\id EZK - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Ezekieli \toc1 Ezekieli \toc2 Ezekieli \toc3 Eze \mt1 Ezekieli \c 1 \s1 Viumbe hai na utukufu wa Mwenyezi Mungu \p \v 1 Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa miongoni mwa waliokuwa uhamishoni kando ya Mto Kebari, mbingu zilifunguka nami nikaona maono ya Mungu. \p \v 2 Katika siku ya tano ya mwezi, mwaka wa tano wa kuhamishwa kwa Mfalme Yehoyakini, \v 3 neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Ezekieli kuhani, mwana wa Buzi, kando ya Mto Kebari, katika nchi ya Wakaldayo. Huko mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yake. \p \v 4 Nilitazama, nikaona dhoruba kubwa ikitoka kaskazini: wingu kubwa sana likiwa na miali ya radi, likizungukwa na mwanga mkali. Katikati ya huo moto kulikuwa kama chuma inavyong’aa ndani ya moto. \v 5 Ndani ya ule moto kulikuwa na mfano wa viumbe wanne wenye uhai. Kuonekana kwao walikuwa na umbo la mwanadamu, \v 6 lakini kila mmoja alikuwa na nyuso nne na mabawa manne. \v 7 Miguu yao ilikuwa imenyooka; nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za miguu ya ndama, nazo zilimetameta kama shaba iliyosuguliwa. \v 8 Chini ya mabawa yao katika pande zao nne walikuwa na mikono ya mwanadamu. Wote wanne walikuwa na nyuso na mabawa, \v 9 nayo mabawa yao yaligusana. Kila mmoja alienda kuelekea mbele moja kwa moja; hawakugeuka walipotembea. \p \v 10 Kuonekana kwa nyuso zao kulikuwa hivi: Kila mmoja wa hao wanne alikuwa na uso wa mwanadamu, na kwa upande wa kulia kila mmoja alikuwa na uso wa simba, na kwa upande wa kushoto alikuwa na uso wa ng’ombe; pia kila mmoja alikuwa na uso wa tai. \v 11 Hivyo ndivyo zilivyokuwa nyuso zao. Kila mmoja wao alikuwa na mabawa mawili yaliokunjuliwa kuelekea juu; kila bawa liligusa bawa la mwenzake kila upande; kila mmoja wao alikuwa na mabawa mawili yaliyofunika mwili wake. \v 12 Kila mmoja alienda kuelekea mbele moja kwa moja. Popote roho alipoenda, walienda pasipo kugeuka. \v 13 Kuonekana kwa wale viumbe hai kulikuwa kama makaa ya mawe yanayowaka au kama mienge. Moto ule ulikuwa ukienda mbele na nyuma katikati ya wale viumbe; ulikuwa na mwangaza mkali na katika ule moto kulitoka miali ya radi. \v 14 Wale viumbe walipiga mbio kwenda na kurudi, kama miali ya radi. \p \v 15 Nilipokuwa nikitazama wale viumbe hai, niliona gurudumu moja juu ya ardhi kando ya kila kiumbe na nyuso zake nne. \v 16 Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa hayo magurudumu na muundo wake: yalimetameta kama zabarajadi, nayo yote manne yalifanana. Kila gurudumu lilionekana kuwa na gurudumu lingine ndani yake. \v 17 Magurudumu yalipoenda, yalielekea upande mmoja wa pande nne walikoelekea wale viumbe; wale viumbe walipoenda, magurudumu hayakugeuka. \v 18 Kingo za magurudumu zilikuwa ndefu kwenda juu na za kutisha, nazo zote nne zilijawa na macho pande zote. \p \v 19 Wale viumbe hai walipoenda, magurudumu yaliyokuwa kando yao yalisogea; wakati hao viumbe hai walipoinuka kutoka ardhini, magurudumu nayo yaliinuka. \v 20 Popote roho alipoenda, wale viumbe nao walienda, nayo magurudumu yaliinuka pamoja nao, kwa sababu roho ya wale viumbe hai alikuwa ndani ya hayo magurudumu. \v 21 Viumbe wale waliposogea, nayo magurudumu yalisogea; viumbe waliposimama, nayo pia yalisimama; viumbe walipoinuka juu ya nchi, magurudumu yaliinuka pamoja nao, kwa kuwa roho ya hao viumbe hai alikuwa ndani ya hayo magurudumu. \p \v 22 Juu ya vichwa vya hao viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa eneo lililokuwa wazi, lililokuwa angavu kabisa na la kutisha. \v 23 Chini ya hiyo nafasi, mabawa yao yalitanda moja kuelekea lingine, na kila mmoja alikuwa na mabawa mawili yaliyofunika mwili wake. \v 24 Viumbe wale waliposogea, nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi\f + \fr 1:24 \fr*\ft Mwenyezi hapa ina maana ya \ft*\fqa Shaddai \fqa*\ft kwa Kiebrania.\ft*\f*, kama kishindo cha jeshi. Waliposimama, walishusha mabawa yao. \p \v 25 Ndipo ikaja sauti toka juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, waliposimama mabawa yao yakiwa yameshushwa. \v 26 Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha utawala cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha utawala kulikuwa na umbo, mfano wa mwanadamu. \v 27 Nikaona kwamba kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea juu, alionekana kama chuma inavyong’aa ikiwa ndani ya moto, na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto; mwanga wenye kung’aa sana ulimzunguka. \v 28 Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mng’ao uliomzunguka. \p Hivi ndivyo mfano wa utukufu wa Mwenyezi Mungu ulionekana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea. \c 2 \s1 Wito wa Ezekieli \p \v 1 Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” \v 2 Alipokuwa akiongea nami, Roho wa Mungu akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami. \p \v 3 Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, taifa ambalo limeniasi mimi; wao na baba zao wameniasi hadi leo. \v 4 Watu ninaokutuma kwao ni wakaidi na wabishi. Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mungu Mwenyezi.’ \v 5 Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya uasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. \v 6 Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao. Usiogope, ijapo michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ijapo wao ni nyumba ya uasi. \v 7 Lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni waasi. \v 8 Lakini wewe mwanadamu, sikiliza ninalokuambia. Usiasi kama hiyo nyumba ya uasi. Fungua kinywa chako na ule nikupacho.” \p \v 9 Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na kitabu, \v 10 ambacho alikikunjua mbele yangu. Pande zote mbili kilikuwa kimeandikwa maneno ya maombolezo, na vilio na ole. \c 3 \p \v 1 Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kilichoko mbele yako, kula kitabu hiki, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.” \v 2 Hivyo, nikafungua kinywa changu, naye akanipa kile kitabu nikile. \p \v 3 Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula kitabu hiki ninachokupa, ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, nao ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu. \p \v 4 Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukawanenee maneno yangu. \v 5 Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli. \v 6 Sikukutuma kwa mataifa mengi yenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu ambao maneno yao hutayaelewa. Hakika ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza. \v 7 Lakini nyumba ya Israeli haitakusikiliza, kwa kuwa hawako radhi kunisikiliza mimi, kwa kuwa nyumba yote ya Israeli ni wenye paji gumu na mioyo ya ukaidi. \v 8 Tazama, nimefanya uso wako mgumu dhidi ya nyuso zao, na paji la uso wako gumu dhidi ya paji za nyuso zao. \v 9 Kama vile almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyolifanya paji la uso wako. Usiwaogope wala usiwahofu, ijapokuwa ni nyumba ya uasi.” \p \v 10 Naye akaniambia, “Mwanadamu, sikiliza kwa makini na uyatie moyoni mwako maneno yote nitakayosema nawe. \v 11 Kisha nenda kwa watu wa taifa lako walio uhamishoni, ukaseme nao. Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi’; iwe watasikiliza au hawatasikiliza.” \p \v 12 Ndipo Roho wa Mungu akaniinua juu, nami nikasikia sauti kubwa ya ngurumo nyuma yangu ikisema, “Utukufu wa Mwenyezi Mungu na utukuzwe katika makao yake!” \v 13 Ilikuwa ni sauti ya mabawa ya wale viumbe hai yakigusana moja kwa lingine, na sauti ya magurudumu kando yao, sauti kubwa ya ngurumo. \v 14 Kisha Roho wa Mungu akaniinua juu na kunipeleka mbali. Nikaenda nikiwa na uchungu na hasira moyoni mwangu, nao mkono wenye nguvu wa Mwenyezi Mungu ukiwa juu yangu. \v 15 Nikafika kwa wale watu waliokuwa uhamishoni huko Tel-Abibu karibu na Mto Kebari. Nikakaa miongoni mwao kwa muda wa siku saba, nikiwa nimejawa na mshangao. \s1 Onyo kwa Israeli \p \v 16 Mwishoni mwa hizo siku saba neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 17 “Mwanadamu, nimekufanya uwe mlinzi wa nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo, ukawape onyo litokalo kwangu. \v 18 Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usimwonye mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu akifa katika dhambi yake, damu yake nitaidai mkononi mwako. \v 19 Lakini ukimwonya mtu mwovu naye akakataa kuacha uovu wake na njia zake mbaya, atakufa katika dhambi yake, lakini wewe utakuwa umejiokoa nafsi yako. \p \v 20 “Tena, mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda maovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake mtu huyo atakufa. Kwa kuwa hukumwonya, atakufa katika dhambi yake. Mambo ya haki aliyotenda, hayatakumbukwa, damu yake nitaidai mkononi mwako. \v 21 Lakini ukimwonya mwenye haki asitende dhambi na akaacha kutenda dhambi, hakika ataishi kwa sababu alipokea maonyo na utakuwa umejiokoa nafsi yako.” \p \v 22 Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu huko, naye akaniambia, “Simama uende sehemu tambarare, nami nitasema nawe huko.” \v 23 Kwa hiyo niliinuka nikaenda mahali tambarare. Utukufu wa Mwenyezi Mungu ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. \p \v 24 Ndipo Roho wa Mungu akaja ndani yangu, akanisimamisha kwa miguu yangu. Akasema nami akaniambia: “Nenda ukajifungie ndani ya nyumba yako. \v 25 Nawe, ee mwanadamu, watakufunga kwa kamba; utafungwa ili usiweze kuwaendea watu. \v 26 Nitaufanya ulimi wako ushikamane kwenye kaakaa la kinywa chako, ili uwe kimya usiweze kuwakemea, kwa kuwa wao ni nyumba ya uasi. \v 27 Lakini nitakaposema nawe, nitafungua kinywa chako nawe utawaambia, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi.’ Yeyote atakayesikiliza na asikilize, na yeyote atakayekataa na akatae; kwa kuwa wao ni nyumba ya uasi. \c 4 \s1 Mfano wa kuzingirwa kwa Yerusalemu \p \v 1 “Mwanadamu, sasa chukua tofali, uliweke mbele yako na uchore juu yake ramani ya mji wa Yerusalemu. \v 2 Kisha uuzingire: Njenga husuru dhidi yake, na upandishe kilima hadi kuta zake, weka kambi dhidi yake pande zote, pamoja na magogo ya kubomoa. \v 3 Kisha chukua bamba la chuma, ukalisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na huo mji, nawe uuelekeze uso wako. Huo mji utakuwa katika hali ya kuzingirwa, nawe ndiwe utakayeuzingira. Hii itakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli. \p \v 4 “Kisha ulale kwa upande wako wa kushoto na uweke dhambi za nyumba ya Israeli juu yako. Utazibeba dhambi zao kwa idadi ya siku utakazolala kwa huo upande mmoja. \v 5 Nimekupangia idadi ya siku kama miaka ya dhambi yao. Kwa hiyo kwa siku mia tatu na tisini (390), utabeba dhambi za nyumba ya Israeli. \p \v 6 “Baada ya kumaliza hili, lala chini tena, wakati huu ulale chini kwa upande wa kuume, uchukue dhambi za nyumba ya Yuda. Nimekupangia siku arobaini, siku moja kwa kila mwaka. \v 7 Geuza uso wako uuelekeze Yerusalemu uone jinsi ulivyozingirwa, na kwa mkono wako usiovikwa nguo, tabiri dhidi yake. \v 8 Nitakufunga kwa kamba ili usiweze kugeuka kutoka upande mmoja hadi upande mwingine, hata utakapotimiza siku za kuzingirwa kwako. \p \v 9 “Chukua ngano na shayiri, maharagwe na dengu, mtama na mawele, uviweke na kuvihifadhi vyote kwenye gudulia la kuhifadhia, na uvitumie kujitengenezea mkate. Utaula mkate huo kwa hizo siku mia tatu na tisini (390) utakazokuwa umelala kwa upande mmoja. \v 10 Pima shekeli ishirini\f + \fr 4:10 \fr*\ft Shekeli 20 ni sawa na gramu 200.\ft*\f* za chakula utakachokula kwa kila siku, nawe utakula kwa wakati uliopangwa. \v 11 Pia pima maji sehemu ya sita ya hini\f + \fr 4:11 \fr*\ft Sehemu ya sita ya hini ni sawa na mililita (ml) 600.\ft*\f*, nawe utakunywa kwa wakati uliopangwa. \v 12 Nawe utakula chakula vile ungekula mkate wa shayiri; uoke mkate mbele ya macho ya watu, ukitumia moto wa kinyesi cha mwanadamu.” \v 13 Mwenyezi Mungu akasema, “Hivi ndivyo watu wa Israeli watakavyokula chakula kilicho najisi miongoni mwa mataifa ninakowapeleka.” \p \v 14 Ndipo nikasema, “Sivyo Bwana Mungu Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu chochote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama pori. Hakuna nyama yoyote najisi iliyoingia kinywani mwangu.” \p \v 15 Akasema, “Vema sana, basi nitakuruhusu uoke mkate wako kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu.” \p \v 16 Kisha Mungu akaniambia, “Mwanadamu! Mimi nitasababisha uhaba wa chakula katika Yerusalemu. Watu watakula chakula cha mgawo kwa wasiwasi, na maji ya mgawo kwa kukata tamaa, \v 17 kwa kuwa chakula na maji vitakuwa adimu. Kila mmoja atastaajabu kumwona mwenzake, nao watadhoofika kwa sababu ya dhambi yao. \c 5 \s1 Upanga dhidi ya Yerusalemu \p \v 1 “Mwanadamu, chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyoa kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani, uzipime na kuzigawanya nywele hizo. \v 2 Siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya nywele ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzikatekate kwa upanga ukiuzunguka mji wote, na theluthi ya mwisho uitawanye kwa upepo, kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliovutwa. \v 3 Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako. \v 4 Tena chukua nywele nyingine chache uzitupe motoni uziteketeze. Moto utaenea kutoka hapo na kufika katika nyumba yote ya Israeli. \p \v 5 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Huu ndio mji wa Yerusalemu, ambao nimeuweka katikati ya mataifa, ukiwa umezungukwa na nchi pande zote. \v 6 Lakini katika uovu wake umeasi sheria na amri zangu kuliko mataifa na nchi zinazouzunguka. Umeasi sheria zangu wala haukufuata amri zangu. \p \v 7 “Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata maagizo yangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata desturi za mataifa yanayowazunguka. \p \v 8 “Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi mwenyewe niko kinyume nawe, Yerusalemu, na nitakupiga kwa adhabu yangu mbele ya mataifa. \v 9 Kwa sababu ya sanamu zako zote za machukizo, nitakufanyia kile ambacho kamwe sijafanya kabla wala kamwe sitafanya tena. \v 10 Kwa hiyo, kati yako baba watakula watoto wao, na watoto watakula baba zao. Nitawapiga kwa adhabu, nami nitawatawanya watu wenu walionusurika pande zote za dunia. \v 11 Kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu mbovu na desturi zenu za machukizo, mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu. \v 12 Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako; theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako; nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne na kuwafuatia kwa upanga. \p \v 13 “Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao kupungua, nami nitakuwa nimejilipizia kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, nimenena katika bidii yangu. \p \v 14 “Nitakuangamiza na kukufanya kitu cha kudharauliwa miongoni mwa mataifa yanayokuzunguka, machoni pa wote wapitao karibu nawe. \v 15 Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha dhihaka, kitu cha onyo na cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena. \v 16 Nitakapokurushia mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitairusha ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako. \v 17 Nitatuma njaa na wanyama pori dhidi yako, navyo vitakuacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu vitapita katikati yako, nami nitaleta upanga juu yako. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena.” \c 6 \s1 Unabii dhidi ya milima ya Israeli \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema, \v 2 “Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake, \v 3 useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana Mungu Mwenyezi. Hili ndilo neno asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa milima na vilima, magenge na mabonde: Nakaribia kuleta upanga dhidi yenu, na nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia. \v 4 Madhabahu yenu yatabomolewa na madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatavunjavunjwa, nami nitawachinja watu wenu mbele ya sanamu zenu. \v 5 Nitazilaza maiti za Waisraeli mbele ya sanamu zao, nami nitatawanya mifupa yenu kuzunguka madhabahu yenu. \v 6 Popote mnapoishi, miji itaangamizwa na mahali pa juu patabomolewa, ili madhabahu zenu ziharibiwe na kuteketezwa; sanamu zenu zitavunjwavunjwa na kuharibiwa, madhabahu zenu za kufukizia uvumba zitabomolewa, na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali. \v 7 Watu wenu watachinjwa kati yenu, nanyi mtatambua Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 8 “ ‘Lakini nitawabakiza hai baadhi yenu, kwa kuwa baadhi yenu watanusurika kuuawa kwa upanga watakapokuwa wametawanyika katika nchi na katika mataifa. \v 9 Ndipo katika mataifa walikochukuliwa mateka, watakaonusurika watanikumbuka. Watakumbuka jinsi nilivyohuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi ambayo imegeuka kuwa mbali nami, na kwa macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa sababu ya uovu walioutenda na desturi zao za kuchukiza. \v 10 Nao watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, sikuwaonya bure kuwa nitaleta maafa hayo yote juu yao. \p \v 11 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Piga makofi, pigisha mguu wako chini, na upige kelele useme, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na desturi za kuchukiza za nyumba ya Israeli, wataangamia kwa upanga, njaa na tauni. \v 12 Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni, naye aliye karibu atauawa kwa upanga, naye yule atakayenusurika na kubaki atakufa kwa njaa. Hivyo ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao. \v 13 Nao watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, wakati maiti za watu wao zitakapokuwa zimelala kati ya sanamu zao kuzunguka madhabahu yao, juu ya kila kilima kilichoinuka na juu ya vilele vyote vya milima, chini ya kila mti uliotanda na kila mwaloni wenye majani, yaani sehemu walizofukizia uvumba kwa sanamu zao zote. \v 14 Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \c 7 \s1 Mwisho umewadia \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa nchi ya Israeli: \q1 “ ‘Mwisho! Mwisho umekuja \q2 juu ya pembe nne za nchi! \q1 \v 3 Sasa mwisho umekuja juu yenu, \q2 nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. \q1 Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu \q2 na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza. \q1 \v 4 Sitawaonea huruma \q2 wala kuwarehemu. \q1 Hakika nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenu \q2 na desturi za machukizo miongoni mwenu. \m Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ \b \p \v 5 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa! \q2 Tazama, yanakuja! \q1 \v 6 Mwisho umewadia! \q2 Mwisho umewadia! \q1 Umejiinua wenyewe dhidi yenu. \q2 Tazama, umewadia! \q1 \v 7 Maangamizi yamekuja juu yenu, \q2 ninyi mnaoishi katika nchi. \q1 Wakati umewadia! Siku imekaribia! \q2 Kuna hofu kuu ya ghafula juu ya milima, wala si furaha. \q1 \v 8 Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenu \q2 na kumaliza hasira yangu dhidi yenu. \q1 Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu \q2 na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo. \q1 \v 9 Sitawaonea huruma \q2 wala kuwarehemu. \q1 Nitawalipiza kwa ajili ya matendo yenu \q2 na desturi za machukizo miongoni mwenu. \b \m “ ‘Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu ambaye huwapiga. \q1 \v 10 “ ‘Tazama, siku imefika! \q2 Tazama, imewadia! \q1 Maangamizi yamezuka ghafula, \q2 fimbo imechanua, \q2 nayo majivuno yamechipua! \q1 \v 11 Jeuri imeinuka \q2 kuwa fimbo ya kuadhibu waovu. \q1 Hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa, \q2 hata mmoja wa kundi hilo: \q1 hakuna utajiri wao utabaki, \q2 wala chochote cha thamani. \q1 \v 12 Wakati umewadia, \q2 siku imefika. \q1 Mnunuzi na asifurahi \q2 wala muuzaji asihuzunike, \q2 kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote. \q1 \v 13 Muuzaji hatajipatia tena \q2 ardhi aliyoiuza \q2 wakati wote wawili wangali hai. \q1 Kwa kuwa maono kuhusu kundi lote \q2 hayatatanguka. \q1 Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja \q2 atakayeokoa maisha yake. \b \q1 \v 14 “ ‘Wajapopiga tarumbeta \q2 na kuweka kila kitu tayari, \q1 hakuna hata mmoja atakayeenda vitani, \q2 kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote. \q1 \v 15 Nje ni upanga, \q2 ndani ni tauni na njaa. \q1 Walio shambani \q2 watakufa kwa upanga, \q1 nao waliomo mjini \q2 njaa na tauni vitawala. \q1 \v 16 Wote watakaopona \q2 na kutoroka watakuwa milimani, \q1 wakiomboleza kama hua wa mabondeni, \q2 kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake. \q1 \v 17 Kila mkono utalegea \q2 na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. \q1 \v 18 Watavaa gunia \q2 na kufunikwa na hofu. \q1 Nyuso zao zitafunikwa na aibu, \q2 na vichwa vyao vitanyolewa. \b \q1 \v 19 “ ‘Watatupa fedha yao barabarani, \q2 nayo dhahabu yao itakuwa najisi. \q1 Fedha yao na dhahabu yao \q2 havitaweza kuwaokoa \q2 katika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. \q1 Hawatashibisha njaa yao \q2 au kujaza tumbo zao kwa hiyo fedha wala dhahabu, \q2 kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini. \q1 \v 20 Walijivunia vito vyao vizuri \q2 na kuvitumia kutengeneza sanamu za machukizo \q2 na vinyago vya upotovu. \q2 Kwa hiyo nitavifanya vitu hivyo kuwa najisi kwao. \q1 \v 21 Nitavitia vyote mikononi mwa wageni \q2 kuwa nyara na kuwa vitu vilivyotekwa mikononi mwa watu waovu wa dunia, \q2 nao watavinajisi. \q1 \v 22 Nitaugeuza uso wangu mbali nao, \q2 nao waovu wa dunia watapanajisi mahali pangu pa thamani. \q1 Wanyang’anyi watapaingia \q2 na kupanajisi. \b \q1 \v 23 “ ‘Andaa minyororo, \q2 kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damu \q2 na mji umejaa udhalimu. \q1 \v 24 Nitaleta taifa ovu kuliko yote \q2 kumiliki nyumba zao. \q1 Nitakomesha kiburi cha wenye nguvu \q2 na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi. \q1 \v 25 Hofu ya ghafula itakapokuja, \q2 watatafuta amani, lakini haitapatikana. \q1 \v 26 Maafa juu ya maafa yatakuja, \q2 tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya. \q1 Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii; \q2 mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea, \q2 vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee. \q1 \v 27 Mfalme ataomboleza, \q2 mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, \q2 nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. \q1 Nitawaadhibu kulingana na matendo yao, \q2 na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. \b \m “ ‘Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \c 8 \s1 Ibada ya sanamu Hekaluni \p \v 1 Katika mwaka wa sita, siku ya tano ya mwezi wa sita, nilipokuwa nimeketi katika nyumba yangu na wazee wa Yuda wakiwa wameketi mbele yangu, mkono wa Bwana Mungu Mwenyezi ulikuja juu yangu. \v 2 Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kiuno kuelekea juu sura yake iling’aa vile chuma king’aavyo kikiwa ndani ya moto. \v 3 Akanyoosha kitu kilichofanana na mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho wa Mungu akaniinua juu kati ya nchi na mbingu, na nikiwa katika maono ya Mungu, akanichukua hadi Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la kaskazini mwa ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu inayochochea wivu. \v 4 Tazama! Palikuwa na utukufu wa Mungu wa Israeli, kama utukufu ule niliouona katika maono kule kwenye nchi tambarare. \p \v 5 Kisha akaniambia, “Mwanadamu, tazama kuelekea kaskazini.” Hivyo nikatazama na kwenye ingilio la kaskazini mwa lango la madhabahu, nikaona sanamu hii ya wivu. \p \v 6 Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayoyafanya: mambo ya kuchukiza kabisa ambayo nyumba ya Israeli wanayatenda hapa, yatakayonifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utayaona mambo yanayochukiza hata zaidi.” \p \v 7 Kisha akanileta hadi ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani. \v 8 Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango. \p \v 9 Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.” \v 10 Hivyo nikaingia ndani na kutazama. Nikaona kuta zote zimechorwa aina mbalimbali ya viumbe vinavyotambaa, na wanyama wanaochukiza, na sanamu zote za nyumba ya Israeli. \v 11 Mbele ya hizo kuta walisimama wazee sabini wa nyumba ya Israeli, naye Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama miongoni mwao. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi, na moshi wa harufu nzuri ya uvumba ulikuwa unapanda juu. \p \v 12 Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa Israeli wakiwa gizani, kila mmoja kwenye mahali pa ibada pa sanamu yake? Wao husema, ‘Mwenyezi Mungu hatuoni, Mwenyezi Mungu ameiacha nchi.’ ” \v 13 Akasema tena, “Utawaona wakifanya mambo yaliyo chukizo zaidi.” \p \v 14 Ndipo akanileta kwenye ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi Mungu, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi. \v 15 Akaniambia, “Je, mwanadamu, unaliona hili? Utayaona mambo yanayochukiza hata zaidi.” \p \v 16 Ndipo akanileta hadi kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, na katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, palikuwa na wanaume wapatao ishirini na watano. Walikuwa wamelipa kisogo Hekalu la Mwenyezi Mungu na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua upande wa mashariki. \p \v 17 Akaniambia, “Je, umeona hili mwanadamu? Je, ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda kufanya machukizo wanayoyafanya hapa? Je, ni lazima pia waijaze nchi dhuluma na kuendelea siku zote kunikasirisha? Watazame wanavyonibania pua kana kwamba ninanuka! \v 18 Kwa hiyo nitawaadhibu kwa hasira; sitawaonea huruma wala kuwarehemu. Hata wakipiga makelele masikioni mwangu, sitawasikiliza.” \c 9 \s1 Waabudu sanamu wauawa \p \v 1 Kisha nikamsikia akiita kwa sauti kubwa akisema, “Walete wasimamizi wa mji hapa, kila mmoja akiwa na silaha mkononi mwake.” \v 2 Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu linalotazama kaskazini, kila mmoja akiwa na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Kati yao palikuwa na mtu aliyevaa mavazi ya kitani safi, naye alikuwa na vifaa vya mwandishi kiunoni mwake. Wakaingia ndani ya Hekalu na kusimama pembeni mwa madhabahu ya shaba. \p \v 3 Basi utukufu wa Mungu wa Israeli ukaondoka hapo juu ya makerubi, ulikokuwa umekaa, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Ndipo Mwenyezi Mungu akamwita yule mtu aliyevaa kitani safi na mwenye vifaa vya mwandishi kiunoni mwake, \v 4 akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama kwenye paji za nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.” \p \v 5 Nikiwa ninasikiliza, akawaambia wale wengine, “Mfuateni anapopita katika mji wote mkiua, pasipo huruma wala masikitiko. \v 6 Waueni wazee, vijana wa kiume na wa kike, wamama na watoto, lakini msimguse mtu yeyote mwenye alama. Anzieni katika mahali pangu patakatifu.” Kwa hiyo wakaanza na wale wazee waliokuwa mbele ya Hekalu. \p \v 7 Ndipo akawaambia, “Linajisini Hekalu na mkazijaze ua zake maiti za wale waliouawa. Nendeni!” Kwa hiyo wakaenda, wakaanza kuua watu mjini kote. \v 8 Walipokuwa wakiwaua watu, nami nikaachwa peke yangu, nilisujudu, nikapaza sauti na kusema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi! Je, utaangamiza mabaki yote ya Israeli, katika kumwagwa huku kwa ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?” \p \v 9 Mwenyezi Mungu akanijibu, “Dhambi ya nyumba ya Israeli na Yuda imekuwa kubwa mno kupita kiasi, nchi imejaa umwagaji damu na mjini kumejaa udhalimu. Kwani wamesema, ‘Mwenyezi Mungu ameiacha nchi; Mwenyezi Mungu haoni.’ \v 10 Kwa hiyo sitawahurumia wala kuwarehemu, lakini nitaleta juu ya vichwa vyao yale waliyoyatenda.” \p \v 11 Ndipo mtu yule aliyevaa nguo ya kitani na mwenye vifaa vya mwandishi kiunoni mwake akarudi na kutoa taarifa, akisema, “Nimefanya kama ulivyoniagiza.” \c 10 \s1 Utukufu unaondoka Hekaluni \p \v 1 Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha utawala cha yakuti samawi. \v 2 Mwenyezi Mungu akamwambia mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, “Ingia kati ya yale magurudumu yaliyo chini ya makerubi. Ukaijaze mikono yako makaa ya mawe ya moto kutoka kati ya makerubi na ukayatawanye juu ya mji.” Nilipokuwa nikiangalia, akaingia ndani. \p \v 3 Basi wale makerubi walikuwa wamesimama upande wa kusini wa Hekalu wakati yule mtu alipoingia ndani, wingu likaujaza ule ukumbi wa ndani. \v 4 Kisha utukufu wa Mwenyezi Mungu ukainuka kutoka juu ya wale makerubi, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mng’ao wa utukufu wa Mwenyezi Mungu. \v 5 Sauti ya mabawa ya wale makerubi ilisikika hadi ua wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi\f + \fr 10:5 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f* anapoongea. \p \v 6 Mwenyezi Mungu alimwamuru yule mtu aliyevaa nguo ya kitani, akisema, “Chukua moto toka kati ya magurudumu, miongoni mwa makerubi.” Basi yule mtu aliingia ndani, akasimama pembeni mwa gurudumu. \v 7 Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao, akauchukua moto. Akautia mikononi mwa yule mtu aliyevaa nguo ya kitani, naye alipoupokea, akatoka nje. \v 8 (Chini ya mabawa ya makerubi palionekana kitu kilichofanana na mikono ya mwanadamu.) \p \v 9 Nikatazama, nikaona magurudumu manne kando ya makerubi, moja kando ya kila kerubi. Magurudumu hayo yalimetameta kama zabarajadi. \v 10 Kule kuonekana kwake, yote manne yalifanana; kila gurudumu lilikuwa kama linazunguka ndani ya lingine. \v 11 Magurudumu yalipoenda, yalielekea upande mmoja wa pande nne walikoelekea wale makerubi. Makerubi walipoenda, magurudumu hayakuzunguka. Makerubi walienda upande wowote ule kichwa kilielekea, pasipo kugeuka. \v 12 Miili yao: migongo yao, mikono na mabawa yao, ilikuwa imejaa macho kote, pamoja na yale magurudumu manne. \v 13 Nikasikia magurudumu yakiitwa “magurudumu ya kisulisuli”. \v 14 Kila mmoja wa wale makerubi alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba, na uso wa nne ulikuwa wa tai. \p \v 15 Kisha makerubi wakapaa juu. Hawa ndio wale viumbe walio hai niliowaona kando ya Mto Kebari. \v 16 Makerubi walipoenda, magurudumu yaliyokuwa kando yao yalienda; na makerubi walipotanda mabawa yao wapate kupaa juu kutoka ardhini, magurudumu yale hayakuondoka pembeni mwa makerubi. \v 17 Makerubi waliposimama, nayo pia yalitulia; nao makerubi walipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya wale viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu hayo. \p \v 18 Kisha utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi. \v 19 Nilipokuwa nikitazama, makerubi wakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Mwenyezi Mungu; nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao. \p \v 20 Hawa walikuwa viumbe hai niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli kando ya Mto Kebari, nami nikatambua kuwa hao walikuwa makerubi. \v 21 Kila mmoja alikuwa na nyuso nne na mabawa manne, na chini ya mabawa yao kulikuwa na kile kilichoonekana kama mikono ya mwanadamu. \v 22 Nyuso zao zilifanana kama zile nilizokuwa nimeziona kando ya Mto Kebari. Kila mmoja alienda mbele moja kwa moja. \c 11 \s1 Hukumu kwa viongozi wa Israeli \p \v 1 Ndipo Roho wa Mungu akaniinua na kunileta hadi kwenye lango la nyumba ya Mwenyezi Mungu linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango palikuwa na wanaume ishirini na watano. Nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu. \v 2 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Mwanadamu, hawa ndio wafanyao hila na kutoa mashauri potovu katika mji huu. \v 3 Wao husema, ‘Je, hivi karibuni hautakuwa wakati wa kujenga nyumba? Mji huu ni chungu cha kupikia, nasi ndio nyama.’ \v 4 Kwa hiyo tabiri dhidi yao; tabiri, ewe mwanadamu.” \p \v 5 Kisha Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yangu, naye akaniambia niseme: “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Hili ndilo ninyi mnalosema, ee nyumba ya Israeli, lakini ninajua mnalowaza mioyoni mwenu. \v 6 Mmewaua watu wengi katika mji huu na kujaza barabara zake maiti. \p \v 7 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Maiti mlizozitupa huko ndizo nyama, na mji huu ndio chungu, lakini nitawaondoa mtoke huko. \v 8 Mnaogopa upanga, nao upanga huo ndio nitakaouleta dhidi yenu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 9 Nitawaondoa mtoke katika mji na kuwatia mikononi mwa wageni nami nitawaadhibu. \v 10 Mtaanguka kwa upanga, nami nitatimiza hukumu dhidi yenu katika mipaka ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 11 Mji huu hautakuwa chungu kwa ajili yenu, wala hamtakuwa nyama ndani yake. Nitatoa hukumu dhidi yenu katika mipaka ya Israeli. \v 12 Nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, kwa kuwa hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu, bali mmefuata mwenendo wa mataifa yanayowazunguka.” \p \v 13 Basi nilipokuwa nikitoa unabii, Pelatia mwana wa Benaya akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu, nikasema, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi! Je, utaangamiza kabisa mabaki ya Israeli?” \s1 Ahadi ya Wayahudi kurejeshwa \p \v 14 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema: \v 15 “Mwanadamu, ndugu zako, ndugu zako ambao ni wa uhusiano wa damu nawe pamoja na nyumba yote ya Israeli, ndio wale ambao watu wa Yerusalemu wamesema kuwahusu, ‘Wako mbali na Mwenyezi Mungu; nchi hii tulipewa sisi kuwa milki yetu.’ \p \v 16 “Kwa hiyo sema, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ingawa niliwapeleka mbali miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali, hata hivyo, kwa kitambo kidogo, nimekuwa mahali patakatifu kwao katika nchi walizoenda.’ \p \v 17 “Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitawakusanya kutoka mataifa na kuwarudisha kutoka nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’ \p \v 18 “Watairudia nchi na kuondoa vinyago vyote vya upotovu na sanamu zote za kuchukiza. \v 19 Nitawapa moyo usiogawanyika na kuweka roho mpya ndani yao; nitaondoa ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. \v 20 Kisha watafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii sheria zangu. Watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao. \v 21 Lakini kwa wale ambao mioyo yao imeambatana na vinyago vyao vya upotovu na sanamu zao za kuchukiza, nitawalipa kikamilifu kulingana na matendo yao,” asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 22 Ndipo wale makerubi, wenye magurudumu pembeni mwao, wakakunjua mabawa yao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. \v 23 Basi utukufu wa Mwenyezi Mungu ukapaa juu kuanzia katika mji na kutua juu ya mlima ulio mashariki mwa mji. \v 24 Roho akaniinua na kunileta kwa watu wa uhamisho huko Ukaldayo nikiwa katika yale maono niliyopewa na Roho wa Mungu. \p Ndipo maono niliyokuwa nimeyaona yakanitoka, \v 25 nami nikawaeleza wale watu wa uhamisho kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amenionesha. \c 12 \s1 Uhamisho waelezewa kwa ishara \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, unaishi miongoni mwa watu waasi. Wana macho ya kuona, lakini hawaoni, na masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa kuwa ni watu waasi. \p \v 3 “Kwa hiyo, mwanadamu, funga mizigo yako kwa kwenda uhamishoni tena wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toka nje na uende mahali pengine kutoka hapo ulipo. Huenda wataelewa, ingawa wao ni nyumba ya uasi. \v 4 Wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toa nje mizigo yako iliyofungwa kwa ajili ya kwenda uhamishoni. Kisha wakati wa jioni, wakiwa wanakutazama toka nje kama wale wanaoenda uhamishoni. \v 5 Wakiwa wanakutazama, toboa ukuta utolee mizigo yako hapo. \v 6 Beba mizigo hiyo begani mwako wakikuangalia uichukue nje wakati wa giza la jioni. Funika uso wako ili usione nchi, kwa maana nimekufanya ishara kwa nyumba ya Israeli.” \p \v 7 Basi nikafanya kama nilivyoamriwa. Wakati wa mchana nilitoa vitu vyangu nje vilivyofungwa tayari kwa uhamishoni. Kisha wakati wa jioni nikatoboa ukuta kwa mikono yangu. Nikachukua mizigo yangu nje wakati wa giza la jioni, nikiwa nimeibeba mabegani mwangu huku wakinitazama. \p \v 8 Asubuhi neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 9 “Mwanadamu, je, nyumba ile ya uasi ya Israeli haikukuuliza, ‘Unafanya nini?’ \p \v 10 “Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Unabii huu unamhusu mkuu aliye katika Yerusalemu na watu wote wa nyumba ya Israeli walio huko.’ \v 11 Waambie, ‘Mimi ni ishara kwenu.’ \p “Kama vile nilivyotenda, basi litatendeka vivyo hivyo kwao. Wataenda uhamishoni kama mateka. \p \v 12 “Mkuu aliye miongoni mwao atabeba mizigo yake begani wakati wa giza la jioni na kuondoka, na tundu litatobolewa ukutani ili apite. Atafunika uso wake ili asiweze kuiona nchi. \v 13 Nitamtandazia wavu wangu, naye atanaswa kwenye mtego wangu; nitamleta hadi Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko. \v 14 Wote wanaomzunguka nitawatawanya pande zote: watumishi wake na majeshi yake yote; nami nitawafuatilia kwa upanga. \p \v 15 “Wao watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapowatawanya miongoni mwa mataifa, na kuwatapanya katika nchi zote. \v 16 Lakini nitawaokoa wachache wao, wasiuawe kwa upanga, njaa na tauni, ili katika mataifa watakakoenda waweze kukiri matendo yao yote ya kuchukiza. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \p \v 17 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 18 “Mwanadamu, tetemeka unapokula chakula chako, tetemeka kwa hofu unapokunywa maji yako. \v 19 Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu wakaaji wa Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyang’anywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo. \v 20 Miji inayokaliwa na watu itaharibiwa na nchi itakuwa ukiwa. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 21 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 22 “Mwanadamu, ni ipi hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yoyote yanayotimia’? \v 23 Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia ambapo kila ono litatimizwa. \v 24 Kwa maana hapatakuwa tena na maono ya uongo wala ubashiri wa kujipendekeza miongoni mwa watu wa Israeli. \v 25 Lakini Mimi Mwenyezi Mungu nitasema neno nitakalo, nalo litatimizwa bila kuchelewa. Kwa kuwa katika siku zako, ewe nyumba ya uasi, nitatimiza kila nisemalo, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \p \v 26 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 27 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli inasema, ‘Maono yale anayoyaona ni kwa ajili ya miaka mingi ijayo, naye hutabiri kuhusu siku zijazo zilizo mbali.’ \p \v 28 “Kwa hiyo, waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakuna maneno yangu yatakayocheleweshwa tena zaidi, lolote nisemalo litatimizwa, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \c 13 \s1 Manabii wa uongo walaumiwa \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la Mwenyezi Mungu! \v 3 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote! \v 4 Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu. \v 5 Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili isimame imara kwenye vita katika siku ya Mwenyezi Mungu. \v 6 Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Mwenyezi Mungu amesema”, wakati Mwenyezi Mungu hakuwatuma; bado wakitarajia maneno yao kutimizwa. \v 7 Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu, hapo msemapo, “Mwenyezi Mungu asema”, wakati Mimi sijasema? \p \v 8 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa sababu ya maneno yenu ya uongo na maono yenu ya udanganyifu, Mimi niko kinyume nanyi, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 9 Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuorodheshwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli, wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 10 “ ‘Kwa sababu wanapotosha watu wangu, wakisema, “Amani”, wakati hakuna amani; pia kwa sababu, wakati ukuta dhaifu unapojengwa, wanaufunika kwa kupaka chokaa, \v 11 kwa hiyo waambie hao wanaoupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwamba ukuta huo utaanguka. Mvua kubwa ya mafuriko itanyesha, nami nitaleta mvua ya mawe inyeshe kwa nguvu, nao upepo wa dhoruba utavuma juu yake. \v 12 Ukuta utakapoanguka, je, watu hawatawauliza, “Iko wapi chokaa mliyopaka ukuta?” \p \v 13 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika ghadhabu yangu nitauachia upepo wa dhoruba, na katika hasira yangu, mvua ya mawe na ya mafuriko itanyesha, ikiwa na ghadhabu ya kuangamiza. \v 14 Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 15 Hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu dhidi ya huo ukuta na dhidi yao walioupaka chokaa. Nitawaambia ninyi, “Ukuta umebomoka na vivyo hivyo wale walioupaka chokaa, \v 16 wale manabii wa Israeli walioitabiria Yerusalemu na kuona maono ya amani kwa ajili yake wakati hakukuwa na amani, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” ’ \p \v 17 “Sasa, mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya binti za watu wako wanaotabiri mambo kutoka mawazo yao wenyewe. Tabiri dhidi yao \v 18 na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu? \v 19 Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwanenea uongo watu wangu, ambao husikiliza uongo, mmewaua watu ambao hawakustahili kufa, na kuwaacha hai wale ambao walistahili kufa. \p \v 20 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi mnazotumia kuwatega watu kama ndege, nami nitazirarua mikononi mwenu; nitawaweka huru watu mliowatega kama ndege. \v 21 Nitazirarua shela zenu na kuwaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu, nao hawatakuwa tena mawindo ya nguvu zenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 22 Kwa sababu mliwavunja moyo wenye haki kwa uongo wenu, wakati mimi sikuwaletea huzuni na kwa kuwa mliwatia moyo waovu ili wasiziache njia zao mbaya na hivyo kuokoa maisha yao, \v 23 kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \c 14 \s1 Waabudu sanamu walaumiwa \p \v 1 Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu. \v 2 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 3 “Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote? \v 4 Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Mwenyezi Mungu nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu. \v 5 Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.’ \p \v 6 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Tubuni! Acheni sanamu zenu, na matendo yenu yote ya machukizo! \p \v 7 “ ‘Mwisraeli au mgeni yeyote anayeishi Israeli anapojitenga nami, na kujiwekea sanamu moyoni mwake, na hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake, na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, Mimi Mwenyezi Mungu nitamjibu mwenyewe. \v 8 Nitamkabili mtu huyo na kumwadhibu, na kumfanya ishara na mithali. Nitamkatilia mbali kutoka kwa watu wangu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 9 “ ‘Na ikiwa nabii ameshawishika kutoa unabii, Mimi Mwenyezi Mungu nitakuwa nimemshawishi nabii huyo; nami nitaunyoosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli. \v 10 Watawajibika kwa hatia yao: nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake. \p \v 11 “ ‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \s1 Hukumu isiyoepukika \p \v 12 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema, \v 13 “Mwanadamu, nchi ikinitenda dhambi kwa kutokuwa waaminifu nami nikaunyoosha mkono wangu dhidi yake ili kukatilia mbali upatikanaji wake wa chakula na kuipelekea njaa na kuua watu wake na wanyama wao, \v 14 hata kama watu hawa watatu: Nuhu, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, wangeweza kujiokoa hao wenyewe tu kwa uadilifu wao, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 15 “Au nikiwaachilia wanyama pori katika nchi hiyo nao wakaiacha bila watoto, nayo ikawa ukiwa hivi kwamba hakuna mtu apitaye kwa sababu ya wanyama pori, \v 16 hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao peke yao wangeokolewa, lakini nchi ingekuwa ukiwa. \p \v 17 “Au nikileta upanga dhidi ya nchi hiyo na kusema, ‘Upanga na upite katika nchi yote,’ nami nikaua watu wa nchi hiyo na wanyama wao, \v 18 hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa. \p \v 19 “Au nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kupitia kumwaga damu, kuua watu wa nchi hiyo na wanyama wao, \v 20 hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hata kama Nuhu, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao. \p \v 21 “Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao! \v 22 Lakini patakuwa na watakaookoka: wana wa kiume na wa kike watakaoletwa kutoka nchi hiyo. Watakuja kwenu, nanyi mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, mtafarijika kuhusu maafa niliyoleta juu ya Yerusalemu, kwa ajili ya maafa yale yote niliyoleta juu yake. \v 23 Mtafarijika mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, kwani mtajua kuwa sikufanya lolote ndani yake bila sababu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 15 \s1 Yerusalemu mzabibu batili \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora kuliko tawi la mti mwingine wowote ndani ya msitu? \v 3 Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza chochote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuning’inizia vitu kutokana na huo mti wake? \v 4 Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote? \v 5 Kama haukufaa kitu chochote ulipokuwa mzima, je, si zaidi sana sasa ambapo hauwezekani kufanyishwa chochote cha kufaa baada ya moto kuuchoma na kuuacha majivu? \p \v 6 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kama nilivyoutoa mti wa mzabibu miongoni mwa miti ya msituni kuwa nishati ya moto, hivyo ndivyo nitakavyowatendea watu wanaoishi Yerusalemu. \v 7 Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 8 Nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekuwa si waaminifu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 16 \s1 Yerusalemu mwanamke asiye mwaminifu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, kabili Yerusalemu kuhusu matendo yake ya kuchukiza, \v 3 useme, ‘Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi, analomwambia Yerusalemu: Asili na kuzaliwa kwako kulikuwa ni katika nchi ya Wakanaani; baba yako alikuwa Mwamori, naye mama yako alikuwa Mhiti. \v 4 Siku uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuogeshwa kwa maji ili kukufanya safi, wala hukusuguliwa kwa chumvi wala kufunikwa kwa nguo. \v 5 Hakuna yeyote aliyekuonea huruma au kukusikitikia kiasi cha kukutendea mojawapo ya mambo haya. Badala yake, ulipozaliwa ulitupwa nje penye uwanja, kwa kuwa katika siku uliyozaliwa ulidharauliwa. \p \v 6 “ ‘Nami nikapita karibu nawe nikakuona ukigaagaa kwenye damu yako, nawe ulipokuwa umelala hapo penye hiyo damu nikakuambia, “Ishi!” \v 7 Nilikufanya uote kama mmea wa shambani. Ukakua na kuongezeka sana, ukawa kito cha thamani kuliko vyote. Matiti yako yakatokeza na nywele zako zikaota, wewe uliyekuwa uchi na bila kitu chochote. \p \v 8 “ ‘Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, niliutandaza upindo wa vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikakuapia na kuingia kwenye agano na wewe, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nawe ukawa wangu. \p \v 9 “ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta. \v 10 Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa. \v 11 Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako, \v 12 nikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako. \v 13 Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; nguo zako zilikuwa za kitani safi, na hariri, na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana, ukainuka kuwa malkia. \v 14 Umaarufu wako ulifahamika miongoni mwa mataifa kwa ajili ya uzuri wako, kwani ulikuwa mkamilifu kwa ajili ya utukufu wangu niliokuwa nimeuweka juu yako, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 15 “ ‘Lakini ulitumainia uzuri wako na kutumia umaarufu wako kuwa kahaba. Ulifanya uasherati na kila mtu aliyepita, nao uzuri wako ukawa wake. \v 16 Ulichukua baadhi ya mavazi yako, ukayatumia kupamba mahali pako pa juu pa kuabudia, ambapo uliendeleza ukahaba wako. Mambo kama hayo hayastahili kutendeka wala kamwe kufanyika. \v 17 Pia ulichukua vito vizuri nilivyokupa, vito vilivyotengenezwa kwa dhahabu yangu na fedha yangu, ukajitengenezea navyo sanamu za kiume na ukafanya ukahaba nazo. \v 18 Ukayachukua mavazi yako yaliyotariziwa, na kuyavalisha hizo sanamu, ukatoa mbele ya hizo sanamu mafuta yangu na uvumba wangu. \v 19 Pia chakula changu nilichokupa ili ule: unga laini, mafuta ya zeituni na asali, ulivitoa mbele yao kuwa uvumba wa harufu nzuri. Hayo ndiyo yaliyotokea, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 20 “ ‘Nawe uliwachukua wanao wa kiume na wa kike ulionizalia na kuwatoa kafara kuwa chakula kwa sanamu. Je, ukahaba wako haukukutosha? \v 21 Uliwachinja watoto wangu na kuwatoa kafara kwa sanamu. \v 22 Katika matendo yako yote ya machukizo pamoja na ukahaba wako, hukukumbuka siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi kabisa bila kitu chochote, ulipokuwa ukigaagaa kwenye damu yako. \p \v 23 “ ‘Ole! Ole wako! Asema Bwana Mungu Mwenyezi. Pamoja na maovu yako yote mengine, \v 24 Ulijijengea jukwaa na kujifanyia mahali pa fahari pa ibada za sanamu kwenye kila uwanja wa mikutano. \v 25 Katika kila mwanzo wa barabara ulijenga mahali pa fahari pa ibada za sanamu, na kuuaibisha uzuri wako, ukizidi kuutoa mwili wako kwa uzinzi kwa kila apitaye. \v 26 Ulifanya ukahaba wako na Wamisri, majirani zako waliojaa tamaa, ukaichochea hasira yangu kwa kuongezeka kwa uzinzi wako. \v 27 Hivyo niliunyoosha mkono wangu dhidi yako na kuipunguza nchi yako; nikakutia kwenye ulafi wa adui zako, binti za Wafilisti, walioshtushwa na tabia yako ya uasherati. \v 28 Ulifanya ukahaba na Waashuru pia, kwa kuwa hukuridhika, hata baada ya hayo, ukawa bado hukutosheleka. \v 29 Ndipo uliuzidisha uzinzi wako kwa kujumuisha Ukaldayo, nchi ya wafanyabiashara; lakini hata katika hili hukutosheka. \p \v 30 “ ‘Tazama jinsi ulivyo na dhamiri dhaifu, asema Bwana Mungu Mwenyezi, unapofanya mambo haya yote, unatenda kama kahaba asiye aibu! \v 31 Ulipojenga jukwaa lako katika mwanzo wa kila barabara, na kutengeneza mahali pako pa fahari pa ibada za sanamu katika kila kiwanja cha wazi, hukuwa kama kahaba, kwa sababu ulidharau malipo. \p \v 32 “ ‘Wewe mke mzinzi! Unapenda wageni, kuliko mume wako mwenyewe. \v 33 Kila kahaba hupokea malipo, lakini wewe hutoa zawadi kwa wapenzi wako wote, ukiwahonga ili waje kwako kutoka kila mahali kwa ajili ya ukahaba wako. \v 34 Kwa hiyo wewe ulikuwa tofauti na wanawake wengine kwenye ukahaba wako. Hakuna aliyekutongoza ili kuzini naye, bali wewe ulikuwa tofauti kabisa, kwani ulilipa wakati hakuna malipo uliyolipwa wewe. \p \v 35 “ ‘Kwa hiyo, wewe kahaba, sikia neno la Mwenyezi Mungu! \v 36 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa kuwa umemwaga tamaa zako na kuonesha uchi wako katika uzinzi wako kwa wapenzi wako na kwa sababu ya sanamu zako zote za machukizo na kwa sababu uliwapa damu ya watoto wako, \v 37 kwa hiyo nitawakusanya wapenzi wako wote, wale uliojifurahisha nao: wale uliowapenda kadhalika na wale uliowachukia. Nitawakusanya wote dhidi yako kutoka pande zote, na nitakuvua nguo mbele yao, nao wataona uchi wako wote. \v 38 Nitakuhukumia adhabu wanayopewa wanawake wafanyao uasherati na hao wanaomwaga damu; nitaleta juu yako kisasi cha damu cha ghadhabu yangu na hasira yangu yenye wivu. \v 39 Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada za sanamu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu. \v 40 Wataleta kundi la watu dhidi yako, watakaokupiga kwa mawe na kukukatakata vipande vipande kwa panga zao. \v 41 Watachoma nyumba zako na kutekeleza adhabu juu yako machoni pa wanawake wengi. Nitakomesha ukahaba wako, nawe hutawalipa tena wapenzi wako. \v 42 Ndipo ghadhabu yangu dhidi yako itapungua, na hasira yangu yenye wivu itakuondokea. Nitatulia, wala sitakasirika tena. \p \v 43 “ ‘Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, lakini ulinighadhibisha kwa mambo haya yote, hakika nitaleta juu ya kichwa chako yale uliyotenda, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Je, hukuongeza uasherati juu ya matendo yako mengine ya kuchukiza? \p \v 44 “ ‘Kila mtu anayetumia mithali atatumia mithali hii kukuhusu: “Alivyo mama, ndivyo alivyo bintiye.” \v 45 Wewe ni binti halisi wa mama yako, ambaye alimdharau mume wake na watoto wake; tena wewe ni dada halisi wa dada zako, waliowadharau waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako alikuwa Mwamori. \v 46 Dada yako mkubwa alikuwa Samaria, aliyeishi upande wako wa kaskazini na binti zake; naye dada yako mdogo, aliyeishi kusini mwako pamoja na binti zake, alikuwa Sodoma. \v 47 Hukuenda katika njia zao tu na kuiga matendo yao ya kuchukiza, bali baada ya muda mfupi, ulipotoka zaidi yao katika njia zako zote \v 48 Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, dada yako Sodoma pamoja na binti zake, kamwe hawakufanya yale ambayo wewe na binti zako mmefanya. \p \v 49 “ ‘Sasa hii ndiyo ilikuwa dhambi ya dada yako Sodoma: yeye na binti zake walikuwa wenye kujigamba, walafi na wasiojali; hawakuwasaidia maskini na wahitaji. \v 50 Walijivuna na kufanya mambo ya kuchukiza sana mbele zangu. Kwa hiyo niliwakatilia mbali nami kama mlivyoona. \v 51 Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi ulizofanya. Wewe umefanya mambo mengi sana ya kuchukiza kuwaliko, nawe umewafanya dada zako waonekane kama wenye haki kwa ajili ya mambo haya yote uliyoyafanya. \v 52 Chukua aibu yako, kwa kuwa umefanya uovu wa dada zako uwe si kitu, nao waonekane kama wenye haki. Kwa kuwa dhambi zako zilikuwa mbaya kuliko zao, wameonekana wenye haki zaidi yako. Kwa hiyo basi, chukua aibu yako, kwa kuwa umewafanya dada zako waonekane wenye haki. \p \v 53 “ ‘Lakini nitarudisha baraka za Sodoma na binti zake na za Samaria na binti zake, nami nitarudisha baraka zako pamoja na zao, \v 54 ili upate kuchukua aibu yako na kufedheheka kwa ajili ya yote uliyotenda ambayo yamekuwa faraja kwao wakijilinganisha na wewe. \v 55 Nao dada zako, Sodoma na binti zake na Samaria na binti zake, watarudishwa kama vile walivyokuwa mwanzoni, nawe pamoja na binti zako mtarudishwa kama mlivyokuwa hapo awali. \v 56 Hukuweza hata kumtaja dada yako Sodoma kwa sababu ya dharau yako katika siku za kiburi chako, \v 57 kabla uovu wako haujafunuliwa. Hata hivyo, sasa unadhihakiwa na binti za Shamu na majirani zake wote, na binti za Wafilisti, wale wote wanaokuzunguka wanakudharau. \v 58 Utachukua matokeo ya uasherati wako na matendo yako ya kuchukiza, asema Mwenyezi Mungu. \p \v 59 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitakutendea kama unavyostahili, kwa kuwa umedharau kiapo changu kwa kuvunja agano. \v 60 Lakini nitakumbuka agano nililolifanya nawe wakati wa ujana wako, nami nitaweka nawe agano imara la milele. \v 61 Ndipo utakapozikumbuka njia zako na kuona aibu utakapowapokea dada zako, wale walio wakubwa wako na wadogo wako. Nitakupa hao wawe binti zako, lakini si katika msingi wa agano langu na wewe. \v 62 Hivyo nitalifanya imara agano langu na wewe, nawe utajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 63 Basi, nitakapofanya upatanisho kwa ajili yako, kwa yale yote uliyoyatenda, utakumbuka na kuaibika, nawe kamwe hutafumbua tena kinywa chako kwa sababu ya aibu yako, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \c 17 \s1 Tai wawili na mizabibu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo. \v 3 Waambie hivi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi, \v 4 akakwanyua ncha yake na kuichukua hadi nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi. \p \v 5 “ ‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi, \v 6 nazo zikaota na kuwa mzabibu mfupi, unaoeneza matawi yake. Matawi yake yakamwelekea huyo tai, mizizi yake ikabaki chini ya huo mzabibu. Kwa hiyo ukawa mzabibu na kutoa matawi na vitawi vyenye majani mengi. \p \v 7 “ ‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa, na kutanda matawi yake kumwelekea ili aunyweshe maji. \v 8 Ulikuwa umepandwa katika udongo mzuri wenye maji mengi ili uweze kutoa matawi, kuzaa matunda, na uweze kuwa mzabibu mzuri sana.’ \p \v 9 “Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Je, utastawi? Je, hautang’olewa na kuondolewa matunda yake, ili uweze kunyauka? Majani yake mapya yanayochipua yote yatanyauka. Hautahitaji mkono wenye nguvu au watu wengi kuung’oa na mizizi yake. \v 10 Hata kama utapandwa pengine, je, utastawi? Je, hautanyauka kabisa wakati upepo wa mashariki utakapoupiga, yaani hautanyauka kabisa katika udongo mzuri ambamo ulikuwa umestawi vizuri?’ ” \p \v 11 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 12 “Waambie nyumba hii ya uasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alienda Yerusalemu na kumchukua mfalme wake na watu wake maarufu, akawaleta Babeli. \v 13 Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya mfalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi, \v 14 ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake. \v 15 Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke? \p \v 16 “ ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha kwenye kiti cha utawala, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake. \v 17 Farao pamoja na jeshi lake kubwa na watu wake wengi hawataweza kusaidia chochote katika vita, watakapozingirwa na jeshi likitaka kuangamiza watu wengi. \v 18 Alidharau kiapo kwa kulivunja agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka. \p \v 19 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakika kama niishivyo, nitamwadhibu kwa kudharau kiapo changu, na kulivunja agano langu. \v 20 Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu. \v 21 Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimesema. \s1 Hatimaye Israeli kutukuzwa \p \v 22 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana. \v 23 Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina watajenga viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake. \v 24 Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. \p “ ‘Mimi Mwenyezi Mungu nimesema, nami nitatenda.’ ” \c 18 \s1 Atendaye dhambi atakufa \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: \q1 “ ‘Baba wamekula zabibu chachu, \q2 nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’? \p \v 3 “Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. \v 4 Kwa kuwa kila roho ni mali yangu; kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. \q1 \v 5 “Mtu aweza kuwa ni mwenye haki \q2 atendaye yaliyo haki na sawa. \q1 \v 6 Hakula katika mahali pa ibada za sanamu \q2 kwenye milima, \q1 wala hakuziinulia macho sanamu \q2 za nyumba ya Israeli. \q1 Hakumtia unajisi mke wa jirani yake, \q2 wala hakukutana kimwili na mwanamke \q2 wakati wa siku zake za hedhi. \q1 \v 7 Hamdhulumu yeyote, \q2 bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake. \q1 Hanyang’anyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake \q2 na huwapa nguo walio uchi. \q1 \v 8 Hakopeshi kwa riba \q2 wala hajipatii faida ya ziada. \q1 Huuzuia mkono wake usifanye mabaya, \q2 naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu. \q1 \v 9 Huzifuata amri zangu \q2 na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu. \q1 Huyo mtu ni mwenye haki; \q2 hakika ataishi, \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 10 “Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya \v 11 (ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya): \q1 “Hula katika mahali pa ibada za sanamu kwenye milima. \q1 Humtia unajisi mke wa jirani yake. \q1 \v 12 Huwadhulumu maskini na wahitaji. \q1 Hunyang’anyana. \q1 Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake. \q1 Huziinulia sanamu macho. \q1 Hufanya mambo ya machukizo. \q1 \v 13 Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada. \m Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. \p \v 14 “Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya: \q1 \v 15 “Hakula katika mahali pa ibada za sanamu \q2 kwenye milima, \q1 wala hainulii macho sanamu \q2 za nyumba ya Israeli. \q1 Hakumtia unajisi \q2 mke wa jirani yake. \q1 \v 16 Hamdhulumu yeyote \q2 wala kutaka rehani kwa ajili ya mkopo. \q1 Hanyang’anyi, \q2 bali huwapa wenye njaa chakula chake \q2 na huwapa nguo walio uchi. \q1 \v 17 Huuzuia mkono wake usitende dhambi, \q2 hakopeshi kwa riba \q2 wala hajipatii faida ya ziada. \q1 Huzishika amri zangu \q2 na kuzifuata sheria zangu. \m Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi. \v 18 Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alikuwa mnyang’anyi, akampokonya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake. \p \v 19 “Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi. \v 20 Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake. \p \v 21 “Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa. \v 22 Hakuna kosa lolote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi. \v 23 Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema Bwana Mungu Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka njia zao mbaya na kuishi? \p \v 24 “Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa. \p \v 25 “Lakini mnasema, ‘Njia ya Bwana si ya haki.’ Sikia, ee nyumba ya Israeli: Je, njia yangu siyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki? \v 26 Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa. \v 27 Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake. \v 28 Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa. \v 29 Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki? \p \v 30 “Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu. \v 31 Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, ee nyumba ya Israeli? \v 32 Kwa maana sifurahii kifo cha mtu yeyote, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi! \c 19 \s1 Maombolezo kwa ajili ya wakuu wa Israeli \p \v 1 “Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli \v 2 na useme: \q1 “ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike \q2 miongoni mwa simba! \q1 Alilala katikati ya wana simba \q2 na kulisha watoto wake. \q1 \v 3 Alimlea mmoja wa watoto wake, \q2 naye akawa simba mwenye nguvu. \q1 Akajifunza kurarua mawindo \q2 naye akala watu. \q1 \v 4 Mataifa wakasikia habari zake, \q2 naye akanaswa katika shimo lao. \q1 Wakamwongoza kwa ndoana \q2 hadi nchi ya Misri. \b \q1 \v 5 “ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki, \q2 nayo matarajio yake yametoweka, \q1 akamchukua mwanawe mwingine \q2 na kumfanya simba mwenye nguvu. \q1 \v 6 Alizungukazunguka miongoni mwa simba, \q2 kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu. \q1 Akajifunza kurarua mawindo \q2 naye akala watu. \q1 \v 7 Akabomoa ngome zao \q2 na kuiharibu miji yao. \q1 Nchi na wote waliokuwa ndani yake \q2 wakatiwa hofu kwa kunguruma kwake. \q1 \v 8 Kisha mataifa wakaja dhidi yake \q2 kutoka sehemu zilizomzunguka. \q1 Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake, \q2 naye akanaswa katika shimo lao. \q1 \v 9 Wakamvutia kwenye tundu kwa kutumia ndoana, \q2 wakamleta kwa mfalme wa Babeli. \q1 Wakamfunga gerezani, hivyo kunguruma kwake \q2 hakukusikika tena \q2 katika milima ya Israeli. \b \q1 \v 10 “ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibu \q2 katika shamba lako la mizabibu \q2 uliopandwa kando ya maji, \q1 ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengi \q2 kwa sababu ya wingi wa maji. \q1 \v 11 Matawi yake yalikuwa na nguvu, \q2 yaliyofaa kuwa fimbo ya mtawala. \q1 Ulikuwa mrefu kupita miti mingine \q2 katikati ya matawi manene; \q1 ulionekana kwa urahisi \q2 kwa ajili ya urefu wake \q2 na wingi wa matawi yake. \q1 \v 12 Lakini uling’olewa kwa hasira kali \q2 na kutupwa chini. \q1 Upepo wa mashariki uliufanya usinyae, \q2 matunda yake yakapukutika, \q1 matawi yake yenye nguvu yakanyauka \q2 na moto ukayateketeza. \q1 \v 13 Sasa umepandwa jangwani \q2 katika nchi kame na ya kiu. \q1 \v 14 Moto ulienea kuanzia mojawapo ya matawi yake makubwa \q2 na kuteketeza matunda yake. \q1 Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yake \q2 linalofaa kuwa fimbo ya mtawala.’ \m Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.” \c 20 \s1 Israeli waasi \p \v 1 Katika mwaka wa saba, mwezi wa tano siku ya kumi, baadhi ya wazee wa Israeli wakaja ili kutaka ushauri kwa Mwenyezi Mungu, wakaketi mbele yangu. \p \v 2 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 3 “Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa nini mmekuja? Je, ni kutaka ushauri kwangu? Hakika kama niishivyo, sitawaruhusu mtake ushauri toka kwangu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ \p \v 4 “Je, utawahukumu? Je, mwanadamu, utawahukumu? Basi uwakabili kwa ajili ya machukizo ya baba zao \v 5 na uwaambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Siku ile nilipochagua Israeli, niliwaapia wazao wa nyumba ya Yakobo kwa mkono ulioinuliwa nami nikajidhihirisha kwao huko Misri. Kwa mkono ulioinuliwa niliwaambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.” \v 6 Siku ile niliwaapia kwamba nitawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta katika nchi niliyowachagulia, nchi inayotiririka maziwa na asali, nchi nzuri kupita zote. \v 7 Nami nikawaambia, “Kila mmoja wenu aondolee mbali sanamu za chukizo ambazo mmekazia macho, nanyi msijitie unajisi kwa sanamu za Misri. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.” \p \v 8 “ ‘Lakini waliniasi na hawakunisikiliza, hawakuondolea mbali sanamu za machukizo ambazo walikuwa wamezikazia macho, wala kuondolea mbali sanamu za Misri. Ndipo nikasema, nitawamwagia ghadhabu yangu na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko Misri. \v 9 Lakini kwa ajili ya Jina langu niliwatoa katika nchi ya Misri. Nilifanya hivyo ili kulinda Jina langu lisinajisiwe machoni mwa mataifa walioishi miongoni mwao, na ambao machoni pao nilikuwa nimejifunua kwa Waisraeli. \v 10 Kwa hiyo nikawaongoza watoke Misri na kuwaleta jangwani. \v 11 Nikawapa amri zangu na kuwajulisha sheria zangu, kwa kuwa mtu anayezitii ataishi kwa hizo. \v 12 Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu niliwafanya watakatifu. \p \v 13 “ ‘Lakini watu wa Israeli waliniasi Mimi jangwani. Hawakufuata amri zangu, bali walikataa sheria zangu, ingawa mtu yule anayezitii ataishi kwa hizo sheria, nao walizinajisi Sabato zangu kabisa. Hivyo nilisema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwaangamiza huko jangwani. \v 14 Lakini kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile ambacho kitalifanya Jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli. \v 15 Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba nisingewaingiza katika nchi niliyowapa, nchi inayotiririka maziwa na asali, nchi nzuri kuliko zote, \v 16 kwa sababu walikataa sheria zangu na hawakufuata amri zangu, na wakazinajisi Sabato zangu. Kwa kuwa mioyo yao iliandama sanamu zao. \v 17 Lakini niliwahurumia, wala sikuwaangamiza wala kuwafuta kabisa jangwani. \v 18 Niliwaambia watoto wao kule jangwani, “Msifuate amri za baba zenu wala kushika sheria zao au kujinajisi kwa sanamu zao. \v 19 Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu; fuateni amri zangu, tena kuweni waangalifu kushika sheria zangu. \v 20 Zitakaseni Sabato zangu ili ziwe ishara kati yangu nanyi. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.” \p \v 21 “ ‘Lakini watoto hao wakaniasi: Hawakufuata amri zangu, wala hawakuwa waangalifu kushika sheria zangu, ingawa mtu anayezitii anaishi kwa hizo sheria, nao wakazinajisi Sabato zangu. Hivyo nikasema ningemwaga ghadhabu yangu juu yao na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko jangwani. \v 22 Lakini nikauzuia mkono wangu, na kwa ajili ya Jina langu nikafanya kile kingezuia Jina langu kunajisiwa machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli. \v 23 Tena kwa mkono ulioinuliwa nikawaapia huko jangwani kwamba ningewatawanya miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali, \v 24 kwa sababu hawakutii sheria zangu lakini walikuwa wamekataa amri zangu na kuzinajisi Sabato zangu, nayo macho yao yakatamani sanamu za baba zao. \v 25 Pia niliwaacha wafuate amri ambazo hazikuwa nzuri na sheria ambazo mtu hawezi kuishi kwa hizo sheria. \v 26 Nikawaacha wanajisiwe kwa matoleo yao ya kuwatoa kafara wazaliwa wao wa kwanza kwa sanamu, ili nipate kuwajaza na hofu hadi wajue kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ \p \v 27 “Kwa hiyo, mwanadamu, sema na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika jambo hili pia, baba zenu walinikufuru kwa kuniacha mimi: \v 28 Nilipowaleta katika nchi niliyokuwa nimeapa kuwapa na kuona kilima chochote kirefu au mti wowote wenye majani mengi, huko walitoa dhabihu zao, wakatoa sadaka ambazo zilichochea hasira yangu, wakafukiza uvumba wenye harufu nzuri na kumimina sadaka zao za kinywaji. \v 29 Ndipo nikawaambia: Ni nini maana yake hapa mahali pa juu pa kuabudia mnapopaendea?’ ” (Basi mahali pale panaitwa Bama\f + \fr 20:29 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mahali pa juu pa kuabudia\fqa*\f* hata leo.) \s1 Hukumu na kurudishwa \p \v 30 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Je, mtajinajisi kama vile baba zenu walivyofanya na kutamani vinyago vyao vya machukizo? \v 31 Mnapotoa matoleo yenu, yaani kutoa kafara watoto wenu motoni, mnaendelea kujinajisi na sanamu zenu zote hadi leo. Je, niulizwe ushauri na ninyi, ee nyumba ya Israeli? Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, mimi sitaulizwa ushauri na ninyi. \p \v 32 “ ‘Lile lililoko mioyoni mwenu kamwe halitatokea, mnaposema, “Tunataka tuwe kama mataifa mengine, kama watu wengine wa dunia, wanaotumikia miti na mawe.” \v 33 Hakika kama niishivyo asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitawatawala kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyooshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika. \v 34 Nitawatoa toka katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mlikotawanywa, kwa mkono wa nguvu na kwa mkono ulionyooshwa na kwa ghadhabu iliyomwagwa. \v 35 Nitawaleta katika jangwa la mataifa na huko nitatekeleza hukumu juu yenu uso kwa uso. \v 36 Kama nilivyowahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, ndivyo nitakavyowahukumu ninyi, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 37 Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, nami nitawaleta katika mkataba wa agano. \v 38 Nitawaondoa miongoni mwenu wale wanaohalifu na wale wanaoasi dhidi yangu. Ingawa nitawatoa katika nchi wanazoishi, hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 39 “ ‘Kwenu ninyi, ee nyumba ya Israeli, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nendeni mkatumikie sanamu zenu, kila mmoja wenu! Lakini baadaye hakika mtanisikiliza mimi nanyi hamtalinajisi tena Jina langu takatifu, kwa matoleo yenu na sanamu zenu. \v 40 Kwa kuwa katika mlima wangu mtakatifu, mlima mrefu wa Israeli, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hapo katika nchi nyumba yote ya Israeli itanitumikia mimi, nami huko nitawakubali. Huko nitataka sadaka zenu na matoleo ya malimbuko yenu, pamoja na dhabihu zenu takatifu zote. \v 41 Nitawakubali ninyi kama uvumba wenye harufu nzuri wakati nitakapowatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mlipokuwa mmetawanyika, nami nitajionesha kuwa mtakatifu miongoni mwenu na machoni mwa mataifa. \v 42 Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, nchi niliyokuwa nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu. \v 43 Hapo ndipo nitakapokumbuka mwenendo wenu na matendo yenu yote ambayo kwayo mlijitia unajisi, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya maovu yote mliyokuwa mmetenda. \v 44 Nanyi mtajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapowatendea kwa ajili ya Jina langu, wala si sawasawa na njia zenu mbaya na matendo yenu maovu, ee nyumba ya Israeli, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \s1 Unabii dhidi ya kusini \p \v 45 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 46 “Mwanadamu, uelekeze uso wako upande wa kusini, hubiri dhidi ya upande wa kusini, na utoe unabii dhidi ya msitu wa Negebu. \v 47 Waambie watu wa Negebu: ‘Sikieni neno la Mwenyezi Mungu. Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninakaribia kukuwasha moto, nao utateketeza miti yako yote, mibichi na iliyokauka. Miali ya moto haitaweza kuzimwa na kila uso kutoka kusini mpaka kaskazini utakaushwa kwa moto huo. \v 48 Kila mmoja ataona kuwa Mimi Mwenyezi Mungu ndiye niliyeuwasha huo moto; nao hautazimwa.’ ” \p \v 49 Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mungu Mwenyezi! Wao hunisema, ‘Huyu si huzungumza mafumbo tu?’ ” \c 21 \s1 Babeli, upanga wa Mungu wa hukumu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, uelekeze uso wako juu ya Yerusalemu na uhubiri dhidi ya mahali patakatifu. Tabiri dhidi ya nchi ya Israeli \v 3 uiambie: ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Mimi niko kinyume nawe. Nitautoa upanga wangu kwenye ala yake na kumkatilia mbali mwenye haki na mwovu. \v 4 Kwa sababu nitamkatilia mbali mwenye haki na mwovu, upanga wangu utatolewa alani mwake uwe dhidi ya kila mtu kuanzia kusini hadi kaskazini. \v 5 Ndipo watu wote watajua ya kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimeutoa upanga wangu kwenye ala yake, nao hautarudi humo tena.’ \p \v 6 “Kwa hiyo lia kwa uchungu, mwanadamu! Lia kwa uchungu mbele yao kwa moyo uliopondeka na kwa huzuni nyingi. \v 7 Nao watakapokuuliza, ‘Kwa nini unalia kwa uchungu?’ Utasema hivi, ‘Kwa sababu ya habari zinazokuja. Kila moyo utayeyuka na kila mkono utalegea, kila roho itazimia na kila goti litalegea kama maji.’ Habari hizo zinakuja! Hakika zitatendeka, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \p \v 8 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema: \v 9 “Mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: \q1 “ ‘Upanga, upanga, \q2 ulionolewa na kusuguliwa: \q1 \v 10 umenolewa kwa ajili ya mauaji, \q2 umesuguliwa ili ung’ae kama miali ya radi! \p “ ‘Je, tuifurahie fimbo ya utawala ya mwanangu Yuda? Upanga unadharau kila fimbo kama hiyo. \q1 \v 11 “ ‘Upanga umewekwa tayari ili kusuguliwa, \q2 ili upate kushikwa mkononi, \q1 umenolewa na kusuguliwa, \q2 umewekwa tayari kwa mkono wa muuaji. \q1 \v 12 Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu, \q2 kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu; \q2 u dhidi ya wakuu wote wa Israeli. \q1 Wametolewa wauawe kwa upanga \q2 pamoja na watu wangu. \q1 Kwa hiyo pigapiga kifua chako. \p \v 13 “ ‘Lazima kuwe na kujaribiwa. Itakuwaje basi ikiwa fimbo ya ufalme ya Yuda inayodharauliwa na upanga haitakuwepo tena? asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ \q1 \v 14 “Hivyo basi, mwanadamu, tabiri \q2 na ukapige makofi. \q1 Upanga wako na upige mara mbili, \q2 naam, hata mara tatu. \q1 Ni upanga wa mauaji, \q2 upanga wa mauaji makuu, \q2 ukiwashambulia kutoka kila upande. \q1 \v 15 Ili mioyo ipate kuyeyuka \q2 na wanaouawa wawe wengi, \q1 nimeweka upanga wa mauaji \q2 kwenye malango yao yote. \q1 Lo! Umetengenezwa umetemete kama miali ya radi, \q2 umeshikwa kwa ajili ya kuua. \q1 \v 16 Ee upanga, kata upande wa kuume, \q2 kisha upande wa kushoto, \q2 mahali popote makali yako yatakapoelekezwa. \q1 \v 17 Mimi nami nitapiga makofi, \q2 nayo ghadhabu yangu itapungua. \q1 Mimi Mwenyezi Mungu nimesema.” \p \v 18 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 19 “Mwanadamu, weka alama njia mbili ambazo upanga wa mfalme wa Babeli utapitia, njia hizo zikianzia katika nchi hiyo hiyo. Weka kibao pale ambapo njia zinagawanyika kuelekea mjini. \v 20 Weka alama njia moja kwa ajili ya upanga upate kuja dhidi ya Raba ya Waamoni na nyingine upate kuja dhidi ya Yuda na Yerusalemu iliyozungushiwa ngome. \v 21 Kwa kuwa mfalme wa Babeli sasa amesimama katika njia panda, katika makutano ya njia mbili, akipiga ramli: anapiga kura kwa kutumia mishale, anataka shauri kwa sanamu zake, anachunguza maini ya wanyama. \v 22 Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka magogo ya kubomoa, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka magogo ya kubomoa dhidi ya malango, kupandisha kilima hadi kuta zako, na kujenga husuru dhidi yako. \v 23 Itakuwa kama kupiga ramli kwa uongo kwa wale watu ambao wameapa kumtii yeye. Lakini mfalme wa Babeli atawakumbusha kuhusu uovu wao na kuwachukua mateka. \p \v 24 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu ninyi mmefanya uovu wenu ukumbukwe kwa kuasi waziwazi, mkidhihirisha dhambi zenu katika yale yote mnayoyafanya: kwa kuwa mmefanya hivi, mtachukuliwa mateka. \p \v 25 “ ‘Ee mtawala kafiri na mwovu wa Israeli, ambaye siku yake imewadia, ambaye wakati wake wa adhabu umefikia kilele chake; \v 26 hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Vua kilemba, ondoa taji. Kwa kuwa mambo hayatakuwa vile yalivyokuwa. Aliye mnyonge atakwezwa, na aliyekwezwa atashushwa. \v 27 Mahame! Mahame! Nitaufanya mji kuwa mahame! Hautajengwa upya hadi aje yule aliye mwenye taji kwa haki; huyo ndiye nitakayempa.’ \p \v 28 “Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kuhusu Waamoni na matukano yao: \q1 “ ‘Upanga, upanga, \q2 umefutwa kwa ajili ya kuua, \q1 umesuguliwa ili kuangamiza \q2 na unametameta kama miali ya radi! \q1 \v 29 Wakati wanatoa maono ya uongo juu yako, \q2 na wanapobashiri uongo juu yako, \q1 upanga utawekwa kwenye shingo \q2 za wapotovu watakaouawa, \q1 wale siku yao imewadia, \q2 wakati wa adhabu yao ya mwisho. \b \q1 \v 30 “ ‘Urudishe upanga kwenye ala yake! \q2 Katika mahali ulipoumbiwa, \q1 katika nchi ya baba zako, \q2 huko nitakuhukumu. \q1 \v 31 Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako \q2 na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako; \q1 nitakutia mikononi mwa watu wakatili, \q2 watu stadi katika kuangamiza. \q1 \v 32 Mtakuwa kuni za kuwashia moto, \q2 damu yenu itamwagwa katika nchi yenu, \q2 wala hamtakumbukwa tena; \q1 kwa maana Mimi Mwenyezi Mungu nimesema.’ ” \c 22 \s1 Dhambi za Yerusalemu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \b \p \v 2 “Mwanadamu, je, wewe utauhukumu? Je, utauhukumu huu mji unaomwaga damu? Basi uujulishe kuhusu matendo yake yote ya machukizo \v 3 uuambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ee mji unaojiletea maangamizi wenyewe kwa kumwaga damu ndani yake na kujinajisi wenyewe kwa kutengeneza sanamu, \v 4 umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga, na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote. \v 5 Wale walio karibu na wale walio mbali watakudhihaki, ewe mji wenye sifa mbaya, uliyejaa ghasia. \p \v 6 “ ‘Tazama jinsi kila mkuu wa Israeli aliye ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu. \v 7 Ndani yako wamewadharau baba na mama; ndani yako wamewatendea wageni udhalimu, na kuwadhulumu yatima na wajane. \v 8 Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu. \v 9 Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za sanamu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati. \v 10 Ndani yako wako wale wanaovunjia heshima vitanda vya baba zao, ndani yako wamo wale wanaowatendea wanawake jeuri wakiwa katika hedhi, wakati wakiwa najisi. \v 11 Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti ya baba yake hasa. \v 12 Ndani yako watu hupokea rushwa ili kumwaga damu, mnapokea riba na faida ya ziada na kupata faida isiyokuwa halali kutoka kwa majirani ili kupata faida kubwa kupita kiasi. Nawe umenisahau mimi, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 13 “ ‘Hakika nitapiga makofi kwa ajili ya faida isiyo halali uliyojipatia na kwa damu uliyoimwaga ndani yako. \v 14 Je, ujasiri wako utadumu au mikono yako itakuwa na nguvu siku hiyo nitakapokuadhibu? Mimi Mwenyezi Mungu nimesema na nitalifanya. \v 15 Nitakutawanya miongoni mwa mataifa na kukutapanya katika nchi mbalimbali nami nitakomesha unajisi wako. \v 16 Baada ya kunajisika mbele ya mataifa, utajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 17 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 18 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa takataka ya chuma kwangu; wote wamekuwa shaba, bati, chuma na risasi iliyoachwa kalibuni. Wao ni taka ya madini ya fedha tu. \v 19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa kuwa wote mmekuwa takataka ya chuma, nitawakusanya Yerusalemu. \v 20 Kama vile watu wakusanyavyo fedha, shaba, chuma, risasi na bati kalibuni ili kuyeyusha kwa moto mkali, ndivyo nitakavyowakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu kuwaweka ndani ya mji na kuwayeyusha. \v 21 Nitawakusanya na kupuliza juu yenu moto wa hasira yangu na ghadhabu yangu nanyi mtayeyushwa ndani ya huo mji. \v 22 Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’ ” \p \v 23 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena kusema: \v 24 “Mwanadamu, iambie nchi, ‘Wewe ni nchi ambayo haijatakaswa wala kunyeshewa katika siku ya ghadhabu.’ \v 25 Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake. \v 26 Makuhani wake wameihalifu sheria yangu na kunajisi vitu vyangu vitakatifu, hawatofautishi kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida. Wanafundisha kuwa hakuna tofauti kati ya vitu vilivyo najisi na visivyo najisi, nao wanafumba macho yao katika kutunza Sabato zangu, hivyo katikati yao nimetiwa unajisi. \v 27 Maafisa wake walio ndani yake ni kama mbwa-mwitu wararuao mawindo yao, wanamwaga damu na kuua watu ili kupata faida ya udhalimu. \v 28 Manabii wake wanapaka chokaa matendo haya kwa maono ya uongo na utabiri wa udanganyifu. Wanasema, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi,’ wakati Mwenyezi Mungu hajasema. \v 29 Watu wa nchi wanatoza kwa nguvu na kufanya unyang’anyi, wanawadhulumu maskini na wahitaji, na kuwaonea wageni, wakiwanyima haki. \p \v 30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, ambaye angejenga ukuta na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka kwa ajili ya watu wa nchi ili nisije nikaiangamiza, lakini sikumwona mtu yeyote. \v 31 Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao na kuwateketeza kwa moto wa hasira yangu, nikiyaleta juu ya vichwa vyao yale yote waliyotenda, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 23 \s1 Dada wawili makahaba \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, palikuwa na wanawake wawili, binti za mama mmoja. \v 3 Wakawa makahaba huko Misri, wakajitia kwenye ukahaba tangu ujana wao. Katika nchi ile vifua vyao vya ubikira vikakumbatiwa, na wakapoteza ubikira wao. \v 4 Mkubwa aliitwa Ohola, na mdogo wake Oholiba. Walikuwa wangu nao wakazaa watoto wa kiume na wa kike. Ohola ni Samaria, Oholiba ni Yerusalemu. \p \v 5 “Ohola akajitia kwenye ukahaba alipokuwa bado ni wangu, akatamani sana wapenzi wake, mashujaa Waashuru, \v 6 waliovaa nguo za buluu, watawala na majemadari, wote walikuwa wanaume vijana wa kuvutia, wapandao farasi. \v 7 Akafanya ukahaba na wakuu wote wa Ashuru, na kujinajisi kwa sanamu zote za kila mwanaume aliyemtamani. \v 8 Hakuacha ukahaba wake aliouanza huko Misri, wakati wa ujana wake ambapo wanaume walilala naye, wakikumbatia kifua cha ubikira wake na kumwaga tamaa zao juu yake. \p \v 9 “Kwa hiyo nilimtia mikononi mwa wapenzi wake, Waashuru, kwa kuwa ndio aliowatamani. \v 10 Wakamvua nguo zake wakamwacha uchi, wakawachukua wanawe wa kiume na wa kike, naye wakamuua kwa upanga. Akawa kitu cha kudharauliwa miongoni mwa wanawake, na adhabu ikatolewa dhidi yake. \p \v 11 “Oholiba dada yake aliliona jambo hili, lakini kwa tamaa zake na ukahaba wake, akaharibu tabia zake kuliko Ohola, dada yake. \v 12 Yeye naye aliwatamani Waashuru, watawala na majemadari, mashujaa waliovalia sare, wapandao farasi, wanaume vijana wote waliovutia. \v 13 Nikaona kuwa yeye pia alijinajisi, wote wawili wakaelekea njia moja. \p \v 14 “Lakini yeye akazidisha ukahaba wake. Akaona wanaume waliochorwa ukutani, picha za Wakaldayo\f + \fr 23:14 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Wababeli\fqa*\f* waliovalia nguo nyekundu, \v 15 wakiwa na mikanda viunoni mwao na vilemba vichwani mwao, wote walifanana na maafisa wa Babeli wapandao magari ya vita, wenyeji wa Ukaldayo\f + \fr 23:15 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Babeli\fqa*\f*. \v 16 Mara tu alipowaona, aliwatamani, akatuma wajumbe kwao huko Ukaldayo. \v 17 Ndipo hao Wababeli wakaja kwake kwenye kitanda cha mapenzi, nao katika tamaa zao wakamtia unajisi. Baada ya kutiwa unajisi, akawaacha kwa kuwachukia. \v 18 Alipofanya ukahaba wake waziwazi na kuonesha uchi wake, nilimwacha kwa kumchukia, kama vile nilivyokuwa nimemwacha dada yake. \v 19 Lakini akazidisha ukahaba wake alipozikumbuka siku za ujana wake, alipokuwa kahaba huko Misri. \v 20 Huko aliwatamani wapenzi wake, ambao viungo vyao vya uzazi ni kama vya punda, na kile kiwatokacho ni kama kiwatokacho farasi. \v 21 Hivyo ulitamani uasherati wa ujana wako wakati ulipokuwa Misri, kifua chako kilipokumbatiwa, na matiti yako machanga yakapapaswa. \p \v 22 “Kwa hiyo, Oholiba, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitawachochea wapenzi wako wawe kinyume na wewe, wale uliowaacha kwa kuchukia, nitawaleta dhidi yako kutoka kila upande: \v 23 Wababeli na Wakaldayo wote, watu kutoka Pekodi, na Shoa na Koa, wakiwa pamoja na Waashuru wote, vijana wazuri, wote wakiwa watawala na majemadari, maafisa wa magari ya vita na watu wa vyeo vya juu, wote wakiwa wamepanda farasi. \v 24 Watakuja dhidi yako wakiwa na silaha, magari ya vita, magari ya kukokota, pamoja na umati mkubwa wa watu. Watakuzingira pande zote kwa ngao na vigao na kwa chapeo. Nitakutia mikononi mwao ili wakuadhibu, nao watakuadhibu sawasawa na sheria zao. \v 25 Nitaelekeza hasira yangu yenye wivu dhidi yako, nao watakuadhibu kwa hasira kali. Watakatilia mbali pua yako na masikio yako, na wale watakaosalia miongoni mwako watauawa kwa upanga. Watachukua wana wako wa kiume na wa kike, na wale watakaosalia miongoni mwenu watateketezwa kwa moto. \v 26 Watakuvua nguo zako pia, na kuchukua mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito na dhahabu. \v 27 Hivyo ndivyo nitakavyokomesha uasherati wako na ukahaba wako uliouanza huko Misri. Hutatazama vitu hivi kwa kuvitamani wala kukumbuka Misri tena. \p \v 28 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninakaribia kukutia mikononi mwa wale unaowachukia, kwa wale uliojitenga nao kwa kuwachukia. \v 29 Watakutenda mambo ya chuki na kukunyang’anya kila kitu ulichokifanyia kazi. Watakuacha uchi na mtupu na aibu ya ukahaba wako itafunuliwa. Uasherati wako na uzinzi wako \v 30 umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao. \v 31 Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako. \p \v 32 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “Utakinywea kikombe cha dada yako, \q2 kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; \q1 kitakuletea dharau na dhihaka, \q2 kwa kuwa kimejaa sana. \q1 \v 33 Utalewa ulevi na kujawa huzuni, \q2 kikombe cha maangamizi na ukiwa, \q2 kikombe cha dada yako Samaria. \q1 \v 34 Utakinywa chote na kukimaliza; \q2 utakivunja vipande vipande \q2 na kuyararua matiti yako. \m Nimenena haya, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \b \p \v 35 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa kuwa ulinisahau mimi na kunitupa nyuma yako, lazima ubebe matokeo ya uasherati wako na ukahaba wako.” \p \v 36 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Mwanadamu, je, utawahukumu Ohola na Oholiba? Basi wakabili kwa ajili ya matendo yao ya machukizo, \v 37 kwa kuwa wamefanya uzinzi na damu imo mikononi mwao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, hata watoto walionizalia wamewatoa kafara, kuwa chakula kwa sanamu hizo. \v 38 Pia wamenifanyia hili: wakati huo huo wamenajisi patakatifu pangu na kuzitangua Sabato zangu. \v 39 Siku ile ile walitoa kafara watoto wao kwa sanamu zao, waliingia patakatifu pangu na kupanajisi. Hilo ndilo walilolifanya katika nyumba yangu. \p \v 40 “Hata waliwatuma wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako wanja, na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu. \v 41 Ukaketi kwenye kiti cha anasa, kukiwa na meza iliyoandaliwa mbele yake ambayo juu yake ulikuwa umeweka uvumba na mafuta ambayo yalikuwa yangu. \p \v 42 “Kelele za umati wa watu wasiojali zilikuwa zimemzunguka, wakaleta watu wengi waliokuwa wakifanya makelele na walevi kutoka nyikani, ambao walitia bangili kwenye mikono ya yule mwanamke na dada yake na pia taji nzuri za kupendeza kwenye vichwa vyao. \v 43 Ndipo nikasema kuhusu yule aliyechakazwa na uzinzi, ‘Basi wamtumie kama kahaba, kwa kuwa ndivyo alivyo.’ \v 44 Nao wakazini naye. Kama vile watu wazinivyo na kahaba, ndiyo hivyo walivyozini na hao wanawake waasherati, Ohola na Oholiba. \v 45 Lakini watu wenye haki, watawahukumia adhabu wanawake wafanyao uzinzi na kumwaga damu, kwa kuwa ni wazinzi na damu iko mikononi mwao. \p \v 46 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Leteni watu wengi wenye makelele dhidi yao na uwaache wapate hofu na watekwe nyara. \v 47 Hao watu wengi watawapiga kwa mawe na kuwaua kwa panga zao, watawaua wana wao wa kiume na wa kike, na kuzichoma nyumba zao. \p \v 48 “Hivyo nitaukomesha uasherati katika nchi, ili wanawake wote wapate onyo nao wasije wakafanya uasherati kama ninyi mlivyofanya. \v 49 Utapata adhabu kwa ajili ya uasherati wako na kuchukua matokeo ya dhambi zako za uasherati. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 24 \s1 Chungu cha kupikia \p \v 1 Katika mwaka wa tisa, mwezi wa kumi, siku ya kumi, neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, weka kumbukumbu ya tarehe hii, tarehe hii hasa, kwa kuwa mfalme wa Babeli ameuzingira mji wa Yerusalemu kwa jeshi siku hii ya leo. \v 3 Nenea nyumba hii ya uasi kwa fumbo, uwaambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Teleka sufuria jikoni; iteleke \q2 na umimine maji ndani yake, \q1 \v 4 Weka vipande vya nyama ndani yake, \q2 vipande vyote vizuri, vya paja na vya bega. \q1 Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri; \q2 \v 5 chagua yule aliye bora wa kundi la kondoo. \q1 Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa; \q2 chochea hadi ichemke \q2 na uitokose hiyo mifupa ndani yake. \b \m \v 6 “ ‘Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Ole wa mji unaomwaga damu, \q2 ole wa sufuria ambayo sasa ina ukoko ndani yake, \q2 ambayo ukoko wake hautoki. \q1 Kipakue kipande baada ya kipande, \q2 bila kuvipigia kura. \b \q1 \v 7 “ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake: \q2 Huyo mwanamke aliimwaga juu ya mwamba ulio wazi; \q1 hakuimwaga kwenye ardhi, \q2 ambako vumbi lingeifunika. \q1 \v 8 Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi, \q2 nimemwaga damu yake \q2 juu ya mwamba ulio wazi, \q2 ili isifunikwe. \b \m \v 9 “ ‘Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Ole wa mji unaomwaga damu! \q2 Mimi nami nitalundikia kuni nyingi. \q1 \v 10 Kwa hiyo lundika kuni \q2 na uwashe moto. \q1 Pika hiyo nyama vizuri, \q2 changanya vikolezo ndani yake, \q2 na uiache mifupa iungue kwenye moto. \q1 \v 11 Kisha teleka sufuria tupu kwenye makaa \q2 hadi iwe na moto sana na shaba yake ing’ae, \q1 ili uchafu wake upate kuyeyuka \q2 na ukoko wake upate kuungua na kuondoka. \q1 \v 12 Imezuia juhudi zote, \q2 ukoko wake mwingi haujaondoka, \q2 hata ikiwa ni kwa moto. \p \v 13 “ ‘Sasa uchafu wako ni uasherati wako. Kwa sababu nilijaribu kukutakasa lakini haikuwezekana kutakaswa kutokana na huo uchafu wako, hutatakasika tena hadi ghadhabu yangu dhidi yako iwe imepungua. \b \p \v 14 “ ‘Mimi Mwenyezi Mungu nimesema, wakati umewadia wa mimi kutenda. Mimi sitazuia, mimi sitaona huruma wala sitapunguza hasira yangu. Utahukumiwa sawasawa na mwenendo na matendo yako, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \s1 Kifo cha mke wa Ezekieli \p \v 15 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 16 “Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote. \v 17 Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya waombolezaji.” \p \v 18 Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Kesho yake asubuhi nilifanya kama nilivyoamriwa. \p \v 19 Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?” \p \v 20 Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Mwenyezi Mungu lilinijia kusema: \v 21 ‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu wa kiume na wa kike mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga. \v 22 Nanyi mtafanya kama nilivyofanya. Hamtafunika sehemu ya chini ya nyuso zenu wala hamtakula vyakula vya kawaida vya waombolezaji. \v 23 Mtajifunga vilemba vichwani mwenu na kuvaa viatu vyenu miguuni mwenu. Hamtaomboleza au kulia, lakini mtadhoofika kwa sababu ya dhambi zenu na kulia kwa uchungu kila mtu na mwenzake. \v 24 Ezekieli atakuwa ishara kwenu, mtafanya kama yeye alivyofanya. Jambo hili litakapotokea, mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi.’ \p \v 25 “Nawe, mwanadamu, siku ile nitakapoondoa ngome yao iliyo furaha yao na utukufu wao, kitu cha kupendeza macho yao, kile kilicho shauku ya mioyo yao, wana wao wa kiume na wa kike vilevile, \v 26 siku hiyo atakayetoroka atakuja kuwapasha habari. \v 27 Katika siku ile kinywa chako kitamfumbukia yeye aliyenusurika, nawe utaongea wala hutanyamaza tena. Hivyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \c 25 \s1 Unabii dhidi ya Amoni \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao. \v 3 Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mungu Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipoenda uhamishoni, \v 4 kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao kati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu. \v 5 Nitaufanya mji wa Raba kuwa malisho ya ngamia na Amoni kuwa mahali pa kondoo pa kupumzikia. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 6 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa kuwa mmepiga makofi yenu na kufanya kishindo kwa miguu, mkifurahia kwa mioyo yenu miovu juu ya yale mabaya yaliyoipata nchi ya Israeli, \v 7 hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yenu na kuwatoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitawakatilia mbali kutoka mataifa na kuwang’oa kutoka nchi. Nitawaangamiza, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \s1 Unabii dhidi ya Moabu \p \v 8 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu Moabu na Seiri wamesema, “Tazama, nyumba ya Yuda imekuwa kama mataifa mengine yote,” \v 9 kwa hiyo nitaiondoa ile miji iliyo kando ya Moabu, kuanzia miji iliyo mipakani: Beth-Yeshimothi, Baal-Meoni na Kiriathaimu, iliyo utukufu wa nchi hiyo. \v 10 Nitaitia Moabu pamoja na Waamoni mikononi mwa watu wa Mashariki kuwa milki yao, ili Waamoni wasikumbukwe miongoni mwa mataifa, \v 11 nami nitatoa adhabu kwa Moabu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \s1 Unabii dhidi ya Edomu \p \v 12 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu Edomu walilipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda, wakakosea sana kwa kufanya hivyo, \v 13 kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaunyoosha mkono wangu dhidi ya Edomu na kuua watu wake na wanyama wao. Nitaufanya ukiwa, na kuanzia Temani hadi Dedani wataanguka kwa upanga. \v 14 Nitalipiza Edomu kisasi kwa mkono wa watu wangu Israeli, nao watawatendea Edomu sawasawa na hasira yangu na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \s1 Unabii dhidi ya Ufilisti \p \v 15 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: ‘Kwa sababu Wafilisti wamewalipiza kisasi kwa uovu wa mioyo yao na kwa uadui wa siku nyingi wakataka kuangamiza Yuda, \v 16 kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi ninakaribia kuunyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi na kuwaangamiza wale waliosalia katika pwani. \v 17 Nitalipiza kisasi kikubwa juu yao na kuwaadhibu katika ghadhabu yangu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapolipiza kisasi juu yao.’ ” \c 26 \s1 Unabii dhidi ya Tiro \p \v 1 Mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema kuhusu Yerusalemu, ‘Aha! Lango la kwenda kwa mataifa limevunjika, nayo milango yake iko wazi mbele yangu, sasa kwa kuwa amekuwa magofu nitastawi.’ \v 3 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi niko kinyume na wewe, ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi dhidi yako, kama bahari inayovurumisha mawimbi yake. \v 4 Watavunja kuta za Tiro na kuibomoa minara yake, nitakwangua udongo wake na kuufanya mwamba mtupu. \v 5 Itakuwa huko katikati ya bahari patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki, kwa maana nimenena, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Atakuwa nyara kwa mataifa, \v 6 nayo makazi yake huko bara yataangamizwa kwa upanga. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 7 “Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kutoka kaskazini nitamleta dhidi ya Tiro Mfalme Nebukadneza wa Babeli, mfalme wa wafalme, akiwa na farasi na magari ya vita, wapanda farasi na jeshi kubwa. \v 8 Atayaharibu makazi yako huko bara kwa upanga; atajenga husuru dhidi yako, na kupandisha kilima hadi kuta zako, na kuinua ngao zake dhidi yako. \v 9 Ataelekeza mapigo ya magogo ya kubomoa boma dhidi ya kuta zako, na kubomoa minara yako kwa silaha zake. \v 10 Farasi wake watakuwa wengi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari ya kukokotwa, na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu wanaoingia mji ambao kuta zake zimebomolewa kote. \p \v 11 “Kwato za farasi wake zitakanyaga barabara zako zote, atawaua watu wako kwa upanga na nguzo zako zilizo imara zitaanguka chini. \v 12 Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako. \v 13 Nitakomesha kelele za nyimbo zako, na uimbaji wako wa kinubi kamwe hautasikika tena. \v 14 Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana Mimi Mwenyezi Mungu nimenena, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 15 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa Tiro: ‘Je, nchi za pwani hazitatetemeka kwa kishindo cha anguko lako, wakati majeruhi wanapolia kwa maumivu makali na wakati mauaji yanaendelea ndani yako? \v 16 Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka viti vyao vya utawala, na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wataketi chini ardhini, wakiwa wamevikwa hofu kuu, wakitetemeka kila dakika na kukustaajabia. \v 17 Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia: \q1 “ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa, \q2 ee mji uliokuwa na sifa, \q2 wewe uliyekaliwa na mabaharia! \q1 Ulikuwa na nguvu kwenye bahari, \q2 wewe na wakaaji wako; \q2 wote walioishi huko, \q2 uliwatia hofu kuu. \q1 \v 18 Sasa nchi za pwani zinatetemeka \q2 katika siku ya anguko lako; \q1 visiwa vilivyomo baharini \q2 vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’ \p \v 19 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitakapokufanya uwe mji wa ukiwa, kama miji isiyokaliwa tena na watu, nitakapoleta vilindi vya bahari juu yako na maji yake makuu yatakapokufunika, \v 20 ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale wanaoshuka shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale wanaoshuka shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai. \v 21 Nitakufikisha mwisho wa kutisha wala hutakuwepo tena. Watu watakutafuta, lakini kamwe hutaonekana tena, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 27 \s1 Maombolezo kwa ajili ya Tiro \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. \v 3 Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Ee Tiro, wewe umesema, \q2 “Mimi ni mkamilifu katika uzuri.” \q1 \v 4 Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari, \q2 wajenzi wako walikamilisha uzuri wako. \q1 \v 5 Walizifanya mbao zako zote \q2 kwa misunobari kutoka Seniri\f + \fr 27:5 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mlima Hermoni\fqa*\f*; \q1 walichukua mwerezi kutoka Lebanoni \q2 kukutengenezea mlingoti. \q1 \v 6 Walichukua mialoni kutoka Bashani \q2 wakakutengenezea makasia yako; \q1 kwa miti ya msanduku \q2 kutoka pwani ya Kitimu \q1 wakatengeneza sitaha yako \q2 na kuipamba kwa pembe za ndovu. \q1 \v 7 Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako, \q2 nacho kilikuwa bendera yako; \q1 chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau \q2 kutoka visiwa vya Al-Yasa. \q1 \v 8 Wakaaji wa Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako; \q2 watu wako wenye ustadi, ee Tiro, \q2 ndio walikuwa mabaharia wako. \q1 \v 9 Wazee wa Gebali\f + \fr 27:9 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bubilo\fqa*\f* pamoja na mafundi stadi \q2 walikuwa mafundi wako kwenye meli. \q1 Meli zote za baharini na mabaharia wao \q2 walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako. \b \q1 \v 10 “ ‘Wanaume wa Uajemi, Ludi na Putu \q2 walikuwa askari katika jeshi lako. \q1 Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako, \q2 wakileta fahari yako. \q1 \v 11 Watu wa Arvadi na wa Heleki \q2 walikuwa juu ya kuta zako pande zote; \q1 watu wa Gamadi \q2 walikuwa kwenye minara yako. \q1 Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako; \q2 wakaukamilisha uzuri wako. \p \v 12 “ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali yako. \p \v 13 “ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki walifanya biashara nawe; walibadilisha binadamu na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako. \p \v 14 “ ‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali yako. \p \v 15 “ ‘Watu wa Dedani\f + \fr 27:15 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Rodo\fqa*\f* walifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo. \p \v 16 “ ‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawe\f + \fr 27:16 \fr*\ft yaani \ft*\fqa marijani\fqa*\ft , jiwe la pwani au baharini\ft*\f* na akiki nyekundu. \p \v 17 “ ‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe; walibadilishana ngano iliyotoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri kwa bidhaa zako. \p \v 18 “ ‘Dameski walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa bidhaa zako na ukuu wa utajiri wa mali zako, wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari. \p \v 19 “ ‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali walikuletea mali ya biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai. \p \v 20 “ ‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi. \p \v 21 “ ‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako; walifanya biashara nawe ya kubadilishana wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi. \p \v 22 “ ‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezo, vito vya thamani na dhahabu. \p \v 23 “ ‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe. \v 24 Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara. \q1 \v 25 “ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo \q2 zinazokusafirishia bidhaa zako. \q1 Umejazwa shehena kubwa \q2 katika moyo wa bahari. \q1 \v 26 Wapiga makasia wako wanakupeleka \q2 mpaka kwenye maji makuu. \q1 Lakini upepo wa mashariki utakuvunja vipande vipande \q2 moyoni mwa bahari. \q1 \v 27 Utajiri wako, bidhaa zako na mali yako, \q2 mabaharia wako, manahodha wako, \q2 mafundi wako wa meli, \q1 wafanyabiashara wako na askari wako wote, \q2 na kila mmoja aliye kwenye meli \q1 atazama kwenye moyo wa bahari \q2 siku ile meli yako itakapovunjika. \q1 \v 28 Nchi za pwani zitatetemeka \q2 wakati mabaharia wako watakapopiga kelele. \q1 \v 29 Wote wapigao makasia \q2 wataacha meli zao, \q1 mabaharia wote na wanamaji wote \q2 watasimama pwani. \q1 \v 30 Watapaza sauti zao \q2 na kulia sana kwa ajili yako; \q1 watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao \q2 na kujivingirisha kwenye majivu. \q1 \v 31 Watanyoa nywele zao kwa ajili yako, \q2 nao watavaa magunia. \q1 Watakulilia kwa uchungu wa moyo \q2 na kwa maombolezo makuu. \q1 \v 32 Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako, \q2 watafanya maombolezo kukuhusu wakisema: \q1 “Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro, \q2 katika moyo wa bahari?” \q1 \v 33 Bidhaa zako zilipotoka baharini, \q2 ulitosheleza mataifa mengi; \q1 kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako \q2 ulitajirisha wafalme wa dunia. \q1 \v 34 Sasa umevunjavunjwa na bahari, \q2 katika vilindi vya maji, \q1 bidhaa zako na kundi lako lote \q2 vimezama pamoja nawe. \q1 \v 35 Wote wanaoishi katika nchi za pwani \q2 wanakustaajabia; \q1 wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu, \q2 nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga. \q1 \v 36 Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka; \q2 umefikia mwisho wa kutisha \q2 nawe hutakuwepo tena.’ ” \c 28 \s1 Unabii dhidi ya mfalme wa Tiro \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna \q2 na umesema, “Mimi ni mungu; \q1 nami ninaketi kwenye kiti cha enzi cha mungu \q2 katika moyo wa bahari.” \q1 Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu, \q2 ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu. \q1 \v 3 Je, wewe una hekima kuliko Danieli? \q2 Je, hakuna siri iliyofichika kwako? \q1 \v 4 Kwa hekima yako na ufahamu wako, \q2 umejipatia utajiri, \q1 nawe umejikusanyia dhahabu \q2 na fedha katika hazina zako. \q1 \v 5 Kwa werevu wako mwingi katika biashara, \q2 umeongeza utajiri wako \q1 na kwa sababu ya utajiri wako \q2 moyo wako umekuwa na kiburi. \p \v 6 “ ‘Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima, \q2 mwenye hekima kama mungu, \q1 \v 7 mimi nitawaleta wageni dhidi yako, \q2 taifa katili kuliko yote; \q1 watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako, \q2 na kuchafua fahari yako inayong’aa. \q1 \v 8 Watakushusha chini shimoni, \q2 nawe utakufa kifo cha kikatili \q2 katika moyo wa bahari. \q1 \v 9 Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,” \q2 mbele ya wale wanaokuua? \q1 Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu, \q2 mikononi mwa hao wanaokuua. \q1 \v 10 Utakufa kifo cha wasiotahiriwa \q2 kwa mkono wa wageni. \m Kwa kuwa mimi nimenena, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \b \p \v 11 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 12 “Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu, ukiwa umejaa hekima \q2 na mkamilifu katika uzuri. \q1 \v 13 Ulikuwa ndani ya Edeni, \q2 bustani ya Mungu; \q1 kila kito cha thamani kilikupamba: \q2 akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi, \q2 krisolitho, shohamu na yaspi, \q2 yakuti samawi, almasi na zabarajadi. \q1 Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake \q2 kulifanywa kwa dhahabu; \q2 siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari. \q1 \v 14 Ulipakwa mafuta kuwa kerubi mlinzi, \q2 kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu. \q1 Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu; \q2 ulitembea katikati ya vito vya moto. \q1 \v 15 Ulikuwa mnyofu katika njia zako \q2 tangu siku ile ya kuumbwa kwako, \q2 hadi uovu ulipoonekana ndani yako. \q1 \v 16 Kutokana na biashara yako iliyoenea, \q2 ulijazwa na dhuluma, \q2 nawe ukatenda dhambi. \q1 Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu, \q2 nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi, \q2 kutoka katikati ya vito vya moto. \q1 \v 17 Moyo wako ukawa na kiburi \q2 kwa ajili ya uzuri wako, \q1 nawe ukaiharibu hekima yako \q2 kwa sababu ya fahari yako. \q1 Kwa hiyo nikakutupa chini; \q2 nimekufanya kioja mbele ya wafalme. \q1 \v 18 Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma, \q2 umenajisi mahali pako patakatifu. \q1 Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako, \q2 nao ukakuteketeza, \q1 nami nikakufanya majivu juu ya nchi, \q2 machoni pa wote waliokuwa wakitazama. \q1 \v 19 Mataifa yote yaliyokujua \q2 yanakustaajabia; \q1 umefikia mwisho wa kutisha \q2 na hutakuwepo tena milele.’ ” \s1 Unabii dhidi ya Sidoni \p \v 20 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 21 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, \v 22 nawe useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni, \q2 nami nitapata utukufu ndani yako. \q1 Nao watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, \q2 nitakapotekeleza hukumu zangu \q2 na kuonesha utakatifu wangu ndani yake. \q1 \v 23 Nitapeleka tauni ndani yake \q2 na kufanya damu itiririke katika barabara zake. \q1 Waliochinjwa wataanguka ndani yake, \q2 kwa upanga dhidi yake kila upande. \q1 Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 24 “ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru, wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 25 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo. \v 26 Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao.’ ” \c 29 \s1 Unabii dhidi ya Misri \s2 Hukumu juu ya Farao \p \v 1 Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili, neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote. \v 3 Nena, nawe useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Mimi ni kinyume nawe, Farao, mfalme wa Misri, \q2 ewe mnyama mkubwa ulalaye katikati ya vijito vyako. \q1 Unasema, “Mto Naili ni wangu mwenyewe; \q2 niliufanya kwa ajili yangu mwenyewe.” \q1 \v 4 Lakini nitatia ndoana katika mataya yako \q2 nami nitawafanya samaki wa vijito vyako \q2 washikamane na magamba yako. \q1 Nitakutoa katikati ya vijito vyako, \q2 pamoja na samaki wote \q2 walioshikamana na magamba yako. \q1 \v 5 Nitakutupa jangwani, \q2 wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako. \q1 Utaanguka uwanjani, \q2 nawe hutakusanywa au kuchukuliwa. \q1 Nitakutoa uwe chakula \q2 kwa wanyama wa nchi \q2 na ndege wa angani. \m \v 6 Ndipo wale wote wanaoishi Misri watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \b \p “ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli. \v 7 Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka. \p \v 8 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao. \v 9 Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p “ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliuumba,” \v 10 kwa hiyo mimi ni kinyume nawe na kinyume na vijito vyako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa magofu na ukiwa kuanzia Migdoli hadi Aswani, hata kufikia mpaka wa Kushi. \v 11 Hakuna unyayo wa mtu au mnyama utakaopita ndani yake, wala hakuna yeyote atakayeishi humo kwa muda wa miaka arobaini. \v 12 Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwatapanya katika nchi nyingine. \p \v 13 “ ‘Lakini hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mwishoni mwa hiyo miaka arobaini, nitawakusanya Wamisri kutoka mataifa walikotawanywa. \v 14 Nitawarejesha hao Wamisri kutoka kutekwa kwao na kuwaweka Pathrosi\f + \fr 29:14 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Misri ya Juu\fqa*\f*, nchi ya baba zao. Huko watakuwa na ufalme usiokuwa na nguvu. \v 15 Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine. \v 16 Misri haitakuwa tena tumaini la watu wa Israeli bali itakuwa kumbukumbu ya dhambi yao kwa kuigeukia kuomba msaada. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \s2 Zawadi ya Nebukadneza \p \v 17 Katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza, neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema: \v 18 “Mwanadamu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliongoza jeshi lake kufanya kazi ngumu dhidi ya Tiro; kila kichwa kilipata upara na kila bega likachunika. Lakini yeye na jeshi lake hawakupata malipo yoyote kutokana na muda wote aliongoza hiyo vita dhidi ya Tiro. \v 19 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaitia Misri mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atachukua utajiri wa Misri. Atateka mateka na kuchukua nyara mali ya Misri kama ujira kwa ajili ya jeshi lake. \v 20 Nimempa mfalme wa Babeli nchi ya Misri kuwa ujira kwa juhudi zake kwa sababu yeye na jeshi lake walifanya kwa ajili yangu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 21 “Katika siku hiyo nitaifanya nyumba ya Israeli iwe na nguvu nami nitakifungua kinywa chako miongoni mwao. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \c 30 \s2 Maombolezo kwa ajili ya Misri \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Ombolezeni ninyi na mseme, \q2 “Ole wa siku ile!” \q1 \v 3 Kwa kuwa siku ile imekaribia, \q2 siku ya Mwenyezi Mungu imekaribia, \q1 siku ya mawingu, \q2 siku ya maangamizi kwa mataifa. \q1 \v 4 Upanga utakuja dhidi ya Misri, \q2 nayo maumivu makuu yataijia Kushi. \q1 Mauaji yatakapoangukia Misri, \q2 utajiri wake utachukuliwa \q2 na misingi yake itabomolewa. \m \v 5 Kushi na Putu, Ludi na Arabia yote, Kubu na watu wa nchi ya agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri. \p \v 6 “ ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka \q2 na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. \q1 Kutoka Migdoli hadi Aswani, \q2 watauawa ndani yake kwa upanga, \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \q1 \v 7 Hizo nchi zitakua ukiwa \q2 miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, \q1 nayo miji yao itakuwa magofu \q2 miongoni mwa miji iliyo magofu. \q1 \v 8 Ndipo watajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu, \q2 nitakapoiwasha Misri moto \q2 na wasaidizi wake wote watapondwa. \p \v 9 “ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja. \b \p \v 10 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Nitakomesha makundi ya Misri \q2 kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. \q1 \v 11 Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili \q2 kuliko mataifa yote, \q2 ataletwa ili kuangamiza nchi. \q1 Watafuta panga zao dhidi ya Misri \q2 na kuijaza nchi kwa waliouawa. \q1 \v 12 Nitakausha vijito vya Mto Naili, \q2 na kuiuza nchi kwa watu waovu; \q1 kwa mkono wa wageni, nitaifanya nchi ukiwa \q2 na kila kitu kilicho ndani yake. \m Mimi Mwenyezi Mungu nimenena haya. \b \p \v 13 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Nitaangamiza sanamu \q2 na kukomesha vinyago katika Memfisi\f + \fr 30:13 \fr*\ft au \ft*\fqa Nofu\fqa*\f*. \q1 Hapatakuwa tena na mkuu katika nchi ya Misri, \q2 nami nitaeneza hofu katika nchi nzima. \q1 \v 14 Nitaifanya Pathrosi\f + \fr 30:14 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Misri ya Juu\fqa*\f* kuwa ukiwa \q2 na kuitia moto Soani, \q2 nami nitaipiga Thebesi\f + \fr 30:14 \fr*\ft yaani \ft*\fqa No \fqa*\ft (au \ft*\fqa No-Amoni\fqa*\fqa )\fqa*\f* kwa adhabu. \q1 \v 15 Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu\f + \fr 30:15 \fr*\ft Kiebrania ni \ft*\fqa Sini\fqa*\f*, \q2 ngome ya Misri, \q1 nami nitakatilia mbali \q2 makundi ya Thebesi. \q1 \v 16 Nitaitia moto nchi ya Misri; \q2 Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu. \q1 Thebesi itachukuliwa na tufani, \q2 Memfisi itakuwa katika taabu daima. \q1 \v 17 Wanaume vijana wa Oni\f + \fr 30:17 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Heliopoli \fqa*\ft (\ft*\fqa Mji wa Jua\fqa*\ft )\ft*\f* na wa Pi-Besethi\f + \fr 30:17 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bubasti\fqa*\f* \q2 wataanguka kwa upanga \q2 nayo hiyo miji itatekwa. \q1 \v 18 Huko Tapanesi mchana utatiwa giza \q2 nitakapovunja nira ya Misri; \q2 hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma. \q1 Atafunikwa na mawingu \q2 na vijiji vyake vitatekwa. \q1 \v 19 Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu, \q2 nao watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \s2 Mkono wa Farao umevunjwa \p \v 20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 21 “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga. \v 22 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake. \v 23 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwatapanya katika nchi zote. \v 24 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha. \v 25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri. \v 26 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwatapanya katika nchi nyingine. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \c 31 \s2 Farao, mwerezi ulioanguka \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema: \v 2 “Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake hivi: \q1 “ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa \q2 na wewe katika fahari. \q1 \v 3 Angalia Ashuru, zamani ulikuwa mwerezi huko Lebanoni, \q2 ukiwa na matawi mazuri \q2 na kutia msitu kivuli; \q1 ulikuwa mrefu sana, kilele chake \q2 kilipita majani ya miti yote. \q1 \v 4 Maji mengi yaliustawisha, \q2 chemchemi zenye maji mengi \q2 ziliufanya urefuke; \q1 vijito vyake vilitiririka pale \q2 ulipoota pande zote \q1 na kupeleka mifereji yake \q2 kwenye miti yote ya shambani. \q1 \v 5 Hivyo ukarefuka \q2 kupita miti yote ya shambani; \q1 vitawi vyake viliongezeka \q2 na matawi yake yakawa marefu, \q2 yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji. \q1 \v 6 Ndege wote wa angani \q2 wakaweka viota kwenye vitawi vyake, \q1 wanyama wote wa shambani \q2 wakazaana chini ya matawi yake, \q1 mataifa makubwa yote \q2 yaliishi chini ya kivuli chake. \q1 \v 7 Ulikuwa na fahari katika uzuri, \q2 ukiwa na matawi yaliyotanda, \q1 kwa kuwa mizizi yake iliteremka \q2 hadi kwenye maji mengi. \q1 \v 8 Mierezi katika bustani ya Mungu \q2 haikuweza kushindana nao, \q1 wala misunobari haikuweza \q2 kulingana na vitawi vyake, \q1 wala miaramoni \q2 haikulinganishwa na matawi yake, \q1 wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu \q2 wa kulinganisha na uzuri wake. \q1 \v 9 Niliufanya kuwa mzuri, \q2 ukiwa na matawi mengi; \q1 nao ulionewa wivu na miti yote ya Edeni \q2 katika bustani ya Mungu. \p \v 10 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake, \v 11 niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye autende sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali, \v 12 nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kivuli chake na kuuacha. \v 13 Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake. \v 14 Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale wanaoshuka shimoni. \p \v 15 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini\f + \fr 31:15 \fr*\ft Kaburini maana yake ni \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\ft ; kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft ; pia \+xt 31:16, 17\+xt*.\ft*\f* nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. \v 16 Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale wanaoshuka shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani. \v 17 Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga. \p \v 18 “ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa pamoja na miti ya Edeni hadi chini kabisa; utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga. \p “ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \c 32 \s2 Maombolezo kwa ajili ya Farao \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Mwenyezi Mungu likanijia, kusema: \v 2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie: \q1 “ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa, \q2 wewe ni kama mnyama mkubwa baharini, \q1 unapiga maji kwa kishindo katika vijito vyako, \q2 unayavuruga maji kwa miguu yako, \q2 na kuchafua vijito. \p \v 3 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu \q2 nitautupa wavu wangu juu yako, \q2 nao watakukokota katika wavu wangu. \q1 \v 4 Nitakutupa nchi kavu \q2 na kukuvurumisha uwanjani. \q1 Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako \q2 na wanyama wote wa nchi \q2 watajishibisha nyama yako. \q1 \v 5 Nitatawanya nyama yako juu ya milima \q2 na kujaza mabonde kwa mabaki yako. \q1 \v 6 Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka \q2 njia yote hadi milimani, \q2 nayo mabonde yatajazwa na nyama yako. \q1 \v 7 Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu \q2 na kuzitia nyota zake giza; \q1 nitalifunika jua kwa wingu, \q2 nao mwezi hautatoa nuru yake. \q1 \v 8 Mianga yote itoayo nuru angani \q2 nitaitia giza juu yako; \q1 nitaleta giza juu ya nchi yako, \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \q1 \v 9 Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi \q2 nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa, \q1 nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi \q2 ambazo hujapata kuzijua. \q1 \v 10 Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie, \q2 wafalme wao watatetemeka \q2 kwa hofu kwa ajili yako \q2 nitakapotikisa upanga wangu mbele yao. \q1 Siku ya anguko lako \q2 kila mmoja wao atatetemeka \q2 kila dakika kwa ajili ya maisha yake. \p \v 11 “ ‘Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli \q2 utakuja dhidi yako. \q1 \v 12 Nitayafanya makundi yako kuanguka \q2 kwa panga za mashujaa: \q2 taifa katili kuliko mataifa yote. \q1 Watakivunjavunja kiburi cha Misri, \q2 nayo makundi yake yote yatashindwa. \q1 \v 13 Nitaangamiza mifugo yake yote \q2 wanaojilisha kando ya maji mengi: \q1 hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu \q2 wala kwato za mnyama \q2 hazitayachafua tena. \q1 \v 14 Kisha nitafanya maji yake yatulie \q2 na kufanya vijito vyake \q2 vitiririke kama mafuta, \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \q1 \v 15 Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa, \q2 na kuiondolea nchi kila kitu kilichomo, \q1 nitakapowapiga wote wanaoishi humo, \q2 ndipo watajua kuwa \q2 Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ \p \v 16 “Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote wataliimba, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \s2 Misri kuteremka Kuzimu \p \v 17 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 18 “Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya Misri na uwatupe Kuzimu, yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao wanaoshuka shimoni. \v 19 Je, ninyi mmekubalika zaidi ya wengine? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa! \v 20 Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa; mwache aburutwe mbali pamoja na hao watu wake wote. \v 21 Kutoka Kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’ \p \v 22 “Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga. \v 23 Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga. \p \v 24 “Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka Kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni. \v 25 Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa. \p \v 26 “Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai. \v 27 Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini\f + \fr 32:27 \fr*\ft Kaburini maana yake ni \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\ft ; kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol.\fqa*\f* wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai. \p \v 28 “Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga. \p \v 29 “Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale wanaoshuka shimoni. \p \v 30 “Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale wanaoshuka shimoni. \p \v 31 “Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote, wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 32 Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 33 \s1 Kuimarishwa kwa wajibu wa Ezekieli \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, sema na watu wako uwaambie, ‘Nitakapoleta upanga dhidi ya nchi, nao watu wa nchi wakamchagua mmoja wa watu wao na kumfanya awe mlinzi wao, \v 3 naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu, \v 4 kama mtu yeyote asikiapo sauti ya tarumbeta hatakubali kuonywa, basi upanga ujapo na kuutoa uhai wake, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. \v 5 Kwa kuwa alisikia sauti ya tarumbeta lakini hakukubali maonyo, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Kama angekubali maonyo, angejiokoa mwenyewe. \v 6 Lakini kama mlinzi akiona upanga unakuja na asipige tarumbeta kuonya watu na upanga ukija na kutoa uhai wa mmoja wao, yule mtu ataondolewa kwa sababu ya dhambi yake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.’ \p \v 7 “Mwanadamu, nimekufanya wewe kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo na uwape maonyo kutoka kwangu. \v 8 Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Ewe mtu mwovu, hakika utakufa,’ nawe hukusema neno la kumwonya ili atoke katika njia zake, yule mtu mwovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini mimi nitaitaka damu yake mkononi mwako. \v 9 Lakini kama utamwonya huyo mtu mwovu aache njia zake mbaya naye hafanyi hivyo, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini utakuwa umejiokoa mwenyewe. \p \v 10 “Mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo mnalosema: “Makosa yetu na dhambi zetu zimetulemea, nasi tunadhoofika kwa sababu ya hayo. Tutawezaje basi kuishi?” ’ \v 11 Waambie, ‘Hakika kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, sifurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe, ee nyumba ya Israeli?’ \p \v 12 “Kwa hiyo, mwanadamu, waambie watu wako, ‘Haki ya mtu mwenye haki haitamwokoa wakati anapoacha kutii, wala uovu wa mtu mwovu hautamsababisha yeye kuanguka anapotubu na kuacha uovu. Mtu mwenye haki akitenda dhambi, hataishi kwa sababu ya uadilifu wake wa awali.’ \v 13 Nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika ataishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa; atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda. \v 14 Nami nikimwambia mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ kisha akageuka kutoka dhambi yake na kufanya lile lililo haki na sawa, \v 15 kama akirudisha kile alichochukua rehani kwa ajili ya deni, akarudisha alichoiba na kufuata amri zile ziletazo uzima, wala hafanyi uovu, hakika ataishi, hatakufa. \v 16 Hakuna dhambi yoyote aliyoitenda itakayokumbukwa juu yake. Ametenda lile lililo haki na sawa, hakika ataishi. \p \v 17 “Lakini watu wako wanasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini ni njia zao ambazo si sawa. \v 18 Kama mtu mwenye haki akigeuka kutoka uadilifu wake na kufanya uovu, atakufa kwa ajili ya huo uovu. \v 19 Naye mtu mwovu akigeuka kutoka uovu wake na kufanya lile lililo haki na sawa, kwa kufanya hivyo ataishi. \v 20 Lakini, ee nyumba ya Israeli, unasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini nitamhukumu kila mmoja wenu sawasawa na njia zake mwenyewe.” \s1 Kuelezea kuanguka kwa Yerusalemu \p \v 21 Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!” \v 22 Basi jioni kabla mtu huyo hajaja, mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu, naye alifungua kinywa changu kabla ya mtu yule aliyenijia asubuhi hajafika. Basi kinywa changu kilifunguliwa na sikuweza tena kunyamaza. \p \v 23 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 24 “Mwanadamu, watu wanaoishi katika magofu hayo katika nchi ya Israeli wanasema hivi, ‘Ibrahimu alikuwa mtu mmoja tu, hata hivyo akaimiliki nchi. Lakini sisi ni wengi, hakika tumepewa nchi kuwa milki yetu.’ \v 25 Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa kuwa mnakula nyama ikiwa na damu, na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi? \v 26 Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humnajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’ \p \v 27 “Waambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni. \v 28 Nitaifanya nchi ukiwa, na kiburi cha nguvu zake kitafikia mwisho, nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa ili mtu yeyote asipite huko. \v 29 Kisha watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapokuwa nimeifanya nchi ukiwa kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’ \p \v 30 “Kwako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule unaotoka kwa Mwenyezi Mungu.’ \v 31 Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali. \v 32 Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi. \p \v 33 “Mambo haya yote yatakapotimia, kwa kuwa hakika yatatokea, ndipo watajua kuwa nabii amekuwa miongoni mwao.” \c 34 \s1 Mwenyezi Mungu atakuwa mchungaji wa Israeli \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ole kwa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo? \v 3 Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi. \v 4 Hamkuwatia nguvu walio dhaifu, wala kuwaganga wenye maradhi, wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili. \v 5 Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwa na mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama mwitu wote. \v 6 Kondoo wangu walitangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika duniani kote, bila yeyote wa kuwaulizia wala kuwatafuta. \p \v 7 “ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Mwenyezi Mungu: \v 8 Kwa hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, kwa sababu kondoo wangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama pori wote na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo wangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo wangu, \v 9 kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno la Mwenyezi Mungu: \v 10 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi ni kinyume na wachungaji, nami nitawadai kondoo wangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo wangu kutoka vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao. \p \v 11 “ ‘Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo wangu na kuwatafuta. \v 12 Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene. \v 13 Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na pia mahali pote panapokaliwa katika nchi. \v 14 Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli. \v 15 Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo wangu na kuwafanya wapumzike, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 16 Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu, lakini wale walionona na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki. \p \v 17 “ ‘Kwenu ninyi, kundi langu, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo, kati ya kondoo dume na mbuzi. \v 18 Je, haiwatoshi ninyi kujilisha kwenye malisho mazuri? Je, ni lazima ninyi kuyakanyaga pia malisho yenu yaliyobaki kwa miguu yenu? Je, haiwatoshi ninyi kunywa maji safi? Je, ni lazima kuyachafua maji mengine kwa miguu yenu? \v 19 Je, ni lazima kundi langu wajilishe kwa yale mliyoyakanyaga na kunywa maji mliyoyachafua kwa miguu yenu? \p \v 20 “ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi awaambialo: Tazama, mimi mwenyewe nitahukumu kati ya kondoo wanono na waliokonda. \v 21 Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu hadi wakawafukuza, \v 22 nitaliokoa kundi langu na hawatatekwa nyara tena. Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo. \v 23 Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao. \v 24 Mimi Mwenyezi Mungu nitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu miongoni mwao. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena. \p \v 25 “ ‘Nitafanya nao agano la amani na kuwaondoa wanyama mwitu kutoka nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama. \v 26 Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwa na mvua za baraka. \v 27 Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa. \v 28 Hawatatekwa tena nyara na mataifa, wala wanyama pori kuwala tena. Wataishi kwa salama, wala hakuna yeyote atakayewatia hofu. \v 29 Nitawapa nchi yenye sifa kutokana na mazao yake, na hawatapatwa na njaa katika nchi tena, wala kudharauliwa na mataifa. \v 30 Ndipo watajua kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, Mungu wao, niko pamoja nao, na kwamba wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 31 Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu; ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \c 35 \s1 Unabii dhidi ya Edomu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Mlima Seiri, utabiri dhidi yake \v 3 na useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi ni kinyume nawe, ee Mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa. \v 4 Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 5 “ ‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake, \v 6 kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hukuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia. \v 7 Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaoenda. \v 8 Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote. \v 9 Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 10 “ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata Mimi Mwenyezi Mungu nilikuwa huko, \v 11 kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu. \v 12 Ndipo utakapojua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.” \v 13 Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia. \v 14 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Dunia yote inaposhangilia, nitakufanya ukiwa. \v 15 Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee Mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \c 36 \s1 Tumaini kwa milima ya Israeli \p \v 1 “Mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno la Mwenyezi Mungu. \v 2 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Adui alisema kuwahusu, “Aha! Mahali palipoinuka pa zamani pamekuwa milki yetu.” ’ \v 3 Kwa hiyo tabiri na useme, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa sababu wamewafanya ukiwa na kuwagandamiza kila upande ili mpate kuwa milki ya mataifa mengine, na mpate kuwa kitu cha kusimangwa na kudhihakiwa na watu; \v 4 kwa hiyo, ee milima ya Israeli, sikieni neno la Bwana Mungu Mwenyezi: Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka, \v 5 hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’ \v 6 Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa. \v 7 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ninaapa kwa mkono wangu ulioinuliwa kwamba mataifa wanaowazunguka nao pia watadharauliwa. \p \v 8 “ ‘Lakini ninyi, ee milima ya Israeli, mtatoa matawi na matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa sababu hivi karibuni watakuja nyumbani. \v 9 Mimi ninawajibika nanyi na nitawaangalia kwa upendeleo, mtalimwa na kupandwa mbegu, \v 10 nami nitaizidisha idadi ya watu kwenu, naam, nyumba yote ya Israeli. Miji itakaliwa na watu na magofu yatajengwa upya. \v 11 Nitaongeza idadi ya watu na wanyama juu yenu, nao watazaana sana na kuwa wengi mno. Nitawakalisha watu ndani yenu kama ilivyokuwa wakati uliopita, nami nitawafanya mfanikiwe kuliko mbeleni. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 12 Nitawafanya watu, watu wangu Israeli, kuishi juu yenu. Watawamiliki ninyi, nanyi mtakuwa urithi wao; hamtawaondolea tena watoto wao. \p \v 13 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Kwa sababu watu wanakuambia, “Unawala watu na kuliondolea taifa lako watoto wake,” \v 14 kwa hiyo hutakula tena watu wala kulifanya tena taifa lako lisiwe na watoto, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 15 Sitakufanya tena usikie dhihaka za mataifa, wala kudharauliwa na makabila ya watu, wala kulifanya taifa lako lianguke, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ” \s1 Israeli kuhakikishiwa urejesho \p \v 16 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena, kusema: \v 17 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi. \v 18 Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa sababu walikuwa wamemwaga damu katika nchi na kwa sababu walikuwa wameitia nchi unajisi kwa sanamu zao. \v 19 Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakatapanywa katika nchi mbalimbali; nikawahukumu kulingana na mwenendo wao na matendo yao. \v 20 Tena popote walipoenda miongoni mwa mataifa walilinajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuwahusu, ‘Hawa ndio watu wa Mwenyezi Mungu, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’ \v 21 Lakini niliwahurumia kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli imelitia unajisi miongoni mwa mataifa huko walikoenda. \p \v 22 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Si kwa ajili yako, ee nyumba ya Israeli, kwamba ninafanya mambo haya, bali ni kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo mmelitia unajisi miongoni mwa mataifa mliyoyaendea. \v 23 Nitauonesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, asema Bwana Mungu Mwenyezi, nitakapojionesha mwenyewe kuwa mtakatifu kupitia kwenu mbele ya macho yao. \p \v 24 “ ‘Kwa kuwa nitawaondoa ninyi toka mataifa, nitawakusanya kutoka nchi zote na kuwarejesha nchi yenu wenyewe. \v 25 Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka uchafu wenu wote na kutoka sanamu zenu zote. \v 26 Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. \v 27 Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu. \v 28 Mtaishi katika nchi niliyowapa baba zenu, ninyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu. \v 29 Nitawaokoa ninyi kutoka unajisi wenu wote. Nitaiita nafaka na kuiongeza iwe nyingi sana nami sitaleta njaa juu yenu. \v 30 Nitaongeza matunda ya miti na mazao ya mashamba, ili msipate tena aibu miongoni mwa mataifa kwa ajili ya njaa. \v 31 Ndipo mtakapozikumbuka njia zenu za uovu na matendo yenu maovu, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya dhambi zote na matendo yenu ya kuchukiza. \v 32 Ninataka ninyi mjue kwamba sifanyi hili kwa ajili yenu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Oneni aibu na mkatahayari kwa ajili ya mwenendo wenu, ee nyumba ya Israeli! \p \v 33 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Siku ile nitakapowasafisha kutoka dhambi zenu zote, nitarudisha watu waishi katika miji yenu na magofu yatajengwa upya. \v 34 Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa badala ya kukaa ukiwa machoni mwa wale wote wanaopita ndani yake. \v 35 Watasema, “Hii nchi iliyokuwa imeachwa ukiwa sasa imekuwa kama bustani ya Edeni, miji ile iliyokuwa magofu, ukiwa na kuangamizwa, sasa imejengewa ngome na kukaliwa na watu.” \v 36 Ndipo mataifa yanayowazunguka yaliyobakia watajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimejenga tena kile kilichoharibiwa, na nimepanda tena kile kilichokuwa ukiwa. Mimi Mwenyezi Mungu nimenena, nami nitalifanya.’ \p \v 37 “Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mara nyingine tena nitasikia maombi ya nyumba ya Israeli na kuwatendea jambo hili: Nitawafanya watu wake kuwa wengi kama kondoo, \v 38 kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \c 37 \s1 Bonde la mifupa iliyokauka \p \v 1 Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa Mwenyezi Mungu na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele. \v 2 Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana. \v 3 Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?” \p Nikajibu, “Ee Bwana Mungu Mwenyezi, wewe peke yako unajua.” \p \v 4 Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la Mwenyezi Mungu! \v 5 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi kwa hii mifupa: Nitatia pumzi\f + \fr 37:5 \fr*\ft pumzi pia ina maana ya \ft*\fqa roho \fqa*\ft au \ft*\fqa upepo \fqa*\ft kwa Kiebrania\ft*\f* ndani yenu, nanyi mtaishi. \v 6 Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 7 Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Nilipokuwa nikitabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. \v 8 Nikatazama: mishipa na nyama vikatokea juu ya mifupa na ngozi ikaifunika, lakini haikuwa na pumzi ndani yake. \p \v 9 Ndipo aliponiambia, “Utabirie pumzi; tabiri, mwanadamu na uiambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Njoo kutoka pande nne za pepo, ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ” \v 10 Hivyo nikatabiri kama alivyoniamuru, nayo pumzi ikawaingia, wakawa hai na wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. \p \v 11 Ndipo akaniambia: “Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli. Nao wanasema, ‘Mifupa yetu imekauka na tumaini letu limetoweka, tumekatiliwa mbali.’ \v 12 Hivyo watabirie na uwaambie: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwatoa ndani yake, nami nitawarudisha tena katika nchi ya Israeli. \v 13 Ndipo ninyi watu wangu, mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa humo. \v 14 Nitatia Roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi; nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe. Ndipo mtajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu nimenena, nami nitalitenda, asema Mwenyezi Mungu!’ ” \s1 Taifa moja chini ya mfalme mmoja \p \v 15 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 16 “Mwanadamu, chukua fimbo na uandike juu yake, ‘Hii ni kwa ajili ya Yuda na Waisraeli waliofungamana naye.’ Kisha chukua fimbo nyingine, uandike juu yake, ‘Fimbo ya Efraimu, ni kwa ajili ya Yusufu na nyumba yote ya Israeli wanaofungamana naye.’ \v 17 Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili ziwe fimbo moja katika mkono wako. \p \v 18 “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’ \v 19 Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaichukua fimbo ya Yusufu iliyo mkononi mwa Efraimu, na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye, na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa mmoja katika mkono wangu.’ \v 20 Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika \v 21 kisha waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wameenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe. \v 22 Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, katika milima ya Israeli. Patakuwa na mfalme mmoja juu yao wote na kamwe hawatagawanyika tena kuwa mataifa mawili au kugawanyika katika falme mbili. \v 23 Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao, au vinyago vyao vinavyochukiza, wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. \p \v 24 “ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu. \v 25 Wataishi katika nchi niliyompa mtumishi wangu Yakobo, nchi ambamo baba zenu waliishi. Wao na watoto wao na watoto wa watoto wao wataishi humo milele, naye Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele. \v 26 Nitafanya agano la amani nao; litakuwa agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele. \v 27 Maskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. \v 28 Ndipo mataifa watajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu ndiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakuwa miongoni mwao milele.’ ” \c 38 \s1 Unabii dhidi ya Gogu \p \v 1 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: \v 2 “Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mtawala mkuu wa\f + \fr 38:2 \fr*\ft au \ft*\fqa Magogu, mkuu wa Roshi na\fqa*\f* Mesheki na Tubali; tabiri dhidi yake \v 3 na useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. \v 4 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao. \v 5 Uajemi, Kushi na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na chapeo, \v 6 pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe. \p \v 7 “ ‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote waliokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe. \v 8 Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo, utaivamia nchi ambayo imepona kutoka vita, na watu wake walikusanywa kutoka mataifa mengi waje katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama. \v 9 Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu. \p \v 10 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya. \v 11 Utasema, “Nitapigana vita na nchi ambayo vijiji vyake havina kuna. Nitawashambulia watu wanaoishi kwa amani na wasiotarajia vita: wote wanaishi bila kuta na bila malango na makomeo. \v 12 Nitateka mateka na kuchukua nyara mali ya wale waliorudi kuishi katika mahame na wale watu waliokusanywa kutoka kwa mataifa, ambao sasa wana mifugo na mali nyingi, wanaoishi katikati ya nchi.” \v 13 Sheba na Dedani, pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ili kuchukua nyara, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyang’anya mifugo na mali, na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’ \p \v 14 “Kwa hiyo, mwanadamu, tabiri na umwambie Gogu: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika siku ile, watu wangu Israeli watakapokuwa wanaishi salama, Je, wewe mwenyewe hutalijua hilo? \v 15 Utakuja kutoka kwako huko kaskazini ya mbali, ukiwa pamoja na mataifa mengi, wote wakiwa wamepanda farasi, kundi kubwa, jeshi kuu. \v 16 Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionesha mtakatifu kupitia kwako mbele ya macho yao. \p \v 17 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Wewe ni yule niliyenena juu yake siku za zamani kupitia kwa watumishi wangu manabii wa Israeli. Wakati ule walitabiri kwa miaka mingi kwamba ningekuleta upigane nao. \v 18 Hili ndilo litakalotokea katika siku ile: Gogu atakaposhambulia nchi ya Israeli, hasira yangu kali itaamka, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 19 Katika wivu wangu na ghadhabu yangu kali, ninasema kuwa wakati ule kutakuwa na tetemeko kuu katika nchi ya Israeli. \v 20 Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kinachotambaa ardhini, na watu wote walio duniani kote watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini. \v 21 Nitaita upanga wa vita dhidi ya Gogu juu ya milima yangu yote, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Upanga wa kila mtu utakuwa dhidi ya ndugu yake. \v 22 Nitatekeleza hukumu juu yake kwa tauni na kwa umwagaji wa damu. Nitaifanya mvua ya mafuriko kunyesha, mvua ya mawe na moto wa kiberiti juu yake na juu ya vikosi vyake na juu ya mataifa mengi walio pamoja naye. \v 23 Nami hivyo ndivyo nitakavyoonesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ \c 39 \s1 Majeshi ya Gogu yataangamizwa \p \v 1 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu useme: ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ee Gogu mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. \v 2 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukuburuta. Nitakuleta kutoka kaskazini ya mbali na kukupeleka wewe dhidi ya milima ya Israeli. \v 3 Kisha nitaupiga upinde wako kutoka mkono wako wa kushoto na kuifanya mishale ianguke kutoka mkono wako wa kuume. \v 4 Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama pori. \v 5 Utaanguka katika uwanja, kwa kuwa nimenena, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 6 Nitatuma moto juu ya Magogu na kwa wale wanaoishi kwa salama huko pwani, nao watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \p \v 7 “ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu ndimi Aliye Mtakatifu wa Israeli. \v 8 Hili jambo linakuja! Hakika litatendeka, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Hii ndiyo siku ile niliyosema habari zake. \p \v 9 “ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni. \v 10 Hawatahitaji kukusanya kuni kutoka mashambani wala kukata kuni kwenye misitu, kwa sababu watatumia silaha kuwa kuni. Nao watawateka mateka wale waliowateka na kuchukua nyara mali ya wale waliochukua mali yao nyara, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 11 “ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki mwa Bahari. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu\f + \fr 39:11 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Makundi ya Gogu\fqa*\f*. \p \v 12 “ ‘Kwa miezi saba nyumba ya Israeli itakuwa ikiwazika ili kuisafisha nchi. \v 13 Watu wote wa nchi watawazika, nayo siku nitakayotukuzwa itakuwa siku ya kumbukumbu kwa ajili yao, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 14 “ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote, na, wakiwa na wengine, watawazika wale waliosalia juu ya ardhi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao. \v 15 Wanapopita nchini kote, na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake hadi wachimba kaburi wauzike katika Bonde la Hamon-Gogu. \v 16 (Pia mji uitwao Hamona\f + \fr 39:16 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kundi\fqa*\f* utakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’ \p \v 17 “Mwanadamu, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ita kila aina ya ndege na wanyama pori wote, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu. \v 18 Mtakula nyama za watu mashujaa na kunywa damu za wakuu wa dunia kana kwamba ni za kondoo dume na kondoo wake, mbuzi na mafahali, wote walionona kutoka Bashani. \v 19 Katika dhabihu ninayoandaa kwa ajili yenu, mtakula mafuta hadi mshibe, na kunywa damu hadi mlewe. \v 20 Kwenye meza yangu watajishibisha kwa farasi na wapanda farasi, watu mashujaa na askari wa kila aina,’ asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 21 “Nitauonesha utukufu wangu miongoni mwa mataifa, nayo mataifa yote wataiona adhabu nitakayotoa na mkono wangu nitakaouweka juu yao. \v 22 Kuanzia siku ile na kuendelea nyumba ya Israeli itajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \v 23 Na mataifa watajua kuwa nyumba ya Israeli walienda utumwani kwa ajili ya dhambi yao, kwa sababu hawakuwa waaminifu kwangu. Hivyo niliwaficha uso wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao, nao wote wakaanguka kwa upanga. \v 24 Niliwatendea sawasawa na uchafu wao na makosa yao, nami nikawaficha uso wangu. \p \v 25 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu. \v 26 Wataisahau aibu yao na jinsi walivyoonesha kutokuwa waaminifu kwangu mimi wakati waliishi salama katika nchi yao, bila kuwa na mtu yeyote wa kuwatia hofu. \v 27 Nitakapokuwa nimewarudisha kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka nchi za adui zao, mimi nitajionesha kuwa mtakatifu kupitia kwao machoni mwa mataifa mengi. \v 28 Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha yeyote nyuma. \v 29 Sitawaficha tena uso wangu, kwa maana nitamimina Roho wangu Mtakatifu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 40 \s1 Eneo la Hekalu jipya \p \v 1 Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko. \v 2 Nikiwa katika maono ya Mungu alinichukua hadi nchi ya Israeli, naye akaniweka kwenye mlima mrefu sana, ambako upande wa kusini kulikuwa na baadhi ya majengo ambayo yalionekana kama mji. \v 3 Akanipeleka huko, nami nikamwona mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba. Alikuwa amesimama kwenye lango akiwa na kamba ya kitani na ufito wa kupimia mkononi mwake. \v 4 Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, fungua macho yako uone, na utege masikio yako usikie, nawe uzingatie yote nitakayokuonesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.” \s2 Lango la mashariki kuelekea ukumbi wa nje \p \v 5 Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita\f + \fr 40:5 \fr*\ft Dhiraa ndefu 6 ni sawa na mita 3.18.\ft*\f*, dhiraa ndefu ikiwa sawa na dhiraa na nyanda nne. Akaupima ule ukuta; ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita, na kimo cha dhiraa ndefu sita. \p \v 6 Kisha akaenda kwenye lango linaloelekea mashariki. Akapanda ngazi zake akapima kizingiti cha lango, nacho kilikuwa na kina cha huo ufito. \v 7 Vyumba vya kupumzikia vya walinzi vilikuwa na urefu wa huo ufito mmoja na upana wa huo ufito, kuta zilizochomoza kati ya vyumba hivyo vya mapumziko zilikuwa na unene wa dhiraa tano\f + \fr 40:7 \fr*\ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\ft*\f*. Nacho kizingiti cha lango lililokuwa karibu na ukumbi unaoelekea hekaluni kilikuwa na kina cha huo ufito. \p \v 8 Kisha akapima baraza ya njia ya lango, \v 9 ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nane\f + \fr 40:9 \fr*\ft Dhiraa 8 ni sawa na mita 3.6.\ft*\f* na miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili\f + \fr 40:9 \fr*\ft Dhiraa 2 ni sawa na sentimita 90.\ft*\f*. Baraza ya lango ilielekea Hekalu. \p \v 10 Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande; vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizochomoza kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. \v 11 Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi, na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu\f + \fr 40:11 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 5.3; dhiraa 13 ni sawa na mita 6.9.\ft*\f*. \v 12 Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwa na ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa moja\f + \fr 40:12 \fr*\ft Dhiraa 1 ni sawa na sentimita 45.\ft*\f* kwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba. \v 13 Kisha akapima njia ya lango kuanzia juu ya ukuta wa nyuma wa chumba kimoja cha kupumzikia hadi juu ya ukuta wa nyuma wa chumba upande wa pili; kukawa na nafasi ya dhiraa ishirini na tano\f + \fr 40:13 \fr*\ft Dhiraa 25 ni sawa na mita 13.\ft*\f* kuanzia lango la ukuta mmoja hadi lango la ukuta uliokuwa upande mwingine. \v 14 Akapima pande za mbele za hizo kuta zilizochomoza kuzunguka hadi ndani ya ingilio. Urefu wake ulikuwa dhiraa sitini\f + \fr 40:14 \fr*\ft Dhiraa 60 ni sawa na mita 27.\ft*\f*. Kipimo kilikuwa hadi baraza iliyoangaliana na ua. \v 15 Umbali kuanzia ingilio la njia ya lango hadi mwisho kabisa wa baraza yake ulikuwa dhiraa hamsini\f + \fr 40:15 \fr*\ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\ft*\f*. \v 16 Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi, na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango; vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua. Juu ya kila nguzo kulikuwa na nakshi za mitende. \s2 Ukumbi wa nje \p \v 17 Kisha akanileta katika ukumbi wa nje. Huko nikaona vyumba vingine pamoja na njia iliyokuwa imejengwa kuzunguka ukumbi wote, kulikuwa na vyumba thelathini vimepangana kando ya hiyo njia. \v 18 Njia hii iliyojengwa iliambaa na lango, ikiwa na urefu sawa na lango; hii ilikuwa ni njia ya chini. \v 19 Kisha akapima umbali kutoka ndani ya lango la chini mpaka nje ya ukumbi wa ndani, nao ulikuwa dhiraa mia moja\f + \fr 40:19 \fr*\ft Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.\ft*\f* upande wa mashariki na dhiraa mia moja upande wa kaskazini. \s2 Lango la kaskazini \p \v 20 Kisha akapima urefu na upana wa lango linaloelekea kaskazini, kukabili ukumbi wa nje. \v 21 Vyumba vyake vilikuwa vitatu kila upande, kuta zilizochomoza kati ya vyumba na baraza zilikuwa na vipimo sawa na zile kuta za lango la kwanza. Zilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano\f + \fr 40:21 \fr*\ft Dhiraa 25 ni sawa na mita 11.25.\ft*\f*. \v 22 Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. \v 23 Kulikuwa na lango kwenye ukumbi wa ndani lililoelekea lile lango la kaskazini, kama vile ilivyokuwa ule upande wa mashariki. Akapima kutoka lango moja hadi lile lililo mkabala nalo, lilikuwa dhiraa mia moja. \s2 Lango la kusini \p \v 24 Ndipo akaniongoza mpaka upande wa kusini, nami nikaona lango linaloelekea kusini. Akaipima miimo yake na baraza yake, navyo vilikuwa na vipimo sawa kama hivyo vingine. \v 25 Lango na baraza yake vilikuwa na madirisha membamba pande zote, kama madirisha ya huko kwingine. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano. \v 26 Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. Ilikuwa na nakshi za mitende kwenye kuta zilizochomoza kati ya vyumba kila upande. \v 27 Ukumbi wa ndani pia ulikuwa na lango lililoelekea kusini. Naye akapima kutoka lango hili hadi kwenye lango la nje upande wa kusini; ilikuwa dhiraa mia moja. \s2 Malango ya kuelekea ukumbi wa ndani \p \v 28 Kisha akanileta mpaka ukumbi wa ndani kupitia lango la kusini, naye akapima lango la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine. \v 29 Vyumba vyake, kuta zilizochomoza kati ya vyumba, na ukumbi wake vyote vilikuwa na vipimo sawa na vile vingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano. \v 30 (Baraza za malango zilizozunguka ukumbi wa ndani zilikuwa na upana wa dhiraa ishirini na tano na kina cha dhiraa tano.) \v 31 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje; miimo yake ilinakshiwa mitende, na kulikuwa na ngazi nane za kupandia. \p \v 32 Kisha akanileta hadi kwenye ukumbi wa ndani ulioko upande wa mashariki, naye akalipima lango hilo; lilikuwa na vipimo vilivyo sawasawa na yale mengine. \v 33 Vyumba vyake, kuta zake zilizochomoza, na baraza yake vilikuwa na vipimo sawa na vile vingine. Lile lango pamoja na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano. \v 34 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje; miimo yake ilinakshiwa mitende pande zote, na kulikuwa na ngazi nane za kupandia. \p \v 35 Kisha akanileta mpaka kwenye lango la kaskazini na kulipima. Lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine, \v 36 kama vile ilivyokuwa kwa vyumba, kuta zake na baraza yake, tena kulikuwa na madirisha pande zote. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano. \v 37 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje; miimo yake ilinakshiwa mitende pande zote, na kulikuwa na ngazi nane za kupandia. \s2 Vyumba vya kutayarishia dhabihu \p \v 38 Kulikuwa na chumba na mlango karibu na baraza katika kila njia ya ndani ya lango ambamo sadaka za kuteketezwa zilioshwa. \v 39 Kwenye baraza ya lile lango kulikuwepo meza mbili kila upande, ambako sadaka za kuteketezwa, sadaka za dhambi na sadaka za hatia zilichinjiwa. \v 40 Karibu na ukuta wa nje wa baraza ya lile lango, karibu na ngazi kwenye ingilio kuelekea kaskazini kulikuwa na meza mbili, nao upande mwingine wa ngazi kulikuwa na meza mbili. \v 41 Kwa hiyo kulikuwa na meza nne upande mmoja wa lango na nyingine nne upande mwingine, zote zilikuwa meza nane, ambapo dhabihu zilichinjiwa. \v 42 Pia kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, kila meza ilikuwa na urefu wa dhiraa moja na nusu\f + \fr 40:42 \fr*\ft Dhiraa 1.5 ni sawa na sentimita 67.5.\ft*\f*, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo cha dhiraa moja. Juu ya meza hizo viliwekwa vyombo vya kuchinjia sadaka za kuteketezwa na dhabihu nyingine mbalimbali. \v 43 Kulikuwa na kulabu, urefu wake nyanda nne\f + \fr 40:43 \fr*\ft Nyanda 4 ni sawa na sentimita 8.\ft*\f*, zilizokuwa zimeshikizwa ukutani pande zote. Meza zilikuwa kwa ajili ya nyama za sadaka. \s2 Vyumba kwa ajili ya makuhani \p \v 44 Nje ya lango la ndani, kwenye ukumbi wa ndani, kulikuwa na vyumba viwili, kimoja upande wa lango la kaskazini nacho kilielekea kusini, kingine upande wa lango la kusini nacho kilielekea kaskazini. \v 45 Akaniambia, “Chumba kinachoelekea upande wa kusini ni kwa ajili ya makuhani ambao wana usimamizi wa hekaluni, \v 46 nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribia Mwenyezi Mungu ili kuhudumu mbele zake.” \p \v 47 Ndipo alipopima ukumbi: nao ulikuwa mraba wa dhiraa mia moja urefu na upana. Madhabahu yalikuwa mbele ya Hekalu. \s1 Hekalu \p \v 48 Akanileta kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu\f + \fr 40:48 \fr*\ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\ft*\f* kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne\f + \fr 40:48 \fr*\ft Dhiraa 14 ni sawa na mita 6.3.\ft*\f* na kuta zake zilizochomoza zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. \v 49 Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili\f + \fr 40:49 \fr*\ft Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4.\ft*\f* kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo. \c 41 \p \v 1 Kisha yule mtu akanileta katika ukumbi mkuu, naye akaipima miimo; upana wake ulikuwa dhiraa sita\f + \fr 41:1 \fr*\ft Dhiraa 6 ni sawa na mita 2.7.\ft*\f* kila upande. \v 2 Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi, na kuta zilizochomoza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima ukumbi mkuu; ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini\f + \fr 41:2 \fr*\ft Dhiraa 40 ni sawa na mita 18.\ft*\f*, na upana wa dhiraa ishirini. \p \v 3 Kisha akaingia mahali patakatifu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizochomoza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba\f + \fr 41:3 \fr*\ft Dhiraa 7 ni sawa na mita 3.15.\ft*\f*. \v 4 Naye akapima urefu wa mahali patakatifu; ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya ukumbi mkuu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.” \p \v 5 Kisha akapima ukuta wa Hekalu, nao ulikuwa na unene wa dhiraa sita, na kila chumba cha pembeni kuzunguka Hekalu kilikuwa na upana wa dhiraa nne. \v 6 Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni; kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu. \v 7 Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyoenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyoenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kupitia kwa sakafu ya kati. \p \v 8 Nikaona kwamba Hekalu lilikuwa na kitako kilichoinuliwa pande zote; huu ukawa msingi wa vile vyumba vya pembeni. Ulikuwa na urefu wa ule ufito mmoja wa kupimia, yaani dhiraa ndefu sita. \v 9 Ukuta wa nje wa vyumba vya pembeni ulikuwa na unene wa dhiraa tano. Eneo la wazi katikati ya vyumba vya pembeni vya Hekalu \v 10 na vyumba vya makuhani lilikuwa na upana wa dhiraa ishirini kuzunguka Hekalu pande zote. \v 11 Kulikuwa na maingilio kwenye vyumba vya pembeni kutokea eneo lililo wazi, moja upande wa kaskazini na lingine upande wa kusini, nao msingi uliounganisha lile eneo la wazi ulikuwa na upana wa dhiraa tano ukilizunguka lote. \p \v 12 Jengo lililoelekeana na ua wa Hekalu upande wa magharibi lilikuwa na upana wa dhiraa sabini. Ukuta wa jengo hilo ulikuwa na unene wa dhiraa tano, kulizunguka lote, urefu ulikuwa wa dhiraa tisini\f + \fr 41:12 \fr*\ft Dhiraa 90 ni sawa na mita 40.5.\ft*\f*. \p \v 13 Kisha akapima Hekalu; lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na ua wa Hekalu na jengo pamoja na kuta zake vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja pia. \v 14 Upana wa ua wa Hekalu upande wa mashariki, pamoja na upande wa mbele wa Hekalu ulikuwa dhiraa mia moja. \p \v 15 Kisha akapima urefu wa jengo lililoelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na baraza zake kila upande, kwa kipimo cha dhiraa mia moja. \p Ukumbi mkuu, na mahali patakatifu, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi, \v 16 pamoja na vizingiti, madirisha membamba na vyumba vyote vitatu, kila kimoja pamoja na kizingiti vilifunikwa kwa mbao. Sakafu, ukuta hadi kwenye madirisha, na madirisha yenyewe vilifunikwa kwa mbao. \v 17 Katika nafasi iliyokuwa juu ya upande wa nje wa ingilio la mahali patakatifu, na katika kuta zilizozunguka mahali patakatifu na sehemu ya nje, kwa nafasi zilizo sawa, \v 18 kulinakshiwa makerubi na mitende; mtende ulikuwa kati ya kerubi na kerubi. Kila kerubi alikuwa na nyuso mbili: \v 19 upande mmoja uso wa mwanadamu kuelekea mti wa mtende na upande mwingine uso wa simba ukielekea mti mwingine wa mtende. Ilinakshiwa kuzunguka Hekalu lote. \v 20 Kuanzia sakafu hadi eneo lililo juu ya ingilio, palinakshiwa makerubi na mitende, pamoja na kwenye ukuta wa nje wa Patakatifu. \p \v 21 Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba; na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulifanana na huo. \v 22 Kulikuwa na madhabahu ya mbao kimo chake dhiraa tatu na ilikuwa dhiraa mbili mraba pande zote, tako lake na pande zake zilikuwa za mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ni meza iliyo mbele za Mwenyezi Mungu.” \v 23 Mahali patakatifu pa nje na Patakatifu Pa Patakatifu zilikuwa na milango miwili. \v 24 Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango. \v 25 Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na mitende kama nakshi zilizokuwa kwenye kuta, na kulikuwa na ubao ulioning’inia mbele ya baraza kwa nje. \v 26 Katika kuta za pembeni za ukumbi kulikuwa na madirisha membamba yaliyonakshiwa mitende kila upande. Vyumba vya pembeni vya Hekalu pia vilikuwa vimefunikwa kwa mbao. \c 42 \s1 Vyumba vya makuhani \p \v 1 Ndipo yule mtu akaniongoza kuelekea kaskazini mpaka kwenye ua wa nje na kunileta mpaka kwenye vyumba vinavyoelekeana na ua wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje upande wa kaskazini. \v 2 Jengo ambalo mlango wake ulielekea kaskazini lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini. \v 3 Mbele ya zile dhiraa ishirini za ule ua wa ndani unaoelekeana na ile njia ya ua wa nje, kuliinuka vyumba virefu kimoja baada ya kingine vya ghorofa tatu. \v 4 Mbele ya hivi vyumba kulikuwa na njia ya ndani yenye upana wa dhiraa kumi na urefu wa dhiraa mia moja. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini. \v 5 Basi vyumba vya juu vilikuwa vyembamba zaidi, kwa kuwa ujia\f + \fr 42:5 \fr*\fq ujia \fq*\ft ina maana ya njia ndani ya nyumba\ft*\f* ulichukua nafasi zaidi ndani yake kuliko katika vyumba vya sakafu ya chini na vya katikati ya jengo. \v 6 Vyumba katika ghorofa ya tatu havikuwa na nguzo, kama kumbi zilivyokuwa nazo, kwa hiyo eneo la sakafu ya vyumba vya juu lilikuwa ni dogo kuliko la sakafu ya chini na ya kati. \v 7 Kulikuwa na ukuta wa nje uliokuwa sambamba na vile vyumba na ukumbi wa nje, ulitokeza urefu wa dhiraa hamsini. \v 8 Wakati safu ya vyumba katika ua wa nje vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini, vile vyumba vilivyokuwa karibu zaidi na Hekalu vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja. \v 9 Vyumba vya chini vilikuwa na ingilio upande wa mashariki unapoingia kutoka ukumbi wa nje. \p \v 10 Upande wa kusini kufuata urefu wa ukuta wa ukumbi wa nje, unaopakana na ukumbi wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje, kulikuwa na vyumba \v 11 vyenye ujia unayopita mbele yake. Hivi vilifanana na vile vyumba vya upande wa kaskazini, vilikuwa na urefu na upana ulio sawa, mahali pa kutokea na vipimo vyake vilikuwa sawa. Kama ilivyokuwa milango ya upande wa kaskazini, \v 12 ndivyo ilivyokuwa milango ya vyumba vya upande wa kusini. Kulikuwa na ingilio kuanzia mwanzo wa njia ambao ulikuwa sambamba na ukuta wa pili uliokuwa upande wa mashariki, ambako ndiko kwa kuingia vyumbani. \p \v 13 Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini, ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu, ni vyumba vya makuhani, ambako wale makuhani ambao humkaribia Mwenyezi Mungu watakulia zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko wataziweka zile sadaka takatifu sana, yaani sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali hapo ni patakatifu. \v 14 Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje hadi wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.” \p \v 15 Alipomaliza kupima vile vilivyokuwa katika eneo la ndani la Hekalu, akanitoa nje kupitia lango la upande wa mashariki na kupima eneo lote linalozunguka: \v 16 Akapima upande wa mashariki kwa ule ufito wa kupimia, nao ulikuwa dhiraa mia tano\f + \fr 42:16 \fr*\ft Dhiraa 500 ni sawa na mita 225.\ft*\f*. \v 17 Akapima upande wa kaskazini, nao ulikuwa dhiraa mia tano kwa ufito ule wa kupimia. \v 18 Tena akapima upande wa kusini, nao ulikuwa dhiraa mia tano kwa ufito ule wa kupimia. \v 19 Kisha akageukia upande wa magharibi na kuupima, ulikuwa dhiraa mia tano kwa ufito ule wa kupimia. \v 20 Hivyo akapima eneo katika pande zote nne. Lilikuwa na ukuta kulizunguka wenye urefu wa dhiraa mia tano na upana wa dhiraa mia tano, uliotenganisha mahali Patakatifu na eneo la watu wote. \c 43 \s1 Utukufu warudi Hekaluni \p \v 1 Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, \v 2 nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikang’aa kwa utukufu wake. \v 3 Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. \v 4 Utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaingia hekaluni kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. \v 5 Kisha Roho wa Mungu akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ulilijaza Hekalu. \p \v 6 Yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu. \v 7 Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi, na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia. \v 8 Walipoweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu na miimo yao ya milango karibu na miimo yangu, pakiwa na ukuta tu kati yangu na wao, walilinajisi Jina langu takatifu kwa matendo yao ya machukizo. Kwa sababu hiyo niliwaangamiza kwa hasira yangu. \v 9 Basi sasa na waweke mbali nami ukahaba wao na sanamu za wafalme wao zisizo na uhai, nami nitakaa miongoni mwao milele. \p \v 10 “Mwanadamu, elezea hilo Hekalu kwa watu wa Israeli, ili wapate kuona aibu kwa ajili ya dhambi zao. Wao na wapime hicho kielelezo. \v 11 Wakishaona aibu kwa ajili ya yale yote waliyotenda, wafahamishe kielelezo cha hilo Hekalu, yaani mpangilio wake, maingilio yake ya kutoka na kuingia, kielelezo chake chote, na masharti yake yote na sheria zake zote. Yaandike haya mbele yao ili wapate kuwa waaminifu kwa hicho kielelezo chake na kufuata masharti yake yote. \p \v 12 “Hii ndiyo sheria ya Hekalu: Eneo lote linalozunguka Hekalu juu ya mlima litakuwa takatifu kuliko yote. Hii ndiyo sheria ya Hekalu. \s1 Madhabahu \p \v 13 “Hivi ndivyo vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ndefu, yaani dhiraa moja na nyanda nne\f + \fr 43:13 \fr*\ft Dhiraa 1 na nyanda 4 ni sawa na sentimita 53.\ft*\f*: Tako lake liwe na kina cha hiyo dhiraa moja, na upana wa hiyo dhiraa moja, ikiwa na ukingo wa shibiri moja\f + \fr 43:13 \fr*\ft Shibiri 1 ni sawa na sentimita 22.5.\ft*\f* kuizunguka pembeni. Hiki kitakuwa ndicho kimo cha madhabahu: \v 14 Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi hadi kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja. \v 15 Pale panapowashwa moto madhabahuni kimo chake kitakuwa dhiraa nne, na pembe nne zinazoelekeza juu kutoka pale panapowashwa moto. \v 16 Pale panapowashwa moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili\f + \fr 43:16 \fr*\ft Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4.\ft*\f* na upana wa dhiraa kumi na mbili. \v 17 Pia sehemu ya juu ni mraba, urefu wake dhiraa kumi na nne na upana wa dhiraa kumi na nne, ikiwa na ukingo wa nusu dhiraa na mfereji kuizunguka madhabahu. Ngazi za kupandia madhabahuni zitaelekea upande wa mashariki.” \p \v 18 Kisha akaniambia, “Mwanadamu, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Haya ndio yatakayokuwa masharti ya kutoa dhabihu za kuteketezwa na kunyunyiza damu juu ya madhabahu itakapokuwa imejengwa. \v 19 Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 20 Itakupasa kuchukua sehemu ya hiyo damu ya mnyama huyo, na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu, na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu, na kufanya upatanisho kwa ajili yake. \v 21 Itakupasa kumchukua huyo fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kumteketeza mahali palipoagizwa katika eneo la Hekalu nje ya mahali Patakatifu. \p \v 22 “Siku ya pili yake utamtoa beberu asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nayo madhabahu itatakaswa kama ilivyotakaswa kwa yule fahali. \v 23 Utakapokuwa umemaliza kazi ya kuitakasa, utamtoa fahali mchanga pamoja na kondoo dume toka kwenye kundi, wote wawe hawana dosari. \v 24 Utawatoa mbele za Mwenyezi Mungu, nao makuhani watanyunyizia chumvi juu yao na kuwatoa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu. \p \v 25 “Kwa siku saba itakupasa kutoa beberu kila siku kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pia itakupasa kutoa fahali mchanga na kondoo dume kutoka zizini, wote wawe hawana dosari. \v 26 Kwa siku saba itawapasa kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuitakasa; hivyo ndivyo watakavyoiweka wakfu. \v 27 Mwishoni mwa hizi siku saba, kuanzia siku ya nane na kuendelea, itawapasa makuhani kutoa sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu. Kisha nitawakubali ninyi, asema Bwana Mungu Mwenyezi.” \c 44 \s1 Mkuu, Walawi, makuhani \p \v 1 Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa. \v 2 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ameingia kupitia lango hili. \v 3 Yeye aliye mkuu peke yake ndiye anayeweza kukaa penye njia ya hilo lango na kula chakula mbele za Mwenyezi Mungu. Itampasa aingie kwa njia hiyo ya lango la ukumbini na kutokea njia hiyo hiyo.” \p \v 4 Kisha yule mtu akanileta kwa njia ya lango la kaskazini mpaka mbele ya Hekalu. Nikatazama nami nikauona utukufu wa Mwenyezi Mungu ukilijaza Hekalu la Mwenyezi Mungu, nami nikaanguka kifudifudi. \p \v 5 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa uangalifu, usikilize kwa makini na uzingatie kila kitu ninachokuambia kuhusu masharti yote yanayohusu Hekalu la Mwenyezi Mungu. Uwe mwangalifu kuhusu wale wanaoruhusiwa hekaluni na wale wasioruhusiwa kuingia mahali patakatifu. \v 6 Iambie nyumba ya uasi ya Israeli, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Matendo yenu ya machukizo yatosha, ee nyumba ya Israeli! \v 7 Zaidi ya matendo yenu yote ya machukizo, mmewaleta wageni wasiotahiriwa mioyo na miili katika patakatifu pangu. Mmelinajisi Hekalu langu, huku mkinitolea chakula, mafuta ya wanyama na damu, nanyi mmevunja agano langu. \v 8 Badala ya kutimiza wajibu wenu kuhusiana na vitu vyangu vitakatifu, mmeweka watu wengine kuwa viongozi katika patakatifu pangu. \v 9 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli. \p \v 10 “ ‘Walawi walioniacha wakati Waisraeli walipopotoka wakatoka kwangu na kutangatanga kwa kufuata sanamu zao, sharti watachukua adhabu ya dhambi zao. \v 11 Wanaweza wakatumika katika mahali patakatifu pangu, wakiwa na uangalizi wa malango ya Hekalu; wanaweza kuchinja wanyama wa sadaka za kuteketezwa, na kutoa dhabihu kwa ajili ya watu, na kusimama mbele ya watu ili kuwahudumia. \v 12 Lakini kwa sababu walitumikia watu wakiwa mbele ya sanamu zao, na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 13 Hawaruhusiwi kukaribia ili kunitumikia kama makuhani wala kukaribia chochote changu kilicho kitakatifu au sadaka iliyo takatifu kupita zote, bali watachukua aibu ya matendo yao ya kuchukiza. \v 14 Lakini nitawaweka katika uangalizi wa Hekalu na kazi zote zile zinazotakiwa kufanyika ndani yake. \p \v 15 “ ‘Lakini makuhani, ambao ni Walawi na wazao wa Sadoki, ambao walitimiza wajibu wao kwa uaminifu katika patakatifu pangu wakati Waisraeli walipopotoka, watakaribia ili kutumika mbele zangu. Itawapasa wasimame mbele zangu ili kutoa dhabihu za mafuta ya wanyama na damu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 16 Wao peke yao ndio wenye ruhusa ya kuingia mahali patakatifu pangu. Wao peke yao ndio watakaokaribia meza yangu ili kuhudumu mbele zangu na kufanya utumishi wangu. \p \v 17 “ ‘Watakapoingia kwenye malango ya ukumbi wa ndani, watavaa nguo za kitani safi, hawaruhusiwi kamwe kuvaa mavazi ya sufu wakati wanapokuwa wakihudumu kwenye malango ya ukumbi wa ndani wala ndani ya Hekalu. \v 18 Watavaa vilemba vya kitani safi vichwani mwao na nguo za ndani za kitani safi viunoni mwao. Hawatavaa chochote kitakachowafanya kutoa jasho. \v 19 Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili wasije wakaambukiza watu utakatifu kupitia mavazi yao. \p \v 20 “ ‘Hawatanyoa nywele za vichwa vyao wala kuziacha ziwe ndefu, bali watazipunguza. \v 21 Kuhani yeyote asinywe mvinyo aingiapo katika ukumbi wa ndani. \v 22 Wasioe wanawake wajane wala walioachika, inawapasa kuoa wanawake bikira wenye heshima wa Israeli au wajane wa makuhani. \v 23 Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida na kuwaonesha jinsi ya kupambanua kati ya vitu najisi na vitu safi. \p \v 24 “ ‘Katika magombano yoyote, makuhani watatumika kama mahakimu na kuamua hilo jambo kufuatana na sheria zangu. Watazishika sheria zangu na maagizo yangu katika sikukuu zangu zote zilizoamriwa, nao watatakasa Sabato zangu. \p \v 25 “ ‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti; lakini, ikiwa mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hakuolewa, basi anaweza kujitia unajisi kwa hao. \v 26 Baada ya kujitakasa, atakaa hali hiyo kwa muda wa siku saba. \v 27 Siku atakapoingia katika ukumbi wa ndani wa mahali patakatifu ili kuhudumu, atatoa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 28 “ ‘Mimi ndio nitakuwa urithi pekee wa makuhani katika Israeli. Msiwape wao milki, mimi nitakuwa milki yao. \v 29 Wao watakula sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia na kila kitu kitakachotolewa kwa Mwenyezi Mungu katika Israeli kitakuwa chao. \v 30 Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili baraka ipate kuwa katika nyumba zenu. \v 31 Makuhani hawaruhusiwi kula chochote, ikiwa ni ndege au mnyama, aliyekutwa amekufa au aliyeraruliwa na wanyama pori. \c 45 \s1 Mgawanyo wa nchi \p \v 1 “ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Mwenyezi Mungu kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa elfu ishirini na tano\f + \fr 45:1 \fr*\ft Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25.\ft*\f*, na upana wake dhiraa elfu ishirini\f + \fr 45:1 \fr*\ft Dhiraa 20,000 ni sawa na kilomita 9.\ft*\f*; eneo hili lote litakuwa takatifu. \v 2 Katika eneo hilo patakuwa na sehemu mraba ambayo ni ya mahali patakatifu; kila upande utakuwa dhiraa mia tano, ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini. \v 3 Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi\f + \fr 45:3 \fr*\ft Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5.\ft*\f*. Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, ndipo Patakatifu pa Patakatifu. \v 4 Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Mwenyezi Mungu. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu. \v 5 Eneo la urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi litakuwa la Walawi, wanaohudumu hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi. \p \v 6 “ ‘Utatoa mji kama mali yao, wenye upana wa dhiraa elfu tano\f + \fr 45:6 \fr*\ft Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25.\ft*\f*, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano karibu na sehemu takatifu; itakuwa mali ya nyumba yote ya Israeli. \p \v 7 “ ‘Mkuu anayetawala atakuwa na eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu kwa upande moja, na eneo la mji upande mwingine. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi, na kuenea mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki, sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila. \v 8 Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawatawadhulumu tena watu wangu, bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao. \p \v 9 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 10 Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa\f + \fr 45:10 \fr*\ft Efa ni kipimo cha ujazo cha kupimia vitu vikavu ambacho ni sawa na omeri 10; efa 1 ni sawa na kilo 22.\ft*\f* na bathi\f + \fr 45:10 \fr*\ft Bathi ni kipimo cha ujazo cha kupimia vitu vya humiminika ambacho ni sawa na 1/10 ya homeri; homeri 1 ni bathi 10 au efa 10.\ft*\f*. \v 11 Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili. \v 12 Shekeli moja itakuwa gera ishirini. Shekeli ishirini, jumlisha na shekeli ishirini na tano, jumlisha na shekeli kumi na tano zitakuwa mina moja\f + \fr 45:12 \fr*\ft Mina 1 hapa ni sawa na shekeli 60; mina ya kawaida ilikuwa sawa na shekeli 50.\ft*\f*. \s1 Sadaka na siku takatifu \r (Kutoka 12:1-20; Walawi 23:33-43) \p \v 13 “ ‘Hili ndilo toleo maalum mtakalotoa: sehemu ya sita ya efa kutoka kila homeri ya ngano, na sehemu ya sita ya efa kutoka kila homeri ya shayiri. \v 14 Sehemu ya mafuta iliyoamriwa, yaliyopimwa kwa bathi, ni sehemu ya kumi ya bathi kutoka kila kori moja (ambayo ina bathi kumi au homeri moja, kwa kuwa bathi kumi ni homeri moja). \v 15 Pia kondoo mmoja atachukuliwa kutoka kila kundi la kondoo mia mbili katika malisho yenye maji mengi ya Israeli. Hivi vitatumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya watu, asema Bwana Mungu Mwenyezi. \v 16 Watu wote wa nchi wataungana pamoja katika kutoa sadaka hii maalum ya kutumiwa na mkuu anayetawala Israeli. \v 17 Utakuwa wajibu wa mkuu anayetawala kutoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji kwenye sikukuu, Mwezi Mwandamo na Sabato, kwenye sikukuu zote zilizoamriwa za nyumba ya Israeli. Atatoa sadaka za dhambi, sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli. \p \v 18 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya huo mwezi utamchukua fahali mchanga asiye na dosari na kutakasa mahali patakatifu. \v 19 Kuhani itampasa achukue sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi na kuipaka kwenye miimo ya Hekalu, kwenye pembe nne za juu za ukingo wa hayo madhabahu na juu ya miimo ya lango la ukumbi wa ndani. \v 20 Itakupasa kufanya vivyo hivyo katika siku ya saba ya mwezi huo kwa ajili ya mtu ambaye hutenda dhambi bila kukusudia au bila kujua; ndivyo utafanya upatanisho kwa ajili ya Hekalu. \p \v 21 “ ‘Katika mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne utaadhimisha Pasaka. Sikukuu itaendelea kwa siku saba, wakati huo wa hizo siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. \v 22 Katika siku hiyo mkuu anayetawala atatoa fahali kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote wa nchi. \v 23 Kila siku wakati wa hizo siku saba za sikukuu atatoa mafahali saba na kondoo dume saba wasio na dosari kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu na beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi. \v 24 Pia atatoa sadaka ya nafaka efa moja kwa kila fahali, na efa moja kwa kila kondoo dume, pamoja na hini moja\f + \fr 45:24 \fr*\ft Hini ni kipimo cha kupimia vitu vya humiminika chenye ujazo wa 1/6 ya bathi, na ni sawa na lita 4.\ft*\f* ya mafuta kwa kila efa. \p \v 25 “ ‘Wakati wa hizo siku saba za sikukuu, ambayo huanza katika mwezi wa saba kwenye siku ya kumi na tano, mkuu anayetawala atatoa mahitaji yale yale kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta. \c 46 \s1 Sheria nyingine mbalimbali \p \v 1 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa. \v 2 Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa hadi jioni. \v 3 Siku za Sabato na za Mwezi Mwandamo watu wote wa nchi wataabudu mbele za Mwenyezi Mungu penye lile ingilio la ile njia. \v 4 Sadaka za kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa Mwenyezi Mungu siku ya Sabato zitakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari. \v 5 Sadaka ya nafaka inayotolewa pamoja na huyo kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya nafaka inayotolewa na hao wana-kondoo itakuwa kiasi apendacho mtu pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa. \v 6 Siku ya Mwezi Mwandamo atatoa fahali mchanga, wana-kondoo sita na kondoo dume, wote wasiwe na dosari. \v 7 Atatoa sadaka ya nafaka ya: efa moja kwa huyo fahali, na efa moja kwa huyo kondoo dume; na kwa wana-kondoo atatoa nafaka nyingi kama atakavyo kutoa; atatoa hini ya mafuta kwa kila efa. \v 8 Mkuu anayetawala atakapoingia, atapitia kwenye baraza ya njia ya lango, naye atatoka nje kwa njia hiyo hiyo. \p \v 9 “ ‘Watu wa nchi wanapokuja mbele za Mwenyezi Mungu katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini; na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia. \v 10 Mkuu anayetawala atakuwa miongoni mwao, akiingia nao ndani wanapoingia, na akitoka nao nje wanapotoka. \p \v 11 “ ‘Kwenye sikukuu na kwenye sikukuu zilizoamriwa, sadaka ya nafaka itakuwa efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja pamoja na kondoo dume mmoja, pamoja na idadi ya wana-kondoo kama mtu apendavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa. \v 12 Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa Mwenyezi Mungu, iwe ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, atafunguliwa lango linaloelekea mashariki. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje. Baada yake kutoka nje, lango litafungwa. \p \v 13 “ ‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu, utaitoa kila siku asubuhi. \v 14 Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa\f + \fr 46:14 \fr*\ft Sehemu ya sita ya efa ni sawa na kilo 2.7.\ft*\f* pamoja na theluthi moja ya hini\f + \fr 46:14 \fr*\ft Theluthi moja ya hini ni sawa na lita 1.3.\ft*\f* ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa Mwenyezi Mungu ni agizo la kudumu. \v 15 Kwa hiyo mwana-kondoo na sadaka ya nafaka na mafuta vitatolewa kila siku asubuhi kwa ajili ya sadaka ya daima ya kuteketezwa. \p \v 16 “ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Ikiwa mkuu anayetawala atatoa zawadi kutoka urithi wake na kumpa mmoja wa wanawe, hiyo zawadi itakuwa pia kwa wazao wake; itakuwa mali yao kwa urithi. \v 17 Hata hivyo, kama atatoa zawadi kutoka urithi wake na kumpa mmoja wa watumishi wake, mtumishi anaweza kuiweka hadi mwaka wa uhuru, kisha itarudishwa kwa mkuu anayetawala. Urithi wake ni wa wanawe peke yao, ni mali yao. \v 18 Mkuu anayetawala hafai kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali yao. Mkuu huyo atawapa wanawe urithi wao katika mali yake mwenyewe, ili pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’ ” \p \v 19 Kisha mtu yule akanileta kupitia kwenye ingilio lililokuwa kando ya lango hadi kwenye vyumba vitakatifu vilivyoelekea kaskazini, ambavyo ni vya makuhani, naye akanionesha mahali fulani upande wa mwisho wa magharibi. \v 20 Akaniambia, “Mahali hapa ndipo makuhani watakapotokosea sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi, na kuoka sadaka ya nafaka, ili kuepuka kuzileta katika ukumbi wa nje na kushirikisha utakatifu kwa watu.” \p \v 21 Baada ya hapo akanileta kwenye ukumbi wa nje na kunizungusha kwenye pembe zake nne, nami nikaona katika kila pembe ya huo ukumbi kulikuwa na ukumbi mwingine. \v 22 Katika pembe nne za huo ukumbi wa nje kulikuwa na kumbi nyingine, zenye urefu wa dhiraa arobaini na upana wake dhiraa thelathini, ambapo hizo kumbi kwenye hizo pembe nne zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. \v 23 Mzunguko wa ndani wa hizo kumbi nne ulikuwa na ukingo wa jiwe, zikiwa na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya moto kuzunguka chini ya huo ukingo. \v 24 Akaniambia, “Hizi ndizo sehemu za kupikia ambazo wale wanaohudumu kwenye Hekalu watatokosea dhabihu za watu.” \c 47 \s1 Mto kutoka Hekaluni \p \v 1 Yule mtu akanirudisha kwenye ingilio la Hekalu, nami nikaona maji yakitoka chini ya kizingiti cha Hekalu yakitiririkia upande wa mashariki (kwa maana upande wa mbele wa Hekalu ulielekea mashariki). Maji yalikuwa yakitoka chini upande wa kusini wa Hekalu, kusini mwa madhabahu. \v 2 Ndipo akanitoa nje kupitia lango la kaskazini na kunizungusha mpaka kwenye lango la nje linaloelekea mashariki, nayo maji yalikuwa yakitiririka kutoka upande wa kusini. \p \v 3 Mtu yule alipoenda upande wa mashariki akiwa na kamba ya kupimia mkononi mwake, akapima dhiraa elfu moja\f + \fr 47:3 \fr*\ft Dhiraa 1,000 ni sawa na mita 450.\ft*\f*, kisha akanipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kwenye vifundo vya miguu. \v 4 Akapima dhiraa elfu moja nyingine na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika magotini. Akapima dhiraa nyingine elfu moja na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kiunoni. \v 5 Akapima tena dhiraa elfu moja nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu angeweza kuuvuka. \v 6 Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?” \p Kisha akanirudisha kwenye ukingo wa huo mto. \v 7 Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto. \p \v 8 Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka hadi Araba\f + \fr 47:8 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bonde la Yordani\fqa*\f*, ambapo huingia Baharini\f + \fr 47:8 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Chumvi\fqa*\f*. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari, maji hayo huponywa na kuwa safi. \v 9 Popote mto huu unatakapofika, kila kiumbe hai kinachoingia ndani ya hayo maji kitaishi. Nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yatakapofika huko. Maji hayo yatakuwa hai, na kila kitu kitaishi popote mto utakapofika. \v 10 Wavuvi watasimama kando ya bahari; kuanzia En-Gedi hadi En-Eglaimu kutakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki. Samaki watakuwa wa aina nyingi, kama samaki wa Bahari Kuu.\f + \fr 47:10 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Mediterania\fqa*\f* \v 11 Lakini madimbwi yake na mabwawa yake hayatakuwa na maji yanayofaa kunywa, bali yatabakia kuwa maji ya chumvi. \v 12 Miti ya matunda ya kila aina itaota kwenye kingo zote mbili za mto huu. Majani yake hayatanyauka wala haitaacha kuwa na matunda katika matawi yake. Kila mwezi kutakuwa na matunda, kwa sababu maji yanayotoka patakatifu yataitiririkia. Matunda yake yatakuwa chakula na majani yake yatakuwa dawa.” \s1 Mipaka ya nchi \p \v 13 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Hii ndiyo mipaka ambayo kwayo mtagawanya hiyo nchi kuwa urithi miongoni mwa hayo makabila kumi na mawili ya Israeli, pamoja na mafungu mawili ya Yusufu. \v 14 Mtagawa kwa usawa miongoni mwao. Kwa sababu niliapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu, nchi hii itakuwa urithi wenu. \b \lh \v 15 “Huu ndio utakuwa mpaka wa hiyo nchi: \b \li1 “Upande wa kaskazini utaanzia Bahari Kuu kwa njia ya Hethloni kupitia Lebo-Hamathi hadi maingilio ya Sedadi. \v 16 Berotha na Sibraimu (ambao uko kwenye mpaka kati ya Dameski na Hamathi), hadi kufikia Haser-Hatikoni, ambao uko katika mpaka wa Haurani. \v 17 Hivyo mpaka utaendelea kuanzia Baharini hadi Hasar-Enoni, ukiambaa na mpaka wa kaskazini wa Dameski, pamoja na mpaka wa Hamathi upande wa kaskazini. Huu utakuwa mpaka wa kaskazini. \li1 \v 18 Upande wa mashariki mpaka utapita kati ya Haurani na Dameski, kuambaa Yordani na kati ya Gileadi na nchi ya Israeli, hadi bahari ya mashariki\f + \fr 47:18 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Chumvi\fqa*\f* na kufika Tamari. Huu utakuwa mpaka wa mashariki. \li1 \v 19 Upande wa kusini utaanzia Tamari hadi kufikia maji ya Meriba-Kadeshi, kisha utaambaa na Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu. Huu utakuwa ndio mpaka wa kusini. \li1 \v 20 Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa mpaka wa magharibi. \b \p \v 21 “Mtagawanya nchi hii miongoni mwenu kufuatana na makabila ya Israeli. \v 22 Mtaigawanya kuwa urithi kwa ajili yenu na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwenu na ambao wana watoto. Wao watakuwa kwenu kama wenyeji wazawa wa Israeli, pamoja na ninyi watagawiwa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli. \v 23 Katika kabila lolote mgeni atakapoishi, hapo ndipo mtakapompatia urithi wake,” asema Bwana Mungu Mwenyezi. \c 48 \s1 Mgawanyo wa nchi \lh \v 1 “Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: \b \li1 “Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja; mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi; Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi. \li1 \v 2 Asheri atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi. \li1 \v 3 Naftali atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 4 Manase atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 5 Efraimu atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 6 Reubeni atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 7 Yuda atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi. \b \p \v 8 “Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa elfu ishirini na tano\f + \fr 48:8 \fr*\ft Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25.\ft*\f*, nao urefu wake kuanzia mashariki hadi magharibi utakuwa sawa na sehemu moja ya kabila; mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo. \p \v 9 “Hiyo sehemu maalum mtakayotoa kwa Mwenyezi Mungu itakuwa na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi\f + \fr 48:9 \fr*\ft Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5.\ft*\f*. \v 10 Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kaskazini, upana wa dhiraa elfu kumi upande wa magharibi, dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Mwenyezi Mungu. \v 11 Hii itakuwa kwa ajili ya makuhani waliowekwa wakfu, Wasadoki, waliokuwa waaminifu katika kunitumikia, nao hawakupotoka kama Walawi walivyofanya wakati Waisraeli walipopotoka. \v 12 Itakuwa toleo maalum kwao kutoka sehemu takatifu ya nchi, yaani sehemu takatifu sana, inayopakana na nchi ya Walawi. \p \v 13 “Kando ya nchi ya makuhani, Walawi watakuwa na mgawo wa urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi. Urefu wake utakuwa jumla dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi. \v 14 Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. \p \v 15 “Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa elfu tano\f + \fr 48:15 \fr*\ft Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25.\ft*\f*, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na maeneo ya malisho. Mji utakuwa katikati yake \v 16 nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa elfu nne na mia tano\f + \fr 48:16 \fr*\ft Dhiraa 4,500 ni sawa na kilomita 2.025.\ft*\f*, upande wa kusini dhiraa elfu nne na mia tano, upande wa mashariki dhiraa elfu nne na mia tano, na upande wa magharibi dhiraa elfu nne na mia tano. \v 17 Eneo la malisho kwa ajili ya mji litakuwa na eneo la dhiraa mia mbili na hamsini\f + \fr 48:17 \fr*\ft Dhiraa 250 ni sawa na sentimita 112.5.\ft*\f* upande wa kaskazini, dhiraa mia mbili na hamsini upande wa kusini, dhiraa mia mbili na hamsini upande wa mashariki, na dhiraa mia mbili na hamsini upande wa magharibi. \v 18 Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na dhiraa elfu kumi upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula. \v 19 Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli. \v 20 Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani dhiraa elfu ishirini na tano kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji. \p \v 21 “Eneo linalobaki pande mbili za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu anayetawala. Eneo hili litaenea upande wa mashariki, kuanzia kwenye dhiraa elfu ishirini na tano za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki, na kuelekea upande wa magharibi, kuanzia kwenye dhiraa elfu ishirini na tano hadi mpaka wa magharibi. Maeneo haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake. \v 22 Kwa hiyo milki ya Walawi na milki ya mji vitakuwa katikati ya eneo lile ambalo ni mali ya mkuu anayetawala. Eneo la mkuu anayetawala litakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini. \b \lh \v 23 “Kuhusu makabila yaliyobaki: \b \li1 “Benyamini atakuwa na sehemu moja; itakayoanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi. \li1 \v 24 Simeoni atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Benyamini kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 25 Isakari atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Simeoni kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 26 Zabuloni atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Isakari kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 27 Gadi atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Zabuloni kuanzia mashariki hadi magharibi. \li1 \v 28 Mpaka wa kusini wa Gadi utapita kusini kuanzia Tamari hadi maji ya Meriba-Kadeshi, kisha kupitia upande wa Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu\f + \fr 48:28 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Mediterania\fqa*\f*. \b \lf \v 29 “Hii ndiyo nchi mtakayogawanya kuwa urithi kwa makabila ya Israeli, nazo zitakuwa sehemu zao,” asema Bwana Mungu Mwenyezi. \s1 Malango ya mji mpya \lh \v 30 “Haya yatakuwa ndiyo malango ya mji ya kutokea: \b \li1 “Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu, \v 31 malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi. \li1 \v 32 Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Yusufu, lango la Benyamini na lango la Dani. \li1 \v 33 Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni. \li1 \v 34 Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali. \b \lf \v 35 “Urefu wote kuzunguka utakuwa dhiraa elfu kumi na nane\f + \fr 48:35 \fr*\ft Dhiraa 18,000 ni sawa na kilomita 8.1.\ft*\f*. \b \p “Nalo jina la mji huo kuanzia wakati huo na kuendelea litakuwa: ‘Mwenyezi Mungu yupo hapa.’ ”