\id 2CH - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 2 Mambo Ya Nyakati \toc1 2 Mambo Ya Nyakati \toc2 2 Nyakati \toc3 2Nya \mt1 2 Mambo Ya Nyakati \c 1 \s1 Sulemani aomba hekima \r (1 Wafalme 3:1-15) \p \v 1 Sulemani mwana wa Daudi alijiimarisha katika ufalme wake, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, naye akamfanya mkuu sana. \p \v 2 Ndipo Sulemani akasema na Waisraeli wote, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, waamuzi na viongozi wote katika Israeli, pamoja na wakuu wa jamaa. \v 3 Naye Sulemani na kusanyiko lote wakakwea hadi mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni. Hema la Kukutania la Mungu, ambalo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alikuwa amelitengeneza huko jangwani, lilikuwa Gibeoni. \v 4 Basi Daudi alikuwa amelipandisha Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu hadi mahali alipokuwa amepatengeneza kwa ajili yake, kwa sababu alikuwa amesimamisha hema kwa ajili ya hilo Sanduku huko Yerusalemu. \v 5 Lakini yale madhabahu ya shaba ambayo Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, alikuwa ametengeneza yalikuwa huko Gibeoni mbele ya Maskani ya Mwenyezi Mungu, hivyo Sulemani na kusanyiko lote walimtafuta Mungu huko. \v 6 Sulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Mwenyezi Mungu katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu elfu moja za sadaka za kuteketezwa juu yake. \p \v 7 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani na kumwambia, “Omba lolote utakalo nikupe.” \p \v 8 Sulemani akamjibu Mungu, “Umemwonesha baba yangu Daudi fadhili nyingi, nawe umeniweka niwe mfalme mahali pake. \v 9 Sasa, Bwana Mwenyezi Mungu, ahadi yako kwa baba yangu Daudi na ithibitike, kwa kuwa umenifanya mimi mfalme juu ya watu ambao ni wengi kama mavumbi ya nchi. \v 10 Nakuomba unipe hekima na maarifa, ili niweze kuongoza watu hawa, kwa kuwa ni nani awezaye kutawala hawa watu wako walio wengi hivi?” \p \v 11 Mungu akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa jambo hili ndilo shauku ya moyo wako na hukuomba mali, utajiri au heshima, wala kifo kwa ajili ya adui zako, nawe kwa kuwa hukuomba maisha marefu, bali umeomba hekima na maarifa ili kuongoza watu wangu ambao nimekufanya uwe mfalme juu yao, \v 12 kwa hiyo utapewa hekima na maarifa. Tena nitakupa pia mali, utajiri na heshima, ambavyo hakuna mfalme yeyote kabla yako amewahi kuwa navyo, na hakuna yeyote baada yako atakayekuwa navyo.” \s1 Fahari ya Sulemani \r (1 Wafalme 10:26-29) \p \v 13 Ndipo Sulemani akaenda Yerusalemu kutoka mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni, kutoka mbele ya Hema la Kukutania. Naye akatawala Israeli. \p \v 14 Sulemani akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari elfu moja mia nne, na farasi elfu kumi na mbili, ambayo aliyaweka katika miji ya magari, na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. \v 15 Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu chini ya vilima. \v 16 Farasi wa Sulemani waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue\f + \fr 1:16 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Kilikia\fqa*\f*. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue. \v 17 Waliagiza magari ya vita kutoka Misri kwa bei ya shekeli mia sita\f + \fr 1:17 \fr*\ft Shekeli 600 ni sawa na kilo 7.\ft*\f* za fedha, na farasi kwa shekeli mia moja na hamsini\f + \fr 1:17 \fr*\ft Shekeli 150 ni sawa na kilo 1.7.\ft*\f*. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu. \c 2 \s1 Maandalizi ya ujenzi wa Hekalu \r (1 Wafalme 5:1-18) \p \v 1 Sulemani akatoa amri kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe. \v 2 Sulemani akaandika watu elfu sabini kuwa wachukuzi wa mizigo, na watu elfu themanini kuwa wachonga mawe vilimani, na watu elfu tatu na mia sita wawe wasimamizi wao. \p \v 3 Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro: \pm “Unitumie magogo ya mwerezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi. \v 4 Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, na kuliweka wakfu kwake kwa ajili ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate ya Wonesho kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamriwa za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli. \pm \v 5 “Hekalu nitakalolijenga litakuwa kubwa, kwa sababu Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote. \v 6 Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kumtosha? Mimi ni nani basi hata nimjengee Hekalu, isipokuwa liwe tu mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake? \pm \v 7 “Hivyo basi nitumie mtu mwenye ustadi wa kufanya kazi ya kutengeneza dhahabu na fedha, shaba na chuma, nyuzi za rangi ya zambarau, nyekundu na buluu, mwenye uzoefu wa kutia nakshi, ili afanye kazi Yuda na Yerusalemu pamoja na mafundi wangu wenye ustadi, ambao baba yangu Daudi aliwaweka. \pm \v 8 “Pia nitumie magogo ya mierezi, misunobari na misandali kutoka Lebanoni kwa maana najua kwamba watu wako wanao ujuzi wa kupasua mbao huko. Watu wangu watafanya kazi pamoja na watu wako \v 9 ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa. \v 10 Nitawapa watumishi wako, yaani maseremala wakatao mbao, kori elfu ishirini\f + \fr 2:10 \fr*\ft Kori 20,000 za ngano ni sawa na lita 4,400.\ft*\f* za unga wa ngano, kori elfu ishirini za shayiri, bathi elfu ishirini\f + \fr 2:10 \fr*\ft Bathi 20,000 za mvinyo au mafuta ni sawa na lita 440,000.\ft*\f* za mvinyo, na bathi elfu ishirini za mafuta ya zeituni.” \p \v 11 Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Sulemani kwa barua: \pm “Kwa sababu Mwenyezi Mungu anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.” \p \v 12 Naye Hiramu akaongeza kusema: \pm “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na busara, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe. \pm \v 13 “Mimi nitamtuma kwako Huram-Abi, mtu mwenye ustadi mwingi, \v 14 ambaye mama yake alitoka Dani na baba yake alitoka Tiro. Yeye ni stadi wa kutengeneza vitu, kufanya kazi zote za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mbao pamoja na kufuma. Ni stadi katika kutia rangi ya zambarau, buluu, nyekundu na nguo za kitani safi. Yeye ana ujuzi katika aina zote za kutia nakshi na anaweza kufuatiliza mchoro wowote wa kazi anayopewa. Atafanya kazi na mafundi wako na wale wa bwana wangu, Daudi baba yako. \pm \v 15 “Sasa basi bwana wangu na awapelekee watumishi wake ngano, shayiri, mafuta ya zeituni na mvinyo kama alivyoahidi, \v 16 nasi tutakata magogo yote yale unayohitaji kutoka Lebanoni nasi tutayafunga pamoja na kuyaweka yaelee baharini hadi Yafa. Kisha utaweza kuyapeleka hadi Yerusalemu.” \p \v 17 Ndipo Sulemani akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu elfu mia moja hamsini na tatu na mia sita. \v 18 Akawaweka watu elfu sabini miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na elfu themanini kuwa wachonga mawe vilimani, na elfu tatu na mia sita wawe wasimamizi ili wawahimize watu kufanya kazi. \c 3 \s1 Sulemani ajenga Hekalu \r (1 Wafalme 6:1-38; 7:15-22) \p \v 1 Ndipo Sulemani akaanza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Mwenyezi Mungu alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna\f + \fr 3:1 \fr*\ft au \ft*\fqa Ornani \fqa*\ft kwa Kiebrania\ft*\f* Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi. \v 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake. \p \v 3 Msingi aliouweka Sulemani kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa na urefu wa dhiraa sitini\f + \fr 3:3 \fr*\ft Dhiraa 60 ni sawa na mita 27.\ft*\f*, na upana wa dhiraa ishirini\f + \fr 3:3 \fr*\ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\ft*\f* kwa kipimo cha kale. \v 4 Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo, na kimo chake dhiraa thelathini\f + \fr 3:4 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\ft*\f*. \p Akaufunika ndani kwa dhahabu safi. \v 5 Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za msunobari, na kufunikwa kwa dhahabu safi, na kuupamba kwa michoro ya mitende na minyororo. \v 6 Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. \v 7 Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta. \p \v 8 Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 600\f + \fr 3:8 \fr*\ft Talanta 600 ni sawa na tani 21.\ft*\f* za dhahabu safi. \v 9 Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini\f + \fr 3:9 \fr*\ft Shekeli 50 ni sawa na gramu 600.\ft*\f*. Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu. \p \v 10 Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu. \v 11 Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano\f + \fr 3:11 \fr*\ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\ft*\f*, nalo liligusa ukuta wa Hekalu; bawa lake lingine lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi mwingine. \v 12 Vivyo hivyo bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na liligusa ukuta mwingine wa pili wa Hekalu, na bawa lake lingine lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano nalo liligusa bawa la kerubi wa kwanza. \v 13 Mabawa ya makerubi hawa yalitanda dhiraa ishirini. Walisimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ukumbi mkubwa. \p \v 14 Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake. \p \v 15 Mbele ya Hekalu Sulemani akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na urefu wa dhiraa thelathini na tano kwenda juu, na kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye kimo cha dhiraa tano. \v 16 Akatengeneza minyororo iliyosokotwa, na kuiweka juu ya zile nguzo. Pia akatengeneza makomamanga mia moja, na kuyaunganisha kwenye minyororo. \v 17 Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini\f + \fr 3:17 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Atathibitisha\fqa*\f*, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi\f + \fr 3:17 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Imo nguvu\fqa*\f*. \c 4 \s1 Vifaa vya Hekalu \r (1 Wafalme 7:23-51) \p \v 1 Mfalme Sulemani akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini\f + \fr 4:1 \fr*\ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\ft*\f*, upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi\f + \fr 4:1 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\ft*\f*. \v 2 Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini\f + \fr 4:2 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\ft*\f* ingeweza kuizunguka. \v 3 Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja\f + \fr 4:3 \fr*\ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\ft*\f*. Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari. \p \v 4 Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini, na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana. \v 5 Unene wake ulikuwa nyanda moja\f + \fr 4:5 \fr*\ft nyanda moja ni sawa na sentimita 7.5\ft*\f*, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Ingejazwa na bathi elfu tatu\f + \fr 4:5 \fr*\ft Bathi 3,000 ni sawa na lita 60,000.\ft*\f*. \p \v 6 Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ya makuhani kunawia. \p \v 7 Akatengeneza vinara kumi vya taa vya dhahabu kama ilivyoainishwa na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini. \p \v 8 Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli mia moja ya dhahabu ya kunyunyizia. \p \v 9 Akatengeneza ukumbi wa makuhani, na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba. \v 10 Akaiweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini-mashariki mwa nyumba. \p \v 11 Huramu pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. \p Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Sulemani alikuwa amemwagiza: \b \li1 \v 12 zile nguzo mbili; \li1 yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo, \li1 zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo; \li1 \v 13 yale makomamanga mia nne kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo); \li1 \v 14 vishikio pamoja na masinia yake; \li1 \v 15 hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake; \li1 \v 16 pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana. \b \p Vitu vyote ambavyo Huram-Abi alimtengenezea Mfalme Sulemani kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. \v 17 Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.\f + \fr 4:17 \fr*\ft au \ft*\fqa Sarethani.\fqa*\f* \v 18 Vitu hivi vyote Mfalme Sulemani alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzani wa shaba haungekadirika. \p \v 19 Sulemani pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu: \b \li1 madhabahu ya dhahabu; \li1 meza za kuweka mikate ya Wonesho; \li1 \v 20 vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya mahali patakatifu kama ilivyoelekezwa; \li1 \v 21 maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa); \li1 \v 22 mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu. \b \c 5 \p \v 1 Hivyo Sulemani alipomaliza kazi ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu. \s1 Sanduku la Agano laletwa Hekaluni \r (1 Wafalme 8:1-9) \p \v 2 Kisha Sulemani akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila, na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. \v 3 Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba. \p \v 4 Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano, \v 5 nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo, \v 6 naye Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli waliokuwa wamemzunguka wakasimama mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu za kondoo na ng’ombe nyingi kiasi kwamba idadi yao haikuweza kuandikwa au kuhesabika. \p \v 7 Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu hadi mahali patakatifu ndani ya Hekalu, pale Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. \v 8 Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea. \v 9 Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. \v 10 Ndani ya Sanduku hapakuwa na kitu kingine chochote isipokuwa vile vibao viwili ambavyo Musa aliviweka ndani yake huko Horebu, mahali Mwenyezi Mungu alipofanya agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri. \p \v 11 Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. \v 12 Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani mia moja na ishirini wakipiga tarumbeta. \v 13 Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Mwenyezi Mungu. Nao wakapaza sauti zao, pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Mwenyezi Mungu, wakisema: \q1 “Yeye ni mwema; \q2 fadhili zake zadumu milele.” \p Ndipo Hekalu la Mwenyezi Mungu likajazwa na wingu, \v 14 nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Mwenyezi Mungu ulijaza Hekalu la Mungu. \c 6 \s1 Kuweka Hekalu wakfu \r (1 Wafalme 8:12-21) \p \v 1 Ndipo Sulemani akasema, “Mwenyezi Mungu alisema kwamba ataishi katika giza nene. \v 2 Nimejenga Hekalu zuri kwa ajili yako, mahali pako pa kukaa milele.” \p \v 3 Kusanyiko lote la Israeli walipokuwa wamesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. \v 4 Kisha akasema: \pm “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mikono yake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, \v 5 ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, wala sikumchagua mtu yeyote kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli. \v 6 Lakini sasa nimeuchagua Yerusalemu ili Jina langu lipate kuwamo humo, na nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’ \pm \v 7 “Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 8 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako. \v 9 Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea Hekalu, bali mwanao, ambaye ni mwili wako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’ \pm \v 10 “Mwenyezi Mungu ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 11 Nimeliweka humo Sanduku la Agano, ambalo ndani yake kuna lile Agano la Mwenyezi Mungu alilofanya na watu wa Israeli.” \s1 Maombi ya Sulemani ya kuweka wakfu \r (1 Wafalme 8:22-53) \p \v 12 Kisha Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu machoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akanyoosha mikono yake. \v 13 Basi Sulemani alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kuelekea mbinguni. \v 14 Akasema: \pm “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote. \v 15 Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umetimiza, kama ilivyo leo. \pm \v 16 “Sasa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, kama wanao wakiwa waangalifu katika yote wanayoyafanya na kuenenda mbele zangu kwa kuzingatia sheria zangu kama ulivyofanya.’ \v 17 Sasa, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, acha neno lako lile ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie. \pm \v 18 “Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga! \v 19 Hata hivyo sikiliza dua la mtumishi wako na maombi yake ya kuhurumiwa, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambalo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. \v 20 Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. \v 21 Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia ukiwa mbinguni, makao yako, na unaposikia, samehe. \pm \v 22 “Mtu anapomkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili, \v 23 basi, sikia ukiwa mbinguni, ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimwadhibu yule mwenye hatia kwa kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie mwenye haki kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kuwa haki kwake. \pm \v 24 “Watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili, \v 25 basi usikie ukiwa mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao. \pm \v 26 “Mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka dhambi zao kwa sababu umewaadhibu, \v 27 basi usikie ukiwa mbinguni, usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi. \pm \v 28 “Njaa au tauni vikija katika nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia, \v 29 kila dua au ombi litakalotolewa na yeyote kati ya watu wako Israeli, akitambua taabu zake na uchungu wake, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili, \v 30 basi usikie ukiwa mbinguni, makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), \v 31 ili wakuogope na kuenenda katika utiifu kwako wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. \pm \v 32 “Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyooshwa, atakapokuja kuomba kuelekea Hekalu hili, \v 33 basi na usikie ukiwa mbinguni, makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli, nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako. \pm \v 34 “Watu wako watakapoenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa Mwenyezi Mungu kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, \v 35 basi usikie dua na maombi yao ukiwa mbinguni, ukawape haki yao. \pm \v 36 “Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu asiyetenda dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi iliyo mbali au karibu \v 37 na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya utumwa na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa na tumetenda uovu’; \v 38 wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, \v 39 basi usikie dua na maombi yao ukiwa mbinguni, makao yako, ukawape haki yao. Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako. \pm \v 40 “Sasa, Mungu wangu, macho yako na yafumbuke na masikio yako yasikie maombi yanayoombwa katika mahali hapa. \qm1 \v 41 “Sasa inuka, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \qm2 na uje mahali pako pa kupumzikia, \qm2 wewe na Sanduku la nguvu zako. \qm1 Makuhani wako, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, \qm2 na wavikwe wokovu, \qm1 watakatifu wako na wafurahi \qm2 katika wema wako. \qm1 \v 42 Ee Bwana Mwenyezi Mungu, usimkatae \qm2 mpakwa mafuta wako. \qm1 Kumbuka upendo mkuu uliomwahidia \qm2 Daudi mtumishi wako.” \c 7 \s1 Hekalu lawekwa wakfu \r (1 Wafalme 8:62-66) \p \v 1 Baada ya Sulemani kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukalijaza Hekalu. \v 2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu kwa sababu utukufu wa Mwenyezi Mungu ulilijaza. \v 3 Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Mwenyezi Mungu ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu, nyuso zao zikigusa chini, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu, wakisema, \q1 “Yeye ni mwema; \q2 fadhili zake zadumu milele.” \m \v 4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Mwenyezi Mungu. \v 5 Naye Mfalme Sulemani akatoa dhabihu ya ng’ombe elfu ishirini na mbili pamoja na kondoo na mbuzi elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu. \v 6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Mwenyezi Mungu ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Mwenyezi Mungu, navyo vilitumika aliposhukuru, akisema, “Fadhili zake zadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama. \p \v 7 Sulemani akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na za mafuta. \p \v 8 Hivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Waisraeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. \v 9 Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa sababu walikuwa wameadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba, na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba. \v 10 Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Sulemani akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Mwenyezi Mungu aliomtendea Daudi na Sulemani na kwa ajili ya watu wake Israeli. \s1 Mwenyezi Mungu amtokea Sulemani \r (1 Wafalme 9:1-9) \p \v 11 Sulemani alipomaliza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu na jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika jumba lake mwenyewe la kifalme, \v 12 Mwenyezi Mungu akamtokea Sulemani usiku na kumwambia: \pm “Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu. \pm \v 13 “Nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, \v 14 ikiwa watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekeza na kuomba na kuutafuta uso wangu, na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na nitaiponya nchi yao. \v 15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yanayoombwa mahali hapa. \v 16 Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili Jina langu lipate kuwa humo milele. Macho yangu na moyo wangu vitakuwepo daima. \pm \v 17 “Kwako wewe, ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda, na kufanya yote ninayokuamuru, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu, \v 18 nitakiimarisha kiti chako cha ufalme kama nilivyoagana na Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala Israeli.’ \pm \v 19 “Lakini mkigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, \v 20 ndipo nitakapoing’oa Israeli kutoka nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote. \v 21 Ingawa Hekalu hili linavutia sana sasa, wote watakaolipita watashangaa na kusema, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’ \v 22 Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, aliyewatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ” \c 8 \s1 Shughuli nyingine za Sulemani \r (1 Wafalme 9:10-28) \p \v 1 Miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alilijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu na jumba lake mwenyewe la kifalme, \v 2 Sulemani akajenga tena vijiji vile ambavyo Hiramu alikuwa amempa, naye akawapa Waisraeli waishi humo. \v 3 Kisha Sulemani akaenda Hamath-Soba na kuuteka. \v 4 Pia akajenga mji wa Tadmori katika jangwa, na miji yote ya kuhifadhia vitu katika Hamathi. \v 5 Akajenga tena Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo. \v 6 Sulemani pia akajenga Baalathi na miji yake yote ya kuhifadhia vitu, na miji kwa ajili ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake, chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni na katika nchi yote aliyotawala. \p \v 7 Watu wote waliosalia kutoka kwa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (haya mataifa hayakuwa Waisraeli), \v 8 yaani wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawakuwa wamewaangamiza: hawa Sulemani akawalazimisha kuwa watumwa katika shokoa, kama ilivyo hadi leo. \v 9 Lakini Sulemani hakuwafanya Waisraeli watumwa kwa ajili ya kazi yake; hao ndio walikuwa wapiganaji wake, majemadari wake, maafisa wake, majemadari wa magari yake ya vita, na wapanda farasi wake. \v 10 Pia walikuwa maafisa wakuu wa Mfalme Sulemani, maafisa wakaguzi mia mbili na hamsini waliosimamia watu. \p \v 11 Sulemani akampandisha mke wake binti Farao kutoka Mji wa Daudi na kumleta jumba la kifalme alilokuwa amemjengea, kwa kuwa alisema, “Mke wangu hataishi katika jumba la kifalme la Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu mahali ambapo Sanduku la Mwenyezi Mungu limefika ni patakatifu.” \p \v 12 Mfalme Sulemani akamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu ambayo alikuwa ameijenga mbele ya ukumbi, \v 13 kulingana na mahitaji ya kila siku kwa ajili ya sadaka zilizoamriwa na Musa kwa ajili ya Sabato, Mwezi Mwandamo na sikukuu nyingine tatu za mwaka: Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma na Sikukuu ya Vibanda. \v 14 Kwa kushika maagizo ya Daudi baba yake, aliweka migawanyo ya makuhani kwa ajili ya kazi zao, nao Walawi kuongoza kusifu na kusaidia makuhani kufuatana na mahitaji ya kila siku. Pia akaweka mabawabu katika migawanyo kwa ajili ya malango mbalimbali, kwa sababu hivi ndivyo Daudi mtu wa Mungu alivyokuwa ameagiza. \v 15 Nao hawakuziacha amri za mfalme alizoamuru makuhani au Walawi katika jambo lolote, ikiwa ni pamoja na zile za hazina. \p \v 16 Kazi yote ya Mfalme Sulemani ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu ulipowekwa hadi kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu la Mwenyezi Mungu likamalizika kujengwa. \p \v 17 Ndipo Sulemani akaenda Esion-Geberi na Elathi katika pwani ya Edomu. \v 18 Naye Hiramu alimpelekea meli zilizoongozwa na maafisa wake mwenyewe, watu waliokuwa na ujuzi wa baharini. Hawa watu pamoja na wale wa Sulemani wakasafiri kwa bahari hadi Ofiri, wakaleta kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Sulemani. \c 9 \s1 Malkia wa Sheba amtembelea Sulemani \r (1 Wafalme 10:1-13) \p \v 1 Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, wenye ngamia waliobeba vikolezo, dhahabu nyingi, na vito vya thamani. Alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake. \v 2 Sulemani alimjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake hata asiweze kumwelezea. \v 3 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, \v 4 chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, alipatwa na mshangao mkubwa. \p \v 5 Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. \v 6 Lakini sikuamini mambo yaliyosemwa hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana kuliko ile taarifa niliyoisikia. \v 7 Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wanaosimama mbele yako daima na kusikia hekima yako! \v 8 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe, na akakuweka kwenye kiti chake cha ufalme utawale kwa niaba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwathibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.” \p \v 9 Naye akampa mfalme talanta mia moja na ishirini\f + \fr 9:9 \fr*\ft Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5.\ft*\f* za dhahabu, kiasi kikubwa cha vikolezo na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa vikolezo vizuri kama vile malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Sulemani. \p \v 10 (Watumishi wa Hiramu na wa Sulemani wakaleta dhahabu kutoka Ofiri, tena wakaleta shehena kubwa ya miti ya msandali na vito vya thamani. \v 11 Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa Yuda tangu siku ile.) \p \v 12 Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake. \s1 Fahari ya Sulemani \r (1 Wafalme 10:14-25) \p \v 13 Uzito wa dhahabu ambayo Sulemani alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta mia sita sitini na sita (666)\f + \fr 9:13 \fr*\ft Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25.\ft*\f*, \v 14 mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha. \p \v 15 Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli mia sita\f + \fr 9:15 \fr*\ft Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5.\ft*\f*. \v 16 Akatengeneza pia ngao ndogo mia tatu za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu\f + \fr 9:16 \fr*\ft Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7.\ft*\f* za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. \p \v 17 Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. \v 18 Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Kila upande wa kiti ulikuwa na mahali pa kuegemeza mkono, na simba aliyesimama kando kila upande. \v 19 Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote. \v 20 Vikombe vyote vya Mfalme Sulemani vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Sulemani. \v 21 Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara\f + \fr 9:21 \fr*\ft au: \ft*\fqa za Tarshishi\fqa*\ft (taz. \+xt 1 Wafalme 10:22; 22:48; 2 Nyakati 20:36; Isaya 2:16; 60:9\+xt*).\ft*\f* baharini zilizoendeshwa na watu wa Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo. \p \v 22 Mfalme Sulemani alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. \v 23 Wafalme wote wa dunia wakatafuta kukutana na Sulemani ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. \v 24 Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezo, farasi na nyumbu. \p \v 25 Sulemani alikuwa na mabanda elfu nne kwa ajili ya farasi na magari ya vita, na farasi elfu kumi na mbili ambao aliwaweka katika miji ya magari ya vita, na wengine akawa nao huko Yerusalemu. \v 26 Sulemani akatawala juu ya wafalme wote kuanzia Mto\f + \fr 9:26 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati.\fqa*\f* hadi kwenye nchi ya Wafilisti na kuendelea hadi mpaka wa Misri. \v 27 Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu chini ya vilima. \v 28 Farasi wa Sulemani waliletwa kutoka Misri na kutoka nchi nyingine zote. \s1 Kifo cha Sulemani \r (1 Wafalme 11:41-43) \p \v 29 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Sulemani, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji kuhusu Yeroboamu mwana wa Nebati? \v 30 Sulemani alitawala Israeli yote miaka arobaini akiwa Yerusalemu. \v 31 Kisha Sulemani akalala na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi, baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 10 \s1 Waisraeli wamwasi Rehoboamu \r (1 Wafalme 12:1-20) \p \v 1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wameenda huko kumfanya mfalme. \v 2 Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Sulemani), akarudi kutoka Misri. \v 3 Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu; yeye na Waisraeli wote wakamwendea Rehoboamu na kumwambia, \v 4 “Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini sasa tupunguzie kazi za kikatili na nira nzito aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.” \p \v 5 Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao. \p \v 6 Kisha Mfalme Rehoboamu akataka ushauri kwa wazee ambao walimtumikia Sulemani baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri niwajibu nini watu hawa?” \p \v 7 Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.” \p \v 8 Lakini Rehoboamu akakataa ushauri aliopewa na wazee, na akataka ushauri kwa vijana wa rika lake waliokuwa wakimtumikia. \v 9 Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu’?” \p \v 10 Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Watu hawa walikuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi,’ Wewe waambie, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. \v 11 Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwapiga mijeledi; mimi nitawapiga kwa nge.’ ” \p \v 12 Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.” \v 13 Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Alikataa ushauri aliopewa na wazee, \v 14 akafuata ushauri wa vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwapiga mijeledi; mimi nitawapiga kwa nge.” \v 15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwa Mungu ili kutimiza neno ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa amenena na Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia kwa Ahiya Mshiloni. \p \v 16 Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: \q1 “Je, tuna fungu gani kwa Daudi? \q2 Tuna urithi gani kwa mwana wa Yese? \q1 Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli, \q2 angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” \m Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao. \v 17 Lakini kwa habari ya Waisraeli walioishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado. \p \v 18 Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu\f + \fr 10:18 \fr*\ft au \ft*\fqa Adoramu\fqa*\ft ; Kiebrania ni Hadoramu.\ft*\f* aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu akafanikiwa kuingia kwenye gari lake la vita, akatorokea Yerusalemu. \v 19 Hivyo, Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo. \c 11 \s1 Utabiri wa Shemaya \r (1 Wafalme 12:21-24) \p \v 1 Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na ya Benyamini, vijana wenye uwezo elfu mia moja na themanini, ili kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli, na kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu. \p \v 2 Lakini neno hili la Mwenyezi Mungu likamjia Shemaya mtu wa Mungu: \v 3 “Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani mfalme wa Yuda, na Waisraeli wote walio Yuda na Benyamini, \v 4 ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Mwenyezi Mungu na kurudi, wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu. \s1 Rehoboamu ajengea Yuda ngome \p \v 5 Rehoboamu akaishi Yerusalemu akajenga miji yenye ngome katika Yuda: \v 6 Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa, \v 7 Beth-Suri, Soko, Adulamu, \v 8 Gathi, Maresha, Zifu, \v 9 Adoraimu, Lakishi, Azeka, \v 10 Sora, Aiyaloni na Hebroni. Hii ilikuwa miji yenye ngome katika Yuda na Benyamini. \v 11 Akaimarisha ulinzi wake na kuweka majemadari ndani yake, pamoja na maghala ya vyakula, ya mafuta ya zeituni, na ya divai. \v 12 Akaweka ngao na mikuki katika miji na kuifanya iwe imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake. \p \v 13 Makuhani na Walawi kutoka sehemu zote za Israeli wakawa upande wake. \v 14 Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali yao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa Mwenyezi Mungu. \v 15 Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza. \v 16 Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu, Mungu wa baba zao. \v 17 Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumuunga mkono Rehoboamu mwana wa Sulemani miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Sulemani katika wakati huu. \s1 Jamaa ya Rehoboamu \p \v 18 Rehoboamu alimwoa Mahalati aliyekuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi; mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese. \v 19 Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu. \v 20 Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, aliyemzalia Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi. \v 21 Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini. \p \v 22 Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka, kuwa mkuu wa wana wa mfalme miongoni mwa ndugu zake ili amfanye mfalme. \v 23 Akatenda kwa busara, akiwasambaza baadhi ya wanawe katika wilaya zote za Yuda na Benyamini, pamoja na miji yote yenye ngome. Akawapa mahitaji tele na kuwaoza wake wengi. \c 12 \s1 Shishaki ashambulia Yerusalemu \r (1 Wafalme 14:25-28) \p \v 1 Baada ya ufalme wa Rehoboamu kuimarika naye akawa na nguvu, yeye na Waisraeli wote waliiacha Torati ya Mwenyezi Mungu. \v 2 Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu. \v 3 Akiwa na magari ya vita elfu moja mia mbili, wapanda farasi elfu sitini, na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi waliokuja pamoja naye kutoka Misri. \v 4 Akateka miji ya Yuda yenye ngome, akaendelea hadi Yerusalemu. \p \v 5 Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, ‘Ninyi mmeniacha, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha mkononi mwa Shishaki.’ ” \p \v 6 Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Mwenyezi Mungu ni mwenye haki.” \p \v 7 Mwenyezi Mungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili la Mwenyezi Mungu likamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza, bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kupitia kwa Shishaki. \v 8 Hata hivyo, watamtumikia Shishaki ili wapate kujifunza tofauti kati ya kunitumikia mimi na kuwatumikia wafalme wa nchi nyingine.” \p \v 9 Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza. \v 10 Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme. \v 11 Kila wakati mfalme alipoenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu walinzi walienda pamoja naye wakiwa wamebeba hizo ngao na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi. \p \v 12 Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya Mwenyezi Mungu ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda. \p \v 13 Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambao Mwenyezi Mungu alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, na alikuwa Mwamoni. \v 14 Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta Mwenyezi Mungu. \p \v 15 Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwa na vita vya mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu. \v 16 Rehoboamu akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Abiya mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 13 \s1 Abiya mfalme wa Yuda \r (1 Wafalme 15:1-8) \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu, Abiya akawa mfalme wa Yuda, \v 2 naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka, binti\f + \fr 13:2 \fr*\ft au \ft*\fqa mjukuu wa\fqa*\f* Urieli wa Gibea. \p Basi kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. \v 3 Abiya aliingia vitani na jeshi la watu elfu mia nne wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu elfu mia nane wenye uwezo. \p \v 4 Abiya akasimama juu ya Mlima Semaraimu, katika nchi ya vilima ya Efraimu, naye akasema, “Yeroboamu na Waisraeli wote, nisikilizeni! \v 5 Hamfahamu kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi na wazao wake ufalme juu ya Israeli milele kwa agano la chumvi? \v 6 Hata hivyo Yeroboamu mwana wa Nebati afisa wa Sulemani mwana wa Daudi, aliasi dhidi ya bwana wake. \v 7 Baadhi ya watu wasiofaa kitu, wabaya kabisa walimkusanyikia na kumpinga Rehoboamu mwana wa Sulemani alipokuwa kijana mdogo asiyekuwa na uamuzi, asiye na nguvu za kuweza kupingana nao. \p \v 8 “Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa Mwenyezi Mungu ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu. \v 9 Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa Mwenyezi Mungu, wana wa Haruni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu. \p \v 10 “Lakini kwetu sisi, Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wetu, wala hatujamwacha. Makuhani wanaomtumikia Mwenyezi Mungu ni wana wa Haruni, nao Walawi wakiwasaidia. \v 11 Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa Mwenyezi Mungu. Wao huweka mikate juu ya meza takatifu, na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu. \v 12 Mungu yu pamoja nasi; yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.” \p \v 13 Basi Yeroboamu alikuwa ametuma jeshi kuzunguka nyuma ya Yuda ili akiwa mbele ya Yuda, jeshi liwavizie kwa nyuma. \v 14 Basi Yuda wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa mbele na nyuma. Ndipo wakamlilia Mwenyezi Mungu. Makuhani wakapiga tarumbeta zao, \v 15 nao wanaume wa Yuda wakapiga ukelele wa vita. Walipopiga ukelele wa vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Waisraeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda. \v 16 Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia mikononi mwao. \v 17 Abiya na askari wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi elfu mia tano miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli. \v 18 Waisraeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. \p \v 19 Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vya miji hiyo. \v 20 Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. Naye Mwenyezi Mungu akampiga Yeroboamu akafa. \p \v 21 Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita. \p \v 22 Matukio mengine ya utawala wa Abiya, pamoja na mambo aliyofanya na aliyosema, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido. \c 14 \s1 Asa mfalme wa Yuda \p \v 1 Naye Abiya akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake. Katika siku zake, nchi ikawa na amani kwa miaka kumi. \p \v 2 Asa akatenda yaliyo mema na haki machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \v 3 Akaziondoa madhabahu za kigeni na mahali pa juu pa kuabudia, akayavunja yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Maashera. \v 4 Akawaamuru Yuda kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, na kutii sheria zake na amri zake. \v 5 Akaondoa mahali pa juu pa kuabudia na madhabahu za kufukizia uvumba kwenye kila mji katika Yuda, nao ufalme ulikuwa na amani katika utawala wake. \v 6 Akajenga miji yenye ngome katika Yuda, wakati nchi ikiwa na amani. Hakuna mtu yeyote aliyepigana vita naye katika miaka hiyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu alimpa amani. \p \v 7 Mfalme akawaambia Yuda, “Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupatia amani kila upande.” Hivyo wakajenga na wakafanikiwa. \p \v 8 Asa alikuwa na jeshi la watu elfu mia tatu kutoka Yuda, wenye ngao kubwa na mikuki, na jeshi la watu elfu mia mbili na themanini kutoka Benyamini, wenye ngao ndogo na pinde. Watu hawa wote walikuwa wapiganaji hodari. \p \v 9 Zera Mkushi akatoka kupigana dhidi yao akiwa na jeshi la watu maelfu ya maelfu na magari ya vita mia tatu, nao wakaja Maresha. \v 10 Asa akatoka kumkabili, nao wakapanga vita katika Bonde la Sefatha karibu na Maresha. \p \v 11 Kisha Asa akamlilia Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kusema, “Ee Mwenyezi Mungu, hakuna yeyote aliye kama wewe wa kuwasaidia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, Ee Mwenyezi Mungu, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. Ee Mwenyezi Mungu, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.” \p \v 12 Mwenyezi Mungu akawapiga Wakushi mbele ya Asa na Yuda. Wakushi wakakimbia, \v 13 naye Asa na jeshi lake wakawafuatia hadi Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za Mwenyezi Mungu na majeshi yake. Watu wa Yuda wakachukua nyara nyingi sana; \v 14 wakaangamiza vijiji vyote vya Gerari, kwa kuwa kicho cha Mwenyezi Mungu kilikuwa kimewaangukia. Wakateka nyara vijiji hivi vyote, kwani kulikuwa na nyara nyingi huko. \v 15 Pia wakashambulia kambi za wachunga makundi ya wanyama wakachukua na kuyaswaga makundi ya kondoo, mbuzi na ngamia. Kisha wakarudi Yerusalemu. \c 15 \s1 Asa afanya matengenezo \p \v 1 Roho wa Mungu akamjia Azaria mwana wa Odedi. \v 2 Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini mkimwacha, naye atawaacha. \v 3 Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria. \v 4 Lakini katika taabu yao walimrudia Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, na kumtafuta, naye akaonekana kwao. \v 5 Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa. \v 6 Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina. \v 7 Lakini ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.” \p \v 8 Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi yule nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji aliyoiteka katika nchi ya vilima ya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 9 Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni walioishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye. \p \v 10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. \v 11 Wakati huo wakamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu za ng’ombe mia saba, kondoo na mbuzi elfu saba kutoka nyara walizoteka. \v 12 Wakafanya agano kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. \v 13 Wale wote ambao hawangemtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. \v 14 Wakamwapia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, kwa kelele, na kupiga tarumbeta na mabaragumu. \v 15 Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawapa amani pande zote. \p \v 16 Mfalme Asa akamwondolea Maaka, bibi yake, wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. \v 17 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu maisha yake yote. \v 18 Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu. \p \v 19 Hapakuwa na vita tena hadi mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa. \c 16 \s1 Miaka ya mwisho ya Mfalme Asa \r (1 Wafalme 15:17-24) \p \v 1 Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda. \p \v 2 Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka hazina ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na kutoka jumba lake la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, aliyekuwa anatawala huko Dameski. \v 3 Akasema, “Na pawe mkataba kati yangu na wewe, kama palivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee.” \p \v 4 Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Wakashinda Iyoni, Dani, Abel-Maimu na miji yote ya hazina ya Naftali. \v 5 Baasha aliposikia jambo hili, akasimamisha kujenga Rama na kuacha kazi yake. \v 6 Ndipo Mfalme Asa akawaleta watu wote wa Yuda, nao wakachukua mawe na miti ambayo Baasha alikuwa anavitumia huko Rama. Kwa vitu hivyo akajenga Geba na Mispa. \p \v 7 Ikawa wakati huo mwonaji Hanani akamjia Mfalme Asa wa Yuda na kumwambia: “Kwa sababu ulimtegemea mfalme wa Aramu nawe hukumtegemea Mwenyezi Mungu, Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limeponyoka mkononi mwako. \v 8 Je, hukumbuki lililotendeka kwa Wakushi na Walibia, hawakuwa jeshi lenye nguvu na magari mengi ya vita na wapanda farasi? Hata hivyo, ulipomtegemea Mwenyezi Mungu yeye aliwatia mkononi mwako. \v 9 Kwa kuwa macho ya Mwenyezi Mungu yanazunguka dunia yote ili kuwatia nguvu wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu, na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.” \p \v 10 Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili. \p \v 11 Matukio ya utawala wa Asa, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. \v 12 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alishikwa na ugonjwa kwa miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu bali kwa matabibu tu. \v 13 Katika mwaka wa arobaini na moja wa utawala wa Asa, alikufa, akalala na baba zake. \v 14 Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amejichongea katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezo na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake. \c 17 \s1 Yehoshafati mfalme wa Yuda \p \v 1 Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake na akajiimarisha dhidi ya Israeli. \v 2 Akaweka jeshi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, na kuweka askari walinzi katika Yuda na katika miji ya Efraimu ambayo baba yake Asa alikuwa ameiteka. \p \v 3 Mwenyezi Mungu alikuwa na Yehoshafati kwa sababu katika miaka yake ya mwanzoni alienenda katika njia za Daudi baba yake. Hakutafuta Mabaali \v 4 bali alimtafuta Mungu wa baba yake na kuzifuata amri zake badala ya kufuata desturi za Waisraeli. \v 5 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akauimarisha ufalme chini ya uongozi wake, nao Yuda wote wakamletea Yehoshafati zawadi, hivyo akawa na utajiri mwingi na heshima. \v 6 Moyo wake ukawa hodari katika njia za Mwenyezi Mungu na zaidi ya yote, akaondoa mahali pa juu pa kuabudia na nguzo za Maashera katika Yuda. \p \v 7 Katika mwaka wa tatu wa utawala wake Yehoshafati, alituma maafisa wake ambao ni Ben-Haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli na Mikaya ili kufundisha katika miji ya Yuda. \v 8 Pamoja nao walikuwa na Walawi kadhaa: Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, Tob-Adonia; na pamoja nao makuhani Elishama na Yehoramu. \v 9 Wakafundisha Yuda yote, wakiwa wamechukua Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu; wakazunguka miji yote ya Yuda na kufundisha watu. \p \v 10 Kicho cha Mwenyezi Mungu kikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati. \v 11 Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi na fedha kama ushuru, nao Waarabu wakamletea mifugo: kondoo dume elfu saba na mia saba, na mbuzi elfu saba na mia saba. \p \v 12 Yehoshafati akaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi, akajenga ngome na miji ya hazina katika Yuda, \v 13 na akawa na vifaa vingi katika miji ya Yuda. Pia aliweka wapiganaji wenye uzoefu huko Yerusalemu. \v 14 Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo: \b \li1 Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu: \li2 Jemadari Adna akiwa na wapiganaji elfu mia tatu; \li2 \v 15 aliyefuata ni jemadari Yehohanani, akiwa na wapiganaji elfu mia mbili na themanini; \li2 \v 16 aliyefuata ni Amasia mwana wa Zikri, ambaye alijitolea kwa ajili ya kazi ya Mwenyezi Mungu, akiwa na wapiganaji elfu mia mbili. \li1 \v 17 Kutoka Benyamini: \li2 Eliada, mpiganaji hodari, akiwa na watu elfu mia mbili wenye nyuta na ngao; \li2 \v 18 aliyefuata ni Yehozabadi, akiwa na wapiganaji elfu mia moja na themanini tayari kwa vita. \b \m \v 19 Hawa ndio wapiganaji waliomtumikia mfalme, mbali na ambao mfalme aliwaweka katika miji yenye ngome katika Yuda yote. \c 18 \s1 Mikaya atabiri dhidi ya Ahabu \r (1 Wafalme 22:1-28) \p \v 1 Basi, Yehoshafati alikuwa na mali nyingi sana na heshima. Naye akafanya urafiki na Ahabu kwa uhusiano wa ndoa. \v 2 Baada ya miaka kadhaa akateremka kumtembelea Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja ng’ombe na kondoo wengi kwa ajili yake na watu aliokuwa amefuatana nao. Kisha Ahabu akamshawishi Yehoshafati kukwea pamoja naye ili kuishambulia Ramoth-Gileadi. \v 3 Ahabu mfalme wa Israeli akamuuliza Yehoshafati mfalme wa Yuda, “Je, utaenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?” \p Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako. Tutakuwa pamoja nawe vitani.” \v 4 Lakini Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta ushauri wa Mwenyezi Mungu.” \p \v 5 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii, wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?” \p Wakajibu, “Naam, nenda kwa kuwa Mungu ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.” \p \v 6 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Mwenyezi Mungu hapa ambaye tunaweza kumuuliza?” \p \v 7 Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia kwake twaweza kuuliza ushauri wa Mwenyezi Mungu, lakini namchukia kwa sababu hatabiri jambo lolote jema kunihusu, ila hunitabiria mabaya kila mara. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” \p Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.” \p \v 8 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.” \p \v 9 Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, huku manabii wote wakitabiri mbele yao. \v 10 Wakati huu Sedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma. Naye akatangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, ‘Kwa hizi pembe utawapiga Waaramu hadi waangamizwe.’ ” \p \v 11 Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho, wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ataitia mkononi mwa mfalme.” \p \v 12 Mjumbe aliyekuwa ameenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.” \p \v 13 Lakini Mikaya akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, nitamwambia kile tu Mwenyezi Mungu atakachoniambia.” \p \v 14 Alipofika, mfalme akamuuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?” \p Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwa watatiwa mkononi mwako.” \p \v 15 Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu chochote ila kweli tu kwa jina la Mwenyezi Mungu?” \p \v 16 Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Mwenyezi Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ” \p \v 17 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu, ila mabaya tu?” \p \v 18 Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Mwenyezi Mungu: Nilimwona Mwenyezi Mungu ameketi kwenye kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama upande wa kulia na wa kushoto. \v 19 Naye Mwenyezi Mungu akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu, mfalme wa Israeli, ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’ \p “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. \v 20 Hatimaye, roho akajitokeza, akasimama mbele za Mwenyezi Mungu na kusema, ‘Nitamshawishi.’ \p “Mwenyezi Mungu akauliza, ‘Kwa njia gani?’ \p \v 21 “Akasema, ‘Nitaenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ \p “Mwenyezi Mungu akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’ \p \v 22 “Kwa hiyo sasa Mwenyezi Mungu ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. Mwenyezi Mungu ameamuru maafa kwa ajili yako.” \p \v 23 Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa Mwenyezi Mungu alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?” \p \v 24 Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapoenda kujificha kwenye chumba cha ndani.” \p \v 25 Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni Mikaya, mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji, na kwa Yoashi mwana wa mfalme. \v 26 Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe chochote ila mkate na maji hadi nitakaporudi salama.’ ” \p \v 27 Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basi Mwenyezi Mungu hajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!” \s1 Ahabu anauawa huko Ramoth-Gileadi \r (1 Wafalme 22:29-35) \p \v 28 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi. \v 29 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani. \p \v 30 Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.” \v 31 Wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati, wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati akapiga kelele, naye Mwenyezi Mungu akamsaidia. Mungu akawaondoa kwake, \v 32 wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli nao wakaacha kumfuatilia. \p \v 33 Lakini mtu fulani akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma. Mfalme akamwambia mwendesha gari lake la vita, “Geuza gari na uniondoe katika mapigano, nimejeruhiwa.” \v 34 Vita vikaendelea mchana kutwa, naye mfalme wa Israeli akajitegemeza ndani ya gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Basi jioni yake akafa. \c 19 \s1 Yehu amkemea Yehoshafati \p \v 1 Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu. \v 2 Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukia Mwenyezi Mungu? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iko juu yako. \v 3 Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.” \s1 Yehoshafati aweka waamuzi \p \v 4 Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza wakamrudia Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. \v 5 Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye ngome. \v 6 Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mnayotenda, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu. \v 7 Basi sasa kicho cha Mwenyezi Mungu na kiwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hakuna jambo la dhuluma, wala upendeleo, wala rushwa.” \p \v 8 Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu. \v 9 Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho cha Mwenyezi Mungu. \v 10 Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine kuhusu sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya Mwenyezi Mungu, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi. \p \v 11 “Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu Mwenyezi Mungu naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja na wale watendao vyema.” \c 20 \s1 Yehoshafati ashinda Wamoabu na Waamoni \p \v 1 Ikawa baada ya jambo hili, Wamoabu na Waamoni, pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja ili wapigane vita na Yehoshafati. \p \v 2 Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Shamu tokea ng’ambo ile nyingine ya Bahari.\f + \fr 20:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari ya Chumvi.\fqa*\f* Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi). \v 3 Yehoshafati akaogopa, akaamua kumtafuta Mwenyezi Mungu, na akatangaza kwa Yuda wote kufunga. \v 4 Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta. \p \v 5 Kisha Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, mbele ya ua mpya, \v 6 akasema: \pm “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe unayetawala juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna yeyote anayeweza kushindana nawe. \v 7 Je, si ni wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, na ukawapa wazao wa rafiki yako Ibrahimu hata milele? \v 8 Wameishi ndani yake na humo wamekujengea mahali patakatifu kwa ajili ya Jina lako, wakisema: \v 9 ‘Kama maafa yakitujia, ikiwa ni upanga, hukumu, tauni, au njaa, tutasimama mbele zako, mbele ya Hekalu hili ambalo limeitwa kwa Jina lako na kukulilia katika shida yetu, nawe utatusikia na kutuokoa.’ \pm \v 10 “Lakini sasa hawa watu wa Amoni, Moabu na Mlima Seiri, ambao hukuwaruhusu Israeli wazivamie nchi zao wakati walitoka Misri; hivyo wakageukia mbali nao na hawakuwaangamiza. \v 11 Tazama jinsi wanavyotulipa kwa kuja kututupa nje ya milki uliyotupatia sisi kuwa urithi. \v 12 Ee Mungu wetu, je, wewe hutawahukumu? Kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja kutushambulia. Sisi hatujui la kufanya, bali macho yetu yanakutazama wewe.” \p \v 13 Wanaume wote wa Yuda pamoja na wake zao, watoto wao na wadogo wao wakasimama pale mbele za Mwenyezi Mungu. \p \v 14 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya mtu mmoja jina lake Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, Mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi mzao wa Asafu alipokuwa amesimama katika kusanyiko. \p \v 15 Akasema: “Sikilizeni, enyi Yuda wote nanyi nyote mnaoishi Yerusalemu, nawe Mfalme Yehoshafati! Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwenu, ‘Msiogope wala msifadhaike kwa sababu ya jeshi hili kubwa. Kwa maana vita hivi si vyenu, bali ni vya Mungu. \v 16 Kesho shukeni kukabiliana nao. Watakwea kwa kupandia Genge la Sisi, nanyi mtawakuta mwisho wa bonde, kabla ya Jangwa la Yerueli. \v 17 Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Mwenyezi Mungu atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja nanyi.’ ” \p \v 18 Yehoshafati akasujudu, uso wake ukigusa chini, nao watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakasujudu na kuabudu mbele za Mwenyezi Mungu. \v 19 Ndipo baadhi ya Walawi kutoka kwa Wakohathi na kwa wana wa Kora wakasimama na kumsifu Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana. \p \v 20 Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.” \v 21 Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: \q1 “Mshukuruni Mwenyezi Mungu \q2 kwa kuwa fadhili zake zadumu milele.” \p \v 22 Walipoanza kuimba na kusifu, Mwenyezi Mungu akaweka waviziaji dhidi ya watu wa Amoni, Moabu na wale wa Mlima Seiri waliokuwa wamekuja kuishambulia Yuda, nao wakashindwa. \v 23 Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakaangamizana wao kwa wao. \p \v 24 Yuda walipofika katika mnara wa ulinzi wa jangwani, wakaliangalia lile jeshi kubwa, wakaona ni maiti tupu zimetapakaa ardhini, wala hakuna yeyote aliyenusurika. \v 25 Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, mavazi na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno. \v 26 Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka\f + \fr 20:26 \fr*\ft Bonde la Beraka maana yake \ft*\fqa Bonde la Kusifu.\fqa*\f*, mahali walikomtukuza Mwenyezi Mungu. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka hadi leo. \p \v 27 Kisha wanaume wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha, kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao. \v 28 Wakaingia Yerusalemu na kwenda hekaluni mwa Mwenyezi Mungu wakiwa na vinubi, zeze na tarumbeta. \p \v 29 Hofu ya Mungu ikazipata falme zote za nchi waliposikia jinsi Mwenyezi Mungu alivyokuwa amepigana dhidi ya adui za Israeli. \v 30 Ufalme wa Yehoshafati ukawa na amani, kwa kuwa Mungu wake alikuwa amempa amani pande zote. \s1 Mwisho wa utawala wa Yehoshafati \r (1 Wafalme 22:41-50) \p \v 31 Hivyo Yehoshafati akatawala Yuda. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na tano. Mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi. \v 32 Alienenda katika njia za Asa baba yake wala hakuenda kinyume chake. Alifanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu. \v 33 Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa, na watu wakawa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa baba zao. \p \v 34 Matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Yehu mwana wa Hanani, ambazo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli. \p \v 35 Hatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya mapatano na Ahazia mfalme wa Israeli, ambaye alifanya maovu sana. \v 36 Akaungana naye kutengeneza meli nyingi za kwenda Tarshishi\f + \fr 20:36 \fr*\ft au: \ft*\fqa za biashara\fqa*\ft (taz. \+xt 1 Wafalme 10:22; 22:48; 2 Nyakati 9:21; Isaya 2:16; 60:9\+xt*).\ft*\f*, nazo zilitengenezwa huko Esion-Geberi. \v 37 Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia, Mwenyezi Mungu ataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kung’oa nanga ili kwenda Tarshishi. \c 21 \s1 Yehoramu mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 8:17-24) \p \v 1 Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake. \v 2 Ndugu zake Yehoramu, wana wa Yehoshafati walikuwa: Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli na Shefatia. Hawa wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli\f + \fr 21:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Yuda.\fqa*\f*. \v 3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali akampa Yehoramu ufalme kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. \p \v 4 Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli. \v 5 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka nane. \v 6 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti Ahabu. Akatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. \v 7 Hata hivyo, kwa sababu ya agano ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa amefanya na Daudi, Mwenyezi Mungu hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele. \p \v 8 Wakati wa utawala wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. \v 9 Basi Yehoramu akaenda huko pamoja na maafisa wake na magari yake ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. \v 10 Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. \p Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake. \v 11 Alikuwa pia ametengeneza mahali pa juu pa kuabudia katika vilima vya Yuda na akawa amewasababisha watu wa Yerusalemu kufanya uzinzi na akawa amewapotosha watu wa Yuda. \p \v 12 Yehoramu akapokea barua kutoka kwa nabii Ilya iliyosema: \pm “Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Daudi baba yako, asemalo: ‘Hukuenenda katika njia za Yehoshafati baba yako au za Asa mfalme wa Yuda. \v 13 Lakini umeenenda katika njia za wafalme wa Israeli, nawe umewaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu kuzini, kama vile nyumba ya Ahabu ilivyofanya. Pia umewaua ndugu zako mwenyewe, watu wa nyumbani mwa baba yako, watu waliokuwa bora kuliko wewe. \v 14 Hivyo basi Mwenyezi Mungu yu karibu kuwapiga watu wako, wanao, wake zako na kila kitu kilicho chako, kwa pigo zito. \v 15 Wewe mwenyewe utaugua sana kwa ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu, hadi ugonjwa utakaposababisha matumbo yako kutoka nje.’ ” \p \v 16 Mwenyezi Mungu akaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu. \v 17 Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali yote iliyopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana yeyote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote. \p \v 18 Baada ya mambo haya yote, Mwenyezi Mungu akampiga Yehoramu kwa ugonjwa wa matumbo usio wa kupona. \v 19 Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake. \p \v 20 Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka nane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme. \c 22 \s1 Ahazia mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 8:25-29; 9:21-28) \p \v 1 Watu wa Yerusalemu wakamfanya Ahazia, mdogo wa wote wa wana wa Yerohamu, kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwa sababu washambuliaji wa ghafula walioingia kambini pamoja na Waarabu, walikuwa wamewaua wana wakubwa wote wa Yehoramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akaanza kutawala. \p \v 2 Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia, mjukuu wa Omri. \p \v 3 Ahazia naye akaenenda katika njia za nyumba ya Ahabu, kwa sababu mama yake alimshawishi kutenda uovu. \v 4 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa wamefanya nyumba ya Ahabu, kwa kuwa baada ya kufa kwa baba yake, nyumba ya Ahabu ndio walikuwa washauri wake, kwa uangamivu wake. \v 5 Pia akafuata ushauri wao alipoenda pamoja na Yoramu\f + \fr 22:5 \fr*\ft au \ft*\fqa Yehoramu\fqa*\f* mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu. \v 6 Hivyo akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyojeruhiwa huko Ramothi\f + \fr 22:6 \fr*\fqa Rama \fqa*\ft kwa Kiebrania.\ft*\f* alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. \p Ndipo Ahazia\f + \fr 22:6 \fr*\ft au \ft*\fqa Azaria\fqa*\f* mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa. \p \v 7 Mungu alisababisha anguko la Ahazia kutokana na Ahazia kwenda kumwona Yoramu. Ahazia alipowasili, wakatoka pamoja na Yoramu ili kwenda kukutana na Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Mwenyezi Mungu alikuwa amempaka mafuta kuangamiza nyumba ya Ahabu. \v 8 Yehu alipokuwa anatekeleza hukumu juu ya nyumba ya Ahabu, akawakuta wakuu wa Yuda na wana wa jamaa ya Ahazia waliokuwa wanamhudumia Ahazia, naye akawaua. \v 9 Ndipo akaenda kumsaka Ahazia, nao watu wake wakamkamata alipokuwa amejificha huko Samaria. Akaletwa kwa Yehu, naye Yehu akamuua. Wakamzika, kwani walisema, “Alikuwa mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Mwenyezi Mungu kwa moyo wake wote.” Hivyo hapakuwa na mtu mwenye uwezo katika nyumba ya Ahazia aliyeweza kushika ufalme. \s1 Athalia na Yoashi \r (2 Wafalme 11:1-3) \p \v 10 Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akainuka na kuangamiza jamaa yote ya mfalme ya nyumba ya Yuda. \v 11 Lakini Yehosheba, binti Mfalme Yehoramu, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala. Kwa kuwa Yehosheba, aliyekuwa binti Mfalme Yehoramu, na pia alikuwa mke wa kuhani Yehoyada, alikuwa dada yake Ahazia, akamficha huyo mtoto ili Athalia asimuue. \v 12 Alibaki amefichwa pamoja nao katika Hekalu la Mungu kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alikuwa akitawala nchi. \c 23 \s1 Uasi dhidi ya Athalia \r (2 Wafalme 11:4-20) \p \v 1 Katika mwaka wa saba, Yehoyada akaonesha nguvu zake. Alifanya agano na wakuu wa vikosi vya mamia: yaani Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri. \v 2 Wakazunguka katika Yuda yote na kukusanya Walawi na viongozi wa jamaa za Israeli kutoka miji yote. Walipofika Yerusalemu, \v 3 kusanyiko lote wakafanya agano na mfalme katika Hekalu la Mungu. \p Yehoyada akawaambia, “Mwana wa mfalme atatawala, kama Mwenyezi Mungu alivyoahidi kuhusu wazao wa Daudi. \v 4 Basi hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Theluthi yenu makuhani na Walawi ambao mnaingia zamu siku ya Sabato mtalinda milangoni, \v 5 theluthi yenu mtalinda jumba la kifalme, na theluthi nyingine mtalinda Lango la Msingi. Walinzi wengine wote mwe ndani ya nyua za Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 6 Hakuna mtu yeyote ataingia katika Hekalu la Mwenyezi Mungu isipokuwa makuhani na Walawi walio kwenye zamu. Wao wanaweza kuingia kwa sababu ni watakatifu, lakini watu wengine wote itawapasa kulinda kile walichoamriwa na Mwenyezi Mungu. \v 7 Walawi watajipanga kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha zake mkononi. Mtu mwingine yeyote aingiaye Hekaluni lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme popote aendapo.” \p \v 8 Walawi na watu wote wa Yuda wakafanya vile kuhani Yehoyada aliagiza. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakiingia zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakienda mapumziko, kwa sababu kuhani Yehoyada hakuruhusu kikosi chochote kiondoke. \v 9 Kisha kuhani Yehoyada akawapa wakuu wa vikosi vya mamia mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa za Mfalme Daudi, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu. \v 10 Akawapanga walinzi wote kumzunguka mfalme, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi mwake, karibu na madhabahu na Hekalu, kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini mwa Hekalu. \p \v 11 Yehoyada na wanawe wakamtoa Yoashi mwana wa mfalme nje na kumvika taji. Wakampa nakala ya agano na kumtangaza kuwa mfalme. Wakampaka mafuta na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!” \p \v 12 Athalia aliposikia kelele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akawaendea watu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 13 Akaangalia, na tazama, mfalme alikuwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta, na waimbaji waliokuwa na vyombo vya uimbaji walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kulia, “Uhaini! Uhaini!” \p \v 14 Kuhani Yehoyada akawatuma majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, na kuwaambia: “Mleteni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Msimuulie ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.” \v 15 Kwa hiyo wakamkamata alipofika kwenye ingilio la Lango la Farasi, katika viwanja vya jumba la mfalme, wakamuua hapo. \p \v 16 Kisha Yehoyada akafanya agano kwamba yeye na watu wote na mfalme watakuwa watu wa Mwenyezi Mungu. \v 17 Watu wote wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu pamoja na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu. \p \v 18 Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu mikononi mwa makuhani, hao Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa za Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kushangilia na kuimba, vile Daudi alikuwa ameagiza. \v 19 Pia akawaweka mabawabu kwenye malango ya Hekalu la Mwenyezi Mungu ili kwa vyovyote asije akaingia mtu yeyote aliye najisi. \p \v 20 Akawachukua majemadari wa mamia, watu waheshimiwa, viongozi wa watu pamoja na watu wote wa nchi na kumteremsha mfalme kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Wakaingia kwenye jumba la mfalme kupitia Lango la Juu na kumkalisha mfalme kwenye kiti cha ufalme; \v 21 nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga. \c 24 \s1 Yoashi akarabati Hekalu \r (2 Wafalme 12:1-16) \p \v 1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba. \v 2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu miaka yote ya Yehoyada kuhani. \v 3 Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike. \p \v 4 Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 5 Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi. \p \v 6 Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada kuhani mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu pamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema la Ushuhuda?” \p \v 7 Kwa kuwa wana wa yule mwanamke mwovu Athalia, walikuwa wamevunja na kuingia katika Hekalu la Mungu, nao wakawa wamevitumia hata vile vitu vilivyowekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu kwa mabaali. \p \v 8 Kwa amri ya mfalme, likatengenezwa kasha, nalo likawekwa nje kwenye lango la Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 9 Tangazo likatolewa katika Yuda na Yerusalemu, kwamba inapasa wamletee Mwenyezi Mungu kodi ambayo Musa, mtumishi wa Mwenyezi Mungu, alikuwa amewaagiza Israeli huko jangwani. \v 10 Maafisa wote na watu wote wakaleta michango yao kwa furaha, wakaweka kwenye kasha hadi likajaa. \v 11 Ikawa kila wakati kasha lilipoletwa ndani na Walawi kwa maafisa wa mfalme na kuona kwamba kuna kiasi kikubwa cha fedha, mwandishi wa mfalme na afisa wa kuhani mkuu walikuwa wanakuja na kumimina, kisha kulirudisha mahali pake. Walifanya hivi mara kwa mara, nao wakakusanya fedha nyingi sana. \v 12 Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la Mwenyezi Mungu, pia wafanyakazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 13 Watu walioshughulika na kazi walikuwa wenye bidii, nayo kazi ya kukarabati ikaendelea vizuri mikononi mwao. Wakalitengeneza upya Hekalu la Mwenyezi Mungu likarudi katika hali yake ya awali, na wakaliimarisha. \v 14 Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada akiwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 15 Basi Yehoyada alikuwa mzee aliyeshiba siku alipofariki. Alikufa akiwa na umri wa miaka mia moja na thelathini. \v 16 Wakamzika pamoja na wafalme katika Mji wa Daudi, kwa sababu ya mema aliyokuwa ametenda katika Israeli kwa ajili ya Mungu na Hekalu lake. \s1 Uovu wa Yoashi \p \v 17 Baada ya kifo cha Yehoyada, wakuu wa Yuda walikuja kumpa mfalme heshima, naye akawasikiliza. \v 18 Wakaacha Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya hatia yao, hasira ya Mungu ikawajia Yuda na Yerusalemu. \v 19 Ingawa Mwenyezi Mungu aliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza. \p \v 20 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za Mwenyezi Mungu? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha Mwenyezi Mungu, naye amewaacha ninyi.’ ” \p \v 21 Lakini wakapanga njama dhidi yake, na kwa amri ya mfalme wakampiga kwa mawe hadi akafa katika ua wa Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 22 Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria, ila alimuua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “Mwenyezi Mungu na alione hili na alipize kisasi.” \p \v 23 Mwishoni mwa ule mwaka, jeshi la Waaramu likaja dhidi ya Yoashi, likavamia Yuda na Yerusalemu na kuwaua viongozi wote wa watu. Wakapeleka nyara zao zote kwa mfalme wao huko Dameski. \v 24 Ingawa jeshi la Waaramu lilikuwa limekuja na watu wachache tu, Mwenyezi Mungu akatia mikononi mwao jeshi kubwa kuliko lao. Kwa sababu Yuda walikuwa wamemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, hukumu ilitekelezwa juu ya Yoashi. \v 25 Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu alikuwa amemuua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamuua kitandani mwake. Hivyo akafa, wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme. \p \v 26 Wale waliopanga njama dhidi yake walikuwa Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabu. \v 27 Kwa habari za wanawe, unabii mwingi kumhusu na kumbukumbu za kutengenezwa upya kwa Hekalu la Mungu, zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme. Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 25 \s1 Amazia mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 14:2-20) \p \v 1 Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Yehoadani kutoka Yerusalemu. \v 2 Akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, lakini sio kwa moyo wake wote. \v 3 Baada ya ufalme kuimarika mkononi mwake, aliwaua maafisa waliomuua mfalme baba yake. \v 4 Hata hivyo hakuwaua watoto wao, lakini akafanya sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati, katika Kitabu cha Musa, ambako Mwenyezi Mungu aliamuru: “Baba hawatauawa kwa ajili ya watoto wao, wala watoto hawatauawa kwa ajili ya baba zao. Kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.” \p \v 5 Amazia akawaita watu wa Yuda pamoja, akawaweka chini ya majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia kufuatana na jamaa zao katika Yuda yote na Benyamini. Kisha akawahesabu wale wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na akakuta kwamba walikuwa wanaume elfu mia tatu walio tayari kwa utumishi wa jeshi, wenye uwezo wa kutumia mkuki na ngao. \v 6 Akawaajiri pia wapiganaji elfu mia moja kutoka Israeli kwa talanta mia moja za fedha.\f + \fr 25:6 \fr*\ft Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.\ft*\f* \p \v 7 Lakini mtu wa Mungu akamjia na kumwambia, “Ee mfalme, haya majeshi kutoka Israeli kamwe usiyaruhusu yaende pamoja na wewe, kwa kuwa Mwenyezi Mungu hayuko pamoja na Israeli, wala hayupo pamoja na yeyote wa watu wa Efraimu. \v 8 Hata ukienda na kupigana kwa ujasiri katika vita, Mungu atakufanya ukimbie mbele ya adui, kwa kuwa Mungu anao uwezo wa kusaidia au wa kuangusha.” \p \v 9 Amazia akamuuliza yule mtu wa Mungu, “Lakini itakuwaje kwa zile talanta mia moja za fedha nilizolipa kwa ajili ya haya majeshi ya Israeli?” \p Yule mtu wa Mungu akajibu, “Mwenyezi Mungu aweza kukupa zaidi ya hizo.” \p \v 10 Hivyo Amazia akayaondoa yale majeshi yaliyokuwa yamekuja kutoka Efraimu na kuyarudisha nyumbani. Waliwakasirikia sana Yuda, nao wakarudi nyumbani wakiwa na hasira kali. \p \v 11 Ndipo Amazia akajitia nguvu na kuliongoza jeshi lake hadi Bonde la Chumvi, ambako aliwaua watu elfu kumi wa Seiri. \v 12 Jeshi la Yuda pia likawateka watu elfu kumi wakiwa hai, likawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini kwa nguvu, wote wakavunjika vipande vipande. \p \v 13 Wakati huo, wanajeshi waliorudishwa na Amazia, ambao hakuwaruhusu kushiriki katika vita, walivamia miji ya Yuda kuanzia Samaria hata Beth-Horoni. Wakawaua watu elfu tatu na kuchukua nyara nyingi sana. \p \v 14 Amazia aliporudi kutoka kuwaua Waedomu, alileta pia kutoka huko miungu ya watu wa Seiri. Akaisimamisha kama miungu yake mwenyewe, akaisujudia na kuitolea sadaka za kuteketezwa. \v 15 Hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Amazia, naye akamtuma nabii kwake, ambaye alisema: “Kwa nini unauliza kwa miungu ya hawa watu, ambayo haikuweza kuwaokoa watu wake wenyewe kutoka mkononi mwako?” \p \v 16 Nabii alipokuwa angali anazungumza, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekuchagua kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza! Kwa nini uuawe?” \p Hivyo nabii akanyamaza lakini akasema, “Najua kuwa Mungu ameazimia kukuangamiza kwa sababu umefanya jambo hili na hukusikiliza ushauri wangu.” \p \v 17 Baada ya Amazia mfalme wa Yuda kushauriana na washauri wake, akatuma ujumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mwana wa Yehu, mfalme wa Israeli, kusema: “Njoo tukabiliane uso kwa uso.” \p \v 18 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akamjibu Amazia mfalme wa Yuda, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi uliokuwa Lebanoni, ‘Mtoe binti yako aolewe na mwanangu.’ Kisha mnyama wa mwituni aliyekuwa Lebanoni akaja na kuukanyaga ule mbaruti. \v 19 Wewe unasema moyoni mwako kwamba umemshinda Edomu, nawe sasa unajigamba na kujivuna. Lakini kaa nyumbani mwako! Kwa nini utafute matatizo na kujiletea anguko lako mwenyewe na la Yuda pia?” \p \v 20 Hata hivyo, Amazia hakutaka kusikia, kwa kuwa Mungu alifanya hivyo ili awatie mikononi mwa Yehoashi, kwa sababu waliitafuta miungu ya Edomu. \v 21 Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea kuwashambulia. Yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakabiliana uso kwa uso huko Beth-Shemeshi katika Yuda. \v 22 Yuda ikashindwa na Israeli na kila mtu akakimbilia nyumbani mwake. \v 23 Yehoashi mfalme wa Israeli akamteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akamleta Yerusalemu na kuubomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia lango la Efraimu hadi Lango la Pembeni, sehemu yenye urefu wa kama dhiraa mia nne\f + \fr 25:23 \fr*\ft Dhiraa 400 ni sawa na mita 180.\ft*\f*. \v 24 Akachukua dhahabu yote, fedha na vyombo vyote vilivyopatikana katika Hekalu la Mungu, ambavyo vilikuwa chini ya uangalizi wa Obed-Edomu, pamoja na hazina za jumba la mfalme na mateka, kisha akarudi Samaria. \p \v 25 Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi mwana wa Yehoahazi mfalme wa Israeli. \v 26 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Amazia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na wa Israeli? \v 27 Kuanzia wakati Amazia alipogeuka na kuacha kumfuata Mwenyezi Mungu, walipanga njama dhidi yake huko Yerusalemu, naye akakimbilia Lakishi. Lakini wakawatuma watu wamfuatilie huko Lakishi, nao wakamuua huko. \v 28 Akarudishwa kwa farasi, akazikwa na baba zake katika Mji wa Yuda. \c 26 \s1 Uzia mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 14:21-22; 15:1-7) \p \v 1 Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, aliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita, nao wakamfanya mfalme mahali pa Amazia baba yake. \v 2 Ndiye aliijenga upya Elathi na kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala na baba zake. \p \v 3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na mbili. Mama yake aliitwa Yekolia, kutoka Yerusalemu. \v 4 Akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, vile Amazia baba yake alivyofanya. \v 5 Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu alimfanikisha. \p \v 6 Alipigana vita dhidi ya Wafilisti na kubomoa kuta za Gathi, Yabne na Ashdodi. Kisha akajenga upya miji karibu na Ashdodi, na mahali pengine katikati ya Wafilisti. \v 7 Mungu akamsaidia dhidi ya Wafilisti na dhidi ya Waarabu walioishi Gur-Baali na dhidi ya Wameuni. \v 8 Waamoni wakamletea Uzia ushuru, na umaarufu wake ukaenea hadi mpaka wa Misri, kwa sababu alikuwa na nguvu sana. \p \v 9 Uzia akajenga minara huko Yerusalemu katika Lango la Pembeni, katika Lango la Bondeni na katika pembe, mahali kuta zikutanapo, kisha akaijengea ngome. \v 10 Akajenga pia minara jangwani na kuchimba visima vingi vya maji, kwa sababu alikuwa na mifugo mingi chini ya vilima na katika nchi tambarare. Alikuwa na watu waliofanya kazi katika mashamba yake, na kwenye mashamba yake ya mizabibu huko vilimani na katika ardhi zenye rutuba, kwa kuwa aliupenda udongo. \p \v 11 Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi lililofunzwa vizuri, lililokuwa tayari kwenda vitani kwa vikosi kufuatana na idadi yao kama walivyokusanywa na Yeieli mwandishi na Maaseya msimamizi chini ya maelekezo ya Hanania, mmoja wa maafisa wa mfalme. \v 12 Idadi yote ya viongozi wa jamaa waliowaongoza wapiganaji walikuwa elfu mbili na mia sita. \v 13 Chini ya uongozi wao kulikuwa na jeshi la watu elfu mia tatu na saba na mia tano waliofundishwa kwa ajili ya vita, jeshi lenye nguvu la kumsaidia mfalme dhidi ya adui zake. \v 14 Uzia akalipatia jeshi lote ngao, mikuki, chapeo, dirii, pinde na mawe ya kombeo. \v 15 Huko Yerusalemu watu wenye utaalamu mkubwa wakatengeneza mitambo iliyotumika katika minara na kwenye pembe za ulinzi ili kurusha mishale na kuvurumisha mawe makubwa. Sifa zake zikaenea mbali sana kwa sababu alisaidiwa mno hadi akawa na nguvu sana. \p \v 16 Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa Mwenyezi Mungu ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba. \v 17 Azaria kuhani akiwa pamoja na makuhani wengine themanini wa Mwenyezi Mungu wenye ujasiri wakamfuata ndani. \v 18 Wakamkabili na kumwambia, “Siyo sawa kwako, Uzia, kumfukizia Mwenyezi Mungu uvumba. Hiyo ni kazi ya makuhani, wazao wa Haruni, ambao wamewekwa wakfu ili kufukiza uvumba. Ondoka mahali patakatifu, kwa kuwa umekosa uaminifu nawe hutaheshimiwa na Bwana Mwenyezi Mungu.” \p \v 19 Uzia, aliyekuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, ukoma ukamtokea kwenye paji la uso wake. \v 20 Azaria kuhani mkuu pamoja na makuhani wengine wote walipomtazama wakaona kwamba alikuwa na ukoma pajini lake, wakaharakisha kumtoa nje. Naam, hata yeye mwenyewe alitamani kuondoka kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amempiga. \p \v 21 Mfalme Uzia alikuwa na ukoma hadi siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la mfalme, pia akawaongoza watu wa nchi. \p \v 22 Matukio mengine ya utawala wa Uzia, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa na nabii Isaya mwana wa Amozi. \v 23 Uzia akalala na baba zake, akazikwa karibu nao katika shamba la kuzikia lililokuwa mali ya wafalme, kwa kuwa watu walisema, “Alikuwa na ukoma.” Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 27 \s1 Yothamu mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 15:32-38) \p \v 1 Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. \v 2 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya. \v 3 Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli. \v 4 Akajenga miji katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na ngome na minara mwituni. \p \v 5 Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta mia moja\f + \fr 27:5 \fr*\ft Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.\ft*\f* za fedha, kori elfu kumi\f + \fr 27:5 \fr*\ft Kori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2.\ft*\f* za ngano, na kori elfu kumi za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu. \p \v 6 Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \p \v 7 Matukio mengine ya utawala wa Yothamu, pamoja na vita vyake vyote na vitu vingine alivyofanya, vimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. \v 8 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. \v 9 Yothamu akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 28 \s1 Ahazi mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 16:1-6) \p \v 1 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala. Akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na sita. Tofauti na Daudi baba yake, hakufanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu. \v 2 Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na pia akasubu sanamu kwa ajili ya kuabudu Mabaali. \v 3 Akatoa sadaka za kuteketezwa katika Bonde la Ben-Hinomu, na kuwatoa kafara watoto wake kwa kuwateketeza kwa moto, akifuata njia za machukizo za yale mataifa Mwenyezi Mungu aliyoyafukuza humo mbele ya Waisraeli. \v 4 Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia, juu ya vilima, na chini ya kila mti uliotanda. \p \v 5 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, Mungu wake, akamtia mikononi mwa mfalme wa Aramu. Waaramu wakamshinda, wakachukua watu wake wengi mateka na kuwaleta Dameski. \p Tena alitiwa mikononi mwa mfalme wa Israeli, ambaye aliwaua watu wake wengi. \v 6 Kwa siku moja Peka mwana wa Remalia aliwaua askari elfu mia moja na ishirini katika Yuda, kwa kuwa Yuda walikuwa wamemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. \v 7 Zikri, askari shujaa Mwefraimu, akamuua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu mkuu wa jumba la kifalme na Elkana aliyekuwa wa pili kwa mfalme. \v 8 Waisraeli wakawachukua mateka kutoka ndugu zao, watu wapatao elfu mia mbili, wakiwa wanawake, pamoja na watoto wa kiume na wa kike. Wakachukua pia kiasi kikubwa cha nyara, ambazo walirudi nazo Samaria. \p \v 9 Lakini huko kulikuwa na nabii wa Mwenyezi Mungu aliyeitwa Odedi; akaondoka ili kukutana na jeshi liliporejea Samaria. Akawaambia, “Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, aliwatia mikononi mwenu. Lakini mmewachinja kwa hasira ambayo imefika hadi mbinguni. \v 10 Nanyi sasa mnakusudia kuwafanya wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu watumwa wenu. Lakini ninyi je, hamna pia hatia ya dhambi mliyotenda dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu? \v 11 Basi nisikilizeni! Mkawarudishe mateka mliowachukua kutoka kwa ndugu zenu, kwa kuwa hasira kali ya Mwenyezi Mungu iko juu yenu.” \p \v 12 Ndipo baadhi ya viongozi katika Efraimu, yaani Azaria mwana wa Yehohanani, Berekia mwana wa Meshilemothi, Yehizkia mwana wa Shalumu na Amasa mwana wa Hadlai, wakawapinga wale waliokuwa wakitoka vitani. \v 13 Wakamwambia, “Hamna ruhusa kuwaleta hao wafungwa hapa, ama sivyo tutakuwa na hatia mbele za Mwenyezi Mungu. Je, mnataka kuongezea dhambi yetu na hatia yetu? Kwa sababu hatia yetu tayari ni kubwa, nayo hasira kali ya Mwenyezi Mungu iko juu ya Israeli.” \p \v 14 Hivyo wale askari wakawaacha wale mateka pamoja na nyara mbele ya hao maafisa na kusanyiko lote. \v 15 Kisha watu waliotajwa kwa majina wakawachukua wale mateka, na kutoka zile nyara wakachukua mavazi, wakawavika wale wafungwa wote waliokuwa uchi. Wakawapatia nguo na viatu, chakula na cha kunywa, wakawapa matibabu, wote waliokuwa dhaifu miongoni mwao wakawapandisha juu ya punda, wakawaleta ndugu zao Yeriko, ndio Mji wa Mitende, kisha wakarudi Samaria. \s1 Waashuru wakataa kusaidia Yuda \r (2 Wafalme 16:7-9) \p \v 16 Wakati ule, Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru kuomba msaada. \v 17 Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuwashambulia Yuda na kuchukua mateka. \v 18 Pia Wafilisti walikuwa wameshambulia miji iliyokuwa chini ya vilima na katika miji ya Negebu ya Yuda. Wakatwaa Beth-Shemeshi, Aiyaloni, Gederothi, Soko pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake, Gimzo pia pamoja na vijiji vyake, wakaishi humo. \v 19 Mwenyezi Mungu aliishusha Yuda kwa sababu ya Ahazi mfalme wa Israeli, kwa kuwa alikuwa ameongeza uovu katika Yuda na kumkosea Mwenyezi Mungu mno. \v 20 Hivyo Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru akaja kumtesa badala ya kumsaidia. \v 21 Ahazi akachukua baadhi ya vitu kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu, jumba la kifalme na kutoka kwa wakuu wake na kumpa mfalme wa Ashuru kama ushuru, lakini hilo halikumsaidia. \p \v 22 Katika wakati wake wa mateso Mfalme Ahazi akazidi kukosa uaminifu kwa Mwenyezi Mungu. \v 23 Akatoa sadaka kwa miungu ya Dameski, waliokuwa wamemshinda, kwa kuwa aliwaza, “Kwa kuwa miungu ya mfalme wa Aramu imewasaidia wao, nitaitolea dhabihu ili inisaidie.” Lakini haya ndio yaliyokuwa maangamizi yake na Waisraeli wote. \p \v 24 Ahazi akakusanya vyombo vya nyumba ya Mungu na kuvivunja vipande vipande. Akafunga milango ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na kusimamisha madhabahu katika kila njia panda ya barabara za Yerusalemu. \v 25 Katika kila mji wa Yuda akajenga mahali pa juu pa kuabudia ili kuitolea miungu mingine sadaka za kuteketezwa na kuchochea hasira ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake. \p \v 26 Matukio mengine ya utawala wake na njia zake nyingine zote, kuanzia mwanzo hadi mwisho, zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. \v 27 Ahazi akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Naye Hezekia mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 29 \s1 Hezekia mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 18:1-12) \p \v 1 Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. \v 2 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Daudi baba yake alivyofanya. \p \v 3 Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wake, alifungua milango ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuikarabati. \v 4 Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki \v 5 na kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkalitakase Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu. \v 6 Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Mwenyezi Mungu wakamgeuzia visogo vyao. \v 7 Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli. \v 8 Kwa hiyo, hasira ya Mwenyezi Mungu ikashuka juu ya Yuda na Yerusalemu, naye akawa amewafanya kitu cha kutisha, cha kushangaza na kitu cha kufanyia mzaha kama mnavyoona kwa macho yenu wenyewe. \v 9 Hii ndiyo sababu baba zetu wameanguka kwa upanga na ndiyo sababu wana wetu wa kiume na wa kike, na pia wake zetu wamekuwa mateka. \v 10 Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kufanya agano na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi. \v 11 Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.” \b \lh \v 12 Ndipo Walawi wafuatao wakaanza kazi: \b \li1 Kutoka kwa Wakohathi, \li2 Mahathi mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria; \li1 kutoka kwa Wamerari, \li2 Kishi mwana wa Abdi na Azaria mwana wa Yahaleleli; \li1 kutoka kwa Wagershoni, \li2 Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa; \li1 \v 13 kutoka kwa wana wa Elisafani, \li2 Shimri na Yeieli; \li1 kutoka kwa wana wa Asafu, \li2 Zekaria na Matania; \li1 \v 14 kutoka kwa wana wa Hemani, \li2 Yehieli na Shimei; \li1 kutoka kwa wana wa Yeduthuni, \li2 Shemaya na Uzieli. \b \p \v 15 Walipomaliza kuwakusanya ndugu zao na kujiweka wakfu, wakaingia ndani ili kutakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu, kama vile mfalme alivyokuwa ameagiza, kwa kufuata neno la Mwenyezi Mungu. \v 16 Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la Mwenyezi Mungu ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni. \v 17 Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa Mwenyezi Mungu. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu lenyewe, wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza. \p \v 18 Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu la Mwenyezi Mungu lote, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote. \v 19 Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu.” \s1 Ibada Hekaluni yarejeshwa \p \v 20 Ndipo Mfalme Hezekia akainuka asubuhi na mapema, akakusanya maafisa wa mji wakakwea hekaluni mwa Mwenyezi Mungu. \v 21 Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na beberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Haruni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya Mwenyezi Mungu. \v 22 Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu. \v 23 Wale beberu waliokuwa kwa ajili ya sadaka ya dhambi wakaletwa mbele ya mfalme na kusanyiko nao wakaweka mikono yao juu hao beberu. \v 24 Ndipo makuhani wakawachinja hao beberu na kuweka damu yao kwenye madhabahu kwa ajili ya sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa sababu mfalme alikuwa ameamuru hiyo sadaka ya kuteketezwa na hiyo sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli wote. \p \v 25 Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na Mwenyezi Mungu kupitia manabii wake. \v 26 Hivyo Walawi wakasimama tayari wakiwa na ala za uimbaji za Daudi na makuhani walikuwa na tarumbeta zao. \p \v 27 Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia Mwenyezi Mungu pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli. \v 28 Kusanyiko lote kusujudu katika kuabudu, huku waimbaji wakiimba na wenye tarumbeta wakipiga tarumbeta zao. Yote haya yaliendelea hadi walipomaliza kutoa ile dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa. \p \v 29 Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na kila mtu aliyekuwa pamoja naye wakapiga magoti na kuabudu. \v 30 Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu Mwenyezi Mungu kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha, nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu. \p \v 31 Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu. Njooni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa Mwenyezi Mungu.” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa. \p \v 32 Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo dume mia mbili. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu. \v 33 Wanyama waliowekwa wakfu kwa sadaka ya kuteketezwa walikuwa mafahali mia sita, pamoja na kondoo na mbuzi elfu tatu. \v 34 Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuweza kuchuna wale wanyama wote wa sadaka za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao Walawi wakawasaidia hadi kazi ile ikakamilika na hadi makuhani wengine walipowekwa wakfu, kwa kuwa Walawi walikuwa makini kujiweka wakfu kuliko makuhani. \v 35 Kulikuwa na sadaka nyingi za kuteketezwa, pamoja na mafuta ya wanyama ya sadaka za amani na sadaka za kinywaji ambazo ziliambatana na sadaka za kuteketezwa. \p Kwa hiyo huduma ya Hekalu la Mwenyezi Mungu ikarudishwa kwa upya. \v 36 Hezekia pamoja na watu wote wakafurahi kwa sababu ya lile Mungu alilolifanya kwa ajili ya watu wake, kwa kuwa lilitendeka papo hapo. \c 30 \s1 Hezekia aadhimisha Pasaka \p \v 1 Hezekia akatuma ujumbe kuwaita Israeli wote na Yuda, pia akaandika barua kwa Efraimu na Manase, kuwakaribisha ili waje hekaluni mwa Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu kuadhimisha Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 2 Mfalme na maafisa wake pamoja na kusanyiko lote katika Yerusalemu waliamua kuadhimisha Pasaka katika mwezi wa pili. \v 3 Kwa sababu makuhani hawakuwa wamejitakasa ya kutosha na watu wakawa hawajakusanyika huko Yerusalemu, hawakuwa wameweza kuadhimisha Pasaka kwa wakati wake wa kawaida. \v 4 Mpango huu ukaonekana wafaa kwa mfalme na kusanyiko lote. \v 5 Wakaamua kupeleka tangazo Israeli kote, kuanzia Beer-Sheba hadi Dani, wakiwaita watu waje Yerusalemu kuadhimisha Pasaka ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Ilikuwa haijaadhimishwa na idadi kubwa ya watu kama hiyo kufuatana na yale yaliyokuwa yameandikwa. \p \v 6 Kwa amri ya mfalme, matarishi wakazunguka Israeli na Yuda kote wakiwa na barua kutoka kwa mfalme na kutoka kwa maafisa wake, zilizoandikwa: \pm “Watu wa Israeli, mrudieni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Israeli, ili naye awarudie ninyi mliosalia, mlionusurika kutoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru. \v 7 Msiwe kama baba zenu na ndugu zenu, ambao hawakuwa waaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, hivyo akawafanya kitu cha kutisha, kama mnavyoona. \v 8 Msiwe na shingo ngumu, kama baba zenu walivyokuwa, bali nyenyekeeni kwa Mwenyezi Mungu. Njooni mahali patakatifu, alipopatakasa milele. Mtumikieni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nanyi. \v 9 Mkimrudia Mwenyezi Mungu, ndipo wale ndugu zenu waliotekwa pamoja na watoto wenu watakapoonewa huruma na wale waliowateka na kuwaachia warudi katika nchi hii, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni mwenye neema na huruma, hatageuzia uso wake mbali nanyi kama mkimrudia yeye.” \p \v 10 Matarishi wakaenda mji hadi mji katika Efraimu na Manase, wakafika Zabuloni, lakini watu wakawadharau na kuwadhihaki. \v 11 Lakini, baadhi ya watu wa Asheri, Manase na Zabuloni, wakajinyenyekeza wakaja Yerusalemu. \v 12 Pia katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa juu ya watu kuwapa umoja katika kutenda yale ambayo mfalme na maafisa wake waliwaamuru, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu. \p \v 13 Basi umati mkubwa wa watu wakakusanyika huko Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu katika mwezi wa pili. \v 14 Wakajitia kazini kuyaondoa yale madhabahu yaliyokuwa huko Yerusalemu, wakayaondoa pia yale madhabahu ya kufukizia uvumba kwa miungu na kuyatupa Bonde la Kidroni. \p \v 15 Kisha wakamchinja mwana-kondoo wa Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketezwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 16 Kisha wakachukua nafasi zao za kawaida kama ilivyoelezwa katika Torati ya Musa mtu wa Mungu. Makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa na Walawi. \v 17 Kwa kuwa wengi waliokuwa katika lile kusanyiko walikuwa hawajajitakasa, iliwapasa Walawi wachinje wana-kondoo wengine wa Pasaka kwa ajili ya wale watu ambao hawakuwa wametakaswa, ili kuwatakasa kwa Mwenyezi Mungu. \v 18 Ingawa watu wengi miongoni mwa wale waliotoka Efraimu, Manase, Isakari na Zabuloni walikuwa hawajajitakasa, hata hivyo walikula Pasaka kinyume na ilivyoandikwa. Lakini Hezekia akawaombea, akisema, “Mwenyezi Mungu, ambaye ni mwema na amsamehe kila mmoja \v 19 ambaye anauelekeza moyo wake kumtafuta Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake, hata kama yeye si safi kulingana na sheria za mahali patakatifu.” \v 20 Naye Mwenyezi Mungu akamsikia Hezekia akawaponya watu. \p \v 21 Waisraeli waliokuwa Yerusalemu wakaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa muda wa siku saba, nao Walawi na makuhani walikuwa wakiimba kila siku, wakiwa na ala za uimbaji za kumsifu Mwenyezi Mungu. \p \v 22 Hezekia akazungumza akiwatia moyo Walawi wote, ambao walionesha ustadi katika kumtumikia Mwenyezi Mungu. Hivyo watu wakala chakula cha sikukuu kwa siku saba, wakitoa sadaka za amani na kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. \p \v 23 Kisha kusanyiko lote wakakubali kuendelea na sikukuu kwa siku saba zaidi; kwa hiyo, kwa siku saba nyingine wakaendelea kuiadhimisha kwa furaha. \v 24 Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali elfu moja, kondoo na mbuzi elfu saba kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali elfu moja, pamoja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu. \v 25 Kusanyiko la Yuda, pamoja na makuhani na Walawi, na wote waliokusanyika kutoka Israeli, pamoja na wageni waliotoka Israeli na wale walioishi Yuda, wote wakafurahi. \v 26 Kulikuwa na furaha kubwa katika Yerusalemu, kwa sababu tangu siku za Mfalme Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli halijakuwepo jambo kama hili huko Yerusalemu. \v 27 Ndipo makuhani na Walawi wakasimama wakawabariki watu, naye Mungu akawasikia, kwa sababu maombi yao yalifika mbinguni, makao yake matakatifu. \c 31 \s1 Matoleo kwa ajili ya ibada \p \v 1 Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwa huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini, na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi miji yao wenyewe na kwenye milki zao. \p \v 2 Hezekia akawapanga makuhani na Walawi katika migawanyo, kila mgawanyo kulingana na wajibu wao, kama ni makuhani au Walawi, ili kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kushukuru na kuimba sifa katika malango ya makao ya Mwenyezi Mungu. \v 3 Mfalme akatoa matoleo kutoka mali yake mwenyewe kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na za jioni na sadaka za kuteketezwa kwa siku za Sabato, kwa Sikukuu za Mwezi Mwandamo na kwa ajili ya sikukuu zilizoamriwa kama ilivyoandikwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu. \v 4 Akawaagiza watu wanaoishi Yerusalemu watoe sehemu iliyo haki ya makuhani na Walawi ili waweze kujitoa kikamilifu kutimiza wajibu wao katika Torati ya Mwenyezi Mungu. \v 5 Mara tu baada ya kutolewa tangazo hilo, Waisraeli wakatoa kwa ukarimu malimbuko ya nafaka zao, divai mpya, mafuta na asali pamoja na vyote vilivyotoka mashambani. Wakaleta kiasi kikubwa cha fungu la kumi la kila kitu. \v 6 Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ng’ombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na kuvikusanya katika malundo. \v 7 Wakaanza kufanya haya katika mwezi wa tatu na kumaliza katika mwezi wa saba. \v 8 Hezekia na maafisa wake walipokuja na kuona yale malundo, wakamsifu Mwenyezi Mungu na kuwabariki watu wake Israeli. \p \v 9 Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu yale malundo, \v 10 naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la Mwenyezi Mungu tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu Mwenyezi Mungu amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.” \s1 Kutambuliwa kwa makuhani na Walawi \p \v 11 Hezekia akatoa agizo la kutengeneza vyumba vya ghala katika Hekalu la Mwenyezi Mungu nalo hili likafanyika. \v 12 Kisha kwa uaminifu wakaleta sadaka zao, mafungu yao ya kumi na vitu vilivyowekwa wakfu. Konania Mlawi, ndiye alikuwa msimamizi wa vitu hivi na Shimei ndugu yake ndiye alikuwa msaidizi wake. \v 13 Yehieli, Azazia, Nahathi, Asaheli, Yeremothi, Yozabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi na Benaya walikuwa waangalizi chini ya Konania na Shimei ndugu yake, waliokuwa wamewekwa na Mfalme Hezekia na Azaria, afisa msimamizi wa Hekalu la Mungu. \p \v 14 Kore mwana wa Imna, Mlawi, bawabu wa Lango la Mashariki, alikuwa msimamizi wa sadaka za hiari zilizotolewa kwa Mungu, akiyagawanya hayo matoleo yaliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu na pia zile sadaka zilizowekwa wakfu. \v 15 Edeni, Miniamini, Yeshua, Shemaya, Amaria na Shekania walimsaidia kwa uaminifu katika miji ya makuhani, wakiwagawia makuhani wenzao kufuatana na migawanyo yao, wazee kwa vijana sawasawa. \p \v 16 Zaidi ya hao wakawagawia wanaume wenye umri wa miaka mitatu au zaidi ambao majina yao yalikuwa kwenye orodha ya vizazi, wale wote ambao wangeingia katika Hekalu la Mwenyezi Mungu ili kufanya kazi zao mbalimbali za kila siku kulingana na wajibu katika mgawanyo wao. \v 17 Kuandikishwa kwa makuhani kulikuwa kwa kufuata chimbuko la nyumba za baba zao na Walawi kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi ilikuwa kufuatana na huduma zao, kwa migawanyo yao. \v 18 Makuhani waliandikishwa pamoja na watoto wao wadogo, wake zao, watoto wao wa kiume na wa kike, jamii yote iliandikishwa kwa kufuata orodha ya vizazi vyao. Kwa kuwa walikuwa waaminifu katika kujitakasa. \p \v 19 Kuhusu makuhani, wazao wa Haruni walioishi kwenye mashamba yaliyozunguka miji yao au katika miji mingine yoyote, watu walitajwa majina ili kumgawia kila mwanaume miongoni mwao na kwa wote waliokuwa katika orodha ya vizazi vya Walawi. \p \v 20 Hivi ndivyo Hezekia alivyofanya katika Yuda yote, akifanya lile lililo jema, sawa na la uaminifu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \v 21 Katika kila kitu alichofanya katika huduma kwenye Hekalu la Mungu na katika kutii sheria na amri, alimtafuta Mungu wake na kufanya kazi kwa moyo wake wote. Naye hivyo akafanikiwa. \c 32 \s1 Senakeribu atishia Yerusalemu \r (2 Wafalme 18:13-37; 19:14-19, 35-37; Isaya 36:1-22; 37:8-38) \p \v 1 Baada ya yale yote aliyokuwa amefanya Hezekia kwa uaminifu mkubwa, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaja na kuvamia Yuda. Akaizingira miji yenye ngome, akikusudia kuiteka iwe yake. \v 2 Hezekia alipoona kuwa Senakeribu amekuja na kwamba alikusudia kufanya vita juu ya Yerusalemu, \v 3 akafanya shauri na maafisa wake na mashujaa wake juu ya kuzuia maji kutoka chemchemi zilizo nje ya mji, nao wakamsaidia. \v 4 Umati mkubwa wa watu wakakusanyika na kuzuia chemchemi zote na vijito vilivyotiririka katika nchi yote, wakisema: “Kwa nini wafalme wa Ashuru waje na kukuta maji tele?” \v 5 Hezekia akafanya kazi kwa bidii kukarabati sehemu zote zilizokuwa zimebomoka za ukuta na kujenga minara juu yake. Akajenga ukuta mwingine nje ya ule uliokuwako, na kuimarisha Milo\f + \fr 32:5 \fr*\ft Milo maana yake Boma la Ngome.\ft*\f* katika Mji wa Daudi. Akatengeneza pia silaha nyingi na ngao. \p \v 6 Akaweka maafisa wa jeshi juu ya watu, wakawakutanisha mbele yake katika uwanja kwenye lango la mji, naye akawatia moyo kwa maneno haya: \v 7 “Kuweni hodari na wenye moyo mkuu. Msiogope, msifadhaike wala msikate tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na hili jeshi kubwa lililo pamoja naye, kwa kuwa aliye pamoja nasi ni mkuu kuliko aliye pamoja naye. \v 8 Kwake uko mkono wa mwili tu, bali kwetu yuko Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kutusaidia na kutupigania vita vyetu.” Nao watu wakatiwa moyo kutokana na maneno aliyowaambia Hezekia mfalme wa Yuda. \p \v 9 Hatimaye Senakeribu mfalme wa Ashuru na majeshi yake yote walipokuwa wameuzingira Lakishi, akawatuma maafisa wake kwenda Yerusalemu wakiwa na ujumbe huu kwa Hezekia mfalme wa Yuda, na kwa watu wote wa Yuda waliokuwa humo, kusema: \pm \v 10 “Hili ndilo asemalo Senakeribu mfalme wa Ashuru: Je, mmeweka tumaini lenu wapi, hata mnaendelea kukaa katika Yerusalemu, hali mmezingirwa na jeshi? \v 11 Hezekia asemapo, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, atatuokoa kutoka mkononi wa mfalme wa Ashuru,’ anawapotosha ninyi, naye atawaacha mfe kwa njaa na kiu. \v 12 Je, si Hezekia mwenyewe aliyeondoa mahali pa juu pa kuabudia pamoja na madhabahu zake, akiwaambia Yuda wa Yerusalemu, ‘Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu moja na kuteketeza dhabihu juu yake’? \pm \v 13 “Je, hamjui yale mimi na baba zangu tuliyoyafanya kwa mataifa yote ya nchi zingine? Je, miungu ya mataifa hayo iliweza kuokoa nchi zao kutoka mkononi mwangu? \v 14 Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya mataifa haya ambayo baba zangu waliyaangamiza ameweza kuwaokoa watu wake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi Mungu wenu kuwaokoa mkononi mwangu? \v 15 Sasa basi, msikubali Hezekia awadanganye na kuwapotosha namna hii. Msimwamini, kwa kuwa hakuna mungu wa taifa lolote wala wa ufalme wowote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu au mkononi mwa baba zangu. Sembuse huyo mungu wenu atawaokoaje kutoka mkononi mwangu!” \p \v 16 Maafisa wa Senakeribu wakaendelea kunena dhidi ya Bwana Mwenyezi Mungu na dhidi ya mtumishi wake Hezekia. \v 17 Mfalme pia aliandika barua akimtukana Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, na kusema haya dhidi yake: “Kama vile miungu ya mataifa ya nchi nyingine ilivyoshindwa kuwaokoa watu wao mkononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu.” \v 18 Kisha wakawaita kwa Kiebrania watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta ili kuwatisha na kuwatia hofu ili waweze kuuteka mji. \v 19 Wakanena kuhusu Mungu wa Yerusalemu kama vile walivyonena kuhusu miungu ya mataifa mengine ya dunia ambayo ni kazi ya mikono ya wanadamu. \p \v 20 Mfalme Hezekia na nabii Isaya mwana wa Amozi wakalilia mbingu katika maombi kuhusu jambo hili. \v 21 Naye Mwenyezi Mungu akamtuma malaika ambaye aliangamiza wapiganaji wote, na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, mfalme wa Ashuru akarudi nchini mwake kwa aibu. Naye alipoenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake mwenyewe wakamuua kwa upanga. \p \v 22 Hivyo Mwenyezi Mungu akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. Mwenyezi Mungu akawapa amani pande zote. \v 23 Watu wengi wakaleta sadaka Yerusalemu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na zawadi za thamani kwa ajili ya Hezekia mfalme wa Yuda. Tangu hapo na kuendelea, Hezekia aliheshimiwa sana na mataifa yote. \s1 Kiburi cha Hezekia, mafanikio na kifo \r (2 Wafalme 20:1-3, 12-19; Isaya 38:1-3; 39:1-8) \p \v 24 Katika siku hizo, Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Akamwomba Mwenyezi Mungu, ambaye alimjibu na kumpa ishara. \v 25 Lakini moyo wa Hezekia ukajaa majivuno na hakuonesha itikio kwa wema aliotendewa, kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ikawa juu yake na juu ya Yuda na Yerusalemu. \v 26 Ndipo Hezekia akatubu kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, kama walivyofanya watu wa Yerusalemu, kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi Mungu haikuja juu yao katika siku za Hezekia. \p \v 27 Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima, naye akajifanyia hazina kwa ajili ya fedha yake na dhahabu na kwa ajili ya vito vyake vya thamani, vikolezo, ngao na aina zote za vyombo vya thamani. \v 28 Akajenga pia maghala ya kuhifadhi mavuno ya nafaka, divai mpya na mafuta. Akatengeneza mabanda kwa ajili ya aina mbalimbali za mifugo, na mazizi kwa ajili ya kondoo na mbuzi. \v 29 Akajenga vijiji na kujipatia idadi kubwa ya kondoo na mbuzi, pamoja na ng’ombe, kwa kuwa Mungu alikuwa amempa utajiri mwingi sana. \p \v 30 Hezekia ndiye aliziba njia za kutolea maji za chemchemi za juu za Gihoni na kuyaelekeza maji kutiririkia upande wa magharibi wa Mji wa Daudi. Akafanikiwa katika kila kitu alichofanya. \v 31 Lakini wajumbe walipotumwa na watawala wa Babeli kumuuliza kuhusu ishara ambayo ilifanyika nchini, Mungu alimwacha ili kumjaribu na kujua kila kitu kilichokuwa moyoni mwake. \p \v 32 Matukio mengine ya utawala wa Hezekia na matendo yake ya kujitoa kwa moyo yameandikwa katika maono ya nabii Isaya mwana wa Amozi kwenye kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. \v 33 Hezekia akalala na baba zake na akazikwa kwenye kilima mahali yalipo makaburi ya wazao wa Daudi. Yuda wote na watu wa Yerusalemu wakamheshimu alipofariki. Naye Manase mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 33 \s1 Manase mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 21:1-18) \p \v 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na tano. \v 2 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli. \v 3 Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akayasujudia majeshi yote ya angani na kuyaabudu. \v 4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu ambamo Mwenyezi Mungu alikuwa amesema, “Jina langu litadumu Yerusalemu milele.” \v 5 Katika nyua zote mbili za Hekalu la Mwenyezi Mungu akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani. \v 6 Akawatoa kafara watoto wake kwa kuwapitishia motoni katika Bonde la Ben-Hinomu; akafanya ulozi, uaguzi, na uchawi, akatafuta ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa Mwenyezi Mungu, akaichochea hasira yake. \p \v 7 Akachukua ile sanamu aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu la Mungu ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, mji niliouchagua kutoka makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele. \v 8 Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli iondoke tena katika nchi niliyowapa baba zenu, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru kuhusu sheria zote, maagizo na amri zilizotolewa kwa mkono wa Musa.” \v 9 Lakini Manase akawaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu katika upotovu, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliangamiza mbele ya Waisraeli. \p \v 10 Mwenyezi Mungu akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. \v 11 Hivyo Mwenyezi Mungu akaleta juu yao majemadari wa jeshi la mfalme wa Ashuru, ambao walimchukua Manase kwenda kifungoni, wakaweka ndoana katika pua yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli. \v 12 Katika dhiki yake akamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. \v 13 Naye alipomwomba, Mwenyezi Mungu akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza dua lake. Kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu. \p \v 14 Baadaye akajenga ukuta wa nje wa Mji wa Daudi, magharibi mwa chemchemi ya Gihoni katika bonde, hadi kufikia ingilio la Lango la Samaki na akakizunguka kilima cha Ofeli; pia akaufanya mrefu zaidi. Akawaweka majemadari katika miji yote ya Yuda iliyokuwa imejengewa ngome. \p \v 15 Akaondolea mbali miungu ya kigeni pamoja na sanamu kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Pia akaondoa madhabahu zote alizojenga katika kilima kilichojengwa Hekalu, na katika Yerusalemu, akazitupa nje ya mji. \v 16 Kisha akarudisha madhabahu ya Mwenyezi Mungu na kutolea juu yake dhabihu za sadaka za amani pamoja na sadaka za shukrani, naye akawaamuru Yuda wamtumikie Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 17 Hata hivyo watu wakaendelea kutoa dhabihu mahali pa juu pa kuabudia, lakini wakawa wakimtolea Mwenyezi Mungu, Mungu wao, peke yake. \p \v 18 Matukio mengine ya utawala wa Manase, maombi yake kwa Mungu wake na maneno aliyoambiwa na waonaji walionena naye kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. \v 19 Maombi yake, pamoja na jinsi Mungu alivyoguswa na kusihi kwake, pia dhambi zake zote na kukosa uaminifu kwake, pamoja na sehemu alizojenga mahali pa juu pa kuabudia, na kusimamisha nguzo za Ashera na sanamu kabla ya kujinyenyekeza kwake: haya yote yameandikwa katika kumbukumbu za waonaji. \v 20 Manase akalala na baba zake, akazikwa katika jumba lake la kifalme. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Amoni mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 21:19-26) \p \v 21 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. \v 22 Akatenda maovu machoni mwa Mwenyezi Mungu, kama baba yake Manase alivyofanya. Amoni akaabudu na kutoa dhabihu kwa sanamu zote alizokuwa ametengeneza Manase. \v 23 Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu, badala yake Amoni alijiongeza hatia zaidi. \p \v 24 Watumishi wa Amoni wakampangia njama, nao wakamuua ndani ya jumba lake la kifalme. \v 25 Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamepanga njama dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake. \c 34 \s1 Yosia afanya matengenezo \r (2 Wafalme 22:1-2) \p \v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka nane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na moja. \v 2 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu na kuenenda katika njia za Daudi baba yake, hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto. \p \v 3 Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kutakasa mahali pa juu pa kuabudia pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga, na sanamu za kusubu. \v 4 Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kutawanya juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea sadaka. \v 5 Akachoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao na kwa njia hiyo akaitakasa Yuda na Yerusalemu. \v 6 Katika miji ya Manase, Efraimu na Simeoni, hadi Naftali na kwenye magofu yanayoizunguka, \v 7 akavunja madhabahu na nguzo za Ashera na kuzipondaponda hizo sanamu hadi zikawa unga na kukata vipande vipande madhabahu zote za kufukizia uvumba katika nchi ya Israeli yote. Kisha akarudi Yerusalemu. \p \v 8 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yosia, ili kutakasa nchi na Hekalu, akawatuma Shafani, mwana wa Azalia na Maaseya mtawala wa mji, pamoja na Yoa mwana wa Yoahazi, mwandishi ili kukarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \p \v 9 Wakamwendea Hilkia kuhani mkuu na kumpa fedha ambazo zilikuwa zimeletwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu ambazo Walawi waliokuwa mabawabu walikuwa wamezikusanya kutoka kwa watu wa Manase, Efraimu na mabaki wote wa Israeli kutoka kwa watu wote wa Yuda na Benyamini na wakazi wa Yerusalemu. \v 10 Kisha wakazikabidhi hizo fedha kwa watu waliowekwa ili kusimamia kazi ya Hekalu la Mwenyezi Mungu. Hawa watu waliwalipa wafanyakazi waliokarabati na kutengeneza Hekalu lipate kurudi katika hali yake. \v 11 Wakawapa pia mafundi seremala na waashi fedha ili kununua mawe yaliyochongwa, mbao kwa ajili ya kufungia na boriti kwa ajili ya majengo ambayo wafalme wa Yuda walikuwa wameyaacha yakawa magofu. \p \v 12 Watu wakafanya kazi kwa uaminifu. Waliokuwa wamewekwa juu yao ili kuwaelekeza ni Yahathi na Obadia, Walawi wa uzao wa Merari, Zekaria na Meshulamu, waliotoka kwenye uzao wa Kohathi. Walawi wote wenye ujuzi wa kupiga ala za uimbaji, \v 13 wakawa wasimamizi wa vibarua na kuwaongoza wale waliofanya kila aina ya kazi. Baadhi ya Walawi walikuwa waandishi, maafisa na mabawabu. \s1 Kitabu cha Torati chapatikana \r (2 Wafalme 22:3-20) \p \v 14 Wakati walikuwa wakizitoa nje fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu, kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu kilichokuwa kimetolewa kwa mkono wa Musa. \v 15 Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.” Akampa Shafani kile Kitabu. \p \v 16 Kisha Shafani akakipeleka kile Kitabu kwa mfalme na kumwambia, “Maafisa wako wanafanya kila kitu kama walivyokabidhiwa kufanya. \v 17 Wamelipa fedha zilizokuwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu na wamewakabidhi wasimamizi na wafanyakazi.” \v 18 Kisha Shafani mwandishi akamwarifu mfalme kuwa, “Kuhani Hilkia amenipa Kitabu.” Naye Shafani akakisoma mbele ya mfalme. \p \v 19 Mfalme aliposikia yale maneno ya Torati, akayararua mavazi yake. \v 20 Akatoa maagizo haya kwa Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwandishi na Asaya mtumishi wa mfalme, \v 21 “Nendeni mkamuulize Mwenyezi Mungu kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki waliosalia katika Israeli na Yuda, kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Mwenyezi Mungu iliyomwagwa juu yetu ni kubwa mno kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la Mwenyezi Mungu wala hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.” \p \v 22 Hilkia pamoja na wale wote mfalme aliokuwa amewatuma pamoja naye wakaenda kuzungumza na nabii mke aitwaye Hulda, aliyekuwa mke wa Shalumu mwana wa Tokhathi, mwana wa Hasra mtunzaji wa chumba cha mavazi. Hulda aliishi Yerusalemu, katika Mtaa wa Pili. \p \v 23 Akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Mwambieni yule mtu aliyewatuma ninyi kwangu, \v 24 ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Nitaleta maafa mahali hapa na kwa watu wake: laana zote zilizoandikwa ndani ya kitabu hicho, ambazo zimesomwa mbele ya mfalme wa Yuda. \v 25 Kwa sababu wameniacha na kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kunighadhibisha kwa kazi yote ya mikono yao, hivyo hasira yangu itamwagwa mahali hapa, wala haitatulizwa.’ \v 26 Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza Mwenyezi Mungu, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kuhusu maneno uliyoyasikia: \v 27 Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu na uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Mwenyezi Mungu. \v 28 Basi nitakukusanya kwa baba zako, nawe utazikwa kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote nitakayoleta juu ya mahali hapa na juu ya wote wanaoishi hapa.’ ” \p Kwa hiyo wakampelekea mfalme jibu lake. \s1 Yosia afanya agano la kutii \r (2 Wafalme 23:1-20) \p \v 29 Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu. \v 30 Akapanda kwenda hekaluni mwa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na Walawi, watu wote, wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, kilichokuwa kimepatikana katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 31 Mfalme akasimama karibu na nguzo yake na kufanya upya agano mbele za Mwenyezi Mungu kwamba atamfuata Mwenyezi Mungu na kuzishika amri zake, maagizo na sheria zake kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, ili kuyatii maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. \p \v 32 Ndipo akamtaka kila mmoja katika Yerusalemu na Benyamini kuweka ahadi zao wenyewe kwa hilo agano, watu wa Yerusalemu wakafanya hivyo kwa kufuata agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. \p \v 33 Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka nchi yote ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuwa katika Israeli wamtumikie Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao. \c 35 \s1 Yosia aadhimisha Pasaka \r (2 Wafalme 23:21-23) \p \v 1 Yosia akaadhimisha Pasaka kwa Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu, mwana-kondoo wa Pasaka akachinjwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. \v 2 Akawaweka makuhani kwenye wajibu wao na kuwatia moyo katika utumishi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 3 Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na waliokuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi ya Mwenyezi Mungu, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa mabegani mwenu. Sasa mtumikieni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na watu wake Israeli. \v 4 Jiandaeni kwa kufuata jamaa zenu katika migawanyo yenu, kufuatana na maelezo yaliyoandikwa na Daudi mfalme wa Israeli na mwanawe Sulemani. \p \v 5 “Simameni mahali patakatifu kwa kufuata migawanyo ya jamaa za baba zenu kulingana na koo zenu na pawepo Walawi kwa ajili ya kila mgawanyo wa nyumba ya baba zenu. \v 6 Chinjeni mwana-kondoo wa Pasaka, jitakaseni, nanyi kwa niaba ya koo zenu fanyeni maandalizi, mkitenda sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu kwa mkono wa Musa.” \p \v 7 Ndipo Yosia akawapa watu wote waliokuwepo wana-mbuzi na kondoo wapatao elfu thelathini kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng’ombe elfu kumi; wote kutoka kwa mali binafsi ya mfalme. \p \v 8 Pia maafisa wake, wakatoa kwa hiari yao wakawapa watu, makuhani na Walawi. Hilkia, Zekaria na Yehieli, waliokuwa maafisa wakuu wa Hekalu la Mungu, wakawapa makuhani sadaka za Pasaka wana-kondoo na wana-mbuzi elfu mbili na mia sita, na mafahali mia tatu. \v 9 Konania na nduguze wawili, Shemaya na Nethaneli, pamoja na Hashabia, Yeieli na Yozabadi waliokuwa viongozi wa Walawi, nao pia wakawapa Walawi wana-kondoo na wana-mbuzi elfu tano, na mafahali mia tano, kwa ajili ya sadaka za Pasaka. \p \v 10 Huduma ilipomalizika kuandaliwa makuhani wakasimama mahali pao na Walawi katika migawanyo yao kama mfalme alivyokuwa ameamuru. \v 11 Wana-kondoo wa Pasaka wakachinjwa, nao makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa, wakati Walawi wakiwa wanawachuna wale wanyama ngozi. \v 12 Wakatenga sadaka za kuteketezwa ili waweze kugawia ili migawanyo kwa kufuata jamaa za baba zao ili watoe sadaka kwa Mwenyezi Mungu kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vivyo hivyo kwa wale mafahali. \v 13 Wakawaoka wale wanyama wa Pasaka kwenye moto kama ilivyoamriwa, wakachemsha zile sadaka takatifu kwenye vyungu, masufuria makubwa na vikaango na kuwagawia watu wote upesi. \v 14 Hatimaye wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu wale makuhani, yaani wazao wa Haruni, walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa pamoja na zile sehemu zilizonona hadi usiku. Hivyo Walawi wakafanya maandalizi kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani wa uzao wa Haruni. \p \v 15 Waimbaji, wazao wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagizwa na Mfalme Daudi, Asafu, Hemani na Yeduthuni mwonaji wa Mfalme. Mabawabu katika kila lango hawakuhitaji kuacha nafasi zao kwa sababu Walawi wenzao walifanya maandalizi kwa ajili yao. \p \v 16 Kwa hiyo wakati ule, huduma yote ya Mwenyezi Mungu ilifanyika katika kuadhimisha Pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, kama alivyoamuru Mfalme Yosia. \v 17 Waisraeli waliokuwepo wakaadhimisha Pasaka wakati huo na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa siku saba. \v 18 Kulikuwa hakujafanyika Pasaka kama hii katika Israeli tangu siku za nabii Samweli wala hakukuwa na mfalme yeyote wa Israeli ambaye kamwe alishaadhimisha Pasaka kama ile aliyofanya Mfalme Yosia, akiwa na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na wa Israeli waliokuwa huko, pamoja na wakaaji wa Yerusalemu. \v 19 Pasaka iliadhimishwa katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia. \s1 Kifo cha Yosia \r (2 Wafalme 23:28-30) \p \v 20 Baada ya haya yote, Yosia alipomaliza kulitengeneza vizuri Hekalu, Neko mfalme wa Misri akapanda ili kupigana huko Karkemishi katika Mto Frati, naye Yosia akatoka kwenda kupigana naye. \v 21 Lakini Neko akamtumia wajumbe kusema, “Kuna ugomvi gani kati yangu mimi na wewe, ee mfalme wa Yuda? Si wewe ninayekushambulia wakati huu, bali ile nyumba niliyo na vita nayo, Mungu ameniambia niharakishe, kwa hivyo acha kumpinga Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.” \p \v 22 Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alienda kupigana naye katika tambarare ya Megido. \p \v 23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, naye akawaambia maafisa wake, “Niondoeni, nimejeruhiwa vibaya sana.” \v 24 Kwa hiyo wakamshusha kutoka gari lake la vita, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea Yosia. \p \v 25 Nabii Yeremia akatunga maombolezo kwa ajili ya kifo chake, nao waimbaji wote, wanaume kwa wanawake, hufanya ukumbusho wa Yosia katika maombolezo hadi leo. Haya yakafanywa desturi katika Israeli, nayo yameandikwa katika Maombolezo. \p \v 26 Matukio mengine ya utawala wa Yosia na matendo yake mema, kulingana na yale yaliyoandikwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu: \v 27 matukio yote, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. \c 36 \s1 Yehoahazi mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 23:30-35) \p \v 1 Watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia na kumfanya mfalme mahali pa baba yake huko Yerusalemu. \p \v 2 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu kwa miezi mitatu. \v 3 Mfalme wa Misri akamwondoa madarakani huko Yerusalemu, na akatoza Yuda kodi ya talanta mia moja\f + \fr 36:3 \fr*\ft Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.\ft*\f* za fedha, na talanta moja\f + \fr 36:3 \fr*\ft Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.\ft*\f* ya dhahabu. \v 4 Mfalme wa Misri akamweka Eliakimu, nduguye Yehoahazi, kuwa mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu na kubadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini Neko akamchukua Yehoahazi, nduguye Eliakimu, akampeleka Misri. \s1 Yehoyakimu mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 23:35–24:7) \p \v 5 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na moja. Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wake. \v 6 Nebukadneza mfalme wa Babeli akamshambulia na kumfunga kwa pingu za shaba akampeleka Babeli. \v 7 Nebukadneza akachukua pia vyombo kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu na kuviweka katika hekalu lake\f + \fr 36:7 \fr*\ft au: katika jumba lake la kifalme.\ft*\f* huko Babeli. \p \v 8 Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu, machukizo aliyoyafanya na yote yaliyoonekana dhidi yake, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Yehoyakini mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 24:8-17) \p \v 9 Yehoyakini alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi. Akafanya yaliyo maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. \v 10 Majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu, nao wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Naye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu. \s1 Sedekia mfalme wa Yuda \r (2 Wafalme 24:18-20; Yeremia 52:1-3) \p \v 11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na moja. \v 12 Alifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la Mwenyezi Mungu. \v 13 Pia alimwasi Mfalme Nebukadneza, aliyekuwa amemwapisha kwa jina la Mungu. Akashupaza shingo na akafanya moyo wake kuwa mgumu wala hakutaka kumgeukia Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 14 Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu la Mwenyezi Mungu alilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu. \s1 Kuanguka kwa Yerusalemu \r (2 Wafalme 25:1-21; Yeremia 52:3-11) \p \v 15 Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, akawapelekea neno kupitia wajumbe wake tena na tena, kwa sababu alikuwa anawahurumia watu wake pamoja na mahali pa Maskani yake. \v 16 Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mwenyezi Mungu wakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake hadi ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ikawa kubwa dhidi ya watu wake, na hakukuwa na namna ya kuituliza. \v 17 Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu. Hakumbakiza kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza. \v 18 Akavichukua kwenda Babeli vyombo vyote kutoka Hekalu la Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu pamoja na hazina za mfalme na za maafisa wake. \v 19 Wakalichoma Hekalu la Mungu na kuzibomoa kuta za Yerusalemu, wakachoma moto majumba yote ya kifalme na kuharibu kila kitu chake cha thamani. \p \v 20 Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli. Nao wakawa watumishi wake na wa wanawe hadi wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi ulifika. \v 21 Nchi ikaendelea kufurahia pumziko zake za sabato; wakati wote wa kufanywa kwake ukiwa ilipumzika, hadi ile miaka sabini ilipotimia katika kutimiza neno la Mwenyezi Mungu lililonenwa na Yeremia. \s1 Koreshi aruhusu watu kurudi Yerusalemu \r (Ezra 1:1-4) \p \v 22 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na nabii Yeremia, Mwenyezi Mungu aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi: \pmo \v 23 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi: \pm “ ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Yeyote kati ya watu wa Mungu miongoni mwenu, Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na awe pamoja naye, wacha apande.’ ”