\id 2JN - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 2 Yohana \toc1 2 Yohana \toc2 2 Yohana \toc3 2Yn \mt1 2 Yohana \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Mzee. \po Kwa mama mteule na watoto wake, ninaowapenda katika kweli; wala si mimi tu, bali na wale wote wanaoijua kweli; \v 2 kwa sababu ya ile kweli inayokaa ndani yetu, na ambayo itaendelea kukaa nasi milele. \po \v 3 Neema, rehema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba\f + \fr 1:3 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* Mwenyezi na kwa Isa Al-Masihi, Mwanawe Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo. \s1 Kweli na upendo \p \v 4 Imenipa furaha kuu kuona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile Baba alivyotuagiza. \v 5 Sasa, mama mteule mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Tupendane kila mmoja na mwenzake. \v 6 Hili ndilo pendo: kwamba tuenende kwa kuzitii amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo. \p \v 7 Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Isa Al-Masihi amekuja katika mwili, wametawanyika ulimwenguni. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na anampinga Al-Masihi. \v 8 Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu. \v 9 Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Al-Masihi bali ameyaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia. \v 10 Msimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu. \v 11 Yeyote amkaribishaye mtu kama huyo anashiriki katika matendo yake maovu. \s1 Salamu za mwisho \p \v 12 Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu. \b \p \v 13 Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amen.