\id 1TH - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 1 Wathesalonike \toc1 1 Wathesalonike \toc2 1 Wathesalonike \toc3 1The \mt1 1 Wathesalonike \c 1 \s1 Salamu \po \v 1 Paulo, Silvano\f + \fr 1:1 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Sila\fqa*\f* na Timotheo. \po Kwa kundi la waumini la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu, Baba\f + \fr 1:1 \fr*\ft Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi.\ft*\f* yetu, na ndani ya Bwana wetu Isa Al-Masihi. \po Neema iwe kwenu na amani. \s1 Shukrani kwa ajili ya imani ya Wathesalonike \p \v 2 Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima. \v 3 Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Isa Al-Masihi. \p \v 4 Ndugu zetu mnaopendwa na Mungu, kwa kuwa tunajua kwamba Mungu amewachagua, \v 5 kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho wa Mungu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda kati yenu kwa ajili yenu. \v 6 Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana Isa, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho wa Mungu. \v 7 Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya. \v 8 Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana Isa limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali, kiasi kwamba hatuna haja ya kusema chochote juu yake. \v 9 Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli, \v 10 na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani Isa, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja. \c 2 \s1 Huduma ya Paulo huko Thesalonike \p \v 1 Ndugu zangu, kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua kwamba kuja kwetu kwenu hakukuwa bure, \v 2 kama vile mjuavyo, tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu wetu, tulikuwa na ujasiri wa kuwaambia Injili ya Mungu ingawa kulikuwa na upinzani mkubwa. \v 3 Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu. \v 4 Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. \v 5 Kama mnavyojua, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya; Mungu ndiye shahidi yetu. \v 6 Hatukuwa tukitafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine yeyote, ingawa kama mitume wa Al-Masihi tungeweza kuwa mzigo kwenu. \v 7 Lakini tulikuwa wapole kati yenu, kama vile mama anawatunza watoto wake wadogo. \v 8 Tuliwapenda sana, kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu. \v 9 Ndugu zetu, mnakumbuka juhudi yetu na taabu yetu. Tulifanya kazi usiku na mchana, ili tusiwe mzigo kwa mtu yeyote tulipokuwa tukiwahubiria Injili ya Mungu. \p \v 10 Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini. \v 11 Maana mnajua kwamba tuliwatendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake. \v 12 Tuliwatia moyo, tukiwafariji na kuwahimiza kuishi maisha yanayompendeza Mungu, anayewaita katika ufalme wake na utukufu wake. \p \v 13 Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, linalotenda kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. \v 14 Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlifanyika wafuasi wa makundi ya waumini wa Mungu walio ndani ya Al-Masihi Isa katika Yudea. Mlipata mateso yale yale kutoka kwa watu wenu wenyewe kama vile waumini hao walivyoteswa na Wayahudi, \v 15 wale waliomuua Bwana Isa na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote, \v 16 wakijitahidi kutuzuia tusizungumze na watu wa Mataifa ili wapate kuokolewa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao hadi kikomo. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia. \s1 Paulo atamani kuwaona Wathesalonike \p \v 17 Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa muda mfupi (ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu, si kwa moyo), tulizidi kuwa na shauku kubwa kuwaona uso kwa uso. \v 18 Maana tulitaka kuja kwenu, hasa mimi Paulo, nilitaka kuja tena na tena, lakini Shetani akatuzuia. \v 19 Kwa maana tumaini letu ni nini, au furaha yetu, au taji letu la kujisifia mbele za Bwana wetu Isa Al-Masihi wakati wa kuja kwake? Je, si ni ninyi? \v 20 Naam, ninyi ndio fahari yetu na furaha yetu. \c 3 \s1 Timotheo atumwa Thesalonike \p \v 1 Kwa hivyo tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliamua tubaki Athene peke yetu. \v 2 Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi mwenzetu wa Mungu katika kuieneza Injili ya Al-Masihi, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo katika imani yenu, \v 3 ili mtu yeyote asifadhaishwe na mateso haya. Mnajua vyema kwamba tumewekewa hayo mateso. \v 4 Kwa kweli, tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa na imekuwa hivyo kama mnavyojua. \v 5 Kwa sababu hii niliposhindwa kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure. \s1 Taarifa ya Timotheo ya kutia moyo \p \v 6 Lakini Timotheo amerejea kwetu hivi sasa kutoka kwenu, na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema, na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi. \v 7 Kwa hiyo, ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa sababu ya imani yenu. \v 8 Sasa kwa kuwa hakika tunaishi, kwa kuwa ninyi mmesimama imara katika Bwana Isa. \v 9 Je, tutawezaje kumshukuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu? \v 10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tupate kuwaona tena na kujaza kile kilichopungua katika imani yenu. \p \v 11 Basi Mungu wetu na Baba yetu mwenyewe na Bwana wetu Isa atengeneze njia ya sisi kuja kwenu. \v 12 Bwana Isa na auongeze upendo wenu na kuuzidisha kati yenu na kwa wengine wote, kama vile tulivyo na upendo mwingi kwenu. \v 13 Tunamwomba Mungu aimarishe mioyo yenu ili msiwe na lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu aliye Baba yetu wakati wa kuja kwake Bwana wetu Isa pamoja na watakatifu wote. \c 4 \s1 Maisha yanayompendeza Mwenyezi Mungu \p \v 1 Na kuhusu mambo mengine, ndugu, tuliwafundisha jinsi ya kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi. Sasa tunawaomba na kuwasihi katika Bwana Isa mfanye hivi zaidi na zaidi. \v 2 Kwa kuwa mnajua maagizo tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Isa. \p \v 3 Mapenzi ya Mungu ni ninyi mtakaswe, ili mjiepushe na uasherati, \v 4 na kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, \v 5 bali si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. \v 6 Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali. \v 7 Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu. \v 8 Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu. \p \v 9 Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. \v 10 Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda. \p \v 11 Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza, \v 12 ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote. \s1 Kurudi kwake Bwana Isa \p \v 13 Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala katika mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini. \v 14 Tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka. Na kwa hivyo, tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja naye wale waliolala katika Isa. \v 15 Kulingana na neno la Bwana Isa mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana Isa, hakika hatutawatangulia waliolala katika mauti. \v 16 Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza. \v 17 Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana Isa hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana Isa milele. \v 18 Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya. \c 5 \s1 Kuweni tayari kwa siku ya Bwana \p \v 1 Basi ndugu, hatuna haja ya kuwaandikia kuhusu nyakati na majira, \v 2 kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Mwenyezi Mungu itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. \v 3 Watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile uchungu unavyomjia mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. \p \v 4 Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. \v 5 Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. \v 6 Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine wanavyolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. \v 7 Kwa kuwa wote wanaolala, hulala usiku, na wale wanaolewa, hulewa usiku. \v 8 Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo. \v 9 Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi. \v 10 Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye. \v 11 Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa. \s1 Maagizo ya mwisho, na hitimisho \p \v 12 Sasa tunawaomba, ndugu, waheshimuni wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana Isa na ambao wanawaonya. \v 13 Waheshimuni sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao. Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi. \v 14 Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote. \v 15 Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. \p \v 16 Furahini siku zote; \v 17 ombeni bila kukoma; \v 18 shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndio mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Al-Masihi Isa. \p \v 19 Msiuzime moto wa Roho wa Mungu. \v 20 Msiyadharau maneno ya unabii. \v 21 Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. \v 22 Jiepusheni na uovu wa kila namna. \p \v 23 Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Isa Al-Masihi. \v 24 Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo. \b \b \p \v 25 Ndugu, tuombeeni. \b \p \v 26 Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu. \b \p \v 27 Ninawaagiza mbele za Bwana Isa mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii. \b \p \v 28 Neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi. Amen.