\id EPH - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h Waefeso \toc1 Waefeso \toc2 Waefeso \toc3 Efe \mt1 Waefeso \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Paulo, mtume wa Al-Masihi Isa, kwa mapenzi ya Mungu. \po Kwa watakatifu walio Efeso, walio waaminifu katika Al-Masihi Isa. \po \v 2 Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba\f + \fr 1:2 \fr*\ft Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi. \s1 Baraka za kiroho katika Al-Masihi Isa \p \v 3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Al-Masihi. \v 4 Kwa maana alituchagua katika yeye kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele zake. Kwa upendo \v 5 alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kupitia kwa Isa Al-Masihi kwa furaha na mapenzi yake. \v 6 Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia sisi katika Mwanawe Mpendwa. \v 7 Ndani yake tunao ukombozi kupitia kwa damu yake, yaani msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake \v 8 aliyotumiminia kwa wingi, kwa hekima yote na maarifa yote. \v 9 Naye alitujulisha siri ya mapenzi yake sawasawa na uradhi wa mapenzi yake, ambayo alikusudia katika Al-Masihi, \v 10 ili yapate kutimizwa wakati mkamilifu utakapowadia, yaani kuvitia vitu vyote vya mbinguni na vya duniani pamoja, chini ya kiongozi mmoja, ndiye Al-Masihi. \p \v 11 Katika Al-Masihi sisi nasi tumepata urithi, tukisha kuchaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi la Mungu, yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na kusudi la mapenzi yake, \v 12 ili, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Al-Masihi, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu wake. \v 13 Ninyi pia mliingia ndani ya Al-Masihi mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Baada ya kuamini, mlitiwa muhuri ndani yake, huyo Roho Mtakatifu wa Mungu mliyeahidiwa, \v 14 yeye ambaye ni amana yetu ya kutuhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu, kwa sifa ya utukufu wake. \s1 Shukrani na maombi \p \v 15 Kwa sababu hii, tangu niliposikia kuhusu imani yenu katika Bwana Isa na upendo wenu kwa watakatifu wote, \v 16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. \v 17 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. \v 18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watakatifu \v 19 na uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno \v 20 aliyoitumia katika Al-Masihi alipomfufua kutoka kwa wafu, na kumketisha mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho, \v 21 juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia. \v 22 Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu yake, na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya jumuiya ya waumini, \v 23 ambayo ni mwili wake, ukamilifu wake yeye aliye yote katika yote. \c 2 \s1 Kufanywa hai ndani ya Al-Masihi \p \v 1 Ninyi mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, \v 2 ambazo mlizitenda mlipofuata njia za ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii. \v 3 Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulistahili ghadhabu, kama watu wengine wote. \v 4 Lakini Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, \v 5 hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Al-Masihi Isa, yaani mmeokolewa kwa neema. \v 6 Mungu alitufufua pamoja na Al-Masihi na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Al-Masihi Isa, \v 7 ili katika ulimwengu ujao apate kuonesha wingi wa neema yake isiyolinganishwa, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Al-Masihi Isa. \v 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kupitia kwa imani, nayo haikutokana na ninyi wenyewe. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, \v 9 si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu. \v 10 Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Al-Masihi Isa, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo. \s1 Wamoja katika Al-Masihi \p \v 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo awali ninyi ambao ni watu wa Mataifa kwa kuzaliwa na kuitwa “wasiotahiriwa” na wale wanaojiita “waliotahiriwa” (yaani tohara ifanyikayo katika mwili kwa mikono ya wanadamu), \v 12 kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi hamkuwa na tumaini wala Mungu duniani. \v 13 Lakini sasa katika Al-Masihi Isa, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kupitia kwa damu ya Al-Masihi. \p \v 14 Kwa maana yeye mwenyewe ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi tuliokuwa vikundi viwili tuwe kikundi kimoja kwa kuvunja kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui uliokuwa kati yetu, \v 15 kwa kuibatilisha ile sheria pamoja na amri zake na maagizo yake alipoutoa mwili wake, ili apate kufanya ndani yake mtu mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo akifanya amani, \v 16 naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mungu kupitia msalaba, ili kwa huo msalaba akaangamiza uadui wao. \v 17 Alikuja na kuhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na pia akahubiri amani kwao waliokuwa karibu. \v 18 Kwa maana kupitia kwake sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. \p \v 19 Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena na wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu. \v 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Al-Masihi Isa ndiye jiwe kuu la pembeni. \v 21 Ndani yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kuinuliwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Mwenyezi Mungu. \v 22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake kupitia kwa Roho wake Mtakatifu. \c 3 \s1 Mpango wa Mwenyezi Mungu kwa watu wa Mataifa \p \v 1 Kwa sababu hii, mimi Paulo, ni mfungwa wa Al-Masihi Isa kwa ajili yenu ninyi watu wa Mataifa. \p \v 2 Kwa hakika mmekwisha kusikia kuhusu ile huduma ya neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu, \v 3 yaani ile siri iliodhihirishwa kwangu kupitia ufunuo, kama nilivyotangulia kuandika kwa kifupi. \v 4 Kwa kusoma haya, basi mtaweza kuelewa ufahamu wangu katika siri ya Al-Masihi. \v 5 Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho wa Mungu kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. \v 6 Siri hii ni kwamba, kupitia kwa Injili, watu wa Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Al-Masihi Isa. \p \v 7 Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi. \v 8 Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii: ili niwahubirie watu wa Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Al-Masihi, \v 9 na kuweka wazi kwa kila mtu siri hii iliyokuwa imefichwa tangu zamani katika Mungu, aliyeumba vitu vyote. \v 10 Ili sasa kupitia kwa jumuiya ya waumini, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho, \v 11 sawasawa na kusudi lake la milele alilolitimiza katika Al-Masihi Isa Bwana wetu. \v 12 Ndani yake na kupitia kwa imani katika yeye twaweza kumkaribia Mungu kwa uhuru na kwa ujasiri. \v 13 Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu. \s1 Maombi ya Paulo kwa Waefeso \p \v 14 Kwa sababu hii nampigia Baba magoti, \v 15 ambaye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unatokana naye. \v 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, \v 17 ili Al-Masihi apate kukaa mioyoni mwenu kupitia kwa imani. Nami ninaomba kwamba mkiwa wenye mizizi tena imara katika msingi wa upendo, \v 18 mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina upendo wa Al-Masihi, \v 19 na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu. \p \v 20 Basi kwa yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza wake ule utendao kazi ndani yetu, \v 21 yeye atukuzwe katika jumuiya ya waumini, na katika Al-Masihi Isa kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen. \c 4 \s1 Umoja katika mwili wa Al-Masihi \p \v 1 Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana Isa, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa. \v 2 Kwa unyenyekevu wote na upole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo. \v 3 Jitahidini kudumisha umoja wa Roho wa Mungu katika kifungo cha amani. \v 4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. \v 5 Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo\f + \fr 4:5 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali. Wafuasi wa Isa Al-Masihi pia wanapokea Roho wa Mungu kama dhibitisho ya imani yao.\ft*\f* mmoja, \v 6 Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote. \p \v 7 Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Al-Masihi. \v 8 Kwa hiyo husema: \q1 “Alipopaa juu zaidi, \q2 aliteka mateka, \q2 akawapa wanadamu vipawa.” \m \v 9 (Asemapo “alipaa juu,” maana yake nini isipokuwa ni kusema kwamba Al-Masihi pia alishuka pande za chini sana za dunia\f + \fr 4:9 \fr*\ft pande za chini sana za dunia hapa maana yake \ft*\fqa Kuzimu\fqa*\f*? \v 10 Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu zaidi kupita mbingu zote, ili apate kuujaza ulimwengu wote.) \v 11 Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, \v 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili mwili wa Al-Masihi upate kujengwa \v 13 hadi sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu\f + \fr 4:13 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f* na kuwa watu wazima, kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Al-Masihi. \p \v 14 Basi hatutakuwa tena watoto wachanga, tukiyumbishwa na mawimbi, na tukipeperushwa hapa na pale na kila upepo wa mafundisho, na kwa ujanja na hila za watu katika njama zao. \v 15 Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani Al-Masihi. \v 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, huku kila kiungo kikifanya kazi yake. \s1 Maisha ya zamani na maisha mapya \p \v 17 Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana Isa kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa wanavyoishi, katika ubatili wa mawazo yao. \v 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. \v 19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kujiingiza katika kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi. \p \v 20 Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Al-Masihi. \v 21 Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Isa. \v 22 Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, \v 23 ili mfanywe upya katika roho ya nia zenu, \v 24 na mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki ya kweli na utakatifu. \s1 Kanuni za maisha mapya \p \v 25 Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja. \v 26 Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, \v 27 wala msimpe ibilisi nafasi. \v 28 Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kinachofaa kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji. \p \v 29 Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yanayofaa kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao. \v 30 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. \v 31 Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu na hasira, makelele na masingizio, pamoja na kila aina ya uovu. \v 32 Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi. \c 5 \s1 Kuenenda katika nuru \p \v 1 Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wanaopendwa, \v 2 mkiishi maisha ya upendo, kama vile Al-Masihi alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. \p \v 3 Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. \v 4 Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu. \v 5 Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Mwasherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya (mtu kama huyo ni mwabudu sanamu) kamwe hataurithi ufalme wa Al-Masihi na wa Mungu. \v 6 Mtu yeyote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama hayo juu ya wale wasiomtii. \v 7 Kwa hiyo, msishirikiane nao. \p \v 8 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana Isa. Nendeni kama watoto wa nuru \v 9 (kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), \v 10 nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana Isa. \v 11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. \v 12 Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. \v 13 Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana, \v 14 kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana: \q1 “Amka, wewe uliyelala, \q2 ufufuke kutoka kwa wafu, \q2 naye Al-Masihi atakuangazia.” \p \v 15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, \v 16 mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. \v 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini mapenzi ya Bwana Isa. \v 18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo mna upotovu, bali mjazwe Roho wa Mungu. \v 19 Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana Isa mioyoni mwenu, \v 20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba\f + \fr 5:20 \fr*\ft Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* Mwenyezi kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi. \p \v 21 Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kutokana na kumcha Al-Masihi. \s1 Mafundisho kuhusu wake na waume \p \v 22 Ninyi wake, watiini waume zenu kama vile mnavyomtii Bwana Isa. \v 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Al-Masihi alivyo kichwa cha jumuiya ya waumini, ambayo ni mwili wake, naye Al-Masihi ni Mwokozi wake. \v 24 Basi, kama vile jumuiya ya waumini wanavyomtii Al-Masihi, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo. \p \v 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Al-Masihi alivyoipenda jumuiya ya waumini na akajitoa kwa ajili yake, \v 26 kusudi aifanye takatifu, akiitakasa kwa kuiosha kwa maji katika neno lake, \v 27 apate kujiletea jumuiya tukufu isiyo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na isiyo na hatia. \v 28 Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. \v 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Al-Masihi anavyoitunza jumuiya yake ya waumini. \v 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. \v 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” \v 32 Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Al-Masihi na jumuiya ya waumini wake. \v 33 Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe. \c 6 \s1 Mafundisho kuhusu watoto na wazazi \p \v 1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana Isa, kwa kuwa hili ni jema. \v 2 “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, \v 3 “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” \p \v 4 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana Isa. \s1 Mafundisho kuhusu watumwa na mabwana \p \v 5 Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa unyofu wa moyo, kama vile mnavyomtii Al-Masihi. \v 6 Watiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Al-Masihi, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. \v 7 Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mngemtumikia, wala si wanadamu, \v 8 mkijua kwamba Bwana Isa atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, awe mtumwa au mtu huru. \p \v 9 Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo. \s1 Silaha za Mwenyezi Mungu \p \v 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana Isa na katika uweza wa nguvu zake. \v 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi. \v 12 Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. \v 13 Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja, nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. \v 14 Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, \v 15 nayo miguu yenu ivalishwe viatu vya utayari tunaopata katika Injili ya amani. \v 16 Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. \v 17 Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho wa Mungu, ambao ni neno la Mungu, \v 18 mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote. \p \v 19 Niombeeni na mimi pia, ili kila nifunguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri, \v 20 ambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni ili nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo. \b \s1 Salamu za mwisho \p \v 21 Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana Isa, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya. \v 22 Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali yetu, na awatie moyo. \b \p \v 23 Amani iwe kwa ndugu, na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba Mwenyezi na kwa Bwana Isa Al-Masihi. \b \p \v 24 Neema iwe na wote wanaompenda Bwana wetu Isa Al-Masihi kwa upendo wa dhati. Amen.