\id 2CO - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 2 Wakorintho \toc1 2 Wakorintho \toc2 2 Wakorintho \toc3 2Kor \mt1 2 Wakorintho \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Barua hii ni kutoka kwangu mimi Paulo, mtume wa Al-Masihi Isa kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu. \po Kwa kundi la waumini wa Mungu walioko Korintho, pamoja na watakatifu wote walio nchi ya Akaya yote. \po \v 2 Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba\f + \fr 1:2 \fr*\ft Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi. \s1 Mungu wa faraja yote \p \v 3 Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. \v 4 Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. \v 5 Kama vile mateso ya Al-Masihi yanavyozidi maishani mwetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kupitia kwa Al-Masihi. \v 6 Ikiwa tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata. \v 7 Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki faraja yetu. \p \v 8 Ndugu wapendwa, hatutaki mkose kujua kuhusu zile taabu tulizopata huko jimbo la Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi. \v 9 Kwa kweli, mioyoni mwetu tulihisi tumekabiliwa na hukumu ya kifo, ili tusijitegemee sisi wenyewe bali tumtegemee Mungu afufuaye wafu. \v 10 Yeye ametuokoa kwenye hatari kubwa ya kifo, na atatuokoa tena. Kwake yeye tumeweka tumaini letu kwamba ataendelea kutuokoa, \v 11 kama vile mnavyoungana kusaidiana nasi katika maombi. Hivyo wengi watatoa shukrani kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka za neema tulizopata kwa majibu ya maombi ya wengi. \s1 Paulo aahirisha ziara \p \v 12 Basi haya ndio majivuno yetu: Dhamiri yetu inatushuhudia kwamba tumeishi katika ulimwengu kwa utakatifu na uaminifu unaotoka kwa Mungu, na hasa katika uhusiano wetu na ninyi. Hatukufanya hivyo kwa hekima ya kidunia bali kwa neema ya Mungu. \v 13 Kwa maana hatuwaandikii mambo ambayo hamwezi kusoma au kuyaelewa. Natumaini kwamba, \v 14 kama vile mlivyotuelewa kwa sehemu, mtakuja kuelewa kwa ukamilifu ili mweze kujivuna kwa ajili yetu, kama na sisi tutakavyojivuna kwa ajili yenu katika siku ya Bwana Isa. \p \v 15 Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilitaka nije kwenu kwanza, ili mpate faida mara mbili. \v 16 Nilipanga kuwatembelea nikiwa safarini kwenda Makedonia, na kurudi tena kwenu nikitoka Makedonia, ili mnisafirishe katika safari yangu ya kwenda Yudea. \v 17 Nilipopanga jambo hili, je, nilikuwa kigeugeu? Au ninafanya mipango yangu kwa hali ya mwili, ili niseme, “Ndiyo, ndiyo” na “Siyo, siyo” wakati huo huo? \p \v 18 Hakika kama Mungu alivyo mwaminifu, maneno yetu kwenu hayajakuwa “Ndiyo” na “Siyo”. \v 19 Kwa kuwa Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silvano\f + \fr 1:19 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Sila\fqa*\f*, na Timotheo tulimhubiri kwenu, hakuwa “Ndiyo” na “Siyo”, bali kwake yeye siku zote ni “Ndiyo”. \v 20 Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Al-Masihi ni “Ndiyo”. Kwa sababu hii, ni kwake yeye tunasema “Amen” kwa utukufu wa Mungu. \v 21 Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Al-Masihi. Alitupaka mafuta \v 22 kwa kututia muhuri wake na kutupatia Roho wake Mtakatifu mioyoni mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia yote aliyotuahidi. \p \v 23 Namwita Mungu awe shahidi wangu kwamba sikurudi Korintho kwa sababu niliwahurumia ninyi. \v 24 Si kwamba tunatawala imani yenu, bali twatenda kazi pamoja nanyi ili mfurahi, kwa sababu ni kwa imani mwasimama imara. \c 2 \p \v 1 Hivyo nilikusudia moyoni mwangu nisifanye ziara nyingine yenye kuwaumiza ninyi. \v 2 Kwa kuwa nikiwahuzunisha ninyi, ni nani aliyebaki wa kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? \v 3 Niliwaandikia hivyo ili nikija nisihuzunishwe na wale watu ambao walipaswa kunifurahisha. Nilikuwa na uhakika na ninyi nyote, kwamba wote mngeshiriki furaha yangu. \v 4 Kwa maana niliwaandikia kutokana na dhiki kubwa na kutaabika sana moyoni mwangu, tena kwa machozi mengi; shabaha yangu haikuwa niwahuzunishe, bali niwaoneshe kina cha upendo wangu kwenu. \s1 Msamaha kwa mwenye dhambi \p \v 5 Lakini ikiwa mtu yeyote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama vile alivyowahuzunisha ninyi nyote. Nasema hivi ili nisiwe mkali kupita kiasi. \v 6 Adhabu hii aliyopewa na wengi inamtosha. \v 7 Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi. \v 8 Kwa hiyo, nawasihi mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwake. \v 9 Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo. \v 10 Mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Al-Masihi kwa ajili yenu, \v 11 ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatujakosa kuzijua hila zake. \s1 Wasiwasi wa Paulo huko Troa \p \v 12 Basi nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Al-Masihi na kukuta kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amenifungulia mlango, \v 13 bado nilikuwa sina amani kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao, nikaenda Makedonia. \p \v 14 Lakini Mungu apewe shukrani, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Al-Masihi. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye. \v 15 Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Al-Masihi miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea. \v 16 Kwa wale wanaopotea, sisi ni harufu ya mauti iletayo mauti; lakini kwa wale wanaookolewa, sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo? \v 17 Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na neno la Mungu ili tujifaidishe. Bali tunalinena neno lake kwa unyofu katika Al-Masihi tukiwa mbele za Mungu, kama watu waliotumwa na Mungu. \c 3 \s1 Wahudumu wa agano jipya \p \v 1 Je, tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine? \v 2 Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu. \v 3 Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua inayotoka kwa Al-Masihi, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu. \p \v 4 Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kupitia kwa Al-Masihi. \v 5 Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu. \v 6 Ndiye alitutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho wa Mungu; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima. \s1 Utukufu wa agano jipya \p \v 7 Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe, ilikuja kwa utukufu hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Musa kwa sababu ya ule utukufu wake, ingawa ulikuwa wa kufifia, \v 8 je, huduma ya Roho wa Mungu haitakuwa na utukufu zaidi? \v 9 Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi? \v 10 Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu, kikilinganishwa na huu utukufu unaozidi. \v 11 Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu! \p \v 12 Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana. \v 13 Sisi si kama Musa, ambaye ilimpasa kuweka utaji wa kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mng’ao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka. \v 14 Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana hadi leo utaji ule ule hufunika Torati inaposomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Al-Masihi peke yake unaondolewa. \v 15 Hata leo Torati ya Musa inaposomwa, utaji hufunika mioyo yao. \v 16 Lakini wakati wowote mtu anapomgeukia Bwana Mungu Mwenyezi, utaji unaondolewa. \v 17 Basi Bwana Isa ndiye Roho. Mahali alipo Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi, hapo pana uhuru. \v 18 Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji, tunadhihirisha utukufu wa Bwana Isa kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, unaotoka kwa Bwana Isa, aliye Roho. \c 4 \s1 Hazina ya mbinguni katika vyombo vya udongo \p \v 1 Kwa hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii kwa rehema za Mungu, hatukati tamaa. \v 2 Lakini tumekataa mambo ya siri na ya aibu; hatufuati njia za udanganyifu, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo. Kinyume cha hayo, tunadhihirisha kweli waziwazi na kujitambulisha wenyewe kwenye dhamiri ya kila mtu mbele za Mungu. \v 3 Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea. \v 4 Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Al-Masihi, aliye sura ya Mungu. \v 5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe, ila tunamhubiri Isa Al-Masihi kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Isa. \v 6 Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ing’ae gizani,” ameifanya nuru yake ing’ae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Al-Masihi. \p \v 7 Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, wala si kwetu. \v 8 Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; \v 9 twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi. \v 10 Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Isa ili uzima wa Isa uweze kudhihirishwa katika miili yetu. \v 11 Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Isa, ili uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti. \v 12 Hivyo basi, mauti inatenda kazi ndani yetu, bali uzima unatenda kazi ndani yenu. \p \v 13 Imeandikwa, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Kwa roho yule yule wa imani pia tuliamini na hivyo tunasema, \v 14 kwa sababu tunajua kwamba yeye aliyemfufua Bwana Isa kutoka kwa wafu atatufufua sisi pia pamoja na Isa na kutuleta sisi pamoja nanyi mbele zake. \v 15 Haya yote ni kwa faida yenu, ili neema ile inavyowafikia watu wengi zaidi na zaidi ipate kusababisha shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu. \p \v 16 Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. \v 17 Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi. \v 18 Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele. \c 5 \s1 Makao yetu ya mbinguni \p \v 1 Kwa maana twajua kama hema letu la dunia tunayoishi likiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. \v 2 Katika hema hili twalia kwa uchungu, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni, \v 3 kwa kuwa tukishavikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. \v 4 Kwa kuwa tukiwa bado katika hema hili twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. \v 5 Basi Mungu ndiye alitufanya kwa ajili ya jambo lilo hilo, naye ametupatia Roho wa Mungu kuwa amana, akituhakikishia ahadi ya kile kijacho. \p \v 6 Kwa hiyo siku zote tuna ujasiri, hata ingawa tunajua kwamba tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana Isa. \v 7 Kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. \v 8 Naam, tuna ujasiri, na tunaona ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana Isa. \v 9 Kwa hiyo, tukiwa katika mwili huu au tukiwa mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana Isa. \v 10 Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Al-Masihi, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya. \s1 Huduma ya upatanisho \p \v 11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Mwenyezi Mungu, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. \v 12 Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu, mweze kuwajibu hao wanaoona fahari kuhusu mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. \v 13 Kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu; kama tuna akili timamu, ni kwa ajili yenu. \v 14 Kwa kuwa upendo wa Al-Masihi unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. \v 15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao. \p \v 16 Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Al-Masihi kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo. \v 17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya. \v 18 Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kupitia kwa Isa Al-Masihi, na kutupatia sisi huduma ya upatanisho: \v 19 kwamba Mungu alikuwa ndani ya Al-Masihi akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. \v 20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Al-Masihi, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Al-Masihi: mpatanishwe na Mungu. \v 21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi\f + \fr 5:21 \fr*\ft au \ft*\fqa kuwa sadaka ya dhambi\fqa*\f* kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kupitia kwake Al-Masihi. \c 6 \p \v 1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. \v 2 Kwa maana asema: \q1 “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia, \q2 siku ya wokovu nilikusaidia.” \m Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo hii. \s1 Taabu za Paulo \p \v 3 Hatuweki kikwazo katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama. \v 4 Bali tunajidhihirisha kuwa watumishi wa Mungu kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida; \v 5 katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga; \v 6 katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho wa Mungu na upendo wa kweli; \v 7 katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu; kwa silaha za haki mkononi wa kuume na mkononi wa kushoto; \v 8 katika utukufu na katika kudharauliwa, katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukionekana kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli; \v 9 tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi; \v 10 tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote. \p \v 11 Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa. \v 12 Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu. \v 13 Sasa nasema kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa. \s1 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini \p \v 14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini. Kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? \v 15 Kuna mapatano gani kati ya Al-Masihi na Beliari\f + \fr 6:15 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Uovu\fqa*\ft , yaani \ft*\fqa Shetani\fqa*\f*? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? \v 16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: \q1 “Nitakaa pamoja nao \q2 na kutembea katikati yao, \q1 nami nitakuwa Mungu wao, \q2 nao watakuwa watu wangu.” \m \v 17 Kwa hiyo, \q1 “Tokeni miongoni mwao, \q2 mkatengwe nao, \q2 asema Mwenyezi Mungu. \q1 Msiguse kitu chochote kilicho najisi, \q2 nami nitawakaribisha.” \m \v 18 Na, \q1 “Mimi nitakuwa Baba kwenu, \q2 nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike, \q2 asema Mwenyezi Mungu, \q2 Mungu wa majeshi ya mbinguni.” \c 7 \p \v 1 Wapendwa, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitu kitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu. \s1 Furaha ya Paulo \p \v 2 Tupatieni nafasi mioyoni mwenu. Hatujamkosea mtu yeyote, wala hatujampotosha mtu yeyote, wala hatujamdhulumu mtu yeyote. \v 3 Sisemi haya ili kuwahukumu, kwa kuwa nilisema mwanzo kwamba ninyi mko mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja au kuishi pamoja. \v 4 Nina ujasiri mwingi kwa ajili yenu; naona fahari juu yenu. Nimejawa na faraja. Nina furaha kupita kiasi katika mateso yetu yote. \p \v 5 Kwa maana hata tulipoingia Makedonia, miili yetu haikuwa na amani. Tulisumbuliwa kila upande; kwa nje kulikuwa na mapigano, na mioyoni mwetu tulikuwa na hofu. \v 6 Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa Tito kufika kwetu. \v 7 Lakini si kule kuja kwa Tito tu, bali pia kwa faraja mliyompa. Alitueleza jinsi mlivyonionea shauku, huzuni yenu kubwa na juhudi yenu kwa ajili yangu, ili furaha yangu ipate kuwa kubwa kuliko wakati wowote. \p \v 8 Hata kama niliwahuzunisha kwa barua yangu, sijutii. Ingawa nilijuta kwa muda mfupi, kwa kuwa najua kwamba barua yangu iliwaumiza, lakini ni kwa kitambo tu. \v 9 Lakini sasa nina furaha, si kwa sababu mlihuzunika, bali kwa kuwa huzuni hiyo iliwafanya mtubu. Kwa maana mlihuzunishwa kama Mungu alivyokusudia watu wahuzunike, na hivyo sisi hatukuwadhuru kwa njia yoyote. \p \v 10 Kwa maana huzuni ya kiungu huleta toba iletayo wokovu, wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti. \v 11 Tazameni jinsi huzuni hii ya kiungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo. \v 12 Hivyo, ingawa niliwaandikia, haikuwa kwa sababu ya huyo aliyekosa au huyo aliyekosewa. Lakini nilitaka ninyi wenyewe mwone mbele za Mungu jinsi mlivyojitoa kwa ajili yetu. \v 13 Kwa ajili ya haya yote tumefarijika. \p Zaidi ya kule sisi kutiwa moyo, tulifurahi sana kumwona Tito alivyo na furaha, kwa sababu roho yake imeburudishwa na ninyi nyote. \v 14 Nilikuwa nimewasifu ninyi kwake, nanyi hamkuniaibisha. Lakini kama vile yale yote tuliyowaambia yalikuwa kweli, hivyo kule kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumethibitishwa kuwa kweli pia. \v 15 Upendo wake kwenu unaongezeka sana anapokumbuka jinsi mlivyokuwa watiifu, mkampokea kwa hofu na kutetemeka. \v 16 Nafurahi kwamba ninaweza kuwatumaini ninyi kabisa. \c 8 \s1 Kutoa kwa ukarimu \p \v 1 Basi sasa ndugu, nataka ninyi mjue kuhusu ile neema ambayo Mungu amewapa waumini wa Makedonia. \v 2 Ingawa walikuwa na majaribu makali, furaha yao kubwa na umaskini wao mkuu zilifurika kwa ukarimu mwingi. \v 3 Kwa maana nashuhudia kwamba wao walitoa kwa kadiri walivyoweza, hata na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao, \v 4 wakitusihi kwa bidii wapewe fursa ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watakatifu. \v 5 Wala hawakufanya tulivyotazamia, bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana Isa kwanza, na ndipo wakajitoa kwa ajili yetu kufuatana na mapenzi ya Mungu. \v 6 Kwa hiyo tulimsihi Tito, kwa kuwa ndiye alianzisha jambo hili, akamilishe tendo hili la neema kwa upande wenu. \v 7 Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote, iwe ni katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa. \p \v 8 Siwaamrishi, lakini nataka kujaribu unyofu wa upendo wenu kwa kuulinganisha na bidii ya wengine. \v 9 Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri. \p \v 10 Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu katika jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo. \v 11 Sasa ikamilisheni kazi hii, ili shauku yenu ya kuitenda iandamane na kuimaliza, mkijitolea kulingana na uwezo wenu. \v 12 Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kulingana na kile mtu alicho nacho, wala si kwa kile ambacho hana. \p \v 13 Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano. \v 14 Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo utasaidia kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu. \v 15 Ndipo patakuwa na usawa, kama ilivyoandikwa: “Aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.” \s1 Tito atumwa Korintho \p \v 16 Ninamshukuru Mungu ambaye amemtia Tito moyo wa kuwajali ninyi kama mimi ninavyowajali. \v 17 Si kwamba Tito amekubali tu ombi letu, bali anakuja kwenu akiwa na shauku kuliko wakati mwingine, tena kwa hiari yake mwenyewe. \v 18 Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makundi yote ya waumini kwa huduma yake ya kuhubiri Injili. \v 19 Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makundi ya waumini ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana Isa mwenyewe, na ili kuonesha hisani yetu kuwasaidia. \v 20 Tunataka kuepuka lawama yoyote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu. \v 21 Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki, si machoni mwa Bwana Isa peke yake, bali pia machoni mwa wanadamu. \p \v 22 Pamoja nao, tunamtuma ndugu yetu ambaye mara kwa mara ametuthibitishia kwa njia nyingi kwamba ana shauku, naam, zaidi sana sasa kwa sababu analo tumaini kuu kwenu. \v 23 Kwa habari ya Tito, yeye ni mwenzangu na mtendakazi pamoja nami miongoni mwenu. Kwa habari za ndugu zetu, wao ni wawakilishi wa makundi ya waumini, na utukufu kwa Al-Masihi. \v 24 Kwa hiyo waonesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu, na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, ili makundi ya waumini yapate kuuona upendo wenu. \c 9 \s1 Wasaidieni wafuasi wa Al-Masihi wenzenu \p \v 1 Hakuna haja ya kuwaandikia kuhusu huduma hii kwa watakatifu. \v 2 Kwa kuwa ninajua mlivyo na shauku ya kusaidia, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili ya jambo hilo kwa Wamakedonia, nikiwaambia kwamba ninyi watu wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana. Na shauku yenu imewachochea wengi wao katika kutoa. \v 3 Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusiwe maneno matupu, bali mpate kuwa tayari kama nilivyosema mngekuwa tayari. \v 4 Kwa maana nikija na Mmakedonia yeyote na kuwakuta hamko tayari, sisi, na hata ninyi pia, tungeona haya kwa kuwa na ujasiri hivi katika ninyi. \v 5 Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu. \s1 Kupanda kwa ukarimu \p \v 6 Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye haba pia atavuna haba, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. \v 7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu. \v 8 Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. \v 9 Kama ilivyoandikwa: \q1 “Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; \q2 haki yake hudumu milele.” \m \v 10 Yeye ampaye mpanzi mbegu ya kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. \v 11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani. \p \v 12 Huduma hii mnayofanya si tu ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi kwake Mungu. \v 13 Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Al-Masihi, na kwa ukarimu wenu wa kuwashirikisha wao na watu wengine wote. \v 14 Nayo mioyo yao itawaonea shauku wanapowaombea, kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu. \v 15 Mungu apewe shukrani kwa karama yake isiyoelezeka! \c 10 \s1 Paulo atetea huduma yake \p \v 1 Basi, mimi Paulo ninawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Al-Masihi, mimi niliye “mwoga” ninapokuwa pamoja nanyi ana kwa ana, lakini mwenye ujasiri nikiwa mbali nanyi! \v 2 Nawaomba nitakapokuja kwenu nisipaswe kuwa na ujasiri dhidi ya watu fulani kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata mtazamo wa ulimwengu huu. \v 3 Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. \v 4 Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. \v 5 Tunaangusha mawazo na kila kitu kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na kuteka nyara kila fikira ipate kumtii Al-Masihi. \v 6 Tena tunakuwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, hapo kutii kwenu kutakapokamilika. \p \v 7 Mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu tu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Al-Masihi, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Al-Masihi, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo. \v 8 Basi hata nikijisifu zaidi kidogo kuhusu mamlaka tuliyo nayo, ambayo Bwana Isa alitupatia ili kuwajenga wala si kuwabomoa, mimi sitaionea haya. \v 9 Sitaki nionekane kama ninayejaribu kuwatisha kwa nyaraka zangu. \v 10 Kwa maana wanasema, “Nyaraka zake ni nzito na zenye nguvu, lakini ana kwa ana ni mdhaifu, na kuzungumza kwake ni kwa kudharauliwa.” \v 11 Watu kama hao wajue ya kuwa yale tusemayo kwa barua tukiwa hatupo pamoja nanyi ndivyo tulivyo, na ndivyo tutakavyofanya tutakapokuwa pamoja nanyi. \p \v 12 Hatuthubutu kujiweka kwenye kundi moja au kujilinganisha na hao wanaojitukuza wenyewe kuwa wao ni wa maana sana. Wanapojipima na kujilinganisha wenyewe kwa wenyewe, wanaonesha ya kuwa hawana busara. \v 13 Lakini sisi hatujajivuna kupita kiasi, bali majivuno yetu yatakuwa katika mipaka ya huduma ile Mungu aliyotuwekea, mipaka ambayo inawafikia hata ninyi. \v 14 Kwa maana hatukuwa tunavuka mipaka katika kujisifu kwetu, kama ambavyo ingekuwa tusingekuja kwenu. Kwa maana sisi ndio tuliokuwa wa kwanza kuja kwenu na Injili ya Al-Masihi. \v 15 Wala hatuvuki mipaka kwa kujisifu kwetu kwa ajili ya kazi iliyofanywa na watu wengine. Tumaini letu ni kwamba imani yenu inavyozidi kukua, ndivyo eneo letu la utendaji miongoni mwenu litapanuka zaidi, \v 16 ili tuweze kuhubiri Injili sehemu zilizo mbali na maeneo yenu. Kwa maana hatutaki kujisifu kwa ajili ya kazi ambayo imekwisha kufanyika tayari katika eneo la mtu mwingine. \v 17 Lakini, “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Mwenyezi Mungu.” \v 18 Kwa maana si yeye ajisifuye mwenyewe akubaliwaye, bali yeye ambaye Mwenyezi Mungu humsifu. \c 11 \s1 Paulo na mitume wa uongo \p \v 1 Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo. \v 2 Ninawaonea wivu, wivu wa kiungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Al-Masihi kama mabikira safi. \v 3 Lakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Al-Masihi. \v 4 Kwa sababu mtu akija na kuwahubiria Isa mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi. \p \v 5 Lakini sidhani ya kuwa mimi ni dhalili sana kuliko hao “mitume wakuu”. \v 6 Inawezekana mimi si mnenaji hodari, lakini ni hodari katika elimu. Jambo hili tumelifanya liwe dhahiri kwenu kwa njia zote. \p \v 7 Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo? \v 8 Niliyanyang’anya makundi mengine ya waumini kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi. \v 9 Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nilipopungukiwa na chochote, sikuwa mzigo kwa mtu yeyote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walitimiza mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yoyote, nami nitaendelea kujizuia. \v 10 Kwa hakika kama vile kweli ya Al-Masihi ilivyo ndani yangu, hakuna mtu yeyote katika Akaya nzima atakayenizuia kujivunia jambo hili. \v 11 Kwa nini? Je, ni kwa sababu siwapendi? Mungu anajua ya kuwa nawapenda! \v 12 Nami nitaendelea kufanya lile ninalofanya sasa ili nisiwape nafasi wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia. \p \v 13 Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Al-Masihi. \v 14 Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. \v 15 Kwa hiyo basi si ajabu kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili. \s1 Paulo ajivunia mateso yake \p \v 16 Nasema tena: mtu yeyote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. \v 17 Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi vile Bwana Isa angesema, bali kama mjinga. \v 18 Kwa kuwa wengi wanajisifu kama vile ulimwengu ufanyavyo, mimi nami nitajisifu. \v 19 Ninyi mwachukuliana na wajinga kwa sababu mna hekima sana! \v 20 Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida, au akiwanyang’anya, au akijitukuza mwenyewe, au akiwadanganya. \v 21 Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo! \p Lakini jambo lolote ambalo mtu mwingine angethubutu kujisifia, ninene kama mjinga, nami nathubutu kujisifu kuhusu hilo. \v 22 Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Je, wao ni Waisraeli? Mimi pia ni Mwisraeli. Je, wao ni wazao wa Ibrahimu? Mimi pia ni mzao wa Ibrahimu. \v 23 Je, wao ni watumishi wa Al-Masihi? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii zaidi yao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimepigwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi. \v 24 Mara tano nimepigwa na Wayahudi mijeledi arobaini kasoro moja. \v 25 Mara tatu nilipigwa mijeledi, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nilivunjikiwa na meli, nilikaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa; \v 26 nimekuwa katika safari za mara kwa mara. Nimekabiliwa na hatari za kwenye mito, hatari za wanyang’anyi, hatari kutoka kwa Wayahudi wenzangu, hatari kutoka kwa watu wa Mataifa; hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini; na hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. \v 27 Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi; nimejua kukaa njaa na kuona kiu; nimefunga kula chakula mara nyingi; nimehisi baridi na kuwa uchi. \v 28 Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa kila siku na mzigo wa wajibu wangu kwa makundi yote ya waumini. \v 29 Je, ni nani aliye mdhaifu, nami nisijisikie mdhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike? \p \v 30 Kama ni lazima nijisifu, basi nitajisifia yale mambo yanayoonesha udhaifu wangu. \v 31 Mungu na Baba\f + \fr 11:31 \fr*\ft Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.\ft*\f* wa Bwana wetu Isa, yeye ambaye anahimidiwa milele, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. \v 32 Huko Dameski, mtawala aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliulinda mji wa Dameski ili kunikamata. \v 33 Lakini niliteremshwa kwa kapu kubwa kupitia dirisha ukutani, nikaokolewa kutoka mkononi mwake. \c 12 \s1 Maono ya Paulo na mwiba aliokuwa nao \p \v 1 Yanipasa nijisifu. Ingawa haifaidi kitu, nitanena kuhusu maono na mafunuo kutoka kwa Bwana Isa. \v 2 Namjua mtu mmoja katika Al-Masihi ambaye miaka kumi na nne iliyopita alichukuliwa juu hadi mbingu ya tatu. Kama ni katika mwili au nje ya mwili, sijui, Mungu ajua. \v 3 Nami najua kwamba mtu huyu, iwe ni katika mwili au nje ya mwili mimi sijui, lakini Mungu ajua, \v 4 alinyakuliwa hadi Paradiso\f + \fr 12:4 \fr*\ft Paradiso maana yake \ft*\fqa bustani nzuri\fqa*\ft ; hapa maana yake \ft*\fqa mbinguni.\fqa*\f*. Huko alisikia mambo yasiyoelezeka, mambo ambayo binadamu hana ruhusa ya kuyasimulia. \v 5 Nitajisifu kwa ajili ya mtu kama huyo, lakini sitajisifu mwenyewe, ila nitajisifia udhaifu wangu. \v 6 Hata kama ningependa kujisifu, sitakuwa mjinga, kwa maana nitakuwa nasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu yeyote asije akaniona mimi kuwa bora kuliko ninavyoonekana katika yale ninayotenda na kusema, \v 7 au kwa sababu ya mafunuo haya makuu. Ili kunizuia nisijivune, nilipewa mwiba katika mwili wangu, mjumbe wa Shetani, ili anitese. \v 8 Kwa habari ya jambo hili, nilimsihi Mwenyezi Mungu mara tatu aniondolee mwiba huu. \v 9 Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Al-Masihi ukae juu yangu. \v 10 Hii ndiyo sababu nafurahia katika udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso na katika shida kwa ajili ya Al-Masihi. Kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu. \s1 Wasiwasi wa Paulo kwa Wakorintho \p \v 11 Nimejifanya mjinga, lakini mmenilazimisha niwe hivyo. Kwa kuwa ilinipasa kusifiwa na ninyi, kwa sababu mimi si dhalili kuliko wale “mitume walio bora”, ingawa mimi si kitu. \v 12 Mambo yanayomtambulisha mtume wa kweli, yaani ishara, miujiza na maajabu, yalifanywa miongoni mwenu kwa saburi nyingi. \v 13 Je, ninyi ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makundi mengine ya waumini, ila tu kwamba mimi sikuwa mzigo kwenu? Nisameheni kwa kosa hili! \p \v 14 Sasa niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Nami sitawalemea, kwa sababu sihitaji chochote chenu, ila ninawahitaji ninyi. Kwa kuwa watoto hawaweki akiba kwa ajili ya wazazi wao, bali wazazi huweka akiba kwa ajili ya watoto wao. \v 15 Hivyo nitafurahi kutumia kila kitu nilicho nacho kwa ajili yenu, hata mwili wangu pia. Je, ninavyozidi kuwapenda, ndivyo upendo wenu kwangu unavyopungua? \v 16 Iwe iwavyo, kwa vyovyote vile, mimi sikuwalemea. Lakini wengine wanadhani mimi ni mjanja, nami niliwapata kwa hila! \v 17 Je, nilijipatia faida kwa kumtumia mtu yeyote niliyemtuma kwenu? \v 18 Nilimshawishi Tito aje kwenu, nami nilimtuma pamoja na ndugu yetu. Je, Tito aliwatumia ninyi ili kujipatia faida? Je, hatukuenenda kwa roho moja, na kwa hatua zile zile? \p \v 19 Je, mmekuwa mkifikiri kwamba sisi tunajaribu kujitetea mbele yenu? Sisi tumekuwa tukinena mbele za Mungu kama wale walio katika Al-Masihi. Na chochote tufanyacho, ndugu wapendwa, ni kwa ajili ya kuwatia nguvu. \v 20 Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza kuwakuta nisivyotaka, nanyi mkanikuta msivyotaka. Nina hofu kwamba panaweza kuwa na ugomvi, wivu, ghadhabu, fitina, masingizio, masengenyo, majivuno na machafuko. \v 21 Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi mbeleni, na wala hawajatubu kwa uchafu wao, uasherati, na ufisadi walioushiriki. \c 13 \s1 Maonyo ya mwisho \p \v 1 Hii itakuwa mara ya tatu mimi kuja kwenu. “Shtaka lolote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” \v 2 Niliwaonya nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili. Sasa narudia wakati sipo, kwamba nikija tena sitawahurumia wale waliokuwa wametenda dhambi hapo awali au wengine wote, \v 3 kwa kuwa mnadai uthibitisho kwamba Al-Masihi anazungumza kwa kunitumia mimi. Yeye si dhaifu katika kushughulika nanyi, bali ana nguvu kati yenu. \v 4 Kwa kuwa alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Vivyo hivyo, sisi tu dhaifu kupitia kwake, lakini katika kuwashughulikia ninyi tutaishi pamoja naye kwa nguvu za Mungu. \p \v 5 Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Isa Al-Masihi yu ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho! \v 6 Natumaini mtaona kuwa sisi hatukushindwa. \v 7 Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa. \v 8 Kwa maana hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, bali kuithibitisha kweli tu. \v 9 Tunafurahi wakati wowote tunapokuwa dhaifu, lakini ninyi mkawa na nguvu. Nayo maombi yetu ni kwamba mpate kuwa wakamilifu. \v 10 Hii ndiyo sababu nawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana Isa aliyonipa ya kuwajenga ninyi wala si ya kuwabomoa. \b \s1 Salamu za mwisho \p \v 11 Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, farijianeni, kuweni na nia moja, na mkae kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. \b \p \v 12 Salimianeni kwa busu takatifu. \p \v 13 Watakatifu wote wanawasalimu. \b \p \v 14 Neema ya Bwana Isa Al-Masihi, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho wa Mungu ukae nanyi nyote.