\id AMO - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Amosi \toc1 Amosi \toc2 Amosi \toc3 Amo \mt1 Amosi \c 1 \p \v 1 Maneno ya Amosi, mmoja wa wachungaji wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yehoashi alikuwa mfalme wa Israeli. \b \b \p \v 2 Alisema: \q1 “Mwenyezi Mungu ananguruma toka Sayuni, \q2 pia ananguruma kutoka Yerusalemu; \q1 malisho ya wachungaji yanakauka, \q2 kilele cha Karmeli kinanyauka.” \s1 Hukumu kwa majirani wa Israeli \p \v 3 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Dameski, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu aliipura Gileadi \q2 kwa vyombo vya chuma vyenye meno. \q1 \v 4 Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli \q2 ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi. \q1 \v 5 Nitalivunja lango la Dameski; \q2 nitamwangamiza mfalme aliye katika Bonde la Aveni\f + \fr 1:5 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Bonde la Uovu\fqa*\f*, \q1 na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni. \q2 Watu wote wa Aramu wataenda uhamishoni huko Kiri,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 6 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Gaza, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima \q2 na kuwauza kwa Edomu, \q1 \v 7 nitatuma moto juu ya kuta za Gaza \q2 ambao utateketeza ngome zake. \q1 \v 8 Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi \q2 na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni. \q1 Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, \q2 hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,” \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \p \v 9 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Tiro, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu, \q2 na kutokujali mapatano ya undugu, \q1 \v 10 Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro \q2 ambao utateketeza ngome zake.” \p \v 11 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Edomu, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, \q2 alikataa kuonesha huruma yoyote, \q1 kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote \q2 na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa. \q1 \v 12 Nitatuma moto juu ya Temani \q2 ambao utateketeza ngome za Bosra.” \p \v 13 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Amoni, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi \q2 ili kuongeza mipaka yake. \q1 \v 14 Nitatuma moto kwenye kuta za Raba \q2 ambao utateketeza ngome zake \q1 katikati ya kelele za vita katika siku ya mapigano, \q2 katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba. \q1 \v 15 Mfalme wake ataenda uhamishoni, \q2 yeye pamoja na maafisa wake,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \c 2 \p \v 1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Moabu, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu, \q2 ikawa kama chokaa. \q1 \v 2 Nitatuma moto juu ya Moabu \q2 ambao utateketeza ngome za Keriothi. \q1 Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa \q2 katikati ya kelele za vita, na sauti ya tarumbeta. \q1 \v 3 Nitamwangamiza mtawala wake \q2 na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \p \v 4 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Yuda, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Kwa sababu wameikataa Torati ya Mwenyezi Mungu \q2 na hawakuzishika amri zake, \q1 kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, \q2 miungu ambayo babu zao waliifuata. \q1 \v 5 Nitatuma moto juu ya Yuda \q2 ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.” \s1 Hukumu kwa Israeli \p \v 6 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kwa dhambi tatu za Israeli, \q2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. \q1 Wanawauza wenye haki kwa fedha, \q2 na maskini kwa jozi ya viatu. \q1 \v 7 Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini, \q2 kama vile juu ya mavumbi ya nchi, \q2 na kukataa haki kwa waliodhulumiwa. \q1 Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja, \q2 kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu. \q1 \v 8 Watu hulala kando ya kila madhabahu \q2 juu ya nguo zilizowekwa rehani. \q1 Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo \q2 ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu. \b \q1 \v 9 “Nilimwangamiza Mwamori mbele yao, \q2 ingawa alikuwa mrefu kama mierezi, \q2 na mwenye nguvu kama mialoni. \q1 Niliyaangamiza matunda yake juu \q2 na mizizi yake chini. \b \q1 \v 10 “Niliwapandisha toka Misri, \q2 na nikawaongoza miaka arobaini jangwani \q2 niwape nchi ya Waamori. \b \q1 \v 11 “Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu \q2 na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu. \q1 Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 12 “Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyo \q2 na kuwaamuru manabii wasitoe unabii. \b \q1 \v 13 “Sasa basi, nitawaponda \q2 kama gari linavyoponda likiwa limejazwa nafaka. \q1 \v 14 Mkimbiaji hodari hatanusurika, \q2 wenye nguvu wataishiwa nguvu zao, \q2 na shujaa hataweza kuokoa maisha yake. \q1 \v 15 Mpiga upinde atakimbia, \q2 askari wapiga mbio hawataweza kutoroka, \q2 na mpanda farasi hataokoa maisha yake. \q1 \v 16 Hata askari walio mashujaa sana \q2 siku hiyo watakimbia uchi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \c 3 \s1 Mashahidi waitwa dhidi ya Israeli \p \v 1 Sikilizeni neno hili alilosema Mwenyezi Mungu dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri: \q1 \v 2 “Ni ninyi tu niliowachagua \q2 kati ya jamaa zote za dunia; \q1 kwa hiyo nitawaadhibu \q2 kwa ajili ya dhambi zenu zote.” \b \q1 \v 3 Je, watu wawili hutembea pamoja \q2 wasipokubaliana kufanya hivyo? \q1 \v 4 Je, simba hunguruma katika kichaka \q2 wakati hana mawindo? \q1 Aweza kuvuma katika pango \q2 wakati ambao hajakamata chochote? \q1 \v 5 Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini \q2 ambapo hajategewa chambo? \q1 Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini \q2 wakati hakuna chochote cha kunasa? \q1 \v 6 Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari, \q2 watu hawatetemeki? \q1 Mji unapopatwa na maafa, \q2 je, si Mwenyezi Mungu amesababisha? \b \q1 \v 7 Hakika Bwana Mungu Mwenyezi hatafanya neno lolote \q2 bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. \b \q1 \v 8 Simba amenguruma: \q2 je, ni nani ambaye hataogopa? \q1 Bwana Mungu Mwenyezi ametamka: \q2 je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii? \b \q1 \v 9 Tangazeni katika ngome za Ashdodi \q2 na katika ngome za Misri: \q1 “Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria; \q2 angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake, \q2 na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.” \b \q1 \v 10 Mwenyezi Mungu asema: “Hawajui kutenda lililo jema, \q2 wale ambao hujilundikia nyara \q2 na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.” \p \v 11 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “Adui ataizingira nchi; \q2 ataangusha chini ngome zenu \q2 na kuteka nyara maboma yenu.” \p \v 12 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba \q2 vipande viwili tu vya mfupa wa mguu \q2 au kipande cha sikio, \q1 hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa, \q2 wale wanaokaa Samaria \q2 kwenye kingo za vitanda vyao, \q1 na katika Dameski \q2 kwenye viti vyao vya fahari.” \p \v 13 “Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, yeye Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. \q1 \v 14 “Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake, \q2 nitaharibu madhabahu za Betheli; \q1 pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali \q2 na kuanguka chini. \q1 \v 15 Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika, \q2 pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi; \q1 nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu \q2 na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \c 4 \s1 Israeli hajamrudia Mwenyezi Mungu \q1 \v 1 Sikilizeni neno hili, ninyi ng’ombe wa Bashani \q2 mlioko juu ya Mlima Samaria, \q1 ninyi wanawake mnaowadhulumu maskini, \q2 na kuwagandamiza wahitaji, \q1 na kuwaambia wanaume wenu, \q2 “Tuleteeni vinywaji!” \q1 \v 2 Bwana Mungu Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake: \q2 “Hakika wakati utakuja \q1 mtakapochukuliwa na kulabu, \q2 na wanaosalia kwa ndoana za samaki. \q1 \v 3 Nanyi mtaenda moja kwa moja \q2 kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta, \q2 nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 4 “Nendeni Betheli mkatende dhambi; \q2 nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi. \q1 Leteni dhabihu zenu kila asubuhi, \q2 zaka zenu kila mwaka wa tatu. \q1 \v 5 Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani, \q2 jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari: \q1 jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli, \q2 kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,” \q2 asema Bwana Mungu Mwenyezi. \b \q1 \v 6 “Niliwapa njaa kwenye kila mji, \q2 na ukosefu wa chakula katika kila mji, \q2 hata hivyo bado hamjanirudia mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 7 “Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu \q2 kabla ya kufikia mavuno. \q1 Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja, \q2 lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine. \q1 Shamba moja lilipata mvua, \q2 na lingine halikupata, nalo likakauka. \q1 \v 8 Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji, \q2 lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa, \q2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 9 “Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu, \q2 niliyapiga kwa kutu na ukungu. \q1 Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni, \q2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 10 “Niliwapelekea tauni miongoni mwenu \q2 kama nilivyofanya kule Misri. \q1 Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga, \q2 na nikawachukua farasi wenu. \q1 Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kambi zenu, \q2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 11 “Niliwaangamiza baadhi yenu kama \q2 nilivyoangamiza Sodoma na Gomora. \q1 Mlikuwa kama kijiti kiwakacho kilichonyakuliwa motoni, \q2 hata hivyo hamjanirudia,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \b \q1 \v 12 “Kwa hiyo hili ndilo nitakalowafanyia, Israeli, \q2 na kwa sababu nitawafanyia hili, \q2 jiandaeni kukutana na Mungu wenu, ee Israeli.” \b \q1 \v 13 Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo, \q2 na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu, \q1 yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza, \q2 na kukanyaga mahali pa juu pa nchi: \q1 Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 ndilo jina lake. \c 5 \s1 Maombolezo na wito wa toba \p \v 1 Sikia neno hili, ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi: \q1 \v 2 “Bikira Israeli ameanguka, \q2 kamwe hatainuka tena, \q1 ameachwa pweke katika nchi yake, \q2 hakuna yeyote wa kumwinua.” \p \v 3 Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: \q1 “Mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, \q2 mia moja tu watarudi; \q1 wakati mji utakapopeleka mia moja, \q2 kumi tu ndio watarudi hai.” \p \v 4 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa nyumba ya Israeli: \q1 “Nitafuteni mpate kuishi; \q2 \v 5 msitafute Betheli, \q1 msiende Gilgali, \q2 msisafiri kwenda Beer-Sheba. \q1 Kwa maana kwa hakika Gilgali itaenda uhamishoni, \q2 na Betheli itafanywa kuwa ubatili\f + \fr 5:5 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Aveni \fqa*\ft kwa Kiebrania, kumaanisha \ft*\fqa Beth-Aveni \fqa*\ft (taz. \+xt Hosea 4:15\+xt*).\ft*\f*.” \q1 \v 6 Mtafuteni Mwenyezi Mungu mpate kuishi, \q2 au atafagia nyumba ya Yusufu kama moto; \q1 utawateketeza, nayo Betheli \q2 haitakuwa na yeyote wa kuuzima. \b \q1 \v 7 Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu \q2 na kuiangusha haki chini \q1 \v 8 (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, \q2 ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko \q2 na mchana kuwa usiku, \q1 ambaye huyaita maji ya bahari \q2 na kuyamwaga juu ya nchi: \q2 Mwenyezi Mungu ndilo jina lake; \q1 \v 9 yeye hufanya maangamizi kwenye ngome \q2 na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa), \q1 \v 10 mnamchukia yule akemeaye mahakamani, \q2 na kumdharau yule ambaye husema kweli. \b \q1 \v 11 Mnamgandamiza maskini \q2 na kumlazimisha awape nafaka. \q1 Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari, \q2 hamtaishi ndani yake; \q1 ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, \q2 hamtakunywa divai yake. \q1 \v 12 Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu \q2 na ukubwa wa dhambi zenu. \b \q1 Mmewadhulumu wenye haki na kupokea rushwa \q2 na kuzuia haki ya maskini mahakamani. \q1 \v 13 Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza nyakati kama hizo, \q2 kwa kuwa nyakati ni mbaya. \b \q1 \v 14 Tafuteni mema, wala si mabaya, \q2 ili mpate kuishi. \q1 Ndipo Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni \q2 atakuwa pamoja nanyi, \q2 kama msemavyo yupo nanyi. \q1 \v 15 Yachukieni maovu, yapendeni mema; \q2 dumisheni haki mahakamani. \q1 Yamkini Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 atawahurumia mabaki ya Yusufu. \p \v 16 Kwa hiyo hili ndilo Bwana, yeye Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asemalo: \q1 “Kutakuwa na maombolezo barabarani zote, \q2 na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. \q1 Wakulima wataitwa kuja kulia, \q2 na waombolezaji waje kuomboleza. \q1 \v 17 Kutakuwa na kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu, \q2 kwa kuwa nitapita kati yenu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \s1 Siku ya Mwenyezi Mungu \q1 \v 18 Ole wenu ninyi mnaoitamani \q2 siku ya Mwenyezi Mungu! \q1 Kwa nini mnaitamani siku ya Mwenyezi Mungu? \q2 Siku hiyo itakuwa giza, si nuru. \q1 \v 19 Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba \q2 kumbe akakutana na dubu, \q1 kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake \q2 na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta, \q2 kumbe akaumwa na nyoka. \q1 \v 20 Je, siku ya Mwenyezi Mungu haitakuwa giza, na si nuru: \q2 giza nene, bila mwali wowote? \b \q1 \v 21 “Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; \q2 siwezi kuvumilia makusanyiko yenu. \q1 \v 22 Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, \q2 sitazikubali. \q1 Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, \q2 sitazitambua. \q1 \v 23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! \q2 Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu. \q1 \v 24 Lakini acheni haki itiririke kama mto, \q2 na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka! \b \q1 \v 25 “Je, mliniletea dhabihu na sadaka \q2 kwa miaka arobaini kule jangwani, \q2 ee nyumba ya Israeli? \q1 \v 26 Mmeyainua madhabahu ya Sikuthi \q2 mungu wenu mtawala, \q1 na Kiuni mungu wenu wa nyota, \q2 ambao mliwatengeneza wenyewe. \q1 \v 27 Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni mbali kupita Dameski,” \q2 asema Mwenyezi Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi ya mbinguni. \c 6 \s1 Ole kwa wanaoridhika \q1 \v 1 Ole wenu ninyi mnaostarehe na kuridhika katika Sayuni, \q2 na ninyi mnaojisikia salama juu ya Mlima Samaria, \q1 ninyi watu mashuhuri wa taifa lililoendelea kuliko mataifa mengine, \q2 ambao watu wa Israeli wanawategemea! \q1 \v 2 Nendeni Kalne mkaone kutoka huko; \q2 mwende hadi Hamathi iliyo kuu, \q2 kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti. \q1 Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili? \q2 Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu? \q1 \v 3 Mnaiweka mbali siku iliyo mbaya \q2 na kuleta karibu utawala wa kuogofya. \q1 \v 4 Ninyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu, \q2 na kujinyoosha juu ya viti vya fahari. \q1 Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri \q2 na ndama walionenepeshwa. \q1 \v 5 Ninyi mnapiga vinubi kama Daudi, \q2 huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali. \q1 \v 6 Mnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa, \q2 na mnajipaka mafuta mazuri, \q2 lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yusufu. \q1 \v 7 Kwa hiyo mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kwenda uhamishoni; \q2 karamu zenu na kustarehe kutakoma. \s1 Mwenyezi Mungu anachukia kiburi cha Israeli \p \v 8 Bwana Mungu Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asema: \q1 “Nachukia kiburi cha Yakobo, \q2 nachukia ngome zake; \q1 nitautoa mji wao na kila kitu \q2 kilicho ndani yake.” \p \v 9 Kama watu kumi watabaki katika nyumba moja, wao pia watakufa. \v 10 Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumuuliza yeyote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu yeyote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza! Haturuhusiwi kutaja jina la Mwenyezi Mungu.” \q1 \v 11 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamuru, \q2 naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande \q2 na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo. \b \q1 \v 12 Je, farasi wanaweza kukimbia \q2 kwenye miamba iliyochongoka? \q2 Je, mtu aweza kulima kwa maksai huko? \q1 Lakini mmegeuza haki kuwa sumu \q2 na matunda ya uadilifu kuwa uchungu: \q1 \v 13 ninyi mnaoshangilia kushindwa kwa Lo-Debari \q2 na kusema, “Je, hatukuteka Karnaimu \q2 kwa nguvu zetu wenyewe?” \b \q1 \v 14 Maana Bwana Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni, asema, \q1 “Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli, \q2 nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi \q2 hadi Bonde la Araba.” \c 7 \s1 Maono ya kwanza: Nzige \p \v 1 Hili ndilo alilonionesha Bwana Mungu Mwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. \v 2 Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mungu Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!” \p \v 3 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaghairi. \p Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Hili halitatokea.” \s1 Maono ya pili: Moto \p \v 4 Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi alilonionesha katika maono: Bwana Mungu Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi. \v 5 Ndipo nikalia, “Bwana Mungu Mwenyezi, nakusihi, zuia! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!” \p \v 6 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaghairi. \p Bwana Mungu Mwenyezi akasema, “Hili nalo halitatokea.” \b \s1 Maono ya tatu: Timazi \p \v 7 Hili ndilo alilonionesha katika maono: Bwana alikuwa amesimama karibu na ukuta ambao ulikuwa umejengwa kwa timazi, akiwa na uzi wa timazi mkononi mwake. \v 8 Naye Mwenyezi Mungu akaniuliza, “Je, Amosi unaona nini?” \p Nikamjibu, “Uzi wa timazi.” \p Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena. \q1 \v 9 “Mahali pa Isaka pa juu pa kuabudia pataangamizwa, \q2 na mahali patakatifu pa Israeli pa kuabudia pataharibiwa; \q1 kwa upanga wangu nitainuka \q2 dhidi ya nyumba ya Yeroboamu.” \s1 Amosi na Amazia \p \v 10 Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote. \v 11 Kwa kuwa hili ndilo Amosi analosema: \q1 “ ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga, \q2 na kwa hakika Israeli wataenda uhamishoni, \q2 mbali na nchi yao.’ ” \p \v 12 Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Nenda zako, ewe mwonaji! Urudi katika nchi ya Yuda. Ujipatie riziki yako huko na kutoa unabii wako. \v 13 Usiendelee kutoa unabii katika Betheli, kwa sababu hapa ni mahali pa mfalme pa kuabudia na Hekalu la ufalme huu.” \p \v 14 Amosi akamjibu Amazia, “Mimi sikuwa nabii wala mwana wa nabii, lakini nilikuwa mchungaji wa kondoo na mtunza mikuyu. \v 15 Lakini Mwenyezi Mungu akanitoa kutoka kuchunga kondoo na kuniambia, ‘Nenda, ukawatabirie watu wangu Israeli.’ \v 16 Sasa basi, sikieni neno la Mwenyezi Mungu. Ninyi mnasema, \q1 “ ‘Usitabiri dhidi ya Israeli, \q2 na uache kuhubiri dhidi ya nyumba ya Isaka.’ \p \v 17 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: \q1 “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, \q2 nao wana wako wa kiume na wa kike watauawa kwa upanga. \q1 Shamba lako litapimwa na kugawanywa, \q2 na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. \q1 Nayo Israeli kwa hakika itaenda uhamishoni, \q2 mbali na nchi yao.’ ” \c 8 \s1 Maono ya nne: Kikapu cha matunda yaliyoiva \p \v 1 Hili ndilo alilonionesha Bwana Mungu Mwenyezi katika maono: kikapu cha matunda yaliyoiva. \v 2 Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” \p Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” \p Ndipo Mwenyezi Mungu akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.” \p \v 3 Bwana Mungu Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!” \q1 \v 4 Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji, \q2 na kuwaonea maskini wa nchi, \m \v 5 mkisema, \q1 “Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita \q2 ili tupate kuuza nafaka, \q1 na Sabato itakwisha lini \q2 ili tuweze kuuza ngano?” \q1 Mkipunguza vipimo, \q2 na kuongeza bei, \q2 na kudanganya kwa mizani zisizo sawa, \q1 \v 6 mkiwanunua maskini kwa fedha, \q2 na wahitaji kwa jozi ya viatu, \q1 na mkiuza hata takataka za ngano \q2 pamoja na ngano. \p \v 7 Mwenyezi Mungu ameapa kwake mwenyewe, aliye Fahari ya Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya. \q1 \v 8 “Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hili, \q2 nao wote wanaoishi ndani yake hawataomboleza? \q1 Nchi yote itainuka kama Mto Naili; \q2 itapanda na kushuka kama mto wa Misri. \p \v 9 “Katika siku ile,” asema Bwana Mungu Mwenyezi, \q1 “Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia \q2 iwe giza wakati wa mchana mwangavu. \q1 \v 10 Nitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo, \q2 na kuimba kwenu kote kuwe kilio. \q1 Nitawafanya ninyi nyote mvae magunia \q2 na kunyoa nywele zenu. \q1 Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee, \q2 na mwisho wake kama siku ya uchungu. \b \q1 \v 11 “Siku zinakuja,” asema Bwana Mungu Mwenyezi, \q2 “wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote: \q1 si njaa ya chakula wala kiu ya maji, \q2 lakini njaa ya kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. \q1 \v 12 Wanaume watayumbayumba kutoka bahari hadi bahari \q2 na kutangatanga kutoka kaskazini mpaka mashariki, \q1 wakitafuta neno la Mwenyezi Mungu, \q2 lakini hawatalipata. \p \v 13 “Katika siku ile \q1 “wasichana wazuri na wavulana wenye nguvu \q2 watazimia kwa sababu ya kiu. \q1 \v 14 Wale waapao kwa aibu ya Samaria, \q2 au kusema, ‘Hakika kama miungu yenu iishivyo, ee Dani,’ \q1 au ‘Hakika kama mungu wa Beer-Sheba aishivyo’: \q2 wataanguka, wala hawatasimama tena.” \c 9 \s1 Israeli kuangamizwa \p \v 1 Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: \q1 “Piga vichwa vya nguzo \q2 ili vizingiti vitikisike. \q1 Viangushe juu ya vichwa vya watu wote; \q2 na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. \q1 Hakuna yeyote atakayekimbia, \q2 hakuna atakayetoroka. \q1 \v 2 Wajapojichimbia chini hadi kwenye vina vya Kuzimu\f + \fr 9:2 \fr*\ft Kuzimu kwa Kiebrania ni \ft*\fqa Sheol\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shimo lisilo na mwisho.\fqa*\f*, \q2 kutoka huko mkono wangu utawatoa. \q1 Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, \q2 kutoka huko nitawashusha. \q1 \v 3 Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli, \q2 huko nitawawinda na kuwakamata. \q1 Wajapojificha uso wangu \q2 katika vilindi vya bahari, \q2 huko nako nitaamuru joka kuwauma. \q1 \v 4 Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, \q2 huko nako nitaamuru upanga uwaue. \q1 Nitawakazia macho yangu kwa mabaya \q2 wala si kwa mazuri.” \b \q1 \v 5 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, \q2 yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, \q2 na wote wanaoishi ndani yake wakaomboleza: \q1 nayo nchi yote huinuka kama Mto Naili, \q2 kisha hushuka kama mto wa Misri; \q1 \v 6 yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu \q2 na kuisimika misingi yake juu ya dunia, \q1 yeye aitaye maji ya bahari \q2 na kuyamwaga juu ya nchi: \q2 Mwenyezi Mungu ndilo jina lake. \b \q1 \v 7 “Je, Waisraeli, \q2 ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, \q2 Wafilisti kutoka Kaftori\f + \fr 9:7 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Krete\fqa*\f*, \q2 na Washamu kutoka Kiri? \b \q1 \v 8 “Hakika macho ya Bwana Mungu Mwenyezi \q2 yako juu ya ufalme wenye dhambi. \q1 Nami nitauangamiza \q2 kutoka uso wa dunia: \q1 hata hivyo sitaiangamiza kabisa \q2 nyumba ya Yakobo,” \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 9 “Kwa kuwa nitatoa amri, \q2 na nitaipepeta nyumba ya Israeli \q2 miongoni mwa mataifa yote, \q1 kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo, \q2 na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini. \q1 \v 10 Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu \q2 watauawa kwa upanga, \q1 wale wote wasemao, \q2 ‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’ \s1 Kurejeshwa kwa Israeli \p \v 11 “Katika siku ile \q1 “Nitalisimamisha hema la Daudi lililoanguka. \q2 Nitakarabati mahali palipobomoka \q2 na kujenga upya magofu yake, \q2 na kuijenga kama ilivyokuwa awali, \q1 \v 12 ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, \q2 na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,” \q2 asema Mwenyezi Mungu ambaye atafanya mambo haya. \p \v 13 “Siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, \q1 “wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima, \q2 naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu. \q1 Divai mpya itadondoka kutoka milimani, \q2 na kutiririka kutoka vilima vyote. \q1 \v 14 Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; \q2 wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, \q2 nao wataishi ndani yake. \q1 Watapanda mizabibu na kunywa divai yake; \q2 watalima bustani na kula matunda yake. \q1 \v 15 Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe, \q2 hawatang’olewa tena \q2 kutoka nchi niliyowapa,” \m asema Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.