\id DAN - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Danieli \toc1 Danieli \toc2 Danieli \toc3 Dan \mt1 Danieli \c 1 \s1 Mafunzo ya Danieli huko Babeli \p \v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja akazingira Yerusalemu. \v 2 Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza, pamoja na baadhi ya vyombo kutoka Hekalu la Mungu. Nebukadneza akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari\f + \fr 1:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Babeli\fqa*\f*, naye akaviweka nyumbani ya hazina ya mungu wake. \p \v 3 Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa mfalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya mfalme na kutoka jamaa kuu: \v 4 vijana wa kiume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonesha kipaji katika kila aina ya elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo. \v 5 Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, na hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme. \p \v 6 Baadhi ya hawa vijana walitoka Yuda: Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. \v 7 Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya: Danieli akamwita jina Belteshaza, Hanania akamwita jina Shadraki, Mishaeli akamwita jina Meshaki, na Azaria akamwita jina Abednego. \p \v 8 Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajinajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii. \v 9 Basi Mungu alikuwa amemfanya huyo mkuu wa maafisa kuonesha upendeleo na huruma kwa Danieli. \v 10 Lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.” \p \v 11 Ndipo Danieli akamwambia mlinzi aliyeteuliwa na huyo mkuu wa maafisa kuwasimamia Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria, \v 12 “Tafadhali wajaribu watumishi wako kwa siku kumi. Usitupe chochote ila nafaka na mboga za majani\f + \fr 1:12 \fr*\ft yaani \ft*\fqa zeroimu \fqa*\ft kwa Kiebrania; ina maana ya aina za ngano na shayiri, na jamii ya kunde kama maharagwe, dengu, choroko, na zingine\ft*\f* tule, na maji ya kunywa. \v 13 Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.” \v 14 Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi. \p \v 15 Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri kuliko yeyote kati ya vijana waliokula chakula cha mfalme. \v 16 Hivyo mlinzi wao akaondoa chakula chao na divai yao waliopangiwa kula na kunywa, akawapa nafaka na mboga za majani badala yake. \p \v 17 Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto. \p \v 18 Mwisho wa muda uliowekwa na mfalme ili kuwaingiza kwake, mkuu wa maafisa akawaleta mbele ya Mfalme Nebukadneza. \v 19 Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme. \v 20 Katika kila jambo la hekima na ufahamu kuhusu kile mfalme alichowauliza, aliwapata kuwa bora mara kumi zaidi ya waganga na wasihiri wote katika ufalme wake wote. \p \v 21 Naye Danieli akabaki huko hadi mwaka wa kwanza wa utawala wa Mfalme Koreshi. \c 2 \s1 Ndoto ya Nebukadneza \p \v 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala. \v 2 Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi, na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia na kusimama mbele ya mfalme, \v 3 akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.” \p \v 4 Ndipo wanajimu wakamjibu mfalme kwa lugha ya Kiaramu\f + \fr 2:4 \fr*\ft Kutoka hapa hadi \+xt Danieli 7:28,\+xt* mwandishi aliandika na Kiaramu.\ft*\f*, “Ee mfalme, uishi milele! Waambie watumishi wako hiyo ndoto, nasi tutaifasiri.” \p \v 5 Mfalme akawajibu wanajimu, “Nimeamua hivi kwa uthabiti: Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu ilikuwa ipi na kuifasiri, mtakatwa vipande vipande, na nyumba zenu zitafanywa kuwa vifusi. \v 6 Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuifasiri, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.” \p \v 7 Wakajibu kwa mara nyingine, “Mfalme na awaambie watumishi wake ndoto yake, nasi tutaifasiri.” \p \v 8 Ndipo mfalme akajibu, “Nina hakika kuwa mnajaribu kupata muda zaidi, kwa sababu mnatambua kuwa nimeamua hivi kwa uthabiti: \v 9 Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu, ipo adhabu moja tu kwenu. Mmepanga njama kuniambia habari za kunipotosha na mambo maovu, mkitumaini kwamba hali itabadilika. Hivyo basi, niambieni hiyo ndoto, nami nitajua kuwa mwaweza kunifasiria.” \p \v 10 Wanajimu wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu duniani ambaye anaweza kufanya analotaka mfalme! Vilevile, hakuna mfalme, hata awe mkuu na mwenye uweza namna gani, aliyeuliza kitu kama hicho kwa mganga, au kwa msihiri, wala kwa mnajimu yeyote. \v 11 Anachouliza mfalme ni kigumu mno. Hakuna yeyote awezaye kumfunulia mfalme isipokuwa miungu, nao hawaishi miongoni mwa wanadamu.” \p \v 12 Jambo hili lilimkasirisha na kumghadhibisha mfalme mno, hata kuagiza kuuawa kwa wenye hekima wote wa Babeli. \v 13 Hivyo amri ikatolewa ya kuwaua wenye hekima, nao watu wakatumwa kuwatafuta Danieli na rafiki zake ili wawaue. \p \v 14 Arioko, mkuu wa askari wa walinzi wa mfalme, alipokuwa ameenda kuwaua wenye hekima wa Babeli, Danieli akazungumza naye kwa hekima na busara. \v 15 Akamuuliza huyo afisa wa mfalme, “Kwa nini mfalme ametoa amri kali hivyo?” Ndipo Arioko akamweleza Danieli jambo hilo. \v 16 Basi Danieli akawaendea mfalme, akamwomba ampe muda ili aweze kumfasiria ile ndoto. \p \v 17 Ndipo Danieli akarudi nyumbani mwake na kuwaeleza rafiki zake Hanania, Mishaeli na Azaria jambo hilo. \v 18 Aliwasihi waombe rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hii, ili yeye na rafiki zake wasije wakauawa pamoja na wenye hekima wengine wa Babeli. \v 19 Wakati wa usiku, lile fumbo lilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Ndipo Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni, \v 20 akasema: \q1 “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; \q2 hekima na uweza ni vyake. \q1 \v 21 Yeye hubadili nyakati na majira; \q2 huwaweka wafalme na kuwaondoa. \q1 Huwapa hekima wenye hekima, \q2 na maarifa wenye ufahamu. \q1 \v 22 Hufunua siri na mambo yaliyofichika; \q2 anajua yale yaliyo gizani, \q2 nayo nuru hukaa kwake. \q1 \v 23 Ninakushukuru na kukuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu: \q2 Umenipa hekima na uwezo; \q1 umenijulisha kile tulichokuomba, \q2 umetujulisha ndoto ya mfalme.” \s1 Danieli aifasiri ndoto \p \v 24 Ndipo Danieli akamwendea Arioko, ambaye mfalme alikuwa amemteua kuwaua wenye hekima wa Babeli, akamwambia, “Usiwaue wenye hekima wa Babeli. Nipeleke kwa mfalme, nami nitamfasiria ndoto yake.” \p \v 25 Arioko akampeleka Danieli kwa mfalme mara moja na kumwambia, “Nimempata mtu miongoni mwa watu wa uhamisho kutoka Yuda ambaye anaweza kumwambia mfalme maana ya ndoto yake.” \p \v 26 Mfalme akamuuliza Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza), “Je, unaweza kuniambia nilichoona katika ndoto yangu na kuifasiri?” \p \v 27 Danieli akajibu, “Hakuna mwenye hekima, msihiri, mganga au mwaguzi anayeweza kumweleza mfalme siri aliyouliza, \v 28 lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri. Amemwonesha Mfalme Nebukadneza kitakachotokea siku zijazo. Ndoto yako na maono yaliyopita mawazoni mwako ulipokuwa umelala kitandani mwako ni haya: \p \v 29 “Ee mfalme, ulipokuwa umelala kitandani, yalikujia mawazo kuhusu mambo yatakayotokea baadaye, naye mfunuaji wa siri akakuonesha ni kitu gani kitakachotokea. \v 30 Kwangu mimi, nimefunuliwa siri hii, si kwa sababu nina hekima kubwa kuliko watu wengine wanaoishi, bali ili wewe, ee mfalme, upate kujua tafsiri, na ili uweze kuelewa kile kilichopita mawazoni mwako. \p \v 31 “Ee mfalme, ulitazama, na mbele yako ilisimama sanamu kubwa mno, iliyong’aa kupita kiasi na yenye kutisha kwa mwonekano wake. \v 32 Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi; kifua chake na mikono yake vilikuwa vya fedha; tumbo lake na mapaja yake vilikuwa vya shaba; \v 33 miguu yake ilikuwa ya chuma; na nyayo zake zilikuwa chuma na sehemu nyingine udongo uliochomwa. \v 34 Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo, na kuivunja. \v 35 Ndipo ile chuma, ule udongo, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja, na vikawa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote. \p \v 36 “Hii ndio ilikuwa ndoto, nasi sasa tutamfasiria mfalme. \v 37 Ee mfalme, wewe ni mfalme wa wafalme. Mungu wa mbinguni amekupa wewe utawala, uweza, nguvu, na utukufu. \v 38 Mikononi mwako amewaweka wanadamu, wanyama wa kondeni, na ndege wa angani. Popote wanapoishi, amekufanya wewe kuwa mtawala wa hao wote. Wewe ndiwe kile kichwa cha dhahabu. \p \v 39 “Baada yako, ufalme mwingine utainuka, ulio dhaifu kuliko wako. Baadaye utafuata ufalme wa tatu, ule wa shaba, nao utaitawala dunia yote. \v 40 Hatimaye kutakuwako na ufalme wa nne, wenye nguvu kama chuma, kwa maana chuma huvunja na kupondaponda kila kitu; kama vile chuma ivunjavyo vitu vipande vipande, ndivyo ufalme huo utakavyopondaponda na kuvunjavunja nyingine zote. \v 41 Kama ulivyoona nyayo na vidole, sehemu moja vikiwa vya udongo uliochomwa na sehemu nyingine vya chuma, kadhalika ufalme huu utakuwa umegawanyika; hata hivyo, utakuwa wenye nguvu ya chuma ndani yake kama ulivyoona chuma kikiwa kimechanganywa na udongo. \v 42 Kama vile vidole vyake vya miguu vilikuwa kwa sehemu chuma na kwa sehemu udongo, ndivyo ufalme huo kwa sehemu utakuwa na nguvu na kwa sehemu udhaifu. \v 43 Kama ulivyoona nyayo na vidole, sehemu moja vikiwa vya udongo uliochomwa na sehemu nyingine vya chuma, kadhalika ufalme huu utakuwa umegawanyika; wala hawatabaki wameungana tena, kama vile chuma kisivyoweza kuchanganyikana na udongo. \p \v 44 “Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atauweka ufalme ambao kamwe hautaangamizwa, wala hautaachiwa taifa lingine. Utaziponda zile falme zote na kuzikomesha, bali wenyewe utadumu milele. \v 45 Hii ndiyo maana ya maono ya jiwe lililochongwa kutoka mlimani, lakini si kwa mikono ya mwanadamu, lile jiwe ambalo lilivunja chuma, shaba, udongo, fedha na dhahabu vipande vipande. \p “Mungu Mkuu amemwonesha mfalme kile kitakachotendeka wakati ujao. Ndoto hii ni ya kweli, na tafsiri yake ni ya kuaminika.” \p \v 46 Ndipo Mfalme Nebukadneza akaanguka kifudifudi mbele ya Danieli kumpa heshima, akaagiza wamtolee Danieli sadaka na uvumba. \v 47 Mfalme akamwambia Danieli, “Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, na mfunuaji wa siri zote, kwa maana umeweza kufunua siri hii.” \p \v 48 Ndipo mfalme akamweka Danieli nafasi ya juu, na kumpa zawadi nyingi tele. Akamfanya mtawala wa jimbo lote la Babeli, na kumweka kuwa mkuu wa wenye hekima wote. \v 49 Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli, mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa mfalme. \c 3 \s1 Sanamu ya dhahabu na tanuru la moto \p \v 1 Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitini\f + \fr 3:1 \fr*\ft Dhiraa sitini ni sawa na mita 27.\ft*\f*, na upana wa dhiraa sita\f + \fr 3:1 \fr*\ft Dhiraa sita ni sawa na mita 2.7.\ft*\f*, akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la Babeli. \v 2 Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. \v 3 Basi wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wote wa jimbo wakakusanyika ili kuizindua sanamu ile Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha, nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu. \p \v 4 Ndipo mpiga mbiu akatangaza kwa sauti kubwa, “Enyi watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha, hili ndilo mnaloamriwa kulifanya: \v 5 Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari, na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima msujudu na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza ameisimamisha. \v 6 Mtu ambaye hataanguka chini na kuiabudu sanamu hiyo, atatupwa saa hiyo hiyo ndani ya tanuru linalowaka moto.” \p \v 7 Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari, na aina zote za sauti za ala za uimbaji, watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha wakasujudu na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. \p \v 8 Wakati huo baadhi ya Wakaldayo walijitokeza na kuwashtaki Wayahudi. \v 9 Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele! \v 10 Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari, na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima asujudu na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu, \v 11 na kwamba yeyote ambaye hatasujudu na kuiabudu atatupwa saa hiyo hiyo ndani ya tanuru linalowaka moto. \v 12 Lakini wako baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu ya mambo ya jimbo la Babeli, yaani Shadraki, Meshaki na Abednego, ambao hawakujali wewe, ee mfalme. Hawaitumikii miungu yako wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.” \p \v 13 Mfalme Nebukadneza, akiwa amekasirika na mwenye ghadhabu kali, akawaita Shadraki, Meshaki na Abednego. Hivyo watu hawa wakaletwa mbele ya mfalme, \v 14 naye Nebukadneza akawauliza, “Je, ni kweli kwamba ninyi Shadraki, Meshaki na Abednego hamuitumikii miungu yangu wala kuiabudu sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? \v 15 Basi wakati mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za ala za uimbaji, kama mtakuwa tayari kusujudu na kuiabudu hiyo sanamu niliyoitengeneza, vyema sana. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa saa hiyo hiyo ndani ya tanuru linalowaka moto. Naye ni mungu yupi ataweza kuwaokoa ninyi kutoka mkononi mwangu?” \p \v 16 Shadraki, Meshaki na Abednego wakamjibu mfalme, “Ee Nebukadneza, hatuhitaji kujitetea mbele zako kuhusu jambo hili. \v 17 Ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru linalowaka moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, ee mfalme. \v 18 Lakini hata ikiwa hatatuokoa, ee mfalme, tunataka ufahamu kwamba hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.” \p \v 19 Ndipo Nebukadneza akawa na ghadhabu kali sana kwa Shadraki, Meshaki na Abednego, nayo nia yake ikabadilika kwao. Akaagiza tanuru lichochewe moto mara saba kuliko kawaida yake, \v 20 na akawaamuru baadhi ya askari wake wenye nguvu zaidi katika jeshi lake kuwafunga Shadraki, Meshaki na Abednego, na kuwatupa ndani ya tanuru lililowaka moto. \v 21 Hivyo watu hawa walifungwa na kutupwa ndani ya tanuru hilo wakiwa wamevaa majoho yao, suruali, vilemba, na nguo zao nyingine. \v 22 Amri ya mfalme ilikuwa ya haraka sana na tanuru lilikuwa na moto mkali kiasi kwamba miali ya moto iliwaua wale askari waliowapeleka Shadraki, Meshaki na Abednego. \v 23 Watu hawa watatu walianguka ndani ya tanuru hilo la moto wakiwa wamefungwa kwa uthabiti sana. \p \v 24 Ndipo Mfalme Nebukadneza akashangaa, akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake, “Je, hawakuwa watu watatu ambao tuliwafunga na kuwatupa ndani ya moto?” \p Washauri wakajibu, “Hakika, ee mfalme.” \p \v 25 Mfalme akasema, “Tazama! Naona watu wanne wakitembeatembea ndani ya moto; hawajafungwa wala kudhurika, naye mtu yule wa nne anaonekana kama mwana wa miungu.” \p \v 26 Ndipo Nebukadneza akaukaribia mdomo wa lile tanuru lililowaka moto na kuita kwa sauti kuu, “Shadraki, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, tokeni! Njooni hapa!” \p Ndipo Shadraki, Meshaki na Abednego wakatoka ndani ya moto. \v 27 Nao maliwali, wasimamizi, watawala na washauri wa mfalme wakakusanyika kuwazunguka. Waliona kwamba moto haukudhuru miili yao, wala unywele wa vichwa vyao haukuungua, majoho yao hayakuungua, wala hawakuwa na harufu ya moto. \p \v 28 Ndipo Nebukadneza akasema, “Ahimidiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego, ambaye amemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake. Walimtumaini na kukaidi amri ya mfalme, nao wakawa tayari kufa kuliko kutumikia au kuabudu mungu mwingine yeyote isipokuwa Mungu wao. \v 29 Kwa hiyo ninaamuru kwamba watu wa taifa lolote au lugha yoyote watakaosema kitu chochote dhidi ya Mungu wa Shadraki, Meshaki na Abednego wakatwe vipande vipande, na nyumba zao zifanywe kuwa malundo ya kokoto, kwa maana hakuna mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.” \p \v 30 Kisha mfalme akawapandisha vyeo Shadraki, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli. \c 4 \s1 Ndoto ya Nebukadneza ya mti \pmo \v 1 Mfalme Nebukadneza, \pmo Kwa watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha wanaoishi duniani kote: \pmo Mafanikio yawe kwenu sana! \pm \v 2 Ni furaha yangu kuwaambia kuhusu ishara za miujiza na maajabu ambayo Mungu Aliye Juu Sana amenifanyia. \qm1 \v 3 Ishara zake ni kuu kama nini! \qm2 Na maajabu yake yana nguvu kama nini! \qm1 Ufalme wake ni ufalme wa milele; \qm2 enzi yake hudumu kizazi hadi kizazi. \pm \v 4 Mimi, Nebukadneza, nilikuwa nyumbani katika jumba langu la kifalme, nikiishi kwa raha na mafanikio. \v 5 Niliota ndoto iliyoniogopesha. Nilipokuwa nimelala kitandani mwangu, njozi na maono yaliyopita mawazoni mwangu vilinitisha. \v 6 Hivyo nikaagiza kwamba wenye hekima wote wa Babeli waletwe mbele yangu kunifasiria ndoto yangu. \v 7 Waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi walipokuja, niliwaambia ndoto yangu, lakini hawakuweza kunifasiria. \v 8 Mwishoni, Danieli alikuja mbele yangu, nikamweleza hiyo ndoto. (Danieli anaitwa Belteshaza, kwa jina la mungu wangu, nayo roho ya miungu mitakatifu inakaa ndani yake.) \pm \v 9 Nikasema, “Belteshaza, mkuu wa waganga, ninajua kuwa roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako, wala hakuna siri iliyo ngumu kwako. Hii ndiyo ndoto yangu, nifasirie. \v 10 Haya ndio maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana. \v 11 Mti ule ulikua, ukawa mkubwa na wenye nguvu, nayo ncha yake ikagusa anga; ulionekana hadi miisho ya dunia. \v 12 Majani yake yalikuwa ya kupendeza, matunda yake yalikuwa mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Chini ya kivuli chake wanyama wa kondeni walipata hifadhi, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Kila kiumbe kililishwa kutokana na mti huo. \pm \v 13 “Katika maono niliyoyaona nikiwa nimelala kitandani mwangu, nilitazama, na mbele yangu nikaona mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni. \v 14 Akaita kwa sauti kubwa: ‘Kateni mti huu, myafyeke matawi yake; yaondoeni majani yake na kuyatawanya matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake, na ndege waondoke kutoka matawi yake. \v 15 Lakini kiacheni kisiki na mizizi yake, kikiwa kimefungwa kwa chuma na shaba, kibaki ardhini, kwenye majani ya kondeni. \pm “ ‘Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, naye aachwe aishi pamoja na wanyama miongoni mwa mimea ya dunia. \v 16 Akili yake na ibadilishwe kutoka ile ya mwanadamu, na apewe akili ya mnyama, hadi nyakati saba zipite juu yake. \pm \v 17 “ ‘Uamuzi huu umetangazwa na wajumbe; watakatifu, wametangaza hukumu ili walio hai wajue kuwa Aliye Juu Sana ndiye anayetawala katika falme zote za dunia, naye humpa amtakaye, na kumtawaza juu yake hata yeye aliye mnyonge sana miongoni mwa wanadamu.’ \pm \v 18 “Hii ndiyo ndoto niliyoipata mimi, Mfalme Nebukadneza. Sasa Belteshaza, niambie maana yake, kwa maana hakuna hata mmoja wa wenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunifasiria. Bali wewe unaweza, kwa sababu roho ya miungu mitakatifu iko ndani yako.” \s1 Danieli anaifasiri ndoto \pm \v 19 Ndipo Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza) alipofadhaika sana kwa muda, nayo mawazo yake yakamtia hofu. Basi mfalme akasema, “Belteshaza, usiruhusu ndoto wala maana yake kukutia hofu.” \pm Belteshaza akajibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii ingewahusu adui zako, na maana yake iwahusu watesi wako! \v 20 Mti uliouona, uliokua ukawa mkubwa na wenye nguvu, nayo ncha yake ikagusa anga na kuonekana duniani kote, \v 21 ukiwa na majani ya kupendeza na matunda mengi, ukitoa chakula kwa wote, na ukiwapa hifadhi wanyama wa kondeni, na kuwa mahali pa viota katika matawi yake kwa ajili ya ndege wa angani: \v 22 Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu; nao ukuu wako umekua hadi kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea hadi miisho ya dunia. \pm \v 23 “Ee mfalme, wewe ulimwona mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akasema, ‘Ukateni mti na kuuangamiza, lakini kiacheni kisiki kikiwa kimefungwa kwa chuma na shaba, kwenye majani ya kondeni, wakati mizizi yake inabaki ardhini. Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, mwacheni aishi kama wanyama pori hadi nyakati saba zipite juu yake.’ \pm \v 24 “Ee mfalme, hii ndiyo tafsiri, na hii ni amri ya Aliye Juu Sana aliyoitoa dhidi ya bwana wangu mfalme: \v 25 Wewe utafukuzwa mbali na wanadamu, nawe utaishi pamoja na wanyama pori; utakula nyasi kama ng’ombe, na kuloana kwa umande wa mbinguni. Nyakati saba zitapita hadi utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala katika falme zote za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye. \v 26 Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejeshwa kwako utakapokubali kwamba Mbingu ndizo hutawala. \v 27 Kwa hiyo, ee mfalme, uwe radhi kupokea ushauri wangu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako na uwe na huruma kwa waliodhulumiwa. Hivyo itawezekana baada ya hayo, mafanikio yako yataendelea.” \s1 Ndoto inatimia \pm \v 28 Haya yote yalimpata Mfalme Nebukadneza. \v 29 Miezi kumi na mbili baadaye, mfalme alipokuwa akitembea juu ya paa la jumba la kifalme la Babeli, \v 30 alisema, “Je, huu si Babeli mji mkuu nilioujenga uwe makao ya kifalme, kwa uwezo wangu mkubwa, na kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?” \pm \v 31 Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya ufalme yameondolewa kwako. \v 32 Utafukuzwa mbali na wanadamu, ukaishi pamoja na wanyama pori, na utakula nyasi kama ng’ombe. Nyakati saba zitapita juu yako, hadi utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala katika falme zote za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye.” \pm \v 33 Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala nyasi kama ng’ombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni, hadi nywele zake zikakua kama manyoya ya tai, nazo kucha zake kama makucha ya ndege. \b \pm \v 34 Mwisho wa wakati huo, mimi Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele. \qm1 Utawala wake ni utawala wa milele; \qm2 ufalme wake hudumu kizazi hadi kizazi. \qm1 \v 35 Mataifa yote ya dunia \qm2 yanahesabiwa kuwa si kitu. \qm1 Hufanya kama atakavyo \qm2 kwa majeshi ya mbinguni, \qm2 na kwa mataifa ya dunia. \qm1 Hakuna anayeweza kuuzuia mkono wake \qm2 au kumwambia, “Umefanya nini wewe?” \pm \v 36 Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, nikarudishiwa heshima yangu na fahari yangu kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme, hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni. \v 37 Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu anachofanya ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao wanaoenda kwa kiburi anaweza kuwashusha. \c 5 \s1 Maandishi ukutani \p \v 1 Mfalme Belshaza aliandaa karamu kubwa kwa ajili ya wakuu wake elfu moja, na akanywa mvinyo pamoja nao. \v 2 Belshaza alipokuwa akinywa divai, aliamuru vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekalu huko Yerusalemu viletwe, ili mfalme na wakuu wake, pamoja na wake zake na masuria wake wapate kuvinywea. \v 3 Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, pamoja na wake zake na masuria wake wakavinywea. \v 4 Walipokuwa wakinywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu na fedha, ya shaba, chuma, miti na mawe. \p \v 5 Ghafula vidole vya mkono wa mwanadamu vilitokea na kuandika juu ya chokaa ya ukuta, karibu na kinara cha taa ndani ya jumba la mfalme. Mfalme akatazama kitanga kilivyokuwa kikiandika. \v 6 Uso wa mfalme ukageuka rangi, naye akaogopa sana, kiasi kwamba magoti yake yaligongana na miguu yake ikalegea. \p \v 7 Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waaguzi waletwe, naye akawaambia hao wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.” \p \v 8 Ndipo wenye hekima wote wa mfalme wakaingia, lakini hawakuweza kusoma yale maandishi wala kumwambia mfalme maana yake. \v 9 Basi Mfalme Belshaza akazidi kujawa na hofu, na uso wake ukageuka rangi zaidi. Wakuu wake wakapigwa na bumbuazi. \p \v 10 Malkia\f + \fr 5:10 \fr*\ft au \ft*\fqa mama malkia \fqa*\ft au \ft*\fqa mamaye mfalme\fqa*\f* aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi hivyo! \v 11 Yuko mtu katika ufalme wako mwenye roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, naam, mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi. \v 12 Mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza, alionekana kuwa na akili nyepesi, maarifa na ufahamu, pia uwezo wa kufasiri ndoto, kueleza mafumbo, na kutatua matatizo magumu. Mwite Danieli, naye atakuambia maana ya haya maandishi.” \p \v 13 Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamuuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Yuda? \v 14 Nimesikia kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na kwamba una ufahamu, akili na hekima ya pekee. \v 15 Watu wenye hekima na wasihiri waliletwa mbele yangu ili kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, lakini hawakuweza kunifafanulia. \v 16 Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu katika ufalme.” \p \v 17 Ndipo Danieli akamjibu mfalme, “Unaweza kubaki na zawadi zako mwenyewe na kumpa mtu mwingine thawabu zako. Hata hivyo, nitasoma maandishi kwa mfalme na kumwambia maana yake. \p \v 18 “Ee mfalme, Mungu Aliye Juu Sana alimpa baba yako Nebukadneza utawala, ukuu, utukufu na fahari. \v 19 Kwa sababu ya ukuu aliompa baba yako, watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha walimhofu na kumwogopa. Wale ambao mfalme alitaka kuwaua, aliwaua; wale aliotaka kuwaacha hai, aliwaacha hai; wale aliotaka kuwapandisha cheo, aliwapandisha; aliotaka kuwashusha, aliwashusha. \v 20 Lakini moyo wake ulipokuwa na majivuno na kuwa mgumu kwa kiburi, aliondolewa kutoka kwa kiti chake cha ufalme na kuvuliwa utukufu wake. \v 21 Akafukuzwa mbali na wanadamu na kupewa akili ya mnyama, akaishi pamoja na punda-mwitu; akala majani kama ng’ombe, nao mwili wake ukaloweshwa kwa umande wa mbingu, hadi alipotambua kwamba Mungu Aliye Juu Sana ndiye mtawala katika falme zote za wanadamu, na kwamba humtawaza juu yao yeyote amtakaye. \p \v 22 “Lakini wewe mwanawe, ee Belshaza, hukujinyenyekeza, ingawa ulifahamu haya yote. \v 23 Badala yake, umejiinua dhidi ya Bwana wa mbingu. Uliletewa vikombe vya Hekalu lake, nawe na wakuu wako, pamoja na wake zako na masuria wako mlivitumia kwa kunywea divai. Uliisifu miungu ya fedha na dhahabu, ya shaba, chuma, miti na mawe, miungu ambayo haiwezi kuona, au kusikia wala kufahamu. Lakini hukumheshimu Mungu ambaye anaushikilia uhai wako na njia zako zote mkononi mwake. \v 24 Kwa hiyo ameutuma mkono ule ulioandika maneno. \p \v 25 “Haya ndio maneno yaliyoandikwa: \pc \sc mene, mene,\sc* \pc \sc tekeli, na peresi\sc* \p \v 26 “Hii ndiyo maana ya maneno haya: \p “\tl Mene\tl*: Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha. \p \v 27 “\tl Tekeli\tl*: Wewe umepimwa katika mizani na kuonekana umepungua. \p \v 28 “\tl Peresi\tl*: Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.” \p \v 29 Kwa amri ya Belshaza, Danieli akavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni, tena akatangazwa kuwa mtawala wa tatu katika ufalme. \p \v 30 Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa, \v 31 naye Dario Mmedi akanyakua ufalme akiwa na miaka sitini na mbili. \c 6 \s1 Danieli katika tundu la simba \p \v 1 Ilimpendeza Dario kuteua wakuu mia moja na ishirini kutawala katika ufalme wake wote, \v 2 pamoja na wasimamizi watatu juu yao, Danieli akiwa mmoja wao. Wakuu walitoa hesabu kwa wasimamizi hao ili mfalme asipate hasara. \v 3 Basi Danieli alijidhihirisha miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee, hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote. \v 4 Walipofahamu hilo, wasimamizi na wakuu wakajaribu kutafuta sababu za kumshtaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu, wala hakupatikana na upotovu au uzembe. \v 5 Mwishoni watu hawa wakasema, “Kamwe hatutapata msingi wa mashtaka dhidi ya huyu Danieli, isipokuwa iwe inahusiana na sheria ya Mungu wake.” \p \v 6 Basi wasimamizi na wakuu wakaingia kwa mfalme kama kikundi, wakasema, “Ee Mfalme Dario, uishi milele! \v 7 Wasimamizi wa ufalme, wasaidizi, wakuu, washauri na watawala wote wamekubaliana kwamba mfalme atoe sheria na kukazia amri kuwa yeyote atakayetoa dua kwa mungu au mwanadamu katika muda huu wa siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, ee mfalme, atupwe ndani ya tundu la simba. \v 8 Sasa, ee mfalme, toa amri na uiandike ili isiweze kubadilishwa: kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.” \v 9 Hivyo Mfalme Dario akaiweka amri hiyo katika maandishi. \p \v 10 Basi Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alienda nyumbani mwake kwenye chumba chake cha ghorofani, ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Akapiga magoti na kuomba mara tatu kwa siku, akimshukuru Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya awali. \v 11 Ndipo watu hawa wakaenda kama kikundi na kumkuta Danieli akiomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada. \v 12 Basi wakaenda kwa mfalme na kusema naye kuhusu amri ya mfalme: “Je, hukutangaza amri kwamba kwa muda huu wa siku thelathini zijazo mtu ambaye atamwomba mungu au mwanadamu yeyote isipokuwa wewe, ee mfalme, angetupwa ndani ya tundu la simba?” \p Mfalme akajibu, “Amri ndivyo ilivyo, kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.” \p \v 13 Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa mahamisho kutoka Yuda, hakuheshimu, ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Bado anaomba mara tatu kwa siku.” \v 14 Mfalme aliposikia hili, akahuzunika mno. Akakusudia kumwokoa Danieli, hivyo akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua. \p \v 15 Ndipo wale watu wakamwendea mfalme kama kikundi na kumwambia, “Ee mfalme, kumbuka kwamba kulingana na sheria ya Wamedi na Waajemi, hakuna amri wala sheria ambayo mfalme ameitoa inayoweza kubadilishwa.” \p \v 16 Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!” \p \v 17 Jiwe likaletwa na kuwekwa kwenye mlango wa tundu, naye mfalme akalitia muhuri kwa pete yake mwenyewe pamoja na kwa pete za wakuu wake, ili hali ya Danieli isiweze kubadilishwa. \v 18 Kisha mfalme akarudi kwenye jumba lake la kifalme, naye usiku kucha hakuweza kula wala kutumia viburudisho alivyoletewa, na hakuweza kulala. \p \v 19 Asubuhi na mapema, mfalme akaondoka na kuharakisha kwenda kwenye tundu la simba. \v 20 Alipokaribia lile tundu, mfalme akamwita Danieli kwa sauti ya uchungu: “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako, unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa kwa simba?” \p \v 21 Danieli akajibu, “Ee mfalme, uishi milele! \v 22 Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.” \p \v 23 Basi Mfalme akafurahi mno, akatoa amri Danieli atolewe kutoka kwa lile tundu. Danieli alipotolewa kutoka kwa lile tundu, hakukutwa na jeraha lolote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake. \p \v 24 Kwa amri ya mfalme, wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote. \p \v 25 Kisha Mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha duniani kote: \pmo “Mafanikio yawe kwenu sana! \pm \v 26 “Natoa amri hii, kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu, lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli. \qm1 “Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai, \qm2 naye hudumu milele. \qm1 Ufalme wake hautaangamizwa, \qm2 nao utawala wake hauna mwisho. \qm1 \v 27 Huponya na kuokoa; \qm2 hufanya ishara na maajabu \qm2 mbinguni na duniani. \qm1 Amemwokoa Danieli \qm2 kutoka nguvu za simba.” \p \v 28 Hivyo Danieli akastawi wakati wa utawala wa Dario, na utawala wa Koreshi Mwajemi. \c 7 \s1 Ndoto ya Danieli ya wanyama wanne \p \v 1 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli, Danieli aliota ndoto, nayo maono yakapita mawazoni mwake alipokuwa amelala kitandani mwake. Akayaandika mambo aliyoyaona katika ndoto yake. \p \v 2 Danieli akasema: “Katika maono yangu usiku nilitazama, na hapo mbele yangu kulikuwa na pepo kutoka pande nne za mbingu, zikivuruga bahari kuu. \v 3 Wanyama wanne wakubwa, kila mmoja tofauti na mwenzake, wakajitokeza kutoka bahari. \p \v 4 “Mnyama wa kwanza alifanana na simba, naye alikuwa na mabawa ya tai. Nikatazama hadi mabawa yake yalipong’olewa, naye akainuliwa katika nchi, akasimama kwa miguu miwili kama mwanadamu, naye akapewa moyo wa binadamu. \p \v 5 “Hapo mbele yangu kulikuwa na mnyama wa pili, aliyefanana na dubu. Upande wake mmoja alikuwa ameinuka, na alikuwa na mbavu tatu katika kinywa chake kati ya meno yake. Akaambiwa, ‘Amka, ule nyama, ushibe!’ \p \v 6 “Baada ya huyo, nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama mwingine, aliyefanana na chui. Juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege. Mnyama huyu alikuwa na vichwa vinne, naye akapewa mamlaka ya kutawala. \p \v 7 “Baada ya huyo, katika maono yangu usiku nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama wa nne, mwenye kutisha na kuogofya, tena mwenye nguvu nyingi. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; akapondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chini ya nyayo zake chochote kilichosalia. Alikuwa tofauti na wanyama wote waliotangulia, naye alikuwa na pembe kumi. \p \v 8 “Nilipokuwa nikifikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni ziling’olewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno. \p \v 9 “Nilipoendelea kutazama, \q1 “viti vya utawala vikawekwa, \q2 naye Mzee wa Siku akaketi. \q1 Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji; \q2 nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. \q1 Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka miali ya moto, \q2 nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto. \q1 \v 10 Mto wa moto ulikuwa unatiririka, \q2 ukipita mbele yake. \q1 Maelfu elfu wakamhudumia; \q2 kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake. \q1 Mahakama ikakaa kuhukumu, \q2 na vitabu vikafunguliwa. \p \v 11 “Kisha nikaendelea kutazama kwa sababu ya yale maneno ya majivuno yaliyosemwa na ile pembe. Nikaendelea kuangalia hadi yule mnyama alipouawa, na mwili wake ukaharibiwa na kutupwa katika ule moto uliowaka. \v 12 (Wanyama wengine walikuwa wamevuliwa mamlaka yao, lakini waliruhusiwa kuishi kwa muda.) \p \v 13 “Katika maono yangu ya usiku nilitazama, na mbele yangu nikamwona mtu kama Mwana wa Adamu, akija pamoja na mawingu ya mbinguni. Akamkaribia huyo Mzee wa Siku, na akaongozwa mbele zake. \v 14 Akapewa mamlaka, utukufu na ufalme wenye nguvu; nao watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha wakamwabudu. Utawala wake ni utawala wa milele ambao hautapita, nao ufalme wake ni ule ambao kamwe hautaangamizwa. \s1 Tafsiri ya ndoto ya hao wanyama \p \v 15 “Mimi Danieli nilipata mahangaiko rohoni, nayo maono yale yaliyopita ndani ya mawazo yangu yalinisumbua. \v 16 Nikamkaribia mmoja wa wale waliosimama pale, nikamuuliza maana halisi ya haya yote. \p “Basi akaniambia na kunipa tafsiri ya vitu hivi: \v 17 ‘Hao wanyama wanne wakubwa ni falme nne zitakazoinuka duniani. \v 18 Lakini watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana watapokea ufalme na kuumiliki milele: naam, milele na milele.’ \p \v 19 “Kisha nilitaka kufahamu maana ya kweli ya mnyama yule wa nne, aliyekuwa tofauti na wale wengine wote, tena wa kutisha sana, na meno yake ya chuma na makucha ya shaba: mnyama ambaye alipondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chochote kilichosalia. \v 20 Pia mimi nilitaka kujua kuhusu zile pembe kumi juu ya kichwa chake, na pia kuhusu ile pembe nyingine iliyojitokeza, ambayo mbele yake zile tatu za mwanzoni zilianguka, ile pembe ambayo ilionekana kuvutia macho kuliko zile nyingine, na ambayo ilikuwa na macho na kinywa kilichonena kwa majivuno. \v 21 Nilipoendelea kutazama, pembe hii ilikuwa inapigana vita dhidi ya watakatifu na kuwashinda, \v 22 hadi huyo Mzee wa Siku alipokuja na kutamka hukumu kwa kuwapa ushindi watakatifu wa Yeye Aliye Juu Sana, na wakati ukawadia walipoumiliki ufalme. \p \v 23 “Alinipa maelezo haya: ‘Mnyama wa nne ni ufalme wa nne ambao utatokea duniani. Utakuwa tofauti na falme nyingine zote, nao utaharibu dunia nzima, ukiikanyaga chini na kuipondaponda. \v 24 Zile pembe kumi ni wafalme kumi watakaotokana na ufalme huu. Baada yao mfalme mwingine atainuka, ambaye atakuwa tofauti na wale waliotangulia, naye atawaangusha wafalme watatu. \v 25 Atanena maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu Sana na kuwatesa watakatifu wake, huku akijaribu kubadili majira na sheria. Watakatifu watatiwa chini ya mamlaka yake kwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati\f + \fr 7:25 \fr*\ft au \ft*\fqa chini ya mamlaka yake kwa mwaka mmoja, miaka miwili, na nusu mwaka\fqa*\f*. \p \v 26 “ ‘Lakini mahakama itakaa kuhukumu, nayo mamlaka yake yataondolewa na kuangamizwa kabisa milele. \v 27 Ndipo ufalme, mamlaka na ukuu wa falme chini ya mbingu yote zitakabidhiwa kwa watakatifu, watu wa Yeye Aliye Juu Sana. Ufalme wake utakuwa ufalme wa milele, nao watawala wote watamwabudu na kumtii yeye.’ \p \v 28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Mimi Danieli nilitaabika sana katika mawazo yangu, nao uso wangu ukabadilika, lakini nililiweka jambo hilo moyoni mwangu.” \c 8 \s1 Maono ya Danieli ya kondoo dume na beberu \p \v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Mfalme Belshaza, mimi Danieli nilipata maono, baada ya maono yaliyokuwa yamenitokea awali. \v 2 Katika maono yangu, nilijiona nikiwa ndani ya ngome ya Shushani katika jimbo la Elamu; katika maono nilikuwa kando ya Mto Ulai\f + \fr 8:2 \fr*\ft huu ni mfereji uliopitia kati ya Shushani\ft*\f*. \v 3 Nikatazama juu, na hapo mbele yangu kulikuwa na kondoo dume mwenye pembe mbili, akiwa amesimama kando ya mto, nazo pembe zake zilikuwa ndefu. Pembe moja ilikuwa ndefu kuliko hiyo nyingine, lakini iliendelea kukua baadaye. \v 4 Nikamtazama yule kondoo dume alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyeweza kusimama mbele yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka nguvu zake. Akafanya kama alivyopenda, naye akawa mkuu. \p \v 5 Nilipokuwa ninatafakari hili, ghafula beberu mwenye pembe moja kubwa katikati ya macho yake alikuja kutoka magharibi, akiruka kasi juu ya dunia yote bila kugusa ardhi. \v 6 Alikuja akimwelekea yule kondoo dume mwenye pembe mbili niliyemwona akisimama kando ya mto, akamshambulia kwa hasira nyingi. \v 7 Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akampiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu; huyo beberu akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu. \v 8 Yule beberu akawa mkubwa sana, lakini katika kilele cha nguvu zake, ile pembe yake ndefu ilivunjika, na mahali pake pakaota pembe nne kubwa kuelekea pande nne za dunia. \p \v 9 Kutoka mojawapo ya zile pembe nne palitokea pembe ndogo, nayo ikaongezeka nguvu kuelekea kusini, na mashariki, na Nchi ya Kupendeza. \v 10 Pembe hiyo ikaendelea kukua hadi kufikia jeshi la mbinguni, nayo ikalitupa baadhi ya nyota za jeshi la angani chini duniani, na kuzikanyaga. \v 11 Pembe hiyo ikajikweza ili iwe kama Mkuu wa hilo jeshi la Mwenyezi Mungu; ikamwondolea Mwenyezi Mungu dhabihu ya kila siku, napo mahali pake patakatifu pakashushwa chini. \v 12 Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mkononi mwake. Pembe hiyo ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini. \p \v 13 Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine, akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie: maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu, na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?” \p \v 14 Akaniambia, “Itachukua jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo mahali patakatifu patawekwa wakfu tena.” \s1 Tafsiri ya maono hayo \p \v 15 Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja aliyefanana na mwanadamu. \v 16 Kisha nikasikia sauti ya mwanadamu kutoka Mto Ulai ikiita, “Jibraili, mwambie mtu huyu maana ya maono haya.” \p \v 17 Alipokuwa akikaribia pale nilipokuwa nimesimama, niliogopa, nikaanguka kifudifudi. Akaniambia, “Mwana wa mwanadamu, fahamu kuwa maono haya yanahusu siku za mwisho.” \p \v 18 Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kunisimamisha wima. \p \v 19 Akaniambia, “Nitakuambia yale yatakayotokea baadaye wakati wa ghadhabu, kwa sababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho ulioamriwa. \v 20 Kondoo dume mwenye pembe mbili ambaye ulimwona anawakilisha wafalme wa Umedi na Uajemi. \v 21 Yule beberu mwenye manyoya mengi ni mfalme wa Uyunani, nayo ile pembe ndefu katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. \v 22 Zile pembe nne zilizoota badala ya ile pembe iliyovunjika zinawakilisha falme nne ambazo zitatokea kutoka taifa lake, lakini hakuna hata mmoja utakaokuwa na nguvu kama ile pembe iliyovunjika. \p \v 23 “Katika sehemu ya mwisho ya utawala wao, waasi watakapokuwa waovu kabisa, atainuka mfalme mwenye uso mkali, aliye stadi wa hila. \v 24 Atakuwa na nguvu nyingi, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe. Atasababisha uharibifu wa kutisha, na atafanikiwa kwa chochote anachofanya. Atawaangamiza watu maarufu na watu watakatifu. \v 25 Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora kuliko wote. Wakati watajisikia kuwa salama, atawaangamiza wengi, na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu. \p \v 26 “Maono kuhusu jioni na asubuhi ambayo umepewa ni kweli, lakini yatie muhuri maono haya, kwa maana yanahusu nyakati za baadaye sana.” \p \v 27 Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaendelea na shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo; sikuweza kuyaelewa. \c 9 \s1 Maombi ya Danieli \p \v 1 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario mwana wa Ahasuero (mzaliwa wa Umedi), ambaye alifanywa mtawala wa ufalme wa Babeli, \v 2 katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, mimi Danieli nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu lililopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. \v 3 Kwa hiyo nikamgeukia Mwenyezi Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, na kuvaa gunia na kujipaka majivu. \p \v 4 Nikamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, na kutubu: \pm “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake, \v 5 tumetenda dhambi na kufanya mabaya. Tumekuwa waovu na tumeasi; tumegeuka mbali na maagizo yako na sheria zako. \v 6 Hatukuwasikiliza watumishi wako manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, wakuu wetu, baba zetu, na watu wote wa nchi. \pm \v 7 “Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini siku hii ya leo tumefunikwa na aibu: watu wa Yuda, na wakaaji wa Yerusalemu, na Waisraeli wote, walio karibu na walio mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa sababu tulikosa uaminifu kwako. \v 8 Ee Mwenyezi Mungu, sisi na wafalme wetu, wakuu wetu na baba zetu tumefunikwa na aibu kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. \v 9 Bwana Mungu wetu ni mwenye rehema na anayesamehe, hata ingawa tumefanya uasi dhidi yake. \v 10 Hatukumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, wala kuzishika sheria alizotupatia kupitia kwa watumishi wake, manabii. \v 11 Israeli wote wamekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. \pm “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. \v 12 Umetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu, kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka kwa Yerusalemu. \v 13 Kama vile ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa kuacha kutenda dhambi na kuisikiliza kweli yake. \v 14 Mwenyezi Mungu hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ni mwenye haki katika kila afanyalo; lakini hata hivyo, hatujamtii. \pm \v 15 “Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu, na kujifanyia Jina linalodumu hadi leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya. \v 16 Ee Bwana, kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako kwa Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka. \pm \v 17 “Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua za mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako angalia kwa huruma ukiwa wa mahali pako patakatifu. \v 18 Ee Mungu, tega sikio, ukasikie; fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi. \v 19 Ee Bwana, sikiliza! Ee Bwana, samehe! Ee Bwana, sikia na ukatende! Kwa ajili yako, Ee Mungu wangu, usikawie, kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa Jina lako.” \s1 Majuma sabini \p \v 20 Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima wake mtakatifu, \v 21 wakati nilipokuwa bado katika maombi, Jibraili, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibu wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. \v 22 Akanielimisha na kuniambia, “Danieli, sasa nimekuja kukupa akili na ufahamu. \v 23 Mara ulipoanza kuomba, jibu lilitolewa, ambalo nimekuja kukupasha habari, kwa maana wewe unapendwa sana. Kwa hiyo, tafakari ujumbe huu na uelewe maono haya: \p \v 24 “Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii, na pia kumpaka mafuta yeye aliye mtakatifu sana. \p \v 25 “Ujue na kuelewa hili: Tangu kutolewa kwa amri ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hadi kuja kwa Mpakwa mafuta, aliye mtawala, kutakuwa na majuma saba, na majuma sitini na mawili. Barabara zitajengwa tena pamoja na mahandaki, lakini katika wakati wa taabu. \v 26 Baada ya majuma sitini na mawili, Mpakwa Mafuta atakatiliwa mbali, wala hatabaki na kitu. Watu wa mtawala atakayekuja watauharibu mji pamoja na mahali patakatifu. Mwisho utakuja kama mafuriko: Vita vitaendelea hadi mwisho, nao ukiwa umeamriwa. \v 27 Mtawala huyo atathibitisha agano na watu wengi kwa juma moja. Katikati ya juma hilo atakomesha dhabihu na sadaka. Mahali pa dhabihu katika Hekalu, atasimamisha chukizo la uharibifu, hadi mwisho ulioamriwa utakapomiminwa juu yake yeye aletaye uharibifu.” \c 10 \s1 Maono ya Danieli kuhusu mtu \p \v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli, nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono. \p \v 2 Wakati huo, mimi Danieli nikaomboleza kwa majuma matatu. \v 3 Sikula chakula kizuri; nyama wala divai havikugusa midomo yangu; nami sikujipaka mafuta kamwe hadi majuma matatu yalipotimia. \p \v 4 Siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilikuwa nimesimama kwenye ukingo wa mto mkubwa Hidekeli\f + \fr 10:4 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Tigrisi\fqa*\f*. \v 5 Nikatazama juu, na mbele yangu palikuwa na mtu aliyevaa mavazi ya kitani na mshipi wa dhahabu safi kutoka Ufazi kiunoni mwake. \v 6 Mwili wake ulikuwa kama zabarajadi safi, uso wake kama radi, macho yake kama miali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mng’ao wa shaba iliyosuguliwa, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu. \p \v 7 Ni mimi Danieli peke yangu niliyeona hayo maono; watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona, lakini waligubikwa na hofu kuu, hata wakakimbia na kujificha. \v 8 Kwa hiyo niliachwa peke yangu, nikitazama maono hayo makubwa; sikubakiwa na nguvu, na rangi ya uso wangu ikabadilika kama aliyekufa, nikakosa nguvu. \v 9 Kisha nikamsikia akisema, nami nilipokuwa nikimsikiliza, nikapatwa na usingizi mzito, nikalala kifudifudi. \p \v 10 Mkono ulinigusa, ukaninyanyua na kuniweka magotini, mikono yangu ikishika chini, huku nikiwa bado ninatetemeka. \v 11 Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayoenda kunena nawe; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka. \p \v 12 Ndipo akaendelea kusema, “Danieli, usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. \v 13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa malaika wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi. \v 14 Sasa nimekuja kukuelezea mambo yatakayowatokea watu wako wakati ujao, kwa maana maono hayo yanahusu wakati ambao haujaja bado.” \p \v 15 Alipokuwa akiniambia haya, nilisujudu, uso wangu ukigusa chini, nikawa bubu. \v 16 Ndipo mmoja aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa midomo yangu, nami nikafungua kinywa changu, nikaanza kunena. Nikamwambia yule aliyesimama mbele yangu, “Nimepatwa na huzuni kubwa kwa sababu ya maono haya, bwana wangu, nami nimeishiwa nguvu. \v 17 Bwana wangu, mimi mtumishi wako nitawezaje kuzungumza na wewe? Nguvu zangu zimeniishia, hata ninashindwa kupumua.” \p \v 18 Tena yule aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa na kunitia nguvu. \v 19 Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa; jipe nguvu.” \p Alipozungumza nami, nilipata nguvu, nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.” \p \v 20 Kwa hiyo akasema, “Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa hivi nitarudi kupigana dhidi ya mkuu wa Uajemi, nami nikienda, mkuu wa Uyunani atakuja. \v 21 Lakini kwanza nitakuambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Kweli. (Hakuna hata mmoja anayenisaidia dhidi yao isipokuwa Mikaeli, mkuu wenu. \c 11 \nb \v 1 Nami katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario Mmedi, nilisimama kumsaidia na kumlinda.) \s1 Wafalme wa kusini na kaskazini \p \v 2 “Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme wengine watatu watatokea Uajemi. Kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi ya ufalme wa Uyunani. \v 3 Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, atakayetawala kwa nguvu nyingi, na kufanya anavyopenda. \v 4 Baada ya kujitokeza, himaya yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautaenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizokuwa nazo, kwa sababu himaya yake itang’olewa na kupewa wengine. \p \v 5 “Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja wa majemadari wake atakuwa na nguvu zaidi yake, naye atatawala ufalme wake mwenyewe kwa nguvu nyingi. \v 6 Baada ya miaka kadhaa, wataungana. Binti ya mfalme wa Kusini ataolewa kwa mfalme wa Kaskazini ili kuimarisha mapatano, lakini nguvu za huyo binti hazitadumu; hata mfalme hatadumu wala nguvu zake. Katika siku hizo atafukuzwa, pamoja na hao wasindikizaji wake wa kifalme, na baba yake, na yeyote aliyemuunga mkono. \p \v 7 “Mmoja kutoka jamaa ya huyo binti atainuka na kuchukua nafasi yake. Atashambulia majeshi ya mfalme wa Kaskazini na kuingia katika ngome yake; atapigana dhidi yao, naye atashinda. \v 8 Tena ataitwaa miungu yao, vinyago vyao vya chuma, na vitu vyao vya thamani vya fedha na dhahabu, na kuvichukua hadi Misri. Kwa miaka kadhaa atamwacha mfalme wa Kaskazini bila kumsumbua. \v 9 Kisha mfalme wa Kaskazini atashambulia nchi ya mfalme wa Kusini, lakini atarudi hadi kwenye nchi yake mwenyewe. \v 10 Wana wa mfalme wa Kaskazini watajiandaa kwa vita na kukusanya jeshi kubwa, ambalo litafagia nchi kama mafuriko yasiyozuilika, na kuendelea na vita hadi kwenye ngome ya mfalme wa Kusini. \p \v 11 “Kisha mfalme wa Kusini atatoka kwa ghadhabu na kupigana dhidi ya mfalme wa Kaskazini, ambaye atakusanya jeshi kubwa, lakini litashindwa. \v 12 Jeshi litakapotekwa, mfalme wa Kusini atajawa na kiburi, na atachinja maelfu mengi; hata hivyo hatabaki na ushindi. \v 13 Kwa maana mfalme wa Kaskazini atakusanya jeshi kubwa kuliko lile la kwanza; baada ya miaka kadhaa, atasonga mbele na jeshi kubwa mno lililoandaliwa vizuri. \p \v 14 “Katika nyakati hizo, wengi watainuka dhidi ya mfalme wa Kusini. Watu wenye ghasia miongoni mwa watu wako mwenyewe wataasi ili kutimiza maono, lakini bila mafanikio. \v 15 Ndipo mfalme wa Kaskazini atakuja na kuuzingira mji kwa majeshi, na kuuteka mji wa ngome. Majeshi ya Kusini yatakosa nguvu za kumzuia; naam, hata vikosi vyao vya askari vilivyo bora zaidi, havitakuwa na nguvu za kuwakabili. \v 16 Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza. \v 17 Ataamua kuja na nguvu za ufalme wake wote, na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kuuangusha ufalme, lakini mipango yake haitafanikiwa wala kumsaidia. \v 18 Ndipo atabadili nia yake na kupigana na nchi za pwani na aziteke nyingi, lakini jemadari mmoja atakomesha ufidhuli wake, na kurudisha ufidhuli wake juu yake. \v 19 Baada ya hili atazigeukia ngome za nchi yake mwenyewe, lakini atajikwaa na kuanguka, wala hataonekana tena. \p \v 20 “Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, baada ya miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita. \p \v 21 “Atakayetawala baada yake atakuwa mtu wa kudharauliwa ambaye hajapewa heshima ya kifalme. Atauvamia ufalme wakati watu wake wanapojiona kuwa salama, naye atautwaa kwa hila. \v 22 Ndipo jeshi kubwa litafagiliwa mbele yake; jeshi pamoja na mkuu mmoja wa agano wataangamizwa. \v 23 Baada ya kufanya mapatano naye, atatenda kwa udanganyifu, na ataingia madarakani akitumia watu wachache tu. \v 24 Wakati majimbo yaliyo tajiri sana yanajiona salama, atayavamia, naye atatimiza kile baba zake na babu zake hawakuweza. Atagawa nyara, mateka na utajiri miongoni mwa wafuasi wake. Atapanga njama ya kupindua miji yenye ngome, lakini kwa muda mfupi tu. \p \v 25 “Atachochea nguvu zake na ushujaa wake kwa jeshi kubwa dhidi ya mfalme wa Kusini. Mfalme wa Kusini atafanya vita na jeshi kubwa lenye nguvu sana, lakini hataweza kusimama kwa sababu ya hila zilizopangwa dhidi yake. \v 26 Wale wanaokula kutoka meza ya mfalme watajaribu kumwangamiza; jeshi lake litafagiliwa mbali, nao wengi watakufa vitani. \v 27 Wafalme hawa wawili, mioyo yao ikiwa imekusudia mabaya, wataketi kwenye meza moja na kudanganyana wao kwa wao, lakini pasipo faida, kwa sababu bado mwisho utakuja katika wakati ulioamriwa. \v 28 Mfalme wa Kaskazini atarudi katika nchi yake na utajiri mwingi, lakini atakuwa ameukaza moyo wake kinyume cha agano takatifu. Atachukua hatua dhidi ya hilo agano, kisha arudi nchi yake. \p \v 29 “Wakati ulioamriwa, atavamia tena Kusini, lakini wakati huu matokeo yake yatakuwa tofauti na yale ya wakati wa kwanza. \v 30 Meli za nchi ya Kitimu zitampinga, naye atavunjika moyo. Ndipo atarudi nyuma na kutoa hasira yake dhidi ya agano takatifu. Atarudi na kuonesha fadhili kwa wale wanaoliacha agano takatifu. \p \v 31 “Majeshi yake yenye silaha yatainuka ili kunajisi ngome ya Hekalu, na kuondolea mbali sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. Ndipo watalisimamisha chukizo la uharibifu linalosababisha ukiwa. \v 32 Kwa udanganyifu, atapotosha wale walionajisi agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti. \p \v 33 “Wenye hekima watawafundisha wengi, ingawa kwa kitambo watauawa kwa upanga au kuchomwa moto, au kukamatwa, au kutekwa nyara. \v 34 Watakapoanguka, watapokea msaada kidogo, nao wengi wasio waaminifu wataungana nao. \v 35 Baadhi ya wenye hekima watajikwaa, ili waweze kusafishwa, kutakaswa na kufanywa wasio na waa hadi wakati wa mwisho, kwa maana bado litakuja kwa wakati ulioamriwa. \s1 Mfalme ajikwezaye mwenyewe \p \v 36 “Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza juu ya kila mungu, naye atasema mambo ambayo hayajawahi kusikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitatukia. \v 37 Hataonesha heshima kwa miungu ya baba zake au kwa yule aliyetamaniwa na wanawake, wala hatajali mungu yeyote, bali atajikweza mwenyewe juu yao wote. \v 38 Badala ya kuwajali miungu, ataheshimu mungu wa ngome; mungu ambaye hakujulikana na baba zake ndiye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani, na zawadi za thamani kubwa. \v 39 Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni, naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala wa watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama. \p \v 40 “Wakati wa mwisho, mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita, askari wapanda farasi, na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kuzikumba nchi hizo kama mafuriko. \v 41 Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu, na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake. \v 42 Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi; hata Misri haitaepuka. \v 43 Atamiliki hazina za dhahabu na fedha na utajiri wote wa Misri, huku Walibia na Wakushi wakijisalimisha kwake. \v 44 Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu wengi kabisa. \v 45 Atasimika mahema yake ya ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia. \c 12 \s1 Nyakati za mwisho \p \v 1 “Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa. \v 2 Wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima wa milele, wengine kwa aibu na kudharauliwa milele. \v 3 Wale wenye hekima watang’aa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watang’aa kama nyota milele na milele. \v 4 Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki hadi wakati wa mwisho. Wengi wataenda hapa na pale, na maarifa yataongezeka.” \b \p \v 5 Ndipo mimi Danieli nikaangalia, nako mbele yangu walisimama wengine wawili, mmoja katika ukingo huu wa mto, na mwingine ukingo wa pili wa mto. \v 6 Mmoja wao akamwambia yule mtu aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, “Je, itachukua muda gani kabla mambo haya ya kushangaza hayajatimizwa?” \p \v 7 Kisha mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, akainua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni, nami nikamsikia akiapa kwa jina lake yeye aishiye milele, akisema, “Itakuwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati\f + \fr 12:7 \fr*\ft Wakati, nyakati mbili na nusu wakati maana yake mwaka mmoja, miaka miwili, na nusu mwaka, yaani miaka mitatu na nusu.\ft*\f*. Nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimevunjwa kabisa, ndipo mambo haya yote yatakapotimizwa.” \p \v 8 Nilisikia, lakini sikuelewa. Kwa hiyo nikauliza, “Bwana wangu, matokeo ya haya yote yatakuwa nini?” \p \v 9 Akajibu, “Danieli, nenda zako, kwa sababu maneno haya yamefungwa na kutiwa muhuri hadi wakati wa mwisho. \v 10 Wengi watatakaswa, na kuondolewa mawaa na kufanywa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu. \p \v 11 “Tangu wakati ule wa kukomeshwa kwa dhabihu ya kila siku, na kuanzishwa kwa chukizo la uharibifu, kutakuwepo siku elfu moja na mia mbili na tisini (1,290). \v 12 Kubarikiwa ni yule atakayevumilia hadi kufikia mwisho wa hizo siku elfu moja mia tatu na thelathini na tano (1,335). \p \v 13 “Lakini wewe, nenda zako hadi mwisho. Utapumzika, nawe mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekewa.”