\id ACT - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h Matendo Ya Mitume \toc1 Matendo Ya Mitume \toc2 Matendo \toc3 Mdo \mt1 Matendo Ya Mitume \c 1 \ms1 Waumini wa Isa wa kwanza \mr (Matendo 1:1–5:42) \s1 Ahadi ya Roho wa Mungu \p \v 1 Katika kitabu changu cha kwanza nilikuandikia, Theofilo, kuhusu mambo yote Isa aliyoyafanya na kufundisha tangu mwanzo, \v 2 hadi siku ile alipochukuliwa kwenda mbinguni, baada ya kuwapa maagizo kupitia kwa Roho Mtakatifu wa Mungu wale mitume aliowachagua. \v 3 Baada ya mateso yake, alijionesha kwao na kuwathibitishia kwa njia nyingi kwamba yeye yu hai. Katika muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake aliwatokea na kunena kuhusu ufalme wa Mungu. \v 4 Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba\f + \fr 1:4 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f*, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. \v 5 Yahya aliwabatiza\f + \fr 1:5 \fr*\ft Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali. Wafuasi wa Isa Al-Masihi pia wanapokea Roho wa Mungu kama dhibitisho ya imani yao.\ft*\f* kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho wa Mungu.” \s1 Isa apaa mbinguni \r (Marko 16:19-20; Luka 24:50-53) \p \v 6 Mitume walipokuwa wamekusanyika pamoja, wakamuuliza Isa, “Bwana, je, huu ndio wakati wa kuwarudishia Israeli ufalme?” \p \v 7 Isa akawaambia, “Sio wajibu wenu kujua nyakati au majira ambayo Baba ameyaweka kwa mamlaka yake mwenyewe. \v 8 Lakini mtapokea nguvu, Roho wa Mungu akiwajilia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Yudea yote, na Samaria, na miisho ya dunia.” \p \v 9 Baada ya kusema mambo haya, walipokuwa wanatazama, akachukuliwa juu mbinguni mbele ya macho yao na wingu likampokea wasimwone tena. \p \v 10 Walipokuwa bado wakikaza macho yao kuelekea juu alipokuwa akienda zake mbinguni, ghafula, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe wakasimama karibu nao. \v 11 Wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Isa aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atarudi tena jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.” \s1 Mathiya achaguliwa nafasi ya Yuda \r (Mathayo 27:3-10) \p \v 12 Ndipo waliporudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, uliokuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa mwendo wa Sabato\f + \fr 1:12 \fr*\ft kama kilomita moja\ft*\f* kutoka mjini. \v 13 Walipowasili mjini Yerusalemu, walienda ghorofani kwenye chumba walichokuwa wakiishi. Waliokuwepo walikuwa: \b \li1 Petro, Yohana, Yakobo na Andrea; \li1 Filipo na Tomaso; \li1 Bartholomayo na Mathayo, \li1 Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote\f + \fr 1:13 \fr*\ft Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi.\ft*\f* na Yuda mwana wa Yakobo. \b \p \v 14 Hawa wote waliungana pamoja katika maombi. Pia walikuwepo wanawake kadhaa, na Mariamu mama yake Isa, na ndugu zake Isa. \p \v 15 Katika siku hizo Petro akasimama katikati ya waumini (jumla yao walikuwa watu wapatao mia moja na ishirini), akasema, \v 16 “Ndugu zangu, ilibidi andiko litimie, ambalo Roho wa Mungu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda, aliyewaongoza wale waliomkamata Isa. \v 17 Yuda alikuwa mmoja wetu, kwa maana na yeye alichaguliwa ashiriki katika huduma hii.” \p \v 18 (Basi Yuda alinunua shamba kwa zile fedha za uovu alizopata; akiwa huko shambani akaanguka, akapasuka na matumbo yote yakatoka nje. \v 19 Kila mtu Yerusalemu akasikia habari hizi, kwa hiyo wakapaita mahali hapo kwa lugha yao, Akeldama, yaani Shamba la Damu.) \p \v 20 “Kama vile ilivyoandikwa katika Kitabu cha Zaburi, \q1 “ ‘Mahali pake na pawe ukiwa, \q2 wala asiwepo yeyote atakayeishi humo,’ \m na, \q1 “ ‘Mtu mwingine aichukue nafasi yake ya uongozi.’ \m \v 21 Kwa hiyo inatubidi tumchague mtu mwingine miongoni mwa wale ambao wamekuwa pamoja nasi wakati wote Bwana Isa alipokuwa akiishi kati yetu, \v 22 kuanzia ubatizo wa Yahya hadi siku aliyochukuliwa kutoka kwetu kwenda Mbinguni. Kwa kuwa mmoja wao inabidi awe shahidi pamoja nasi wa ufufuo wake.” \p \v 23 Wakapendekeza majina ya watu wawili: Yusufu, aitwaye Barsaba (ambaye pia alijulikana kama Yusto) na Mathiya. \v 24 Kisha wakaomba, wakasema, “Mwenyezi Mungu, wewe waujua moyo wa kila mtu. Tuoneshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua \v 25 ili achukue nafasi ya huduma ya utume, ambayo Yuda aliiacha ili aende anapostahili.” \v 26 Kisha wakawapigia kura, nayo kura ikamwangukia Mathiya, naye akaongezwa kwenye wale mitume kumi na mmoja. \c 2 \s1 Kushuka kwa Roho wa Mungu \p \v 1 Siku ya Pentekoste ilipowadia, waumini wote walikuwa mahali pamoja. \v 2 Ghafula, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali ikatoka mbinguni, ikaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. \v 3 Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao. \v 4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia. \p \v 5 Basi walikuwako Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu. \v 6 Waliposikia sauti hii, umati wa watu walikusanyika pamoja wakistaajabu, kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. \v 7 Wakiwa wameshangaa na kustaajabu, wakauliza, “Je, hawa wote wanaozungumza si Wagalilaya? \v 8 Imekuwaje basi kila mmoja wetu anawasikia wakinena kwa lugha yake ya kuzaliwa? \v 9 Wapathi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea, Kapadokia, Ponto na jimbo la Asia, \v 10 Frigia, Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni kutoka Rumi \v 11 (Wayahudi na wale walioongokea dini ya Kiyahudi), Wakrete na Waarabu: sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.” \v 12 Wakiwa wameshangaa na kufadhaika wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?” \p \v 13 Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa kwa divai!” \s1 Petro ahutubia umati \p \v 14 Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akapaza sauti yake na kuhutubia umati ule wa watu, akasema: “Wayahudi wenzangu na nyote mnaoishi Yerusalemu, nisikilizeni kwa makini, ili jambo hili lijulikane kwenu. \v 15 Hakika watu hawa hawajalewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi! \v 16 La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema: \q1 \v 17 “ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, \q2 nitamimina Roho wangu \q2 juu ya wote wenye mwili. \q1 Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri, \q2 vijana wenu wataona maono, \q2 na wazee wenu wataota ndoto. \q1 \v 18 Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, \q2 katika siku zile nitamimina Roho wangu, \q2 nao watatabiri. \q1 \v 19 Nami nitaonesha maajabu juu mbinguni, \q2 na ishara chini duniani: \q2 damu, moto, na mawimbi ya moshi. \q1 \v 20 Jua litakuwa giza \q2 na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, \q1 kabla ya kuja siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu \q2 iliyo tukufu. \q1 \v 21 Na kila mtu atakayeliitia \q2 jina la Mwenyezi Mungu, ataokolewa.’ \p \v 22 “Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Isa Al-Nasiri alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo. \v 23 Baada ya huyu mtu kutolewa kwenu kwa mpango wa Mungu uliokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani, ninyi mlimuua kwa kumsulubisha msalabani, kwa mikono ya watu waovu. \v 24 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana yeye kushikiliwa na nguvu za mauti. \v 25 Kwa maana Daudi asema hivi kumhusu: \q1 “ ‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima. \q2 Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, \q2 sitatikisika. \q1 \v 26 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, \q2 na ulimi wangu unashangilia; \q2 mwili wangu nao utapumzika kwa tumaini. \q1 \v 27 Kwa maana hutaniacha kaburini, \q2 wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu. \q1 \v 28 Umenionesha njia za uzima, \q2 utanijaza na furaha mbele zako.’ \p \v 29 “Ndugu zangu Waisraeli, nataka niwaambie kwa uhakika kwamba baba yetu wa zamani Daudi alikufa na kuzikwa, nalo kaburi lake lipo hapa hadi leo. \v 30 Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo, kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha utawala. \v 31 Daudi, akiona mambo yaliyo mbele, akanena kuhusu kufufuka kwa Al-Masihi\f + \fr 2:31 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*, kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu. \v 32 Mungu alimfufua huyu Isa, na sisi sote ni mashahidi wa jambo hilo. \v 33 Basi yeye ametukuzwa hadi mkono wa kuume wa Mungu, na amepokea kutoka kwa Baba\f + \fr 2:33 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* ahadi ya Roho Mtakatifu wa Mungu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia. \v 34 Kwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema, \q1 “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: \q2 “Keti mkono wangu wa kuume, \q1 \v 35 hadi nitakapowaweka adui zako \q2 chini ya miguu yako.” ’ \p \v 36 “Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Isa, ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa Bwana na Al-Masihi.” \s1 Waumini waongezeka \p \v 37 Watu waliposikia maneno haya yakawachoma mioyo yao, wakawauliza Petro na wale mitume wengine, “Ndugu zetu tufanye nini?” \p \v 38 Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mungu. \v 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.” \p \v 40 Petro akawaonya kwa maneno mengine mengi na kuwasihi akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kilichopotoka.” \v 41 Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa, na siku ile waliongezeka watu wapatao elfu tatu. \s1 Ushirika wa waumini \p \v 42 Nao wakadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. \v 43 Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. \v 44 Waumini wote walikuwa mahali pamoja, nao wakashirikiana katika mambo yote. \v 45 Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. \v 46 Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu\f + \fr 2:46 \fr*\ft Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu.\ft*\f*, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, \v 47 wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa. \c 3 \s1 Petro amponya mlemavu kwa jina la Isa \p \v 1 Siku moja, Petro na Yohana walikuwa wanapanda kwenda Hekaluni kusali, yapata saa tisa alasiri. \v 2 Basi palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa. Alichukuliwa na kuwekwa kwenye lango la Hekalu liitwalo Zuri, kila siku ili aombe msaada kwa watu wanaoingia Hekaluni. \v 3 Huyu mtu alipowaona Petro na Yohana wakikaribia kuingia Hekaluni, akawaomba wampe sadaka. \v 4 Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tutazame sisi.” \v 5 Hivyo yule mtu akawatazama, akitazamia kupata kitu kutoka kwao. \p \v 6 Ndipo Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nitakachokupa. Kwa jina la Isa Al-Masihi wa Nasiri, tembea!” \v 7 Petro akamshika yule mtu kwa mkono wa kuume akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikapata nguvu. \v 8 Akaruka juu na kusimama, akaanza kutembea. Kisha akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akitembea na kurukaruka na kumsifu Mungu. \v 9 Watu wote walipomwona akitembea na kumsifu Mungu, \v 10 wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu kwa yale yaliyomtukia. \s1 Petro ashuhudia kuwa Isa anaponya \p \v 11 Aliyeponywa alipokuwa akiambatana na Petro na Yohana, watu wote walishangaa mno, wakaja wakiwakimbilia pale Ukumbi wa Sulemani. \v 12 Petro alipoona watu wamekusanyika akawaambia, “Enyi Waisraeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao kana kwamba ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumemfanya mtu huyu kutembea? \v 13 Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Mwanawe Isa, ambaye ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato, ingawa yeye alikuwa ameamua kumwachia aende zake. \v 14 Ninyi mlimkataa huyo Mtakatifu na Mwenye Haki, mkaomba mpewe yule muuaji. \v 15 Hivyo mkamuua aliye chanzo cha uzima, lakini Mungu akamfufua kutoka kwa wafu. Sisi tu mashahidi wa mambo haya. \v 16 Kwa imani katika jina la Isa, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni jina la Isa na imani kutoka kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama nyote mnavyoona. \p \v 17 “Sasa ndugu zangu, najua ya kuwa ninyi mlitenda bila kujua, kama walivyofanya viongozi wenu. \v 18 Lakini kwa njia hii Mungu alitimiza kile ambacho alikuwa ametabiri kwa vinywa vya manabii wake wote, kwamba Al-Masihi\f + \fr 3:18 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* atateswa. \v 19 Tubuni basi mkamgeukie Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kutoka kwake Mwenyezi Mungu, \v 20 naye apate kumtuma Al-Masihi, ambaye ameteuliwa kwa ajili yenu, yaani Isa. \v 21 Ilimpasa mbingu zimpokee hadi wakati wa kufanywa upya kila kitu, kama Mungu alivyoahidi zamani kupitia kwa manabii wake watakatifu. \v 22 Kwa maana Musa alisema, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia. \v 23 Mtu ambaye hatamsikiliza huyo nabii, atatupiliwa mbali kabisa na watu wake.’ \p \v 24 “Naam, manabii wote tangu Samweli na waliokuja baada yake, wote walitabiri kuhusu siku hizi. \v 25 Ninyi ndio wana wa manabii na wa agano ambalo Mungu alifanya na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, ‘Kupitia kwa uzao wako, watu wote wa ulimwengu watabarikiwa.’ \v 26 Mungu alipomfufua Isa Mwanawe, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kumgeuza kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya.” \c 4 \s1 Petro na Yohana mbele ya Baraza \p \v 1 Petro na Yohana walipokuwa wakisema na watu, makuhani, mkuu wa walinzi wa Hekalu na Masadukayo\f + \fr 4:1 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; waliamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho.\ft*\f* wakawajia, \v 2 huku wakiwa wamekasirika sana kwa sababu mitume walikuwa wanawafundisha watu na kuhubiri kwamba kuna ufufuo wa wafu ndani ya Isa. \v 3 Wakawakamata Petro na Yohana na kuwafunga gerezani hadi kesho yake kwa kuwa ilikuwa jioni. \v 4 Lakini wengi waliosikia lile neno waliamini, idadi yao ilikuwa yapata wanaume elfu tano. \p \v 5 Kesho yake, viongozi wa Wayahudi, wazee na walimu wa Torati walikusanyika Yerusalemu. \v 6 Walikuwemo kuhani mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda, na wengi wa jamaa ya kuhani mkuu. \v 7 Baada ya kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa uwezo gani au kwa jina la nani mmefanya jambo hili?” \p \v 8 Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu wa Mungu, akajibu, “Enyi watawala na wazee wa watu, \v 9 kama leo tukihojiwa kwa habari ya mambo mema aliyotendewa yule kiwete na kuulizwa jinsi alivyoponywa, \v 10 ijulikane kwenu nyote na kwa watu wote wa Israeli kwamba: Ni kwa jina la Isa Al-Masihi wa Nasiri, ambaye ninyi mlimsulubisha lakini Mungu akamfufua kutoka kwa wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mbele yenu akiwa mzima kabisa. \v 11 Huyu ndiye \q1 “ ‘jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa, \q2 ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.’ \m \v 12 Wala hakuna wokovu katika mwingine yeyote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu linalopasa kutuokoa.” \s1 Ujasiri wa Petro na Yohana washangaza watu \p \v 13 Viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa walikuwa watu wa kawaida, wasio na elimu, walishangaa sana, wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Isa. \v 14 Lakini kwa kuwa walikuwa wanamwona yule kiwete aliyeponywa amesimama pale pamoja nao, hawakuweza kusema lolote kuwapinga. \v 15 Wakawaamuru watoke nje ya Baraza la Wayahudi\f + \fr 4:15 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*, ili wasemezane jambo hilo wao wenyewe. \v 16 Wakaulizana, “Tuwafanyie nini watu hawa? Hatuwezi kukanusha muujiza huu mkubwa walioufanya, ambao ni dhahiri kwa kila mtu Yerusalemu. \v 17 Lakini ili kuzuia jambo hili lisiendelee kuenea zaidi kwa watu, ni lazima tuwaonye watu hawa ili wasiseme tena na mtu yeyote kwa jina la Isa.” \p \v 18 Kisha wakawaita tena ndani na kuwaamuru wasiseme wala kufundisha kamwe kwa hili jina la Isa. \s1 Imetupasa kumtii Mwenyezi Mungu kuliko wanadamu \p \v 19 Lakini Petro na Yohana wakajibu, “Amueni ninyi wenyewe iwapo ni haki mbele za Mungu kuwatii ninyi kuliko kumtii Mungu. \v 20 Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema yale tuliyoyaona na kuyasikia.” \p \v 21 Baada ya vitisho vingi, wakawaachia waende zao. Hawakuona njia yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu, kwa kuwa watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetukia. \v 22 Kwa kuwa umri wa yule mtu aliyekuwa ameponywa kwa muujiza ulikuwa zaidi ya miaka arobaini. \s1 Maombi ya waumini \p \v 23 Punde Petro na Yohana walipoachiliwa, walirudi kwa waumini wenzao wakawaeleza waliyoambiwa na viongozi wa makuhani na wazee. \v 24 Watu waliposikia hayo, wakapaza sauti zao, wakamwomba Mungu kwa pamoja, wakisema, “Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeziumba mbingu na nchi na bahari, na vitu vyote vilivyomo. \v 25 Wewe ulinena kwa Roho wa Mungu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema: \q1 “ ‘Mbona mataifa wanaghadhibika, \q2 na makabila ya watu kuwaza ubatili? \q1 \v 26 Wafalme wa dunia wamejipanga, \q2 na watawala wanakusanyika pamoja \q1 dhidi ya Mwenyezi Mungu \q2 na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.’ \m \v 27 Ni kweli Herode na Pontio Pilato, pamoja na watu wa Mataifa na Waisraeli, walikusanyika katika mji huu kupanga njama dhidi ya mwanao mtakatifu Isa, uliyempaka mafuta. \v 28 Wakafanya yale uweza wako na mapenzi yako yalikusudia yatokee tangu zamani. \v 29 Sasa, Mwenyezi Mungu, angalia vitisho vyao na utuwezeshe sisi watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri mkuu. \v 30 Nyoosha mkono wako ili kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miujiza kwa jina la Mwanao mtakatifu Isa.” \p \v 31 Walipokwisha kuomba, mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. \s1 Waumini washirikiana mali yao \p \v 32 Waumini wote walikuwa na moyo mmoja na nia moja. Wala hakuna hata mmoja aliyesema chochote alichokuwa nacho ni mali yake mwenyewe, lakini walishirikiana kila kitu walichokuwa nacho. \v 33 Mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwa Bwana Isa kwa nguvu nyingi na neema ya Mungu ilikuwa juu yao wote. \v 34 Wala hapakuwa mtu yeyote miongoni mwao aliyekuwa mhitaji, kwa sababu mara kwa mara wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliviuza, wakaleta thamani ya vitu vilivyouzwa, \v 35 wakaiweka miguuni pa mitume, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. \p \v 36 Yusufu, Mlawi kutoka Kipro, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake Mwana wa Faraja), \v 37 aliuza shamba alilokuwa nalo, akaleta hizo fedha alizopata na kuziweka miguuni pa mitume. \c 5 \s1 Anania na Safira \p \v 1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. \v 2 Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume. \p \v 3 Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho wa Mungu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? \v 4 Je, kabla hujauza hicho kiwanja, si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, je, fedha ulizozipata, si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.” \p \v 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. \v 6 Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakampeleka nje kumzika. \p \v 7 Muda wa saa tatu baadaye, mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia. \v 8 Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.” \p \v 9 Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakupeleka nje.” \p \v 10 Wakati ule ule, akaanguka chini miguuni mwake na kufa. Nao wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua wakamzika kando ya mumewe. \v 11 Hofu kuu ikalipata kundi la waumini wa Isa lote, pamoja na watu wote waliosikia kuhusu matukio haya. \s1 Mitume waponya watu wengi \p \v 12 Mitume walifanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Waumini wote walikuwa wakikusanyika katika Ukumbi wa Sulemani. \v 13 Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kuambatana nao, ijapokuwa waliheshimiwa sana na watu. \v 14 Hata hivyo, waliomwamini Bwana Isa wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake. \v 15 Hata wakawa wanawaleta wagonjwa na kuwalaza kwenye magodoro na kwenye vitanda barabarani ili yamkini Petro akipita kivuli chake kiwaguse baadhi yao. \v 16 Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa. \s1 Mitume washtakiwa \p \v 17 Kisha kuhani mkuu na wenzake wote waliokuwa pamoja naye, waliokuwa wa kundi la Masadukayo\f + \fr 5:17 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; waliamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho.\ft*\f*, wakajawa na wivu. \v 18 Wakawakamata mitume na kuwafunga gerezani. \v 19 Lakini wakati wa usiku, malaika wa Mwenyezi Mungu akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia, \v 20 “Nendeni, mkasimame Hekaluni, mkawaambie watu maneno yote ya maisha haya mapya.” \p \v 21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. \p Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya Baraza la Wayahudi, yaani wazee wote wa Israeli. Wakatumana wale mitume waletwe kutoka gerezani. \v 22 Lakini wale walinzi wa Hekalu walipoenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. \v 23 Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na askari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu yeyote.” \v 24 Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje. \p \v 25 Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Tazameni watu mliowafunga gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.” \v 26 Ndipo yule mkuu wa walinzi wa Hekalu wakaenda pamoja na askari wakawaleta wale mitume, lakini bila ghasia kwa sababu waliogopa kupigwa mawe na watu. \p \v 27 Waliwaleta mitume, wakawasimamisha mbele ya Baraza la Wayahudi ili kuhani mkuu awahoji. \v 28 “Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.” \p \v 29 Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. \v 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Isa kutoka kwa wafu, ambaye ninyi mlimuua kwa kumtundika kwenye msalaba. \v 31 Mungu alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume kuwa Kiongozi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi. \v 32 Nasi tu mashahidi wa mambo haya, vivyo hivyo na Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.” \p \v 33 Wale wajumbe wa Baraza la Wazee waliposikia haya, walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua mitume. \v 34 Lakini Farisayo\f + \fr 5:34 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa Torati, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya Baraza la Wayahudi, akaamuru mitume watolewe nje kwa muda. \v 35 Ndipo alipowaambia wazee wa Baraza, “Enyi wanaume wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mnayotaka kuwatendea watu hawa. \v 36 Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao mia nne walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu. \v 37 Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika. \v 38 Kwa hiyo, kwa habari ya jambo hili nawashauri, jiepusheni na watu hawa. Waachieni waende zao! Kwa maana kama kusudi lao na shughuli yao imetokana na mwanadamu, haitafanikiwa. \v 39 Lakini ikiwa imetoka kwa Mungu, hamtaweza kuwazuia watu hawa. Badala yake mtajikuta mnapigana na Mungu.” \p \v 40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Isa, wakawaachia waende zao. \p \v 41 Nao mitume wakatoka nje ya Baraza la Wayahudi, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Isa. \v 42 Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri Habari Njema kwamba Isa ndiye Al-Masihi\f + \fr 5:42 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*. \c 6 \ms1 Mateso na kuenea kwa Injili \mr (Matendo 6:1–9:31) \s1 Saba wachaguliwa kuhudumu \p \v 1 Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, Wayahudi wa Kiyunani\f + \fr 6:1 \fr*\ft Wayahudi waliofuata lugha na desturi za Kiyunani\ft*\f* walinung’unika dhidi ya Waebrania\f + \fr 6:1 \fr*\ft Wayahudi walioshikilia lugha na desturi zao za Kiebrania\ft*\f* kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawo wa chakula wa kila siku. \v 2 Wale mitume kumi na wawili wakakusanya wanafunzi wote pamoja wakasema, “Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya neno la Mungu ili kuhudumu mezani. \v 3 Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu wa Mungu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii, \v 4 nasi tutatumia muda wetu kuomba na katika huduma ya neno.” \p \v 5 Yale waliyosema yakawapendeza watu wote, nao wakamchagua Stefano (mtu aliyejawa na imani na Roho wa Mungu) pamoja na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na Nikolao kutoka Antiokia, mtu wa Mataifa aliyeongokea dini ya Kiyahudi. \v 6 Wakawaleta watu hawa mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono. \p \v 7 Neno la Mungu likazidi kuenea. Idadi ya wanafunzi ikazidi kuongezeka sana katika Yerusalemu, hata makuhani wengi wakaitii ile imani. \s1 Kukamatwa kwa Stefano \p \v 8 Stefano, akiwa amejaa neema na nguvu za Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa miongoni mwa watu. \v 9 Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi\f + \fr 6:9 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa) la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na jimbo la Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano. \v 10 Lakini hawakuweza kushindana na ile hekima aliyopewa na Roho wa Mungu alipokuwa akisema. \p \v 11 Ndipo kwa siri wakawashawishi watu fulani waseme, “Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kufuru dhidi ya Musa na dhidi ya Mungu.” \s1 Stefano afikishwa mbele ya Baraza \p \v 12 Wakawachochea watu, wazee na walimu wa Torati, nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya Baraza la Wayahudi\f + \fr 6:12 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*. \v 13 Wakawaleta mashahidi wa uongo ambao walishuhudia, wakasema, “Mtu huyu kamwe haachi kusema dhidi ya mahali hapa patakatifu na dhidi ya Torati. \v 14 Kwa maana tumemsikia akisema kwamba Isa Al-Nasiri atapaharibu mahali patakatifu na kubadili desturi zote tulizopewa na Musa.” \p \v 15 Watu wote waliokuwa wameketi katika Baraza la Wayahudi wakamkazia macho Stefano, wakaona uso wake unang’aa kama uso wa malaika. \c 7 \s1 Hotuba ya Stefano kwa Baraza \p \v 1 Ndipo kuhani mkuu akamuuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?” \p \v 2 Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa bado yuko Mesopotamia, kabla hajaishi Harani, \v 3 akamwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na katika jamii yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha.’ \p \v 4 “Hivyo aliondoka katika nchi ya Wakaldayo akaenda kukaa Harani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungu akamtoa huko akamleta katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. \v 5 Mungu hakumpa urithi wowote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto. \v 6 Mungu akasema naye hivi: ‘Wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.’ \v 7 Mungu akasema, ‘Lakini mimi nitaliadhibu taifa watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka katika nchi hiyo na wataniabudu mahali hapa.’ \v 8 Ndipo akampa Ibrahimu agano la tohara. Naye Ibrahimu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale baba zetu wa zamani kumi na wawili. \p \v 9 “Kwa sababu hao baba zetu wa zamani walimwonea wivu Yusufu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye. \v 10 Akamwokoa kutoka mateso yote yaliyompata. Tena Mungu akampa Yusufu kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Naye Farao akamweka kuwa mtawala wa Misri na wa jumba lote la kifalme. \p \v 11 “Basi kukawa na njaa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, ikasababisha dhiki kubwa, nao baba zetu wakawa hawana chakula. \v 12 Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka huko Misri, aliwatuma baba zetu, wakaenda huko kwa mara yao ya kwanza. \v 13 Walipoenda mara ya pili, Yusufu alijitambulisha kwa ndugu zake; naye Farao akapata habari kuhusu ndugu za Yusufu. \v 14 Ndipo Yusufu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote; kwa jumla walikuwa watu sabini na watano. \v 15 Hivyo Yakobo akaenda Misri ambako yeye na baba zetu walifia. \v 16 Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Ibrahimu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha. \p \v 17 “Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Ibrahimu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri. \v 18 Ndipo ‘mfalme mwingine ambaye hakufahamu habari za Yusufu akatawala Misri’. \v 19 Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe. \p \v 20 “Wakati huo Musa alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani mwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu. \v 21 Walipomweka nje mtoni, binti Farao akamchukua akamlea kama mtoto wake. \v 22 Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo. \p \v 23 “Musa alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. \v 24 Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi. \v 25 Musa alidhani kuwa ndugu zake wangetambua kwamba Mungu anamtumia ili kuwaokoa, lakini wao hawakuelewa. \v 26 Siku iliyofuata Musa aliwakuta Waisraeli wawili wakigombana, akajaribu kuwapatanisha kwa kuwaambia, ‘Enyi watu, ninyi ni ndugu, mbona mnataka kudhulumiana?’ \p \v 27 “Lakini yule mtu aliyekuwa akimdhulumu mwenzake akamsukuma Musa kando, akamuuliza, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? \v 28 Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana?’ \v 29 Musa aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume. \p \v 30 “Baada ya miaka arobaini kupita, malaika wa Mungu akamtokea Musa jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto. \v 31 Alipoona mambo haya, alishangaa yale maono. Aliposogea ili aangalie kwa karibu, akaisikia sauti ya Mwenyezi Mungu, ikisema: \v 32 ‘Mimi ndimi Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.’ Musa alitetemeka kwa hofu na hakuthubutu kutazama. \p \v 33 “Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu. \v 34 Hakika nimeona mateso ya watu wangu huko Misri. Nimesikia kilio chao cha uchungu, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa njoo, nami nitakutuma Misri.’ \p \v 35 “Huyu ndiye Musa waliyemkataa waliposema, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?’ Alikuwa ametumwa na Mungu mwenyewe kuwa mtawala na mkombozi wao, kupitia kwa yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka. \v 36 Aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu\f + \fr 7:36 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Mafunjo\fqa*\f*, na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini. \p \v 37 “Huyu ndiye yule Musa aliyewaambia Waisraeli, ‘Mungu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe.’ \v 38 Huyu ndiye yule Musa aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie. \p \v 39 “Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena. \v 40 Wakamwambia Haruni, ‘Tufanyie miungu itakayotuongoza, kwa maana mtu huyu Musa aliyetutoa nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’ \v 41 Huu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe. \v 42 Ndipo Mungu akageuka, akawaachia waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii: \q1 “ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka \q2 kwa miaka arobaini kule jangwani, \q2 ee nyumba ya Israeli? \q1 \v 43 La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki, \q2 na nyota ya mungu wenu Refani, \q2 vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu. \q1 Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli. \p \v 44 “Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani, ambalo lilitengenezwa kama Mungu alivyomwelekeza Musa, kulingana na kielelezo alichokiona. \v 45 Baada ya kupokea Hema, baba zetu waliingia nalo walipokuja na Yoshua wakati walimiliki nchi, Mungu alipoyafukuza mataifa mbele yao. Nalo lilidumu katika nchi hadi wakati wa Daudi, \v 46 ambaye alipata kibali kwa Mungu, naye akaomba kwamba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. \v 47 Lakini Sulemani ndiye aliyemjengea Mungu nyumba. \p \v 48 “Hata hivyo, Yeye Aliye Juu Sana hakai kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kama nabii alivyosema: \q1 \v 49 “ ‘Mbingu ni kiti changu cha enzi, \q2 nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu. \q1 Mtanijengea nyumba ya namna gani? \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q2 Au mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi? \q1 \v 50 Je, mkono wangu haukuumba vitu hivi vyote?’ \p \v 51 “Enyi watu wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, daima hamwachi kumpinga Roho wa Mungu, kama walivyofanya baba zenu. \v 52 Je, kuna nabii gani ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki. Nanyi sasa mmekuwa wasaliti wake na wauaji. \v 53 Ninyi ndio mlipokea sheria zilizoletwa kwenu na malaika, lakini hamkuzitii.” \s1 Stefano apigwa mawe \p \v 54 Wazee wa Baraza la Wayahudi\f + \fr 7:54 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f* waliposikia haya wakaghadhibika, wakamsagia meno. \v 55 Lakini Stefano, akiwa amejawa na Roho wa Mungu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Isa akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. \v 56 Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.” \p \v 57 Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. \v 58 Wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka mavazi yao miguuni mwa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. \p \v 59 Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, “Bwana Isa, pokea roho yangu.” \v 60 Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala. \c 8 \p \v 1 Naye Sauli alikua pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano. \s1 Waumini wateswa na kutawanyika \p Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya waumini wa Isa huko Yerusalemu, nao waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Yudea na Samaria. \v 2 Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwomboleza sana. \v 3 Lakini Sauli alianza kuangamiza kundi la waumini. Aliingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanaume na wanawake, na kuwafunga gerezani. \s1 Filipo ahubiri Injili huko Samaria \p \v 4 Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipoenda. \v 5 Filipo akaenda mji mmoja wa Samaria akawahubiria habari za Al-Masihi\f + \fr 8:5 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*. \v 6 Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza alizofanya, wakasikiliza kwa makini yale aliyosema. \v 7 Pepo wachafu wakawa wakiwatoka watu wengi huku wakipiga kelele, na wengi waliopooza na viwete wakaponywa. \v 8 Hivyo pakawa na furaha kuu katika mji huo. \s1 Simoni mchawi \p \v 9 Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu, \v 10 nao watu wote, wakubwa kwa wadogo, wakamsikiliza na kustaajabu, wakisema, “Mtu huyu ndiye ajulikanaye kama Uweza Mkuu wa Mungu.” \v 11 Wakamfuata kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake. \v 12 Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri Injili ya ufalme wa Mungu na jina la Isa Al-Masihi, wakabatizwa, wanaume na wanawake. \v 13 Simoni naye akaamini na akabatizwa. Akamfuata Filipo kila mahali, akistaajabishwa na ishara kuu na miujiza aliyoiona. \p \v 14 Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria wamelipokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana waende huko. \v 15 Nao walipofika wakawaombea ili wampokee Roho Mtakatifu wa Mungu, \v 16 kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa bado hajawashukia hata mmoja ila wamebatizwa tu katika jina la Bwana Isa. \v 17 Ndipo Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea Roho wa Mungu. \p \v 18 Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho wa Mungu mitume walipoweka mikono juu yao, akataka kuwapa fedha \v 19 akisema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apate kupokea Roho wa Mungu.” \p \v 20 Petro akamjibu, “Fedha yako na iangamie pamoja nawe, kwa sababu ulidhani unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha! \v 21 Wewe huna sehemu wala fungu katika huduma hii kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. \v 22 Kwa hiyo tubu kwa uovu huu wako na umwombe Mwenyezi Mungu. Yamkini aweza kukusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako. \v 23 Kwa maana ninaona kwamba wewe umejawa na uchungu na ni mfungwa wa dhambi.” \p \v 24 Ndipo Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Mwenyezi Mungu, ili hayo mliyosema lolote lisinitokee.” \p \v 25 Nao walipokwisha kutoa ushuhuda na kuhubiri neno la Bwana Isa, wakarudi Yerusalemu wakihubiri Injili katika vijiji vingi vya Samaria. \s1 Filipo na towashi wa Kushi \p \v 26 Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara inayotoka Yerusalemu kuelekea Gaza ambayo ni jangwa.” \v 27 Hivyo akaondoka. Akiwa njiani akakutana na towashi wa Kushi, aliyekuwa afisa mkuu, mwenye mamlaka juu ya hazina zote za Kandake, Malkia wa Kushi. Huyu towashi alikuwa ameenda Yerusalemu ili kuabudu, \v 28 naye akiwa njiani kurudi nyumbani alikuwa ameketi kwenye gari lake la vita akisoma kitabu cha nabii Isaya. \v 29 Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.” \p \v 30 Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, “Je, unaelewa hayo unayoyasoma?” \p \v 31 Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye. \p \v 32 Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko: \q1 “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni, \q2 kama mwana-kondoo anyamazavyo \q1 mbele yake yule amkataye manyoya, \q2 hivyo hakufungua kinywa chake. \q1 \v 33 Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake. \q2 Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? \q1 Kwa maana maisha yake yaliondolewa \q2 kutoka duniani.” \p \v 34 Yule towashi akamuuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?” \v 35 Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza Injili ya Isa. \p \v 36 Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamuuliza Filipo, “Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?” \p [ \v 37 \f + \fr 8:37 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana aya hii.\ft*\f*Filipo akamwambia, “Ukiamini kwa moyo wako wote, unaweza kubatizwa.” \p Akajibu, “Naamini kuwa Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu.”] \v 38 Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Filipo na yule towashi wakateremka kwenye maji pamoja, naye Filipo akambatiza. \v 39 Nao walipotoka kwenye maji, ghafula Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi. \v 40 Filipo akajikuta Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote hadi akafika Kaisaria. \c 9 \s1 Kuokoka kwa Sauli \r (Matendo 22:6-16; 26:12-18) \p \v 1 Wakati ule ule, Sauli alikuwa bado anazidisha vitisho vya kuua wanafunzi wa Bwana Isa, akamwendea kuhani mkuu, \v 2 naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mfuasi yeyote wa Njia Ile\f + \fr 9:2 \fr*\fq Njia Ile \fq*\ft maana yake \ft*\fqa wafuasi wa Isa \fqa*\ft (\+xt Yohana 14:6\+xt*; \+xt Matendo 24:14\+xt*); walichukuliwa kuwa dhehebu la dini ya Wayahudi.\ft*\f*, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu. \v 3 Basi akiwa katika safari yake, alipokaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ikamwangaza pande zote. \v 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?” \p \v 5 Sauli akajibu, “U nani wewe, Bwana?” \p Ile sauti ikajibu, “Mimi ni Isa unayemtesa. \v 6 Sasa inuka uingie mjini, nawe utaambiwa unachopaswa kufanya.” \p \v 7 Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. \v 8 Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza hadi Dameski. \v 9 Kwa muda wa siku tatu alikuwa kipofu; naye hakula wala kunywa chochote. \p \v 10 Huko Dameski kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana Isa alimwita katika maono, “Anania!” \p Akajibu, “Mimi hapa Bwana.” \p \v 11 Bwana Isa akamwambia, “Ondoka uende katika barabara iitwayo Nyofu ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu kutoka Tarso, jina lake Sauli, kwa maana wakati huu anaomba, \v 12 katika maono amemwona mtu aitwaye Anania akija na kuweka mikono juu yake ili apate kuona tena.” \p \v 13 Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi habari nyingi kuhusu mtu huyu na madhara yote aliyowatendea watakatifu wako huko Yerusalemu. \v 14 Naye amekuja hapa Dameski akiwa na mamlaka kutoka kwa viongozi wa makuhani ili awakamate wote wanaotaja jina lako.” \p \v 15 Lakini Bwana Isa akamwambia Anania, “Nenda! Mtu huyu ni chombo nilichochagua kutangaza jina langu kwa watu wa Mataifa na wafalme wao na watu wa Israeli. \v 16 Nami nitamwonesha jinsi impasavyo kuteseka kwa ajili ya Jina langu.” \p \v 17 Kisha Anania akaenda kwenye ile nyumba, akaingia ndani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu Sauli, Bwana Isa aliyekutokea njiani amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu wa Mungu.” \v 18 Ghafula vitu kama magamba vikaanguka chini, kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa. \v 19 Baada ya kula chakula, akapata nguvu tena. Sauli akakaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski. \s1 Sauli ahubiri Dameski \p \v 20 Papo hapo akaanza kuhubiri kwenye masinagogi kwamba Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu\f + \fr 9:20 \fr*\ft Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (\+xt Yohana 1:1-2\+xt*), wa kiroho, bali si wa kimwili.\ft*\f*. \v 21 Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa na kuuliza, “Huyu si yule mtu aliyesababisha maangamizi makuu huko Yerusalemu miongoni mwa watu waliolitaja jina hili? Naye si amekuja hapa kwa kusudi la kuwakamata na kuwapeleka wakiwa wafungwa mbele ya viongozi wa makuhani?” \v 22 Sauli akazidi kuwa hodari na kuwashangaza Wayahudi walioishi Dameski kwa kuthibitisha kuwa Isa ndiye Al-Masihi\f + \fr 9:22 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*. \p \v 23 Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi wakapanga njama kumuua Sauli. \v 24 Lakini Sauli akagundua njama yao. Wayahudi wakawa wanalinda malango yote ya mji, usiku na mchana ili wapate kumuua. \v 25 Lakini wafuasi wake wakamchukua usiku wakamshusha akiwa ndani ya kapu kupitia mahali penye nafasi ukutani. \s1 Sauli huko Yerusalemu \p \v 26 Sauli alipofika Yerusalemu akajaribu kujiunga na wanafunzi lakini wote walimwogopa, kwa maana hawakuamini kwamba kweli naye alikuwa mwanafunzi. \v 27 Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana Isa, jinsi Bwana alivyosema naye na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Isa huko Dameski. \v 28 Kwa hiyo Sauli akakaa nao akitembea kwa uhuru kila mahali huko Yerusalemu, akihubiri kwa ujasiri katika jina la Bwana Isa. \v 29 Alinena na kuhojiana na Wayahudi wenye asili ya Kiyunani, lakini wao walijaribu kumuua. \v 30 Wale ndugu walipopata habari wakampeleka hadi Kaisaria, wakamsafirisha kwenda Tarso. \p \v 31 Ndipo waumini katika Yudea yote, Galilaya na Samaria wakawa na wakati wa amani. Likatiwa nguvu; na kwa kuwezeshwa na Roho wa Mungu, idadi yao ikaongezeka, na wakaendelea kudumu katika kumcha Bwana. \ms1 Matendo ya Petro \mr (Matendo 9:32–12:25) \s1 Kuponywa kwa Ainea \p \v 32 Petro alipokuwa akisafiri sehemu mbalimbali, alienda kuwatembelea watakatifu walioishi huko Lida. \v 33 Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, aliyekuwa amepooza na kwa muda wa miaka nane alikuwa hajatoka kitandani. \v 34 Petro akamwambia, “Ainea, Isa Al-Masihi anakuponya, inuka utandike kitanda chako.” Mara Ainea akainuka. \v 35 Watu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana Isa. \s1 Petro amfufua Dorkasi \p \v 36 Huko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi\f + \fr 9:36 \fr*\fq Tabitha \fq*\ft kwa Kiaramu na \ft*\fqa Dorkasi \fqa*\ft kwa Kiyunani yote yamaanisha \ft*\fqa Paa.\fqa*\f*). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. \v 37 Wakati huo akaugua, akafa, na wakauosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani. \v 38 Kwa kuwa Yafa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kwamba Petro yuko huko waliwatuma watu wawili kwake ili kumwomba, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” \p \v 39 Kwa hiyo Petro akainuka akaenda nao. Alipowasili, wakampeleka hadi kwenye chumba cha ghorofani alipokuwa amelazwa. Wajane wengi walisimama karibu naye wakilia na kuonesha majoho na nguo nyingine ambazo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa pamoja nao. \p \v 40 Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi. \v 41 Petro akamshika mkono akamwinua, ndipo akawaita wale watakatifu na wajane akamkabidhi kwao akiwa hai. \v 42 Habari hizi zikajulikana sehemu zote za Yafa na watu wengi wakamwamini Bwana Isa. \v 43 Petro akakaa Yafa kwa siku nyingi akiishi na Simoni mtengenezaji ngozi. \c 10 \s1 Kornelio amwita Petro \p \v 1 Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu aliyeitwa Kornelio, aliyekuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia. \v 2 Yeye na jamaa yake yote walikuwa wacha Mungu; alitoa kwa ukarimu kwa wale walio na mahitaji na kumwomba Mungu mara kwa mara. \v 3 Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!” \p \v 4 Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?” \p Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. \v 5 Sasa tuma watu waende Yafa wakamwite mtu mmoja jina lake Simoni aitwaye Petro. \v 6 Yeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.” \p \v 7 Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia. \v 8 Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa. \s1 Maono ya Petro \p \v 9 Siku iliyofuata, walipokuwa wanaukaribia mji, yapata saa sita mchana, Petro alipanda juu ya nyumba kuomba. \v 10 Alipokuwa akiomba akahisi njaa, akatamani kupata chakula. Lakini wakati walikuwa wakiandaa chakula, akalala usingizi mzito sana. \v 11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama kitambaa kikubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. \v 12 Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. \v 13 Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.” \p \v 14 Petro akajibu, “La hasha, Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.” \p \v 15 Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.” \p \v 16 Jambo hili lilitokea mara tatu, na ghafula kile kitambaa kikarudishwa mbinguni. \p \v 17 Petro alipokuwa akisumbuka kuhusu maana ya maono hayo, wale watu waliotumwa na Kornelio waliipata nyumba ya Simoni, wakasimama kwenye lango. \v 18 Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo. \p \v 19 Wakati Petro akiwa anafikiria kuhusu yale maono, Roho wa Mungu akamwambia, “Simoni, kuna watu watatu wanaokutafuta. \v 20 Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.” \p \v 21 Petro akashuka na kuwaambia wale watu waliokuwa wametumwa kutoka kwa Kornelio, “Mimi ndiye mnayenitafuta. Mmekuja kwa sababu gani?” \p \v 22 Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani mwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.” \v 23 Basi Petro akawakaribisha ndani wawe wageni wake. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye. \s1 Petro nyumbani mwa Kornelio \p \v 24 Siku iliyofuata wakawasili Kaisaria. Kornelio alikuwa akiwangoja pamoja na jamaa na rafiki zake wa karibu. \v 25 Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akaanguka miguuni mwake kwa heshima. \v 26 Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.” \p \v 27 Petro alipokuwa akizungumza naye, akaingia ndani na kuwakuta watu wengi wamekusanyika. \v 28 Akawaambia, “Mnajua kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi. \v 29 Ndiyo sababu ulipotuma niitwe nilikuja bila kupinga lolote. Basi sasa naomba unieleze kwa nini umeniita?” \p \v 30 Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu aliyevaa nguo zilizong’aa akasimama mbele yangu, \v 31 akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na misaada yako kwa maskini imekumbukwa mbele za Mungu. \v 32 Basi tuma watu waende Yafa wakaulize mtu mmoja Simoni aitwaye Petro, yeye ni mgeni katika nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi, ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.’ \v 33 Nilituma watu kwako mara moja, nawe umefanya vyema kuja. Basi sasa sisi sote tuko hapa mbele za Mungu kuyasikiliza yote ambayo Bwana amekuamuru kutuambia.” \s1 Hotuba ya Petro \p \v 34 Ndipo Petro akafungua kinywa chake akasema, “Mungu hana upendeleo, \v 35 lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye. \v 36 Ninyi mnajua ule ujumbe uliotumwa kwa Israeli, ukitangaza Injili ya amani kupitia kwa Isa Al-Masihi. Yeye ni Bwana wa wote. \v 37 Mnajua yale yaliyotukia katika Yudea yote kuanzia Galilaya baada ya mahubiri ya Yahya: \v 38 Jinsi Mungu alivyompaka mafuta Isa Al-Nasiri katika Roho wa Mungu, na jinsi alivyoenda kila mahali akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za ibilisi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. \p \v 39 “Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Yudea na Yerusalemu. Wakamuua kwa kumtundika msalabani. \v 40 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na akamwezesha kuonekana na watu. \v 41 Hakuonekana kwa watu wote, lakini kwetu sisi tuliochaguliwa na Mungu kuwa mashahidi, ambao tulikula na kunywa naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. \v 42 Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote na kushuhudia kwamba ndiye alipakwa mafuta na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na wafu. \v 43 Manabii wote walishuhudia juu yake kwamba kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika Jina lake.” \s1 Watu wa mataifa wapokea Roho wa Mungu \p \v 44 Petro alipokuwa akisema maneno haya, Roho Mtakatifu wa Mungu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe. \v 45 Wale waumini waliokuwa wametahiriwa waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho wa Mungu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa. \v 46 Kwa kuwa waliwasikia wakinena kwa lugha mpya na kumwadhimisha Mungu. \p Ndipo Petro akasema, \v 47 “Je, kuna mtu yeyote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu wa Mungu kama sisi tulivyompokea.” \v 48 Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Isa Al-Masihi. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache. \c 11 \s1 Petro aeleza alivyotumwa kwa watu wa Mataifa \p \v 1 Mitume na waumini waliokuwa huko Yudea wakasikia kuwa watu wa Mataifa nao wamepokea neno la Mungu. \v 2 Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, waumini waliotahiriwa wakamshutumu, \v 3 wakisema, “Ulienda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.” \p \v 4 Ndipo Petro akaanza kuwaeleza kuhusu mambo yote yalivyotokea hatua kwa hatua akisema, \v 5 “Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama kitambaa kikubwa kikishuka kutoka mbinguni, kikashushwa kwa ncha zake nne, nacho kikanikaribia. \v 6 Nilipoangalia ndani yake kwa karibu niliona wanyama wenye miguu minne wa nchini, wanyama mwitu, wanyama watambaao, na ndege wa angani. \v 7 Ndipo nikasikia sauti ikiniambia, ‘Petro, ondoka uchinje na ule.’ \p \v 8 “Nikajibu, ‘La hasha, Bwana! Kitu chochote kilicho najisi hakijaingia kinywani mwangu.’ \p \v 9 “Sauti ikasema kutoka mbinguni mara ya pili, ‘Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.’ \v 10 Jambo hili lilitokea mara tatu, ndipo kile kitu kikavutwa tena mbinguni. \p \v 11 “Wakati ule ule watu watatu, waliokuwa wametumwa kutoka Kaisaria waliwasili katika nyumba niliyokuwa nikikaa. \v 12 Roho Mtakatifu wa Mungu akaniambia niende nao bila kuwa na ubaguzi kati yao na sisi. Hawa ndugu sita pia walifuatana nami, nasi tukaingia nyumbani mwa huyo Kornelio. \v 13 Akatuambia jinsi alivyoona malaika aliyekuwa amesimama katika nyumba yake na kusema, ‘Tuma watu waende Yafa wakamlete Simoni aitwaye Petro. \v 14 Yeye atakupa ujumbe ambao kwa huo wewe na wa nyumbani mwako wote mtaokoka.’ \p \v 15 “Nami nilipoanza kusema, Roho wa Mungu akashuka juu yao kama vile alivyotushukia sisi hapo mwanzo. \v 16 Nami nikakumbuka yale Bwana Isa aliyosema, ‘Yahya alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho wa Mungu.’ \v 17 Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupatia sisi tuliomwamini Bwana Isa Al-Masihi, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?” \p \v 18 Waliposikia haya hawakuwa na lingine la kupinga. Nao wakamsifu Mungu, wakisema, “Basi, Mungu amewapa hata watu wa Mataifa toba iletayo uzima wa milele.” \s1 Kundi la waumini la Antiokia \p \v 19 Basi wale waliotawanyika kwa ajili ya mateso yaliyotokea Stefano alipouawa walisafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Nao hawakuhubiri lile Neno kwa mtu yeyote isipokuwa Wayahudi. \v 20 Lakini baadhi yao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria Injili kuhusu Bwana Isa. \v 21 Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa pamoja nao, nayo idadi kubwa ya watu wakaamini na kumgeukia Bwana Isa. \p \v 22 Habari hizi zilipofika masikioni mwa waumini wa Isa huko Yerusalemu, wakamtuma Barnaba aende Antiokia. \v 23 Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana Isa kwa mioyo yao yote. \v 24 Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho wa Mungu, mwenye imani, nayo idadi kubwa ya watu wakaongezeka kwa Bwana Isa. \p \v 25 Kisha Barnaba akaenda Tarso kumtafuta Sauli, \v 26 naye alipompata akamleta Antiokia. Hivyo kwa mwaka mzima Barnaba na Sauli wakakutana na waumini na kufundisha idadi kubwa ya watu. Wanafunzi waliitwa wafuasi wa Al-Masihi mara ya kwanza huko Antiokia. \p \v 27 Wakati huo manabii walishuka toka Yerusalemu hadi Antiokia. \v 28 Mmoja wao aliyeitwa Agabo akasimama, akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu kwamba njaa kubwa ingeenea ulimwengu mzima. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.) \v 29 Mitume wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada kwa ajili ya ndugu wanaoishi Yudea. \v 30 Wakafanya hivyo, misaada yao ikapelekwa kwa wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli. \c 12 \s1 Yakobo auawa, Petro atiwa gerezani \p \v 1 Wakati huo huo Mfalme Herode Agripa aliwakamata baadhi ya waumini wa Isa. \v 2 Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. \v 3 Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata Petro pia. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. \v 4 Baada ya kumkamata alimfunga gerezani chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka\f + \fr 12:4 \fr*\ft Sherehe iliyowakumbusha Waisraeli jinsi Mwenyezi Mungu alivyowakomboa kutoka utumwani huko Misri.\ft*\f*. \p \v 5 Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini waumini wa Isa walikuwa wakimwombea kwa Mungu kwa bidii. \p \v 6 Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda lango la gereza. \v 7 Ghafula malaika wa Mwenyezi Mungu akatokea, na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro. \p \v 8 Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Jifunge vazi lako na unifuate.” \v 9 Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono. \v 10 Walipita kundi la kwanza la walinzi na la pili, wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo, wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro. \p \v 11 Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yoyote kuwa Mwenyezi Mungu amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka makucha ya Herode Agripa na kutoka matazamio yote ya Wayahudi.” \p \v 12 Mara Petro alipotambua hili alienda nyumbani mwa Mariamu, mama yake Yohana aliyeitwa pia Marko, ambako watu wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. \v 13 Petro alipobisha hodi kwenye lango la nje, mjakazi aliyeitwa Roda akaja kumfungulia. \v 14 Alipoitambua sauti ya Petro, alifurahi mno akarudi bila kufungua lango, akapaza sauti, akasema, “Petro yuko langoni!” \p \v 15 Wakamwambia yule mjakazi, “Umerukwa na akili.” Alipozidi kusisitiza kuwa ni kweli, wakasema, “Lazima awe ni malaika wake.” \p \v 16 Lakini Petro aliendelea kugonga langoni, nao walipofungua lango na kumwona Petro, walistaajabu sana. \v 17 Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Mwenyezi Mungu alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine. \p \v 18 Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale askari kuhusu yaliyomtukia Petro. \v 19 Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Yudea akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda. \s1 Kifo cha Herode Agripa \p \v 20 Basi Herode Agripa alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Hivyo watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakataka kukutana naye. Baada ya kuungwa mkono na Blasto, mtumishi maalum wa Mfalme Herode Agripa aliyeaminika, wakaomba mapatano ya amani maana nchi zao zilitegemea nchi ya huyo mfalme kwa mahitaji yao ya chakula. \p \v 21 Katika siku iliyochaguliwa Herode Agripa akavaa mavazi yake ya kifalme, akaketi kwenye kiti chake cha utawala, akawahutubia watu. \v 22 Watu waliokuwa wamekusanyika wakapaza sauti, wakisema, “Hii si sauti ya mwanadamu, bali ni ya Mungu!” \v 23 Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Mwenyezi Mungu akampiga, naye akaliwa na chango, akafa. \p \v 24 Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo. \p \v 25 Barnaba na Sauli walipomaliza ile huduma yao iliyowapeleka, wakarudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana aitwaye Marko. \c 13 \ms1 Safari ya kwanza ya Paulo kueneza Injili \mr (Matendo 13:1–14:28) \s1 Barnaba na Sauli wanatumwa \p \v 1 Katika kundi la waumini wa Isa huko Antiokia kulikuwa na manabii na walimu: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli. \v 2 Walipokuwa wakimwabudu Mwenyezi Mungu na kufunga, Roho Mtakatifu wa Mungu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi niliyowaitia.” \v 3 Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao. \s1 Barnaba na Sauli waenda Kipro \p \v 4 Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho wa Mungu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini hadi kisiwa cha Kipro. \v 5 Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kama msaidizi wao. \p \v 6 Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu. \v 7 Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu. \v 8 Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani. \v 9 Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho wa Mungu, akamkazia macho Elima huyo mchawi, \v 10 akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Mwenyezi Mungu zilizo nyoofu? \v 11 Nawe sasa sikiliza, mkono wa Mwenyezi Mungu u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.” \p Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akapapasa akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwoneshe njia. \v 12 Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana Isa. \s1 Paulo na Barnaba huko Antiokia ya Pisidia \p \v 13 Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perga huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko, akarejea Yerusalemu. \v 14 Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi. \v 15 Baada ya Torati ya Musa na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.” \p \v 16 Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu. \v 17 Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile. \v 18 Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani. \v 19 Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba yaliyokuwa yakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao. \v 20 Haya yote yalichukua kama muda wa miaka mia nne na hamsini. \p “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi hadi wakati wa nabii Samweli. \v 21 Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini. \v 22 Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Mungu pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’ \p \v 23 “Kutoka uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Isa, kama alivyoahidi. \v 24 Kabla ya kuja kwa Isa, Yahya alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli. \v 25 Yahya alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’ \p \v 26 “Ndugu zangu, wana wa Ibrahimu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu. \v 27 Kwa sababu watu wa Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua, wala kuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye. \v 28 Ijapokuwa hawakupata sababu yoyote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe. \v 29 Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini. \v 30 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. \v 31 Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu. \p \v 32 “Nasi tunawaletea Habari Njema: kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu \v 33 sasa ameyatimiza kwetu sisi, watoto wao, kwa kumfufua Isa, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: \q1 “ ‘Wewe ni Mwanangu; \q2 leo mimi nimekuwa Baba yako.’ \m \v 34 Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: \q1 “ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika \q2 nilizomwahidi Daudi.’ \m \v 35 Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi, \q1 “ ‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’ \p \v 36 “Basi Daudi alipokwisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa na baba zake, na mwili wake ukaoza. \v 37 Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu. \p \v 38 “Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kupitia kwa huyu Isa msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. \v 39 Kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa. \v 40 Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate: \q1 \v 41 “ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka, \q2 mkastaajabu, mkaangamie, \q1 kwa maana nitatenda jambo wakati wenu \q2 ambalo hamtasadiki, \q2 hata kama mtu akiwaambia.’ ” \p \v 42 Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata. \v 43 Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na watu wa Mataifa walioongokea dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. \p \v 44 Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Mwenyezi Mungu. \v 45 Lakini Wayahudi walipoona umati ule mkubwa wa watu, walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema. \p \v 46 Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa. \v 47 Kwa maana hili ndilo Mwenyezi Mungu alilotuamuru: \q1 “ ‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu wa Mataifa, \q2 ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’ ” \p \v 48 Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Mwenyezi Mungu; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. \p \v 49 Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote. \v 50 Lakini viongozi wa Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo. \v 51 Hivyo Paulo na Barnaba wakakung’uta mavumbi ya miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio. \v 52 Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho wa Mungu. \c 14 \s1 Paulo na Barnaba huko Ikonio \p \v 1 Huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi kama ilivyokuwa desturi yao. Huko wakahubiri kwa uwezo mkubwa kiasi kwamba Wayahudi pamoja na watu wa Mataifa wakaamini. \v 2 Lakini wale Wayahudi waliokataa kuamini wakawachochea watu wa Mataifa, wakatia chuki ndani ya mioyo yao dhidi ya waumini. \v 3 Hivyo Paulo na Barnaba wakakaa huko kwa muda wa kutosha wakihubiri kwa ujasiri kuhusu Bwana Isa, ambaye alithibitisha ujumbe wa neema yake kwa kuwawezesha kufanya ishara na miujiza. \v 4 Lakini watu wa mji ule waligawanyika, wengine wakakubaliana na Wayahudi na wengine na mitume. \v 5 Watu wa Mataifa na Wayahudi wakajiunga na baadhi ya viongozi, wakafanya mpango wa kuwatendea mitume mabaya na kuwapiga mawe. \v 6 Lakini mitume walipopata habari hizi wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya Likaonia na sehemu zilizopakana nayo. \v 7 Huko wakaendelea kuhubiri Injili. \s1 Paulo na Barnaba huko Listra \p \v 8 Katika mji wa Listra, kulikuwa na kiwete, aliyekuwa amelemaa tangu kuzaliwa, na hakuwa ametembea kamwe. \v 9 Alimsikiliza Paulo alipokuwa akihubiri. Paulo alipomtazama akaona ana imani ya kuponywa. \v 10 Paulo akapaza sauti, “Simama kwa miguu yako!” Mara yule mtu akasimama upesi akaanza kutembea! \p \v 11 Umati ule wa watu walipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapaza sauti, wakasema kwa lugha yao ya Kilikaonia, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!” \v 12 Wakamwita Barnaba Zeu na Paulo wakamwita Herme kwa kuwa ndiye alikuwa msemaji mkuu. \v 13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye na umati ule wa watu walitaka kuwatolea dhabihu. \p \v 14 Lakini mitume Paulo na Barnaba waliposikia haya, wakararua nguo zao, wakawaendea wale watu kwa haraka, wakawapigia kelele, wakisema, \v 15 “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea Habari Njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo. \v 16 Zamani aliwaachia mataifa waishi walivyotaka. \v 17 Lakini hakuacha kuwaonesha watu uwepo wake: Ameonesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.” \v 18 Hata kwa maneno haya yote, ilikuwa vigumu kuzuia umati ule wa watu kuwatolea dhabihu. \p \v 19 Ndipo wakaja baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio wakawashawishi wale watu, wakampiga Paulo kwa mawe, wakamburuta hadi nje ya mji, wakidhani amekufa. \v 20 Lakini baada ya wanafunzi kukusanyika akainuka na kurudi mjini. Kesho yake yeye na Barnaba wakaondoka kwenda Derbe. \s1 Paulo na Barnaba warudi Antiokia ya Siria \p \v 21 Wakahubiri Injili katika mji huo na kupata wanafunzi wengi. Kisha wakarudi Listra, Ikonio na Antiokia, \v 22 wakiwaimarisha wanafunzi na kuwatia moyo waendelee kudumu katika imani. Wakawaonya wakisema, “Imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kupitia katika taabu nyingi.” \v 23 Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kundi la waumini wa Isa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana Isa waliyemwamini. \v 24 Kisha wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. \v 25 Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia. \p \v 26 Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha. \v 27 Walipowasili Antiokia wakawaita waumini pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa. \v 28 Nao wakakaa huko pamoja na wanafunzi kwa muda mrefu. \c 15 \ms1 Baraza la Yerusalemu na matokeo yake \mr (Matendo 15:1-35) \s1 Baraza la Yerusalemu \p \v 1 Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Yudea, nao wakawa wanawafundisha waumini: “Msipotahiriwa kulingana na desturi aliyofundisha Musa, hamwezi kuokoka.” \v 2 Baada ya Paulo na Barnaba kutokubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kwenda Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na mitume na wazee. \v 3 Hivyo wakatumwa na waumini. Wakapitia Foinike na Samaria, wakielezea jinsi watu wa Mataifa walivyoongoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote. \v 4 Walipofika Yerusalemu, walipokelewa na kundi la waumini na mitume pamoja na wazee. Ndipo Paulo na Barnaba wakawaarifu kila kitu Mungu alichokuwa amefanya kupitia kwao. \p \v 5 Ndipo baadhi ya waumini waliokuwa wa dhehebu la Mafarisayo\f + \fr 15:5 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f* wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii Torati ya Musa.” \p \v 6 Mitume na wazee wakakutana pamoja ili kufikiri jambo hili. \v 7 Baada ya majadiliano mengi, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za kwanza Mungu alinichagua ili kwa midomo yangu watu wa Mataifa wapate kusikia ujumbe wa Injili na kuamini. \v 8 Mungu, ajuaye mioyo ya watu, alionesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu wa Mungu kama vile alivyotupatia sisi. \v 9 Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa imani. \v 10 Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka nira shingoni mwa wanafunzi ambayo baba zetu wala sisi hatukuweza kuibeba? \v 11 Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, kama wao wanavyookolewa.” \p \v 12 Kusanyiko lote wakakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa Mataifa. \v 13 Walipomaliza kunena, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. \v 14 Simoni amekwisha kutueleza jinsi Mungu, kwa mara ya kwanza alivyoonesha kuhusika kwa kujichagulia watu kutoka watu wa Mataifa kwa ajili ya Jina lake. \v 15 Maneno ya manabii yanakubaliana na jambo hili, kama ilivyoandikwa: \q1 \v 16 “ ‘Baada ya mambo haya nitarudi, \q2 nami nitajenga upya \q2 nyumba ya Daudi iliyoanguka. \q1 Nitajenga tena magofu yake \q2 na kuisimamisha, \q1 \v 17 ili wanadamu wengine wote \q2 wapate kumtafuta Mwenyezi Mungu, \q1 hata wale watu wa Mataifa wote \q2 ambao wanaitwa kwa Jina langu, \q1 asema Mwenyezi Mungu, anayefanya mambo haya,’ \q2 \v 18 ambayo yamejulikana tangu zamani. \p \v 19 “Kwa hivyo uamuzi wangu ni kwamba, tusiwataabishe watu wa Mataifa wanaomgeukia Mungu. \v 20 Badala yake, tuwaandikie kwamba wajiepushe na vyakula vilivyonajisiwa kwa kutolewa sanamu, wajiepushe na uasherati, au kula mnyama aliyenyongwa, na damu. \v 21 Kwa maana katika kila mji kwa vizazi vilivyopita, Musa amekuwa na wale wanaotangaza sheria yake kwa kuwa imekuwa ikisomwa kwa sauti kubwa katika masinagogi\f + \fr 15:21 \fr*\ft Nyumba za ibada na mafunzo.\ft*\f* kila Sabato.” \s1 Barua kwa waumini wa Mataifa \p \v 22 Mitume na wazee, pamoja na kundi la waumini wote, wakaamua kuwachagua baadhi ya watu wao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Wakamchagua Yuda aitwaye Barsaba, pamoja na Sila, watu wawili waliokuwa viongozi miongoni mwa ndugu. \v 23 Wakatumwa na barua ifuatayo: \pmo Sisi mitume na wazee, ndugu zenu. \pmo Kwa waumini wa Mataifa mlio Antiokia, Siria na Kilikia. \pmo Salamu. \pm \v 24 Tumesikia kwamba kuna baadhi ya watu waliokuja huko kutoka kwetu bila ruhusa yetu na kuwasumbua, wakiyataabisha mawazo yenu. \v 25 Hivyo tumekubaliana wote kuwachagua baadhi ya watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, \v 26 watu ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi. \v 27 Kwa hiyo tunawatuma Yuda na Sila, kuthibitisha kwa maneno ya mdomo mambo haya tunayowaandikia. \v 28 Kwa maana imempendeza Roho wa Mungu na sisi tusiwatwike mzigo wowote mkubwa zaidi ya mambo haya yafuatayo ambayo ni ya lazima: \v 29 Kwamba mjiepushe na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya, mtakuwa mmefanya vyema. \pmc Kwaherini. \p \v 30 Hivyo wakaagwa, wakashuka kwenda Antiokia. Baada ya kulikusanya kundi la waumini pamoja, wakawapa ile barua. \v 31 Baada ya hao watu kuisoma, wakafurahishwa sana kwa ujumbe wake wa kutia moyo. \v 32 Yuda na Sila, ambao wenyewe walikuwa manabii, wakanena maneno mengi ya kuwatia moyo na kuwajenga waumini katika imani. \v 33 Baada ya kukaa huko Antiokia kwa muda, wakaagwa kwa amani na wale ndugu ili waende kwa wale waliowatuma. [ \v 34 Lakini Sila bado akaendelea kukaa huko.]\f + \fr 15:34 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \v 35 Lakini Paulo na Barnaba walibaki Antiokia ambako wao pamoja na wengine wengi walifundisha na kuhubiri neno la Bwana Isa. \ms1 Safari ya pili ya Paulo kueneza Injili \mr (Matendo 15:36–18:22) \s1 Paulo na Barnaba wagawanyika \p \v 36 Baada ya muda, Paulo akamwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee ndugu katika miji yote tuliyohubiri neno la Bwana Isa tuone jinsi wanavyoendelea.” \v 37 Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. \v 38 Lakini Paulo aliona si vyema kwa sababu aliwahi kuwaacha walipokuwa huko Pamfilia, hakutaka kuendelea kufanya kazi naye. \v 39 Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba kuhusu jambo hili, hivyo wakagawanyika. Barnaba akamchukua Yohana Marko wakasafiri baharini kwenda Kipro. \v 40 Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana Isa. \v 41 Akapitia Siria na Kilikia, akiimarisha makundi ya waumini ya huko. \c 16 \s1 Timotheo aungana na Paulo na Sila \p \v 1 Paulo akafika Derbe na kisha Listra, ambako kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, ambaye mama yake alikuwa Myahudi aliyeamini, lakini baba yake alikuwa Myunani. \v 2 Alikuwa amesifiwa sana na wale ndugu waliokuwa wameamini huko Listra na Ikonio \v 3 Paulo alitaka Timotheo aandamane naye, hivyo akamtahiri kwa sababu ya Wayahudi walioishi eneo lile, kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani. \v 4 Walipokuwa wakienda mji kwa mji, wakawa wanawapa maamuzi yaliyotolewa na mitume na wazee huko Yerusalemu ili wayafuate. \v 5 Hivyo makundi ya waumini yakaimarika katika imani, na wakaongezeka kwa idadi kila siku. \p \v 6 Paulo pamoja na wenzake wakasafiri sehemu za Frigia na Galatia, kwa kuwa Roho wa Mungu hakuwaruhusu kulihubiri neno huko jimbo la Asia. \v 7 Walipofika mpaka wa Misia, wakajaribu kuingia Bithinia lakini Roho wa Isa hakuwaruhusu. \v 8 Kwa hiyo wakapita Misia, wakafika Troa. \v 9 Wakati wa usiku Paulo akaona maono, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, “Vuka uje huku Makedonia utusaidie.” \v 10 Baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kwa haraka kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kuwa Mungu alikuwa ametuita kuhubiri Injili huko. \s1 Kuokoka kwa Lidia \p \v 11 Tukasafiri kwa meli kutoka Troa na kwenda moja kwa moja hadi Samothrake, na kesho yake tukafika Neapoli. \v 12 Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa. \p \v 13 Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, ambapo tulitarajia kupata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko. \v 14 Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanyabiashara wa nguo za zambarau, raia wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Mwenyezi Mungu akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo. \v 15 Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumba yake, alitukaribisha nyumbani mwake, akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana Isa, karibuni mkae nyumbani mwangu.” Naye akatushawishi. \s1 Paulo na Sila watiwa gerezani \p \v 16 Siku moja, tulipokuwa tukienda mahali pa kusali, tulikutana na mjakazi aliyekuwa na pepo wa uaguzi. Naye alikuwa amewapa mabwana zake mapato makubwa ya fedha kwa ubashiri. \v 17 Huyu mjakazi alikuwa akimfuata Paulo na sisi akipaza sauti na kusema, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye Juu Sana, wao wanawatangazieni njia ya wokovu.” \v 18 Akaendelea kufanya hivi kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa ameudhika sana, akageuka na kumwambia yule pepo mchafu, “Ninakuamuru katika jina la Isa Al-Masihi, umtoke!” Yule pepo mchafu akamtoka mara hiyo. \p \v 19 Basi mabwana wa yule mjakazi walipoona kuwa tumaini lao la kuendelea kujipatia fedha limetoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawaburuta hadi sokoni mbele ya viongozi wa mji. \v 20 Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi. \v 21 Wanafundisha desturi ambazo sisi raia wa Rumi hatuwezi kuzikubali au kuzitimiza.” \p \v 22 Umati wa watu wakajiunga kuwashambulia Paulo na Sila, na wale mahakimu wakaamuru wavuliwe nguo zao na wapigwe mijeledi. \v 23 Baada ya kuwapiga sana, wakawatupa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu. \v 24 Kufuata maelekezo haya, yule mkuu wa gereza akawaweka katika chumba cha ndani sana mle gerezani, na akawafunga miguu yao kwa minyororo. \p \v 25 Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. \v 26 Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka. \v 27 Yule mkuu wa gereza alipoamka na kuona milango ya gereza iko wazi, akachomoa upanga wake akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wote wametoroka. \v 28 Lakini Paulo akapaza sauti kwa nguvu, akisema, “Usijidhuru kwa maana sisi sote tuko hapa!” \p \v 29 Yule askari wa gereza akaagiza taa ziletwe, akaingia ndani ya kile chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka mbele ya Paulo na Sila. \v 30 Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?” \p \v 31 Wakamjibu, “Mwamini Bwana Isa Al-Masihi, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako.” \v 32 Wakamwambia neno la Bwana Isa, yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake. \v 33 Wakati ule ule, yule mkuu wa gereza akawachukua, akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa. \v 34 Akawapandisha nyumbani mwake akawaandalia chakula, yeye pamoja na nyumba yake yote wakafurahi sana kwa kuwa sasa walikuwa wamemwamini Mungu. \p \v 35 Kulipopambazuka wale mahakimu wakawatuma maafisa wao kwa mkuu wa gereza wakiwa na agizo linalosema, “Wafungue wale watu, waachie waende zao.” \v 36 Mkuu wa gereza akamwambia Paulo “Mahakimu wameagiza niwaachie huru, kwa hiyo tokeni na mwende zenu kwa amani.” \p \v 37 Lakini Paulo akawaambia wale maafisa, “Wametupiga hadharani bila kutufanyia mashtaka na kutuhoji, nao wakatutupa gerezani, hata ingawa sisi ni raia wa Rumi. Nao sasa wanataka kututoa gerezani kwa siri? Hapana! Wao na waje wenyewe watutoe humu gerezani.” \p \v 38 Wale maafisa wakarudi na kuwaambia wale mahakimu maneno haya, wakaogopa sana walipofahamu kuwa Paulo na Sila ni raia wa Rumi. \v 39 Kwa hiyo wakaja wakawaomba msamaha, wakawatoa gerezani, wakawaomba waondoke katika ule mji. \v 40 Baada ya Paulo na Sila kutoka gerezani walienda nyumbani mwa Lidia, ambapo walikutana na waumini, wakawatia moyo, ndipo wakaondoka. \c 17 \s1 Ghasia huko Thesalonike \p \v 1 Wakasafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. \v 2 Kama ilivyokuwa desturi yake, Paulo aliingia ndani ya sinagogi, na kwa muda wa Sabato tatu akawa anahojiana nao kutoka kwa Maandiko, \v 3 akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Al-Masihi\f + \fr 17:3 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* ateswe na afufuke kutoka kwa wafu. Akasema, “Huyu Isa ninayewaambia habari zake, ndiye Al-Masihi.” \v 4 Baadhi ya Wayahudi wakasadiki, wakaungana na Paulo na Sila, wakiwepo idadi kubwa ya Wayunani waliomcha Mungu na wanawake wengi mashuhuri. \p \v 5 Lakini Wayahudi ambao hawakuwa wameamini wakawa na wivu, wakawakodi watu waovu kutoka sokoni, wakakutanisha umati wa watu, wakaanzisha ghasia mjini. Wakaenda mbio nyumbani mwa Yasoni wakiwatafuta Paulo na Sila ili kuwaleta nje penye umati ule wa watu. \v 6 Lakini walipowakosa wakamburuta Yasoni na ndugu wengine mbele ya maafisa wa mji, wakipaza sauti na kusema: “Watu hawa walioupindua ulimwengu wamekuja huku, \v 7 naye Yasoni amewakaribisha nyumbani mwake. Hawa wote wanaasi amri za Kaisari wakisema yuko mfalme mwingine aitwaye Isa.” \v 8 Waliposikia haya, umati ule wa watu na maafisa wa mji wakaongeza ghasia. \v 9 Nao baada ya kuchukua dhamana kwa ajili ya Yasoni na wenzake wakawaachia waende zao. \s1 Paulo na Sila huko Beroya \p \v 10 Usiku ule ule, wale ndugu wakawapeleka Paulo na Sila waende zao Beroya. Walipowasili huko wakaenda kwenye sinagogi la Wayahudi. \v 11 Hawa Waberoya walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli. \v 12 Wayahudi wengi wakaamini pamoja na wanawake na wanaume Wayunani wa tabaka la juu. \p \v 13 Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko ili kuwashawishi watu na kuwachochea. \v 14 Mara hiyo, wale ndugu wakamsafirisha Paulo hadi pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya. \v 15 Wale waliomsindikiza Paulo wakaenda naye hadi Athene, kisha wakarudi Beroya wakiwa na maagizo kutoka kwa Paulo kuhusu Sila na Timotheo kwamba wamfuate upesi iwezekanavyo. \s1 Paulo huko Athene \p \v 16 Paulo alipokuwa akiwasubiri huko Athene, alisumbuka sana moyoni mwake kuona vile mji huo ulivyojaa sanamu. \v 17 Hivyo akahojiana kwenye sinagogi na Wayahudi pamoja na Wayunani waliomcha Mungu, na pia sokoni kila siku na watu aliopatana nao huko. \v 18 Kundi la wenye falsafa, Waepikureo\f + \fr 17:18 \fr*\ft Waepikureo waliamini kwamba anasa aina mbalimbali, hasa za mawazo, ndizo lengo la maisha.\ft*\f* na Wastoiko\f + \fr 17:18 \fr*\ft Wastoiko waliamini kwamba maisha hayapaswi kuwa ya hisia ya furaha wala huzuni kupita kiasi.\ft*\f*, wakajibizana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri Injili kuhusu Isa na ufufuo wa wafu. \v 19 Hivyo wakamchukua na kumleta kwenye mkutano wa Areopago\f + \fr 17:19 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa baraza la viongozi \fqa*\ft au \ft*\fqa wanafalsafa wa mji wa Athene\fqa*\ft ; walikutana katika kilima cha Aresi\ft*\f*, walikomwambia, “Je, tunaweza kujua mafundisho haya mapya unayofundisha ni nini? \v 20 Wewe unaleta mambo mapya masikioni mwetu, hivyo tungetaka kujua maana yake ni nini.” \v 21 (Waathene na wageni wote walioishi humo hawakutumia muda wao kufanya chochote kingine isipokuwa kueleza au kusikia mambo mapya.) \p \v 22 Ndipo Paulo akasimama katikati ya mkutano wa Areopago, akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana. \v 23 Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa makini vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: \pc \sc Kwa Mungu Asiyejulikana.\sc* \m Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria. \p \v 24 “Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo, ndiye Bwana wa mbingu na nchi; hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu. \v 25 Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote. \v 26 Kutoka kwa mtu mmoja, yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote, naye akaweka nyakati za kuishi. \v 27 Mungu alifanya hivyo ili wanadamu wamtafute na huenda wakamfikia ingawa kwa kupapasapapasa ijapokuwa kwa kweli hakai mbali na kila mmoja wetu. \v 28 ‘Kwa kuwa ndani yake tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu.’ Kama baadhi ya watunga mashairi wenu walivyosema, ‘Sisi ni uzao wake.’ \p \v 29 “Kwa kuwa sisi ni uzao wa Mungu, haitupasi kudhani kuwa uungu ni kama sanamu ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe, mfano uliotengenezwa kwa ubunifu na ustadi wa mwanadamu. \v 30 Zamani wakati wa ujinga, Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu. \v 31 Kwa kuwa ameweka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua. Amewahakikishia watu wote mambo haya kwa kumfufua Al-Masihi kutoka kwa wafu.” \p \v 32 Waliposikia habari za ufufuo wa wafu, baadhi yao wakadhihaki, lakini wengine wakasema, “Tunataka kukusikia tena ukizungumza juu ya jambo hili.” \v 33 Kwa hiyo Paulo akaondoka katikati yao. \v 34 Lakini baadhi yao wakaungana naye wakaamini. Kati yao walikuwemo Dionisio, mmoja wa mkutano wa Areopago, na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari, na wengine wengi. \c 18 \s1 Paulo huko Korintho \p \v 1 Baada ya haya, Paulo akaondoka Athene akaenda Korintho. \v 2 Huko akakutana na Myahudi mmoja jina lake Akila, mzawa wa Ponto, aliyekuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona, \v 3 naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, akakaa na kufanya kazi pamoja nao. \v 4 Kila Sabato Paulo alikuwa akihojiana nao katika sinagogi\f + \fr 18:4 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f*, akijitahidi kuwashawishi Wayahudi na Wayunani. \p \v 5 Sila na Timotheo walipowasili kutoka Makedonia, walimkuta Paulo akiwa amejitolea muda wake wote katika kuhubiri, akiwashuhudia Wayahudi kwamba Isa ndiye Al-Masihi\f + \fr 18:5 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f*. \v 6 Wayahudi walipompinga Paulo na kukufuru, yeye aliyakung’uta mavazi yake, akawaambia, “Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu! Mimi sina hatia, nimetimiza wajibu wangu. Kuanzia sasa nitawaendea watu wa Mataifa.” \p \v 7 Kisha akaondoka kwenye sinagogi, akaenda nyumbani mwa Tito Yusto, aliyekuwa mcha Mungu; nyumba yake ilikuwa karibu na sinagogi. \v 8 Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana, yeye pamoja na watu wote wa nyumbani mwake. Nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo pia wakaamini na kubatizwa. \p \v 9 Usiku mmoja Bwana Isa akamwambia Paulo katika maono, “Usiogope, lakini endelea kusema wala usinyamaze, \v 10 kwa maana mimi niko pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayeweza kukushambulia ili kukudhuru, kwa kuwa nina watu wengi katika mji huu.” \v 11 Hivyo Paulo akakaa huko kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, akiwafundisha Maandiko ya Mungu. \p \v 12 Lakini wakati Galio alipokuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala huko Akaya, Wayahudi waliungana kumshambulia Paulo, wakamkamata na kumpeleka mahakamani. \v 13 Wakamshtaki wakisema, “Mtu huyu anawashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.” \p \v 14 Paulo alipotaka kujitetea, Galio akawaambia Wayahudi, “Kama ninyi Wayahudi mlikuwa mkilalamika kuhusu makosa makubwa ya uhalifu ingekuwa haki kwangu kuwasikiliza. \v 15 Lakini kwa kuwa linahusu maneno, majina na sheria yenu, amueni ninyi wenyewe. Mimi sitakuwa mwamuzi wa mambo haya.” \v 16 Akawafukuza kutoka mahakamani. \v 17 Ndipo wote wakamkamata Sosthene kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya mahakama, lakini Galio hakujali kitendo chao hata kidogo. \s1 Paulo arudi Antiokia \p \v 18 Baada ya kukaa Korintho kwa muda, Paulo akaagana na ndugu, akasafiri kwa meli kwenda Siria akiwa amefuatana na Prisila na Akila. Walipofika Kenkrea, Paulo alinyoa nywele zake kwa kuwa alikuwa ameweka nadhiri. \v 19 Walipofika Efeso, Paulo aliwaacha Prisila na Akila huko, lakini yeye akaingia kwenye sinagogi akawa anajadiliana na Wayahudi. \v 20 Walipomwomba akae nao kwa muda mrefu zaidi hakukubali. \v 21 Lakini alipokuwa akiondoka, akaahidi, “Nitarudi kama Mungu akipenda.” Kisha akasafiri kwa meli kutoka Efeso. \v 22 Alitia nanga Kaisaria, akaenda Yerusalemu na kuwasalimu waumini, kisha akaenda Antiokia. \ms1 Safari ya tatu ya Paulo kueneza Injili \mr (Matendo 18:23–21:16) \p \v 23 Baada ya kukaa huko kwa muda, akaondoka na kwenda sehemu moja hadi nyingine huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha wanafunzi wote. \s1 Huduma ya Apolo huko Efeso na Korintho \p \v 24 Basi akaja Efeso Myahudi aliyeitwa Apolo, mzawa wa Iskanderia. Alikuwa na elimu kubwa, pia alikuwa na ujuzi wa Maandiko. \v 25 Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi kuhusu Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya. \v 26 Apolo alianza kunena kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikia, walimwalika kwao na kumweleza njia ya Mungu kwa ufasaha zaidi. \p \v 27 Naye Apolo alipotaka kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo, wakawaandikia wanafunzi huko ili wamkaribishe. Alipofika huko, aliwasaidia sana wale ambao, kwa neema ya Mungu, walikuwa wameamini. \v 28 Kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga, akithibitisha kwa Maandiko kwamba Isa ndiye Al-Masihi. \c 19 \s1 Paulo huko Efeso \p \v 1 Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, \v 2 akawauliza, “Je, mlipokea Roho wa Mungu mlipoamini?” \p Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho wa Mungu.” \v 3 Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yahya.” \p \v 4 Paulo akasema, “Ubatizo wa Yahya ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani Isa.” \v 5 Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Bwana Isa. \v 6 Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu wa Mungu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri. \v 7 Walikuwa wapatao wanaume kumi na wawili. \p \v 8 Paulo akaingia katika sinagogi na kunena humo kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu, akijadiliana na watu na kuwashawishi katika mambo ya ufalme wa Mungu. \v 9 Lakini baadhi yao wakakaidi; walikataa kuamini, na wakakashifu Njia Ile\f + \fr 19:9 \fr*\fq Njia Ile \fq*\ft maana yake \ft*\fqa wafuasi wa Isa \fqa*\ft (\+xt Yohana 14:6\+xt*; \+xt Matendo 24:14\+xt*); walichukuliwa kuwa dhehebu la dini ya Wayahudi.\ft*\f* hadharani. Basi Paulo aliachana nao. Akaenda na wanafunzi wale, akahojiana nao kila siku katika darasa la Tirano. \v 10 Jambo hili likaendelea kwa muda wa miaka miwili, kiasi kwamba Wayahudi na Wayunani wote walioishi huko jimbo la Asia wakawa wamesikia neno la Bwana Isa. \s1 Wana wa Skewa wajaribu kutoa pepo mchafu \p \v 11 Mungu akafanya miujiza mingi isiyo ya kawaida kupitia kwa Paulo, \v 12 hivi kwamba leso au vitambaa vilivyokuwa vimegusa mwili wa Paulo viliwekwa juu ya wagonjwa, nao wakapona magonjwa yao, na pepo wachafu wakawatoka. \p \v 13 Baadhi ya Wayahudi waliotangatanga wakitoa pepo wachafu wakajaribu kutumia jina la Bwana Isa kwa wale wenye pepo, wakisema, “Kwa jina la Isa, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.” \v 14 Wana saba wa Skewa, Myahudi aliyekuwa kiongozi wa makuhani, walikuwa wanafanya hivyo. \v 15 Siku moja pepo mchafu akawajibu, “Isa namjua na Paulo pia namjua, lakini ninyi ni nani?” \v 16 Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha. \p \v 17 Habari hii ikajulikana kwa Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawajaa wote, nalo jina la Bwana Isa likaheshimiwa sana. \v 18 Wengi wa wale waliokuwa wameamini wakati huu wakaja na kutubu waziwazi kuhusu matendo yao maovu. \v 19 Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma elfu hamsini\f + \fr 19:19 \fr*\ft Drakma moja ilikuwa na thamani sawa na mshahara wa kibarua wa siku moja.\ft*\f* za fedha. \v 20 Hivyo neno la Bwana Isa likaenea sana na kuwa na nguvu. \p \v 21 Baada ya mambo haya kutukia, Paulo akakusudia rohoni kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya. Akasema, “Baada ya kufika huko, yanipasa pia kwenda Rumi.” \v 22 Hivyo akatuma wasaidizi wake wawili, Timotheo na Erasto, waende Makedonia, wakati yeye mwenyewe alibaki kwa muda kidogo huko jimbo la Asia. \s1 Ghasia huko Efeso \p \v 23 Wakati huo huo pakatokea dhiki kubwa kwa sababu ya Njia Ile. \v 24 Mtu mmoja jina lake Demetrio mfua fedha aliyekuwa akitengeneza vinyago vya fedha vya Artemi na kuwapatia mafundi wake biashara kubwa, \v 25 aliwaita pamoja watu wengine waliofanya kazi ya ufundi kama yake na kusema, “Enyi watu, mnajua ya kuwa utajiri wetu unatokana na biashara hii! \v 26 Mnaona na kusikia jinsi huyu Paulo amewashawishi na kuwapoteza watu wengi hapa Efeso na karibu jimbo lote la Asia. Anasema kwamba miungu iliyofanywa kwa mikono ya wanadamu si miungu hata kidogo. \v 27 Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu wa kike Artemi aliye mkuu, anayeabudiwa jimbo lote la Asia na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.” \p \v 28 Waliposikia maneno haya, wakaghadhibika, wakaanza kupiga kelele wakisema, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” \v 29 Mara mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawakamata Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia waliokuwa wakisafiri na Paulo, wakakimbilia nao katika ukumbi wa maonesho. \v 30 Paulo akataka kuingia katikati ya umati, lakini wanafunzi hawakumruhusu. \v 31 Hata baadhi ya viongozi wa sehemu ile, waliokuwa rafiki zake Paulo, wakatuma watu wakitamani asiingie katika ule ukumbi wa maonesho. \p \v 32 Umati wa watu walikuwa na taharuki. Walikuwa wakipiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Idadi kubwa ya watu hawakujua hata ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko. \v 33 Wayahudi wakamsukumia Iskanda mbele na baadhi ya watu kwenye umati ule wakampa maelekezo. Akawaashiria kwa mkono ili watulie aweze kujitetea mbele ya watu. \v 34 Lakini walipotambua kwamba alikuwa Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa karibu muda wa saa mbili, wakisema, “Artemi wa Efeso ni mkuu!” \p \v 35 Baadaye karani wa mji akanyamazisha umati ule wa watu na kusema, “Enyi watu wa Efeso, je, ulimwengu wote haujui ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu yake iliyoanguka kutoka mbinguni? \v 36 Kwa hiyo, kwa kuwa mambo haya hayawezi kukanushwa, inawapasa mnyamaze na wala msifanye lolote kwa haraka. \v 37 Kwa kuwa mmewaleta hawa watu hapa, ingawa hawajaiba hekaluni wala kumkufuru huyu mungu wetu wa kike. \v 38 Basi, ikiwa Demetrio na mafundi wenzake wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na wasaidizi wa mwakilishi wa mtawala. Wanaweza kufungua mashtaka. \v 39 Lakini kama kuna jambo jingine lolote zaidi mnalotaka kulileta, itabidi lisuluhishwe katika kusanyiko halali. \v 40 Kama ilivyo sasa, tuko hatarini kushtakiwa kwa kufanya ghasia kwa sababu ya tukio la leo. Kwa kuwa hakuna sababu tutakayoweza kutoa kuhalalisha msukosuko huu.” \v 41 Baada ya kusema haya akavunja mkutano. \c 20 \s1 Paulo apita Makedonia na Uyunani \p \v 1 Baada ya zile ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawatia moyo, akawaaga, akaanza safari kwenda Makedonia. \v 2 Alipita katika sehemu zile, akinena na watu maneno mengi ya kuwatia moyo. Ndipo hatimaye akawasili Uyunani, \v 3 ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Kwa sababu baadhi ya Wayahudi walikuwa wamepanga njama dhidi yake alipokuwa karibu kusafiri kwa meli kwenda Siria, aliamua kurudi kupitia Makedonia. \v 4 Paulo aliandamana na Sopatro mwana wa Piro kutoka Beroya, Aristarko na Sekundo kutoka Thesalonike, na Gayo kutoka Derbe, pia Timotheo pamoja na Tikiko na Trofimo kutoka jimbo la Asia. \v 5 Hawa watu walitutangulia wakaenda kutungojea Troa. \v 6 Lakini sisi tukasafiri kwa meli kwa siku tano kutoka Filipi baada ya siku za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, nasi tukaungana na wengine huko Troa, ambako tulikaa kwa siku saba. \s1 Eutiko afufuliwa huko Troa \p \v 7 Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu, naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea hadi usiku wa manane. \v 8 Kwenye chumba cha ghorofani walimokuwa wamekutania kulikuwa na taa nyingi. \v 9 Kijana mmoja jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akihubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamchukua akiwa amekufa. \v 10 Paulo akashuka chini, akajitupa juu yake na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, bado yuko hai!” \v 11 Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate na kula. Baada ya kuongea hadi mapambazuko, akaondoka. \v 12 Watu wakamrudisha yule kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana. \s1 Paulo awaaga wazee wa Efeso \p \v 13 Tukatangulia kwenye meli, tukasafiri kwenda Aso ambako tungemchukua Paulo. Alikuwa amefanya utaratibu huu kwa sababu alikuwa akienda huko kwa miguu. \v 14 Alipotukuta huko Aso, alijiunga nasi kwenye meli, tukasafiri hadi Mitilene. \v 15 Kutoka huko tuliendelea kwa meli, na kesho yake tukafika mahali panapokabili Kio. Siku iliyofuata tukavuka kwenda Samo, na kesho yake tukawasili Mileto. \v 16 Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi huko jimbo la Asia. Alikuwa na haraka ya kufika Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste kama ingewezekana. \p \v 17 Paulo akiwa Mileto, alituma mjumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kundi la waumini waje wakutane naye. \v 18 Walipofika akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua jinsi nilivyoishi muda wote nilikuwa nanyi, tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa jimbo la Asia. \v 19 Nilimtumikia Bwana Isa kwa unyenyekevu wote na kwa machozi nikivumilia taabu na mapingamizi yaliyonipata kutokana na hila za Wayahudi. \v 20 Mnajua kwamba sikusita kuhubiri jambo lolote ambalo lingekuwa la kuwafaa ninyi, lakini nilifundisha hadharani na nyumba kwa nyumba. \v 21 Nimewashuhudia Wayahudi na Wayunani kwamba inawapasa kumgeukia Mungu kwa kutubu dhambi na kumwamini Bwana wetu Isa Al-Masihi. \p \v 22 “Nami sasa nimesukumwa na Roho wa Mungu, ninaenda Yerusalemu wala sijui ni nini kitakachonipata huko. \v 23 Ila ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu wa Mungu amenionya kuwa vifungo na mateso vinaningoja. \v 24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Isa aliyonipa, yaani kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu. \p \v 25 “Nami sasa najua kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu niliowahubiria ufalme wa Mungu atakayeniona tena. \v 26 Kwa hiyo nawatangazia leo, sina hatia ya damu ya mtu yeyote. \v 27 Kwa kuwa sikusita kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu. \v 28 Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho wa Mungu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Chungeni jumuiya ya waumini ya Mungu, aliowanunua kwa damu yake mwenyewe. \v 29 Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa-mwitu wakali watakuja kati yenu, ambao hawatalihurumia kundi. \v 30 Hata kutoka miongoni mwenu watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate. \v 31 Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana. \p \v 32 “Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa. \v 33 Sikutamani fedha wala dhahabu wala vazi la mtu yeyote. \v 34 Ninyi wenyewe mnajua kwamba mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. \v 35 Katika kila jambo nimewaonesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Isa mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ” \p \v 36 Paulo alipomaliza kusema haya akapiga magoti pamoja nao wote akaomba. \v 37 Wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kumbusu. \v 38 Kilichowahuzunisha zaidi ni kwa sababu ya yale maneno aliyosema kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Wakaenda naye hadi kwenye meli. \c 21 \s1 Paulo aenda Yerusalemu \p \v 1 Tulipokwisha kujitenga nao, tukasafiri kwa meli moja kwa moja hadi Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo, na kutoka huko tukaenda Patara. \v 2 Hapo tukapata meli iliyokuwa inavuka kwenda Foinike tukapanda tukasafiri nayo. \v 3 Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri hadi Siria. Tukatia nanga katika bandari ya Tiro, ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake. \v 4 Baada ya kuwatafuta wanafunzi wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale wanafunzi wakiongozwa na Roho wa Mungu wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu. \v 5 Lakini muda wetu ulipokwisha, tukaondoka tukaendelea na safari yetu. Wale wanafunzi pamoja na wake zao na watoto wakatusindikiza hadi nje ya mji. Wote tukapiga magoti pale pwani tukaomba. \v 6 Baada ya kuagana, tukapanda kwenye meli, nao wakarudi manyumbani mwao. \p \v 7 Tukaendelea na safari yetu toka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu ndugu wa huko, tukakaa nao kwa siku moja. \v 8 Siku iliyofuata tukaondoka, tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani mwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo, aliyekuwa mmoja wa wale Saba, tukakaa kwake. \v 9 Filipo alikuwa na binti wanne mabikira waliokuwa wanatoa unabii. \p \v 10 Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nabii aliyeitwa Agabo akateremka kutoka Yudea. \v 11 Alipotufikia, akachukua mshipi wa Paulo, akajifunga, akautumia kufunga mikono na miguu yake mwenyewe, akasema, “Roho wa Mungu anasema: ‘Hivi ndivyo viongozi wa Wayahudi huko Yerusalemu watakavyomfunga mwenye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa Mataifa.’ ” \p \v 12 Tuliposikia maneno haya sisi na ndugu wengine tukamsihi Paulo asiende Yerusalemu. \v 13 Lakini Paulo akajibu, “Kwa nini mnalia na kunivunja moyo? Mimi niko tayari si kufungwa tu, bali hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Isa.” \v 14 Alipokataa kushawishika, tukaacha kumsihi, tukasema, “Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na yatendeke.” \p \v 15 Baada ya haya, tukajiandaa, tukaondoka kwenda Yerusalemu. \v 16 Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria wakafuatana nasi na kutupeleka nyumbani mwa Mnasoni, ambaye tungekaa kwake. Yeye alikuwa mtu wa Kipro, mmoja wa wanafunzi wa zamani. \ms1 Kukamatwa kwa Paulo, na safari yake kwenda Rumi \mr (Matendo 21:17–28:31) \s1 Paulo awasili Yerusalemu \p \v 17 Tulipofika Yerusalemu, ndugu wakatukaribisha kwa furaha. \v 18 Kesho yake Paulo pamoja na wengine wetu tulienda kumwona Yakobo, na wazee wote walikuwako. \v 19 Baada ya kuwasalimu, Paulo akatoa taarifa kamili ya mambo yote ambayo Mungu alikuwa amefanya miongoni mwa watu wa Mataifa kupitia huduma yake. \p \v 20 Baada ya kusikia mambo haya, wakamsifu Mungu. Ndipo wakamwambia Paulo, “Ndugu, unaona kulivyo na maelfu ya Wayahudi walioamini, nao wote wana juhudi kwa ajili ya sheria. \v 21 Lakini wameambiwa habari zako kwamba unafundisha Wayahudi wote wanaoishi miongoni mwa watu wa Mataifa kumkataa Musa, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao wala kufuata desturi zetu. \v 22 Sasa tufanyeje? Bila shaka watasikia kwamba umekuja Yerusalemu. \v 23 Kwa hiyo fanya lile tunalokuambia. Tuna watu wanne hapa ambao wameweka nadhiri. \v 24 Jiunge na watu hawa, mfanye utaratibu wa ibada ya kujitakasa pamoja nao, na ulipe gharama ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unaishika sheria. \v 25 Lakini kuhusu wale watu wa Mataifa walioamini, tumewaandikia uamuzi wetu: kwamba wajitenge na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.” \p \v 26 Ndipo kesho yake Paulo akaenda na wale watu, akajitakasa pamoja nao. Akaingia ndani ya Hekalu ili atoe taarifa ya tarehe ambayo siku zao za utakaso zingemalizika na sadaka ingetolewa kwa ajili ya kila mmoja wao. \s1 Paulo akamatwa \p \v 27 Zile siku saba zilipokaribia kumalizika, baadhi ya Wayahudi kutoka jimbo la Asia waliokuwa wamemwona Paulo ndani ya Hekalu, wakachochea umati wote wa watu, nao wakamkamata. \v 28 Wakapiga kelele wakisema, “Waisraeli wenzetu, tusaidieni! Huyu ndiye yule mtu anayefundisha kila mtu na kila mahali, kinyume na watu wetu, sheria zetu na hata Hekalu hili. Zaidi ya hayo amewaleta Wayunani ndani ya Hekalu na kupanajisi mahali hapa patakatifu.” \v 29 (Walikuwa wamemwona Trofimo Mwefeso, akiwa mjini pamoja na Paulo, wakadhani kuwa Paulo alikuwa amemwingiza Hekaluni.) \p \v 30 Mji wote ukataharuki, watu wakaja wakikimbia kutoka pande zote wakamkamata Paulo, wakamburuta kutoka Hekaluni. Milango ya Hekalu ikafungwa. \v 31 Walipokuwa wakitaka kumuua, habari zikamfikia jemadari wa jeshi la askari Warumi kwamba mji wa Yerusalemu wote ulikuwa katika machafuko. \v 32 Mara yule jemadari akachukua maafisa wengine wa jeshi pamoja na askari, wakakimbia kwenye ule umati wa watu. Wale watu waliokuwa wakifanya ghasia walipomwona yule jemadari na askari wakija, wakaacha kumpiga Paulo. \p \v 33 Yule jemadari akaja, akamkamata Paulo akaamuru afungwe kwa minyororo miwili. Akauliza yeye ni nani, na alikuwa amefanya nini. \v 34 Baadhi ya watu katika umati ule wakapiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya taharuki, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi. \v 35 Paulo alipofika penye ngazi, ilibidi askari wambebe juu juu kwa sababu fujo za umati ule wa watu zilikuwa kubwa. \v 36 Umati wa watu waliofuata waliendelea kupaza sauti na kusema, “Mwondoe huyu!” \s1 Paulo anajitetea \p \v 37 Mara tu Paulo alipokaribia kuingizwa kwenye ngome ya jeshi, akamwambia yule jemadari, “Je, naweza kukuambia jambo moja?” \p Yule jemadari akamjibu, “Je, unajua Kiyunani? \v 38 Je, wewe si yule Mmisri ambaye siku hizi za karibuni alianzisha uasi akaongoza kundi la magaidi elfu nne wenye silaha jangwani?” \p \v 39 Paulo akajibu, “Mimi ni Myahudi kutoka Tarso huko Kilikia, raia wa mji maarufu. Tafadhali niruhusu nizungumze na hawa watu.” \p \v 40 Baada ya kupata ruhusa kwa yule jemadari, Paulo akasimama penye ngazi, akawapungia watu mkono ili wanyamaze. Wote waliponyamaza, Paulo akazungumza nao kwa lugha ya Kiebrania, akasema: \c 22 \s1 Ushuhuda wa Paulo kwa Wayahudi wa Yerusalemu \p \v 1 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” \p \v 2 Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakanyamaza kabisa. \p Ndipo Paulo akasema, \v 3 “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu. Miguuni mwa Gamalieli, nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, na nikawa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama nyote mlivyo leo. \v 4 Niliwatesa wafuasi wa Njia hii hadi kufa, nikiwakamata wanaume na wanawake, na kuwatupa gerezani, \v 5 kama kuhani mkuu na baraza zima la wazee wanavyoweza kushuhudia kunihusu. Hata nilipokea barua kutoka kwao kwenda kwa ndugu wale wa Dameski, nami nikaenda huko ili kuwaleta watu hawa Yerusalemu kama wafungwa ili waadhibiwe. \s1 Paulo aeleza juu ya kuokoka kwake \r (Matendo 9:1-19; 26:12-18) \p \v 6 “Nilipokuwa njiani kuelekea Dameski, yapata saa sita mchana, ghafula nuru kubwa kutoka mbinguni ikanimulika kotekote. \v 7 Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli! Sauli! Mbona unanitesa?’ \p \v 8 “Nikajibu, ‘Wewe ni nani, Bwana?’ \p “Naye akaniambia, ‘Mimi ni Isa Al-Nasiri unayemtesa.’ \v 9 Basi wale watu waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. \p \v 10 “Nikauliza, ‘Nifanye nini, Bwana?’ \p “Naye Bwana Isa akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski, huko utaambiwa yote unayopaswa kufanya.’ \v 11 Kwa kuwa nilikuwa siwezi kuona kwa ajili ya mng’ao wa ile nuru, wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza kuingia Dameski. \p \v 12 “Mtu mmoja mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona. Alizishika sana sheria zetu, na aliheshimiwa sana na Wayahudi walioishi huko Dameski. \v 13 Akasimama karibu nami, akasema, ‘Ndugu Sauli, pata kuona tena!’ Nami mara hiyo nikaweza kumwona. \p \v 14 “Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ili ujue mapenzi yake, umwone yeye Aliye Mwenye Haki na upate kusikia maneno kutoka kinywani mwake. \v 15 Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu kuhusu kile ulichokiona na kukisikia. \v 16 Sasa basi, mbona unakawia? Inuka, ukabatizwe na dhambi zako zikasafishwe, ukiliita Jina lake.’ \s1 Paulo atumwa kwa watu wa Mataifa \p \v 17 “Baada ya kurudi Yerusalemu, nilipokuwa ninaomba Hekaluni, nilipitiwa na usingizi wa ghafula, \v 18 nikamwona Bwana Isa akiniambia, ‘Harakisha utoke Yerusalemu upesi, maana hawataukubali ushuhuda wako kunihusu.’ \p \v 19 “Nami nikasema, ‘Bwana, wao wenyewe wanajua jinsi nilivyoenda kwenye kila sinagogi\f + \fr 22:19 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* ili kuwatupa gerezani na kuwapiga wale waliokuamini. \v 20 Damu ya shahidi wako Stefano ilipomwagwa, mimi mwenyewe nilikuwa nimesimama kando, nikikubaliana na kitendo hicho na kutunza mavazi ya wale waliomuua.’ \p \v 21 “Ndipo Bwana Isa akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa Mataifa.’ ” \s1 Paulo na jemadari wa Kirumi \p \v 22 Umati ule wa watu wakamsikiliza Paulo hadi aliposema neno hilo, ndipo wakapaza sauti zao na kupiga kelele wakisema, “Mwondoeni duniani, hafai kuishi!” \p \v 23 Walipokuwa wakipiga kelele na kutoa mavazi yao huku wakirusha mavumbi juu hewani, \v 24 yule jemadari akaamuru Paulo aingizwe kwenye ngome. Akaelekeza kwamba apigwe mijeledi na ahojiwe ili kujua kwa nini watu walikuwa wanampigia kelele namna hiyo. \v 25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wampige mijeledi, Paulo akamwambia kiongozi wa askari aliyekuwa amesimama pale karibu naye, “Je, ni halali kwenu kwa mujibu wa sheria kumpiga mtu ambaye ni raia wa Rumi hata kabla hajapatikana na hatia?” \p \v 26 Yule kiongozi aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari na kumwambia, “Unataka kufanya nini? Kwa maana huyu mtu ni raia wa Rumi.” \p \v 27 Yule jemadari akaja akamuuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Rumi?” \p Paulo akajibu, “Naam, hakika.” \p \v 28 Ndipo yule jemadari akasema, “Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu.” \p Paulo akasema “Lakini mimi ni raia wa Rumi kwa kuzaliwa.” \p \v 29 Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka, naye yule jemadari akaingiwa na hofu alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raia wa Rumi, kwa minyororo. \s1 Paulo apelekwa mbele ya Baraza \p \v 30 Kesho yake, kwa kuwa yule jemadari alitaka kujua hakika kwa nini Paulo alikuwa anashutumiwa na Wayahudi, alimfungua, na akawaagiza viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi\f + \fr 22:30 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f* lote likutane. Kisha akamleta Paulo, akamsimamisha mbele yao. \c 23 \p \v 1 Paulo akawakazia macho wale wajumbe wa Baraza la Wayahudi\f + \fr 23:1 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*, akasema, “Ndugu zangu, nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu kwa dhamiri safi kabisa hadi leo.” \v 2 Kwa ajili ya jambo hili kuhani mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi kinywani. \v 3 Ndipo Paulo akamwambia, “Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa! Wewe umeketi hapo ili kunihukumu kwa mujibu wa sheria, lakini wewe mwenyewe unakiuka sheria kwa kuamuru kwamba nipigwe kinyume cha sheria!” \p \v 4 Wale watu waliokuwa wamesimama karibu na Paulo wakamwambia, “Je, wewe wathubutu kumtukana kuhani mkuu wa Mungu?” \p \v 5 Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye alikuwa kuhani mkuu. Kwa maana imeandikwa, ‘Usimnenee mabaya kiongozi wa watu wako.’ ” \p \v 6 Paulo alipotambua ya kuwa baadhi yao walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo\f + \fr 23:6 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f*, akapaza sauti kwenye Baraza la Wayahudi, akasema, “Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana Farisayo. Hapa nimeshtakiwa kuhusu tumaini langu katika ufufuo wa wafu.” \v 7 Aliposema haya, kukazuka mabishano kati ya Mafarisayo na Masadukayo, na baraza lote likagawanyika. \v 8 (Kwa maana Masadukayo wanasema kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho, lakini Mafarisayo wanaamini haya yote.) \p \v 9 Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa Torati ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lolote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye” \v 10 Ugomvi ukawa mkubwa kiasi kwamba yule jemadari akahofu kuwa wangemrarua Paulo vipande vipande, akaamuru vikosi vya askari vishuke na kumwondoa Paulo katikati yao kwa nguvu na kumleta ndani ya ngome ya jeshi. \p \v 11 Usiku uliofuata, Bwana Isa akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama vile ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, hivyo imekupasa kunishuhudia huko Rumi pia.” \s1 Njama za kumuua Paulo \p \v 12 Kulipopambazuka Wayahudi wakapanga njama pamoja na kujifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala kunywa hadi wawe wamemuua Paulo. \v 13 Waliofanya mpango huo walikuwa zaidi ya watu arobaini. \v 14 Wakaenda kwa viongozi wa makuhani na wazee na kusema, “Tumeapa kwamba hatutakula chochote hadi tuwe tumemuua Paulo. \v 15 Sasa basi, wewe pamoja na Baraza la Wayahudi mwombeni jemadari amlete Paulo mbele yenu kwa kisingizio cha kutaka taarifa sahihi zaidi kuhusu kesi yake. Nasi tuko tayari kumuua kabla hajafika hapa.” \p \v 16 Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia kuhusu njama hiyo, alienda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo. \p \v 17 Ndipo Paulo akamwita mmoja wa viongozi wa askari, akamwambia, “Mpeleke huyu kijana kwa jemadari, ana jambo la kumweleza.” \v 18 Hivyo yule kiongozi wa askari akampeleka yule kijana kwa jemadari, akamwambia, “Paulo yule mfungwa aliniita na kuniomba nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukueleza.” \p \v 19 Yule jemadari akamshika yule kijana mkono, akampeleka kando na kumuuliza, “Unataka kuniambia nini?” \p \v 20 Yule kijana akasema, “Wayahudi wamekubaliana wakuombe umpeleke Paulo kwenye Baraza la Wayahudi kesho kwa kisingizio kwamba wanataka kufanya uchunguzi wa kina kumhusu. \v 21 Lakini usishawishiwe nao kwa maana zaidi ya watu arobaini wanamvizia. Wameapa kwamba hawatakula wala kunywa hadi wamuue Paulo. Sasa wako tayari, wanangoja idhini yako kwa ombi lao.” \p \v 22 Yule jemadari akamruhusu yule kijana aende na akamwonya, akisema, “Usimwambie mtu yeyote kwamba umenieleza habari hizi.” \s1 Paulo ahamishiwa Kaisaria \p \v 23 Kisha yule jemadari akawaita viongozi wake wawili wa askari akawaambia, “Jiandaeni kuondoka saa tatu usiku huu kuelekea Kaisaria pamoja na askari mia mbili, wapanda farasi sabini, na watu mia mbili wenye mikuki. \v 24 Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mkampeleke salama kwa mtawala Feliksi.” \p \v 25 Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo: \pmo \v 26 Klaudio Lisia. \pmo Kwa Mtawala, Mtukufu Feliksi. \pmo Salamu. \pm \v 27 Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi wakakaribia kumuua, lakini nikaja na vikosi vyangu vya askari nikamwokoa, kwa kuwa nilipata habari kwamba yeye ni raia wa Rumi. \v 28 Nilitaka kujua kwa nini walikuwa wanamshutumu, hivyo nikamleta mbele ya Baraza la Wayahudi. \v 29 Ndipo nikaona kuwa alikuwa anashutumiwa kwa mambo yanayohusu sheria yao, lakini hakuwa ameshtakiwa kwa jambo lolote linalostahili kifo au kifungo. \v 30 Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na njama dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara moja. Niliwaagiza washtaki wake pia waeleze mashtaka yao dhidi yake mbele yako. \p \v 31 Hivyo askari, kwa kufuata maelekezo waliyopewa, wakamchukua Paulo wakati wa usiku na kumleta hadi Antipatri. \v 32 Kesho yake wakawaacha wale wapanda farasi waendelee na safari wakiwa na Paulo, wao wakarudi kwenye ngome ya askari. \v 33 Askari walipofika Kaisaria, walimpa mtawala ile barua, na kumkabidhi Paulo kwake. \v 34 Mtawala alipokwisha kuisoma ile barua alimuuliza Paulo alikuwa mtu wa jimbo gani. Alipojua kuwa anatoka Kilikia, \v 35 alisema, “Nitasikiliza kesi yako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode. \c 24 \s1 Mbele ya Feliksi huko Kaisaria \p \v 1 Baada ya siku tano, kuhani mkuu Anania akateremka hadi Kaisaria pamoja na baadhi ya wazee na mwanasheria aitwaye Tertulo, wakaleta mashtaka yao dhidi ya Paulo mbele ya mtawala. \v 2 Paulo alipoitwa aingie ndani, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akisema, “Mtukufu Feliksi, kwa muda mrefu tumefurahia amani na mabadiliko mengi mazuri yamefanywa kwa ajili ya watu hawa kwa sababu ya upeo wako wa kuona mambo ya mbele. \v 3 Wakati wote na kila mahali, kwa namna yoyote, mtukufu Feliksi, tumeyapokea mambo haya yote kwa shukrani nyingi. \v 4 Lakini nisije nikakuchosha zaidi, ningekuomba kwa hisani yako utusikilize kwa kifupi. \p \v 5 “Tumemwona mtu huyu kuwa ni msumbufu, anayechochea ghasia miongoni mwa Wayahudi duniani pote. Yeye ndiye kiongozi wa dhehebu la Wanasiri, \v 6 na hata amejaribu kulinajisi Hekalu, hivyo tukamkamata. [Tukataka kumhukumu kufuatana na sheria zetu. \v 7 Lakini jemadari Lisia alitujia na nguvu nyingi, akamwondoa mikononi mwetu, \v 8 akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako.]\f + \fr 24:6-8 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* Kwa kumchunguza mwenyewe utaweza kujua ukweli kuhusu mashtaka haya yote tunayoleta dhidi yake.” \p \v 9 Pia wale Wayahudi wakaunga mkono wakithibitisha kuwa mashtaka haya yote ni kweli. \s1 Paulo ajitetea mbele ya Feliksi \p \v 10 Mtawala Feliksi alipompungia Paulo mkono ili ajitetee, yeye akajibu, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi, hivyo natoa utetezi wangu kwa furaha. \v 11 Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu. \v 12 Hawa wanaonishtaki hawakunikuta nikibishana na mtu yeyote Hekaluni au kuchochea umati wa watu katika sinagogi\f + \fr 24:12 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* au mahali pengine popote mjini. \v 13 Wala hawawezi kabisa kukuthibitishia mashtaka haya wanayoleta dhidi yangu. \v 14 Lakini ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kama mfuasi wa Njia Ile, ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Torati na kile kilichoandikwa katika Manabii, \v 15 nami ninalo tumaini kwa Mungu, ambalo hata wao wenyewe wanalikubali kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kwa wenye haki na wasio na haki. \v 16 Kwa hiyo ninajitahidi siku zote kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu. \p \v 17 “Basi, baada ya miaka mingi nilikuja Yerusalemu ili kuwaletea watu wangu msaada kwa ajili ya maskini na kutoa dhabihu. \v 18 Nilikuwa nimetakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya. Hapakuwa na umati wa watu pamoja nami, wala sikuhusika katika ghasia yoyote. \v 19 Lakini kuna Wayahudi fulani kutoka jimbo la Asia ambao walipaswa kuwa hapa mbele yako na kunishtaki kama wana jambo lolote dhidi yangu. \v 20 Au, watu hawa walio hapa waseme ni kosa gani walilonipata nalo waliponisimamisha mbele ya Baraza la Wayahudi\f + \fr 24:20 \fr*\fq Baraza la Wayahudi \fq*\ft ina maana ya \ft*\fqa Sanhedrin \fqa*\ft ambalo lilikuwa baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi; liliundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.\ft*\f*, \v 21 isipokuwa ni kuhusu jambo hili moja nililopaza sauti mbele yao na kusema, ‘Mimi nashtakiwa mbele yenu leo kwa sababu ya ufufuo wa wafu.’ ” \p \v 22 Basi Feliksi, ambaye alifahamu vizuri habari za Njia Ile\f + \fr 24:22 \fr*\fq Njia Ile \fq*\ft maana yake \ft*\fqa wafuasi wa Isa \fqa*\ft (\+xt Yohana 14:6\+xt*; \+xt Matendo 24:14\+xt*); walichukuliwa kuwa dhehebu la dini ya Wayahudi.\ft*\f*, akaahirisha kesi ile, akasema, “Jemadari Lisia atakapoteremka huku, nitaamua kesi yenu.” \v 23 Ndipo akaamuru kiongozi wa askari amweke chini ya ulinzi lakini ampe uhuru na kuwaruhusu rafiki zake wamhudumie. \p \v 24 Baada ya siku kadhaa, Feliksi alikuja pamoja na Drusila mkewe, aliyekuwa Myahudi. Alituma aitiwe Paulo, naye akamsikiliza alipokuwa akinena kuhusu imani katika Al-Masihi Isa. \v 25 Naye Paulo alipokuwa akinena kuhusu haki, kuwa na kiasi na kuhusu hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu, akasema, “Hiyo yatosha sasa! Unaweza kuondoka. Nitakapokuwa na muda, nitakuita.” \v 26 Wakati huo Feliksi alitazamia kwamba Paulo angempa rushwa. Hivyo akawa anamwita mara kwa mara na kuzungumza naye. \p \v 27 Baada ya miaka miwili kupita, Porkio Festo akaingia kwenye utawala mahali pa Feliksi, lakini kwa kuwa Feliksi alitaka kuwapendeza Wayahudi, akamwacha Paulo gerezani. \c 25 \s1 Paulo mbele ya Festo \p \v 1 Siku tatu baada ya Festo kuwasili Kaisaria kuchukua wajibu wake mpya, alipanda kwenda Yerusalemu, \v 2 ambako viongozi wa makuhani na viongozi wa Wayahudi walikuja mbele yake na kuleta mashtaka yao dhidi ya Paulo. \v 3 Wakamsihi sana Festo, kama upendeleo kwao, aamuru Paulo ahamishiwe Yerusalemu, kwa kuwa walikuwa wanaandaa kumvizia ili wamuue akiwa njiani. \v 4 Festo akawajibu, “Paulo amezuiliwa huko Kaisaria, nami mwenyewe ninaenda huko hivi karibuni. \v 5 Baadhi ya viongozi wenu wafuatane nami na kutoa mashtaka dhidi ya mtu huyo huko, kama amekosa jambo lolote.” \p \v 6 Baada ya Festo kukaa miongoni mwao kwa karibu siku nane au kumi, akashuka kwenda Kaisaria na siku iliyofuata akaitisha mahakama, akaketi penye kiti chake cha hukumu, akaamuru Paulo aletwe mbele yake. \v 7 Paulo alipotokea, wale Wayahudi waliokuwa wameteremka toka Yerusalemu wakasimama wakiwa wamemzunguka, wakileta mashtaka mengi mazito dhidi yake ambayo hawakuweza kuyathibitisha. \p \v 8 Ndipo Paulo akajitetea, akasema, “Mimi sikufanya jambo lolote kinyume cha sheria ya Wayahudi au dhidi ya Hekalu au kinyume cha Kaisari.” \p \v 9 Festo, akitaka kuwapendeza Wayahudi, akamuuliza Paulo, “Je, ungependa kwenda Yerusalemu na kukabili mashtaka mbele yangu huko?” \p \v 10 Paulo akasema, “Mimi sasa nimesimama mbele ya mahakama ya Kaisari, ambako ninastahili kushtakiwa. Kama vile wewe mwenyewe unavyojua vyema kabisa sijawatendea Wayahudi kosa lolote. \v 11 Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lolote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna yeyote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!” \p \v 12 Baada ya Festo kufanya shauri pamoja na baraza lake, akatangaza, “Wewe umeomba rufaa kwa Kaisari, nako kwa Kaisari utaenda!” \s1 Festo aomba ushauri kwa Agripa \p \v 13 Baada ya siku kadhaa Mfalme Agripa na Bernike wakapanda kuja Kaisaria kumsalimu Festo. \v 14 Kwa kuwa walikuwa wakae huko Kaisaria kwa siku nyingi, Festo alijadili kesi ya Paulo na mfalme, akisema, “Kuna mtu mmoja hapa ambaye Feliksi alimwacha gerezani. \v 15 Nilipokuwa huko Yerusalemu, viongozi wa makuhani na wazee wa Wayahudi walinijulisha habari zake na wakaomba hukumu dhidi yake. \p \v 16 “Lakini mimi nikawaambia kwamba si desturi ya Kirumi kumtoa mtu yeyote auawe kabla mshtakiwa kuonana uso kwa uso na washtaki wake, naye awe amepewa nafasi ya kujitetea kuhusu mashtaka anayoshutumiwa. \v 17 Hivyo walipokutana hapa, sikukawia, kesho yake niliitisha baraza, nikaketi kwenye kiti changu cha hukumu, nikaagiza huyo mtu aletwe. \v 18 Washtaki wake walipoinuka kuzungumza, hawakumshtaki kwa uhalifu wowote kama nilivyotarajia. \v 19 Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu aitwaye Isa aliyekufa, lakini Paulo alidai kwamba yu hai. \v 20 Kwa kuwa sikujua jinsi ya kupeleleza jambo hili, nilimuuliza kama angependa kwenda Yerusalemu na kuhojiwa huko kuhusu mashtaka haya. \v 21 Lakini Paulo alipoomba afadhiliwe ili rufaa yake isikilizwe na Mfalme Agusto, nilimwamuru alindwe hadi nitakapoweza kumpeleka kwa Kaisari.” \p \v 22 Ndipo Agripa akamwambia Festo, “Ningependa kumsikiliza mtu huyo mimi mwenyewe.” \p Yeye akajibu, “Kesho utamsikia.” \s1 Paulo mbele ya Agripa \p \v 23 Siku iliyofuata Agripa na Bernike walifika kwa fahari kubwa wakaingia katika ukumbi wa mahakama, pamoja na majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa mji. Ndipo Paulo akaletwa ndani kwa amri ya Festo. \v 24 Festo akasema, “Mfalme Agripa, nanyi nyote mlio hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu! Jumuiya yote ya Kiyahudi wamenilalamikia kuhusu mtu huyu huko Yerusalemu na hapa Kaisaria, wakipiga kelele kwamba hapaswi kuendelea kuishi. \v 25 Sikuona kwamba ametenda jambo lolote linalostahili kifo, ila kwa kuwa alikuwa ameomba rufaa yake kwa mfalme, niliamua kumpeleka Rumi. \v 26 Lakini mimi sina kitu maalum cha kumwandikia Bwana Mtukufu kumhusu mtu huyu. Hivyo basi, nimemleta mbele yenu ninyi nyote, hasa mbele yako, Mfalme Agripa, ili kutokana na matokeo ya uchunguzi huu, niweze kupata kitu cha kuandika. \v 27 Kwa kuwa naona hakuna sababu ya kumpeleka mfungwa bila kuainisha mashtaka dhidi yake.” \c 26 \s1 Paulo ajitetea mbele ya Agripa \p \v 1 Ndipo Agripa akamwambia Paulo, “Una ruhusa kujitetea.” \p Hivyo Paulo akawaashiria kwa mkono wake, akaanza kujitetea, akasema: \v 2 “Mfalme Agripa, najiona kuwa na heri kusimama mbele yako leo ninapojitetea kuhusu mashtaka yote ya Wayahudi, \v 3 hasa kwa sababu unajua vyema desturi zote za Kiyahudi na ya kuwa wewe unajua kwa undani mila na masuala ya mabishano. Kwa hiyo, nakusihi unisikilize kwa uvumilivu. \p \v 4 “Wayahudi wote wanajua jinsi nilivyoishi tangu nilipokuwa mtoto, kuanzia mwanzo wa maisha yangu katika nchi yangu na pia huko Yerusalemu. \v 5 Wao wamenifahamu kwa muda mrefu, na wanaweza kushuhudia wakipenda kushuhudia, kwamba kutokana na misimamo mikali sana ya dhehebu letu kwenye dini yetu, niliishi nikiwa Farisayo\f + \fr 26:5 \fr*\ft Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.\ft*\f*. \v 6 Nami sasa ni kwa sababu ya tumaini langu katika kile ambacho Mungu aliwaahidi baba zetu, ninashtakiwa leo. \v 7 Hii ndiyo ahadi ambayo makabila yetu kumi na mawili yanatarajia kuiona ikitimizwa wanapomtumikia Mungu kwa bidii usiku na mchana. Ee mfalme, ninashtakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hili. \v 8 Kwa nini yeyote miongoni mwenu afikiri kwamba ni jambo lisilosadikika Mungu kufufua wafu? \p \v 9 “Mimi pia nilikuwa nimeshawishika kwamba imenipasa kufanya yote yale yaliyowezekana kupinga Jina la Isa Al-Nasiri. \v 10 Nami hayo ndiyo niliyoyafanya huko Yerusalemu. Kwa mamlaka ya viongozi wa makuhani, niliwafunga watakatifu wengi gerezani, na walipokuwa wakiuawa nilipiga kura yangu kuunga mkono. \v 11 Mara nyingi nilienda kutoka sinagogi\f + \fr 26:11 \fr*\ft Nyumba ya ibada na mafunzo.\ft*\f* moja hadi lingine nikiamuru waadhibiwe, nami nilijaribu kuwalazimisha wakufuru. Katika shauku yangu dhidi yao, hata nilienda miji ya kigeni ili kuwatesa. \s1 Paulo aeleza kuhusu kuokoka kwake \r (Matendo 9:1-19; 22:6-16) \p \v 12 “Siku moja nilipokuwa katika mojawapo ya safari hizi nikiwa ninaenda Dameski, nilikuwa na mamlaka na agizo kutoka kwa kiongozi wa makuhani. \v 13 Ilikuwa yapata adhuhuri, ee mfalme, nilipokuwa njiani, niliona nuru kutoka mbinguni iliyong’aa kuliko jua, ikatuangaza pande zote, mimi na wale niliokuwa pamoja nao. \v 14 Wote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, ‘Sauli, Sauli, mbona unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’ \p \v 15 “Nikauliza, ‘Ni nani wewe, Bwana?’ \p “Naye Bwana akajibu, ‘Ni mimi Isa unayemtesa. \v 16 Sasa inuka usimame kwa miguu yako. Nimekutokea ili nikuteue uwe mtumishi na shahidi wa mambo ambayo umeyaona, na yale nitakayokuonesha. \v 17 Nitakuokoa kutoka kwa watu wako na watu wa Mataifa ambao ninakutuma kwao, \v 18 uyafumbue macho yao ili wageuke kutoka gizani waingie nuruni, na kutoka kwa nguvu za Shetani wamgeukie Mungu, ili wapate msamaha wa dhambi na sehemu miongoni mwa wale waliotakaswa kwa kuniamini mimi.’ \p \v 19 “Hivyo basi, Mfalme Agripa, sikuacha kuyatii yale maono yaliyotoka mbinguni, \v 20 bali niliyatangaza kwanza kwa wale wa Dameski, kisha Yerusalemu na katika vijiji vyote vya Yudea na pia kwa watu wa Mataifa, kwamba inawapasa kutubu na kumgeukia Mungu na kuthibitisha toba yao kwa matendo yao. \v 21 Ni kwa sababu hii Wayahudi walinikamata nilipokuwa Hekaluni, wakataka kuniua. \v 22 Hadi leo nimepata msaada kutoka kwa Mungu, na hivyo nasimama hapa nikishuhudia kwa wakubwa na wadogo. Sisemi chochote zaidi ya yale ambayo manabii na Musa walisema yatatukia: \v 23 kwamba Al-Masihi\f + \fr 26:23 \fr*\fq Al-Masihi \fq*\ft maana yake \ft*\fqa Aliyetiwa mafuta.\fqa*\f* atateswa, na kwamba yeye atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, na atatangaza nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.” \s1 Paulo aeleza juu ya kuhubiri kwake \p \v 24 Paulo alipokuwa akifanya utetezi huu, Festo akasema kwa sauti kubwa, “Paulo, wewe umerukwa na akili! Kusoma kwingi kunakufanya uwe kichaa!” \p \v 25 Lakini Paulo akajibu, “Mimi sijarukwa na akili, mtukufu sana Festo, bali nanena kweli nikiwa na akili zangu timamu. \v 26 Naam, mfalme anajua kuhusu mambo haya yote, nami nasema naye kwa uhuru. Kwa sababu nina hakika kwamba hakuna hata mojawapo ya mambo haya asilolijua, kwa kuwa hayakufanyika mafichoni. \v 27 Mfalme Agripa, je, unaamini manabii? Najua kuwa unaamini.” \p \v 28 Agripa akamwambia Paulo, “Je, unanishawishi kwa haraka namna hii niwe mfuasi wa Al-Masihi?” \p \v 29 Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.” \p \v 30 Baada ya kusema hayo, mfalme akainuka pamoja na mtawala na Bernike na wale waliokuwa wameketi pamoja nao. \v 31 Walipokuwa wakiondoka, wakaambiana, “Mtu huyu hafanyi jambo lolote linalostahili kifo au kifungo.” \p \v 32 Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeachwa huru kama hangekuwa amekata rufaa kwa Kaisari.” \c 27 \s1 Paulo asafiri kwenda Rumi \p \v 1 Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa meli kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa kiongozi mmoja wa askari aliyeitwa Juliasi, aliyekuwa wa Kikosi cha Walinzi wa Kaisari. \v 2 Tulipanda meli iliyotoka Adramitio, iliyokuwa inakaribia kusafiri kwenda kwenye bandari zilizopo pwani ya jimbo la Asia, tukaanza safari yetu tukiwa pamoja na Aristarko, Mmakedonia kutoka Thesalonike. \p \v 3 Kesho yake tukatia nanga Sidoni, naye Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kwa rafiki zake ili wamtimizie mahitaji yake. \v 4 Kutoka huko tukaingia baharini tena na tukapita upande wa chini wa kisiwa cha Kipro kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. \v 5 Baada ya sisi kuvuka bahari iliyo upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira huko Likia. \v 6 Huko yule kiongozi wa askari akapata meli ya Iskanderia ikielekea Italia, akatupandisha humo. \v 7 Tukasafiri polepole kwa siku nyingi na kwa shida, hatimaye tukafika karibu na Nido. Kwa kuwa upepo wa mbisho ulituzuia tusiweze kushika mwelekeo tuliokusudia, tukapita chini ya Krete mkabala na Salmone. \v 8 Tukaambaa na pwani kwa shida, tukafika sehemu iitwayo Bandari Nzuri, karibu na mji wa Lasea. \p \v 9 Muda mwingi ulikuwa umepotea, na kusafiri baharini kulikuwa hatari, kwa sababu wakati huu ulikuwa baada ya Siku ya Kufunga\f + \fr 27:9 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Siku ya Upatanisho \fqa*\ft ambayo iliadhimishwa kwa kufunga (\+xt Walawi 16:29\+xt*; \+xt Walawi 23:26-32\+xt*)\ft*\f*. Hivyo Paulo akawaonya akasema, \v 10 “Mabwana, naona kuwa hii safari ni yenye maafa na ya kuleta hasara kubwa kwa meli na shehena, pia kwa maisha yetu.” \v 11 Lakini badala ya yule kiongozi wa askari kusikiliza yale Paulo aliyosema, akafuata zaidi ushauri wa nahodha na mwenye meli. \v 12 Kwa kuwa ile bandari ilikuwa haifai kukaa wakati wa majira ya baridi, wengi wakashauri kwamba tuendelee na safari wakitarajia kufika Foinike na kukaa huko kwa majira ya baridi. Hii ilikuwa bandari iliyo katika kisiwa cha Krete ikikabili upande wa kusini-magharibi na kaskazini-magharibi. \s1 Dhoruba baharini \p \v 13 Upepo mtulivu ulipoanza kuvuma toka kusini, wakadhani kuwa wangeweza kufikia lengo lao, hivyo wakang’oa nanga na kusafiri wakipita kandokando ya pwani ya kisiwa cha Krete. \v 14 Lakini baada ya muda mfupi, ikavuma tufani kubwa iitwayo Eurakilo\f + \fr 27:14 \fr*\ft yaani \ft*\fqa upepo wa kaskazini-mashariki\fqa*\f* kutoka kisiwa cha Krete. \v 15 Meli ikapigwa na dhoruba na haikuweza kushindana na ule upepo, tukarudishwa baharini upepo ulikokuwa unaelekea. \v 16 Hatimaye tukisafiri kupita chini ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu. \v 17 Watu walipokwisha kuivuta mashua hiyo na kuiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba chini ya meli yenyewe ili kuzishikanisha pamoja. Wakiogopa kupelekwa kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, wakashusha matanga wakaiacha meli isukumwe na huo upepo. \v 18 Tulikuwa tunapigwa na dhoruba kwa nguvu, kiasi kwamba kesho yake walianza kutupa shehena toka kwenye meli. \v 19 Siku ya tatu, wakatupa vyombo vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe. \v 20 Wakati jua wala nyota hazikuonekana kwa siku nyingi, na dhoruba iliendelea kuvuma, hatimaye tulikata tamaa ya kuokolewa. \p \v 21 Baada ya watu kukaa siku nyingi bila kula chakula, Paulo akasimama mbele yao na kusema: “Enyi watu, kama mngekubali ushauri wangu wa kutosafiri kwa meli kutoka Krete, basi mngejiepusha na uharibifu na hasara hii. \v 22 Sasa ninawasihi sana, jipeni moyo kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake, ila meli itaangamia. \v 23 Jana usiku, malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake na ninayemwabudu alisimama karibu nami, \v 24 akaniambia, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amekupa kwa neema uhai wa wote wanaosafiri pamoja nawe.’ \v 25 Hivyo jipeni moyo, enyi watu, kwa kuwa ninamwamini Mungu kwamba yatakuwa kama vile alivyoniambia. \v 26 Lakini hata hivyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani.” \s1 Meli yavunjika \p \v 27 Usiku wa kumi na nne ulipofika, tulikuwa bado tunasukumwa na upepo katika Bahari ya Adria. Ilipokuwa yapata usiku wa manane, mabaharia wakahisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu. \v 28 Kwa hiyo wakapima kina cha maji na kukuta kilikuwa pima ishirini\f + \fr 27:28 \fr*\ft Pima 20 ni kama mita 37.\ft*\f*; baada ya kuendelea mbele kidogo, wakapima tena wakapata kina cha pima kumi na tano\f + \fr 27:28 \fr*\ft Pima 15 ni kama mita 27.\ft*\f*. \v 29 Wakiogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, wakashusha nanga nne za nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke. \v 30 Katika jaribio la kutoroka kutoka kwa meli, mabaharia wakashusha mashua ya kuokolea watu baharini, wakijifanya kwamba wanaenda kushusha nanga za omo\f + \fr 27:30 \fr*\ft au \ft*\fqa gubeti\fqa*\f*. \v 31 Ndipo Paulo akamwambia yule jemadari na askari, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokoka.” \v 32 Hivyo basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua ya kuokolea watu kwenye meli, wakaiacha ianguke humo baharini. \p \v 33 Kabla ya mapambazuko, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi mkiwa mmefunga na bila kula chochote. \v 34 Kwa hiyo nawasihi mle chakula, kwa maana itawasaidia ili mweze kuishi. Kwa kuwa hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza unywele hata mmoja kutoka kichwani mwake.” \v 35 Baada ya kusema maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula. \v 36 Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chakula. \v 37 Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu mia mbili na sabini na sita (276). \v 38 Baada ya watu wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini. \p \v 39 Kulipopambazuka, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga, ambako waliamua kuipweleza meli kama ingewezekana. \v 40 Kwa hiyo wakatupa nanga zote na kuziacha baharini, na wakati huo huo wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli. Kisha wakatweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani. \v 41 Lakini wakafika mahali bahari mbili zinakutana, wakaipweleza meli ufuoni; omo ikakwama sana, ikawa haiwezi kuondolewa; lakini sehemu ya shetri\f + \fr 27:41 \fr*\ft au \ft*\fqa tezi\fqa*\f* ikavunjika vipande vipande kutokana na kupigwa kwa mawimbi yenye nguvu. \p \v 42 Wale askari wakapanga kuwaua wale wafungwa ili kuzuia hata mmoja wao asiogelee na kutoroka. \v 43 Lakini yule jemadari alitaka kuokoa maisha ya Paulo, basi akawazuia askari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee hadi nchi kavu. \v 44 Waliosalia wangefika nchi kavu kwa kutumia mbao au vipande vya meli iliyovunjika, hivyo wote wakafika nchi kavu salama. \c 28 \s1 Paulo kisiwani Malta \p \v 1 Baada ya kufika nchi kavu salama, ndipo tukafahamu kwamba jina la kile kisiwa ni Malta. \v 2 Wenyeji wa kile kisiwa walituonesha ukarimu usio wa kawaida. Waliwasha moto na kutukaribisha sisi sote kwa sababu mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi. \v 3 Paulo alikusanya mzigo wa kuni, na alipokuwa anaweka kuni kwenye moto, nyoka mwenye sumu akatoka humo kwa ajili ya joto na kujisokotea mkononi mwake. \v 4 Wale wenyeji wa kile kisiwa walipomwona yule nyoka akining’inia mkononi mwa Paulo, wakaambiana, “Huyu mtu lazima awe ni muuaji, ingawa ameokoka kutoka baharini, haki haijamwacha aishi.” \v 5 Lakini Paulo akamkung’utia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yoyote. \v 6 Watu walikuwa wanangoja avimbe au aanguke ghafula na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichomtokea, wakabadili mawazo yao na kuanza kusema kwamba yeye ni mungu. \p \v 7 Basi karibu na sehemu ile, palikuwa na shamba kubwa la kiongozi mkuu wa kile kisiwa, aliyeitwa Publio. Alitupokea kwake, na akatuhudumia kwa ukarimu mkubwa kwa muda wa siku tatu. \v 8 Baba yake Publio alikuwa mgonjwa kitandani, akiwa anaugua homa na kuhara damu. Paulo akaingia ndani ili kumwona na baada ya maombi, akaweka mikono juu yake na kumponya. \v 9 Jambo hili lilipotukia, watu wote wa kisiwa kile waliokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. \v 10 Wakatupatia heshima nyingi, nasi tulipokuwa tayari kusafiri kwa meli, wakatupakilia vitu vyote tulivyokuwa tunavihitaji. \s1 Paulo awasili Rumi \p \v 11 Miezi mitatu baadaye tukaanza safari kwa meli iliyokuwa imetia nanga kwenye kisiwa hicho kwa ajili ya majira ya baridi. Hii ilikuwa meli ya Iskanderia yenye alama ya miungu pacha waitwao Kasta na Poluksi. \v 12 Kituo chetu cha kwanza kilikuwa Sirakusa na tukakaa huko siku tatu. \v 13 Kisha tukang’oa nanga, tukafika Regio. Siku iliyofuata, upepo mkali wa kusi ukavuma, na siku ya pili yake tukafika Puteoli. \v 14 Huko tukawakuta ndugu, nasi tukakaribishwa tukae nao kwa siku saba. Hivyo tukaendelea na safari hadi Rumi. \v 15 Ndugu wa huko Rumi waliposikia habari zetu, walikuja hadi Soko la Apio na mahali paitwapo Mikahawa Mitatu kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akatiwa moyo. \v 16 Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda. \s1 Paulo ahubiri Rumi chini ya ulinzi \p \v 17 Siku tatu baadaye Paulo akawaita pamoja viongozi wa Wayahudi. Walipokwisha kukusanyika akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lolote dhidi ya watu wetu au dhidi ya desturi za baba zetu, lakini nilikamatwa huko Yerusalemu nikakabidhiwa kwa Warumi. \v 18 Wao walipokwisha kunihoji, wakataka kuniachia huru kwa sababu hawakuona kosa lolote nililolifanya linalostahili adhabu ya kifo. \v 19 Lakini Wayahudi walipopinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ingawa sikuwa na lalamiko lolote juu ya taifa langu. \v 20 Basi hii ndiyo sababu nimewatumania, ili niseme nanyi. Kwa kuwa ni kwa ajili ya tumaini la Israeli nimefungwa kwa minyororo.” \p \v 21 Wakamjibu, “Hatujapokea barua zozote kutoka Yudea zinazokuhusu, wala hapana ndugu yeyote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lolote baya juu yako. \v 22 Lakini tungependa kusikia kutoka kwako unalofikiri kwa sababu tunajua kwamba kila mahali watu wanazungumza mabaya kuhusu jamii hii.” \p \v 23 Baada ya kupanga siku ya kuonana naye, watu wengi wakaja kuanzia asubuhi hadi jioni akawaeleza na kutangaza kuhusu ufalme wa Mungu akijaribu kuwahadithia juu ya Isa kutoka Torati ya Musa na kutoka Manabii. \v 24 Baadhi wakasadiki yale aliyosema, lakini wengine hawakuamini. \v 25 Hivyo hawakukubaliana, nao walipokuwa wanaondoka, Paulo akatoa kauli moja zaidi: “Roho wa Mungu alinena kweli na baba zenu aliposema mambo yale yaliyomhusu Bwana Isa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba: \q1 \v 26 “ ‘Nenda kwa watu hawa na useme, \q1 “Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa; \q2 na pia mtatazama, lakini hamtaona.” \q1 \v 27 Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu; \q2 hawasikii kwa masikio yao, \q2 na wamefumba macho yao. \q1 Wasije wakaona kwa macho yao, \q2 na wakasikiliza kwa masikio yao, \q2 wakaelewa kwa mioyo yao, \q1 na kugeuka nami nikawaponya.’ \p \v 28 “Basi na ijulikane kwenu kwamba, huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, nao watasikiliza.” [ \v 29 Baada yake kusema maneno haya, Wayahudi wakaondoka wakiwa na hoja nyingi miongoni mwao.]\f + \fr 28:29 \fr*\ft Maandiko mengine ya kale hayana maneno haya.\ft*\f* \p \v 30 Kwa miaka miwili mizima Paulo alikaa huko kwa nyumba aliyokuwa amepanga. Akawakaribisha wote walioenda kumwona. \v 31 Akahubiri ufalme wa Mungu na kufundisha mambo yale yaliyomhusu Bwana Isa Al-Masihi, kwa ujasiri wote na bila kizuizi chochote.