\id HAG - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Hagai \toc1 Hagai \toc2 Hagai \toc3 Hag \mt1 Hagai \c 1 \s1 Wito wa kujenga Hekalu \p \v 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, katika siku ya kwanza ya mwezi wa sita, neno la Mwenyezi Mungu lilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na kwa Yoshua\f + \fr 1:1 \fr*\ft kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Yeshua\fqa*\ft , maana yake \ft*\fqa Yehova ni wokovu\fqa*\f* mwana wa kuhani mkuu Yehosadaki: \p \v 2 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 3 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likaja kupitia kwa nabii Hagai: \v 4 “Je, ni wakati wenu ninyi wa kuishi katika nyumba zenu zilizojengwa vizuri, wakati hii nyumba ikibaki gofu?” \p \v 5 Sasa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Zitafakarini vyema njia zenu. \v 6 Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.” \p \v 7 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Zitafakarini vyema njia zenu. \v 8 Pandeni milimani mkalete miti na kujenga nyumba, ili nipate kuifurahia, na nitukuzwe,” asema Mwenyezi Mungu. \v 9 “Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe. \v 10 Kwa hiyo, mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake kwa sababu yenu. \v 11 Niliita ukame mashambani na milimani, kwenye nafaka, mvinyo mpya, mafuta pamoja na chochote kinachozalishwa na ardhi, juu ya watu na ng’ombe, pamoja na kazi za mikono yenu.” \b \p \v 12 Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Watu walimwogopa Mwenyezi Mungu. \p \v 13 Kisha Hagai, mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akawapa watu ujumbe huu wa Mwenyezi Mungu: “Mimi niko pamoja nanyi,” asema Mwenyezi Mungu. \v 14 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja, wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wao, \v 15 siku ya ishirini na nne ya mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario. \c 2 \s1 Utukufu ulioahidiwa wa Hekalu jipya \p \v 1 Katika siku ya ishirini na moja ya mwezi wa saba, neno la Mwenyezi Mungu lilikuja kupitia nabii Hagai, kusema: \v 2 “Sema na Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, na mabaki ya watu. Uwaulize, \v 3 ‘Ni nani miongoni mwenu aliyebaki ambaye aliiona hii nyumba katika utukufu wake wa mwanzo? Sasa inaonekanaje kwenu? Je, haionekani kwenu kama si kitu? \v 4 Lakini sasa uwe imara, ee Zerubabeli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Kuwa imara, ee kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Mwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \v 5 ‘Hili ndilo nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri. Pia Roho wangu Mtakatifu anadumu kati yenu. Msiogope.’ \p \v 6 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Baada ya muda kidogo kwa mara nyingine nitazitikisa mbingu na nchi, bahari na nchi kavu. \v 7 Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \v 8 ‘Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \v 9 ‘Utukufu wa nyumba hii ya sasa utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa ile nyumba ya mwanzoni,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. ‘Na mahali hapa nitawapa amani,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.” \s1 Baraka kwa watu waliotiwa unajisi \p \v 10 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilikuja kwa nabii Hagai: \v 11 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Ulizeni makuhani jinsi sheria inavyosema: \v 12 Kama mtu akibeba nyama iliyowekwa wakfu katika pindo la vazi lake, kisha lile pindo likagusa mkate au mchuzi, divai, mafuta au chakula kingine, je, kitu hicho kitakuwa kimewekwa wakfu?’ ” \p Makuhani wakajibu, “La.” \p \v 13 Kisha Hagai akasema, “Je, kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti akigusa mojawapo ya vitu hivi, kitu hicho kitakuwa kimetiwa unajisi?” \p Makuhani wakajibu, “Ndiyo, huwa kimenajisiwa.” \p \v 14 Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Lolote wafanyalo na chochote watoacho hapo ni najisi. \p \v 15 “ ‘Sasa fikirini kwa uangalifu kuanzia leo na kuendelea: tafakarini jinsi mambo yalivyokuwa kabla halijawekwa jiwe moja juu ya lingine katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 16 Mtu alipoendea lundo la nafaka la vipimo ishirini, kulikuwa na vipimo kumi tu. Mtu alipoendea pipa la mvinyo ili kuchota vipimo hamsini, kulikuwa na vipimo ishirini tu. \v 17 Kazi zenu zote za mikono nilizipiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo, hamkunigeukia mimi,’ asema Mwenyezi Mungu. \v 18 ‘Tangu leo na kuendelea, kuanzia siku hii ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, tafakarini siku ambayo msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu uliwekwa. Tafakarini: \v 19 Je, bado kuna mbegu iliyobakia ghalani? Hadi sasa, hakuna mzabibu au mtini, mkomamanga wala mzeituni uliozaa tunda. \p “ ‘Kuanzia leo na kuendelea, nitawabariki.’ ” \s1 Zerubabeli pete ya muhuri ya Mwenyezi Mungu \p \v 20 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema: \v 21 “Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi. \v 22 Nitapindua viti vya falme, na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake. \p \v 23 “ ‘Katika siku ile,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.”