\id 2TH - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 2 Wathesalonike \toc1 2 Wathesalonike \toc2 2 Wathesalonike \toc3 2The \mt1 2 Wathesalonike \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Paulo, Silvano\f + \fr 1:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Sila\fqa*\f* na Timotheo. \po Kwa kundi la waumini la Wathesalonike mlio katika Mungu, Baba\f + \fr 1:1 \fr*\ft Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yetu, na Bwana Isa Al-Masihi. \po \v 2 Neema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba Mwenyezi na kwa Bwana Isa Al-Masihi ziwe nanyi. \s1 Shukrani na maombi \p \v 3 Ndugu, inatupasa kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, na inastahili hivyo kwa sababu imani yenu inazidi kukua sana, nao upendo wa kila mmoja wenu kwa mwenzake unazidi kuongezeka. \v 4 Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivunia saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili. \p \v 5 Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili yake. \v 6 Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wanaowatesa ninyi, \v 7 na kuwapa ninyi mnaoteseka amani pamoja na sisi, wakati Bwana Isa atadhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. \v 8 Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Isa. \v 9 Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa uweza wake, \v 10 siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu. \p \v 11 Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mungu wetu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu. \v 12 Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Isa lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Isa Al-Masihi. \c 2 \s1 Yule mtu wa kuasi \p \v 1 Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Isa Al-Masihi na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, \v 2 msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho, wala neno la unabii, au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, kusema kwamba siku ya Mwenyezi Mungu imekwisha kuwepo. \v 3 Mtu yeyote asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja hadi uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. \v 4 Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu. \p \v 5 Je, hamkumbuki kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? \v 6 Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. \v 7 Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo hadi atakapoondolewa. \v 8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Isa atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. \v 9 Kuja kwa yule mwasi kutalingana na vile Shetani hufanya kazi. Atatumia nguvu za aina mbalimbali katika miujiza, na ishara na ajabu za uongo, \v 10 na katika njia zote ambazo uovu hudanganya wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli ili wapate kuokolewa. \v 11 Kwa sababu hii, Mungu anawatumia nguvu ya udanganyifu, ili waamini uongo, \v 12 na hivyo wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu. \s1 Simameni imara \p \v 13 Lakini inatupasa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana Isa, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho wa Mungu kwa kuiamini kweli. \v 14 Kwa kusudi hili Mungu aliwaita ninyi kupitia Injili tuliyowahubiria, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi. \p \v 15 Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua. \p \v 16 Bwana wetu Isa Al-Masihi mwenyewe na Mungu, Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, \v 17 awafariji mioyo yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema. \c 3 \s1 Hitaji la maombi \p \v 1 Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana Isa lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu. \v 2 Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini. \v 3 Lakini Bwana Isa ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu. \v 4 Nasi tuna tumaini katika Bwana Isa ya kuwa mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. \v 5 Mwenyezi Mungu aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika saburi ya Al-Masihi. \s1 Onyo dhidi ya uvivu \p \v 6 Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Isa Al-Masihi, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. \v 7 Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, \v 8 wala hatukula chakula cha mtu yeyote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote miongoni mwenu. \v 9 Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe mfano wenu wa kufuata. \v 10 Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.” \p \v 11 Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi, bali hujishughulisha na mambo ya wengine. \v 12 Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Isa Al-Masihi, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe. \v 13 Lakini kwenu ninyi, ndugu, kamwe msichoke katika kutenda mema. \p \v 14 Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyo katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu. \v 15 Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu. \b \s1 Salamu za mwisho \p \v 16 Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Mwenyezi Mungu awe nanyi nyote. \b \p \v 17 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo. \b \p \v 18 Neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi nyote. Amen.