\id EXO - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Kutoka \toc1 Kutoka \toc2 Kutoka \toc3 Kut \mt1 Kutoka \c 1 \s1 Waisraeli wagandamizwa \lh \v 1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, kila mmoja na jamaa yake: \b \li1 \v 2 Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; \li1 \v 3 Isakari, Zabuloni na Benyamini; \li1 \v 4 Dani na Naftali, Gadi na Asheri. \b \lf \v 5 Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yusufu alikuwa tayari yuko Misri. \b \p \v 6 Basi Yusufu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, \v 7 lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, hadi wakaijaza nchi. \p \v 8 Kisha mfalme mwingine ambaye hakufahamu habari za Yusufu akatawala Misri. \v 9 Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kuliko sisi. \v 10 Njooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana nasi, na kuondoka katika nchi hii.” \p \v 11 Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao. \v 12 Lakini walivyozidi kuteswa, ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi. Wamisri wakawaogopa Waisraeli, \v 13 kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili. \v 14 Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili. \p \v 15 Mfalme wa Misri akawaita wakunga waliowazalisha Waebrania, ambao majina yao yalikuwa Shifra na Pua, akawaambia, \v 16 “Mtakapowazalisha wanawake Waebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni; lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” \v 17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. \v 18 Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?” \p \v 19 Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Waebrania ni tofauti na wanawake wa Misri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.” \p \v 20 Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. \v 21 Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe. \p \v 22 Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.” \c 2 \s1 Kuzaliwa kwa Musa \p \v 1 Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, \v 2 naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. \v 3 Lakini alipoona hawezi kuendelea kumficha, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha kwenye matete kando ya ukingo wa Mto Naili. \v 4 Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto. \p \v 5 Ndipo binti Farao akateremka kwenye Mto Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti Farao akaona kisafina kwenye matete, akamtuma mmoja wa wajakazi wake kukichukua. \v 6 Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Waebrania.” \p \v 7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Waebrania akulelee huyu mtoto?” \p \v 8 Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. \v 9 Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. \v 10 Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina Musa, akisema, “Nilimtoa kwenye maji.” \s1 Musa akimbilia Midiani \p \v 11 Siku moja, Musa alipokuwa mtu mzima, alienda mahali walipokuwa ndugu zake, na akaona jinsi walivyokuwa wakifanyishwa kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmoja wa watu wake. \v 12 Musa akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha kwenye mchanga. \v 13 Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamuuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?” \p \v 14 Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.” \p \v 15 Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Musa, lakini Musa akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima. \v 16 Kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja kisimani ili kuchota maji na kujaza birika kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya baba yao. \v 17 Baadhi ya wachungaji wakaja wakawafukuza hao wasichana. Ndipo Musa akainuka, akawasaidia kunywesha mifugo yao. \p \v 18 Wasichana hao waliporudi nyumbani, baba yao Reueli akawauliza, “Imekuwaje leo mmerudi mapema hivyo?” \p \v 19 Wakamjibu, “Mmisri mmoja alituokoa kutoka mikono ya wachungaji. Pia mtu huyo alituchotea maji na kunywesha mifugo.” \p \v 20 Akawauliza binti zake, “Yuko wapi? Mbona mmemwacha? Mkaribisheni ale chakula.” \p \v 21 Musa akakubali kukaa kwa huyo mtu, ambaye alimpa Musa binti yake aliyeitwa Sipora amwoe. \v 22 Sipora alizaa mtoto wa kiume, naye Musa akamwita jina Gershomu, akisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” \p \v 23 Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu. \v 24 Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka agano alilofanya na Ibrahimu pamoja na Isaka na Yakobo. \v 25 Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia. \c 3 \s1 Musa na kichaka kilichowaka moto \p \v 1 Basi Musa alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Musa akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. \v 2 Huko malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Musa katika mwali wa moto kutoka kichakani. Musa akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. \v 3 Ndipo Musa akawaza, “Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei.” \p \v 4 Mwenyezi Mungu alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, “Musa! Musa!” \p Naye Musa akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 5 Mungu akamwambia, “Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.” \v 6 Kisha akamwambia, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.” Musa aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu. \p \v 7 Mwenyezi Mungu akamwambia, “Hakika nimeona mateso ya watu wangu katika Misri. Nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao, nami nimeguswa na mateso yao. \v 8 Basi nimeshuka niwaokoe kutoka mkono wa Wamisri, niwatoe na kuwapandisha kutoka nchi hiyo, niwapeleke katika nchi nzuri na kubwa, nchi inayotiririka maziwa na asali, nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 9 Sasa kilio cha Waisraeli kimenifikia, nami nimeona jinsi Wamisri wanavyowatesa. \v 10 Basi, sasa nenda. Ninakutuma kwa Farao ili kuwatoa watu wangu Waisraeli kutoka Misri.” \p \v 11 Lakini Musa akamwambia Mungu, “Mimi ni nani hata niende kwa Farao kuwatoa Waisraeli nchini Misri?” \p \v 12 Naye Mungu akasema, “Mimi nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako kwamba ni Mimi nimekutuma: Utakapokuwa umewatoa watu Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.” \p \v 13 Musa akamwambia Mungu, “Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani?’ Nitawaambia nini?” \p \v 14 Mungu akamwambia Musa, “\nd Mimi niko ambaye niko\nd*\f + \fr 3:14 \fr*\ft au \ft*\fqa \+nd Nitakuwa kama Nitakavyokuwa\+nd*\fqa*\ft ; au, \+nd Mimi Ndiye\+nd*\ft*\f*. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘\nd Mimi niko\nd* amenituma kwenu.’ ” \p \v 15 Vilevile Mungu akamwambia Musa, “Waambie Waisraeli, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’ \q1 “Hili ndilo Jina langu milele, \q2 Jina ambalo mtanikumbuka kwalo \q2 kizazi hadi kizazi. \p \v 16 “Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyotendewa huku Misri. \v 17 Nami nimeahidi kuwapandisha kutoka kwenye mateso yenu katika nchi ya Misri, niwapeleke nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, nchi inayotiririka maziwa na asali.’ \p \v 18 “Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtaenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, ametutokea. Turuhusu twende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.’ \v 19 Lakini nafahamu kwamba mfalme wa Misri hatawaruhusu kwenda, hadi mkono wenye nguvu umlazimishe. \v 20 Kwa hiyo nitaunyoosha mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa maajabu yote nitakayofanya miongoni mwao. Baada ya hayo, atawaruhusu mwondoke. \p \v 21 “Nami nitawapa hawa watu upendeleo mbele ya Wamisri, kwa hiyo mtakapoondoka nchini hamtaondoka mikono mitupu. \v 22 Kila mwanamke Mwisraeli atamwomba jirani yake Mmisri na mwanamke yeyote anayeishi nyumbani mwake ampe vyombo vya fedha, dhahabu na mavazi, ambavyo mtawavika wana wenu wa kiume na wa kike. Hivyo mtawateka nyara Wamisri.” \c 4 \s1 Ishara za Musa \p \v 1 Musa akamjibu, “Itakuwaje wasiponiamini au kunisikiliza, waseme, ‘Mwenyezi Mungu hakukutokea’?” \p \v 2 Ndipo Mwenyezi Mungu akamuuliza, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?” \p Akamjibu, “Ni fimbo.” \p \v 3 Mwenyezi Mungu akasema, “Itupe chini.” \p Musa akaitupa fimbo chini, nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. \v 4 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate kwenye mkia.” Basi Musa akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. \v 5 Mwenyezi Mungu akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.” \p \v 6 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia, “Weka mkono wako ndani ya joho lako.” Basi Musa akaweka mkono wake ndani ya joho lake, naye alipoutoa, ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji. \p \v 7 Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Musa akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake. \p \v 8 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia, “Kama hawatakuamini wewe, au kutojali ishara ya kwanza, wataamini ishara ya pili. \v 9 Lakini kama hawataamini ishara hizi mbili au hawatawasikiliza ninyi, chukua kiasi cha maji kutoka Mto Naili uyamimine juu ya ardhi kavu. Maji mtakayotoa mtoni yatakuwa damu juu ya ardhi.” \p \v 10 Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha hapo awali, wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.” \p \v 11 Mwenyezi Mungu akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu uwezo wa kuona au upofu? Je, si mimi, Mwenyezi Mungu? \v 12 Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.” \p \v 13 Lakini Musa akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.” \p \v 14 Ndipo hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Musa, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Haruni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona. \v 15 Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya. \v 16 Haruni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake. \v 17 Lakini chukua fimbo hii mkononi mwako ili uweze kuitumia kufanya ishara hizo za ajabu.” \s1 Musa anarudi Misri \p \v 18 Kisha Musa akarudi kwa Yethro mkwewe akamwambia, “Niruhusu nirudi kwa watu wangu Misri kuona kama yuko hata mmoja wao ambaye bado anaishi.” \p Yethro akamwambia, “Nenda, nami nakutakia mema.” \p \v 19 Basi Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa huko Midiani, “Rudi Misri kwa maana watu wote waliotaka kukuua wamekufa.” \v 20 Basi Musa akamchukua mkewe na wanawe, akawapandisha juu ya punda na kuanza safari kurudi Misri. Naye akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake. \p \v 21 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Utakaporudi Misri, hakikisha kwamba utafanya mbele ya Farao maajabu yote niliyokupa uwezo wa kuyafanya. Lakini nitafanya moyo wake kuwa mgumu ili asiwaruhusu watu waende. \v 22 Kisha mwambie Farao, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Israeli ni mwanangu mzaliwa wa kwanza, \v 23 nami nilikuambia, “Ruhusu mwanangu aondoke, ili aweze kuniabudu mimi.” Lakini ukakataa kumruhusu aende; basi nitaua mwana wako mzaliwa wa kwanza.’ ” \p \v 24 Musa alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, Mwenyezi Mungu akakutana naye, akataka kumuua. \v 25 Lakini Sipora akachukua kisu cha gumegume, akakata govi la mwanawe na kugusa miguu ya Musa nalo. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.” \v 26 (Sipora alipomwita Musa, “Bwana arusi wa damu”, alikuwa anamaanisha ile tohara.) Baada ya hayo Mwenyezi Mungu akamwacha. \p \v 27 Mwenyezi Mungu akamwambia Haruni, “Nenda jangwani ukamlaki Musa.” Basi akakutana na Musa kwenye mlima wa Mungu, akambusu. \v 28 Kisha Musa akamwambia Haruni kila kitu Mwenyezi Mungu alichomtuma kusema, vilevile habari za ishara na maajabu alizokuwa amemwamuru kufanya. \p \v 29 Musa na Haruni wakawakusanya wazee wote wa Waisraeli, \v 30 naye Haruni akawaambia kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amemwambia Musa. Pia akafanya ishara mbele ya watu, \v 31 nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa Mwenyezi Mungu anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu. \c 5 \s1 Matofali bila nyasi \p \v 1 Baadaye Musa na Haruni wakaenda kwa Farao, wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Waruhusu watu wangu waende, ili waweze kunifanyia sikukuu huko jangwani.’ ” \p \v 2 Farao akasema, “Huyo Mwenyezi Mungu ni nani, hata nimtii na kuruhusu Waisraeli waende? Simjui huyo Mwenyezi Mungu wala sitawaruhusu Waisraeli waende.” \p \v 3 Ndipo Musa na Haruni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtolee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.” \p \v 4 Lakini mfalme wa Misri akasema, “Mbona ninyi Musa na Haruni mnawaondoa watu kutoka kwenye kazi zao? Rudini kwenye kazi zenu!” \v 5 Kisha Farao akasema, “Tazama, sasa watu hawa ni wengi, nanyi mnawazuia kufanya kazi.” \p \v 6 Siku hiyo hiyo, Farao akatoa amri hii kwa viongozi wa watumwa na wasimamizi wa watu, akawaambia: \v 7 “Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali; wakusanye nyasi zao wenyewe. \v 8 Lakini watakeni kutengeneza matofali kiasi kile kile cha mwanzo, kiwango kisipunguzwe. Wao ni wavivu, ndiyo sababu wanalia, wakisema, ‘Turuhusiwe twende kumtolea Mungu wetu dhabihu.’ \v 9 Fanyeni kazi kuwa ngumu zaidi kwa watu hao ili wakazane na kazi na kuacha kusikiliza uongo.” \p \v 10 Basi viongozi wa watumwa na wasimamizi wakaenda kuwaambia watu, “Hivi ndivyo Farao asemavyo: ‘Sitawapa nyasi tena. \v 11 Nendeni mkatafute nyasi wenyewe popote mnapoweza kuzipata, lakini kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo.’ ” \v 12 Basi watu wakatawanyika kote nchini Misri kukusanya mabua ya kutumia badala ya nyasi. \v 13 Viongozi wa watumwa wakasisitiza wakisema, “Timizeni kazi mnayotakiwa kwa kila siku, kama wakati ule mlipokuwa mkipewa nyasi.” \v 14 Wasimamizi wa Waisraeli waliochaguliwa na viongozi wa watumwa wa Farao walipigwa na kuulizwa, “Kwa nini hamkutimiza kiwango chenu cha kutengeneza matofali jana na leo, kama mwanzoni?” \p \v 15 Ndipo wasimamizi wa Waisraeli wakaenda kumlilia Farao, wakisema: “Mbona umewatendea watumishi wako hivi? \v 16 Watumishi wako hawapewi nyasi, hata hivyo tumeambiwa, ‘Tengenezeni matofali!’ Watumishi wako wanapigwa, lakini kosa ni la watu wako wenyewe.” \p \v 17 Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtolee Mwenyezi Mungu dhabihu.’ \v 18 Sasa nendeni kazini. Hamtapewa nyasi zozote, nanyi ni lazima mtengeneze matofali.” \p \v 19 Wasimamizi wa Waisraeli walitambua kuwa wako taabani walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.” \v 20 Walipoondoka kwa Farao, wakawakuta Musa na Haruni wakingojea kukutana nao, \v 21 wakawaambia Musa na Haruni, “Mwenyezi Mungu na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tuwe chukizo kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.” \s1 Mwenyezi Mungu anaahidi ukombozi \p \v 22 Musa akarudi kwa Mwenyezi Mungu na kumwambia, “Ee Bwana, mbona umewaletea watu hawa taabu? Kwa nini basi ukanituma mimi? \v 23 Tangu nilipokwenda kuzungumza na Farao kwa jina lako, amewaletea watu hawa taabu, nawe kamwe hujawakomboa watu wako.” \c 6 \p \v 1 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.” \p \v 2 Pia Mungu akamwambia Musa, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 3 Nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo kama Mungu Mwenyezi\f + \fr 6:3 \fr*\ft Kiebrania \ft*\fqa El-Shaddai \fqa*\ft (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\ft*\f*, ingawa kwa Jina langu, \nd Yehova\nd*, sikujitambulisha kwao. \v 4 Pia niliweka agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. \v 5 Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka agano langu. \p \v 6 “Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, nami nitawatoa katika nira ya Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu. \v 7 Nitawachukua ninyi kuwa watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa chini ya nira ya Wamisri. \v 8 Nami nitawaleta hadi nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 9 Musa akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya kuvunjika moyo na kazi yao ngumu. \p \v 10 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 11 “Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.” \p \v 12 Lakini Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?” \s1 Orodha ya jamaa ya Musa na Haruni \p \v 13 Ndipo Mwenyezi Mungu akanena na Musa na Haruni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri. \b \lh \v 14 Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao: \b \li1 Wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa: \li2 Hanoki na Palu, Hesroni na Karmi. \lf Hizo zilikuwa koo za Reubeni. \b \li1 \v 15 Wana wa Simeoni walikuwa: \li2 Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. \lf Hizo zilikuwa koo za Simeoni. \b \li1 \v 16 Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na orodha zao: \li2 Gershoni, Kohathi na Merari. \lf Lawi aliishi miaka mia moja na thelathini na saba (137). \li2 \v 17 Wana wa Gershoni kwa koo walikuwa: \li3 Libni na Shimei. \li2 \v 18 Wana wa Kohathi walikuwa: \li3 Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. \li2 Kohathi aliishi miaka mia moja na thelathini na tatu (133). \li2 \v 19 Wana wa Merari walikuwa: \li3 Mahli na Mushi. \lf Hizo zilikuwa koo za Lawi, kulingana na orodha zao. \b \li1 \v 20 Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, aliyemzalia Haruni na Musa. \lf Amramu aliishi miaka mia moja na thelathini na saba (137). \li1 \v 21 Wana wa Ishari walikuwa: \li2 Kora, Nefegi na Zikri. \li1 \v 22 Wana wa Uzieli walikuwa: \li2 Mishaeli, Elisafani na Sithri. \li1 \v 23 Haruni akamwoa Elisheba binti Aminadabu, ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. \b \li1 \v 24 Wana wa Kora walikuwa: \li2 Asiri, Elkana na Abiasafu. \lf Hizo zilikuwa koo za Kora. \b \li1 \v 25 Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. \b \lf Hao walikuwa wakuu wa jamaa za Walawi, kufuatana na koo zao. \b \p \v 26 Hawa walikuwa Haruni na Musa, wale wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” \v 27 Hao ndio waliozungumza na Farao, mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Musa na huyo Haruni. \s1 Haruni kuzungumza badala ya Musa \p \v 28 Mwenyezi Mungu aliponena na Musa huko Misri, \v 29 akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.” \p \v 30 Lakini Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?” \c 7 \p \v 1 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Tazama, nimekufanya kama Mungu kwa Farao, naye Haruni ndugu yako atakuwa nabii wako. \v 2 Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Haruni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake. \v 3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri, \v 4 hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka mkono wangu juu ya Misri, na kwa matendo makuu ya hukumu nitavitoa vikosi vyangu, watu wangu Waisraeli. \v 5 Nao Wamisri watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu nitakapounyoosha mkono wangu dhidi ya Misri na kuwatoa Waisraeli humo.” \p \v 6 Musa na Haruni wakafanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaamuru. \v 7 Musa alikuwa na umri wa miaka themanini na Haruni alikuwa na umri wa miaka themanini na tatu walipozungumza na Farao. \s1 Fimbo ya Haruni yawa nyoka \p \v 8 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa na Haruni, \v 9 “Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni muujiza,’ basi mwambie Haruni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.” \p \v 10 Ndipo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao, wakafanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyoagiza. Haruni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. \v 11 Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Misri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. \v 12 Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Haruni ikazimeza zile fimbo zao. \v 13 Hata hivyo, moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Musa na Haruni, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema. \s1 Pigo la kwanza: Damu \p \v 14 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Moyo wa Farao ni mgumu; anakataa kuwaacha watu waondoke. \v 15 Nenda kwa Farao asubuhi anapoenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Mto Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka. \v 16 Kisha umwambie, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, amenituma nikuambie: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu jangwani. Lakini hadi sasa hujasikiliza. \v 17 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Kwa hili utajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu: Kwa fimbo iliyo mkononi mwangu nitapiga maji ya Mto Naili, nayo yatabadilika kuwa damu. \v 18 Samaki walio katika Mto Naili watakufa, nao mto utanuka vibaya; Wamisri hawataweza kunywa maji yake.’ ” \p \v 19 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Mwambie Haruni, ‘Chukua ile fimbo yako unyooshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya chemchemi na mifereji, juu ya madimbwi na mabwawa yote,’ navyo vitabadilika kuwa damu. Damu itakuwa kila mahali katika Misri, hata kwenye vyombo vya miti na vya mawe.” \p \v 20 Musa na Haruni wakafanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Naili, na maji yote yakabadilika kuwa damu. \v 21 Samaki katika Mto Naili wakafa, nao mto ukanuka vibaya sana kiasi kwamba Wamisri hawakuweza kunywa maji yake. Damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri. \p \v 22 Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Musa na Haruni, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema. \v 23 Badala yake, Farao akageuka, akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni. \v 24 Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Naili kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto. \s1 Pigo la pili: Vyura \p \v 25 Zilipita siku saba baada ya Mwenyezi Mungu kuyapiga maji ya Mto Naili. \c 8 \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. \v 2 Ukikataa kuwaruhusu kuondoka, basi nitaipiga nchi yako yote kwa kuwaletea vyura. \v 3 Mto Naili utafurika vyura. Watakuja kwenye jumba lako la kifalme na katika chumba chako cha kulala na kitandani mwako, katika nyumba za maafisa wako na kwa watu wako, vyura hao wataingia katika meko yenu na kwenye vyombo vya kukandia unga. \v 4 Vyura watapanda juu yako, juu ya watu wako na maafisa wako wote.’ ” \p \v 5 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Mwambie Haruni, ‘Nyoosha mkono wako ukiwa na ile fimbo yako juu ya vijito, mifereji na madimbwi, fanya vyura waje juu ya nchi ya Misri.’ ” \p \v 6 Ndipo Haruni akaunyoosha mkono wake juu ya maji ya Misri, nao vyura wakatokea na kuifunika nchi. \v 7 Lakini waganga wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao, nao pia wakafanya vyura kuja juu ya nchi ya Misri. \p \v 8 Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kusema, “Mwombeni Mwenyezi Mungu awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu.” \p \v 9 Musa akamwambia Farao, “Ninakupa heshima ya kuamua ni wakati gani wa kukuombea wewe, maafisa wako, na watu wako ili vyura watoke kwenu na kwenye nyumba zenu, isipokuwa wale walio katika Mto Naili.” \p \v 10 Farao akasema, “Kesho.” \p Musa akamjibu, “Itakuwa kama unavyosema, ili upate kujua kwamba hakuna yeyote kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \v 11 Vyura wataondoka kwako na katika nyumba zako, kwa maafisa wako na kwa watu wako, ila watabakia katika Mto Naili tu.” \p \v 12 Baada ya Musa na Haruni kuondoka kwa Farao, Musa akamlilia Mwenyezi Mungu kuhusu vyura aliokuwa amewaleta kwa Farao. \v 13 Naye Mwenyezi Mungu akafanya lile Musa alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani. \v 14 Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka. \v 15 Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Musa na Haruni, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema. \s1 Pigo la tatu: Viroboto \p \v 16 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Mwambie Haruni, ‘Nyoosha fimbo yako uyapige mavumbi ya ardhi,’ nayo nchi yote ya Misri mavumbi yatakuwa viroboto.” \v 17 Wakafanya hivyo, Haruni aliponyoosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto. \v 18 Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama. \p \v 19 Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema. \s1 Pigo la nne: Mainzi \p \v 20 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Amka asubuhi na mapema, usimame mbele ya Farao wakati anapoenda mtoni, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. \v 21 Usipowaruhusu watu wangu waondoke, nitatuma makundi ya inzi juu yako na maafisa wako, juu ya watu wako, na ndani ya nyumba zenu. Nyumba za Wamisri zitajaa inzi; hata ardhi itafunikwa na inzi. \p \v 22 “ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwa na makundi ya inzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, Mwenyezi Mungu, niko katika nchi hii. \v 23 Nitaweka tofauti kati ya watu wangu na watu wenu. Ishara hii ya ajabu itatokea kesho.’ ” \p \v 24 Naye Mwenyezi Mungu akafanya hivyo. Makundi makubwa ya inzi walimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na inzi. \p \v 25 Ndipo Farao akamwita Musa na Haruni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.” \p \v 26 Lakini Musa akamwambia, “Hilo halitakuwa sawa. Dhabihu tutakazomtolea Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, zitakuwa chukizo kwa Wamisri. Tukitoa dhabihu ambazo ni chukizo mbele yao, je, hawatatupiga mawe? \v 27 Ni lazima twende mwendo wa siku tatu hadi tufike jangwani ili tumtolee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, dhabihu, kama alivyotuagiza.” \p \v 28 Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.” \p \v 29 Musa akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba Mwenyezi Mungu na kesho inzi wataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake, na kwa watu wake. Ila hakikisha kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu.” \p \v 30 Ndipo Musa akamwacha Farao na kumwomba Mwenyezi Mungu, \v 31 naye Mwenyezi Mungu akafanya lile Musa alilomwomba. Inzi wakaondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake, wala hakuna hata inzi aliyebakia. \v 32 Lakini wakati huu pia Farao akaufanya moyo wake kuwa mgumu, wala hakuwaruhusu Waisraeli waondoke. \c 9 \s1 Pigo la tano: Vifo vya mifugo \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” \v 2 Usipowaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, \v 3 mkono wa Mwenyezi Mungu utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ng’ombe wako, kondoo na mbuzi. \v 4 Lakini Mwenyezi Mungu ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ” \p \v 5 Mwenyezi Mungu akaweka wakati na kusema, “Kesho Mwenyezi Mungu atalitenda hili katika nchi.” \v 6 Siku iliyofuata Mwenyezi Mungu akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. \v 7 Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende. \s1 Pigo la sita: Majipu \p \v 8 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa na Haruni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Musa ayarushe angani mbele ya Farao. \v 9 Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura kwenye miili ya watu na ya wanyama katika nchi yote.” \p \v 10 Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Musa akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea kwenye miili ya watu na ya wanyama. \v 11 Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya majipu yaliyokuwa kwenye miili yao, na kwenye miili ya Wamisri wote. \v 12 Lakini Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Musa na Haruni, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwambia Musa. \s1 Pigo la saba: Mvua ya mawe \p \v 13 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Amka asubuhi na mapema, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili waweze kuniabudu, \v 14 au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama mimi duniani kote. \v 15 Kwa kuwa hadi sasa ningekuwa nimenyoosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi. \v 16 Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nikuoneshe uwezo wangu, na jina langu litangazwe duniani kote. \v 17 Bado unaendelea kujiinua dhidi ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende. \v 18 Hivyo basi, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa hadi leo. \v 19 Sasa toa amri mifugo yako na kila kitu ulicho nacho shambani, kipelekwe mahali pa usalama. Kwa sababu mvua ya mawe itamwangukia kila mtu na mnyama ambaye hajaletwa ndani, na ambaye bado yuko nje shambani; nao watakufa.’ ” \p \v 20 Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la Mwenyezi Mungu wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani. \v 21 Lakini wale waliopuuza neno la Mwenyezi Mungu wakawaacha watumwa wao na mifugo yao shambani. \p \v 22 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili mvua ya mawe inyeshe Misri yote: juu ya watu, wanyama, na juu ya kila kitu kinachoota katika mashamba ya Misri.” \v 23 Musa alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, Mwenyezi Mungu akatuma ngurumo na mvua ya mawe; mwanga wa radi ukamulika hadi nchi. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akanyesha mvua ya mawe juu ya nchi ya Misri; \v 24 mvua ya mawe ikanyesha, na radi ikamulika pote. Ikawa dhoruba ya kutisha zaidi, ambayo haijawahi kutokea katika Misri tangu nchi hiyo iwe taifa. \v 25 Mvua ya mawe ikaharibu kila kitu katika nchi ya Misri kilichokuwa katika mashamba: watu na wanyama; ikaharibu kila kitu kilichoota mashambani na kung’oa kila mti. \v 26 Mahali pekee ambapo mvua ya mawe haikunyesha ni nchi ya Gosheni, ambako Waisraeli waliishi. \p \v 27 Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, “Wakati huu nimetenda dhambi. Mwenyezi Mungu ni mwenye haki, mimi na watu wangu ni wakosaji. \v 28 Mwombeni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kutosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.” \p \v 29 Musa akamjibu, “Nitakapokuwa nimetoka nje ya mji, nitanyoosha mikono yangu juu kumwomba Mwenyezi Mungu. Ngurumo zitakoma na hapatakuwa mvua ya mawe tena, ili upate kujua kuwa nchi ni mali ya Mwenyezi Mungu. \v 30 Lakini ninajua kuwa wewe na maafisa wako bado hammwogopi Bwana Mwenyezi Mungu.” \p \v 31 (Kitani na shayiri viliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa na masuke, na kitani ilikuwa imechanua maua. \v 32 Hata hivyo, ngano na kusemethi hazikuharibiwa kwa sababu zilikuwa hazijakomaa.) \p \v 33 Kisha Musa akaondoka kwa Farao, akaenda nje ya mji. Musa akanyoosha mikono yake kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, ngurumo na mvua ya mawe vikakoma, mvua haikuendelea tena kunyesha nchini. \v 34 Farao alipoona kwamba mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akafanya dhambi tena. Yeye na maafisa wake wakafanya mioyo yao kuwa migumu. \v 35 Kwa hiyo, moyo wa Farao ukawa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waende, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema kupitia Musa. \c 10 \s1 Pigo la nane: Nzige \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na mioyo ya maafisa wake ili nipate kutenda ishara hizi zangu za ajabu miongoni mwao, \v 2 ili upate kuwaeleza watoto wako na wajukuu wako jinsi nilivyowatendea Wamisri kwa ukali, na jinsi nilivyofanya ishara zangu miongoni mwao, nanyi mpate kujua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” \p \v 3 Kwa hiyo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili waniabudu. \v 4 Ukikataa kuwaachia waende, kesho nitaleta nzige katika nchi yako. \v 5 Nao watafunika uso wa ardhi hata usionekane. Watatafuna mabaki machache yaliyobakizwa baada ya ile mvua ya mawe, yaani pamoja na kila mti unaoota katika mashamba yenu. \v 6 Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii hadi leo.’ ” Ndipo Musa akageuka na kumwacha Farao. \p \v 7 Maafisa wa Farao wakamwambia, “Hadi lini huyu mtu atakuwa tanzi kwetu? Waachie hao watu waende zao, ili wapate kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Je, bado hutambui kuwa Misri imeangamia?” \p \v 8 Ndipo Musa na Haruni wakaletwa kwa Farao. Farao akawaambia, “Nendeni, mkamwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Lakini ni nani hasa watakaoenda?” \p \v 9 Musa akajibu, “Tutaenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na mbuzi, kondoo, na ng’ombe wetu kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa Mwenyezi Mungu.” \p \v 10 Farao akasema, “Kama kweli nitawaruhusu mwondoke pamoja na wanawake wenu na watoto wenu, Mwenyezi Mungu awe pamoja nanyi! Ni wazi kwamba mna makusudi mabaya. \v 11 La hasha! Wanaume peke yao na waende, wakamwabudu Mwenyezi Mungu, kwa kuwa hilo ndilo mmekuwa mkiomba.” Kwa hiyo Musa na Haruni wakaondolewa mbele ya Farao. \p \v 12 Basi Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako juu ya Misri, ili kundi la nzige liweze kuvamia nchi na kutafuna kila kitu kinachoota katika mashamba na kila kitu kilichosazwa na ile mvua ya mawe.” \p \v 13 Kwa hiyo Musa akanyoosha fimbo yake juu ya Misri, Mwenyezi Mungu akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige. \v 14 Wakaivamia Misri yote na kukaa katika kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe halijapata kutokea pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwa tena. \v 15 Wakafunika ardhi yote hata ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kila kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe: kila kitu kilichoota shambani, pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu chochote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri. \p \v 16 Farao akawaita Musa na Haruni kwa haraka na kuwaambia, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na dhidi yenu pia. \v 17 Sasa unisamehe dhambi yangu mara moja tena na umwombe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aondoe pigo hili baya kwangu.” \p \v 18 Kisha Musa akaondoka kwa Farao akamwomba Mwenyezi Mungu. \v 19 Naye Mwenyezi Mungu akaugeuza upepo kuwa upepo mkali sana kutoka magharibi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki popote katika nchi ya Misri. \v 20 Lakini Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke. \s1 Pigo la tisa: Giza \p \v 21 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.” \v 22 Kwa hiyo Musa akaunyoosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. \v 23 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo waliyokuwa wanaishi. \p \v 24 Ndipo Farao akamwita Musa na kusema, “Nendeni, mkamwabudu Mwenyezi Mungu. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ng’ombe wenu waacheni.” \p \v 25 Lakini Musa akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu, na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. \v 26 Sisi ni lazima tuondoke na mifugo yetu pia, wala hakuna ukwato utakaoachwa nyuma. Inatupasa kutumia baadhi ya hiyo mifugo katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa kuwa hadi tutakapofika huko, hatutakuwa tumefahamu ni nini tutakachotumia katika kumwabudu Mwenyezi Mungu.” \p \v 27 Lakini Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hakuwa radhi kuwaachia waondoke. \v 28 Farao akamwambia Musa, “Ondoka mbele yangu! Hakikisha kuwa hutakuja mbele yangu tena! Siku ile utakapouona uso wangu utakufa.” \p \v 29 Musa akamjibu, “Iwe kama ulivyosema! Kamwe sitauona uso wako tena.” \c 11 \s1 Pigo la kumi: Kuuawa wazaliwa wa kwanza \p \v 1 Basi Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa. \v 2 Waambie watu wote kwamba kila mwanaume na kila mwanamke amwombe jirani yake vitu vya fedha na vya dhahabu.” \v 3 (Mwenyezi Mungu akawafanya Wamisri wawe na moyo wa ukarimu kwa Waisraeli, naye Musa mwenyewe akaheshimiwa sana na maafisa wa Farao na watu wote katika nchi ya Misri.) \p \v 4 Kwa hiyo Musa akasema, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Usiku wa manane, Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri. \v 5 Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, anayeketi kwenye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mjakazi, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo. \v 6 Kutakuwa na kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio ambacho hakijakuwa, wala kamwe hakitakuwa tena. \v 7 Lakini miongoni mwa Waisraeli hakuna hata mbwa atakayembwekea mwanadamu wala mnyama yeyote.’ Ndipo mtajua kuwa Mwenyezi Mungu huweka tofauti kati ya Misri na Israeli. \v 8 Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Musa, akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao. \p \v 9 Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa, “Farao atakataa kukusikiliza, ili maajabu yangu yapate kuongezeka katika nchi ya Misri.” \v 10 Musa na Haruni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakini Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake. \c 12 \s1 Pasaka na pigo la mwisho \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa na Haruni katika nchi ya Misri, \v 2 “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu. \v 3 Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya jamaa yake, mmoja kwa kila nyumba. \v 4 Ikiwa nyumba yoyote ina watu wachache wasioweza kumaliza huyo mwana-kondoo mzima, nyumba hiyo itabidi ishirikiane na nyumba ya jirani wa karibu, baada ya kuzingatia idadi ya watu waliomo. Mtaangalia ni kiasi gani cha nyama kitahitajika kulingana na mahitaji ya kila mtu. \v 5 Wanyama mtakaowachagua, lazima wawe wa kiume wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari, mwaweza kuwachukua kati ya kondoo au mbuzi. \v 6 Tunzeni wanyama hao hadi siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni. \v 7 Ndipo watakapochukua sehemu ya hiyo damu na kuipaka kwenye vizingiti vya juu, na miimo ya milango ya nyumba ambamo watakula wana-kondoo hao. \v 8 Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu. \v 9 Msile nyama mbichi wala iliyochemshwa, lakini iwe imeokwa kwenye moto, kichwa, miguu na nyama zake za ndani. \v 10 Msibakize nyama yoyote hadi asubuhi; nazo kama zitabakia hadi asubuhi, lazima mziteketeze kwa moto. \v 11 Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka\f + \fr 12:11 \fr*\ft Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.\ft*\f* ya Mwenyezi Mungu. \p \v 12 “Usiku huo huo nitapita katika nchi yote ya Misri na kumuua kila mzaliwa wa kwanza, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitaihukumu miungu yote ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. \v 13 Damu itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonesha nyumba ambazo mtakuwamo; nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri. \p \v 14 “Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu, mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa Mwenyezi Mungu, katika vizazi vyenu vyote: mtalishika kuwa agizo la kudumu. \v 15 Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. Katika siku ya kwanza mtaondoa chachu yote ndani ya nyumba zenu, kwa maana yeyote atakayekula chochote chenye chachu kuanzia siku ya kwanza hadi ya saba lazima akatiliwe mbali kutoka Israeli. \v 16 Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, na kusanyiko jingine katika siku ya saba. Katika siku hizo msifanye kazi kamwe isipokuwa kutayarisha chakula cha kila mmoja; hilo ndilo tu mtakalofanya. \p \v 17 “Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa agizo la kudumu. \v 18 Katika mwezi wa kwanza mtakula mikate isiyotiwa chachu, kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne hadi jioni ya siku ya ishirini na moja. \v 19 Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yoyote katika nyumba zenu. Yeyote alaye chochote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa. \v 20 Msile chochote kilichotiwa chachu. Popote mnapoishi, ni lazima mle mikate isiyotiwa chachu.” \p \v 21 Ndipo Musa akawaita wazee wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni mara moja mkachague wanyama kwa ajili ya jamaa zenu, mkachinje mwana-kondoo wa Pasaka. \v 22 Chukueni kitawi cha hisopo, mkichovye kwenye damu iliyopo kwenye sinia, na kuipaka sehemu ya hiyo damu kwenye vizingiti, na kwenye miimo yote miwili ya milango. Mtu yeyote asitoke nje ya mlango wa nyumba yake hadi asubuhi. \v 23 Mwenyezi Mungu apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi. \p \v 24 “Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu. \v 25 Mtakapoingia katika nchi Mwenyezi Mungu atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii. \v 26 Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ \v 27 Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri, na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo Waisraeli walisujudu na kuabudu. \v 28 Waisraeli wakafanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa na Haruni. \p \v 29 Ilipofika usiku wa manane, Mwenyezi Mungu akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia. \v 30 Farao, na maafisa wake wote, na Wamisri wote wakaamka usiku, na kulikuwa na kilio kikubwa katika nchi ya Misri, kwa kuwa hapakuwa nyumba hata moja ambayo hakufa mtu. \s1 Kutoka \p \v 31 Wakati huo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni kwa watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu Mwenyezi Mungu kama mlivyoomba. \v 32 Chukueni makundi yenu ya kondoo na mbuzi pamoja na ng’ombe, kama mlivyosema, nanyi mwende zenu. Nanyi pia mnibariki.” \p \v 33 Wamisri wakawahimiza Waisraeli waondoke kwa haraka na kuacha nchi yao. Kwa kuwa walisema, “La sivyo, tutakufa wote!” \v 34 Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika mavazi na kuyabeba mabegani mwao. \v 35 Waisraeli wakafanya kama Musa alivyowaelekeza, nao wakawaomba Wamisri wawapatie vitu vya fedha, dhahabu na mavazi. \v 36 Basi Mwenyezi Mungu alikuwa amewafanya Wamisri kuwa wakarimu kwa hawa watu, wakawapatia Waisraeli vile walivyotaka kwao; kwa hiyo wakawateka nyara Wamisri. \p \v 37 Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesesi hadi Sukothi. Walikuwa wanaume wapatao elfu mia sita waliotembea kwa miguu, bila kuhesabu wanawake na watoto. \v 38 Watu wengine wengi wakafuatana nao, pamoja na makundi makubwa ya mifugo, wakiwemo kondoo, mbuzi na ng’ombe. \v 39 Wakatengeneza maandazi yasiyotiwa chachu kwa ule unga uliokandwa waliokuwa wameutoa Misri, donge hilo la unga halikuwa limetiwa chachu, kwa kuwa walikuwa wameondolewa Misri kwa haraka nao hawakuwa na muda wa kujiandalia chakula. \p \v 40 Waisraeli waliishi Misri kwa muda wa miaka mia nne na thelathini (430). \v 41 Siku ya mwisho ya hiyo miaka mia nne na thelathini (430), vikosi vyote vya Mwenyezi Mungu viliondoka Misri. \v 42 Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, basi Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha usiku huu kwa kukesha ili kumheshimu Mwenyezi Mungu katika vizazi vijavyo. \s1 Masharti kwa ajili ya Pasaka \p \v 43 Mwenyezi Mungu akawaambia Musa na Haruni, “Haya ndio masharti kwa ajili ya Pasaka: \p “Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka. \v 44 Mtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri, \v 45 lakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula. \p \v 46 “Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote. \v 47 Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo. \p \v 48 “Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Mwenyezi Mungu ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila. \v 49 Sheria hiyo hiyo itamuhusu mzawa na mgeni anayeishi miongoni mwenu.” \p \v 50 Waisraeli wote walifanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa na Haruni. \v 51 Siku ile ile Mwenyezi Mungu akawatoa Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao. \c 13 \s1 Kuwekwa wakfu kwa wazaliwa wa kwanza \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua mimba miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.” \p \v 3 Ndipo Musa akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu. \v 4 Leo, katika mwezi wa Abibu\f + \fr 13:4 \fr*\ft mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiyahudi\ft*\f*, mnatoka. \v 5 Mwenyezi Mungu atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi inayotiririka maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu: \v 6 Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Mwenyezi Mungu sikukuu. \v 7 Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako. \v 8 Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Mwenyezi Mungu alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ \v 9 Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Mwenyezi Mungu inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. \v 10 Ni lazima ulishike agizo hili kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka. \p \v 11 “Baada ya Mwenyezi Mungu kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako, \v 12 inakupasa kumtolea Mwenyezi Mungu kila mzaliwa wa kwanza. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Mwenyezi Mungu. \v 13 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hutamkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa. \p \v 14 “Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu Mwenyezi Mungu alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. \v 15 Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, Mwenyezi Mungu aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila tumbo, na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’ \v 16 Jambo hili litakuwa kama ishara kwenye mkono wako na kama alama kwenye paji la uso wako, kwamba Mwenyezi Mungu alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.” \s1 Nguzo ya wingu na moto \p \v 17 Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.” \v 18 Kwa hiyo Mungu akawaongoza watu kupitia njia ya kuzunguka kupitia jangwani, kuelekea Bahari ya Shamu. Waisraeli walipanda kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiandaa kwa vita. \p \v 19 Musa akachukua mifupa ya Yusufu kwa sababu Yusufu alikuwa amewaapisha wana wa Israeli. Alikuwa amewaambia, “Hakika Mungu atakuja kuwasaidia, nanyi ni lazima mwichukue mifupa yangu mwende nayo kutoka mahali hapa.” \p \v 20 Baada ya Waisraeli kuondoka Sukothi wakapiga kambi huko Ethamu pembeni mwa jangwa. \v 21 Wakati wa mchana Mwenyezi Mungu aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku. \v 22 Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu. \c 14 \s1 Kuvuka Bahari ya Shamu \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waambie Waisraeli wageuke nyuma na wapige kambi karibu na Pi-Hahirothi, kati ya Migdoli na bahari. Watapiga kambi kando ya bahari, mkabala na Baal-Sefoni. \v 3 Farao atafikiri kwamba, ‘Hao Waisraeli wanatangatanga katika nchi kwa kuchanganyikiwa, nalo jangwa limewafungia.’ \v 4 Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo. \p \v 5 Mfalme wa Misri alipoambiwa kuwa Waisraeli wamekimbia, Farao na maafisa wake wakabadili nia zao kuhusu Waisraeli, wakasema, “Tumefanya nini? Tumewaachia Waisraeli waende zao na tumeukosa utumishi wao!” \v 6 Kwa hiyo akaandaliwa gari lake la vita, naye akaenda pamoja na jeshi lake. \v 7 Akachukua magari ya vita mia sita bora, pamoja na magari ya vita mengine yote ya Misri, pamoja na maafisa wa magari hayo yote. \v 8 Mwenyezi Mungu akaufanya moyo wa Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri. \v 9 Nao Wamisri, yaani farasi wote wa Farao na magari ya vita, wapanda farasi na vikosi vya askari, wakawafuatia Waisraeli, wakawakuta karibu na Pi-Hahirothi, mkabala na Baal-Sefoni walipokuwa wamepiga kambi kando ya bahari. \p \v 10 Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia Mwenyezi Mungu. \v 11 Wakamwambia Musa, “Je, ni kwamba hakukuwa na makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani? Umetufanyia nini kututoa Misri? \v 12 Hatukukuambia tulipokuwa huko Misri, ‘Tuache tuwatumikie Wamisri’? Ingekuwa vyema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!” \p \v 13 Musa akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu Mwenyezi Mungu atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. \v 14 Mwenyezi Mungu atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu.” \p \v 15 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele. \v 16 Inua fimbo yako na unyooshe mkono wako juu ya bahari ili kuyagawa maji, ili Waisraeli wapate kupita mahali pakavu baharini. \v 17 Nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu kusudi waingie baharini wakiwafuatia. Nami nitajipatia utukufu kupitia Farao pamoja na jeshi lake lote, kupitia magari yake ya vita na wapanda farasi wake. \v 18 Nao Wamisri watajua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu nitakapojipatia utukufu kupitia Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake.” \p \v 19 Ndipo malaika wa Mungu, aliyekuwa akisafiri mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akakaa nyuma yao. Pia ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao na kusimama nyuma, \v 20 ikakaa kati ya majeshi ya Misri na Israeli. Usiku kucha wingu likaleta giza upande mmoja na nuru kwa upande mwingine, kwa hiyo hakuna aliyemkaribia mwenzake usiku kucha. \p \v 21 Ndipo Musa akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye Mwenyezi Mungu akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika, \v 22 nao Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, maji yakiwa ukuta upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto. \p \v 23 Wamisri wakawafuatia ndani ya bahari, pamoja na farasi wote wa Farao, magari ya vita na wapanda farasi. \v 24 Kukaribia mapambazuko, Mwenyezi Mungu akaliangalia jeshi la Wamisri kutoka ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha. \v 25 Mungu akayaondoa magurudumu ya magari yao ya vita, kwa hivyo wakayaendesha kwa shida. Nao Wamisri wakasema, “Tuachane na Waisraeli! Mwenyezi Mungu anawapigania dhidi ya Misri.” \s1 Wafuatiaji wazama \p \v 26 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudi yawafunike Wamisri, magari yao ya vita, na wapanda farasi wao.” \v 27 Musa akanyoosha mkono wake juu ya bahari, kulipopambazuka bahari ikarudi mahali pake. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini Mwenyezi Mungu akawasukumia ndani ya bahari. \v 28 Maji yakarudiana na kuyafunika magari ya vita na wapanda farasi pamoja na jeshi lote la Farao lililokuwa limewafuata Waisraeli ndani ya bahari. Hakuna hata mmoja wao aliyenusurika. \p \v 29 Lakini Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, ukiwepo ukuta wa maji upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto. \v 30 Siku ile Mwenyezi Mungu akawaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wamisri, nao Waisraeli wakawaona Wamisri wamelala ufuoni mwa bahari wakiwa wamekufa. \v 31 Basi Waisraeli walipoona uwezo mkubwa Mwenyezi Mungu aliodhihirisha dhidi ya Wamisri, watu wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakaweka tumaini lao kwake na kwa Musa mtumishi wake. \c 15 \s1 Wimbo wa Musa na Miriamu \p \v 1 Ndipo Musa na Waisraeli wakamwimbia Mwenyezi Mungu wimbo huu: \q1 “Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, \q2 kwa kuwa ametukuzwa sana. \q1 Farasi na mpanda farasi \q2 amewatosa baharini. \b \q1 \v 2 “Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na wimbo wangu; \q2 amekuwa wokovu wangu. \q1 Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, \q2 Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. \q1 \v 3 Mwenyezi Mungu ni shujaa wa vita; \q2 Mwenyezi Mungu ndilo jina lake. \q1 \v 4 Magari ya vita ya Farao na jeshi lake \q2 amewatosa baharini. \q1 Maafisa wa Farao walio bora sana \q2 wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. \q1 \v 5 Maji yenye kina yamewafunika, \q2 wamezama vilindini kama jiwe. \q1 \v 6 Mkono wako wa kuume, Ee Mwenyezi Mungu \q2 ulitukuka kwa uweza. \q1 Mkono wako wa kuume, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 ukamponda adui. \b \q1 \v 7 “Katika ukuu wa utukufu wako, \q2 ukawaangusha chini wale waliokupinga. \q1 Uliachia hasira yako kali, \q2 ikawateketeza kama kapi. \q1 \v 8 Kwa pumzi ya pua yako \q2 maji yalijilundika. \q1 Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta, \q2 vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. \q1 \v 9 Adui alijivuna, \q2 ‘Nitawafuatia, nitawapata. \q1 Nitagawanya nyara; \q2 nitajishibisha kwao. \q1 Nitafuta upanga wangu \q2 na mkono wangu utawaangamiza.’ \q1 \v 10 Lakini ulipuliza kwa pumzi yako, \q2 bahari ikawafunika. \q1 Wakazama kama risasi \q2 kwenye maji makuu. \q1 \v 11 Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu? \q1 Ni nani kama Wewe: \q2 uliyetukuka katika utakatifu, \q1 utishaye katika utukufu, \q2 ukitenda maajabu? \b \q1 \v 12 “Uliunyoosha mkono wako wa kuume \q2 na nchi ikawameza. \q1 \v 13 Katika upendo wako usiokoma utawaongoza \q2 watu uliowakomboa. \q1 Katika nguvu zako utawaongoza \q2 hadi makao yako matakatifu. \q1 \v 14 Mataifa watasikia na kutetemeka, \q2 uchungu utawakamata Wafilisti. \q1 \v 15 Wakuu wa Edomu wataogopa, \q2 viongozi wa Moabu watatetemeka kwa hofu, \q1 Wakanaani watayeyuka, \q2 \v 16 vitisho na hofu vitawaangukia. \q1 Kwa nguvu ya mkono wako \q2 watatulia kama jiwe, \q1 hadi watu wako wapite, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 hadi watu uliowanunua wapite. \q1 \v 17 Utawaingiza na kuwapandikiza \q2 juu ya mlima wa urithi wako: \q1 hapo mahali, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 ulipopafanya kuwa makao yako, \q1 mahali patakatifu, Ee Mwenyezi Mungu, \q2 ulipopajenga kwa mikono yako. \b \q1 \v 18 “Mwenyezi Mungu atatawala \q2 milele na milele.” \p \v 19 Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, Mwenyezi Mungu aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini Waisraeli walipita baharini mahali pakavu. \v 20 Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Haruni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. \v 21 Miriamu akawaimbia: \q1 “Mwimbieni Mwenyezi Mungu, \q2 kwa maana ametukuka sana. \q1 Farasi na mpanda farasi \q2 amewatosa baharini.” \s1 Maji ya Mara na Elimu \p \v 22 Kisha Musa akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. \v 23 Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara\f + \fr 15:23 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Chungu\fqa*\f*.) \v 24 Kwa hiyo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, “Tunywe nini?” \p \v 25 Ndipo Musa akamlilia Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu akamwonesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. \p Huko Mwenyezi Mungu akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. \v 26 Mungu akasema, “Mkisikiliza kwa makini sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuyafanya yaliyo mema machoni pake, na mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, niwaponyaye.” \p \v 27 Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji. \c 16 \s1 Mana na kware \p \v 1 Jumuiya yote ya Waisraeli wakaondoka Elimu, wakafika Jangwa la Sini, lililokuwa kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka Misri. \v 2 Huko jangwani, jumuiya yote wakawanung’unikia Musa na Haruni. \v 3 Waisraeli wakawaambia, “Laiti tungekufa kwa mkono wa Mwenyezi Mungu huko Misri! Huko tuliketi tukizunguka masufuria ya nyama na tukala vyakula tulivyovitaka, lakini ninyi mmetuleta huku jangwani ili mpate kuua mkutano huu wote kwa njaa.” \p \v 4 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Tazama! Nitawanyeshea mikate kutoka mbinguni. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. \v 5 Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku.” \p \v 6 Kwa hiyo Musa na Haruni wakawaambia Waisraeli wote, “Jioni mtajua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliwatoa Misri, \v 7 kisha asubuhi mtauona utukufu wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu amesikia manung’uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani hata mtunung’unikie?” \v 8 Kisha Musa akasema, “Mtajua kuwa alikuwa Mwenyezi Mungu wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manung’uniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnung’uniki dhidi yetu, bali dhidi ya Mwenyezi Mungu.” \p \v 9 Kisha Musa akamwambia Haruni, “Iambie jumuiya yote ya Waisraeli kwamba, ‘Mje mbele zake Mwenyezi Mungu, kwa maana amesikia manung’uniko yenu.’ ” \p \v 10 Haruni alipokuwa akizungumza na jumuiya yote ya Waisraeli, wakatazama kuelekea jangwani, na huko wakaona utukufu wa Mwenyezi Mungu ukitokeza katika wingu. \p \v 11 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 12 “Nimesikia manung’uniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ” \p \v 13 Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na utando wa umande kuzunguka kambi. \v 14 Umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya mchanga wa jangwa. \v 15 Waisraeli walipoona, wakaambiana, “Hiki ni nini?” Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani. \p Musa akawaambia, “Huu ndio mkate ambao Mwenyezi Mungu amewapa mle. \v 16 Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu ameamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi\f + \fr 16:16 \fr*\ft yaani omeri moja, sawa na kilo mbili\ft*\f* moja kwa kila mtu mliye naye katika hema lenu.’ ” \p \v 17 Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa; baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. \v 18 Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji. \p \v 19 Kisha Musa akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote hadi asubuhi.” \p \v 20 Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Musa, wakahifadhi kiasi fulani hadi asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Musa akawakasirikia. \p \v 21 Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka. \v 22 Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Musa. \v 23 Musa akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza Mwenyezi Mungu: ‘Kesho itakuwa Sabato ya mapumziko, Sabato takatifu kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke hadi asubuhi.’ ” \p \v 24 Kwa hiyo wakavihifadhi hadi asubuhi, kama Musa alivyoagiza, na havikunuka wala kuwa na mabuu. \v 25 Musa akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. \v 26 Kwa siku sita mtakusanya, lakini siku ya saba, yaani Sabato, hakutakuwa chochote.” \p \v 27 Hata hivyo, baadhi ya watu wakatoka kwenda kukusanya siku ya saba, lakini hawakupata chochote. \v 28 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu hadi lini? \v 29 Fahamuni kuwa Mwenyezi Mungu amewapa ninyi Sabato, ndiyo sababu katika siku ya sita amewapa mikate ya siku mbili. Kila mmoja inampasa kukaa pale alipo katika siku ya saba. Hata mmoja haruhusiwi kutoka.” \v 30 Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba. \p \v 31 Waisraeli wakaita ile mikate mana\f + \fr 16:31 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa mkate kutoka mbinguni\fqa*\f*. Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama, na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. \v 32 Musa akasema, “Hivi ndivyo alivyoagiza Mwenyezi Mungu: ‘Chukueni pishi ya mana na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo ili vione mikate niliyowapa mle jangwani nilipowatoa katika nchi ya Misri.’ ” \p \v 33 Kwa hiyo Musa akamwambia Haruni, “Chukua gudulia na uweke pishi moja ya mana ndani yake. Kisha uweke mbele za Mwenyezi Mungu ili kihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.” \p \v 34 Kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa, hatimaye Haruni aliiweka ile mana ndani ya Sanduku la Ushuhuda ili aweze kuihifadhi. \v 35 Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu; walikula mana hadi walipofika mpakani mwa Kanaani. \p \v 36 (Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa\f + \fr 16:36 \fr*\ft Efa moja ni sawa na kilo 22.\ft*\f*.) \c 17 \s1 Maji kutoka mwamba \r (Hesabu 20:1-13) \p \v 1 Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Mwenyezi Mungu alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. \v 2 Kwa hiyo wakagombana na Musa wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” \p Musa akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu Mwenyezi Mungu?” \p \v 3 Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanung’unika dhidi ya Musa, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?” \p \v 4 Kisha Musa akamlilia Mwenyezi Mungu, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.” \p \v 5 Mwenyezi Mungu akamjibu Musa, “Nenda mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, na uchukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. \v 6 Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Musa akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. \v 7 Naye akapaita mahali pale Masa\f + \fr 17:7 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kujaribu\fqa*\f* na Meriba\f + \fr 17:7 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kugombana\fqa*\f*, kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Mwenyezi Mungu wakisema, “Je, Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi au la?” \s1 Vita na Waamaleki \p \v 8 Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu. \v 9 Musa akamwambia Yoshua, “Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu.” \p \v 10 Kwa hiyo Yoshua akapigana na Waamaleki kama Musa alivyomwagiza, nao Musa, Haruni na Huri wakapanda juu ya kilima. \v 11 Ikawa wakati wote Musa alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. \v 12 Mikono ya Musa ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Haruni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Musa, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti hadi jua lilipozama. \v 13 Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga. \p \v 14 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Andika mambo haya katika kitabu ili yakumbukwe, na uhakikishe kwamba Yoshua amesikia, kwa sababu nitafuta kabisa kumbukumbu la Amaleki chini ya mbingu.” \p \v 15 Musa akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi\f + \fr 17:15 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Mwenyezi Mungu ni Bendera yangu\fqa*\f*. \v 16 Musa akasema, “Kwa maana mikono iliinuliwa dhidi ya kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, sasa Mwenyezi Mungu atakuwa na vita dhidi ya Waamaleki kizazi hadi kizazi.” \c 18 \s1 Yethro amtembelea Musa \p \v 1 Basi Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wa Musa, akawa amesikia kila kitu Mungu alichomfanyia Musa na watu wake wa Israeli, pia jinsi Mwenyezi Mungu alivyowatoa Israeli Misri. \p \v 2 Baada ya Musa kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea \v 3 pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershomu, kwa kuwa Musa alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” \v 4 Mwingine aliitwa Eliezeri, kwa kuwa alisema, “Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa kutoka upanga wa Farao.” \p \v 5 Yethro, baba mkwe wa Musa, pamoja na wana wawili wa Musa na mkewe, wakamjia Musa huko jangwani, mahali alipokuwa amepiga kambi karibu na mlima wa Mungu. \v 6 Yethro alikuwa ametuma ujumbe kwake Musa, kusema, “Mimi Yethro baba mkwe wako ninakuja kwako pamoja na mke wako na wanao wawili.” \p \v 7 Kwa hiyo Musa akatoka kumlaki baba mkwe wake, akainama na kumbusu. Wakasalimiana, kisha wakaingia kwenye hema. \v 8 Musa akamwambia baba mkwe wake kuhusu kila kitu Mwenyezi Mungu alichomfanyia Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na pia kuhusu shida zote walizokutana nazo njiani, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaokoa. \p \v 9 Yethro akafurahishwa sana kusikia kuhusu mambo yote mazuri Mwenyezi Mungu aliyowatendea Waisraeli kuwaokoa kutoka mkono wa Wamisri. \v 10 Yethro akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri. \v 11 Sasa najua ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mkuu kuliko miungu mingine yote, kwa kuwa amewatendea hivi wale waliowatenda Israeli kwa ujeuri.” \v 12 Kisha Yethro, baba mkwe wa Musa, akaleta sadaka ya kuteketezwa na dhabihu nyingine kwa Mungu, naye Haruni pamoja na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula pamoja na baba mkwe wa Musa mbele za Mungu. \s1 Ushauri wa Yethro \r (Kumbukumbu 1:9-18) \p \v 13 Siku iliyofuata, Musa akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. \v 14 Baba mkwe wake alipoona yote Musa anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi hadi jioni?” \p \v 15 Musa akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. \v 16 Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake, na kuwaeleza hukumu na sheria zake Mungu.” \p \v 17 Baba mkwe wa Musa akamjibu, “Unachofanya sio kizuri. \v 18 Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe. \v 19 Sasa nisikilize mimi, nitakupa ushauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake. \v 20 Wafundishe hukumu na sheria zake, na uwaoneshe jinsi wanavyopaswa kuishi, na jinsi wanavyopaswa kuenenda. \v 21 Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. \v 22 Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe. \v 23 Ukifanya hivi, na ikiwa Mungu ameagiza hivyo, utaweza kushinda uchovu, nao watu hawa wote watarudi nyumbani wameridhika.” \s1 Kuchaguliwa kwa waamuzi \p \v 24 Musa akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. \v 25 Musa akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya wawe viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. \v 26 Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Musa, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe. \p \v 27 Kisha Musa akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake. \c 19 \s1 Waisraeli kwenye Mlima Sinai \p \v 1 Siku ya kwanza ya mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kuondoka Misri, walifika Jangwa la Sinai siku hiyo hiyo. \v 2 Baada ya kuondoka Refidimu, waliingia katika Jangwa la Sinai na Israeli wakapiga kambi pale jangwani mbele ya mlima. \p \v 3 Kisha Musa akakwea kwenda kwa Mungu, naye Mwenyezi Mungu akamwita kutoka ule mlima, akasema, “Hivi ndivyo utakavyosema na nyumba ya Yakobo na utakachowaambia Waisraeli: \v 4 ‘Ninyi wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mabawa ya tai na kuwaleta kwangu. \v 5 Sasa, mkinitii kikamilifu na kutunza agano langu, basi ninyi mtakuwa hazina yangu ya pekee miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, \v 6 ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndio maneno utakayosema kwa Waisraeli.” \p \v 7 Kwa hiyo Musa akarudi, akawaita wazee wa watu na kuwaambia maneno yote ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa amemwamuru ayaseme. \v 8 Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu Mwenyezi Mungu alichokisema.” Naye Musa akarudisha majibu yao kwa Mwenyezi Mungu. \p \v 9 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nitakujia katika wingu zito, ili watu wanisikie nikinena nawe na kila mara waweke tumaini lao kwako.” Kisha Musa akamwambia Mwenyezi Mungu yale ambayo watu walikuwa wamesema. \p \v 10 Naye Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu leo na kesho. Waambie wafue nguo zao \v 11 na wawe tayari siku ya tatu, kwa sababu siku hiyo, Mwenyezi Mungu atashuka juu ya Mlima Sinai machoni pa watu wote. \v 12 Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Yeyote atakayeugusa mlima atauawa. \v 13 Hakika atapigwa mawe au kupigwa mishale; mkono wa mtu hautamgusa. Akiwa mwanadamu au mnyama, hataruhusiwa kuishi.’ Ila tu wakati baragumu itakapopigwa kwa mfululizo, ndipo watu wote watakapopanda mlimani.” \p \v 14 Baada ya Musa kushuka kutoka mlimani akawaendea watu na kuwaweka wakfu, wakafua nguo zao. \v 15 Kisha akawaambia watu, “Jitayarisheni kwa ajili ya siku ya tatu. Mwanaume yeyote asimkaribie mwanamke.” \p \v 16 Asubuhi ya siku ya tatu kulikuwa na ngurumo na radi pamoja na wingu nene juu ya mlima na mlio mkubwa sana wa tarumbeta. Kila mmoja aliyekuwa kambini akatetemeka. \v 17 Kisha Musa akawaongoza watu kutoka kambini kukutana na Mungu, nao wakasimama chini ya mlima. \v 18 Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka tanuru kubwa, na mlima wote ukatetemeka kwa kishindo, \v 19 nayo sauti ya tarumbeta ikawa kubwa zaidi na zaidi. Kisha Musa akazungumza, nayo sauti ya Mungu ikamjibu. \p \v 20 Mwenyezi Mungu akashuka juu ya Mlima Sinai na akamwita Musa apande juu mlimani. Kwa hiyo Musa akapanda juu, \v 21 naye Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Shuka ukawaonye watu ili wasijipenyeze kutafuta kumwona Mwenyezi Mungu, na wengi wao wakaangamia. \v 22 Hata makuhani, watakaomkaribia Mwenyezi Mungu ni lazima wajiweke wakfu, la sivyo Mwenyezi Mungu atawaadhibu.” \p \v 23 Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Watu hawawezi kupanda Mlima Sinai kwa sababu wewe mwenyewe ulituonya ukisema, ‘Wekeni mipaka kuuzunguka mlima na kuutenga kama patakatifu.’ ” \p \v 24 Mwenyezi Mungu akajibu, “Shuka ukamlete Haruni pamoja nawe. Lakini makuhani pamoja na watu wasije wakalazimisha kuja kwa Mwenyezi Mungu, nisije nikawaadhibu.” \p \v 25 Basi Musa akashuka kwa watu na kuwaambia lile aliloambiwa. \c 20 \s1 Amri Kumi \r (Kumbukumbu 5:1-21) \p \v 1 Ndipo Mungu akasema maneno haya yote: \b \lh \v 2 “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. \b \li1 \v 3 “Usiwe na miungu mingine ila mimi. \li1 \v 4 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. \v 5 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanaonichukia, \v 6 lakini ninaonesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaonipenda na kuzishika amri zangu. \li1 \v 7 Usilitaje bure jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa kuwa Mwenyezi Mungu hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. \li1 \v 8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. \v 9 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, \v 10 lakini siku ya saba ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. \v 11 Kwa kuwa kwa siku sita, Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu. \li1 \v 12 Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \li1 \v 13 Usiue. \li1 \v 14 Usizini. \li1 \v 15 Usiibe. \li1 \v 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. \li1 \v 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.” \s1 Watu wanaogopa \r (Kumbukumbu 5:22-33) \p \v 18 Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali \v 19 na wakamwambia Musa, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.” \p \v 20 Musa akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili hofu ya Mungu iwe nanyi kuwasaidia msitende dhambi.” \p \v 21 Watu wakabaki mbali, wakati Musa alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa. \s1 Sanamu na madhabahu \p \v 22 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Waambie Waisraeli hivi: ‘Mmejionea wenyewe kwamba nimesema nanyi kutoka mbinguni: \v 23 Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu. \p \v 24 “ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo na mbuzi, na ng’ombe wako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki. \v 25 Ikiwa unanitengenezea madhabahu ya mawe, usiijenge kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia chombo cha kuchongea mtaitia unajisi. \v 26 Usitumie ngazi kupanda kwenye madhabahu yangu, uchi wako usije ukadhihirika kwa chini.’ \c 21 \s1 Sheria mbalimbali \p \v 1 “Hizi ndizo sheria utakazoweka mbele ya Waisraeli. \s2 Watumishi wa Kiebrania \r (Kumbukumbu 15:12-18) \p \v 2 “Ukimnunua mtumwa Mwebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye ataenda zake pasipo kulipa chochote. \v 3 Akija peke yake, ataenda huru peke yake, lakini akija na mke, ataondoka pamoja naye. \v 4 Ikiwa bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake, na huyo mwanaume ataondoka peke yake. \p \v 5 “Lakini mtumishi akisema, ‘Ninampenda bwana wangu, mke wangu pamoja na watoto na sitaki kuwa huru,’ \v 6 basi bwana wake atalazimika kumpeleka mbele ya waamuzi. Kisha atampeleka kwenye mlango, au kizingiti na kutoboa sikio lake kwa shazia. Naye atamtumikia bwana wake maisha yake yote. \p \v 7 “Mtu akimuuza binti yake kuwa mtumwa, hataachwa huru kama watumwa wa kiume wanavyoachiwa. \v 8 Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu. \v 9 Akimchagua aolewe na mwanawe, ni lazima ampe haki za kuwa binti yake. \v 10 Ikiwa huyo mwana aliyeozwa mtumwa mwanamke ataoa mwanamke mwingine, ni lazima aendelee kumtosheleza huyo mke wa kwanza kwa chakula, mavazi na haki zote za ndoa. \v 11 Iwapo hatamtosheleza kwa mambo hayo matatu, huyo mke wa kwanza ataondoka na kuwa huru bila malipo yoyote ya fedha. \s2 Majeraha ya mwilini \p \v 12 “Yeyote anayempiga mtu na kumuua ni lazima auawe. \v 13 Hata hivyo, kama hakumuua kwa makusudi, lakini Mungu akaruhusu itendeke, basi atakimbilia mahali nitakapomchagulia. \v 14 Lakini kama mtu akipanga na kumuua mwingine kwa makusudi, mwondoe katika madhabahu yangu na kumuua. \p \v 15 “Yeyote anayemshambulia baba yake au mama yake ni lazima auawe. \p \v 16 “Yeyote anayemteka nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe. \p \v 17 “Yeyote atakayemlaani baba yake au mama yake ni lazima auawe. \p \v 18 “Watu wakigombana, naye mmoja akampiga mwingine kwa jiwe au kwa ngumi yake na hakufa, bali akaugua na kulala kitandani, \v 19 yule aliyempiga ngumi hatahesabiwa kuwa na hatia ikiwa mwenzake ataamka na kujikongoja kwa fimbo yake, lakini hata hivyo, ni lazima amlipe fidia ya muda aliopoteza na awajibike hadi apone kabisa. \p \v 20 “Mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe \v 21 lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake. \p \v 22 “Watu wawili wakipigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. \v 23 Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, \v 24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, \v 25 kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko. \p \v 26 “Mtu akimpiga mtumwa wa kiume au wa kike kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho. \v 27 Akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino. \p \v 28 “Fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika. \v 29 Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe. \v 30 Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake. \v 31 Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. \v 32 Fahali akimpiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini\f + \fr 21:32 \fr*\ft Shekeli 30 ni sawa na gramu 300.\ft*\f* za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe. \p \v 33 “Mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ng’ombe au punda akatumbukia ndani yake, \v 34 mwenye shimo ni lazima alipe hasara iliyotokea; ni lazima amlipe mwenye mnyama. Mnyama aliyekufa atakuwa wake. \p \v 35 “Fahali wa mtu fulani akimuumiza fahali wa mtu mwingine na akafa, watamuuza yule aliye hai na wagawane sawa fedha pamoja na mnyama aliyekufa. \v 36 Hata hivyo, ikifahamika kwamba fahali huyo alikuwa na tabia ya kupiga kwa pembe na mwenyewe hakumfunga, ni lazima mwenye fahali alipe mnyama kwa mnyama, na mnyama aliyekufa atakuwa wake. \c 22 \s2 Ulinzi wa mali \p \v 1 “Mtu yeyote akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ng’ombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. \p \v 2 “Mwizi akishikwa akivunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya kumwaga damu; \v 3 lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu. \p “Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake. \p \v 4 “Mnyama aliyeibwa akikutwa hai mkononi mwake, iwe ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili. \p \v 5 “Mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia walishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu. \p \v 6 “Moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe. \p \v 7 “Mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, vitu vile vikiibwa kutoka nyumba ya huyo jirani, kama mwizi akishikwa, lazima alipe mara mbili. \v 8 Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake. \v 9 Pakiwepo jambo lolote la mali isiyo halali, iwe ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yoyote iliyopotea, ambayo mtu fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ kila upande utaleta shauri lake mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watathibitisha kuwa ana hatia atamlipa jirani yake mara mbili. \p \v 10 “Mtu akimpa jirani yake punda, ng’ombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, yule mnyama akifa, au akijeruhiwa, au akiibiwa bila mtu kuona, \v 11 jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa mbele za Mwenyezi Mungu, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika. \v 12 Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama. \v 13 Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa mnyama aliyeraruliwa. \p \v 14 “Mtu akiazima mnyama kutoka kwa jirani yake, huyo mnyama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama. \v 15 Lakini mwenye mnyama akiwa bado ako na mnyama wake, aliyeazima hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara. \s2 Uwajibikaji wa kijamii \p \v 16 “Mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akalala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo. \v 17 Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu binti yake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira. \p \v 18 “Usiruhusu mwanamke mchawi aishi. \p \v 19 “Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe. \p \v 20 “Mtu yeyote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Mwenyezi Mungu, lazima aangamizwe. \p \v 21 “Usimtendee mgeni vibaya au kumdhulumu, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri. \p \v 22 “Usimdhulumu mjane wala yatima. \v 23 Ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. \v 24 Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima. \p \v 25 “Ukimkopesha mmoja wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. \v 26 Ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, \v 27 kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma. \p \v 28 “Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako. \p \v 29 “Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako. \p “Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako. \v 30 Ufanye vivyo hivyo kwa ng’ombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe. \p \v 31 “Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa. \c 23 \s1 Sheria za haki na rehema \p \v 1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine. \p \v 2 “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, \v 3 nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. \p \v 4 “Ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. \v 5 Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia. \p \v 6 “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. \v 7 Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia. \p \v 8 “Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki. \p \v 9 “Usimdhulumu mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri. \s1 Sheria za Sabato \p \v 10 “Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, \v 11 lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni. \p \v 12 “Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kuburudishwa. \p \v 13 “Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako. \s1 Sikukuu tatu za mwaka \r (Kutoka 34:18-26; Kumbukumbu 16:1-17) \p \v 14 “Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu. \p \v 15 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu\f + \fr 23:15 \fr*\ft mwezi wa nne katika kalenda ya Kiyahudi\ft*\f*, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri. \p “Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu. \p \v 16 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako. \p “Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani. \p \v 17 “Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 18 “Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu chochote kilicho na chachu. \p “Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe hadi asubuhi. \p \v 19 “Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake. \s1 Malaika wa Mwenyezi Mungu kuandaa njia \p \v 20 “Tazama, ninamtuma malaika akutangulie mbele yako akulinde njiani na kukuleta mahali nilipoandaa. \v 21 Mtamtii na kusikiliza kile anachokisema. Usiasi dhidi yake; hatakusamehe uasi wako, kwa maana Jina langu limo ndani yake. \v 22 Ukizingatia atakachosema na kufanya yote ninayosema, nitakuwa adui wa adui zako, na nitawapinga wale wakupingao. \v 23 Malaika wangu atatangulia mbele yako na kukuleta katika nchi ya Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanaani, Wahivi na Wayebusi, nami nitawafutilia mbali. \v 24 Usiisujudie miungu yao, au kuiabudu, wala kufuata desturi yao. Utayabomoa kabisa na kuvunjavunja mawe yao ya ibada vipande vipande. \v 25 Utamwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na baraka zake zitakuwa juu ya vyakula vyako na maji yako. Nami nitaondoa maradhi miongoni mwako, \v 26 na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu. \p \v 27 “Nitapeleka utisho wangu mbele yako na kufadhaisha kila taifa utakalolifikia. Nitafanya adui zako wote wakupe kisogo na kukimbia. \v 28 Nitatanguliza nyigu mbele yako kuwafukuza Wahivi, Wakanaani na Wahiti waondoke njiani mwako. \v 29 Lakini sitawafukuza kwa mara moja, kwa sababu nchi itabaki ukiwa na wanyama pori watakuwa wengi mno kwako. \v 30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hadi uwe umeongezeka kiasi cha kutosha kuimiliki nchi. \p \v 31 “Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto\f + \fr 23:31 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f*. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako. \v 32 Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao. \v 33 Usiwaache waishi katika nchi yako, la sivyo watakusababisha utende dhambi dhidi yangu, kwa sababu ibada ya miungu yao hakika itakuwa mtego kwako.” \c 24 \s1 Agano lathibitishwa \p \v 1 Kisha Mungu akamwambia Musa, “Njooni huku juu kwa Mwenyezi Mungu, wewe na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, \v 2 lakini Musa peke yake ndiye atakayemkaribia Mwenyezi Mungu; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.” \p \v 3 Musa alipoenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Mwenyezi Mungu, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Mwenyezi Mungu tutakifanya.” \v 4 Ndipo Musa akaandika kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amesema. \p Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli. \v 5 Kisha akawatuma vijana wanaume Waisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa Mwenyezi Mungu. \v 6 Musa akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli, na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. \v 7 Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema Mwenyezi Mungu, nasi tutatii.” \p \v 8 Ndipo Musa akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo Mwenyezi Mungu amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.” \p \v 9 Musa na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani, \v 10 nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu. \v 11 Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa. \p \v 12 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.” \p \v 13 Basi Musa akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Musa akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. \v 14 Musa akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa hadi tutakapowarudia. Haruni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na shauri aweza kuwaendea wao.” \p \v 15 Musa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, \v 16 nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Mwenyezi Mungu akamwita Musa kutoka kati ya lile wingu. \v 17 Kwa Waisraeli utukufu wa Mwenyezi Mungu ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. \v 18 Kisha Musa akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana. \c 25 \s1 Sadaka kwa ajili ya maskani ya Mungu \r (Kutoka 35:4-9) \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. \b \lh \v 3 “Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: \b \li1 “dhahabu, fedha na shaba; \li1 \v 4 nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; \li1 singa za mbuzi; \li1 \v 5 ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo\f + \fr 25:5 \fr*\ft pengine ni mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili\ft*\f*; \li1 mbao za mshita; \li1 \v 6 mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; \li1 vikolezo kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; \li1 \v 7 na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kizibau na kile kifuko cha kifuani. \b \p \v 8 “Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. \v 9 Tengeneza Maskani\f + \fr 25:9 \fr*\ft hema takatifu lililoambatana na vitu vilivyotumika katika ibada za Kiyahudi kabla ya kujengwa kwa Hekalu la Sulemani\ft*\f* hii na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonesha. \s1 Sanduku la Agano \r (Kutoka 37:1-9) \p \v 10 “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu\f + \fr 25:10 \fr*\ft Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5.\ft*\f*, upana wa dhiraa moja na nusu\f + \fr 25:10 \fr*\ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.\ft*\f*, na kimo cha dhiraa moja na nusu. \v 11 Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. \v 12 Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. \v 13 Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. \v 14 Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. \v 15 Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa. \v 16 Kisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa. \p \v 17 “Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu. \v 18 Tengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. \v 19 Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. \v 20 Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. \v 21 Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. \v 22 Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walio juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli. \s1 Meza ya mikate ya Wonesho \r (Kutoka 37:10-16) \p \v 23 “Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili\f + \fr 25:23 \fr*\ft Dhiraa 2 ni sawa na sentimita 90.\ft*\f*, upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu. \v 24 Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. \v 25 Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda moja\f + \fr 25:25 \fr*\ft Nyanda moja ni sawa na sentimita 7.5.\ft*\f*, na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. \v 26 Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. \v 27 Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. \v 28 Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza. \v 29 Tengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka. \v 30 Utaweka mikate ya Wonesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima. \s1 Kinara cha taa \r (Kutoka 37:17-24) \p \v 31 “Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja. \v 32 Matawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. \v 33 Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa. \v 34 Juu ya kinara chenyewe vitakuwa vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi, yakiwa na matovu yake na maua yake. \v 35 Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla. \v 36 Matovu na matawi yote yatakuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakifuliwa kwa dhahabu safi. \p \v 37 “Kisha tengeneza taa zake saba na uziweke juu ya kinara hicho ili ziangaze mbele yake. \v 38 Mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote zitakuwa za dhahabu safi. \v 39 Utatumia talanta moja\f + \fr 25:39 \fr*\ft Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.\ft*\f* ya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na vifaa vyake vyote. \v 40 Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano uliooneshwa kule mlimani. \c 26 \s1 Maskani ya Mungu \r (Kutoka 36:8-38) \p \v 1 “Tengeneza maskani ya Mungu kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo. \v 2 Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane\f + \fr 26:2 \fr*\ft Dhiraa 28 ni sawa na mita 13.\ft*\f*, na upana wa dhiraa nne\f + \fr 26:2 \fr*\ft Dhiraa 4 ni sawa na mita 1.8.\ft*\f*. \v 3 Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. \v 4 Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. \v 5 Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, navyo vitanzi vyote vielekeane. \v 6 Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya maskani ya Mungu iwe kitu kimoja. \p \v 7 “Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika Maskani. \v 8 Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo sawa, yaani urefu wa dhiraa thelathini\f + \fr 26:8 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\ft*\f*, na upana wa dhiraa nne. \v 9 Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya Maskani. \v 10 Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. \v 11 Kisha tengeneza vifungo hamsini vya shaba, uviingize katika vile vitanzi ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. \v 12 Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia za hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaning’inizwa upande wa nyuma wa maskani ya Mungu. \v 13 Mapazia ya hema yatakuwa na urefu wa dhiraa moja zaidi pande zote, sehemu itakayobaki itaning’inia pande zote za Maskani ili kuifunika. \v 14 Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo\f + \fr 26:14 \fr*\ft pengine ni mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili\ft*\f*. \p \v 15 “Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani ya Mungu. \v 16 Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumi\f + \fr 26:16 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\ft*\f* na upana wa dhiraa moja na nusu, \v 17 zikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba kila mmoja na mwingine. Tengeneza mihimili yote ya Maskani jinsi hii. \v 18 Tengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa Maskani, \v 19 kisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. \v 20 Kuhusu upande wa kaskazini wa Maskani, tengeneza mihimili ishirini \v 21 na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \v 22 Kisha tengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa Maskani, \v 23 na pia utengeneze mihimili miwili ya pembe za upande ulio mbali. \v 24 Katika pembe hizi mbili ni lazima mihimili yake iwe miwili kuanzia chini hadi juu, na iingizwe kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili itafanana. \v 25 Kwa hiyo kutakuwa mihimili nane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \p \v 26 “Pia tengeneza mataruma ya mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa Maskani, \v 27 matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili ya mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa Maskani. \v 28 Taruma la katikati litapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. \v 29 Funika hiyo mihimili kwa dhahabu, kisha tengeneza pete za dhahabu ambazo zitashikilia hayo mataruma. Pia funika hayo mataruma kwa dhahabu. \p \v 30 “Simamisha maskani ya Mungu sawasawa na mfano uliooneshwa kule mlimani. \p \v 31 “Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia. \v 32 Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha. \v 33 Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu. \v 34 Weka kifuniko cha kiti cha rehema juu ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. \v 35 Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa maskani ya Mungu, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa maskani. \p \v 36 “Kwa ajili ya ingilio la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. \v 37 Tengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya hilo pazia, na nguzo tano za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kisha subu vitako vitano vya shaba kwa ajili yake. \c 27 \s1 Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa \r (Kutoka 38:1-7) \p \v 1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu\f + \fr 27:1 \fr*\ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\ft*\f*; itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano\f + \fr 27:1 \fr*\ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\ft*\f*, na upana wake dhiraa tano. \v 2 Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. \v 3 Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. \v 4 Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu. \v 5 Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. \v 6 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. \v 7 Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. \v 8 Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyooneshwa mlimani. \s1 Ua wa Hema la Kukutania \r (Kutoka 38:9-20) \p \v 9 “Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja\f + \fr 27:9 \fr*\ft Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.\ft*\f*, na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, \v 10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \v 11 Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \p \v 12 “Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini\f + \fr 27:12 \fr*\ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\ft*\f*, nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. \v 13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. \v 14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \v 15 Kutakuwa na mapazia ya dhiraa kumi na tano\f + \fr 27:15 \fr*\ft Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.\ft*\f* kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \p \v 16 “Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini\f + \fr 27:16 \fr*\ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\ft*\f* la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. \v 17 Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. \v 18 Ua utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. \v 19 Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani ya Mungu kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba. \s1 Mafuta ya kinara cha taa \r (Walawi 24:1-4) \p \v 20 “Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. \v 21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Haruni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni hadi asubuhi mbele za Mwenyezi Mungu. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vijavyo. \c 28 \s1 Mavazi ya kikuhani \r (Kutoka 39:1-7) \p \v 1 “Mtwae Haruni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. \v 2 Mshonee Haruni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima. \v 3 Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Haruni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani. \v 4 Haya ndio mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kizibau, kanzu, joho lililofumwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Haruni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. \v 5 Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi. \s1 Kizibau \p \v 6 “Tengeneza kizibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi. \v 7 Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kizibau. \v 8 Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kizibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri. \p \v 9 “Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli \v 10 kufuatana na walivyozaliwa: majina sita katika kito kimoja, na mengine sita katika kito kingine. \v 11 Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu, \v 12 na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kizibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Haruni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za Mwenyezi Mungu. \v 13 Tengeneza vijalizo vya dhahabu \v 14 na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo. \s1 Kifuko cha kifuani \r (Kutoka 39:8-21) \p \v 15 “Tengeneza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kizibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. \v 16 Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja\f + \fr 28:16 \fr*\ft Shibiri moja ni sawa na sentimita 22.\ft*\f* na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili. \v 17 Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; \v 18 katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; \v 19 safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; \v 20 na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. \v 21 Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili. \p \v 22 “Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. \v 23 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake, uzifungie kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. \v 24 Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete zilizo katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, \v 25 nazo zile ncha nyingine za mkufu zifunge kwenye vile vijalizo viwili, na uziunganishe na vile vipande vya mabega vya kile kizibau upande wa mbele. \v 26 Tengeneza pete mbili za dhahabu, uziunganishe kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kizibau. \v 27 Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uziunganishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega, upande wa mbele wa kile kizibau, karibu na pindo, juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kizibau. \v 28 Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa kwenye pete zile za kizibau kwa kamba ya buluu, ziunganishwe na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwa kile kizibau. \p \v 29 “Wakati wowote Haruni anapoingia Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi, kama kumbukumbu ya kudumu mbele za Mwenyezi Mungu. \v 30 Pia weka Urimu na Thumimu\f + \fr 28:30 \fr*\ft Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.\ft*\f* ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Haruni kila mara aingiapo mbele za Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo siku zote Haruni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya Waisraeli mbele za Mwenyezi Mungu. \s1 Mavazi mengine ya kikuhani \r (Kutoka 39:22-31) \p \v 31 “Shona joho la kizibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, \v 32 na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike. \v 33 Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, na uweke pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga. \v 34 Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka upindo wa joho lile. \v 35 Ni lazima Haruni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za Mwenyezi Mungu, ili asije akafa. \p \v 36 “Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: \pc \sc Mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu.\sc* \m \v 37 Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba. \v 38 Haruni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Haruni daima ili zikubalike kwa Mwenyezi Mungu. \p \v 39 “Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. \v 40 Watengenezee wana wa Haruni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. \v 41 Baada ya kumvika Haruni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, wapake mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. \p \v 42 “Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. \v 43 Haruni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. \p “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Haruni na vizazi vyake. \c 29 \s1 Kuweka wakfu makuhani \r (Walawi 8:1-36) \p \v 1 “Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo dume wawili wasio na dosari. \v 2 Kutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate myembamba iliyopakwa mafuta. \v 3 Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo dume wawili. \v 4 Kisha mlete Haruni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. \v 5 Chukua yale mavazi na umvike Haruni koti, joho la kizibau, na kizibau chenyewe, pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kizibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi. \v 6 Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu lishikamane na hicho kilemba. \v 7 Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. \v 8 Walete wanawe na uwavike makoti, \v 9 pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Haruni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Haruni na wanawe. \p \v 10 “Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 11 Mchinje huyo fahali mbele za Mwenyezi Mungu kwenye mlango wa Hema la Kukutania. \v 12 Chukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuipaka kwenye pembe za hayo madhabahu kwa kidole chako, na damu iliyobaki uimwage sehemu ya chini ya madhabahu. \v 13 Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, na kipande kirefu cha ini, na figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu. \v 14 Lakini nyama ya huyo fahali na ngozi yake na matumbo yake utavichoma nje ya kambi. Hii ni sadaka ya dhambi. \p \v 15 “Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 16 Mchinje huyo kondoo dume, chukua damu yake na uinyunyize pande zote za hayo madhabahu. \v 17 Mkate huyo kondoo dume vipande vipande na usafishe sehemu za ndani pamoja na miguu, ukiviweka pamoja na kichwa na vipande vingine. \v 18 Kisha mteketeze huyo kondoo dume mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \p \v 19 “Mchukue yule kondoo dume mwingine, naye Haruni na wanawe waweke mikono yao juu ya kichwa chake. \v 20 Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Haruni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu. \v 21 Pia chukua sehemu ya damu iliyo juu ya madhabahu na sehemu ya mafuta ya upako, umnyunyizie Haruni na mavazi yake, pia wanawe na mavazi yao. Ndipo Haruni na wanawe pamoja na mavazi yao watakuwa wamewekwa wakfu. \p \v 22 “Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani, kipande kirefu cha ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu.) \v 23 Kutoka kwa kile kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichoko mbele za Mwenyezi Mungu, chukua mkate, andazi lililokandwa kwa mafuta, na mkate mwembamba. \v 24 Viweke vitu hivi vyote mikononi mwa Haruni na wanawe na uviinue mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa. \v 25 Kisha vichukue vitu hivyo kutoka mikononi mwao, uviteketeze juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kupendeza kwa Mwenyezi Mungu, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \v 26 Baada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Haruni, kiinue mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako. \p \v 27 “Weka wakfu zile sehemu za kondoo dume aliyetumika kwa kumweka wakfu Haruni na wanawe: kidari kile kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. \v 28 Siku zote hili litakuwa fungu la milele kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Haruni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa Mwenyezi Mungu kutoka sadaka zao za amani. \p \v 29 “Mavazi matakatifu ya Haruni yatakuwa ya wazao wake ili waweze kupakwa mafuta na kuwekwa wakfu wakiwa wameyavaa. \v 30 Mwana atakayeingia mahali pake kuwa kuhani na kuja kwenye Hema la Kukutania kuhudumu katika Mahali Patakatifu atayavaa kwa siku saba. \p \v 31 “Chukua nyama ya huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu uipike katika Mahali Patakatifu. \v 32 Haruni na wanawe wataila ile nyama ya huyo kondoo dume pamoja na ile mikate iliyo kwenye hicho kikapu wakiwa hapo ingilio la Hema la Kukutania. \v 33 Watakula sadaka hizi ambazo upatanisho ulifanywa kwazo kwa ajili ya kuwaweka wakfu na kuwatakasa. Lakini hakuna mtu mwingine yeyote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu. \v 34 Ikiwa nyama yoyote ya huyo kondoo dume iliyotumika kwa kuwaweka wakfu au mkate wowote umebaki hadi asubuhi, vichomwe. Kamwe visiliwe, kwa sababu ni vitakatifu. \p \v 35 “Hivyo utamfanyia Haruni na wanawe kila kitu kama vile nilivyokuamuru: Utachukua muda wa siku saba kuwaweka wakfu. \v 36 Utatoa dhabihu ya fahali kila siku kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho. Takasa madhabahu kwa kufanya upatanisho kwa ajili yake, nayo uipake mafuta na kuiweka wakfu. \v 37 Kwa muda wa siku saba fanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuiweka wakfu. Ndipo madhabahu itakuwa takatifu sana na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. \p \v 38 “Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. \v 39 Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. \v 40 Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja\f + \fr 29:40 \fr*\ft Efa moja ni sawa na kilo 22.\ft*\f* ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini\f + \fr 29:40 \fr*\ft Robo ya hini ni sawa na lita moja.\ft*\f* ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji. \v 41 Huyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. \p \v 42 “Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Mwenyezi Mungu. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi, \v 43 Huko ndipo nitakapokutana na Waisraeli, nalo Hema la Kukutania litatakaswa na utukufu wangu. \p \v 44 “Kwa hiyo nitaliweka wakfu Hema la Kukutania pamoja na madhabahu, nami nitamweka wakfu Haruni na wanawe ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani. \v 45 Ndipo nitakapofanya makao miongoni mwa Waisraeli na kuwa Mungu wao. \v 46 Nao watajua kuwa Mimi Ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi Ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \c 30 \s1 Madhabahu ya kufukizia uvumba \r (Kutoka 37:25-28) \p \v 1 “Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. \v 2 Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja\f + \fr 30:2 \fr*\ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\ft*\f*, na kimo cha dhiraa mbili\f + \fr 30:2 \fr*\ft Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.\ft*\f*, nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo. \v 3 Funika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. \v 4 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu. \v 5 Tengeneza mipiko kwa miti ya mshita na uifunike kwa dhahabu. \v 6 Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la ule Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ule Ushuhuda, mahali nitakapokutana nawe. \p \v 7 “Itampasa Haruni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa. \v 8 Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele za Mwenyezi Mungu kwa vizazi vijavyo. \v 9 Usifukize uvumba mwingine wowote juu ya madhabahu haya au sadaka nyingine yoyote ya kuteketezwa wala sadaka ya nafaka, wala usimimine sadaka ya kinywaji juu yake. \v 10 Mara moja kwa mwaka Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Mwenyezi Mungu.” \s1 Fedha ya upatanisho \p \v 11 Naye Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 12 “Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Mwenyezi Mungu fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. \v 13 Kila mmoja anayeenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli\f + \fr 30:13 \fr*\ft Nusu shekeli ni sawa na gramu 6.\ft*\f*, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini\f + \fr 30:13 \fr*\ft Gera 20 ni sawa na shekeli moja au gramu 12.\ft*\f*. Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Mwenyezi Mungu. \v 14 Wote wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Mwenyezi Mungu. \v 15 Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu. \v 16 Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Mwenyezi Mungu kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.” \s1 Sinia la kunawia \p \v 17 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 18 “Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake. \v 19 Haruni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji ya hilo sinia. \v 20 Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, \v 21 watanawa mikono na miguu yao ili wasije wakafa. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Haruni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.” \s1 Mafuta ya upako \p \v 22 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 23 “Chukua vikolezo bora vifuatavyo: shekeli mia tano\f + \fr 30:23 \fr*\ft Shekeli 500 ni sawa na kilo 6.\ft*\f* za manemane ya maji, shekeli mia mbili na hamsini\f + \fr 30:23 \fr*\ft Shekeli 250 ni sawa na kilo 3.\ft*\f* za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli mia mbili na hamsini za miwa yenye harufu nzuri, \v 24 shekeli mia tano za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini\f + \fr 30:24 \fr*\ft Hini moja ni sawa na lita 4.\ft*\f* ya mafuta ya zeituni. \v 25 Vitengeneze vikolezo hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako. \v 26 Kisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda, \v 27 meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, \v 28 madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake. \v 29 Utaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. \p \v 30 “Mpake Haruni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani. \v 31 Waambie Waisraeli, ‘Haya yatakuwa mafuta matakatifu yangu ya upako kwa vizazi vijavyo. \v 32 Usiyamimine juu ya miili ya wanadamu wala usitengeneze mafuta ya aina nyingine kwa utaratibu huu. Ni mafuta matakatifu na ni lazima myaone kuwa ni matakatifu. \v 33 Mtu yeyote atakayetengeneza manukato kama hayo na kuyamimina juu ya mtu ambaye si kuhani atakatiliwa mbali na watu wake.’ ” \s1 Uvumba \p \v 34 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Chukua vikolezo vyenye harufu nzuri vifuatavyo: natafi, shekelethi, kelbena na uvumba safi vyote vikiwa na vipimo sawa, \v 35 pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu. \v 36 Saga baadhi yake kuwa unga na uweke mbele ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, mahali nitakapokutana nawe. Itakuwa takatifu sana kwenu. \v 37 Msitengeneze uvumba mwingine wowote wa namna hii kwa ajili yenu wenyewe; uoneni kuwa ni mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu. \v 38 Yeyote atakayetengeneza uvumba kama huu ili kufurahia harufu yake nzuri lazima akatiliwe mbali na watu wake.” \c 31 \s1 Bezaleli na Oholiabu \r (Kutoka 35:30–36:1) \p \v 1 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, \v 3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, \v 4 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, \v 5 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. \v 6 Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. \b \lh “Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe: \b \li1 \v 7 “Hema la Kukutania, \li1 Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, \li1 pia na vifaa vyote vya kwenye hema: \li2 \v 8 meza na vifaa vyake, \li2 kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, \li2 madhabahu ya kufukizia uvumba, \li2 \v 9 madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, \li2 sinia na kinara chake, \li1 \v 10 pamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Haruni, \li2 na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani, \li1 \v 11 pia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. \b \lf “Watavitengeneza jinsi nilivyokuagiza.” \s1 Sabato \p \v 12 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, \v 13 “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi Mwenyezi Mungu, niwafanyaye ninyi watakatifu. \p \v 14 “ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake. \v 15 Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya mapumziko, takatifu kwa Mwenyezi Mungu. Yeyote afanyaye kazi yoyote siku ya Sabato ni lazima auawe. \v 16 Waisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa agano la milele. \v 17 Itakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sita Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na dunia, akapumzika siku ya saba, akastarehe.’ ” \p \v 18 Mwenyezi Mungu alipomaliza kusema na Musa juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu. \c 32 \s1 Ndama wa dhahabu \r (Kumbukumbu 9:6-29) \p \v 1 Watu walipoona kuwa Musa amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimsonga Haruni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Musa aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui yaliyompata.” \p \v 2 Haruni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu, na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” \v 3 Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Haruni. \v 4 Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akasubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.” \p \v 5 Haruni alipoona hili, akajenga madhabahu mbele ya yule ndama na kutangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa Mwenyezi Mungu.” \v 6 Kwa hiyo siku iliyofuata watu wakaamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketeza na sadaka za amani. Baadaye watu wakaketi kula na kunywa, nao wakasimama, wakajizamisha katika sherehe. \p \v 7 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Shuka, kwa sababu watu wako, uliowatoa Misri, wamepotoka. \v 8 Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kusubu yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ” \p \v 9 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nimeona watu hawa, nao ni watu wenye shingo ngumu. \v 10 Sasa niache ili hasira yangu ipate kuwaka dhidi yao, nami nipate kuwaangamiza. Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa.” \p \v 11 Lakini Musa akamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wake, akasema, “Ee Mwenyezi Mungu, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu? \v 12 Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako. \v 13 Wakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote niliyowaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ” \v 14 Kisha Mwenyezi Mungu akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia. \p \v 15 Musa akageuka, akateremka kutoka mlimani akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake. Vilikuwa vimeandikwa pande zote mbili, mbele na nyuma. \v 16 Vibao hivyo vilikuwa kazi ya Mungu; maandishi yalikuwa mwandiko wa Mungu, yaliyochorwa kama muhuri juu ya vibao. \p \v 17 Yoshua aliposikia sauti za watu wakipiga kelele, akamwambia Musa, “Kuna sauti ya vita kambini.” \p \v 18 Musa akajibu: \q1 “Si sauti ya ushindi, \q2 wala si sauti ya kushindwa; \q2 ni sauti ya kuimba ninayosikia.” \p \v 19 Musa alipoikaribia kambi na kuona yule ndama na ile michezo, hasira yake ikawaka, akatupa vile vibao vilivyokuwa mikononi mwake, akavipasua vipande vipande pale chini ya mlima. \v 20 Kisha akamchukua yule ndama waliokuwa wamemtengeneza na kumchoma kwenye moto, kisha akamsaga kuwa unga, akanyunyiza kwenye maji na kuwafanya Waisraeli wanywe. \p \v 21 Musa akamwambia Haruni, “Watu hawa walikufanyia nini, hata ukawaongoza kufanya dhambi kubwa hivyo?” \p \v 22 Haruni akamwambia, “Usikasirike bwana wangu. Unajua jinsi watu hawa walivyo tayari kwa maovu. \v 23 Waliniambia, ‘Tufanyie miungu itakayotuongoza. Kwa kuwa huyu jamaa yetu Musa aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui yaliyompata.’ \v 24 Kwa hiyo nikawaambia, ‘Yeyote aliye na kito chochote cha dhahabu avue.’ Kisha wakanipa hiyo dhahabu, nami nikaitupa motoni, akatokea huyu ndama!” \p \v 25 Musa akaona kuwa watu wameasi, kwa kuwa Haruni alikuwa amewaacha waasi, na hivyo kuwa kichekesho kwa adui zao. \v 26 Kwa hiyo Musa akasimama kwenye ingilio la kambi, akasema, “Yeyote aliye upande wa Mwenyezi Mungu, aje upande wangu.” Walawi wote wakamjia. \p \v 27 Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ” \v 28 Walawi wakafanya kama Musa alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao elfu tatu. \v 29 Kisha Musa akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.” \p \v 30 Siku iliyofuata Musa akawaambia watu, “Mmefanya dhambi kubwa. Lakini sasa nitapanda juu kwa Mwenyezi Mungu, labda nitaweza kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.” \p \v 31 Hivyo Musa akarudi kwa Mwenyezi Mungu na kumwambia, “Lo! Hawa watu wamefanya dhambi kubwa namna gani! Wamejitengenezea miungu ya dhahabu. \v 32 Lakini sasa nakusihi, wasamehe dhambi yao; lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kitabu ulichoandika.” \p \v 33 Mwenyezi Mungu akamjibu Musa, “Yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kitabu changu. \v 34 Sasa nenda, uongoze hao watu hadi mahali nilipokuambia, naye malaika wangu atakutangulia. Pamoja na hayo, wakati utakapofika wa mimi kuwaadhibu, nitawaadhibu kwa ajili ya dhambi yao.” \p \v 35 Ndipo Mwenyezi Mungu akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya na ndama yule ambaye alitengenezwa na Haruni. \c 33 \s1 Amri ya kuondoka Sinai \p \v 1 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Ondoka mahali hapa, wewe pamoja na hao watu uliowapandisha kutoka Misri, mpande hadi nchi niliyomwahidi Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kiapo, nikisema, ‘Nitawapa wazao wenu nchi hii.’ \v 2 Nitamtuma malaika mbele yenu, naye atawafukuza Wakanaani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 3 Pandeni mwende katika nchi inayotiririka maziwa na asali. Lakini mimi sitaenda pamoja nanyi, kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu, nisije nikawaangamiza njiani.” \p \v 4 Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote. \v 5 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa, “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni watu wenye shingo ngumu. Kama ningefuatana nanyi hata kwa muda mfupi, ningewaangamiza. Sasa vueni mapambo yenu, nami nitaamua nitakalowatendea.’ ” \v 6 Hivyo Waisraeli wakavua mapambo yao katika Mlima Horebu. \s1 Hema la Kukutania \p \v 7 Basi Musa alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania”. Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa Mwenyezi Mungu, angeenda hadi Hema la Kukutania, nje ya kambi. \v 8 Wakati wowote Musa alipoenda kwenye Hema, watu wote waliinuka na kusimama kwenye maingilio ya mahema yao, wakimwangalia Musa hadi aingie kwenye Hema. \v 9 Kila mara Musa alipoingia ndani ya Hema, nguzo ya wingu ingeshuka chini na kukaa kwenye ingilio, wakati Mwenyezi Mungu akizungumza na Musa. \v 10 Kila mara watu walipoona hiyo nguzo ya wingu ikiwa imesimama kwenye ingilio la Hema, wote walisimama wakaabudu, kila mmoja kwenye ingilio la hema lake. \v 11 Mwenyezi Mungu angezungumza na Musa uso kwa uso, kama vile mtu anavyozungumza na rafiki yake. Kisha Musa angerudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka kwenye Hema. \s1 Musa na utukufu wa Mwenyezi Mungu \p \v 12 Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Umekuwa ukiniambia, ‘Ongoza watu hawa,’ lakini hujanifahamisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Umesema, ‘Ninakujua wewe kwa jina lako, nawe umepata kibali mbele zangu.’ \v 13 Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako.” \p \v 14 Mwenyezi Mungu akajibu, “Uso wangu utaenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.” \p \v 15 Kisha Musa akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. \v 16 Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipoenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?” \p \v 17 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.” \p \v 18 Kisha Musa akasema, “Basi nioneshe utukufu wako.” \p \v 19 Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, Mwenyezi Mungu, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.” \v 20 Lakini Mungu akasema, “Hutaweza kuuona uso wangu, kwa kuwa hakuna mtu yeyote awezaye kuniona akaishi.” \p \v 21 Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Kuna mahali karibu nami ambapo unaweza kusimama juu ya mwamba. \v 22 Utukufu wangu unapopita, nitakuweka gengeni kwenye mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hadi nitakapokuwa nimepita. \v 23 Kisha nitaondoa mkono wangu nawe utaona mgongo wangu; lakini kamwe uso wangu hautaonekana.” \c 34 \s1 Vibao vipya vya mawe \r (Kumbukumbu 10:1-5) \p \v 1 Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. \v 2 Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. \v 3 Mtu yeyote asije nawe, wala asionekane mtu popote mlimani; wala kondoo na mbuzi au ng’ombe wasilishe mbele ya huo mlima.” \p \v 4 Kwa hiyo Musa akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake. \v 5 Kisha Mwenyezi Mungu akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, Mwenyezi Mungu. \v 6 Mwenyezi Mungu akapita mbele ya Musa, akitangaza, “Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, \v 7 akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.” \p \v 8 Mara Musa akasujudu na kuabudu. \v 9 Musa akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.” \s1 Kufanya agano upya \r (Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17) \p \v 10 Kisha Mwenyezi Mungu akasema: “Tazama, ninafanya agano nanyi. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza kazi nitakayowafanyia Mimi, Mwenyezi Mungu wenu. \v 11 Tii yale ninayokuamuru leo. Tazama nawafukuza mbele yako Waamori, Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 12 Uwe mwangalifu, usifanye agano na wale wanaokaa katika nchi ile unayoiendea, la sivyo watakuwa mtego katikati yako. \v 13 Bomoa madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, na ukatekate nguzo zao za Ashera. \v 14 Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu. \p \v 15 “Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe, nawe utakula sadaka za matambiko yao. \v 16 Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo. \p \v 17 “Usijifanyie sanamu za kusubu. \p \v 18 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri. \p \v 19 “Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ng’ombe au wa kondoo au mbuzi. \v 20 Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume. \p “Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu. \p \v 21 “Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike. \p \v 22 “Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka. \v 23 Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watakuja mbele za Bwana Mungu Mwenyezi, Mungu wa Israeli. \v 24 Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapoenda mara tatu kila mwaka kuonana na Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p \v 25 “Usinitolee damu ya dhabihu pamoja na kitu chochote chenye chachu, wala usibakize dhabihu yoyote ya Sikukuu ya Pasaka hadi asubuhi. \p \v 26 “Leta matunda ya kwanza yaliyo bora zaidi ya ardhi yako katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \p “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.” \p \v 27 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya agano na wewe pamoja na Israeli.” \v 28 Musa alikuwa huko pamoja na Mwenyezi Mungu kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya agano, yaani zile Amri Kumi. \s1 Mng’ao wa uso wa Musa \p \v 29 Musa alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa uking’aa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Mwenyezi Mungu. \v 30 Haruni na Waisraeli wote walipomwona Musa, kuwa uso wake unang’aa, waliogopa kumkaribia. \v 31 Lakini Musa akawaita, kwa hiyo Haruni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. \v 32 Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Mwenyezi Mungu alizompa katika Mlima Sinai. \p \v 33 Musa alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake. \v 34 Lakini kila wakati Musa alipoingia mbele za Mwenyezi Mungu kuzungumza naye, aliondoa ule utaji hadi alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa, \v 35 waliona kuwa uso wake unang’aa. Kisha Musa angerudisha utaji juu ya uso wake hadi alipoingia ili kuzungumza na Mwenyezi Mungu. \c 35 \s1 Masharti ya Sabato \p \v 1 Musa akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndio mambo ambayo Mwenyezi Mungu amewaamuru ninyi mfanye: \v 2 Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya mapumziko kwa Mwenyezi Mungu. Yeyote atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe. \v 3 Msiwashe moto mahali popote katika makazi yenu siku ya Sabato.” \s1 Vifaa kwa ajili ya maskani ya Mungu \r (Kutoka 25:1-9) \p \v 4 Musa akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo Mwenyezi Mungu aliloamuru: \v 5 Toeni sadaka kwa Mwenyezi Mungu kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea Mwenyezi Mungu sadaka ya: \b \li1 “dhahabu, fedha na shaba; \li1 \v 6 nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; \li1 singa za mbuzi; \li1 \v 7 ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo\f + \fr 35:7 \fr*\ft pengine ni mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili\ft*\f*; \li1 mbao za mshita; \li1 \v 8 mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; \li1 vikolezo kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; \li1 \v 9 vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kizibau na kile kifuko cha kifuani. \b \p \v 10 “Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Mwenyezi Mungu alichoamuru: \b \li1 \v 11 “Maskani ya Mungu pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako; \li1 \v 12 Sanduku la Agano pamoja na mipiko yake, kifuniko cha kiti cha rehema na pazia linalokizuia; \li1 \v 13 meza na mipiko yake, pamoja na vyombo vyake vyote, mikate ya Wonesho; \li1 \v 14 kinara cha taa kwa ajili ya mwanga pamoja na vifaa vyake vyote, taa na mafuta kwa ajili ya mwanga; \li1 \v 15 madhabahu ya kufukiza uvumba pamoja na mipiko yake, mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri; \li1 pazia la mlangoni mahali pa kuingilia ndani ya Maskani; \li1 \v 16 madhabahu ya sadaka za kuteketeza pamoja na wavu wake wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote; \li1 sinia la shaba pamoja na tako lake; \li1 \v 17 pazia la eneo la ua pamoja na nguzo zake na vitako vyake, na pazia la ingilio la ua; \li1 \v 18 vigingi vya hema kwa ajili ya Maskani pamoja na ua na kamba zake; \li1 \v 19 mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu kwa ajili ya kuhani Haruni, na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.” \b \p \v 20 Ndipo jumuiya yote ya Waisraeli ilipoondoka mbele ya Musa, \v 21 na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu. \v 22 Wote waliopenda, wanaume na wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Mwenyezi Mungu. \v 23 Kila mmoja aliyekuwa na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi, au singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, au ngozi za pomboo, wakavileta. \v 24 Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta. \v 25 Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi. \v 26 Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi. \v 27 Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kizibau na kwenye kifuko cha kifuani. \v 28 Wakaleta pia vikolezo na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri. \v 29 Waisraeli wote, wanaume na wanawake, waliopenda wakaleta mbele za Mwenyezi Mungu kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya Mwenyezi Mungu aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Musa. \s1 Bezaleli na Oholiabu \r (Kutoka 31:1-11) \p \v 30 Kisha Musa akawaambia Waisraeli, “Tazameni, Mwenyezi Mungu amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, \v 31 naye amemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, na uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, \v 32 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, \v 33 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi wa kupendeza. \v 34 Tena amempa yeye pamoja na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, uwezo wa kufundisha wengine. \v 35 Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zinazofanywa na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari. \c 36 \nb \v 1 Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu Mwenyezi Mungu aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile Mwenyezi Mungu alivyoagiza.” \p \v 2 Ndipo Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Mwenyezi Mungu alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi. \v 3 Wakapokea kutoka kwa Musa sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi. \v 4 Ikafika wakati mafundi wote wenye ujuzi waliokuwa wakiifanya kazi yote ya mahali patakatifu wakasimamisha kazi zao, \v 5 wakaja na kumwambia Musa, “Watu wanaleta vitu vingi kuliko tunavyohitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo Mwenyezi Mungu ameagiza ifanyike.” \p \v 6 Ndipo Musa akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi yote: “Mwanaume au mwanamke yeyote asilete tena kitu chochote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu wakazuiliwa kuleta zaidi, \v 7 kwa sababu walivyokuwa navyo tayari vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote. \s1 Maskani ya Mungu \r (Kutoka 26:1-37) \p \v 8 Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani ya Mungu kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. \v 9 Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane\f + \fr 36:9 \fr*\ft Dhiraa 28 ni sawa na mita 12.6.\ft*\f*, na upana wa dhiraa nne\f + \fr 36:9 \fr*\ft Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.\ft*\f*. \v 10 Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. \v 11 Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. \v 12 Wakatengeneza pia vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, navyo vitanzi vyote vikaelekeana. \v 13 Kisha wakatengeneza vifungo hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha zile fungu mbili za mapazia pamoja ili maskani ya Mungu ipate kuwa kitu kimoja. \p \v 14 Wakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika Maskani. \v 15 Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo sawa, yaani urefu wa dhiraa thelathini\f + \fr 36:15 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\ft*\f*, na upana wa dhiraa nne. \v 16 Wakaunganisha mapazia matano kuwa fungu moja, na hayo mengine sita kuwa fungu lingine. \v 17 Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. \v 18 Wakatengeneza vifungo hamsini vya shaba ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. \v 19 Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo\f + \fr 36:19 \fr*\ft pengine ni mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili\ft*\f*. \p \v 20 Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani ya Mungu. \v 21 Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi\f + \fr 36:21 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\ft*\f*, na upana wa dhiraa moja na nusu\f + \fr 36:21 \fr*\ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.\ft*\f*, \v 22 zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya Maskani jinsi hii. \v 23 Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa Maskani, \v 24 na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. \v 25 Kwa upande wa kaskazini wa Maskani wakatengeneza mihimili ishirini \v 26 na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \v 27 Wakatengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa Maskani, \v 28 na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za Maskani za upande uliokuwa mbali. \v 29 Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini hadi juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana. \v 30 Kwa hiyo kulikuwa na mihimili nane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \p \v 31 Wakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa Maskani, \v 32 matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa Maskani. \v 33 Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. \v 34 Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika hayo mataruma kwa dhahabu. \p \v 35 Wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye hilo pazia. \v 36 Wakatengeneza nguzo nne za mti wa mshita kwa ajili yake na kuzifunika kwa dhahabu. Wakatengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya nguzo hizo, na kusubu vitako vinne vya fedha. \v 37 Kwa ajili ya ingilio la hema wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. \v 38 Pia wakatengeneza nguzo tano zenye kulabu. Wakafunika ncha za juu za hizo nguzo pamoja na tepe zake kwa dhahabu, na pia wakatengeneza vitako vyake vitano vya shaba. \c 37 \s1 Sanduku la Agano \r (Kutoka 25:10-22) \p \v 1 Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu\f + \fr 37:1 \fr*\ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na mita 1.13.\ft*\f*, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. \v 2 Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. \v 3 Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. \v 4 Kisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. \v 5 Akaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. \p \v 6 Akatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. \v 7 Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. \v 8 Akatengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; akawatengeneza kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. \v 9 Makerubi hao walikuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao walielekeana, wakitazama hicho kifuniko. \s1 Meza \r (Kutoka 25:23-30) \p \v 10 Akatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili\f + \fr 37:10 \fr*\ft Dhiraa 2 ni sawa na sentimita 90.\ft*\f*, upana wa dhiraa moja\f + \fr 37:10 \fr*\ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\ft*\f*, na kimo cha dhiraa moja na nusu. \v 11 Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. \v 12 Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda moja\f + \fr 37:12 \fr*\ft Nyanda moja ni sawa na sentimita 7.5\ft*\f*, na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. \v 13 Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. \v 14 Pete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. \v 15 Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. \v 16 Vyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi: yaani sahani zake, masinia, na bakuli na bilauri zake kwa ajili ya kumiminia sadaka za vinywaji. \s1 Kinara cha taa \r (Kutoka 25:31-40) \p \v 17 Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja. \v 18 Matawi sita yalitokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. \v 19 Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vilikuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyotokeza kwenye kile kinara cha taa. \v 20 Juu ya kinara chenyewe kulikuwa vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. \v 21 Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla. \v 22 Matovu na matawi yote yalikuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakiwa yamefuliwa kwa dhahabu safi. \p \v 23 Akatengeneza taa zake saba, na pia mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote kwa dhahabu safi. \v 24 Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutumia talanta\f + \fr 37:24 \fr*\ft Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.\ft*\f* moja ya dhahabu safi. \s1 Madhabahu ya kufukizia uvumba \r (Kutoka 30:1-5) \p \v 25 Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo. \v 26 Akafunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia zile pembe zake kwa dhahabu safi, na akayafanyizia ukingo wa dhahabu kuizunguka. \v 27 Akatengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, zikiwa mbili kila upande, za kushikilia mipiko iliyotumika kubebea madhabahu. \v 28 Akatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu. \p \v 29 Pia akatengeneza mafuta matakatifu ya upako, na uvumba safi wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. \c 38 \s1 Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa \r (Kutoka 27:1-8) \p \v 1 Akatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu\f + \fr 38:1 \fr*\ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\ft*\f*; nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wa dhiraa tano\f + \fr 38:1 \fr*\ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\ft*\f*. \v 2 Akatengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu zikawa zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. \v 3 Akatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama na vyombo vya kuchukulia moto. \v 4 Akatengeneza wavu wa shaba chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. \v 5 Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya zile pembe nne za huo wavu wa shaba. \v 6 Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba. \v 7 Akaiingiza ile mipiko kwenye zile pete, ili iwe pande mbili za madhabahu kwa ajili ya kuibeba. Akaitengeneza madhabahu yenye uvungu ndani yake akitumia mbao. \s1 Sinia la kunawia \r (Kutoka 30:18) \p \v 8 Akatengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kutoka kwa vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu pale ingilio la Hema la Kukutania. \s1 Ua wa Hema la Kukutania \r (Kutoka 27:9-19) \p \v 9 Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja\f + \fr 38:9 \fr*\ft Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.\ft*\f*, na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, \v 10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \v 11 Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \p \v 12 Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini\f + \fr 38:12 \fr*\ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\ft*\f*, na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \v 13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, pia ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. \v 14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano\f + \fr 38:14 \fr*\ft Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.\ft*\f* yalikuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \v 15 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio la ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \v 16 Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. \v 17 Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha. \p \v 18 Pazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano, \v 19 likiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, na ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. \v 20 Vigingi vyote vya maskani ya Mungu na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba. \s1 Vifaa vilivyotumika \p \v 21 Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani ya Mungu, hiyo Maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Musa, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Haruni. \v 22 (Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu Mwenyezi Mungu alichomwamuru Musa, \v 23 akiwa pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, fundi stadi wa kutia nakshi, kubuni michoro, mtarizi kwa rangi ya buluu, ya zambarau, nyekundu na kitani safi.) \v 24 Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta ishirini na tisa na shekeli mia saba na thelathini (730\f + \fr 38:24 \fr*\ft Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja.\ft*\f*), kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. \p \v 25 Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli elfu moja mia saba sabini na tano (1,775)\f + \fr 38:25 \fr*\ft Talanta 100 na shekeli 1,775 za fedha ni sawa na tani 3.4.\ft*\f*, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. \v 26 Kila mtu alitoa beka moja, ambayo ni sawa na nusu shekeli ya fedha, kwa kazi ya mahali patakatifu, kutoka kwa kila mtu aliyekuwa amehesabiwa mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, ambao jumla yao walikuwa wanaume elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550). \v 27 Talanta hizo mia moja za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani talanta moja kwa kila kitako. \v 28 Akatumia hizo shekeli elfu moja mia saba sabini na tano (1,775) kutengeneza kulabu za nguzo, kufunika ncha za nguzo, na kutengeneza vitanzi vyake. \p \v 29 Shaba iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa ilikuwa na uzito wa talanta sabini na shekeli elfu mbili mia nne\f + \fr 38:29 \fr*\ft Talanta 70 na shekeli 2,400 ni sawa na tani 2.4.\ft*\f*. \v 30 Akaitumia hiyo shaba kutengeneza vitako vya ingilio la Hema la Kukutania, madhabahu ya shaba pamoja na ule wavu wake na vyombo vyake vyote, \v 31 vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya maskani ya Mungu, pamoja na vigingi vya ule ua uliozunguka. \c 39 \s1 Mavazi ya Kikuhani \r (Kutoka 28:1-14) \p \v 1 Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Haruni mavazi matakatifu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \s1 Kizibau \p \v 2 Akatengeneza kizibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kitani iliyosokotwa vizuri. \v 3 Akafua vipande vyembamba vya dhahabu kwa nyundo na kutengeneza nyuzi nyembamba ili kuzifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi, kazi ya fundi stadi. \v 4 Akatengeneza vipande vya mabegani vya kizibau, vilivyounganishwa kwenye pembe zake mbili kwa ajili ya kufungia. \v 5 Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kizibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 6 Akatengeneza vito vya shohamu vilivyowekwa katika vijalizo vya dhahabu, navyo vilichorwa na majina ya wana wa Israeli kama vile muhuri huchorwa. \v 7 Kisha akavifungia kwenye vipande vya mabega ya kizibau kuwa vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \s1 Kifuko cha kifuani \r (Kutoka 28:15-30) \p \v 8 Akatengeneza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kizibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. \v 9 Kifuko hicho kilikuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja\f + \fr 39:9 \fr*\ft Shibiri moja ni sawa na sentimita 22.\ft*\f* na upana wa shibiri moja, nacho kilikunjwa mara mbili. \v 10 Kifuko hicho kilipambwa kwa safu nne za vito vya thamani. Safu ya kwanza ilikuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; \v 11 safu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; \v 12 safu ya tatu ilikuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; \v 13 katika safu ya nne ilikuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Vito hivyo vilitiwa kwenye vijalizo vya dhahabu. \v 14 Kulikuwa na vito kumi na viwili, kimoja kwa kila jina la wana wa Israeli; kila kimoja kilichorwa kama muhuri kwa jina mojawapo la makabila yale kumi na mawili. \p \v 15 Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani alitengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. \v 16 Akatengeneza vijalizo viwili vya dhahabu na pete mbili za dhahabu, na kuzifungia pete hizo kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. \v 17 Akafunga hiyo mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, \v 18 nazo zile ncha nyingine za mkufu akazifunga kwenye vile vijalizo viwili, na kuziunganisha na vile vipande vya mabega vya kile kizibau upande wa mbele. \v 19 Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuziunganisha kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kizibau. \v 20 Kisha akatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuziunganisha sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kizibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kizibau. \v 21 Akafunga pete za hicho kifuko cha kifuani kwenye pete za kizibau kwa kamba ya buluu, wakiziunganisha na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwa kile kizibau, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \s1 Mavazi mengine ya kikuhani \r (Kutoka 28:31-43) \p \v 22 Akashona joho la kizibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, kazi ya mfumaji, \v 23 na lilikuwa na nafasi ya shingo katikati ya joho lile iliyofanana na ukosi, na utepe ulioshonwa kuizunguka nafasi hiyo ili isichanike. \v 24 Akatengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na ya kitani iliyosokotwa vizuri kuzunguka pindo la hilo joho. \v 25 Kisha akatengeneza vikengele vya dhahabu safi na kuviunganisha kuzunguka pindo hilo kati ya hayo makomamanga. \v 26 Hivyo vikengele na makomamanga vilipishana kuzunguka upindo wa joho ili livaliwe kwa kuhudumu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 27 Pia akamtengenezea Haruni na wanawe makoti ya kitani safi, kazi ya mfumaji, \v 28 na kilemba cha kitani safi, tepe za kichwani za kitani, na nguo za ndani za kitani iliyosokotwa vizuri. \v 29 Mshipi ulikuwa wa kitani iliyosokotwa vizuri ya rangi ya buluu, na zambarau, na nyekundu, kazi ya mtarizi, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 30 Kisha akatengeneza lile bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: \pc \sc Mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu.\sc* \m \v 31 Kisha wakalifunga kwa kamba ya rangi ya buluu ili kuliunganisha na kile kilemba, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \s1 Musa akagua maskani ya Mungu \r (Kutoka 35:10-19) \p \v 32 Kwa hiyo kazi yote ya maskani ya Mungu, lile Hema la Kukutania, ikakamilika. Waisraeli wakafanya kila kitu sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \v 33 Ndipo wakaleta maskani ya Mungu kwa Musa: \b \li1 hema pamoja na vifaa vyake vyote, vibanio vyake, mihimili yake, mataruma yake, nguzo na vitako vyake; \li1 \v 34 kifuniko cha ngozi za kondoo dume kilichotiwa rangi nyekundu, na kifuniko cha ngozi za pomboo\f + \fr 39:34 \fr*\ft pengine ni mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili\ft*\f*, na pazia la kufunikia; \li1 \v 35 Sanduku la Ushuhuda pamoja na mipiko yake na kiti cha rehema, \li1 \v 36 meza pamoja na vyombo vyake vyote, na mikate ya Wonesho; \li1 \v 37 kinara cha taa cha dhahabu safi, safu zake za taa pamoja na vifaa vyake vyote, pamoja na mafuta kwa ajili ya taa; \li1 \v 38 madhabahu ya dhahabu, mafuta ya upako, uvumba wenye harufu nzuri, na pazia la ingilio la hema; \li1 \v 39 madhabahu ya shaba, pamoja na wavu wa shaba, nguzo zake na vyombo vyake vyote, \li1 sinia, na tako lake; \li1 \v 40 mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia la ingilio la ua; \li1 kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; \li1 vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani ya Mungu, lile Hema la Kukutania; \li1 \v 41 na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Haruni na mavazi ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani. \b \p \v 42 Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza Musa. \v 43 Musa akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Musa akawabariki. \c 40 \s1 Kuweka wakfu maskani ya Mungu \p \v 1 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: \v 2 “Simika maskani ya Mungu, lile Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. \v 3 Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake. \v 4 Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake. \v 5 Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la maskani ya Mungu. \p \v 6 “Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania; \v 7 weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake. \v 8 Tengeneza ua kuzunguka maskani ya Mungu, na uweke pazia penye ingilio la ua. \p \v 9 “Chukua mafuta ya upako, upake maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilicho ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo, nayo itakuwa takatifu. \v 10 Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana. \v 11 Paka sinia mafuta pamoja na kishikilio chake na uviweke wakfu. \p \v 12 “Mlete Haruni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. \v 13 Kisha mvike Haruni yale mavazi matakatifu, umpake mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia kama kuhani. \v 14 Walete wanawe na uwavike makoti. \v 15 Kisha wapake mafuta kama ulivyomtia baba yao, ili nao pia wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Kupakwa mafuta kwao kutakuwa kwa ajili ya ukuhani utakaoendelea kwa vizazi vyote vijavyo.” \v 16 Musa akafanya kila kitu sawa kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \p \v 17 Kwa hiyo maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili. \v 18 Musa alipoweka wakfu maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo. \v 19 Kisha akalitandaza hema juu ya maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \p \v 20 Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. \v 21 Kisha Musa akalileta Sanduku ndani ya maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \p \v 22 Musa akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini mwa maskani ya Mungu nje ya pazia \v 23 na kupanga mikate juu yake mbele za Mwenyezi Mungu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \p \v 24 Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa maskani ya Mungu \v 25 na kuziweka taa mbele za Mwenyezi Mungu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \p \v 26 Musa akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia, \v 27 na akafukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \v 28 Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la maskani ya Mungu. \p \v 29 Musa akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. \p \v 30 Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia. \v 31 Naye Musa, Haruni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. \v 32 Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. \p \v 33 Kisha Musa akatengeneza ua kuizunguka maskani ya Mungu na madhabahu, na pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Musa akaikamilisha kazi. \s1 Utukufu wa Mwenyezi Mungu \r (Hesabu 9:15-23) \p \v 34 Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaijaza maskani ya Mungu. \v 35 Musa hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaijaza maskani ya Mungu. \p \v 36 Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya maskani ya Mungu, wangeondoka; \v 37 lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, hadi siku lilipoinuka. \v 38 Kwa hiyo wingu la Mwenyezi Mungu lilikuwa juu ya maskani ya Mungu mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.