\id JDG - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Waamuzi \toc1 Waamuzi \toc2 Waamuzi \toc3 Amu \mt1 Waamuzi \c 1 \s1 Waisraeli wapigana na Wakanaani waliobaki \p \v 1 Baada ya kifo cha Yoshua, Waisraeli wakamuuliza Mwenyezi Mungu, “Ni nani atakayetangulia apande mbele yetu kutupigania dhidi ya Wakanaani?” \p \v 2 Mwenyezi Mungu akajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia; nimewapa hiyo nchi mikononi mwao.” \p \v 3 Ndipo wanaume wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. Sisi pia tutaenda pamoja nanyi katika sehemu yenu mliyopewa.” Basi Wasimeoni wakaenda pamoja nao. \p \v 4 Yuda aliposhambulia, Mwenyezi Mungu akawatia Wakanaani na Waperizi mikononi mwao, nao wakawaua watu elfu kumi huko Bezeki. \v 5 Huko ndiko walipomkuta huyo Adoni-Bezeki, nao wakapigana naye na kuwafukuza Wakanaani na Waperizi. \v 6 Adoni-Bezeki pia alikimbia, nao wakamfuata na kumkamata, wakamkata vidole vyake gumba vya mikono na vya miguu. \p \v 7 Ndipo Adoni-Bezeki akasema, “Wafalme sabini waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu walikuwa wakiokota makombo chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa haya kwa yale niliyowatendea.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko. \p \v 8 Wanaume wa Yuda wakashambulia pia Yerusalemu na kuiteka. Wakaupiga mji kwa upanga na kuuchoma kwa moto. \p \v 9 Baada ya hayo, watu wa Yuda wakateremka kupigana na Wakanaani walioishi katika nchi ya vilima, na Negebu, na nchi ya Shefela\f + \fr 1:9 \fr*\ft au \ft*\fqa upande wa magharibi chini ya vilima\fqa*\f*. \v 10 Yuda wakakabiliana na Wakanaani walioishi Hebroni (mji huu hapo awali uliitwa Kiriath-Arba) na kuwashinda Sheshai, Ahimani na Talmai. \p \v 11 Kutoka huko wakasonga mbele kukabiliana na watu walioishi Debiri (mji huu hapo awali uliitwa Kiriath-Seferi). \v 12 Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayepigana dhidi ya Kiriath-Seferi na kuuteka.” \v 13 Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa huyo Kalebu, akawashinda; kwa hiyo Kalebu akamtoa binti yake Aksa, akaolewa naye. \p \v 14 Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?” \p \v 15 Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Ndipo Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini. \p \v 16 Wazao wa yule Mkeni, baba mkwe wa Musa, wakapanda pamoja na watu wa Yuda kutoka Mji wa Mitende\f + \fr 1:16 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Yeriko\fqa*\f*, wakaenda kuishi miongoni mwa watu wa jangwa la Yuda huko Negebu karibu na mji wa Aradi. \p \v 17 Basi wanaume wa Yuda wakaenda na Wasimeoni ndugu zao, wakawashambulia Wakanaani walioishi Sefathi, nao wakauangamiza huo mji kabisa. Kwa hiyo huo mji ukaitwa Horma\f + \fr 1:17 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Maangamizi\fqa*\f*. \v 18 Watu wa Yuda wakatwaa pia Gaza, Ashkeloni na Ekroni, kila mji na vijiji vyake vinavyouzunguka. \p \v 19 Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na watu wa Yuda. Wakaimiliki nchi ya vilima, lakini hawakuweza kuwafukuza watu waliokaa katika hiyo tambarare, kwa sababu walikuwa na magari ya vita ya chuma. \v 20 Kama vile Musa alivyoahidi, Kalebu alipewa Hebroni, naye akawafukuza wana watatu wa Anaki. \v 21 Hata hivyo, Wabenyamini walishindwa kuwafukuza Wayebusi, walioishi Yerusalemu; hivyo hadi leo Wayebusi huishi humo pamoja na Wabenyamini. \p \v 22 Basi nyumba ya Yusufu wakashambulia Betheli, naye Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja nao. \v 23 Walipotuma watu kwenda kupeleleza Betheli (ambao hapo awali uliitwa Luzu), \v 24 wale wapelelezi wakaona mtu anatoka mjini, nao wakamwambia, “Tuoneshe jinsi ya kuingia mjini nasi tutakutendea wema.” \v 25 Hivyo akawaonesha, nao wakaupiga mji kwa upanga lakini wakamhifadhi hai yule mtu na jamaa yake yote. \v 26 Yule mtu akaenda hadi nchi ya Wahiti, ambapo aliujenga mji na kuuita Luzu, ambalo ndilo jina lake hadi leo. \p \v 27 Lakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na makazi yake, au watu wa Taanaki na makazi yake, au watu wa Dori na makazi yake, au watu wa Ibleamu na makazi yake, au watu wa Megido na makazi yake, kwa kuwa Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi ile. \v 28 Israeli walipopata nguvu, wakawatia Wakanaani katika kazi ya kulazimishwa, lakini kamwe hawakuwafukuza watoke kabisa. \v 29 Wala Efraimu hawakuwafukuza kabisa Wakanaani walioishi Gezeri, bali Wakanaani waliendelea kuishi miongoni mwao. \v 30 Vivyo hivyo Zabuloni hawakuwafukuza Wakanaani walioishi huko Kitroni, na walioishi Nahaloli, bali Wakanaani hao walibaki miongoni mwao; lakini waliwatia katika kazi ya kulazimishwa. \v 31 Wala Asheri hawakuwafukuza wale walioishi huko Ako, Sidoni, Alabu, Akzibu, Helba, Afeki wala Rehobu, \v 32 na kwa sababu ya jambo hili Waasheri wakaishi miongoni mwa Wakanaani, wenyeji wa nchi. \v 33 Wala Naftali hawakuwafukuza wale walioishi Beth-Shemeshi wala wale walioishi Beth-Anathi; lakini Naftali nao pia wakaishi miongoni mwa Wakanaani, wenyeji wa nchi, nao wale walioishi Beth-Shemeshi na Beth-Anathi wakawa watumishi wao katika kazi ya kulazimishwa. \v 34 Waamori wakawazuilia Wadani kwenye nchi ya vilima, na hawakuwaacha washuke kuingia kwenye sehemu tambarare. \v 35 Waamori pia walikuwa wameamua kuendelea kuishi katika Mlima Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu; lakini nguvu ya nyumba ya Yusufu ilipoongezeka, wao pia wakashindwa na wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa. \v 36 Mpaka wa Waamori ulikuwa kuanzia Genge la Akrabimu, kuendelea hadi Sela na kuelekea juu. \c 2 \s1 Malaika wa Mwenyezi Mungu huko Bokimu \p \v 1 Malaika wa Mwenyezi Mungu akakwea kutoka Gilgali hadi Bokimu, naye akasema, “Niliwapandisha kutoka Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyoapa kuwapa baba zenu. Nikasema, ‘Kamwe sitalivunja agano langu nanyi. \v 2 Msifanye agano na watu wa nchi hii, bali mtabomoa madhabahu yao.’ Lakini ninyi hamkunitii mimi. Kwa nini mmefanya jambo hili? \v 3 Sasa basi ninawaambia kuwa sitawafukuza watoke kati yenu, ila watakuwa mitego kwenu, nayo miungu yao itakuwa tanzi kwenu.” \p \v 4 Malaika wa Mwenyezi Mungu alipomaliza kusema mambo haya kwa Waisraeli wote, watu wakalia kwa sauti kuu. \v 5 Wakapaita mahali pale Bokimu. Nao wakamtolea Mwenyezi Mungu sadaka. \s1 Kifo cha Yoshua \p \v 6 Baada ya Yoshua kuwapa watu ruhusa waende zao, Waisraeli wakaenda kwenye urithi wao wenyewe ili kumiliki nchi yao. \v 7 Watu wakamtumikia Mwenyezi Mungu siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, wale waliokuwa wameona mambo makuu ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli. \p \v 8 Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Mwenyezi Mungu, akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. \v 9 Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Heresi\f + \fr 2:9 \fr*\ft Unajulikana pia kama \ft*\fqa Timnath-Sera\fqa*\ft (taz. \+xt Yoshua 19:50; 24:30\+xt*).\ft*\f* katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaashi. \p \v 10 Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua Mwenyezi Mungu, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli. \v 11 Kwa hiyo Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu na kuwatumikia Mabaali. \v 12 Wakamwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, aliyekuwa amewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata na kuiabudu miungu mbalimbali ya mataifa yaliyowazunguka. Wakamkasirisha Mwenyezi Mungu, \v 13 kwa sababu walimwacha na kutumikia Baali na Maashtorethi. \v 14 Hivyo hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao. \v 15 Wakati wowote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa kinyume nao ili awashinde, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa. \p \v 16 Ndipo Mwenyezi Mungu akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa kutoka mikononi mwa hao wavamizi. \v 17 Lakini hawakuwasikiliza hata waamuzi wao, bali walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine na kuiabudu. Waligeuka upesi na kuiacha njia ambayo baba zao waliiendea, yaani njia ya kutii amri za Mwenyezi Mungu. \v 18 Kila mara Mwenyezi Mungu alipowainulia mwamuzi, Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha. \v 19 Lakini kila mara mwamuzi alipofariki, watu walirudia katika hali mbaya ya uovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine, ili kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao maovu na njia zao za ukaidi. \p \v 20 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawakasirikia sana Israeli na kusema, “Kwa kuwa taifa hili limevunja agano lile nililofanya na baba zao na hawakunisikiliza, \v 21 mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki. \v 22 Nitawatumia mataifa hao ili nipate kuwapima Israeli, nione kama wataishika njia ya Mwenyezi Mungu na kuenenda kwa njia hiyo jinsi baba zao walivyofanya.” \v 23 Mwenyezi Mungu alikuwa ameyaacha hayo mataifa yabaki; hakuyaondoa mara moja kwa kuyatia mikononi mwa Yoshua. \c 3 \s1 Mataifa yaliyobaki katika nchi \p \v 1 Haya ndio mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliyaacha ili kuwajaribu Waisraeli wote ambao hawakushiriki vita yoyote huko Kanaani \v 2 (alifanya hivi ili tu kuwafundisha vita wazao wa Waisraeli ambao hawakuwa na uzoefu wa vita hapo awali): \v 3 watawala watano wa Wafilisti, pamoja na Wakanaani wote, Wasidoni, na Wahivi walioishi katika milima ya Lebanoni kuanzia Mlima wa Baal-Hermoni hadi Lebo-Hamathi. \v 4 Waliachwa ili kuwajaribu Waisraeli, kuona kama wangetii amri za Mwenyezi Mungu, alizokuwa amewapa baba zao kwa mkono wa Musa. \p \v 5 Waisraeli wakaishi miongoni mwa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 6 Wakaoa binti za hao mataifa, na wakawatoa binti zao wenyewe waolewe na wana wa hao mataifa, na wakaitumikia miungu yao. \s1 Othnieli \p \v 7 Waisraeli wakafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, wakamsahau Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na kutumikia Mabaali na Maashera. \v 8 Hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Israeli. Hivyo akawauza mikononi mwa Kushan-Rishathaimu mfalme wa Mesopotamia, nao Waisraeli wakamtumikia kwa muda wa miaka nane. \v 9 Waisraeli walipomlilia Mwenyezi Mungu, yeye akawainulia mkombozi, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, ambaye aliwaokoa. \v 10 Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake; hivyo akawa mwamuzi wa Israeli, na akaenda vitani. Mwenyezi Mungu akamtia Kushan-Rishathaimu mfalme wa Mesopotamia mikononi mwa Othnieli, naye akamshinda. \v 11 Hivyo nchi ikawa na amani kwa muda wa miaka arobaini, hadi Othnieli mwana wa Kenazi alipofariki. \s1 Ehudi \p \v 12 Waisraeli wakafanya maovu mbele za Mwenyezi Mungu tena; na kwa kuwa walifanya maovu hayo, Mwenyezi Mungu akamtia nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli. \v 13 Egloni akawakusanya Waamoni na Waamaleki kwake, wakashambulia Israeli, na wakatwaa Mji wa Mitende\f + \fr 3:13 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Yeriko\fqa*\f*. \v 14 Waisraeli wakawa chini ya Egloni mfalme wa Moabu kwa muda wa miaka kumi na nane. \p \v 15 Waisraeli wakamlilia tena Mwenyezi Mungu, naye akawapa mkombozi: Ehudi, mtu wa shoto, mwana wa Gera Mbenyamini. Waisraeli wakatuma kwa Egloni mfalme wa Moabu ushuru kwa mkono wa Ehudi. \v 16 Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga ukatao kuwili, ukiwa na urefu wa kama dhiraa moja\f + \fr 3:16 \fr*\ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\ft*\f*, naye akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake, kwenye paja lake la mkono wa kuume. \v 17 Akamkabidhi ushuru Egloni mfalme wa Moabu, aliyekuwa mtu mnene sana. \v 18 Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, akawatuma wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru waende zao. \v 19 Ehudi akafuatana nao hadi kwenye sanamu za mawe karibu na Gilgali, ndipo yeye akarudi, akafika kwa Egloni na kusema, “Ee Mfalme, ninao ujumbe wa siri kwako.” \p Mfalme akasema, “Nyamazeni kimya!” Nao wale waliomhudumia wote wakamwacha, wakatoka nje. \p \v 20 Ndipo Ehudi akamsogelea alipokuwa ameketi peke yake kwenye chumba cha juu cha jumba lake la kifalme la majira ya kiangazi, na kusema, “Ninao ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yako.” Mfalme alipokuwa anainuka kutoka kiti chake, \v 21 Ehudi akaunyoosha mkono wake wa kushoto na kuufuta ule upanga aliokuwa ameufunga kwenye paja lake la kulia, akamdunga Mfalme Egloni tumboni mwake. \v 22 Hata mpini nao ukazama tumboni pamoja na upanga wenyewe, nao upanga ukatokea mgongoni mwake. Ehudi hakuuchomoa huo upanga, nayo mafuta yakashikamana juu ya upanga. \v 23 Ehudi akatoka nje barazani; akamfungia milango ya chumba cha juu, na kuifunga kwa funguo. \p \v 24 Baada yake kuondoka, watumishi wakaja na kupata milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka anajisaidia chumba cha ndani.” \v 25 Wakangoja hadi wakawa na fadhaa, na wakati hakuifungua milango ya chumba, wakachukua funguo na kuifungua. Tazama, wakaona bwana wao amelala sakafuni, amekufa. \p \v 26 Walipokuwa wangali wanangoja, Ehudi akatoroka, akapita hapo kwenye sanamu ya kuchora kwenye mawe na kukimbilia Seira. \v 27 Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza. \p \v 28 Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakateremka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakumwacha mtu yeyote kuvuka. \v 29 Wakati huo wakawaua Wamoabu wapatao elfu kumi wenye nguvu na mashujaa; hakuna yeyote aliyetoroka. \v 30 Siku ile Moabu wakashindwa na Israeli, nayo nchi ikawa na amani kwa miaka themanini. \s1 Shamgari \p \v 31 Baada ya Ehudi akaja Shamgari mwana wa Anathi, aliyewapiga Wafilisti mia sita kwa fimbo ya ng’ombe. Naye pia akawaokoa Waisraeli. \c 4 \s1 Debora \p \v 1 Baada ya Ehudi kufa, Waisraeli wakafanya tena maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. \v 2 Hivyo Mwenyezi Mungu akawatia mikononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Jemadari wa jeshi lake alikuwa Sisera, aliyeishi huko Haroshethi-Hagoyimu\f + \fr 4:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Haroshethi ya Mataifa\fqa*\f*. \v 3 Kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya vita ya chuma yapatayo mia tisa, naye alikuwa amewatesa Waisraeli kwa ukatili kwa muda wa miaka ishirini, Waisraeli wakamlilia Mwenyezi Mungu wakaomba msaada. \p \v 4 Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye alikuwa anaamua Israeli wakati ule. \v 5 Debora alikuwa akiketi chini ya Mtende wa Debora uliokuwa kati ya Rama na Betheli katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakaja kwake ili awaamue. \v 6 Akatuma wamwite Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali na kumwambia, “Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, anakuagiza: ‘Nenda, chukua wanaume elfu kumi toka Naftali na Zabuloni, mwende Mlima Tabori. \v 7 Nitamshawishi Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, pamoja na magari yake ya vita na jeshi lake, hadi Mto Kishoni na kumtia mikononi mwako.’ ” \p \v 8 Baraka akamwambia, “Ukienda pamoja nami nitaenda, lakini usipoenda pamoja nami, sitaenda.” \p \v 9 Debora akamwambia, “Hakika nitaenda pamoja nawe, lakini njia unayoiendea haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Mwenyezi Mungu atamtia Sisera mikononi mwa mwanamke.” Hivyo Debora akaenda pamoja na Baraka hadi Kedeshi, \v 10 ambapo Baraka aliwaita Zabuloni na Naftali. Watu elfu kumi wakamfuata Baraka, na Debora pia akaenda naye. \p \v 11 Basi Heberi, Mkeni, alikuwa amejitenga na Wakeni wale wengine, yaani wazao wa Hobabu, mkwewe Musa, naye akapiga hema lake karibu na ule mti mkubwa wa mwaloni ulio Saananimu, karibu na Kedeshi. \p \v 12 Sisera alipoambiwa kuwa Baraka mwana wa Abinoamu alikuwa amepanda Mlima Tabori, \v 13 Sisera akakusanya magari yake ya vita ya chuma mia tisa, na watu wote waliokuwa pamoja naye, kuanzia Haroshethi-Hagoyimu hadi Mto wa Kishoni. \p \v 14 Ndipo Debora akamwambia Baraka, “Nenda! Hii ndiyo siku ambayo Mwenyezi Mungu amemtia Sisera mikononi mwako. Je, Mwenyezi Mungu hakukutangulia mbele yako?” Hivyo Baraka akashuka kutoka Mlima Tabori, akifuatwa na watu elfu kumi. \v 15 Mwenyezi Mungu akamfadhaisha Sisera na magari yake ya vita yote, pamoja na jeshi lake lote kwa upanga mbele ya Baraka, naye Sisera akaliacha gari lake la vita na kukimbia kwa miguu. \v 16 Lakini Baraka akafuata magari ya vita pamoja na jeshi hadi Haroshethi-Hagoyimu. Jeshi lote la Sisera likaanguka kwa upanga, wala hakuna hata mtu mmoja aliyesalia. \p \v 17 Sisera, hata hivyo, akakimbia kwa miguu hadi kwenye hema la Yaeli, mkewe Heberi, Mkeni, kwa sababu palikuwa na uhusiano wa kirafiki kati ya Yabini mfalme wa Hazori na ukoo wa Heberi, Mkeni. \p \v 18 Yaeli akaenda kumlaki Sisera na kumwambia, “Karibu, bwana wangu, karibu ingia ndani kabisa. Usiogope.” Basi Sisera akaingia ndani ya hema la Yaeli, naye akamfunika kwa blanketi nene. \p \v 19 Akamwambia, “Nina kiu, tafadhali nipe maji ya kunywa.” Ndipo akafungua kiriba cha maziwa na kumpa akanywa, kisha akamfunika. \p \v 20 Naye Sisera akamwambia, “Simama mlangoni pa hema na mtu yeyote akija na kukuuliza, ‘Je, kuna mtu yeyote hapa?’ sema, ‘Hapana.’ ” \p \v 21 Lakini Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akachukua nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akiwa amelala usingizi kwa kuchoka. Akakipigilia kile kigingi kwenye paji la uso wake, kikapenya hata kuingia ardhini, naye akafa. \p \v 22 Baraka akakaribia akimfuatia Sisera, Yaeli akatoka kumlaki. Akamwambia, “Njoo, nitakuonesha mtu unayemtafuta.” Hivyo wakaingia ndani ya hema, na tazama, Sisera alikuwa amelala humo akiwa amekufa, na hicho kigingi cha hema kikiwa kimepigiliwa kupitia paji la uso wake. \p \v 23 Basi siku ile Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani, mbele ya Israeli. \v 24 Nao mkono wa Waisraeli ukaendelea kuwa na nguvu zaidi na zaidi dhidi ya Yabini, mfalme wa Kanaani, hadi wakamwangamiza. \c 5 \s1 Wimbo wa Debora \p \v 1 Siku hiyo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu: \q1 \v 2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza, \q2 wakati watu wanapojitoa \q2 kwa hiari yao wenyewe: \q2 mhimidini Mwenyezi Mungu! \b \b \q1 \v 3 “Sikieni hili, enyi wafalme! \q2 Sikilizeni, enyi watawala! \q1 Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, nitaimba; \q2 kwa wimbo nitamhimidi Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa Israeli. \b \b \q1 \v 4 “Ee Mwenyezi Mungu, ulipotoka katika Seiri, \q2 ulipopita katika mashamba ya Edomu, \q1 nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, \q2 naam, mawingu yakamwaga maji. \q1 \v 5 Milima ilitetemeka mbele za Mwenyezi Mungu, Yule wa Sinai, \q2 mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \b \q1 \v 6 “Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, \q2 katika siku za Yaeli, \q1 barabara kuu hazikuwa na watu; \q2 wasafiri walipita njia za kando. \q1 \v 7 Mashujaa walikoma katika Israeli, \q2 walikoma hadi mimi, Debora, nilipoinuka, \q2 nilipoinuka kama mama katika Israeli. \q1 \v 8 Mungu alichagua viongozi wapya \q2 vita vilipokuja malangoni ya mji; \q1 lakini hapakuonekana ngao wala mkuki \q2 miongoni mwa watu elfu arobaini katika Israeli. \q1 \v 9 Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, \q2 u pamoja na wale wanaojitoa kwa hiari yao \q2 miongoni mwa watu. \q2 Mhimidini Mwenyezi Mungu! \b \q1 \v 10 “Ninyi mpandao punda weupe, \q2 mkiketi juu ya matandiko ya thamani, \q2 nanyi mnaotembea barabarani, \q1 fikirini \v 11 kuhusu sauti za waimbaji \q2 mahali pa kunyweshea maji. \q1 Wanasimulia matendo ya haki ya Mwenyezi Mungu, \q2 matendo ya haki ya mashujaa wake \q2 katika Israeli. \b \q1 “Ndipo watu wa Mwenyezi Mungu \q2 walipoteremka malangoni pa mji. \q1 \v 12 ‘Amka, amka! Debora! \q2 Amka, amka, uimbe! \q1 Ee Baraka! Inuka, \q2 chukua mateka wako uliowateka, \q2 ee mwana wa Abinoamu.’ \b \q1 \v 13 “Ndipo mabaki ya watu \q2 wakashuka dhidi ya wakuu, \q1 watu wa Mwenyezi Mungu wakashuka kwangu \q2 dhidi ya wenye nguvu. \q1 \v 14 Baadhi yao walitoka Efraimu, \q2 ambao chimbuko lao ni Amaleki; \q1 Benyamini alikuwa miongoni \q2 mwa watu waliokufuata. \q1 Kutoka Makiri wakashuka viongozi, \q2 na kutoka Zabuloni wale washikao \q2 fimbo ya jemadari. \q1 \v 15 Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora; \q2 naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka, \q1 wakija nyuma yake kwa mbio \q2 wakielekea bondeni. \q1 Katika jamaa za Reubeni, \q2 palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. \q1 \v 16 Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo \q2 kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? \q1 Kwa jamaa za Reubeni, \q2 palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. \q1 \v 17 Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani. \q2 Naye Dani, kwa nini alikaa \q2 kwenye merikebu siku nyingi? \q1 Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari, \q2 akikaa kwenye ghuba zake ndogo. \q1 \v 18 Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, \q2 vilevile nao watu wa Naftali. \b \q1 \v 19 “Wafalme walikuja na kufanya vita; \q2 wafalme wa Kanaani walipigana \q2 huko Taanaki, karibu na maji ya Megido, \q2 lakini hawakuchukua nyara za fedha. \q1 \v 20 Kutoka mbinguni nyota zilipigana, \q2 nyota kutoka njia zake \q2 zilipigana na Sisera. \q1 \v 21 Mto wa Kishoni uliwasomba, \q2 ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. \q1 Songa mbele, ee nafsi yangu, \q2 kwa ujasiri! \q1 \v 22 Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: \q2 farasi wake wenye nguvu \q2 huenda mbio kwa kurukaruka. \q1 \v 23 Malaika wa Mwenyezi Mungu akasema, ‘Laani Merozi. \q2 Laani watu wake kwa uchungu, \q1 kwa kuwa hawakuja kumsaidia Mwenyezi Mungu, \q2 kumsaidia Mwenyezi Mungu dhidi ya hao wenye nguvu.’ \b \b \q1 \v 24 “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, \q2 mkewe Heberi, Mkeni, \q1 abarikiwe kuliko wanawake wote \q2 wanaoishi kwenye mahema. \q1 \v 25 Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa; \q2 kwenye bakuli la heshima \q2 akamletea maziwa mgando. \q1 \v 26 Akanyoosha mkono wake \q2 akashika kigingi cha hema, \q1 mkono wake wa kuume \q2 ukashika nyundo ya fundi. \q1 Akampiga Sisera kwa nyundo, \q2 akamponda kichwa chake, \q1 akamvunjavunja na kumtoboa \q2 paji lake la uso. \q1 \v 27 Aliinama miguuni pa Yaeli, \q2 akaanguka; akalala hapo. \q1 Alipoinama miguuni pake, \q2 alianguka; \q1 pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, \q2 akiwa amekufa. \b \q1 \v 28 “Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; \q2 nyuma ya dirisha alilia, akasema, \q1 ‘Mbona gari lake la vita linachelewa kufika? \q2 Mbona vishindo vya magari yake ya vita \q2 vimechelewa?’ \q1 \v 29 Wajakazi wale wenye busara \q2 kuliko wengine wote wanamjibu; \q2 naam, naye anasema moyoni mwake, \q1 \v 30 ‘Je, hawapati na kugawanya nyara: \q2 msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, \q1 mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, \q2 mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, \q1 mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: \q2 haya yote yakiwa nyara?’ \b \b \q1 \v 31 “Adui zako wote na waangamie hivyo, Ee Mwenyezi Mungu! \q2 Bali wote wanaokupenda na wawe kama jua \q2 linavyochomoza kwa nguvu zake.” \p Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini. \c 6 \s1 Gideoni \p \v 1 Waisraeli wakafanya tena yaliyo maovu mbele za Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu akawatia mikononi mwa Wamidiani kwa muda wa miaka saba. \v 2 Kwa kuwa Wamidiani walikuwa na nguvu juu yao, Waisraeli walijitengenezea maficho milimani, kwenye mapango, na katika ngome. \v 3 Kila wakati Waisraeli walipopanda mazao mashambani, Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki walivamia nchi yao. \v 4 Wakapiga kambi katika mashamba yao na kuharibu mazao ya nchi yote hadi kufikia Gaza, wala hawakuacha kiumbe chochote kilicho hai kwa Waisraeli, iwe kondoo au ng’ombe au punda. \v 5 Walipanda na mifugo yao na mahema yao, mfano wa makundi ya nzige. Ilikuwa haiwezekani kuwahesabu watu na ngamia wao; wakavamia nchi ili kuiharibu. \v 6 Wamidiani wakaifanya Israeli kuwa maskini sana, hata Waisraeli wakamlilia Mwenyezi Mungu kumwomba msaada. \p \v 7 Waisraeli walipomlilia Mwenyezi Mungu kwa sababu ya Wamidiani, \v 8 Mwenyezi Mungu akawapelekea nabii, ambaye aliwaambia, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: Niliwapandisha mtoke Misri, toka nchi ya utumwa. \v 9 Nikawaokoa kutoka mikononi mwa Wamisri na kutoka mikononi mwa watesi wenu wote. Nikawafukuza watoke mbele yenu, nami nikawapa ninyi nchi yao. \v 10 Nikawaambia, ‘Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu; msiiabudu miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao!’ Lakini ninyi hamkuitii sauti yangu.” \p \v 11 Malaika wa Mwenyezi Mungu akaja akaketi chini ya mwaloni ulio Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi Mwabiezeri, pale Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione. \v 12 Malaika wa Mwenyezi Mungu alipomtokea Gideoni, akamwambia, “Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe, ewe shujaa mwenye nguvu.” \p \v 13 Gideoni akajibu, “Nisamehe, Ee Bwana wangu. Kama Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi yale matendo yake makuu ambayo baba zetu walitusimulia juu yake waliposema, ‘Je, Mwenyezi Mungu hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa Mwenyezi Mungu ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” \p \v 14 Mwenyezi Mungu akamgeukia na kusema “Nenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kutoka mikononi mwa Wamidiani. Je, si mimi ninayekutuma wewe?” \p \v 15 Gideoni akauliza, “Ee Bwana wangu, nitawezaje kuwaokoa Israeli? Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.” \p \v 16 Mwenyezi Mungu akamjibu, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.” \p \v 17 Gideoni akajibu, “Kama basi nimepata kibali machoni pako, nipe ishara kuonesha kuwa kweli ni wewe unayesema nami. \v 18 Tafadhali nakuomba usiondoke hapa hadi nitakaporudi, nilete sadaka yangu na kuiweka mbele yako.” \p Naye Mwenyezi Mungu akamwambia, “Nitangoja hadi utakaporudi.” \p \v 19 Gideoni akaingia ndani ya nyumba yake na kuandaa mwana-mbuzi pamoja na kuoka mikate isiyotiwa chachu kutokana na efa moja\f + \fr 6:19 \fr*\ft Efa moja ni sawa na lita 22.\ft*\f* ya unga. Akaweka nyama kwenye kikapu na mchuzi kwenye chungu, akamletea huyo malaika hapo nje chini ya mwaloni, akampa. \p \v 20 Malaika wa Mungu akamwambia, “Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uviweke juu ya mwamba huu na umimine huo mchuzi juu yake.” Gideoni akafanya hivyo. \v 21 Malaika wa Mwenyezi Mungu akainyoosha fimbo iliyokuwa mkononi mwake, ncha yake ikagusa ile nyama na ile mikate isiyotiwa chachu, nao moto ukatoka kwenye mwamba ukateketeza ile nyama na ile mikate. Malaika wa Mwenyezi Mungu akatoweka machoni pake. \v 22 Gideoni alipotambua kuwa ni malaika wa Mwenyezi Mungu, akapaza sauti, akasema, “Ole wangu, Bwana Mungu Mwenyezi! Kwa kuwa nimemwona malaika wa Mwenyezi Mungu uso kwa uso!” \p \v 23 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope. Hutakufa.” \p \v 24 Hivyo Gideoni akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu mahali pale na kupaita Yehova-Shalomu\f + \fr 6:24 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwenyezi Mungu ni Amani\fqa*\f*. Hata leo imesimama huko Ofra ya Waabiezeri. \p \v 25 Usiku ule ule Mwenyezi Mungu akamwambia, “Mchukue ng’ombe dume wa baba yako, yule wa pili mwenye miaka saba, ubomoe madhabahu ya Baali aliyo nayo baba yako, na ukaikate nguzo ya Ashera iliyo karibu nayo. \v 26 Kisha mjengee Mwenyezi Mungu, Mungu wako, madhabahu kwa taratibu zake juu ya mwamba katika ngome hii. Kwa kutumia kuni za hiyo nguzo ya Ashera uliyoikatakata, mtoe sadaka huyo dume wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa.” \p \v 27 Basi Gideoni akawachukua watumishi wake kumi na kufanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwambia. Lakini kwa kuwa aliwaogopa jamaa yake na watu wa mji, akafanya haya usiku badala ya mchana. \p \v 28 Watu wa mji walipoamka asubuhi, tazama madhabahu ya Baali imebomolewa, na nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwakatwa, na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya madhabahu iliyojengwa upya! \p \v 29 Wakaulizana, “Ni nani aliyetenda mambo haya?” \p Walipochunguza kwa makini, wakaambiwa, “Ni Gideoni mwana wa Yoashi, ndiye alitenda hivi.” \p \v 30 Watu wa mji wakamwambia Yoashi, “Mlete mwanao hapa. Ni lazima afe, kwa sababu amebomoa madhabahu ya Baali na kukatakata nguzo ya Ashera iliyokuwa karibu nayo.” \p \v 31 Lakini Yoashi akaambia umati wa watu waliomzunguka wakiwa kinyume naye, “Je, ninyi mtamtetea Baali? Mnajaribu kumwokoa? Yeyote mwenye kumpigania atauawa kufikia kesho asubuhi! Kama Baali ni mungu kweli, anaweza kujitetea mwenyewe wakati mtu anapobomoa madhabahu yake.” \v 32 Basi siku ile wakamwita Gideoni “Yerub-Baali,” yaani “Baali na ashindane naye,” kwa sababu alibomoa madhabahu yake. \p \v 33 Basi Wamidiani wote, Waamaleki na mataifa mengine ya mashariki wakaunganisha majeshi yao, wakavuka ng’ambo ya Yordani na kupiga kambi katika Bonde la Yezreeli. \v 34 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akamjia Gideoni, naye Gideoni akapiga tarumbeta kuwaita Waabiezeri ili wamfuate. \v 35 Akatuma wajumbe waende katika Manase yote, akiwataka wachukue silaha na pia katika Asheri, Zabuloni na Naftali, nao wakakwea ili kukutana nao. \p \v 36 Gideoni akamwambia Mungu, “Kama utawaokoa Waisraeli kwa mkono wangu, kama ulivyoahidi: \v 37 tazama, nitaweka manyoya ya kondoo kwenye sakafu ya kupuria nafaka, na kama utakuwepo umande juu ya manyoya tu, na ardhi yote ikiwa kavu, ndipo nitakapojua kuwa utaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema.” \v 38 Hivyo ndivyo ilivyotokea. Gideoni akaamka asubuhi na mapema kesho yake, akayakamua yale manyoya yenye umande, yakatoka maji kiasi cha kujaa bakuli. \p \v 39 Kisha Gideoni akamwambia Mwenyezi Mungu, “Usinikasirikie. Ninaomba nifanye ombi moja lingine. Niruhusu nifanye jaribio jingine moja kwa manyoya haya. Wakati huu uyafanye manyoya kuwa kavu, na ardhi yote ifunikwe na umande.” \v 40 Usiku ule Mungu akafanya hivyo. Manyoya yakawa kavu, na ardhi yote ikafunikwa na umande. \c 7 \s1 Gideoni awashinda Wamidiani \p \v 1 Ndipo Yerub-Baali (yaani Gideoni) na lile jeshi lililokuwa pamoja naye, wakaondoka asubuhi na mapema na kupiga kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Wamidiani ilikuwa kaskazini mwao katika bonde, karibu na kilima cha More. \v 2 Mwenyezi Mungu akamwambia Gideoni, “Jeshi lililo pamoja nawe ni kubwa sana kwangu kuwatia Wamidiani mikononi mwao, Israeli asije akajisifu juu yangu, akisema, ‘Mkono wangu ndio uliniokoa.’ \v 3 Kwa hiyo sasa tangaza jeshi lote likiwa linasikia, kwamba: ‘Yeyote anayeogopa na kutetemeka, yeye na arudi nyumbani, aondoke katika Mlima Gileadi.’ ” Hivyo, watu elfu ishirini na mbili wakarudi nyumbani, wakabaki elfu kumi. \p \v 4 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia Gideoni, “Idadi ya jeshi bado ni kubwa. Wapeleke kwenye maji, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako. Nikikuambia, ‘Huyu ataenda pamoja nawe,’ yeye ataenda; lakini nikisema, ‘Huyu hataenda pamoja nawe,’ yeye hataenda.” \p \v 5 Gideoni akalipeleka lile jeshi kwenye maji, naye Mwenyezi Mungu akamwambia Gideoni, “Watenganishe watakaoramba maji kwa ulimi kama mbwa, na wale watakaopiga magoti ili kunywa.” \v 6 Waliokunywa kwa kuramba maji kutoka mikononi mwao walikuwa watu mia tatu. Wengine wote walipiga magoti ili kunywa. \p \v 7 Mwenyezi Mungu akamwambia Gideoni, “Kupitia hao watu mia tatu walioramba maji nitawaokoa ninyi, nami nitawatia Wamidiani mkononi mwako. Waache hao watu wengine wote warudi kila mmoja nyumbani mwake.” \v 8 Hivyo Gideoni akawaruhusu wale Waisraeli wengine kila mmoja aende kwenye hema lake. Akabakia na wale mia tatu, nao wakachukua vyakula na tarumbeta za wenzao. \p Basi kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake bondeni. \v 9 Usiku ule ule Mwenyezi Mungu akamwambia Gideoni, “Ondoka, ushuke ushambulie kambi, kwa kuwa nimeitia mkononi mwako. \v 10 Lakini kama unaogopa kushambulia, shuka kambini pamoja na mtumishi wako Pura, \v 11 nawe sikiliza wanayosema. Hatimaye, utatiwa moyo kushambulia kambi.” Basi yeye na Pura, mtumishi wake, wakashuka na kuwafikia walinzi wa mbele wa kambi. \v 12 Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine yote ya mashariki walikaa bondeni, nao walikuwa mfano wa nzige kwa wingi wao. Ngamia wao hawangehesabika, wingi wao ulikuwa kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. \p \v 13 Gideoni alifika mara tu mtu mmoja alipokuwa akimweleza mwenzake ndoto yake, akisema, “Tazama, niliota ndoto, mkate wa shayiri ulioviringana ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukaipiga hema kwa nguvu, na kusababisha hema hilo kupinduka na kuporomoka.” \p \v 14 Rafiki yake akamjibu, “Habari hii si kitu kingine isipokuwa upanga wa Gideoni mwana wa Yoashi, Mwisraeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote mkononi mwake.” \p \v 15 Gideoni alipoisikia hiyo ndoto na tafsiri yake, akasujudu na kuabudu. Akarudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, “Inukeni! Mwenyezi Mungu amelitia jeshi la Wamidiani mikononi mwenu.” \v 16 Akawagawa wale watu mia tatu katika makundi matatu, akawakabidhi tarumbeta mikononi mwao wote, na mitungi mitupu, na mienge ikawekwa ndani yake. \p \v 17 Akawaambia, “Nitazameni, fanyeni kama nitakavyofanya. Nitakapofika mwisho wa kambi, mfanye kama nitakavyofanya. \v 18 Mimi na wote walio pamoja nami tutakapopiga tarumbeta zetu, ninyi nanyi pigeni tarumbeta pande zote za kambi na mpige kelele, mseme, ‘Upanga wa Mwenyezi Mungu na wa Gideoni.’ ” \p \v 19 Gideoni na wale watu mia moja waliokuwa pamoja naye wakafika mwisho wa kambi usiku mwanzoni mwa zamu ya kati, mara tu walipokuwa wamebadili zamu. Wakapiga zile tarumbeta zao, na kuvunja ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao. \v 20 Yale makundi matatu wakapiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Wakashika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga. Wakapaza sauti zao, wakisema, “Upanga wa Mwenyezi Mungu, na wa Gideoni!” \v 21 Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote, Wamidiani wote wakakimbia, huku wakipiga kelele. \p \v 22 Walipozipiga zile tarumbeta mia tatu, Mwenyezi Mungu akafanya watu katika kambi yote kugeukiana kila mmoja na mwenziwe kwa upanga. Jeshi likakimbia hadi Beth-Shita kuelekea Serera\f + \fr 7:22 \fr*\ft au \ft*\fqa Seretha\fqa*\f*, hadi mpakani mwa Abel-Mehola karibu na Tabathi. \v 23 Wanaume Waisraeli wakaitwa kutoka Naftali, Asheri na Manase yote, nao wakawafuatia Wamidiani. \v 24 Gideoni akatuma wajumbe katika nchi yote ya vilima ya Efraimu, akisema, “Teremkeni dhidi ya Wamidiani na mkazuie vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani.” \p Hivyo wanaume wote wa Efraimu wakakutanika pamoja na kuzingira vivuko vya maji mbele yao hadi Beth-Bara na pia Yordani. \v 25 Wakawakamata Orebu na Zeebu, wakuu wawili wa Midiani. Wakamuua Orebu pale penye mwamba wa Orebu, na Zeebu wakamuua pale penye shinikizo la kukamulia zabibu la Zeebu. Wakawafuatia Wamidiani na kuleta vichwa vya Orebu na Zeebu kwa Gideoni, huko ng’ambo ya Yordani. \c 8 \s1 Ushindi wa Gideoni na kulipiza kisasi \p \v 1 Basi Waefraimu wakamuuliza Gideoni, “Mbona umetutenda hivi? Kwa nini hukutuita ulipoenda kupigana na Wamidiani?” Wakamlaumu kwa ukali sana. \p \v 2 Gideoni akawajibu, “Nilichofanya mimi ni nini kulinganisha na kile ninyi mlichofanya? Je, kuokoa masazo ya zabibu za Efraimu si bora kuliko mavuno kamili ya zabibu ya Abiezeri? \v 3 Mungu amewatia Orebu na Zeebu, hao viongozi wa Wamidiani, mikononi mwenu. Je, mimi niliweza kufanya nini kulinganisha na mlichofanya ninyi?” Aliposema hili, hasira yao dhidi yake ikatulia. \p \v 4 Gideoni pamoja na watu wake mia tatu, wakiwa wamechoka sana lakini bado wakiwafuatia, wakafika Yordani na kuuvuka. \v 5 Akawaambia wanaume wa Sukothi, “Tafadhali lipatieni jeshi langu mikate, kwa maana wamechoka, nami ningali ninawafuatia Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani.” \p \v 6 Lakini viongozi wa Sukothi wakasema, “Je, tayari umewakamata Zeba na Salmuna ili tulipatie jeshi lako mikate?” \p \v 7 Gideoni akajibu, “Kwa ajili ya hilo tu, Mwenyezi Mungu atakapowatia Zeba na Salmuna mkononi mwangu, nitaichana nyama ya miili yenu kwenye miiba ya nyikani na kwenye michongoma.” \p \v 8 Kutoka hapo alikwea hadi Penieli na kutoa ombi lile lile, lakini nao wanaume wa Penieli wakamjibu kama wanaume wa Sukothi walivyokuwa wamemjibu. \v 9 Hivyo akawaambia wanaume wa Penieli, “Nitakaporudi kwa ushindi, nitaubomoa mnara huu.” \p \v 10 Wakati huu Zeba na Salmuna walikuwa Karkori, wakiwa na jeshi la watu wapatao elfu kumi na tano waliokuwa wamesalia wa mataifa ya mashariki, kwa kuwa watu wapatao elfu mia moja na ishirini wenye panga walikuwa wameuawa. \v 11 Basi Gideoni akakwea kwa njia ya wafugaji wahamaji mashariki mwa Noba na Yogbeha, na kulishambulia jeshi ambalo halikushuku lolote. \v 12 Zeba na Salmuna, hao wafalme wawili wa Midiani, wakakimbia lakini yeye Gideoni akawafuata na kuwakamata, akalishinda hilo jeshi lao lote kabisa. \p \v 13 Gideoni mwana wa Yoashi akarudi kutoka vitani kupitia Mwinuko wa Heresi. \v 14 Akamkamata kijana mmoja wa Sukothi na kumuuliza maswali, naye yule kijana akamwandikia majina ya viongozi sabini na saba wa Sukothi, ambao ni wazee wa mji. \v 15 Ndipo Gideoni akaja na kuwaambia wanaume wa Sukothi, “Tazameni Zeba na Salmuna mlionisimanga kwa ajili yao mkisema, ‘Je, tayari umewakamata Zeba na Salmuna ili tulipatie jeshi lako mikate?’ ” \v 16 Akawachukua hao wazee wa mji, na kuwaadhibu wanaume wa Sukothi kwa kuwachapa kwa miiba na michongoma ya nyikani. \v 17 Pia akaubomoa mnara wa Penieli na kuwaua wanaume wa huo mji. \p \v 18 Kisha akawauliza Zeba na Salmuna, “Ni wanaume wa aina gani mliowaua huko Tabori?” \p Wakajibu, “Ni wanaume kama wewe, kila mmoja wao akiwa anafanana na mwana wa mfalme.” \p \v 19 Gideoni akajibu, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu hasa. Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, kama mngekuwa mmewaacha hai, mimi nisingewaua ninyi.” \v 20 Akamgeukia Yetheri, mwanawe mzaliwa wa kwanza, akasema, “Waue hawa!” Lakini Yetheri hakuufuta upanga wake, kwa sababu aliogopa, kwa kuwa alikuwa bado kijana mdogo tu. \p \v 21 Zeba na Salmuna wakasema, “Njoo ufanye hivyo wewe mwenyewe. ‘Alivyo mwanaume, ndivyo zilivyo nguvu zake.’ ” Hivyo, Gideoni akajitokeza na kuwaua, naye akayaondoa mapambo kwenye shingo za ngamia wao. \s1 Kizibau cha Gideoni \p \v 22 Waisraeli wakamwambia Gideoni, “Ututawale, wewe, mwanao, na mjukuu wako, kwa kuwa umetuokoa kutoka mikononi mwa Wamidiani.” \p \v 23 Lakini Gideoni akawaambia, “Mimi sitawatawala ninyi, wala mwanangu hatawatawala. Mwenyezi Mungu ndiye atakayewatawala ninyi.” \v 24 Naye akasema, “Ninalo ombi moja, kwamba kila mmoja wenu anipatie kipuli kutoka fungu lake la nyara.” (Ilikuwa desturi ya Waishmaeli kuvaa vipuli vya dhahabu.) \p \v 25 Wakajibu, “Tutafurahi kuvitoa.” Hivyo wakatanda vazi chini na kila mwanaume akatupia juu yake pete kutoka fungu lake la nyara. \v 26 Uzito wa pete za dhahabu alizoomba ulikuwa shekeli elfu moja na mia saba\f + \fr 8:26 \fr*\ft Shekeli 1,700 ni sawa na kilo 19.5.\ft*\f*, bila kuhesabu mapambo mengine, vidani, na mavazi ya zambarau yaliyovaliwa na wafalme wa Midiani, au mikufu iliyokuwa kwenye shingo za ngamia wao. \v 27 Gideoni akatengeneza kizibau kwa kutumia ile dhahabu, ambacho alikiweka katika mji wake, yaani Ofra. Waisraeli wote wakafanya uasherati kwa kukiabudu huko, nacho kikawa mtego kwa Gideoni na jamaa yake. \p \v 28 Hivyo Midiani wakashindwa mbele ya Waisraeli, nao hawakuinua vichwa vyao tena. Wakati wa siku za uhai wa Gideoni, nchi ikafurahia amani miaka arobaini. \s1 Kifo cha Gideoni \p \v 29 Yerub-Baali mwana wa Yoashi akarudi kwenda kuishi katika nyumba yake. \v 30 Alikuwa na wana sabini wa kwake mwenyewe, kwa kuwa alikuwa na wake wengi. \v 31 Suria wake, aliyekuwa anaishi huko Shekemu, pia alimzalia mwana, akamwita jina Abimeleki. \v 32 Gideoni mwana wa Yoashi akafa akiwa na umri mzuri wa uzee, akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake huko Ofra ya Waabiezeri. \p \v 33 Mara tu alipofariki Gideoni, Waisraeli wakarudia hali ya uovu na kufanya uasherati kwa kuabudu Mabaali. Wakamsimamisha Baal-Berithi kuwa mungu wao na \v 34 wala hawakumkumbuka Mwenyezi Mungu, Mungu wao, aliyewaokoa kutoka mikononi mwa adui zao wote kutoka kila upande. \v 35 Pia wakashindwa kuitendea mema jamaa ya Yerub-Baali (yaani Gideoni) kwa ajili ya mambo yote mema aliyokuwa amefanyia Israeli. \c 9 \s1 Abimeleki ajaribu kuanzisha ufalme \p \v 1 Siku moja Abimeleki mwana wa Yerub-Baali akaenda kwa ndugu za mama yake huko Shekemu, akawaambia wao na ukoo wote wa mama yake, \v 2 “Waulizeni watu wote wa Shekemu, ‘Lipi lililo bora kwenu: Kutawaliwa na wana wote sabini wa Yerub-Baali, au mtu mmoja peke yake?’ Kumbukeni kwamba mimi ni mwili wenu na damu yenu.” \p \v 3 Ndugu za mama yake walipowaeleza watu wote wa Shekemu, wakaelekea kumkubali Abimeleki, kwa kuwa walisema, “Yeye ni ndugu yetu.” \v 4 Wakampa shekeli sabini\f + \fr 9:4 \fr*\ft Shekeli 70 za fedha ni sawa na gramu 800.\ft*\f* za fedha kutoka hekalu la Baal-Berithi, naye Abimeleki akazitumia kuajiri watu ovyo na wasiojali, wakawa ndio wafuasi wake. \v 5 Akaenda nyumbani mwa baba yake huko Ofra, na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, ambao ni wana wa Yerub-Baali. Lakini Yothamu, mwana mdogo kwa wote wa Yerub-Baali, akaokoka kwa kujificha. \v 6 Ndipo wenyeji wa Shekemu na Beth-Milo wakakusanyika pamoja chini ya mwaloni mkubwa, penye nguzo iliyo Shekemu, wakamtawaza Abimeleki kuwa mfalme. \p \v 7 Yothamu alipoambiwa hayo, akapanda juu ya kilele cha mlima Gerizimu, akapaza sauti, akawaambia, “Nisikilizeni enyi wenyeji wa Shekemu, ili Mungu naye apate kuwasikiliza. \v 8 Siku moja miti ilitoka ili kwenda kujitawazia mfalme. Ikauambia mzeituni, ‘Wewe uwe mfalme wetu.’ \p \v 9 “Lakini mzeituni ukaijibu, ‘Je, niache kutoa mafuta yangu ambayo kwake miungu na wanadamu huheshimiwa, ili nikatawale miti?’ \p \v 10 “Kisha miti ikauambia mtini, ‘Njoo na uwe mfalme wetu!’ \p \v 11 “Lakini mtini ukaijibu, ‘Je, niache kutoa matunda yangu mazuri na matamu, ili nikatawale miti?’ \p \v 12 “Ndipo miti ikauambia mzabibu, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’ \p \v 13 “Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikatawale miti?’ \p \v 14 “Mwishoni miti yote ikauambia mchongoma, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’ \p \v 15 “Nao mchongoma ukaijibu, ‘Kama kweli mnataka kunitawaza niwe mfalme wenu, basi njooni mpate kupumzika chini ya kivuli changu. Lakini kama sivyo, moto na utoke kwenye mchongoma ukateketeze mierezi ya Lebanoni!’ \p \v 16 “Basi, je, mmetenda kwa uaminifu na heshima kwa kumtawaza Abimeleki kuwa mfalme? Je, mmetendea mema Yerub-Baali na jamaa yake, na mkamtendea kama alivyostahili? \v 17 Baba yangu aliwapigania na kuhatarisha nafsi yake ili kuwaokoa kutoka mikononi mwa Wamidiani, \v 18 lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja. Nanyi mmemtawaza Abimeleki mwana wa mjakazi wake kuwa mfalme juu ya wenyeji wa Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu. \v 19 Ikiwa kweli mmemtendea Yerub-Baali na jamaa yake kwa heshima na uaminifu, basi Abimeleki na awe furaha yenu, nanyi mwe furaha yake pia! \v 20 Lakini kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na uwateketeze, ninyi wenyeji wa Shekemu na Beth-Milo; nao moto utoke kwenu, wenyeji wa Shekemu na Beth-Milo, na umteketeze Abimeleki!” \p \v 21 Ndipo Yothamu akakimbia, akatoroka akaenda Beeri, akaishi huko, kwa sababu alimwogopa ndugu yake Abimeleki. \p \v 22 Baada ya Abimeleki kutawala Israeli kwa muda wa miaka mitatu, \v 23 Mungu akaruhusu roho mbaya kati ya Abimeleki na wenyeji wa Shekemu, nao wenyeji wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa hila. \v 24 Hili lilitendeka ili ule ukatili waliotendewa hao wana sabini wa Yerub-Baali upatilizwe, na damu yao iwe juu ya Abimeleki ndugu yao aliyewaua, na pia iwe juu ya wenyeji wa Shekemu, ambao walimsaidia kuua ndugu zake. \v 25 Hivyo, kutokana na uadui juu yake, wenyeji wa Shekemu wakaweka watu wa kumvizia katika vilele vya milima. Wakawanyang’anya watu wote waliopita karibu nao, nayo haya yakaarifiwa kwa Abimeleki. \p \v 26 Basi Gaali mwana wa Ebedi akaenda pamoja na ndugu zake wakaingia Shekemu, nao wenyeji wa huko wakawa na imani naye. \v 27 Wakaenda mashambani mwao kuvuna zabibu na kuzisindika hizo zabibu, baadaye wakafanya sherehe katika hekalu la mungu wao. Walipokuwa wakila na kunywa, wakamlaani Abimeleki. \v 28 Gaali mwana wa Ebedi akasema, “Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, yeye si mwana wa Yerub-Baali? Naye Zebuli si ndiye msaidizi wake? Basi watumikieni watu wa Hamori, babaye Shekemu. Kwa nini tumtumikie Abimeleki? \v 29 Laiti watu hawa wangekuwa chini ya amri yangu! Basi mimi ningemwondoa huyo Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, ‘Ondoa jeshi lako lote.’ ” \p \v 30 Zebuli aliyekuwa mtawala wa mji aliposikia aliyosema Gaali mwana wa Ebedi, akakasirika sana. \v 31 Akatuma wajumbe waende kwa Abimeleki kwa siri, na kusema, “Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wamekuja Shekemu, na wanauchochea mji huu kinyume chako. \v 32 Sasa basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani. \v 33 Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Gaali na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.” \p \v 34 Kwa hiyo Abimeleki pamoja na jeshi lake lote wakaondoka usiku na kujificha karibu na Shekemu wakiwa vikosi vinne. \v 35 Basi Gaali mwana wa Ebedi alikuwa ametoka nje akawa amesimama katika ingilio la mji wakati ule ule ambao Abimeleki na watu wake walipokuwa wanatoka sehemu zao za maficho. \p \v 36 Gaali alipowaona, akamwambia Zebuli, “Tazama, watu wanashuka kutoka vilele vya milima!” \p Zebuli akajibu, “Wewe unaona vivuli vya milima kana kwamba ni watu.” \p \v 37 Lakini Gaali akasema tena, “Tazama, watu wanashuka kutoka katikati ya nchi na kikosi kimoja kinakuja kutoka Tabur-Ezeri na kikosi kingine kutoka upande wa mwaloni wa Meonenimu.” \p \v 38 Ndipo Zebuli akamwambia, “Kuko wapi kujivuna kwako sasa, wewe uliyesema, ‘Huyo Abimeleki ni nani hata tumtumikie?’ Hawa si wale watu uliowadharau? Toka nje sasa ukapigane nao!” \p \v 39 Basi Gaali akawaongoza wenyeji wa Shekemu kupigana na Abimeleki. \v 40 Abimeleki akamfukuza, naye akatoroka. Nao watu wengi wakaanguka njia yote hadi kwenye ingilio la lango, wakiwa wamejeruhiwa katika kule kutoroka. \v 41 Abimeleki akaishi Aruma, naye Zebuli akawafukuza Gaali na ndugu zake watoke Shekemu. \p \v 42 Kesho yake watu wa Shekemu wakatoka wakaenda mashambani, Abimeleki akaambiwa jambo hilo. \v 43 Hivyo akawachukua watu wake, akawagawanya katika vikosi vitatu na kuwaweka waviziaji huko mashambani. Alipowaona watu wanatoka kwenda nje ya mji, akainuka dhidi yao na kuwashambulia. \v 44 Abimeleki pamoja na vikosi vyake wakaharakisha kwenda mbele kwenye nafasi iliyokuwa katika ingilio la lango la mji. Vikosi viwili vikawashambulia wale waliokuwa mashambani, na kuwaua. \v 45 Siku hiyo nzima Abimeleki akazidisha mashambulizi yake dhidi ya mji hadi akawa ameuteka na kuwaua watu wa mji huo. Kisha akauangamiza mji na kusambaza chumvi juu yake. \p \v 46 Kwa kusikia jambo hilo, watu wote katika mnara wa Shekemu wakaingia kwenye ngome ya hekalu la El-Berithi. \v 47 Abimeleki aliposikia kuwa wamekusanyika huko, \v 48 yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Abimeleki akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua begani mwake. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Haraka! Fanyeni kile mmeona nikifanya!” \v 49 Basi watu wote wakakata matawi na kumfuata Abimeleki. Wakayakusanya hayo matawi juu ya ngome, na kuitia moto ili kuwachoma watu wote waliokuwa ndani. Hivyo watu wote katika mnara wa Shekemu, yamkini wanaume na wanawake elfu moja, pia wakafa. \p \v 50 Baadaye Abimeleki akaenda Thebesi na kuuzingira kwa jeshi na kuuteka. \v 51 Hata hivyo, ndani ya huo mji kulikuwa na mnara imara, ambako watu wote wa mji, wanaume na wanawake, walikimbilia ndani yake. Wakajifungia ndani, na kupanda juu ya paa la mnara. \v 52 Abimeleki akaja kwenye ule mnara na kuushambulia. Lakini alipokaribia kwenye ingilio la mnara ili kuuchoma kwa moto, \v 53 mwanamke mmoja akaangusha sehemu ya juu ya jiwe la kusagia kwa kichwa cha Abimeleki, likapasua fuvu la kichwa chake. \p \v 54 Akamwita kwa haraka kijana yule aliyechukua silaha zake, na kumwambia, “Chukua upanga wako na uniue, watu wasije wakasema, ‘Mwanamke amemuua.’ ” Basi yule kijana akamchoma upanga, naye akafa. \v 55 Waisraeli walipoona kuwa Abimeleki amekufa, kila mtu akaenda nyumbani mwake. \p \v 56 Hivyo ndivyo Mungu alivyolipiza uovu ule ambao Abimeleki alikuwa ameutenda kwa baba yake kwa kuwaua ndugu zake sabini. \v 57 Mungu akawapatiliza wanaume wa Shekemu uovu wao juu ya vichwa vyao, na juu yao ikaja laana ya Yothamu mwana wa Yerub-Baali. \c 10 \s1 Tola \p \v 1 Baada ya Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyeishi huko Shamiri, katika nchi ya vilima ya Efraimu, akainuka kuokoa Israeli. \v 2 Akawa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini na tatu. Ndipo akafa, naye akazikwa huko Shamiri. \s1 Yairi \p \v 3 Baada yake akafuatiwa na Yairi, Mgileadi, aliyekuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini na mbili. \v 4 Alikuwa na wana thelathini waliopanda punda thelathini. Nao walikuwa na miji thelathini huko Gileadi, inayoitwa Hawoth-Yairi hadi leo. \v 5 Yairi akafa, naye akazikwa huko Kamoni. \s1 Yefta \p \v 6 Tena Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, na miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni, na miungu ya Wafilisti. Na kwa kuwa Waisraeli walimwacha Mwenyezi Mungu wala hawakuendelea kumtumikia, \v 7 hivyo hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Waisraeli. Naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni, \v 8 ambao waliowaonea na kuwatesa mwaka huo. Kwa miaka kumi na nane wakawatesa Waisraeli wote upande wa mashariki mwa Mto Yordani huko Gileadi, katika nchi ya Waamori. \v 9 Waamoni nao wakavuka Yordani ili kupigana na Yuda, Benyamini na nyumba ya Efraimu, nayo nyumba ya Israeli ikawa katika taabu kubwa. \v 10 Ndipo Waisraeli wakamlilia Mwenyezi Mungu wakasema, “Tumetenda dhambi dhidi yako, kumwacha Mungu wetu na kutumikia Mabaali.” \p \v 11 Mwenyezi Mungu akawaambia, “Wamisri, Waamori, Waamoni, Wafilisti, \v 12 Wasidoni, Waamaleki na Wamaoni walipowadhulumu ninyi, nanyi mkanililia na kuomba msaada, je, sikuwaokoa mikononi mwao? \v 13 Lakini ninyi mmeniacha na kuitumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena. \v 14 Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!” \p \v 15 Lakini Waisraeli wakamwambia Mwenyezi Mungu, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.” \v 16 Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni kati yao nao wakamtumikia Mwenyezi Mungu. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli. \p \v 17 Waamoni walipoitwa vitani na kupiga kambi kule Gileadi, Waisraeli walikusanyika na kupiga kambi huko Mispa. \v 18 Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana wao kwa wao, “Yeyote atakayeanzisha mashambulizi dhidi ya Waamoni atakuwa kiongozi wa wote wanaoishi Gileadi.” \c 11 \p \v 1 Basi Yefta Mgileadi alikuwa shujaa mwenye nguvu. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba. \v 2 Mke wa Gileadi pia akamzalia wana, nao walipokua, wakamfukuza Yefta, na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” \v 3 Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata. \p \v 4 Baada ya muda Waamoni wakafanya vita na Israeli, \v 5 viongozi wa Gileadi wakaenda kumchukua Yefta katika nchi ya Tobu. \v 6 Wakamwambia Yefta, “Njoo, uwe jemadari wetu, ili tuweze kupigana na Waamoni.” \p \v 7 Yefta akawaambia viongozi wa Gileadi, “Je, si mlinichukia na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mwanijia sasa, wakati mko taabuni?” \p \v 8 Viongozi wa Gileadi wakamwambia Yefta, “Lakini sasa tumegeuka kukuelekea wewe, ili uende pamoja nasi kupigana na Waamoni, nawe utakuwa kiongozi wetu juu ya watu wote wa Gileadi.” \p \v 9 Yefta akawaambia viongozi wa Gileadi, “Ikiwa mtanirudisha kwetu kupigana na Waamoni, naye Mwenyezi Mungu akanisaidia kuwashinda, je, ni kweli nitakuwa kiongozi wenu?” \p \v 10 Viongozi wa Gileadi wakamjibu Yefta, “Mwenyezi Mungu ndiye shahidi wetu. Kwa hakika tutafanya kama usemavyo.” \v 11 Basi Yefta akaenda na viongozi wa Gileadi, nao watu wakamfanya kiongozi na jemadari wao. Naye akarudia maneno yake yote mbele za Mwenyezi Mungu huko Mispa. \p \v 12 Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini nasi, hata umekuja kushambulia nchi yetu?” \p \v 13 Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Mto Arnoni hadi Mto Yaboki, hadi kufikia Mto Yordani. Sasa irudishe kwa amani.” \p \v 14 Yefta akarudisha wajumbe kwa mfalme wa Waamoni, \v 15 kusema: \pm “Hili ndilo asemalo Yefta: Waisraeli hawakuchukua nchi ya Moabu wala nchi ya Waamoni. \v 16 Lakini walipopanda kutoka Misri, Waisraeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu na wakafika Kadeshi. \v 17 Ndipo Waisraeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako.’ Lakini mfalme wa Edomu hakutusikia. Wakatuma wajumbe pia kwa mfalme wa Moabu, naye akakataa. Kwa hiyo Waisraeli wakakaa huko Kadeshi. \pm \v 18 “Baadaye wakasafiri kupitia jangwa, wakiambaa na nchi za Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, na kupiga kambi upande ule mwingine wa Mto Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Mto Arnoni ulikuwa mpaka wake. \pm \v 19 “Kisha Waisraeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, na kumwambia, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako ili kufikia mahali petu.’ \v 20 Hata hivyo, Sihoni hakuwaamini Waisraeli kupita katika nchi yake. Akaandaa jeshi lake lote na kupiga kambi huko Yahasa, nao wakapigana na Waisraeli. \pm \v 21 “Ndipo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Waisraeli, nao wakawashinda. Waisraeli wakaimiliki nchi yote ya Waamori walioishi nchi hiyo, \v 22 wakiiteka nchi yote kuanzia Mto Arnoni hadi Mto Yaboki, na kutoka jangwani hadi Mto Yordani. \pm \v 23 “Basi kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, amewafukuza Waamori watoke mbele ya watu wake Israeli, wewe unayo haki gani ya kuitamalaki? \v 24 Je, haikupasi kuchukua kile ambacho mungu wako Kemoshi amekupa? Vivyo hivyo, chochote kile Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, alichotupatia sisi, tutakimiliki. \v 25 Je, wewe ni bora kuliko Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu? Je, yeye alishagombana na Waisraeli au kupigana nao wakati wowote? \v 26 Kwa maana kwa miaka mia tatu, Waisraeli wameishi Heshboni na makazi yake, Aroeri na makazi yake, na katika miji yote iliyo kando ya Mto Arnoni. Kwa nini wewe hukuyachukua wakati huo? \v 27 Mimi sijakukosea, bali wewe ndiwe unanikosea kwa kufanya vita nami. Basi Mwenyezi Mungu, aliye Mwamuzi, leo na aamue ugomvi kati ya Waisraeli na Waamoni.” \m \v 28 Hata hivyo, mfalme wa Waamoni hakuyajali maneno ya ujumbe wa Yefta. \p \v 29 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Yefta. Akapita katikati ya Gileadi na Manase, pia akapita katika Mispa ya Gileadi, na kutokea huko akasonga mbele kushambulia Waamoni. \v 30 Naye Yefta akaweka nadhiri mbele za Mwenyezi Mungu akisema, “Ikiwa utawatia Waamoni mikononi mwangu, \v 31 chochote kile kitakachotoka katika mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda Waamoni, kitakuwa ni cha Mwenyezi Mungu na nitakitoa kuwa sadaka ya kuteketezwa.” \p \v 32 Ndipo Yefta akavuka kupigana na hao Waamoni, naye Mwenyezi Mungu akawatia mkononi mwake. \v 33 Akaharibu kabisa miji ishirini kuanzia Aroeri hadi karibu na Minithi, na kuendelea hadi Abel-Keramimu. Hivyo, Waisraeli wakawashinda Waamoni. \p \v 34 Yefta aliporudi nyumbani mwake huko Mispa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa mwanawe wa pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine. \v 35 Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyong’onyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, ambayo siwezi kuivunja.” \p \v 36 Akajibu, “Baba yangu, umetoa neno lako kwa Mwenyezi Mungu. Nitendee mimi kama vile ulivyoahidi, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekupa ushindi dhidi ya adui zako Waamoni.” \v 37 Naye akamwambia baba yake, “Naomba nifanyiwe jambo hili. Nipewe miezi miwili ili kuzunguka vilimani nikaulilie ubikira wangu, mimi na wenzangu.” \p \v 38 Baba yake akamwambia, “Unaweza kwenda.” Naye akamwacha aende kwa miezi miwili. Hivyo akaondoka pamoja na wenzake, naye akaulilia ubikira wake huko vilimani kwa sababu hangeolewa kamwe. \v 39 Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba yake, naye baba yake akamtendea kama alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa bikira. \p Nayo ikawa desturi katika Israeli, \v 40 kwamba kila mwaka binti za Israeli huenda kwa siku nne ili kumkumbuka huyo binti Yefta Mgileadi. \c 12 \s1 Yefta na Efraimu \p \v 1 Watu wa Efraimu wakaita majeshi yao, wakavuka kwenda Zafoni. Wakamwambia Yefta, “Kwa nini mmeenda kupigana na Waamoni bila kutuita ili twende pamoja nawe? Basi tutaichoma moto nyumba yako, pamoja nawe ukiwa ndani yake.” \p \v 2 Yefta akajibu, “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa na Waamoni. Ingawa niliwaita, hamkuniokoa kutoka mkono wao. \v 3 Nilipoona kuwa hamniokoi, nikauhatarisha uhai wangu, nikavuka kupigana na Waamoni. Naye Mwenyezi Mungu akanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?” \p \v 4 Ndipo Yefta akakusanya wanaume wa Gileadi pamoja na kupigana na Efraimu. Wagileadi wakawashinda Waefraimu, kwa kuwa Waefraimu walisema, “Ninyi Wagileadi ni waasi mliotoroka toka Efraimu na Manase.” \v 5 Wagileadi wakaviteka vivuko vya Mto Yordani kuelekea Efraimu. Kisha ilikuwa yeyote aliyenusurika kutoka Efraimu aliposema, “Niache nivuke,” hao wanaume wa Gileadi walimuuliza, “Je wewe ni Mwefraimu?” Akijibu “Hapana,” \v 6 walimwambia, “Sawa, sema ‘Shibolethi’.” Iwapo alitamka, “Sibolethi”, kwa sababu hakuweza kutamka hilo neno sawasawa, walimkamata na kumuua hapo kwenye vivuko vya Mto Yordani. Waefraimu elfu arobaini na mbili waliuawa wakati huo. \p \v 7 Yefta akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa muda wa miaka sita. Kisha Yefta akafa, akazikwa katika mmoja wa miji ya Gileadi. \s1 Ibzani, Eloni na Abdoni \p \v 8 Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. \v 9 Alikuwa na wana thelathini na binti thelathini. Akawaoza binti zake kwa watu wengine nje ya ukoo wake, na kuwatwalia wanawe wanawake thelathini toka nje ya ukoo wake. Ibzani akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka saba. \v 10 Kisha Ibzani akafa, akazikwa huko Bethlehemu. \p \v 11 Baada yake, Eloni Mzabuloni akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka kumi. \v 12 Kisha Eloni akafa, akazikwa huko Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni. \p \v 13 Baada yake, Abdoni mwana wa Hileli Mpirathoni akawa mwamuzi wa Israeli. \v 14 Naye alikuwa na wana arobaini, na wajukuu thelathini waliopanda punda sabini. Akawa mwamuzi wa Israeli kwa muda wa miaka nane. \v 15 Kisha Abdoni mwana wa Hileli Mpirathoni akafa, akazikwa Pirathoni huko Efraimu, katika nchi ya vilima ya Waamaleki. \c 13 \s1 Kuzaliwa kwa Samsoni \p \v 1 Waisraeli wakafanya maovu tena mbele za Mwenyezi Mungu. Hivyo Mwenyezi Mungu akawatia mikononi mwa Wafilisti kwa muda wa miaka arobaini. \p \v 2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, aliyeitwa Manoa, wa ukoo wa Wadani, naye alikuwa na mke aliyekuwa tasa, asiyeweza kuzaa watoto. \v 3 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na huna mtoto, lakini utachukua mimba na utamzaa mtoto wa kiume. \v 4 Lakini ujihadhari sana usinywe divai wala kileo kingine chochote, wala usile kitu chochote kilicho najisi, \v 5 kwa kuwa utachukua mimba na utamzaa mtoto wa kiume. Wembe usipite kwenye kichwa chake, kwa kuwa huyo mwana atakuwa Mnadhiri aliyetengwa kwa Mungu tangu tumboni mwa mama yake. Naye atawaongoza na kuwaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti.” \p \v 6 Ndipo huyo mwanamke akamwendea mumewe na kumwambia, “Mtu wa Mungu alinijia. Alionekana kama malaika wa Mungu, wa kutisha sana. Sikumuuliza alikotoka wala hakuniambia jina lake. \v 7 Lakini aliniambia, ‘Utachukua mimba na utazaa mtoto wa kiume. Basi sasa, usinywe divai wala kileo kingine chochote, wala usile kitu kilicho najisi, kwa kuwa huyo mtoto atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake hadi kufa kwake.’ ” \p \v 8 Ndipo Manoa akamwomba Mwenyezi Mungu, akasema: “Ee Bwana, nakusihi huyo mtu wa Mungu uliyemtuma kwetu aje tena, ili atufundishe jinsi ya kumlea huyo mwana atakayezaliwa.” \p \v 9 Mungu akamsikia Manoa, naye malaika wa Mungu akamjia tena huyo mwanamke alipokuwa shambani; lakini mumewe Manoa hakuwa naye. \v 10 Basi yule mwanamke akaenda haraka na kumwambia mumewe, “Tazama mtu yule aliyenitokea siku ile yupo hapa!” \p \v 11 Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamuuliza, “Je, wewe ndiwe ulisema na mke wangu?” \p Akasema, “Ni mimi.” \p \v 12 Basi Manoa akamuuliza, “Maneno yako yatakapotimia, je, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa ni yapi, na kazi yake itakuwa ni ipi?” \p \v 13 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamjibu, “Mke wako hana budi kufanya yale yote niliyomwambia. \v 14 Kamwe asile kitu chochote kitakachotoka katika mzabibu, wala asinywe divai yoyote wala kileo chochote, wala asile kitu chochote kilicho najisi. Hana budi kufanya kila kitu nilichomwagiza.” \p \v 15 Manoa akamjibu yule malaika wa Mwenyezi Mungu, “Twakuomba usubiri kwanza ili tuweze kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako.” \p \v 16 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula chochote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi Mungu.” \p (Manoa hakumtambua kuwa huyu alikuwa malaika wa Mwenyezi Mungu.) \p \v 17 Kisha Manoa akamuuliza yule malaika wa Mwenyezi Mungu, “Jina lako ni nani, ili tuweze kukupa heshima wakati maneno uliyonena yatakapotimia?” \p \v 18 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamjibu, “Kwa nini unauliza jina langu? Ni jina la ajabu.” \v 19 Ndipo Manoa akamchukua mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, naye akamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu hapo juu ya mwamba. Naye yule malaika wa Mwenyezi Mungu akafanya jambo la ajabu wakati Manoa na mkewe wakiwa wanaangalia: \v 20 Mwali wa moto kutoka hapo madhabahuni ulipowaka kuelekea mbinguni, malaika wa Mwenyezi Mungu akapaa ndani ya huo mwali. Manoa na mkewe, kwa kuona jambo hili, wakaanguka kifudifudi. \v 21 Malaika wa Mwenyezi Mungu hakumtokea tena Manoa na mkewe. Ndipo Manoa akatambua kuwa huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi Mungu. \p \v 22 Manoa akamwambia mkewe, “Hakika tutakufa, kwa kuwa tumemwona Mungu.” \p \v 23 Lakini mkewe akamwambia, “Ikiwa Mwenyezi Mungu alikuwa amekusudia kutuua, hangepokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo haya yote wala kututangazia mambo haya wakati huu.” \p \v 24 Yule mwanamke akazaa mtoto wa kiume, akamwita jina Samsoni. Kijana akakua, naye Mwenyezi Mungu akambariki. \v 25 Roho wa Mwenyezi Mungu akaanza kumpa msukumo alipokuwa huko Mahane-Dani, kati ya Sora na Eshtaoli. \c 14 \s1 Ndoa ya Samsoni \p \v 1 Samsoni akateremka Timna, na huko akamwona mwanamke Mfilisti. \v 2 Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke Mfilisti huko Timna; basi mnitwalie awe mke wangu.” \p \v 3 Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa watu wetu wote, hata ulazimike kwenda kujitwalia mke kutoka kwa hao Wafilisti wasiotahiriwa?” \p Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Nipatieni huyo kwa maana ndiye alinipendeza.” \v 4 (Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.) \v 5 Samsoni akateremka Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia. \v 6 Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Samsoni kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono mitupu kama ambavyo angempasua mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake alichokifanya. \v 7 Basi akateremka na kuongea na yule mwanamke, naye akampendeza Samsoni. \p \v 8 Baada ya muda, Samsoni aliporudi ili akamwoe, akageuka kando ili kuutazama mzoga wa yule simba. Tazama! Ndani ya ule mzoga akaona kundi la nyuki na asali kiasi. \v 9 Akachukua asali mkononi mwake, akala huku akitembea. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa kiasi cha ile asali, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa aliitwaa asali katika mzoga wa simba. \p \v 10 Basi baba yake akateremka kumwona huyo mwanamke. Samsoni akafanya karamu huko, kama ilivyokuwa desturi ya vijana. \v 11 Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye. \p \v 12 Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini. \v 13 Lakini msipoweza kufumbua, ndipo ninyi mtanipa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.” \p Wakamwambia, “Tuambie hicho kitendawili, hebu na tukisikie.” \p \v 14 Akawaambia, \q1 “Ndani ya mlaji, \q2 kulitoka kitu cha kuliwa, \q1 ndani ya mwenye nguvu, \q2 kulitoka kitu kitamu.” \m Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu. \p \v 15 Siku ya nne, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atutegulie hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyang’anya kile tulicho nacho?” \p \v 16 Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.” \p Samsoni akamwambia, “Tazama, sijamweleza baba yangu wala mama yangu, kwa nini nikufumbulie?” \v 17 Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye mkewe akawaeleza watu wake kile kitendawili. \p \v 18 Siku ya saba, kabla ya jua kutua, wanaume wa mji wakamwambia Samsoni, \q1 “Ni nini kilicho kitamu kuliko asali? \q2 Ni nini chenye nguvu kuliko simba?” \p Samsoni akawaambia, \q1 “Kama hamkulima na mtamba wangu, \q2 msingekitegua kitendawili changu.” \p \v 19 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akamjia Samsoni kwa nguvu. Samsoni akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini wa mji huo, akatwaa mali yao, akawapa watu wale waliotegua kile kitendawili nguo zao. Akiwa amejaa hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake. \v 20 Naye mke wa Samsoni akakabidhiwa kwa rafiki yake Samsoni aliyekuwa msaidizi wake siku ya arusi. \c 15 \s1 Kisasi cha Samsoni kwa Wafilisti \p \v 1 Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia. \p \v 2 Baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimchukia, hivyo nikampeana kwa rafiki yako. Je, dada yake mdogo si mzuri kuliko yeye? Mchukue huyo badala yake.” \p \v 3 Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” \v 4 Hivyo Samsoni akaondoka na kuwakamata mbweha mia tatu, akawafunga wawili wawili, mikia kwa mikia. Kisha akafungia mwenge wa moto kwenye kila jozi la mikia hiyo. \v 5 Akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka, pamoja na mashamba ya mizabibu na mashamba ya mizeituni. \p \v 6 Wafilisti walipouliza, “Ni nani aliyetenda jambo hili?” Wakaambiwa, “Ni Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu mkewe alipeanwa kwa rafiki yake.” \p Hivyo Wafilisti wakapanda, wakamteketeza kwa moto yeye huyo mwanamke pamoja na baba yake. \v 7 Samsoni akawaambia, “Kwa kuwa mmetenda hivyo, hakika sitatulia hadi niwe nimelipiza kisasi juu yenu.” \v 8 Akawashambulia kwa ukali na kuwaua watu wengi sana. Kisha akateremka na kukaa kwenye pango katika mwamba wa Etamu. \p \v 9 Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi. \v 10 Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?” \p Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.” \p \v 11 Ndipo watu elfu tatu wa Yuda waliteremka hadi kwenye pango katika mwamba wa Etamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?” \p Akawajibu, “Nimewatendea tu kile walichonitendea.” \p \v 12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” \p Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.” \p \v 13 Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya na kumchukua toka huko kwenye pango katika mwamba. \v 14 Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. \v 15 Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao elfu moja. \p \v 16 Ndipo Samsoni akasema, \q1 “Kwa taya la punda \q2 malundo juu ya lundo, \q1 kwa taya la punda \q2 nimeua watu elfu moja.” \m \v 17 Alipomaliza kusema, akautupa ule mfupa wa taya; na mahali pale pakaitwa Ramath-Lehi\f + \fr 15:17 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kilima cha Taya\fqa*\f*. \p \v 18 Kwa kuwa alihisi kiu sana, akamlilia Mwenyezi Mungu, akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?” \v 19 Ndipo Mungu akafunua shimo huko Lehi, na maji yakatoka. Samsoni alipoyanywa maji hayo, nguvu zikamrudia, akahuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore\f + \fr 15:19 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Chemchemi ya Aliyeita\fqa*\f*, nayo iko hadi leo huko Lehi. \p \v 20 Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini. \c 16 \s1 Samsoni na Delila \p \v 1 Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. \v 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo, wakapazingira mahali pale, nao wakamvizia usiku kucha penye lango la mji. Wakakaa kimya usiku kucha, wakiwaza, “Kutakapopambazuka, tutamuua.” \p \v 3 Samsoni akalala tu hadi usiku wa manane. Akaamka, na kushika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na makomeo yake. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka hadi kilele cha mlima unaokabili Hebroni. \p \v 4 Baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika Bonde la Soreki aliyeitwa Delila. \v 5 Viongozi wa Wafilisti wakamwendea yule mwanamke na kumwambia, “Mshawishi ili upate kujua siri ya nguvu zake zilizo nyingi na jinsi tutakavyoweza kumshinda ili tuweze kumfunga na kumtiisha. Kila mmoja wetu atakupa shekeli elfu moja na mia moja\f + \fr 16:5 \fr*\ft Shekeli 1,100 ni sawa na kilo 13.\ft*\f* za fedha.” \p \v 6 Hivyo Delila akamwambia Samsoni, “Naomba uniambie siri ya hizi nguvu zako nyingi, na jinsi unavyoweza kufungwa ili kukutiisha.” \p \v 7 Samsoni akamjibu, “Kama nikifungwa kwa kamba saba za upinde ambazo hazijakauka, hapo ndipo nitakapokuwa dhaifu kama mtu mwingine yeyote.” \p \v 8 Basi viongozi wa Wafilisti wakamletea yule mwanamke kamba saba za upinde ambazo hazijakauka, naye akamfunga Samsoni. \v 9 Wakati watu wakiwa wanamvizia katika chumba cha ndani, yule mwanamke akamwambia, “Samsoni, Wafilisti wanakujia!” Lakini yeye akazikata zile kamba za upinde, kama vile uzi wa pamba unapoguswa na moto. Hivyo siri ya nguvu zake haikujulikana. \p \v 10 Ndipo Delila akamwambia Samsoni, “Umenifanyia mzaha na kuniambia uongo. Tafadhali niambie unaweza kufungwa kwa kitu gani?” \p \v 11 Akamwambia, “Kama nikifungwa kwa uthabiti kwa kamba mpya ambazo hazijatumika, basi nitakuwa dhaifu kama mtu mwingine yeyote.” \p \v 12 Hivyo, Delila akachukua kamba mpya na kumfunga nazo. Kisha akamwambia, “Samsoni, Wafilisti wanakujia!” Wale watu waliokuwa wanamvizia walikuwa katika chumba cha ndani. Lakini akazikata zile kamba zilizokuwa zimefunga mikono yake kama nyuzi. \p \v 13 Ndipo Delila akamwambia Samsoni, “Hata sasa umenifanyia mzaha na kuniambia uongo. Nieleze ni jinsi gani unavyoweza kufungwa.” \p Samsoni akamwambia, “Kama ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu kwa nguo iliyo katika mtande, na kuukaza kwa msumari, ndipo nitakuwa dhaifu kama mtu mwingine yeyote.” Hivyo, Samsoni alipokuwa amelala, Delila akachukua vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake na kuvifuma pamoja na nguo kwenye mtande, \v 14 na kuukaza kwa msumari. \p Kisha akamwambia, “Samsoni, Wafilisti wanakujia!” Samsoni akaamka kutoka usingizini na kung’oa msumari na mtande, pamoja na ile nguo. \p \v 15 Ndipo Delila akamwambia, “Wawezaje kusema, ‘Nakupenda,’ wakati moyo wako haupo pamoja nami? Umenifanyia mzaha mara hizi tatu na hujaniambia siri ya hizi nguvu zako nyingi.” \v 16 Hatimaye, baada ya kusumbuliwa kwa maneno kwa siku nyingi na kuudhiwa, roho yake ikataabika kiasi cha kufa. \p \v 17 Hivyo, akamwambia yule mwanamke siri yake yote, akisema, “Wembe haujapita kamwe kichwani mwangu, kwa kuwa mimi ni Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yangu. Kama nywele za kichwa changu zikinyolewa, nguvu zangu zitanitoka, na nitakuwa dhaifu kama mtu mwingine yeyote!” \p \v 18 Delila alipoona kuwa amemweleza siri yake yote, akatuma ujumbe kwa viongozi wa Wafilisti na kusema, “Njooni tena mara nyingine, maana amenieleza siri yake yote.” Basi viongozi wa Wafilisti wakarudi kwa Delila, wakiwa na fedha mikononi mwao. \v 19 Delila akamfanya alale usingizi magotini pake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake. Delila akaanza kumnyong’onyesha Samsoni, nazo nguvu zake zikamtoka. \p \v 20 Yule mwanamke akamwita, “Samsoni! Hao, Wafilisti wanakujia!” \p Akaamka toka usingizini, akisema, “Nitatoka nje kama hapo awali; nitajinyoosha, niwe huru.” Lakini hakujua kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemwacha. \p \v 21 Basi Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho yake, wakamteremsha hadi Gaza. Wakamfunga kwa pingu za shaba, wakamweka gerezani ili asage ngano. \v 22 Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. \s1 Kifo cha Samsoni \p \v 23 Basi viongozi wa Wafilisti wakakusanyika pamoja ili kutoa kafara kuu kwa mungu wao Dagoni, wakisherehekea na kusema, “Mungu wetu amemtia adui yetu Samsoni mikononi mwetu.” \p \v 24 Watu walipomwona Samsoni wakamsifu mungu wao, wakisema: \q1 “Sasa mungu wetu amemtia adui yetu \q2 mikononi mwetu, \q1 yule aliyeharibu nchi yetu \q2 na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.” \p \v 25 Mioyo yao ilipokuwa imefurahishwa, wakapaza sauti, wakisema, “Mleteni Samsoni aje ili atutumbuize.” Basi wakamleta Samsoni kutoka gerezani, naye akawatumbuiza. \p Wakamsimamisha katikati ya nguzo mbili. \v 26 Samsoni akamwambia mtumishi aliyeushika mkono wake, “Niweke mahali ambapo ninaweza kuzigusa nguzo ambazo zinategemeza jengo ili nipate kuziegemea.” \v 27 Basi lile jengo lilikuwa na wanaume na wanawake wengi; viongozi wote wa Wafilisti walikuwa humo, na kwenye dari walikuwepo watu wapatao elfu tatu, wanaume kwa wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza. \v 28 Ndipo Samsoni akamwomba Mwenyezi Mungu, akasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tu, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa sababu ya macho yangu mawili.” \v 29 Ndipo Samsoni akazikaribia zile nguzo mbili za katikati zilizokuwa zimelisimamisha lile jengo. Akazishika moja kwa mkono wa kuume, na nyingine kwa mkono wa kushoto. \v 30 Samsoni akasema, “Acha nife pamoja na Wafilisti!” Ndipo akazisukuma zile nguzo kwa nguvu zake zote, nalo jengo lile likaanguka juu ya viongozi na watu wote waliokuwamo ndani. Hivyo, akawaua watu wengi wakati wa kufa kwake kuliko siku za uhai wake. \p \v 31 Basi ndugu zake na jamaa yote ya baba yake wakateremka kwenda kumchukua. Wakampandisha na kumzika kati ya Sora na Eshtaoli, kwenye kaburi la Manoa baba yake. Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini. \c 17 \s1 Sanamu za Mika \p \v 1 Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. \v 2 Akamwambia mama yake, “Zile shekeli elfu moja na mia moja\f + \fr 17:2 \fr*\ft Shekeli 1,100 ni sawa na kilo 13.\ft*\f* za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua.” \p Ndipo mama yake akamwambia, “Mwenyezi Mungu na akubariki, mwanangu.” \p \v 3 Alipozirudisha zile shekeli elfu moja na mia moja za fedha kwa mama yake, mama yake akamwambia, “Mimi nimeiweka fedha hii wakfu kwa Mwenyezi Mungu ili mwanangu atengeneze sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu. Mimi nitakurudishia wewe.” \p \v 4 Hivyo akamrudishia mama yake ile fedha, naye mama yake akachukua shekeli mia mbili\f + \fr 17:4 \fr*\ft Shekeli 200 za fedha ni sawa na kilo 2.3 za fedha.\ft*\f* za hiyo fedha na kumpa mfua fedha, ambaye aliifanyiza kinyago na sanamu. Navyo vikawekwa ndani ya nyumba ya Mika. \p \v 5 Basi Mika alikuwa na mahali pa ibada za sanamu. Akatengeneza kizibau, pamoja na miungu ya nyumbani, na kumweka mmoja wa wanawe kuwa kuhani wake. \v 6 Katika siku hizo, Waisraeli hawakuwa na mfalme; kila mtu alifanya alivyoona ni vyema machoni pake. \p \v 7 Palikuwa na kijana Mlawi kutoka Bethlehemu ya Yuda, aliyekuwa akiishi miongoni mwa watu wa kabila la Yuda. \v 8 Huyu kijana akatoka mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine pa kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya vilima ya Efraimu. \p \v 9 Mika akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?” \p Akamjibu, “Mimi ni Mlawi kutoka Bethlehemu ya Yuda, ninatafuta mahali pa kuishi.” \p \v 10 Ndipo Mika akamwambia, “Ishi pamoja nami, uwe baba yangu na kuhani wangu, nami nitakupa shekeli kumi\f + \fr 17:10 \fr*\ft Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 115 za fedha.\ft*\f* za fedha kila mwaka, pamoja na nguo na chakula.” \v 11 Hivyo yule Mlawi akakubali kuishi pamoja na Mika, naye akawa kama mmoja wa wanawe. \v 12 Basi Mika akamweka wakfu huyo kijana Mlawi, naye huyo akawa kuhani wake na kuishi nyumbani mwake. \v 13 Mika akasema, “Sasa najua Mwenyezi Mungu atanitendea mema, kwa kuwa Mlawi huyu amekuwa kuhani wangu.” \c 18 \s1 Wadani wahamia Laishi \p \v 1 Katika siku hizo, Waisraeli hawakuwa na mfalme. \p Katika siku hizo, watu wa kabila la Dani walikuwa wanatafuta mahali pao wenyewe pa kuishi, kwa sababu walikuwa hawajafika kwenye urithi wao miongoni mwa makabila ya Israeli. \v 2 Hivyo Wadani wakatuma mashujaa watano kutoka Sora na Eshtaoli ili kupeleleza nchi na kuichunguza. Hawa mashujaa waliwakilisha koo zao zote. Waliwaambia, “Nendeni mkaichunguze hiyo nchi.” \p Wanaume hao wakaingia katika nchi ya vilima ya Efraimu, wakafika nyumba ya Mika, ambako walilala usiku huo. \v 3 Walipofika karibu na nyumba ya Mika, waliitambua sauti ya yule kijana Mlawi; hivyo wakaingia humo na kumuuliza, “Ni nani aliyekuleta hapa? Unafanya nini mahali hapa? Kwa nini uko hapa?” \p \v 4 Akawaeleza yale Mika aliyomtendea, akasema, “Ameniajiri, nami ni kuhani wake.” \p \v 5 Kisha wakamwambia, “Tafadhali tuulizie kwa Mungu kama safari yetu itafanikiwa.” \p \v 6 Yule kuhani akawajibu, “Nendeni kwa amani. Safari yenu ina kibali cha Mwenyezi Mungu.” \p \v 7 Basi hao wanaume watano wakaondoka na kufika Laishi, mahali ambapo waliwakuta watu wanaishi salama, kama Wasidoni, kwa amani na utulivu. Nchi yao haikupungukiwa kitu, hivyo wakastawi. Pia walikaa mbali sana na Wasidoni, wala hawakushughulika na mtu yeyote. \p \v 8 Waliporudi kwa ndugu zao huko Sora na Eshtaoli, ndugu zao wakawauliza, “Mlionaje mambo huko?” \p \v 9 Wakajibu, “Twendeni, tukawavamie! Tumeona kuwa nchi ni nzuri sana. Je, hamtafanya chochote? Msisite kupanda ili kuimiliki. \v 10 Mtakapofika huko, mtawakuta watu walio salama, na nchi kubwa ambayo Mungu ameitia mikononi mwenu, isiyopungukiwa kitu chochote duniani.” \p \v 11 Ndipo wanaume mia sita kutoka ukoo wa Wadani, waliojifunga silaha za vita, wakaondoka Sora na Eshtaoli. \v 12 Walipokuwa wakisafiri wakapiga kambi huko Kiriath-Yearimu katika Yuda. Hii ndiyo sababu sehemu ya magharibi ya Kiriath-Yearimu inaitwa Mahane-Dani\f + \fr 18:12 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Kambi ya Dani\fqa*\f* hadi leo. \v 13 Kutoka hapo wakaenda hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kufika katika nyumba ya Mika. \p \v 14 Ndipo wale wanaume watano waliopeleleza nchi ya Laishi wakawaambia ndugu zao, “Je, mnajua kuwa katika mojawapo ya nyumba hizi kuna kizibau, miungu ya nyumbani, sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu? Sasa basi, fikirini mtakalofanya.” \v 15 Basi wakaelekea huko, wakafika kwa yule kijana Mlawi, katika nyumba ya Mika, wakamsalimu. \v 16 Wale Wadani mia sita, wakiwa wamejifunga silaha, wakasimama penye ingilio la lango. \v 17 Wale watu watano walioenda kupeleleza nchi wakaingia ndani na kuchukua ile sanamu ya kuchonga, kile kizibau, na ile miungu ya nyumbani, na ile sanamu ya kusubu, wakati yule kuhani akiwa amesimama pale penye ingilio la lango pamoja na wale watu mia sita waliojifunga silaha. \p \v 18 Hao watu walipoingia katika nyumba ya Mika na kuchukua ile sanamu ya kuchonga, kile kizibau, na ile miungu ya nyumbani, na ile sanamu ya kusubu, yule kuhani akawauliza, “Mnafanya nini?” \p \v 19 Wakamjibu, “Nyamaza! Weka mkono wako juu ya kinywa chako na ufuatane nasi, uwe baba yetu na kuhani wetu. Si ni afadhali utumikie kabila na ukoo katika Israeli kama kuhani kuliko kumtumikia mtu mmoja na watu wa nyumbani mwake?” \v 20 Yule kuhani akafurahi. Akachukua kile kizibau, ile miungu ya nyumbani, na sanamu ya kuchonga, naye akaenda pamoja na wale watu. \v 21 Ndipo wakageuka na kuondoka, wakiwatanguliza mbele watoto wao wadogo, mifugo na mali yao. \p \v 22 Walipokuwa wamefika mbali toka nyumbani kwa Mika, watu walioishi karibu na Mika walikusanywa pamoja, nao wakawakimbiza Wadani. \v 23 Walipofuatilia huku wakipiga kelele, Wadani wakageuka, wakamwambia Mika, “Una nini wewe hata ukawaita watu waje kupigana nasi?” \p \v 24 Akawajibu, “Mmechukua miungu niliyoitengeneza, mkamchukua kuhani wangu, nanyi mkaondoka. Nimebaki na nini kingine? Mnawezaje kuniuliza, ‘Una nini wewe?’ ” \p \v 25 Wadani wakamjibu, “Usibishane nasi, la sivyo watu wenye hasira watakushambulia, nawe na watu wa nyumbani mwako mtapoteza maisha yenu.” \v 26 Basi Wadani wakaenda zao, naye Mika alipoona kuwa wana nguvu kuliko yeye, akageuka na kurudi nyumbani mwake. \p \v 27 Kisha wakachukua vitu vile Mika alikuwa amevitengeneza, na kuhani wake, wakaendelea hadi Laishi, dhidi ya watu walioishi na amani na utulivu. Wakawashambulia kwa upanga na kuuteketeza mji wao. \v 28 Hapakuwa na yeyote wa kuwaokoa, kwa kuwa waliishi mbali na Sidoni, na hawakuwa na ushirikiano na mtu mwingine yeyote. Mji huo ulikuwa kwenye bonde karibu na Beth-Rehobu. \p Wadani wakaujenga upya huo mji na kuishi humo. \v 29 Wakauita ule mji Dani kwa kufuata jina la baba yao aliyezaliwa na Israeli, ingawa mji huo uliitwa Laishi hapo awali. \v 30 Kule Wadani wakajisimamishia ile sanamu ya kuchonga, naye Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa pamoja na wanawe walikuwa makuhani kwa kabila la Dani hadi nchi hiyo ilipotekwa. \v 31 Wakaendelea kuiabudu ile sanamu ambayo Mika alizitengeneza, wakati wote ule nyumba ya Mungu ilikuwa huko Shilo. \c 19 \s1 Mlawi na suria wake \p \v 1 Katika siku hizo, Waisraeli hawakuwa na mfalme. \p Basi Mlawi mmoja aliyeishi sehemu za mbali katika nchi ya vilima ya Efraimu, akamchukua suria mmoja kutoka Bethlehemu ya Yuda. \v 2 Lakini suria wake akafanya ukahaba, akamwacha na kurudi nyumbani mwa baba yake huko Bethlehemu ya Yuda. Baada ya kukaa huko kwa muda wa miezi minne, \v 3 mume wake akaenda kumsihi arudi. Alienda na mtumishi wake na punda wawili. Yule mwanamke akamkaribisha nyumbani mwa baba yake, naye baba yake alipomwona akamkaribisha kwa furaha. \v 4 Baba mkwe wake, yaani baba yake yule msichana, akamsihi akae. Hivyo akakaa na huyo baba mkwe wake kwa siku tatu, wakila na kunywa, na kulala huko. \p \v 5 Siku ya nne wakaamka mapema naye akajiandaa kuondoka, lakini baba wa yule msichana akamwambia mkwewe, “Ujiburudishe kwa kitu cha kula, ndipo uweze kwenda.” \v 6 Basi wakaketi wote wawili ili kula na kunywa pamoja. Baadaye baba wa msichana akamwambia, “Tafadhali ubakie usiku huu upate kujifurahisha.” \v 7 Basi yule mtu alipotaka kuondoka, baba mkwe wake akamsihi, hivyo akabaki usiku ule. \v 8 Asubuhi ya siku ya tano, alipoamka ili aondoke, baba wa yule msichana akamwambia, “Jiburudishe nafsi yako. Ngoja hadi alasiri!” Kwa hiyo wote wawili wakala chakula pamoja. \p \v 9 Kisha yule mtu alipoinuka aende zake pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani baba wa yule msichana, akamwambia, “Tazama sasa jioni inakaribia. Ulale hapa, usiku unakaribia. Ukae, ukajifurahishe nafsi yako. Kesho unaweza kuamka asubuhi na mapema uende nyumbani kwako.” \v 10 Lakini akakataa kulala tena, akaondoka na kuelekea Yebusi (ndio Yerusalemu), akiwa na punda wake wawili waliotandikwa, pamoja na suria wake. \p \v 11 Alipokaribia Yebusi na usiku ukiwa umekaribia, mtumishi akamwambia bwana wake, “Haya sasa natuingie katika mji huu wa Wayebusi tulale humo.” \p \v 12 Lakini bwana wake akamjibu, “Hapana. Hatutaingia kwenye mji wa kigeni, ambao watu wake si Waisraeli. Tutaendelea hadi Gibea.” \v 13 Tena akasema, “Haya, tujitahidi tufike Gibea au Rama, nasi tutalala katika mji huo.” \v 14 Hivyo wakaendelea na safari, nalo jua likazama walipokaribia Gibea ya Benyamini. \v 15 Wakageuka ili kuingia na kulala Gibea. Wakaingia humo, wakaketi kwenye uwanja wa mji, wala hakuna mtu yeyote aliyewakaribisha kwake ili wapate kulala. \p \v 16 Jioni ile, mzee mmoja toka nchi ya vilima ya Efraimu, aliyekuwa anaishi huko Gibea (watu wa sehemu ile walikuwa Wabenyamini), akarudi kutoka kwenye kazi zake za shamba. \v 17 Alipotazama na kuwaona hao wasafiri katika uwanja wa mji, yule mzee akawauliza, “Ninyi mnaenda wapi? Nanyi mmetoka wapi?” \p \v 18 Akamwambia, “Tumepita kutoka Bethlehemu ya Yuda, tunaelekea katika nchi ya vilima ya Efraimu ninakoishi. Nilienda Bethlehemu ya Yuda na sasa ninaenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Hakuna mtu yeyote aliyenikaribisha katika nyumba yake. \v 19 Tunazo nyasi na chakula cha punda wetu, pia mkate na divai kwa ajili yetu sisi watumishi wako: mimi, mtumishi wako mwanamke, pamoja na huyu kijana tuliye naye. Hatuhitaji kitu zaidi.” \p \v 20 Yule mzee akawaambia, “Amani iwe kwenu! Karibuni nyumbani mwangu. Nitawapa mahitaji yenu yote, ila tu msilale katika uwanja huu.” \v 21 Hivyo akamwingiza nyumbani mwake na kuwalisha punda wake. Baada ya kunawa miguu yao, wakala na kunywa. \p \v 22 Walipokuwa wakijiburudisha, wanaume waovu wa mji huo wakaizingira ile nyumba. Wakagonga mlango na kusema kwa sauti kuu kwa yule mzee mwenye nyumba, “Mtoe nje yule mwanaume aliyeingia kwako, tupate kumlawiti.” \p \v 23 Yule mwenye nyumba akatoka nje na kuwaambia, “Hapana, ndugu zangu, msiwe waovu namna hii, ninawasihi. Kwa kuwa huyu mwanaume ni mgeni wangu, msifanye jambo hili la aibu. \v 24 Tazameni, hapa yupo binti yangu ambaye ni bikira, na suria wa mtu huyu. Nitawatoleeni hawa sasa, mkawatwae kwa nguvu na kuwafanyia lolote mtakalo. Lakini kwa mwanaume huyu msimfanyie jambo ovu hivyo.” \p \v 25 Lakini wale wanaume hawakumsikiliza. Hivyo yule mwanaume akamtoa yule suria wake nje kwa wale watu, nao wakambaka na kumnajisi usiku kucha hadi asubuhi. Kulipoanza kupambazuka, wakamwachia aende. \v 26 Alfajiri yule mwanamke akarudi kwenye ile nyumba bwana wake alikokuwa, akaanguka chini mlangoni, akalala pale hata kulipopambazuka. \p \v 27 Bwana wake alipoamka asubuhi na kufungua mlango wa nyumba na kutoka nje ili kuendelea na safari yake, tazama, yule suria wake alikuwa ameangukia penye ingilio la nyumba, mikono yake ikiwa penye kizingiti. \v 28 Akamwambia yule suria, “Inuka, twende.” Lakini hakujibu. Yule bwana akamwinua, akampandisha juu ya punda wake, na wakaondoka kwenda nyumbani. \p \v 29 Alipofika nyumbani, akachukua kisu na kumkatakata yule suria kiungo kwa kiungo, vipande kumi na mbili, na kuvipeleka katika sehemu zote za Israeli. \v 30 Kila mtu aliyeona akasema, “Jambo la namna hii halijaonekana wala kutendeka, tangu Waisraeli walipopanda kutoka Misri. Fikirini juu ya jambo hili! Tafakarini juu ya jambo hili! Tuambieni tufanye nini!” \c 20 \s1 Waisraeli wapigana na Wabenyamini \p \v 1 Ndipo Waisraeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na wa kutoka nchi ya Gileadi wakatoka kama mtu mmoja, wakakusanyika mbele za Mwenyezi Mungu huko Mispa. \v 2 Viongozi wote wa makabila ya Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, ambao walikuwa askari elfu mia nne walioenda kwa miguu wenye panga. \v 3 (Wabenyamini wakasikia kuwa Waisraeli wamepanda kwenda Mispa.) Ndipo Waisraeli wakasema, “Tuelezeni jinsi jambo hili ovu lilivyotendeka.” \p \v 4 Hivyo yule Mlawi, mume wa yule mwanamke aliyeuawa, akasema, “Mimi na suria wangu tulifika Gibea ya Benyamini ili tulale huko. \v 5 Wakati wa usiku wanaume wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu hata akafa. \v 6 Ndipo nikamchukua suria wangu, nikamkatakata vipande vipande na kuvipeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli, kwa kuwa wametenda uasherati mkubwa na jambo la aibu katika Israeli. \v 7 Sasa, ninyi Waisraeli wote, semeni na mtoe uamuzi wenu.” \p \v 8 Watu wote wakainuka wakasema, kama mtu mmoja, “Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda nyumbani. Hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake. \v 9 Sasa hili ndilo tutakaloitendea Gibea: Tutaikabili jinsi kura itakavyotuongoza. \v 10 Tutatoa watu kumi katika kila mia moja kutoka kwenye makabila yote ya Israeli, watu mia moja katika kila elfu moja, na watu elfu moja katika kila elfu kumi, ili waende wakalete mahitaji kwa ajili ya jeshi. Basi wakati jeshi litakapofika Gibea ya Benyamini, watawatendea yale wanayostahili, kwa ajili ya uovu huu walioutenda katika Israeli.” \v 11 Hivyo wanaume wote wa Israeli wakakutanika pamoja na kujiunga kama mtu mmoja dhidi ya huo mji. \p \v 12 Makabila ya Israeli yakatuma watu kwenda katika kabila la Benyamini lote na kuwaambia, “Ni uovu gani huu wa kutisha uliotendeka kati yenu? \v 13 Basi watoeni hao wanaume waovu wa Gibea, ili tupate kuwaua na kuuondoa uovu katika Israeli.” \p Lakini Wabenyamini hawakuwasikia ndugu zao, Waisraeli. \v 14 Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli. \v 15 Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu elfu ishirini na sita kutoka miji yao waliojifunga panga, mbali na hao vijana wenye uwezo mia saba kutoka wale walioishi Gibea. \v 16 Miongoni mwa askari hao, palikuwa na askari mia saba waliochaguliwa waliotumia mkono wa kushoto; kila mmoja wao angetupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele bila kukosa. \p \v 17 Nao wanaume wa Israeli, mbali na hao wa Benyamini, wakakusanya wanaume elfu mia nne hodari wenye panga. \p \v 18 Waisraeli wakapanda Betheli na kumuuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?” \p Mwenyezi Mungu akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.” \p \v 19 Kesho yake asubuhi, Waisraeli wakaamka na kupiga kambi karibu na Gibea. \v 20 Waisraeli wakaondoka ili kupigana na Wabenyamini, nao Waisraeli wakachukua nafasi zao katika vita huko Gibea. \v 21 Wabenyamini wakatoka Gibea na kuwaua Waisraeli elfu ishirini na mbili siku hiyo. \v 22 Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakachukua tena nafasi zao katika vile vita mahali pale walipokuwa siku ya kwanza. \v 23 Waisraeli wakapanda mbele za Mwenyezi Mungu na kulia mbele zake hadi jioni. Nao wakamuuliza Mwenyezi Mungu, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?” \p Mwenyezi Mungu akajibu, “Pandeni mkapigane nao.” \p \v 24 Ndipo Waisraeli wakawakaribia Wabenyamini siku ya pili. \v 25 Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana na Waisraeli, wakawaua wanaume elfu kumi na nane wenye panga. \p \v 26 Ndipo jeshi lote, na Waisraeli wote, wakapanda Betheli, na huko wakakaa mbele za Mwenyezi Mungu wakilia. Wakafunga siku hiyo hadi jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu. \v 27 Nao Waisraeli wakauliza ushauri kwa Mwenyezi Mungu. (Katika siku hizo Sanduku la Agano la Mungu lilikuwa huko, \v 28 na Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anahudumu mbele za hilo Sanduku.) Wakauliza, “Je, tupande tena kwenda vitani kupigana na Wabenyamini, ndugu zetu, au la?” \p Mwenyezi Mungu akajibu, “Nendeni, kwa kuwa kesho nitawatia mikononi mwenu.” \p \v 29 Basi Waisraeli wakaweka waviziaji kuizunguka Gibea. \v 30 Kisha Waisraeli wakapanda kupigana na Wabenyamini katika siku ya tatu na kuchukua nafasi zao dhidi ya Gibea kama walivyokuwa wamefanya hapo awali. \v 31 Wabenyamini wakatoka ili kukabiliana na Waisraeli, ambao waliwavuta Wabenyamini watoke katika mji. Wakaanza kupigana na wakawaua watu wapatao thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika uwanja na katika njia kuu, moja iendayo Betheli na nyingine Gibea. \p \v 32 Wabenyamini walipokuwa wakiambiana, “Wanapigwa mbele yetu kama hapo awali,” nao Waisraeli waliambiana, “Turudini nyuma ili tuwavute wauache mji, waende kuelekea barabarani.” \p \v 33 Wanaume wote wa Israeli wakaondoka kwenye nafasi zao na kujipanga huko Baal-Tamari, nao wale waviziaji wa Waisraeli wakatoka ghafula walipokuwa kwenye uwanda wa magharibi mwa Gibea. \v 34 Ndipo vijana wenye uwezo elfu kumi katika Israeli wakaja kuishambulia Gibea. Vita vilikuwa vikali sana, hata Wabenyamini hawakutambua kuwa maangamizi yalikuwa karibu nao. \v 35 Mwenyezi Mungu akawashinda Wabenyamini mbele ya Waisraeli, na siku hiyo Waisraeli wakawaua Wabenyamini elfu ishirini na tano na mia moja wenye panga. \v 36 Hivyo Wabenyamini wakaona kuwa wameshindwa. \p Basi Waisraeli walikuwa wamewaondokea Wabenyamini, kwa sababu Waisraeli waliwategemea hao waviziaji waliokuwa wamewaweka karibu na Gibea. \v 37 Wale waviziaji wakafanya haraka kuingia Gibea, wakasambaa na kuwaua watu wote wa mji kwa upanga. \v 38 Waisraeli walikuwa wamekubaliana na hao waviziaji kuwa wangesababisha wingu kubwa la moshi lipande kutoka huo mji, \v 39 ndipo Waisraeli wangegeuka kupigana. \p Wabenyamini walikuwa wameanza kuwapiga na kuwaua Waisraeli (wapatao thelathini), hivyo wakasema, “Hakika tunawashinda kama tulivyowashinda katika vita hapo awali.” \v 40 Lakini nguzo ya moshi ilipoanza kupanda kutoka mji ule, Wabenyamini wakageuka, na tazama: katika mji mzima, moshi ulikuwa ukipaa angani. \v 41 Ndipo Waisraeli wakawageukia, nao Wabenyamini wakatiwa hofu, kwa kuwa walitambua kwamba maafa yamewajia. \v 42 Basi wakakimbia mbele ya Waisraeli kuelekea nyikani, lakini hawakuweza kukwepa vile vita. Nao Waisraeli waliotoka katika ile miji wakawaua huko. \v 43 Wakawazingira Wabenyamini pande zote, wakawafuatia na kuwafikia karibu na Gibea upande wa mashariki. \v 44 Wakaanguka Wabenyamini elfu kumi na nane, wote wapiganaji hodari. \v 45 Walipogeuka na kukimbia kuelekea nyikani hata kufikia mwamba wa Rimoni, Waisraeli wakawaua watu elfu tano huko njiani. Wakawafuatia kwa karibu hadi Gidomu, na huko wakawaua wanaume wengine elfu mbili. \p \v 46 Siku hiyo wakawaua Wabenyamini elfu ishirini na tano wenye panga, wapiganaji hodari. \v 47 Lakini watu mia sita wakakimbia kuelekea nyikani katika mwamba wa Rimoni, na kukaa huko muda wa miezi minne. \v 48 Waisraeli wakarudi na kuwaua kwa upanga Wabenyamini wote, pamoja na wanyama na kila walichokipata. Pia kila mji waliouona wakauchoma kwa moto. \c 21 \s1 Wabenyamini watafutiwa wake \p \v 1 Wanaume wa Israeli walikuwa wameapa kiapo kule Mispa, wakasema: “Hapana mtu yeyote wetu atakayemwoza binti yake kwa Mbenyamini.” \p \v 2 Watu wakaenda Betheli, wakaketi mbele za Mungu hadi jioni, wakapaza sauti zao wakilia kwa uchungu. \v 3 Wakasema, “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limewapata Waisraeli? Kwa nini kabila moja la Israeli limekosekana?” \p \v 4 Kesho yake asubuhi na mapema watu wakajenga madhabahu na kuleta sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. \p \v 5 Ndipo Waisraeli wakauliza, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikukusanyika mbele za Mwenyezi Mungu?” Kwa kuwa walikuwa wameapa kiapo kikuu kuwa yeyote asiyefika mbele za Mwenyezi Mungu huko Mispa, kwa hakika angeuawa. \p \v 6 Basi Waisraeli wakahuzunika kwa ajili ya ndugu zao Wabenyamini, wakasema, “Leo kabila moja limekatiliwa mbali na Israeli. \v 7 Sasa tutawezaje kuwapa binti zetu kuwa wake zao, hao waliobaki, na tumeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hatutawapa binti zetu kuwa wake zao?” \v 8 Ndipo wakasema, “Ni kabila lipi la Israeli ambalo halikukusanyika mbele za Mwenyezi Mungu huko Mispa?” Wakagundua kuwa hakuna hata mmoja kutoka Yabesh-Gileadi aliyefika kambini kwa kusanyiko. \v 9 Kwa kuwa walipohesabu waliona hapakuwa mtu yeyote wa Yabesh-Gileadi. \p \v 10 Ndipo mkutano wakatuma wapiganaji elfu kumi na mbili, wakawaamuru kwenda Yabesh-Gileadi na kuua kwa panga wale wote walioishi huko, wakiwemo wake na watoto. \v 11 Wakasema, “Hili ndilo mtakalofanya: Ueni kila mwanaume na kila mwanamke ambaye si bikira.” \v 12 Wakapata kati ya watu walioishi Yabesh-Gileadi wanawali mia nne, mabikira, nao wakawachukua kwenye kambi huko Shilo katika nchi ya Kanaani. \p \v 13 Ndipo mkutano ukatuma ujumbe wa amani kwa Wabenyamini huko katika mwamba wa Rimoni. \v 14 Basi Wabenyamini wakarudi wakati ule, nao wakapewa wale wanawali wa Yabesh-Gileadi waliohifadhiwa. Lakini hawakuwatosha wanaume wote. \p \v 15 Waisraeli wakahuzunika kwa ajili ya Wabenyamini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa ameweka ufa katika makabila ya Israeli. \v 16 Viongozi wa kusanyiko wakasema, “Kwa kuwa wanawake wa Wabenyamini wameangamizwa, tufanyeje ili kuwapatia wake wale wanaume waliosalia?” \v 17 Wakaendelea kusema, “Lazima tuwape Wabenyamini waliopona wake ili wawe na warithi, nalo kabila lolote katika Israeli lisifutike. \v 18 Hatuwezi kuwapa binti zetu kuwa wake, kwa kuwa sisi Waisraeli tumeapa kiapo hiki: ‘Alaaniwe mtu yeyote ampaye Mbenyamini mke.’ ” \v 19 Ndipo waliposema, “Tazama iko sikukuu ya kila mwaka ya Mwenyezi Mungu katika Shilo, kaskazini mwa Betheli na mashariki mwa ile barabara inayotoka Betheli kwenda Shekemu, upande wa kusini wa Lebona.” \p \v 20 Hivyo wakawaelekeza Wabenyamini, wakisema, “Nendeni mkajifiche kwenye mashamba ya mizabibu, \v 21 na mkae macho. Wasichana wa Shilo watakapojiunga kwenye kucheza, tokeni kwenye hayo mashamba ya mizabibu, na kila mmoja ajinyakulie mke kutoka miongoni mwa hao wasichana wa Shilo, nanyi mwende nao katika nchi ya Benyamini. \v 22 Baba zao au ndugu zao watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Kuweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpa kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia, kwa kuwa hamkuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ” \p \v 23 Basi hivyo ndivyo Wabenyamini walivyofanya. Wasichana walipokuwa wakicheza, kila mtu akanyakua msichana mmoja, akaenda naye ili awe mke wake. Kisha wakarudi katika urithi wao na kuijenga upya miji na kuishi humo. \p \v 24 Wakati huo Waisraeli wakaondoka sehemu ile na kwenda nyumbani kwao, kwa makabila yao na kwa jamaa zao, kila mmoja kwenye urithi wake mwenyewe. \p \v 25 Katika siku hizo, Waisraeli hawakuwa na mfalme; kila mtu alifanya alivyoona ni vyema machoni pake.