\id GEN - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Mwanzo \toc1 Mwanzo \toc2 Mwanzo \toc3 Mwa \mt1 Mwanzo \c 1 \s1 Siku sita za uumbaji \p \v 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. \v 2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji. \b \p \v 3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. \v 4 Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema; ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. \v 5 Mungu akaiita nuru “mchana”, na giza akaliita “usiku”. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza. \b \p \v 6 Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji, igawe maji na maji.” \v 7 Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. \v 8 Mungu akaiita hiyo nafasi “anga”. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili. \b \p \v 9 Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo. \v 10 Mungu akaiita nchi kavu “ardhi”, nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. \p \v 11 Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo. \v 12 Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema. \v 13 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu. \b \p \v 14 Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka, \v 15 nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo. \v 16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota. \v 17 Mungu akaiweka hiyo mianga katika nafasi ya anga iangaze dunia, \v 18 itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema. \v 19 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne. \b \p \v 20 Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.” \v 21 Kwa hiyo Mungu akaumba wanyama wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. \v 22 Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.” \v 23 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano. \b \p \v 24 Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: mifugo, viumbe vinavyotambaa ardhini na wanyama pori, kila kiumbe kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo. \v 25 Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, mifugo kulingana na aina zake, na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. \p \v 26 Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na mifugo na wanyama pori wote, na dunia yote, na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini.” \q1 \v 27 Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, \q2 kwa mfano wa Mungu alimuumba; \q2 mwanaume na mwanamke aliwaumba. \p \v 28 Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.” \p \v 29 Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. \v 30 Nao wanyama wote wa nchi, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo. \p \v 31 Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, vilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita. \b \c 2 \p \v 1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. \b \p \v 2 Kufikia siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya; hivyo siku hiyo ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. \v 3 Mungu akaibariki siku ya saba, akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika baada ya kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. \s1 Adamu na Hawa \p \v 4 Haya ndio maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. \b \p Bwana Mwenyezi Mungu alipoziumba mbingu na dunia, \v 5 hapakuwa na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwa na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kuilima ardhi, \v 6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi. \v 7 Bwana Mwenyezi Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi\f + \fr 2:7 \fr*\ft Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu.\ft*\f* ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai. \p \v 8 Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni; huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. \v 9 Bwana Mwenyezi Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Mti wa uzima ulikuwa katikati ya bustani, na pia mti wa kujua mema na mabaya. \p \v 10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni; kuanzia hapo ukagawanyika kuwa mito minne. \v 11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. \v 12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri; bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) \v 13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. \v 14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati. \p \v 15 Bwana Mwenyezi Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. \v 16 Bwana Mwenyezi Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani; \v 17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.” \p \v 18 Bwana Mwenyezi Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” \p \v 19 Basi Bwana Mwenyezi Mungu alikuwa ametengeneza kutoka ardhi wanyama pori wote, na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa jina lake. \v 20 Hivyo Adamu akawapa majina mifugo wote, ndege wa angani, na wanyama pori wote. \p Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. \v 21 Hivyo Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. \v 22 Kisha Bwana Mwenyezi Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwa ule ubavu alioutoa kwa mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa mwanaume. \p \v 23 Huyo mwanaume akasema, \q1 “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu, \q2 na nyama ya nyama yangu, \q1 ataitwa ‘mwanamke’, \q2 kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” \m \v 24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. \p \v 25 Adamu na mkewe wote walikuwa uchi, wala hawakuona aibu. \c 3 \s1 Kuanguka kwa mwanadamu \p \v 1 Basi nyoka alikuwa mjanja kuliko wanyama pori wote ambao Bwana Mwenyezi Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?” \p \v 2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyo katika bustani, \v 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ” \p \v 4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. \v 5 Kwa maana Mungu anajua kwamba mtakapokula tunda hilo, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” \p \v 6 Mwanamke alipotambua kwamba tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma matunda yake, akala. Pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, akala. \v 7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. \p \v 8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani. \v 9 Lakini Bwana Mwenyezi Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?” \p \v 10 Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.” \p \v 11 Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?” \p \v 12 Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa matunda ya huo mti, nami nikala.” \p \v 13 Ndipo Bwana Mwenyezi Mungu akamuuliza mwanamke, “Umefanya jambo gani?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.” \p \v 14 Hivyo Bwana Mwenyezi Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili, \q1 “Umelaaniwa kuliko mifugo wote \q2 na wanyama pori wote! \q1 Utatambaa kwa tumbo lako \q2 na kula mavumbi \q2 siku zote za maisha yako. \q1 \v 15 Nami nitaweka uadui \q2 kati yako na huyu mwanamke, \q2 na kati ya uzao wako na wake; \q1 yeye atakuponda kichwa, \q2 nawe utamuuma kisigino.” \p \v 16 Kwa mwanamke akasema, \q1 “Nitakuzidishia sana uchungu wakati wa kuzaa kwako; \q2 kwa uchungu utazaa watoto. \q1 Tamaa yako itakuwa kwa mumeo, \q2 naye atakutawala.” \p \v 17 Akamwambia Adamu, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’ \q1 “Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; \q2 kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo \q2 siku zote za maisha yako. \q1 \v 18 Itakuzalia miiba na mibaruti, \q2 nawe utakula mimea ya shambani. \q1 \v 19 Kwa jasho la uso wako \q2 utakula chakula chako \q1 hadi utakaporudi ardhini, \q2 kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo; \q1 wewe u mavumbi \q2 na mavumbini utarudi.” \p \v 20 Adamu akamwita mkewe jina Hawa, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai. \p \v 21 Bwana Mwenyezi Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. \v 22 Kisha Bwana Mwenyezi Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.” \v 23 Hivyo Bwana Mwenyezi Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa. \v 24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki mwa Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika kila upande kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima. \c 4 \s1 Kaini na Habili \p \v 1 Adamu akakutana kimwili na mkewe Hawa, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Hawa akasema, “Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu nimemzaa mtoto wa kiume.” \v 2 Baadaye akamzaa Habili ndugu yake. \p Basi Habili akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. \v 3 Baada ya muda, Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba ikiwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu. \v 4 Lakini Habili akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Mwenyezi Mungu akamkubali Habili pamoja na sadaka yake, \v 5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni. \p \v 6 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? \v 7 Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, ikikutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.” \p \v 8 Basi Kaini akamwambia ndugu yake Habili, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Habili ndugu yake, akamuua. \p \v 9 Kisha Mwenyezi Mungu akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” \p Akamjibu, “Sijui. Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” \p \v 10 Mwenyezi Mungu akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. \v 11 Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako. \v 12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani bila utulivu.” \p \v 13 Kaini akamwambia Mwenyezi Mungu, “Adhabu yangu ni zaidi ya ninavyoweza kustahimili. \v 14 Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga duniani bila utulivu, na yeyote anionaye ataniua.” \p \v 15 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia, “La, sivyo! Ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini, atalipizwa kisasi mara saba.” Kisha Mwenyezi Mungu akamwekea Kaini alama ili yeyote angemwona asimuue. \v 16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Mwenyezi Mungu, akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni. \p \v 17 Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Idrisi. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Idrisi, jina la mtoto wake. \v 18 Idrisi akamzaa Iradi; Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; naye Methushaeli akamzaa Lameki. \p \v 19 Lameki alioa wanawake wawili: mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila. \v 20 Ada akamzaa Yabali; huyu akawa baba wa wale wanaoishi katika mahema na kufuga wanyama. \v 21 Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi. \v 22 Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini, ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. \p \v 23 Lameki akawaambia wake zake, \q1 “Ada na Sila, nisikilizeni mimi; \q2 wake wa Lameki sikieni maneno yangu. \q1 Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, \q2 kijana mdogo kwa kuniumiza. \q1 \v 24 Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba, \q2 basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.” \p \v 25 Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita jina Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuua.” \v 26 Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita jina Enoshi. \p Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Mwenyezi Mungu. \c 5 \s1 Kutoka Adamu hadi Nuhu \r (1 Nyakati 1:1-4) \p \v 1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. \b \p Mungu alipomuumba mwanadamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. \v 2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “Binadamu.” \b \li1 \v 3 Adamu alipokuwa ameishi miaka mia moja na thelathini, alimzaa mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita jina Sethi. \v 4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka mia nane, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 5 Adamu aliishi jumla ya miaka mia tisa na thelathini, ndipo akafa. \li1 \v 6 Sethi alipokuwa ameishi miaka mia moja na tano, akamzaa Enoshi. \v 7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka mia nane na saba (807), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 8 Sethi aliishi jumla ya miaka mia tisa na kumi na mbili (912), ndipo akafa. \li1 \v 9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. \v 10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka mia nane na kumi na tano (815), naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 11 Enoshi aliishi jumla ya miaka mia tisa na tano (905), ndipo akafa. \li1 \v 12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. \v 13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka mia nane na arobaini, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 14 Kenani aliishi jumla ya miaka mia tisa na kumi, ndipo akafa. \li1 \v 15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Yaredi. \v 16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka mia nane na thelathini, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka mia nane tisini na tano (895), ndipo akafa. \li1 \v 18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka mia moja na sitini na mbili (162), akamzaa Idrisi. \v 19 Baada ya kumzaa Idrisi, Yaredi aliishi miaka mia nane, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 20 Yaredi aliishi jumla ya miaka mia tisa na sitini na mbili (962), ndipo akafa. \li1 \v 21 Idrisi alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela. \v 22 Baada ya kumzaa Methusela, Idrisi alitembea na Mungu miaka mia tatu, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 23 Idrisi aliishi jumla ya miaka mia tatu sitini na tano (365). \v 24 Idrisi akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua. \li1 \v 25 Methusela alipokuwa ameishi miaka mia moja na themanini na saba (187), akamzaa Lameki. \v 26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka mia saba na themanini na mbili (782), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 27 Methusela aliishi jumla ya miaka mia tisa sitini na tisa (969), ndipo akafa. \li1 \v 28 Lameki alipokuwa ameishi miaka mia moja na themanini na mbili (182), alimzaa mwana. \v 29 Akamwita jina Nuhu. Naye akasema, “Huyu ndiye atakayetufariji katika kazi ngumu ya mikono yetu yenye maumivu makali yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Mwenyezi Mungu.” \v 30 Baada ya Nuhu kuzaliwa, Lameki aliishi miaka mia tano na tisini na tano (595), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 31 Lameki aliishi jumla ya miaka mia saba sabini na saba (777), ndipo akafa. \li1 \v 32 Baada ya Nuhu kuishi miaka mia tano, aliwazaa Shemu, Hamu, na Yafethi. \c 6 \s1 Gharika kuu \p \v 1 Idadi ya watu ilipoanza kuongezeka duniani, na watoto wa kike wakazaliwa kwao, \v 2 wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua. \v 3 Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa; siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.” \p \v 4 Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na hata baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa wa zamani, na watu mashuhuri. \p \v 5 Mwenyezi Mungu akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. \v 6 Mwenyezi Mungu akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, na moyo wa Mungu ukasikitika sana. \v 7 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” \v 8 Lakini Nuhu akapata kibali machoni pa Mwenyezi Mungu. \b \p \v 9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. \b \p Nuhu alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. \v 10 Nuhu alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. \p \v 11 Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. \v 12 Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. \v 13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Nuhu, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika nitaangamiza watu pamoja na dunia. \v 14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje; tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. \v 15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa mia tatu\f + \fr 6:15 \fr*\ft Dhiraa 300 ni sawa na mita 135.\ft*\f*, upana wake dhiraa hamsini\f + \fr 6:15 \fr*\ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5.\ft*\f*, na kimo chake dhiraa thelathini\f + \fr 6:15 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5.\ft*\f*. \v 16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja\f + \fr 6:16 \fr*\ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\ft*\f* juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. \v 17 Nitaleta gharika ya maji juu ya dunia ili kuangamiza kila chenye uhai chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya dunia kitaangamia. \v 18 Lakini mimi nitaweka agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao. \v 19 Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe. \v 20 Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama, na wa kila aina ya kiumbe kinachotambaa ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai. \v 21 Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.” \p \v 22 Nuhu akafanya kila kitu kama vile Mungu alimwamuru. \c 7 \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Nuhu, “Ingia katika safina, wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. \v 2 Chukua wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike; na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi, wa kiume na wa kike. \v 3 Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote. \v 4 Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya dunia kwa siku arobaini, usiku na mchana; nami nitafutilia mbali kutoka uso wa dunia kila kiumbe hai nilichokiumba.” \p \v 5 Nuhu akafanya yote Mwenyezi Mungu aliyomwamuru. \p \v 6 Nuhu alikuwa na umri wa miaka mia sita gharika ilipokuja juu ya dunia. \v 7 Nuhu na mkewe, na wanawe na wake zao, wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. \v 8 Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vinavyotambaa ardhini, \v 9 wa kiume na wa kike, walikuja kwa Nuhu, wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Nuhu. \v 10 Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia. \p \v 11 Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili, mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, siku hiyo chemchemi zote za vilindi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. \v 12 Mvua ikanyesha juu ya dunia siku arobaini usiku na mchana. \p \v 13 Siku hiyo Nuhu na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao, wakaingia katika ile safina. \v 14 Nao walikuwa pamoja na kila mnyama pori kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kinachotambaa juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. \v 15 Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai vikaja kwa Nuhu viwili viwili, vikaingia katika safina. \v 16 Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Nuhu; ndipo Mwenyezi Mungu akamfungia ndani. \p \v 17 Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani; maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka uso wa dunia. \v 18 Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya dunia, na safina ikaelea juu ya maji. \v 19 Maji yakazidi kujaa juu ya dunia, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. \v 20 Maji yakaendelea kujaa, yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano\f + \fr 7:20 \fr*\ft Dhiraa 15 ni sawa na mita 7.\ft*\f*. \v 21 Kila kiumbe hai kinachotambaa juu ya dunia kikaangamia: ndege, mifugo, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi, na wanadamu wote. \v 22 Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. \v 23 Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali; watu, wanyama pori, viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Nuhu peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. \p \v 24 Maji yakaifunika dunia kwa siku mia moja na hamsini. \c 8 \s1 Mwisho wa gharika \p \v 1 Mungu akamkumbuka Nuhu na wanyama pori na mifugo wote waliokuwa naye ndani ya safina; akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakapungua. \v 2 Chemchemi za vilindi zikawa zimefungwa, na malango ya mafuriko ya mbinguni pia yakawa yamefungwa; nayo mvua ikawa imekoma kunyesha. \v 3 Maji yakaendelea kupungua taratibu katika dunia. Mwishoni mwa siku ya mia moja na hamsini, maji yakawa yamepungua. \v 4 Na katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati. \v 5 Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana. \p \v 6 Baada ya siku arobaini, Nuhu akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina, \v 7 akamtoa kunguru, naye akawa akiruka kwenda na kurudi hadi maji yalipokwisha kukauka juu ya dunia. \v 8 Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya ardhi. \v 9 Lakini hua hakupata mahali pa kutua, kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Nuhu ndani ya safina. Nuhu akanyoosha mkono akamchukua yule hua, akamrudisha ndani ya safina. \v 10 Nuhu akangojea siku saba zaidi, kisha akamtoa tena hua kutoka safina. \v 11 Jioni hua aliporudi kwa Nuhu alikuwa amebeba jani bichi la mzeituni lililochumwa wakati ule ule katika mdomo wake! Ndipo Nuhu akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya dunia. \v 12 Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Nuhu. \p \v 13 Kufikia siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa mia sita na moja (601) wa maisha ya Nuhu, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Nuhu akatoa kifuniko juu ya safina, akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka. \v 14 Kufikia siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili, dunia ilikuwa imekauka kabisa. \p \v 15 Ndipo Mungu akamwambia Nuhu, \v 16 “Toka katika safina, wewe na mkeo, na wanao na wake zao. \v 17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe, wakiwamo ndege, wanyama na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.” \p \v 18 Kwa hiyo Nuhu akatoka nje pamoja na mkewe, na wanawe na wake zao. \v 19 Wanyama wote na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini, na ndege wote, kila kitu kinachoenda juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina. \s1 Nuhu atoa dhabihu \p \v 20 Kisha Nuhu akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. \v 21 Mwenyezi Mungu akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya. \q1 \v 22 “Kwa muda dunia idumupo, \q1 majira ya kupanda na ya kuvuna, \q1 wakati wa baridi na wa joto, \q1 wakati wa kiangazi na wa masika, \q1 usiku na mchana \q1 kamwe havitakoma.” \c 9 \s1 Mwenyezi Mungu aweka agano na Nuhu \p \v 1 Ndipo Mungu akawabariki Nuhu na wanawe, akiwaambia, “Zaeni, mkaongezeke kwa idadi, na mkaijaze tena dunia. \v 2 Wanyama wote wa nchi, na ndege wote wa angani, na kila kiumbe kinachotambaa juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. \v 3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu. \p \v 4 “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu, kwa maana damu ni uhai. \v 5 Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa binadamu mwenzake. \q1 \v 6 “Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu, \q2 damu yake itamwagwa na mwanadamu; \q1 kwa kuwa katika mfano wa Mungu, \q2 Mungu alimuumba mwanadamu. \m \v 7 Bali ninyi, zaeni mwongezeke kwa idadi; zidini duniani na kuijaza.” \p \v 8 Ndipo Mungu akamwambia Nuhu na wanawe pamoja naye: \v 9 “Sasa mimi ninaweka agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, \v 10 pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: ndege, mifugo, na wanyama pori wote, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi: kila kiumbe hai duniani. \v 11 Ninaweka agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika; kamwe hakutakuwa tena gharika ya kuangamiza dunia.” \p \v 12 Mungu akasema, “Hii ni ishara ya agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, agano kwa vizazi vyote vijavyo: \v 13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nifanyalo kati yangu na dunia. \v 14 Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukatokea mawinguni, \v 15 nitakumbuka agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. \v 16 Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.” \p \v 17 Hivyo Mungu akamwambia Nuhu, “Hii ndiyo ishara ya agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.” \s1 Wana wa Nuhu \p \v 18 Wana wa Nuhu waliotoka ndani ya safina walikuwa: Shemu, na Hamu, na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) \v 19 Hao walikuwa wana watatu wa Nuhu, na kutokana nao watu walienea katika dunia. \p \v 20 Nuhu akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. \v 21 Alipokunywa huo mvinyo wake, akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. \v 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. \v 23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo, wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao. \p \v 24 Nuhu alipolevuka na kujua lile mwanawe mdogo alilomtendea, \v 25 akasema, \q1 “Alaaniwe Kanaani! \q2 Atakuwa mtumwa wa chini kabisa \q2 kwa ndugu zake.” \p \v 26 Pia akasema, \q1 “Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Shemu! \q2 Kanaani na awe mtumwa wa Shemu. \q1 \v 27 Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; \q2 Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, \q2 na Kanaani na awe mtumwa wake.” \p \v 28 Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka mia tatu na hamsini. \v 29 Nuhu aliishi jumla ya miaka mia tisa na hamsini, ndipo akafa. \c 10 \s1 Mataifa yaliyotokana na Nuhu \r (1 Nyakati 1:5-23) \lh \v 1 Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, yaani Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika. \s2 Wazao wa Yafethi \li1 \v 2 Wana wa Yafethi walikuwa: \li2 Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. \li1 \v 3 Wana wa Gomeri walikuwa: \li2 Ashkenazi, Rifathi na Togarma. \li1 \v 4 Wana wa Yavani walikuwa: \li2 Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. \v 5 (Kutokana na hawa mataifa ya pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.) \s2 Wazao wa Hamu \li1 \v 6 Wana wa Hamu walikuwa: \li2 Kushi, Misri\f + \fr 10:6 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Misraimu\fqa*\f*, Putu na Kanaani. \li1 \v 7 Wana wa Kushi walikuwa: \li2 Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. \li1 Wana wa Raama walikuwa: \li2 Sheba na Dedani. \lf \v 8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa shujaa mwenye nguvu duniani. \v 9 Alikuwa mwindaji hodari mbele za Mwenyezi Mungu; Ndiyo maana watu husema, “Kama Nimrodi, mwindaji hodari mbele za Mwenyezi Mungu.” \v 10 Vituo vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne, katika nchi ya Shinari. \v 11 Kutoka nchi ile alienda Ashuru, ambako alijenga miji ya Ninawi, na Rehoboth-Iri, na Kala, \v 12 na Reseni, mji ulio kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa. \li1 \v 13 Misri alikuwa baba wa: \li2 Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, \v 14 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori. \li1 \v 15 Kanaani alikuwa baba wa: \li2 Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, \v 16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, \v 17 Wahivi, Waarki, Wasini, \v 18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. \li2 (Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, \v 19 na mipaka ya Kanaani ikaenea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.) \lf \v 20 Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao. \s2 Wazao wa Shemu \lh \v 21 Shemu, ndugu mkubwa wa Yafethi, alizaa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi. \li1 \v 22 Wana wa Shemu walikuwa: \li2 Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. \li1 \v 23 Wana wa Aramu walikuwa: \li2 Usi, Huli, Getheri na Mashi\f + \fr 10:23 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mesheki\fqa*\f*. \li1 \v 24 Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, \li2 naye Shela akamzaa Eberi. \li1 \v 25 Eberi akapata wana wawili: \li2 Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. \li1 \v 26 Yoktani alikuwa baba wa: \li2 Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, \v 27 Hadoramu, Uzali, Dikla, \v 28 Obali, Abimaeli, Seba, \v 29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani. \li2 \v 30 (Eneo waliloishi lilienea kutoka Mesha kuelekea Sefari, kwenye nchi ya vilima iliyo mashariki.) \lf \v 31 Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao. \b \lf \v 32 Hizi ndizo koo za wana wa Nuhu, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika. \c 11 \s1 Mnara wa Babeli \p \v 1 Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. \v 2 Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari\f + \fr 11:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Babeli\fqa*\f*, nao wakaishi huko. \p \v 3 Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kuunganisha hayo matofali. \v 4 Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina, tusije tukatawanyika duniani kote.” \p \v 5 Lakini Mwenyezi Mungu akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu walikuwa wanaujenga. \v 6 Mwenyezi Mungu akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. \v 7 Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” \p \v 8 Hivyo Mwenyezi Mungu akawatawanya kutoka mahali pale waende duniani kote; nao wakaacha kuujenga huo mji. \v 9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Mwenyezi Mungu akawatawanya duniani kote. \s1 Vizazi vya Shemu hadi Abramu \r (1 Nyakati 1:24-27) \p \v 10 Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. \b \li1 Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na umri wa miaka mia moja, akamzaa Arfaksadi. \v 11 Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka mia tano, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 12 Arfaksadi alipokuwa ameishi miaka thelathini na tano, akamzaa Shela. \v 13 Baada ya kumzaa Shela, Arfaksadi aliishi miaka mia nne na tatu (403), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 14 Shela alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. \v 15 Baada ya kumzaa Eberi, Shela aliishi miaka mia nne na tatu (403), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 16 Eberi alipokuwa ameishi miaka thelathini na nne, akamzaa Pelegi. \v 17 Baada ya kumzaa Pelegi, Eberi aliishi miaka mia nne na thelathini (430), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 18 Pelegi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Reu. \v 19 Baada ya kumzaa Reu, Pelegi aliishi miaka mia mbili na tisa (209), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 20 Reu alipokuwa ameishi miaka thelathini na mbili, akamzaa Serugi. \v 21 Baada ya kumzaa Serugi, Reu aliishi miaka mia mbili na saba (207), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 22 Serugi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. \v 23 Baada ya kumzaa Nahori, Serugi aliishi miaka mia mbili, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 24 Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. \v 25 Baada ya kumzaa Tera, Nahori aliishi miaka mia moja na kumi na tisa (119), akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \li1 \v 26 Tera alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na baadaye akawazaa Nahori na Harani. \s1 Wazao wa Tera \p \v 27 Hivi ndivyo vizazi vya Tera. \b \p Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Lutu. \v 28 Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa katika Uru ya Wakaldayo, nchi aliyozaliwa. \v 29 Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, naye mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. \v 30 Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. \p \v 31 Tera akawachukua Abramu mwanawe, mjukuu wake Lutu mwana wa Harani, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka Uru ya Wakaldayo pamoja, wakaenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko. \p \v 32 Tera aliishi miaka mia mbili na mitano (205), akafa huko Harani. \c 12 \s1 Wito wa Abramu \p \v 1 Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha. \q1 \v 2 “Nitakufanya taifa kubwa \q2 na nitakubariki, \q1 Nitalikuza jina lako, \q2 nawe utakuwa baraka. \q1 \v 3 Nitawabariki wale wanaokubariki, \q2 na yeyote akulaaniye nitamlaani; \q1 na kupitia kwako mataifa yote duniani \q2 yatabarikiwa.” \p \v 4 Hivyo Abramu akaondoka kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwambia; naye Lutu akaondoka pamoja naye. Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na umri wa miaka sabini na tano. \v 5 Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Lutu mwana wa ndugu yake, mali yote waliyokuwa nayo, pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri kwenda nchi ya Kanaani, na wakafika huko. \p \v 6 Abramu akasafiri katika nchi hiyo hadi huko Shekemu, mahali penye mwaloni wa More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo. \v 7 Mwenyezi Mungu akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapo akamjengea madhabahu Mwenyezi Mungu aliyekuwa amemtokea. \p \v 8 Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki mwa Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea Mwenyezi Mungu madhabahu na akaliitia jina la Mwenyezi Mungu. \p \v 9 Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu. \s1 Abramu akiwa Misri \p \v 10 Basi kulikuwa na njaa katika nchi hiyo, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali. \v 11 Alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. \v 12 Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Kisha wataniua, lakini wewe watakuacha hai. \v 13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yahifadhiwe kwa sababu yako.” \p \v 14 Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura. \v 15 Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akapelekwa kwa nyumba ya mfalme. \v 16 Kwa ajili ya Sarai, Farao akamtendea Abramu mema, naye Abramu akapata kondoo, ng’ombe, punda, ngamia, na watumishi wa kiume na wa kike. \p \v 17 Lakini Mwenyezi Mungu akamwadhibu Farao na nyumba yake kwa maradhi ya kufisha kwa sababu ya kumchukua Sarai, mke wa Abramu. \v 18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akamuuliza, “Umenifanyia nini? Kwa nini hukuniambia yeye ni mke wako? \v 19 Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!” \v 20 Kisha Farao akawapa watu wake amri kuhusu Abramu, wakamsindikiza pamoja na mke wake na kila alichokuwa nacho. \c 13 \s1 Abramu na Lutu watengana \p \v 1 Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho; pia Lutu akaenda pamoja naye. \v 2 Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu. \p \v 3 Kutoka Negebu, akasafiri sehemu mbalimbali hadi akafika Betheli, mahali ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai, \v 4 pale alipokuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la Mwenyezi Mungu. \p \v 5 Basi Lutu, aliyekuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na mifugo na mahema. \v 6 Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali yao. \v 7 Ukazuka ugomvi kati ya wafugaji wa wanyama wa Abramu na wale wa Lutu. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi pia waliishi katika nchi hiyo. \p \v 8 Hivyo Abramu akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu. \v 9 Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Ukielekea kushoto, nitaenda kulia; ukielekea kulia, mimi nitaenda kushoto.” \p \v 10 Lutu akatazama, akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya Mwenyezi Mungu, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla Mwenyezi Mungu hajaharibu Sodoma na Gomora.) \v 11 Hivyo Lutu akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana. \v 12 Abramu aliishi nchi ya Kanaani, naye Lutu akaishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma. \v 13 Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakitenda dhambi nyingi dhidi ya Mwenyezi Mungu. \p \v 14 Baada ya Lutu kuondoka, Mwenyezi Mungu akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. \v 15 Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. \v 16 Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo ikiwa kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. \v 17 Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” \p \v 18 Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni. Naye akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu huko. \c 14 \s1 Abramu amwokoa Lutu \p \v 1 Wakati huo Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu \v 2 walienda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari). \v 3 Wafalme wa kundi hili la pili waliunganisha majeshi yao katika Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi). \v 4 Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na mbili, lakini mwaka wa kumi na tatu wakaasi. \p \v 5 Mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walienda vitani na wakawashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu, \v 6 na Wahori katika nchi ya vilima ya Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa. \v 7 Kisha wakarudi, wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori walioishi Hasason-Tamari. \p \v 8 Ndipo mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu \v 9 dhidi ya Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari; yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. \v 10 Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani. \v 11 Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao. \v 12 Pia walimteka Lutu, mwana wa ndugu yake Abramu, pamoja na mali yake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma. \p \v 13 Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, ndugu ya Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu. \v 14 Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu mia tatu na kumi na nane (318) wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. \v 15 Wakati wa usiku, Abramu aliwapanga watu wake katika vikosi, wakawashambulia na kuwashinda, wakawafukuza hadi Hoba, kaskazini mwa Dameski. \v 16 Abramu akarudisha mali yote, na akamrudisha Lutu jamaa yake na mali yake, pamoja na wanawake na watu wengine. \p \v 17 Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme). \p \v 18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. \v 19 Naye akambariki Abramu, akisema, \q1 “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, \q2 Muumba wa mbingu na nchi. \q1 \v 20 Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana, \q2 ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.” \m Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu. \p \v 21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu, nawe uchukue hizo mali.” \p \v 22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa \v 23 kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’ \v 24 Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula, na sehemu ambayo ni fungu la watu walioenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.” \c 15 \s1 Agano la Mwenyezi Mungu na Abramu \p \v 1 Baada ya jambo hili, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Abramu katika maono, akaambiwa: \q1 “Usiogope, Abramu. \q2 Mimi ni ngao yako, \q2 na thawabu yako kubwa sana.” \p \v 2 Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina mtoto, na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” \v 3 Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.” \p \v 4 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu lilipomjia, likanena: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.” \v 5 Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.” \p \v 6 Abramu akamwamini Mwenyezi Mungu, naye kwake jambo hili likahesabiwa kuwa haki. \p \v 7 Pia akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, niliyekutoa Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.” \p \v 8 Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitaimiliki?” \p \v 9 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia, “Niletee ndama jike, mbuzi, na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.” \p \v 10 Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege hakuwapasua vipande viwili. \v 11 Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza. \p \v 12 Jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, na giza nene na la kutisha likaja juu yake. \v 13 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni katika nchi isiyo yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. \v 14 Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi. \v 15 Wewe hata hivyo utaenda kwa baba zako kwa amani, na kuzikwa katika uzee mwema. \v 16 Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana uovu wa Waamori bado haujafikia kipimo.” \p \v 17 Jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama. \v 18 Siku hiyo Mwenyezi Mungu akafanya agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri\f + \fr 15:18 \fr*\fq Kijito cha Misri \fq*\ft ina maana \ft*\fqa Wadi-el-Arish \fqa*\ft kwenye mpaka wa kusini wa Yuda.\ft*\f* hadi mto ule mkubwa, Frati: \v 19 yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, \v 20 Wahiti, Waperizi, Warefai, \v 21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.” \c 16 \s1 Hajiri na Ishmaeli \p \v 1 Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mjakazi Mmisri jina lake Hajiri. \v 2 Hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Mwenyezi Mungu amenizuilia kupata watoto. Basi nenda ukutane kimwili na mjakazi wangu; huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” \p Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. \v 3 Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mjakazi wake Mmisri aliyeitwa Hajiri, na kumpa mumewe awe mke wake. \v 4 Abramu akakutana kimwili na Hajiri, naye akapata mimba. \p Hajiri alipojua kuwa ana mimba, akaanza kumdharau Sarai. \v 5 Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na mateso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mkononi mwako. Sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Mwenyezi Mungu na aamue kati yako na mimi!” \p \v 6 Abramu akamwambia, “Haya, mtumishi wako yuko mkononi mwako. Mtendee lolote utakalo!” Ndipo Sarai akamtesa Hajiri, naye akamtoroka. \p \v 7 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamkuta Hajiri karibu na chemchemi huko jangwani; chemchemi hiyo ilikuwa kando ya barabara iendayo Shuri. \v 8 Malaika akamwambia, “Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi, na unaenda wapi?” \p Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.” \p \v 9 Ndipo malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” \v 10 Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.” \p \v 11 Pia malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia: \q1 “Wewe sasa una mimba \q2 nawe utamzaa mwana. \q1 Utamwita jina lake Ishmaeli\f + \fr 16:11 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mungu husikia\fqa*\f*, \q2 kwa sababu Mwenyezi Mungu amesikia kuhusu huzuni yako. \q1 \v 12 Atakuwa kama punda-mwitu kati ya wanadamu; \q2 mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu, \q2 na mkono wa kila mtu utakuwa dhidi yake, \q1 naye ataishi kwa uhasama \q2 na ndugu zake wote.” \p \v 13 Hajiri akampa Mwenyezi Mungu aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.” \v 14 Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi\f + \fr 16:14 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Yeye Aliye Hai Anionaye\fqa*\f*; bado kipo hata leo kati ya Kadeshi na Beredi. \p \v 15 Hivyo Hajiri akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hajiri aliyemzalia jina la Ishmaeli. \v 16 Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita Hajiri alipomzalia Ishmaeli. \c 17 \s1 Agano la Tohara \p \v 1 Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi Mungu akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi\f + \fr 17:1 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f*; nenda mbele zangu na uishi kwa unyofu. \v 2 Nitafanya agano kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana.” \p \v 3 Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, \v 4 “Kwangu mimi, hili ndilo agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. \v 5 Hutaitwa tena Abramu\f + \fr 17:5 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Baba aliyetukuka\fqa*\f*, bali jina lako litakuwa Ibrahimu\f + \fr 17:5 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Baba wa wengi\fqa*\f*, kwa maana nimekufanya baba wa mataifa mengi. \v 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana; kwako yatatoka mataifa, na wafalme watatoka kwako. \v 7 Nitalithibitisha agano langu kama agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo, nami nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazao wako. \v 8 Nchi yote ya Kanaani, unayoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na ya uzao wako; nami nitakuwa Mungu wao.” \p \v 9 Ndipo Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwako wewe, lazima ushike agano langu, wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo. \v 10 Hili ni agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. \v 11 Mtatahiriwa, na hii itakuwa ni alama ya agano kati yangu na ninyi. \v 12 Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio wa uzao wako. \v 13 Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima atahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni agano la milele. \v 14 Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.” \p \v 15 Pia Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai, bali jina lake litakuwa Sara. \v 16 Nitambariki, na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki ili awe mama wa mataifa; wafalme wa mataifa watatoka kwake.” \p \v 17 Ibrahimu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” \v 18 Ibrahimu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!” \p \v 19 Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaka.\f + \fr 17:19 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Anacheka\fqa*\f* Nitalithibitisha agano langu naye kama agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. \v 20 Kuhusu Ishmaeli, nimekusikia. Hakika nitambariki; nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. \v 21 Lakini agano langu nitalithibitisha kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” \v 22 Alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, Mungu akaondoka kwa Ibrahimu. \p \v 23 Siku hiyo hiyo, Ibrahimu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake, pamoja na wale walionunuliwa kwa fedha zake; kila mwanaume wa nyumbani mwake akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. \v 24 Ibrahimu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa; \v 25 naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na tatu. \v 26 Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku hiyo hiyo. \v 27 Wanaume wote nyumbani mwa Ibrahimu, waliozaliwa nyumbani mwake na walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa wageni, walitahiriwa pamoja naye. \c 18 \s1 Wageni watatu \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. \v 2 Ibrahimu akainua macho, akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, akaharakisha kutoka ingilio la hema lake, akawalaki na kusujudu hadi chini. \p \v 3 Ibrahimu akasema, “Bwana wangu, ikiwa nimepata kibali machoni mwako, usimpite mtumishi wako. \v 4 Acha yaletwe maji kidogo, nanyi mnawe miguu yenu, na mpumzike chini ya mti huu. \v 5 Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.” \p Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.” \p \v 6 Hivyo Ibrahimu akaharakisha akaingia kwenye hema kwa Sara, akamwambia, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.” \p \v 7 Kisha Ibrahimu akakimbia kwenye kundi, akachagua ndama mzuri laini, na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha. \v 8 Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti. \p \v 9 Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?” \p Akasema, “Yuko ndani ya hema.” \p \v 10 Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Hakika nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, na Sara mkeo atakuwa na mwana.” \p Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema lililokuwa nyuma ya Ibrahimu. \v 11 Ibrahimu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amepita umri wa kuzaa mtoto. \v 12 Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?” \p \v 13 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ \v 14 Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Mwenyezi Mungu? Nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, naye Sara atakuwa na mwana.” \p \v 15 Sara akaogopa, hivyo akadanganya na kusema, “Mimi sikucheka.” \p Lakini Mwenyezi Mungu akasema, “Ndiyo, ulicheka!” \s1 Ibrahimu aiombea Sodoma \p \v 16 Watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, naye Ibrahimu akatembea nao ili awasindikize. \v 17 Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Je, nimfiche Ibrahimu jambo ninalokusudia kufanya? \v 18 Hakika Ibrahimu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa. \v 19 Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Mwenyezi Mungu atimize ahadi yake kwa Ibrahimu.” \p \v 20 Basi Mwenyezi Mungu akamwambia Ibrahimu, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi zao zinanisikitisha sana, \v 21 hivyo nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.” \p \v 22 Basi wale watu wakageuka, wakaelekea Sodoma, lakini Ibrahimu akabaki amesimama mbele za Mwenyezi Mungu. \v 23 Ibrahimu akamsogelea, akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu? \v 24 Je, ikiwa watakuwepo watu hamsini wenye haki katika mji huo, kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo? \v 25 Na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo: kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Liwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya haki?” \p \v 26 Mwenyezi Mungu akajibu, “Nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitauacha huo mji wote kwa ajili yao.” \p \v 27 Kisha Ibrahimu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu. \v 28 Je, kama hesabu ya wenye haki imepungua watano katika hamsini, utauangamiza huo mji wote kwa ajili ya hao watano waliopungua?” \p Bwana akamjibu, “Nikiwakuta huko watu arobaini na watano, sitauangamiza.” \p \v 29 Ibrahimu akazungumza naye kwa mara nyingine, “Je, kama huko watapatikana watu arobaini tu?” \p Akamjibu, “Kwa ajili ya hao arobaini, sitauangamiza.” \p \v 30 Ndipo akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze. Je, kama huko watakuwepo thelathini tu?” \p Akajibu, “Sitauangamiza ikiwa nitawakuta huko watu thelathini.” \p \v 31 Ibrahimu akasema, “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri sana kuzungumza na Bwana, je, wakipatikana huko watu ishirini tu?” \p Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao ishirini, sitauangamiza.” \p \v 32 Ibrahimu akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze tena mara moja tu. Itakuwaje kama watapatikana huko watu kumi tu?” \p Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao kumi, sitauangamiza.” \p \v 33 Mwenyezi Mungu alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, akaondoka, naye Ibrahimu akarudi nyumbani. \c 19 \s1 Kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora \p \v 1 Malaika wale wawili walifika Sodoma wakati wa jioni, naye Lutu alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Alipowaona, alienda kuwalaki, akasujudu, uso wake ukagusa chini. \v 2 Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa, kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari yenu.” \p Wakamjibu, “La, tutalala hapa uwanjani.” \p \v 3 Lakini aliwasihi sana hadi wakaingia nyumbani mwake. Akawaandalia chakula, mikate isiyotiwa chachu, nao wakala. \v 4 Kabla hawajaenda kulala, wanaume wote kutoka kila sehemu ya mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba. \v 5 Wakamwita Lutu wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuwalawiti.” \p \v 6 Lutu akatoka nje kuongea nao, akaufunga mlango nyuma yake. \v 7 Akawaambia, “La hasha, rafiki zangu! Msifanye jambo hili ovu. \v 8 Tazama, ninao binti zangu wawili ambao ni bikira. Acha niwatoe kwenu, nanyi mnaweza kuwafanyia lolote mnalotaka. Lakini msiwafanyie chochote wanaume hawa, kwa sababu wako chini ya ulinzi wa dari langu.” \p \v 9 Wakamjibu, “Tuondokee mbali!” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Lutu na kuusogelea mlango ili kuuvunja. \p \v 10 Lakini wanaume wale waliokuwa ndani wakanyoosha mikono yao, wakamvuta Lutu ndani ya nyumba na kuufunga mlango. \v 11 Kisha wakawapiga kwa upofu wale wanaume waliokuwa mlangoni mwa ile nyumba, vijana kwa wazee, hivyo hawakuweza kuupata mlango. \p \v 12 Wale wanaume wawili wakamwambia Lutu, “Una mtu mwingine yeyote hapa: wakwe, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa, \v 13 kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.” \p \v 14 Kwa hiyo Lutu alitoka ili kuzungumza na wakwe wake waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe wake walifikiri kwamba alikuwa akitania. \p \v 15 Kulipopambazuka, malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walio huku, la sivyo utaangamizwa mji huu utakapoadhibiwa.” \p \v 16 Alipositasita, wale wanaume wakamshika mkono wake, na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwahurumia. \v 17 Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!” \p \v 18 Lakini Lutu akawajibu, “La hasha, bwana zangu, tafadhalini! \v 19 Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani; janga hili litanikumba, nami nitakufa. \v 20 Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo: Ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.” \p \v 21 Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja. \v 22 Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote hadi ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari\f + \fr 19:22 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mdogo\fqa*\f*.) \p \v 23 Lutu alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi. \v 24 Ndipo Mwenyezi Mungu akanyesha moto wa kiberiti juu ya Sodoma na Gomora kutoka kwake Mwenyezi Mungu mbinguni. \v 25 Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote walioishi katika miji hiyo, hata pia mimea yote katika nchi. \v 26 Lakini mke wa Lutu akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi. \p \v 27 Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Ibrahimu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za Mwenyezi Mungu. \v 28 Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka nchi, kama moshi unaotoka katika tanuru. \p \v 29 Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare, alimkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu kutoka lile janga lililoharibu miji ile ambamo Lutu alikuwa ameishi. \s1 Lutu na binti zake \p \v 30 Lutu na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango. \v 31 Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani. \v 32 Tumnyweshe baba yetu mvinyo, kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” \p \v 33 Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo; alipolewa, binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka. \p \v 34 Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” \v 35 Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka. \p \v 36 Hivyo binti wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. \v 37 Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina Moabu\f + \fr 19:37 \fr*\ft Kiebrania ni kama kusema \ft*\fqa Kutoka kwa baba.\fqa*\f*; ndiye baba wa Wamoabu hata leo. \v 38 Binti mdogo pia akamzaa mwana, naye akamwita jina Benami\f + \fr 19:38 \fr*\ft Kiebrania ni kama kusema \ft*\fqa Mwana wa jamaa ya baba.\fqa*\f*; ndiye baba wa Waamoni hata leo. \c 20 \s1 Ibrahimu na Abimeleki \p \v 1 Basi Ibrahimu akaondoka huko akaenda hadi nchi ya Negebu, akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari. \v 2 Huko Ibrahimu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akaagiza Sara aletwe, naye akamchukua awe mkewe. \p \v 3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.” \p \v 4 Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? \v 5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu’; naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri safi na mikono safi.” \p \v 6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto ile, “Ndiyo, najua kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. \v 7 Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa.” \p \v 8 Kesho yake asubuhi na mapema, Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotukia, waliogopa sana. \v 9 Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii kwangu na kwa ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.” \v 10 Abimeleki akamuuliza Ibrahimu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?” \p \v 11 Ibrahimu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ \v 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti ya baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. \v 13 Mungu aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapoenda, sema hivi kunihusu, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ” \p \v 14 Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ng’ombe, na watumwa wa kiume na wa kike, akampa Ibrahimu, na akamrudisha Sara kwa mumewe. \v 15 Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako; ishi popote unapotaka.” \p \v 16 Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.” \p \v 17 Kisha Ibrahimu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na wajakazi wake ili waweze kupata watoto tena, \v 18 kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa amefunga tumbo za wanawake wote wa nyumba ya Abimeleki kwa sababu ya Sara, mke wa Ibrahimu. \c 21 \s1 Kuzaliwa kwa Isaka \p \v 1 Wakati huu Mwenyezi Mungu akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, na Mwenyezi Mungu akamtendea Sara kama alivyoahidi. \v 2 Sara akapata mimba, na akamzalia Ibrahimu mwana katika uzee wake, katika majira yale Mungu alikuwa amemwahidi. \v 3 Ibrahimu akampa huyo mwana ambaye Sara alimzalia jina Isaka\f + \fr 21:3 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kicheko \fqa*\ft au \ft*\fqa Anacheka\fqa*\f*. \v 4 Isaka alipokuwa na umri wa siku nane, Ibrahimu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. \v 5 Ibrahimu alikuwa na umri wa miaka mia moja Isaka mwanawe alipozaliwa. \p \v 6 Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, na kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” \v 7 Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Ibrahimu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Lakini nimemzalia mwana katika uzee wake.” \s1 Hajiri na Ishmaeli wafukuzwa \p \v 8 Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya. Siku ile Isaka aliyoachishwa kunyonya, Ibrahimu alifanya sherehe kubwa. \v 9 Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hajiri Mmisri alimzalia Ibrahimu alikuwa anadhihaki. \v 10 Hivyo Sara akamwambia Ibrahimu, “Mwondoe mjakazi huyu mtumwa pamoja na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mjakazi huyo kamwe hatarithi na mwanangu Isaka.” \p \v 11 Jambo hili lilimhuzunisha sana Ibrahimu kwa sababu lilimhusu mwanawe. \v 12 Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana huyo na mjakazi wako. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaka. \v 13 Nitamfanya huyu mwana wa mjakazi wako kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.” \p \v 14 Kesho yake asubuhi na mapema, Ibrahimu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hajiri. Akaviweka begani mwa Hajiri, akamwondoa pamoja na kijana. Hajiri akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba. \p \v 15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, Hajiri akamwacha kijana chini ya kichaka. \v 16 Kisha akaenda akaketi kama umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Akiwa ameketi pale, akaanza kulia kwa huzuni. \p \v 17 Mungu akamsikia kijana akilia. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini, Hajiri? Usiogope, Mungu amesikia kijana akilia akiwa amelala pale. \v 18 Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.” \p \v 19 Ndipo Mungu akamfumbua Hajiri macho, akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe. \p \v 20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde. \v 21 Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akamtwalia mke kutoka Misri. \s1 Mapatano katika Beer-Sheba \p \v 22 Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Ibrahimu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. \v 23 Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.” \p \v 24 Ibrahimu akasema, “Ninaapa hivyo.” \p \v 25 Ndipo Ibrahimu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamemnyang’anya. \v 26 Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ametenda hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.” \p \v 27 Hivyo Ibrahimu akaleta kondoo na ng’ombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. \v 28 Ibrahimu akatenga kondoo jike saba kutoka kwa kundi. \v 29 Abimeleki akamuuliza Ibrahimu, “Ni nini maana ya hawa kondoo jike saba uliowatenga peke yao?” \p \v 30 Ibrahimu akamjibu, “Pokea hawa kondoo jike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.” \p \v 31 Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu hao wawili waliapiana hapo. \p \v 32 Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi nchi ya Wafilisti. \v 33 Ibrahimu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa milele. \v 34 Naye Ibrahimu akakaa nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu. \c 22 \s1 Kujua uthabiti wa Ibrahimu \p \v 1 Baadaye Mungu akamjaribu Ibrahimu. Akamwambia, “Ibrahimu!” \p Ibrahimu akamjibu, “Mimi hapa.” \p \v 2 Kisha Mungu akamwambia, “Mchukue mwanao, mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, uende nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima nitakaokuambia.” \p \v 3 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. \v 4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. \v 5 Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunaenda kule. Tutaabudu na kisha tutawarudia.” \p \v 6 Ibrahimu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaka mwanawe, naye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, \v 7 Isaka akamwambia Ibrahimu baba yake, “Baba yangu!” \p Ibrahimu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.” \p Isaka akasema, “Moto na kuni zipo. Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?” \p \v 8 Ibrahimu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja. \p \v 9 Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaka mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. \v 10 Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. \v 11 Lakini malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Ibrahimu! Ibrahimu!” \p Akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 12 Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.” \p \v 13 Ibrahimu akainua macho, akaona nyuma yake kondoo dume akiwa amenaswa pembe zake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. \v 14 Ibrahimu akapaita mahali pale Yehova-Yire.\f + \fr 22:14 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwenyezi Mungu atapata\fqa*\f* Hadi leo inasemekana, “Katika mlima wa Mwenyezi Mungu itapatikana.” \p \v 15 Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita Ibrahimu kutoka mbinguni mara ya pili, \v 16 akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Mwenyezi Mungu, kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee: \v 17 Hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga wa pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, \v 18 na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.” \p \v 19 Ndipo Ibrahimu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wote, wakaenda hadi Beer-Sheba. Naye Ibrahimu akaishi huko Beer-Sheba. \s1 Wana wa Nahori \li1 \v 20 Baada ya muda, Ibrahimu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto; amemzalia ndugu yako Nahori wana: \li2 \v 21 Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, \li2 Kemueli (baba wa Aramu), \li2 \v 22 Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” \li3 \v 23 Bethueli akamzaa Rebeka. \lf Milka alimzalia Nahori nduguye Ibrahimu hao wana wanane. \b \li1 \v 24 Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alizaa wana: \li2 Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka. \c 23 \s1 Kifo cha Sara \p \v 1 Sara aliishi miaka mia moja na ishirini na saba (127). \v 2 Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, naye Ibrahimu akalia na kumwomboleza Sara. \p \v 3 Ndipo Ibrahimu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema, \v 4 “Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.” \p \v 5 Wahiti wakamjibu Ibrahimu, \v 6 “Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.” \p \v 7 Ibrahimu akainuka, akasujudu mbele ya Wahiti, wenyeji wa nchi hiyo. \v 8 Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni, mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu \v 9 ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.” \p \v 10 Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake; akamjibu Ibrahimu mbele ya Wahiti wote waliokuwa katika lango la mji: \v 11 “La, bwana wangu, nisikilize. Nakupa shamba, na pia nakupa pango lililo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu, uzike maiti wako.” \p \v 12 Ibrahimu akasujudu tena mbele ya wenyeji wa nchi, \v 13 akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.” \p \v 14 Efroni akamjibu Ibrahimu, \v 15 “Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli mia nne za fedha\f + \fr 23:15 \fr*\ft Shekeli 400 za fedha ni sawa na kilo 4.5.\ft*\f*, lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.” \p \v 16 Ibrahimu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: shekeli mia nne za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara. \p \v 17 Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwa ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa \v 18 kwa Ibrahimu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji. \v 19 Baada ya hayo Ibrahimu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani. \v 20 Hivyo Wahiti wakamkabidhi Ibrahimu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia. \c 24 \s1 Isaka na Rebeka \p \v 1 Wakati huu Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, naye Mwenyezi Mungu alikuwa amembariki katika mambo yote. \v 2 Ibrahimu akamwambia mtumishi wake mkuu katika nyumba yake, aliyekuwa msimamizi wa mali yake yote, “Weka mkono wako chini ya paja langu. \v 3 Ninataka uape kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao. \v 4 Bali nenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaka mwanangu mke.” \p \v 5 Yule mtumishi akamuuliza, “Je, itakuwaje huyo mwanamke akikataa kuja nami katika nchi hii? Je, nimrudishe mwanao katika hiyo nchi uliyotoka?” \p \v 6 Ibrahimu akasema, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu huko. \v 7 Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbingu, alinitoa nyumbani mwa baba yangu na nchi yangu niliyozaliwa. Ndiye alisema nami na akaniahidi kwa kiapo, akasema, ‘Nitawapa uzao wako nchi hii.’ Yeye atatuma malaika wake akutangulie ili umtwalie mwanangu mke kutoka huko. \v 8 Huyo mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi utafunguliwa kutoka kiapo nilichokuapisha. Ila usimrudishe mwanangu huko.” \v 9 Basi yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la bwana wake Ibrahimu, akamwapia kuhusu shauri hili. \p \v 10 Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia wa bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Mesopotamia, akaenda hadi mji wa Nahori. \v 11 Akawapigisha ngamia magoti karibu na kisima cha maji nje ya mji; ilikuwa inaelekea jioni, wakati wanawake huteka maji. \p \v 12 Kisha akaomba, “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nipatie ushindi leo, uoneshe ukarimu kwa bwana wangu Ibrahimu. \v 13 Tazama, nimesimama karibu na kisima hiki cha maji, nao binti za watu wa mji huu wanakuja kuteka maji. \v 14 Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmoja, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji’; naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia’: basi na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka. Kwa hili nitajua umemtendea bwana wangu ukarimu.” \p \v 15 Ikawa kabla hajamaliza kuomba, Rebeka akatokea akiwa na mtungi begani mwake. Alikuwa binti Bethueli. Bethueli alikuwa mwana wa Milka, aliyekuwa mke wa Nahori ndugu wa Ibrahimu. \v 16 Huyu msichana alikuwa mzuri sana wa sura, bikira, ambaye hakuna mwanaume aliyekuwa amekutana naye kimwili. Aliteremka kisimani, akajaza mtungi wake, tena akapanda juu. \p \v 17 Ndipo yule mtumishi akaharakisha kukutana naye, akamwambia, “Tafadhali nipe maji kidogo katika mtungi wako.” \p \v 18 Yule msichana akasema, “Kunywa, bwana wangu.” Akashusha kwa haraka mtungi mkononi mwake na akampa, akanywa. \p \v 19 Baada ya kumpa yule mtumishi yale maji, akamwambia, “Nitawatekea ngamia wako maji pia hadi wote watosheke.” \v 20 Akafanya haraka kumimina maji kwenye birika ya kunyweshea wanyama, akakimbia kisimani kuteka maji mengine, na akateka ya kuwatosha ngamia wake wote. \v 21 Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama Mwenyezi Mungu ameifanikisha safari yake, au la. \p \v 22 Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja\f + \fr 24:22 \fr*\ft Beka moja ya dhahabu ni sawa na gramu 5.5.\ft*\f*, na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi\f + \fr 24:22 \fr*\ft Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110.\ft*\f*. \v 23 Kisha akamuuliza, “Wewe ni binti ya nani? Tafadhali niambie. Je, kuna nafasi katika nyumba ya baba yako tunapoweza kulala?” \p \v 24 Yule msichana akamjibu, “Mimi ni binti ya Bethueli, mwana wa Milka aliyemzalia Nahori.” \v 25 Akaendelea kusema, “Kwetu kuna majani mengi na malisho, tena kuna nafasi kwa ajili yenu kulala.” \p \v 26 Yule mtumishi akasujudu na kumwabudu Mwenyezi Mungu, \v 27 akisema, “Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami, Mwenyezi Mungu ameniongoza safarini, akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu.” \p \v 28 Yule msichana akakimbia, akawaeleza watu wa nyumbani mwa mama yake kuhusu mambo haya. \v 29 Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani; huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani. \v 30 Mara alipoiona ile pete puani, na bangili mikononi mwa dada yake, na kusikia yale maneno Rebeka aliyoambiwa na huyo mtumishi, alimwendea huyo mtumishi, akamkuta amesimama karibu na ngamia wake pale karibu na kisima. \v 31 Akamwambia, “Karibu nyumbani wewe uliyebarikiwa na Mwenyezi Mungu. Kwa nini unasimama huko nje? Mimi nimekuandalia nyumba na mahali kwa ajili ya ngamia.” \p \v 32 Hivyo yule mtumishi akaingia nyumbani, nayo mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia, na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu. \v 33 Ndipo chakula kikaandaliwa kwa ajili yake, lakini akasema, “Sitakula hadi niwe nimewaambia yale niliyo nayo ya kusema.” \p Labani akasema, “Basi tuambie.” \p \v 34 Hivyo akasema, “Mimi ni mtumishi wa Ibrahimu. \v 35 Mwenyezi Mungu amembariki sana bwana wangu, amekuwa tajiri. Amempa kondoo na ng’ombe, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda. \v 36 Sara mkewe bwana wangu amemzalia mwana katika uzee wake, naye amempa kila kitu alichokuwa nacho. \v 37 Naye bwana wangu ameniapisha na akasema, ‘Kamwe usimtwalie mwanangu mke katika binti za Wakanaani, ambao ninaishi katika nchi yao, \v 38 ila uende hadi kwa jamaa ya baba yangu na ukoo wangu mwenyewe, ukamtwalie mwanangu mke huko.’ \p \v 39 “Kisha nikamuuliza bwana wangu, ‘Je, kama huyo mwanamke hatakubali kurudi nami?’ \p \v 40 “Akanijibu, ‘Mwenyezi Mungu, ambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka jamaa ya baba yangu. \v 41 Kisha, utakapoenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu. Hata wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’ \p \v 42 “Nilipokuja kisimani leo nilisema, ‘Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ikikupendeza, naomba uifanikishe safari niliyoijia. \v 43 Tazama, ninasimama kando ya kisima hiki. Mwanamwali akija kuteka maji, nami nikimwambia: Tafadhali niruhusu ninywe maji kidogo kutoka mtungi wako. \v 44 Naye akiniambia, “Kunywa, nami nitawatekea ngamia wako maji pia,” basi huyo awe ndiye mke Mwenyezi Mungu amemchagulia mwana wa bwana wangu.’ \p \v 45 “Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani, akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ninywe.’ \p \v 46 “Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa, na nitawanywesha ngamia wako pia.’ Basi nikanywa, naye akawanywesha na ngamia pia. \p \v 47 “Nikamuuliza, ‘Wewe ni binti ya nani?’ \p “Akasema, ‘Mimi ni binti ya Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia.’ \p “Ndipo nilipotia pete puani mwake na bangili mikononi mwake, \v 48 nikasujudu na nikamwabudu Mwenyezi Mungu. Nikamtukuza Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake. \v 49 Ikiwa mtaonesha wema na uaminifu kwa bwana wangu, mniambie; la sivyo, mniambie, ili niweze kujua njia ya kugeukia.” \p \v 50 Labani na Bethueli wakajibu, “Jambo hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu; hatuwezi kukuambia jambo lolote baya au jema. \v 51 Rebeka yuko hapa, mchukue na uende, awe mke wa mwana wa bwana wako, sawasawa na Mwenyezi Mungu alivyoongoza.” \p \v 52 Ikawa huyo mtumishi wa Ibrahimu aliposikia waliyosema, alisujudu, uso wake ukagusa chini mbele za Mwenyezi Mungu. \v 53 Ndipo huyo mtumishi akatoa vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kwa fedha, pamoja na mavazi, akampa Rebeka; pia akawapa zawadi za thamani kubwa nduguye na mamaye. \v 54 Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala palepale. \p Walipoamka asubuhi, yule mtumishi akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.” \p \v 55 Lakini ndugu yake Rebeka pamoja na mama yake wakajibu, “Acha binti akae kwetu siku kumi au zaidi, ndipo mwondoke.” \p \v 56 Lakini yule mtumishi akawaambia, “Msinicheleweshe, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amefanikisha safari yangu. Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.” \p \v 57 Ndipo wakasema, “Acha tumwite huyo binti tumuulize, tusikie atakavyosema.” \v 58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je, utaenda na mtu huyu?” \p Akasema, “Nitaenda.” \p \v 59 Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, na mtumishi wa Ibrahimu na watu wake. \v 60 Wakambariki Rebeka, wakamwambia, \q1 “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, \q2 mara elfu nyingi; \q1 nao wazao wako wamiliki \q2 malango ya adui zao.” \p \v 61 Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia wao, wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka, wakaondoka. \p \v 62 Basi Isaka alikuwa ametoka Beer-Lahai-Roi, kwa kuwa alikuwa akiishi nchi ya Negebu. \v 63 Isaka akaenda shambani kutafakari wakati wa jioni; alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja. \v 64 Rebeka pia akainua macho, akamwona Isaka. Akashuka kutoka ngamia wake, \v 65 akamuuliza yule mtumishi, “Ni nani mtu yule kule shambani anayekuja kutulaki?” \p Yule mtumishi akajibu, “Huyu ndiye bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake, akajifunika. \p \v 66 Kisha yule mtumishi akamweleza Isaka mambo yote aliyoyatenda. \v 67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake. Isaka akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaka akampenda; akafarijika baada ya kifo cha mama yake. \c 25 \s1 Kifo cha Ibrahimu \p \v 1 Ibrahimu alioa mke mwingine aliyeitwa Ketura. \v 2 Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. \v 3 Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani; wazao wa Dedani walikuwa Waashuru, Waletushi na Waleumi. \v 4 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura. \p \v 5 Ibrahimu akamwachia Isaka kila kitu alichokuwa nacho. \v 6 Lakini Ibrahimu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaka. \p \v 7 Kwa jumla, Ibrahimu aliishi miaka mia moja na sabini na tano (175). \v 8 Ndipo Ibrahimu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku; naye akakusanywa pamoja na watu wake. \v 9 Watoto wake Isaka na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, \v 10 shamba ambalo Ibrahimu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Ibrahimu alipozikwa pamoja na mkewe Sara. \v 11 Baada ya kifo cha Ibrahimu, Mungu akambariki mwanawe Isaka, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi. \s1 Wana wa Ishmaeli \p \v 12 Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ambaye Hajiri Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Ibrahimu. \b \lh \v 13 Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, walioorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: \b \li1 Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, \li1 akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu, \li1 \v 14 Mishma, Duma, Masa, \li1 \v 15 Hadadi, Tema, Yeturi, \li1 Nafishi na Kedema. \b \lf \v 16 Hawa walikuwa wana wa Ishmaeli, na haya ni majina ya viongozi wa makabila yao kumi na mbili, kufuatana na makazi yao na kambi zao. \b \p \v 17 Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba (137). Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake. \v 18 Wazao wa Ishmaeli waliishi kuanzia nchi ya Havila hadi Shuri, karibu na mpaka wa Misri, kuelekea Ashuru. Hao waliishi kwa uhasama na ndugu zao wote. \s1 Yakobo na Esau \p \v 19 Hivi ndivyo vizazi vya Isaka mwana wa Ibrahimu. \b \p Ibrahimu akamzaa Isaka. \v 20 Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu\f + \fr 25:20 \fr*\ft au \ft*\fqa Mshami\fqa*\f* kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu. \p \v 21 Isaka akamwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Mwenyezi Mungu akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. \v 22 Watoto wakashindana tumboni mwake, naye akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Mwenyezi Mungu. \p \v 23 Mwenyezi Mungu akamjibu, \q1 “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, \q2 na mataifa hayo mawili \q2 kutoka ndani yako watatenganishwa. \q1 Mmoja atakuwa na nguvu kuliko mwingine, \q2 na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.” \p \v 24 Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. \v 25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, na mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina Esau\f + \fr 25:25 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwenye nywele nyingi\fqa*\f*. \v 26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina Yakobo\f + \fr 25:26 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Ashikaye kisigino\fqa*\ft , au \ft*\fqa Atwaaye mahali pa mwingine\fqa*\ft , au \ft*\fqa Mdanganyaji\fqa*\f*. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini Rebeka alipowazaa. \p \v 27 Watoto wakakua. Esau akawa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, naye Yakobo akawa mtu mtulivu, mwenye kukaa nyumbani. \v 28 Isaka, aliyekuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo. \p \v 29 Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu. Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali. \v 30 Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu\f + \fr 25:30 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwekundu\fqa*\f*.) \p \v 31 Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” \p \v 32 Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?” \p \v 33 Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. \p \v 34 Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu, naye akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake. \p Kwa hiyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza. \c 26 \s1 Isaka na Abimeleki \p \v 1 Basi njaa kubwa ikatokea katika nchi hiyo, mbali na njaa iliyotokea wakati wa Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. \v 2 Mwenyezi Mungu akamtokea Isaka, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. \v 3 Kaa katika nchi hii kwa kitambo; mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote, na nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. \v 4 Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote, na kupitia uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, \v 5 kwa sababu Ibrahimu alinitii mimi, na akatenda yote niliyomwagiza, akahifadhi amri zangu, na hukumu zangu, pamoja na sheria zangu.” \v 6 Hivyo Isaka akaishi huko Gerari. \p \v 7 Wanaume wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Wanaume wa huku wanaweza kuniua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa sura.” \p \v 8 Isaka alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake. \v 9 Abimeleki akamwita Isaka, akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu’?” \p Isaka akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.” \p \v 10 Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotutendea? Ingewezekana mtu yeyote akakutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia kwetu.” \p \v 11 Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.” \p \v 12 Isaka akapanda mazao katika nchi hiyo, na kwa mwaka huo huo akavuna mara mia, kwa sababu Mwenyezi Mungu alimbariki. \v 13 Isaka akawa tajiri, nayo mali yake ikaendelea kuongezeka hata akawa tajiri sana. \v 14 Akawa na mifugo ya kondoo na ng’ombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu. \v 15 Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Ibrahimu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo. \p \v 16 Ndipo Abimeleki akamwambia Isaka, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.” \p \v 17 Basi Isaka akatoka huko, akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. \v 18 Ndipo Isaka akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Ibrahimu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya Ibrahimu kufa, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa. \p \v 19 Watumishi wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakagundua huko kisima chenye maji safi. \v 20 Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki\f + \fr 26:20 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Ugomvi\fqa*\f*, kwa sababu waligombana naye. \v 21 Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania; akakiita Sitna\f + \fr 26:21 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Upinzani\fqa*\f*. \v 22 Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi\f + \fr 26:22 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mungu ametufanyia nafasi\fqa*\f*, akisema, “Sasa Mwenyezi Mungu ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.” \p \v 23 Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. \v 24 Usiku ule Mwenyezi Mungu akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe. Nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.” \p \v 25 Isaka akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Mwenyezi Mungu. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima. \p \v 26 Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake. \v 27 Isaka akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu, na ninyi mlinichukia na kunifukuza?” \p \v 28 Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu,’ yaani kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe, \v 29 kwamba hutatudhuru, kama vile nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote, na tukawaaga kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Mwenyezi Mungu.” \p \v 30 Basi Isaka akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. \v 31 Kesho yake asubuhi na mapema wakaapiana. Kisha Isaka akawaruhusu waende zao, wakamwacha kwa amani. \p \v 32 Siku hiyo watumishi wa Isaka wakaja, wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!” \v 33 Naye akakiita Shiba\f + \fr 26:33 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Saba \fqa*\ft au \ft*\fqa Kiapo\fqa*\f*; hadi leo mji huo unaitwa Beer-Sheba\f + \fr 26:33 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kisima cha saba \fqa*\ft au \ft*\fqa Kisima cha kiapo\fqa*\f*. \p \v 34 Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti. \v 35 Hawa walikuwa chanzo cha huzuni kwa Isaka na Rebeka. \c 27 \s1 Isaka ambariki Yakobo \p \v 1 Isaka alipokuwa mzee na macho yake yakapofuka kwa kukosa nguvu, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” \p Akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 2 Isaka akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kufa kwangu. \v 3 Sasa basi chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukaniwindie mawindo. \v 4 Uniandalie chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili nikubariki kabla sijafa.” \p \v 5 Rebeka alikuwa akisikiliza Isaka akizungumza na mwanawe Esau. Basi Esau alipoenda nyikani kuwinda mawindo ayalete, \v 6 Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, \v 7 ‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili nikubariki mbele za Mwenyezi Mungu kabla sijafa.’ \v 8 Sasa mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: \v 9 Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili nimwandalie baba yako chakula kitamu kile anachokipenda. \v 10 Kisha umpelekee baba yako ale, ili akubariki kabla hajafa.” \p \v 11 Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Lakini ndugu yangu Esau ana nywele mwilini, nami nina ngozi nyororo. \v 12 Itakuwaje baba yangu akinigusa? Ataona kama ninamfanyia ujanja, nami nijiletee laana badala ya baraka.” \p \v 13 Mama yake akamwambia, “Mwanangu, laana na iwe juu yangu. Fanya tu ninalokuambia: nenda ukaniletee hao wana-mbuzi.” \p \v 14 Kwa hiyo alienda akawaleta, akampa mama yake, naye Rebeka akaandaa chakula kitamu, kile alichokipenda baba yake. \v 15 Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. \v 16 Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi. \v 17 Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka. \p \v 18 Yakobo akaenda kwa baba yake, akasema, “Baba yangu.” \p Akajibu, “Naam, mwanangu. Wewe ni nani?” \p \v 19 Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili unibariki.” \p \v 20 Isaka akamuuliza mwanawe, “Umepataje mawindo haraka hivi, mwanangu?” \p Akajibu, “Mwenyezi Mungu, Mungu wako, amenifanikisha.” \p \v 21 Kisha Isaka akamwambia Yakobo, “Mwanangu, tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.” \p \v 22 Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaka, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.” \v 23 Hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na nywele kama ya ndugu yake Esau, kwa hiyo akambariki. \v 24 Akamuuliza, “Kweli wewe ni mwanangu Esau?” \p Akajibu, “Ni mimi.” \p \v 25 Kisha Isaka akasema, “Mwanangu, niletee sehemu ya mawindo yako nile, ili nikubariki.” \p Yakobo akamletea, naye akala; kisha akamletea na divai akanywa. \v 26 Ndipo Isaka baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.” \p \v 27 Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaka aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema, \q1 “Aha, harufu ya mwanangu \q2 ni kama harufu ya shamba \q2 ambalo Mwenyezi Mungu amelibariki. \q1 \v 28 Mungu na akupe umande wa mbinguni \q2 na utajiri wa duniani: \q2 wingi wa nafaka na divai mpya. \q1 \v 29 Mataifa yakutumikie, \q2 na mataifa yakusujudie. \q1 Uwe bwana juu ya ndugu zako, \q2 na wana wa mama yako wakusujudie. \q1 Walaaniwe wale wanaokulaani, \q2 na wabarikiwe wale wanaokubariki.” \p \v 30 Baada ya Isaka kumbariki Yakobo, na punde tu alipoondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni. \v 31 Naye pia akaandaa chakula kitamu, akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.” \p \v 32 Isaka baba yake akamuuliza, “Wewe ni nani?” \p Akamjibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.” \p \v 33 Isaka akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!” \p \v 34 Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia kwa sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki! Nibariki mimi pia, baba yangu!” \p \v 35 Lakini akamjibu, “Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu, akachukua baraka yako.” \p \v 36 Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?” \p \v 37 Isaka akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako; pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, na nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?” \p \v 38 Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa. \p \v 39 Baba yake Isaka akamjibu, \q1 “Makao yako yatakuwa \q2 mbali na utajiri wa dunia, \q2 mbali na umande wa mbinguni. \q1 \v 40 Utaishi kwa upanga, \q2 nawe utamtumikia ndugu yako. \q1 Lakini utakapokuwa umejikomboa, \q2 utatupa nira yake \q2 kutoka shingoni mwako.” \p \v 41 Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia; ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.” \p \v 42 Rebeka alipoambiwa yale Esau mwanawe mkubwa aliyoyasema, akamtumania Yakobo mwanawe mdogo, akamwambia, “Ndugu yako Esau anajifariji kwa wazo la kukuua. \v 43 Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani. \v 44 Ukae naye kwa muda hadi ghadhabu ya ndugu yako itulie. \v 45 Ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze nyote wawili siku moja?” \p \v 46 Kisha Rebeka akamwambia Isaka, “Nimechukia maisha kwa sababu ya hawa wanawake Wahiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake Wahiti kama hawa, sitaona haja ya kuendelea kuishi.” \c 28 \s1 Yakobo akimbilia kwa Labani \p \v 1 Basi Isaka akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke Mkanaani. \v 2 Nenda mara moja hadi Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli, baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako. \v 3 Mungu Mwenyezi\f + \fr 28:3 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f* na akubariki, uwe na uzao, uongezeke idadi yako hadi upate kuwa jamii kubwa ya watu. \v 4 Akupe wewe na uzao wako baraka aliyopewa Ibrahimu, upate kumiliki nchi unayoishi sasa kama mgeni, nchi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu.” \v 5 Kisha Isaka akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu\f + \fr 28:5 \fr*\ft au \ft*\fqa Mshami\fqa*\f*, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau. \p \v 6 Basi Esau akajua kuwa Isaka amembariki Yakobo na kumtuma Padan-Aramu ili achukue mke huko, na kwamba alipombariki alimwamuru, akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,” \v 7 tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake, naye ameenda Padan-Aramu. \v 8 Esau akatambua jinsi baba yake Isaka alivyowachukia binti za Wakanaani. \v 9 Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti ya Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao. \s1 Ndoto ya Yakobo huko Betheli \p \v 10 Yakobo akatoka Beer-Sheba kwenda Harani. \v 11 Alipofika mahali fulani, akalala hapo kwa sababu jua lilikuwa limetua. Akachukua jiwe moja la mahali pale, akaliweka chini ya kichwa chake, akajinyoosha na akalala usingizi. \v 12 Akaota ndoto, na katika ndoto hiyo aliona ngazi imesimamishwa juu ya ardhi, ncha yake ikiwa imefika mbinguni. Nao malaika wa Mungu walikuwa wakipanda na kushuka kwa ngazi hiyo. \v 13 Juu yake alisimama Mwenyezi Mungu, akasema, “Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba yako Ibrahimu, na Mungu wa Isaka. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako. \v 14 Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako, mataifa yote ya duniani yatabarikiwa. \v 15 Niko pamoja nawe, nami nitakulinda popote utakapoenda, na nitakurudisha katika nchi hii. Sitakuacha hadi nitakapofanya hayo niliyokuahidi.” \p \v 16 Yakobo alipoamka kutoka usingizi, akawaza, “Hakika Mwenyezi Mungu yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.” \v 17 Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo; hili ni lango la mbinguni.” \p \v 18 Kesho yake asubuhi na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. \v 19 Mahali pale akapaita Betheli\f + \fr 28:19 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Nyumba ya Mungu\fqa*\f*, ingawa mji ule hapo awali uliitwa Luzu. \p \v 20 Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, “Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari hii, akinipa chakula nile na nguo nivae, \v 21 na nirudi salama nyumbani mwa baba yangu, hapo ndipo Mwenyezi Mungu atakuwa Mungu wangu. \v 22 Nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu, na katika yote utakayonipa nitakutolea sehemu ya kumi.” \c 29 \s1 Yakobo awasili Padan-Aramu \p \v 1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake, na akafika nchi ya watu wa mashariki. \v 2 Huko akaona kisima katika shamba, pamoja na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu na kisima hicho, kwa sababu walikuwa wakinyweshwa kutoka kisima hicho. Jiwe lililokuwa juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa. \v 3 Kondoo walipokusanyika hapo, wachungaji walilivingirisha jiwe hilo kutoka mdomo wa kisima. Kisha walilirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima. \p \v 4 Yakobo aliwauliza wachungaji, “Ndugu zangu, ninyi mmetoka wapi?” \p Wakamjibu, “Tumetoka Harani.” \p \v 5 Akawauliza, “Je, mnamfahamu Labani, mjukuu wa Nahori?” \p Wakamjibu, “Ndiyo, tunamfahamu.” \p \v 6 Kisha Yakobo akawauliza, “Je, yeye ni mzima?” \p Wakasema, “Ndiyo, ni mzima; na hapa yuaja Raheli binti yake akiwa na kondoo.” \p \v 7 Akawaambia, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya mifugo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.” \p \v 8 Wakamjibu, “Haiwezekani, hadi kondoo wote wakusanyike, nalo jiwe livingirishwe kutoka mdomo wa kisima. Ndipo tutawanywesha kondoo.” \p \v 9 Alipokuwa akizungumza nao, Raheli akaja na kondoo wa baba yake, kwa maana alikuwa mchunga kondoo. \v 10 Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alienda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake. \v 11 Kisha Yakobo akambusu Raheli, na akaanza kulia kwa sauti. \v 12 Yakobo alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake, na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake. \p \v 13 Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani mwake, naye Yakobo akamwambia mambo hayo yote. \v 14 Ndipo Labani akamwambia, “Wewe ni mwili wangu na damu yangu mwenyewe.” \s1 Yakobo awaoa Lea na Raheli \p Baada ya Yakobo kukaa kwa Labani mwezi mzima, \v 15 Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo sababu unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.” \p \v 16 Labani alikuwa na binti wawili; binti mkubwa aliitwa Lea, naye binti mdogo aliitwa Raheli. \v 17 Lea alikuwa na macho dhaifu, lakini Raheli alikuwa na umbo la kupendeza na mzuri wa sura. \v 18 Yakobo akampenda Raheli; akamwambia Labani, “Nitakutumikia kwa miaka saba kwa ajili ya kumpata Raheli binti yako mdogo.” \p \v 19 Labani akasema, “Ni bora zaidi nikupe Raheli kuliko kumpa mtu mwingine yeyote. Kaa pamoja na mimi hapa.” \v 20 Kwa hiyo Yakobo akatumika miaka saba ili kumpata Raheli, lakini ilionekana kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli. \p \v 21 Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka niingie kwake.” \p \v 22 Basi Labani akaalika watu wote wa mahali pale na akafanya karamu. \p \v 23 Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake, akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili. \v 24 Naye Labani akamtoa Zilpa mjakazi wake kuwa mtumishi wa Lea, binti yake. \p \v 25 Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, sivyo? Kwa nini umenidanganya?” \p \v 26 Labani akajibu, “Si desturi yetu kumwoza binti mdogo kabla ya kumwoza binti mkubwa. \v 27 Maliza juma la arusi ya binti huyu, kisha pia nitakupa huyu binti mdogo, kwa kutumika miaka mingine saba.” \p \v 28 Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake. \v 29 Labani akamtoa Bilha mjakazi wake kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake. \v 30 Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba. \s1 Wana wa Yakobo \p \v 31 Mwenyezi Mungu alipoona kwamba Lea hapendwi, akamwezesha kupata watoto, lakini Raheli alikuwa tasa. \v 32 Lea akapata mimba, akazaa mwana. Akamwita jina Reubeni\f + \fr 29:32 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Ona mwana\fqa*\f*, kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.” \p \v 33 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita jina Simeoni\f + \fr 29:33 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Anasikia\fqa*\f*. \p \v 34 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Sasa mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita jina Lawi\f + \fr 29:34 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Nimeunganishwa\fqa*\f*. \p \v 35 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Wakati huu nitamsifu Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo akamwita jina Yuda\f + \fr 29:35 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Sifa\fqa*\f*. Kisha akaacha kuzaa watoto. \c 30 \p \v 1 Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea dada yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!” \p \v 2 Yakobo akamkasirikia, akamwambia, “Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia kuzaa watoto?” \p \v 3 Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mjakazi wangu. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto, na kupitia kwake mimi pia niweze kuwa na uzao.” \p \v 4 Hivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili, \v 5 naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. \v 6 Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu; amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa hiyo akamwita jina Dani\f + \fr 30:6 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Anahukumu\fqa*\f*. \p \v 7 Bilha mjakazi wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. \v 8 Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na dada yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita jina Naftali\f + \fr 30:8 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Nimeshindana\fqa*\f*. \p \v 9 Lea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mjakazi wake Zilpa, naye akampa Yakobo awe mke wake. \v 10 Zilpa mjakazi wa Lea akamzalia Yakobo mwana. \v 11 Ndipo Lea akasema, “Hii ni bahati nzuri aje!” Kwa hiyo akamwita jina Gadi\f + \fr 30:11 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Jeshi laja\fqa*\f*. \p \v 12 Mjakazi wa Lea akamzalia Yakobo mwana wa pili. \v 13 Ndipo Lea akasema, “Nina furaha kiasi gani! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita jina Asheri\f + \fr 30:13 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Nimefurahi\fqa*\f*. \p \v 14 Msimu wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akachuma tunguja ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.” \p \v 15 Lakini Lea akamwambia, “Haikukutosha kuninyang’anya mume wangu? Je, utachukua na tunguja za mwanangu pia?” \p Raheli akasema, “Vema sana! Yakobo atakutana nawe kimwili leo usiku, kwa malipo ya tunguja za mwanao.” \p \v 16 Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule. \p \v 17 Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano. \v 18 Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mjakazi wangu.” Kwa hiyo akamwita jina Isakari\f + \fr 30:18 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Zawadi\fqa*\f*. \p \v 19 Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita. \v 20 Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Sasa mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita jina Zabuloni\f + \fr 30:20 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Heshima\fqa*\f*. \p \v 21 Baadaye akamzaa mtoto wa kike, akamwita jina Dina\f + \fr 30:21 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Tetea haki\fqa*\f*. \p \v 22 Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. \v 23 Akapata mimba na akamzaa mwana; akasema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.” \p \v 24 Akamwita jina Yusufu\f + \fr 30:24 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Yeye na aongeze\fqa*\f*, akasema, “Mwenyezi Mungu na anipe mwana mwingine.” \s1 Makundi ya Yakobo yaongezeka \p \v 25 Baada ya Raheli kumzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu. \v 26 Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua kazi niliyokufanyia.” \p \v 27 Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa uaguzi kwamba Mwenyezi Mungu amenibariki kwa sababu yako.” \v 28 Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.” \p \v 29 Yakobo akamwambia, “Unajua jinsi nimekutumikia na jinsi wanyama wako walivyolishwa vizuri chini ya uangalizi wangu. \v 30 Kidogo ulichokuwa nacho kabla sijaja kimeongezeka sana, naye Mwenyezi Mungu amekubariki popote nilipokuwa. Lakini sasa, ni lini nitashughulikia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?” \p \v 31 Labani akamuuliza, “Nikupe nini?” \p Yakobo akamjibu, “Usinipe chochote, lakini kama utanifanyia jambo hili moja, nitaendelea kuchunga na kuyaangalia makundi yako. \v 32 Niruhusu nipite katika makundi yako yote leo niondoe humo kila kondoo mwenye mabaka mabaka au madoadoa, kila mwana-kondoo mweusi, na kila mbuzi mwenye madoadoa au mabaka mabaka. Hawa watakuwa ujira wangu. \v 33 Uadilifu wangu utanishuhudia siku zijazo, kila utakapochunguza ujira ambao umenilipa mimi. Mbuzi yeyote wangu ambaye hana mabaka mabaka wala madoadoa, au mwana-kondoo ambaye si mweusi, atahesabika ameibwa.” \p \v 34 Labani akasema, “Ninakubali; na iwe kama ulivyosema.” \v 35 Siku ile ile Yakobo akawaondoa beberu wote waliokuwa na mistari au madoadoa, na mbuzi jike wote waliokuwa na mistari au madoadoa (wote waliokuwa na alama nyeupe juu yao), na wana-kondoo weusi wote, akawaweka chini ya uangalizi wa wanawe. \v 36 Kisha Labani akamwacha Yakobo kwa mwendo wa safari ya siku tatu, naye Yakobo akaendelea kuchunga lile kundi la Labani lililobaki. \p \v 37 Lakini Yakobo akachukua fito mbichi zilizokatwa wakati huo huo za miti ya mlubna, mlozi na mwaramoni, akazibambua ili mistari myeupe ionekane katika fito hizo. \v 38 Kisha akaweka fito hizo katika mabirika yote ya kunyweshea mifugo, ili ziwe mbele ya makundi walipokuja kunywa maji. Wanyama walipokuja kunywa maji, hali wakiwa wanahitaji mbegu, \v 39 wakapandwa hizo fito zikiwa mbele yao. Wanyama waliopata mimba mbele ya hizo fito walizaa wanyama wenye mistari, madoadoa na mabaka mabaka. \v 40 Yakobo akawatenga wadogo wa kundi peke yao, lakini akazielekeza nyuso za hao waliobaki kwenye wale wenye mistari na weusi waliokuwa mali ya Labani. Hivyo akatenga makundi yake mwenyewe, wala hakuwachanganya na wanyama wa Labani. \v 41 Kila mara wanyama wenye nguvu walipohitaji mbegu, Yakobo aliweka zile fito kwenye mabirika mbele ya hao wanyama, ili wapandwe karibu na hizo fito, \v 42 lakini ikiwa wanyama walikuwa wadhaifu hakuziweka hizo fito. Hivyo wanyama wadhaifu wakawa wa Labani, na wanyama wenye nguvu wakawa wa Yakobo. \v 43 Hivyo Yakobo akastawi sana, tena akawa na makundi makubwa, mjakazi na watumishi, na ngamia na punda. \c 31 \s1 Yakobo akimbia kutoka kwa Labani \p \v 1 Yakobo akawasikia wana wa Labani wakisema, “Yakobo amechukua mali yote ya baba yetu, naye amepata utajiri huu wote kutokana na mali ya baba yetu.” \v 2 Yakobo akatambua kwamba moyo wa Labani kwake umebadilika. \p \v 3 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe.” \p \v 4 Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje malishoni kwenye makundi yake. \v 5 Akawaambia, “Naona moyo wa baba yenu kwangu umebadilika, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami. \v 6 Mnajua kwamba nimemtumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote, \v 7 lakini baba yenu amenidanganya kwa kubadilisha ujira wangu mara kumi. Hata hivyo, Mungu hakumruhusu kunidhuru. \v 8 Aliposema, ‘Wenye madoadoa watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye madoadoa. Aliposema, ‘Wenye mistari watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye mistari. \v 9 Hivyo Mungu amechukua mifugo ya baba yenu na amenipa mimi. \p \v 10 “Majira ya kuzaliana niliota ndoto. Niliinua macho na kuona kwamba wale beberu waliokuwa wakiwapanda mbuzi walikuwa wana mistari, madoadoa na mabaka mabaka. \v 11 Malaika wa Mungu akaniita katika ndoto, ‘Yakobo.’ Nikamjibu, ‘Mimi hapa.’ \v 12 Akaniambia, ‘Inua macho yako uone wale beberu wote wanaowapanda mbuzi wana mistari, madoadoa au mabaka mabaka, kwa maana nimeona yale yote Labani amekutendea. \v 13 Mimi ndiye Mungu wa Betheli, ulikomiminia nguzo mafuta, na ukaniwekea nadhiri. Sasa ondoka katika nchi hii mara moja urudi katika nchi uliyozaliwa.’ ” \p \v 14 Ndipo Raheli na Lea wakajibu, “Je bado tunalo fungu lolote katika urithi wa nyumba ya baba yetu? \v 15 Je, yeye hatuhesabu sisi kama wageni? Sio kwamba ametuuza tu, bali ametumia hata mali tuliyolipiwa. \v 16 Hakika utajiri wote ambao Mungu ameuchukua kutoka kwa baba yetu ni mali yetu na watoto wetu. Hivyo fanya lolote lile Mungu alilokuambia.” \p \v 17 Ndipo Yakobo akawapandisha watoto wake na wake zake juu ya ngamia. \v 18 Naye akawaswaga wanyama wote mbele yake, pamoja na mali yote aliyokuwa amepata huko Padan-Aramu ili aende kwa baba yake Isaka katika nchi ya Kanaani. \p \v 19 Labani alipokuwa ameenda kukata kondoo wake manyoya, Raheli aliiba miungu ya nyumbani mwa baba yake. \v 20 Zaidi ya hayo, Yakobo alimdanganya Labani Mwaramu\f + \fr 31:20 \fr*\ft au \ft*\fqa Mshami\fqa*\f* kwa kutokumwambia kwamba anakimbia. \v 21 Hivyo akakimbia pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuvuka Mto\f + \fr 31:21 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f*, akaelekea nchi ya vilima ya Gileadi. \s1 Labani amfuatilia Yakobo \p \v 22 Siku ya tatu, Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia. \v 23 Akiwachukua jamaa zake, akamfuatia Yakobo kwa siku saba na kumkuta kwenye nchi ya vilima ya Gileadi. \v 24 Ndipo Mungu akamjia Labani Mwaramu katika ndoto usiku na kumwambia, “Jihadhari usiseme neno lolote kwa Yakobo, liwe zuri au baya.” \p \v 25 Yakobo alikuwa amepiga hema lake katika nchi ya vilima ya Gileadi wakati Labani alimfikia; naye Labani na jamaa yake wakapiga kambi huko pia. \v 26 Ndipo Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini? Umenidanganya na umewachukua binti zangu kama mateka katika vita. \v 27 Kwa nini ulikimbia kwa siri na kunidanganya? Kwa nini hukuniambia ili nikuage kwa furaha na nyimbo za matari na vinubi? \v 28 Hata hukuniruhusu niwabusu wajukuu zangu na kuwaaga binti zangu. Umefanya kitu cha kipumbavu. \v 29 Nina uwezo wa kukudhuru, lakini usiku uliopita Mungu wa baba yako alisema nami, akaniambia, ‘Jihadhari, usiseme neno lolote kwa Yakobo, liwe zuri au baya.’ \v 30 Sasa umeondoka kwa sababu umetamani kurudi nyumbani mwa baba yako. Lakini kwa nini umeiiba miungu yangu?” \p \v 31 Yakobo akamjibu Labani, “Niliogopa, kwa sababu nilifikiri ungeweza kuninyang’anya binti zako kwa nguvu. \v 32 Lakini ukimkuta yeyote na miungu yako, huyo mtu hataishi. Mbele ya jamaa zetu, angalia mwenyewe uone kama kuna chochote chako hapa nilicho nacho; kama kipo, kichukue.” Basi Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiiba hiyo miungu. \p \v 33 Kwa hiyo Labani akaingia ndani ya hema la Yakobo, na ndani ya hema la Lea, na ndani ya hema la wajakazi wale wawili, lakini hakuipata hiyo miungu. Baadaye alipotoka hema la Lea, akaingia hema la Raheli. \v 34 Basi Raheli ndiye alikuwa ameichukua ile miungu ya nyumbani mwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia, na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata chochote. \p \v 35 Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike bwana wangu, kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani mwake. \p \v 36 Yakobo akakasirika na kumshutumu Labani, akisema, “Uhalifu wangu ni nini?” Akamuuliza Labani, “Ni dhambi gani niliyofanya hata unaniwinda? \v 37 Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote, umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu. \p \v 38 “Hadi sasa nimekuwa pamoja nawe miaka ishirini. Kondoo wako na mbuzi wako hawajaharibu mimba, wala sijala kondoo dume kutoka makundi yako. \v 39 Sijakuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, bali nimegharimia hasara mwenyewe. Tena umenidai malipo kwa chochote kilichoibwa mchana au usiku. \v 40 Hali yangu imekuwa hivi: Nimechomwa kwa joto la mchana, na kupigwa na baridi usiku, pia usingizi ulinipotea. \v 41 Imekuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na nne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi. \v 42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hakuwa pamoja nami, hakika ungenifukuza mikono mitupu. Lakini Mungu ameona taabu yangu na kazi ngumu ya mikono yangu, naye usiku uliopita amekukemea.” \p \v 43 Labani akamjibu Yakobo, “Wanawake hawa ni binti zangu, watoto hawa ni watoto wangu, na makundi haya ni makundi yangu. Vyote unavyoviona ni vyangu. Lakini hata hivyo ninaweza kufanya nini kuhusu hawa binti zangu, au kuhusu watoto waliowazaa? \v 44 Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.” \p \v 45 Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. \v 46 Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo; wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. \v 47 Labani akaliita Yegar-Sahadutha\f + \fr 31:47 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Lundo la ushahidi \fqa*\ft kwa Kiaramu\ft*\f* na Yakobo akaliita Galeedi.\f + \fr 31:47 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Lundo la ushahidi \fqa*\ft kwa Kiebrania\ft*\f* \p \v 48 Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. \v 49 Pia liliitwa Mispa\f + \fr 31:49 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mnara wa ulinzi\fqa*\f*, kwa sababu alisema, “Mwenyezi Mungu na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati hatuko pamoja. \v 50 Ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.” \p \v 51 Pia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi. \v 52 Lundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru. \v 53 Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba zao, aamue kati yetu.” \p Hivyo Yakobo akaapa kwa jina la Hofu ya baba yake Isaka. \v 54 Yakobo akatoa dhabihu huko nchi ya vilima na akawaalika jamaa zake kula chakula. Baada ya kula, wakalala huko. \p \v 55 Kesho yake asubuhi na mapema, Labani akawabusu wajukuu zake na binti zake, na kuwabariki. Kisha akaondoka, akarudi nyumbani. \c 32 \s1 Yakobo ajiandaa kukutana na Esau \p \v 1 Yakobo pia akaondoka akaenda zake, nao malaika wa Mungu wakakutana naye. \v 2 Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu!” Kwa hiyo akapaita mahali pale Mahanaimu\f + \fr 32:2 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kambi mbili\fqa*\f*. \p \v 3 Yakobo akatuma wajumbe kumtangulia kwa Esau ndugu yake huko Seiri, katika nchi ya Edomu. \v 4 Akawaagiza, akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: ‘Mtumishi wako Yakobo anasema: nimekuwa nikiishi pamoja na Labani na nimekuwa huko hadi sasa. \v 5 Ninao ng’ombe na punda, kondoo na mbuzi, watumishi wa kiume na wa kike. Sasa ninatuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili nipate kibali machoni pako.’ ” \p \v 6 Wajumbe waliporudi kwa Yakobo, wakamwambia, “Tulienda kuonana na ndugu yako Esau, naye sasa anakuja kukulaki akifuatana na wanaume mia nne.” \p \v 7 Kwa hofu kuu na huzuni, Yakobo akagawanya watu aliokuwa nao katika makundi mawili; pia akagawanya makundi ya kondoo na mbuzi, na vilevile ng’ombe na ngamia. \v 8 Yakobo alifikiri, “Kama Esau akija na kushambulia kundi moja, kundi lililobaki litanusurika.” \p \v 9 Ndipo Yakobo akaomba, “Ee Mungu wa baba yangu Ibrahimu, Mungu wa baba yangu Isaka, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe uliniambia, ‘Rudi katika nchi yako na jamaa yako, nami nitakufanya ustawi.’ \v 10 Sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi, mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa nimekuwa makundi mawili. \v 11 Nakuomba uniokoe kutoka kwa mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia kina mama pamoja na watoto wao. \v 12 Lakini umeshasema, ‘Hakika nitakufanya ustawi na kuufanya uzao wako kuwa mwingi kama mchanga wa baharini ambao hauwezi kuhesabika!’ ” \p \v 13 Akalala pale usiku ule. Miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake: \v 14 beberu ishirini na mbuzi jike mia mbili, kondoo dume ishirini na kondoo jike mia mbili, \v 15 ngamia jike thelathini pamoja na ndama zao, ng’ombe arobaini na mafahali kumi, punda jike ishirini, na punda wa kiume kumi. \v 16 Akaviweka chini ya uangalizi wa watumishi wake, kila kundi peke yake, na kuwaambia, “Nitangulieni na kuacha nafasi kati ya makundi.” \p \v 17 Akamwagiza yule aliyetangulia hivi, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, ‘Wewe ni wa nani? Unaenda wapi? Wanyama hawa wote mbele yako ni mali ya nani?’ \v 18 utamjibu hivi, ‘Ni mali ya mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi iliyotumwa kwa bwana wangu Esau, naye anakuja nyuma yetu.’ ” \p \v 19 Akamwagiza pia yule mtumishi wa kundi la pili, na wa kundi la tatu, na kila mtumishi wa yale mengine yaliyofuata, hivi: “Mtamwambia Esau maneno hayo hayo mtakapokutana naye. \v 20 Hakikisheni mmesema, ‘Mtumishi wako Yakobo anakuja nyuma yetu.’ ” Kwa kuwa alifikiri, “Nitaweza kumtuliza kwa zawadi hizi ninazotanguliza; hatimaye nitakapomwona, huenda atanikubali.” \v 21 Kwa hiyo zawadi za Yakobo zilitangulia mbele yake, lakini yeye mwenyewe alilala kambini usiku ule. \s1 Yakobo amenyana na Mungu \p \v 22 Usiku ule Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wajakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Mto Yaboki. \v 23 Baada ya kuwavusha ng’ambo ya kijito, alivusha pia mali yake yote. \v 24 Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake; naye mtu mmoja akashikana naye mweleka hadi mapambazuko. \v 25 Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo; kwa hiyo nyonga yake ikateguka alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. \v 26 Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” \p Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.” \p \v 27 Yule mtu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” \p Akamjibu, “Ni Yakobo.” \p \v 28 Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli\f + \fr 32:28 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Yeye ashindanaye na Mungu\fqa*\f*, kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.” \p \v 29 Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.” \p Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko. \p \v 30 Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli\f + \fr 32:30 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Uso wa Mungu\fqa*\ft ; sawa na \ft*\fqa Penueli \fqa*\ft kwa Kiebrania\ft*\f*, akisema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso, na bado uhai wangu umehifadhiwa.” \p \v 31 Jua lilikuwa linachomoza Yakobo alipoondoka Penueli, naye alikuwa akichechemea kwa sababu ya nyonga yake. \v 32 Kwa hiyo hadi leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo. \c 33 \s1 Yakobo akutana na Esau \p \v 1 Yakobo akainua macho, akamwona Esau akija na watu wake mia nne. Kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale wajakazi wake wawili. \v 2 Akawaweka wale wajakazi na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, nao Raheli na Yusufu wakaja nyuma. \v 3 Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu hadi chini mara saba alipomkaribia ndugu yake. \p \v 4 Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia. \v 5 Esau akainua macho, akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa waliofuatana nawe ni nani?” \p Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.” \p \v 6 Kisha wale wajakazi na watoto wao wakakaribia na kusujudu. \v 7 Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yusufu na Raheli, nao pia wakasujudu. \p \v 8 Esau akauliza, “Makundi hayo yote niliyokutana nayo yana maana gani?” \p Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.” \p \v 9 Lakini Esau akamwambia, “Ndugu yangu, tayari nina wingi wa mali. Ulivyo navyo viwe vyako mwenyewe.” \p \v 10 Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa kibali kikubwa. \v 11 Tafadhali kubali zawadi iliyoletwa kwako, kwa kuwa Mungu amenineemesha na ninavyo vyote ninavyohitaji.” Kwa sababu Yakobo alisisitiza, Esau akapokea. \p \v 12 Ndipo Esau akasema, “Tuendelee na safari; nitakusindikiza.” \p \v 13 Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu, unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa ng’ombe na kondoo wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa. \v 14 Hivyo bwana wangu, mtangulie mtumishi wako, nami nije polepole kwa mwendo wa makundi yaliyo mbele yangu na mwendo wa watoto, hadi nifike kwa bwana wangu huko Seiri.” \p \v 15 Esau akamwambia, “Basi kubali nikuachie baadhi ya watu wangu.” \p Yakobo akauliza, “Lakini kwa nini ufanye hivyo? Niache tu nipate kibali machoni pa bwana wangu.” \p \v 16 Hivyo siku hiyo Esau akashika njia, akarudi Seiri. \v 17 Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi\f + \fr 33:17 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Vibanda\fqa*\f*. Akajijengea makazi na pia vibanda vya mifugo yake. Hii ndiyo sababu mahali pale panaitwa Sukothi. \p \v 18 Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani, na kuweka kambi yake karibu na mji huo. \v 19 Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia moja vya fedha, akapiga hema lake hapo. \v 20 Akajenga madhabahu pale na kupaita El-Elohe-Israeli\f + \fr 33:20 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mungu, Mungu wa Israeli \fqa*\ft au \ft*\fqa Mwenye Nguvu ni Mungu wa Israeli\fqa*\f*. \c 34 \s1 Dina na Washekemu \p \v 1 Basi Dina, binti Yakobo aliyezaliwa na Lea, akaenda kuwatembelea wanawake wa nchi ile. \v 2 Ikawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile, alipomwona, akamchukua na kumnajisi. \v 3 Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza. \v 4 Shekemu akamwambia Hamori, baba yake, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.” \p \v 5 Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake. Kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo hadi waliporudi nyumbani. \p \v 6 Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo. \v 7 Basi wana wa Yakobo wakarudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotukia. Walijawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti Yakobo, jambo ambalo halikupasa kutendwa. \p \v 8 Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake. \v 9 Oaneni na sisi; tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu. \v 10 Mwaweza kuishi nasi, nchi ni wazi kwenu. Ishini ndani yake, mfanye biashara humu na mjipatie mali.” \p \v 11 Kisha Shekemu akamwambia baba yake Dina pamoja na ndugu zake, “Naomba nipate kibali machoni penu, nami nitawapa chochote mtakachosema. \v 12 Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoileta, hata iwe kubwa kiasi gani, nami nitawalipa chochote mtakachodai. Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.” \p \v 13 Kwa sababu dada yao Dina alikuwa amenajisiwa, wana wa Yakobo wakajibu kwa udanganyifu walipozungumza na Shekemu pamoja na Hamori, baba yake. \v 14 Wakawaambia, “Hatuwezi kufanya jambo kama hili. Hatuwezi kumtoa dada yetu kwa mtu ambaye hajatahiriwa. Hiyo itakuwa aibu kwetu. \v 15 Tutakuruhusu kwa sharti moja tu, kwamba mtakuwa kama sisi kwa kuwatahiri wanaume wenu wote. \v 16 Kisha tutawapa binti zetu na sisi tutawachukua binti zenu. Tutaishi kwenu na tutakuwa watu wamoja nanyi. \v 17 Lakini mkikataa kutahiriwa, tutamchukua dada yetu na kuondoka.” \p \v 18 Pendekezo lao likakubalika kwa Hamori na Shekemu mwanawe. \v 19 Kijana huyo, aliyekuwa ameheshimiwa kati ya wote walioishi nyumbani mwa baba yake, hakupoteza muda kufanya waliyoyasema, kwa sababu alikuwa amependezwa sana na binti Yakobo. \v 20 Kwa hiyo Hamori na Shekemu mwanawe walienda kwenye lango la mji kuzungumza na wanaume wa mji wao. \v 21 Wakasema, “Hawa wanaume ni rafiki zetu. Tuwaruhusu waishi katika nchi yetu na kufanya biashara ndani yake; nchi ina nafasi tele kwa ajili yao. Tunaweza kuoa binti zao, nao wanaweza kuoa binti zetu. \v 22 Lakini wanaume hawa watakubali kuishi nasi kama watu wamoja nao kwa sharti kwamba wanaume wetu watahiriwe, kama wao. \v 23 Je, si mifugo yao, mali yao na wanyama wao wengine wote watakuwa wetu? Basi tukubali sharti lao, nao wataishi miongoni mwetu.” \p \v 24 Wanaume wote waliotoka nje ya lango la mji walikubaliana na Hamori na Shekemu mwanawe, na kila mwanaume katika mji ule akatahiriwa. \p \v 25 Baada ya siku tatu, wakati wote wakiwa wangali katika maumivu, wana wawili wa Yakobo, yaani Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua panga zao na kuvamia mji ambao haukutazamia vita, wakaua kila mwanaume. \v 26 Wakawaua Hamori na Shekemu mwanawe kwa panga, kisha wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka. \v 27 Wana hao wengine wa Yakobo wakaingia mji uliojaa maiti na kuteka nyara katika mji huo dada yao alikuwa amenajisiwa. \v 28 Wakateka kondoo na mbuzi, ng’ombe, punda, na kila kitu kilichokuwa ndani ya mji ule na mashambani. \v 29 Waliteka utajiri wao wote, pamoja na wanawake na watoto wao, wakapora kila kitu ndani ya nyumba zao. \p \v 30 Kisha Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, “Mmenitaabisha kwa kunifanya ninuke kama uvundo kwa Wakanaani na Waperizi, watu wanaoishi nchi hii. Sisi ni wachache; wakiunganisha nguvu zao dhidi yangu na kunishambulia, mimi na nyumba yangu tutaangamizwa.” \p \v 31 Lakini wakamjibu, “Je, ilikuwa vyema kumtendea dada yetu kama kahaba?” \c 35 \s1 Yakobo arudi Betheli \p \v 1 Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko. Ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.” \p \v 2 Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni mliyo nayo, mjitakase na mkabadilishe nguo zenu. \v 3 Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipoenda.” \v 4 Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mwaloni ulio Shekemu. \v 5 Kisha wakaondoka, na utisho wa Mungu ukaipata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo. \p \v 6 Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. \v 7 Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli\f + \fr 35:7 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mungu wa Betheli\fqa*\f*, kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alijifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake. \p \v 8 Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mwaloni ulio nje ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi\f + \fr 35:8 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwaloni wa kilio\fqa*\f*. \p \v 9 Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. \v 10 Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo\f + \fr 35:10 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Ashikaye kisigino\fqa*\ft , au \ft*\fqa Atwaaye mahali pa mwingine\fqa*\ft , au \ft*\fqa Mdanganyaji\fqa*\f*. Lakini hutaitwa tena Yakobo; jina lako litakuwa Israeli\f + \fr 35:10 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Yeye ashindanaye na Mungu\fqa*\f*.” Kwa hiyo akamwita Israeli. \p \v 11 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi\f + \fr 35:11 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f*; ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. \v 12 Nchi niliyowapa Ibrahimu na Isaka nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” \v 13 Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye. \p \v 14 Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. \v 15 Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli\f + \fr 35:15 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Nyumba ya Mungu\fqa*\f*. \s1 Vifo vya Raheli na Isaka \p \v 16 Kisha wakaondoka Betheli. Kabla hawajafika Efrata, Raheli akaanza kujifungua na akapata shida kuu. \v 17 Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” \v 18 Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe jina Benoni\f + \fr 35:18 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwana wa huzuni yangu\fqa*\f*. Lakini babaye akamwita jina Benyamini\f + \fr 35:18 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwana wa mkono wangu wa kuume\fqa*\f*. \p \v 19 Kwa hiyo Raheli akafa, na akazikwa kando ya njia iendayo Efrata (ndio Bethlehemu). \v 20 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ambayo hadi leo inatambulisha kaburi la Raheli. \p \v 21 Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema baada ya kupita Mnara wa Ederi. \v 22 Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aliyeitwa Bilha, naye Israeli akasikia jambo hilo. \b \lh Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili: \b \li1 \v 23 Wana wa Lea walikuwa: \li2 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, \li2 Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni. \li1 \v 24 Wana wa Raheli walikuwa: \li2 Yusufu na Benyamini. \li1 \v 25 Wana waliozaliwa na Bilha mjakazi wa Raheli walikuwa: \li2 Dani na Naftali. \li1 \v 26 Wana waliozaliwa na Zilpa mjakazi wa Lea walikuwa: \li2 Gadi na Asheri. \b \lf Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu. \b \p \v 27 Yakobo akarudi nyumbani mwa baba yake Isaka huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Ibrahimu na Isaka. \v 28 Isaka aliishi miaka mia moja na themanini. \v 29 Kisha Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho, akafa; akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee aliyeshiba siku. Nao Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika. \c 36 \s1 Wazao wa Esau \r (1 Nyakati 1:34-42) \p \v 1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu). \b \p \v 2 Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti Eloni Mhiti, Oholibama binti Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi; \v 3 pia akaoa Basemathi binti Ishmaeli, dada yake Nebayothi. \p \v 4 Ada akamzalia Esau Elifazi; Basemathi akamzaa Reueli; \v 5 Oholibama akawazaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani. \p \v 6 Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike, na watu wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote, na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. \v 7 Mali yao ilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja; nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. \v 8 Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya vilima ya Seiri. \b \lh \v 9 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya vilima ya Seiri. \b \li1 \v 10 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: \li2 Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia. \li1 \v 11 Wana wa Elifazi ni: \li2 Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi. \v 12 Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, aliyemzalia Amaleki. Hao walikuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau. \li1 \v 13 Wana wa Reueli ni: \li2 Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hao walikuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau. \li1 \v 14 Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni: \li2 Yeushi, Yalamu na Kora. \b \lh \v 15 Hawa walikuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: \li1 Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: \li2 Temani, Omari, Sefo, Kenazi, \v 16 Kora, Gatamu na Amaleki. Hao walikuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu; walikuwa wajukuu wa kiume wa Ada. \li1 \v 17 Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: \li2 Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu; walikuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau. \li1 \v 18 Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni: \li2 Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana. \lf \v 19 Hao walikuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hao walikuwa wakuu wao. \b \li1 \v 20 Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, walioishi katika nchi ile: \li2 Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, \v 21 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori. \li1 \v 22 Wana wa Lotani walikuwa: \li2 Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani. \li1 \v 23 Wana wa Shobali walikuwa: \li2 Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. \li1 \v 24 Wana wa Sibeoni walikuwa: \li2 Aya na Ana. (Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda wa Sibeoni, baba yake.) \li1 \v 25 Watoto wa Ana walikuwa: \li2 Dishoni na Oholibama binti Ana. \li1 \v 26 Wana wa Dishoni walikuwa: \li2 Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. \li1 \v 27 Wana wa Eseri walikuwa: \li2 Bilhani, Zaavani na Akani. \li1 \v 28 Wana wa Dishani walikuwa: \li2 Usi na Arani. \li1 \v 29 Hawa walikuwa wakuu wa Wahori: \li2 Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, \v 30 Dishoni, Eseri na Dishani. \lf Hao walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri. \s1 Watawala wa Edomu \r (1 Nyakati 1:43-54) \lh \v 31 Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala: \li1 \v 32 Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba. \li1 \v 33 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. \li1 \v 34 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. \li1 \v 35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. \li1 \v 36 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. \li1 \v 37 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ng’ambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake. \li1 \v 38 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. \li1 \v 39 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. \b \lh \v 40 Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao: \li1 Timna, Alva, Yethethi, \li1 \v 41 Oholibama, Ela, Pinoni, \li1 \v 42 Kenazi, Temani, Mibsari, \li1 \v 43 Magdieli na Iramu. \lf Hao walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki. \b \lf Hivi ndivyo vizazi vya Esau, baba wa Waedomu. \c 37 \p \v 1 Yakobo akaishi Kanaani katika nchi ambayo baba yake alikuwa ameishi. \s1 Ndoto za Yusufu \p \v 2 Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. \b \p Yusufu, kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga makundi ya kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake, yaani wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake za baba yake, naye akamletea baba yao taarifa mbaya kuhusu hao ndugu zake. \p \v 3 Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko ndugu zake wote, kwa sababu alikuwa mwanawe wa uzeeni; akamshonea joho lililofumwa vizuri sana. \v 4 Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yusufu kuliko yeyote kati yao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema. \p \v 5 Yusufu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. \v 6 Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: \v 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani. Ghafula mganda wangu ukasimama wima, nayo miganda yenu ikauzunguka na kuuinamia.” \p \v 8 Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakazidi kumchukia kwa sababu ya ndoto yake, pamoja na yale aliyowaambia. \p \v 9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akisema, “Sikilizeni: nimeota ndoto nyingine. Wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.” \p \v 10 Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako, na mimi, na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe?” \v 11 Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni. \s1 Yusufu auzwa na ndugu zake \p \v 12 Basi ndugu zake walikuwa wameenda kuchunga makundi ya baba yao karibu na Shekemu. \v 13 Israeli akamwambia Yusufu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.” \p Yusufu akajibu, “Vema sana, niko tayari.” \p \v 14 Kwa hiyo akamwambia, “Nenda uone kama ndugu zako wako salama, na makundi pia, kisha uniletee habari.” Basi akamtuma Yusufu kutoka Bonde la Hebroni. \p Yusufu alipofika Shekemu, \v 15 mtu mmoja akamkuta akizungukazunguka mashambani, akamuuliza, “Unatafuta nini?” \p \v 16 Akamjibu, “Ninawatafuta ndugu zangu. Unaweza kuniambia wanachunga wapi makundi yao?” \p \v 17 Yule mtu akajibu, “Wamehama hapa. Nilisikia wakisema, ‘Twendeni Dothani.’ ” \p Kwa hiyo Yusufu akawafuatilia ndugu zake na kuwakuta karibu na Dothani. \v 18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga njama za kumuua. \p \v 19 Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja! \v 20 Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo, na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.” \p \v 21 Reubeni aliposikia jambo hili, akajaribu kumwokoa kutoka mikononi mwao, akasema, “Tusimuue. \v 22 Msimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani mwa baba yake. \p \v 23 Kwa hiyo Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililofumwa vizuri alilokuwa amevaa. \v 24 Kisha wakamchukua, wakamtupa katika shimo. Hilo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji. \p \v 25 Walipokaa ili wale chakula chao, wakainua macho wakaona msafara wa Waishmaeli ukija kutoka Gileadi. Ngamia wao walikuwa wamepakizwa mizigo ya vikolezo, uvumba na manemane, nao walikuwa njiani kuvipeleka Misri. \p \v 26 Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutafaidi nini tukimuua ndugu yetu na kuificha damu yake? \v 27 Njooni, tumuuze kwa hawa Waishmaeli. Tusimguse, kwa kuwa hata hivyo yeye ni ndugu yetu, mwili wetu na damu yetu wenyewe.” Ndugu zake wakakubali. \p \v 28 Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yusufu kutoka lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini\f + \fr 37:28 \fr*\ft Shekeli 20 ni sawa na gramu 200.\ft*\f* za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri. \p \v 29 Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yusufu hayupo, alirarua nguo zake. \v 30 Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?” \p \v 31 Kisha wakalichukua lile joho la Yusufu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. \v 32 Wakalichukua lile joho lililofumwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.” \p \v 33 Baba yao akalitambua, akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yusufu ameraruliwa vipande vipande.” \p \v 34 Kisha Yakobo akararua nguo zake, akavaa gunia na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi. \v 35 Wanawe wote wa kiume na wa kike wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu hadi nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia. \p \v 36 Basi Wamidiani wakamuuza Yusufu huko Misri kwa Potifa, mmoja wa maafisa wa Farao, aliyekuwa mkuu wa walinzi. \c 38 \s1 Yuda na Tamari \p \v 1 Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami. \v 2 Huko Yuda akakutana na binti ya Mkanaani aitwaye Shua. Akamwoa na akakutana naye kimwili, \v 3 naye akapata mimba, na akamzaa mwana, aliyeitwa jina Eri. \v 4 Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita jina Onani. \v 5 Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita jina Shela. Huyu alimzalia huko Kezibu. \p \v 6 Yuda akamtwalia Eri, mzaliwa wake wa kwanza, mke aliyeitwa Tamari. \v 7 Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamuua. \p \v 8 Kisha Yuda akamwambia Onani, “Kutana kimwili na mke wa ndugu yako, na utimize wajibu wako kwake kama mke wa ndugu yako, ili umpatie ndugu yako uzao.” \v 9 Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga mbegu chini ili asimpatie ndugu yake uzao. \v 10 Alichofanya kilikuwa kiovu machoni pa Mwenyezi Mungu, hivyo Mwenyezi Mungu akamuua Onani pia. \p \v 11 Kisha Yuda akamwambia Tamari mkwewe, “Ishi kama mjane nyumbani mwa baba yako hadi mwanangu Shela atakapokua.” Kwa maana alifikiri, “Anaweza kufa pia kama ndugu zake.” Kwa hiyo Tamari akaenda kuishi nyumbani mwa baba yake. \p \v 12 Baada ya muda mrefu, mke wa Yuda, binti Shua, akafariki. Baada ya msiba, Yuda alienda Timna kwa watu waliokuwa wakikata kondoo wake manyoya, naye alifuatana na rafiki yake Hira Mwadulami. \p \v 13 Tamari alipoambiwa, “Baba mkwe wako yuko njiani akielekea Timna kukata kondoo wake manyoya,” \v 14 alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike. Akaketi kwenye mlango wa Enaimu, njiani ya kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba ingawa Shela sasa alikuwa mtu mzima, bado hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe. \p \v 15 Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake. \v 16 Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.” \p Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?” \p \v 17 Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” \p Akamuuliza, “Utanipa amana hadi utakapompeleka?” \p \v 18 Akamuuliza, “Nikupe amana gani?” \p Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo, kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake. \v 19 Tamari akaondoka, akavua shela yake, akavaa tena nguo zake za ujane. \p \v 20 Baadaye Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke. \v 21 Akawauliza watu walioishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa ibada za sanamu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?” \p Wakamjibu, “Hakujawahi kuwa kahaba wa mahali pa ibada za sanamu hapa.” \p \v 22 Kwa hiyo akamrudia Yuda na kumwambia, “Sikumpata. Zaidi ya hayo, watu wanaoishi mahali pale walisema, ‘Hakujawahi kuwa kahaba wa mahali pa ibada za sanamu hapa.’ ” \p \v 23 Kisha Yuda akasema, “Mwache avichukue vitu hivyo, ama sivyo tutaaibika. Hata hivyo, nilimpelekea mwana-mbuzi, lakini hukumkuta.” \p \v 24 Baada ya miezi mitatu, Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na sasa ana mimba.” \p Yuda akasema, “Mtoeni nje, achomwe moto hadi afe!” \p \v 25 Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.” \p \v 26 Yuda akavitambua na kusema, “Yeye ana haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumkabidhi kwa mwanangu Shela ili awe mkewe.” Tangu hapo hakukutana naye kimwili tena. \p \v 27 Wakati ulipofika wa kujifungua, kukawa na wana mapacha tumboni mwake. \v 28 Alipokuwa akijifungua, mmoja akatoa mkono wake nje, kwa hiyo mkunga akachukua uzi mwekundu na kuufunga mkononi mwa yule mtoto, akasema, “Huyu ametoka kwanza.” \v 29 Lakini alipourudisha mkono wake, ndugu yake akatangulia kutoka, naye mkunga akasema, “Hivi ndivyo ulivyotoka kwa nguvu!” Akaitwa Peresi\f + \fr 38:29 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kutoka kwa nguvu\fqa*\f*. \v 30 Kisha ndugu yake, aliyekuwa na uzi mwekundu mkononi, akatoka, naye akaitwa Zera\f + \fr 38:30 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Wekundu \fqa*\ft au \ft*\fqa Kung’aa\fqa*\f*. \c 39 \s1 Yusufu na mke wa Potifa \p \v 1 Wakati huu Yusufu alikuwa amechukuliwa hadi Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa, mmoja wa maafisa wa Farao, na aliyekuwa mkuu wa walinzi, akamnunua Yusufu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. \p \v 2 Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na Yusufu, naye akastawi. Yusufu akaishi nyumbani mwa bwana wake Mmisri. \v 3 Potifa alipoona kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na Yusufu, na kwamba Mwenyezi Mungu alimfanikisha kwa kila kitu alichokifanya, \v 4 Yusufu alipata kibali machoni pa Potifa, akamfanya mhudumu wake. Potifa akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, naye akamweka kuwa mwangalizi wa mali yake yote. \v 5 Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yusufu kuwa msimamizi wa nyumba na mali yake yote aliyokuwa nayo, Mwenyezi Mungu aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yusufu. Baraka ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani. \v 6 Kwa hiyo Potifa akamwachia Yusufu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho. Yusufu alipokuwa msimamizi wa mali yake, Potifa hakujishughulisha na kitu chochote isipokuwa chakula alichokula. \p Yusufu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia. \v 7 Baada ya kitambo, mke wa Potifa akamtamani Yusufu, akamwambia, “Njoo, ukutane nami kimwili!” \p \v 8 Lakini Yusufu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa msimamizi, bwana wangu hajishughulishi na kitu chochote katika nyumba hii; kila kitu alicho nacho amenikabidhi. \v 9 Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” \v 10 Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yusufu siku baada ya siku, Yusufu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye. \p \v 11 Siku moja Yusufu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwa mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. \v 12 Mke wa Potifa akashika vazi Yusufu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yusufu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia. \p \v 13 Yule mwanamke alipoona kwamba Yusufu amemwachia vazi lake mkononi na kukimbilia nje ya nyumba, \v 14 akawaita watumishi wake wa nyumbani, akawaambia, “Tazameni! Huyu Mwebrania ameletwa hapa kutudhihaki! Aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga yowe. \v 15 Aliposikia nikipiga yowe, akaacha vazi lake kando yangu, akakimbilia nje.” \p \v 16 Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye hadi Potifa aliporudi nyumbani. \v 17 Mwanamke akamweleza mumewe kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu alinijia ili kunidhihaki. \v 18 Lakini mara nilipopiga yowe kuomba msaada, akaliacha vazi lake kando yangu, akakimbia nje ya nyumba.” \p \v 19 Potifa aliposikia kisa alichosimuliwa na mkewe, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda,” hasira yake ikawaka. \v 20 Potifa akamchukua Yusufu na kumtia gerezani, mahali wahalifu wa mfalme walipokuwa wamefungwa. \p Lakini Yusufu alipokuwa huko gerezani, \v 21 Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja naye, akamhurumia na kumpa kibali mbele ya msimamizi wa gereza. \v 22 Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yusufu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani. \v 23 Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yusufu, kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja na Yusufu, akimfanikisha kwa kila alichofanya. \c 40 \s1 Mnyweshaji na mwokaji \p \v 1 Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. \v 2 Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu. \v 3 Akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa walinzi, katika gereza lile lile alimofungwa Yusufu. \v 4 Mkuu wa walinzi akawakabidhi kwa Yusufu, naye akawahudumia. \p Walipokuwa wamekaa chini ya ulinzi kwa muda, \v 5 kila mmoja wa hao wawili waliokuwa wamewekwa gerezani, yaani mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, waliota ndoto usiku mmoja, na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti. \p \v 6 Yusufu alipowajia asubuhi yake, akawaona kwamba walikuwa na huzuni. \v 7 Ndipo Yusufu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake hivi, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?” \p \v 8 Wakamjibu, “Sisi sote tumeota ndoto, lakini hakuna wa kuzifasiri.” \p Ndipo Yusufu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si ni kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.” \p \v 9 Basi mkuu wa wanyweshaji akamweleza Yusufu ndoto yake. Akamwambia, “Katika ndoto yangu niliona mzabibu mbele yangu, \v 10 nao mzabibu ulikuwa na matawi matatu. Mara tu ulipoanza kuchipua, maua yalichanua na vishada vyake vikawa zabibu zilizoiva. \v 11 Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu. Nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, na nikaweka kikombe mkononi mwake.” \p \v 12 Yusufu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. \v 13 Baada ya siku tatu, Farao atakutoa gerezani na kukurudisha kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mkononi mwake, jinsi ulivyofanya ulipokuwa mnyweshaji wake awali. \v 14 Lakini mambo yako yatakapokuwa mazuri, unikumbuke, unifanyie wema. Useme mema kunihusu kwa Farao ili unitoe huku gerezani. \v 15 Kwa maana nilichukuliwa kwa nguvu kutoka nchi ya Waebrania, na hata hapa nilipo sikufanya lolote linalostahili niwekwe gerezani.” \p \v 16 Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yusufu amefasiri vizuri, akamwambia Yusufu, “Mimi pia niliota ndoto. Kichwani mwangu kulikuwa vikapu vitatu vya mikate. \v 17 Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kikapu nilichobeba kichwani.” \p \v 18 Yusufu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. \v 19 Baada ya siku tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.” \p \v 20 Siku ya tatu ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake. \v 21 Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mkononi mwa Farao tena. \v 22 Lakini akamwangika yule mwokaji mkuu, kama Yusufu alivyowafasiria. \p \v 23 Lakini mnyweshaji mkuu hakumkumbuka Yusufu, bali alimsahau. \c 41 \s1 Ndoto za Farao \p \v 1 Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto. Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, \v 2 wakati ng’ombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. \v 3 Baada yao ng’ombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea Mto Naili, wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. \v 4 Wale ng’ombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka. \p \v 5 Farao akaingia usingizini tena, akaota ndoto ya pili. Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja. \v 6 Baadaye, masuke mengine saba yakachipua, yakiwa membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki. \v 7 Masuke yale membamba yakameza yale masuke saba yenye afya na yaliyojaa. Basi Farao akaamka kutoka usingizini, na kumbe ilikuwa ndoto. \p \v 8 Kesho yake asubuhi, alifadhaika akilini. Hivyo akawaita waaguzi wote pamoja na watu wenye busara wa Misri. Walipokuja, Farao akawaeleza ndoto zake, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumfasiria. \p \v 9 Ndipo mnyweshaji mkuu alimwambia Farao, “Leo nimekumbushwa kosa langu. \v 10 Farao alipowakasirikia watumishi wake, alinifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa walinzi. \v 11 Katika usiku mmoja, kila mmoja wetu aliota ndoto, na kila ndoto ilikuwa na maana yake. \v 12 Basi kuna kijana Mwebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, mtumishi wa mkuu wa walinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupatia kila mtu tafsiri ya ndoto yake. \v 13 Nayo mambo yakawa jinsi alivyotufasiria ndoto zetu: Mimi nilirudishwa kazini mwangu, naye huyo mwingine akaangikwa.” \p \v 14 Basi, Farao akatuma Yusufu aitwe, naye akatolewa kifungoni haraka. Baada ya kunyoa na kubadilisha nguo zake, akaenda mbele ya Farao. \p \v 15 Farao akamwambia Yusufu, “Nimeota ndoto, wala hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuifasiri. Lakini nimesikia habari yako kwamba unapoelezwa ndoto unaweza kuifasiri.” \p \v 16 Yusufu akamjibu Farao, “Siwezi kuifasiri, lakini Mungu atampa Farao jibu analolihitaji.” \p \v 17 Kisha Farao akamwambia Yusufu, “Katika ndoto yangu nilikuwa nimesimama ukingoni mwa Mto Naili. \v 18 Nikawaona ng’ombe saba, wazuri na wanono, wakijitokeza kutoka mtoni, wakaja kujilisha kwenye matete. \v 19 Baada ya hao, ng’ombe wengine saba wadhaifu wakatokea, wabaya sana na waliokonda. Kamwe sikuwahi kuona ng’ombe wabaya jinsi hiyo katika nchi yote ya Misri. \v 20 Hao ng’ombe waliokonda na wabaya sana wakawala wale ng’ombe saba walionona waliojitokeza kwanza. \v 21 Lakini hata baada ya kuwala, hakuna mtu ambaye angeweza kusema kwamba wamekula, bado walionekana wabaya kama mwanzoni. Kisha nikaamka kutoka usingizini. \p \v 22 “Pia katika ndoto zangu niliona masuke saba ya nafaka, yamejaa na mazuri, yanakua katika bua moja. \v 23 Baada ya hayo, masuke mengine saba yakachipua, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki. \v 24 Yale masuke membamba ya nafaka yakayameza yale masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka. Nimewaeleza waaguzi, wala hakuna yeyote aliyeweza kunifasiria.” \p \v 25 Ndipo Yusufu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto hiyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. \v 26 Ng’ombe saba wazuri ni miaka saba, nayo masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka ni miaka saba; ni ndoto hiyo hiyo moja. \v 27 Ng’ombe saba waliokonda na wabaya waliojitokeza baadaye ni miaka saba, vivyo hivyo masuke saba ya ngano yaliyodhoofika na kukaushwa na upepo wa mashariki: Ni miaka saba ya njaa. \p \v 28 “Ni kama nilivyomwambia Farao. Mungu amemwonesha Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. \v 29 Miaka saba ya shibe inakuja katika nchi yote ya Misri, \v 30 lakini itafuata miaka saba ya njaa. Ndipo shibe yote ya Misri itasahaulika na njaa itaikumba nchi. \p \v 31 “Shibe iliyokuwa katika nchi haitakumbukwa, kwa sababu njaa itakayofuata itakuwa kali mno. \v 32 Sababu ya ndoto kumjia Farao kwa namna mbili ni kwamba jambo hilo Mungu ameshaamua kwa hakika, naye Mungu atalifanya karibuni. \p \v 33 “Basi sasa Farao na atafute mtu mwenye akili na hekima ili amweke kuwa msimamizi wa nchi ya Misri. \v 34 Farao na aweke wasimamizi nchini kote, wakusanye sehemu ya tano ya mavuno ya Misri katika miaka hii saba ya shibe. \v 35 Wakusanye chakula chote katika miaka hii saba ya neema inayokuja na kuhifadhi nafaka chini ya mamlaka ya Farao, iwe akiba ya chakula katika miji. \v 36 Chakula hiki kitakuwa akiba ya tahadhari kwa ajili ya nchi, ili kitumike katika ile miaka saba ya njaa itakayokuja Misri, ili nchi isiharibiwe na njaa.” \s1 Yusufu afanywa msimamizi wa Misri \p \v 37 Mpango huu ulionekana mzuri kwa Farao na kwa maafisa wake wote. \v 38 Hivyo Farao akawauliza, “Je, tunaweza kumpata yeyote kama mtu huyu, aliye na Roho wa Mungu ndani yake?” \p \v 39 Ndipo Farao akamwambia Yusufu, “Maadamu Mungu amekufunulia haya yote, hakuna yeyote mwenye akili na hekima kama wewe. \v 40 Wewe utakuwa msimamizi wa jumba langu la kifalme, na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.” \p \v 41 Kwa hiyo Farao akamwambia Yusufu, “Sasa nakuweka uwe msimamizi wa nchi yote ya Misri.” \v 42 Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yusufu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. \v 43 Akampandisha katika gari lake la vita kama msaidizi wake; watu wakamtangulia wakipaza sauti na kusema, “Fungueni njia!” Ndivyo Farao alimweka Yusufu kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri. \p \v 44 Kisha Farao akamwambia Yusufu, “Mimi ni Farao, lakini pasipo neno lako, hakuna mtu mwenye ruhusa kuinua mkono au mguu katika nchi yote ya Misri.” \v 45 Farao akamwita Yusufu jina Safenath-Panea; pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni\f + \fr 41:45 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Heliopoli \fqa*\ft (Mji wa jua)\ft*\f*, kuwa mke wake. Ndipo Yusufu akaitembelea nchi yote ya Misri. \p \v 46 Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao, mfalme wa Misri. Naye Yusufu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri. \v 47 Katika ile miaka saba ya shibe nchi ilizaa mazao kwa wingi sana. \v 48 Yusufu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya shibe nchini Misri, akakihifadhi katika miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo. \v 49 Yusufu alihifadhi nafaka nyingi, mfano wa mchanga wa bahari; ilikuwa nyingi mno kiasi kwamba walishindwa kuweka kumbukumbu kwa sababu akiba ilizidi kipimo. \p \v 50 Kabla ya miaka ya njaa kuanza, Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yusufu wana wawili wa kiume. \v 51 Yusufu akamwita mzaliwa wake wa kwanza jina Manase, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenifanya nisahau taabu zangu zote pamoja na jamaa yote ya nyumba ya baba yangu.” \v 52 Mwana wa pili akamwita jina Efraimu, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenistawisha katika nchi ya mateso yangu.” \p \v 53 Ile miaka saba ya shibe huko Misri ikaisha, \v 54 nayo miaka ile saba ya njaa ikaanza, sawasawa na alivyosema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi nyingine zote, bali katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula. \v 55 Nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao aliwaagiza Wamisri wote, “Nendeni kwa Yusufu, nanyi mfanye anachowaambia.” \p \v 56 Njaa ilipokuwa imeenea katika nchi yote, Yusufu akafungua maghala ya vyakula na kuwauzia Wamisri nafaka, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno katika nchi yote ya Misri. \v 57 Pia nchi nyingine zote zilikuja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yusufu, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno duniani kote. \c 42 \s1 Ndugu za Yusufu waenda Misri \p \v 1 Yakobo alipofahamu kuwa kuna nafaka kule Misri, akawaambia wanawe, “Mbona mnakaa tu hapa mkitazamana?” \v 2 Akaendelea kuwaambia, “Nimesikia kuwa huko Misri kuna nafaka. Teremkeni huko mkatununulie chakula, ili tuweze kuishi wala tusife.” \p \v 3 Ndipo ndugu kumi wa Yusufu wakateremka huko Misri kununua nafaka. \v 4 Lakini Yakobo hakumtuma Benyamini, ndugu yake Yusufu, pamoja na wengine, kwa sababu aliogopa asije akapatwa na madhara. \v 5 Hivyo wana wa Israeli walikuwa miongoni mwa wale walioenda Misri kununua nafaka, kwani njaa ilikuwa katika nchi ya Kanaani pia. \p \v 6 Wakati huo Yusufu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, na ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yusufu walifika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi. \v 7 Mara Yusufu alipowaona ndugu zake, akawatambua. Lakini akajifanya mgeni na kuzungumza nao kwa ukali, akiwauliza, “Ninyi mnatoka wapi?” \p Wakamjibu, “Tumetoka nchi ya Kanaani kuja kununua chakula.” \p \v 8 Ingawa Yusufu aliwatambua ndugu zake, wao hawakumtambua. \v 9 Ndipo Yusufu alipokumbuka ndoto zake kuwahusu, akawaambia, “Ninyi ni wapelelezi! Mmekuja kuangalia mahali nchi yetu haina ulinzi.” \p \v 10 Wakamjibu, “Sivyo, bwana. Watumishi wako wamekuja kununua chakula. \v 11 Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Watumishi wako ni watu waaminifu, wala sio wapelelezi.” \p \v 12 Akawaambia, “La, hasha! Mmekuja kuangalia mahali nchi yetu haina ulinzi.” \p \v 13 Lakini wakamjibu, “Watumishi wako walikuwa ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja ambaye anaishi katika nchi ya Kanaani. Sasa mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu, na mwingine alikufa.” \p \v 14 Yusufu akawaambia, “Kama nilivyowaambia: Ninyi ni wapelelezi! \v 15 Hivi ndivyo mtakavyojaribiwa: Hakika kama Farao aishivyo, hamtaondoka mahali hapa hadi ndugu yenu mdogo aje hapa. \v 16 Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu. Wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!” \v 17 Akawaweka wote chini ya ulinzi kwa siku tatu. \p \v 18 Siku ya tatu, Yusufu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu: \v 19 Ikiwa ninyi ni watu waaminifu, mmoja wa ndugu zenu na abaki kifungoni, nanyi wengine pelekeni nafaka kwa jamaa yenu wanaoteseka kwa njaa. \v 20 Lakini lazima mniletee ndugu yenu mdogo hapa, ili maneno yenu yathibitike na kwamba msife.” Wakakubali kufanya hivyo. \p \v 21 Wakaambiana wao kwa wao, “Hakika tunaadhibiwa kwa sababu ya ndugu yetu. Tuliona jinsi alivyohuzunika alipokuwa anatusihi kuokoa maisha yake, lakini hatukumsikiliza. Hiyo ndiyo sababu dhiki hii imetupata.” \p \v 22 Reubeni akawajibu, “Sikuwaambieni msitende dhambi dhidi ya kijana? Lakini hamkunisikiliza! Sasa ni lazima tuadhibiwe kwa ajili ya damu yake.” \v 23 Hawakujua kuwa Yusufu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani. \p \v 24 Yusufu akajitenga nao, akaanza kulia, kisha akawarudia na kuzungumza nao tena. Akaamuru Simeoni akamatwe na kufungwa mbele yao. \p \v 25 Yusufu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe chakula cha njiani. Baada ya kutendewa hayo yote, \v 26 wakapakiza nafaka juu ya punda wao, wakaondoka. \p \v 27 Walipofika mahali pa kulala huko njiani, mmoja wao akafungua gunia lake ili amlishe punda wake; akakuta fedha yake ndani ya gunia lake. \v 28 Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.” \p Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?” \p \v 29 Walipofika kwa Yakobo baba yao katika nchi ya Kanaani, wakamweleza mambo yote yaliyowapata. Wakasema, \v 30 “Huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alisema nasi kwa ukali, akatutendea kana kwamba sisi tulikuwa tunaipeleleza nchi. \v 31 Lakini tulimwambia, ‘Sisi ni watu waaminifu, sio wapelelezi. \v 32 Tulizaliwa ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja. Mmoja alikufa, na mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu huko Kanaani.’ \p \v 33 “Ndipo huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alipotuambia, ‘Hivi ndivyo nitafahamu kuwa ninyi ni watu waaminifu: Mwacheni mmoja wa ndugu zenu hapa kwangu, kisha nendeni mpeleke chakula kwa jamaa yenu inayoteseka kwa njaa. \v 34 Lakini mleteni huyo ndugu yenu mdogo kwangu. Ndipo nitajua kuwa ninyi sio wapelelezi, ila ni watu waaminifu. Kisha nitamrudisha ndugu yenu, nanyi mtaweza kufanya biashara katika nchi hii.’ ” \p \v 35 Walipokuwa wanamimina nafaka kutoka magunia yao, tazama! Wakapata ndani ya gunia la kila mtu mfuko wa fedha. Wakati wao na baba yao waliona mifuko ya fedha, wakaogopa. \v 36 Yakobo baba yao akawaambia, “Ninyi mmenipokonya watoto wangu. Yusufu hayupo na Simeoni hayupo; tena na sasa mnataka kumchukua Benyamini. Kila kitu ni kinyume nami!” \p \v 37 Ndipo Reubeni akamwambia baba yake, “Unaweza kuwaua wanangu wote wawili, ikiwa sitamrudisha Benyamini kwako. Mkabidhi Benyamini katika uangalizi wangu, nami nitamrudisha.” \p \v 38 Lakini Yakobo akasema, “Mwanangu hatashuka huko pamoja nanyi; ndugu yake amekufa, naye ndiye peke yake aliyebaki. Akipatwa na madhara katika safari mnayoiendea, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini kwa masikitiko.” \c 43 \s1 Safari ya pili kwenda Misri \p \v 1 Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi. \v 2 Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine.” \p \v 3 Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena hadi mje na ndugu yenu.’ \v 4 Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutaenda kuwanunulia chakula. \v 5 Lakini ikiwa hutamruhusu aende, hatutaenda, kwa sababu mtu yule alituambia, ‘Hamtauona uso wangu tena hadi mje na ndugu yenu.’ ” \p \v 6 Israeli akauliza, “Kwa nini mkaniletea taabu hii kwa kumwambia yule mtu mlikuwa na ndugu mwingine?” \p \v 7 Wakamjibu, “Yule mtu alituhoji kwa undani sana habari zetu na za jamaa yetu. Alituuliza, ‘Je, baba yenu bado angali hai? Je, mnaye ndugu mwingine?’ Sisi tulimjibu maswali yake tu. Tungewezaje kujua kwamba angesema, ‘Mleteni mdogo yenu hapa’?” \p \v 8 Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara moja, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife. \v 9 Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake; mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Nisipomrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote. \v 10 Hakika, kama hatukuchelewa kuondoka, tungekuwa tumeenda na kurudi mara mbili.” \p \v 11 Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni sehemu ya bidhaa bora za nchi katika mifuko yenu, na mmpelekee yule mtu kama zawadi: zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi. \v 12 Chukueni fedha mara mbili, kwa kuwa mtazirudisha zile fedha zilizowekwa midomoni mwa magunia yenu. Labda ziliwekwa kwa makosa. \v 13 Mchukueni ndugu yenu pia, mrudi kwa huyo mtu mara moja. \v 14 Naye Mungu Mwenyezi\f + \fr 43:14 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f* awajalie rehema mbele ya huyo mtu ili apate kumwachia yule ndugu yenu na Benyamini mweze kurudi pamoja. Kwangu mimi, kama nikufiwa, nimefiwa.” \p \v 15 Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na wakajionesha kwa Yusufu. \v 16 Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Wachukue watu hawa nyumbani mwangu, mchinje mnyama na kuandalia chakula, kwa kuwa watakula chakula cha mchana pamoja nami.” \p \v 17 Msimamizi akafanya kama Yusufu alivyomwambia na akawachukua wale watu nyumbani mwa Yusufu. \v 18 Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani mwa Yusufu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda wetu.” \p \v 19 Hivyo wakamwendea msimamizi wa nyumba wa Yusufu na kuzungumza naye kwenye ingilio la nyumba. \v 20 Wakasema, “Tafadhali bwana, tulikuja hapa mara ya kwanza kununua chakula. \v 21 Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake katika gunia lake, kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha. \v 22 Pia tumeleta fedha nyingine kwa ajili ya kununulia chakula. Hatujui ni nani aliziweka fedha hizo katika magunia yetu.” \p \v 23 Akawaambia, “Vema, msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni. \p \v 24 Msimamizi akawapeleka wale watu nyumbani mwa Yusufu, akawapa maji ya kunawa miguu, na kuwapa punda wao majani. \v 25 Wakaandaa zawadi zao ili wampe Yusufu atakapofika adhuhuri, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba watakula chakula huko. \p \v 26 Yusufu alipokuja nyumbani, walimkabidhi zile zawadi ambazo walikuwa wamezileta mle nyumbani, nao wakamsujudia. \v 27 Akawauliza kuhusu hali yao, kisha akawaambia, “Yule baba yenu mzee mliyeniambia habari zake, yu hali gani? Je, bado yu hai?” \p \v 28 Wakamjibu, “Mtumishi wako, baba yetu, bado anaishi na ni mzima.” Kisha wakainama, wakamsujudia. \p \v 29 Alipotazama na kumwona Benyamini ndugu yake, mwana wa mama yake hasa, akauliza, “Je, huyu ndiye ndugu yenu wa mwisho, ambaye mlinieleza habari zake?” Ndipo akasema, “Mungu na akufadhili, mwanangu.” \v 30 Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yusufu akaondoka kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo. \p \v 31 Baada ya kunawa uso wake, akarudi; huku akijizuia kulia, akasema, “Pakueni chakula.” \p \v 32 Wakampakulia Yusufu peke yake, nao ndugu zake peke yao, na Wamisri waliokula pamoja naye peke yao, kwa sababu Wamisri wasingeweza kula pamoja na Waebrania, kwa maana ilikuwa ni chukizo kwa Wamisri. \v 33 Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao. \v 34 Walipopelekewa sehemu ya chakula kutoka meza ya Yusufu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye. \c 44 \s1 Kikombe cha fedha ndani ya gunia \p \v 1 Kisha Yusufu akampa yule msimamizi wa nyumbani mwake maagizo haya: “Jaza magunia ya watu hawa kiasi cha chakula ambacho wanaweza kuchukua, na uweke fedha ya kila mtu katika gunia lake. \v 2 Kisha weka kikombe changu kile cha fedha katika gunia la yule mdogo wa wote, pamoja na fedha zake ambazo alinunulia nafaka yake.” Naye akafanya kama Yusufu alivyosema. \p \v 3 Kulipopambazuka, hao watu wakaruhusiwa kuondoka pamoja na punda wao. \v 4 Kabla hawajafika mbali kutoka mjini, Yusufu akamwambia mtumishi wake, “Wafuatilie wale watu mara moja; utakapowakuta, waambie, ‘Kwa nini mmelipiza wema kwa ubaya? \v 5 Je, kikombe hiki sicho anachonywea bwana wangu, na pia hukitumia kwa kubashiri? Hili ni jambo ovu mlilolitenda.’ ” \p \v 6 Alipowafikia, akarudia maneno haya kwao. \v 7 Lakini wakamwambia mtumishi, “Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Liwe mbali na watumishi wako kufanya jambo kama hilo! \v 8 Tazama, tulikurudishia zile fedha kutoka nchi ya Kanaani ambazo tulizikuta kwenye magunia yetu. Hivyo, kwa nini tuibe fedha au dhahabu kutoka nyumbani mwa bwana wako? \v 9 Ikiwa yeyote miongoni mwa watumishi wako atapatikana nacho, auawe, na sisi wengine tutakuwa watumwa wa bwana wangu.” \p \v 10 Akajibu, “Vema sana; na iwe kama msemavyo. Yeyote atakayekutwa nacho atakuwa mtumwa wangu, lakini ninyi wengine mtakuwa hamna lawama.” \p \v 11 Kila mmoja wao akafanya haraka kushusha gunia lake chini na kulifungua. \v 12 Ndipo msimamizi akaendelea kutafuta, akianzia kwa mkubwa wa wote na akaishia kwa mdogo wa wote. Basi kikombe kikapatikana katika gunia la Benyamini. \v 13 Kwa hilo, wakararua nguo zao. Ndipo wote wakapakiza mizigo yao juu ya punda wao na kurudi mjini. \p \v 14 Yusufu alikuwa bado yuko nyumbani mwake Yuda na ndugu zake walipoingia. Wote wakajitupa chini mbele yake. \v 15 Yusufu akawaambia, “Ni jambo gani hili mlilolifanya? Hamjui kuwa mtu kama mimi anaweza kufahamu mambo kwa njia ya kubashiri?” \p \v 16 Yuda akajibu, “Tuseme nini kwa bwana wangu? Tutaweza kuzungumza nini? Tutawezaje kuthibitisha kwamba hatuna hatia? Mungu amefunua hatia ya watumishi wako. Sasa sisi tu watumwa wa bwana wangu, sisi pamoja na yule aliyepatikana na kikombe.” \p \v 17 Lakini Yusufu akasema, “Liwe mbali nami kufanya jambo kama hili! Mtu yule tu aliyekutwa na kikombe ndiye atakuwa mtumwa wangu. Ninyi wengine rudini kwa baba yenu kwa amani.” \p \v 18 Ndipo Yuda akamwendea na kumwambia: “Tafadhali bwana wangu, mruhusu mtumishi wako aseme neno kwa bwana wangu. Usimkasirikie mtumishi wako, ingawa wewe ni sawa na Farao mwenyewe. \v 19 Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, ‘Mnaye baba au ndugu?’ \v 20 Nasi tukakujibu, ‘Tunaye baba yetu ambaye ni mzee; pia yupo mwanawe mdogo aliyezaliwa katika uzee wake. Ndugu yake amekufa, na huyu mdogo ndiye mwana pekee kwa mama yake aliyebaki, naye baba yake anampenda.’ \p \v 21 “Ndipo ulipowaambia watumishi wako, ‘Mleteni kwangu ili niweze kumwona kwa macho yangu mwenyewe.’ \v 22 Nasi tukamwambia bwana wangu, ‘Kijana hawezi kumwacha baba yake; akimwacha, baba yake atakufa.’ \v 23 Lakini ukawaambia watumishi wako, ‘Ndugu yenu mdogo asiposhuka pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.’ \v 24 Tuliporudi kwa mtumwa wako baba yangu, tulimwambia lile bwana wangu alilokuwa amesema. \p \v 25 “Ndipo baba yetu alisema, ‘Rudini Misri mkanunue chakula kingine.’ \v 26 Lakini tukamwambia, ‘Hatuwezi kushuka Misri hadi ndugu yetu mdogo awe pamoja nasi ndipo tutaenda. Hatutaweza kuuona uso wa yule mtu hadi ndugu yetu mdogo awe pamoja nasi.’ \p \v 27 “Mtumwa wako baba yangu alituambia, ‘Mnajua mke wangu alinizalia wana wawili. \v 28 Mmoja alipotea, nami nikasema, “Hakika ameraruliwa vipande vipande.” Nami sijamwona tangu wakati huo. \v 29 Ikiwa mtaniondolea huyu tena na akapatwa na madhara, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini nikiwa mwenye huzuni.’ \p \v 30 “Hivyo sasa, kama kijana hatakuwa pamoja nasi nitakaporudi kwa mtumishi wako baba yangu, na kama baba yangu, ambaye maisha yake yamefungamanishwa na uhai wa kijana huyu, \v 31 akiona kijana hayupo nasi, atakufa. Watumishi wako watashusha kichwa chenye mvi cha baba yetu kaburini kwa huzuni. \v 32 Mtumwa wako alimhakikishia baba yangu usalama wa kijana. Nikamwambia, ‘Kama sitamrudisha kwako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako, baba yangu, maisha yangu yote!’ \p \v 33 “Sasa basi, tafadhali mruhusu mtumishi wako abaki hapa kama mtumwa wa bwana wangu badala ya kijana, naye kijana umruhusu arudi na ndugu zake. \v 34 Ninawezaje kurudi kwa baba yangu kama kijana hatakuwa pamoja nami? La hasha! Usiniache nikaone huzuni ile itakayompata baba yangu.” \c 45 \s1 Yusufu ajitambulisha \p \v 1 Basi Yusufu hakuweza kujizuia tena mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye. Akapaza sauti, akasema, “Mwondoeni kila mtu mbele yangu!” Kwa hiyo hapakuwa mtu mwingine na Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake. \v 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari. \p \v 3 Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yusufu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake. \p \v 4 Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake, “Sogeeni karibu nami.” Waliposogea, akasema, “Mimi ni ndugu yenu Yusufu, yule ambaye mlimuuza Misri! \v 5 Sasa msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. \v 6 Kwa miaka miwili sasa njaa imekuwa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwa na kulima wala kuvuna. \v 7 Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuwahifadhia mabaki katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu. \p \v 8 “Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kama baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote. \v 9 Sasa rudini haraka kwa baba yangu, mkamwambie, ‘Hili ndilo mwanao Yusufu asemalo: Mungu amenifanya mimi kuwa mtawala wa Misri yote. Shuka uje kwangu, wala usikawie. \v 10 Nawe utaishi katika nchi ya Gosheni na kuwa karibu nami: wewe, watoto wako na wajukuu wako, makundi yako ya kondoo, mbuzi na ng’ombe, pamoja na vyote ulivyo navyo. \v 11 Nitawatunza huko, kwa sababu bado iko miaka mingine mitano inayokuja ya njaa. La sivyo, wewe na nyumba yako na wote ulio nao mtakuwa fukara.’ \p \v 12 “Mnaweza kujionea wenyewe, hata ndugu yangu Benyamini, kwamba hakika ni mimi ninayezungumza nanyi. \v 13 Mwambieni baba yangu kuhusu heshima yote niliyopewa huku Misri, na kuhusu kila kitu mlichokiona. Mleteni baba yangu huku haraka.” \p \v 14 Ndipo akamkumbatia Benyamini ndugu yake na kulia, naye Benyamini akamkumbatia akilia. \v 15 Pia akawabusu ndugu zake wote, huku akilia. Baada ya hayo, ndugu zake wakazungumza naye. \p \v 16 Habari zilipofika kwenye jumba la Farao kwamba ndugu zake Yusufu wamefika, Farao na maafisa wake wote wakafurahi. \v 17 Farao akamwambia Yusufu, “Waambie ndugu zako, ‘Fanyeni hivi: Pakieni wanyama wenu mrudi hadi nchi ya Kanaani, \v 18 mkamlete baba yenu na jamaa zenu kwangu. Nitawapa sehemu nzuri sana ya nchi ya Misri, nanyi mtafurahia unono wa nchi.’ \p \v 19 “Mnaagizwa pia kuwaambia, ‘Fanyeni hivi: Chukueni magari ya kukokotwa kutoka Misri kwa ajili ya watoto wenu na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje. \v 20 Msijali kamwe kuhusu mali yenu, kwa sababu mema yote ya Misri yatakuwa yenu.’ ” \p \v 21 Hivyo wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yusufu akawapa magari ya kukokotwa kama Farao alivyoagiza, na pia akawapa chakula cha safari yao. \v 22 Akampa kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli mia tatu\f + \fr 45:22 \fr*\ft Shekeli 300 za fedha ni sawa na kilo 3.4.\ft*\f* za fedha, na jozi tano za nguo. \v 23 Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliobeba vitu vizuri vya Misri, punda jike kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari. \v 24 Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!” \p \v 25 Basi wakatoka Misri na kufika kwa baba yao Yakobo katika nchi ya Kanaani. \v 26 Wakamwambia baba yao, “Yusufu angali hai! Ukweli ni kwamba yeye ndiye mtawala wa Misri yote.” Yakobo akapigwa na bumbuazi; hakuwasadiki. \v 27 Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yusufu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yusufu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa. \v 28 Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yusufu bado yu hai. Nitaenda nikamwone kabla sijafa.” \c 46 \s1 Yakobo aenda Misri \p \v 1 Hivyo Israeli akaondoka na mali yake yote. Alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaka baba yake. \p \v 2 Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!” \p Akamjibu, “Mimi hapa.” \p \v 3 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. \v 4 Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yusufu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.” \p \v 5 Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba, nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo, na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao alikuwa amempelekea kumsafirisha. \v 6 Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani; Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. \v 7 Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote hadi Misri. \b \lh \v 8 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), walioenda Misri: \b \li1 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. \li1 \v 9 Wana wa Reubeni ni: \li2 Hanoki, Palu, Hesroni, na Karmi. \li1 \v 10 Wana wa Simeoni ni: \li2 Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari, na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. \li1 \v 11 Wana wa Lawi ni: \li2 Gershoni, Kohathi, na Merari. \li1 \v 12 Wana wa Yuda ni: \li2 Eri, Onani, Shela, Peresi, na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). \li2 Wana wa Peresi ni: \li3 Hesroni na Hamuli. \li1 \v 13 Wana wa Isakari ni: \li2 Tola, Puva, Yashubu, na Shimroni. \li1 \v 14 Wana wa Zabuloni ni: \li2 Seredi, Eloni, na Yaleeli. \lf \v 15 Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu, pamoja na binti yake Dina. Jumla ya hawa wanawe wa kiume na wa kike walikuwa thelathini na watatu. \b \li1 \v 16 Wana wa Gadi ni: \li2 Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi, na Areli. \li1 \v 17 Wana wa Asheri ni: \li2 Imna, Ishva, Ishvi, na Beria. Dada yao alikuwa Sera. \li2 Wana wa Beria ni: \li3 Heberi na Malkieli. \lf \v 18 Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita. \b \li1 \v 19 Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni: \li2 Yusufu na Benyamini. \li3 \v 20 Huko Misri, Asenathi binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni\f + \fr 46:20 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Heliopoli \fqa*\ft (Mji wa jua)\ft*\f*, alimzalia Yusufu wana wawili: Manase na Efraimu. \li1 \v 21 Wana wa Benyamini ni: \li2 Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu, na Ardi. \lf \v 22 Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne. \b \li1 \v 23 Mwana wa Dani ni: \li2 Hushimu. \li1 \v 24 Wana wa Naftali ni: \li2 Yaseeli, Guni, Yeseri, na Shilemu. \lf \v 25 Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba. \b \lf \v 26 Wote walioenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe wake, walikuwa watu sitini na sita. \v 27 Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yusufu huko Misri, jumla ya jamaa ya Yakobo walioenda Misri walikuwa sabini. \b \p \v 28 Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yusufu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni, \v 29 Yusufu aliandaa gari lake la vita, na akaenda Gosheni kumlaki baba yake, Israeli. Mara Yusufu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu. \p \v 30 Israeli akamwambia Yusufu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.” \p \v 31 Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, walioishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu. \v 32 Watu hao ni wafugaji; wao huchunga mifugo, na wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ng’ombe, pamoja na kila kitu walicho nacho.’ \v 33 Farao atakapowaita na kuwauliza, ‘Kazi yenu ni nini?’ \v 34 mjibuni, ‘Watumishi wako wamekuwa wafugaji wa wanyama tangu ujana wetu hadi sasa, kama baba zetu walivyokuwa.’ Ndipo mtaruhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wafugaji wote ni chukizo kwa Wamisri.” \c 47 \s1 Yakobo ambariki Farao \p \v 1 Yusufu akaenda na kumwambia Farao, “Baba yangu na ndugu zangu wamekuja kutoka nchi ya Kanaani wakiwa na makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng’ombe, pamoja na kila kitu walicho nacho, nao sasa wako Gosheni.” \v 2 Akawachagua ndugu zake watano na kuwapeleka mbele ya Farao. \p \v 3 Farao akawauliza hao ndugu zake, “Kazi yenu ni nini?” \p Wakamjibu, “Watumishi wako ni wafugaji, kama baba zetu walivyokuwa.” \v 4 Pia wakamwambia Farao, “Tumekuja kukaa huku kwa muda mfupi, kwa sababu njaa ni kali huko Kanaani, na mifugo ya watumishi wako haina malisho. Kwa hiyo sasa, tafadhali uruhusu watumishi wako wakae huko Gosheni.” \p \v 5 Farao akamwambia Yusufu, “Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako, \v 6 nayo nchi ya Misri ipo mbele yako; wakalishe baba yako na ndugu zako katika sehemu iliyo bora kupita zote katika nchi. Na waishi Gosheni. Kama unawafahamu walio na uwezo maalum miongoni mwao, wafanye kuwa wasimamizi wa mifugo yangu.” \p \v 7 Ndipo Yusufu akamleta Yakobo baba yake na kumtambulisha mbele ya Farao. Baada ya Yakobo kumbariki Farao, \v 8 Farao akamuuliza, “Je, una umri gani?” \p \v 9 Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka mia moja na thelathini. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya maisha ya baba zangu.” \v 10 Yakobo akambariki Farao, kisha akaondoka mbele yake. \p \v 11 Ndipo Yusufu akawakalisha baba yake na ndugu zake katika nchi ya Misri, akawapa milki katika sehemu bora sana ya nchi, ile wilaya ya Ramesesi, kama Farao alivyoelekeza. \v 12 Pia Yusufu akampa baba yake, na ndugu zake, na wote wa nyumbani mwa baba yake vyakula, kulingana na hesabu ya watoto wao. \s1 Uongozi wa Yusufu wakati wa njaa \p \v 13 Hata hivyo, hapakuwa na chakula katika eneo lote; kwa kuwa njaa ilikuwa kali sana; Misri na Kanaani zote zikaharibiwa kwa sababu ya njaa. \v 14 Yusufu akakusanya fedha zote zilizopatikana kutoka mauzo ya nafaka huko Misri na Kanaani, akazileta kwenye jumba la kifalme la Farao. \v 15 Fedha za watu wa Misri na Kanaani zilipokwisha, Wamisri wote wakamjia Yusufu na kumwambia, “Tupatie chakula. Kwa nini tufe mbele ya macho yako? Fedha zetu zimekwisha.” \p \v 16 Yusufu akawaambia, “Basi leteni mifugo yenu. Nitawauzia chakula kwa kubadilisha na mifugo yenu, kwa kuwa fedha zenu zimekwisha.” \v 17 Kwa hiyo wakaleta mifugo yao kwa Yusufu, naye akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo na mbuzi, ng’ombe, na punda wao. Katika mwaka huo wote Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote. \p \v 18 Mwaka ule ulipokwisha, wakamjia mwaka uliofuata na kumwambia, “Hatuwezi kuficha ukweli mbele za bwana wetu kwamba, kwa kuwa fedha zetu zimekwisha na wanyama wetu ni mali yako, sasa hakuna chochote kilichosalia kwa ajili ya bwana wetu isipokuwa miili yetu na ardhi yetu. \v 19 Kwa nini tuangamie mbele ya macho yako, sisi pamoja na nchi yetu? Tununue sisi pamoja na ardhi yetu ili kubadilishana kwa chakula. Nasi pamoja na nchi yetu tutakuwa watumwa wa Farao. Tupe sisi mbegu ili tuweze kuishi wala tusife, nchi yetu isije ikawa ukiwa.” \p \v 20 Kwa hiyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Wamisri, mmoja baada ya mwingine, waliuza mashamba yao, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana kwao. Nchi ikawa mali ya Farao, \v 21 naye Yusufu akawafanya watu watumike kama watumwa, kuanzia upande mmoja wa Misri hadi upande mwingine. \v 22 Hata hivyo hakununua nchi ya makuhani, kwa sababu walipokea mgawo wao wa kawaida kutoka kwa Farao, nao walikuwa na chakula cha kuwatosha kutokana na mgawo waliopewa na Farao. Hii ndiyo sababu hawakuuza ardhi yao. \p \v 23 Yusufu akawaambia watu, “Kwa vile nimewanunua ninyi pamoja na nchi yenu leo kuwa mali ya Farao, hapa kuna mbegu kwa ajili yenu ili mweze kuziotesha. \v 24 Lakini wakati mazao yatakapokuwa tayari, mpeni Farao sehemu ya tano. Sehemu hizo nne zitakazobaki mtaziweka kama mbegu kwa ajili ya mashamba, na kwa ajili ya chakula chenu wenyewe, na cha watu wa nyumbani mwenu na watoto wenu.” \p \v 25 Wakamwambia, “Umeokoa maisha yetu. Basi na tupate kibali mbele ya macho ya bwana wetu; tutakuwa watumwa wa Farao.” \p \v 26 Basi Yusufu akaiweka iwe sheria ya ardhi katika nchi ya Misri, ambayo inatumika hata leo, kwamba sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni ardhi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao. \p \v 27 Basi Waisraeli wakaishi Misri katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali huko, wakastawi na kuongezeka kwa idadi. \p \v 28 Yakobo akaishi Misri miaka kumi na saba, nayo miaka ya maisha yake ilikuwa mia moja na arobaini na saba (147). \v 29 Wakati ulipokaribia wa Israeli kufa, akamwita mwanawe Yusufu na kumwambia, “Kama nimepata kibali machoni pake, weka mkono wako chini ya paja langu na uniahidi kuwa utanifanyia fadhili na uaminifu. Usinizike Misri, \v 30 lakini nitakapopumzika na baba zangu, unichukue kutoka Misri, ukanizike walipozikwa.” \p Yusufu akamwambia, “Nitafanya kama unavyosema.” \p \v 31 Akamwambia, “Niapie.” Ndipo Yusufu akamwapia, naye Israeli akaabudu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake. \c 48 \s1 Manase na Efraimu \p \v 1 Baada ya muda Yusufu akaambiwa, “Baba yako ni mgonjwa.” Kwa hiyo akawachukua wanawe wawili Manase na Efraimu pamoja naye. \v 2 Yakobo alipoambiwa, “Mwanao Yusufu amekuja kukuona,” Israeli akajitia nguvu, akaketi kitandani. \p \v 3 Yakobo akamwambia Yusufu, “Mungu Mwenyezi\f + \fr 48:3 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f* alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani. Akanibariki, \v 4 naye akaniambia, ‘Nitakufanya ustawi na uongezeke kwa idadi. Nitakufanya kuwa jamii ya mataifa, nami nitakupa nchi hii uimiliki milele, wewe na wazao wako baada yako.’ \p \v 5 “Sasa basi, wanao wawili waliozaliwa kwako huku Misri kabla sijaja hapa kwako watahesabiwa kuwa wangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu, vile Reubeni na Simeoni walivyo wangu. \v 6 Lakini watoto utakaowazaa baada yao watakuwa wako. Katika nchi watakayoirithi, watatambuliwa kwa jina la ndugu zao. \v 7 Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, nilihuzunika sana kwa sababu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrata. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrata” (yaani Bethlehemu). \p \v 8 Israeli alipowaona wana wa Yusufu, akauliza, “Hawa ni nani?” \p \v 9 Yusufu akamjibu baba yake, “Hawa ni wana ambao Mungu amenipa nikiwa huku.” \p Ndipo Israeli akasema, “Walete kwangu ili niwabariki.” \p \v 10 Basi macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee, naye aliona kwa shida. Kwa hiyo Yusufu akawaleta wanawe karibu na baba yake, naye Israeli akawabusu na kuwakumbatia. \p \v 11 Israeli akamwambia Yusufu, “Kamwe sikutazamia kuuona uso wako tena, lakini sasa Mungu ameniruhusu kuwaona watoto wako pia.” \p \v 12 Ndipo Yusufu akawaondoa wanawe magotini mwa Israeli, naye akasujudu, uso wake ukagusa chini. \v 13 Yusufu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao. \v 14 Lakini Israeli akaupeleka mkono wake wa kuume, akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, ingawa ndiye alikuwa mdogo; nao mkono wake wa kushoto, ukipishana na mkono wa kuume, akauweka juu ya kichwa cha Manase, ingawa Manase ndiye alikuwa mzaliwa wa kwanza. \p \v 15 Ndipo akambariki Yusufu akisema, \q1 “Mungu ambaye baba zangu \q2 Ibrahimu na Isaka walimtii, \q1 Mungu ambaye amekuwa mchungaji \q2 wa maisha yangu yote hadi leo, \q1 \v 16 Malaika ambaye aliniokoa kutoka madhara yote, \q2 yeye na awabariki vijana hawa. \q1 Na waitwe kwa jina langu \q2 na kwa majina ya baba zangu \q2 Ibrahimu na Isaka, \q1 wao na waongezeke kwa wingi \q2 katika dunia.” \p \v 17 Yusufu alipoona baba yake akiweka mkono wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, hakupendezwa, kwa hiyo akauchukua mkono wa baba yake kutoka kichwa cha Efraimu na kuuweka juu ya kichwa cha Manase. \v 18 Yusufu akamwambia, “Hapana, baba yangu, huyu ndiye mzaliwa wa kwanza; uweke mkono wako wa kuume juu ya kichwa chake.” \p \v 19 Lakini baba yake akakataa, akasema, “Ninajua, mwanangu, ninajua. Yeye pia atakuwa taifa, naye pia atakuwa mkuu. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, nao wazao wake watakuwa kundi la mataifa.” \v 20 Akawabariki siku ile na kusema, \q1 “Kwa jina lenu Israeli watatamka baraka hii: \q2 ‘Mungu na awafanye kama Efraimu na Manase.’ ” \m Kwa hiyo akamtanguliza Efraimu mbele ya Manase. \p \v 21 Ndipo Israeli akamwambia Yusufu, “Ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu. \v 22 Kwako wewe, kama aliye juu ya ndugu zako, ninakupa sehemu moja zaidi ya ndugu zako, lile eneo nililoteka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu.” \c 49 \s1 Yakobo abariki wanawe \p \v 1 Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni, mnizunguke ili niweze kuwaambia yale yatakayowatokea siku zijazo. \q1 \v 2 “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo; \q2 msikilizeni baba yenu Israeli. \b \q1 \v 3 “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, \q2 nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu; \q2 umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. \q1 \v 4 Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, \q2 kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, \q2 kwenye kitanda changu na kukinajisi. \b \q1 \v 5 “Simeoni na Lawi ni ndugu: \q2 panga zao ni silaha za jeuri. \q1 \v 6 Mimi na nisiingie katika baraza lao, \q2 nami nisiunganike katika kusanyiko lao, \q1 kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, \q2 na kukata mishipa ya miguu ya mafahali \q2 kama walivyopenda. \q1 \v 7 Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, \q2 nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! \q1 Nitawatawanya katika Yakobo, \q2 na kuwasambaza katika Israeli. \b \q1 \v 8 “Yuda, ndugu zako watakusifu; \q2 mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; \q2 wana wa baba yako watakusujudia. \q1 \v 9 Ee Yuda, wewe ni mwana simba; \q2 unarudi toka mawindoni, mwanangu. \q1 Kama simba hunyemelea na kulala chini, \q2 kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? \q1 \v 10 Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, \q2 wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, \q1 hadi aje yeye ambaye milki ni yake, \q2 ambaye utii wa mataifa ni wake. \q1 \v 11 Atamfunga punda wake katika mzabibu, \q2 naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; \q1 atafua mavazi yake katika divai, \q2 majoho yake katika damu ya mizabibu. \q1 \v 12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, \q2 meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. \b \q1 \v 13 “Zabuloni ataishi pwani ya bahari \q2 na kuwa bandari za kuegesha meli; \q2 mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni. \b \q1 \v 14 “Isakari ni punda mwenye nguvu \q2 ambaye amelala kati ya mizigo yake. \q1 \v 15 Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika \q2 na jinsi nchi yake inavyopendeza, \q1 atainamisha bega lake kwenye mzigo \q2 na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu. \b \q1 \v 16 “Dani atahukumu watu wake kwa haki \q2 kama mmoja wa makabila ya Israeli. \q1 \v 17 Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, \q2 nyoka mwenye sumu kando ya njia, \q1 yule aumaye visigino vya farasi \q2 ili yule ampandaye aanguke chali. \b \q1 \v 18 “Ee Mwenyezi Mungu, nautafuta wokovu wako. \b \q1 \v 19 “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, \q2 lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. \b \q1 \v 20 “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, \q2 naye atatoa chakula kitamu kinachomfaa mfalme. \b \q1 \v 21 “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru \q2 azaaye watoto wazuri. \b \q1 \v 22 “Yusufu ni mzabibu uzaao, \q2 mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, \q2 ambao matawi yake hutanda ukutani. \q1 \v 23 Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, \q2 wakampiga mshale kwa ukatili. \q1 \v 24 Lakini upinde wake ulibaki imara, \q2 mikono yake ikatiwa nguvu, \q1 na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, \q2 kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, \q1 \v 25 kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, \q2 kwa sababu ya Mwenyezi\f + \fr 49:25 \fr*\ft Mwenyezi hapa ina maana ya \ft*\fqa Shaddai \fqa*\ft kwa Kiebrania.\ft*\f*, yeye anayekubariki \q1 kwa baraka za juu mbinguni, \q2 baraka za kilindi kilichoko chini, \q2 baraka za matitini na za tumbo la uzazi. \q1 \v 26 Baraka za baba yako ni kubwa \q2 kuliko baraka za milima ya kale, \q2 nyingi kuliko vilima vya kale. \q1 Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yusufu, \q2 juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. \b \q1 \v 27 “Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye njaa kuu; \q2 asubuhi hurarua mawindo yake, \q2 jioni hugawa nyara.” \p \v 28 Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka iliyomfaa. \s1 Kifo cha Yakobo \p \v 29 Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti, \v 30 pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua liwe mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. \v 31 Huko ndiko Ibrahimu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaka na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. \v 32 Shamba hilo na pango lililo ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.” \p \v 33 Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake. \c 50 \p \v 1 Basi Yusufu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu. \v 2 Ndipo Yusufu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze, \v 3 wakatumia siku arobaini, muda uliohitajika kutia dawa asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini. \p \v 4 Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yusufu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni, \v 5 ‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ” \p \v 6 Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.” \p \v 7 Hivyo Yusufu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake, na watu mashuhuri wote wa Misri. \v 8 Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani mwa Yusufu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng’ombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni. \v 9 Magari ya vita na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana. \p \v 10 Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu. Yusufu akakaa huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake. \v 11 Wakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu.\f + \fr 50:11 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Maombolezo ya Wamisri\fqa*\f* \p \v 12 Hivyo wana wa Yakobo wakafanya kama baba yao alivyowaagiza: \v 13 Wakamchukua hadi nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Ibrahimu alilinunua kutoka kwa Efroni Mhiti pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia. \v 14 Baada ya Yusufu kumzika baba yake, akarudi Misri pamoja na ndugu zake na wale wote waliokuwa wameenda naye kumzika baba yake. \s1 Yusufu awaondolea ndugu zake mashaka \p \v 15 Ndugu zake Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yusufu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” \v 16 Kwa hiyo wakampelekea Yusufu ujumbe, wakasema, “Kabla baba yako hajafa aliacha maagizo haya: \v 17 ‘Hili ndilo mtakalomwambia Yusufu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako.” Ujumbe huu ulipomfikia, Yusufu akalia. \p \v 18 Ndipo ndugu zake wakaja na kujitupa chini mbele yake. Wakasema, “Sisi ni watumwa wako.” \p \v 19 Lakini Yusufu akawaambia, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? \v 20 Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. \v 21 Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu.” Akawafariji na kusema nao kwa wema. \s1 Kifo cha Yusufu \p \v 22 Yusufu akakaa katika nchi ya Misri, yeye pamoja na jamaa yote ya baba yake. Akaishi miaka mia moja na kumi, \v 23 naye akaona kizazi cha tatu cha watoto wa Efraimu. Pia akaona watoto wa Makiri mwana wa Manase, wakawekwa magotini mwa Yusufu walipozaliwa. \p \v 24 Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Ibrahimu, Isaka na Yakobo.” \v 25 Naye Yusufu akawaapisha wana wa Israeli na kuwaambia, “Hakika Mungu atawasaidia, nanyi ni lazima mhakikishe mmepandisha mifupa yangu kutoka mahali hapa.” \p \v 26 Kwa hiyo Yusufu akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. Baada ya kumtia dawa asioze, akawekwa kwenye jeneza huko Misri.