya kama wa kahaba; \q2 unakataa kutahayari kwa aibu. \q1 \v 4 Je, wewe hujaniita hivi punde tu: \q2 ‘Baba yangu, rafiki yangu tangu ujana wangu, \q1 \v 5 je, utakasirika siku zote? \q2 Je, ghadhabu yako itaendelea milele?’ \q1 Hivi ndivyo unavyozungumza, \q2 lakini unafanya maovu yote uwezayo.” \s1 Israeli asiye mwaminifu \p \v 6 Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Mwenyezi Mungu aliniambia, “Je, umeona yale Israeli asiye mwaminifu ameyatenda? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda, na amefanya uzinzi huko. \v 7 Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya haya yote angenirudia; lakini hakurudi, na dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili. \v 8 Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa sababu ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi. \v 9 Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti. \v 10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asema Mwenyezi Mungu. \p \v 11 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu. \v 12 Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini: \q1 “ ‘Rudi, Israeli usiye mwaminifu,’ \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q2 ‘sitakutazama tena kwa uso uliokunjamana, \q1 kwa kuwa mimi ni mwenye huruma,’ \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q2 ‘Sitashika hasira yangu milele. \q1 \v 13 Ungama dhambi zako tu: \q2 kwamba umemwasi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, \q1 umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni \q2 chini ya kila mti unaotanda, \q2 nawe hukunitii mimi,’ ” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 14 “Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka mji, na wawili kutoka ukoo, nami nitawaleta Sayuni. \v 15 Kisha nitawapeni wachungaji wanaoupendeza moyo wangu, ambao watawaongoza kwa maarifa na ufahamu. \v 16 Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu,’ ” asema Mwenyezi Mungu. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine. \v 17 Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina la Mwenyezi Mungu. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu. \v 18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi. \p \v 19 “Mimi mwenyewe nilisema, \q1 “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana \q2 na kuwapa nchi nzuri, \q2 urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’ \q1 Nilidhani mngeniita ‘Baba,’ \q2 na msingegeuka, mkaacha kunifuata. \q1 \v 20 Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe, \q2 vivyo hivyo mmekosa uaminifu kwangu, \q2 ee nyumba ya Israeli,” asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 21 Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame, \q2 kulia na kuomboleza kwa watu wa Israeli, \q1 kwa sababu wamepotoka katika njia zao \q2 na wamemsahau Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \b \q1 \v 22 “Rudini, enyi watu msio waaminifu, \q2 nami nitawaponya ukengeufu wenu.” \b \q1 “Naam, tutakuja kwako, \q2 kwa maana wewe ni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \q1 \v 23 Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima \q2 na milimani ni udanganyifu; \q1 hakika katika Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 uko wokovu wa Israeli. \q1 \v 24 Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala \q2 matunda ya kazi za baba zetu: \q1 makundi yao ya kondoo na ng’ombe, \q2 wana wao wa kiume na wa kike. \q1 \v 25 Sisi na tulale chini katika aibu yetu, \q2 na fedheha yetu itufunike. \q1 Tumetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 sisi na mababa zetu; \q1 tangu ujana wetu hadi leo \q2 hatukumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.” \b \c 4 \q1 \v 1 “Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli, \q2 nirudie mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yangu \q2 na usiendelee kutangatanga, \q1 \v 2 ikiwa utaapa katika kweli, kwa haki na kwa unyofu, \q2 ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo,’ \q1 ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye, \q2 na ndani yake watajitukuza.” \p \v 3 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu: \q1 “Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu, \q2 wala msipande katikati ya miiba. \q1 \v 4 Jitahirini katika Mwenyezi Mungu, \q2 tahirini mioyo yenu, \q1 enyi wanaume wa Yuda \q2 na watu wa Yerusalemu, \q1 la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvu \q2 na kuwaka kama moto \q1 kwa sababu ya uovu mliotenda, \q2 ikiwaka pasipo wa kuizima. \s1 Maafa kutoka kaskazini \q1 \v 5 “Tangaza katika Yuda \q2 na upige mbiu katika Yerusalemu, useme: \q2 ‘Piga tarumbeta katika nchi yote!’ \q1 Piga kelele na kusema: \q2 ‘Kusanyikeni pamoja! \q2 Tukimbilie katika miji yenye ngome!’ \q1 \v 6 Inueni ishara ili kwenda Sayuni! \q2 Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa! \q1 Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini, \q2 maangamizi ya kutisha.” \b \q1 \v 7 Simba ametoka nje ya pango lake, \q2 mwangamizi wa mataifa amejipanga. \q1 Ametoka mahali pake \q2 ili aangamize nchi yenu. \q1 Miji yenu itakuwa magofu \q2 pasipo mtu wa kuishi humo. \q1 \v 8 Hivyo vaeni magunia, \q2 ombolezeni na kulia kwa huzuni, \q1 kwa kuwa hasira kali ya Mwenyezi Mungu \q2 haijaondolewa kwetu. \b \q1 \v 9 “Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu \q2 “mfalme na maafisa watakata tamaa, \q1 makuhani watafadhaika, \q2 na manabii watashangazwa mno.” \p \v 10 Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mungu Mwenyezi, hakika umewadanganya watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kooni!” \p \v 11 Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame jangwani unavuma kuelekea kwa watu wangu, lakini sio upepo wa kupepeta na kutakasa; \v 12 upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.” \q1 \v 13 Tazama! Anakuja kama mawingu, \q2 magari yake ya vita yanakuja kama upepo wa kisulisuli, \q1 farasi wake wana mbio kuliko tai. \q2 Ole wetu! Tunaangamia! \q1 \v 14 Ee Yerusalemu, usafishe uovu \q2 kutoka moyoni mwako, uokolewe. \q2 Utaendelea kuficha mawazo yako potovu hadi lini? \q1 \v 15 Sauti inatangaza kutoka Dani, \q2 ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu. \q1 \v 16 “Waambie mataifa jambo hili, \q2 piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu: \q1 ‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali, \q2 likipiga kelele za vita dhidi ya miji ya Yuda. \q1 \v 17 Wamemzunguka kama watu walindao shamba, \q2 kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 18 “Mwenendo wako na matendo yako mwenyewe \q2 vimeleta haya juu yako. \q1 Hii ndiyo adhabu yako. \q2 Tazama jinsi ilivyo chungu! \q2 Tazama jinsi inavyochoma moyo!” \b \q1 \v 19 Ee mtima wangu, mtima wangu! \q2 Ninagaagaa kwa maumivu. \q1 Ee maumivu makuu ya moyo wangu! \q2 Moyo wangu umefadhaika ndani yangu, \q2 siwezi kunyamaza, \q1 kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta; \q2 nimesikia kelele za vita. \q1 \v 20 Maafa baada ya maafa, \q2 nchi yote imekuwa magofu. \q1 Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa, \q2 makazi yangu kwa muda mfupi. \q1 \v 21 Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita \q2 na kusikia sauti za tarumbeta? \b \q1 \v 22 “Watu wangu ni wapumbavu, \q2 hawanijui mimi. \q1 Ni watoto wasio na akili, \q2 hawana ufahamu. \q1 Ni hodari kutenda mabaya, \q2 hawajui kutenda yaliyo mema.” \b \q1 \v 23 Niliitazama dunia, \q2 nayo haikuwa na umbo tena ni tupu; \q1 niliziangalia mbingu, \q2 mianga ilikuwa imetoweka. \q1 \v 24 Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka, \q2 vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba. \q1 \v 25 Nilitazama, wala hapakuwa na watu; \q2 kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake. \q1 \v 26 Nilitazama, nayo nchi iliyokuwa imestawi vizuri \q2 imekuwa jangwa, \q1 miji yake yote ilikuwa magofu \q2 mbele za Mwenyezi Mungu, \q2 mbele ya hasira yake kali. \q1 \v 27 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q2 “Nchi yote itaharibiwa, \q2 ingawa sitaiangamiza kabisa. \q1 \v 28 Kwa hiyo dunia itaomboleza \q2 na mbingu zilizo juu zitakuwa giza, \q1 kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma, \q2 nimeamua na wala sitageuka.” \b \q1 \v 29 Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde \q2 kila mji unakimbia. \q1 Baadhi wanakimbilia vichakani, \q2 baadhi wanapanda juu ya miamba. \q1 Miji yote imeachwa, \q2 hakuna aishiye ndani yake. \b \q1 \v 30 Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa? \q2 Kwa nini unajivika vazi jekundu \q2 na kuvaa vito vya dhahabu? \q1 Kwa nini unapaka macho yako wanja? \q2 Unajipamba bure. \q1 Wapenzi wako wanakudharau, \q2 wanautafuta uhai wako. \b \q1 \v 31 Nasikia kilio kama cha mwanamke \q2 katika uchungu wa kuzaa, \q1 kilio cha uchungu kama cha anayemzaa \q2 mtoto wake wa kwanza: \q1 kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua, \q2 akiinua mikono yake, akisema, \q1 “Ole wangu! Ninazimia; \q2 maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.” \c 5 \s1 Hakuna hata mmoja aliye mkamilifu \q1 \v 1 “Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu, \q2 tazameni pande zote na mtafakari, \q2 tafuteni katika viwanja vyake. \q1 Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu \q2 atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli, \q2 nitausamehe mji huu. \q1 \v 2 Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo,’ \q2 bado wanaapa kwa uongo.” \b \q1 \v 3 Ee Mwenyezi Mungu, je, macho yako hayaitafuti kweli? \q2 Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, \q2 uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo. \q1 Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe \q2 nao walikataa kutubu. \q1 \v 4 Ndipo nikasema, “Hawa ni maskini tu; \q2 wao ni wapumbavu, \q1 kwa maana hawaijui njia ya Mwenyezi Mungu, \q2 sheria ya Mungu wao. \q1 \v 5 Kwa hiyo nitaenda kwa wakuu \q2 na kuzungumza nao, \q1 hakika wao wanaijua njia ya Mwenyezi Mungu, \q2 sheria ya Mungu wao.” \q1 Lakini kwa nia moja nao pia walikuwa wameivunja nira \q2 na kuvivunja vifungo. \q1 \v 6 Kwa hiyo simba wa mwituni atawashambulia, \q2 mbwa-mwitu wa jangwani atawaangamiza, \q1 chui atawavizia karibu na miji yao, \q2 ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje, \q1 kwa maana uasi wao ni makubwa, \q2 na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi. \b \q1 \v 7 “Kwa nini niwasamehe? \q2 Watoto wenu wameniacha kwa kuapa kwa miungu batili. \q1 Niliwapatia mahitaji yao yote, \q2 lakini bado wamefanya uzinzi na kusongamana katika nyumba za makahaba. \q1 \v 8 Wamelishwa vizuri, kama farasi dume wenye tamaa nyingi, \q2 kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine. \q1 \v 9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Je, nisijilipizie kisasi \q2 juu ya taifa kama hili? \b \q1 \v 10 “Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu, \q2 lakini msiangamize kabisa. \q1 Pogoeni matawi yake, \q2 kwa kuwa watu hawa sio wa Mwenyezi Mungu. \q1 \v 11 Nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda \q2 wamekuwa si waaminifu kwangu kabisa,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 12 Wamedanganya kuhusu Mwenyezi Mungu. \q2 Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote! \q1 Hakuna dhara litakalotupata; \q2 kamwe hatutaona upanga wala njaa. \q1 \v 13 Manabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao; \q2 kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.” \p \v 14 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya, \q2 nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto, \q1 na watu hawa wawe kuni \q2 zinazoliwa na huo moto. \q1 \v 15 Ee nyumba ya Israeli,” asema Mwenyezi Mungu, \q2 “Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako, \q1 taifa la kale na linaloendelea kudumu, \q2 taifa ambalo lugha yao huijui, \q2 wala msemo wao huwezi kuuelewa. \q1 \v 16 Podo lao ni kama kaburi lililo wazi, \q2 wote ni mashujaa hodari. \q1 \v 17 Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu, \q2 watawaangamiza wana wenu wa kiume na wa kike; \q1 watayaangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ng’ombe, \q2 wataiangamiza mizabibu yenu na mitini yenu. \q1 Kwa upanga wataiangamiza \q2 miji yenye ngome mliyoitumainia. \p \v 18 “Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Mwenyezi Mungu. \v 19 “Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama mlivyoniacha mimi kwa kuitumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’ \q1 \v 20 “Itangazie nyumba ya Yakobo hili \q2 na ulipigie mbiu katika Yuda: \q1 \v 21 Sikieni hili, enyi watu wapumbavu, msio na akili, \q2 mlio na macho lakini hamwoni, \q2 mlio na masikio lakini hamsikii: \q1 \v 22 Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? \q1 Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, \q2 kizuizi cha milele ambacho bahari haiwezi kuupita. \q1 Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; \q2 yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka. \q1 \v 23 Lakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi, \q2 wamegeukia mbali na kwenda zao. \q1 \v 24 Wao hawaambiani wenyewe, \q2 ‘Sisi na tumwogope Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q1 anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake, \q2 anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’ \q1 \v 25 Matendo yenu mabaya yamezuia haya yote, \q2 dhambi zenu zimewazuia msipate mema. \b \q1 \v 26 “Miongoni mwa watu wangu wamo walio waovu \q2 wanaovizia kama watu wanaotega ndege, \q1 na kama wale wanaoweka mitego \q2 kuwakamata watu. \q1 \v 27 Kama vitundu vilivyojaa ndege, \q2 nyumba zao zimejaa udanganyifu; \q1 wamekuwa matajiri na wenye nguvu, \q2 \v 28 wamenenepa na kunawiri. \q1 Matendo yao maovu hayana kikomo; \q2 hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda, \q2 hawatetei haki za maskini. \q1 \v 29 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Je, nisijilipizie kisasi \q2 juu ya taifa kama hili? \b \q1 \v 30 “Jambo la kutisha na kushtusha \q2 limetokea katika nchi hii: \q1 \v 31 Manabii wanatabiri uongo, \q2 makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe, \q1 nao watu wangu wanapenda hivyo. \q2 Lakini mtafanya nini mwisho wake? \c 6 \s1 Yerusalemu kuzingirwa na jeshi \q1 \v 1 “Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini! \q2 Kimbieni kutoka Yerusalemu! \q1 Pigeni tarumbeta katika Tekoa! \q2 Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu! \q1 Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini, \q2 na uharibifu wa kutisha. \q1 \v 2 Nitamwangamiza Binti Sayuni, \q2 aliye mzuri sana na mwororo. \q1 \v 3 Wachungaji pamoja na makundi yao \q2 watakuja dhidi yake; \q1 watapiga mahema yao kumzunguka, \q2 kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” \b \q1 \v 4 “Jiandaeni kwa vita dhidi yake! \q2 Inukeni tumshambulie mchana! \q1 Lakini, ole wetu, mchana unaisha, \q2 na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu. \q1 \v 5 Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, \q2 na kuharibu ngome zake!” \p \v 6 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Kateni miti mjenge boma \q2 kuzingira Yerusalemu. \q1 Mji huu ni lazima uadhibiwe; \q2 umejazwa na uonevu. \q1 \v 7 Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, \q2 ndivyo anavyomwaga uovu wake. \q1 Ukatili na maangamizi vyasikika ndani yake, \q2 ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima. \q1 \v 8 Pokea onyo, ee Yerusalemu, \q2 la sivyo nitageukia mbali nawe \q1 na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa, \q2 asiweze mtu kuishi ndani yake.” \p \v 9 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli \q2 kwa uangalifu kama kwenye mzabibu; \q1 pitisha mkono wako kwenye matawi tena, \q2 kama yeye avunaye zabibu.” \b \q1 \v 10 Niseme na nani na kumpa onyo? \q2 Ni nani atakayenisikiliza mimi? \q1 Masikio yao yameziba\f + \fr 6:10 \fr*\ft kwa Kiebrania \ft*\fqa masikio yao hayajatahiriwa\fqa*\f*, \q2 kwa hiyo hawawezi kusikia. \q1 Neno la Mwenyezi Mungu ni chukizo kwao, \q2 hawalifurahii. \q1 \v 11 Lakini nimejaa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, \q2 nami siwezi kuizuia. \b \q1 “Wamwagie watoto walio barabarani, \q2 na juu ya vijana wa kiume waliokusanyika; \q1 mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake, \q2 hata nao wazee waliolemewa na miaka. \q1 \v 12 Nyumba zao zitapewa watu wengine, \q2 pamoja na mashamba yao na wake zao, \q1 nitakapounyoosha mkono wangu \q2 dhidi ya wale wanaoishi katika nchi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 13 “Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa, \q2 wote wana tamaa ya kupata faida zaidi; \q1 manabii na makuhani wanafanana, \q2 wote wanafanya udanganyifu. \q1 \v 14 Wanafunga majeraha ya watu wangu \q2 bila uangalifu. \q1 Wanasema, ‘Amani, amani,’ \q2 wakati hakuna amani. \q1 \v 15 Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao \q2 inayochukiza mno? \q1 Hapana, hawana haya hata kidogo; \q2 hawajui hata kuona aibu. \q1 Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, \q2 watashushwa chini nitakapowaadhibu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 16 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q1 “Simama kwenye njia panda utazame, \q2 ulizia mapito ya zamani, \q1 ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo, \q2 nanyi mtapata amani nafsini mwenu. \q2 Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita njia hiyo.’ \q1 \v 17 Niliweka walinzi juu yenu na kusema, \q2 ‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’ \q2 Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’ \q1 \v 18 Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa, \q2 angalieni, enyi mashahidi, \q2 lile litakalowatokea. \q1 \v 19 Sikia, ee nchi: \q1 Ninaleta maafa juu ya watu hawa, \q2 matunda ya mipango yao, \q1 kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu \q2 na wameikataa sheria yangu. \q1 \v 20 Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba, \q2 au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali? \q1 Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki, \q2 dhabihu zako hazinifurahishi mimi.” \p \v 21 Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q1 “Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa. \q2 Baba na wana wao watajikwaa juu yake, \q2 majirani na rafiki wataangamia.” \p \v 22 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q1 “Tazama, jeshi linakuja \q2 kutoka nchi ya kaskazini, \q1 taifa kubwa linaamshwa \q2 kutoka miisho ya dunia. \q1 \v 23 Wamejifunga pinde na mkuki, \q2 ni wakatili na hawana huruma. \q1 Wanatoa sauti kama bahari inayounguruma \q2 wanapoendesha farasi wao. \q1 Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita \q2 ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.” \b \q1 \v 24 Tumesikia taarifa zao, \q2 nayo mikono yetu imelegea. \q1 Uchungu umetushika, \q2 maumivu kama ya mwanamke katika uchungu wa kuzaa. \q1 \v 25 Usitoke kwenda mashambani \q2 au kutembea barabarani, \q1 kwa kuwa adui ana upanga, \q2 na kuna vitisho kila upande. \q1 \v 26 Enyi watu wangu, vaeni magunia \q2 mjivingirishe kwenye majivu, \q1 ombolezeni kwa kilio cha uchungu \q2 kama amliliaye mwana pekee, \q1 kwa maana ghafula \q2 mharibu atatujia. \b \q1 \v 27 “Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma, \q2 nao watu wangu kama mawe yenye madini, \q2 ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao. \q1 \v 28 Wote ni waasi sugu, \q2 wakienda huku na huko kusengenya. \q1 Wao ni shaba na chuma, \q2 wote wanatenda upotovu. \q1 \v 29 Mivuo inavuma kwa nguvu, \q2 kinachoungua kwa huo moto ni risasi, \q1 lakini pamoja na kusafisha kote huku ni bure; \q2 waovu hawaondolewi. \q1 \v 30 Wanaitwa fedha iliyokataliwa, \q2 kwa sababu Mwenyezi Mungu amewakataa.” \c 7 \s1 Dini za uongo ni batili \p \v 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 “Simama kwenye lango la nyumba ya Mwenyezi Mungu, na huko upige mbiu ya ujumbe huu: \p “ ‘Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi watu wote wa Yuda mliokuja kupitia malango haya ili kumwabudu Mwenyezi Mungu. \v 3 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Tengenezeni njia zenu na matendo yenu, nami nitawaacha mkae mahali hapa. \v 4 Msitumainie maneno ya udanganyifu na kusema, “Hili ni Hekalu la Mwenyezi Mungu, Hekalu la Mwenyezi Mungu, Hekalu la Mwenyezi Mungu!” \v 5 Kama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake, \v 6 kama hamdhulumu mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama hamtafuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe, \v 7 ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele. \v 8 Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana. \p \v 9 “ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo, na kufukiza uvumba kwa Baali, na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua, \v 10 kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza? \v 11 Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyang’anyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! asema Mwenyezi Mungu. \p \v 12 “ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli. \v 13 Mlipokuwa mnafanya haya yote, asema Mwenyezi Mungu, nilisema nanyi tena na tena, lakini hamkusikiliza; niliwaita, lakini hamkujibu. \v 14 Kwa hiyo, nililolifanyia Shilo, nitalifanya sasa kwa nyumba hii iitwayo kwa Jina langu, Hekalu mnalolitumainia, mahali nilipowapa ninyi na baba zenu. \v 15 Nitawafukuza mbele yangu, kama nilivyowafanyia ndugu zenu, watu wa Efraimu.’ \p \v 16 “Kwa hiyo usiombe kwa ajili ya watu hawa, wala usinililie, na usifanye maombi kwa ajili yao; usinisihi, kwa sababu sitakusikiliza. \v 17 Je, huyaoni hayo wanayoyatenda katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu? \v 18 Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha. \v 19 Lakini je, mimi ndiye wanayenikasirisha? asema Mwenyezi Mungu. Je, hawajiumizi wenyewe na kujiaibisha? \p \v 20 “ ‘Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana Mungu Mwenyezi: Hasira yangu na ghadhabu yangu vitamwagwa mahali hapa, juu ya mwanadamu na mnyama, juu ya miti ya shambani na juu ya matunda ya ardhini, nayo itaungua pasipo kuzimwa. \p \v 21 “ ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Endeleeni, ongezeni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya dhabihu zenu nyingine, mle nyama hiyo wenyewe! \v 22 Kwa kuwa nilipowaleta baba zenu kutoka Misri na kusema nao, sikuwapa amri kuhusu sadaka za kuteketezwa na dhabihu tu, \v 23 lakini niliwapa amri hii nikisema: Nitiini mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Nendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa. \v 24 Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Walirudi nyuma badala ya kusonga mbele. \v 25 Tangu wakati ule baba zenu walipotoka Misri hadi sasa, siku baada ya siku, tena na tena nimewatumia watumishi wangu manabii. \v 26 Lakini hawakunisikiliza wala hawakujali. Walikuwa na shingo ngumu na kufanya maovu kuliko baba zao.’ \p \v 27 “Utakapowaambia haya yote, hawatakusikiliza; utakapowaita, hawatajibu. \v 28 Kwa hiyo waambie, ‘Hili ni taifa ambalo halimtii Mwenyezi Mungu, Mungu wao, wala kukubali maonyo. Kweli imekufa, imetoweka midomoni mwao. \v 29 Nyoeni nywele zenu na kuzitupa, ombolezeni katika miinuko iliyo kame, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekikataa na kukiacha kizazi hiki kilichomkasirisha. \s1 Bonde la machinjo \p \v 30 “ ‘Watu wa Yuda wamefanya maovu machoni pangu, asema Mwenyezi Mungu. Wameziweka sanamu zao za machukizo ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu, na wameitia unajisi. \v 31 Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia sanamu pa Tofethi kwenye Bonde la Ben-Hinomu ili kuwateketeza watoto wao wa kiume na wa kike kwenye moto, kitu ambacho sikuamuru, wala hakikuingia akilini mwangu. \v 32 Kwa hiyo mjihadhari, siku zinakuja, asema Mwenyezi Mungu, wakati watu watakapokuwa hawapaiti Tofethi au Bonde la Ben-Hinomu, lakini watapaita Bonde la Machinjo, kwa sababu watawazika wafu huko Tofethi hadi pasiwe tena nafasi. \v 33 Ndipo mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwa na yeyote wa kuwafukuza. \v 34 Nitazikomesha sauti za shangwe na furaha, na sauti za bwana arusi na bibi arusi katikati ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, kwa sababu nchi itakuwa ukiwa. \c 8 \s1 Dhambi na uasi wa Yuda \p \v 1 “ ‘Wakati huo, asema Mwenyezi Mungu, mifupa ya wafalme na maafisa wa Yuda, mifupa ya makuhani na manabii, na mifupa ya watu wa Yerusalemu itaondolewa kutoka makaburi yao. \v 2 Itawekwa wazi kwa jua, na mwezi, na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia, na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama kinyesi juu ya ardhi. \v 3 Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.’ \s1 Dhambi na adhabu \p \v 4 “Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki? \q2 Je, mtu anapopotea harudi? \q1 \v 5 Kwa nini basi watu hawa waliasi? \q2 Kwa nini Yerusalemu wanaasi kila mara? \q1 Wanang’ang’ania udanganyifu \q2 na wanakataa kurudi. \q1 \v 6 Nimewasikiliza kwa makini, \q2 lakini hawataki kusema lililo sawa. \q1 Hakuna anayetubu makosa yake \q2 akisema, “Nimefanya nini?” \q1 Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe \q2 kama farasi anayeenda vitani. \q1 \v 7 Hata korongo aliye angani \q2 anayajua majira yake yaliyoamriwa, \q1 nao njiwa, mbayuwayu na koikoi \q2 hufuata majira yao ya kurudi. \q1 Lakini watu wangu hawajui \q2 Mwenyezi Mungu anachotaka kwao. \b \q1 \v 8 “ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara \q2 kwa sababu tunayo Torati ya Mwenyezi Mungu,” \q1 wakati kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi \q2 imeandika kwa udanganyifu? \q1 \v 9 Wenye hekima wataaibika, \q2 watafadhaika na kunaswa. \q1 Kwa kuwa wamelikataa neno la Mwenyezi Mungu, \q2 hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani? \q1 \v 10 Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao, \q2 na mashamba yao kwa wamiliki wengine. \q1 Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa, \q2 wote wana tamaa ya kupata zaidi; \q1 manabii na makuhani wanafanana, \q2 wote wanafanya udanganyifu. \q1 \v 11 Wanafunga majeraha ya watu wangu \q2 bila uangalifu. \q1 Wanasema, “Amani, amani,” \q2 wakati hakuna amani. \q1 \v 12 Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno? \q2 Hapana, hawana haya hata kidogo, \q2 hawajui hata kuona aibu. \q1 Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, \q2 watashushwa chini watakapoadhibiwa, \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 13 “ ‘Nitayaondoa mavuno yao, \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 Hapatakuwa zabibu kwenye mzabibu. \q1 Hapatakuwa na tini kwenye mtini, \q2 na majani yake yatanyauka. \q1 Kile nilichowapa \q2 watanyang’anywa.’ ” \b \q1 \v 14 Kwa nini tunaketi hapa? \q2 Kusanyikeni pamoja! \q1 Tukimbilie kwenye miji yenye ngome, \q2 tukaangamie huko! \q1 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, \q2 ametuhukumu kuangamia, \q1 na kutupatia maji yenye sumu tunywe, \q2 kwa sababu tumemtenda dhambi. \q1 \v 15 Tulitegemea amani, \q2 lakini hakuna jema lililokuja, \q1 tulitegemea wakati wa kupona, \q2 lakini kulikuwa hofu tu. \q1 \v 16 Mkoromo wa farasi wa adui \q2 umesikika kuanzia Dani, \q1 kwa mlio wa madume yao ya farasi, \q2 nchi yote inatetemeka. \q1 Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo, \q2 mji na wote wanaoishi ndani yake. \b \q1 \v 17 “Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali kati yenu, \q2 fira ambao hawawezi kulogwa, \q2 nao watawauma,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 18 Ee Mfariji wangu katika huzuni, \q2 moyo wangu umezimia ndani yangu. \q1 \v 19 Sikia kilio cha watu wangu \q2 kutoka nchi ya mbali: \q1 “Je, Mwenyezi Mungu hayuko Sayuni? \q2 Je, Mfalme wake hayuko tena huko?” \b \q1 “Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao, \q2 kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?” \b \q1 \v 20 “Mavuno yamepita, \q2 kiangazi kimekwisha, \q2 nasi hatujaokolewa.” \b \q1 \v 21 Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia; \q2 ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika. \q1 \v 22 Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi? \q2 Je, hakuna tabibu huko? \q1 Kwa nini basi hakuna uponyaji \q2 wa majeraha ya watu wangu? \c 9 \q1 \v 1 Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji \q2 na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi! \q1 Ningelia usiku na mchana \q2 kwa kuuawa kwa watu wangu. \q1 \v 2 Laiti ningekuwa na nyumba \q2 ya kukaa wasafiri jangwani, \q1 ningewaacha watu wangu \q2 na kwenda mbali nao, \q1 kwa kuwa wote ni wazinzi, \q2 kundi la watu wadanganyifu. \b \q1 \v 3 “Huweka tayari ndimi zao kama upinde, \q2 ili kurusha uongo; \q1 wamekuwa na nguvu katika nchi \q2 lakini si katika ukweli. \q1 Wanatoka dhambi moja hadi nyingine, \q2 hawanitambui mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 4 “Jihadhari na rafiki zako; \q2 usiwaamini ndugu zako. \q1 Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu, \q2 na kila rafiki ni msingiziaji. \q1 \v 5 Rafiki humdanganya rafiki, \q2 hakuna yeyote asemaye kweli. \q1 Wamefundisha ndimi zao kudanganya, \q2 wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi. \q1 \v 6 Unakaa katikati ya udanganyifu; \q2 katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 7 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu, \q2 kwani ni nini kingine niwezacho kufanya \q2 kwa sababu ya dhambi ya watu wangu? \q1 \v 8 Ndimi zao ni mshale wenye sumu, \q2 hunena kwa udanganyifu. \q1 Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake, \q2 lakini moyoni mwake humtegea mtego. \q1 \v 9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Je, nisijilipizie kisasi \q2 kwa taifa kama hili?” \b \q1 \v 10 Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima \q2 na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani. \q1 Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo, \q2 milio ya ng’ombe haisikiki. \q1 Ndege wa angani wametoroka \q2 na wanyama wamekimbia. \b \q1 \v 11 “Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu, \q2 makao ya mbweha; \q1 nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, \q2 asiwepo atakayeishi humo.” \p \v 12 Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Mwenyezi Mungu awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita? \p \v 13 Mwenyezi Mungu akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu. \v 14 Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama baba zao walivyowafundisha.” \v 15 Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu. \v 16 Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuyajua, nikiwafuata kwa upanga hadi niwaangamize kabisa.” \b \p \v 17 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezaji waje, \q2 waite wale walio na ustadi kati yao. \q1 \v 18 Nao waje upesi \q2 waomboleze juu yetu, \q1 hadi macho yetu yatiririke machozi \q2 na kope zetu zibubujike maji. \q1 \v 19 Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni: \q2 ‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa! \q2 Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa! \q1 Ni lazima tuihame nchi yetu \q2 kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ” \b \q1 \v 20 Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Mwenyezi Mungu; \q2 fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake. \q1 Wafundisheni binti zenu kuomboleza; \q2 fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo. \q1 \v 21 Mauti imeingia ndani kupitia madirishani, \q2 imeingia kwenye majumba yetu ya fahari; \q1 imewakatilia mbali watoto katika barabara \q2 na vijana wa kiume kutoka viwanja vya miji. \p \v 22 Sema, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Mizoga ya watu italala \q2 kama kinyesi katika mashamba, \q1 kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji, \q2 wala hakuna atakayeikusanya.’ ” \p \v 23 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake, \q2 au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake, \q2 wala tajiri ajisifu katika utajiri wake, \q1 \v 24 lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hii: \q2 kwamba ananifahamu na kunijua mimi, \q1 kwamba mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitendaye wema, \q2 hukumu na haki duniani, \q2 kwa kuwa napendezwa na haya,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 25 “Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema Mwenyezi Mungu, \v 26 yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.” \c 10 \s1 Mwenyezi Mungu na sanamu \p \v 1 Sikieni lile Mwenyezi Mungu anasema nanyi, ee nyumba ya Israeli. \v 2 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Usijifunze njia za mataifa \q2 wala usitishwe na ishara katika anga, \q2 ingawa mataifa yanatishwa nazo. \q1 \v 3 Kwa maana desturi za mataifa hazina maana, \q2 wanakata mti msituni, \q2 na fundi anauchonga kwa patasi. \q1 \v 4 Wanauremba kwa fedha na dhahabu, \q2 wanaukaza kwa nyundo na misumari ili usitikisike. \q1 \v 5 Sanamu zao ni kama kinyago \q2 kilichowekwa katika shamba la matango kutishia ndege, \q2 nazo haziwezi kuongea; \q2 na kwa kuwa haziwezi kutembea zinabebwa. \q1 Usiziogope. Haziwezi kudhuru \q2 wala kutenda lolote jema.” \b \q1 \v 6 Hakuna aliye kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu; \q2 wewe ni mkuu, \q2 jina lako ni lenye nguvu na uweza. \q1 \v 7 Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe, \q2 Ee Mfalme wa mataifa? \q2 Hii ni stahili yako. \q1 Miongoni mwa watu wote wenye hekima \q2 katika mataifa na katika falme zao zote, \q2 hakuna aliye kama wewe. \q1 \v 8 Wote hawana akili, tena ni wapumbavu; \q2 wanafundishwa na sanamu batili za miti. \q1 \v 9 Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi \q2 na dhahabu kutoka Ufazi. \q1 Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza \q2 huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: \q1 vyote vikiwa vimetengenezwa \q2 na mafundi stadi. \q1 \v 10 Lakini Mwenyezi Mungu ni Mungu wa kweli, \q2 yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. \q1 Anapokasirika, dunia hutetemeka, \q2 mataifa hayawezi kustahimili hasira yake. \p \v 11 “Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia duniani na chini ya mbingu.’ ” \q1 \v 12 Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, \q2 akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, \q2 na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake. \q1 \v 13 Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; \q2 huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. \q1 Hupeleka miali ya radi pamoja na mvua, \q2 naye huuleta upepo kutoka ghala zake. \b \q1 \v 14 Kila mtu ni mjinga na hana maarifa; \q2 kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. \q1 Vinyago vyake ni vya udanganyifu; \q2 havina pumzi. \q1 \v 15 Ni ubatili tu, vitu vya kufanyia mzaha; \q2 wakati wa hukumu yao, wataangamia. \q1 \v 16 Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, \q2 kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, \q1 pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: \q2 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake. \s1 Maangamizi yajayo \q1 \v 17 Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii, \q2 enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi. \q1 \v 18 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q2 “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu \q2 wote wanaoishi katika nchi hii; \q1 nitawataabisha \q2 ili wapate kutekwa.” \b \q1 \v 19 Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu! \q2 Jeraha langu ni kubwa! \q1 Lakini nilisema, \q2 “Kweli hii ni adhabu yangu, \q2 nami sharti niistahimili.” \q1 \v 20 Hema langu limeangamizwa; \q2 kamba zake zote zimekatwa. \q1 Wana wangu wametekwa na hawapo tena; \q2 hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu \q2 wala wa kusimamisha kibanda changu. \q1 \v 21 Wachungaji hawana akili \q2 wala hawamuulizi Mwenyezi Mungu, \q1 hivyo hawastawi \q2 na kundi lao lote la kondoo limetawanyika. \q1 \v 22 Sikilizeni! Taarifa inakuja: \q2 ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! \q1 Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa, \q2 na kuwa makao ya mbweha. \s1 Maombi ya Yeremia \q1 \v 23 Ninajua, Ee Mwenyezi Mungu, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; \q2 hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe. \q1 \v 24 Unirudi, Ee Mwenyezi Mungu, lakini kwa kipimo cha haki: \q2 si katika hasira yako, \q2 usije ukaniangamiza. \q1 \v 25 Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa \q2 wasiokujua wewe, \q2 juu ya mataifa wasioliitia jina lako. \q1 Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo; \q2 wamemwangamiza kabisa \q2 na kuiharibu nchi yake. \c 11 \s1 Agano limevunjwa \p \v 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 “Sikia maneno ya agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu. \v 3 Waambie kwamba hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu ambaye hatayatii maneno ya agano hili, \v 4 maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, kutoka tanuru la kuyeyushia vyuma.’ Nilisema, ‘Nitiini mimi na mfanye kila kitu ninachowaamuru, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. \v 5 Kisha nitatimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi inayotiririka maziwa na asali,’ nchi ambayo mnaimiliki leo.” \p Nikajibu, “Amen, Mwenyezi Mungu.” \p \v 6 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Tangaza maneno haya yote katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu: ‘Sikilizeni maneno ya agano hili na kuyafuata. \v 7 Tangu wakati ule niliwapandisha baba zenu kutoka Misri hadi leo, niliwaonya tena na tena, nikisema, “Nitiini mimi.” \v 8 Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Hivyo nikaleta juu yao laana zote za agano nililokuwa nimewaamuru wao kulifuata, lakini hawakulishika.’ ” \p \v 9 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Kuna fitina inayoendelea miongoni mwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu. \v 10 Wamerudia dhambi za baba zao waliokataa kusikiliza maneno yangu. Wameifuata miungu mingine na kuitumikia. Nyumba zote mbili za Israeli na Yuda zimelivunja agano nililofanya na baba zao. \v 11 Kwa hivyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nitaleta juu yao maafa ambayo hawawezi kuyakimbia. Hata wakinililia, sitawasikiliza. \v 12 Miji ya Yuda na watu wa Yerusalemu wataenda kuililia miungu ambayo wameifukizia uvumba, lakini haitawasaidia kamwe wakati maafa yatakapowapiga. \v 13 Mnayo miungu mingi kama miji mliyo nayo, ee Yuda, nazo madhabahu mlizozijenga za kumfukizia uvumba huyo mungu wa aibu, Baali ni nyingi kama barabara za Yerusalemu.’ \p \v 14 “Wewe usiwaombee watu hawa wala kufanya maombezi yoyote au kunisihi kwa ajili yao, kwa sababu sitawasikiliza watakaponiita wakati wa taabu yao. \q1 \v 15 “Mpendwa wangu anafanya nini hekaluni mwangu, \q2 anapofanya mashauri yake maovu na wengi? \q1 Je, nyama iliyowekwa wakfu yaweza \q2 kukuondolea uovu wako? \q1 Unashangilia unapojiingiza \q2 katika uovu wako.” \b \q1 \v 16 Mwenyezi Mungu alikuita jina lako Mzeituni uliostawi, \q2 wenye matunda yakupendeza. \q1 Lakini kwa ngurumo ya mawimbi makuu \q2 atautia moto, \q2 nayo matawi yake yatavunjika. \m \v 17 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, aliyekupanda, ametamka maafa juu yako, kwa sababu nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda mmefanya maovu na kunikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba. \s1 Njama dhidi ya Yeremia \p \v 18 Kwa sababu Mwenyezi Mungu alinifunulia na kunionesha hila zao mbaya, na waliyokuwa wanayafanya niliyafahamu. \v 19 Nilikuwa kama mwana-kondoo mpole aliyeongozwa machinjoni; mimi sikutambua kwamba walikuwa wamepanga njama dhidi yangu, wakisema, \q1 “Sisi na tuuangamize mti na matunda yake; \q2 nasi tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai, \q2 ili jina lake lisikumbukwe tena.” \q1 \v 20 Lakini, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, wewe uhukumuye kwa haki, \q2 uchunguzaye moyo na akili, \q1 acha nione ukiwalipiza wao kisasi, \q2 kwa maana kwako nimeweka shauri langu. \p \v 21 “Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu watu wa Anathothi wanaotafuta uhai wako, wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi Mungu, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’: \v 22 kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Nitawaadhibu. Vijana wao wa kiume watakufa kwa upanga, wana wao wa kiume na wa kike watakufa kwa njaa. \v 23 Hayatabakizwa mabaki kwao kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa kuadhibiwa kwao.’ ” \c 12 \s1 Lalamiko la Yeremia \q1 \v 1 Wewe daima u mwenye haki, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 niletapo mashtaka mbele yako. \q1 Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: \q2 Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? \q1 Kwa nini wasio waaminifu \q2 wote wanaishi salama? \q1 \v 2 Umewapanda, nao wameota, \q2 wanakua na kuzaa matunda. \q1 Daima u midomoni mwao, \q2 lakini mbali na mioyo yao. \q1 \v 3 Hata hivyo unanijua mimi, Ee Mwenyezi Mungu; \q2 unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. \q1 Wakokote kama kondoo wanaoenda kuchinjwa! \q2 Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa! \q1 \v 4 Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza hadi lini, \q2 na majani katika kila shamba kunyauka? \q1 Kwa sababu wale wanaoishi ndani yake ni waovu, \q2 wanyama na ndege wameangamia. \q1 Zaidi ya hayo, watu wanasema, \q2 “Mwenyezi Mungu hataona yatakayotupata sisi.” \s1 Jibu la Mwenyezi Mungu \q1 \v 5 “Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda, \q2 unawezaje kushindana na farasi? \q1 Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama, \q2 utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani? \q1 \v 6 Ndugu zako na jamaa zako nao wamekusaliti, \q2 wameinua kilio kikubwa dhidi yako. \q1 Usiwaamini hata wakisema \q2 mema juu yako. \b \q1 \v 7 “Nitaiacha nyumba yangu, \q2 nitupe urithi wangu; \q1 nitamtia yeye nimpendaye \q2 mikononi mwa adui zake. \q1 \v 8 Urithi wangu umekuwa kwangu \q2 kama simba wa msituni. \q1 Nauchukia kwa kuwa \q2 unaningurumia. \q1 \v 9 Je, urithi wangu haukuwa \q2 kama ndege wa mawindo wa madoadoa \q1 ambaye ndege wengine wawindao \q2 humzunguka na kumshambulia? \q1 Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; \q2 walete ili wale. \q1 \v 10 Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu \q2 na kulikanyaga shamba langu; \q1 watalifanya shamba langu zuri \q2 kuwa jangwa la ukiwa. \q1 \v 11 Litafanywa kuwa jangwa, \q2 lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu; \q1 nchi yote itafanywa jangwa \q2 kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali. \q1 \v 12 Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani \q2 waangamizi watavamia, \q1 kwa maana upanga wa Mwenyezi Mungu utawala, \q2 kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine; \q2 hakuna hata mmoja atakayekuwa salama. \q1 \v 13 Watapanda ngano lakini watavuna miiba; \q2 watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote. \q1 Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako \q2 kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi Mungu.” \p \v 14 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa habari ya majirani zangu wote wabaya wanaonyang’anya urithi ambao ninawapa watu wangu Israeli, nitawang’oa kutoka nchi zao, nami nitaing’oa nyumba ya Yuda kutoka katikati yao. \v 15 Lakini baada ya kuwang’oa, nitawahurumia tena na kumrudisha kila mmoja wao kwenye urithi wake mwenyewe na kwenye nchi yake mwenyewe. \v 16 Ikiwa watajifunza vyema njia za watu wangu na kuapa kwa Jina langu, wakisema, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo,’ hata kama wakati fulani walifundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watafanywa imara katikati ya watu wangu. \v 17 Lakini kama taifa lolote halitasikiliza na kutii, nitaling’oa kabisa na kuliangamiza,” asema Mwenyezi Mungu. \c 13 \s1 Mkanda wa kitani \p \v 1 Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia: “Nenda ununue mkanda wa kitani, ujivike kiunoni mwako, lakini usiuache uguse maji.” \v 2 Kwa hiyo nikanunua mkanda, kama Mwenyezi Mungu alivyoniagiza, nikajivika kiunoni. \p \v 3 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kwa mara ya pili: \v 4 “Chukua mkanda ulionunua ambao umeuvaa kiunoni mwako, uende sasa Frati uufiche ndani ya ufa mdogo kwenye mwamba.” \v 5 Ndipo nikaenda na kuuficha ule mkanda huko Frati, kama Mwenyezi Mungu alivyoniamuru. \p \v 6 Baada ya siku nyingi Mwenyezi Mungu akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.” \v 7 Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa. \p \v 8 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia: \v 9 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Vivyo hivyo ndivyo nitakavyokiharibu kiburi cha Yuda na kiburi kikuu cha Yerusalemu. \v 10 Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine wakiitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mshipi huu ambao haufai kabisa! \v 11 Kwa maana kama vile mshipi ufungwavyo kiunoni mwa mtu, ndivyo nilivyoifunga nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘ili wawe watu wangu kwa ajili ya utukufu wangu, sifa na heshima yangu. Lakini hawajasikiliza.’ \s1 Viriba vya mvinyo \p \v 12 “Waambie: ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo.’ Wakikuambia, ‘Kwani hatujui kwamba kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo?’ \v 13 Uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: nitawajaza ulevi wote wanaoishi katika nchi hii, pamoja na wafalme wanaoketi kwenye kiti cha ufalme cha Daudi, makuhani, manabii na wakaaji wote wa Yerusalemu. \v 14 Nitawagombanisha kila mmoja na mwenzake, baba na wana wao, asema Mwenyezi Mungu. Sitawarehemu wala kuwahurumia ili niache kuwaangamiza.’ ” \s1 Tishio la kutekwa \q1 \v 15 Sikieni na mzingatie, \q2 msiwe na kiburi, \q2 kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenena. \q1 \v 16 Mpeni utukufu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, \q2 kabla hajaleta giza, \q1 kabla miguu yenu haijajikwaa \q2 juu ya vilima vitakavyotiwa giza. \q1 Mlitarajia nuru, \q2 lakini ataifanya kuwa giza nene \q2 na kuibadili kuwa huzuni kubwa. \q1 \v 17 Lakini kama hamtasikiliza, \q2 nitalia sirini \q2 kwa ajili ya kiburi chenu; \q1 macho yangu yatalia kwa uchungu, \q2 yakitiririka machozi, \q1 kwa sababu kundi la kondoo la Mwenyezi Mungu \q2 litachukuliwa mateka. \b \q1 \v 18 Mwambie mfalme na mama malkia, \q2 “Shukeni kutoka viti vyenu vya utawala, \q1 kwa kuwa taji zenu za utukufu \q2 zitaanguka kutoka vichwani mwenu.” \q1 \v 19 Miji ya Negebu itafungwa, \q2 wala hapatakuwa na mtu wa kuifungua. \q1 Watu wa Yuda wote watapelekwa uhamishoni, \q2 wakichukuliwa kabisa waende mbali. \b \q1 \v 20 Inua macho yako uone \q2 wale wanaokuja kutoka kaskazini. \q1 Liko wapi lile kundi ulilokabidhiwa, \q2 wale kondoo uliojivunia? \q1 \v 21 Utasema nini Mwenyezi Mungu atakapowaweka juu yako \q2 wale ulioungana nao kama rafiki zako maalum? \q1 Je, hutapatwa na uchungu kama mwanamke \q2 aliye katika uchungu wa kuzaa? \q1 \v 22 Nawe ukijiuliza, \q2 “Kwa nini haya yamenitokea?” \q1 Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingi \q2 marinda yako yameraruliwa \q2 na mwili wako umetendewa vibaya. \q1 \v 23 Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yake \q2 au chui kubadili madoadoa yake? \q1 Vivyo hivyo, wewe uliyezoea kutenda mabaya \q2 huwezi kufanya mema. \b \q1 \v 24 “Nitawatawanya kama makapi \q2 yapeperushwayo na upepo wa jangwani. \q1 \v 25 Hii ndiyo kura yako, \q2 fungu nililokuamulia,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “kwa sababu umenisahau mimi \q2 na kuamini miungu ya uongo. \q1 \v 26 Nitayafunua marinda yako juu ya uso wako \q2 ili aibu yako ionekane, \q1 \v 27 yaani uzinzi wako na kulia kwako kulikojaa tamaa kama farasi, \q2 na ukahaba wako usio na aibu! \q1 Nimeyaona matendo yako ya machukizo \q2 juu ya vilima na mashambani. \q1 Ole wako, ee Yerusalemu! \q2 Utaendelea kuwa najisi hadi lini?” \c 14 \s1 Ukame, njaa na upanga \p \v 1 Hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu kwa Yeremia kuhusu ukame: \q1 \v 2 “Yuda anaomboleza, \q2 kudhoofika kwa miji yake; \q1 wanaomboleza kwa ajili ya nchi, \q2 nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu. \q1 \v 3 Wakuu wanawatuma watumishi wao maji; \q2 nao wanakwenda visimani \q2 lakini huko hakuna maji. \q1 Wanarudi na vyombo bila maji; \q2 wakiwa na hofu na kukata tamaa, \q2 wanafunika vichwa vyao. \q1 \v 4 Ardhi imepasuka nyufa \q2 kwa sababu hakuna mvua katika nchi; \q1 wakulima wana hofu \q2 na wanafunika vichwa vyao. \q1 \v 5 Hata kulungu kondeni \q2 anaacha kinda lake lililotoka kutotolewa \q2 kwa sababu hakuna majani. \q1 \v 6 Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kame \q2 na kutweta kama mbweha; \q1 macho yao yanakosa nguvu za kuona \q2 kwa sababu ya kukosa malisho.” \b \q1 \v 7 Ingawa dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, tenda jambo kwa ajili ya jina lako. \q1 Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa, \q2 nasi tumetenda dhambi dhidi yako. \q1 \v 8 Ee Tumaini la Israeli, \q2 Mwokozi wake wakati wa taabu, \q1 kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi, \q2 kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu? \q1 \v 9 Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa, \q2 kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa? \q1 Wewe uko katikati yetu, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 nasi tunaitwa kwa jina lako; \q2 usituache! \p \v 10 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu watu hawa: \q1 “Wanapenda sana kutangatanga, \q2 hawaizuii miguu yao. \q1 Hivyo Mwenyezi Mungu hawakubali; \q2 sasa ataukumbuka uovu wao \q2 na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.” \p \v 11 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. \v 12 Ingawa wanafunga, sitasikiliza kilio chao; hata wakitoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za nafaka, sitazikubali. Badala yake, nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.” \p \v 13 Lakini nikasema, “Aa, Bwana Mungu Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’ ” \p \v 14 Ndipo Mwenyezi Mungu akaniambia, “Manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwatuma, wala sikuwachagua, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, uaguzi usio na faida, udanganyifu wa mioyo yao, na ubatili. \v 15 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu manabii wanaotabiri kwa jina langu: Mimi sikuwatuma, lakini wanasema, ‘Hakuna upanga wala njaa itakayoigusa nchi hii.’ Manabii hao hao watakufa kwa upanga na njaa. \v 16 Nao watu hao wanaowatabiria watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga. Hapatakuwa na mtu wa kuwazika wao au wake zao, watoto wao wa kiume au wa kike. Nitawamwagia maafa wanayostahili. \p \v 17 “Nena nao neno hili: \q1 “ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi \q2 usiku na mchana bila kukoma; \q1 kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu, \q2 amepata jeraha baya, \q2 pigo la kuangamiza. \q1 \v 18 Ninapokwenda shambani, \q2 ninaona wale waliouawa kwa upanga; \q1 ninapokwenda mjini, \q2 huko ninaona maangamizi ya njaa. \q1 Nabii na kuhani kwa pamoja \q2 wameenda katika nchi wasiyoijua.’ ” \b \q1 \v 19 Je, umemkataa Yuda kabisa? \q2 Umemchukia Sayuni kabisa? \q1 Kwa nini umetuumiza \q2 hata hatuwezi kuponyeka? \q1 Tulitarajia amani, \q2 lakini hakuna jema lililotujia; \q1 tulitarajia wakati wa kupona \q2 lakini kuna hofu kuu tu. \q1 \v 20 Ee Mwenyezi Mungu, tunatambua uovu wetu \q2 na kosa la baba zetu; \q2 kweli tumetenda dhambi dhidi yako. \q1 \v 21 Kwa ajili ya jina lako usituchukie kabisa; \q2 usikidharau kiti chako cha enzi kilichotukuka. \q1 Kumbuka agano lako nasi \q2 na usilivunje. \q1 \v 22 Je, kuna sanamu batili yoyote ya mataifa \q2 iwezayo kuleta mvua? \q1 Je, anga peke yake zinaweza kuleta mvua? \q2 La hasha! Ni wewe peke yako, \q2 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \q1 Kwa hiyo tumaini letu liko kwako, \q2 kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote. \c 15 \s1 Adhabu isiyoepukika \p \v 1 Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia: “Hata kama Musa na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende! \v 2 Nao wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, na wafe; \q2 waliowekewa kufa kwa upanga, kwa upanga; \q1 waliowekewa kufa kwa njaa, kwa njaa; \q2 na waliowekewa kupelekwa uhamishoni, \q2 wapelekwe uhamishoni.’ ” \p \v 3 Mwenyezi Mungu asema, “Nitatuma aina nne za waangamizi: upanga ili kuua, mbwa ili kukokota mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili wale na waangamize. \v 4 Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu. \q1 \v 5 “Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu? \q2 Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? \q1 Ni nani atakayesimama ili kuuliza \q2 kuhusu hali yako? \q1 \v 6 Umenikataa mimi,” asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Unazidi kukengeuka. \q1 Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza, \q2 siwezi kuendelea kukuonea huruma. \q1 \v 7 Nitawapepeta kwa ungo \q2 kwenye malango ya miji ya nchi. \q1 Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu, \q2 kwa maana hawajabadili njia zao. \q1 \v 8 Nitawafanya wajane wao kuwa wengi \q2 kuliko mchanga wa bahari. \q1 Wakati wa adhuhuri nitamleta mwangamizi \q2 dhidi ya mama wa vijana wao wa kiume; \q1 kwa ghafula nitaleta juu yao \q2 maumivu makuu na hofu kuu. \q1 \v 9 Mama mwenye watoto saba atazimia \q2 na kupumua pumzi yake ya mwisho. \q1 Jua lake litatua kukiwa bado mchana, \q2 atatahayarika na kufedheheka. \q1 Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga \q2 mbele ya adui zao,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 10 Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa, \q2 mtu ambaye ulimwengu wote \q2 unashindana na kugombana naye! \q1 Sikukopa wala sikukopesha, \q2 lakini kila mmoja ananilaani. \p \v 11 Mwenyezi Mungu akasema, \q1 “Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema, \q2 hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaada \q2 nyakati za maafa na nyakati za dhiki. \b \q1 \v 12 “Je, mtu aweza kuvunja chuma, \q2 chuma kinachotoka kaskazini, au avunje shaba? \b \q1 \v 13 “Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara, \q2 bila gharama, \q1 kwa sababu ya dhambi zako zote \q2 katika nchi yako yote. \q1 \v 14 Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zako \q2 katika nchi usiyoijua, \q1 kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwa \q2 utakaowaka juu yako daima.” \b \q1 \v 15 Wewe unafahamu, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 unikumbuke na unitunze mimi. \q2 Lipiza kisasi juu ya watesi wangu. \q1 Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali; \q2 kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa. \q1 \v 16 Maneno yako yalipokuja, niliyala; \q2 yakawa shangwe yangu \q2 na furaha ya moyo wangu, \q1 kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako, \q2 Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni. \q1 \v 17 Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe, \q2 wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao; \q1 niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu, \q2 na wewe ulikuwa umenijaza hasira. \q1 \v 18 Kwa nini maumivu yangu hayakomi, \q2 na jeraha langu ni la kuhuzunisha, \q2 wala haliponyeki? \q1 Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu, \q2 kama chemchemi iliyokauka? \p \v 19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Ukitubu, nitakurejesha \q2 ili uweze kunitumikia; \q1 ukinena maneno yenye maana, \q2 wala si ya upuzi, \q2 utakuwa mnenaji wangu. \q1 Watu hawa ndio watakaokugeukia, \q2 wala si wewe utakayewageukia wao. \q1 \v 20 Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa, \q2 ngome ya ukuta wa shaba; \q1 watapigana nawe \q2 lakini hawatakushinda, \q1 kwa maana mimi niko pamoja nawe \q2 kukuponya na kukuokoa,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 21 “Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu, \q2 na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.” \c 16 \s1 Siku ya maafa \p \v 1 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likanijia: \v 2 “Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.” \v 3 Kwa maana hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu wana wa kiume na wa kike wanaozaliwa katika nchi hii, na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao, na wale wanaume ambao ni baba zao: \v 4 “Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa, lakini watakuwa kama kinyesi juu ya ardhi. Watakufa kwa upanga na kwa njaa. Mizoga yao itakuwa chakula cha ndege na wanyama wa porini.” \p \v 5 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Usiingie katika nyumba ambayo kuna chakula cha matanga; usiende kuwaombolezea wala kuwahurumia, kwa sababu nimeondoa amani yangu, upendo wangu na huruma zangu kutoka kwa watu hawa,” asema Mwenyezi Mungu. \v 6 “Wakubwa na wadogo watakufa katika nchi hii. Hawatazikwa wala kuombolezewa, na hakuna atakayejikatakata au kunyoa nywele za kichwa chake kwa ajili yao. \v 7 Hakuna yeyote atakayewapa chakula ili kuwafariji wanaoomboleza kwa ajili ya waliokufa, hata akiwa amefiwa na baba au mama, wala hakuna yeyote atakayewapa kinywaji ili kuwafariji. \p \v 8 “Usiingie katika nyumba ambayo kuna karamu, na kuketi humo ili kula na kunywa. \v 9 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, aliye Mungu wa Israeli: ‘Mbele ya macho yako na katika siku zako, nitakomesha sauti zote za shangwe na za furaha, na pia sauti za bibi arusi na bwana arusi mahali hapa.’ \p \v 10 “Utakapowaambia watu hawa mambo haya yote na wakakuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu ameamuru maafa makubwa kama haya dhidi yetu? Tumefanya kosa gani? Tumetenda dhambi gani dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu?’ \v 11 Basi waambie, ‘Ni kwa sababu baba zenu waliniacha mimi, wakafuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Waliniacha mimi na hawakuishika sheria yangu,’ asema Mwenyezi Mungu. \v 12 ‘Lakini ninyi mmetenda uovu kupita baba zenu. Tazama jinsi kila mmoja wenu anafuata ukaidi wa moyo wake mbaya, badala ya kunitii mimi. \v 13 Kwa hiyo nitawaondoa katika nchi hii na kuwatupa katika nchi ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua, na huko mtaitumikia miungu mingine usiku na mchana, kwa maana sitawapa fadhili zangu.’ \p \v 14 “Hata hivyo, siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “wakati watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ \v 15 bali watasema, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao. \p \v 16 “Lakini sasa nitawaagiza wavuvi wengi,” asema Mwenyezi Mungu, “nao watawavua. Baada ya hilo, nitawaagizia wawindaji wengi, nao watawawinda kwenye kila mlima na kilima, na katika nyufa za miamba. \v 17 Macho yangu yanaziona njia zao zote, hazikufichika kwangu, wala dhambi yao haikusitirika. \v 18 Nitawalipiza maradufu kwa ajili ya uovu wao na dhambi yao, kwa sababu wameinajisi nchi yangu kwa maumbo yasiyo na uhai ya vinyago vyao vibaya, na kuujaza urithi wangu na sanamu za kuchukiza.” \q1 \v 19 Ee Mwenyezi Mungu, nguvu zangu na ngome yangu, \q2 kimbilio langu wakati wa taabu, \q1 kwako mataifa watakujia \q2 kutoka miisho ya dunia na kusema, \q1 “Baba zetu hawakuwa na chochote isipokuwa miungu ya uongo, \q2 sanamu batili \q2 ambazo hazikuwafaidi kitu. \q1 \v 20 Je, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe? \q2 Lakini hiyo si Mungu!” \b \q1 \v 21 “Kwa hiyo nitawafundisha: \q2 wakati huu nitawafundisha \q2 nguvu zangu na uwezo wangu. \q1 Ndipo watajua \q2 kuwa Jina langu ndimi Mwenyezi Mungu. \c 17 \s1 Dhambi ya Yuda na adhabu yake \q1 \v 1 “Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma, \q2 imeandikwa kwa ncha ya almasi, \q1 kwenye vibao vya mioyo yao \q2 na kwenye pembe za madhabahu zao. \q1 \v 2 Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao \q2 na nguzo za Ashera \q1 kandokando ya miti iliyotanda \q2 na juu ya vilima virefu. \q1 \v 3 Mlima wangu katika nchi pamoja na utajiri \q2 na hazina zako zote nitavitoa viwe nyara, \q1 pamoja na mahali pako pa juu pa kuabudia \q2 kwa sababu ya dhambi katika nchi yako yote. \q1 \v 4 Kwa kosa lako mwenyewe utaupoteza \q2 urithi niliokupa. \q1 Nitakufanya mtumwa wa adui zako \q2 katika nchi usiyoijua, \q1 kwa kuwa umeiwasha hasira yangu, \q2 nayo itawaka milele.” \p \v 5 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu, \q2 amtegemeaye mwenye mwili \q2 kwa ajili ya nguvu zake, \q1 ambaye moyo wake \q2 umemwacha Mwenyezi Mungu. \q1 \v 6 Atakuwa kama kichaka cha jangwani; \q2 hataona mafanikio yatakapokuja. \q1 Ataishi katika sehemu zisizo na maji, \q2 katika nchi ya chumvi ambapo \q2 hakuna yeyote aishiye humo. \b \q1 \v 7 “Lakini amebarikiwa mtu anayemtumaini Mwenyezi Mungu, \q2 ambaye matumaini yake ni katika Mwenyezi Mungu. \q1 \v 8 Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji \q2 uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji. \q1 Hauogopi wakati wa joto ujapo; \q2 majani yake ni mabichi daima. \q1 Hauna hofu katika mwaka wa ukame \q2 na hautaacha kuzaa matunda.” \b \q1 \v 9 Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, \q2 ni mwovu kupita kiasi. \q2 Ni nani awezaye kuujua? \b \q1 \v 10 “Mimi Mwenyezi Mungu ninauchunguza moyo \q2 na kuzijaribu nia, \q1 ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, \q2 kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.” \b \q1 \v 11 Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga, \q2 ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki. \q1 Maisha yake yatakapofika katikati, siku zitamwacha, \q2 na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu. \b \q1 \v 12 Kiti cha enzi kilichotukuzwa, kilichoinuliwa tangu mwanzo, \q2 ndiyo sehemu yetu ya mahali patakatifu. \q1 \v 13 Ee Mwenyezi Mungu, uliye tumaini la Israeli, \q2 wote wakuachao wataaibika. \q1 Wale wanaogeukia mbali nawe wataandikwa mavumbini \q2 kwa sababu wamemwacha Mwenyezi Mungu, \q2 chemchemi ya maji yaliyo hai. \b \q1 \v 14 Uniponye, Ee Mwenyezi Mungu, nami nitaponyeka; \q2 uniokoe nami nitaokoka, \q2 kwa maana wewe ndiwe ninayekusifu. \q1 \v 15 Wao huendelea kuniambia, \q2 “Liko wapi neno la Mwenyezi Mungu? \q2 Sasa na litimie!” \q1 \v 16 Sijakukimbia na kuacha kuwa mchungaji wako; \q2 unajua sijaitamani siku ya kukata tamaa. \q1 Kile kipitacho mdomoni mwangu \q2 ki wazi mbele yako. \q1 \v 17 Usiwe kwangu kitu cha kunitia hofu kuu; \q2 wewe ndiwe kimbilio langu katika siku ya maafa. \q1 \v 18 Watesi wangu na waaibishwe, \q2 lakini nilinde mimi nisiaibike; \q1 wao na watiwe hofu kuu, \q2 lakini unilinde mimi na hofu kuu. \q1 Waletee siku ya maafa; \q2 waangamize kwa maangamizi maradufu. \s1 Kuiadhimisha Sabato \p \v 19 Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia: “Nenda ukasimame kwenye lango la watu, mahali ambako wafalme wa Yuda huingilia na kutokea; simama pia kwenye malango mengine yote ya Yerusalemu. \v 20 Waambie, ‘Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi wafalme wa Yuda, nanyi watu wote wa Yuda, na kila mmoja aishiye Yerusalemu apitaye katika malango haya. \v 21 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Jihadharini msije mkabeba mzigo siku ya Sabato, wala kuingiza mzigo kupitia malango ya Yerusalemu. \v 22 Msitoe mizigo nje ya nyumba zenu wala kufanya kazi yoyote siku ya Sabato, lakini itakaseni siku ya Sabato, kama nilivyowaamuru baba zenu. \v 23 Hata hivyo hawakusikiliza wala kujali, walishupaza shingo zao, na hawakutaka kusikia wala kukubali adhabu. \v 24 Lakini mkiwa waangalifu kunitii, asema Mwenyezi Mungu, nanyi msipoleta mzigo wowote kupitia malango ya mji huu wakati wa Sabato, lakini mkaitakasa siku ya Sabato kwa kutofanya kazi siku hiyo, \v 25 ndipo wafalme wanaokaa kwenye kiti cha utawala cha Daudi wataingia kupitia malango ya mji huu, pamoja na maafisa wao. Wafalme na maafisa wao watakuja wakiwa wamepanda magari ya vita na farasi, wakiandamana na watu wote wa Yuda na wakaaji wa Yerusalemu, nao mji huu utakaliwa na watu daima. \v 26 Watu watakuja kutoka miji ya Yuda na vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na Shefela\f + \fr 17:26 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*, kutoka nchi ya vilima na Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa na dhabihu, sadaka za nafaka, uvumba na sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 27 Lakini ikiwa hamtanitii mimi kwa kuitakasa Sabato na kwa kutochukua mzigo wowote mnapoingia katika malango ya Yerusalemu wakati wa Sabato, basi nitawasha moto usiozimika katika malango ya Yerusalemu utakaoteketeza ngome zake.’ ” \c 18 \s1 Katika nyumba ya mfinyanzi \p \v 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 “Shuka uende hadi nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” \v 3 Kwa hiyo nikashuka hadi nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. \v 4 Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake; hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo kingine, umbo jingine kwa namna alivyoona ni vyema machoni pake. \p \v 5 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 6 “Ee nyumba ya Israeli, je, siwezi kuwafanyia kama huyu mfinyanzi afanyavyo?” asema Mwenyezi Mungu. “Kama vile udongo ulivyo katika mikono ya mfinyanzi, ndivyo mlivyo katika mkono wangu, ee nyumba ya Israeli. \v 7 Wakati wowote nitatangaza kuwa taifa au ufalme utang’olewa, utaangushwa na kuangamizwa, \v 8 Lakini ikiwa taifa nililolionya litatubu na kuacha uovu wake nitaghairi, wala sitaleta maafa niliyokuwa nimekusudia kwa taifa hilo. \v 9 Wakati mwingine nitakapotangaza kuwa taifa au ufalme utasimikwa na kujengwa, \v 10 ikiwa litafanya uovu mbele zangu na halitaitii sauti yangu, nitaghairi kutenda jema nililokuwa nimekusudia. \p \v 11 “Basi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalemu, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tazama! Ninaandaa maafa juu yenu, nami ninapanga mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka njia zenu mbaya, kila mmoja wenu. Tengenezeni njia zenu na matendo yenu.’ \v 12 Lakini wao watajibu, ‘Hakuna faida. Tutaendelea na mipango yetu wenyewe, kila mmoja wetu atafuata ukaidi wa moyo wake mbaya.’ ” \p \v 13 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Ulizia miongoni mwa mataifa: \q2 Ni nani alishasikia jambo kama hili? \q1 Jambo la kutisha sana limefanywa \q2 na Bikira Israeli. \q1 \v 14 Je, barafu ya Lebanoni iliwahi kutoweka \q2 kwenye miteremko yake ya mawe wakati wowote? \q1 Je, maji yake baridi kutoka vyanzo vilivyo mbali \q2 yaliwahi kukoma kutiririka? \q1 \v 15 Lakini watu wangu wamenisahau mimi, \q2 wanafukizia uvumba sanamu batili, \q1 zilizowafanya wajikwae katika njia zao \q2 na katika mapito ya zamani. \q1 Zimewafanya wapite kwenye vichochoro \q2 na kwenye barabara ambazo hazikujengwa. \q1 \v 16 Nchi yao itakuwa kitu cha kutisha, \q2 na cha kudharauliwa daima; \q1 wote wapitao karibu nayo watashangaa \q2 na kutikisa vichwa vyao. \q1 \v 17 Kama upepo unaotoka mashariki, \q2 nitawatawanya mbele ya adui zao; \q1 nitawapa kisogo wala sio uso, \q2 katika siku ya maafa yao.” \p \v 18 Wakasema, “Njooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.” \q1 \v 19 Nisikilize, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 sikia wanayosema washtaki wangu! \q1 \v 20 Je, mema yalipwe kwa mabaya? \q2 Lakini wao wamenichimbia shimo. \q1 Kumbuka kwamba nilisimama mbele yako \q2 na kunena mema kwa ajili yao, \q2 ili wewe ugeuze hasira yako kali mbali nao. \q1 \v 21 Kwa hiyo uwaache watoto wao waone njaa; \q2 uwaache wauawe kwa makali ya upanga. \q1 Wake zao wasiwe na watoto, na wawe wajane; \q2 wanaume wao wauawe, \q1 nao vijana wao wa kiume \q2 wachinjwe kwa upanga vitani. \q1 \v 22 Kilio na kisikike kutoka nyumba zao \q2 ghafula uwaletapo adui dhidi yao, \q1 kwa kuwa wamechimba shimo ili kunikamata \q2 na wameitegea miguu yangu mitego. \q1 \v 23 Lakini unajua, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 hila zao zote za kuniua. \q1 Usiyasamehe makosa yao \q2 wala usifute dhambi zao \q2 mbele za macho yako. \q1 Wao na waangamizwe mbele zako; \q2 uwaadhibu wakati wa hasira yako. \c 19 \s1 Gudulia la udongo lililovunjika \p \v 1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani \v 2 na mtoke mwende hadi Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia, \v 3 nawe useme, ‘Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi wafalme wa Yuda na watu wa Yerusalemu. Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Sikilizeni! Nitaleta maafa mahali hapa, ambayo yatafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yawashe. \v 4 Kwa kuwa wameniacha na kupafanya mahali hapa kuwa pa miungu ya kigeni. Wamefukizia uvumba miungu ambayo wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda kamwe hawakuijua, nao wamelijaza eneo hili kwa damu isiyo na hatia. \v 5 Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia pa Baali ili kuteketeza wana wao katika moto kuwa sadaka kwa Baali, kitu ambacho sikukiamuru wala kukitaja, wala hakikuingia akilini mwangu. \v 6 Hivyo jihadharini, siku zinakuja, asema Mwenyezi Mungu, wakati watu hawatapaita tena mahali hapa Tofethi ama Bonde la Ben-Hinomu, bali Bonde la Machinjo. \p \v 7 “ ‘Nitaiharibu mipango ya Yuda na Yerusalemu mahali hapa. Nitawafanya waanguke kwa upanga mbele ya adui zao, katika mikono ya wale wanaotafuta uhai wao, nami nitaitoa mizoga yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi. \v 8 Nitauharibu mji huu na kuufanya kitu cha kutisha na cha kudharauliwa. Wote wapitao karibu watashangaa na kuudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote. \v 9 Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao wa kiume na wa kike; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzingirwa na jeshi la adui wanaotafuta uhai wao.’ \p \v 10 “Kisha livunje lile gudulia wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia, \v 11 uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi. \v 12 Hivi ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa wale wanaoishi ndani yake, asema Mwenyezi Mungu. Nitaufanya mji huu kama Tofethi. \v 13 Nyumba zilizo Yerusalemu na zile za wafalme wa Yuda zitatiwa unajisi kama mahali hapa, Tofethi: yaani nyumba zote ambazo walifukiza uvumba juu ya mapaa yake kwa jeshi lote la angani, na kumimina dhabihu za vinywaji kwa miungu mingine.’ ” \p \v 14 Kisha Yeremia akarudi kutoka Tofethi, mahali Mwenyezi Mungu alikuwa amemtuma kutoa unabii, akasimama katika ua wa Hekalu la Mwenyezi Mungu na kuwaambia watu wote, \v 15 “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya mji huu pamoja na vijiji vinavyouzunguka kila maafa niliyosema dhidi yake, kwa sababu wamekuwa na shingo ngumu, na hawakuyasikiliza maneno yangu.’ ” \c 20 \s1 Yeremia ateswa na Pashuri \p \v 1 Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu la Mwenyezi Mungu, alipomsikia Yeremia akitoa unabii kuhusu mambo haya, \v 2 akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa kwenye mkatale katika Lango la Juu la Benyamini katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 3 Siku ya pili Pashuri alipomwachia kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Mwenyezi Mungu hakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu\f + \fr 20:3 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Vitisho pande zote\fqa*\f*. \v 4 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nitakufanya uwe tisho kwako na rafiki wako wote; na macho yako mwenyewe yataona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua mateka na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga. \v 5 Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli. \v 6 Nawe Pashuri pamoja na wote wanaoishi katika nyumba yako mtaenda uhamishoni Babeli. Mtafia huko na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ” \s1 Malalamiko ya Yeremia \q1 \v 7 Ee Mwenyezi Mungu, umenidanganya, \q2 nami nikadanganyika; \q1 wewe una nguvu kuliko mimi, \q2 nawe umenishinda. \q1 Ninadharauliwa mchana kutwa, \q2 kila mmoja ananidhihaki. \q1 \v 8 Kila ninenapo, ninapiga kelele \q2 nikitangaza ukatili na uharibifu. \q1 Kwa hiyo neno la Mwenyezi Mungu limeniletea matukano \q2 na mashutumu mchana kutwa. \q1 \v 9 Lakini nikisema, “Sitamtaja \q2 wala kusema tena kwa jina lake,” \q1 neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto, \q2 moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu. \q1 Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu; \q2 kweli, siwezi kujizuia. \q1 \v 10 Ninasikia minong’ono mingi, \q2 “Hofu iko pande zote! \q2 Mshtakini! Twendeni tumshtaki!” \q1 Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze, \q2 wakisema, \q1 “Labda atadanganyika; \q2 kisha tutamshinda \q2 na kulipiza kisasi juu yake.” \b \q1 \v 11 Lakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nami \q2 kama mpiganaji mwenye nguvu; \q1 kwa hiyo watesi wangu watajikwaa, \q2 Hawatashinda, nao wataaibika sana; \q2 aibu yao haitasahaulika milele. \q1 \v 12 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 wewe umjaribuye mwenye haki \q2 na kupima moyo na nia, \q1 hebu nione ukilipiza kisasi juu yao, \q2 kwa maana kwako \q2 nimeliweka shauri langu. \b \q1 \v 13 Mwimbieni Mwenyezi Mungu! \q2 Mpeni Mwenyezi Mungu sifa! \q1 Yeye huokoa uhai wa mhitaji \q2 kutoka mikononi mwa waovu. \b \q1 \v 14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa! \q2 Nayo isibarikiwe ile siku \q2 mama yangu aliyonizaa! \q1 \v 15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari, \q2 yule aliyemfanya afurahi sana, akisema, \q1 “Mtoto amezaliwa kwako, \q2 tena mtoto wa kiume!” \q1 \v 16 Mtu huyo na awe kama ile miji ambayo \q2 Mwenyezi Mungu aliiangamiza bila huruma. \q1 Yeye na asikie maombolezo asubuhi, \q2 na ukelele wa vita adhuhuri. \q1 \v 17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni, \q2 hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu, \q1 nalo tumbo lake la uzazi \q2 lingebaki kuwa kubwa daima. \q1 \v 18 Kwa nini basi nilitoka tumboni \q2 ili kuona taabu na huzuni, \q2 na kuzimaliza siku zangu katika aibu? \c 21 \s1 Mwenyezi Mungu anakataa ombi la Sedekia \p \v 1 Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake, kusema: \v 2 “Tuulizie sasa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Mwenyezi Mungu atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.” \p \v 3 Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia, \v 4 ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo walio nje ya ukuta wakiwazingira kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu. \v 5 Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu, kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi. \v 6 Nitawaangamiza wakaaji wa mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha. \v 7 Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa, mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga; hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asema Mwenyezi Mungu. \p \v 8 “Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. \v 9 Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayeenda na kujisalimisha kwa Wakaldayo, ambao wameuzingira mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi. \v 10 Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya, wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto, asema Mwenyezi Mungu.’ \p \v 11 “Zaidi ya hayo, iambie nyumba ya mfalme ya Yuda, ‘Sikia neno la Mwenyezi Mungu, \v 12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi, \q2 mwokoeni mikononi mwa mdhalimu \q2 yeye aliyetekwa nyara, \q1 la sivyo ghadhabu yangu italipuka \q2 na kuwaka kama moto \q1 kwa sababu ya uovu mlioufanya: \q2 itawaka na hakuna wa kuizima. \q1 \v 13 Niko kinyume nawe, ee Yerusalemu, \q2 wewe uishiye juu ya bonde hili \q2 kwenye uwanda wa juu wa miamba, \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 wewe usemaye, “Ni nani awezaye kuja kinyume chetu? \q2 Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?” \q1 \v 14 Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu, \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 Nitawasha moto katika misitu yenu \q2 ambao utateketeza kila kitu kinachowazunguka.’ ” \c 22 \s1 Hukumu dhidi ya wafalme waovu \p \v 1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko: \v 2 ‘Sikia neno la Mwenyezi Mungu, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha utawala cha Daudi: wewe, wakuu wako na watu wako mnaopitia malango haya. \v 3 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa. \v 4 Ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, wafalme watakaokalia kiti cha utawala cha Daudi wataingia kupitia malango ya jumba la kifalme wakiwa wamepanda magari na farasi huku wakifuatana na watumishi wao na watu wao. \v 5 Lakini kama hutayatii maagizo haya, asema Mwenyezi Mungu, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ” \p \v 6 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda: \q1 “Ingawa uko kama Gileadi kwangu, \q2 kama kilele cha Lebanoni, \q1 hakika nitakufanya uwe kama jangwa, \q2 kama miji ambayo haijakaliwa na watu. \q1 \v 7 Nitawatuma waharibifu dhidi yako, \q2 kila mtu akiwa na silaha zake, \q1 nao watazikata boriti zako bora za mwerezi \q2 na kuzitupa motoni. \p \v 8 “Watu kutoka mataifa mengi watapita karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu amefanya jambo la namna hii kwa mji huu mkubwa?’ \v 9 Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ” \q1 \v 10 Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee; \q2 badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu \q2 yule aliyepelekwa uhamishoni, \q1 kwa sababu kamwe hatairudia \q2 wala kuiona tena nchi yake aliyozaliwa. \m \v 11 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu Shalumu\f + \fr 22:11 \fr*\ft pia anaitwa \ft*\fqa Yehoahazi\fqa*\f* mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. \v 12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.” \q1 \v 13 “Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa dhuluma, \q2 vyumba vyake vya juu kwa udhalimu, \q1 akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo, \q2 bila kuwalipa kwa utumishi wao. \q1 \v 14 Anasema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme, \q2 na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’ \q1 Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa, \q2 huweka kuta za mbao za mwerezi, \q2 na kuzipaka kwa rangi nyekundu. \b \q1 \v 15 “Je, huko kuongeza idadi ya mierezi \q2 kutakufanya uwe mfalme? \q1 Je, baba yako hakula na kunywa? \q2 Alifanya yaliyo sawa na haki, \q2 naye akafanikiwa kwa yote. \q1 \v 16 Aliwatetea maskini na wahitaji, \q2 hivyo yeye akafanikiwa katika yote. \q1 Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu \q2 katika mapato ya udhalimu, \q1 kumwaga damu isiyo na hatia, \q2 na katika uonevu na ukatili.” \m \v 18 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: \q1 “Hawatamwombolezea wakisema: \q2 ‘Ole, ndugu yangu! Ole, dada yangu!’ \q1 Hawatamwombolezea wakisema: \q2 ‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’ \q1 \v 19 Atazikwa maziko ya punda: \q2 ataburutwa na kutupwa \q2 nje ya malango ya Yerusalemu.” \b \q1 \v 20 “Panda Lebanoni ukapige kelele, \q2 sauti yako na isikike huko Bashani, \q1 piga kelele toka Abarimu, \q2 kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa. \q1 \v 21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama, \q2 lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’ \q1 Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako; \q2 hujanitii mimi. \q1 \v 22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote, \q2 na wandani wako wataenda uhamishoni. \q1 Kisha utaaibika na kufedheheka \q2 kwa sababu ya uovu wako wote. \q1 \v 23 Wewe uishiye Lebanoni, \q2 wewe uliyetulia kwenye majengo ya mwerezi, \q1 tazama jinsi utakavyoomboleza \q2 maumivu makali yatakapokupata, \q1 maumivu kama ya mwanamke \q2 mwenye uchungu wa kuzaa! \p \v 24 “Hakika kama niishivyo,” asema Mwenyezi Mungu, “hata kama wewe, Yekonia\f + \fr 22:24 \fr*\ft au \ft*\fqa Konia\fqa*\ft ; pia anaitwa \ft*\fqa Yehoyakini\fqa*\f* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung’oa hapo. \v 25 Nitakutia mikononi mwa wanaoutafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. \v 26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. \v 27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.” \q1 \v 28 Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa, \q2 chungu kilichovunjika, \q2 chombo kisichotakiwa na mtu yeyote? \q1 Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu, \q2 na kutupwa kwenye nchi wasioijua? \q1 \v 29 Ee nchi, nchi, nchi, \q2 sikia neno la Mwenyezi Mungu! \q1 \v 30 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto, \q2 mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote, \q1 kwa maana hakuna mzao wake atakayefanikiwa, \q2 wala kukaa kwenye kiti cha utawala cha Daudi \q2 wala kuendelea kutawala katika Yuda.” \c 23 \s1 Tawi la haki \p \v 1 “Ole wao wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” asema Mwenyezi Mungu. \v 2 Kwa hiyo hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asema Mwenyezi Mungu. \v 3 “Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia, nami nitawarudisha katika malisho yao, ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao. \v 4 Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu asema, “Siku zinakuja, \q2 nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki, \q1 Mfalme atakayetawala kwa hekima, \q2 na kutenda lililo haki na sawa katika nchi. \q1 \v 6 Katika utawala wake., Yuda ataokolewa \q2 na Israeli ataishi salama. \q1 Hili ndilo jina atakaloitwa: \q2 Mwenyezi Mungu ni Haki Yetu.” \b \m \v 7 Mwenyezi Mungu asema, “Hivyo basi, siku zinakuja, ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ \v 8 bali watasema, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.” \s1 Manabii wasemao uongo \p \v 9 Kuhusu manabii: \q1 Moyo wangu umevunjika ndani yangu; \q2 mifupa yangu yote inatetemeka. \q1 Nimekuwa kama mtu aliyelewa, \q2 kama mtu aliyelemewa na divai, \q1 kwa sababu ya Mwenyezi Mungu \q2 na maneno yake matakatifu. \q1 \v 10 Nchi imejaa wazinzi; \q2 kwa sababu ya laana, nchi imekauka, \q2 na malisho ya nyikani yamekauka. \q1 Mwenendo wa manabii ni mbaya \q2 na mamlaka yao si ya haki. \b \q1 \v 11 “Nabii na kuhani wote si wacha Mungu; \q2 hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 12 “Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi, \q2 watafukuziwa mbali gizani \q2 na huko wataanguka. \q1 Nitaleta maafa juu yao \q2 katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 13 “Miongoni mwa manabii wa Samaria \q2 nililiona jambo la kuchukiza: \q1 Walitabiri kwa Baali \q2 na kuwapotosha Israeli watu wangu. \q1 \v 14 Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu \q2 nimeona jambo baya sana: \q1 Wanafanya uzinzi \q2 na kuenenda katika uongo. \q1 Wanatia nguvu mikono ya watenda maovu, \q2 kwa ajili hiyo hakuna yeyote \q2 anayeachana na uovu wake. \q1 Wote wako kama Sodoma kwangu; \q2 watu na Yerusalemu wako kama Gomora.” \p \v 15 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni kuhusu manabii: \q1 “Nitawafanya wale chakula kichungu \q2 na kunywa maji yaliyotiwa sumu, \q1 kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu \q2 kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.” \p \v 16 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Msisikilize wanachowatabiria manabii, \q2 wanawajaza matumaini ya uongo. \q1 Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe, \q2 hayatoki katika kinywa cha Mwenyezi Mungu. \q1 \v 17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi, \q2 ‘Mwenyezi Mungu asema: Mtakuwa na amani.’ \q1 Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao, \q2 wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’ \q1 \v 18 Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Mwenyezi Mungu \q2 ili kuona au kusikia neno lake? \q1 Ni nani aliyesikiliza \q2 na kusikia neno lake? \q1 \v 19 Tazama, dhoruba ya Mwenyezi Mungu \q2 itatokea kwa ghadhabu, \q1 kisulisuli kitazunguka na kuanguka \q2 juu ya vichwa vya waovu. \q1 \v 20 Hasira ya Mwenyezi Mungu haitageuka \q2 hadi amelitimiza kusudi la moyo wake. \q1 Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi. \q1 \v 21 Mimi sikuwatuma manabii hawa, \q2 lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao. \q1 Mimi sikusema nao, \q2 lakini wametabiri. \q1 \v 22 Lakini kama wangesimama barazani pangu, \q2 wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu, \q1 nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya \q2 na kutoka matendo yao maovu. \b \q1 \v 23 “Je, mimi ni Mungu aliye karibu tu, \q2 wala si Mungu aliye pia mbali?” \q2 Mwenyezi Mungu asema. \q1 \v 24 “Je, mtu yeyote aweza kujificha \q2 mahali pa siri nisiweze kumwona?” \q2 Mwenyezi Mungu asema. \q1 “Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?” \q2 Mwenyezi Mungu asema. \p \v 25 “Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ \v 26 Mambo haya yataendelea hata lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe? \v 27 Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau kwa kumwabudu Baali. \v 28 Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema Mwenyezi Mungu. \v 29 “Je, neno langu si kama moto,” asema Mwenyezi Mungu, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande? \p \v 30 “Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asema Mwenyezi Mungu. \v 31 “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotumia ndimi zao wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi Mungu asema.’ \v 32 Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asema Mwenyezi Mungu. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo,” asema Mwenyezi Mungu. \s1 Unabii wa uongo \p \v 33 “Basi watu hawa, au nabii, au kuhani, watakapokuuliza, ‘Ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni nini?’ Wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio ujumbe. Nami nitawavua kama vazi, asema Mwenyezi Mungu.’ \v 34 Nabii, kuhani, au mtu yeyote akisema, ‘Huu ndio ujumbe wa Mwenyezi Mungu,’ nitamwadhibu huyo na nyumba yake. \v 35 Mnaambiana kila mmoja na mwenzake, au kwa mtu wa nyumba yao: ‘Mwenyezi Mungu amejibu nini?’ au ‘Mwenyezi Mungu amesema nini?’ \v 36 Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina ujumbe wa Mwenyezi Mungu,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wetu. \v 37 Hivi ndivyo utakavyoendelea kumuuliza nabii: ‘Mwenyezi Mungu amekujibu nini?’ au ‘Je, Mwenyezi Mungu amesema nini?’ \v 38 Ingawa unadai, ‘Huu ndio ujumbe wa Mwenyezi Mungu,’ asema Mwenyezi Mungu. Ulitumia maneno, ‘Huu ndio ujumbe wa Mwenyezi Mungu,’ Ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu.’ \v 39 Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutenga mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu. \v 40 Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu: yaani aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.” \c 24 \s1 Vikapu viwili vya tini \p \v 1 Baada ya Yekonia\f + \fr 24:1 \fr*\ft au \ft*\fqa Konia\fqa*\ft ; pia anaitwa \ft*\fqa Yehoyakini\fqa*\f* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli na Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Mwenyezi Mungu akanionesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 2 Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama zile za mavuno ya kwanza. Kikapu cha pili kilikuwa na tini dhaifu sana, mbovu mno zisizofaa kuliwa. \p \v 3 Kisha Mwenyezi Mungu akaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?” \p Nikamjibu, “Ninaona tini zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo mbaya, ni mbaya sana zisizofaa kuliwa.” \p \v 4 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likanijia: \v 5 “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo. \v 6 Macho yangu yatakuwa juu yao kwa ajili ya kuwapatia mema, nami nitawarudisha tena katika nchi hii. Nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawang’oa, \v 7 nitawapa moyo wa kunifahamu mimi, kwamba mimi ndimi Mwenyezi Mungu. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, kwa maana watanirudia kwa moyo wote. \p \v 8 “ ‘Lakini kama zilivyo zile tini dhaifu, ambazo ni mbovu mno zisizofaa kuliwa,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘ndivyo nitakavyomtendea Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake, na mabaki wengine kutoka Yerusalemu, wawe wamebaki katika nchi hii, au wanaishi Misri. \v 9 Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, popote nitakapowafukuzia. \v 10 Nitautuma upanga, njaa na tauni dhidi yao hadi wawe wameangamia kutoka nchi niliyowapa wao na baba zao.’ ” \c 25 \s1 Miaka sabini ya kuwa mateka \p \v 1 Neno likamjia Yeremia kuhusu watu wote wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. \v 2 Nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wote wanaoishi Yerusalemu: \v 3 Kwa miaka ishirini na tatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, hadi siku hii ya leo, neno la Mwenyezi Mungu limekuwa likinijia, nami nimesema nanyi mara kwa mara, lakini hamkusikiliza. \p \v 4 Ingawa Mwenyezi Mungu aliwatuma kwenu mara kwa mara watumishi na manabii wake wote, ninyi hamkusikiliza wala hamkujali. \v 5 Walisema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya na matendo yake maovu, ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa ninyi na baba zenu milele. \v 6 Msiifuate miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Msinikasirishe kwa vitu mlivyovitengeneza kwa mikono yenu.” \p \v 7 “Lakini ninyi hamkunisikiliza, tena mkanikasirisha kwa vitu mlivyovitengeneza kwa mikono yenu, nanyi mmejiletea madhara juu yenu wenyewe,” asema Mwenyezi Mungu. \p \v 8 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu, \v 9 nitayaita mataifa yote ya kaskazini na mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawaleta waishambulie nchi hii na wakazi wake wote, na dhidi ya mataifa yote yanayowazunguka. Nitawaangamiza kabisa na kuwafanya kitu cha kuchukiwa na kudharauliwa, na kuwa magofu daima. \v 10 Nitawaondolea sauti ya shangwe na furaha, sauti ya bibi arusi na ya bwana arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na mwanga wa taa. \v 11 Nchi hii yote itakuwa ukiwa na isiyofaa kitu, nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini. \p \v 12 “Miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele. \v 13 Nitaleta juu ya nchi hiyo mambo yote niliyosema dhidi yake, yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki, na kutolewa unabii na Yeremia dhidi ya mataifa yote. \v 14 Wao wenyewe watakuwa watumwa wa mataifa mengi na wafalme wakuu. Nitawalipizia sawasawa na matendo yao na kazi ya mikono yao.” \s1 Kikombe cha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu \p \v 15 Hili ndilo neno ambalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliwaambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote, ninaokutuma kwao. \v 16 Watakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.” \v 17 Hivyo, nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwa Mwenyezi Mungu, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa: \b \li1 \v 18 Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na wakuu wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kutisha, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo; \li1 \v 19 Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote, \v 20 na wageni wote walio huko; \li1 wafalme wote wa nchi ya Usi; \li1 wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni, na watu walioachwa huko Ashdodi); \li1 \v 21 Edomu, Moabu na Amoni; \li1 \v 22 wafalme wote wa Tiro na Sidoni; \li1 wafalme wa nchi za pwani ng’ambo ya bahari; \li1 \v 23 Dedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali; \li1 \v 24 wafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa; \li1 \v 25 wafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi; \li1 \v 26 na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote duniani. \li1 Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshaki\f + \fr 25:26 \fr*\ft Sheshaki ni \ft*\fqa Babeli \fqa*\ft kwa fumbo\ft*\f* atakunywa pia. \b \p \v 27 “Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’ \v 28 Lakini wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Ni lazima mnywe! \v 29 Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta upanga dhidi ya wote wanaoishi duniani, asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.’ \p \v 30 “Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie: \q1 “ ‘Mwenyezi Mungu atanguruma kutoka juu; \q2 atatoa sauti ya ngurumo \q2 kutoka makao yake matakatifu \q1 na kunguruma kwa nguvu sana \q2 dhidi ya nchi yake. \q1 Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu, \q2 atapiga kelele dhidi ya wote wanaoishi katika nchi. \q1 \v 31 Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia, \q2 kwa maana Mwenyezi Mungu ataleta hukumu dhidi ya mataifa; \q1 ataleta hukumu juu ya wanadamu wote \q2 na kuwaua waovu wote kwa upanga,’ ” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 32 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Tazama! Maafa yanaenea \q2 kutoka taifa moja hadi jingine; \q1 tufani kubwa inainuka \q2 kutoka miisho ya dunia.” \m \v 33 Wakati huo, hao waliouawa na Mwenyezi Mungu watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama kinyesi juu ya ardhi. \q1 \v 34 Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji, \q2 mjigaragaze katika majivu, \q2 ninyi viongozi wa kundi. \q1 Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia; \q2 mtaanguka na kuvunjwavunjwa \q2 kama vyombo vizuri vya udongo. \q1 \v 35 Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia, \q2 viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea. \q1 \v 36 Sikia kilio cha wachungaji, \q2 maombolezo ya viongozi wa kundi, \q1 kwa maana Mwenyezi Mungu \q2 anayaharibu malisho yao. \q1 \v 37 Makao yao ya amani yataharibiwa \q2 kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 38 Kama simba ataacha pango lake, \q2 nchi yao itakuwa ukiwa \q1 kwa sababu ya upanga wa mdhalimu, \q2 na kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi Mungu. \c 26 \s1 Yeremia atishiwa kuuawa \p \v 1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Simama katika ua wa nyumba ya Mwenyezi Mungu na useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno. \v 3 Huenda watasikia na kugeuka, kisha kila mmoja kutubu na kuacha njia yake mbaya. Nami nitaghairi kuleta maafa niliyopanga kufanya dhidi yao kwa sababu ya matendo yao maovu. \v 4 Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu niliyoiweka mbele yenu, \v 5 na msipoyasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza), \v 6 ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ” \p \v 7 Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 8 Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kitu Mwenyezi Mungu alichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe! \v 9 Kwa nini unatoa unabii katika jina la Mwenyezi Mungu kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. \p \v 10 Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 11 Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!” \p \v 12 Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Mwenyezi Mungu amenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia. \v 13 Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu, na kumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Ndipo Mwenyezi Mungu atawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu. \v 14 Lakini mimi niko mikononi mwenu; nifanyieni lolote mnaloona kuwa jema na haki. \v 15 Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, kwa kumwaga damu isiyo na hatia, mtakuwa mmejipatia dhambi juu yenu wenyewe, juu ya mji huu, na juu ya wote wanaoishi ndani yake, kwa kuwa ni kweli Mwenyezi Mungu amenituma kwenu ili niseme maneno haya masikioni mwenu.” \p \v 16 Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.” \p \v 17 Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele, wakaliambia kusanyiko lote la watu, \v 18 “Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “ ‘Sayuni italimwa kama shamba, \q2 Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, \q1 na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu \q2 kilichofunikwa na vichaka.’ \m \v 19 Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha Mwenyezi Mungu na kuhitaji msaada wake? Je, Mwenyezi Mungu hakuwahurumia na kughairi maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizi ya kutisha sisi wenyewe!” \p \v 20 Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina la Mwenyezi Mungu. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia. \v 21 Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumuua. Lakini Uria alipata habari, na kwa kuogopa akakimbilia Misri. \v 22 Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria. \v 23 Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimuua kwa upanga, na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo. \p \v 24 Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shafani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe. \c 27 \s1 Yuda kumtumikia Nebukadneza \p \v 1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu\f + \fr 27:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Sedekia\fqa*\f* mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloniambia: “Tengeneza nira, ujivike shingoni mwako, uifunge kwa kamba za ngozi. \v 3 Kisha utume ujumbe kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro na Sidoni kupitia wajumbe ambao wamekuja Yerusalemu kwa Sedekia\f + \fr 27:3 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Yehoyakimu\fqa*\f* mfalme wa Yuda. \v 4 Wape ujumbe kwa ajili ya mabwana zao na uwaambie: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: ‘Waambieni hivi mabwana zenu: \v 5 Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooka nimeumba dunia na watu wake na wanyama walio ndani yake, nami humpa yeyote ninayependa. \v 6 Sasa nitazitia nchi zenu zote mkononi mwa mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, na nitawafanya hata wanyama pori wamtumikie. \v 7 Mataifa yote yatamtumikia yeye, pamoja na mwanawe, na mjukuu wake, hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda. \p \v 8 “ ‘ “Lakini kama kukiwa na taifa lolote au ufalme ambao hautamtumikia Nebukadneza mfalme wa Babeli, ama kuinamisha shingo yake chini ya nira yake, nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa na tauni, asema Mwenyezi Mungu, hadi nitakapoliangamiza taifa hilo kwa mkono wake. \v 9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi: Hamtamtumikia mfalme wa Babeli. \v 10 Wanawatabiria uongo ambao utawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka nchi yenu. Nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia. \v 11 Lakini ikiwa taifa lolote litainama na kuweka shingo yake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asema Mwenyezi Mungu.” ’ ” \p \v 12 Nilitoa ujumbe huo huo kwa Sedekia mfalme wa Yuda. Nilisema, “Ingiza shingo yako katika nira ya mfalme wa Babeli, umtumikie yeye na watu wake, nawe utaishi. \v 13 Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni, ambazo Mwenyezi Mungu ameonya kuhusu taifa lolote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli? \v 14 Msiyasikilize maneno ya manabii wanaowaambia kwamba, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli,’ kwa sababu wanawatabiria uongo. \v 15 ‘Sikuwatuma hao,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ” \p \v 16 Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba ya Mwenyezi Mungu vitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo. \v 17 Msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli, nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu? \v 18 Kama wao ni manabii na wanalo neno la Mwenyezi Mungu, basi na wamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ili vyombo vilivyobaki katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli. \v 19 Kwa maana hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo vinavyoweza kuhamishwa, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu, \v 20 ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli hakuvichukua alipomchukua Yekonia\f + \fr 27:20 \fr*\ft au \ft*\fqa Konia\fqa*\ft ; pia anaitwa \ft*\fqa Yehoyakini\fqa*\f* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda kwenda uhamishoni huko Babeli kutoka Yerusalemu, pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu. \v 21 Naam, hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu vitu ambavyo vimebaki ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, na ndani ya jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, na katika Yerusalemu: \v 22 ‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, na huko vitabaki hadi siku nitakayovijilia,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha mahali hapa.’ ” \c 28 \s1 Hanania nabii wa uongo \p \v 1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mbele ya makuhani na watu wote: \v 2 “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. \v 3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi Mungu ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli. \v 4 Pia nitamrudisha mahali hapa Yekonia\f + \fr 28:4 \fr*\ft au \ft*\fqa Konia\fqa*\ft ; pia anaitwa \ft*\fqa Yehoyakini\fqa*\f* mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walienda Babeli,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’ ” \p \v 5 Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 6 Akasema, “Amen! Mwenyezi Mungu na afanye hivyo! Mwenyezi Mungu na ayatimize maneno ya unabii uliyoyatoa kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya Mwenyezi Mungu na watu wote walio uhamishoni. \v 7 Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote: \v 8 Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa. \v 9 Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa na Mwenyezi Mungu ikiwa unabii wake utatimia.” \p \v 10 Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja, \v 11 naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake. \p \v 12 Kitambo kidogo baada ya nabii Hanania kuivunja nira kutoka shingo ya nabii Yeremia, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia: \v 13 “Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma. \v 14 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Pia nitampa kutawala hata wanyama pori.’ ” \p \v 15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania! Mwenyezi Mungu hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo. \v 16 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Hivi karibuni nitakuondoa duniani. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa. \c 29 \s1 Barua kwa watu wa uhamisho \p \v 1 Haya ndio maneno ya barua ambayo nabii Yeremia aliituma kutoka Yerusalemu kwenda kwa wazee waliobaki miongoni mwa waliopelekwa uhamishoni, na kwa makuhani, manabii na watu wengine wote ambao Nebukadneza alikuwa amewachukua kwenda uhamishoni Babeli kutoka Yerusalemu. \v 2 (Hii ilikuwa ni baada ya Mfalme Yekonia\f + \fr 29:2 \fr*\ft au \ft*\fqa Konia\fqa*\ft ; pia anaitwa \ft*\fqa Yehoyakini\fqa*\f* na mama malkia, maafisa wa mahakama, viongozi wa Yuda na wa Yerusalemu, mafundi na wahunzi kwenda uhamishoni kutoka Yerusalemu.) \v 3 Barua ilikabidhiwa kwa Elasa mwana wa Shafani, na kwa Gemaria mwana wa Hilkia, ambao Sedekia mfalme wa Yuda aliwatuma kwa Mfalme Nebukadneza huko Babeli. Barua yenyewe ilisema: \pm \v 4 Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, awaambialo wale wote niliowapeleka kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli: \v 5 “Jengeni nyumba na mwishi humo, pandeni bustani na mle mazao yake. \v 6 Oeni wake na mzae watoto wa kiume na wa kike; watafutieni wake watoto wenu wa kiume, na waozeni binti zenu ili nao wazae watoto wa kiume na wa kike; mkaongezeke huko, wala msipungue idadi. \v 7 Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. Mwombeni Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mji huo, kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi.” \pm \v 8 Naam, hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: “Msikubali manabii na waaguzi walio miongoni mwenu wawadanganye. Msisikilize ndoto ambazo mmewatia moyo kuota. \v 9 Wanawatabiria ninyi uongo kwa jina langu. Sikuwatuma,” asema Mwenyezi Mungu. \pm \v 10 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Miaka sabini itakapotimia kwa ajili ya Babeli, nitakuja kwenu na kutimiza ahadi yangu ya rehema ya kuwarudisha mahali hapa. \v 11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema Mwenyezi Mungu, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. \v 12 Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. \v 13 Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wote. \v 14 Nitaonekana kwenu,” asema Mwenyezi Mungu, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali nilipokuwa nimewatoa walipopelekwa uhamishoni,” asema Mwenyezi Mungu. \pm \v 15 Mnaweza mkasema, “Mwenyezi Mungu ameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,” \v 16 lakini hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu mfalme aketiye katika kiti cha utawala cha Daudi, na watu wa kwenu wote wanaobaki katika mji huu, ndugu zenu ambao hawakuenda pamoja nanyi uhamishoni. \v 17 Naam, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu zilizooza, zisizofaa kuliwa. \v 18 Nitawafukuza kwa upanga, kwa njaa na kwa tauni, nami nitawafanya kuwa chukizo kwa falme zote za dunia, kitu cha laana na cha kutisha, kisichofaa na cha kuzomewa miongoni mwa mataifa nitakakowafukuzia. \v 19 Kwa kuwa hawakuyasikiliza maneno yangu,” asema Mwenyezi Mungu, “maneno niliyoyatuma kwao mara kwa mara kupitia kwa watumishi wangu manabii. Wala ninyi watu wa uhamisho hamkusikiliza pia,” asema Mwenyezi Mungu. \pm \v 20 Kwa hiyo, sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi nyote mlio uhamishoni, niliowapeleka Babeli kutoka Yerusalemu. \v 21 Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya, na Sedekia mwana wa Maaseya, wanaowatabiria uongo kwa jina langu: “Nitawatia mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atawaua mbele ya macho yenu hasa. \v 22 Kwa ajili yao, watu wote wa Yuda walio uhamishoni Babeli watatumia laana hii: ‘Mwenyezi Mungu na akutendee kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwachoma moto.’ \v 23 Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya. Nami nayajua haya, na ni shahidi wa jambo hilo,” asema Mwenyezi Mungu. \s1 Ujumbe kwa Shemaya \p \v 24 Mwambie Shemaya Mnehelami, \v 25 “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania, \v 26 ‘Mwenyezi Mungu amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu. Unapaswa kumfunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii. \v 27 Kwa nini basi hukumkemea Yeremia Mwanathothi, aliyejifanya kama nabii miongoni mwenu? \v 28 Ametutumia ujumbe huu huku Babeli: Mtakuwa huko muda mrefu. Kwa hiyo jengeni nyumba mkakae; pandeni mashamba na mle mazao yake.’ ” \p \v 29 Kuhani Sefania, hata hivyo, akamsomea nabii Yeremia ile barua. \v 30 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 31 “Tuma ujumbe huu kwa watu wote walio uhamishoni kusema: ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, hata ingawa sikumtuma, naye amewafanya kuamini uongo, \v 32 hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asema Mwenyezi Mungu, kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ” \c 30 \s1 Kurejeshwa kwa Israeli \p \v 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Andika katika kitabu maneno yote niliyonena na wewe. \v 3 Siku zinakuja,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema Mwenyezi Mungu.” \p \v 4 Haya ndio maneno aliyoyanena Mwenyezi Mungu kuhusu Israeli na Yuda: \v 5 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Vilio vya woga vinasikika: \q2 hofu kuu, wala si amani. \q1 \v 6 Ulizeni na mkaone: \q2 Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? \q1 Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu \q2 ameweka mikono yake tumboni \q1 kama mwanamke aliye na uchungu wa kuzaa, \q2 kila uso ukigeuka rangi kabisa? \q1 \v 7 Ole! Kwa kuwa siku ile itakuwa ya kutisha. \q2 Hakutakuwa na nyingine kama hiyo. \q1 Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo, \q2 lakini ataokolewa kutoka dhiki hiyo. \b \q1 \v 8 “ ‘Katika siku ile,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 ‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwao \q1 na kuvipasua vifungo vyao; \q2 wageni hawatawafanya tena watumwa. \q1 \v 9 Badala yake, watamtumikia Mwenyezi Mungu, Mungu wao, \q2 na Daudi mfalme wao, \q2 nitakayemwinua kwa ajili yao. \b \q1 \v 10 “ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, \q2 usifadhaike, ee Israeli,’ \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 ‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali, \q2 wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. \q1 Yakobo atakuwa tena na amani na usalama, \q2 wala hakuna atakayemtia hofu. \q1 \v 11 Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’ \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 ‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote \q2 nilikokuwa nimewatawanya, \q2 sitawaangamiza ninyi kabisa. \q1 Nitawaadhibu, lakini kwa haki. \q2 Sitawaacha kabisa bila adhabu.’ \p \v 12 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Kidonda chako hakina dawa, \q2 jeraha lako haliponyeki. \q1 \v 13 Hakuna yeyote wa kukutetea katika shauri lako, \q2 hakuna dawa ya kidonda chako, \q2 wewe hutapona. \q1 \v 14 Wale walioungana nawe wote wamekusahau, \q2 hawajali chochote kukuhusu wewe. \q1 Nimekupiga vile adui angekupiga, \q2 na kukuadhibu vile mtu mkatili angekuadhibu, \q1 kwa sababu hatia yako ni kubwa mno, \q2 na dhambi zako ni nyingi sana. \q1 \v 15 Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako, \q2 yale maumivu yako yasiyoponyeka? \q1 Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyingi \q2 nimekufanyia mambo haya. \b \q1 \v 16 “ ‘Lakini watu wote wakuangamizao wataangamizwa; \q2 adui zako wote wataenda uhamishoni. \q1 Wale wote wakutekao nyara watatekwa nyara; \q2 wote wakufanyao mateka nitawafanya mateka. \q1 \v 17 Lakini nitakurudishia afya yako \q2 na kuyaponya majeraha yako,’ \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 ‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa, \q2 Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’ \p \v 18 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo, \q2 na kuhurumia maskani zake. \q1 Mji utajengwa tena juu ya magofu yake, \q2 nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi. \q1 \v 19 Nyimbo za kushukuru zitatoka kwao \q2 na sauti ya furaha. \q1 Nitaiongeza idadi yao \q2 wala hawatapungua, \q1 nitawapa heshima \q2 na hawatadharauliwa. \q1 \v 20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa \q2 siku za zamani, \q1 nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu; \q2 nitawaadhibu wote wanaowadhulumu. \q1 \v 21 Mmoja wao atakuwa kiongozi wao; \q2 mtawala wao atainuka miongoni mwao. \q1 Nitamleta karibu nami, \q2 naye atanikaribia mimi, \q1 kwa maana ni nani yule atakayejitolea \q2 kuwa karibu nami?’ \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 22 ‘Kwa hiyo ninyi mtakuwa watu wangu, \q2 nami nitakuwa Mungu wenu.’ ” \b \q1 \v 23 Tazama, tufani ya Mwenyezi Mungu \q2 italipuka kwa ghadhabu, \q1 upepo wa kisulisuli uendao kasi \q2 utashuka juu ya vichwa vya waovu. \q1 \v 24 Hasira kali ya Mwenyezi Mungu haitarudi nyuma \q2 hadi atakapotimiza makusudi yote ya moyo wake. \q1 Siku zijazo \q2 mtayaelewa haya. \c 31 \s1 Mahamisho kurudi kwa shangwe \p \v 1 “Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu,” asema Mwenyezi Mungu. \p \v 2 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Watu watakaopona upanga \q2 watapata upendeleo jangwani; \q2 nitakuja niwape Israeli pumziko.” \p \v 3 Mwenyezi Mungu alitutokea zamani, akisema: \q1 “Nimekupenda kwa upendo wa milele, \q2 nimekuvuta kwa wema. \q1 \v 4 Nitakujenga tena, nawe utajengeka upya, \q2 ewe Bikira Israeli. \q1 Utachukua tena matari yako \q2 na kwenda kucheza na wanaofurahi. \q1 \v 5 Utapanda tena shamba la mizabibu \q2 juu ya vilima vya Samaria, \q1 wakulima watapanda \q2 na kufurahia matunda yake. \q1 \v 6 Siku inakuja ambapo walinzi watapiga kelele \q2 juu ya vilima vya Efraimu, wakisema, \q1 ‘Njooni, twendeni juu Sayuni, \q2 kwake Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.’ ” \p \v 7 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Mwimbieni Yakobo kwa furaha, \q2 mshangilieni aliye mkuu wa mataifa. \q1 Zifanyeni sifa zenu zisikike, nanyi mseme, \q2 ‘Ee Mwenyezi Mungu, okoa watu wako, \q2 mabaki ya Israeli.’ \q1 \v 8 Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini \q2 na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia. \q1 Miongoni mwao watakuwa vipofu na viwete, \q2 mama wajawazito na wenye uchungu wa kuzaa. \q2 Umati mkubwa wa watu watarudi. \q1 \v 9 Watakuja wakilia; \q2 wataomba wakati ninawarudisha. \q1 Nitawaongoza kando ya vijito vya maji, \q2 katika njia iliyonyooka hawatajikwaa, \q1 kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, \q2 naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza. \b \q1 \v 10 “Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi mataifa, \q2 litangazeni katika nchi za pwani ya mbali: \q1 ‘Yeye aliyewatawanya Israeli atawakusanya \q2 na atalichunga kundi lake la kondoo kama mchungaji.’ \q1 \v 11 Mwenyezi Mungu atamlipia fidia Yakobo \q2 na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao. \q1 \v 12 Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni; \q2 watashangilia ukarimu wa Mwenyezi Mungu: \q1 nafaka, divai mpya na mafuta, \q2 wana-kondoo wachanga \q2 na ndama wa makundi ya ng’ombe nitakaowapa. \q1 Watakuwa kama bustani iliyoneshewa vizuri, \q2 wala hawatahuzunika tena. \q1 \v 13 Kisha wanawali watacheza na kufurahi, \q2 vijana wa kiume na wazee pia. \q1 Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha, \q2 nitawapa faraja na furaha badala ya huzuni. \q1 \v 14 Nitawashibisha makuhani kwa wingi, \q2 nao watu wangu watajazwa kwa ukarimu wangu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 15 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Sauti imesikika huko Rama, \q2 maombolezo na kilio kikubwa, \q1 Raheli akiwalilia watoto wake \q2 na anakataa kufarijiwa, \q2 kwa sababu watoto wake hawako tena.” \p \v 16 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Izuie sauti yako kulia, \q2 na macho yako yasitoe machozi, \q1 kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Watarudi kutoka nchi ya adui. \q1 \v 17 Kwa hiyo kuna tumaini kwa siku zijazo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Watoto wako watarudi nchi yao yenyewe. \b \q1 \v 18 “Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu: \q2 ‘Ulinirudi kama ndama mkaidi, \q2 nami nimekubali kutii. \q1 Unirudishe, nami nitarudi, \q2 kwa sababu wewe ndiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. \q1 \v 19 Baada ya kupotea, nilitubu; \q2 baada ya kuelewa, nilijipiga kifua. \q1 Niliaibika na kuona haya \q2 kwa sababu niliibeba aibu ya ujana wangu.’ \q1 \v 20 Je, Efraimu si mwanangu mpendwa, \q2 mtoto ninayependezwa naye? \q1 Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake, \q2 bado ninamkumbuka. \q1 Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku, \q2 nina huruma kubwa kwa ajili yake,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 21 “Weka alama za barabara, \q2 weka vibao vya kuelekeza. \q1 Zingatia vyema njia kuu, \q2 barabara ile unayoipita. \q1 Rudi, ee Bikira Israeli, \q2 rudi kwenye miji yako. \q1 \v 22 Utatangatanga hata lini, \q2 ee binti usiye mwaminifu? \q1 Mwenyezi Mungu ameumba kitu kipya duniani: \q2 mwanamke atamlinda mwanaume.” \p \v 23 Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo, “Nitakapowarudisha toka nchi ya kutekwa kwenu, watu walio katika nchi ya Yuda na miji yake kwa mara nyingine tena watatumia maneno haya: ‘Mwenyezi Mungu akubariki, ee makao ya haki, ee mlima mtakatifu.’ \v 24 Watu wataishi pamoja katika Yuda na miji yake yote, wakulima na wote wanaohamahama na mifugo yao. \v 25 Nitawaburudisha waliochoka na kuwatuliza walio na huzuni.” \p \v 26 Kwa jambo hili niliamka na kuangalia pande zote. Usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu. \p \v 27 Mwenyezi Mungu asema, “Siku zinakuja, nitakapoongeza idadi ya watu, na kuzidisha hesabu ya mifugo katika nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. \v 28 Kama vile nilivyowaangalia ili kung’oa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema Mwenyezi Mungu. \v 29 “Katika siku hizo, watu hawatasema tena, \q1 “ ‘Baba wamekula zabibu chachu, \q2 nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’ \m \v 30 Badala yake, kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe; yeyote alaye zabibu chachu, meno yake mwenyewe yatatiwa ganzi. \q1 \v 31 “Siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, \q2 “nitakapofanya agano jipya \q1 na nyumba ya Israeli \q2 na nyumba ya Yuda. \q1 \v 32 Halitafanana na agano \q2 nililofanya na baba zao \q1 wakati nilipowashika mkono \q2 kuwaongoza watoke Misri, \q1 kwa sababu walivunja agano langu, \q2 ijapokuwa nilikuwa mume kwao,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 33 “Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli \q2 baada ya siku zile,” asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Nitaweka sheria yangu katika nia zao, \q2 na kuiandika mioyoni mwao. \q1 Nitakuwa Mungu wao, \q2 nao watakuwa watu wangu. \q1 \v 34 Mtu hatamfundisha tena jirani yake, \q2 wala mtu kumfundisha ndugu yake, akisema, \q2 ‘Mjue Mwenyezi Mungu,’ \q1 kwa sababu wote watanijua mimi, \q2 kuanzia aliye mdogo hata aliye mkubwa kuliko wote,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena.” \p \v 35 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, \q1 yeye aliyefanya jua \q2 liwake mchana, \q1 yeye anayeamuru mwezi na nyota \q2 kung’aa usiku, \q1 yeye anayeichafua bahari \q2 ili mawimbi yake yangurume; \q2 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 ndilo jina lake: \q1 \v 36 “Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “ndipo wazao wa Israeli watakoma \q2 kuwa taifa mbele yangu daima.” \p \v 37 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Ikiwa mbingu zilizo juu zitaweza kupimika \q2 na misingi ya dunia chini \q2 ikaweza kuchunguzwa, \q1 ndipo nitakapowakataa wazao wote wa Israeli \q2 kwa sababu ya yote waliyoyatenda,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 38 “Siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “mji huu utakapojengwa upya kwa ajili yangu, kuanzia mnara wa Hananeli hadi Lango la Pembeni. \v 39 Kamba ya kupimia itaanzia hapo kuendelea hadi kwenye kilima cha Garebu, na kisha kugeuka kuelekea Goa, \v 40 wanakotupa maiti na majivu, na maeneo yote kuanzia Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi patakuwa mahali patakatifu kwa Mwenyezi Mungu. Mji huu kamwe hautang’olewa wala kubomolewa tena.” \c 32 \s1 Yeremia anunua shamba \p \v 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, katika mwaka wa kumi wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Nebukadneza. \v 2 Wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzingira mji wa Yerusalemu, naye nabii Yeremia alikuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi katika jumba la kifalme la Yuda. \p \v 3 Basi Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga huko akisema, “Kwa nini unatabiri hivyo? Wewe unasema, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ninakaribia kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteka. \v 4 Sedekia mfalme wa Yuda hataweza kuponyoka mikononi mwa Wakaldayo, lakini kwa hakika atatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atazungumza naye ana kwa ana na kumwona kwa macho yake mwenyewe. \v 5 Atamchukua Sedekia hadi Babeli, mahali atakapoishi hadi nitakapomshughulikia, asema Mwenyezi Mungu. Kama utapigana dhidi ya Wakaldayo, hutashinda.’ ” \p \v 6 Yeremia akasema, “Neno la Mwenyezi Mungu lilinijia kusema: \v 7 Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako atakuja kwako na kusema, ‘Nunua shamba langu huko Anathothi, kwa sababu wewe kama jamaa ya karibu ni haki na wajibu wako kulikomboa.’ \p \v 8 “Kisha, kama Mwenyezi Mungu alivyosema, binamu yangu Hanameli alinijia katika ua wa walinzi na kusema: ‘Nunua shamba langu lililoko Anathothi katika nchi ya Benyamini. Kwa kuwa ni haki yako kulikomboa na kulimiliki, jinunulie.’ \p “Nilijua kwamba hili lilikuwa neno la Mwenyezi Mungu. \v 9 Hivyo nikalinunua shamba hilo lililoko Anathothi kutoka kwa binamu yangu Hanameli, nami nikampimia shekeli kumi na saba\f + \fr 32:9 \fr*\ft Shekeli 17 ni sawa na gramu 200.\ft*\f* za fedha. \v 10 Nikatia sahihi na kuweka muhuri hati ya kumiliki, nikaweka mashahidi, na kupima ile fedha kwenye mizani. \v 11 Nikachukua ile hati ya kununulia, nakala iliyotiwa muhuri yenye makubaliano na masharti, pia pamoja na ile nakala isiyo na muhuri, \v 12 nami nikampa Baruku mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, hati hii mbele ya binamu yangu Hanameli, na mbele ya mashahidi waliokuwa wameweka sahihi kwenye hati hii na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ua wa walinzi. \p \v 13 “Nilimpa Baruku maelezo haya mbele yao: \v 14 ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Chukua hati hizi, yaani nakala zote zenye muhuri na zisizo na muhuri za hati ya kununulia, na uziweke kwenye gudulia la udongo wa mfinyanzi ili zidumu kwa muda mrefu. \v 15 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Nyumba, mashamba na mashamba ya mizabibu yatanunuliwa tena katika nchi hii.’ \p \v 16 “Baada ya kumkabidhi Baruku mwana wa Neria hii hati ya kununulia, nilimwomba Mwenyezi Mungu: \pm \v 17 “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza. \v 18 Wewe huonesha upendo kwa maelfu, lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \v 19 mashauri yako ni makuu, na matendo yako ni yenye uwezo. Macho yako yanaona njia zote za wanadamu, nawe humlipa kila mmoja kulingana na mwenendo wake, na kwa kadri ya matendo yake. \v 20 Ulitenda ishara za miujiza na maajabu huko Misri, na unafanya hivyo hadi leo, katika Israeli na miongoni mwa wanadamu wote, nawe umejulikana na kufahamika hivyo hadi leo. \v 21 Uliwatoa watu wako Israeli kutoka Misri kwa ishara na maajabu, kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa na kwa utisho mkuu. \v 22 Uliwapa nchi hii uliyokuwa umeapa kuwapa baba zao, nchi inayotiririka maziwa na asali. \v 23 Waliingia na kuimiliki, lakini hawakukutii wala kuifuata sheria yako. Hawakufanya kile ulichowaamuru kufanya. Hivyo ukaleta maafa haya yote juu yao. \pm \v 24 “Tazama jinsi jeshi lilivyouzingira mji huu ili kuuteka. Kwa sababu ya upanga, njaa, na tauni, mji utatiwa mkononi mwa Wakaldayo wanaoushambulia. Ulilolisema limetokea kama unavyoona. \v 25 Ingawa mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo, wewe, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, uliniambia, ‘Nunua shamba kwa fedha mbele ya mashahidi.’ ” \p \v 26 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 27 “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza? \v 28 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa Wakaldayo, na mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ambaye atauteka. \v 29 Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine. \p \v 30 “Watu wa Israeli na wa Yuda hawakufanya kitu kingine ila uovu mbele zangu tangu ujana wao. Naam, watu wa Israeli hawakufanya kitu kingine ila kunikasirisha kwa kazi ambazo mikono yao imetengeneza, asema Mwenyezi Mungu. \v 31 Tangu siku ulipojengwa hadi sasa, mji huu umenikasirisha na kunighadhibisha kiasi kwamba ni lazima niuondoe machoni pangu. \v 32 Watu wa Israeli na wa Yuda wamenikasirisha kwa uovu wote waliofanya: wao, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao, watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. \v 33 Walinigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao. Ingawa niliwafundisha tena na tena, hawakupenda kusikiliza wala kuitikia adhabu. \v 34 Waliweka miungu yao ya kuchukiza sana katika nyumba iitwayo kwa Jina langu na kuinajisi. \v 35 Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia Baali katika Bonde la Ben-Hinomu, ambapo waliwatoa kafara watoto wao wa kiume na wa kike kwa Moleki, ingawa kamwe sikuwaamuru, wala sikuwaza kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi. \p \v 36 “Mnasema kuhusu mji huu, ‘Kwa upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli,’ lakini hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: \v 37 Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi salama. \v 38 Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. \v 39 Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao. \v 40 Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili wasinigeuke. \v 41 Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote. \p \v 42 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Kama nilivyoleta maafa haya makubwa kwa watu hawa, ndivyo nitakavyowapa mafanikio niliyowaahidi. \v 43 Kwa mara nyingine tena mashamba yatanunuliwa katika nchi hii ambayo mlisema, ‘Imekuwa ukiwa, isiyo na watu wala wanyama, kwa sababu imetiwa mikononi mwa Wakaldayo.’ \v 44 Mashamba yatanunuliwa kwa fedha, na hati zitatiwa sahihi, zitatiwa muhuri na kushuhudiwa katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, katika miji ya Yuda na katika miji ya nchi ya vilima, sehemu za magharibi katika miji ya tambarare na katika Negebu, kwa sababu nitarudisha tena mafanikio yao\f + \fr 32:44 \fr*\ft au \ft*\fqa kwa sababu nitawarudisha tena kutoka utumwani\fqa*\f*, asema Mwenyezi Mungu.” \c 33 \s1 Ahadi ya kurejeshwa \p \v 1 Yeremia alipokuwa angali amefungwa kwenye ua wa walinzi, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia mara ya pili kusema: \v 2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, yeye aliyeumba dunia, Mwenyezi Mungu aliyeifanya na kuithibitisha, Mwenyezi Mungu ndilo jina lake: \v 3 ‘Niite, nami nitakuitikia, nitakuonesha mambo makubwa, yasiyochunguzika na usiyoyajua.’ \v 4 Kwa maana hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba zilizo mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda, zote ambazo zimebomolewa ili zitumiwe kupinga kuzingirwa na jeshi na dhidi ya upanga \v 5 katika kupigana na Wakaldayo: ‘Zitajazwa na maiti za watu nitakaowangamiza kwa hasira na ghadhabu yangu. Nitauficha uso wangu kwa sababu ya maovu yake yote. \p \v 6 “ ‘Hata hivyo, nitauletea afya na uponyaji, nitawaponya watu wangu na kuwafanya wafurahie amani tele na salama. \v 7 Nitawarudisha Yuda na Israeli kutoka uhamishoni, na kuwajenga tena kama walivyokuwa hapo awali. \v 8 Nitawatakasa dhambi zote walizofanya dhidi yangu, na nitawasamehe dhambi zote za uasi dhidi yangu. \v 9 Kisha mji huu utaniletea utukufu, furaha, sifa na heshima mbele ya mataifa yote ya dunia yatakayosikia mambo yote mazuri ninayoufanyia. Nao watashangaa na kutetemeka kwa ajili ya wingi wa mafanikio na amani nitakayoupatia.’ \p \v 10 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Mnasema kuhusu mahali hapa kwamba, “Ni mahali palipoachwa ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama.” Lakini katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu ambazo zimeachwa, ambazo hazikaliwi na wanadamu wala wanyama, huko kutasikika kwa mara nyingine \v 11 sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi arusi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, wakisema, \q1 “ ‘ “Mshukuruni Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema; \q2 fadhili zake zadumu milele.” \m Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama ilivyokuwa hapo awali,’ asema Mwenyezi Mungu. \p \v 12 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Mahali hapa, palipo ukiwa, bila wanadamu wala wanyama: katika miji yake, yatakuwa tena malisho ya wachungaji kuyalaza makundi yao. \v 13 Katika miji ya nchi ya vilima, ya vilima vya magharibi na ya Negebu, katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mkono wa yeye anayehesabu,’ asema Mwenyezi Mungu. \p \v 14 “ ‘Siku zinakuja,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘wakati nitakapotimiza ahadi yangu ya rehema niliyoifanya kwa nyumba ya Israeli na kwa nyumba ya Yuda. \q1 \v 15 “ ‘Katika siku hizo na wakati huo \q2 nitalifanya Tawi la haki lichipuke kutoka ukoo wa Daudi, \q1 naye atafanya lile lililo haki na sawa \q2 katika nchi. \q1 \v 16 Katika siku hizo, Yuda ataokolewa \q2 na Yerusalemu ataishi salama. \q1 Hili ndilo jina atakaloitwa: \q2 Mwenyezi Mungu ni Haki Yetu.’ \m \v 17 Kwa maana hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Daudi kamwe hatakosa mtu wa kukalia kiti cha utawala cha nyumba ya Israeli, \v 18 wala makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, sadaka ya nafaka, na dhabihu.’ ” \p \v 19 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 20 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake, \v 21 basi agano langu na Daudi mtumishi wangu, na agano langu na Walawi ambao ni makuhani wanaohudumu mbele zangu, linaweza kuvunjwa, na Daudi hatakuwa tena na mzao wa kutawala kwenye kiti chake cha utawala. \v 22 Nitawafanya wazao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi wanaohudumu mbele zangu wengi, wasioweza kuhesabika kama nyota za angani, tena wasiopimika kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.’ ” \p \v 23 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 24 “Je, hujasikia kwamba watu hawa wanasema, ‘Mwenyezi Mungu amezikataa zile falme mbili alizozichagua’? Kwa hiyo wamewadharau watu wangu, na hawawaoni tena kama taifa. \v 25 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Kama sijathibitisha agano langu na usiku na mchana, na kuziweka wakfu sheria za mbingu na nchi, \v 26 basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala wazao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ” \c 34 \s1 Onyo kwa Sedekia \p \v 1 Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote, pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walikuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote iliyoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \v 2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nenda kwa Sedekia mfalme wa Yuda umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto. \v 3 Hutaweza kuepuka mkono wake, bali hakika utatekwa na kukabidhiwa kwake. Utamwona mfalme wa Babeli kwa macho yako mwenyewe, naye atazungumza nawe ana kwa ana. Nawe utaenda Babeli. \p \v 4 “ ‘Lakini sikia ahadi ya Mwenyezi Mungu, ee Sedekia mfalme wa Yuda. Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu wewe: Hutakufa kwa upanga, \v 5 bali utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee Mwenyezi Mungu!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 6 Ndipo nabii Yeremia akamwambia Sedekia mfalme wa Yuda mambo haya yote huko Yerusalemu, \v 7 wakati jeshi la mfalme wa Babeli lilipokuwa likipigana dhidi ya Yerusalemu na miji mingine ya Yuda iliyokuwa bado imara, yaani Lakishi na Azeka. Hii ilikuwa miji pekee yenye ngome iliyobaki katika Yuda. \s1 Uhuru kwa watumwa \p \v 8 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, baada ya Mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote huko Yerusalemu ili kutangaza uhuru kwa watumwa. \v 9 Kila mmoja alipaswa kuwaacha huru watumwa wake Waebrania, wanawake na wanaume. Hakuna yeyote aliyeruhusiwa kumfanya Myahudi mwenzake kuwa mtumwa. \v 10 Kwa hiyo maafisa wote na watu walioingia katika agano hili wakakubali kwamba watawaacha huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na hawatawashikilia tena. Wakakubali na wakawaacha huru. \v 11 Lakini baadaye wakabadili mawazo yao, na kuwarudisha wale watumwa waliokuwa wamewaacha huru, wakawafanya tena watumwa. \p \v 12 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 13 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nilifanya agano na baba zenu nilipowatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. Nilisema, \v 14 ‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu ni lazima amwache huru mtumwa ambaye ni Mwebrania mwenzenu aliyejiuza kwenu. Baada ya kukutumikia kwa miaka sita, ni lazima umwache huru aende zake.’ Hata hivyo baba zenu hawakunisikiliza wala kunijali. \v 15 Hivi karibuni tu mlitubu na kufanya yaliyo sawa machoni pangu: Kila mmoja wenu aliwatangazia uhuru Waebrania wake. Hata mlifanya agano mbele zangu ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu. \v 16 Lakini sasa mmegeuka na kulinajisi jina langu. Kila mmoja wenu amemrudisha mtumwa wa kiume na wa kike ambao mlikuwa mmewaacha huru waende zao walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa wenu tena. \p \v 17 “Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Hamkunitii mimi. Hamkutangaza uhuru kwa ndugu zenu. Hivyo sasa, ninawatangazia ninyi ‘uhuru,’ asema Mwenyezi Mungu: ‘uhuru’ ili kuanguka kwa upanga, tauni na njaa. Nitawafanya mwe chukizo kwa falme zote za dunia. \v 18 Watu waliovunja agano langu, na ambao hawakutunza masharti ya agano walilofanya mbele zangu, nitawafanya kama ndama waliyemkata vipande viwili, kisha wakatembea kati ya vile vipande vya huyo ndama. \v 19 Viongozi wa Yuda na Yerusalemu, maafisa wa mahakama, makuhani na watu wote wa nchi waliopita kati ya vile vipande vya ndama, \v 20 nitawatia mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao. Maiti zao zitakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi. \p \v 21 “Nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda na maafisa wake mikononi mwa adui zao wanaotafuta uhai wao, kwa jeshi la mfalme wa Babeli, lililokuwa limeondoka kwenu. \v 22 Nitatoa amri, asema Mwenyezi Mungu, nami nitawarudisha tena katika mji huu. Watapigana dhidi yake, wautwae na kuuteketeza kwa moto. Nami nitaiangamiza miji ya Yuda ili pasiwe na yeyote atakayeweza kuishi humo.” \c 35 \s1 Warekabi wasifiwa \p \v 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: \v 2 “Nenda kwa jamaa ya Warekabi, uwaalike waje kwenye moja ya vyumba vya pembeni vya nyumba ya Mwenyezi Mungu, na uwape divai wanywe.” \p \v 3 Basi nikaenda kumwita Yaazania mwana wa Yeremia, mwana wa Habazinia, na ndugu zake na wanawe wote, yaani jamaa nzima ya Warekabi. \v 4 Nikawaleta katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, ndani ya chumba cha wana wa Hanani mwana wa Igdalia mtu wa Mungu. Kilikuwa karibu na chumba cha maafisa, kilichokuwa juu ya kile cha Maaseya mwana wa Shalumu, aliyekuwa bawabu. \v 5 Kisha nikaweka mabakuli yaliyojaa divai na baadhi ya vikombe mbele ya watu wa jamaa ya Warekabi na kuwaambia, “Kunyweni divai.” \p \v 6 Lakini wao wakajibu, “Sisi hatunywi divai, kwa sababu baba yetu Yonadabu mwana wa Rekabu, alitupatia agizo hili: ‘Ninyi wala wazao wenu msinywe divai. \v 7 Pia msijenge nyumba wala kuotesha mbegu au kupanda mashamba ya mizabibu. Kamwe msiwe na kitu chochote katika hivi, bali mtaishi katika mahema. Ndipo mtakapoishi kwa muda mrefu katika nchi ambayo ninyi ni wahamiaji.’ \v 8 Tumetii kila kitu ambacho baba yetu Yonadabu mwana wa Rekabu alituamuru. Sisi wenyewe, wake zetu, watoto wetu wa kiume na wa kike hatujawahi kunywa divai, \v 9 wala kujenga nyumba za kuishi au kuwa na mashamba ya mizabibu, mashamba au mazao. \v 10 Tumeishi katika mahema na tumetii kikamilifu kila kitu alichotuamuru baba yetu Yonadabu. \v 11 Lakini wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi hii, tulisema, ‘Njooni, lazima twende Yerusalemu ili kukimbia majeshi ya Wakaldayo na ya Washamu.’ Kwa hiyo tumeishi Yerusalemu.” \p \v 12 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 13 “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, aliye Mungu wa Israeli, asemalo: Nenda ukawaambie watu wa Yuda na watu wa Yerusalemu, ‘Je, hamwezi kujifunza kutoka kwa wana wa Rekabu, na kuyatii maneno yangu?’ asema Mwenyezi Mungu. \v 14 ‘Yonadabu mwana wa Rekabu aliwaagiza wanawe wasinywe divai, na agizo hilo wamelishika. Hadi leo hawanywi divai, kwa sababu wanatii amri ya baba yao. Nimenena nanyi tena na tena, lakini hamkunitii. \v 15 Mara kwa mara nimewatuma kwenu watumishi wangu wote, manabii wakisema, “Geukeni, kila mmoja aiache njia yake mbaya, na kutengeneza matendo yake. Msiifuate wala kuitumikia miungu mingine. Ndipo mtakapoishi katika nchi niliyowapa ninyi na baba zenu.” Lakini hamkujali wala kunisikiliza. \v 16 Wazao wa Yonadabu mwana wa Rekabu walitimiza amri ambayo baba yao aliwapa, lakini watu hawa hawakunitii mimi.’ \p \v 17 “Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Sikilizeni! Nitaleta juu ya Yuda na juu ya kila mmoja aishiye Yerusalemu kila aina ya maafa niliyotamka dhidi yao. Nilinena nao, lakini hawakusikiliza. Niliwaita, lakini hawakujibu.’ ” \p \v 18 Kisha Yeremia akaiambia jamaa ya Warekabi, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: ‘Mmetii amri ya baba yenu Yonadabu, na mmefuata mafundisho yake yote na mmefanya kila kitu alichowaamuru.’ \v 19 Kwa hiyo hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Yonadabu mwana wa Rekabu hatakosa kamwe kuwa na mtu wa kunitumikia mimi.’ ” \c 36 \s1 Yehoyakimu achoma kitabu cha Yeremia \p \v 1 Katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia nabii Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kusema: \v 2 “Chukua kitabu uandike ndani yake maneno yote niliyonena nawe kuhusu Israeli, Yuda na mataifa mengine yote, tangu nilipoanza kunena nawe wakati wa utawala wa Yosia hadi sasa. \v 3 Labda watu wa Yuda watakaposikia maafa ninayokusudia kuwapiga nayo, kila mmoja wao atageuka kutoka njia zake mbaya, kisha nitasamehe uovu wao na dhambi yao.” \p \v 4 Hivyo Yeremia akamwita Baruku mwana wa Neria, naye Yeremia alipokuwa akiyakariri maneno yote aliyoyasema Mwenyezi Mungu, Baruku akayaandika katika kitabu. \v 5 Kisha Yeremia akamwambia Baruku, “Nimezuiliwa; mimi siwezi kuingia katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 6 Basi wewe nenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu siku ya kufunga, uwasomee watu maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka kitabu hiki yale uliyoyaandika kutoka kinywani mwangu. Wasomee watu wote wa Yuda waliofika kutoka miji yao. \v 7 Labda wataomba na kusihi mbele za Mwenyezi Mungu na kila mmoja akageuka kutoka njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na Mwenyezi Mungu ni kubwa.” \p \v 8 Baruku mwana wa Neria akafanya kila kitu nabii Yeremia alichomwambia kufanya. Alisoma maneno ya Mwenyezi Mungu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu kutoka kile kitabu. \v 9 Katika mwezi wa tisa wa mwaka wa tano wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati wa kufunga mbele za Mwenyezi Mungu, ilitangazwa kwa watu wote waliokuwa Yerusalemu, na wale wote waliokuwa wamekuja kutoka miji ya Yuda. \v 10 Kutoka chumba cha Gemaria mwana wa Shafani mwandishi, kilichokuwa katika ua wa juu kwenye ingilio la Lango Jipya la Hekalu, Baruku akawasomea watu wote waliokuwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu maneno ya Yeremia katika kile kitabu. \p \v 11 Basi Mikaya mwana wa Gemaria, mwana wa Shafani, aliposikia maneno yote ya Mwenyezi Mungu kutoka kile kitabu, \v 12 alishuka hadi chumba cha mwandishi kwenye jumba la kifalme, mahali walipokuwa wameketi maafisa wote: yaani Elishama mwandishi, Delaya mwana wa Shemaya, Elnathani mwana wa Akbori, Gemaria mwana wa Shafani, Sedekia mwana wa Hanania, na maafisa wengine wote. \v 13 Baada ya Mikaya kuwaambia kila kitu ambacho alikuwa amesikia Baruku akiwasomea watu katika kile kitabu, \v 14 maafisa wote wakamtuma Yehudi mwana wa Nethania, mwana wa Shelemia, mwana wa Kushi, kumwambia Baruku, “Leta hicho kitabu ambacho umewasomea watu, nawe mwenyewe uje.” Ndipo Baruku mwana wa Neria akawaendea akiwa na hicho kitabu mkononi mwake. \v 15 Wakamwambia, “Tafadhali, keti na utusomee hicho kitabu.” \p Ndipo Baruku akawasomea kile kitabu. \v 16 Walipoyasikia maneno hayo yote, wakatazamana wao kwa wao kwa woga na kumwambia Baruku, “Lazima tutoe taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme.” \v 17 Kisha wakamuuliza Baruku, “Tuambie, uliandikaje haya yote? Je, yalitoka kinywani mwa Yeremia?” \p \v 18 Baruku akajibu, “Ndiyo, maneno haya yote yalitoka kinywani mwa Yeremia, nami nikayaandika kwa wino katika hiki kitabu.” \p \v 19 Ndipo wale maafisa wakamwambia Baruku, “Wewe na Yeremia nendeni mkajifiche. Mtu yeyote asijue mahali mlipo.” \p \v 20 Baada ya kuhifadhi kile kitabu ndani ya chumba cha Elishama mwandishi, wakamwendea mfalme katika ua wa nje na kumwarifu kila kitu. \v 21 Mfalme akamtuma Yehudi akachukue kile kitabu. Yehudi akakileta hicho kitabu kutoka chumba cha Elishama mwandishi, na akakisoma mbele ya mfalme na maafisa wakiwa wamesimama kando ya mfalme. \v 22 Ulikuwa mwezi wa tisa, na mfalme alikuwa ameketi chumba cha wakati wa baridi akiota moto. \v 23 Hata ikawa kila wakati Yehudi alipomaliza kusoma kurasa tatu au nne za hicho kitabu, mfalme alizikata kwa kisu cha mwandishi na kuzitupia motoni, hadi kitabu chote kikateketea. \v 24 Mfalme na watumishi wake wote waliosikia yote yaliyosomwa hawakuonesha hofu yoyote, wala hawakuyararua mavazi yao. \v 25 Hata ingawa Elnathani, Delaya na Gemaria walimsihi mfalme asikichome kile kitabu, yeye hakuwasikiliza. \v 26 Badala yake, mfalme akamwamuru Yerameeli, mwana wa mfalme, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kuwakamata mwandishi Baruku na nabii Yeremia. Lakini Mwenyezi Mungu alikuwa amewaficha. \p \v 27 Baada ya mfalme kuchoma kile kitabu kilichokuwa na yale maneno Baruku aliyokuwa ameyaandika kutoka kinywani mwa Yeremia, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Yeremia likisema: \v 28 “Chukua kitabu kingine na uandike juu yake maneno yote yaliyokuwa katika kile kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda amekiteketeza kwa moto. \v 29 Mwambie pia Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Ulikiteketeza kile kitabu ukasema, “Kwa nini uliandika kwenye kitabu kwamba kwa hakika mfalme wa Babeli angekuja na kuangamiza nchi hii, na kuwakatilia mbali watu na wanyama kutoka humo?” \v 30 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu Yehoyakimu mfalme wa Yuda: Hatakuwa na mtu yeyote atakayekalia kiti cha utawala cha Daudi; maiti yake itatupwa nje kwenye joto wakati wa mchana na kupigwa na baridi wakati wa usiku. \v 31 Nitamwadhibu yeye, watoto wake na watumishi wake kwa ajili ya uovu wao. Nitaleta juu yao na wote wanaoishi Yerusalemu na watu wa Yuda kila maafa niliyoyasema dhidi yao, kwa sababu hawajasikiliza.’ ” \p \v 32 Kisha Yeremia akachukua kitabu kingine na kumpa mwandishi Baruku mwana wa Neria, naye kama Yeremia alivyosema, Baruku akaandika juu yake maneno yote ya kile kitabu ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikuwa amekichoma moto, na maneno mengine mengi yaliyofanana na hayo yaliyoongezewa humo. \c 37 \s1 Yeremia gerezani \p \v 1 Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye akatawala mahali pa Yehoyakini\f + \fr 37:1 \fr*\ft au \ft*\fqa Yekonia\fqa*\ft , \ft*\fqa Konia\fqa*\f* mwana wa Yehoyakimu. \v 2 Lakini sio Sedekia, wala watumishi wake, wala watu wa nchi walisikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu aliyonena kupitia kwa nabii Yeremia. \p \v 3 Hata hivyo, Mfalme Sedekia akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia, pamoja na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwa nabii Yeremia na ujumbe huu: “Tafadhali utuombee kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.” \p \v 4 Wakati huu Yeremia alikuwa huru kuingia na kutoka katikati ya watu, kwa sababu alikuwa bado hajatiwa gerezani. \v 5 Jeshi la Farao lilikuwa limetoka Misri, nao Wakaldayo waliokuwa wameuzingira Yerusalemu kwa majeshi waliposikia taarifa kuhusu jeshi hilo walijiondoa Yerusalemu. \p \v 6 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia nabii Yeremia kusema: \v 7 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Mwambie mfalme wa Yuda aliyekutuma uniulize mimi, ‘Jeshi la Farao lililokuja kukusaidia litarudi katika nchi yake yenyewe, yaani Misri. \v 8 Kisha Wakaldayo watarudi na kushambulia mji huu, watauteka na kuuchoma moto.’ \p \v 9 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msijidanganye wenyewe mkifikiri, ‘Hakika Wakaldayo watatuacha na kwenda zao.’ Hakika hawatawaacha! \v 10 Hata kama mngelishinda jeshi lote la Wakaldayo linalowashambulia ninyi, na wakawa ni watu waliojeruhiwa tu waliobaki kwenye mahema yao, wangetoka na kuuchoma mji huu moto.” \p \v 11 Baada ya jeshi la Wakaldayo kujiondoa kutoka Yerusalemu kwa sababu ya jeshi la Farao, \v 12 Yeremia akaondoka mjini kwenda nchi ya Benyamini ili akapate huko sememu yake ya milki miongoni mwa watu. \v 13 Lakini alipofika kwenye Lango la Benyamini, mkuu wa walinzi aliyeitwa Iriya mwana wa Shelemia, mwana wa Hanania, akamkamata Yeremia na kusema, “Wewe unaenda kujiunga na Wakaldayo!” \p \v 14 Yeremia akasema, “Hiyo si kweli, mimi sijiungi na Wakaldayo.” Lakini Iriya hakumsikiliza; badala yake, akamkamata Yeremia na kumpeleka kwa maafisa. \v 15 Wakamkasirikia Yeremia, wakaamuru apigwe, na akafungwa katika nyumba ya Yonathani mwandishi waliyokuwa wameifanya kuwa gereza. \p \v 16 Yeremia akawekwa kwenye chumba kilichofukuliwa chini, kilichojengwa kwa zege ndani ya gereza chini ya ngome, akakaa huko kwa muda mrefu. \v 17 Kisha Mfalme Sedekia akatumana aletwe katika jumba la kifalme, mahali alipomuuliza kwa siri, “Je, kuna neno lolote kutoka kwa Mwenyezi Mungu?” \p Yeremia akajibu, “Ndiyo, utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli.” \p \v 18 Kisha Yeremia akamwambia Mfalme Sedekia, “Nimefanya kosa gani dhidi yako na maafisa wako au watu hawa, hata ukanifunga gerezani? \v 19 Wako wapi manabii wako waliokutabiria wakisema, ‘Mfalme wa Babeli hatakushambulia wewe wala nchi hii’? \v 20 Lakini sasa, bwana wangu mfalme, tafadhali sikiliza. Niruhusu nilete maombi yangu mbele yako, usinirudishe kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, nisije nikafia humo.” \p \v 21 Ndipo Mfalme Sedekia akatoa maagizo Yeremia awekwe katika ua wa walinzi, na apewe mkate kutoka mitaa ya waokaji kila siku hadi mikate yote katika mji itakapokwisha. Kwa hiyo Yeremia akabaki katika ua wa walinzi. \c 38 \s1 Yeremia atupwa kwenye kisima \p \v 1 Shefatia mwana wa Matani, na Gedalia mwana wa Pashuri, na Yehukali mwana wa Shelemia, na Pashuri mwana wa Malkiya wakasikia kile Yeremia alichokuwa akiwaambia watu wote aliposema, \v 2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Yeyote akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni, lakini yeyote atakayejisalimisha kwa Wakaldayo ataishi. Atakayeyatoa maisha yake kama nyara, ataishi.’ \v 3 Tena hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Mji huu kwa hakika utatiwa mikononi mwa jeshi la mfalme wa Babeli, ambaye atauteka.’ ” \p \v 4 Ndipo maafisa wakamwambia mfalme, “Mtu huyu imempasa kuuawa. Anawakatisha tamaa askari waliobaki katika mji huu na watu wote kutokana na mambo anayowaambia. Mtu huyu hawatakii mema watu hawa, bali maangamizi yao.” \p \v 5 Mfalme Sedekia akajibu, “Yeye yuko mikononi mwenu! Mfalme hawezi kufanya lolote kuwapinga ninyi.” \p \v 6 Basi wakamchukua Yeremia na kumtia kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme, kilichokuwa katika ua wa walinzi. Wakamteremsha Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. Hakikuwa na maji ndani yake, ila tope tu, naye Yeremia akazama ndani ya matope. \p \v 7 Lakini Ebed-Meleki Mkushi, aliyekuwa afisa katika jumba la kifalme, akasikia kuwa walikuwa wamemtia Yeremia ndani ya kisima. Mfalme alipokuwa ameketi katika Lango la Benyamini, \v 8 Ebed-Meleki akatoka nje ya jumba la kifalme na kumwambia, \v 9 “Mfalme bwana wangu, watu hawa wamefanya uovu kwa yote waliomtendea nabii Yeremia. Wamemtupa ndani ya kisima, ambamo atakufa kwa njaa chakula kitakapokosekana katika mji.” \p \v 10 Basi mfalme akamwamuru Ebed-Meleki Mkushi, akisema, “Chukua watu thelathini kutoka hapa pamoja nawe, mkamtoe nabii Yeremia huko kwenye kisima kabla hajafa.” \p \v 11 Basi Ebed-Meleki akawachukua watu pamoja naye, wakaenda kwenye chumba kilicho chini ya hazina, ndani ya jumba la kifalme. Akachukua matambaa makuukuu pamoja na nguo zilizochakaa kutoka huko, na kumshushia Yeremia kwa kamba ndani ya kisima. \v 12 Ebed-Meleki Mkushi akamwambia Yeremia, “Weka haya matambaa makuukuu na hizo nguo zilizochakaa makwapani ili kuzuia kamba.” Yeremia akafanya hivyo, \v 13 nao wakamvuta juu kwa kamba na kumtoa katika kisima. Yeremia akakaa katika ua wa walinzi. \s1 Sedekia amhoji Yeremia tena \p \v 14 Ndipo Mfalme Sedekia akatuma watu wamwitie nabii Yeremia wamlete kwake kwenye ingilio la tatu la Hekalu la Mwenyezi Mungu. Mfalme akamwambia Yeremia, “Ninataka kukuuliza jambo fulani, usinifiche kitu chochote.” \p \v 15 Yeremia akamwambia Sedekia, “Nikikupa jibu, je, hutaniua? Hata nikikupa ushauri, wewe hutanisikiliza.” \p \v 16 Lakini Mfalme Sedekia akamwapia Yeremia kiapo hiki kwa siri, akisema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, ambaye ametupatia pumzi, sitakuua wala sitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako.” \p \v 17 Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika, na mji huu hautateketezwa kwa moto. Pia wewe na jamaa yako mtaishi. \v 18 Lakini ikiwa hutajisalimisha kwa maafisa wa jeshi la mfalme wa Babeli, mji huu utatiwa mikononi mwa Wakaldayo; nao watauteketeza kwa moto, nawe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao.’ ” \p \v 19 Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, “Ninawaogopa Wayahudi ambao wamekimbilia kwa Wakaldayo, kwa kuwa Wakaldayo wanaweza kunitia mikononi mwao, nao wakanitenda vibaya.” \p \v 20 Yeremia akajibu, “Hawatakutia mikononi mwao. Mtii Mwenyezi Mungu kwa kufanya kile ninachokuambia. Kisha utafanikiwa na maisha yako yatakuwa salama. \v 21 Lakini ukikataa kujisalimisha, hili ndilo Mwenyezi Mungu alilonifunulia: \v 22 Wanawake wote walioachwa katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda wataletwa mbele ya maafisa wa mfalme wa Babeli. Wanawake hao watakuambia: \q1 “ ‘Walikupotosha na kukushinda, \q2 wale rafiki zako uliowaamini. \q1 Miguu yako imezama matopeni; \q2 rafiki zako wamekuacha.’ \p \v 23 “Wake zako wote na watoto wataletwa na kutiwa mikononi mwa Wakaldayo. Wewe mwenyewe hutaweza kujiokoa mikononi mwao. Lakini utatekwa na mfalme wa Babeli, na mji huu utateketezwa kwa moto.” \p \v 24 Kisha Sedekia akamwambia Yeremia, “Usiruhusu mtu yeyote ajue kuhusu haya mazungumzo, la sivyo utakufa. \v 25 Maafisa wakisikia kwamba nimezungumza nawe, nao wakakujia na kusema, ‘Tuambie kile ulichozungumza na mfalme na kile mfalme alichokuambia, usitufiche au sivyo tutakuua,’ \v 26 basi waambie, ‘Nilikuwa ninamsihi mfalme asinirudishe kwenye nyumba ya Yonathani nisije nikafia humo.’ ” \p \v 27 Viongozi wote wakamjia Yeremia na kumuuliza, naye Yeremia akawaambia kila kitu mfalme alichomwagiza kusema. Kisha hawakusema lolote zaidi na Yeremia kwa sababu hakuna hata mmoja aliyekuwa amesikia mazungumzo yake na mfalme. \p \v 28 Naye Yeremia akabaki katika ua wa walinzi hadi siku Yerusalemu ilipotekwa. \s1 Kuanguka kwa Yerusalemu \p Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa: \c 39 \nb \v 1 Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu na akauzingira. \v 2 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia, ukuta wa mji ulibomolewa. \v 3 Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli wakaja na kuketi kwenye Lango la Kati: Nergal-Shareza wa Samgari, Nebo-Sarsekimu afisa mkuu, Nergal-Shareza afisa mwenye cheo cha juu, na maafisa wengine wote wa mfalme wa Babeli. \v 4 Mfalme Sedekia wa Yuda na askari wote walipowaona, wakakimbia na kuondoka mjini usiku kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili, wakaelekea Araba\f + \fr 39:4 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bonde la Yordani\fqa*\f*. \p \v 5 Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia na kumpata Sedekia katika nchi tambarare za Yeriko. Wakamkamata na kumpeleka kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ambapo alimtangazia hukumu. \v 6 Huko Ribla, mfalme wa Babeli aliwachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na pia akawaua wakuu wote wa Yuda. \v 7 Kisha akayang’oa macho ya Sedekia na kumfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. \p \v 8 Jeshi la Wakaldayo likachoma moto jumba la kifalme na nyumba za watu, na kuzibomoa kuta za Yerusalemu. \v 9 Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme akawachukua na kuwapeleka uhamishoni Babeli watu waliokuwa wamebaki ndani ya mji, pamoja na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake, na watu wengine wote. \v 10 Lakini Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine. \p \v 11 Basi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa maagizo kuhusu Yeremia kupitia Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme akisema: \v 12 “Mchukue umtunze. Usimdhuru, lakini umfanyie chochote anachotaka.” \v 13 Basi Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi, Nebushazbani afisa mkuu, Nergal-Shareza afisa wa cheo cha juu, na maafisa wengine wote wa mfalme wa Babeli \v 14 wakatuma watu kumwondoa Yeremia kutoka ua wa walinzi. Wakamkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ili amrudishe nyumbani mwake. Kwa hiyo akabaki miongoni mwa watu wake mwenyewe. \p \v 15 Yeremia alipokuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia kusema: \v 16 “Nenda ukamwambie Ebed-Meleki Mkushi, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kutimiza maneno yangu dhidi ya mji huu kwa maafa, wala si kwa mema. Wakati huo, hayo yatatimizwa mbele ya macho yako. \v 17 Lakini siku hiyo nitakuokoa, asema Mwenyezi Mungu; hutatiwa mikononi mwa wale unaowaogopa. \v 18 Nitakuokoa; hutaanguka kwa upanga, maisha yako yatakuwa salama, kwa sababu unanitumaini, asema Mwenyezi Mungu.’ ” \c 40 \s1 Yeremia aachiwa huru \p \v 1 Neno likamjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu baada ya Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli. \v 2 Mkuu wa askari walinzi alipomwona Yeremia, akamwambia, “Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aliamuru maafa haya kutokea mahali hapa. \v 3 Sasa Mwenyezi Mungu ameyaleta haya, amefanya sawasawa na alivyosema angefanya. Yote haya yametokea kwa sababu ninyi mlifanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu na hamkumtii. \v 4 Lakini leo ninakufungua minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Ukiona ni vema, twende pamoja hadi Babeli; nami nitakutunza. Lakini kama hutaki, basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda kokote unakotaka.” \v 5 Lakini kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au uende popote panapokupendeza.” \p Kisha huyo kiongozi akampa posho yake na zawadi, akamwacha aende zake. \v 6 Kwa hiyo Yeremia akaenda kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa, na kuishi naye miongoni mwa watu walioachwa katika nchi. \s1 Gedalia auawa \r (2 Wafalme 25:22-26) \p \v 7 Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi, na amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini zaidi katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli, \v 8 wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani na Yonathani wana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi, wana wa Efai Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao. \v 9 Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani akaapa ili kuwatia moyo, wao na watu wao. Akasema: “Msiogope kuwatumikia Wakaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu. \v 10 Mimi mwenyewe nitakaa Mispa ili kuwawakilisha mbele ya Wakaldayo wanaotujia, lakini ninyi mtavuna divai, matunda ya kiangazi na mafuta, nanyi mtaweka katika vyombo vyenu vya kuhifadhia, na kuishi katika miji mliyojitwalia.” \p \v 11 Wayahudi wote waliokuwa Moabu, Amoni, Edomu na nchi nyingine zote waliposikia kwamba mfalme wa Babeli ameacha mabaki ya watu katika Yuda na amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kuwa mtawala wao, \v 12 wakarudi wote katika nchi ya Yuda kwa Gedalia huko Mispa, kutoka nchi zote ambazo walikuwa wametawanywa. Nao wakavuna divai na matunda tele wakati wa kiangazi. \p \v 13 Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi wakamjia Gedalia huko Mispa \v 14 na kumwambia, “Je, hujui kwamba Baalisi mfalme wa Waamoni amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania akuue?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu hakuwaamini. \p \v 15 Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko Mispa, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokuzunguka watawanyike, na mabaki wa Yuda waangamie?” \p \v 16 Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu akamwambia Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo hilo! Unalosema kuhusu Ishmaeli si kweli.” \c 41 \p \v 1 Katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme, naye alikuwa mmoja wa maafisa wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa. Walipokuwa wakila pamoja huko, \v 2 Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga; wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi. \v 3 Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari Wakaldayo waliokuwa huko. \p \v 4 Siku moja baada ya kuuawa kwa siri kwa Gedalia, kabla mtu yeyote hajafahamu jambo hilo, \v 5 watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 6 Ishmaeli mwana wa Nethania akaondoka Mispa ili kwenda kuwalaki, huku akilia alipokuwa akienda. Alipokutana nao, akasema, “Karibuni kwa Gedalia mwana wa Ahikamu.” \v 7 Walipoingia mjini, Ishmaeli mwana wa Nethania na wale watu waliokuwa pamoja naye wakawachinja na kuwatupa ndani ya kisima. \v 8 Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine. \v 9 Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya kuwa sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti. \p \v 10 Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao, yaani, binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni. \p \v 11 Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye waliposikia kuhusu uhalifu wote ambao Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa ameufanya, \v 12 waliwachukua watu wao wote kwenda kupigana na Ishmaeli mwana wa Nethania. Wakakutana naye karibu na bwawa kubwa huko Gibeoni. \v 13 Ikawa watu wote waliokuwa na Ishmaeli walipomwona Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa pamoja naye, wakafurahi. \v 14 Watu wote ambao Ishmaeli alikuwa amewachukua mateka huko Mispa wakageuka na kumfuata Yohanani mwana wa Karea. \v 15 Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na watu wake wanane wakamtoroka Yohanani na kukimbilia kwa Waamoni. \s1 Kukimbilia Misri \p \v 16 Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu. Mabaki yao walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni. \v 17 Kisha wakasafiri hadi Geruth-Kimhamu karibu na Bethlehemu wakiwa njiani kwenda Misri \v 18 ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, aliyekuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi. \c 42 \s1 Yeremia ashauri walionusurika wasihame Yuda \p \v 1 Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea, na Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia \v 2 Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa tumesalia wachache tu. \v 3 Omba ili Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atuambie twende wapi na tufanye nini.” \p \v 4 Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho Mwenyezi Mungu, wala sitawaficha chochote.” \p \v 5 Kisha wakamwambia Yeremia, “Mwenyezi Mungu na awe shahidi mwaminifu na wa kweli dhidi yetu, ikiwa hatutafanya kila kitu jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakachokutuma utuambie. \v 6 Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.” \p \v 7 Baada ya siku kumi, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia. \v 8 Kwa hiyo akawaita Yohanani mwana wa Karea, maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye, na watu wote kuanzia mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana. \v 9 Akawaambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kuwasilisha maombi yenu: \v 10 ‘Mkikaa katika nchi hii, nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawang’oa, kwani ninahuzunishwa na maafa niliyowapiga nayo. \v 11 Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asema Mwenyezi Mungu, kwa kuwa niko pamoja nanyi, nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mkononi mwake. \v 12 Nitawaonea huruma ili naye awe na huruma kwenu na kuwarudisha katika nchi yenu.’ \p \v 13 “Lakini mkisema, ‘Hatutakaa katika nchi hii,’ hivyo mkaacha kumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, \v 14 na kama mkisema, ‘Hapana, tutaenda kuishi Misri, mahali ambapo hatutaona vita au kusikia sauti ya tarumbeta, au kuwa na njaa ya chakula,’ \v 15 basi sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi mabaki ya Yuda. Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Ikiwa mmekusudia kwenda Misri na kufanya makazi huko, \v 16 basi ule upanga mnaouogopa utawapata huko, na njaa mnayoihofia itawafuata huko Misri, nanyi mtafia huko. \v 17 Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’ \v 18 Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama vile hasira yangu na ghadhabu yangu ilivyomwagwa juu ya wale walioishi Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu mtakapoenda Misri. Mtakuwa kitu cha kulaaniwa na kutishiwa, cha kuhukumiwa, na cha kuaibisha; nanyi hamtapaona mahali hapa tena.’ \p \v 19 “Enyi mabaki ya Yuda, Mwenyezi Mungu amewaambia, ‘Msiende Misri.’ Hakikisheni jambo hili: Ninawaonya leo \v 20 kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kusema, ‘Mwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’ \v 21 Nimewaambieni leo, lakini bado ninyi hamtaki kumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, katika yote aliyonituma niwaambie. \v 22 Basi sasa, hakikisheni jambo hili: Mtakufa kwa upanga, njaa na tauni mahali pale mnataka kwenda kuishi.” \c 43 \s1 Yeremia apelekwa Misri \p \v 1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, yaani kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amemtuma kuwaambia, \v 2 Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ \v 3 Lakini Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu ili ututie mikononi mwa Wakaldayo, ili watuue au watuchukue uhamishoni Babeli.” \p \v 4 Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya Mwenyezi Mungu ya kukaa katika nchi ya Yuda. \v 5 Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa. \v 6 Pia wakawaongoza wanaume wote, wanawake na watoto, na binti za mfalme ambao Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha na Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, na nabii Yeremia, na Baruku mwana wa Neria. \v 7 Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtii Mwenyezi Mungu, wakaenda hadi Tapanesi. \p \v 8 Huko Tapanesi neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: \v 9 “Wayahudi wakiwa wanaona, chukua baadhi ya mawe makubwa na kuyazika katika udongo wa mfinyanzi katika njia iliyojengwa kwa matofali katika lango la jumba la kifalme la Farao huko Tapanesi. \v 10 Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha utawala juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema lake la ufalme juu yake. \v 11 Atakuja na kuishambulia Misri; atawaua waliokusudiwa kuuawa, atawateka waliokusudiwa kutekwa, na atawaua kwa upanga waliokusudiwa kuuawa kwa upanga. \v 12 Atachoma moto mahekalu ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama mchungaji ajizungushiavyo vazi lake, ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo kwa amani. \v 13 Huko, ndani ya hekalu la jua\f + \fr 43:13 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Heliopoli \fqa*\ft (\ft*\fqa Mji wa Jua\fqa*\ft )\ft*\f* nchini Misri, atabomoa nguzo za ibada, na kuteketeza kwa moto mahekalu ya miungu ya Misri.’ ” \c 44 \s1 Maafa kwa sababu ya ibada za sanamu \p \v 1 Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi Misri, huko Migdoli, Tapanesi na Memfisi\f + \fr 44:1 \fr*\ft au \ft*\fqa Nofu\fqa*\f*, katika nchi ya Pathrosi\f + \fr 44:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Misri ya Juu\fqa*\f*, kusema: \v 2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu \v 3 kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo haikuwahi kujulikana kwao, wala kwenu na mababu zenu. \v 4 Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’ \v 5 Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine. \v 6 Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo. \p \v 7 “Basi hili ndilo Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki? \v 8 Kwa nini kuichochea hasira yangu kwa kazi ya mikono yenu, kuifukizia uvumba miungu mingine huko Misri, mahali mlipokuja kuishi? Mtajiangamiza wenyewe na kujifanya kitu cha kulaania na shutumu miongoni mwa mataifa yote duniani. \v 9 Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu? \v 10 Hadi leo hawajajinyenyekeza au kuonesha heshima, wala hawajafuata sheria yangu na amri nilizoweka mbele yenu na baba zenu. \p \v 11 “Kwa hiyo, hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Mimi nimekusudia kuleta maafa juu yenu, na kuiangamiza Yuda yote. \v 12 Nitawaondoa mabaki ya Yuda waliokusudia kwenda Misri kukaa huko. Wote wataangamia huko Misri, wataanguka kwa upanga au kufa kwa njaa. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana, watakufa kwa upanga au njaa. Watakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha laumu na shutumu. \v 13 Nitawaadhibu wanaoishi Misri kwa upanga, njaa na tauni kama nilivyoiadhibu Yerusalemu. \v 14 Hakuna hata mmoja wa mabaki ya Yuda ambaye ameenda kuishi Misri atakayeepuka au kunusurika ili kurudi katika nchi ya Yuda, ambayo wanaitamani sana kurudi na kuishi ndani yake, hakuna hata mmoja atakayerudi isipokuwa wakimbizi wachache.” \p \v 15 Kisha wanaume wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakifukiza uvumba kwa miungu mingine, pamoja na wanawake wote waliokuwako, yaani kusanyiko kubwa na watu wote walioishi nchi ya Misri na Pathrosi, wakamwambia Yeremia, \v 16 “Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina la Mwenyezi Mungu! \v 17 Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama sisi na baba zetu, wafalme na wakuu wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote. \v 18 Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.” \p \v 19 Wanawake wakaongeza kusema, “Tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni, na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?” \p \v 20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu, \v 21 “Je, Mwenyezi Mungu hakukumbuka na kufikiri kuhusu uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi? \v 22 Mwenyezi Mungu alipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaaniwa na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo. \v 23 Kwa sababu mmefukiza uvumba na kufanya dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, nanyi hamkumtii wala kufuata sheria yake au amri zake au maagizo yake, maafa haya yamekuja juu yenu, kama mnavyoona sasa.” \p \v 24 Kisha Yeremia akawaambia watu wote, pamoja na wanawake, “Sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi watu wote wa Yuda mlioko Misri. \v 25 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’ \p “Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu! \v 26 Lakini sikieni neno la Mwenyezi Mungu, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kama Bwana Mungu Mwenyezi aishivyo.” \v 27 Kwa maana ninawaangalia kwa ajili ya madhara, wala sio kwa mema. Kila Myahudi aliyeko nchi ya Misri ataangamia kwa upanga au kwa njaa, hadi wote waangamie. \v 28 Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watajua ni neno la nani litakalosimama: kwamba ni langu au ni lao. \p \v 29 “ ‘Hii itakuwa ndiyo ishara kwenu kwamba nitawaadhibu mahali hapa, asema Mwenyezi Mungu, ili mpate kujua kuwa onyo langu la madhara dhidi yenu hakika litatimizwa.’ \v 30 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nitamtia Farao Hofra mfalme wa Misri mikononi mwa adui zake wanaoutafuta uhai wake, kama nilivyomtia Sedekia mfalme wa Yuda mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui aliyekuwa akiutafuta uhai wake.’ ” \c 45 \s1 Ujumbe kwa Baruku \p \v 1 Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule: \v 2 “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku: \v 3 Ulisema, ‘Ole wangu! Mwenyezi Mungu ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ” \p \v 4 Lakini Mwenyezi Mungu akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kung’oa kile nilichokipanda katika nchi yote. \v 5 Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asema Mwenyezi Mungu, lakini popote utakapoenda, nitayaokoa maisha yako.’ ” \c 46 \s1 Ujumbe kuhusu Misri \p \v 1 Hili ni neno la Mwenyezi Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa: \b \p \v 2 Kuhusu Misri: \b \p Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: \q1 \v 3 “Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo, \q2 mtoke kwa ajili ya vita! \q1 \v 4 Fungieni farasi lijamu, \q2 pandeni farasi! \q1 Shikeni nafasi zenu \q2 mkiwa mmevaa chapeo! \q1 Isugueni mikuki yenu, \q2 vaeni dirii vifuani! \q1 \v 5 Je, ninaona nini? \q2 Wametiwa hofu, \q1 wanarudi nyuma, \q2 mashujaa wao wameshindwa. \q1 Wanakimbia kwa haraka \q2 pasipo kutazama nyuma, \q2 tena kuna hofu kuu kila upande,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 6 Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia, \q2 wala wenye nguvu hawawezi kutoroka. \q1 Kaskazini, kando ya Mto Frati, \q2 wanajikwaa na kuanguka. \b \q1 \v 7 “Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili, \q2 kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi? \q1 \v 8 Misri hujiinua kama Mto Naili, \q2 kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi. \q1 Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia, \q2 nitaiangamiza miji na watu wake.’ \q1 \v 9 Songeni mbele, enyi farasi! \q2 Endesheni kwa kasi, enyi mnaoendesha magari ya vita! \q1 Endeleeni mbele, enyi mashujaa: \q2 wanaume wa Kushi na Putu mnaobeba ngao, \q2 wanaume wa Ludi mnaovuta upinde. \q1 \v 10 Lakini ile siku ni ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 siku ya kulipiza kisasi, \q2 kisasi juu ya adui zake. \q1 Upanga utakula hata utakapotosheka, \q2 hadi utakapozima kiu yake kwa damu. \q1 Kwa maana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 atatoa dhabihu kwenye nchi ya kaskazini, \q2 kando ya Mto Frati. \b \q1 \v 11 “Panda hadi Gileadi ukapate zeri, \q2 ee Bikira Binti Misri. \q1 Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; \q2 huwezi kupona. \q1 \v 12 Mataifa yatasikia juu ya aibu yako, \q2 kilio chako kitaijaza dunia. \q1 Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine, \q2 nao wataanguka chini pamoja.” \p \v 13 Huu ndio ujumbe ambao Mwenyezi Mungu alimwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri: \q1 \v 14 “Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli, \q2 hubiri pia katika Memfisi\f + \fr 46:14 \fr*\ft au \ft*\fqa Nofu\fqa*\f* na Tapanesi: \q1 ‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari, \q2 kwa kuwa upanga unawala wanaokuzunguka.’ \q1 \v 15 Kwa nini mashujaa wako wamesombwa \q2 na kupelekwa mbali? \q1 Hawawezi kusimama, kwa maana Mwenyezi Mungu \q2 atawasukuma awaangushe chini. \q1 \v 16 Watajikwaa mara kwa mara, \q2 wataangukiana wao kwa wao. \q1 Watasema, ‘Amka, turudi \q2 kwa watu wetu na nchi yetu, \q2 mbali na upanga wa mtesi.’ \q1 \v 17 Huko watu watatangaza, \q2 ‘Farao, mfalme wa Misri, ni makelele tu, \q2 muda alioandikiwa umekwisha.’ \b \q1 \v 18 “Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme, \q2 ambaye jina lake ni Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 “mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima, \q2 kama Karmeli kando ya bahari. \q1 \v 19 Funga mizigo yako kwenda uhamishoni, \q2 wewe ukaaye Misri, \q1 kwa kuwa Memfisi utaangamizwa \q2 na kuwa magofu pasipo mkazi. \b \q1 \v 20 “Misri ni mtamba mzuri, \q2 lakini mbung’o anakuja dhidi yake kutoka kaskazini. \q1 \v 21 Askari wake waliokodiwa katika safu zake \q2 wako kama ndama walionenepeshwa. \q1 Wao pia watageuka na kukimbia pamoja, \q2 hawataweza kuhimili vita, \q1 kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao, \q2 wakati wao wa kuadhibiwa. \q1 \v 22 Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia \q2 kadiri adui anavyowasogelea na majeshi, \q1 watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka, \q2 kama watu wakatao miti. \q1 \v 23 Wataufyeka msitu wake,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q2 “hata kama umesongamana kiasi gani. \q1 Ni wengi kuliko nzige, \q2 hawawezi kuhesabika. \q1 \v 24 Binti Misri ataaibishwa, \q2 atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.” \p \v 25 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asema: “Ninakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi\f + \fr 46:25 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa No \fqa*\ft (au \ft*\fqa No-Amoni\fqa*\ft )\ft*\f*, na juu ya Farao, juu ya Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wanaomtegemea Farao. \v 26 Nitawatia mikononi mwa wanaoutafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Mwishowe, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 27 “Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, \q2 usifadhaike, ee Israeli. \q1 Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali, \q2 uzao wako kutoka nchi walioishi uhamishoni. \q1 Yakobo atakuwa tena na amani na salama, \q2 wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu. \q1 \v 28 Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, \q2 kwa maana mimi niko pamoja nawe,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote \q2 ambayo miongoni mwake nimekutawanya, \q2 sitakuangamiza wewe kabisa. \q1 Nitakurudi, lakini kwa haki tu, \q2 wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.” \c 47 \s1 Ujumbe kuhusu Wafilisti \p \v 1 Hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza: \p \v 2 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini, \q2 yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana. \q1 Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyo ndani yake, \q2 miji na wanaoishi ndani yake. \q1 Watu watapiga kelele; \q2 wote wanaoishi katika nchi wataomboleza \q1 \v 3 kwa sauti ya kwato za farasi wanaoenda mbio, \q2 kwa sauti ya magari ya vita ya adui, \q2 na mngurumo wa magurudumu yake. \q1 Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao, \q2 mikono yao italegea. \q1 \v 4 Kwa maana siku imewadia \q2 kuwaangamiza Wafilisti wote \q1 na kuwakatilia mbali walionusurika wote \q2 ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni. \q1 Mwenyezi Mungu anakaribia kuwaangamiza Wafilisti, \q2 mabaki toka pwani za Kaftori\f + \fr 47:4 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Krete\fqa*\f*. \q1 \v 5 Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza, \q2 Ashkeloni atanyamazishwa. \q1 Enyi mabaki kwenye tambarare, \q2 mtajikatakata wenyewe hadi lini? \b \q1 \v 6 “Mnalia, ‘Aa, upanga wa Mwenyezi Mungu, \q2 utaendelea hadi lini ndipo upumzike? \q1 Rudi ndani ya ala yako; \q2 acha na utulie.’ \q1 \v 7 Lakini upanga utatuliaje \q2 wakati Mwenyezi Mungu ameuamuru, \q1 wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni \q2 pamoja na pwani yake?” \c 48 \s1 Ujumbe kuhusu Moabu \p \v 1 Kuhusu Moabu: \b \p Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: \q1 “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa. \q2 Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; \q2 Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa. \q1 \v 2 Moabu haitasifiwa tena; \q2 huko Heshboni watu watapanga jinsi ya kumwangusha: \q2 ‘Njooni na tuliangamize taifa lile.’ \q1 Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; \q2 upanga utakufuatia. \q1 \v 3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, \q2 kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. \q1 \v 4 Moabu utavunjwa, \q2 wadogo wake watapiga kelele. \q1 \v 5 Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, \q2 wakilia kwa uchungu wanapotembea, \q1 kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, \q2 kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika. \q1 \v 6 Kimbieni! Okoeni maisha yenu, \q2 kuweni kama kichaka jangwani. \q1 \v 7 Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali yenu, \q2 ninyi pia mtachukuliwa mateka, \q1 naye Kemoshi\f + \fr 48:7 \fr*\ft mungu wa Wamoabu\ft*\f* ataenda uhamishoni, \q2 pamoja na makuhani wake na maafisa wake. \q1 \v 8 Mwangamizi atakuja dhidi ya kila mji, \q2 wala hakuna mji utakaookoka. \q1 Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa, \q2 kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema. \q1 \v 9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, \q2 kwa kuwa ataangamizwa; \q1 miji yake itakuwa ukiwa, \q2 hakutakuwa na mtu atakayeishi ndani yake. \b \q1 \v 10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Mwenyezi Mungu kwa ulegevu! \q2 Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu! \b \q1 \v 11 “Moabu amestarehe tangu ujana wake, \q2 kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, \q1 haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, \q2 hajaenda uhamishoni. \q1 Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, \q2 nayo harufu yake haijabadilika. \q1 \v 12 Lakini siku zinakuja,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “nitakapotuma watu wamiminao kutoka magudulia, \q2 nao watamimina; \q1 wataacha magudulia yake yakiwa matupu \q2 na kuvunja mitungi yake. \q1 \v 13 Kisha Moabu atamwonea aibu Kemoshi, \q2 kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu \q2 walipotegemea Betheli. \b \q1 \v 14 “Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa, \q2 watu hodari katika vita’? \q1 \v 15 Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, \q2 vijana wake wa kiume walio bora sana watachinjwa,” \q1 asema Mfalme, ambaye jina lake \q2 ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \q1 \v 16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia, \q2 janga kubwa litamjia kwa haraka. \q1 \v 17 Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka, \q2 ninyi nyote mnaojua sifa zake, \q1 semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika \q2 fimbo ya kifalme yenye nguvu, \q1 tazama jinsi ilivyovunjika \q2 fimbo iliyotukuka!’ \b \q1 \v 18 “Shuka kutoka fahari yako \q2 uketi katika ardhi iliyokauka, \q2 enyi wenyeji wa Binti Diboni, \q1 kwa maana yeye aangamizaye Moabu \q2 atakuja dhidi yako, \q2 na kuangamiza miji yako yenye ngome. \q1 \v 19 Simama kando ya barabara na utazame, \q2 wewe unayeishi Aroeri. \q1 Muulize mwanaume anayekimbia \q2 na mwanamke anayetoroka, \q2 waulize, ‘Kumetokea nini?’ \q1 \v 20 Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa. \q2 Lieni kwa huzuni na kupiga kelele! \q1 Tangazeni kando ya Mto Arnoni \q2 kwamba Moabu ameangamizwa. \q1 \v 21 Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: \q2 katika Holoni, Yahasa na Mefaathi, \q1 \v 22 katika Diboni, Nebo \q2 na Beth-Diblathaimu, \q1 \v 23 katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli \q2 na Beth-Meoni, \q1 \v 24 katika Keriothi na Bosra; \q2 kwa miji yote ya Moabu, \q2 iliyo mbali na karibu. \q1 \v 25 Pembe\f + \fr 48:25 \fr*\ft pembe inawakilisha nguvu\ft*\f* ya Moabu imekatwa, \q2 mkono wake umevunjwa,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 26 “Mleweshe, \q2 kwa kuwa amemdharau Mwenyezi Mungu. \q1 Moabu atagaagaa katika matapishi yake, \q2 awe kichekesho. \q1 \v 27 Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa? \q2 Je, alikamatwa miongoni mwa wezi, \q1 kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau \q2 kila mara unapozungumza juu yake? \q1 \v 28 Ondokeni miji yenu, mkaishi katikati ya miamba, \q2 enyi mnaoishi Moabu. \q1 Kuweni kama njiwa ambaye hutengeneza kiota chake \q2 kwenye mlango wa pango. \b \q1 \v 29 “Tumesikia kuhusu kiburi cha Moabu: \q2 kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, \q1 kiburi chake na ufidhuli wake, \q2 na kujivuna kwa moyo wake. \q1 \v 30 Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q2 “nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. \q1 \v 31 Kwa hiyo namlilia Moabu, \q2 kwa ajili ya Moabu yote ninalia, \q1 ninaomboleza kwa ajili \q2 ya watu wa Kir-Haresethi. \q1 \v 32 Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, \q2 enyi mizabibu ya Sibma. \q1 Matawi yako yameenea hadi baharini; \q2 yamefika hadi bahari ya Yazeri. \q1 Mwangamizi ameyaangukia \q2 matunda yako yaliyoiva \q2 na mizabibu yako iliyoiva. \q1 \v 33 Shangwe na furaha vimetoweka \q2 kutoka bustani na mashamba ya Moabu. \q1 Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo; \q2 hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe. \q1 Ingawa kuna kelele, \q2 sio kelele za shangwe. \b \q1 \v 34 “Sauti ya kilio chao inapanda \q2 kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi, \q1 kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya, \q2 kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka. \q1 \v 35 Nitakomesha wote katika Moabu \q2 watoao sadaka mahali pa juu pa kuabudia, \q2 na kufukiza uvumba kwa miungu yao,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 36 “Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi; \q2 unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. \q2 Utajiri waliojipatia umetoweka. \q1 \v 37 Kila kichwa kimenyolewa \q2 na kila mwenye ndevu zimekatwa; \q1 kila mkono umekatwa \q2 na kila kiuno kimevalishwa gunia. \q1 \v 38 Juu ya mapaa yote katika Moabu \q2 na katika viwanja \q1 hakuna kitu isipokuwa maombolezo, \q2 kwa kuwa nimemvunja Moabu \q2 kama gudulia lisilotakiwa na mtu yeyote,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika! \q2 Jinsi wanavyolia kwa huzuni! \q1 Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu! \q2 Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa, \q1 kitu cha kutisha kwa wale wote \q2 wanaomzunguka.” \p \v 40 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Tazama! Tai anashuka chini, \q2 akitanda mabawa yake juu ya Moabu. \q1 \v 41 Miji itatekwa na ngome zake \q2 zitatwaliwa. \q1 Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu \q2 itakuwa kama moyo wa mwanamke katika uchungu wa kuzaa. \q1 \v 42 Moabu ataangamizwa kama taifa \q2 kwa sababu amemdharau Mwenyezi Mungu. \q1 \v 43 Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, \q2 enyi watu wa Moabu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 44 “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu \q2 ataanguka ndani ya shimo, \q1 yeyote atakayepanda kutoka shimoni, \q2 atanaswa katika mtego, \q1 kwa sababu nitailetea Moabu \q2 mwaka wa adhabu yake,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 45 “Katika kivuli cha Heshboni, \q2 wakimbizi wamesimama pasipo msaada, \q1 kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni, \q2 Mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni; \q1 unaunguza paji za nyuso za Wamoabu, \q2 mafuvu ya wanaojivuna kwa kelele. \q1 \v 46 Ole wako, ee Moabu! \q2 Watu wa Kemoshi wameangamizwa; \q1 watoto wako wa kiume wamepelekwa uhamishoni, \q2 na binti zako wamechukuliwa mateka. \b \q1 \v 47 “Lakini nitarudisha mateka wa Moabu, \q2 katika siku zijazo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p Huu ndio mwisho wa hukumu ya Moabu. \c 49 \s1 Ujumbe kuhusu Amoni \p \v 1 Kuhusu Waamoni: \b \p Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Je, Israeli hana wana? \q2 Je, hana warithi? \q1 Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi? \q2 Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake? \q1 \v 2 Lakini siku zinakuja,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “nitakapopiga ukelele wa vita \q2 dhidi ya Raba, mji wa Waamoni; \q1 utakuwa kilima cha magofu, \q2 navyo vijiji vinavyouzunguka \q2 vitateketezwa kwa moto. \q1 Kisha Israeli atawafukuza \q2 wale waliomfukuza,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 3 “Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa! \q2 Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba! \q1 Vaeni gunia na kuomboleza, \q2 kimbieni hapa na pale ndani ya kuta, \q1 kwa kuwa Moleki ataenda uhamishoni, \q2 yeye pamoja na makuhani na maafisa wake. \q1 \v 4 Kwa nini unajivunia mabonde yako, \q2 kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana? \q1 Ee binti usiye mwaminifu, \q2 unayeutumainia utajiri wako na kusema, \q2 ‘Ni nani atakayenishambulia?’ \q1 \v 5 Nitaleta hofu kuu juu yako \q2 kutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \q1 “Kila mmoja wenu ataondolewa, \q2 wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi. \b \q1 \v 6 “Lakini hatimaye, \q2 nitarudisha mateka wa Waamoni,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \s1 Ujumbe kuhusu Edomu \p \v 7 Kuhusu Edomu: \b \p Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Je, hakuna tena hekima katika Temani? \q2 Je, shauri limewapotea wenye busara? \q2 Je, hekima yao imechakaa? \q1 \v 8 Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa, \q2 wewe uishiye Dedani, \q1 kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau \q2 wakati nitakapomwadhibu. \q1 \v 9 Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako, \q2 wasingebakiza zabibu chache? \q1 Kama wezi wangekujia usiku, \q2 je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji? \q1 \v 10 Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi, \q2 nitayafunua maficho yake, \q2 ili asiweze kujificha. \q1 Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia, \q2 naye hatakuwepo tena. \q1 \v 11 Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao. \q1 Wajane wako pia \q2 wanaweza kunitumaini mimi.” \p \v 12 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kama wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe. \v 13 Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema Mwenyezi Mungu, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.” \q1 \v 14 Nimesikia ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu: \q2 Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, \q1 “Jikusanyeni ili kuushambulia! \q2 Inukeni kwa ajili ya vita!” \b \q1 \v 15 “Sasa nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa, \q2 uliyedharauliwa miongoni mwa watu. \q1 \v 16 Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako \q2 vimekudanganya, \q1 wewe unayeishi katika majabali ya miamba, \q2 wewe unayedumu katika miinuko ya kilima. \q1 Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai, \q2 nitakushusha chini kutoka huko,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 17 “Edomu atakuwa kitu cha kutisha; \q2 wote wapitao karibu \q1 watashangaa na kuzomea \q2 kwa sababu ya majeraha yake yote. \q1 \v 18 Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa, \q2 pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo. \q2 Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo. \b \q1 \v 19 “Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani \q2 kuja kwenye nchi ya malisho mengi, \q1 ndivyo nitakavyomfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula. \q2 Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili? \q1 Ni nani aliye kama mimi, \q2 na ni nani awezaye kunipinga? \q1 Tena ni mchungaji yupi awezaye \q2 kusimama kinyume nami?” \q1 \v 20 Kwa hiyo, sikia kile Mwenyezi Mungu alichokipanga dhidi ya Edomu, \q2 kile alichokusudia dhidi ya wale wanaoishi Temani: \q1 Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali; \q2 yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao. \q1 \v 21 Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka. \q2 Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu\f + \fr 49:21 \fr*\ft au \ft*\fqa Bahari ya Mafunjo\fqa*\f*. \q1 \v 22 Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula, \q2 akitandaza mabawa yake juu ya Bosra. \q1 Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu \q2 itakuwa kama moyo wa mwanamke katika uchungu wa kuzaa. \s1 Ujumbe kuhusu Dameski \p \v 23 Kuhusu Dameski: \q1 “Hamathi na Arpadi imetahayarika, \q2 kwa kuwa wamesikia habari mbaya. \q1 Wamevunjika moyo na wametaabika \q2 kama bahari iliyochafuka. \q1 \v 24 Dameski amedhoofika, \q2 amegeuka na kukimbia, \q2 hofu ya ghafula imemkamata sana; \q1 amepatwa na uchungu na maumivu, \q2 maumivu kama ya mwanamke katika uchungu wa kuzaa. \q1 \v 25 Kwa nini mji unaosifika haujaachwa, \q2 mji wenye sifa, na wa furaha yangu? \q1 \v 26 Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; \q2 askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \q1 \v 27 “Nitatia moto kuta za Dameski; \q2 utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.” \s1 Ujumbe kuhusu Kedari na Hazori \p \v 28 Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia: \b \p Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Inuka, ushambulie Kedari \q2 na kuwaangamiza watu wa mashariki. \q1 \v 29 Mahema yao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa; \q2 vibanda vyao vitatwaliwa, \q2 pamoja na mali yao yote na ngamia wao. \q1 Watu watawapigia kelele, \q2 ‘Hofu kuu iko kila upande!’ \b \q1 \v 30 “Kimbieni haraka! \q2 Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mnaoishi Hazori,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga njama dhidi yenu; \q2 amebuni hila dhidi yenu. \b \q1 \v 31 “Inuka na ulishambulie taifa lililostarehe, \q2 linaloishi kwa kujiamini,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “taifa lisilo na malango wala makomeo; \q2 watu wake wanaishi peke yao. \q1 \v 32 Ngamia wao watakuwa nyara, \q2 nayo mifugo yao itatekwa. \q1 Walio maeneo ya mbali \q2 nitawatawanya pande zote, \q1 nami nitaleta maafa juu yao \q2 kutoka kila upande,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 33 “Hazori itakuwa makao ya mbweha, \q2 mahali pa ukiwa milele. \q1 Hakuna atakayeishi humo; \q2 hakuna mtu atakayekaa ndani yake.” \s1 Ujumbe kuhusu Elamu \p \v 34 Hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda: \b \p \v 35 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Tazama, nitavunja upinde wa Elamu, \q2 ulio tegemeo la nguvu zao. \q1 \v 36 Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu \q2 toka pande nne za mbingu, \q1 nitawatawanya katika hizo pande nne, \q2 wala hapatakuwa na taifa \q1 ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa \q2 hawataenda. \q1 \v 37 Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao, \q2 mbele yao wanaoutafuta uhai wao; \q1 nitaleta maafa juu yao, \q2 naam, hasira yangu kali,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Nitawafuatia kwa upanga \q2 hadi nitakapowamaliza. \q1 \v 38 Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu \q2 na kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 39 “Lakini nitarudisha mateka wa Elamu \q2 katika siku zijazo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \c 50 \s1 Ujumbe kuhusu Babeli \p \v 1 Hili ndilo neno alilosema Mwenyezi Mungu kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo: \q1 \v 2 “Tangazeni! Hubirini katikati ya mataifa, \q2 Inueni bendera na mkahubiri; \q2 msiache kitu chochote, bali semeni, \q1 ‘Babeli utatekwa; \q2 Beli ataaibishwa, \q2 Merodaki atajazwa na hofu kuu. \q1 Sanamu zake zitaaibishwa \q2 na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’ \q1 \v 3 Taifa kutoka kaskazini litamshambulia, \q2 na kuifanya nchi yake ukiwa. \q1 Hakuna atakayeishi ndani yake, \q2 watu na wanyama wataikimbia. \b \q1 \v 4 “Katika siku hizo, wakati huo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda \q2 wataenda wakilia ili kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \q1 \v 5 Wataulizia njia iendayo Sayuni \q2 na kuelekeza nyuso zao huko. \q1 Watakuja na kuambatana na Mwenyezi Mungu \q2 katika agano la milele \q2 ambalo halitasahaulika. \b \q1 \v 6 “Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; \q2 wachungaji wao wamewapotosha \q2 na kuwafanya wazurure mlimani. \q1 Walitangatanga juu ya mlima na kilima, \q2 na kusahau mahali pao pa kupumzikia. \q1 \v 7 Yeyote aliyewakuta aliwala; \q2 adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, \q1 kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya \q2 Mwenyezi Mungu, malisho yao halisi, \q2 Mwenyezi Mungu, aliye tumaini la baba zao.’ \b \q1 \v 8 “Kimbieni kutoka Babeli; \q2 ondokeni katika nchi ya Wakaldayo, \q2 kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi. \q1 \v 9 Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli \q2 muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. \q1 Watashika nafasi zao dhidi yake, \q2 naye kutokea kaskazini atatekwa. \q1 Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, \q2 ambao hawawezi kurudi mikono mitupu. \q1 \v 10 Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara; \q2 wote wanaouteka, watapata nyara za kutosha,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 11 “Kwa sababu hushangilia na kufurahi, \q2 wewe utekaye urithi wangu, \q1 kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka, \q2 na kulia kama farasi dume, \q1 \v 12 mama yako ataaibika mno, \q2 yeye aliyekuzaa atatahayari. \q1 Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote, \q2 atakuwa nyika, nchi kame na jangwa. \q1 \v 13 Kwa sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu hatakaliwa na mtu, \q2 lakini ataachwa ukiwa kabisa. \q1 Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki \q2 kwa sababu ya majeraha yake yote. \b \q1 \v 14 “Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, \q2 enyi nyote mvutao upinde. \q1 Mpigeni! Msibakize mshale wowote, \q2 kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 15 Piga kelele dhidi yake kila upande! \q2 Anajisalimisha, minara yake inaanguka, \q2 kuta zake zimebomoka. \q1 Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Mwenyezi Mungu, \q2 mlipizeni kisasi; \q2 mtendeeni kama alivyowatendea wengine. \q1 \v 16 Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, \q2 pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. \q1 Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu \q2 kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, \q1 kila mmoja na akimbilie \q2 kwenye nchi yake mwenyewe. \b \q1 \v 17 “Israeli ni kundi lililotawanyika \q2 ambalo simba wamelifukuzia mbali. \q1 Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, \q2 wa mwisho kuponda mifupa yake \q2 alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.” \p \v 18 Kwa hiyo hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: \q1 “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake \q2 kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru. \q1 \v 19 Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe \q2 naye atalisha huko Karmeli na Bashani; \q1 njaa yake itashibishwa \q2 juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi. \q1 \v 20 Katika siku hizo, wakati huo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, \q2 lakini halitaonekana, \q1 na kwa ajili ya dhambi za Yuda, \q2 lakini haitapatikana hata moja, \q1 kwa kuwa nitawasamehe \q2 mabaki nitakaowaacha. \b \q1 \v 21 “Shambulieni nchi ya Merathaimu \q2 na wale wanaoishi huko Pekodi. \q1 Wafuatieni, waueni \q2 na kuwaangamiza kabisa,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru. \q1 \v 22 Kelele ya vita iko ndani ya nchi, \q2 kelele ya maangamizi makuu! \q1 \v 23 Tazama jinsi nyundo ya dunia yote \q2 ilivyovunjika na kuharibika! \q1 Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa \q2 miongoni mwa mataifa! \q1 \v 24 Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, \q2 nawe ukakamatwa kabla hujafahamu; \q1 ulipatikana na ukakamatwa \q2 kwa sababu ulimpinga Mwenyezi Mungu. \q1 \v 25 Mwenyezi Mungu amefungua ghala lake la silaha \q2 na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, \q1 kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 anayo kazi ya kufanya \q2 katika nchi ya Wakaldayo. \q1 \v 26 Njooni dhidi yake kutoka mbali. \q2 Zifungueni ghala zake za nafaka; \q2 mlundikeni kama lundo la nafaka. \q1 Mwangamizeni kabisa \q2 na msimwachie mabaki yoyote. \q1 \v 27 Waueni mafahali wake wachanga wote; \q2 waacheni washuke machinjoni! \q1 Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, \q2 wakati wao wa kuadhibiwa. \q1 \v 28 Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli \q2 wakitangaza katika Sayuni \q1 jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wetu \q2 alivyolipiza kisasi, \q2 kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. \b \q1 \v 29 “Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, \q2 wote wavutao upinde. \q1 Pigeni kambi kumzunguka kabisa, \q2 asitoroke mtu yeyote. \q1 Mlipizeni kwa matendo yake; \q2 mtendeeni kama alivyotenda. \q1 Kwa kuwa alimdharau Mwenyezi Mungu, \q2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. \q1 \v 30 Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; \q2 askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 31 “Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 “kwa kuwa siku yako imewadia, \q2 yaani wakati wako wa kuadhibiwa. \q1 \v 32 Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, \q2 wala hakuna yeyote atakayemuinua; \q1 nitawasha moto katika miji yake, \q2 utakaowateketeza wote wanaomzunguka.” \p \v 33 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Watu wa Israeli wamedhulumiwa, \q2 hata watu wa Yuda pia. \q1 Wote waliowateka wamewashikilia sana, \q2 wanakataa kuwaachia waende. \q1 \v 34 Lakini Mkombozi wao ana nguvu; \q2 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake. \q1 Atatetea shauri lao kwa nguvu \q2 ili alete amani nchini mwao, \q1 lakini ataleta msukosuko \q2 kwa wale wanaoishi Babeli. \b \q1 \v 35 “Upanga dhidi ya Wakaldayo!” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “dhidi ya wale wanaoishi Babeli, \q2 na dhidi ya maafisa wake na wenye busara! \q1 \v 36 Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! \q2 Watakuwa wapumbavu. \q1 Upanga dhidi ya mashujaa wake! \q2 Watajazwa na hofu kuu \q1 \v 37 Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita \q2 pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! \q2 Wao watakuwa kama wanawake. \q1 Upanga dhidi ya hazina zake! \q2 Hizo zitatekwa nyara. \q1 \v 38 Ukame juu ya maji yake! \q2 Nayo yatakauka. \q1 Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, \q2 wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu. \b \q1 \v 39 “Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, \q2 nao bundi watakaa humo. \q1 Kamwe haitakaliwa tena \q2 wala watu hawataishi humo kizazi hadi kizazi. \q1 \v 40 Kama Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora \q2 pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q1 “vivyo hivyo hakuna mtu atakayeishi humo. \q1 Naam, hakuna mtu atakayekaa humo. \b \q1 \v 41 “Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; \q2 taifa kubwa na wafalme wengi \q2 wanaamshwa kutoka miisho ya dunia. \q1 \v 42 Wamejifunga pinde na mikuki; \q2 ni wakatili na hawana huruma. \q1 Wanatoa sauti kama bahari inayounguruma \q2 wanapoendesha farasi wao; \q1 wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita \q2 ili kukushambulia, ee Binti Babeli. \q1 \v 43 Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, \q2 nayo mikono yake imelegea. \q1 Uchungu umemshika, \q2 maumivu kama ya mwanamke katika uchungu wa kuzaa. \q1 \v 44 Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani \q2 kuja kwenye nchi ya malisho mengi, \q1 ndivyo nitakavyomfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula. \q2 Ni nani aliye mteule, \q2 nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili? \q1 Ni nani aliye kama mimi, \q2 na ni nani awezaye kunipinga? \q1 Tena ni mchungaji yupi \q2 awezaye kusimama kinyume nami?” \q1 \v 45 Kwa hiyo, sikia ambacho Mwenyezi Mungu amepanga dhidi ya Babeli, \q2 kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: \q1 Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. \q2 Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao. \q1 \v 46 Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka; \q2 kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa. \c 51 \p \v 1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Tazama nitaamsha roho ya mwangamizi \q2 dhidi ya Babeli na wenyeji wa Leb-Kamai\f + \fr 51:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Ukaldayo\fqa*\ft , \ft*\fqa Babeli \fqa*\ft kwa fumbo\ft*\f*. \q1 \v 2 Nitawatuma wageni Babeli \q2 kumpepeta na kuiharibu nchi yake; \q1 watampinga kila upande \q2 katika siku ya maafa yake. \q1 \v 3 Usimwache mpiga upinde afunge kamba upinde wake, \q2 wala usimwache avae silaha zake. \q1 Usiwaonee huruma vijana wake; \q2 angamiza jeshi lake kabisa. \q1 \v 4 Wataanguka barabarani waliouawa katika nchi ya Wakaldayo, \q2 wakiwa na majeraha ya kutisha. \q1 \v 5 Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa \q2 na Mungu wao, Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q1 ingawa nchi yao imejaa uovu \q2 mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. \b \q1 \v 6 “Kimbieni kutoka Babeli! \q2 Okoeni maisha yenu! \q2 Msiangamizwe kwa sababu ya dhambi zake. \q1 Ni wakati wa kisasi cha Mwenyezi Mungu, \q2 atamlipa kile anachostahili. \q1 \v 7 Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu katika mkono wa Mwenyezi Mungu; \q2 aliufanya ulimwengu wote ulewe. \q1 Mataifa walikunywa mvinyo wake; \q2 kwa hiyo sasa wameingiwa na wazimu. \q1 \v 8 Babeli ataanguka ghafula na kuvunjika. \q2 Mwombolezeni! \q1 Tafuteni zeri ya kutuliza maumivu yake, \q2 labda anaweza kupona. \b \q1 \v 9 “ ‘Tungemponya Babeli, \q2 lakini hawezi kuponyeka; \q1 tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe, \q2 kwa kuwa hukumu yake inafika angani, \q2 inapanda juu hadi mawinguni.’ \b \q1 \v 10 “ ‘Mwenyezi Mungu amethibitisha haki yetu; \q2 njooni, tutangaze katika Sayuni \q2 kitu ambacho Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, amefanya.’ \b \q1 \v 11 “Noeni mishale, \q2 chukueni ngao! \q1 Mwenyezi Mungu amewaamsha wafalme wa Wamedi, \q2 kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli. \q1 Mwenyezi Mungu atalipiza kisasi, \q2 kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. \q1 \v 12 Inueni bendera dhidi ya kuta za Babeli! \q2 Imarisheni ulinzi, \q1 wekeni walinzi, \q2 andaeni waviziaji! \q1 Mwenyezi Mungu atatimiza kusudi lake, \q2 amri yake juu ya watu wa Babeli. \q1 \v 13 Wewe uishiye kando ya maji mengi \q2 na uliye na wingi wa hazina, \q1 mwisho wako umekuja, \q2 wakati wako wa kukatiliwa mbali. \q1 \v 14 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: \q1 ‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige, \q2 nao watashangilia kwa ushindi juu yako.’ \b \q1 \v 15 “Aliiumba dunia kwa uweza wake; \q2 akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, \q2 na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake. \q1 \v 16 Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; \q2 huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. \q1 Hupeleka miali ya radi pamoja na mvua, \q2 naye huuleta upepo kutoka ghala zake. \b \q1 \v 17 “Kila mtu ni mjinga na hana maarifa; \q2 kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. \q1 Vinyago vyake ni vya udanganyifu; \q2 havina pumzi. \q1 \v 18 Ni ubatili tu, vitu vya kufanyia mzaha; \q2 wakati wa hukumu yao, wataangamia. \q1 \v 19 Yeye Aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, \q2 kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, \q1 pamoja na kabila la urithi wake: \q2 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake. \b \q1 \v 20 “Wewe ndiwe rungu langu la vita, \q2 silaha yangu ya vita: \q1 kwa wewe navunjavunja mataifa, \q2 kwa wewe naangamiza falme, \q1 \v 21 kwa wewe navunjavunja \q2 farasi na mpanda farasi, \q1 kwa wewe navunjavunja \q2 gari la vita na mwendeshaji wake, \q1 \v 22 kwa wewe napondaponda \q2 mwanaume na mwanamke, \q1 kwa wewe napondaponda \q2 mzee na kijana, \q1 kwa wewe napondaponda \q2 kijana wa kiume na mwanamwali, \q1 \v 23 kwa wewe nampondaponda \q2 mchungaji na kundi, \q1 kwa wewe nampondaponda \q2 mkulima na maksai, \q1 kwa wewe nawapondaponda \q2 watawala na maafisa. \p \v 24 “Mbele ya macho yako nitamlipiza Babeli na wote wanaoishi Ukaldayo kwa ajili ya makosa yote waliyofanya katika Sayuni,” asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 25 “Mimi niko kinyume nawe, ee mlima unaoharibu, \q2 wewe uangamizaye dunia yote,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Nitanyoosha mkono wangu dhidi yako, \q2 nikuvingirishe kutoka kilele cha mwamba, \q2 na kukufanya mlima ulioteketezwa kwa moto. \q1 \v 26 Hakuna jiwe litakalochukuliwa kutoka kwako \q2 kwa ajili ya kufanywa jiwe la pembeni, \q1 wala jiwe lolote kwa ajili ya msingi, \q2 kwa maana utakuwa ukiwa milele,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 27 “Inueni bendera katika nchi! \q2 Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa! \q1 Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake, \q2 iteni falme hizi dhidi yake: \q2 Ararati, Mini na Ashkenazi. \q1 Wekeni jemadari dhidi yake, \q2 pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige. \q1 \v 28 Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake, \q2 wafalme wa Wamedi, \q1 watawala wao na maafisa wao wote, \q2 pamoja na nchi zote wanazotawala. \q1 \v 29 Nchi inatetemeka na kugaagaa, \q2 kwa kuwa makusudi ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Babeli yanasimama: \q1 yaani kuangamiza nchi ya Babeli \q2 ili pasiwepo atakayeishi humo. \q1 \v 30 Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana, \q2 wamebaki katika ngome zao. \q1 Nguvu zao zimekwisha, \q2 wamekuwa kama wanawake. \q1 Makazi yake yameteketezwa kwa moto, \q2 makomeo ya malango yake yamevunjika. \q1 \v 31 Tarishi mmoja humfuata mwingine, \q2 na mjumbe humfuata mjumbe, \q1 kumtangazia mfalme wa Babeli \q2 kwamba mji wake wote umetekwa, \q1 \v 32 Vivuko vya mito vimekamatwa, \q2 mabwawa yenye mafunjo yametiwa moto, \q2 nao askari wameingiwa na hofu kuu.” \p \v 33 Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: \q1 “Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria \q2 wakati inapokanyagwa; \q2 wakati wa kumvuna utakuja upesi.” \b \q1 \v 34 “Nebukadneza mfalme wa Babeli ametula, \q2 ametufanya tuchangayikiwe, \q2 ametufanya tuwe gudulia tupu. \q1 Ametumeza kama mnyama wa baharini, \q2 na kujaza tumbo lake kwa vyakula vyetu vizuri, \q2 kisha akatutapika. \q1 \v 35 Jeuri iliyotendewa miili yetu\f + \fr 51:35 \fr*\ft au \ft*\fqa Jeuri tuliyotendewa sisi na watoto wetu\fqa*\f* na iwe juu ya Babeli,” \q2 ndivyo wasemavyo wakaaji wa Sayuni. \q1 “Damu yetu na iwe juu ya wakaaji wa Babeli,” \q2 asema Yerusalemu. \p \v 36 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Tazama, nitakutetea \q2 na kukulipizia kisasi; \q1 nitaikausha bahari yake \q2 na kuzikausha chemchemi zake. \q1 \v 37 Babeli utakuwa lundo la magofu \q2 na makao ya mbweha, \q1 kitu cha kutisha na kudharauliwa, \q2 mahali asipoishi mtu. \q1 \v 38 Watu wake wote wananguruma kama simba wadogo, \q2 wanakoroma kama wana simba. \q1 \v 39 Lakini wakiwa wameamshwa, \q2 nitawaandalia karamu \q2 na kuwafanya walewe, \q1 ili washangilie kwa kicheko, \q2 kisha walale milele na wasiamke,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 40 “Nitawateremsha kama wana-kondoo \q2 wanaoenda machinjoni, \q2 kama kondoo dume na mbuzi. \b \q1 \v 41 “Tazama jinsi Sheshaki\f + \fr 51:41 \fr*\ft Sheshaki ni Babeli kwa fumbo.\ft*\f* atakavyokamatwa, \q2 majivuno ya dunia yote yatakavyonyakuliwa. \q1 Babeli atakuwa mwenye hofu kiasi gani \q2 kati ya mataifa! \q1 \v 42 Bahari itainuka juu ya Babeli; \q2 mawimbi yake yanayonguruma yatamfunika. \q1 \v 43 Miji yake itakuwa ukiwa, \q2 kame na jangwa, \q1 nchi isiyokuwa na mtu anayeishi ndani yake, \q2 ambayo hakuna mwanadamu atakayepita humo. \q1 \v 44 Nitamwadhibu Beli katika Babeli, \q2 na kumfanya atapike kitu alichokimeza. \q1 Mataifa hayatamiminika tena kwake. \q2 Nao ukuta wa Babeli utaanguka. \b \q1 \v 45 “Tokeni ndani yake, enyi watu wangu! \q2 Okoeni maisha yenu! \q2 Ikimbieni hasira kali ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 46 Msikate tamaa wala msiogope tetesi \q2 zitakaposikika katika nchi; \q1 tetesi moja inasikika mwaka huu, \q2 nyingine mwaka unaofuata; \q1 tetesi juu ya jeuri katika nchi, \q2 na ya mtawala dhidi ya mtawala. \q1 \v 47 Kwa kuwa hakika wakati utawadia \q2 nitakapoziadhibu sanamu za Babeli; \q1 nchi yake yote itatiwa aibu, \q2 na watu wake wote waliouawa \q2 wataangukia ndani yake. \q1 \v 48 Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo \q2 vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, \q1 kwa kuwa kutoka kaskazini \q2 waangamizi watamshambulia,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 49 “Babeli ni lazima aanguke kwa sababu ya kuwaua Waisraeli, \q2 kama vile waliouawa duniani kote \q2 walivyoanguka kwa sababu ya Babeli. \q1 \v 50 Wewe uliyepona upanga, \q2 ondoka wala usikawie! \q1 Mkumbuke Mwenyezi Mungu ukiwa katika nchi ya mbali, \q2 na utafakari juu ya Yerusalemu.” \b \q1 \v 51 “Tumetahayari, kwa sababu tumetukanwa \q2 na aibu imefunika nyuso zetu, \q1 kwa sababu wageni wameingia \q2 mahali patakatifu pa nyumba ya Mwenyezi Mungu.” \b \q1 \v 52 “Lakini siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, \q2 “nitakapoziadhibu sanamu zake, \q1 na katika nchi yake yote \q2 waliojeruhiwa watalia kwa maumivu makali. \q1 \v 53 Hata kama Babeli ikifika angani \q2 na kuziimarisha ngome zake ndefu, \q2 nitatuma waangamizi dhidi yake,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 54 “Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli, \q2 sauti ya uharibifu mkuu \q2 kutoka nchi ya Wakaldayo. \q1 \v 55 Mwenyezi Mungu ataiangamiza Babeli, \q2 atanyamazisha makelele ya kishindo chake. \q1 Mawimbi ya adui yatanguruma kama maji makuu, \q2 ngurumo ya sauti zao itavuma. \q1 \v 56 Mwangamizi atakuja dhidi ya Babeli; \q2 mashujaa wake watakamatwa, \q2 nazo pinde zao zitavunjwa. \q1 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa kisasi, \q2 yeye atalipiza kikamilifu. \q1 \v 57 Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, \q2 watawala wao, maafisa, pamoja na mashujaa wao; \q1 watalala milele na hawataamka,” \q2 asema Mfalme, ambaye jina lake ni Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni. \p \v 58 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: \q1 “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, \q2 na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; \q1 mataifa yanajichosha bure, \q2 taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.” \p \v 59 Huu ndio ujumbe ambao nabii Yeremia alimpa msimamizi wa nyumba ya mfalme, Seraya mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wake. \v 60 Yeremia alikuwa ameandika ndani ya kitabu kuhusu maafa yote yatakayoipata Babeli, yaani yote yaliyokuwa yameandikwa kuhusu Babeli. \v 61 Yeremia akamwambia Seraya, “Utakapofika Babeli, hakikisha kwamba umesoma maneno haya yote kwa sauti kubwa. \v 62 Kisha sema, ‘Ee Mwenyezi Mungu, umesema utaangamiza mahali hapa ili mtu wala mnyama asiishi ndani yake, napo patakuwa ukiwa milele.’ \v 63 Utakapomaliza kusoma hiki kitabu, kifungie jiwe kisha ukitupe ndani ya Mto Frati. \v 64 Kisha sema, ‘Hivi ndivyo Babeli utakavyozama na usiinuke tena, kwa sababu ya maafa nitakayoleta juu yake. Nao watu wake wataanguka.’ ” \b \p Maneno ya Yeremia yanaishia hapa. \c 52 \s1 Kuanguka kwa Yerusalemu \r (2 Wafalme 24:18–25:30) \p \v 1 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na moja. Mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna. \v 2 Alifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kama alivyofanya Yehoyakimu. \v 3 Haya yote yalitendeka Yerusalemu na Yuda kwa sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. \p Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli. \p \v 4 Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akiwa na jeshi lake lote alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Wakapiga kambi nje ya mji na kuuzingira pande zote. \v 5 Mji ulizingirwa na jeshi hadi mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Mfalme Sedekia. \p \v 6 Ilipowadia siku ya tisa ya mwezi wa nne, njaa ikazidi kuwa kali sana ndani ya mji, hadi hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu. \v 7 Kisha ukuta wa mji ukavunjwa na jeshi lote likakimbia. Wakaondoka mjini usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba. \v 8 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia Mfalme Sedekia na kumpata katika nchi tambarare za Yeriko. Askari wake wote wakatengwa naye na kutawanyika, \v 9 naye akakamatwa. \p Akapelekwa kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ambapo alimtangazia hukumu. \v 10 Huko Ribla mfalme wa Babeli aliwachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake. Pia akawaua maafisa wote wa Yuda. \v 11 Kisha akayang’oa macho ya Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli, alipomweka gerezani hadi siku ya kifo chake. \p \v 12 Siku ya kumi ya mwezi wa tano, katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme, aliyemtumikia mfalme wa Babeli, alikuja Yerusalemu. \v 13 Alichoma moto Hekalu la Mwenyezi Mungu, jumba la kifalme, na nyumba zote za Yerusalemu. Aliteketeza kila jengo muhimu. \v 14 Jeshi lote la Wakaldayo chini ya mkuu wa askari walinzi wa mfalme walivunja kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu. \v 15 Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawapeleka uhamishoni baadhi ya watu maskini sana na wale waliobaki katika mji, pamoja na mabaki ya watu wa kawaida, na wale waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli. \v 16 Lakini Nebuzaradani akawaacha mabaki ya wale watu maskini kabisa ili watunze mashamba ya mizabibu na mashamba mengine. \p \v 17 Wakaldayo walivunja nguzo za shaba, vishikilio vya shaba, na Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Kisha wakaichukua shaba yote wakaipeleka Babeli. \v 18 Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, sahani na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika Hekaluni. \v 19 Mkuu wa askari walinzi wa mfalme akachukua yale masinia, vile vyetezo, yale mabakuli ya kunyunyizia, zile sufuria, vile vinara vya taa, zile sahani na yale mabakuli yaliyotumika kwa sadaka za vinywaji, vitu vyote vile vilivyokuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi au fedha. \p \v 20 Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na wale mafahali kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, pamoja na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Mfalme Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ilikuwa na uzito mwingi usioweza kupimika. \v 21 Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane, kimo chake na mzunguko dhiraa kumi na mbili, na unene wa nyanda nne\f + \fr 52:21 \fr*\ft Nyanda 4 ni sawa na sentimita 30.\ft*\f*, na zote zilikuwa wazi ndani. \v 22 Sehemu ya shaba juu ya ile nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tano, na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na makomamanga yake ilifanana na hiyo ya kwanza. \v 23 Kulikuwa na makomamanga tisini na sita pembeni; jumla ya makomamanga juu ya wavu uliokuwa umezunguka yalikuwa mia moja. \p \v 24 Yule mkuu wa askari walinzi akawachukua kama wafungwa Seraya kuhani mkuu, kuhani Sefania aliyefuata kwa cheo, na mabawabu watatu. \v 25 Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri saba wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji. \v 26 Nebuzaradani jemadari akawachukua hao wote na kuwapeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. \v 27 Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe. \p Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao. \b \lh \v 28 Hii ndiyo hesabu ya watu ambao Nebukadneza aliwachukua kwenda uhamishoni: \b \li1 katika mwaka wa saba, \li2 Wayahudi elfu tatu na ishirini na watatu (3,023); \li1 \v 29 katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Nebukadneza, \li2 watu mia nane na thelathini na wawili (832) kutoka Yerusalemu; \li1 \v 30 katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake, \li2 Wayahudi mia saba na arobaini na watano (745) walichukuliwa kwenda uhamishoni na Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi wa mfalme. \lf Jumla ya watu wote walikuwa elfu nne mia sita. \b \s1 Yehoyakini aachiwa huru \p \v 31 Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki\f + \fr 52:31 \fr*\ft au \ft*\fqa Ameli-Mariduki\fqa*\f* alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini mfalme wa Yuda, na kumfungua kutoka gerezani siku ya ishirini na tano ya mwezi wa kumi na mbili. \v 32 Alizungumza naye kwa upole na kumpa kiti cha heshima kuliko wafalme wengine aliokuwa nao huko Babeli. \v 33 Hivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya gerezani, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme. \v 34 Siku kwa siku mfalme wa Babeli alimpa Yehoyakini posho siku zote za maisha yake, hadi siku ya kifo chake.