\id 2KI - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \ide UTF-8 \h 2 Wafalme \toc1 2 Wafalme \toc2 2 Wafalme \toc3 2Fal \mt1 2 Wafalme \c 1 \s1 Hukumu ya Mwenyezi Mungu juu ya Ahazia \p \v 1 Baada ya kifo cha Mfalme Ahabu, nchi ya Moabu iliasi dhidi ya Israeli. \v 2 Basi Ahazia alikuwa ameanguka huko Samaria kutoka baraza ya chumba chake cha juu, akaumia. Hivyo akatuma wajumbe, akiwaambia, “Nendeni mkaulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, mkaone kama nitapona kutokana na kuumia huku.” \p \v 3 Lakini malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Ilya Mtishbi, “Panda uende ukakutane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, uwaulize, ‘Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana mnaenda kumuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni?’ \v 4 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, ‘Hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!’ ” Hivyo Ilya akaenda. \p \v 5 Wajumbe waliporudi kwa mfalme, akawauliza, “Kwa nini mmerudi?” \p \v 6 Wakamjibu, “Mtu mmoja alikuja kukutana nasi, naye akatuambia, ‘Rudini kwa mfalme aliyewatuma na mkamwambie, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ndiyo maana unawatuma watu kwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa hiyo hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” ’ ” \p \v 7 Mfalme akawauliza, “Alikuwa mtu wa namna gani ambaye mlikutana naye, akawaambia hili?” \p \v 8 Wakamjibu, “Alikuwa mtu aliyekuwa na vazi la manyoya na mkanda wa ngozi kiunoni mwake.” \p Mfalme akasema, “Huyo alikuwa ni Ilya Mtishbi.” \p \v 9 Ndipo mfalme akamtuma mkuu mmoja wa kikosi pamoja na kikosi chake cha askari hamsini kwa nabii Ilya. Yule mkuu wa kikosi akamwendea Ilya, aliyekuwa ameketi juu ya kilima, na kumwambia, “Mtu wa Mungu, mfalme anasema, ‘Shuka chini!’ ” \p \v 10 Ilya akamjibu yule mkuu wa kikosi, “Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na watu wako hamsini!” Ndipo moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza yule mkuu wa kikosi pamoja na watu wake. \p \v 11 Aliposikia hili, mfalme akatuma kwa Ilya mkuu wa kikosi mwingine na askari wake hamsini. Yule mkuu wa kikosi akamwambia Ilya, “Mtu wa Mungu, hili ndilo asemalo mfalme, ‘Shuka chini mara moja!’ ” \p \v 12 Ilya akajibu, “Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke kutoka mbinguni ukuteketeze wewe na watu wako hamsini!” Ndipo moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza yeye na watu wake hamsini. \p \v 13 Hivyo mfalme akatuma mkuu wa kikosi wa tatu na watu wake hamsini. Huyu mkuu wa kikosi wa tatu akapanda na kupiga magoti mbele ya Ilya, akiomba, “Mtu wa Mungu, tafadhali niachie uhai wangu na uhai wa hawa watu hamsini, watumishi wako! \v 14 Tazama, moto umeshuka kutoka mbinguni na kuwateketeza wale wakuu wa vikosi viwili vya kwanza pamoja na watu wao. Lakini sasa niachie uhai wangu!” \p \v 15 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Ilya, “Shuka pamoja naye, usimwogope.” Hivyo Ilya akainuka na kushuka pamoja naye kwa mfalme. \p \v 16 Akamwambia mfalme, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Je, ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli wa kumuuliza habari, ndiyo maana ukatuma wajumbe kuuliza Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni? Kwa sababu umefanya hili, kamwe hutaondoka kwenye kitanda unachokilalia. Hakika utakufa!” \v 17 Hivyo akafa, sawasawa na lile neno la Mwenyezi Mungu ambalo Ilya alikuwa amesema. \p Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yoramu\f + \fr 1:17 \fr*\ft au \ft*\fqa Yehoramu\fqa*\f* akawa mfalme baada yake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. \v 18 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Ahazia na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \c 2 \s1 Ilya achukuliwa mbinguni \p \v 1 Mwenyezi Mungu alipokuwa karibu kumchukua Ilya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Ilya na Al-Yasa walikuwa njiani wakitoka Gilgali. \v 2 Ilya akamwambia Al-Yasa, “Kaa hapa. Mwenyezi Mungu amenituma Betheli.” \p Lakini Al-Yasa akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo wakaenda Betheli pamoja. \p \v 3 Wana wa manabii waliokuwa Betheli wakamjia Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mwenyezi Mungu atakuondolea bwana wako leo?” \p Al-Yasa akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze kuhusu jambo hilo.” \p \v 4 Kisha Ilya akamwambia, “Baki hapa, Al-Yasa. Mwenyezi Mungu amenituma Yeriko.” \p Naye akajibu, “Kwa hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko. \p \v 5 Wana wa manabii waliokuwa Yeriko wakamwendea Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mwenyezi Mungu atakuondolea bwana wako leo?” \p Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.” \p \v 6 Kisha Ilya akamwambia, “Kaa hapa. Mwenyezi Mungu amenituma kwenda Yordani.” \p Naye akamjibu, “Kwa hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja. \p \v 7 Wana hamsini wa manabii wakaenda na kusimama kwa mbali, kuelekea mahali Ilya na Al-Yasa waliposimama kando ya Mto Yordani. \v 8 Ilya akatoa vazi lake, akalikunja na kupiga maji nalo. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu. \p \v 9 Walipokwisha kuvuka, Ilya akamwambia Al-Yasa, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?” \p Al-Yasa akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.” \p \v 10 Ilya akasema, “Umeomba jambo gumu. Lakini kama utaniona wakati ninapoondolewa kutoka kwako litakuwa lako. La sivyo, hutalipata.” \p \v 11 Walipokuwa wakitembea pamoja na kuzungumza, ghafula gari la farasi la moto na farasi wa moto vilitokea na kuwatenganisha wao wawili, naye Ilya akapanda mbinguni katika upepo wa kisulisuli. \v 12 Al-Yasa aliliona hili, naye akapaza sauti, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!” Naye Al-Yasa hakumwona tena. Kisha akaishika nguo yake na kuirarua vipande viwili. \p \v 13 Akaliokota lile vazi lililoanguka kutoka kwa Ilya, kisha akarudi na kusimama ukingoni mwa Yordani. \v 14 Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Ilya, naye akayapiga yale maji nalo. Akauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ilya?” Al-Yasa alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka. \p \v 15 Wale wana wa manabii kutoka Yeriko waliokuwa wakitazama wakasema, “Roho ya Ilya inamkalia Al-Yasa.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi chini mbele yake. \v 16 Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho wa Mwenyezi Mungu amemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.” \p Al-Yasa akajibu, “Hapana, msiwatume.” \p \v 17 Lakini wakasisitiza, hata akaona aibu kuwakatalia. Hivyo akasema, “Watumeni.” Nao wakawatuma watu hamsini, wakamtafuta kwa siku tatu, lakini hawakumpata. \v 18 Walipomrudia Al-Yasa, aliyekuwa akingojea huko Yeriko, akawaambia, “Je, sikuwaambia msiende?” \s1 Kuponywa kwa maji \p \v 19 Watu wa mji wakamwambia Al-Yasa, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu anavyoona, lakini maji yake ni mabaya, na nchi haina mazao.” \p \v 20 Akasema, “Nileteeni bakuli mpya, mweke chumvi ndani yake.” Kwa hiyo wakamletea. \p \v 21 Kisha akaenda kwenye chemchemi na kuitupa ile chumvi ndani yake, akisema, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Nimeyaponya maji haya. Kamwe hayatasababisha mauti tena wala kutozaa.’ ” \v 22 Nayo yale maji yakaponywa hadi leo, sawasawa na neno la Al-Yasa alilokuwa amesema. \s1 Al-Yasa afanyiwa mzaha \p \v 23 Kutoka huko Al-Yasa akakwea kwenda Betheli. Ikawa alipokuwa akitembea barabarani, baadhi ya vijana wakatoka mjini na kumfanyia mzaha. Wakasema, “Paa, wewe mwenye upara! Paa, wewe mwenye upara!” \v 24 Akageuka, akawatazama na kuwalaani kwa Jina la Mwenyezi Mungu. Kisha dubu jike wawili wakatokea mwituni na kuwararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao. \v 25 Naye akaondoka huko, akaenda Mlima Karmeli, na kutoka huko akarudi Samaria. \c 3 \s1 Moabu wanaasi \p \v 1 Yehoramu\f + \fr 3:1 \fr*\ft au \ft*\fqa Yoramu\fqa*\f* mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na mbili. \v 2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, lakini sio kama baba yake na mama yake walivyokuwa wamefanya. Akaondoa nguzo ya ibada ya Baali ambayo baba yake alikuwa ameitengeneza. \v 3 Hata hivyo akashikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, wala hakuziacha. \p \v 4 Basi Mesha mfalme wa Moabu alikuwa mfuga kondoo; naye akatakiwa kumlipa mfalme wa Israeli ushuru wa wana-kondoo elfu mia moja, na sufu ya kondoo dume elfu mia moja. \v 5 Lakini baada ya Ahabu kufa, mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli. \v 6 Kwa hiyo wakati ule Mfalme Yehoramu akaondoka kutoka Samaria na kukusanya Israeli yote tayari kwenda vitani. \v 7 Akapeleka pia ujumbe ufuatao kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda: “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je, utaenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” \p Akajibu, “Nitaenda pamoja nawe. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.” \p \v 8 Akauliza, “Je, tutashambulia kupitia njia gani?” \p Akajibu, “Kupitia Jangwa la Edomu.” \p \v 9 Hivyo mfalme wa Israeli akaondoka akiwa pamoja na mfalme wa Yuda na mfalme wa Edomu. Baada ya kuzunguka kwa siku saba, jeshi likawa limeishiwa maji kwa matumizi yao na kwa ajili ya wanyama waliokuwa nao. \p \v 10 Mfalme wa Israeli akapaza sauti, akasema, “Nini! Je, Mwenyezi Mungu ametuita sisi wafalme watatu ili tu kututia mikononi mwa Moabu?” \p \v 11 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Mwenyezi Mungu hapa, ili tuweze kumuuliza Mwenyezi Mungu kupitia kwake?” \p Afisa mmoja wa mfalme wa Israeli akajibu, “Al-Yasa mwana wa Shafati yuko hapa. Ndiye alikuwa akimimina maji juu ya mikono ya Ilya.” \p \v 12 Yehoshafati akasema, “Neno la Mwenyezi Mungu liko pamoja naye.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli na Yehoshafati pamoja na mfalme wa Edomu wakamwendea. \p \v 13 Al-Yasa akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina uhusiano gani nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.” \p Mfalme wa Israeli akajibu, “La, sivyo, kwa sababu ni Mwenyezi Mungu ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.” \p \v 14 Al-Yasa akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni aishivyo, ninayemtumikia, kama si kwa heshima niliyo nayo kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekujali hata kidogo. \v 15 Lakini sasa, nileteeni mpiga kinubi.” \p Mpiga kinubi alipokuwa akipiga, mkono wa Mwenyezi Mungu ukaja juu ya Al-Yasa, \v 16 naye akasema, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, ‘Chimbeni bonde hili lijae mahandaki.’ \v 17 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Hamtaona upepo wala mvua, lakini bonde hili litajaa maji, nanyi pamoja na ng’ombe wenu na wanyama wenu wengine mtakunywa. \v 18 Hili ni jambo rahisi machoni pa Mwenyezi Mungu. Pia ataitia Moabu mikononi mwenu. \v 19 Mtaushinda kila mji wenye ngome na kila mji mkubwa. Mtakata kila mti ulio mzuri, mtaziba chemchemi zote, na kuharibu kila shamba zuri kwa mawe.” \p \v 20 Kesho yake asubuhi, karibu na wakati wa kutoa dhabihu ya asubuhi, tazama, maji yakawa yanatiririka kutoka upande wa Edomu! Nayo nchi ikajaa maji. \p \v 21 Basi Wamoabu wote walikuwa wamesikia kuwa wale wafalme wamekuja kupigana dhidi yao. Hivyo kila mtu, kijana na mzee, ambaye angeweza kushika silaha akaitwa na kuwekwa mpakani. \v 22 Walipoamka asubuhi na mapema, jua likawa linamulika juu ya maji. Wamoabu waliokuwa upande wa pili wakaona maji ni mekundu, kama damu. \v 23 Wamoabu wakasema, “Ile ni damu! Lazima hao wafalme wamepigana na kuchinjana wao kwa wao. Sasa Moabu, twendeni tukateke nyara!” \p \v 24 Lakini Wamoabu walipofika kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakainuka na kuwapiga hata wakakimbia. Nao Waisraeli wakaivamia nchi na kuwachinja Wamoabu. \v 25 Wakaiharibu miji, kila mtu akatupa jiwe juu ya kila shamba zuri hadi likafunikwa. Wakaziba chemchemi zote na kukata kila mti mzuri. Kir-Haresethi peke yake ndio uliobaki na mawe yake yakiwa mahali pake. Lakini hata hivyo watu waliokuwa na makombeo wakauzunguka na kuushambulia. \p \v 26 Mfalme wa Moabu alipoona kuwa vita vimekuwa vikali dhidi yake, akachukua watu mia saba wenye panga ili kuingia kwa mfalme wa Edomu, lakini wakashindwa. \v 27 Ndipo akamchukua mwanawe mzaliwa wake wa kwanza, ambaye angekuwa mfalme baada yake, akamtoa kama dhabihu ya kuteketezwa juu ya ukuta wa mji. Ghadhabu ikawa kubwa dhidi ya Israeli; wakajiondoa kwake na kurudi katika nchi yao wenyewe. \c 4 \s1 Mafuta ya mjane \p \v 1 Mke wa mmoja wa wana wa manabii akamlilia Al-Yasa, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu, amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha Mwenyezi Mungu. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake.” \p \v 2 Al-Yasa akamjibu, “Nitawezaje kukusaidia? Niambie, una nini ndani ya nyumba yako?” \p Akasema, “Mtumishi wako hana kitu chochote kabisa, isipokuwa mafuta kidogo.” \p \v 3 Al-Yasa akasema, “Zunguka kwa majirani zako wote ukaombe vyombo vitupu. Usiombe vichache. \v 4 Kisha ingia ndani na ujifungie mlango, wewe na wanao. Mimina mafuta kwenye vyombo vyote, na kila kimoja kinapojaa, kiweke kando.” \p \v 5 Yule mjane akaondoka na kujifungia ndani, yeye na wanawe. Wao wakamletea vyombo, naye akaendelea kumimina mafuta. \v 6 Vyombo vyote vilipojaa, akamwambia mwanawe, “Niletee chombo kingine.” \p Lakini mwanawe akajibu, “Hakuna chombo kingine kilichobaki.” Basi mafuta yakakoma kutiririka. \p \v 7 Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.” \s1 Mwana wa Mshunami afufuliwa \p \v 8 Siku moja Al-Yasa akaenda Shunemu. Huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo, naye akamsisitiza Al-Yasa aje kula chakula. Kwa hiyo kila mara alipitia pale, akaingia humo ili ale. \v 9 Akamwambia mumewe, “Ninajua kwamba huyu mtu ambaye anakuja kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. \v 10 Tutengeneze chumba kidogo juu darini na tuweke ndani yake kitanda na meza, kiti na taa kwa ajili yake. Kisha anaweza kukaa humo kila mara akija kwetu.” \p \v 11 Siku moja Al-Yasa alipofika, akapanda chumbani kwake na kulala humo. \v 12 Akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Mwite huyo Mshunami.” Hivyo akamwita, naye akaja akasimama mbele yake. \v 13 Al-Yasa akamwambia mtumishi wake, “Mwambie huyu mwanamke, ‘Umetaabika sana kwa ajili yetu. Sasa utendewe nini? Je, tunaweza kuzungumza na mfalme au jemadari wa jeshi kwa niaba yako?’ ” \p Akajibu, “Mimi ninaishi kwangu miongoni mwa watu wangu.” \p \v 14 Al-Yasa akamuuliza mtumishi wake, “Je, ni nini kinachoweza kufanyika kwa ajili yake?” \p Gehazi akasema, “Hakika, hana mwana, na mume wake ni mzee.” \p \v 15 Ndipo Al-Yasa akasema, “Mwite huyo mwanamke.” Kwa hiyo akamwita, naye akaja akasimama mlangoni. \v 16 Al-Yasa akamwambia, “Mwaka ujao, wakati kama huu utabeba mwana mikononi mwako.” \p Yule mama akapinga, akasema, “La hasha, bwana wangu! Usimdanganye mtumishi wako, ee mtu wa Mungu!” \p \v 17 Lakini yule mwanamke akapata mimba, na mwaka uliofuata wakati kama ule ule akamzaa mwana, kama vile Al-Yasa alivyokuwa amemwambia. \p \v 18 Mtoto akakua, naye siku moja akamwendea baba yake, aliyekuwa pamoja na wavunaji. \v 19 Akamwambia baba yake, “Kichwa changu! Kichwa changu!” \p Baba yake akamwambia mtumishi, “Mchukue umpeleke kwa mama yake.” \v 20 Baada ya mtumishi kumbeba na kumpeleka kwa mama yake, mtoto akaketi mapajani mwa mama yake hadi adhuhuri, kisha akafa. \v 21 Mama akampandisha na kumlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, kisha akafunga mlango, akatoka nje. \p \v 22 Akamwita mume wake na kusema, “Tafadhali mtume mmoja miongoni mwa mtumishi pamoja na punda ili niweze kwenda kwa mtu wa Mungu haraka na kurudi.” \p \v 23 Mume wake akamuuliza, “Kwa nini uende kwake leo? Leo si mwandamo wa mwezi, wala si Sabato.” \p Mwanamke akasema, “Yote ni sawa.” \p \v 24 Akatandika punda na kumwambia mtumishi wake, “Mwongoze huyo punda. Usinipunguzie mwendo hadi nikuambie.” \v 25 Kwa hiyo akaenda na kumfikia huyo mtu wa Mungu katika Mlima Karmeli. \p Alipomwona kwa mbali, huyo mtu wa Mungu akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Tazama, yule Mshunami! \v 26 Kimbia ukamlaki, umuulize, ‘Je, wewe hujambo? Mume wako hajambo? Mtoto wako ni mzima?’ ” \p Akasema, “Kila kitu ni sawasawa.” \p \v 27 Alipomfikia huyo mtu wa Mungu pale mlimani, akashika miguu yake. Gehazi akaja ili amwondoe, lakini yule mtu wa Mungu akasema, “Mwache! Yuko katika uchungu mkubwa, lakini Mwenyezi Mungu amenificha jambo hili na hajaniambia kwa nini.” \p \v 28 Yule mwanamke akasema, “Je, bwana wangu, mimi nilikuomba mwana? Je, sikukuambia, ‘Usiamshe matumaini yangu’?” \p \v 29 Al-Yasa akamwambia Gehazi, “Jikaze viuno, chukua fimbo yangu mkononi mwako na ukimbie. Ikiwa utakutana na mtu yeyote, usimsalimie, na mtu yeyote akikusalimu, usimjibu. Ilaze fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.” \p \v 30 Lakini mama mtoto akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo Al-Yasa akainuka, akafuatana naye. \p \v 31 Gehazi akatangulia mbele na kuilaza fimbo juu ya uso wa mtoto, lakini hapakuwa na sauti wala itikio. Hivyo Gehazi akarudi kukutana na Al-Yasa, na kumwambia, “Mtoto hajaamka.” \p \v 32 Al-Yasa alipofika kwenye ile nyumba, mtoto alikuwa amelala juu ya kitanda chake angali amekufa. \v 33 Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba Mwenyezi Mungu. \v 34 Kisha akapanda kitandani, akalala juu ya yule mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, macho yake juu ya macho ya mtoto, mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Naye alipojinyoosha juu yake, mwili wa mtoto ukapata joto. \v 35 Al-Yasa akajiondoa juu yake na kuanza kutembeatembea ndani ya chumba, kisha akarudi tena kitandani na kujinyoosha tena juu ya mtoto mara nyingine. Mtoto akapiga chafya mara saba, akafungua macho yake. \p \v 36 Al-Yasa akamwita Gehazi na kumwambia, “Mwite huyo Mshunami.” Naye akafanya hivyo. Yule Mshunami alipokuja, Al-Yasa akasema, “Mchukue mwanao.” \v 37 Akaingia ndani, akaanguka miguuni pa Al-Yasa na kusujudu hadi chini. Kisha akamchukua mwanawe na kutoka nje. \s1 Mauti ndani ya chungu \p \v 38 Al-Yasa akarudi Gilgali, nako huko kulikuwa na njaa katika eneo lile. Wana wa kundi la manabii walipokuwa wanakutana naye, akamwambia mtumishi wake, “Teleka chungu kikubwa jikoni uwapikie manabii.” \p \v 39 Mmoja wao akatoka kwenda mashambani kuchuma mboga na akapata mtango-mwitu. Akachuma matango na kujaza nguo yake aliyoikunja ili kubebea. Aliporudi, akayakatakata na kuyatumbukiza ndani ya chungu, ingawa hakuna aliyejua ni nini. \v 40 Mchuzi ukagawiwa watu, lakini walipoanza kula, wakalia, “Ee mtu wa Mungu, kuna mauti ndani ya chungu.” Nao hawakuweza kula. \p \v 41 Al-Yasa akasema, “Leteni unga.” Akauweka ndani ya chungu na kusema, “Wagawie watu ili wale.” Wala hapakuwa na kitu chochote chenye madhara ndani ya chungu. \s1 Watu mia wanalishwa \p \v 42 Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutoka kwa nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Al-Yasa akasema, “Wape watu ili wale.” \p \v 43 Mtumishi wake akamuuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia moja?” \p Lakini Al-Yasa akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Watakula na kusaza.’ ” \v 44 Basi akaiandaa mbele yao ile mikate, wakala na baadhi yake wakasaza, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu. \c 5 \s1 Naamani aponywa ukoma \p \v 1 Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Mwenyezi Mungu alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ukoma.\f + \fr 5:1 \fr*\fq ukoma \fq*\ft ni neno lililotumika kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi\ft*\f* \p \v 2 Siku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimeenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani. \v 3 Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angemwona nabii aliye huko Samaria! Angemponya ukoma wake.” \p \v 4 Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. \v 5 Mfalme wa Aramu\f + \fr 5:5 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Shamu\fqa*\f* akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi\f + \fr 5:5 \fr*\ft Talanta 10 za fedha ni sawa na kilo 340.\ft*\f* za fedha, shekeli elfu sita za dhahabu\f + \fr 5:5 \fr*\ft Shekeli 6,000 za dhahabu ni sawa na kilo 70.\ft*\f*, na mavazi kumi. \v 6 Barua aliyopelekea mfalme wa Israeli iliandikwa hivi: “Pamoja na barua hii ninamtuma mtumishi wangu, Naamani, kwako ili uweze kumponya ukoma wake.” \p \v 7 Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, “Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!” \p \v 8 Al-Yasa mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alikuwa amerarua mavazi yake, akamtumia ujumbe huu: “Kwa nini umerarua mavazi yako? Mwamuru mtu huyo aje kwangu, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.” \v 9 Kwa hiyo Naamani akaenda, akiwa na farasi wake na magari yake ya vita, na kusimama mlangoni mwa nyumba ya Al-Yasa. \v 10 Al-Yasa akamtuma mjumbe kumwambia, “Nenda uoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itapona, nawe utatakasika.” \p \v 11 Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kupitisha mkono wake juu ya mahali penye ugonjwa ili aniponye ukoma wangu. \v 12 Je, Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko mito yoyote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga ndani ya hiyo mito na kutakasika?” Basi akageuka na kuondoka kwa hasira kuu. \p \v 13 Watumishi wa Naamani wakamwendea na kumwambia, “Baba yangu, kama huyo nabii angekuambia kufanya jambo lililo kubwa, je, hungelifanya? Je, si zaidi sana basi, anapokuambia, ‘Oga na utakasike!’ ” \v 14 Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. \p \v 15 Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.” \p \v 16 Nabii akajibu, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, ninayemtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa. \p \v 17 Naamani akasema, “Ikiwa hutapokea, tafadhali mtumishi wako na apewe udongo kiasi cha mzigo wa kuweza kubebwa na punda wawili, kwa sababu mtumishi wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa na dhabihu kwa mungu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu. \v 18 Lakini Mwenyezi Mungu na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, Mwenyezi Mungu na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.” \p \v 19 Al-Yasa akamwambia, “Nenda kwa amani.” \p Baada ya Naamani kusafiri umbali fulani, \v 20 Gehazi, mtumishi wa Al-Yasa mtu wa Mungu, akajiambia mwenyewe, “Bwana wangu amemwachia kirahisi sana Naamani, huyu Mwaramu\f + \fr 5:20 \fr*\ft au \ft*\fqa Mshami\fqa*\f*, kwa kutokupokea kutoka kwake vile alivyovileta. Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, nitamkimbilia na kupata kitu kutoka kwake.” \p \v 21 Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka gari lake la vita na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?” \p \v 22 Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha\f + \fr 5:22 \fr*\ft Talanta ni sawa na kilo 34.\ft*\f* na mavazi mawili.’ ” \p \v 23 Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mavazi mawili. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi. \v 24 Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka. \v 25 Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Al-Yasa bwana wake. \p Al-Yasa akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?” \p Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakuenda popote.” \p \v 26 Lakini Al-Yasa akamwambia, “Je, roho yangu haikuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka gari lake la vita ili kukulaki? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea nguo, mashamba ya mizeituni, mashamba ya mizabibu, makundi ya kondoo na mbuzi, makundi ya ng’ombe, au watumishi wa kiume na wa kike? \v 27 Ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Al-Yasa, mwenye ukoma, mweupe kama theluji. \c 6 \s1 Shoka laelea \p \v 1 Wana wa manabii wakamwambia Al-Yasa, “Tazama, mahali hapa tunapokutana nawe ni padogo sana kwetu. \v 2 Twendeni Yordani, ambapo kila mmoja wetu anaweza kupata nguzo moja, nasi tujenge huko mahali petu pa kuishi.” \p Naye akawaambia, “Nendeni.” \p \v 3 Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?” \p Al-Yasa akajibu, “Nitakuja.” \v 4 Naye akaenda pamoja nao. \p Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. \v 5 Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!” \p \v 6 Mtu wa Mungu akauliza, “Je, liliangukia wapi?” Alipomwonesha mahali penyewe, Al-Yasa akakata kijiti na kukitupa mahali pale, nalo shoka likaelea. \v 7 Akasema, “Lichukue.” Kisha yule mtu akanyoosha mkono wake, akalichukua. \s1 Al-Yasa awanasa Waaramu waliopofushwa \p \v 8 Wakati huo mfalme wa Aramu alikuwa akipigana vita na Israeli. Baada ya kukubaliana na maafisa wake, akasema, “Nitapiga kambi yangu mahali fulani na fulani.” \p \v 9 Mtu wa Mungu akatuma ujumbe kwa mfalme wa Israeli: “Jihadhari usije ukapita mahali pale, kwa sababu Waaramu wanashuka huko.” \v 10 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akatuma neno la tahadhari mahali pale alikokuwa ameelekezwa na mtu wa Mungu. Mara kwa mara Al-Yasa alimwonya mfalme kwamba watu wawe macho kwenye maeneo kama hayo. \p \v 11 Hili lilimfadhaisha sana mfalme wa Aramu. Akawaita maafisa wake, akawauliza, “Je, hamtaniambia ni nani miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?” \p \v 12 Mmoja wa maafisa wake akasema, “Mfalme bwana wangu, hakuna hata mmoja wetu. Lakini Al-Yasa, yule nabii aliye Israeli, humwambia mfalme wa Israeli hata yale maneno unayozungumza katika chumba chako cha kulala.” \p \v 13 Mfalme akaagiza akisema, “Nendeni, mkatafute aliko, ili niweze kutuma watu kumkamata.” Taarifa ikarudi kwamba, “Yuko Dothani.” \v 14 Ndipo akatuma farasi na magari ya vita na jeshi lenye nguvu huko. Walienda usiku na kuuzunguka mji. \p \v 15 Kesho yake asubuhi na mapema, mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka na kutoka nje, jeshi, pamoja na farasi na magari ya vita, likawa limeuzunguka mji. Mtumishi wake akasema, “Ole wetu, bwana wangu! Tutafanya nini?” \p \v 16 Nabii akajibu, “Usiogope. Wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.” \p \v 17 Kisha Al-Yasa akaomba, “Ee Mwenyezi Mungu, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo Mwenyezi Mungu akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya vita yaliyowaka moto yamemzunguka Al-Yasa pande zote. \p \v 18 Adui waliposhuka kumwelekea, Al-Yasa akamwomba Mwenyezi Mungu: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Al-Yasa alivyoomba. \p \v 19 Al-Yasa akawaambia, “Hii sio njia yenyewe, na huu sio huo mji. Nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa huyo mtu mnayemtafuta.” Naye akawapeleka Samaria. \p \v 20 Baada ya kuingia mjini, Al-Yasa akasema, “Mwenyezi Mungu, yafungue macho ya watu hawa ili wapate kuona.” Ndipo Mwenyezi Mungu akayafungua macho yao, na walipotazama, kumbe hapo ndipo walipojikuta, ndani ya Samaria. \p \v 21 Wakati mfalme wa Israeli aliwaona, akamuuliza Al-Yasa, “Je, baba yangu, niwaue?” \p \v 22 Naye akajibu, “Usiwaue. Je, utawaua watu uliowateka kwa upanga wako mwenyewe na upinde wako? Wape chakula na maji ili wapate kula na kunywa, na kisha wamrudie bwana wao.” \v 23 Basi akawaandalia karamu kubwa, na baada ya kula na kunywa, akawaaga nao wakarudi kwa bwana wao. Hivyo, vikosi kutoka Aramu vikakoma kuvamia nchi ya Israeli. \s1 Njaa katika Samaria iliyozingirwa \p \v 24 Baada ya kitambo kidogo, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akaandaa jeshi lake lote akapanda kwenda kuizingira Samaria. \v 25 Kukawa na njaa kuu katika mji. Samaria ilizingirwa kwa muda mrefu, kiasi kwamba kichwa cha punda kiliuzwa kwa shekeli themanini\f + \fr 6:25 \fr*\ft Shekeli 80 za fedha ni sawa na kilo moja.\ft*\f* za fedha, na robo ya kibaba\f + \fr 6:25 \fr*\ft Robo ya kibaba ni sawa na lita 0.3.\ft*\f* cha mavi ya njiwa kiliuzwa kwa shekeli tano\f + \fr 6:25 \fr*\ft Shekeli 5 ni sawa na gramu 55.\ft*\f* za fedha. \p \v 26 Mfalme wa Israeli alipokuwa anapita juu ya ukuta, mwanamke mmoja akamlilia, “Bwana wangu mfalme, nisaidie!” \p \v 27 Mfalme akajibu, “Ikiwa Mwenyezi Mungu hakusaidii, nitakutolea wapi msaada? Je, ni kwenye sakafu ya kupuria? Au ni kwenye shinikizo la kukamulia zabibu?” \v 28 Kisha akamuuliza, “Kwani kuna nini?” \p Yule mwanamke akamjibu, “Huyu mwanamke aliniambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate kumla leo, na kesho tutamla mwanangu.’ \v 29 Basi tukampika mwanangu na kumla. Siku iliyofuata nikamwambia, ‘Mtoe mwanao ili tupate kumla.’ Lakini akawa amemficha.” \p \v 30 Mfalme aliposikia maneno ya yule mwanamke, akararua mavazi yake. Naye alipoendelea kutembea ukutani, watu wakamtazama, na ndani ya mavazi yake alikuwa amevaa gunia mwilini mwake. \v 31 Akasema, “Mungu na aniadhibu vikali zaidi ikiwa kichwa cha Al-Yasa mwana wa Shafati kitabaki juu ya mabega yake leo!” \p \v 32 Wakati huu, Al-Yasa alikuwa ameketi ndani ya nyumba yake, akiwa pamoja na wazee. Mfalme akatuma mjumbe kumtangulia, lakini kabla hajafika, Al-Yasa akawaambia wale wazee, “Hammwoni huyu muuaji jinsi anavyotuma mtu kukata kichwa changu? Tazama, wakati mjumbe huyo atakapofika, fungeni mlango na mzuieni asiingie. Je, vishindo vya nyayo za bwana wake haviko nyuma yake?” \p \v 33 Alipokuwa angali bado anazungumza nao, mjumbe akamfikia. Naye mfalme akasema, “Maafa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa nini niendelee kumngoja Mwenyezi Mungu zaidi?” \c 7 \p \v 1 Al-Yasa akasema, “Sikiliza neno la Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja\f + \fr 7:1 \fr*\ft Kipimo kimoja cha unga ni sawa na kilo 3.\ft*\f* cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha\f + \fr 7:1 \fr*\ft Shekeli moja ni sawa na gramu 11.\ft*\f*, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.” \p \v 2 Yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake akamwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama Mwenyezi Mungu atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” \p Al-Yasa akajibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!” \s1 Mwisho wa kuzingirwa \p \v 3 Basi kulikuwa na watu wanne wenye ukoma katika ingilio la lango la mji. Wakaambiana, “Kwa nini tukae hapa hadi tufe? \v 4 Tukisema, ‘Tutaingia mjini,’ mjini kuna njaa, nasi tutakufa humo. Tukikaa hapa, tutakufa. Kwa hiyo twende kambi ya Waaramu, tujisalimishe. Wakituacha hai, tutaishi; wakituua, basi na tufe.” \p \v 5 Wakati wa mapambazuko, wakaondoka na kwenda kwenye kambi ya Waaramu. Walipofika mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu, \v 6 kwa kuwa Bwana alilifanya jeshi la Waaramu lisikie sauti kama ya magari ya vita, farasi na jeshi kubwa, kiasi kwamba waliambiana, “Tazama, mfalme wa Israeli ameajiri mfalme wa Wahiti na mfalme wa Wamisri kuja kutushambulia sisi!” \v 7 Kwa hiyo wakaondoka na kukimbia wakati wa giza la jioni na kuacha mahema yao, farasi wao na punda wao. Wakakimbia kuokoa maisha yao na kuacha kila kitu ndani ya kambi kama kilivyokuwa. \p \v 8 Wale watu wenye ukoma walipofika mwanzoni mwa kambi, wakaingia kwenye mojawapo ya mahema. Wakala na kunywa, na kuchukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuvificha. Wakarudi na kuingia katika hema lingine, na kuchukua baadhi ya vitu kutoka ndani yake na kuvificha pia. \p \v 9 Kisha wakaambiana, “Hili tunalolifanya sio jema. Hii ni siku ya habari njema, nasi tunakaa kimya. Tukisubiri hadi mapambazuko, maafa yatatupata. Twendeni mara moja tukatoe habari hizi katika jumba la mfalme.” \p \v 10 Hivyo wakaenda mjini na kuwaita walinzi wa langoni, wakawaambia, “Tulienda katika kambi ya Waaramu lakini hapakuwa na mtu huko, hata sauti ya mtu yeyote, ila farasi na punda waliofungwa, na mahema yaliyoachwa kama yalivyokuwa.” \v 11 Walinzi wa langoni wakatangaza habari ile kwa sauti kuu, na taarifa hii ikatolewa ndani ya jumba la mfalme. \p \v 12 Mfalme akaamka usiku na kuwaambia maafisa wake, “Nitawaambia kile Waaramu walichotufanyia. Wanajua kwamba tuna njaa, hivyo wameacha kambi yao ili kujificha mashambani, wakifikiri, ‘Kwa hakika watatoka nje ya mji, nasi tutawakamata wakiwa hai na kuingia ndani ya mji.’ ” \p \v 13 Mmoja wa maafisa wake akajibu, “Waamuru watu wachache wakawachukue farasi watano kati ya wale waliobaki katika mji. Hatima yao itakuwa kama ya Waisraeli wote walio hapa. Watakuwa tu kama Waisraeli hawa ambao wanangoja kifo. Hivyo tuwatumeni wajue kumetendeka nini.” \p \v 14 Ndipo wakachagua magari mawili ya vita pamoja na farasi wake, naye mfalme akawatuma wafuatilie jeshi la Waaramu. Akawaamuru waendeshaji akisema, “Nendeni mkaone ni nini kilichotokea.” \v 15 Wakawafuatia hadi Yordani, nao wakakuta barabara yote ikiwa imetapakaa mavazi na vyombo Waaramu walivyokuwa wamevitupa walipokuwa wakitoroka. Basi wale wajumbe wakarudi na kutoa taarifa kwa mfalme. \v 16 Kisha watu wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kwa hiyo kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema. \p \v 17 Basi mfalme alikuwa amemweka yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake awe msimamizi wa lango. Nao watu wakamkanyaga walipoingia langoni, naye akafa, kama vile mtu wa Mungu alivyokuwa ametangulia kusema wakati mfalme alipofika nyumbani mwake. \v 18 Ikatokea kama vile mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia mfalme: “Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.” \p \v 19 Yule afisa alikuwa amemwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama Mwenyezi Mungu atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Naye yule mtu wa Mungu alikuwa amemjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!” \v 20 Ndivyo hasa ilivyotokea kwake, kwa kuwa watu walimkanyaga langoni, naye akafa. \c 8 \s1 Ardhi ya Mshunami yarudishwa \p \v 1 Basi Al-Yasa alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa, “Ondoka wewe na jamaa yako ukaishi mahali popote unapoweza kwa kitambo kidogo, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamuru njaa katika nchi hii ambayo itadumu kwa miaka saba.” \v 2 Yule mwanamke akafanya kama vile yule mtu wa Mungu alivyosema. Yeye na jamaa yake wakaondoka na kwenda kuishi katika nchi ya Wafilisti kwa miaka saba. \p \v 3 Baada ya miaka saba, yule mwanamke akarudi kutoka nchi ya Wafilisti, akaenda kwa mfalme kumsihi kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. \v 4 Mfalme alikuwa anazungumza na Gehazi, mtumishi wa mtu wa Mungu, naye alikuwa amesema, “Hebu niambie mambo yote makuu yaliyofanywa na Al-Yasa.” \v 5 Gehazi alipokuwa akimweleza mfalme jinsi Al-Yasa alivyomfufua mtu, yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa na Al-Yasa akaja ili amsihi mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. \p Gehazi akasema, “Huyu ndiye huyo mwanamke, bwana wangu mfalme, na huyu ndiye mwanawe ambaye Al-Yasa alimfufua.” \v 6 Mfalme akamuuliza yule mwanamke kuhusu mambo hayo, naye akamweleza. \p Ndipo akaamuru afisa amshughulikie, kwa kumwambia, “Mrudishie huyu mwanamke kila kitu kilichokuwa mali yake, pamoja na mapato yote yaliyotokana na shamba lake tangu siku alipoondoka nchini hadi sasa.” \s1 Hazaeli amuua Ben-Hadadi \p \v 7 Al-Yasa akaenda Dameski, naye Ben-Hadadi mfalme wa Aramu alikuwa mgonjwa. Mfalme alipoambiwa, “Mtu wa Mungu amekuja hadi hapa,” \v 8 mfalme akamwambia Hazaeli, “Chukua zawadi na uende kumlaki mtu wa Mungu. Muulize Mwenyezi Mungu kupitia yeye, kwamba, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ” \p \v 9 Hazaeli akaenda kumlaki Al-Yasa, akiwa amechukua zawadi ya kila kitu kizuri kilichopatikana Dameski, mizigo iliyobebwa na ngamia arobaini. Akaingia ndani na kusimama mbele yake, akasema, “Mwanao Ben-Hadadi mfalme wa Aramu amenituma niulize, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ” \p \v 10 Al-Yasa akajibu, “Nenda ukamwambie, ‘Hakika utapona’; lakini Mwenyezi Mungu amenifunulia kwamba kweli atakufa.” \v 11 Al-Yasa akamkazia Hazaeli macho kwa nguvu hata akaona aibu. Kisha mtu wa Mungu akaanza kulia. \p \v 12 Hazaeli akauliza “Kwa nini bwana wangu analia?” \p Al-Yasa akajibu, “Kwa sababu najua mabaya utakayowatendea Waisraeli. Utachoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, kuwatupa chini kwa nguvu watoto wachanga, na kuwatumbua wanawake wenye mimba.” \p \v 13 Hazaeli akasema, “Itawezekanaje mtumishi wako, aliye mbwa tu, kufanya tendo la ajabu hivyo?” \p Al-Yasa akamjibu, “Mwenyezi Mungu amenionesha kuwa utakuwa mfalme wa Aramu.” \p \v 14 Kisha Hazaeli akamwacha Al-Yasa na kumrudia bwana wake. Ben-Hadadi akamuuliza, “Al-Yasa alikuambia nini?” Hazaeli akajibu, “Aliniambia kwamba hakika utapona.” \v 15 Lakini kesho yake Hazaeli akachukua nguo nzito, akailoweka ndani ya maji, akaitandaza juu ya uso wa mfalme, hivyo akafa. Kisha Hazaeli akawa mfalme baada yake. \s1 Yehoramu mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 21:1-20) \p \v 16 Katika mwaka wa tano wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, wakati huo Yehoshafati akiwa mfalme wa Yuda, Yehoramu mwana wa Yehoshafati akaanza kutawala kama mfalme wa Yuda. \v 17 Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka nane. \v 18 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti Ahabu. Akatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. \v 19 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, Mwenyezi Mungu hakutaka kuiangamiza Yuda. Alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili ya Daudi na wazao wake milele. \p \v 20 Wakati wa utawala wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. \v 21 Basi Yehoramu akaenda Sairi pamoja na magari yake yote ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. Hata hivyo, jeshi lake likatorokea nyumbani mwao. \v 22 Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. Libna pia wakaasi wakati huo huo. \p \v 23 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehoramu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 24 Yehoramu akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Ahazia mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 22:1-6) \p \v 25 Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda alianza kutawala. \v 26 Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia, mjukuu wa Omri mfalme wa Israeli. \v 27 Akaenenda katika njia za nyumba ya Ahabu, na kutenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alikuwa ameoa kutoka nyumba ya Ahabu. \p \v 28 Ahazia akaenda vitani na Yoramu mwana wa Ahabu kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu. \v 29 Hivyo Mfalme Yoramu akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyojeruhiwa na Waaramu huko Ramothi\f + \fr 8:29 \fr*\fqa Rama \fqa*\ft kwa Kiebrania\ft*\f* alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. \p Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa. \c 9 \s1 Yehu atiwa mafuta kuwa Mfalme \p \v 1 Nabii Al-Yasa akamwita mtu mmoja kutoka kwa wana wa manabii na kumwambia, “Jikaze viuno, uichukue hii chupa ya mafuta, na uende Ramoth-Gileadi. \v 2 Ukifika huko, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi. Nenda kwake, umtenge na wenzake, na umpeleke katika chumba cha ndani. \v 3 Kisha chukua hii chupa na umimine mafuta juu ya kichwa chake, nawe utangaze, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Ninakupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.’ Kisha ufungue mlango na ukimbie; usikawie!” \p \v 4 Basi yule kijana nabii akaenda Ramoth-Gileadi. \v 5 Alipofika, akawakuta maafisa wa jeshi wameketi pamoja, akasema, “Nina ujumbe wako, ee jemadari.” \p Yehu akauliza, “Kwa yupi miongoni mwetu?” \p Akamjibu, “Kwako wewe, jemadari.” \p \v 6 Yehu akainuka na kuingia ndani ya nyumba. Ndipo yule nabii akamimina mafuta juu ya kichwa cha Yehu, na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Ninakupaka mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Mwenyezi Mungu, yaani Israeli. \v 7 Inakupasa uiangamize nyumba ya bwana wako Ahabu, nami nitalipiza kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii na damu ya watumishi wote wa Mwenyezi Mungu iliyomwagwa na Yezebeli. \v 8 Nyumba yote ya Ahabu itaangamia. Nitamkatilia mbali kila mzaliwa wa kiume wa Ahabu katika Israeli, aliye mtumwa ama aliye huru. \v 9 Nitaifanya nyumba ya Ahabu kuwa kama ile nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama ile nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya. \v 10 Kuhusu Yezebeli, mbwa watamla kwenye kiwanja huko Yezreeli, wala hakuna mtu atakayemzika.’ ” Kisha akafungua mlango na kukimbia. \p \v 11 Yehu alipotoka nje na kurudi kwenda kwa maafisa wenzake, mmoja wao akamuuliza, “Je, kila kitu ni salama? Kwa nini huyu mwenye wazimu alikuja kwako?” \p Yehu akajibu, “Wewe unamfahamu huyo mtu, na aina ya mambo ambayo yeye husema.” \p \v 12 Wakasema, “Hiyo siyo kweli! Tuambie.” \p Yehu akasema, “Haya ndio aliyoniambia: ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Ninakupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.’ ” \p \v 13 Wakaharakisha kuvua mavazi yao, na kuyatandaza chini ya Yehu ili akanyage juu kwenye ngazi ya nje. Kisha wakapiga tarumbeta na kupaza sauti wakisema, “Yehu ni mfalme!” \s1 Yehu awaua Yoramu na Ahazia \p \v 14 Basi Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akapanga njama dhidi ya Yoramu. (Wakati huu, Yoramu na Waisraeli wote walikuwa wakiilinda Ramoth-Gileadi dhidi ya Hazaeli mfalme wa Aramu, \v 15 lakini Mfalme Yoramu alikuwa amerudishwa Yezreeli ili kujiuguza kutokana na majeraha ambayo Waaramu walimtia katika vita na Hazaeli mfalme wa Aramu.) Yehu akasema, “Kama hii ndiyo nia yenu, msimruhusu hata mmoja kutoroka nje ya mji kwenda kupeleka habari huko Yezreeli.” \v 16 Ndipo Yehu akaingia katika gari lake la vita na kuendesha kwenda Yezreeli, kwa sababu Yoramu alikuwa amepumzika huko, na Ahazia mfalme wa Yuda alikuwa ameenda kumwona. \p \v 17 Mlinzi aliyesimama juu ya kinara cha Yezreeli alipoona askari wa Yehu wanakuja, akaita akisema, “Naona askari wanakuja.” \p Yoramu akaamuru, “Mtwae mpanda farasi umtume akakutane nao na kuuliza, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ” \p \v 18 Mpanda farasi akaondoka kwenda kukutana na Yehu na kusema, “Hivi ndivyo asemavyo mfalme: ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ” \p Yehu akamjibu, “Una nini na amani? Unga msafara nyuma yangu.” \p Mlinzi akatoa habari, “Mjumbe amewafikia lakini harudi.” \p \v 19 Basi mfalme akamtuma mpanda farasi wa pili. Alipowafikia akasema, “Hivi ndivyo asemavyo mfalme, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ” \p Yehu akajibu, “Una nini na amani? Unga msafara nyuma yangu.” \p \v 20 Yule mlinzi akatoa taarifa akasema, “Mjumbe amewafikia, lakini hata yeye harudi. Uendeshaji ule ni kama wa Yehu mwana wa Nimshi, anaendesha kama mwenye wazimu!” \p \v 21 Yoramu akaagiza, akasema, “Weka tayari gari langu la vita.” Na baada ya gari kuwa tayari, Yoramu mfalme wa Israeli, na Ahazia mfalme wa Yuda, wakaondoka kila mmoja kwenye gari lake ili kukutana na Yehu. Walikutana naye katika shamba lililokuwa mali ya Nabothi, Myezreeli. \v 22 Yoramu alipomwona Yehu, akauliza, “Je, Yehu, umekuja kwa amani?” \p Yehu akajibu, “Kunawezaje kuwa na amani wakati ibada za sanamu na uchawi wa mama yako Yezebeli bado ziko?” \p \v 23 Yoramu akageuka nyuma na kukimbia, akimwambia Ahazia, “Huu ni uhaini, Ahazia!” \p \v 24 Kisha Yehu akatwaa upinde wake na kumchoma Yoramu katikati ya mabega. Mshale ukapenya kwenye moyo wake, naye akaanguka ghafula ndani ya gari lake la vita. \v 25 Yehu akamwambia Bidkari, mwendeshaji wa gari lake la vita, “Mwinue na umtupe katika shamba lililokuwa mali ya Nabothi, Myezreeli. Kumbuka jinsi mimi na wewe tulivyokuwa tukiendesha pamoja magari yetu ya vita nyuma ya Ahabu baba yake, wakati Mwenyezi Mungu alitoa unabii huu kumhusu: \v 26 ‘Jana niliona damu ya Nabothi na damu ya wanawe, nami kwa hakika nitakufanya uilipe juu ya shamba hili, asema Mwenyezi Mungu.’ Sasa basi, mwinue na umtupe juu ya kiwanja, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu.” \p \v 27 Ahazia mfalme wa Yuda alipoona kilichotokea, akakimbia kupitia barabara ya Beth-Hagani. Yehu akamkimbiza akipaza sauti na kusema, “Muue naye pia!” Wakamjeruhi katika gari lake la vita kwenye njia inayoelekea Guri karibu na Ibleamu, lakini akatorokea Megido, akafia huko. \v 28 Watumishi wake wakambeba kwa gari la vita na kumpeleka Yerusalemu, wakamzika pamoja na baba zake kwenye kaburi lake katika Mji wa Daudi. \v 29 (Katika mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu, Ahazia alianza kutawala katika Yuda.) \s1 Yezebeli auawa \p \v 30 Kisha Yehu akaenda Yezreeli. Yezebeli aliposikia habari hii, akayapaka macho yake wanja, akatengeneza nywele zake na kutazama nje dirishani. \v 31 Yehu alipokuwa akiingia langoni, Yezebeli akasema, “Je, umekuja kwa amani, Zimri, wewe muuaji wa bwana wako?” \p \v 32 Yehu akaangalia juu dirishani na kuita, “Je, ni nani aliye upande wangu? Ni nani?” Matowashi wawili au watatu wakamtazama. \v 33 Yehu akasema, “Mtupeni huyo mwanamke chini!” Kwa hiyo wakamtupa chini, nayo sehemu ya damu yake ikatapanyika ukutani, na nyingine juu ya farasi walipokuwa wakimkanyaga kwa miguu yao. \p \v 34 Yehu akaingia ndani, akala na akanywa. Akasema, “Mshughulikieni huyo mwanamke aliyelaaniwa. Mzikeni, kwa sababu alikuwa binti ya mfalme.” \v 35 Lakini walipotoka kwenda kumzika, hawakukuta kitu chochote isipokuwa fuvu la kichwa, miguu yake na mikono. \v 36 Wakarudi na kumwambia Yehu, ambaye alisema, “Hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu alilosema kwa kinywa cha mtumishi wake Ilya Mtishbi, kwamba: Katika kiwanja cha Yezreeli, mbwa wataila nyama ya Yezebeli. \v 37 Maiti ya Yezebeli itakuwa kama kinyesi juu ya ardhi katika uwanja wa Yezreeli, kwamba hakutakuwa mtu atakayeweza kusema, ‘Huyu ni Yezebeli.’ ” \c 10 \s1 Jamii ya Ahabu wauawa \p \v 1 Basi huko Samaria walikuwepo wana sabini wa nyumba ya Ahabu. Kwa hiyo Yehu akaandika barua na kuzituma Samaria: kwa maafisa wa Yezreeli, kwa wazee, na kwa walezi wa watoto wa Ahabu. Akasema, \v 2 “Mara tu barua hii itakapokufikia, kwa kuwa wana wa bwana wako wapo pamoja nawe, nawe una magari ya vita na farasi, mji wenye ngome na silaha, \v 3 mchague mwenye uwezo zaidi kati ya wana wa bwana wako, na umweke kwenye kiti cha utawala cha baba yake. Kisha upigane kwa ajili ya nyumba ya bwana wako.” \p \v 4 Lakini wakaogopa sana na kusema, “Ikiwa wafalme wawili hawakuweza kupambana na Yehu, sisi tutawezaje?” \p \v 5 Basi msimamizi wa jumba la mfalme, mtawala wa mji, na wazee na walezi wakatuma ujumbe huu kwa Yehu: “Sisi tu watumishi wako, na tutafanya kila kitu utakachosema. Hatutamteuwa mtu yeyote kuwa mfalme. Wewe fanya uonalo kuwa ni bora.” \p \v 6 Kisha Yehu akawaandikia barua ya pili, akisema, “Ikiwa ninyi mko upande wangu na mtanitii mimi, twaeni vichwa vya wana wa bwana wenu, na mnijie huku Yezreeli kesho wakati kama huu.” \p Wakati huo wana sabini wa mfalme walikuwa wakiishi pamoja na viongozi wa mji wa Samaria, waliokuwa wakiwalea. \v 7 Hiyo barua ilipowafikia, watu hawa wakawachukua wale wana sabini wa mfalme na kuwachinja wote. Wakaweka vichwa vyao ndani ya makapu na kumpelekea Yehu huko Yezreeli. \v 8 Mjumbe alipofika, akamwambia Yehu, “Wameleta vichwa vya wana wa mfalme.” \p Ndipo Yehu akaagiza, “Viwekeni malundo mawili katika ingilio la lango la mji hadi asubuhi.” \p \v 9 Kesho yake asubuhi, Yehu akatoka nje. Akasimama mbele ya watu wote na akasema, “Hamna hatia. Ni mimi niliyepanga njama dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua wote hawa? \v 10 Fahamuni basi kwamba, hakuna neno ambalo Mwenyezi Mungu amesema dhidi ya nyumba ya Ahabu ambalo halitatimia. Mwenyezi Mungu amefanya lile aliloahidi kupitia mtumishi wake Ilya.” \v 11 Hivyo Yehu akaua kila mtu huko Yezreeli aliyekuwa amebaki wa nyumba ya Ahabu, ikiwa ni pamoja na wakuu wake, rafiki zake wa karibu, na makuhani wake. Hakuacha yeyote anusurike. \p \v 12 Kisha Yehu akaondoka kuelekea Samaria. Alipokuwa njiani karibu na nyumba ya kukatia manyoya ya kondoo, yaani Beth-Ekedi ya wachunga kondoo, \v 13 Yehu akakutana na watu wa jamaa ya Ahazia mfalme wa Yuda, akauliza, “Ninyi ni nani?” \p Wao wakasema, “Sisi ni jamaa ya Ahazia, nasi tumeshuka kuwasalimu jamaa ya mfalme na ya mama malkia.” \p \v 14 Yehu akaagiza, “Wakamateni wakiwa hai!” Kwa hiyo wakawachukua wakiwa hai, watu arobaini na wawili, na kuwachinja kando ya kisima cha Beth-Ekedi. Hakuacha yeyote anusurike. \p \v 15 Baada ya kuondoka hapo, alimkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu, aliyekuwa akienda kumlaki. Yehu akamsalimu na kusema, “Je, moyo wako ni mnyofu kwangu kama moyo wangu ulivyo kwako?” \p Yehonadabu akajibu, “Ndiyo.” \p Yehu akasema, “Kama ndivyo, nipe mkono wako.” Yeye akampa mkono, naye Yehu akampandisha kwenye gari lake la vita. \v 16 Yehu akasema, “Twende pamoja ukaone wivu wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” Hivyo wakasafiri pamoja kwenye gari lake la vita. \p \v 17 Yehu alipofika Samaria, akawaua wale wote waliokuwa wamesalia wa jamaa ya Ahabu, akawaangamiza, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu alilosema kupitia Ilya. \s1 Watumishi wa Baali wauawa \p \v 18 Kisha Yehu akawaleta watu wote pamoja na kuwaambia, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo. Lakini Yehu atamtumikia zaidi. \v 19 Sasa waiteni manabii wote wa Baali, watumishi wake wote na makuhani wake wote. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja atakayekosekana, kwa sababu ninaenda kutoa kafara kubwa sana kwa Baali. Yeyote atakayeshindwa kuja hataendelea kuishi.” Lakini Yehu alifanya hivyo kwa hila ili apate kuwaangamiza watumishi wote wa Baali. \p \v 20 Yehu akasema, “Itisheni kusanyiko kwa heshima ya Baali.” Basi wakatangaza jambo hilo. \v 21 Kisha Yehu akapeleka ujumbe katika Israeli yote, nao watumishi wote wa Baali wakaja, hakuna hata mmoja ambaye hakufika. Wakasongamana ndani ya hekalu la Baali hadi likajaa tangu mlango hadi mwisho wake. \v 22 Naye Yehu akamwambia yule aliyekuwa mtunza chumba cha mavazi, “Leta majoho kwa ajili ya watumishi wote wa Baali.” Basi akawaletea majoho. \p \v 23 Kisha Yehu na Yehonadabu mwana wa Rekabu wakaingia ndani ya hekalu la Baali. Yehu akawaambia watumishi wa Baali, “Tazameni kila mahali mhakikishe kwamba hakuna hata mtumishi mmoja wa Mwenyezi Mungu aliye hapa pamoja nanyi, ila ni watumishi wa Baali tu.” \v 24 Kwa hiyo wakaingia ndani ili kutoa kafara na sadaka ya kuteketezwa. Wakati huu, Yehu alikuwa amewaweka watu wake themanini akiwa amewapa onyo kwamba, “Ikiwa mmoja wenu atamwachia mtu yeyote ninayemweka mikononi mwenu atoroke, itakuwa uhai wako kwa uhai wake.” \p \v 25 Mara baada ya Yehu kutoa sadaka ya kuteketezwa, akawaamuru walinzi na maafisa: “Ingieni ndani, waueni; asitoroke hata mmoja.” Basi wakawakatakata kwa upanga. Walinzi na maafisa wakazitupa zile maiti nje, kisha wakaingia mahali pa ndani pa ibada katika hekalu la Baali. \v 26 Wakaileta ile nguzo ya kuabudiwa nje ya hekalu la Baali, na wakaichoma moto. \v 27 Wakabomoa ile nguzo ya kuabudiwa ya Baali pamoja na hekalu la Baali, nao watu wakapafanya kuwa choo hadi leo. \p \v 28 Kwa hiyo Yehu akaangamiza kuabudiwa kwa Baali katika Israeli. \v 29 Hata hivyo, Yehu hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, yaani kuabudu ndama za dhahabu huko Betheli ya Dani. \p \v 30 Mwenyezi Mungu akamwambia Yehu, “Kwa kuwa umefanya vyema kwa kutimiza yaliyo sawa machoni pangu, na umetenda kwa nyumba ya Ahabu yale yote niliyokuwa nimekusudia kutenda, wazao wako wataketi kwenye kiti cha utawala cha Israeli hadi kizazi cha nne.” \v 31 Lakini Yehu hakuwa mwangalifu kushika sheria za Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda. \p \v 32 Katika siku hizo, Mwenyezi Mungu akaanza kupunguza ukubwa wa Israeli. Hazaeli akawashinda Waisraeli sehemu zote za nchi yao \v 33 mashariki mwa Yordani, katika nchi yote ya Gileadi (eneo la Gadi, Reubeni na Manase), kutoka Aroeri karibu na Bonde la Arnoni kupitia Gileadi hadi Bashani. \p \v 34 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehu, yote aliyofanya na mafanikio yake yote, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \p \v 35 Yehu akalala na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Yehoahazi mwanawe akawa mfalme baada yake. \v 36 Muda Yehu aliotawala Israeli huko Samaria ulikuwa miaka ishirini na nane. \c 11 \s1 Athalia na Yoashi \r (2 Nyakati 22:10–23:21) \p \v 1 Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akainuka na kuangamiza jamaa yote ya mfalme. \v 2 Lakini Yehosheba, binti ya Mfalme Yehoramu, aliyekuwa pia dada yake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala na kumficha humo ili Athalia asimwone; kwa hiyo hakuuawa. \v 3 Alibaki amefichwa pamoja na yaya wake katika Hekalu la Mwenyezi Mungu kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alikuwa akitawala nchi. \p \v 4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada akatumania wakuu wa vikundi vya mamia, na Wakari\f + \fr 11:4 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Wakerethi \fqa*\ft (taz. \+xt 1 Samweli 30:14; Ezekieli 25:16; Sefania 2:5, 6\+xt*).\ft*\f* na walinzi, nao wakaletwa kwake katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Alifanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Ndipo akawaonesha mwana wa mfalme. \v 5 Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi moja italinda jumba la kifalme, \v 6 theluthi nyingine Lango la Suri, na theluthi nyingine lango lililo nyuma ya walinzi, ambao hupeana zamu kulinda Hekalu. \v 7 Nanyi ambao mko katika makundi mengine mawili ambao kwa kawaida hupumzika siku ya Sabato, wote mtalinda Hekalu kwa ajili ya mfalme. \v 8 Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi. Yeyote anayesogelea safu zenu lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme popote aendapo.” \p \v 9 Wakuu wa vikosi vya mamia wakafanya vile kuhani Yehoyada aliagiza. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakiingia zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakienda mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada. \v 10 Ndipo akawapa wale wakuu mikuki na ngao zilizokuwa za Mfalme Daudi, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 11 Wale walinzi, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi mwake, wakajipanga kumzunguka mfalme, karibu na madhabahu na Hekalu, kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini mwa Hekalu. \p \v 12 Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano, na kumtangaza kuwa mfalme. Wakampaka mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!” \p \v 13 Athalia aliposikia kelele za walinzi pamoja na watu, akawaendea watu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 14 Akaangalia, na tazama, mfalme alikuwa amesimama karibu na nguzo, kama ilivyokuwa desturi. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kulia, “Uhaini! Uhaini!” \p \v 15 Kuhani Yehoyada akawaamuru majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, “Mtoeni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.” \v 16 Basi wakamkamata Athalia alipofika mahali farasi huingilia katika viwanja vya jumba la mfalme, wakamuua hapo. \p \v 17 Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Mwenyezi Mungu na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa Mwenyezi Mungu. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu. \v 18 Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu. \p Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 19 Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha ufalme; \v 20 nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia, kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga nyumbani mwa mfalme. \p \v 21 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala. \c 12 \s1 Yoashi akarabati Hekalu \p \v 1 Katika mwaka wa saba wa utawala wa Yehu, Yoashi alianza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia, kutoka Beer-Sheba. \v 2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza. \v 3 Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. \p \v 4 Yoashi akawaambia makuhani, “Kusanyeni fedha zote zitakazoletwa kama sadaka takatifu kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu, yaani fedha zilizokusanywa watu walipohesabiwa, fedha zilizopokelewa kutokana na nadhiri za watu binafsi, na fedha zilizoletwa kwa hiari hekaluni. \v 5 Kila kuhani na apokee fedha kutoka kwa mmoja wa watunza hazina, nazo zitumike kukarabati uharibifu wowote unaoonekana katika Hekalu.” \p \v 6 Lakini ikawa kufikia mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Mfalme Yoashi, makuhani walikuwa bado hawajalikarabati Hekalu. \v 7 Kwa hiyo Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na makuhani wengine, akawauliza, “Kwa nini hamtengenezi uharibifu uliofanyika hekaluni? Msichukue fedha zaidi kutoka kwa watunza hazina wenu kwa ajili ya matumizi yenu, lakini kuanzia sasa ni lazima fedha yote itumike kwa ajili ya kukarabati Hekalu.” \v 8 Makuhani wakakubali kuwa hawatakusanya tena fedha kutoka kwa watu na kwamba hawatakarabati Hekalu wenyewe. \p \v 9 Yehoyada kuhani akachukua kisanduku na akatoboa tundu kwenye kifuniko chake. Akakiweka kando ya madhabahu upande wa kulia unapoingia hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. Makuhani waliolinda ingilio wakaweka ndani ya kisanduku fedha zote ambazo zililetwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 10 Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuziweka katika mifuko. \v 11 Walipothibitisha kiasi cha hizo fedha, waliwapa watu walioteuliwa kusimamia kazi katika Hekalu. Kwa fedha hizo, wakawalipa wale watu waliofanya kazi katika Hekalu la Mwenyezi Mungu: maseremala na wajenzi, \v 12 waashi na wakata mawe. Walinunua mbao na mawe ya kuchongwa kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kulipia gharama nyingine zote za kulitengeneza. \p \v 13 Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu; \v 14 zililipwa kwa wafanyakazi, ambao walizitumia kwa kukarabati Hekalu. \v 15 Wao hawakudai hesabu ya fedha kutoka kwa wale waliowapa ili kuwalipa wafanyakazi, kwa sababu walifanya kwa uaminifu wote. \v 16 Fedha zilizopatikana kutokana na sadaka za hatia na sadaka za dhambi hazikuletwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu; zilikuwa mali ya makuhani. \p \v 17 Basi Hazaeli mfalme wa Aramu akapanda kuishambulia Gathi, akaiteka. Kisha akageuka ili kuishambulia Yerusalemu. \v 18 Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, wafalme wa Yuda, na vyombo vyake vyote ambavyo alikuwa ameviweka wakfu, pamoja na dhahabu yote iliyokuwa katika hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika jumba la kifalme; akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu. \p \v 19 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yoashi na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 20 Maafisa wake wakapanga njama dhidi yake, nao wakamuua Yoashi huko Beth-Milo, kwenye barabara inayoteremka kuelekea Sila. \v 21 Maafisa waliomuua walikuwa Yozabadi mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri. Akafa na akazikwa na baba zake katika Mji wa Daudi. Naye Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 13 \s1 Yehoahazi mfalme wa Israeli \p \v 1 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wa Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoahazi mwana wa Yehu alianza kutawala Israeli katika Samaria, naye akatawala miaka kumi na saba. \v 2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu kwa kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, na wala hakuziacha. \v 3 Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Israeli na kwa muda mrefu akawaweka chini ya utawala wa Hazaeli mfalme wa Aramu, na Ben-Hadadi mwanawe. \p \v 4 Ndipo Yehoahazi akamsihi Mwenyezi Mungu ampe rehema, naye Mwenyezi Mungu akamsikiliza, kwa maana aliona jinsi mfalme wa Aramu alivyokuwa akiwatesa Israeli vikali. \v 5 Mwenyezi Mungu akamtoa mwokozi kwa ajili ya Israeli, nao wakaokoka kutoka mamlaka ya Aramu. Hivyo Waisraeli wakaishi katika nyumba zao wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali. \v 6 Lakini hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda, bali wakaendelea kuzitenda. Nguzo ya Ashera pia iliendelea kusimama katika Samaria. \p \v 7 Hapakubaki kitu chochote katika jeshi la Yehoahazi isipokuwa wapanda farasi hamsini, magari kumi ya vita na askari wa miguu elfu kumi, kwa kuwa mfalme wa Aramu alikuwa amewaangamiza hao wengine na kuwafanya kama mavumbi wakati wa kupura nafaka. \p \v 8 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehoahazi, yote aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 9 Yehoahazi akalala na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Yehoashi\f + \fr 13:9 \fr*\ft au \ft*\fqa Yoashi\fqa*\f* mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Yehoashi mfalme wa Israeli \p \v 10 Katika mwaka wa thelathini na saba wa utawala wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala Israeli huko Samaria, naye akatawala miaka kumi na sita. \v 11 Alifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, na hakuacha dhambi yoyote kati ya zile za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda, bali aliendelea kuzitenda. \p \v 12 Na kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehoashi, yote aliyoyafanya na mafanikio yake, pamoja na vita vyake dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 13 Yehoashi akalala na baba zake, naye Yeroboamu akawa mfalme baada yake. Yehoashi akazikwa Samaria na wafalme wa Israeli. \p \v 14 Wakati huu, Al-Yasa alikuwa anaugua ugonjwa ambao baadaye ulimuua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!” \p \v 15 Al-Yasa akasema, “Leta upinde na baadhi ya mishale,” naye mfalme akafanya hivyo. \v 16 Al-Yasa akamwambia mfalme wa Israeli, “Shika upinde mikononi mwako.” Alipokwisha kuuchukua, Al-Yasa akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme. \p \v 17 Al-Yasa akasema, “Fungua dirisha la mashariki,” naye akalifungua. Al-Yasa akasema, “Piga mshale!” Naye akapiga mshale. Al-Yasa akasema, “Mshale wa ushindi wa Mwenyezi Mungu, mshale wa ushindi juu ya Aramu! Utawaangamiza Waaramu kabisa huko Afeki.” \v 18 Kisha akasema, “Chukua mishale,” naye mfalme akaichukua. Al-Yasa akamwambia, “Piga ardhi kwa hiyo mishale.” Akaipiga mara tatu, halafu akaacha. \p \v 19 Mtu wa Mungu akamkasirikia na akasema, “Ungepiga chini mara tano au sita, ndipo ungeishinda Aramu na kuiangamiza kabisa. Lakini sasa utaishinda mara tatu tu.” \p \v 20 Al-Yasa akafa, nao wakamzika. \p Vikosi vya Wamoabu vilikuwa vinashambulia nchi kwa vita kila mwaka wakati wa vuli. \v 21 Ikawa Waisraeli fulani walipokuwa wanamzika mtu, ghafula wakaona kikosi cha washambuliaji, basi wakaitupa ile maiti ya yule mtu ndani ya kaburi la Al-Yasa. Ile maiti ilipogusa mifupa ya Al-Yasa, yule mtu akafufuka na kusimama kwa miguu yake. \p \v 22 Hazaeli mfalme wa Aramu aliwatesa Israeli wakati wote wa utawala wa Yehoahazi. \v 23 Lakini Mwenyezi Mungu akawarehemu na akawahurumia, akaonesha kujishughulisha nao kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Hadi leo, hajawaangamiza wala kuwafukuza mbele zake. \p \v 24 Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, naye Ben-Hadadi mwanawe akawa mfalme baada yake. \v 25 Kisha Yehoashi mwana wa Yehoahazi akateka tena kutoka kwa Ben-Hadadi mwana wa Hazaeli ile miji aliyokuwa ameitwaa kwa vita kutoka kwa baba yake Yehoahazi. Yehoashi alimshinda mara tatu, hivyo akaweza kuiteka tena ile miji ya Waisraeli. \c 14 \s1 Amazia mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 25) \p \v 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda alianza kutawala. \v 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Yehoadani, kutoka Yerusalemu. \v 3 Akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, lakini sio kama Daudi baba yake alivyokuwa amefanya. Katika kila kitu alifuata mfano wa Yoashi baba yake. \p \v 4 Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. \p \v 5 Baada ya ufalme kuimarika mkononi mwake, aliwaua maafisa waliomuua mfalme baba yake. \v 6 Hata hivyo, hakuwaua wana wa wale wauaji, sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa, ambako Mwenyezi Mungu aliamuru, “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto kwa ajili ya baba zao. Kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.” \p \v 7 Ndiye aliwashinda Waedomu elfu kumi katika Bonde la Chumvi, na akauteka Sela katika vita, naye akauita Yoktheeli, jina ambalo mji huo unalo hadi leo. \p \v 8 Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tukabiliane uso kwa uso.” \p \v 9 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda: “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi uliokuwa Lebanoni, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni aliyekuwa Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti. \v 10 Hakika umeishinda Edomu, na sasa unajivuna. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani mwako! Kwa nini unachokoza na kujiletea anguko lako mwenyewe na la Yuda pia?” \p \v 11 Hata hivyo, Amazia hakusikia, hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akashambulia. Yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth-Shemeshi katika Yuda. \v 12 Yuda ikashindwa na Israeli, na kila mtu akakimbilia nyumbani mwake. \v 13 Yehoashi mfalme wa Israeli akamteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akaenda Yerusalemu na kuubomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi Lango la Pembeni, sehemu yenye urefu wa kama dhiraa mia nne\f + \fr 14:13 \fr*\ft Dhiraa 400 ni sawa na mita 180.\ft*\f*. \v 14 Akachukua dhahabu yote na fedha na vyombo vyote vilivyopatikana ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika hazina zote za jumba la mfalme. Akachukua pia mateka na akarudi Samaria. \p \v 15 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehoashi, aliyoyafanya na mafanikio yake, pamoja na vita vyake dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 16 Yehoashi akalala na baba zake, akazikwa Samaria na wafalme wa Israeli. Naye Yeroboamu mwanawe akawa mfalme baada yake. \p \v 17 Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli. \v 18 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Amazia, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \p \v 19 Wakapanga njama dhidi ya Amazia huko Yerusalemu, naye akakimbilia Lakishi, lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi, nao wakamuua huko. \v 20 Akarudishwa kwa farasi, akazikwa huko Yerusalemu pamoja na baba zake katika Mji wa Daudi. \p \v 21 Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Azaria\f + \fr 14:21 \fr*\ft au \ft*\fqa Uzia\fqa*\f* aliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita, na kumfanya mfalme mahali pa Amazia baba yake. \v 22 Ndiye aliijenga upya Elathi na kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala na baba zake. \s1 Yeroboamu wa pili mfalme wa Israeli \p \v 23 Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yehoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala huko Samaria, naye akatawala kwa miaka arobaini na moja. \v 24 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, na hakuacha dhambi hata moja ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alikuwa amesababisha Israeli kuzitenda. \v 25 Ndiye alirudishia mipaka ya Israeli kuanzia Lebo-Hamathi hadi Bahari ya Araba, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, lililosemwa kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, nabii kutoka Gath-Heferi. \p \v 26 Mwenyezi Mungu alikuwa ameona jinsi kila mmoja katika Israeli, awe mtumwa au aliye huru, alivyoteseka kwa uchungu; hapakuwa na yeyote wa kuwasaidia. \v 27 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa hajasema kuwa atafuta jina la Israeli chini ya mbingu, akawaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi. \p \v 28 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, yote aliyoyafanya na mafanikio yake ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na jinsi alivyorudisha Dameski na Hamathi kwa Israeli, ambayo ilikuwa mali ya Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 29 Yeroboamu akalala na baba zake, wafalme wa Israeli. Naye Zekaria mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 15 \s1 Azaria mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 26) \p \v 1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala. \v 2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na mbili. Mama yake aliitwa Yekolia, kutoka Yerusalemu. \v 3 Akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama Amazia baba yake alivyofanya. \v 4 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. \p \v 5 Mwenyezi Mungu akampiga mfalme kwa ukoma hadi siku aliyokufa, naye aliishi katika nyumba iliyotengwa peke yake. Yothamu mwana wa mfalme akawa msimamizi wa jumba la mfalme, na akawatawala watu wa nchi. \p \v 6 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Azaria na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 7 Azaria akalala na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi. Naye Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Zekaria mfalme wa Israeli \p \v 8 Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, naye akatawala miezi sita. \v 9 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kama baba zake walivyofanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda. \p \v 10 Shalumu mwana wa Yabeshi akapanga njama dhidi ya Zekaria. Akamshambulia mbele ya watu, akamuua, na akawa mfalme baada yake. \v 11 Matukio mengine ya utawala wa Zekaria yameandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. \v 12 Kwa hiyo neno la Mwenyezi Mungu lililonenwa kwa Yehu likatimia, kwamba, “Wazao wako wataketi kwenye kiti cha utawala cha Israeli hadi kizazi cha nne.” \s1 Shalumu mfalme wa Israeli \p \v 13 Shalumu mwana wa Yabeshi akawa mfalme katika mwaka wa thelathini na tisa wa Uzia mfalme wa Yuda, naye akatawala katika Samaria kwa mwezi mmoja. \v 14 Kisha Menahemu mwana wa Gadi akaenda kutoka Tirsa hadi Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamuua, na akawa mfalme baada yake. \p \v 15 Matukio mengine ya utawala wa Shalumu, na njama alizozipanga, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. \p \v 16 Wakati ule, akianzia Tirsa, Menahemu alishambulia Tifsa na kila mtu ndani yake, na wale waliokuwa maeneo jirani, kwa sababu walikataa kufungua malango yao. Akaiangamiza Tifsa yote, na kuwapasua tumbo wanawake wote wenye mimba. \s1 Menahemu mfalme wa Israeli \p \v 17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akawa mfalme wa Israeli, akatawala huko Samaria kwa miaka kumi. \v 18 Akatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Katika wakati wa utawala wake wote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati ambazo alisababisha Israeli kuzitenda. \p \v 19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaishambulia Israeli. Menahemu mfalme wa Israeli akampa talanta elfu moja\f + \fr 15:19 \fr*\ft Talanta 1,000 ni sawa na tani 34.\ft*\f* za fedha ili amsaidie na kumwezesha katika utawala wake. \v 20 Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini\f + \fr 15:20 \fr*\ft Shekeli 50 ni sawa na gramu 600.\ft*\f* za fedha ambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi. \p \v 21 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Menahemu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 22 Menahemu akalala na baba zake. Naye Pekahia mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Pekahia mfalme wa Israeli \p \v 23 Katika mwaka wa hamsini wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, akatawala miaka miwili. \v 24 Pekahia akafanya uovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda. \v 25 Mmoja wa maafisa wake wakuu, Peka mwana wa Remalia, akapanga njama dhidi yake. Akachukua watu hamsini wa Gileadi pamoja naye, akamuua Pekahia, pamoja na Argobu na Aria, katika ngome ya jumba la kifalme huko Samaria. Kwa hiyo Peka akamuua Pekahia, naye akawa mfalme baada yake. \p \v 26 Matukio mengine ya utawala wa Pekahia na yote aliyoyafanya yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. \s1 Peka mfalme wa Israeli \p \v 27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini. \v 28 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo alisababisha Israeli kuzitenda. \p \v 29 Wakati wa utawala wa Peka mfalme wa Israeli, Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alikuja na kuteka Iyoni, Abel-Beth-Maaka, Yanoa, Kedeshi na Hazori. Akateka miji ya Gileadi na Galilaya, pamoja na nchi yote ya Naftali, na kuwahamishia watu wote Ashuru. \v 30 Kisha Hoshea mwana wa Ela akapanga njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Hoshea akamshambulia Peka na kumuua, kisha akawa mfalme baada yake katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia. \p \v 31 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Peka na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \s1 Yothamu mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 27) \p \v 32 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala. \v 33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. \v 34 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya. \v 35 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 36 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yothamu na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 37 (Katika siku hizo, Mwenyezi Mungu akaanza kuwatuma Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia dhidi ya Yuda.) \v 38 Yothamu akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi, mji wa baba zake. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 16 \s1 Ahazi mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 28) \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala. \v 2 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \v 3 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na hata akamtoa kafara mwanawe katika moto, akifuata njia za machukizo za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli. \v 4 Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia, juu ya vilima, na chini ya kila mti uliotanda. \p \v 5 Kisha Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli wakaondoka kwenda kupigana dhidi ya Yerusalemu na kumzingira Ahazi kwa jeshi, lakini hawakuweza kumshinda. \v 6 Wakati ule, Resini mfalme wa Aramu akaurudisha mji wa Elathi kwa Aramu kwa kuwafukuza watu wa Yuda. Kisha Waedomu wakahamia Elathi, nao wanaishi huko hadi leo. \p \v 7 Ahazi akatuma wajumbe kumwambia Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru kwamba, “Mimi ni mtumishi na mtumwa wako. Njoo na uniokoe kutoka mkononi mwa mfalme wa Aramu na wa mfalme wa Israeli, ambao wananishambulia.” \v 8 Naye Ahazi akachukua fedha na dhahabu zilizopatikana ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika hazina ya jumba la mfalme, na kuzituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru. \v 9 Mfalme wa Ashuru akamwitikia kwa kushambulia Dameski na kuiteka. Akawahamishia wenyeji wake huko Kiri, na kumuua Resini. \p \v 10 Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaona madhabahu huko Dameski, naye akamtumia Uria kuhani mchoro wa hayo madhabahu, pamoja na maelezo ya mpango kamili wa ujenzi wake. \v 11 Kwa hiyo Uria kuhani akajenga madhabahu kulingana na mipango yote ambayo Mfalme Ahazi alikuwa ameituma kutoka Dameski, na akamaliza ujenzi kabla ya Mfalme Ahazi kurudi. \v 12 Mfalme aliporudi kutoka Dameski na kuona hayo madhabahu, akayasogelea na kutoa sadaka juu yake. \v 13 Akatoa sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka, akamimina sadaka ya kinywaji na kunyunyizia damu ya sadaka zake za amani juu ya hayo madhabahu. \v 14 Mfalme Ahazi akayaondoa madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, yaliyokuwa yamesimama kati ya ingilio la Hekalu na hayo madhabahu mapya, naye akayaweka upande wa kaskazini mwa hayo madhabahu mapya. \p \v 15 Ndipo Mfalme Ahazi akatoa amri zifuatazo kwa Uria kuhani: “Juu ya hayo madhabahu kubwa mapya, toa sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa na sadaka ya jioni ya nafaka, sadaka ya mfalme ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa ya watu wote wa nchi, pamoja na sadaka yao ya nafaka na sadaka yao ya kinywaji. Unyunyize juu ya hayo madhabahu damu yote ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu. Lakini mimi nitatumia hayo madhabahu ya zamani ya shaba kwa ajili ya kutafuta uongozi.” \v 16 Naye Uria kuhani akafanya kama Mfalme Ahazi alivyoagiza. \p \v 17 Mfalme Ahazi akaondoa mbao za pembeni na kuondoa masinia kwenye vile vishikilio vilivyohamishika. Akaondoa ile Bahari kutoka mafahali wa shaba walioishikilia, na kuiweka kwenye kitako cha jiwe. \v 18 Kwa heshima ya mfalme wa Ashuru, akaliondoa pia pazia la Sabato lililokuwa limewekwa ndani ya Hekalu, na akaondoa ile njia ya kifalme ya kuingia kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 19 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Ahazi na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 20 Ahazi akalala na baba zake, naye akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 17 \s1 Hoshea, mfalme wa mwisho wa Israeli \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Ahazi mfalme wa Yuda, Hoshea mwana wa Ela akawa mfalme wa Israeli katika Samaria, naye akatawala miaka tisa. \v 2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, lakini si kama wafalme wengine wa Israeli waliomtangulia. \p \v 3 Mfalme Shalmanesa wa Ashuru akaenda na kumshambulia Mfalme Hoshea, ambaye hapo awali alikuwa akimlipa ushuru kwa sababu alikuwa mtumishi wake. \v 4 Lakini mfalme wa Ashuru akagundua kuwa Hoshea alikuwa msaliti, kwa kuwa alikuwa ametuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri. Wala hakuendelea kulipa ushuru kwa mfalme wa Ashuru tena kama alivyokuwa anafanya kila mwaka. Kwa hiyo Shalmanesa akamkamata na kumfunga gerezani. \p \v 5 Mfalme wa Ashuru akaishambulia nchi yote, akapigana dhidi ya Samaria na kuuzingira kwa miaka mitatu. \s1 Israeli kutekwa kwa sababu ya dhambi \p \v 6 Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaiteka Samaria na kuwahamishia Waisraeli huko Ashuru. Akawakalisha huko Hala, na Gozani karibu na Mto Habori, na katika miji ya Wamedi. \p \v 7 Yote haya yalitukia kwa sababu Waisraeli walikuwa wametenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, aliyekuwa amewapandisha kutoka Misri akiwatoa chini ya utawala wa nguvu wa Farao mfalme wa Misri. Waliabudu miungu mingine, \v 8 na kufuata desturi za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ameyafukuza mbele yao, pamoja na desturi ambazo wafalme wa Israeli walizileta. \v 9 Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye ngome, walijijengea mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote. \v 10 Wakaweka mawe ya kuabudiwa na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda. \v 11 Wakafukiza uvumba kila mahali pa juu pa kuabudia, kama yalivyofanya yale mataifa ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ameyafukuza mbele yao. Wakafanya mambo maovu ambayo yalimghadhibisha Mwenyezi Mungu. \v 12 Wakatumikia sanamu, ingawa Mwenyezi Mungu alikuwa amesema, “Msifanye mambo haya.” \v 13 Mwenyezi Mungu akawaonya Israeli na Yuda kupitia kwa manabii na waonaji wake wote: “Acheni njia zenu mbaya. Shikeni amri na maagizo yangu, kufuatana na Torati yangu yote niliyowaagiza baba zenu kuitii, na ambayo niliileta kwenu kupitia kwa watumishi wangu, manabii.” \p \v 14 Lakini hawakusikiliza, walikuwa na shingo ngumu kama baba zao, ambao hawakumwamini Mwenyezi Mungu, Mungu wao. \v 15 Walizikataa amri zake, na agano alilolifanya na baba zao, na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu batili, nao wenyewe wakawa batili. Wakayaiga mataifa yaliyowazunguka, ingawa Mwenyezi Mungu alikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya.” \p \v 16 Wakayaacha maagizo yote ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na kujitengenezea sanamu mbili, walizozisubu katika sura ya ndama na nguzo ya Ashera. Wakasujudia mianga yote ya angani, na wakamtumikia Baali. \v 17 Wakawatoa kafara watoto wao wa kiume na wa kike katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni pa Mwenyezi Mungu, wakamghadhibisha. \p \v 18 Basi Mwenyezi Mungu akawakasirikia sana Israeli na kuwaondoa kwenye uwepo wake. Ni kabila la Yuda tu lililobaki. \v 19 Hata hivyo, Yuda nao hawakuzishika amri za Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Wakafuata desturi ambazo Israeli walikuwa wamezianzisha. \v 20 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu aliwakataa watu wote wa Israeli; akawatesa na kuwaachia katika mikono ya wateka nyara hadi alipowaondoa kwenye uwepo wake. \p \v 21 Alipokwisha kuwatenga Israeli mbali na nyumba ya Daudi, wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nebati kuwa mfalme wao. Yeroboamu akawashawishi Israeli waache kumfuata Mwenyezi Mungu na akawasababisha kutenda dhambi kuu. \v 22 Nao Israeli wakadumu katika dhambi zote za Yeroboamu mwana wa Nebati, nao hawakuziacha \v 23 hadi Mwenyezi Mungu alipowaondoa kwenye uwepo wake, kama vile alivyokuwa ameonya kupitia watumishi wake wote manabii. Hivyo watu wa Israeli wakaondolewa kutoka nchi yao kwenda uhamishoni Ashuru, nao wako huko hata leo. \s1 Samaria inakaliwa tena \p \v 24 Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria badala ya Waisraeli. Wakaimiliki Samaria na kuishi katika miji yake. \v 25 Wakati walianza kuishi humo, hawakumwabudu Mwenyezi Mungu, kwa hiyo akatuma simba miongoni mwao, wakawaua baadhi ya watu. \v 26 Habari ikapelekwa kwa mfalme wa Ashuru, kusema: “Watu uliowahamisha na kuwaweka katika miji ya Samaria hawajui kile Mungu wa nchi hiyo anachokitaka. Ametuma simba miongoni mwao, ambao wanawaua, kwa sababu watu hawajui anachokitaka.” \p \v 27 Ndipo mfalme wa Ashuru akaamuru hivi: “Mtwae mmoja wa makuhani uliowachukua mateka kutoka Samaria ili arudi kuishi humo na awafundishe watu kile ambacho Mungu wa nchi anataka.” \v 28 Basi mmoja wa makuhani aliyekuwa amepelekwa uhamishoni kutoka Samaria akaja kuishi Betheli, akawafundisha jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu. \p \v 29 Hata hivyo, kila kikundi cha taifa lililoletwa Samaria kilitengeneza miungu yao wenyewe katika miji kadhaa mahali walipoishi, nao wakaiweka katika nyumba za ibada za sanamu ambazo watu wa Samaria walikuwa wametengeneza katika mahali pa juu pa kuabudia. \v 30 Watu kutoka Babeli wakatengeneza Sukoth-Benothi kuwa mungu wao, watu kutoka Kutha wakatengeneza Nergali, na watu kutoka Hamathi wakatengeneza Ashima; \v 31 Waavi wakatengeneza Nibhazi na Tartaki, nao Wasefarvi wakachoma watoto wao kama kafara kwa Adrameleki na Anameleki, miungu ya Sefarvaimu. \v 32 Walimwabudu Mwenyezi Mungu, lakini pia waliteua aina zote za watu wao ili kuwawakilisha kama makuhani katika mahali pa ibada kwenye mahali pa juu pa kuabudia. \v 33 Walimwabudu Mwenyezi Mungu, lakini pia waliitumikia miungu yao kulingana na desturi za mataifa walikotoka. \p \v 34 Hadi leo wanashikilia desturi zao za zamani. Hawamwabudu Mwenyezi Mungu wala kuzishika hukumu na maagizo, sheria na amri ambazo Mwenyezi Mungu aliwapa uzao wa Yakobo, ambaye alimwita Israeli. \v 35 Mwenyezi Mungu alipofanya agano na Waisraeli, aliwaamuru: “Msiiabudu miungu mingine yoyote wala kuisujudia, wala kuitumikia wala kuitolea dhabihu. \v 36 Bali imewapasa kumwabudu Mwenyezi Mungu aliyewapandisha kutoka Misri kwa uwezo wake mkuu na kwa mkono wake ulionyooshwa. Kwake yeye mtasujudu, na kwake yeye mtatoa dhabihu. \v 37 Imewapasa daima kuwa waangalifu kutunza hukumu na maagizo, sheria na amri alizowaandikia. Msiabudu miungu mingine. \v 38 Msisahau agano nililofanya nanyi, wala msiabudu miungu mingine. \v 39 Bali, mtamwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwani yeye ndiye atakayewakomboa kutoka mikononi mwa adui zenu wote.” \p \v 40 Hata hivyo hawakusikiliza, lakini waliendelea na desturi zao za awali. \v 41 Hata wakati watu hawa walipokuwa wanamwabudu Mwenyezi Mungu, walikuwa bado wakitumikia sanamu zao. Hadi leo watoto wao na wajukuu wao wanaendelea kufanya kama baba zao walivyofanya. \c 18 \s1 Hezekia mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 29:1–31:21) \p \v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi mfalme wa Yuda alianza kutawala. \v 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. \v 3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama Daudi baba yake alivyofanya. \v 4 Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Musa aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo Waisraeli walikuwa wanaifukizia uvumba. (Ilikuwa ikiitwa Nehushtani\f + \fr 18:4 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Kipande cha shaba\fqa*\f*). \p \v 5 Hezekia aliweka tumaini lake kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Hapakuwa na mfalme mwingine wa kufanana naye miongoni mwa wafalme wa Yuda, kabla yake au baada yake. \v 6 Alishikamana na Mwenyezi Mungu kwa bidii wala hakuacha kumfuata; alishika amri ambazo Mwenyezi Mungu alikuwa amempa Musa. \v 7 Naye Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja naye, akafanikiwa katika kila alichokifanya. Aliasi dhidi ya mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia. \v 8 Kuanzia mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye ngome, aliwashinda Wafilisti, hadi kufikia Gaza na himaya yake yote. \p \v 9 Mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela kutawala Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru alienda kushambulia Samaria na kuuzingira. \v 10 Baada ya miaka mitatu Waashuru wakautwaa. Kwa hiyo Samaria ulitekwa katika mwaka wa sita wa utawala wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa utawala wa Hoshea mfalme wa Israeli. \v 11 Mfalme wa Ashuru akawahamishia Waisraeli huko Ashuru na akawaweka Hala, na Gozani karibu na Mto Habori, na katika miji ya Wamedi. \v 12 Hili lilitokea kwa sababu hawakumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wao, lakini walikuwa wamevunja agano lake, yale yote ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwaamuru. Hawakuzisikiliza amri wala kuzitimiza. \p \v 13 Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka. \v 14 Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa chochote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta mia tatu\f + \fr 18:14 \fr*\ft Talanta 300 ni sawa na tani 10.\ft*\f* za fedha, na talanta thelathini\f + \fr 18:14 \fr*\ft Talanta 30 ni sawa na tani moja.\ft*\f* za dhahabu. \v 15 Basi Hezekia akampa fedha yote iliyopatikana ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika hazina ya jumba la mfalme. \p \v 16 Wakati huu Hezekia mfalme wa Yuda akabandua dhahabu yote iliyokuwa imefunika milango na miimo ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, akampa mfalme wa Ashuru. \s1 Senakeribu anaitishia Yerusalemu \r (2 Nyakati 32:1-19; Isaya 36:1-22) \p \v 17 Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi, pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja Yerusalemu na kusimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi. \v 18 Wakaagiza mfalme aitwe. Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la mfalme, Shebna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakawaendea. \p \v 19 Yule jemadari wa jeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia: \pm “ ‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi unapoweka hili tumaini lako? \v 20 Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata ukaniasi mimi? \v 21 Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea. \v 22 Nawe ukiniambia, “Tunamtumainia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya katika Yerusalemu”? \pm \v 23 “ ‘Njooni sasa, fanyeni mapatano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapandisha waendesha farasi juu yao! \v 24 Utawezaje kumzuia hata afisa mmoja aliye mdogo kati ya maafisa wa bwana wangu, ijapo unategemea Misri kwa magari ya vita na wapanda farasi? \v 25 Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza mahali hapa pasipo neno kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye aliniambia niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ” \p \v 26 Ndipo Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania, watu walio juu ya ukuta wakiwa wanasikia.” \p \v 27 Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mkojo wao wenyewe?” \p \v 28 Kisha yule jemadari wa jeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, akasema: “Sikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru! \v 29 Hili ndilo asemalo mfalme: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa mkononi mwangu. \v 30 Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini Mwenyezi Mungu kwa kuwaambia, ‘Hakika Mwenyezi Mungu atatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’ \p \v 31 “Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwa mzabibu wake na mtini wake mwenyewe, na kunywa maji kutoka kisima chake mwenyewe, \v 32 hadi nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya mizeituni na asali. Chagueni uzima, sio mauti! \p “Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa anawapotosha asemapo, ‘Mwenyezi Mungu atatuokoa.’ \v 33 Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru? \v 34 Iko wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena na Iva? Je, imeokoa Samaria kutoka mkononi mwangu? \v 35 Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi ameweza kuokoa nchi yake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi Mwenyezi Mungu aiokoe Yerusalemu mkononi mwangu?” \p \v 36 Lakini wale watu wakakaa kimya, wala hawakujibu lolote, kwa kuwa mfalme alikuwa amewaamuru, “Msimjibu lolote.” \p \v 37 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia vile jemadari wa jeshi alivyosema. \c 19 \s1 Hezekia autafuta msaada wa Mwenyezi Mungu \r (Isaya 37:1-13) \p \v 1 Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa gunia, naye akaenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 2 Akawatuma Eliakimu msimamizi wa nyumba ya mfalme, Shebna mwandishi, na viongozi wa makuhani, wote wakiwa wamevaa magunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi. \v 3 Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa. \v 4 Yamkini Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.” \p \v 5 Maafisa wa Mfalme Hezekia walipofika kwa Isaya, \v 6 Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo. \v 7 Sikiliza! Nitatia roho fulani ndani yake, naye atakaposikia ujumbe fulani, atarudi nchi yake mwenyewe; nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ” \p \v 8 Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna. \p \v 9 Basi Senakeribu akapata taarifa kwamba Tirhaka Mkushi, mfalme wa Misri, alikuwa anaenda kupigana naye. Basi akatuma tena wajumbe kwa Hezekia na neno hili: \v 10 “Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda: Usikubali huyo Mungu unayemtumainia akudanganye wakati anaposema, ‘Yerusalemu haitatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’ \v 11 Hakika umesikia yale ambayo wafalme wa Ashuru wametenda kwa nchi zote, wakiwaangamiza kabisa. Je, wewe utaokolewa? \v 12 Je, miungu ya mataifa ambayo yaliangamizwa na baba zangu iliweza kuwaokoa, hiyo miungu ya Gozani, Harani, Resefu, na ya watu wa Edeni waliokuwa Telasari? \v 13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa mji wa Sefarvaimu, au wa Hena au wa Iva?” \s1 Maombi ya Hezekia \r (Isaya 37:14-20) \p \v 14 Hezekia akapokea barua kutoka kwa wale wajumbe, naye akaisoma. Kisha akapanda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, akaikunjua mbele za Mwenyezi Mungu. \v 15 Naye Hezekia akamwomba Mwenyezi Mungu akisema: “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, unayeketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi. \v 16 Tega sikio, Ee Mwenyezi Mungu, usikie; fungua macho yako, Ee Mwenyezi Mungu, uone; sikiliza maneno ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai. \p \v 17 “Ni kweli, Ee Mwenyezi Mungu, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao. \v 18 Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu, bali miti na mawe tu iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. \v 19 Sasa basi, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Mungu pekee.” \s1 Kuanguka kwa Senakeribu \r (Isaya 37:21-38) \p \v 20 Kisha Isaya mwana wa Amozi akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akasema: “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nimesikia maombi yako kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru. \v 21 Hili ndilo neno ambalo Mwenyezi Mungu amelisema dhidi yake: \q1 “ ‘Bikira Binti Sayuni anakudharau na kukudhihaki. \q2 Binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake unapokimbia. \q1 \v 22 Ni nani uliyemtukana na kumkufuru? \q2 Ni nani uliyepaza sauti yako dhidi yake, \q1 na kumwinulia macho yako kwa kiburi? \q2 Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli! \q1 \v 23 Kupitia kwa wajumbe wako \q2 umelundika matukano juu ya Bwana. \q1 Nawe umesema, \q2 “Kwa magari yangu mengi ya vita, \q1 nimepanda juu ya vilele vya milima, \q2 vilele vya juu sana katika Lebanoni. \q1 Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu, \q2 misunobari yake iliyo bora sana. \q1 Nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana, \q2 misitu yake iliyo mizuri sana. \q1 \v 24 Nimechimba visima katika nchi za kigeni \q2 na kunywa maji yake. \q1 Kwa nyayo za miguu yangu \q2 nimekausha vijito vyote vya Misri.” \b \q1 \v 25 “ ‘Je, hujasikia? \q2 Zamani sana niliamuru hili. \q1 Siku za kale nilipanga hili; \q2 sasa nimelifanya litokee, \q1 kwamba umegeuza miji yenye ngome \q2 kuwa malundo ya mawe. \q1 \v 26 Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, \q2 wanavunjika mioyo na kuaibishwa. \q1 Wao ni kama mimea katika shamba, \q2 kama machipukizi mororo ya kijani, \q1 kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, \q2 ambayo hukauka kabla ya kukua. \b \q1 \v 27 “ ‘Lakini ninajua mahali ukaapo, \q2 kutoka kwako na kuingia kwako, \q2 na jinsi unavyoghadhibika dhidi yangu. \q1 \v 28 Kwa sababu unaghadhibika dhidi yangu, \q2 na ufidhuli wako umefika masikioni mwangu, \q1 nitaweka ndoana yangu puani mwako \q2 na hatamu yangu kinywani mwako, \q2 nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.’ \p \v 29 “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia: \q1 “Mwaka huu utakula kile kinachoota chenyewe, \q2 na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake. \q1 Lakini katika mwaka wa tatu, panda na uvune, \q2 panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake. \q1 \v 30 Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda \q2 wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu. \q1 \v 31 Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki, \q2 na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika. \m Wivu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni utatimiza jambo hili. \b \p \v 32 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu mfalme wa Ashuru: \q1 “Hataingia katika mji huu \q2 wala hatapiga mshale hapa. \q1 Hatakuja mbele yake akiwa na ngao, \q2 wala kupanga majeshi kuuzingira. \q1 \v 33 Kwa njia ile aliyoijia, ndiyo atakayorudi; \q2 hataingia katika mji huu, \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 \v 34 Nitaulinda mji huu na kuuokoa, \q2 kwa ajili yangu mwenyewe, \q2 na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.” \p \v 35 Usiku ule, malaika wa Mwenyezi Mungu akaenda, akawaua wanajeshi elfu mia moja na themanini na tano katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali! \v 36 Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko. \p \v 37 Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 20 \s1 Ugonjwa wa Hezekia \r (2 Nyakati 32:24-26; Isaya 38:1-8, 21-22) \p \v 1 Katika siku hizo, Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.” \p \v 2 Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Mwenyezi Mungu: \v 3 “Ee Mwenyezi Mungu, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu. \p \v 4 Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la Mwenyezi Mungu likamjia, akaambiwa: \v 5 “Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako; nitakuponya. Siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 6 Nitakuongezea miaka kumi na tano katika maisha yako. Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi!’ ” \p \v 7 Kisha Isaya akasema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini.” Wakafanya hivyo na kuiweka kwenye jipu, naye akapona. \p \v 8 Hezekia alimuuliza Isaya, “Kutakuwa na ishara gani kwamba Mwenyezi Mungu ataniponya mimi, na kwamba nitapanda kwenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu siku ya tatu tangu leo?” \p \v 9 Isaya akajibu, “Hii ndiyo ishara ya Mwenyezi Mungu kwako kwamba Mwenyezi Mungu atafanya kile alichoahidi: Je, kivuli kiende hatua kumi mbele, au kivuli kirudi nyuma hatua kumi?” \p \v 10 Hezekia akasema, “Ni jambo rahisi kwa kivuli kutangulia mbele hatua kumi, kuliko kukifanya kirudi nyuma hatua kumi.” \p \v 11 Ndipo nabii Isaya akamwita Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu akakifanya kivuli kurudi nyuma hatua kumi ambazo kilikuwa kimeshuka kwenye ngazi ya Ahazi. \s1 Wajumbe kutoka Babeli \r (Isaya 39:1-8) \p \v 12 Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia. \v 13 Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonesha vitu vyote vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina yake. Hapakuwa na kitu katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonesha. \p \v 14 Ndipo nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumuuliza, “Watu hao walisema nini, na wametoka wapi?” \p Hezekia akamjibu, “Wametoka nchi ya mbali. Walikuja kutoka Babeli.” \p \v 15 Nabii akauliza, “Waliona nini katika jumba lako la kifalme?” \p Hezekia akajibu, “Waliona kila kitu katika jumba langu. Hakuna kitu katika hazina yangu ambacho sikuwaonesha.” \p \v 16 Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Mwenyezi Mungu: \v 17 Hakika wakati unakuja ambapo vitu vyote katika jumba lako, na vyote ambavyo baba zako waliweka akiba hadi siku hii, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna chochote kitakachosalia, asema Mwenyezi Mungu. \v 18 Nao baadhi ya wazao wako, mwili wako na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa mateka, nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.” \p \v 19 Hezekia akamjibu Isaya, “Neno la Mwenyezi Mungu ulilosema ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, “Si patakuwa na amani na usalama wakati wa uhai wangu?” \p \v 20 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Hezekia, mafanikio yake yote, na jinsi alivyotengeneza bwawa na mfereji ulioleta maji katika mji, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 21 Hezekia akalala na baba zake. Naye Manase mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 21 \s1 Manase mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 33:1-20) \p \v 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na tano. Mama yake aliitwa Hefsiba. \v 2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli. \v 3 Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia ambapo Hezekia baba yake alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu. \v 4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, ambamo Mwenyezi Mungu alikuwa amesema, “Katika Yerusalemu nitaliweka Jina langu.” \v 5 Katika nyua zote mbili za Hekalu la Mwenyezi Mungu, akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani. \v 6 Akamtoa kafara mwanawe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa Mwenyezi Mungu na kumghadhibisha. \p \v 7 Akachukua nguzo ya Ashera aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu, ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, mji niliouchagua kutoka makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele. \v 8 Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli itangetange kutoka nchi niliyowapa baba zao, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru, na kuishika Torati yote ambayo walipewa na Musa mtumishi wangu.” \v 9 Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliangamiza mbele ya Waisraeli. \p \v 10 Mwenyezi Mungu akasema kupitia watumishi wake manabii: \v 11 “Manase mfalme wa Yuda ametenda dhambi hizi za kuchukiza. Amefanya maovu mengi kuliko Waamori waliokuwa kabla yake, na ameiongoza Yuda katika dhambi kwa sanamu zake. \v 12 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda, kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha. \v 13 Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kamba ya kupimia iliyotumika dhidi ya Samaria, na timazi iliyotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu. Nitaifutilia mbali Yerusalemu kama mtu afutavyo sahani, nikiifuta na kuifunikiza. \v 14 Nitawakataa mabaki wa urithi wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao. Watapokonywa mali yao na kutekwa nyara na adui zao wote, \v 15 kwa sababu wametenda uovu machoni pangu na kunighadhibisha tangu siku baba zao walipotoka Misri hadi leo.” \p \v 16 Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, hivi kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, na hivyo wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. \p \v 17 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 18 Manase akalala na baba zake, akazikwa katika bustani ya jumba lake la kifalme, katika bustani ya Uza. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Amoni mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 33:21-25) \p \v 19 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. Mamaye aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, kutoka Yotba. \v 20 Akatenda maovu machoni mwa Mwenyezi Mungu, kama baba yake Manase alivyofanya. \v 21 Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia. \v 22 Akamwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za Mwenyezi Mungu. \p \v 23 Watumishi wa Amoni wakampangia njama, nao wakamuua ndani ya jumba lake la kifalme. \v 24 Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamepanga njama dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake. \p \v 25 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Amoni na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 26 Akazikwa kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza. Naye Yosia mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 22 \s1 Yosia mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 34; 35:20-27) \p \v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka nane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na moja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi. \v 2 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake. Hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto. \p \v 3 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Akasema: \v 4 “Panda uende kwa Hilkia, kuhani mkuu, umwambie ahesabu zile fedha ambazo zimeletwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, ambazo mabawabu wamekusanya kutoka kwa watu. \v 5 Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu: \v 6 wale maseremala, wajenzi na waashi. Waambie pia wanunue mbao na mawe yaliyochongwa ili kukarabati Hekalu. \v 7 Lakini hawahitajiki kutoa maelezo ya fedha walizokabidhiwa, kwa sababu wanafanya kazi kwa uaminifu.” \p \v 8 Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma. \v 9 Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.” \v 10 Ndipo Shafani mwandishi akampasha mfalme habari, akisema: “Hilkia kuhani amenipa kitabu hiki.” Naye Shafani akakisoma kile kitabu mbele ya mfalme. \p \v 11 Mfalme aliposikia maneno ya kile Kitabu cha Torati, akararua mavazi yake. \v 12 Akatoa maagizo haya kwa Hilkia kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya mtumishi wa mfalme: \v 13 “Nendeni mkamuulize Mwenyezi Mungu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Mwenyezi Mungu ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki. Hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu.” \p \v 14 Hilkia kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani na Asaya wakaenda kuongea na nabii mke Hulda, aliyekuwa mke wa Shalumu mwana wa Tikwa, mwana wa Harhasi mtunzaji wa chumba cha mavazi. Hulda aliishi Yerusalemu katika Mtaa wa Pili. \p \v 15 Akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Mwambieni yule mtu aliyewatuma ninyi kwangu, \v 16 ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Nitaleta maafa juu ya mahali hapa na watu wake, kulingana na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hicho mfalme wa Yuda alichosoma. \v 17 Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’ \v 18 Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza Mwenyezi Mungu, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kuhusu maneno uliyoyasikia: \v 19 Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake, kwamba wangelaaniwa na kuachwa ukiwa, basi kwa sababu uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Mwenyezi Mungu. \v 20 Kwa hiyo nitakukusanya kwa baba zako, nawe utazikwa kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote nitakayoleta juu ya mahali hapa.’ ” \p Basi wakapeleka jibu lake kwa mfalme. \c 23 \s1 Yosia analifanya upya agano \r (2 Nyakati 34:3-7, 29-33) \p \v 1 Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu. \v 2 Akapanda kwenda hekaluni mwa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, kilichokuwa kimepatikana katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 3 Mfalme akasimama karibu na nguzo, na kufanya upya agano mbele za Mwenyezi Mungu: kwamba atamfuata Mwenyezi Mungu na kuzishika amri zake, maagizo na sheria zake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, na hivyo kuyathibitisha maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kisha watu wote wakajifunga wenyewe kwa kiapo katika agano. \p \v 4 Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani mkuu, makuhani waliomfuata kwa cheo, na mabawabu kuondoa kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali na Ashera na jeshi lote la mianga ya angani! Akavichoma nje ya Yerusalemu katika mashamba ya Bonde la Kidroni, na kuyachukua hayo majivu hadi Betheli. \v 5 Akawafukuza makuhani wa kipagani waliokuwa wameteuliwa na wafalme wa Yuda kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia katika miji ya Yuda na ile iliyozunguka Yerusalemu, yaani wale waliofukiza uvumba kwa Baali, kwa jua na mwezi, kwa makundi ya nyota, na jeshi lote la angani. \v 6 Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu, akaiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wasio na cheo. \v 7 Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, nyumba ambazo wanawake walifumia pazia kwa ajili ya Ashera. \p \v 8 Yosia akawaleta makuhani wote wa Mwenyezi Mungu kutoka miji yote ya Yuda, na kunajisi mahali pa juu pa kuabudia, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la Lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji. \v 9 Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia hawakuhudumu katika madhabahu ya Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu pamoja na ndugu zao. \p \v 10 Kisha mfalme akapanajisi Tofethi, palipokuwa katika Bonde la Ben-Hinomu, ili mtu yeyote asiweze kupatumia kumtoa kafara mwanawe wa kiume au wa kike katika moto kwa Moleki. \v 11 Akaondoa kutoka ingilio la Hekalu la Mwenyezi Mungu wale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathan-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari ya vita yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa jua. \p \v 12 Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la Mwenyezi Mungu. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande, na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni. \v 13 Mfalme pia akanajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, zilizokuwa mashariki mwa Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alikuwa amejenga mahali pa kuabudia kwa ajili ya Ashtorethi mungu wa kike wa Wasidoni, aliyekuwa chukizo; na kwa ajili ya Kemoshi mungu wa Wamoabu, aliyekuwa chukizo; na kwa ajili ya Moleki mungu wa watu wa Amoni, aliyekuwa chukizo. \v 14 Yosia akapasua yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Ashera. Kisha akafunika hayo maeneo kwa mifupa ya wanadamu. \p \v 15 Hata madhabahu yaliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, alibomoa hata hayo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia na kupasaga hadi pakawa vumbi, na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia. \v 16 Kisha Yosia akatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu ya Betheli ili kupanajisi. Hili lilitendeka kulingana na neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya. \p \v 17 Mfalme akauliza, “Lile kaburi lenye mnara wa ukumbusho ninaloliona ni kwa ajili gani?” \p Watu wa mji wakasema, “Hii ni alama ya kaburi la mtu wa Mungu aliyekuja kutoka Yuda, naye akanena dhidi ya madhabahu ya Betheli mambo yale yale uliyoifanyia leo.” \p \v 18 Akasema, “Liacheni, msiliguse. Msimruhusu mtu yeyote kuiondoa mifupa yake.” Basi wakaiacha mifupa yake pamoja na ile ya yule nabii aliyekuwa amekuja kutoka Samaria. \p \v 19 Kama alivyokuwa amefanya huko Betheli, Yosia akabomoa nyumba za ibada katika mahali pa juu pa kuabudia, ambazo wafalme wa Israeli walikuwa wamejenga ndani ya miji ya Samaria, na ambazo zilikuwa zimemghadhibisha Mwenyezi Mungu. \v 20 Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia katika madhabahu zao wenyewe, na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu. \s1 Yosia aadhimisha Pasaka \p \v 21 Mfalme akatoa agizo hili kwa watu wote: “Adhimisheni Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu hiki cha Agano.” \v 22 Hapakuwahi kuwa na adhimisho lingine la Pasaka kama hilo tangu nyakati za waamuzi walioamua Israeli, wala katika nyakati zote za wafalme wa Israeli na wafalme wa Yuda. \v 23 Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia, Pasaka hii iliadhimishwa kwa Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. \p \v 24 Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa waaguzi, waabudu mizimu, miungu ya nyumbani, sanamu za kuabudiwa, na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana huko Yuda na Yerusalemu. Aliyafanya haya ili kutimiza matakwa ya sheria iliyoandikwa katika kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikipata ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 25 Hapakuwepo mfalme mwingine kabla na baada ya Yosia aliyempenda Mwenyezi Mungu kama yeye; kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, kulingana na Torati yote ya Musa. \p \v 26 Hata hivyo, Mwenyezi Mungu hakuacha ghadhabu yake iliyowaka dhidi ya Yuda kwa sababu ya yale yote ambayo Manase alikuwa amefanya kumghadhibisha. \v 27 Hivyo Mwenyezi Mungu akasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua, na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Jina langu litakaa humo.’ ” \p \v 28 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yosia na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \p \v 29 Yosia alipokuwa mfalme, Farao Neko mfalme wa Misri akapanda hadi Mto Frati kumsaidia mfalme wa Ashuru. Mfalme Yosia akatoka kwenda kupigana naye, lakini Neko akamkabili na kumuua huko Megido. \v 30 Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake katika gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu, wakamzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakampaka mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake. \s1 Yehoahazi mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 36:2-4) \p \v 31 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miezi mitatu. Mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna. \v 32 Akafanya maovu machoni mwa Mwenyezi Mungu, kama baba zake walivyofanya. \p \v 33 Farao Neko akamfunga kwa minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akatoza kodi ya talanta mia moja\f + \fr 23:33 \fr*\ft Talanta 100 ni sawa na tani 3.4.\ft*\f* za fedha, na talanta moja\f + \fr 23:33 \fr*\ft Talanta moja ni sawa na kilo 34.\ft*\f* ya dhahabu katika Yuda. \s1 Yehoyakimu mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 36:5-8) \p \v 34 Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, na kulibadilisha jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua Yehoahazi na kumpeleka Misri, naye akafia huko. \p \v 35 Yehoyakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoyakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadirio ya mapato yao. \p \v 36 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na moja. Mama yake aliitwa Zebida binti Pedaya kutoka Ruma. \v 37 Naye akafanya maovu machoni mwa Mwenyezi Mungu, kama baba zake walivyokuwa wamefanya. \c 24 \p \v 1 Wakati wa utawala wa Yehoyakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoyakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza. \v 2 Mwenyezi Mungu akatuma wavamiaji wa Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na watumishi wake manabii. \v 3 Hakika mambo haya yalitokea Yuda kulingana na agizo la Mwenyezi Mungu, ili kuwaondoa kutoka machoni pake kwa sababu ya dhambi za Manase na yote aliyoyafanya, \v 4 ikiwa ni pamoja na kumwaga damu isiyo na hatia. Kwa kuwa aliijaza Yerusalemu kwa damu isiyo na hatia, naye Mwenyezi Mungu hakuwa radhi kusamehe. \p \v 5 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 6 Yehoyakimu akalala na baba zake. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake. \p \v 7 Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati. \s1 Yehoyakini mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 36:9-10) \p \v 8 Yehoyakini alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu. \v 9 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya. \p \v 10 Wakati huo, maafisa wa Nebukadneza mfalme wa Babeli walikuja kushambulia Yerusalemu, nao wakauzingira kwa jeshi. \v 11 Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzingira. \v 12 Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza. \p Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa. \v 13 Kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 14 Akawachukua watu wa Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani maafisa wote na wapiganaji, watu wenye ustadi wa ufundi na wahunzi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana tu ndio walibaki katika nchi. \p \v 15 Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini hadi Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake, na viongozi wote wa nchi. \v 16 Mfalme wa Babeli pia akawahamishia Babeli wapiganaji elfu saba wenye nguvu na tayari kwa vita, na mafundi na wahunzi elfu moja. \v 17 Akamfanya Matania, ndugu wa baba yake Yehoyakini, kuwa mfalme mahali pake, na akalibadilisha jina lake kuwa Sedekia. \s1 Sedekia mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 36:11-12; Yeremia 52:1-3) \p \v 18 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na moja. Mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia, kutoka Libna. \v 19 Alifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, kama alivyofanya Yehoyakimu. \v 20 Haya yote yalitendeka Yerusalemu na Yuda kwa sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. \p Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli. \c 25 \s1 Kuanguka kwa Yerusalemu \r (2 Nyakati 36:13-21; Yeremia 52:3-30) \p \v 1 Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli, akiwa na jeshi lake lote, alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Akapiga kambi nje ya mji na kuuzingira pande zote. \v 2 Mji ulizingirwa na jeshi hadi mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Mfalme Sedekia. \v 3 Ilipofika siku ya tisa ya mwezi wa nne, njaa ikazidi kuwa kali sana ndani ya mji, hadi hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu. \v 4 Kisha ukuta wa mji ukavunjwa, na jeshi lote likakimbia. Wakaondoka mjini usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba. \v 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata katika nchi tambarare za Yeriko. Askari wake wote wakatengwa naye na kutawanyika, \v 6 naye akakamatwa. Akapelekwa kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, ambapo hukumu yake ilitangazwa. \v 7 Wakawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake. Kisha wakayang’oa macho yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. \p \v 8 Siku ya saba ya mwezi wa tano, katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme, afisa wa mfalme wa Babeli, alikuja Yerusalemu. \v 9 Alichoma moto Hekalu la Mwenyezi Mungu, jumba la kifalme, na nyumba zote za Yerusalemu. Aliteketeza kila jengo muhimu. \v 10 Jeshi lote la Wakaldayo, chini ya mkuu wa askari walinzi wa mfalme, walivunja kuta zilizoizunguka Yerusalemu. \v 11 Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi akawapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebaki katika mji, pamoja na mabaki ya watu wa kawaida, na wale waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli. \v 12 Lakini yule jemadari wa askari walinzi akawaacha baadhi ya wale watu maskini kabisa ili watunze mashamba ya mizabibu na mashamba mengine. \p \v 13 Wakaldayo walivunja vipande vipande zile nguzo za shaba, vile vishikilio vya shaba vilivyohamishika, na ile Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Hivyo wakaichukua hiyo shaba na kuipeleka Babeli. \v 14 Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia tambi, sahani na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika katika huduma ya Hekalu. \v 15 Mkuu wa askari walinzi wa mfalme akachukua vile vyetezo na yale mabakuli ya kunyunyizia, vitu vyote vile vilivyokuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi au fedha. \p \v 16 Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ilikuwa na uzito mwingi usioweza kupimika. \v 17 Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane\f + \fr 25:17 \fr*\ft Dhiraa 18 ni sawa na mita 8.2.\ft*\f*. Sehemu ya shaba juu ya nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tatu\f + \fr 25:17 \fr*\ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\ft*\f* na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na wavu wake ilifanana na hiyo ya kwanza. \p \v 18 Yule mkuu wa askari walinzi akawachukua kama wafungwa Seraya kuhani mkuu, kuhani Sefania aliyefuata kwa cheo, na mabawabu watatu. \v 19 Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua kiongozi wa wapiganaji, na washauri watano wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji. \v 20 Nebuzaradani jemadari akawachukua hao wote na kuwapeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla. \v 21 Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe. \p Hivyo Yuda wakaenda utumwani mbali na nchi yao. \p \v 22 Nebukadneza mfalme wa Babeli akamteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, awe msimamizi wa watu aliowaacha Yuda. \v 23 Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia kuwa mtawala, wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao. \v 24 Gedalia akaapa ili kuwatia moyo wao na watu wao. Akasema, “Msiwaogope maafisa wa Wakaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu.” \p \v 25 Hata hivyo, katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi, nao wakamuua Gedalia, na pia watu wa Yuda, pamoja na Wakaldayo waliokuwa naye huko Mispa. \v 26 Baada ya haya, watu wote kuanzia aliye mdogo sana hadi aliye mkubwa kabisa, pamoja na maafisa wa jeshi, wakakimbilia Misri kwa kuwaogopa Wakaldayo. \s1 Yehoyakini anaachiwa \r (Yeremia 52:31-34) \p \v 27 Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki\f + \fr 25:27 \fr*\ft au \ft*\fqa Ameli-Mariduki\fqa*\f* alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini kutoka gerezani siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili. \v 28 Alizungumza naye kwa upole na kumpa kiti cha heshima kuliko wafalme wengine aliokuwa nao huko Babeli. \v 29 Hivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya gerezani, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme. \v 30 Siku kwa siku mfalme alimpa Yehoyakini posho siku zote za maisha yake.