\id 3JN - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 3 Yohana \toc1 3 Yohana \toc2 3 Yohana \toc3 3Yn \mt1 3 Yohana \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Mzee. \po Kwa Gayo rafiki yangu nimpendaye katika kweli. \s1 Gayo anatiwa moyo \p \v 2 Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo. \v 3 Ilinifurahisha sana baadhi ya ndugu walipokuja na kutueleza kuhusu uaminifu wako katika kweli na jinsi unavyoendelea kuenenda katika hiyo kweli. \v 4 Sina furaha kubwa kuliko hii, ya kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli. \p \v 5 Rafiki mpendwa, wewe ni mwaminifu kwa yale unayowatendea ndugu, ingawa wao ni wageni kwako. \v 6 Wameshuhudia kuhusu upendo wako mbele ya jumuiya ya waumini. Utafanya vyema ukiwasafirisha kama inavyostahili kwa Mungu. \v 7 Ilikuwa ni kwa ajili ya hilo Jina waliondoka, bila kukubali kupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasiomwamini Al-Masihi. \v 8 Kwa hiyo imetupasa sisi kuonesha ukarimu kwa watu kama hao ili tuweze kutenda kazi pamoja kwa ajili ya kweli. \s1 Deotrefe anakemewa \p \v 9 Nililiandikia kundi la waumini, lakini Deotrefe, yeye apendaye kujifanya wa kwanza, hakubali mamlaka yetu. \v 10 Hivyo nikija, nitakumbuka matendo yake atendayo, akitusingizia kwa maneno ya hila. Wala hatosheki na hayo anayotusingizia, bali pia hukataa kuwakaribisha ndugu, na hata huwazuia wale walio tayari kufanya hivyo na kuwafukuza watoke miongoni mwa waumini. \s1 Demetrio anasifiwa \p \v 11 Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema anatoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu. \p \v 12 Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli. \b \b \s1 Hitimisho \p \v 13 Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino. \v 14 Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana. \b \p \v 15 Amani iwe kwako. \b \p Rafiki zetu walio hapa wanakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu walio huko, kila mmoja kwa jina lake.