\id EZR - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Ezra \toc1 Ezra \toc2 Ezra \toc3 Ezr \mt1 Ezra \c 1 \s1 Koreshi aruhusu watu kurudi Yerusalemu \r (2 Nyakati 36:22-23) \p \v 1 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na nabii Yeremia, Mwenyezi Mungu aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi: \pmo \v 2 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: \pm “ ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. \v 3 Yeyote kati ya watu wa Mungu miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko Yerusalemu. \v 4 Nao wakazi wa popote manusura wanapoishi sasa, wawape manusura fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ” \p \v 5 Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. \v 6 Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari. \v 7 Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalu la mungu wake. \v 8 Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda. \b \lh \v 9 Hii ilikuwa orodha ya vifaa: \b \li1 masinia ya dhahabu yalikuwa thelathini; \li1 masinia ya fedha yalikuwa elfu moja; \li1 vyetezo vya fedha vilikuwa ishirini na tisa; \li1 \v 10 mabakuli ya dhahabu yalikuwa thelathini; \li1 mabakuli ya fedha yaliyofanana yalikuwa mia nne na kumi; \li1 vifaa vingine vilikuwa elfu moja. \b \lf \v 11 Kwa jumla, kulikuwa na vyombo elfu tano na mia nne vya dhahabu na vya fedha. \b \p Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu. \c 2 \s1 Orodha ya watu waliorudi kutoka uhamishoni \r (Nehemia 7:4-73) \lh \v 1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, \v 2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): \b \lh Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa: \li1 \v 3 wazao wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili (2,172); \li1 \v 4 wazao wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili (372); \li1 \v 5 wazao wa Ara, mia saba sabini na watano (775); \li1 \v 6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu), elfu mbili mia nane na kumi na wawili (2,812); \li1 \v 7 wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254); \li1 \v 8 wazao wa Zatu, mia tisa arobaini na watano (945); \li1 \v 9 wazao wa Zakai, mia saba na sitini (760); \li1 \v 10 wazao wa Bani, mia sita arobaini na wawili (642); \li1 \v 11 wazao wa Bebai, mia sita ishirini na watatu (623); \li1 \v 12 wazao wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili (1,222); \li1 \v 13 wazao wa Adonikamu, mia sita sitini na sita (666); \li1 \v 14 wazao wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita (2,056); \li1 \v 15 wazao wa Adini, mia nne hamsini na wanne (454); \li1 \v 16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia), tisini na nane (98); \li1 \v 17 wazao wa Besai, mia tatu ishirini na watatu (323); \li1 \v 18 wazao wa Yora, mia moja na kumi na wawili (112); \li1 \v 19 wazao wa Hashumu, mia mbili na ishirini na watatu (223); \li1 \v 20 wazao wa Gibari, tisini na watano (95); \li1 \v 21 watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu (123); \li1 \v 22 watu wa Netofa, hamsini na sita (56); \li1 \v 23 watu wa Anathothi, watu mia moja ishirini na nane (128); \li1 \v 24 watu wa Azmawethi, arobaini na wawili (42); \li1 \v 25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi, mia saba arobaini na watatu (743); \li1 \v 26 wazao wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja (621); \li1 \v 27 watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili (122); \li1 \v 28 watu wa Betheli na Ai, mia mbili na ishirini na watatu (223); \li1 \v 29 wazao wa Nebo, hamsini na wawili (52); \li1 \v 30 wazao wa Magbishi, mia moja hamsini na sita (156); \li1 \v 31 wazao wa Elamu ile ingine, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254); \li1 \v 32 wazao wa Harimu, mia tatu na ishirini (320); \li1 \v 33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono, mia saba ishirini na watano (725); \li1 \v 34 wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345); \li1 \v 35 wazao wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini (3,630). \b \lh \v 36 Makuhani: \li1 wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973); \li1 \v 37 wazao wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili (1,052); \li1 \v 38 wazao wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba (1,247); \li1 \v 39 wazao wa Harimu, elfu moja na kumi na saba (1,017). \b \lh \v 40 Walawi: \li1 wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia), sabini na wanne (74). \b \lh \v 41 Waimbaji: \li1 wazao wa Asafu, mia moja ishirini na nane (128). \b \lh \v 42 Mabawabu wa lango la Hekalu: \li1 wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai, mia moja thelathini na tisa (139). \b \lh \v 43 Watumishi wa Hekalu\f + \fr 2:43 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Wanethini \fqa*\ft (pia \+xt 2:58, 70\+xt*).\ft*\f*: \li1 wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, \li1 \v 44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni, \li1 \v 45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu, \li1 \v 46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani, \li1 \v 47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya, \li1 \v 48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu, \li1 \v 49 wazao wa Uza, Pasea, Besai, \li1 \v 50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu, \li1 \v 51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, \li1 \v 52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, \li1 \v 53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, \li1 \v 54 wazao wa Nesia na Hatifa. \b \lh \v 55 Wazao wa watumishi wa Sulemani: \li1 wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda, \li1 \v 56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli, \li1 \v 57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. \lf \v 58 Watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani, mia tatu tisini na wawili (392). \b \lh \v 59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: \li1 \v 60 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda, mia sita hamsini na wawili (652). \b \lh \v 61 Kutoka miongoni mwa makuhani: \li1 Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). \lf \v 62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. \v 63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu\f + \fr 2:63 \fr*\ft Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.\ft*\f*. \b \lf \v 64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili na mia tatu na sitini (42,360); \v 65 tena zaidi ya hao walikuwa na watumwa wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili. \v 66 Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), \v 67 ngamia mia nne thelathini na watano (435), na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720). \b \p \v 68 Walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. \v 69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni elfu sitini na moja\f + \fr 2:69 \fr*\ft Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500.\ft*\f* za dhahabu, mane elfu tano\f + \fr 2:69 \fr*\ft Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900.\ft*\f* za fedha, na mavazi mia moja ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. \p \v 70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao. \c 3 \s1 Madhabahu yajengwa tena \p \v 1 Mwezi wa saba ulipowadia baada ya Waisraeli kukaa katika miji yao, watu wote walikusanyika huko Yerusalemu kama mtu mmoja. \v 2 Yeshua mwana wa Yosadaki na makuhani wenzake, Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na wenzake walianza kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli ili kumtolea dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto, kulingana na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa mtu wa Mungu. \v 3 Ingawa waliwaogopa watu waliowazunguka, walijenga madhabahu juu ya ule msingi wake, wakamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu za sadaka za kuteketezwa za asubuhi na za jioni. \v 4 Kisha kulingana na kile kilichoandikwa, wakaiadhimisha Sikukuu ya Vibanda wakitoa idadi ya sadaka za kuteketezwa kama ilivyohitajika kila siku sawasawa na ilivyoagizwa. \v 5 Baada ya hayo, walitoa sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za Mwezi Mwandamo na dhabihu zote za sikukuu takatifu za Mwenyezi Mungu zilizoamriwa, pamoja na zile sadaka za hiari zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu. \v 6 Ingawa bado msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu ulikuwa haujawekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba. \s1 Kujenga upya Hekalu \p \v 7 Kisha watu wakawapa mafundi wa uashi na useremala fedha, wakawapa watu wa Sidoni na Tiro vyakula, vinywaji na mafuta ili waweze kuleta magogo ya mwerezi kupitia bahari kutoka Lebanoni hadi Yafa, kama alivyoagiza Koreshi mfalme wa Uajemi. \p \v 8 Katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kufika kwenye nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zao wengine (makuhani, Walawi na wote waliorejea Yerusalemu kutoka uhamishoni) walianza kazi, wakiteua Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi kusimamia ujenzi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu. \v 9 Yeshua na wanawe, pamoja na ndugu zake, Kadmieli na wanawe (wazao wa Hodavia), wana wa Henadadi na wana wao na ndugu zao, Walawi wote walijiunga pamoja kusimamia wale waliofanya kazi katika nyumba ya Mungu. \p \v 10 Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumhimidi Mwenyezi Mungu, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli. \v 11 Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa Mwenyezi Mungu hivi: \q1 “Yeye ni mwema; \q2 upendo wake kwa Israeli \q2 wadumu milele.” \m Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu msingi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu ulikuwa umewekwa. \v 12 Lakini wengi wa makuhani wazee, Walawi na viongozi wa jamaa waliokuwa wameona Hekalu la mwanzoni, walilia kwa sauti walipoona msingi wa Hekalu hili ukiwekwa, huku wengine wengi wakipiga kelele kwa furaha. \v 13 Hakuna mtu ambaye angeweza kutofautisha sauti hizo za furaha na za kilio, kwa sababu watu walipiga kelele sana. Nayo hiyo sauti ikasikika mbali. \c 4 \s1 Upinzani kuhusu ujenzi mpya \p \v 1 Adui za Yuda na Benyamini waliposikia kwamba watu waliorudi kutoka uhamishoni wanajenga Hekalu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, \v 2 wakamjia Zerubabeli na viongozi wa jamaa, nao wakasema, “Turuhusuni tuwasaidie kujenga, kwa sababu sisi tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi na tumekuwa tukimtolea dhabihu tangu wakati wa Esar-Hadoni mfalme wa Ashuru, aliyetuleta hapa.” \p \v 3 Lakini Zerubabeli, Yeshua na viongozi wengine wa jamaa ya Israeli wakawajibu, “Ninyi hamna sehemu nasi katika kujenga Hekalu la Mungu wetu. Sisi peke yetu tutajenga Hekalu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kama Mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi alivyotuagiza.” \p \v 4 Ndipo watu waliowazunguka wakajipanga kuwakatisha tamaa watu wa Yuda na kuwafanya waogope walipokuwa wakiendelea na ujenzi. \v 5 Wakaajiri washauri kuwapinga katika kazi yao, nao wakaipinga mipango yao wakati wote wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi hadi wakati wa utawala wa Dario mfalme wa Uajemi. \s1 Upinzani wakati wa wafalme Ahasuero na Artashasta \p \v 6 Hapo mwanzo wa utawala wa Ahasuero, hao adui waliandika mashtaka dhidi ya watu wa Yuda na Yerusalemu. \p \v 7 Pia katika siku za utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli pamoja na wenzao waliandika barua kwa Artashasta. Barua hiyo iliandikwa kwa mwandiko wa Kiaramu na katika lugha ya Kiaramu. \p \v 8 Rehumu afisa msimamizi na mwandishi Shimshai waliandika barua kwa Mfalme Artashasta dhidi ya watu wa Yerusalemu kama ifuatavyo: \pmo \v 9 Rehumu afisa msimamizi na mwandishi Shimshai, pamoja na wenzao, yaani mahakimu na maafisa walio juu ya watu kuanzia Tripoli, Uajemi, Ereki na Babeli, Waelami wa Shushani, \v 10 na watu wengine ambao mheshimiwa Asur-Banipali\f + \fr 4:10 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Osnapali\fqa*\ft au \ft*\fqa Asnapali\fqa*\ft kwa Kiaramu.\ft*\f* aliwahamisha na kuwakalisha katika mji wa Samaria na mahali pengine Ng’ambo ya Mto Frati. \p \v 11 (Hii ndiyo nakala ya barua waliyompelekea.) \pmo Kwa Mfalme Artashasta, \pmo Kutoka kwa watumishi wako, watu wa Ng’ambo ya Mto Frati: \pm \v 12 Yapasa Mfalme ajue kuwa Wayahudi waliopanda kuja kwetu kutoka kwenu, wameenda Yerusalemu nao wanaujenga upya ule mji wa uasi na uovu. Wanajenga kuta upya na kukarabati misingi yake. \pm \v 13 Zaidi ya hayo, yampasa mfalme ajue kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikafanywa upya, hakutakuwa na ulipaji wa kodi wala ada au ushuru, hivyo hazina za mfalme zitaathirika. \v 14 Sisi sasa kwa kuwa tunawajibika kwa jumba la kifalme na kwamba siyo sawasawa kwetu kuona mfalme akidharauliwa, basi tunatuma ujumbe huu kumtaarifu mfalme, \v 15 ili ufanyike uchunguzi kwenye kumbukumbu ya maandishi ya waliokutangulia. Katika kumbukumbu hizi utagundua kwamba mji huu ni mwasi, unaowataabisha wafalme na majimbo, ni mahali pa maasi tangu zamani. Ndiyo maana mji huu uliharibiwa. \v 16 Tunamjulisha mfalme kwamba kama mji huu ukijengwa na kuta zake zikifanywa upya, hutabakiwa na chochote Ng’ambo ya Mto Frati. \p \v 17 Mfalme alirudisha jibu hili: \pmo Kwa Rehumu, afisa msimamizi, mwandishi Shimshai na wenzenu wote wanaoishi katika Samaria na penginepo Ng’ambo ya Mto Frati: \pmo Salamu. \pm \v 18 Barua mliyotutumia imesomwa na kutafsiriwa mbele yangu. \v 19 Nilitoa amri na uchunguzi ukafanyika na imegundulika kwamba mji huu una historia ndefu ya maasi dhidi ya wafalme na pamekuwa mahali pa maasi na uchochezi. \v 20 Yerusalemu umepata kuwa na wafalme wenye nguvu wakitawala nchi yote iliyo Ng’ambo ya Mto Frati, wakitoza kodi, ada na ushuru huko. \v 21 Kwa hiyo toeni amri kwa watu hawa wasimamishe ujenzi, ili mji huu usiendelee kujengwa hadi nitakapoagiza. \v 22 Mwe waangalifu msipuuze jambo hili. Kwa nini kuruhusu tishio hili kuendelea na kusababisha hasara kwa ufalme? \p \v 23 Mara waliposomewa nakala ya barua ya Mfalme Artashasta, Rehumu na Shimshai aliyekuwa mwandishi na wenzao, walienda mara moja kwa Wayahudi huko Yerusalemu na kuwalazimisha kwa nguvu kusimamisha ujenzi. \b \p \v 24 Hivyo kazi ya ujenzi wa nyumba ya Mungu huko Yerusalemu ikasimamishwa kabisa hadi mwaka wa pili wa utawala wa Dario mfalme wa Uajemi. \c 5 \s1 Barua ya Tatenai kwa Dario \p \v 1 Ndipo nabii Hagai na nabii Zekaria mzao wa Ido, wakawatolea unabii Wayahudi waliokuwa Yuda na Yerusalemu kwa jina la Mungu wa Israeli, aliyekuwa pamoja nao. \v 2 Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli na Yeshua mwana wa Yosadaki wakaanza kujenga tena nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Nao manabii wa Mungu walikuwa pamoja nao, wakiwasaidia. \p \v 3 Wakati ule Tatenai mtawala wa ng’ambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao waliwaendea, wakawauliza, “Ni nani aliyewapa ruhusa ya kujenga tena Hekalu hili na kurudishia upya kama lilivyokuwa?” \v 4 Pia waliwauliza, “Je, majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni nani?” \v 5 Lakini jicho la Mungu wao lilikuwa likiwaangalia wazee wa Wayahudi, nao hawakuzuiliwa kujenga hadi taarifa ikaandikwa kwa Dario na majibu yake kupokelewa. \p \v 6 Hii ni nakala ya barua ile Tatenai, mtawala wa ng’ambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao maafisa wa ng’ambo ya mto Frati waliyompelekea Mfalme Dario. \v 7 Taarifa waliyompelekea ilisomeka kama ifuatavyo: \pmo Kwa Mfalme Dario: \pmo Salamu kwa moyo mkunjufu. \b \pm \v 8 Inampasa Mfalme ajue kwamba tulienda katika eneo la Yuda, kwenye Hekalu la Mungu mkuu. Watu wanalijenga kwa mawe makubwa na kuweka mbao kwenye kuta. Kazi inafanyika kwa bidii na inaendelea kwa haraka chini ya uongozi wao. \pm \v 9 Tuliwauliza viongozi, “Ni nani aliyewapa ruhusa kujenga upya Hekalu hili na kurejesha hali ya jengo kama lilivyokuwa?” \v 10 Pia tuliwauliza majina yao, ili tukuandikie kukujulisha majina ya viongozi wao. \pm \v 11 Hili ndilo jibu walilotupatia: \b \pm “Sisi ni watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi, nasi tunalijenga upya Hekalu ambalo lilijengwa miaka mingi iliyopita, lile ambalo mfalme mkuu wa Israeli alilijenga na kulikamilisha. \v 12 Lakini kwa sababu baba zetu walimkasirisha Mungu wa mbinguni, basi aliwatia mkononi mwa Nebukadneza, Mkaldayo, mfalme wa Babeli, ambaye aliliharibu Hekalu hili na kuwaondoa watu na kuwapeleka uhamishoni huko Babeli. \pm \v 13 “Pamoja na hayo, katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Babeli, Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujengwa upya nyumba hii ya Mungu. \v 14 Yeye hata aliviondoa vyombo vya dhahabu na fedha vya nyumba ya Mungu, kutoka Hekalu la Babeli ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka ndani ya Hekalu huko Yerusalemu na kuvileta katika Hekalu la Babeli. \pm “Vyombo hivyo Mfalme Koreshi alimkabidhi mtu aliyeitwa Sheshbaza, ambaye Koreshi alikuwa amemteua awe mtawala, \v 15 naye akamwambia, ‘Chukua vyombo hivi uende ukaviweke ndani ya Hekalu huko Yerusalemu. Nawe uijenge upya nyumba ya Mungu mahali pake.’ \pm \v 16 “Hivyo huyu Sheshbaza alikuja na kuweka misingi ya nyumba ya Mungu iliyo Yerusalemu. Tangu siku hiyo hadi sasa imekuwa ikiendelea kujengwa lakini bado haijamalizika.” \b \pm \v 17 Sasa, ikimpendeza mfalme, uchunguzi na ufanyike katika kumbukumbu za maandishi ya ufalme mjini Babeli, kuona kama kweli Mfalme Koreshi alitoa amri ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika Yerusalemu. Kisha tunaomba mfalme na atutumie uamuzi wake kuhusu jambo hili. \c 6 \s1 Amri ya Dario \p \v 1 Kisha Mfalme Dario alitoa amri, nao wakafanya uchunguzi katika kumbukumbu zilizohifadhiwa katika hazina huko Babeli. \v 2 Kitabu kilipatikana katika ngome la Ekbatana katika jimbo la Umedi; kilikuwa kimeandikwa hivi: \pmo Kumbukumbu: \pm \v 3 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Mfalme Koreshi, mfalme alitoa amri kuhusu Hekalu la Mungu katika Yerusalemu: \b \pm Hekalu na lijengwe upya likiwa mahali pa kutolea dhabihu, na misingi yake ijengwe. Iwe na kimo cha mikono sitini\f + \fr 6:3 \fr*\ft Mikono 60 ni sawa na mita 27.\ft*\f*, upana wa mikono sitini, \v 4 kuta zijengwe kwa safu tatu za mawe makubwa kisha ifuate safu moja ya mbao. Gharama zitalipwa kutoka hazina ya mfalme. \v 5 Pia, vyombo vya dhahabu na vya fedha vya nyumba ya Mungu, ambavyo Nebukadneza alivichukua kutoka Hekalu huko Yerusalemu akavileta Babeli, yapasa virudishwe mahali pake ndani ya Hekalu huko Yerusalemu, yapasa viwekwe ndani ya nyumba ya Mungu. \b \pm \v 6 Sasa basi, Tatenai, mtawala wa Ng’ambo ya Mto Frati na Shethar-Bozenai pamoja na ninyi, maafisa wenzao wa jimbo hilo kaeni mbali na mahali hapo. \v 7 Msiingilie kazi ya Hekalu hili la Mungu. Mwacheni mtawala wa Wayahudi na viongozi Wayahudi wajenge upya nyumba hii ya Mungu mahali pake. \pm \v 8 Zaidi ya hayo, hapa natoa amri kuhusu mtakalofanya kwa ajili ya wazee wa Wayahudi katika ujenzi wa nyumba hii ya Mungu: \pm Gharama za watu hawa zitalipwa kikamilifu kutoka hazina ya mfalme, kutoka mapato ya Ng’ambo ya Mto Frati, ili ujenzi usisimame. \v 9 Chochote kinachohitajika kama mafahali wachanga, kondoo dume, wana-kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kama vitakavyohitajika na makuhani huko Yerusalemu, lazima wapewe kila siku pasipo kukosa, \v 10 ili waweze kutoa dhabihu inayompendeza Mungu wa mbinguni na kumwombea mfalme na wanawe hali njema. \pm \v 11 Zaidi ya hayo, ninaamuru kwamba mtu yeyote atakayebadilisha amri hii, boriti itang’olewa kutoka nyumba yake, ichongwe upande mmoja na atumbuliwe nayo. Kwa ajili ya kosa hili nyumba yake ifanywe lundo la taka. \v 12 Naye Mungu, aliyeliweka Jina lake huko, amwangushe mfalme yeyote au watu watakaoinua mikono kubadili amri hii au kuharibu Hekalu hili ambalo liko Yerusalemu. \pm Mimi Dario nimetoa amri hii. Nayo itekelezwe kwa bidii na kwa makini. \s1 Hekalu linakamilika na kuwekwa wakfu \p \v 13 Kwa sababu ya amri aliyotoa Mfalme Dario, Tatenai mtawala wa Ng’ambo ya Mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao wakaitekeleza kwa bidii na kwa makini. \v 14 Hivyo wazee wa Wayahudi waliendelea kujenga na kustawi kutokana na mahubiri ya manabii Hagai na Zekaria, wa uzao wa Ido. Wakakamilisha ujenzi wa Hekalu kulingana na agizo la Mungu wa Israeli na amri ya Koreshi, Dario na Artashasta wafalme wa Uajemi. \v 15 Hekalu lilikamilika siku ya kumi na mbili ya mwezi wa Adari, ndio mwezi wa tatu, katika mwaka wa sita wa utawala wa Mfalme Dario. \p \v 16 Kisha watu wa Israeli: makuhani, Walawi na wengine wote waliohamishwa, wakaadhimisha kule kuwekwa wakfu nyumba ya Mungu kwa shangwe. \v 17 Kwa ajili ya kuwekwa wakfu nyumba hii ya Mungu walitoa mafahali mia moja, kondoo dume mia mbili, wana-kondoo mia nne; sadaka kwa ajili ya dhambi ya Israeli wote walitoa beberu kumi na wawili, mmoja kwa ajili ya kila kabila la Israeli. \v 18 Wakawaweka makuhani katika nafasi zao na Walawi wakawekwa katika makundi yao ya huduma kwa Mungu huko Yerusalemu, kulingana na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. \s1 Pasaka \p \v 19 Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, waliorudi kutoka uhamishoni wakaadhimisha Pasaka. \v 20 Makuhani na Walawi walikuwa wamekwisha kujitakasa na hivyo wakatakasika. Walawi wakachinja kondoo wa Pasaka kwa ajili ya wana wa waliorudi kutoka utumwani uhamishoni, kwa ajili ya ndugu zao makuhani na wao wenyewe. \v 21 Hivyo Waisraeli waliorudi kutoka uhamishoni wakala Pasaka, pamoja na wale waliokuwa wamejitenga na matendo ya unajisi wa Mataifa jirani ili kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 22 Kwa muda wa siku saba waliiadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa furaha, kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amewajaza furaha kwa kubadilisha nia ya mfalme wa Ashuru kwamba awasaidie ujenzi wa nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli. \c 7 \s1 Ezra awasili Yerusalemu \p \v 1 Baada ya mambo haya, wakati wa utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia, \v 2 mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu, \v 3 mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi, \v 4 mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa Buki, \v 5 mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani mkuu Haruni. \v 6 Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwandishi mwenye ujuzi mwingi katika Torati ya Musa, ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye. \v 7 Baadhi ya Waisraeli, wakiwemo makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu na watumishi wa Hekalu\f + \fr 7:7 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Wanethini \fqa*\ft (pia \+xt 7:24\+xt*).\ft*\f*, nao walikuja Yerusalemu mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta. \p \v 8 Ezra aliwasili Yerusalemu mwezi wa tano wa mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta. \v 9 Ezra alianza safari yake kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa kuwa mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake. \v 10 Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika Torati ya Mwenyezi Mungu na kuwafundisha Waisraeli amri na sheria zake. \s1 Barua ya Ezra kutoka kwa Mfalme Artashasta \p \v 11 Hii ni nakala ya barua ambayo Mfalme Artashasta alimpa Ezra aliyekuwa kuhani na mwalimu, mtu aliyeelimika katika mambo kuhusu maagizo na amri za Mwenyezi Mungu kwa Israeli. \pmo \v 12 Artashasta, mfalme wa wafalme, \pmo Kwa Ezra kuhani, mwalimu wa Torati ya Mungu wa mbinguni: \pmo Salamu. \b \pm \v 13 Sasa naamuru kwamba mtu yeyote Mwisraeli katika ufalme wangu, pamoja na makuhani na Walawi, ambaye anataka kwenda Yerusalemu pamoja nawe aweza kwenda. \v 14 Unatumwa na mfalme na washauri wake saba kuchunguza habari za Yuda na Yerusalemu kulingana na Torati ya Mungu wako, iliyo mkononi mwako. \v 15 Zaidi ya hayo, uchukue fedha na dhahabu ambazo mfalme na washauri wake wamempa Mungu wa Israeli kwa hiari, Mungu ambaye maskani yake yako Yerusalemu, \v 16 pia fedha na dhahabu zote unazoweza kupata kutoka jimbo la Babeli, pamoja na sadaka za hiari watakazotoa watu na makuhani kwa ajili ya Hekalu la Mungu wao ambalo liko Yerusalemu. \v 17 Hakikisha kwamba fedha hizi zimetumika kununua mafahali, kondoo dume na wana-kondoo pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, uvitoe dhabihu juu ya madhabahu ya Hekalu la Mungu wenu katika Yerusalemu. \pm \v 18 Kisha wewe na Wayahudi ndugu zako mnaweza kufanya lolote linaloonekana jema sana kwa fedha na dhahabu zilizosalia, kulingana na mapenzi ya Mungu wenu. \v 19 Uvitoe kwa Mungu wa Yerusalemu vyombo vyote ulivyokabidhiwa kwa ajili ya ibada katika Hekalu la Mungu wako. \v 20 Kitu kingine chochote kinachohitajika kwa ajili ya Hekalu la Mungu wenu ambacho unatakiwa kukitoa, unaweza kukitoa kutoka hazina ya mfalme. \pm \v 21 Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ng’ambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Torati ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu, \v 22 talanta mia moja\f + \fr 7:22 \fr*\ft Talanta 100 za fedha ni sawa na kilo 3,400.\ft*\f* za fedha, ngano kori mia moja\f + \fr 7:22 \fr*\ft Kori 100 za ngano ni sawa na kilo 10,000.\ft*\f*, divai bathi mia moja\f + \fr 7:22 \fr*\ft Bathi 100 za divai ni sawa na lita 2,000.\ft*\f*, mafuta ya zeituni bathi mia moja, na chumvi kiasi chochote. \v 23 Chochote ambacho Mungu wa mbinguni ameagiza, kifanyike kwa ukamilifu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wa mbinguni. Kwa nini pawepo ghadhabu dhidi ya utawala wa mfalme na wanawe? \v 24 Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu. \pm \v 25 Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu, ili watoe haki kwa watu wote wa Ng’ambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu. \v 26 Yeyote ambaye hataitii Torati ya Mungu wenu na pia sheria ya mfalme, hakika lazima aadhibiwe kwa kuuawa, kuhamishwa, kunyang’anywa mali au kufungwa gerezani. \p \v 27 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zetu, Mungu ambaye kwa njia hii ameweka ndani ya moyo wa mfalme kuipa heshima nyumba ya Mwenyezi Mungu iliyo Yerusalemu, kwa namna hii \v 28 ambaye ameniongezea kibali chake mbele ya mfalme, washauri wake na maafisa wote wa mfalme wenye uwezo. Kwa kuwa mkono wa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, ulikuwa pamoja nami, nilijipa moyo nikakusanya watu walio viongozi kutoka Israeli wakwee pamoja nami. \c 8 \s1 Orodha ya viongozi wa jamaa waliorudi na Ezra \lh \v 1 Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta: \b \li1 \v 2 wa wazao wa Finehasi, \li2 alikuwa Gershoni; \li1 wa wazao wa Ithamari, \li2 alikuwa Danieli; \li1 wa wazao wa Daudi, \li2 alikuwa Hatushi \v 3 wa wazao wa Shekania; \li1 wa wazao wa Paroshi, \li2 alikuwa Zekaria, na watu mia moja na hamsini walioandikishwa; \li1 \v 4 wa wazao wa Pahath-Moabu, \li2 alikuwa Eliehoenai mwana wa Zerahia na wanaume mia mbili; \li1 \v 5 wa wazao wa Zatu, \li2 alikuwa Shekania mwana wa Yahazieli na wanaume mia tatu; \li1 \v 6 wa wazao wa Adini, \li2 alikuwa Ebedi mwana wa Yonathani na wanaume hamsini; \li1 \v 7 wa wazao wa Elamu, \li2 alikuwa Yeshaya mwana wa Athalia, na wanaume sabini; \li1 \v 8 wa wazao wa Shefatia, \li2 alikuwa Zebadia mwana wa Mikaeli na wanaume themanini; \li1 \v 9 wa wazao wa Yoabu, \li2 alikuwa Obadia mwana wa Yehieli na wanaume mia mbili kumi na nane; \li1 \v 10 wa wazao wa Bani, \li2 alikuwa Shelomithi mwana wa Yosifia na wanaume mia moja na sitini; \li1 \v 11 wa wazao wa Bebai, \li2 alikuwa Zekaria mwana wa Bebai na wanaume ishirini na nane; \li1 \v 12 wa wazao wa Azgadi, \li2 alikuwa Yohanani mwana wa Hakatani na wanaume mia moja na kumi; \li1 \v 13 wa wazao wa Adonikamu: \li2 hawa walikuwa wa mwisho ambao majina yao ni Elifeleti, Yeueli, Shemaya na wanaume sitini; \li1 \v 14 wa wazao wa Bigwai, \li2 walikuwa Uthai na Zakuri na wanaume sabini. \s1 Kurudi Yerusalemu \p \v 15 Niliwakusanya kwenye mto unaotiririka kuelekea Ahava, nasi tukapiga kambi pale siku tatu. Nilipokagua kati ya watu na makuhani, sikuwapata Walawi. \v 16 Basi niliwaita Eliezeri, Arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu, Elnathani, Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na Yoyaribu na Elnathani waliokuwa wasomi, \v 17 nikawatuma kwa Ido kiongozi huko Kasifia. Niliwaambia watakayomwambia Ido na ndugu zake, watumishi wa Hekalu\f + \fr 8:17 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Wanethini \fqa*\ft (pia \+xt 8:20\+xt*).\ft*\f* huko Kasifia, ili waweze kutuletea wahudumu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. \v 18 Kwa sababu mkono wa neema wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, walituletea Sherebia, mtu mwenye busara kutoka wazao wa Mahli mwana wa Lawi, mwana wa Israeli, na wana wa Sherebia pamoja na ndugu zao wanaume kumi na nane. \v 19 Naye Hashabia, pamoja na Yeshaya kutoka wazao wa Merari na ndugu zake na wapwa wake, walikuwa wanaume ishirini. \v 20 Vilevile walileta watumishi wa Hekalu mia mbili na ishirini, kikundi ambacho Daudi na maafisa walikuwa wamekianzisha ili kusaidia Walawi. Wote waliorodheshwa kwa majina. \p \v 21 Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeze mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali yetu yote. \v 22 Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.” \v 23 Kwa hiyo tulifunga na kumwomba Mungu wetu kuhusu jambo hili, naye akajibu maombi yetu. \p \v 24 Kisha niliwatenga viongozi wa makuhani kumi na wawili, pamoja na Sherebia, Hashabia na ndugu zao kumi, \v 25 nami nikawapimia fedha, dhahabu na vifaa ambavyo mfalme, washauri wake, maafisa wake na Waisraeli wote waliokuwepo walikuwa wamevitoa sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. \v 26 Niliwapimia talanta mia sita na hamsini\f + \fr 8:26 \fr*\ft Talanta 650 za fedha ni sawa na tani 25.\ft*\f* za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja\f + \fr 8:26 \fr*\ft Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.\ft*\f*, talanta mia moja za dhahabu, \v 27 mabakuli ishirini ya dhahabu ya thamani ya darkoni elfu moja\f + \fr 8:27 \fr*\ft Darkoni 1,000 ni sawa na kilo 8.5.\ft*\f*, na vyombo viwili vya shaba iliyosuguliwa, ya thamani kama dhahabu. \p \v 28 Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Mwenyezi Mungu. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu. \v 29 Vilindeni kwa uangalifu hadi mtakapovipima ndani ya vyumba vya nyumba ya Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu mbele ya makuhani, viongozi na Walawi pamoja na wakuu wa jamaa za Israeli.” \v 30 Ndipo makuhani na Walawi wakapokea fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu ambavyo vilipimwa na kupelekwa katika nyumba ya Mungu wetu mjini Yerusalemu. \p \v 31 Tulianza safari kutoka Mto Ahava kwenda Yerusalemu siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza. Mkono wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, naye njiani alitulinda dhidi ya adui na wanyang’anyi. \v 32 Kwa hiyo tuliwasili Yerusalemu ambapo tulipumzika kwa siku tatu. \p \v 33 Katika siku ya nne, ndani ya nyumba ya Mungu wetu, tulipima fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu, tukakabidhi mikononi mwa kuhani Meremothi mwana wa Uria. Eleazari mwana wa Finehasi alikuwa pamoja naye, na pia Walawi wawili, Yozabadi mwana wa Yeshua, na Noadia mwana wa Binui. \v 34 Kila kitu kilihesabiwa kwa idadi na kupimwa kwa uzito, nao uzito wote uliandikwa wakati ule. \p \v 35 Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba, na beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu. \v 36 Pia walikabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa Ng’ambo ya Mto Frati maagizo ya mfalme, ambao baadaye walitoa msaada kwa watu na kwa nyumba ya Mungu. \c 9 \s1 Maombi ya Ezra kuhusu kuoa wake wa kigeni \p \v 1 Baada ya mambo haya kutendeka, viongozi walinijia na kusema, “Watu wa Israeli, wakiwemo makuhani na Walawi, hawakujitenga na majirani zao katika kufanya machukizo, kama yale ya Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori. \v 2 Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.” \p \v 3 Niliposikia jambo hili nilirarua koti langu na joho langu, nikazing’oa nywele za kichwa changu na ndevu zangu na kuketi nikishangaa. \v 4 Kisha kila mmoja aliyetetemeshwa na maneno ya Mungu wa Israeli alikusanyika kunizunguka kwa sababu ya upotovu huu wa hao watu waliorudi kutoka utumwani. Nami niliketi pale nikishangaa hadi wakati wa dhabihu ya jioni. \p \v 5 Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. \v 6 Nami nikaomba: \pm “Ee Mungu wangu, natahayari na kuona aibu kukuinulia uso wangu Mungu wangu, kwa sababu dhambi zetu zimejikusanya hata kupita juu ya vichwa vyetu na hatia yetu imefika mbinguni. \v 7 Tokea siku za babu zetu hadi sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo. \pm \v 8 “Lakini sasa, kwa muda mfupi, Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupatia mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu anatupatia mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu. \v 9 Ingawa tu watumwa, Mungu wetu hajatuacha katika kufungwa kwetu. Ametuonesha huruma mbele ya wafalme wa Uajemi: Ametujalia maisha mapya kwa kujenga upya nyumba ya Mungu wetu na kukarabati magofu yake, naye ametupatia ukuta wa ulinzi katika Yuda na Yerusalemu. \pm \v 10 “Lakini sasa, Ee Mungu wetu, tunaweza kusema nini baada ya hili? Kwa maana tumedharau maagizo \v 11 uliyoyatoa kupitia watumishi wako manabii uliposema: ‘Nchi mnayoiingia kuimiliki ni nchi iliyochafuliwa na uovu wa watu wake. Kwa matendo yao ya machukizo wameijaza nchi kwa unajisi wao kutoka mwisho mmoja hadi mwingine. \v 12 Kwa hiyo, msiwaoze binti zenu kwa wana wao wala binti zao kwa wana wenu. Msitafute mkataba wa urafiki nao kwa wakati wowote. Ndipo mtakapofanikiwa na kula mema ya nchi na kuwaachia watoto wenu nchi hiyo kama urithi wao wa milele.’ \pm \v 13 “Yale yaliyotupata ni matokeo ya matendo yetu mabaya, pia hatia yetu kubwa. Hata hivyo, wewe Mungu wetu, umetuadhibu kidogo kuliko dhambi zetu zilivyostahili na umetupatia mabaki kama haya. \v 14 Je, tutavunja maagizo yako tena na kuoana na watu ambao hufanya mambo ya machukizo? Je, hutakuwa na hasira ya kutosha juu yetu na kutuangamiza, bila kutuachia mabaki wala atakayenusurika? \v 15 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wewe ni mwenye haki! Siku ya leo tumeachwa kama mabaki. Tupo hapa mbele zako na hatia yetu, ingawa katika hali hii hakuna hata mmoja wetu anayeweza kusimama mbele zako.” \c 10 \s1 Toba ya watu \p \v 1 Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli wakiwemo wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana. \v 2 Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli. \v 3 Sasa na tufanye agano mbele za Mungu wetu kuwafukuza hawa wanawake wote pamoja na watoto wao, kulingana na maonyo ya bwana wangu pamoja na wale ambao wanaogopa amri za Mungu wetu. Hili na lifanyike sawasawa na hii Torati. \v 4 Inuka, suala hili lipo mikononi mwako. Sisi tutaungana nawe, uwe na ujasiri ukatende hili.” \p \v 5 Basi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Waisraeli wote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa. \v 6 Ndipo Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu akaenda kwenye chumba cha Yehohanani mwana wa Eliashibu. Alipokuwa hapo, hakula chakula wala hakunywa maji, kwa sababu aliendelea kuomboleza kwa kuwa watu wa uhamishoni walikosa uaminifu kwa Mungu. \p \v 7 Ndipo lilipotolewa tangazo Yuda yote na Yerusalemu kwa watu wote waliokuwa uhamishoni kukusanyika Yerusalemu. \v 8 Yeyote ambaye hangejitokeza kwa muda wa siku tatu angepoteza mali yake yote, kulingana na uamuzi wa maafisa na wazee. Naye mtu huyo angefukuzwa kutoka kusanyiko la watu waliokuwa uhamishoni. \b \p \v 9 Katika muda wa siku tatu, watu wote wa Yuda na Benyamini wakawa wamekusanyika huko Yerusalemu. Kwenye siku ya ishirini ya mwezi wa tisa, watu wote walikuwa wameketi ndani ya uwanja mbele ya nyumba ya Mungu, wakiwa na majonzi mno kwa tukio hilo na kwa sababu ya mvua kubwa. \v 10 Ndipo Kuhani Ezra aliposimama akawaambia, “Mmekosa uaminifu, mmeoa wanawake wa kigeni, mkaongezea hatia ya Israeli. \v 11 Sasa tubuni kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, mkafanye mapenzi yake. Jitengeni na mataifa wanaowazunguka na wake zenu wa kigeni.” \p \v 12 Kusanyiko lote wakajibu kwa sauti kubwa: “Uko sawa kabisa! Ni lazima tufanye kama unavyosema. \v 13 Lakini hapa pana watu wengi na ni wakati wa mvua, hivyo hatuwezi kusimama nje. Hata hivyo, shauri hili haliwezi kumalizika kwa siku moja au mbili, kwa sababu tumetenda dhambi kubwa katika jambo hili. \v 14 Maafisa wetu na watende kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.” \v 15 Yonathani mwana wa Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa peke yao, wakiungwa mkono na Meshulamu na Shabethai Mlawi, ndio waliopinga jambo hili. \p \v 16 Basi watu wa uhamishoni wakafanya kama ilivyokuwa imependekezwa. Kuhani Ezra akachagua wanaume waliokuwa viongozi wa jamaa, mmoja kutoka kila mgawanyo wa jamaa, nao wote wakachaguliwa kwa majina. Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi waliketi kuchunguza mashauri hayo. \v 17 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kushughulikia wanaume wote waliokuwa wameoa wanawake wa kigeni. \s1 Wenye hatia ya kuoa wake wa kigeni \lh \v 18 Miongoni mwa wazao wa makuhani, wafuatao walikuwa wameoa wanawake wa kigeni: \li1 Kutoka wazao wa Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zake: \li2 Maaseya, Eliezeri, Yaribu na Gedalia. \v 19 (Wote walitoa nadhiri kwa kuandika kwa mikono yao kuwafukuza wake zao, kwa hatia yao, kila mmoja akatoa kondoo dume kutoka kundini mwake kuwa sadaka ya hatia.) \li1 \v 20 Kutoka wazao wa Imeri: \li2 Hanani na Zebadia. \li1 \v 21 Kutoka wazao wa Harimu: \li2 Maaseya, Ilya, Shemaya, Yehieli na Uzia. \li1 \v 22 Kutoka wazao wa Pashuri: \li2 Elioenai, Maaseya, Ishmaeli, Nethaneli, Yozabadi na Elasa. \b \lh \v 23 Miongoni mwa Walawi: \li2 Yozabadi, Shimei, Kelaya (ndiye Kelita), Pethahia, Yuda na Eliezeri. \li1 \v 24 Kutoka waimbaji: \li2 Eliashibu. \li1 Kutoka mabawabu: \li2 Shalumu, Telemu na Uri. \b \lh \v 25 Miongoni mwa Waisraeli wengine: \li1 Kutoka wazao wa Paroshi: \li2 Ramia, Izia, Malkiya, Miyamini, Eleazari, Malkiya na Benaya. \li1 \v 26 Kutoka wazao wa Elamu: \li2 Matania, Zekaria, Yehieli, Abdi, Yeremothi na Ilya. \li1 \v 27 Kutoka wazao wa Zatu: \li2 Elioenai, Eliashibu, Matania, Yeremothi, Zabadi na Aziza. \li1 \v 28 Kutoka uzao wa Bebai: \li2 Yehohanani, Hanania, Zabai na Athlai. \li1 \v 29 Kutoka wazao wa Bani: \li2 Meshulamu, Maluki, Adaya, Yashubu, Sheali na Yeremothi. \li1 \v 30 Kutoka wazao wa Pahath-Moabu: \li2 Adna, Kelali, Benaya, Maaseya, Matania, Bezaleli, Binui na Manase. \li1 \v 31 Kutoka wazao wa Harimu: \li2 Eliezeri, Ishiya, Malkiya, Shemaya, Shimeoni, \v 32 Benyamini, Maluki, na Shemaria. \li1 \v 33 Kutoka wazao wa Hashumu: \li2 Matenai, Matata, Zabadi, Elifeleti, Yeremai, Manase na Shimei. \li1 \v 34 Kutoka wazao wa Bani: \li2 Maadai, Amramu, Ueli, \v 35 Benaya, Bedeya, Keluhi, \v 36 Vania, Meremothi, Eliashibu, \v 37 Matania, Matenai na Yaasu. \li1 \v 38 Kutoka wazao wa Binui: \li2 Shimei, \v 39 Shelemia, Nathani, Adaya, \v 40 Maknadebai, Shashai, Sharai, \v 41 Azareli, Shelemia, Shemaria, \v 42 Shalumu, Amaria na Yusufu. \li1 \v 43 Kutoka wazao wa Nebo: \li2 Yeieli, Matithia, Zabadi, Zebina, Yadai, Yoeli na Benaya. \b \lf \v 44 Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni, na baadhi yao walikuwa wamezaa nao watoto.