\id 1KI - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures (Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu) \usfm 3.0 \ide UTF-8 \h 1 Wafalme \toc1 1 Wafalme \toc2 1 Wafalme \toc3 1Fal \mt1 1 Wafalme \c 1 \s1 Adoniya ajitangaza mfalme \p \v 1 Mfalme Daudi alipokuwa mzee umri ukiwa umesogea, hakuweza kupata joto hata walipomfunika kwa nguo. \v 2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Turuhusu tumtafute mwanamwali bikira amhudumie mfalme na kumtunza. Anaweza kulala pembeni mwake ili bwana wetu mfalme apate joto.” \p \v 3 Kisha wakatafuta katika Israeli yote ili kumpata msichana mzuri wa sura na wakampata Abishagi Mshunami, wakamleta kwa mfalme. \v 4 Msichana huyo alikuwa mzuri sana wa sura. Akamtunza mfalme na kumhudumia, lakini mfalme hakufanya naye tendo la ndoa. \p \v 5 Basi Adoniya mwana wa Hagithi akajigamba na kusema, “Mimi nitakuwa mfalme.” Hivyo akaweka tayari magari ya vita na wapanda farasi, pamoja na watu hamsini wa kumtangulia wakikimbia. \v 6 (Baba yake hakuwa ameingilia na kumuuliza, “Kwa nini unafanya hivyo?” Alikuwa pia kijana mzuri sana wa sura, na alizaliwa baada ya Absalomu.) \p \v 7 Adoniya akashauriana na Yoabu mwana wa Seruya, na kuhani Abiathari, nao wakamsaidia. \v 8 Lakini kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Nathani, Shimei, Rei na walinzi maalum wa Daudi hawakujiunga na Adoniya. \p \v 9 Ndipo Adoniya akatoa dhabihu ya kondoo, ng’ombe na ndama walionona kwenye Jiwe la Zohelethi karibu na En-Rogeli. Akawaalika ndugu zake wote wana wa mfalme, na wanaume wote wa Yuda waliokuwa maafisa wa mfalme, \v 10 lakini hakumwalika nabii Nathani, wala Benaya, wala walinzi maalum wa mfalme, wala ndugu yake Sulemani. \p \v 11 Ndipo Nathani akamuuliza Bathsheba, mama yake Sulemani, “Je, hujasikia kwamba Adoniya mwana wa Hagithi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili? \v 12 Sasa basi, acha nikushauri jinsi utakavyookoa uhai wako mwenyewe na uhai wa mwanao Sulemani. \v 13 Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: “Hakika mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme”? Kwa nini basi Adoniya amekuwa mfalme?’ \v 14 Utakapokuwa ukizungumza na mfalme, nitaingia na kuthibitisha hayo uliyoyasema.” \p \v 15 Hivyo Bathsheba akaenda kumwona mfalme chumbani mwake, ambapo Abishagi Mshunami alikuwa akimhudumia; naye mfalme alikuwa mzee sana. \v 16 Bathsheba akainama na kusujudu, uso wake ukagusa chini mbele ya mfalme. \p Mfalme akauliza, “Ni nini unachokitaka?” \p \v 17 Akamwambia, “Bwana wangu, wewe mwenyewe uliniapia mimi mtumishi wako kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwamba: ‘Sulemani Mwanao atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme.’ \v 18 Lakini sasa Adoniya amekuwa mfalme, nawe, bwana wangu mfalme huna habari kuhusu jambo hilo. \v 19 Ametoa dhabihu idadi kubwa ya ng’ombe, ndama walionona na kondoo, naye amewaalika wana wa mfalme wote, kuhani Abiathari, na Yoabu jemadari wa jeshi, lakini hakumwalika Sulemani mtumishi wako. \v 20 Bwana wangu mfalme, macho ya Israeli yote yanakutazama wewe wajue kutoka kwako kuwa ni nani atakayeketi kwenye kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake. \v 21 Kama sivyo, mara tu bwana wangu mfalme atakapopumzishwa pamoja na baba zake, mimi na mwanangu Sulemani tutatendewa kama wahalifu.” \p \v 22 Alipokuwa angali anazungumza na mfalme, nabii Nathani akafika. \v 23 Wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa.” Kisha akaenda mbele ya mfalme na kumsujudia hadi uso wake ukagusa chini. \p \v 24 Nathani akasema, “Je, bwana wangu mfalme, umetangaza kuwa Adoniya atakuwa mfalme baada yako na kwamba ataketi kwenye kiti chako cha ufalme? \v 25 Leo ameshuka na kutoa dhabihu idadi kubwa ya ng’ombe, ndama walionona na kondoo. Amewaalika wana wote wa mfalme, jemadari wa jeshi, na kuhani Abiathari. Sasa hivi, wanakula na kunywa pamoja naye wakisema, ‘Aishi maisha marefu, Mfalme Adoniya!’ \v 26 Lakini mimi mtumishi wako, na kuhani Sadoki, Benaya mwana wa Yehoyada, na mtumishi wako Sulemani hakutualika. \v 27 Je, hili ni jambo ambalo bwana wangu mfalme amelifanya pasipo kuwajulisha watumishi wake ili wapate kujua ni nani atakayeketi kwenye kiti cha ufalme cha bwana wangu mfalme baada yake?” \s1 Daudi amteua Sulemani kuwa mfalme \p \v 28 Ndipo Mfalme Daudi akasema, “Mwite Bathsheba, aingie ndani.” Hivyo akaingia mbele ya mfalme na kusimama mbele yake. \p \v 29 Ndipo mfalme akaapa: “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, ambaye ameniokoa kutoka kila taabu, \v 30 hakika nitatekeleza leo kile nilichokuapia kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha ufalme baada yangu.” \p \v 31 Kisha Bathsheba akasujudu, uso wake ukigusa chini mbele ya mfalme, akasema, “Bwana wangu Mfalme Daudi na aishi milele!” \p \v 32 Mfalme Daudi akasema, “Mwite kuhani Sadoki ndani, na nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada.” Walipofika mbele ya mfalme, \v 33 akawaambia: “Wachukueni watumishi wa bwana wenu pamoja nanyi na mkamkalishe mwanangu Sulemani juu ya nyumbu wangu mwenyewe, kisha mkamteremshe hadi Gihoni. \v 34 Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wampake mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, mkisema, ‘Mfalme Sulemani aishi maisha marefu!’ \v 35 Kisha mtapanda pamoja naye, atakuja na kuketi kwenye kiti changu cha ufalme na kutawala baada yangu. Nimemweka atawale juu ya Israeli na Yuda.” \p \v 36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, “Amen! Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu mfalme, na aamuru vivyo hivyo. \v 37 Kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa na bwana wangu mfalme, vivyo hivyo na awe na Sulemani kukifanya kiti chake cha utawala kuwa kikuu kuliko kile cha bwana wangu Mfalme Daudi!” \p \v 38 Hivyo kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi wakaenda na kumpandisha Sulemani juu ya nyumbu wa Mfalme Daudi, nao wakamsindikiza hadi Gihoni. \v 39 Kuhani Sadoki akachukua pembe ya mafuta kutoka hema takatifu na kumtia Sulemani mafuta. Kisha wakapiga tarumbeta na watu wote wakapaza sauti wakisema, “Mfalme Sulemani aishi maisha marefu!” \v 40 Na watu wote wakakwea wakimfuata, huku wakipiga filimbi na kushangilia sana, hata ardhi ikatikisika kwa ile sauti. \p \v 41 Adoniya pamoja na wageni wote waliokuwa pamoja naye wakasikia sauti hiyo walipokuwa wakimalizia karamu yao. Waliposikia sauti ya tarumbeta, Yoabu akauliza, “Nini maana ya makelele haya yote katika mji?” \p \v 42 Hata alipokuwa anaongea, Yonathani mwana wa kuhani Abiathari akafika. Adoniya akasema, “Ingia ndani. Mtu wa maana kama wewe ni lazima awe amelete habari njema.” \p \v 43 Yonathani akamjibu, “La hasha! Mfalme Daudi bwana wetu amemfanya Sulemani kuwa mfalme. \v 44 Mfalme ametuma pamoja naye kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi, nao wamempandisha juu ya nyumbu wa mfalme, \v 45 nao kuhani Sadoki na nabii Nathani wamempaka mafuta huko Gihoni kuwa mfalme. Kutoka hapo wamepanda wakishangilia, na sauti zimeenea kote katika mji. Hizo ndizo kelele unazosikia. \v 46 Zaidi ya hayo, Sulemani ameketi kwenye kiti chake cha ufalme. \v 47 Pia, maafisa wa mfalme wamekuja ili kumpongeza bwana wetu Mfalme Daudi, wakisema, ‘Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa mashuhuri kuliko lako, na kiti chake cha ufalme kiwe na ukuu kuliko chako!’ Naye mfalme akasujudu akiabudu kitandani mwake, \v 48 akasema, ‘Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye ameruhusu macho yangu kuona mrithi kwenye kiti changu cha ufalme leo.’ ” \p \v 49 Waliposikia haya, wageni wote wa Adoniya wakainuka kwa hofu na kutawanyika. \v 50 Lakini Adoniya kwa kumwogopa Sulemani, akaenda na kushika pembe za madhabahu. \v 51 Kisha Sulemani akaambiwa, “Adoniya anamwogopa Mfalme Sulemani na ameshikilia pembe za madhabahu. Anasema, ‘Mfalme Sulemani na aniapie leo kwamba hatamuua mtumishi wake kwa upanga.’ ” \p \v 52 Sulemani akajibu, “Akijionesha kuwa mtu muungwana, hakuna unywele wake utakaoanguka juu ya ardhi; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.” \v 53 Ndipo Mfalme Sulemani akawatuma watu, nao wakamshusha kutoka madhabahuni. Naye Adoniya akaja akamwinamia Mfalme Sulemani, naye Sulemani akamwambia, “Nenda nyumbani mwako.” \c 2 \s1 Maagizo ya Daudi kwa Sulemani \p \v 1 Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa mwanawe Sulemani agizo. \p \v 2 Akasema, “Ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jioneshe kuwa mwanaume, \v 3 shika lile Mwenyezi Mungu, Mungu wako, analokuagiza: Nenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote utakapoenda, \v 4 na ili Mwenyezi Mungu aweze kunitimizia ahadi yake: ‘Kama wazao wako wakiangalia sana wanavyoishi, na wakienenda kwa uaminifu mbele zangu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, kamwe hutakosa kuwa na mtu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli.’ \p \v 5 “Sasa wewe mwenyewe unafahamu lile Yoabu mwana wa Seruya alilonitendea, lile alilofanya kwa majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yetheri. Aliwaua, akimwaga damu yao wakati wa amani kama vile ni kwenye vita, tena akaipaka damu ile kwenye mkanda uliokuwa kiunoni mwake na viatu alivyovaa miguuni mwake. \v 6 Mtendee kwa kadiri ya hekima yako, lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie kaburi kwa amani. \p \v 7 “Lakini uwaoneshe wema wana wa Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe miongoni mwa wale walao mezani pako. Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako Absalomu. \p \v 8 “Ukumbuke, unaye Shimei mwana wa Gera, Mbenyamini kutoka Bahurimu, aliyenilaani kwa laana kali siku niliyoenda Mahanaimu. Aliposhuka kunilaki huko Yordani, nilimwapia kwa Mwenyezi Mungu: ‘Sitakuua kwa upanga!’ \v 9 Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.” \p \v 10 Kisha Daudi akalala na baba zake, naye akazikwa katika Mji wa Daudi. \v 11 Daudi alikuwa ametawala Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na tatu. \v 12 Kwa hiyo Sulemani akaketi kwenye kiti cha ufalme cha baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika sana. \s1 Kiti cha ufalme cha Sulemani chaimarishwa \p \v 13 Basi Adoniya, mwana wa Hagithi, akaenda kwa Bathsheba, mama yake Sulemani. Bathsheba akamuuliza, “Je, umekuja kwa amani?” \p Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.” \v 14 Kisha akaongeza, “Ninalo jambo la kukuambia.” \p Akajibu, “Unaweza kulisema.” \p \v 15 Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, na ufalme umeenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa Mwenyezi Mungu. \v 16 Sasa ninalo ombi moja ninalokuomba. Usinikatalie.” \p Bathsheba akasema, “Unaweza kuliomba.” \p \v 17 Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Sulemani, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.” \p \v 18 Bathsheba akamjibu, “Vema sana, nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.” \p \v 19 Bathsheba alipoenda kwa Mfalme Sulemani kuzungumza naye kwa ajili ya Adoniya, mfalme alisimama kumlaki mama yake, akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa ajili ya mama yake mfalme, naye akamketisha mkono wake wa kuume. \p \v 20 Bathsheba akamwambia mfalme, “Ninalo ombi moja dogo la kukuomba; usinikatalie.” \p Mfalme akajibu, “Omba, mama yangu; sitakukatalia.” \p \v 21 Akasema, “Mruhusu Abishagi, Mshunami, aolewe na ndugu yako Adoniya.” \p \v 22 Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi Mshunami, kwa ajili ya Adoniya? Mwombee na ufalme pia kwani yeye ni ndugu yangu mkubwa: naam, kwa ajili yake, na kwa ajili ya kuhani Abiathari, na Yoabu mwana wa Seruya!” \p \v 23 Mfalme Sulemani akaapa kwa Mwenyezi Mungu, akasema: “Mungu na aniadhibu vikali zaidi ikiwa Adoniya hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili! \v 24 Basi sasa, hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, yeye ambaye ameniimarisha salama kwenye kiti cha ufalme cha Daudi baba yangu, naye amenipa ufalme wa kudumu kama alivyoahidi, Adoniya atauawa leo!” \v 25 Hivyo Mfalme Sulemani akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akampiga Adoniya akafa. \p \v 26 Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la Bwana Mungu Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.” \v 27 Hivyo Sulemani akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa Mwenyezi Mungu, akilitimiza neno la Mwenyezi Mungu alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli. \p \v 28 Habari zilipomfikia Yoabu, aliyekuwa amepanga njama na Adoniya, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la Mwenyezi Mungu na kushika pembe za madhabahu. \v 29 Mfalme Sulemani akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema la Mwenyezi Mungu naye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Sulemani akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamuue!” \p \v 30 Ndipo Benaya akaingia kwenye hema la Mwenyezi Mungu na kumwambia Yoabu, “Mfalme anasema, ‘Toka nje!’ ” \p Lakini akajibu, “La! Nitafia hapa hapa.” \p Benaya akamwarifu mfalme, “Hivi ndivyo Yoabu alivyonijibu.” \p \v 31 Kisha mfalme akamwamuru Benaya, “Fanya kama asemavyo. Muue na kumzika, ili uniondolee mimi na nyumba ya baba yangu dhambi ya damu isiyokuwa na hatia ile Yoabu aliyoimwaga. \v 32 Mwenyezi Mungu atamlipiza kwa ajili ya damu aliyoimwaga, kwa sababu pasipo Daudi baba yangu kujua, aliwashambulia watu wawili na kuwaua kwa upanga. Wote wawili, Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda, walikuwa watu wazuri na wanyofu kuliko yeye. \v 33 Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya Mwenyezi Mungu milele.” \p \v 34 Basi Benaya mwana wa Yehoyada akakwea, akamgonga na kumuua Yoabu, naye akazikwa katika shamba lake mwenyewe jangwani. \v 35 Mfalme akamweka Benaya mwana wa Yehoyada juu ya jeshi kwenye nafasi ya Yoabu, na kumweka kuhani Sadoki badala ya Abiathari. \p \v 36 Kisha mfalme akatuma ujumbe kwa Shimei na kumwambia, “Ujijengee nyumba huko Yerusalemu uishi huko, lakini usiende mahali pengine popote. \v 37 Siku utakayoondoka kuvuka Bonde la Kidroni, uwe na hakika utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe.” \p \v 38 Shimei akamjibu mfalme, “Ulilolisema ni jema. Mtumishi wako atatenda kama bwana wangu mfalme alivyosema.” Naye Shimei akakaa Yerusalemu kwa muda mrefu. \p \v 39 Lakini baada ya miaka mitatu, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi, naye Shimei akaambiwa, “Watumwa wako wameenda Gathi.” \v 40 Kwa ajili ya hili, Shimei akatandika punda wake, akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumwa wake. Basi Shimei akaondoka na kuwarudisha watumwa wake kutoka Gathi. \p \v 41 Sulemani alipoambiwa kuwa Shimei ametoka Yerusalemu na kwenda Gathi na amekwisha kurudi, \v 42 mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa Mwenyezi Mungu na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa’? Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’ \v 43 Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa Mwenyezi Mungu na kutii amri niliyokupa?” \p \v 44 Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua moyoni mwako makosa yote uliyomtendea baba yangu Daudi. Sasa Mwenyezi Mungu atakulipiza kwa ajili ya mabaya yako uliyotenda. \v 45 Lakini Mfalme Sulemani atabarikiwa, na kiti cha ufalme cha Daudi kitaimarishwa mbele za Mwenyezi Mungu milele.” \p \v 46 Kisha mfalme akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akatoka nje, akamgonga Shimei na kumuua. \p Sasa ufalme ukawa umeimarika mikononi mwa Sulemani. \c 3 \s1 Sulemani aomba hekima \r (2 Nyakati 1:3-12) \p \v 1 Sulemani akafanya mapatano na Mfalme Farao wa Misri na akamwoa binti yake. Akamleta huyo binti Farao katika Mji wa Daudi hadi alipomaliza kujenga jumba lake la kifalme na Hekalu la Mwenyezi Mungu, pamoja na ukuta kuzunguka Yerusalemu. \v 2 Hata hivyo, watu bado walikuwa wakitoa dhabihu huko kwenye mahali pa juu pa kuabudia, kwa sababu Hekalu lilikuwa bado halijajengwa kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu. \v 3 Sulemani akaonesha upendo wake kwa Mwenyezi Mungu kwa kuenenda sawasawa na amri za Daudi baba yake, ila yeye alitoa dhabihu na kufukiza uvumba huko mahali pa juu pa kuabudia. \p \v 4 Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali pa juu pa kuabudia pakuu, naye Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hayo madhabahu. \v 5 Mwenyezi Mungu akamtokea Sulemani huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, “Omba lolote utakalo nikupe.” \p \v 6 Sulemani akajibu, “Umemfanyia mtumishi wako, baba yangu Daudi, fadhili nyingi, kwa kuwa alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki, tena mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii kuu kwani umempa mwana wa kuketi kwenye kiti chake cha ufalme, kama ilivyo leo. \p \v 7 “Sasa, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme mahali pa baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu, wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu. \v 8 Mtumishi wako yuko hapa miongoni mwa watu uliowachagua: taifa kubwa, watu wengi wasioweza kuhesabika wala kutoa idadi yao. \v 9 Hivyo mpe mtumishi wako moyo wa ufahamu ili kutawala watu wako na kupambanua kati ya mema na mabaya. Kwa maana, ni nani awezaye kutawala watu wako hawa walio wengi hivi?” \p \v 10 Bwana akapendezwa kwamba Sulemani ameliomba jambo hili. \v 11 Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba busara katika kutoa haki, \v 12 nitafanya uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwa mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwa baada yako. \v 13 Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba: utajiri na heshima; siku za maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme. \v 14 Nawe ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu vile baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.” \v 15 Ndipo Sulemani akaamka, akatambua kuwa ilikuwa ndoto. \p Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu. \s1 Uamuzi wa hekima \p \v 16 Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. \v 17 Mmoja wao akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami. \v 18 Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili. \p \v 19 “Usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia. \v 20 Hivyo akaondoka katikati ya usiku na kumchukua mwanangu kutoka ubavuni pangu wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa nimelala. Akamweka kifuani mwake na kumweka mwanawe aliyekufa kifuani mwangu. \v 21 Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia kwa makini katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyemzaa.” \p \v 22 Huyo mwanamke mwingine akasema, “Hapana! Mwana aliye hai ndiye wangu, aliyekufa ni wako.” \p Lakini yule wa kwanza akasisitiza, “Hapana! Mwana aliyekufa ni wako; aliye hai ni wangu.” Hivi ndivyo walivyobishana mbele ya mfalme. \p \v 23 Mfalme akasema, “Huyu anasema, ‘Mwanangu ndiye aliye hai, na aliyekufa ndiye mwanao,’ maadamu yule anasema, ‘Hapana! Aliyekufa ni wako, na aliye hai ni wangu.’ ” \p \v 24 Kisha mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Basi wakamletea mfalme upanga. \v 25 Ndipo mfalme akatoa amri: “Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu.” \p \v 26 Mwanamke ambaye mwanawe alikuwa hai akajawa na huruma kwa ajili ya mwanawe na kumwambia mfalme, “Tafadhali, bwana wangu, mpe yeye mtoto aliye hai! Usimuue!” \p Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Mkate vipande viwili. Asiwe wangu au wake!” \p \v 27 Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake.” \p \v 28 Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki. \c 4 \s1 Maafisa na watawala wa Sulemani \p \v 1 Basi Mfalme Sulemani akatawala Israeli yote. \b \lh \v 2 Hawa walikuwa maafisa wake wakuu: \b \li1 Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki; \li1 \v 3 Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi; \li1 Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani; \li1 \v 4 Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi; \li1 Sadoki na Abiathari: makuhani; \li1 \v 5 Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya; \li1 Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme; \li1 \v 6 Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme; \li1 Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha. \b \p \v 7 Pia Sulemani alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioshughulikia mahitaji ya mfalme na ya watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka. \b \lh \v 8 Majina yao ni haya: \b \li1 Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu; \li1 \v 9 Ben-Dekari: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Beth-Hanani; \li1 \v 10 Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake); \li1 \v 11 Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Sulemani); \li1 \v 12 Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu; \li1 \v 13 Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makazi ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa yake, kadhalika wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini iliyozungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba); \li1 \v 14 Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu; \li1 \v 15 Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Sulemani); \li1 \v 16 Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi; \li1 \v 17 Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari; \li1 \v 18 Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini; \li1 \v 19 Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa mtawala pekee katika eneo hilo. \s1 Mahitaji ya Sulemani ya kila siku \p \v 20 Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi. \v 21 Mfalme Sulemani akatawala katika falme zote kuanzia Mto\f + \fr 4:21 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f* hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Sulemani, siku zote za maisha yake. \p \v 22 Mahitaji ya Sulemani ya kila siku yalikuwa kori thelathini\f + \fr 4:22 \fr*\ft Kori 30 ni sawa na madebe 360.\ft*\f* za unga laini, kori sitini\f + \fr 4:22 \fr*\ft Kori 60 ni sawa na madebe 720.\ft*\f* za unga wa kawaida. \v 23 Ng’ombe kumi wa zizini, ng’ombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana. \v 24 Kwa kuwa Sulemani alitawala falme zote magharibi ya Mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote. \v 25 Wakati wa maisha ya Sulemani, watu wa Yuda na Israeli, kuanzia Dani hadi Beer-Sheba, waliishi salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake. \p \v 26 Sulemani alikuwa na mabanda elfu nne\f + \fr 4:26 \fr*\ft maandishi mengine yanasema \ft*\fqa elfu arobaini \fqa*\ft (taz. \+xt 2 Nyakati 9:25\+xt*).\ft*\f* ya magari ya vita, na farasi elfu kumi na mbili. \p \v 27 Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Sulemani na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua. \v 28 Pia walileta kiasi walichopangiwa cha shayiri na majani kwa ajili ya farasi wa magari ya vita na farasi wengine mahali palipostahili. \s1 Hekima ya Sulemani \p \v 29 Mungu akampa Sulemani hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari. \v 30 Hekima ya Sulemani ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri. \v 31 Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi; kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka. \v 32 Akanena mithali elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano (1,005). \v 33 Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wanaotambaa na samaki. \v 34 Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Sulemani, wakiwa wametumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia kuhusu hekima yake. \c 5 \s1 Maandalizi ya ujenzi wa Hekalu \r (2 Nyakati 2:1-18) \p \v 1 Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Sulemani amepakwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Sulemani, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi. \v 2 Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu: \pm \v 3 “Unajua kwamba baba yangu Daudi hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi yake kutoka pande zote, hadi Mwenyezi Mungu alipowaweka adui zake chini ya miguu yake. \v 4 Lakini sasa Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa. \v 5 Kwa hiyo, ninakusudia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kama Mwenyezi Mungu alivyomwambia baba yangu Daudi, aliposema, ‘Mwanao nitakayemweka kwenye kiti cha ufalme mahali pako, ndiye atajenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’ \pm \v 6 “Hivyo toa amri ili mierezi ya Lebanoni ikatwe kwa ajili yangu. Watu wangu watafanya kazi na watu wako, nami nitakulipa kwa ajili ya watu wako kwa ujira wowote utakaoupanga. Unajua kwamba hatuna mtu yeyote mwenye ustadi katika kukata miti kama Wasidoni.” \p \v 7 Hiramu aliposikia ujumbe wa Sulemani, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima ya kutawala taifa hili kubwa.” \p \v 8 Hivyo Hiramu akapeleka ujumbe kwa Sulemani: \pm “Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mwerezi na misunobari. \v 9 Watu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga katika mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.” \p \v 10 Kwa njia hii Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji, \v 11 naye Sulemani akampa Hiramu kori elfu ishirini\f + \fr 5:11 \fr*\ft Kori 20,000 ni sawa na madebe 240,000.\ft*\f* za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi elfu ishirini\f + \fr 5:11 \fr*\ft Bathi 20,000 ni sawa na madebe 200.\ft*\f*. Sulemani aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. \v 12 Mwenyezi Mungu akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwa na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Sulemani, na wote wawili wakafanya mkataba. \p \v 13 Mfalme Sulemani akakusanya wafanyakazi elfu thelathini kutoka Israeli yote. \v 14 Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu elfu kumi kila mwezi. Hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja, na miezi miwili wakakaa nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa. \v 15 Sulemani alikuwa na wachukuzi wa mizigo elfu sabini, na wachonga mawe elfu themanini huko vilimani, \v 16 pamoja na wasimamizi elfu tatu mia tatu ambao walisimamia mradi huo na kuwaelekeza wafanyakazi. \v 17 Kwa amri ya mfalme, walitoa mawe makubwa na bora kwenye machimbo ya mawe kwa kujengea msingi wa mawe yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu. \v 18 Mafundi wa Sulemani, wa Hiramu na watu wa Gebali\f + \fr 5:18 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bubilo\fqa*\f* walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu. \c 6 \s1 Sulemani ajenga Hekalu \r (2 Nyakati 3) \p \v 1 Katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani katika Israeli, katika mwezi wa Zivu\f + \fr 6:1 \fr*\ft mwezi wa tano katika kalenda ya Kiyahudi\ft*\f*, uliokuwa mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 2 Hekalu ambalo Mfalme Sulemani alilijenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini\f + \fr 6:2 \fr*\ft Dhiraa 60 ni sawa na mita 27.\ft*\f*, upana wa dhiraa ishirini\f + \fr 6:2 \fr*\ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\ft*\f*, na kimo cha dhiraa thelathini\f + \fr 6:2 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\ft*\f* kwenda juu. \v 3 Baraza iliyokuwa mbele ya ukumbi mkuu wa Hekalu iliongeza upana wa Hekalu kwa dhiraa ishirini, na kuchomoza dhiraa kumi mbele ya Hekalu. \v 4 Akatengeneza madirisha membamba katika Hekalu. \v 5 Akajenga vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote, vikishikamana na kuta za ukumbi wa Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu. \v 6 Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano\f + \fr 6:6 \fr*\ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\ft*\f*, ya kati ilikuwa dhiraa sita\f + \fr 6:6 \fr*\ft Dhiraa 6 ni sawa na mita 2.7.\ft*\f*, na ya tatu ilikuwa dhiraa saba\f + \fr 6:6 \fr*\ft Dhiraa 7 ni sawa na mita 3.15.\ft*\f*. Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu. \p \v 7 Katika kujenga Hekalu, yalitumika tu mawe yaliyochongwa huko machimboni, wala hakuna nyundo, patasi au chombo kingine chochote cha chuma kilichosikika katika eneo la ujenzi wa Hekalu wakati lilipokuwa likijengwa. \p \v 8 Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu; ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutoka hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu. \v 9 Basi Sulemani akajenga Hekalu na kulikamilisha, akiliweka paa za boriti na mbao za mwerezi. \v 10 Mfalme Sulemani akajenga vyumba vya pembeni kuzunguka Hekalu lote. Kimo cha kila kimoja kilikuwa dhiraa tano. Navyo vilikuwa vimeunganishwa na Hekalu kwa boriti za mwerezi. \p \v 11 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Sulemani kusema: \v 12 “Kuhusu Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, nitatimiza kupitia kwako ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako. \v 13 Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.” \p \v 14 Basi Sulemani akajenga Hekalu na kulikamilisha. \v 15 Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mwerezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari, na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari. \v 16 Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mwerezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu. \v 17 Ukumbi mkuu uliokuwa mbele ya chumba hiki ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini\f + \fr 6:17 \fr*\ft Dhiraa 40 ni sawa na mita 18.\ft*\f*. \v 18 Ndani, Hekalu lilipambwa na mbao za mwerezi zilizonakshiwa mifano ya maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi; hakuna jiwe ambalo lilionekana. \p \v 19 Ndani ya Hekalu akatengeneza mahali patakatifu pa kuliweka Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu. \v 20 Mahali patakatifu palikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, upana wa dhiraa ishirini, na kimo cha dhiraa ishirini. Akapafunika upande wa ndani, na madhabahu ya mwerezi pia, kwa dhahabu safi. \v 21 Sulemani akalifunika Hekalu upande wa ndani kwa dhahabu safi, na akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande mmoja hadi ule mwingine mbele ya mahali patakatifu, palipofunikwa kwa dhahabu. \v 22 Basi akafunika upande wote wa ndani kwa dhahabu. Pia akafunika kwa dhahabu yale madhabahu yaliyokuwa ndani ya mahali patakatifu. \p \v 23 Katika mahali patakatifu, akatengeneza makerubi wawili kwa mzeituni, kila moja likiwa na dhiraa kumi\f + \fr 6:23 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\ft*\f* kwenda juu. \v 24 Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na bawa jingine dhiraa tano, hivyo urefu kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa jingine ulikuwa dhiraa kumi. \v 25 Kerubi wa pili alikuwa na urefu wa dhiraa kumi pia, kwa kuwa makerubi hao wawili walifanana kwa vipimo na kwa umbo. \v 26 Kimo cha kila kerubi kilikuwa dhiraa kumi. \v 27 Aliwaweka makerubi hao katika chumba cha ndani kabisa cha Hekalu, mabawa yao yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta wa upande mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba. \v 28 Akafunika wale makerubi kwa dhahabu. \p \v 29 Kuta zote za Hekalu, za vyumba vya ndani na vya nje, zilipambwa kwa nakshi za makerubi, mitende na maua yaliyochanua. \v 30 Pia alifunika sakafu zote za vyumba vya ndani na vya nje vya Hekalu kwa dhahabu. \p \v 31 Katika ingilio la mahali patakatifu sana, alitengeneza milango ya mbao za mzeituni, yenye miimo ya sehemu moja ya tano ya upana wa madhabahu. \v 32 Kwenye milango hiyo miwili ya mbao za mzeituni, alinakshi makerubi, mitende, pamoja na maua yaliyochanua, na kufunika makerubi na mitende kwa dhahabu iliyofuliwa. \v 33 Kwa namna hiyo hiyo, alitengeneza miimo kwa mbao za mzeituni yenye upana wa robo ya upana wa ukumbi mkuu kwa ajili ya ingilio la ukumbi huo. \v 34 Pia akatengeneza milango miwili kwa mbao za msunobari, kila mmoja ukiwa na vipande viwili ambavyo vilikunjwa kwa bawaba. \v 35 Akanakshi makerubi, mitende na maua yaliyochanua juu yake, na kufunika kwa dhahabu iliyonyoshwa vizuri juu ya michoro. \p \v 36 Tena akajenga ua wa ndani safu tatu za mawe yaliyochongwa, na safu moja ya boriti za mwerezi zilizosawazishwa. \p \v 37 Msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu. \v 38 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Sulemani. Alilijenga kwa miaka saba. \c 7 \s1 Sulemani ajenga jumba la kifalme \p \v 1 Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kukamilisha ujenzi wa jumba lake la kifalme. \v 2 Alijenga jumba lililoitwa Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. Lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja\f + \fr 7:2 \fr*\ft Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.\ft*\f*, upana wa dhiraa hamsini\f + \fr 7:2 \fr*\ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\ft*\f*, na kimo cha dhiraa thelathini\f + \fr 7:2 \fr*\ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\ft*\f*, na safu nne za nguzo za mwerezi zilizoshikilia boriti za mwerezi zilizosawazishwa. \v 3 Lilipauliwa kwa mbao za mwerezi juu ya boriti arobaini na tano zilizolalia nguzo, boriti kumi na tano kwa kila safu. \v 4 Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. \v 5 Milango yenye miimo ya mstatili ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana. \p \v 6 Akajenga safu ya nguzo, yenye urefu wa dhiraa hamsini\f + \fr 7:6 \fr*\ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\ft*\f* na upana wa dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwa na baraza. Mbele ya baraza kulikuwa na nguzo na paa lililoning’inia. \p \v 7 Akajenga ukumbi wa kiti cha ufalme, yaani Ukumbi wa Hukumu, mahali ambapo angetolea hukumu, akaufunika kwa mbao za mwerezi kutoka sakafu hadi dari. \v 8 Jumba la kifalme ambamo angeishi, aliliweka nyuma kidogo, na lilijengwa kama jumba hilo la hukumu. Pia Sulemani akajenga jumba la kifalme lililofanana na hilo kwa ajili ya binti Farao, aliyekuwa amemwoa. \p \v 9 Majengo haya yote, kuanzia nje hadi kwenye ua mkuu, na kuanzia msingi hadi upenuni, yalijengwa kwa mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo kwa msumeno, na nyuso zake za ndani na za nje zililainishwa. \v 10 Misingi ilijengwa kwa mawe makubwa yaliyo bora, yenye urefu wa dhiraa kumi\f + \fr 7:10 \fr*\ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\ft*\f*, na mengine urefu wa dhiraa nane\f + \fr 7:10 \fr*\ft Dhiraa nane ni sawa na mita 3.6.\ft*\f*. \v 11 Sehemu za juu kulikuwa na boriti za mwerezi, na mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo. \v 12 Ule ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa, na safu moja ya boriti za mwerezi zilizosawazishwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Mwenyezi Mungu na baraza yake. \s1 Samani za Hekalu \r (2 Nyakati 4) \p \v 13 Mfalme Sulemani akatuma watu Tiro kumleta Hiramu\f + \fr 7:13 \fr*\ft au \ft*\fqa Huramu\fqa*\f*, \v 14 ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Sulemani na kufanya kazi zake zote alizopangiwa. \p \v 15 Hiramu akasubu nguzo mbili za shaba, kila moja ikiwa na urefu wa dhiraa kumi na nane\f + \fr 7:15 \fr*\ft Dhiraa 18 ni sawa na mita 8.1.\ft*\f*, na mzingo wa dhiraa kumi na mbili\f + \fr 7:15 \fr*\ft Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4.\ft*\f* kwa mstari. \v 16 Pia alitengeneza mataji mawili ya shaba ya kusubu ili kuyaweka juu ya hizo nguzo; kila taji lilikuwa na kimo cha dhiraa tano\f + \fr 7:16 \fr*\ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\ft*\f* kwenda juu. \v 17 Wavu wa mikufu iliyosokotewa kwenye zile taji juu ya zile nguzo, saba kwa kila taji. \v 18 Akatengeneza makomamanga katika safu mbili kuzunguka kila wavu kuremba mataji yaliyo juu ya nguzo. Alifanya hivyo kwa kila nguzo. \v 19 Mataji yaliyokuwa juu ya nguzo kwenye baraza, yalikuwa katika umbo la yungiyungi, kimo chake ni dhiraa nne\f + \fr 7:19 \fr*\ft Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.\ft*\f*. \v 20 Juu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga mia mbili katika safu kuzunguka pande zote. \v 21 Hiramu akazisimamisha zile nguzo barazani pa Hekalu. Nguzo iliyokuwa upande wa kusini akaiita Yakini\f + \fr 7:21 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Atathibitisha\fqa*\f*, na ile ya upande wa kaskazini akaiita Boazi\f + \fr 7:21 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Imo nguvu\fqa*\f*. \v 22 Mataji yaliyokuwa juu yalikuwa na umbo la yungiyungi. Hivyo kazi ya nguzo ikakamilika. \p \v 23 Hiramu akasubu Bahari ya chuma, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo, na kimo cha dhiraa tano. Mzunguko wake ulikuwa dhiraa thelathini. \v 24 Chini ya ukingo, ilizungukwa na mapambo ya maboga kumi kwa kila dhiraa. Maboga hayo yalikuwa yamesubiwa katika safu mbili ili kuwa kitu kimoja na hiyo Bahari. \p \v 25 Ile Bahari iliwekwa juu ya mafahali kumi na wawili, watatu wakielekea kaskazini, watatu wakielekea magharibi, watatu wakielekea kusini, na watatu wakielekea mashariki. Hiyo Bahari iliwekwa juu yao, na sehemu zao za nyuma zilielekeana. \v 26 Bahari hiyo ilikuwa na unene wa nyanda moja\f + \fr 7:26 \fr*\ft Nyanda moja ni sawa na sentimita 7.5.\ft*\f*, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi lililochanua; nayo ingejazwa na bathi elfu mbili\f + \fr 7:26 \fr*\ft Bathi 2,000 ni sawa na lita 40,000.\ft*\f*. \p \v 27 Pia akatengeneza vitako kumi vya shaba vinavyoweza kuhamishika, kila kimoja kilikuwa na urefu wa dhiraa nne, upana dhiraa nne na kimo chake dhiraa tatu\f + \fr 7:27 \fr*\ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\ft*\f*. \v 28 Hivi ndivyo vile vitako vilivyotengenezwa: Vilikuwa na mbao za pembeni zilizounganishwa na mihimili. \v 29 Juu ya mbao kati ya hiyo mihimili kulikuwa na simba, mafahali na makerubi, pia kwenye mihimili yake. Juu na chini ya simba na mafahali kulikuwa na shada za maua yaliyofuliwa. \v 30 Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya kuyazungusha. Kila kitako kilikuwa na sinia iliyowekwa juu ya vishikizo vinne viliyosubiwa shada za maua kila upande. \v 31 Ndani ya kitako kulikuwa na nafasi ya wazi iliyokuwa na umbile la mviringo lenye kina cha dhiraa moja\f + \fr 7:31 \fr*\ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\ft*\f*. Nafasi hii ya wazi ilikuwa ya mviringo, pamoja na kitako chake ilikuwa dhiraa moja na nusu\f + \fr 7:31 \fr*\ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.\ft*\f*. Kuzunguka huo mdomo wake kulitiwa nakshi. Papi za vitako zilikuwa mraba na si za mviringo. \v 32 Yale magurudumu manne yalikuwa chini ya papi, na vyuma vya kuyazungushia viliunganishwa kwenye kitako. Kipenyo cha kila gurudumu kilikuwa dhiraa moja na nusu. \v 33 Magurudumu hayo yalitengenezwa kama ya magari ya kukokotwa na farasi; vyuma vya kuzungushia magurudumu, duara zake, matindi yake na vitovu vyake, vyote vilikuwa vya kusubu. \p \v 34 Kila kitako kilikuwa na mikono minne, moja kwenye kila pembe, ukichomoza kutoka kile kitako. \v 35 Juu ya kitako kulikuwa na utepe wa mviringo wenye kina cha nusu dhiraa. Vishikio na papi vilishikamana upande wa juu wa kitako. \v 36 Aliweka nakshi za makerubi, simba na mitende juu ya vishikio na juu ya papi, katika kila nafasi, na shada za maua kuzunguka. \v 37 Hivi ndivyo Hiramu alivyotengeneza vile vitako kumi. Vyote vilisubiwa kwenye kalibu moja na vilifanana kwa vipimo na kwa umbo. \p \v 38 Kisha akatengeneza masinia kumi ya shaba, kila moja likiwa na ujazo wa bathi arobaini\f + \fr 7:38 \fr*\ft Bathi 40 ni sawa na lita 800.\ft*\f*, yakiwa na kipenyo cha dhiraa nne\f + \fr 7:38 \fr*\ft Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.\ft*\f* kila sinia moja kwa kila kimoja cha vile vitako kumi. \v 39 Aliweka vitako vitano upande wa kusini wa Hekalu na vingine vitano upande wa kaskazini. Akaweka ile Bahari upande wa kusini, katika pembe ya kusini-mashariki ya Hekalu. \v 40 Pia akatengeneza masinia, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. \p Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi zote katika Hekalu la Mwenyezi Mungu kama vile Mfalme Sulemani alikuwa amemwagiza: \b \li1 \v 41 nguzo mbili; \li1 mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo; \li1 nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo; \li1 \v 42 makomamanga mia nne kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo); \li1 \v 43 vitako kumi pamoja na masinia yake kumi; \li1 \v 44 ile Bahari ya chuma na wale mafahali kumi na wawili chini yake; \li1 \v 45 masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. \b \p Vyombo hivi vyote ambavyo Huramu alimtengenezea Mfalme Sulemani kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu vilikuwa vya shaba iliyong’arishwa. \v 46 Mfalme akaamuru wavisubu katika kalibu ya udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani ulio kati ya Sukothi na Sarethani. \v 47 Sulemani hakupima vitu hivi vyote kwa sababu vilikuwa vingi sana; hivyo, uzani wa shaba haukukadiriwa. \p \v 48 Sulemani pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu: \b \li1 madhabahu ya dhahabu; \li1 meza ya dhahabu za kuweka mikate ya Wonesho; \li1 \v 49 vinara vya taa vya dhahabu safi (vitano upande wa kuume na vitano upande wa kushoto, mbele ya mahali patakatifu); \li1 shada za maua, na taa, na makoleo, vyote vikiwa vya dhahabu; \li1 \v 50 vyombo vya dhahabu safi: masinia, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, vyano na vyetezo; \li1 na bawaba za dhahabu kwa ajili ya milango ya chumba cha ndani sana, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na pia kwa ajili ya milango ya ukumbi mkuu wa Hekalu. \b \p \v 51 Hivyo, Mfalme Sulemani alipomaliza kazi zote za Hekalu la Mwenyezi Mungu, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu. \c 8 \s1 Sanduku la Agano laletwa Hekaluni \r (2 Nyakati 5) \p \v 1 Kisha Mfalme Sulemani akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. \v 2 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa Mfalme Sulemani wakati wa sikukuu ya mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba. \p \v 3 Wazee wote wa Israeli walipofika, makuhani wakajitwika lile Sanduku, \v 4 nao wakalipandisha Sanduku la Mwenyezi Mungu, na Hema la Kukutania, pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani na Walawi wakavibeba, \v 5 naye Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli waliokuwa wamemzunguka wakasimama mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu za kondoo na ng’ombe nyingi kiasi kwamba idadi yao haikuweza kuandikwa au kuhesabika. \p \v 6 Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu hadi mahali pake ndani ya mahali patakatifu sana humo Hekaluni, ndipo Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. \v 7 Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kutia kivuli Sanduku pamoja na mipiko yake ya kubebea. \v 8 Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilionekana kutoka Mahali Patakatifu mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. \v 9 Ndani ya Sanduku hapakuwa na kitu kingine isipokuwa vile vibao viwili vya mawe ambavyo Musa aliviweka ndani yake huko Horebu, mahali Mwenyezi Mungu alipofanya agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri. \p \v 10 Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Mwenyezi Mungu. \v 11 Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Mwenyezi Mungu ulijaza Hekalu lake. \p \v 12 Ndipo Sulemani akasema, “Mwenyezi Mungu alisema kwamba ataishi katika giza nene; \v 13 naam, hakika nimekujengea Hekalu zuri sana, mahali pako pa kuishi milele.” \s1 Hotuba ya Sulemani \r (2 Nyakati 6:3-11) \p \v 14 Kusanyiko lote la Israeli walipokuwa wamesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. \v 15 Kisha akasema: \pm “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, \v 16 ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo na Jina langu liwe humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’ \pm \v 17 “Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 18 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako. \v 19 Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea Hekalu, bali mwanao, ambaye ni mwili wako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’ \pm \v 20 “Mwenyezi Mungu ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu, na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile Mwenyezi Mungu alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \v 21 Nimetenga nafasi humo kwa ajili ya Sanduku la Agano, ambalo ndani yake kuna lile Agano la Mwenyezi Mungu alilofanya na baba zetu alipowatoa Misri.” \s1 Maombi ya Sulemani ya kuweka Hekalu wakfu \r (2 Nyakati 6:12-42) \p \v 22 Kisha Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kuelekea mbinguni, \v 23 na kusema: \pm “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote. \v 24 Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umetimiza, kama ilivyo leo. \pm \v 25 “Sasa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, ikiwa wanao watakuwa waangalifu kwa yote wayafanyayo ili kuenenda mbele zangu kama ulivyofanya.’ \v 26 Sasa, Ee Mungu wa Israeli, ruhusu neno lako ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie. \pm \v 27 “Je, hakika Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga! \v 28 Hata hivyo, sikiliza dua la mtumishi wako na maombi yake ya kuhurumiwa, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambalo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. \v 29 Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwa humo,’ ili upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. \v 30 Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia ukiwa mbinguni, makao yako, na unaposikia, samehe. \pm \v 31 “Mtu akimkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili, \v 32 basi, sikia ukiwa mbinguni, ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimhukumu yule mwenye hatia na kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie mwenye haki kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kuwa haki kwake. \pm \v 33 “Watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, nao wakakugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili, \v 34 basi usikie ukiwa mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao. \pm \v 35 “Mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka dhambi zao kwa sababu umewaadhibu, \v 36 basi usikie ukiwa mbinguni, usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi, na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi. \pm \v 37 “Njaa au tauni itakapotokea katika nchi, koga au ukungu, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia, \v 38 kila dua au ombi litakalotolewa na yeyote kati ya watu wako Israeli, akitambua taabu za moyo wake mwenyewe, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili, \v 39 basi usikie ukiwa mbinguni, makao yako. Usamehe na utende; umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), \v 40 ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. \pm \v 41 “Kuhusu mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako, \v 42 kwa maana watu watasikia kuhusu Jina lako kuu na kuhusu mkono wako wenye nguvu na mkono wako ulionyooshwa, atakapokuja na kuomba kuelekea Hekalu hili, \v 43 basi na usikie ukiwa mbinguni, makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli, na pia wapate kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako. \pm \v 44 “Watu wako watakapoenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa Mwenyezi Mungu kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, \v 45 basi usikie dua na maombi yao ukiwa mbinguni, ukawape haki yao. \pm \v 46 “Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu asiyetenda dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi yake mwenyewe, mbali au karibu; \v 47 na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya wale waliowashinda na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa, tumetenda uovu’; \v 48 wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako; \v 49 basi usikie dua na maombi yao ukiwa mbinguni, makao yako, ukawape haki yao. \v 50 Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako; uwasamehe makosa yote waliyoyatenda dhidi yako, na ukawafanye wale waliowashinda kuwaonea huruma; \v 51 kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka lile tanuru la kuyeyushia chuma. \pm \v 52 “Macho yako na yafumbuke kwa ombi la mtumishi wako na ombi la watu wako Israeli, nawe uwasikilize wakati wowote wanapokulilia. \v 53 Kwa maana uliwachagua kati ya mataifa yote ya ulimwengu wawe urithi wako mwenyewe, kama ulivyotangaza kupitia mtumishi wako Musa wakati wewe, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, ulipowatoa baba zetu kutoka Misri.” \p \v 54 Sulemani alipomaliza dua na maombi haya yote kwa Mwenyezi Mungu, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiwa amenyoosha mikono yake kuelekea mbinguni. \v 55 Akasimama na kubariki kusanyiko lote la Israeli kwa sauti kubwa, akisema: \pm \v 56 “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Musa. \v 57 Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, na awe pamoja nasi kama alivyokuwa na baba zetu, kamwe asituache wala kutukataa. \v 58 Yeye na aielekeze mioyo yetu kwake, ili tutembee katika njia zake zote na kushika amri, maagizo, na masharti aliyowapa baba zetu. \v 59 Nami maneno yangu haya, ambayo nimeyaomba mbele za Mwenyezi Mungu, yawe karibu na Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, usiku na mchana, ili awape haki mtumishi wake na watu wake Israeli, kulingana na mahitaji yao ya kila siku, \v 60 ili mataifa yote ya dunia wajue kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu na kwamba hakuna mwingine. \v 61 Lazima mwiweke mioyo yenu kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, mwishi kwa maagizo yake na kutii amri zake, kama ilivyo wakati huu.” \s1 Hekalu lawekwa wakfu \r (2 Nyakati 7:4-10) \p \v 62 Kisha mfalme na Waisraeli wote pamoja naye wakatoa dhabihu mbele za Mwenyezi Mungu. \v 63 Sulemani akatoa dhabihu sadaka za amani kwa Mwenyezi Mungu: ng’ombe elfu ishirini na mbili, pamoja na kondoo na mbuzi elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mwenyezi Mungu. \p \v 64 Siku hiyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Mwenyezi Mungu ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani. \p \v 65 Hivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu kwa wakati ule, na Waisraeli wote pamoja naye: walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. Wakaiadhimisha mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kwa siku saba na siku saba zaidi, yaani jumla siku kumi na nne. \v 66 Siku iliyofuata, aliwaruhusu watu waondoke. Wakambariki mfalme, kisha wakaenda nyumbani wakiwa na mashangilio na furaha moyoni kwa ajili ya mambo yote mema ambayo Mwenyezi Mungu alimtendea kwa ajili ya Daudi mtumishi wake na watu wake Israeli. \c 9 \s1 Mwenyezi Mungu amtokea Sulemani \r (2 Nyakati 7:11-22) \p \v 1 Sulemani alipomaliza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu na jumba la kifalme, na alipokwisha kufanya yote aliyotaka kufanya, \v 2 Mwenyezi Mungu akamtokea mara ya pili, vile alivyomtokea huko Gibeoni. \v 3 Mwenyezi Mungu akamwambia: \pm “Nimesikia dua na maombi uliyofanya mbele zangu, nimeliweka wakfu Hekalu hili ambalo umelijenga, kwa kuweka Jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwa humo siku zote. \pm \v 4 “Kwako wewe, kama ukienenda kwa unyofu wa moyo na uadilifu, kama baba yako Daudi alivyofanya na kutenda yote ninayoyaagiza kwa kutunza maagizo yangu na sheria, \v 5 nitakiimarisha kiti chako cha utawala juu ya Israeli milele kama nilivyomwahidi Daudi baba yako niliposema, ‘Hutakosa kamwe kuwa na mtu kwenye kiti cha utawala cha Israeli.’ \pm \v 6 “Lakini ninyi au wana wenu mkinigeukia mbali na kuziacha amri na maagizo yangu niliyowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, \v 7 basi nitakatilia mbali Israeli kutoka nchi niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Ndipo Israeli itakuwa kitu cha kudharauliwa na watu na kuwa kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote. \v 8 Ingawa hekalu hili linavutia sasa, wote watakaolipita watashangaa na kudhihaki wakisema, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’ \v 9 Watu watajibu, ‘Kwa sababu wamemwacha Mwenyezi Mungu, Mungu wao, aliyewatoa baba zao Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, ndiyo sababu Mwenyezi Mungu ameyaleta maafa haya yote juu yao.’ ” \s1 Shughuli nyingine za Sulemani \r (2 Nyakati 8) \p \v 10 Miaka ishirini ilipopita, muda ambao Sulemani alijenga majengo haya mawili, yaani Hekalu la Mwenyezi Mungu na jumba la kifalme, \v 11 Mfalme Sulemani akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi na misunobari yote na dhahabu yote kama alivyohitaji. \v 12 Lakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. \v 13 Hiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?” \p Naye akaiita nchi ya Kabul\f + \fr 9:13 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Isiyofaa kitu\fqa*\f*, jina lililoko hadi leo. \v 14 Basi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta mia moja na ishirini\f + \fr 9:14 \fr*\ft Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5.\ft*\f* za dhahabu. \p \v 15 Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Sulemani aliwafanyiza watu ili kulijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, na jumba lake la kifalme, na Milo\f + \fr 9:15 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Boma la Ngome\fqa*\ft ; pia \+xt 9:24\+xt*\ft*\f*, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri. \v 16 (Farao mfalme wa Misri alikuwa ameushambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Sulemani, kama zawadi ya arusi. \v 17 Sulemani akaujenga tena Gezeri.) Akajenga Beth-Horoni ya Chini, \v 18 akajenga Baalathi na Tamari kwenye jangwa katika eneo la nchi yake. \v 19 Vilevile, alijenga miji ya ghala na ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake na wapanda farasi: alijenga kila alichotaka katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika eneo lote alilotawala. \p \v 20 Watu wote waliosalia miongoni mwa Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi (watu wasiokuwa Waisraeli), \v 21 yaani, wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawakuwaangamiza kabisa, Sulemani akawalazimisha kuwa shokoa, kama ilivyo hadi leo. \v 22 Lakini Sulemani hakumfanya Mwisraeli yeyote kuwa mtumwa; hao ndio walikuwa wapiganaji wake, viongozi wa serikali yake, maafisa wake, wakuu wake wa jeshi, majemadari wa magari yake ya vita, na wapanda farasi wake. \v 23 Pia walikuwa maafisa wakuu wasimamizi wa miradi ya Sulemani: maafisa mia tano na hamsini waliwasimamia watu waliofanya kazi. \p \v 24 Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Sulemani alikuwa amemjengea, Sulemani akajenga Milo. \p \v 25 Sulemani akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka juu ya madhabahu aliyokuwa amemjengea Mwenyezi Mungu. Pamoja na hizo dhabihu, akafukiza uvumba mbele za Mwenyezi Mungu, hivyo kutimiza kanuni za Hekalu. \p \v 26 Mfalme Sulemani pia akatengeneza meli huko Esion-Geberi, iliyo karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu\f + \fr 9:26 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Bahari Nyekundu \fqa*\ft au \ft*\fqa Bahari ya Mafunjo\fqa*\f*. \v 27 Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Sulemani. \v 28 Wakasafiri kwa bahari hadi Ofiri na kurudi na talanta mia nne na ishirini (420)\f + \fr 9:28 \fr*\ft Talanta 420 za dhahabu ni sawa na tani 14.\ft*\f* za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Sulemani. \c 10 \s1 Malkia wa Sheba amtembelea Sulemani \r (2 Nyakati 9:1-12) \p \v 1 Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani na uhusiano wake na jina la Mwenyezi Mungu, akaja kumjaribu kwa maswali magumu. \v 2 Alifika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana wenye ngamia waliobeba vikolezo, dhahabu nyingi, na vito vya thamani. Akaenda kwa Sulemani na kuzungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake. \v 3 Sulemani alimjibu maswali yake yote; hapakuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwa mfalme hata asiweze kumwelezea. \v 4 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, \v 5 chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, alipatwa na mshangao mkubwa. \p \v 6 Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. \v 7 Lakini sikuamini mambo haya hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana ile taarifa niliyoisikia. \v 8 Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wanaosimama mbele yako daima na kusikia hekima yako! \v 9 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe na kukuweka kwenye kiti cha ufalme cha Israeli. Kwa sababu ya upendo wake Mwenyezi Mungu wa milele kwa Israeli, amekufanya mfalme, ili kudumisha haki na uadilifu.” \p \v 10 Naye akampa mfalme talanta mia moja na ishirini\f + \fr 10:10 \fr*\ft Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5.\ft*\f* za dhahabu, kiasi kikubwa sana cha vikolezo na vito vya thamani. Kamwe havijawahi kuletwa tena vikolezo vingi kama vile malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Sulemani. \p \v 11 (Meli za Hiramu zilileta dhahabu kutoka Ofiri; tena zikaleta shehena kubwa ya miti ya msandali, na vito vya thamani kutoka huko. \v 12 Mfalme alitumia miti ya msandali kutengenezea nguzo za Hekalu la Mwenyezi Mungu na za jumba la kifalme, na kutengenezea vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Miti mingi ya msandali kiasi hicho haijawahi kuletwa au kuonekana tangu wakati ule.) \p \v 13 Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, kando na vile mfalme alivyokuwa amempa kwa ukarimu wake wa kifalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake. \s1 Fahari ya Sulemani \r (2 Nyakati 9:13-28) \p \v 14 Uzito wa dhahabu ambayo Sulemani alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta mia sita sitini na sita (666)\f + \fr 10:14 \fr*\ft Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25.\ft*\f*, \v 15 mbali na mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi, na kutoka kwa wafalme wote wa Waarabu na watawala wa nchi. \p \v 16 Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili kwa dhahabu iliyofuliwa; kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli mia sita\f + \fr 10:16 \fr*\ft Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5.\ft*\f*. \v 17 Akatengeneza pia ngao ndogo mia tatu za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu\f + \fr 10:17 \fr*\ft Mane 3 za dhahabu ni sawa na kilo 1.7.\ft*\f* za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. \p \v 18 Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. \v 19 Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita, na egemeo lenye mviringo juu yake. Kila upande wa kiti ulikuwa na mahali pa kuegemeza mkono, na simba aliyesimama kando kila upande. \v 20 Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kiti kama hicho kiliwahi kutengenezwa katika ufalme mwingine wowote. \p \v 21 Vyombo vyote vya Mfalme Sulemani vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo siku za Sulemani. \v 22 Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara\f + \fr 10:22 \fr*\ft au \ft*\fqa za Tarshishi \fqa*\ft (taz. \+xt 1 Wafalme 22:48; 2 Nyakati 9:21; 20:36; Isaya 2:16; 60:9\+xt*).\ft*\f* baharini zilizokuwa zikiandamana na meli za Hiramu. Mara moja katika kila miaka mitatu zilirudi zikiwa zimebeba dhahabu, fedha na pembe za ndovu, na sokwe na nyani. \p \v 23 Mfalme Sulemani alikuwa na utajiri mkubwa na mwenye hekima kuliko wafalme wote wa dunia. \v 24 Dunia yote ikatafuta kukutana na Sulemani ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. \v 25 Kila mwaka, kila mtu aliyekuja alileta zawadi: vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezo, farasi na nyumbu. \p \v 26 Sulemani alikusanya magari ya vita na farasi. Akawa na magari ya vita elfu moja mia nne, na farasi elfu kumi na mbili, ambayo aliyaweka katika miji ya magari ya vita, na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. \v 27 Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu chini ya vilima. \v 28 Farasi wa Sulemani waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue\f + \fr 10:28 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Kilikia\fqa*\f*. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue. \v 29 Walinunua magari ya vita kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha\f + \fr 10:29 \fr*\ft Shekeli 600 za fedha ni sawa na kilo 7.\ft*\f* kila moja, na kila farasi kwa shekeli mia moja na hamsini\f + \fr 10:29 \fr*\ft Shekeli 150 za fedha ni sawa na kilo 1.7.\ft*\f*; na wakawauzia wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu\f + \fr 10:29 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Washamu\fqa*\f*. \c 11 \s1 Wakeze Sulemani \p \v 1 Mbali na binti Farao, Mfalme Sulemani aliwapenda wanawake wengi wa kigeni: Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti. \v 2 Walitoka katika mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Sulemani akakaza kuwapenda. \v 3 Alikuwa na wake mia saba, binti za uzao wa kifalme, na masuria mia tatu; nao wake zake wakampotosha. \v 4 Kadiri Sulemani alivyozidi kuzeeka, wake zake wakaugeuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukujitoa kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake. \v 5 Sulemani akafuata Ashtorethi, mungu wa kike wa Wasidoni, na Moleki\f + \fr 11:5 \fr*\ft Moleki au \ft*\fqa Milkomu \fqa*\ft ni mungu aliyekuwa akiabudiwa na Waamoni; alikuwa chukizo kwa sababu watoto walitolewa kafara kwake.\ft*\f* mungu wa Waamoni, aliyekuwa chukizo. \v 6 Kwa hiyo Sulemani akafanya uovu machoni pa Mwenyezi Mungu; hakumfuata Mwenyezi Mungu kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake. \p \v 7 Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Sulemani alijenga mahali pa juu pa kuabudia Kemoshi mungu wa Wamoabu, aliyekuwa chukizo, na pa kuabudia Moleki mungu wa Waamoni, aliyekuwa chukizo. \v 8 Akafanya vivyo hivyo kwa wake zake wote wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa dhabihu kwa miungu yao. \p \v 9 Mwenyezi Mungu akamkasirikia Sulemani kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliyekuwa amemtokea mara mbili. \v 10 Ingawa alikuwa amemkataza Sulemani kufuata miungu mingine, Sulemani hakutii amri ya Mwenyezi Mungu. \v 11 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa huu ndio msimamo wako, na hukushika agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitakunyang’anya ufalme na kumpa mmoja wa walio chini yako. \v 12 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. \v 13 Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua.” \s1 Adui za Sulemani \p \v 14 Kisha Mwenyezi Mungu akamwinua adui dhidi ya Sulemani, Hadadi, Mwedomu, kutoka ukoo wa ufalme wa Edomu. \v 15 Hapo awali Daudi alipokuwa akipigana na Edomu, Yoabu jemadari wa jeshi, aliyekuwa ameenda kuzika waliouawa, alikuwa amewaua wanaume wote katika Edomu. \v 16 Yoabu na Waisraeli wote walikaa huko kwa miezi sita, hadi walipomaliza kuwaangamiza wanaume wote huko Edomu. \v 17 Lakini Hadadi, akiwa bado mvulana mdogo, alikimbilia Misri akiwa na baadhi ya maafisa wa Edomu waliokuwa wamemhudumia baba yake. \v 18 Wakatoka Midiani wakaenda hadi Parani. Wakawachukua watu kutoka Parani, wakaenda nao Misri kwa Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimpa Hadadi nyumba na shamba, na pia chakula. \p \v 19 Farao akapendezwa sana na Hadadi, hata akampa dada ya mkewe, Malkia Tapenesi, awe mke wake. \v 20 Huyo dada yake Tapenesi akamzalia Hadadi mwana aliyeitwa Genubathi, ambaye alilelewa na Tapenesi katika jumba la kifalme. Huko, Genubathi akaishi pamoja na watoto wa Farao. \p \v 21 Alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kwamba Daudi amelala na baba zake, na kwamba Yoabu aliyekuwa jemadari wa jeshi pia amekufa. Ndipo Hadadi akamwambia Farao, “Niruhusu niende ili nirudi nchi yangu.” \p \v 22 Farao akauliza, “Umekosa nini hapa, kwamba unataka kurudi katika nchi yako?” \p Hadadi akajibu, “Hakuna, lakini niruhusu niende!” \p \v 23 Mungu akamwinua adui mwingine dhidi ya Sulemani, Rezoni mwana wa Eliada, aliyekuwa amemkimbia bwana wake Hadadezeri, mfalme wa Soba. \v 24 Akawakusanya watu, naye akawa kiongozi wa kundi la waasi, wakati Daudi alipoangamiza majeshi ya Soba; waasi walienda Dameski, mahali walipokaa na kumiliki. \v 25 Rezoni alikuwa adui wa Israeli kwa muda wote alioishi Sulemani, kuongezea matatizo yaliyosababishwa na Hadadi. Kwa hiyo Rezoni akatawala katika Aramu\f + \fr 11:25 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Shamu\fqa*\f* na akawa mkatili kwa Israeli. \s1 Yeroboamu anaasi dhidi ya Sulemani \p \v 26 Pia, Yeroboamu mwana wa Nebati aliasi dhidi ya mfalme. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Sulemani, Mwefraimu kutoka Sereda, ambaye mama yake alikuwa mjane aliyeitwa Serua. \p \v 27 Haya ndio maelezo ya jinsi alivyomwasi mfalme: Sulemani alikuwa amejenga Milo\f + \fr 11:27 \fr*\ft maana yake \ft*\fqa Boma la Ngome\fqa*\f* naye akawa ameziba mwanya katika ukuta wa mji wa Daudi baba yake. \v 28 Basi Yeroboamu alikuwa mtu mwenye nguvu na hodari; naye Sulemani alipoona jinsi kijana alivyofanya kazi yake, akamweka kuwa kiongozi wa kazi yote ya mikono ya nyumba ya Yusufu. \p \v 29 Karibu na wakati ule Yeroboamu alikuwa anatoka nje ya Yerusalemu, Ahiya nabii Mshiloni akakutana naye njiani, akiwa amevaa joho jipya. Hawa wawili walikuwa peke yao mashambani, \v 30 naye Ahiya akachukua joho jipya alilokuwa amevaa akalirarua vipande kumi na viwili. \v 31 Kisha akamwambia Yeroboamu, “Jichukulie vipande kumi, kwa kuwa hivi ndivyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemavyo: ‘Tazama, ninaenda kumnyang’anya Sulemani ufalme na kukupa makabila kumi. \v 32 Lakini kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na mji wa Yerusalemu, ambao nimeuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli, atakuwa na kabila moja. \v 33 Nitafanya haya kwa sababu wameniacha na kuabudu Ashtorethi mungu wa kike wa Wasidoni, Kemoshi mungu wa Wamoabu, na Moleki mungu wa Waamoni, nao hawakuenda katika njia zangu wala kufanya yaliyo sawa machoni pangu, wala kushika amri na sheria zangu kama Daudi, babaye Sulemani, alivyofanya. \p \v 34 “ ‘Lakini sitauondoa ufalme wote mkononi mwa Sulemani; nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu. \v 35 Nitauondoa ufalme kutoka mikononi mwa mwanawe na kukupa wewe makabila kumi. \v 36 Nitampa mwanawe kabila moja ili Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu. \v 37 Lakini wewe, Yeroboamu, nitakutwaa, nawe utatawala yale yote moyo wako unayotamani; utakuwa mfalme wa Israeli. \v 38 Ikiwa utafanya kila nitakalokuamuru, kuenenda katika njia zangu na kufanya yaliyo sawa mbele za macho yangu kwa kushika amri zangu na maagizo yangu kama alivyofanya Daudi mtumishi wangu, nitakuwa pamoja nawe. Nitakujengea ufalme utakaodumu kama ule niliomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli. \v 39 Nitawatesa wazao wa Daudi kwa ajili ya haya, lakini siyo milele.’ ” \p \v 40 Sulemani akajaribu kumuua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akakimbilia Misri, kwa Mfalme Shishaki, naye akakaa huko hadi Sulemani alipofariki. \s1 Kifo cha Sulemani \r (2 Nyakati 9:29-31) \p \v 41 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Sulemani, yote aliyoyafanya na hekima aliyoionesha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za Sulemani? \v 42 Sulemani alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. \v 43 Kisha Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi, baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 12 \s1 Waisraeli wamwasi Rehoboamu \r (2 Nyakati 10:1-19) \p \v 1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wameenda huko kumfanya mfalme. \v 2 Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Sulemani), akarudi kutoka Misri. \v 3 Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu; yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea Rehoboamu na kumwambia, \v 4 “Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini sasa tupunguzie kazi za kikatili na nira nzito aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.” \p \v 5 Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao. \p \v 6 Kisha Mfalme Rehoboamu akataka ushauri kwa wazee ambao walimtumikia Sulemani baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri niwajibu nini watu hawa?” \p \v 7 Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.” \p \v 8 Lakini Rehoboamu akakataa ushauri aliopewa na wazee, na akataka ushauri kwa vijana wa rika lake waliokuwa wakimtumikia. \v 9 Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu’?” \p \v 10 Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Watu hawa walikuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi.’ Wewe waambie, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. \v 11 Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwapiga mijeledi; mimi nitawapiga kwa nge.’ ” \p \v 12 Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.” \v 13 Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Alikataa ushauri alilopewa na wazee, \v 14 akafuata ushauri wa vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwapiga mijeledi; mimi nitawapiga kwa nge.” \v 15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwa Mwenyezi Mungu, ili kutimiza neno ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa amenena na Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia kwa Ahiya Mshiloni. \p \v 16 Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: \q1 “Je, tuna fungu gani kwa Daudi? \q2 Tuna urithi gani kwa mwana wa Yese? \q1 Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli! \q2 Angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” \m Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao. \v 17 Lakini kwa habari ya Waisraeli walioishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado. \p \v 18 Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake la vita na kutorokea Yerusalemu. \v 19 Hivyo, Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo. \p \v 20 Waisraeli wote waliposikia kwamba Yeroboamu amerudi, wakatuma watu na kumwita kwenye kusanyiko na kumfanya mfalme juu ya Israeli yote. Ni kabila la Yuda peke yake lililobaki kuwa tiifu kwa nyumba ya Daudi. \p \v 21 Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda na kabila la Benyamini, vijana wenye uwezo elfu mia moja na themanini, ili kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani. \p \v 22 Lakini neno la Mungu likamjia Shemaya mtu wa Mungu: \v 23 “Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na nyumba yote ya Yuda na Benyamini, na watu wengine wote, \v 24 ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu, Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Mwenyezi Mungu na kurudi nyumbani, kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameagiza. \s1 Ndama za dhahabu huko Betheli na Dani \p \v 25 Kisha Yeroboamu akaimarisha Shekemu, na kuuzungushia ngome katika nchi ya vilima ya Efraimu, na akaishi huko. Kutoka huko, akaenda akajenga Penueli\f + \fr 12:25 \fr*\ft au \ft*\fqa Penieli\fqa*\f*. \p \v 26 Yeroboamu akawaza moyoni mwake, “Kuna uwezekano wa ufalme kurudia nyumba ya Daudi. \v 27 Kama watu hawa watapanda kwenda kutoa dhabihu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu, mioyo yao itamrudia bwana wao, Rehoboamu mfalme wa Yuda. Wataniua mimi na kurudi kwa Mfalme Rehoboamu.” \p \v 28 Baada ya kutafuta ushauri, mfalme akatengeneza ndama wawili wa dhahabu. Akawaambia watu, “Ni gharama kubwa kwenu kukwea kwenda Yerusalemu. Hii hapa miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.” \v 29 Ndama mmoja akamweka Betheli, na mwingine akamweka Dani. \v 30 Nalo jambo hili likawa dhambi, watu wakawa wanaenda hadi Dani kumwabudu huyo aliyewekwa huko. \p \v 31 Yeroboamu akajenga nyumba za ibada katika mahali pa juu pa kuabudia, na kuwateua makuhani kutoka watu wa aina zote, ijapokuwa hawakuwa Walawi. \v 32 Pia Yeroboamu akaanzisha sikukuu katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, kama sikukuu iliyokuwa ikifanyika huko Yuda, na akatoa dhabihu juu ya madhabahu. Haya aliyafanya huko Betheli, akitoa dhabihu kwa ndama alizotengeneza. Huko Betheli akawaweka makuhani katika mahali pa juu pa kuabudia miungu aliyotengeneza. \v 33 Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouchagua mwenyewe, alitoa dhabihu juu ya madhabahu aliyokuwa amejenga huko Betheli. Kwa hiyo akaanzisha sikukuu kwa ajili ya Waisraeli, na akapanda madhabahuni kutoa sadaka. \c 13 \s1 Mtu wa Mwenyezi Mungu kutoka Yuda \p \v 1 Kwa neno la Mwenyezi Mungu, mtu wa Mungu alifika Betheli kutoka Yuda wakati Yeroboamu alipokuwa amesimama kando ya madhabahu ili kutoa sadaka. \v 2 Akapiga kelele dhidi ya madhabahu kwa neno la Mwenyezi Mungu: “Ee madhabahu, ee madhabahu! Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika nyumba ya Daudi. Juu yako atawatoa dhabihu makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia ambao hutoa sadaka hapa, nayo mifupa ya wanadamu itateketezwa juu yako.’ ” \v 3 Siku hiyo hiyo, mtu wa Mungu akatoa ishara: “Hii ndiyo ishara Mwenyezi Mungu aliyotangaza: Madhabahu haya yatapasuka na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.” \p \v 4 Mfalme Yeroboamu aliposikia kile mtu wa Mungu alichosema, alipopiga kelele dhidi ya madhabahu huko Betheli, akanyoosha mkono wake kutoka madhabahuni na kusema, “Mkamateni!” Lakini mkono aliounyoosha kumwelekea yule mtu ukakauka kiasi kwamba hakuweza kuurudisha. \v 5 Pia, madhabahu yakapasuka na majivu yakamwagika, sawasawa na ishara iliyotolewa na mtu wa Mungu kwa neno la Mwenyezi Mungu. \p \v 6 Kisha mfalme akamwambia mtu wa Mungu, “Niombee kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ili mkono wangu upate kupona.” Kwa hiyo mtu wa Mungu akamwombea kwa Mwenyezi Mungu, nao mkono wa mfalme ukapona na kurudi ulivyokuwa hapo awali. \p \v 7 Mfalme akamwambia yule mtu wa Mungu, “Twende nyumbani mwangu upate chakula, nami nitakupa zawadi.” \p \v 8 Lakini yule mtu wa Mungu akamjibu mfalme, “Hata kama ungenipa nusu ya mali yako, nisingeenda pamoja nawe, wala nisingekula mkate au kunywa maji hapa. \v 9 Kwa kuwa niliagizwa kwa neno la Mwenyezi Mungu: ‘Kamwe usile mkate wala usinywe maji au kurudi kwa njia uliyojia.’ ” \v 10 Hivyo, akafuata njia nyingine na hakurudi kupitia njia aliyokuwa ameijia Betheli. \p \v 11 Basi kulikuwa na nabii fulani mzee aliyekuwa anaishi Betheli, ambaye wanawe walikuja kumwambia yote ambayo mtu wa Mungu alikuwa ameyafanya pale siku ile. Pia wakamwambia baba yao yale aliyomwambia mfalme. \v 12 Baba yao akawauliza, “Ameelekea njia gani?” Nao wanawe wakamwonesha ile njia yule mtu wa Mungu kutoka Yuda aliyopita. \v 13 Hivyo akawaambia wanawe, “Nitandikieni punda.” Walipokwisha kumtandikia punda, akampanda \v 14 na kumfuatilia yule mtu wa Mungu. Akamkuta ameketi chini ya mwaloni na kumuuliza, “Je, wewe ndiwe mtu wa Mungu kutoka Yuda?” \p Akamjibu, “Mimi ndiye.” \p \v 15 Basi nabii akamwambia, “Karibu nyumbani pamoja na mimi, ule.” \p \v 16 Yule mtu wa Mungu akasema, “Siwezi kurudi na kwenda nawe, wala siwezi kula mkate au kunywa maji pamoja nawe mahali hapa. \v 17 Nimeambiwa kwa neno la Mwenyezi Mungu: ‘Kamwe usile mkate au kunywa maji huko au kurudia njia uliyojia.’ ” \p \v 18 Yule nabii mzee akajibu, “Mimi pia ni nabii, kama wewe. Naye malaika alisema nami kwa neno la Mwenyezi Mungu: ‘Mrudishe aje katika nyumba yako ili apate kula mkate na kunywa maji.’ ” (Lakini alikuwa akimwambia uongo.) \v 19 Hivyo mtu wa Mungu akarudi pamoja naye na akala na kunywa katika nyumba yake. \p \v 20 Walipokuwa wameketi mezani, neno la Mwenyezi Mungu likamjia yule nabii mzee aliyemrudisha huyo mtu wa Mungu. \v 21 Akampazia sauti yule mtu wa Mungu aliyekuwa ametoka Yuda, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Umeasi neno la Mwenyezi Mungu na hukushika amri uliyopewa na Mwenyezi Mungu, Mungu wako. \v 22 Ulirudi, ukala mkate na kunywa maji mahali alipokuambia usile wala usinywe. Kwa hiyo maiti yako haitazikwa katika kaburi la baba zako.’ ” \p \v 23 Huyo mtu wa Mungu alipomaliza kula na kunywa, nabii aliyekuwa amemrudisha akamtandikia punda wake. \v 24 Alipokuwa akienda akakutana na simba njiani, akamuua na maiti yake ikabwagwa barabarani, huku punda wake na simba wakiwa wamesimama kando yake. \v 25 Watu waliopita pale, waliona maiti iliyokuwa imebwagwa, simba akiwa amesimama kando yake. Nao wakaenda kutoa habari katika mji ambao nabii mzee alikuwa anaishi. \p \v 26 Yule nabii aliyekuwa amemrudisha kutoka safari yake aliposikia habari hii akasema, “Ni yule mtu wa Mungu aliyeliasi neno la Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amemtoa kwa simba, ambaye amemrarua na kumuua, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu lilivyokuwa limemwonya.” \p \v 27 Nabii akawaambia wanawe, “Nitandikieni punda,” nao wakafanya hivyo. \v 28 Akaondoka na akakuta maiti imetupwa barabarani, punda na simba wakiwa wamesimama kando yake. Simba hakuwa amekula ile maiti wala kumrarua punda. \v 29 Basi yule nabii mzee akachukua maiti ya mtu wa Mungu, akailaza juu ya punda na akairudisha katika mji wake, ili amwombolezee na kumzika. \v 30 Kisha akailaza ile maiti katika kaburi lake huyo nabii mzee, nao wakaomboleza juu yake na kusema, “Ee ndugu yangu!” \p \v 31 Baada ya kumzika, akawaambia wanawe, “Nitakapokufa, mnizike kwenye kaburi alimozikwa huyu mtu wa Mungu; lazeni mifupa yangu kando ya mifupa yake. \v 32 Kwa maana ujumbe alioutangaza kwa neno la Mwenyezi Mungu dhidi ya madhabahu huko Betheli, na dhidi ya nyumba zote za ibada katika mahali pa juu pa kuabudia ndani ya miji ya Samaria, hakika utatimia.” \p \v 33 Hata baada ya haya, Yeroboamu hakubadili njia zake mbaya, lakini mara nyingine tena akaweka makuhani kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia kutoka watu wa aina zote. Yeyote aliyetaka kuwa kuhani alimweka wakfu kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia. \v 34 Hii ilikuwa ndiyo dhambi ya nyumba ya Yeroboamu ambayo iliisababishia kuanguka na kuangamia kwake hadi kutoweka kwenye uso wa dunia. \c 14 \s1 Unabii wa Ahiya dhidi ya Yeroboamu \p \v 1 Wakati ule, Abiya mwana wa Yeroboamu akaugua, \v 2 naye Yeroboamu akamwambia mke wake, “Nenda ukajibadilishe, ili watu wasijue kwamba wewe ni mke wa Yeroboamu. Kisha uende Shilo. Nabii Ahiya, yule aliyeniambia kuwa nitakuwa mfalme wa watu hawa, yuko huko. \v 3 Chukua mikate kumi, maandazi kadhaa na gudulia la asali na umwendee. Atakuambia kitakachotokea kwa kijana.” \v 4 Basi mke wa Yeroboamu akafanya kama mumewe alivyosema, akaenda kwenye nyumba ya Ahiya huko Shilo. \p Wakati huu Ahiya alikuwa kipofu naye alishindwa kuona kwa sababu ya umri wake. \v 5 Lakini Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Ahiya, “Mke wa Yeroboamu anakuja kukuuliza kuhusu mwanawe, kwa kuwa ni mgonjwa, nawe utamjibu hivi na hivi. Atakapowasili, atajifanya kuwa ni mtu mwingine.” \p \v 6 Hivyo, Ahiya aliposikia kishindo cha hatua zake mlangoni, akasema, “Karibu ndani, mke wa Yeroboamu. Kwa nini unajifanya kuwa si wewe? Nimetumwa kwako kukupa habari mbaya. \v 7 Nenda, ukamwambie Yeroboamu kwamba hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Nilikuinua miongoni mwa watu na kukufanya mtawala wa watu wangu Israeli. \v 8 Nikararua ufalme kutoka kwa nyumba ya Daudi na kukupa wewe, lakini hukuwa kama mtumishi wangu Daudi, ambaye aliyashika maagizo yangu na kunifuata kwa moyo wake wote, akifanya tu lile lililokuwa sawa machoni pangu. \v 9 Umefanya maovu mengi kuliko wote waliokutangulia. Umejitengenezea miungu mingine, sanamu za chuma, umenighadhibisha na kunigeuka. \p \v 10 “ ‘Kwa sababu hii, nitaleta maafa juu ya nyumba ya Yeroboamu. Nitakatilia mbali kutoka kwa Yeroboamu kila mzaliwa wa mwisho wa kiume katika Israeli, mtumwa au mtu huru. Nitachoma nyumba ya Yeroboamu hadi iteketee yote kama mtu anavyochoma kinyesi. \v 11 Mbwa watawala walio wa nyumba ya Yeroboamu watakaofia ndani ya mji, na ndege wa angani watawala wale watakaofia mashambani. Mwenyezi Mungu amenena!’ \p \v 12 “Lakini wewe, rudi nyumbani. Utakapofika mji wako, kijana atakufa. \v 13 Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Ni yeye pekee wa nyumba ya Yeroboamu atakayezikwa, kwa sababu ni yeye tu ndani ya nyumba ya Yeroboamu ambaye Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ameona kitu chema kwake. \p \v 14 “Mwenyezi Mungu atajiinulia mwenyewe mfalme juu ya Israeli ambaye ataikatilia mbali jamaa ya Yeroboamu. Siku hiyo itakuwa lini? Hata sasa yameanza kutokea. \v 15 Naye Mwenyezi Mungu ataipiga Israeli, hata iwe kama mwanzi unaoyumbayumba kwenye maji. Ataing’oa Israeli kutoka nchi hii nzuri aliyowapa baba zao na kuwatawanya ng’ambo ya Mto\f + \fr 14:15 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Mto Frati\fqa*\f*, kwa sababu wamemghadhibisha Mwenyezi Mungu kwa kutengeneza nguzo za Ashera. \v 16 Naye atawaacha Israeli kwa sababu ya dhambi Yeroboamu alizozitenda na kuisababisha Israeli kuzitenda.” \p \v 17 Kisha, mke wa Yeroboamu akainuka, akaondoka kwenda Tirsa. Mara alipokanyaga kizingiti cha mlango, kijana akafa. \v 18 Wakamzika na Israeli yote ikamwombolezea, kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema kupitia kwa mtumishi wake, nabii Ahiya. \p \v 19 Matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, vita vyake na jinsi alivyotawala, vimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. \v 20 Yeroboamu akawatawala kwa miaka ishirini na mbili, kisha akalala na baba zake. Naye Nadabu mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Rehoboamu mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 11:5–12:15) \p \v 21 Rehoboamu mwana wa Sulemani alikuwa mfalme wa Yuda. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipoanza kuwa mfalme, naye akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji ambao Mwenyezi Mungu alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili apate kuliweka humo Jina lake. Mama yake aliitwa Naama, na alikuwa Mwamoni. \p \v 22 Yuda wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Kwa dhambi walizotenda wakachochea hasira yake yenye wivu kuliko baba zao walivyofanya. \v 23 Pia wakajijengea mahali pa juu pa kuabudia, mawe ya kuabudiwa, na nguzo za Ashera juu ya kila kilima kilichoinuka na kila mti uliotanda. \v 24 Kulikuwa na hata mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu katika nchi. Watu wakajiingiza katika kutenda machukizo ya mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliyafukuza mbele ya Waisraeli. \p \v 25 Katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu. \v 26 Akachukua hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao zote za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa amezitengeneza. \v 27 Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme. \v 28 Kila wakati mfalme alipoenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, walinzi walizichukua hizo ngao, na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi. \p \v 29 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Rehoboamu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 30 Kulikuwa na vita vinavyoendelea kati ya Rehoboamu na Yeroboamu. \v 31 Naye Rehoboamu akalala na baba zake, na akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mama yake aliitwa Naama; alikuwa Mwamoni. Naye Abiya\f + \fr 14:31 \fr*\ft au \ft*\fqa Abiyamu\fqa*\f* mwanawe akawa mfalme baada yake. \c 15 \s1 Abiya mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 13:1–14:1) \p \v 1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda, \v 2 naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu\f + \fr 15:2 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Absalomu\fqa*\f*. \p \v 3 Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa. \v 4 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, Mwenyezi Mungu, Mungu wake, akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale baada yake ili kuifanya Yerusalemu kuwa imara. \v 5 Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, wala hakushindwa kuzishika amri zote za Mwenyezi Mungu siku zote za maisha yake, isipokuwa kwa suala la Uria, Mhiti. \p \v 6 Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya. \v 7 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. \v 8 Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Asa mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 15:16–16:6) \p \v 9 Katika mwaka wa ishirini wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda, \v 10 naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na moja. Bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu. \p \v 11 Asa akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama alivyokuwa ametenda Daudi, baba yake. \v 12 Akawafukuza mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu kutoka nchi, na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza. \v 13 Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye wadhifa wake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. \v 14 Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu maisha yake yote. \v 15 Akaleta ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu fedha na dhahabu na vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu. \p \v 16 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha, mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao. \v 17 Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome katika mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia katika nchi ya Mfalme Asa wa Yuda. \p \v 18 Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu zilizokuwa zimeachwa katika hazina za Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika jumba lake la kifalme. Kisha akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu\f + \fr 15:18 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Shamu\fqa*\f*, aliyekuwa akitawala Dameski. \v 19 Akasema, “Na tufanye mkataba kati yangu na wewe, kama ilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea zawadi ya fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha, mfalme wa Israeli ili aniondokee.” \p \v 20 Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote, pamoja na Naftali. \v 21 Baasha aliposikia jambo hili, akasimamisha ujenzi wa Rama, akaenda kuishi Tirsa. \v 22 Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumwacha hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akizitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyo Benyamini na Mispa. \p \v 23 Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Hata hivyo, katika uzee wake alishikwa na ugonjwa wa miguu. \v 24 Kisha Asa akalala na baba zake, naye akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi, baba yake. Naye Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Nadabu mfalme wa Israeli \p \v 25 Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili. \v 26 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, aliyoisababisha Israeli kutenda. \p \v 27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akapanga njama dhidi ya Nadabu, naye akamuua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walikuwa wameuzingira. \v 28 Baasha akamuua Nadabu katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, naye Baasha akawa mfalme baada yake. \p \v 29 Mara tu alipoanza kutawala, aliwaua watu wote wa nyumba ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu hata mtu mmoja akiwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni. \v 30 Haya yalitendeka kwa sababu ya dhambi alizozitenda Yeroboamu, zilizosababisha Israeli kutenda dhambi, na kwa sababu alimkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. \p \v 31 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Nadabu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \p \v 32 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli wakati wote wa utawala wao. \s1 Baasha mfalme wa Israeli \p \v 33 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirsa, naye akatawala kwa miaka ishirini na nne. \v 34 Akatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akienenda katika njia ya Yeroboamu na dhambi yake, aliyosababisha Israeli kuitenda. \c 16 \p \v 1 21 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yehu mwana wa Hanani dhidi ya Baasha, kusema: \v 2 “Nilikuinua kutoka mavumbini na kukufanya mtawala wa watu wangu Israeli, lakini ukaenenda katika njia za Yeroboamu na kusababisha watu wangu Israeli kutenda dhambi na kunikasirisha kwa dhambi zao. \v 3 Basi nitamwangamiza Baasha pamoja na nyumba yake, nami nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwanawe Nebati. \v 4 Mbwa watawala walio wa nyumba ya Baasha watakaofia ndani ya mji, na ndege wa angani watawala wale watakaofia mashambani.” \p \v 5 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Baasha, aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 6 Baasha akalala na baba zake naye akazikwa huko Tirsa. Naye Ela mwanawe akawa mfalme baada yake. \p \v 7 Zaidi ya hayo, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa nabii Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa Mwenyezi Mungu, akimkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu aliyoiangamiza. \s1 Ela mfalme wa Israeli \p \v 8 Katika mwaka wa ishirini na sita wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala huko Tirsa kwa miaka miwili. \p \v 9 Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akapanga njama dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirsa, akilewa katika nyumba ya Arsa, aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirsa. \v 10 Zimri akaingia, akampiga na kumuua katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda. Kisha Zimri akawa mfalme baada yake. \p \v 11 Mara tu alipoanza kutawala na kukalia kiti chake cha kifalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki. \v 12 Hivyo, Zimri akawaangamiza jamaa yote ya Baasha, kama Mwenyezi Mungu alivyonena dhidi ya Baasha kupitia kwa nabii Yehu: \v 13 kwa sababu ya dhambi zote Baasha na mwanawe Ela walizokuwa wametenda na wakasababisha Israeli kuzitenda, basi wakamkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa sanamu zao batili. \p \v 14 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Ela, na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \s1 Zimri mfalme wa Israeli \p \v 15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirsa siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti. \v 16 Waisraeli waliokuwa kambini waliposikia kuwa Zimri amepanga njama ya kumuua mfalme, wakamtangaza Omri, jemadari wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli yote siku hiyo hiyo huko kambini. \v 17 Ndipo Omri na Waisraeli wote pamoja naye wakaondoka Gibethoni na kuizingira Tirsa. \v 18 Zimri alipoona kuwa mji umechukuliwa, alienda ndani ya ngome ya jumba la kifalme na kulichoma moto hilo jumba na kujiteketeza ndani yake. Kwa hiyo akafa, \v 19 kwa sababu ya dhambi alizotenda, akifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu na kuenenda katika njia za Yeroboamu na katika dhambi alizotenda na kusababisha Israeli kuzifanya. \p \v 20 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Zimri, na uasi alioutenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \s1 Omri mfalme wa Israeli \p \v 21 Kisha, watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamuunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme, na nusu nyingine wakamuunga mkono Omri. \v 22 Lakini wafuasi wa Omri wakajionesha kuwa wenye nguvu kuliko wale wa Tibni, mwana wa Ginathi. Hivyo Tibni akafa, na Omri akawa mfalme. \p \v 23 Katika mwaka wa thelathini na moja wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na mbili, sita kati ya hiyo katika Tirsa. \v 24 Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili\f + \fr 16:24 \fr*\ft Talanta 2 za fedha ni sawa na kilo 70.\ft*\f* za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho. \p \v 25 Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia. \v 26 Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa sanamu zao batili. \p \v 27 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na mafanikio aliyokuwa nayo, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 28 Omri akalala na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Ahabu mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Ahabu afanywa mfalme wa Israeli \p \v 29 Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na mbili. \v 30 Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni pa Mwenyezi Mungu kuliko yeyote aliyemtangulia. \v 31 Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu. \v 32 Akatengeneza madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali alilolijenga huko Samaria. \v 33 Pia Ahabu alitengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia. \p \v 34 Wakati wa Ahabu, Hieli ule Mbetheli, akaijenga Yeriko upya. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kama Mwenyezi Mungu alivyonena kupitia kwa Yoshua, mwana wa Nuni. \c 17 \s1 Ilya atangaza ukame \p \v 1 Basi Ilya Mtishbi, kutoka Tishbi katika Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli ninayemtumikia, aishivyo, hapatakuwa na umande wala mvua katika miaka kadhaa ijayo, isipokuwa kwa neno langu.” \s1 Ilya alishwa na kunguru \p \v 2 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likamjia Ilya, kusema, \v 3 “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche karibu na Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani. \v 4 Utakunywa maji kutoka kile kijito, nami nimeagiza kunguru wakulishe huko.” \p \v 5 Naye akafanya kama alivyoambiwa na Mwenyezi Mungu. Akaenda katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani na akakaa huko. \v 6 Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka kile kijito. \p \v 7 Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi. \s1 Ilya na mjane wa Sarepta \p \v 8 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likamjia Ilya, kusema, \v 9 “Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni, ukae huko. Nimemwagiza mjane wa huko ili akuhudumie.” \v 10 Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, alimkuta mjane akiokota kuni pale. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.” \v 11 Alipokuwa anaenda kumletea, akamwita akasema, “Tafadhali niletee pia kipande cha mkate.” \p \v 12 Akamjibu, “Hakika kama Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aishivyo, sina mkate wowote, isipokuwa konzi moja ya unga kwenye chungu, na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili tule, kiishe, tukafe.” \p \v 13 Ilya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unitengenezee mkate mdogo kutoka vile ulivyo navyo kisha uniletee na ndipo utayarishe chochote kwa ajili yako na mwanao. \v 14 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Kile chungu cha unga hakitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ile Mwenyezi Mungu atakapoleta mvua juu ya nchi.’ ” \p \v 15 Akaondoka na kufanya kama Ilya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Ilya, yule mwanamke na jamaa yake. \v 16 Kwa kuwa kile chungu hakikuisha unga na ile chupa ya mafuta haikukauka sawasawa na lile neno la Mwenyezi Mungu lililonenwa na Ilya. \p \v 17 Baada ya muda, mwana wa yule mwanamke mwenye nyumba akaugua. Hali yake ikaendelea kuwa mbaya sana, na hatimaye akaacha kupumua. \v 18 Yule mjane akamwambia Ilya, “Una nini dhidi yangu, ewe mtu wa Mungu? Umekuja ili kunikumbusha dhambi yangu, na kusababisha kifo cha mwanangu?” \p \v 19 Ilya akamjibu, “Nipe mwanao.” Ilya akampokea kutoka kifuani mwake, akambeba hadi chumba cha juu alipokuwa anaishi, akamlaza kitandani pake. \v 20 Kisha akamlilia Mwenyezi Mungu, akasema “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi kwake, kwa kusababisha mwanawe kufa?” \v 21 Kisha akajinyoosha juu ya kijana mara tatu na kumlilia Mwenyezi Mungu, akisema, “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!” \p \v 22 Mwenyezi Mungu akasikia kilio cha Ilya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. \v 23 Ilya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumba chake cha juu, akamshusha, akampa mama yake na kusema, “Tazama, mwanao yu hai!” \p \v 24 Ndipo yule mwanamke akamwambia Ilya, “Sasa ninajua kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la Mwenyezi Mungu kutoka kinywani mwako ni kweli.” \c 18 \s1 Ilya na Obadia \p \v 1 Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Ilya kusema, “Nenda ukajioneshe kwa Ahabu nami nitaleta mvua juu ya nchi.” \v 2 Kwa hiyo Ilya akaenda kujionesha kwa Ahabu. \p Wakati huo njaa ilikuwa kali sana katika Samaria, \v 3 naye Ahabu alikuwa amemwita Obadia aliyekuwa msimamizi wa jumba la mfalme. (Obadia alimcha Mwenyezi Mungu sana. \v 4 Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa Mwenyezi Mungu, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja, na akawa akiwapa chakula na maji.) \v 5 Ahabu alikuwa amemwambia Obadia, “Nenda katika nchi yote kwenye vijito vyote na mabonde. Huenda tunaweza kupata majani ya kuwalisha farasi na nyumbu ili wapate kuishi, tusilazimike kumuua hata mmoja wa wanyama wetu.” \v 6 Kwa hiyo wakagawanya nchi waliyokusudia kutafuta majani, Ahabu akaenda upande mmoja na Obadia upande mwingine. \p \v 7 Obadia alipokuwa akitembea njiani, Ilya akakutana naye. Obadia akamtambua, akasujudu, uso wake ukigusa chini, na kusema, “Je, hivi kweli ni wewe, bwana wangu Ilya?” \p \v 8 Ilya akamjibu, “Ndiyo, nenda ukamwambie bwana wako, ‘Ilya yuko hapa.’ ” \p \v 9 Obadia akamuuliza, “Ni kosa gani nimefanya, hata ukaamua kumkabidhi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu ili aniue? \v 10 Hakika kama Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aishivyo, hakuna taifa hata moja au ufalme ambapo bwana wangu hajamtuma mtu kukutafuta. Kila wakati taifa au ufalme walipodai kwamba haupo huko, aliwafanya waape kwamba hawakuweza kukupata. \v 11 Lakini sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kusema, ‘Ilya yuko hapa.’ \v 12 Sijui ni wapi Roho wa Mwenyezi Mungu ataamua kukupeleka wakati nitakapokuacha. Nikienda kumwambia Ahabu na asikupate, ataniua; lakini mimi mtumishi wako nimekuwa nikimwabudu Mwenyezi Mungu tangu ujana wangu. \v 13 Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa Mwenyezi Mungu? Niliwaficha manabii wa Mwenyezi Mungu mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, na nikawapatia chakula na maji. \v 14 Nawe sasa unaniambia niende kwa bwana wangu na kumwambia, ‘Ilya yuko hapa.’ Yeye ataniua!” \p \v 15 Ilya akasema, “Kama Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni aishivyo, yeye ninayemtumikia, hakika nitajionesha kwa Ahabu leo.” \s1 Ilya juu ya Mlima Karmeli \p \v 16 Basi Obadia akaenda kukutana na Ahabu na kumwambia; naye Ahabu akaenda kukutana na Ilya. \v 17 Ahabu alipomwona Ilya, akamwambia, “Je, ni wewe, mtaabishaji wa Israeli?” \p \v 18 Ilya akamjibu, “Mimi sijaitaabisha Israeli. Lakini wewe na jamaa ya baba yako ndio mnaofanya hivyo. Mmeziacha amri za Mwenyezi Mungu na mkafuata Mabaali. \v 19 Sasa waite watu kutoka Israeli yote tukutane nao juu ya Mlima Karmeli. Nawe uwalete hao manabii wa Baali mia nne na hamsini na hao manabii mia nne wa Ashera, walao chakula mezani mwa Yezebeli.” \p \v 20 Ndipo Ahabu akatuma ujumbe katika Israeli yote na kuwakusanya manabii hao juu ya Mlima Karmeli. \v 21 Ilya akasimama mbele ya watu na kusema, “Mtayumbayumba katikati ya mawazo mawili hadi lini? Ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye.” \p Lakini watu hawakusema kitu. \p \v 22 Kisha Ilya akawaambia, “Ni mimi peke yangu nabii wa Mwenyezi Mungu aliyebaki, lakini Baali ana manabii mia nne na hamsini. \v 23 Leteni mafahali wawili. Wao na wajichagulie mmoja, wamkate vipande vipande na wamweke juu ya kuni, lakini wasimwashie moto. Nitamwandaa huyo fahali mwingine na kumweka juu ya kuni, lakini sitamwashia moto. \v 24 Kisha mliitie jina la mungu wenu, nami nitaliitia jina la Mwenyezi Mungu yule ambaye atajibu kwa moto, huyo ndiye Mungu.” \p Kisha watu wote wakasema, “Hilo unalosema ni jema.” \p \v 25 Ilya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja kati ya hawa mafahali na mwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi mko wengi sana. Liitieni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.” \v 26 Kwa hiyo wakamchukua yule fahali waliyepewa, nao wakamwandaa. \p Kisha wakaliitia jina la Baali kutoka asubuhi hadi adhuhuri, wakapiga kelele, “Ee Baali, utujibu!” Lakini hapakuwa na jibu; hakuna aliyejibu. Nao wakacheza kuizunguka madhabahu waliyoijenga. \p \v 27 Wakati wa adhuhuri, Ilya akaanza kuwadhihaki, akisema, “Pigeni kelele zaidi! Hakika yeye ni mungu! Labda amezama katika mawazo mazito, au ana shughuli nyingi, au amesafiri. Labda amelala usingizi mzito, naye ni lazima aamshwe.” \v 28 Kwa hiyo wakapiga kelele zaidi na kama ilivyokuwa desturi yao wakajichanja kwa visu na vyembe, hadi damu ikachuruzika. \v 29 Adhuhuri ikapita, nao wakaendelea na utabiri wao wa kiwazimu hadi wakati wa dhabihu ya jioni. Lakini hapakuwa na itikio, hakuna aliyejibu, na hakuna aliyezingatia. \p \v 30 Kisha Ilya akawaambia watu wote, “Sogeeni karibu nami.” Wakamkaribia, naye akaikarabati madhabahu ya Mwenyezi Mungu, iliyokuwa imeharibiwa. \v 31 Ilya akachukua mawe kumi na mbili, moja kwa ajili ya kila kabila la wana wa Yakobo, ambaye neno la Mwenyezi Mungu lilimjia, kusema, “Jina lako litakuwa Israeli.” \v 32 Kwa mawe hayo, akajenga madhabahu katika jina la Mwenyezi Mungu, na akachimba handaki kuizunguka, ukubwa wa kutosha vipimo viwili vya mbegu. \v 33 Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, “Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni.” \p \v 34 Akawaambia, “Fanyeni hivyo tena.” Nao wakafanya hivyo tena. \p Akaagiza, “Fanyeni kwa mara ya tatu.” Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu. \v 35 Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki. \p \v 36 Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Ilya akasogea mbele na kuomba, akisema: “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kama ulivyoagiza. \v 37 Unijibu, Ee Mwenyezi Mungu! Unijibu ili watu hawa wajue kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena.” \p \v 38 Kisha moto wa Mwenyezi Mungu ukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki. \p \v 39 Watu wote walipoona hili, wakaanguka kifudifudi na kulia, “Mwenyezi Mungu: yeye ndiye Mungu! Mwenyezi Mungu: yeye ndiye Mungu!” \p \v 40 Kisha Ilya akawaamuru, “Wakamateni hao manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja atoroke!” Wakawakamata, naye Ilya akawaleta Bonde la Kishoni na kuwachinja huko. \p \v 41 Ilya akamwambia Ahabu, “Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa.” \v 42 Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Ilya akapanda kileleni mwa Karmeli, akainama hadi chini, na kuweka kichwa chake katikati ya magoti. \p \v 43 Akamwambia mtumishi wake, “Nenda ukatazame kuelekea bahari.” Akaenda na kutazama. \p Akasema, “Hakuna kitu chochote huko.” \p Mara saba Ilya akasema, “Nenda tena.” \p \v 44 Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, “Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini.” \p Hivyo Ilya akasema, “Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Tandika gari lako la vita, ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ ” \p \v 45 Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli. \v 46 Nguvu za Mwenyezi Mungu zikamjia Ilya, naye akajikaza viuno, akakimbia mbele ya Ahabu njia yote hadi ingilio la Yezreeli. \c 19 \s1 Ilya akimbilia Horebu \p \v 1 Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Ilya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. \v 2 Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Ilya, kusema, “Miungu waniadhibu vikali zaidi, ikiwa kesho wakati kama huu sitakuwa nimeondoa uhai wako kama mmoja wa hao manabii.” \p \v 3 Ilya aliogopa, na akatoroka kuokoa maisha yake. Alipofika Beer-Sheba katika Yuda, akamwacha mtumishi wake huko, \v 4 lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, Mwenyezi Mungu, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.” \v 5 Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi. \p Mara malaika akamgusa na kumwambia, “Inuka ule.” \v 6 Akatazama pande zote, na hapo karibu na kichwa chake palikuwa na mkate uliookwa kwenye makaa ya moto, na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena. \p \v 7 Yule malaika wa Mwenyezi Mungu akaja tena mara ya pili, akamgusa na kumwambia, “Inuka ule, kwa kuwa bado una safari ndefu mbele yako.” \v 8 Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana hadi akafika Horebu, mlima wa Mungu. \v 9 Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule. \s1 Mwenyezi Mungu amtokea Ilya \p Nalo neno la Mwenyezi Mungu likamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Ilya?” \p \v 10 Akajibu, “Nimekuwa nikifanya bidii sana kwa ajili ya Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Waisraeli wamelikataa agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi peke yangu niliyebaki, sasa wananitafuta ili waniue pia.” \v 11 Mwenyezi Mungu akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kupita hapo.” \p Kisha upepo mzito na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la ardhi, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo kwenye lile tetemeko. \v 12 Baada ya tetemeko la ardhi moto ukaja, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona. \v 13 Ilya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mlango wa pango. \p Kisha ile sauti ikamwambia, “Ilya, unafanya nini hapa?” \p \v 14 Akajibu, “Nimekuwa nikifanya bidii sana kwa ajili ya Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Waisraeli wamelikataa agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi peke yangu niliyebaki, sasa wananitafuta ili waniue pia.” \p \v 15 Mwenyezi Mungu akamwambia, “Rudi kwa njia uliyoijia, uende kwenye Jangwa la Dameski. Utakapofika huko, mpake Hazaeli mafuta awe mfalme wa Aramu\f + \fr 19:15 \fr*\ft yaani \ft*\fqa Shamu\fqa*\f*. \v 16 Pia mpake mafuta Yehu, mwana wa Nimshi awe mfalme wa Israeli, na umpake mafuta Al-Yasa mwana wa Shafati kutoka Abel-Mehola awe nabii baada yako. \v 17 Yehu atamuua yeyote atakayeutoroka upanga wa Hazaeli, naye Al-Yasa atamuua yeyote atakayeutoroka upanga wa Yehu. \v 18 Hata sasa nimeweka akiba ya watu elfu saba katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, na wote ambao midomo yao haijambusu.” \s1 Wito wa Al-Yasa \p \v 19 Hivyo Ilya akaondoka huko na kumkuta Al-Yasa mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliiongoza ile jozi ya kumi na mbili. Ilya akamwendea, na kumvisha vazi lake. \v 20 Kisha Al-Yasa akawaacha maksai wake, akamkimbilia Ilya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.” \p Ilya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekufanya nini?” \p \v 21 Basi Al-Yasa akamwacha Ilya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Ilya, akamtumikia. \c 20 \s1 Ben-Hadadi aishambulia Samaria \p \v 1 Basi, Ben-Hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote. Akifuatana na wafalme thelathini na wawili wakiwa na farasi na magari ya vita, akakwea kuuzingira Samaria na kuishambulia kwa jeshi. \v 2 Akawatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi: \v 3 ‘Fedha yako na dhahabu yako ni vyangu; nao wake zako walio wazuri sana na watoto ni wangu.’ ” \p \v 4 Mfalme wa Israeli akajibu, “Iwe kama usemavyo, bwana wangu mfalme. Mimi na vyote nilivyo navyo ni mali yako.” \p \v 5 Wale wajumbe wakaja tena na kusema, “Hivi ndivyo asemavyo Ben-Hadadi: ‘Nimewatuma kutaka fedha yako na dhahabu, wake zako na watoto wako. \v 6 Lakini kesho wakati kama huu, nitawatuma maafisa wangu kukagua jumba lako la kifalme na nyumba za maafisa wako. Watatwaa kitu unachokithamini nao watakichukua.’ ” \p \v 7 Mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi, akawaambia, “Tazama jinsi mtu huyu anavyochochea matatizo! Alipotuma apelekewe wake zangu na watoto wangu, fedha zangu na dhahabu yangu, sikumkatalia.” \p \v 8 Wazee na watu wote wakajibu, “Usimsikilize, wala usiyakubali matakwa yake.” \p \v 9 Kwa hiyo akawajibu wajumbe wa Ben-Hadadi, “Mwambieni bwana wangu mfalme, ‘Mtumishi wako atafanya yote uliyoyadai mwanzoni, lakini dai hili la sasa siwezi kulitekeleza.’ ” Wakaondoka na kupeleka jibu kwa Ben-Hadadi. \p \v 10 Kisha Ben-Hadadi akatuma ujumbe mwingine kwa Ahabu, kusema, “Miungu waniadhibu vikali zaidi ikiwa vumbi la Samaria litatosheleza konzi moja ya kila mtu ya wale wanaofuatana nami.” \p \v 11 Mfalme wa Israeli akajibu, “Mwambieni, ‘Yule anayevaa mavazi ya vita asije akajisifu kama yule anayevua.’ ” \p \v 12 Ben-Hadadi alisikia ujumbe huu wakati yeye na wafalme walikuwa wakinywa katika mahema yao, akawaamuru watu wake, “Jiandaeni kushambulia.” Kwa hiyo wakajiandaa kushambulia mji. \s1 Ahabu amshinda Ben-Hadadi \p \v 13 Wakati huo huo nabii akamjia Ahabu, mfalme wa Israeli na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Je, unaona jeshi hili kubwa? Nitalitia mkononi mwako leo, nawe utajua kwamba mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 14 Ahabu akauliza, “Ni nani atakayefanya hili?” \p Nabii akamjibu, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Maafisa vijana majemadari wa majimbo watafanya hili.’ ” \p Akauliza, “Ni nani atakayeanzisha vita?” \p Nabii akamjibu, “Ni wewe.” \p \v 15 Hivyo, Ahabu akawaita maafisa vijana wapatao mia mbili thelathini na wawili (232) waliokuwa chini ya majemadari wa majimbo. Kisha akawakusanya Waisraeli waliobaki, ambao idadi yao walikuwa elfu saba. \v 16 Wakaondoka wakati wa adhuhuri, Ben-Hadadi na wale wafalme thelathini na wawili walioungana naye walipokuwa katika mahema yao wakilewa. \v 17 Maafisa vijana majemadari wa majimbo waliondoka kwanza. \p Wakati huu Ben-Hadadi alikuwa amewatuma wapelelezi, ambao walileta taarifa kusema kwamba, “Askari wanasonga mbele kutoka Samaria.” \p \v 18 Akasema, “Ikiwa wamekuja kwa amani, wakamate wakiwa hai; ikiwa wamekuja kwa vita, wakamate wakiwa hai.” \p \v 19 Wale maafisa vijana majemadari wa majimbo wakatoka nje ya mji jeshi likiwa nyuma yao, \v 20 kila mmoja akamuua adui yake. Hii ilisababisha Waaramu kukimbia, huku Waisraeli wakiwafuatia. Lakini Ben-Hadadi, mfalme wa Aramu akapanda farasi na kutoroka pamoja na baadhi ya wapanda farasi wake. \v 21 Mfalme wa Israeli akasonga mbele, akawashinda farasi na magari ya vita ya adui, na kuwasababishia Waaramu hasara kubwa. \p \v 22 Baadaye nabii akaja kwa mfalme wa Israeli na kusema, “Jiandae vizuri ufikirie la kufanya, kwa sababu mwakani mfalme wa Aramu atakuja tena kukushambulia.” \p \v 23 Wakati huo, maafisa wa mfalme wa Aramu wakamshauri, wakamwambia, “Miungu yao ni miungu ya vilimani. Ndiyo sababu walikuwa na nguvu sana kutuzidi. Lakini tukipigana nao katika nchi tambarare, hakika tutawashinda. \v 24 Fanya hivi: Waondoe hao wafalme wote kutoka nafasi zao na uweke maafisa wengine mahali pao. \v 25 Ni lazima pia uandae jeshi lingine kama lile ulilopoteza, farasi kwa farasi, gari la vita kwa gari la vita, ili tuweze kupigana na Israeli katika nchi tambarare. Kisha kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.” Akakubaliana nao naye akashughulika ipasavyo. \p \v 26 Mwaka uliofuata, majira kama hayo, Ben-Hadadi akawakusanya Waaramu, akaenda Afeki kupigana dhidi ya Israeli. \v 27 Baada ya Waisraeli kukusanywa na kupewa mahitaji, walienda kukabiliana nao. Waisraeli wakapiga kambi mkabala nao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, Waaramu wakiwa wameenea katika nchi. \p \v 28 Yule mtu wa Mungu akaja na kumwambia mfalme wa Israeli, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Kwa sababu Waaramu wanafikiri Mwenyezi Mungu ni Mungu wa vilimani na sio Mungu wa mabondeni, nitalitia jeshi hili kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ndimi Mwenyezi Mungu.’ ” \p \v 29 Kwa siku saba walipiga kambi wakitazamana, na siku ya saba vita vikaanza. Waisraeli wakawajeruhi askari wa miguu wa Waaramu wapatao elfu mia moja kwa siku moja. \v 30 Waliobaki walikimbilia mji wa Afeki ambako elfu ishirini na saba kati yao waliangukiwa na ukuta. Naye Ben-Hadadi alikimbilia mjini na kujificha kwenye chumba cha ndani. \p \v 31 Maafisa wake wakamwambia, “Tazama, tumesikia kwamba wafalme wa nyumba ya Israeli wana huruma. Twendeni kwa mfalme wa Israeli tukiwa tumevaa gunia viunoni mwetu na kamba kuzunguka vichwa vyetu. Huenda akakuacha hai.” \p \v 32 Wakiwa wamevaa magunia viunoni mwao na kamba kuzunguka vichwa vyao, wakaenda kwa mfalme wa Israeli na kusema, “Mtumishi wako Ben-Hadadi anasema: ‘Tafadhali, naomba uniache hai.’ ” \p Mfalme akajibu, “Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu.” \p \v 33 Wale watu wakalipokea jambo lile kama dalili nzuri nao wakawa wepesi kulichukua neno lake wakisema, “Ndiyo, yeye ni ndugu yako Ben-Hadadi!” \p Mfalme akawaambia, “Nendeni mkamlete.” Ikawa Ben-Hadadi alipokuja, Ahabu akampandisha katika gari lake la vita. \p Ben-Hadadi akajitolea, akisema, \v 34 “Nitairudisha miji ambayo baba yangu aliiteka kutoka kwa baba yako. Nawe utaweka mitaa yako katika Dameski, kama baba yangu alivyofanya kule Samaria.” \p Ahabu akasema, “Kwa makubaliano, nitakuacha huru.” Hivyo, akaweka mkataba naye, kisha akamruhusu aende zake. \s1 Nabii amlaumu Ahabu \p \v 35 Kwa neno la Mwenyezi Mungu, mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake, “Nipige kwa silaha yako,” lakini yule mtu akakataa. \p \v 36 Kwa hiyo yule nabii akasema, “Kwa sababu hukumtii Mwenyezi Mungu, mara tu tutakapoachana utauawa na simba.” Na baada ya yule mtu kuondoka, simba akatokea na kumuua. \p \v 37 Nabii akamkuta mtu mwingine na kumwambia, “Nipige, tafadhali!” Kisha yule mtu akampiga na kumjeruhi. \v 38 Ndipo nabii akaenda na kusimama barabarani akimsubiri mfalme. Akajibadilisha kwa kushusha kitambaa cha kichwani mwake hadi kwenye macho. \v 39 Mfalme alipopita pale, yule nabii akamwita, “Mtumishi wako alienda vitani mahali vilikuwa kali. Mtu mmoja akanijia akiwa na mateka, akasema, ‘Mlinde mtu huyu. Akitoroka, itakuwa uhai wako kwa uhai wake, ama utalipa talanta ya fedha\f + \fr 20:39 \fr*\ft Talanta moja ni sawa na kilo 34.\ft*\f*.’ \v 40 Mtumishi wako alipokuwa na shughuli nyingi hapa na pale, yule mtu akatoweka.” \p Mfalme wa Israeli akasema, “Hiyo ndiyo hukumu yako. Wewe umeitaja mwenyewe.” \p \v 41 Kisha yule nabii akajifunua macho yake haraka, na mfalme wa Israeli akamtambua kama mmoja wa manabii. \v 42 Akamwambia mfalme, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Umemwacha huru mtu niliyekusudia afe. Kwa hivyo ni uhai wako kwa uhai wake, watu wako kwa watu wake.’ ” \v 43 Kwa uchungu na hasira, mfalme wa Israeli akaenda kwenye jumba lake huko Samaria. \c 21 \s1 Shamba la mizabibu la Nabothi \p \v 1 Baada ya hayo, pakawa na tukio lililohusisha shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli. Shamba hilo lilikuwa Yezreeli, karibu na jumba la kifalme la Ahabu, mfalme wa Samaria. \v 2 Ahabu akamwambia Nabothi, “Nipe shamba lako la mizabibu liwe langu, nilime bustani ya mboga kwa kuwa liko karibu na jumba langu. Nitakupa shamba jingine la mizabibu lililo zuri zaidi, au kama utapenda, nitakulipa kulingana na thamani ya shamba lako.” \p \v 3 Lakini Nabothi akamjibu, “Mwenyezi Mungu na apishe mbali kukupa wewe urithi wa baba zangu.” \p \v 4 Basi Ahabu akaenda nyumbani kwa uchungu na hasira kwa sababu Nabothi Myezreeli alikuwa amemwambia, “Sitakupa urithi wa baba zangu.” Akajinyoosha juu ya kitanda akisononeka, na akakataa kula. \p \v 5 Yezebeli mke wake akaingia na akamuuliza, “Kwa nini unahuzunika hivi? Kwa nini huli chakula?” \p \v 6 Akamjibu, “Kwa sababu nilimwambia Nabothi Myezreeli, ‘Niuzie shamba lako la mizabibu, au ukipenda, nitakupa shamba jingine la mizabibu badala yake.’ Lakini akasema, ‘Sitakupa shamba langu la mizabibu.’ ” \p \v 7 Yezebeli mke wake akamuuliza, “Hivi ndivyo unavyofanya, nawe ni mfalme wa Israeli yote? Inuka na ule! Changamka. Nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli.” \p \v 8 Kwa hiyo akaandika barua kwa jina la Ahabu, akaweka muhuri wa Ahabu juu ya hizo barua; kisha akazituma kwa wazee na kwa watu wenye vyeo walioishi na Nabothi katika mji wake. \v 9 Katika barua hizo aliandika: \pm “Tangazeni siku ya watu kufunga, na mkamketishe Nabothi mbele ya watu. \v 10 Waketisheni walaghai wawili mkabala naye, nao washuhudie dhidi yake kuwa amemlaani Mungu na mfalme pia. Kisha mtoeni nje na kumpiga kwa mawe hadi afe.” \p \v 11 Hivyo wazee na watu wenye vyeo walioishi katika mji wa Nabothi wakafanya kama Yezebeli alivyoelekeza katika barua alizowaandikia. \v 12 Wakatangaza mfungo na kumketisha Nabothi mbele ya watu. \v 13 Kisha walaghai wawili wakaja wakaketi mkabala naye; nao wakaleta mashtaka dhidi ya Nabothi mbele ya watu, wakisema, “Nabothi amemlaani Mungu na mfalme pia.” Kwa hiyo wakamtoa nje na kumpiga kwa mawe hadi akafa. \v 14 Kisha wakatuma ujumbe kwa Yezebeli, kusema, “Nabothi amepigwa mawe na amekufa.” \p \v 15 Mara tu Yezebeli aliposikia kwamba Nabothi amepigwa mawe na amekufa, akamwambia Ahabu, “Amka na umiliki lile shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ambalo alikataa kukuuzia. Hayuko hai tena, bali amekufa.” \v 16 Ahabu aliposikia Nabothi amekufa, akainuka, kisha akashuka kwenda kulimiliki shamba la mizabibu la Nabothi. \p \v 17 Kisha neno la Mwenyezi Mungu likamjia Ilya Mtishbi, kusema: \v 18 “Shuka ukakutane na Ahabu mfalme wa Israeli, anayetawala Samaria. Sasa yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ambalo ameenda kulimiliki. \v 19 Umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Je, hujamuua mtu na kuitwaa mali yake?’ Kisha umwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Mahali mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba damu yako pia; naam, yako wewe!’ ” \p \v 20 Ahabu akamwambia Ilya, “Kwa hiyo umenipata, wewe adui yangu!” \p Akajibu, “Ndiyo, nimekupata. Kwa sababu umejiuza mwenyewe kwa kufanya uovu mbele za macho ya Mwenyezi Mungu. \v 21 ‘Nitaleta maafa juu yako. Nitaangamiza uzao wako na kukatilia mbali kila mwanaume wa jamaa ya Ahabu katika Israeli, awe mtumwa au mtu huru. \v 22 Nitaifanya nyumba yako kuwa kama ile ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa sababu umenighadhibisha kwa kusababisha Israeli kutenda dhambi.’ \p \v 23 “Pia Mwenyezi Mungu anasema kumhusu Yezebeli: ‘Mbwa watamla Yezebeli karibu na ukuta wa Yezreeli.’ \p \v 24 “Mbwa watawala wale wa nyumba ya Ahabu watakaofia mjini, nao wale watakaofia mashambani wataliwa na ndege wa angani.” \p \v 25 (Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe. \v 26 Alitenda uovu sana kwa kuzifuata sanamu, kama Waamori ambao Mwenyezi Mungu aliowafukuza mbele ya Israeli.) \p \v 27 Ahabu aliposikia maneno haya, akararua nguo zake, akavaa gunia na kufunga. Akalala na kujifunika gunia na kwenda kwa unyenyekevu. \p \v 28 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu lilipomjia Ilya Mtishbi kusema, \v 29 “Umeona jinsi Ahabu alivyojinyenyekeza mbele zangu? Kwa kuwa amejishusha mwenyewe, sitaleta maafa haya wakati akiwa hai, lakini nitayaleta juu ya nyumba yake katika siku za mwanawe.” \c 22 \s1 Mikaya atabiri dhidi ya Ahabu \r (2 Nyakati 18:2-27) \p \v 1 Kwa miaka mitatu hapakuwa na vita kati ya Aramu na Israeli. \v 2 Lakini katika mwaka wa tatu, Yehoshafati mfalme wa Yuda akateremka kwenda kumwona mfalme wa Israeli. \v 3 Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia maafisa wake, “Je, hamjui Ramoth-Gileadi ni mali yetu, na bado hatufanyi chochote kuirudisha kwetu kutoka kwa mfalme wa Aramu?” \p \v 4 Kwa hiyo akamuuliza Yehoshafati, “Je, utaenda pamoja nami kupigana dhidi ya Ramoth-Gileadi?” \p Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.” \v 5 Lakini Yehoshafati pia akamwambia mfalme wa Israeli, “Kwanza tafuta ushauri wa Mwenyezi Mungu.” \p \v 6 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akawaleta pamoja manabii, wanaume wapatao mia nne, akawauliza, “Je, niende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi, au niache?” \p Wakajibu, “Naam, nenda, kwa kuwa Bwana ataiweka Ramoth-Gileadi mkononi mwa mfalme.” \p \v 7 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Mwenyezi Mungu hapa ambaye tunaweza kumuuliza?” \p \v 8 Mfalme wa Israeli akamjibu Yehoshafati, “Bado yupo mtu mmoja ambaye kupitia kwake twaweza kuuliza ushauri wa Mwenyezi Mungu, lakini namchukia kwa sababu hatabiri jambo lolote jema kunihusu, ila hunitabiria mabaya kila mara. Yeye ni Mikaya mwana wa Imla.” \p Yehoshafati akajibu, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.” \p \v 9 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwita mmoja wa maafisa wake na kusema, “Mlete Mikaya mwana wa Imla mara moja.” \p \v 10 Wakiwa wamevalia majoho yao ya kifalme, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi juu ya viti vyao vya kifalme katika sakafu ya kupuria, kwenye ingilio la lango la Samaria, huku manabii wote wakitabiri mbele yao. \v 11 Wakati huu Sedekia mwana wa Kenaana alikuwa ametengeneza pembe za chuma. Naye akatangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, ‘Kwa hizi pembe utawapiga Waaramu hadi waangamizwe.’ ” \p \v 12 Manabii wengine wote walikuwa wanatabiri kitu hicho hicho wakisema, “Ishambulie Ramoth-Gileadi na uwe mshindi. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ataitia mkononi mwa mfalme.” \p \v 13 Mjumbe aliyekuwa ameenda kumwita Mikaya akamwambia, “Tazama, manabii wote kama mtu mmoja wanatabiri ushindi kwa mfalme. Neno lako na likubaliane na lao, nawe unene mema kuhusu mfalme.” \p \v 14 Lakini Mikaya akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, nitamwambia kile tu Mwenyezi Mungu atakachoniambia.” \p \v 15 Alipofika, mfalme akamuuliza, “Mikaya, je, twende vitani dhidi ya Ramoth-Gileadi au niache?” \p Akamjibu, “Shambulia na ushinde, kwa kuwa Mwenyezi Mungu atawatia mkononi mwa mfalme.” \p \v 16 Mfalme akamwambia, “Je, ni mara ngapi nitakuapisha ili usiniambie kitu chochote ila kweli tu kwa jina la Mwenyezi Mungu?” \p \v 17 Ndipo Mikaya akajibu, “Niliona Israeli wote wametawanyika vilimani kama kondoo wasio na mchungaji, naye Mwenyezi Mungu akasema, ‘Watu hawa hawana kiongozi. Mwache kila mmoja aende nyumbani kwa amani.’ ” \p \v 18 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba huwa hatabiri jambo lolote jema kunihusu, ila mabaya tu?” \p \v 19 Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Mwenyezi Mungu: Nilimwona Mwenyezi Mungu ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto. \v 20 Naye Mwenyezi Mungu akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’ \p “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile. \v 21 Hatimaye, pepo mchafu akajitokeza, akasimama mbele za Mwenyezi Mungu na kusema, ‘Nitamshawishi.’ \p \v 22 “Mwenyezi Mungu akauliza, ‘Kwa njia gani?’ \p “Akasema, ‘Nitaenda na kuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ \p “Mwenyezi Mungu akasema, ‘Utafanikiwa katika kumshawishi. Nenda ukafanye hivyo.’ \p \v 23 “Kwa hiyo sasa Mwenyezi Mungu ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. Mwenyezi Mungu ameamuru maafa kwa ajili yako.” \p \v 24 Kisha Sedekia mwana wa Kenaana akatoka na kumpiga Mikaya kofi usoni. Akauliza, “Huyo Roho kutoka kwa Mwenyezi Mungu alipita njia gani alipotoka kwangu ili kusema nawe?” \p \v 25 Mikaya akajibu, “Utagundua siku hiyo utakapoenda kujificha kwenye chumba cha ndani.” \p \v 26 Kisha mfalme wa Israeli akaagiza, “Mchukueni Mikaya, mkamrudishe kwa Amoni mtawala wa mji, na kwa Yoashi mwana wa mfalme. \v 27 Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe chochote ila mkate na maji hadi nitakaporudi salama.’ ” \p \v 28 Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, basi Mwenyezi Mungu hajanena kupitia kwangu.” Kisha akaongeza kusema, “Zingatieni maneno yangu, enyi watu wote!” \s1 Ahabu auawa huko Ramoth-Gileadi \r (2 Nyakati 18:28-34) \p \v 29 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakaenda Ramoth-Gileadi. \v 30 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitaingia vitani nikiwa nimejibadilisha, lakini wewe uvae majoho yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na kwenda vitani. \p \v 31 Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.” \v 32 Wale majemadari wa magari ya vita walipomwona Yehoshafati wakafikiri, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo wakageuka ili wamshambulie, lakini Yehoshafati alipopiga kelele, \v 33 wale majemadari wakaona kwamba hakuwa mfalme wa Israeli, wakaacha kumfuatilia. \p \v 34 Lakini mtu mmoja akavuta upinde pasipo lengo na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya kiungio cha mavazi yake ya chuma. Mfalme akamwambia mwendesha gari lake la vita, “Geuza gari na uniondoe katika mapigano, nimejeruhiwa.” \v 35 Vita vikaendelea mchana kutwa, naye Mfalme Ahabu akategemezwa ndani ya gari lake la vita kuelekea Waaramu. Damu kutoka jeraha lake ikatiririka ndani ya gari lake, na jioni yake akafa. \v 36 Jua lilipokuwa linazama, mbiu ikaenea katika jeshi lote: “Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake!” \p \v 37 Basi mfalme akafa na akaletwa Samaria, nao wakamzika huko. \v 38 Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakaramba damu yake, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu lilivyokuwa limesema. \p \v 39 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Ahabu, pamoja na yote aliyoyafanya, jumba la kifalme alilojenga na kupambwa kwa pembe za ndovu, nayo miji aliyoijengea ngome, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? \v 40 Ahabu akalala na baba zake. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Yehoshafati mfalme wa Yuda \r (2 Nyakati 20:31–21:1) \p \v 41 Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme wa Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli. \v 42 Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka ishirini na tano. Mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi. \v 43 Katika kila jambo alitembea katika njia za Asa baba yake wala hakuenda kinyume chake. Alifanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. \v 44 Yehoshafati pia alikuwa na amani na mfalme wa Israeli. \p \v 45 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, mafanikio aliyokuwa nayo na uhodari wake katika vita, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? \v 46 Aliondolea mbali katika nchi mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu waliobaki huko hata baada ya utawala wa baba yake Asa. \v 47 Wakati ule, hakukuwa na mfalme katika Edomu; naibu ndiye alitawala. \p \v 48 Wakati huu Yehoshafati akaunda merikebu nyingi za biashara\f + \fr 22:48 \fr*\ft au \ft*\fqa za Tarshishi \fqa*\ft (taz. \+xt 1 Wafalme 10:22; 2 Nyakati 9:21; 20:36; Isaya 2:16; 60:9\+xt*).\ft*\f* ili kwenda Ofiri kuchukua dhahabu; lakini kamwe hazikusafiri, kwa maana zilivunjikia huko Esion-Geberi. \v 49 Wakati ule, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Waache watu wangu wasafiri baharini pamoja na watu wako,” lakini Yehoshafati akakataa. \p \v 50 Kisha Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Yehoramu mwanawe akawa mfalme baada yake. \s1 Ahazia mfalme wa Israeli \p \v 51 Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Naye akatawala katika Israeli kwa miaka miwili. \v 52 Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi. \v 53 Alimtumikia na kumwabudu Baali na kumghadhibisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.